Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1377 | 1378 | (Page 1379) | 1380 | 1381 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Ben Pol  na Maua Sama wakipagawisha  wakazi wa jiji la Mwanza katika Tamasha  la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jumapili katika viwanja vya CCM Kirumba.
  Ommy Dimpoz akiburudisha wakazi wa jiji la Mwanza katika vviwanja via Tigo Fiesta mapema jana katika vviwanja vya CCM kirumba usiku wa kuamkia jumapili.
  Alikba na Ommy dimpoz wakilishambulia jukwaa la Tigo fiesta mapema usiku wa jana katika vviwanja vya CCM kirumba
  GNAKO na JUX wakiwaburudisha maelfu ya wakazi wa Mwanza katika Tamasha la Tigo Fiesta.
  Lulu DIVA akiwa na wacheza shoo wake wakitoa burudani ya kukata na shoka.
  NanDy akiimba kwa hisia katika jukwaa la Tigo Fiesta mapema jana katika viwanja via CCM kirumba.
  Maua Sama naye akilishambulia jukwaa la Tigo fiesta

  Msanii wa bongo fleva Rayvanny akiwapa burudani wapenzi wa muziki kwenye tamasha la Tigo Fiesta katika uwanja wa CCM kirumba jijini Mwanza usiku wa kuamkia Jumapili.


  Rosa Ree akipagawawisha maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza.
  0 0

  Marehemu Mohamed Idi Mturuma aka Muddy enzi za uhai wake.

  Umoja wa Wa Watanzania Ujerumani kwa ushirikiano na watanzania wanaoishi England na Spain kwa masikitiko makubwa sana tulipata msiba wa ndugu yetu mtanzania mwenzetu mcheza sarakasi Mohamed Idi Mturuma aliekuwa akiishi koloni Ujerumani na kufariki nchini spain alikokwenda kikazi.

  Aliaga dunia tarehe 19.09.17 Kwa ushirikiano wa Watanzania wanaoishi nchi hizo tumeazimia kufanya kila liwezekanalo ili kuweza kusafisrisha mwili wa Marehemu ndugu yetu Mohamed Idi Mturuma kwenda kuzikwa nyumbani Tanzania Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU.e.V ) Unawatangazia watanzania wote wanaoishi popote pale Duniani kuunga mkono azma yetu kwa kutoa michango ya hali na mali ili tumsafirishe mwenzetu.

  Shukran nyingi kwa msanii Mussa FAB Moses Kutoka England ambaye alisafiri mara baada ya msiba kutokea kwenda Spain kwa ajili ya kusaidia mchakato wa kuandaa kusafirisha mwili wa marehemu. Mussa Fab Moses anategemea kusafiri na mwili wa Merehem kwenda Tanzania kwa Mazishi

  Watanzania wanaoishi England mnaweza kuwasiliana moja kwa moja na Saidi Kanda ili kuwasilisha michango yenu namba ya kiganjani +447404066607

  Watanzania wanaoishi Tanzania mnaweza kuwasiliana na Eddy Sengo ili kuwasilisha michango yenu namba ya kiganjani +255656210725

  Watanzania wanaoishi Ujerumani mnaweza kuwasiliana na Makamo mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTUe.V) Malumbo Salim Malumbo namba ya simu +49 1522 4082848

  Mwili wa Marehemu ulisaliwa msikitini siku ya ijumaa iliyopita tarehe 22.09.17 na kupelekewa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kwa ajili ya kusubiria safari.

  UMOJA NI NGUVU; PENYENIA PANA NJIA; TUKITAKA TUTAWEZA KWA KUDRAZA MWENYEZIMUNGU INSHALLAH WABILAHI TAWFIQ

  UMOJA WA WATANZANIA UJERUMANI (UTU e.V)
   Waumini wa kiisalam nchini spain wakijiandaa kuusalia mwili wa marehem Mohamedi Idi Mturuma nchi spain.
   Waumini wakiislam wakielekea msikitini kuusalia mwili wa marehemu Mohamedi Idd Mturuma.
  baadhi ya marafiki  zake marehemu Mohamedi Idi Mturuma baada ya kutoka kuusalia mwili wa marehemu.

  0 0

  Benny Mwaipaja, WFM, Pwani

  SERIKALI imeahidi kuyafanyiakazi malalamiko ya wamiliki wa shule za binafsi nchini kuhusu kodi mbalimbali wanazotozwa kwa kuwa Serikali inathamini mchango mkubwa wa taasisi binafsi za elimu katika mapambano dhidi ya adui ujinga.

  Ahadi hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, wakati wa sherehe za mahafali ya kumi ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Baobab, iliyoko Mapinga, Wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.

  Dokta Kijaji amesema kuwa tayari Serikali imeondoa baadhi ya kodi kwa shule hizo ikiwemo kodi ya mabango, Usalama mahali pa kazi-OSHA, Ada ya zimamoto, na kwamba kikosi kazi kilichoundwa na Serikali kupitia upya kodi zingine zinazoonekana kuwa kikwazo katika utoaji wa elimu, kinaendelea na kazi na matokeo yake yataonekana hivi karibuni.

  “Niko kwenye kikosikazi kinachoshughulikia changamoto za kodi kwenye shule za watu binafsi ninaamini suluhisho litapatikana kutokana na Serikali kuthamini mchango wenu mkubwa katika kuwapatia vijana wetu elimu” alisema Dkt. Kijaji

  Alieleza kuwa katika Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2017/2018, suala hilo litazingatiwa na kuwataka wamiliki wa shule binafsi nchini kuwa watulivu wakati jambo hilo linafanyiwakazi tena kwa umakini mkubwa.

  Awali Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari Baobab, Bw. Halfan Swai, pamoja na kuiomba Serikali ifute kodi mbalimbali wanazotozwa kwa kuwa hawafanyibiashara bali wanaisaidia Serikali kutoa huduma kwa jamii, ameomba pia isaidie  kuangalia viwango vya riba vinavyotozwa na taasisi za fedha nchini kwa kuwa zinawawekeka katika mazingira magumu wanapohitaji mikopo ya kuendeleza shule zao.

