Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

SERIKALI YA BRAZIL IMETANGAZA RASMI KUFUNGUA MILANGO YA USHIRIKIANO WA KIFEDHA NA BIASHARA NA TANZANIA

$
0
0

Serikali ya Brazil imesamehe Tanzania deni la jumla ya Dolaza Marekani milioni 203 ambazo ni sawa na shilingi za Kitanzania zaidi ya Bilioni 445. Deni hilo lilitokana na mkopo uliotolewa kwaajili ya ujenzi wa barabara ya Morogoro-Dodoma mwaka 1979 pamoja Riba.

Balozi wa Tanzania Nchini Brazil Dkt. Emmanuel Nchimbi alisaini mkataba huo kwaniaba ya Tanzania huku Wakili wa Hazina ya Taifa Dkt. Sonia Portella Nunes akisaini kwa niaba ya Serikali ya Brazil.

Balozi Nchimbi alishukuru Serikali ya Brazil kwa Msamaha huo ambao alisema umeunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Pombe Magufuli kujenga uchumi imara wa Tanzania.

Balozi Nchimbi pia aliihakikishia Serikali ya Brazil utayari wa Tanzania katika kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uchumi na Brazil.

Kiongozi wa ujumbe wa Brazil kwenye sherehe hiyo Bw. Guilheme Laux, Undersecretary of Credit and Guarantee kutoka Wizara ya Fedha ya Brazil alimtamka rasmi kufunguliwa kwa milango ya ushirikiano wa kifedha na kibiashara iliyokuwa imefungwa kutokana na Deni hilo lililofanya Tanzania kuwa moja ya nchi zenye madeni sugu ya Brazil.

Hivyo kutoka sasa Makampuni ya Brazil yanaruhusiwa kukopa katika Benki za Brazil kwa ajili ya kutekeleza miradi nchini Tanzania lakini pia Serikali ya Tanzania inaruhusiwa kuanzisha majadiliano ya miradi mipya ya maendeleo.


Balozi Dkt. Emmanuel J. Nchimbi akisaini Mkataba kwa niaba ya Serikali ya Jamnhuri ya Muungano wa Tanzania wa Msamaha wa Deni la Tanzania kwa Serikali ya Brazil .Kwa upande wa Brazil mkataba huo ulisainiwa na Dkt. Sonia Nunes, Wakili wa Serikali ya Brazil. 
Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akibadilishana mkabataba huo na Dkt. Sonia Nunes, Wakili wa Serikali ya Brazil mara baada ya kusaini mkataba wa msamaha wa deni.
BaloziDkt. Emmanuel Nchimbi akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo na Serikali ya Brazil. 
Balozi Dkt. Emmanuel J.Nchimbi pamoja na Mkuu wa Ujumbe wa Serikali ya Brazil Bw.Guilheme Laux (kulia kwa Balozi Nchimbi) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wapande zote mbili (Tanzania na Brazil)
1. Balozi Dkt. Nchimbi akiendelea na mazungumzo na ujumbe wa Serikali ya Brazil (Hawapo pichani)./

MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU MAHUSUSI WA KOROSHO TANZANIA

$
0
0
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akifungua mkutano wa wadau mahususi wa korosho katika hotel ya Tanga Beach mjini Tanga unaolenga kutoa muongozo wa ununuzi wa korosho ghafi kwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza 0ctober 01, 2017 ambapo mkutano huo ulihusisha wakuu wa mikoa inayolima zao la Korosho,wilaya na Halmashauri.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Dkt Charles Tizeba akizungumza katika mkutano huo unaolenga kutoa muongozo wa ununuzi wa korosho ghafi kwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza Octoba 1 mwaka huu. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Hassani Jarufu akizungumza wakati wa mkutano huo unaolenga kutoa muongozo wa ununuzi wa korosho ghafi kwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza 0ctober 01, 2017 ambapo mkutano huo ulihusisha wakuu wa mikoa inayolima zao la Korosho,wilaya na Halmashauri .
Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania,Mama Anna Abdallah akizungumza wakati wa mkutano huo unaolenga kutoa muongozo wa ununuzi wa korosho ghafi kwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza 0ctober 01, 2017 ambapo mkutano huo ulihusisha wakuu wa mikoa inayolima zao la Korosho,wilaya na Halmashauri .
Wasjhiriki wa mkutano huo wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo 
Wadau wakifuatilia makrabasha mbalimbali kwenye mkutano huo
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,Alhaj Majid Mwanga kushoto akifurahia jambo wakati wa mkutano huo
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete kulia akiteta jambo na baadhi wa washiriki wa mkutano huo leo uliofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort mjini Tanga.
Mbunge wa Jimbo la Mtama (CCM) Nape Mnauye akiteta jambo kabla