  Wanafunzi 149, (wavulana 14 na wasichana 135)  wa Shule hiyo wanaotarajiwa kuhitimu masomo yao ya kidato cha nne hivi karibuni, wameahidi kufanya vizuri katika mitihani yao kwa kuwa wameandaliwa vizuri na walimu waliobobea katika ufundishaji pamoja na mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia shuleni hapo.

  Dokta Ashatu Kijaji, mbali na kuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo, yeye na familia yake wameshuhudia mtoto wao Samira, akiagwa wakati wa mahafali hayo yaliyohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wazazi, ndugu na jamaa wa wanafunzi hao.
  Meza Kuu ikiongozwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (Katikati), wakiimba Wimbo wa Taifa wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Nne ya Shule mchanganyiko ya Sekondari Baobab, iliyoko eneo la Mapinga, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, ambapo wanafunzi 149 wanatarajiwa kuhitimu masomo yao majuma machache yajayo.
  Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari Baobab Bw. Halfan Swai, akiiomba Serikali iangalie changamoto ya riba ya mikopo inayotolewa an taasisi za fedha pamoja na kuondoa kodi mbalimbali zinazotozwa shule binafsi kwakuwa taasisi hizo zinaisaidia Serikali kutoa huduma kwa wananchi wake, wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Nne ya Shule hiyo.
  Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Baobab, wakionyesha ishara ya umoja, upendo na mshikamano wakati wakiimba wimbo wa kuwaaga wanafunzi wenzao wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Nne ya shule yao. 
  Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 10 ya Shule ya Sekondari Baobab, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akihutubia Jumuiya ya Shule ya Sekondari Baobab, wakati wa mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Kidato cha Nne wanaotarajiwa kufanya mitihani yao siku chache zijazo.
  Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 10 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Baobab, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akimkabidhi zawadi mmoja wa wanafunzi mwenye ulemavu aliyefanya vizuri katika baadhi ya masomo wakati wa sherehe ya kuwaaga, iliyofanyika shuleni hapo.
  Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 10 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Baobab, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), (Katikati), akikabidhi keki kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Baobab, iliyoko Mapinga, Bagamoyo, mkoani Pwani, ikiwa ni alama ya kusherehekea siku yao ya kuagwa shuleni hapo.
  Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 10 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Baobab, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akiwa katika Picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Nne wanaotarajiwa kuhitimu masomo yao hivi karibuni, wakati wa sherehe ya kuwaaga shuleni hapo.
  Familia ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akiwa na mumewe Dkt. Kachwamba, wakimpongeza binti yao Samira anayetarajiwa kuhitimu masomo yake ya Kidato cha Nne katika Shule ya Seondari Baobab, iliyoko Mapinga, Bagamoyo mkoani Pwani ambapo Naibu Waziri alikuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo ya 10 ya Kidato cha Nne. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango.

  0 0  0 0

  Wamiliki wa Showroom za kuuza Magari leo wamepelekwa Kigamboni kwenye eneo maalumu lililotengwa kwaajili ya Kuuza Magari (Dar es Salaam Automobile Zone) kwaajili ya kukagua  eneo hilo na kuonyeshwa namna ya kumilikishwa.

  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa amesema eneo hilo litamilikishwa kwa Wamiliki wa Showroom kwa Muda wa Miaka Mitatu ya Mwazo Bure kisha Baada hapo watawekewa utaratibu wa Malipo.

  Amesema Wamiliki hao watatakiwa kutoa kiasi cha Shilingi 300,000 kama dhamana ya kuonyesha nia. Amesema kuwa ukubwa wa eneo lilitengwa kwaajili ya Showroom ni Square Meter 750,000 ambapo lipo eneo lingine la ziada lenye ukubwa wa kiasi cha Square Meter zaidi ya 300,000.

  Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya Kigamboni Rahel Mhando amesema mradi huo ni fursa kubwa ya Maendeleo kwa Wilaya hiyo. Amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kubuni Mpango huo ambao pia utafanya Wilaya ya Kigamboni kuwa kwenye mpangilio Mzuri.

  Nae Salim Chicago ambae ni mmiliki wa Showroom amesema Mpango huo utawapa unafuu wa kupata huduma zote ikiwemo TRA, TPA,BIMA,SUMATRA,Kituo cha Polisi na huduma za Kibank ndani ya eneo moja. Aidha amesema Mpango huo utawarahisishia kupata Wateja wengi na wa uhakika kutoka ndani na Nje ya Nchi.
  Hata hivyo amesema utaratibu huo utawawezesha kulipa kodi ya Serikali na kuwabana wale Wafanyabiashara wanaofanya biashara za magari kwenye maeneo bubu.

  Ikumbukwe kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alitoa agizo la kuwataka wenye Showroom na Yard za kuuza Magari kuhakikisha wanahamia Kigamboni kwenye eneo maalumu lililotengwa kwaajili ya Showroom kabla ya Mwezi January Mosi mwakani.
  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa (wakwanza kushoto) akizungumza na wamiliki wa Showroom za kuuza Magari katika eneo maalumu lililotengwa kwaajili ya Kuuza Magari (Dar es Salaam Automobile Zone).
  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa (katikati) akiwaonesha wamiliki wa showroom eneo lililotengwa kwaajili ya biashara ya magari Kigamboni jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari-TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kuhusu mafuta yanavyopakuliwa kutoka kwenye meli, alipotembelea bandarini hapo ili kupata maelezo kuhusu mchakato wa kupata mita mpya za kupimia mafuta (Flow Meters), Jijini Dar es salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko (kushoto) akimuonesha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), namna maharamia wa mafuta walivyoharibu miundombinu ya bomba la mafuta baharini, baada ya kufanikiwa kukamata boti moja na vifaa vyake lililokuwa likitumiwa na wahalifu hao kuiba mafuta.
  Boti Jeupe lililonaswa na kikosi maalumu cha kuzuia uhalifu cha Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) juzi wakati wahalifu wakijiandaa kutoboa bomba na kuiba mafuta kwenye kina kirefu cha Bahari ya Hindi. Wahalifu walifanikiwa kutokomea kusikojulikana baada ya kujitosa baharini, Dar es Salaam.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akiwapongeza askari wa doria waliofanikisha kukamata boti moja pamoja na vifaa vyake muhimu ikiwemo injini baada ya kuwadhibiti maharamia waliotaka kutoboa bomba na kuiba mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.
  Mmoja wa maafisa wa TPA walioongoza zoezi la kupambana na wahalifu wanaoiba mafuta kwenye bomba la mafuta akionesha vilipuzi vilivyokamatwa vilivyokuwa vitumiwe na wahalifu waliokuwa wakijaribu kuiba mafuta kwenye bomba la mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.
  Kaimu Kamisha na Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Elijah Mwandumbya, akitoa maelezo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), kuhusu hatua zilizochukuliwa kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali upande wa mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko, akitoa maelezo walipokuwa wakiagana na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)Katika ziara hiyo Waziri Mpango amepongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania na Mamlaka ya Mpato katika kudhibiti ukwepaji kodi.
  Mmoja wa maafisa wa TPA walioongoza zoezi la kupambana na wahalifu wanaoiba mafuta kwenye bomba la mafuta akionesha vilipuzi vilivyokamatwa vilivyokuwa vitumiwe na wahalifu waliokuwa wakijaribu kuiba mafuta kwenye bomba la mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (mbele), akiwa ametoka kukagua mitambo ya kupitisha mafuta kutoka kwenye Meli ili kujihakikishia kama hakuna namna ya ubadhilifu au hujuma kwa mapato ambayo Serikali inatakiwa kuyapata.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia)na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko (kulia) na wengine, walipotembela Bandari ya Dar es Salaam, kitengo cha Mafuta, kukagua flow meters na tukio la kukamatwa kwa boti lililokuwa likitumika kuhujumu bomba la mafuta.


  Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango

  0 0

   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akikagua uwanja wa Machinga uliopo mjini Tukuyu ambao umebadilishwa matumizi na Halmashauri ya Rungwe kwa kukosa sifa w badala yake uwanja wa michezo sasa utakuwa unatumika ule wa Tandale mjini humo.03
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akiongea na wananchi na wanamichezo (hawapo pichani) waliokuwa wanashiriki Tamasha la Ngoma za Jadi linaloratibiwa na Taasisis ya Tulia Trust mjini Tukuyu
  04
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura         (wa pili kushoto) na Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson wakibeba nyoka anyetumiwa kwa kucheza ngoma ya Bogobogobo kutoka Bujora Mwanza.
  (Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Tukuyu)
  ………………………………………………………………………………
  Na Eleuteri Mangi, Tukuyu, Mbeya.
  Halmashauri ya Rungwe imebadilisha matumizi ya uwanja wa zamani wa mpira wa miguu uliopo mjini Tukuyu unaojulikana kama machinga kuendelea kutumika kwa matumizi mengine kutokana na kukosa sifa za uwanja huo kukosa sifa.
  Badala yake Halmashauri hiyo imetoa uwanja wa Tandale uliopo mjini Tukuyu kutumika kwa michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu na matamasha mbalimbali.
  Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Tukuyu Bw. Julius Chalya alipokuwa akitoa taarifa fupi ya shughuli za maendeleo katika wilaya hiyo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura alipokuwa katika ziara ya kikazi mkoani Mbeya.
  “Uwanja wa mwanzo unaojulikana kama uwanja wa Machinga uliokuwa unatumika kwa michezo kwa sasa haufai kwa matumizi ya michezo kwa kukosa sifa, hivyo halmashauri imebadilisha matumizi yake ili uendelee kutumika kwa matumizi mengine ikiwemo kituo cha mabasi yanayotoa huduma katika halmashauri na bishashara nyingine” alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
  Akizungumzia kuhusu uamuzi wa halmashauri wa kubadilisha matumizi ya uwanja huo wakati wa kufunga Tamasha la pili la Ngoma za Asili linaloendeshwa na Taasisi ya Tulia Trust, Naibu Waziri Wambura amesema kuwa Serikali inaendelea kusisitiza halmashauri ziendelee kutenga maeneo yanayofaa kwa michezo kwa kutimiza vigezo vinavyotakiwa kwa ajili ya michezo.
  Uwanja wa Tukuyu uliokuwa unatumika zamani kwa michezo umekosa vigezo vya kuendelea kutumika kama uwanja wa michezo kutokana na vipimo vyake kuonesha kuwa ni mdogo kwa kiwango cha halisi unatakiwa kuwa na urefu wa mita 68 na huo wa Tukuyu una mita 44.
  Kuhusu kuendeleza kiwanja cha Tandale ambao umetolewa na halmashauri kwa ajili ya michezo, Naibu Waziri Wambura ameliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kupitia Katibu Mtendaji wake Mohamed Kiganja kushirikiana na halmashauri hiyo kwa kutoa ushauri wa kitaalamu kuendeleza uwanja huo ili wananchi wa Rungwe waweze kuutumia kuboresha afya zao kwa kufanya mazoezi pamoja kunufaika na fursa za kiuchumi wakati wa mashindano mbalilmbali yatakayofanyika uwanjani hapo.
  Kupatikana kwa uwanja wa Tandale utnaotumika kwa sasa kwa michezo mbalimbali mjini Tukuyu kumepokelwa na kwa furaha na wananchi waliofurika viwanja hivyo wakati wa kuhitimisha Tamamsha la pili la Ngoma za Jadi linaloratibiwa na Taasisi ya Tulia Trust ambapo mwasisi wake Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameanza kampeni ya kuirudisha timu ya Tukuyu Stars kwa kuwahamasisha Wabunge wa mkoa wa Mbeya na wananchi kuiwezesha  timu hiyo kurudi Ligi Kuu ya Tanzania ya Vodacom.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Dkt,Idris Muslim Hija kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja,[Picha na Ikulu.] 24/09/2017.


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Joseph Abdalla Meza kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi,hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,[Picha na Ikulu.] 24/09/2017.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Juma Ali Juma kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko,hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi,[Picha na Ikulu.] 24/09/2017.


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Bakari Haji Bakari kuwa Katibu Mtendaji wa Bazara la Biashara la Zanzibar hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko,[Picha na Ikulu.] 24/09/2017.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Ali Khamis Juma kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko,hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Naibu Katibu Wizara ya Fedha na Mipango,[Picha na Ikulu.] 24/09/2017.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Iddi Haji Makame kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 24/09/2017. 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Abeid Juma Ali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba[Picha na Ikulu.] 24/09/2017. 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Rashid Hadid Rashid kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba[Picha na Ikulu.] 24/09/2017. 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bibi Salama Mbarouk Khatibu kuwa Mkuu wa Wilaya yaMicheweni Pemba katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba[Picha na Ikulu.] 24/09/2017.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Kapteni Khatib Khamis Mwadini kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A.Unguja, hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 24/09/2017.

  0 0

  Na Agness Francis Blogu ya jamii.

  Katika tamasha la tamasha la muziki Mnene lililokonga nyoyo za mashabiki  ambalo limefanyika  katika ukumbi wa New Msasani Jijini Dar es Salaam  ambapo wasanii kama Chidi Benzi, Nuhu Mziwanda, Izzo Business, Bob Junior, Makomando pamoja na Kayumba Asosiye  mshindi wa BSS walitoa burudani ya kutosha  kwa wakazi hao wa Kinondoni.

  Hata hivyo Michuzi Blog imezungumza na msanii Kayumba Asosiyee ambaye mpaka hivi sasa yupo chini ya meneja wake Mkubwa Fella ametanabaisha kuwa kuwepo kwa tamasha  hilo la Mziki nene linasaidia kukuza  vipaji vya wasanii chipukizi vilivyolala.

  Vile vile msanii huyo amesema  kuwa changamoto ya muziki wa sasa mchuano umekuwa mkali sana kwa sababu mashabiki wanajua muziki mzuri, inabidi kupambana ili kuhakikisha unatoa kitu chenye ubora, na amewaahidi mashabiki wake wake mkao wa kula anatarajia kutoa ngoma yake hivi karibuni.                      
  Mwanamuziki wa kizazi kipya Chidi Benzi akiwaburudisha mashabiki wake na kuwa acha midomo wazi Kwa kazi nzuri alioifanya katika tamasha la muziki Mnene katika  klabu  ya New Msasani Jijini Dar es Salaam.
  Mwanamuziki wa kizazi kipya  Izzo Business akifanya yake jukwaani    kuwaburudisha mashabiki  wake na wapenzi wa hip hop waliojitokeza Kwa wingi katika tamasha hilo la muziki mnene katika  klabu  ya New Msasani Jijini Dar es Salaam.
  Mwanamuziki wa kizazi kipya Nuhu Mziwanda akizima kiki na kuwasha muziki katika kuhakikisha wakazi wa Kinondoniwanapata Burundi  kabambe akiimba  nyimbo yake mpya ambayo inajulikana kama  bao  la ushindi katika tamasha hilo la  muziki mnene katika  klabu  ya New Msasani Jijini Dar es Salaam.
  Mwanamuziki wa kizazi kipya  kundi La Masada sita  wakitia burudani Kwa kuimba na kucheza kuwaburudisha wazi wa maeneo hayo  ambao hawakuachwa salama Kwa shoo nzuri iliofanywa na wadada hawa katika tamasha la  muziki mnene katika  klabu  ya New Msasani Jijini Dar es Salaam.
  Mashabiki na wakazi wa Kinondoni waliojitokeza Kwa wingi kushuhudia shoo ya kukata na shoka kutoka Kwa wasanii Mbalimbali wa hapa nchini wakitoa burudani  kwao katika tamasha la  muziki mnene katika  klabu  ya New Msasani Jijini Dar es Salama. Picha na Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.

  0 0


  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Prof. Norman Sigalla King (wa kwanza kushoto) na wajumbe wengine wa Kamati wakiwa wamekalia mnara wa Halotel wakipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel Bwana Philemon Joel (hayupo pichani) kuhusu utayari wa kampuni hiyo kujenga mnara baada ya mgogoro wa ardhi kumalizika kwenye kijiji kijiji cha Timbolo, kata ya Sambasha Wilaya ya Arumeru mkoani Manyara
  Meneja wa TTCL Mkoa wa Arusha na Manyara Bwana Brown Japhet (wa pili kushoto) akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu (hawapo pichani) ilipofanya ziara ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini kwenye kijiji cha Sigino kata ya Singo iliyopo wilaya ya Babati Mjini mkoani Manyara. Wa kwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Eng. Peter Ulanga.
  Kaimu Mkurugenzi wa kampuni ya simu ya Halotel wa Mkoa wa Arusha Bwana Philemon Joel (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu (hawapo pichani) kuhusu utayari wa kampuni hiyo kujenga mnara kwenye kijiji cha Timbolo, kata ya Sambasha Wilaya ya Arumeru mkoani Manyara baada ya mgogoro wa ardhi kumalizika. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Bwana Albert Richard.
  Mwenyekiti wa kijiji cha Timbolo, kata ya Sambasha wilaya ya Arumeru mkoani Manyara Bwana Samwel Saning’o akisisitiza umuhimu wa uwepo wa mawasiliano vijijini mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakati wa ziara ya Kamati kwenye kijiji hicho ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini.


  ……………………………

  Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote imeendelea na kazi ya kuhakikisha kuwa wanachi wote waishio vijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara wanapata huduma za mawasiliano kwa wakati ili kuweza kuchangia ukuaji wa uchumi na upatikanaji wa huduma za kijamii na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

  Hayo yameelezwa na Mtendajii Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu ya kukagua ujenzi wa minara ya simu za mkononi na upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwenye maeneo mbalimbali vijijini ya mkoa wa Arusha na Manyara. Eng. Ulanga amesema kuwa migogoro ya ardhi kwenye baadhi ya vijiji mbalimbali nchini inachangia ucheleweshaji wa ujenzi wa minara na ufikishaji wa huduma za mawasiliano vijijini.

  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Mfuko huu uliweka lengo la kufikisha mawasiliano kwenye vijiji 4,000 nchi nzima ifikapo mwezi Novemba mwaka huu. Uwepo wa migogoro ya ardhi unachangia kuchelewesha kampuni za simu zilizopatiwa ruzuku na Serikali kujenga minara, “mgogoro wa ardhi kwenye kijiji cha Timbolo kata ya Sambasha Wilayani Arumeru umeichelewesha kampuni ya Halotel kujenga mnara na hivyo wananchi wa kata hii kukosa mawasiliano kwa kuwa mgogoro huo umechukua zaidi ya miaka miwili kukamilika mahakamani,”amesema Eng. Ulanga.

  Kaimu Mkurugenzi wa kampuni ya simu ya Halotel wa Mkoa wa Arusha Bwana Philemon Joel amesema kuwa mahakama iliweka zuio la ujenzi wa mnara kwenye eneo la kijiji cha Timbolo kata ya Sambasha ambapo kesi ya mgogoro huo umechukua miaka miwili kufanyiwa maamuzi kwenye ngazi ya mahakama. “Tumekuwa tukienda mahakamani mara kwa mara na kupigwa tarehe kuambiwa Hakimu hayupo na mara nyingine inapita miezi minne bila ya kesi kusikilizwa hivyo imetuchelewesha kuanza ujenzi,”amesema Bwana Joel.

  Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Timbolo, kata ya Sambasha Bwana Samwel Saning’o amesema kuwa Serikali ya kijiji ilisimama na kusema kuwa wanataka mawasiliano na sio utalii kwa kuwa kulikuwa na mgogoro baina ya mmiliki wa eneo la jirani na eneo la mwingine ambapo mnara unatakiwa kujengwa. 

  Bwana Saning’o amemshukuru sana Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Bwana Alexandra Mnyeti kwa kuingilia kati mgogoro huu, kusimamia na kuhakikisha kuwa unakamilika ili wananchi waweze kupata mawasiliano. Eng. Ulanga amesema ujenzi wa mnara wa Halotel kwenye eneo hili hauwezi kukamilika mwezi Novemba mwaka huu, hivyo sisi kama Mfuko wa UCSAF tutawapatia muda wa ziada ili waweze kukamilisha ujenzi wa mnara na wananchi waweze kupata mawasiliano. Pia Eng. Ulanga amewataka wanachi wa vijiji husika kushirikiana na kampuni za simu kulinda miundombinu ya mawasiliano na minara ili mawasiliano yaweze kupatikana muda wote.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Prof. Norman Sigalla King ametoa rai kwa mamlaka zinazosimamia haki na vyombo vya ulinzi viambata vya Jeshi la Polisi na mahakama kufanya uchunguzi na kuendesha kesi kwa wakati ili kuharakisha kutoa haki. “Ukichelewa kutoa shauri la hukumu kwa jambo la umma linalogusa maslahi ya wananchi unachelewesha maendeleo ya wananchi,”amesema Prof. Norman Sigalla King. Ameongeza kuwa wananchi washirikiane na kampuni za simu za mkononi kulinda minara na kutoa ardhi bila migogoro ili waweze kupata huduma za mawasiliano kwenye vijiji vyao kwa wakati.


  Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Prof. Norman Sigalla King ameitaka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kukamilisha ujenzi wa minara yake ya simu kwa wakati kwenye vijiji mbalimbali nchini ili wananchi wa maeneo husika waweze kupata huduma za mawasiliano. Hayo ameyasema Prof. Norman Sigalla King wakati wa ziara ya Kamati yake walipotembelea kijiji cha Sigino kata ya Singo iliyopo wilaya ya Babati Mjini mkoani Manyara. 

  Naye Meneja wa TTCL Mkoa wa Arusha na Manyara Bwana Brown Japhet amesema kuwa TTCL imekamilisha ujenzi wa minara kwenye vituo vyote vya Mkoa wa Arusha na viko hewani wananchi wanapata mawasiliano. Bwana Japhet ameilieza Kamati kuwa kwa vituo viwili vilivyobaki vya TTCL kama pale Saitabau, Arusha kulikuwa na mgogoro wa ardhi ambapo Serikali ya Mkoa imeingilia kati na kumaliza mgogoro huo na vituo vingine viwili vipo kwenye hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ambapo vinasubiri tathmini ya mazingira ikamilike ili ujenzi wa minara kwenye vituo hivyo uweze kuanza na suala hili limefikishwa Wizara ya Maliasili na Utalii ili liweze kukamilishwa.

  Prof. Norman Sigalla King ameyataka makampuni ya simu kuhakikisha kuwa mawasiliano yanasambaa nchi nzima. Pia ameitaka TTCL kukamilisha ujenzi wa minara yake kwa wakati na kuhakikisha kuwa kila wanapopatiwa ruzuku na Serikali wakamilishe jukumu lao kwa wakati na wafanye kazi kwa ushindani. Ameoneza kuwa Kamati yake imeridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na TTCL. Kamati inazitaka mamlaka nyingine zinazohusika na ujenzi wa minara na upatikanaji wa mawasiliano vijijini washirikiane kwa pamoja na kufanya maamuzi kwa wakati ili kuwawezesha wananchi kupata huduma za mawasiliano vijijini kwa wakati. 

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0

   


  0 0

  Mabalozi wa Nordic Foundation Tanzania, Hilary Daudi’ Zembwela’ na Najma Abdallah wakiendesha Bahati nasibu ya Afyabando ya pili ambapo washindi 10 watapatiwa kadi za bima za afya zenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu baada ya kushiriki mchezo huo kwa shilingi 500 tu. Mchezo huo umechezeshwa jijini Dar es Salaam leo Septemba 24 2017. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogspot)

  Mabalozi wa Nordic Foundation Tanzania Hilary Daudi’ Zembwela’ na Najma Abdallah wakiwa na Mkaguzi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya kubahatisha, Bakari Maggid aliyesimamia zoezi la kuendesha kampeni ya Afyabando kuwapata washindi 10 watakaokabidhiwa kadi za Bima ya afya zenye thamani ya shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya matibabu pamoja na familia. Mchezo huo umechezeshwa jijini Dar es Salaam leo Septemba 24 2017.


  Balozi wa Nordic Foundation Tanzania, Najma Abdallah akiwasiliana na Mwalimu wa Shule ya Msingi iliyopo Songwe Mkoani Mbeya, Hassan Mwamburi baada ya kuibuka mmoja wa washindi 10 katika droo ya Pili ya kampeni ya Afyabando iliyofanyika jijini humo leo. Washindi watakaokabidhiwa kadi za Bima ya afya zenye thamani ya shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya matibabu pamoja na familia.


  Balozi wa Nordic Foundation Tanzania Najma Abdallah akiwasiliana na Diana Peter Mkazi wa Morogoro baada ya kuibuka mmoja wa washindi 10 watakaokabidhiwa kadi za Bima ya afya zenye thamani ya shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya matibabu pamoja na familia, katika droo ya kwanza ya Afyabando mchezo uliochezeshwa jijini Dar es Salaam leo Septemba 24 2017

  0 0

  Rais wa Palestina “Mahmoud Abbas” amesisitiza kuwa uhuru  wa nchi yake upo karibu hauepukiki na kwamba uvamizi wa Israeli unafikia mwisho, akisema: "Aidha upatikane uhuru au haki kamili ya wote katika nchi ya Palestina ya kihistoria."
  Rais Abbas Jumatano tarehe 20/09/2017 jioni akihutubia Mkutano wa 72 wa Umoja wa Mataifa, ameongeza kusema kwamba, imepita miaka ishirini na minne tangu kusainiwa kwa Mikataba ya mpito ya Oslo, ambayo ilionesha ukomo wa uvamizi wa Israeli na kuwapa matumaini Wapalestina, ya kuanzishwa kwa Dola yao huru, huku akihoji " Tuko wapi sasa na matumaini haya?."

  Amesema:"Tumekubali uwepo wa Dola ya Israeli  kupitia mipaka ya mwaka 1967, lakini Israeli kutokubali uwepo wa Dola ya Palestina kunatupa maswali mengi. Badala ya kuzingatia sababu, inafanya juhudi kuteka misimamo ya kimataifa kwa masuala yasiyo na uzito wowote, yatokanayo na sera zake za kikoloni. Tunapoitaka na kutakiwa na jumuiya ya kimataifa kukomesha uvamizi wake, inadai ni uchochezi na kukosekana  ushiriki wa Palestina na kuwekwa kwa masharti yasiyowezekana."
  Rais Abbas ameongeza kusema kuwa,anaelea machafuko ni Utawala wa kivamizi wa Israeli katika ardhi yetu,uvamizi ambao umefikia zaidi ya nusu karne,huku zaidi ya miaka kumi sasa tumekubaliana  kuunda kamati ya pande tatu ambazo ni Marekani,Israeli na Palestina, ili kumaliza suala la uchochezi.Kamati  imefanya kazi kwa muda, lakini tumekuwa tunatoa wito wa kufufuliwa wa kamati hiyo hatupati mrejesho. Hivi ni nani anaekaribisha hilo na kufanya juhudi ya kulifanya liwepo?.
  Amesema pia,kuendelea kwa uvamizi ni aibu kwa Israeli na Jumuiya ya Kimataifa,ni wajibu wa Umoja wa Mataifa kumaliza uvamizi huo ili kuwezesha jamii ya Palestina kuishi kwa uhuru na ustawi katika ardhi yake,huku mji mkuu wake ukiwa ni Jerusalemu ya Mashariki."Kukomesha uvamizi na vitendo vyake vya kidhalimu, vitakuwa na athari kubwa mno katika kupambana na udaidi pia mashirika yake kukosa karatasi muhimu ambazo huzitumia kwa kuuza fikra zao."Tunatilia mkazo la kukaliza uvamizi ili kukamilisha juhudi zetu katika kukabiliana na mashirika hayo ya kigaidi,kwani Wapalestina wapo dhidi ya ugaidi wa ndani,kikanda na wa kimataifa.
  "Tuliwasilisha mpango wa amani wa Kiarabu  unaoitaka Israeli kuondoka katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kimabavu tangu  mwaka 1967 lakini Israeli haikujibu,kama ilivyoufanyia ule mpango ujulikanao kama “Road Map” uliowasilishwa na pande nne na kupitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,hali inayoonekana kana kwamba Israeli ipo juu ya sheria. Vilevile ukaja mpango wa amani wa Ufaransa ukifuatiwa na mkutano husika mjini Paris,lakini juhudi zote hizi zilikataliwa na kupigwa na Israeli."

  Ameongeza kusema:”Tulimuomba Waziri Mkuu wa Israeli akubali ufumbuzi wa dola mbili, kisha tukae kuzungumzia suala la mipaka akakataa,licha ya jitihada zetu kufikia amani ya kweli, lakini Israeli inaendelea kuvuruga na kuendeleza ujenzi wa makazi ya walowezi Ukingo wa Magharibi na kila mahali, hatimae hakuna tena nafasi kwa ajili ya taifa la Palestina."Vitendo viovu vya Israeli katika mji mtakatifu, vitachochea hisia za uadui wa kidini, ambao unaweza kugeuka mgogoro mkubwa wa kidini, tumeiomba serikali ya Israeli kuheshimu sheria na historia ya sehemu hizo takatifu lakini Israel tangu ilipoikalia kimabavu Jerusalemu mwaka 1976, imekuwa ikiihodhi kwa azimio la upande mmoja.

  Rais Abbas amesema kuwa, “Jerusalemu imekaliwa kimabavu na hatua zote za Israeli ni batili kama ilivyo katika ujenzi wake wa makazi ya walowezi Jerusalemu ya Mashariki na maeneo mengine ya Palestina. Ieleweke wazi kuwa,ubadilishaji wa historia ya Jerusalemu na kuuchafua Msikiti wa Aqswa ni kuchezea hatari,pia ni kushambulia majukumu ya Palestina na yale ya Jordan.Tunaitahadharisha hilo, isijaribu kusababisha vita vya kidini wakati mgogoro wetu ni wa kisiasa”.
  "Chaguo letu kama Waarabu na chaguo la dunia ni sheria za kimataifa, uhalali wa kimataifa na uwepo wa dola huru ya Palestina kwa mujibu wa mipaka ya 1967.Tutatoa ushirikiano wote katika kufanikisha hilo la kihistoria,ili tupate kuishi kwa amani pamoja na Israeli. Lakini kama ufumbuzi wa dola mbili utaharibiwa na kuimarisha dola moja yenye serikali mbili,hapatakuwa na linguine kwetu wala kwenu ila mapambano na kutaka kupata haki zetu kamili ndani ya Palestina ya kihistoria. Hivi si vitisho ila ni kutaka haki zetu kama wapalestina”.

  Tatizo letu kwa utawala wa kivamizi wa Israeli sio Uyahudi kama dini, kwani hiyo ni dini ya Mungu kama Uislamu na Ukristo.Tumebeba majukumu yetu katika Ukanda wa Gaza,ambayo haiwezekani kuwepo Palestina bila hiyo,ninafarijika leo kuona kufikiwa kwa makubaliano mjini Cairo kufuatia juhudi nzuri za Misri.Yamekomesha vitendo vya Hamas vilivyoleta mgawanyiko na hatimae kufanyika kwa uchaguzi mkuu,hatimae serikali yetu mwisho wa wiki ijayo itakwenda Ukanda wa Gaza ili kufanya kazi huko.
  "Ukimya wa jumuiya ya kimataifa juu ya vitendo dhalimu vya Israeli,ndio uliohamasisha vitendo hivyo tangu awali hadi inakiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake, uko wapi Umoja huo na maazimio yake?Vipi unatendea mataifa kwa viwango tofauti? Basi huu ni wajibu wa Umoja wa Mataifa." Aidha ameuomba kumaliza uvamizi wa Israeli ndani ya muda maalumu,kwani haiwezi tena kutoa data huru kuhusu mpango wa amani wa kiarabu,hasa kuhusiana na faili wakimbizi kwa mujibu wa azimio la Umoja wa Mataifa 194,huku akiashiria kuwa maazimio ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kupuuzwa na Israeli”.

  Rais Abbas amesisitiza haja ya kusitisha shughuli za ujenzi wa makazi ya walowezi katika maeneo ya Palestina,kwani hatuna uwezo wa kulinda raia zetu chini ya utawala wa mabavu,Umoja wa Mataifa uitake Israeli kutambua mipaka Palestina ya mwaka 1967 na kupunguza mpaka na kuomba wajumbe wote wa Umoja wa Mataifa kutangaza kwamba kutambuliwa kwao kwa msingi wa mipaka ya 1967,pia wanachama wote wa Umoja huo kutambua mipaka hiyo ili kutilia mkazo maazimio ya sheria za kimataifa.

  Amesema:"Iko wapi mipaka ya Israeli mlioitambua wakati Israeli yenyewe haijaikubali,sheria za kimataifa zinaitaka dunia kuweka hiyo mipaka". Aidha Rais ametoa wito kwa nchi zote duniani kutoshiriki katika ujenzi wa makazi ya kikoloni ulio kinyume na sheria,huku zikichukua hatua stahiki dhidi yake kama ilivyofanya jumuiya ya kimataifa dhidi ya utawala wa kibaguzi wa Afrika ya kusini na tunataka kutangaza habari mbaya za mashirika ambayo yanafanya kinyume cha sheria na makazi."

  Hivyo, amezihimiza nchi wanachama kuitambua dola ya Palestina kwa mujibu wa mipaka ya mwaka 1967,huku akitilia mkazo kuwa hatua hiyo haitoathiri mpango wa amani,hasa hasa ikiwa Wapalestina wanaitambua dola ya Israeli. Tunauhimiza Umoja wa Mataifa kuikubali Palestina kama mwanachama wake kamili,huku tukiiomba jumuiya ya kimataifa kuendelea kuisaidia kiuchumi na kifedha ili iweze kujitegemea na kujiamini.  

  Aidha Rais Abbas, ametahadharisha juhudi za kutaka kubadilisha majukumu ya shirika la misaada  UNRWA na kanuni zake,pia kufuta kipengele cha saba katika Baraza la haki za binaadamu au kuzuia kutoa orodha chafu ya mashirika yanayofanya kazi katika makazi ya walowezi wa Israeli nchini Palestina inayokaliwa kimabavu. 

  Rais Abbas amehitimisha hotuba yake kwa kutilia mkazo msimamo wa nchi yake,katika kuheshimu haki za binaadamu na kutekeleza mikataba ya Umoja wa Mataifa na ile yote iliyosaini,kwani Palestina ni sehemu ya jumuiya ya kimataifa na si vingine. Huku nchi yake pia itaandaa matakwa hayo kwa maazimio yatayokwenda sambamba na misingi husika,kisha kuyawasilisha kwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

  0 0  0 0

   Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wa Singisi kata ya Akeri nje kidogo ya jiji la Arusha kwenye njia panda ya KIA waliosimamisha msafara wake akiwa njiani kurejea Dar es salaam leo asubuhi Septemba 25, 2017 baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano mkoani Arusha.

   Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisindikizwa na wakuu wa mikoa ya Kilimanjaro, Mama Anna Mghwira na wa Arusha Mhe Mrisho Gambo akati akielekea kupanda ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)  kurejea  Dar es salaam leo asubuhi Septemba 25, 2017 baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano mkoani Arusha.
   Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa mikoa ya Kilimanjaro, Mama Anna Mghwira kabla ya  kupanda ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)  kurejea  Dar es salaam leo asubuhi Septemba 25, 2017 baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano mkoani Arusha.

   Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo kabla ya kupanda ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)  kurejea  Dar es salaam leo asubuhi Septemba 25, 2017 baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano mkoani Arusha.
   Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungiwa mikono na  Mkuu wa mikoa ya Kilimanjaro, Mama Anna Mghwira na Mkuu wa \Mkoa wa Arusha wakati ndege yake ikiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)  kurejea  Dar es salaam leo asubuhi Septemba 25, 2017 baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano mkoani Arusha.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo na Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo wakiondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)  baada ya kumsindikisza Rais Dkt John Pombe Magufuli leo asubuhi Septemba 25, 2017 baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano mkoani Arusha.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda pamoja na viongozi wengine wa Mkoa wa Dar es Salaam mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam wakati akitokea Mkoani Arusha.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam wakati akitokea Mkoani Arusha.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam wakati akitokea Mkoani Arusha. PICHA NA IKULU

  0 0

  NA BASHIR NKOROMO

  Lucas Rutainurwa ametawazwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa Jumuiya hiyo uliofanyika jana.

  Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Lugano Mwafongo, amesema katika Uchaguzi huo uliofanyika Segerea, Rutainurwa (pichani), alipata kura 278 dhidi ya Mohamed Honelo aliyepata kura 148 baada ya hao wawili kuingia katika kinyang'anyiro kwa mara ya pili kufuatia kutopatikana mshindi aliyepata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa  katika uchaguzi wa awali.

  Wakati katika awamu ya kwanza  Lutainurwa alipata kura 277 Honelo alipata kura 243 huku Celestine Nyalusi akipata kura 67.

  Nafasi ya Mjumbe wa Halimashauri Kuu aliyeshinda ni George MJtambalike ambaye amepata kura 195 dhidi ya Edward Haule aliyepata kura 181. PICHA ZA UCHAGUZI HUO/>BOFYA HAPA


  0 0

  Na Benedict Liwenga-WHUSM.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amelipongeza Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kuhifadhi vema kumbukumbu za Mashujaa wa Tanzania waliopigana vita na kusaidia ukombozi katika baadhi ya nchi za jirani ikiwemo nchi ya Msumbiji.

  Pongezi hizo amezitoa leo Mkoani Mtwara wakati alipotembelea maeneo ya kumbukumbu ya Kitaifa ambapo kwa Mkoani hapo ametembelea eneo la Mashujaa lililopo Nailendele lengo likiwa ni kujionea maeneo yaliyoweza kuhifadhiwa kumbukumbu zake za ukumbozi wa Bara la Afrika ikiwemo mahitaji ya ziada ya maeneo hayo.

  Mhe. Mwakyembe amesema kwamba, kazi kubwa inayofanyika katika kuyatembelea maeneo hayo ni kujua kumbukumbu za maeneo hayo ikiwemo kuongea na mashuhuda wa matukio ya kumbukumu za maeneo husika kwa ajili ya kuandika historia ya Afrika kwa ushahidi uliotafutwa na Waafrika wenyewe.

  “Tunakipinid kifupi kuhakikisha kuwa kumbukumbu zote tuizonazo tunazihifadhi, tunaandika historia yetu sisi wenyewe Waafrika badala ya kuandikiwa na Waliotutawala huko nyuma kwa ushahidi tulioutafuta wenyewe”, alisema Dkt. Mwakyembe.

  Ameongeza kuwa JWTZ imefanya kazi kubwa ya kuhifadhi baadhi ya maeneo ya kumbukumbu za kitaifa, jambo ambalo litarahisisha utunzaji wa kumbukumbu hizo kwa ajili ya Mradi wa Ukumbozi wa Bara la Afrika.

  “Tumeanza kukubaliana wote katika SADC na katika nchi za Afrika, ni lazima tuingize katika mitaala ya shule zetu hizi harakati za ukombozi wa Bara la Afrika ili vizazi vijavyo viweze kufahamu mambo haya hususani tulikotoka na tunakoelekea”, alisema Dkt. Mwakyembe.

  Aidha, katika ziara hiyo Mhe. Mwakyembe alipata wasaa wa kuongea na Uongozi wa Mkoa wa Mtwara ambapo ameupongeza kwa uongozi huo kwa kuja na Mpango wa Usajili wa Vizazi vya Watoto waliopo chini ya Umri wa Miaka Mitano ambapo Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kesho Wilayani Tandahimba.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia baadhi ya picha za Mashujaa wa Ukombozi waliopigana Vita nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akionyeshwa ramani iliyotumika wakati wa Ukombozi nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiangalia bango linaloelezea kumbukumbu za Mashujaa wa Ukombozi waliopigana Vita nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia mchanga wa makaburi yaliyofukuliwa ya Mashujaa wa Ukombozi waliopigana Vita nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia moja ya silaha za kivita iliyotumiwa na Mashujaa wa Tanzania wakati wa Vita vya Ukombozi nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)

older | 1 | .... | 1377 | 1378 | (Page 1379) | 1380 | 1381 | .... | 1897 | newer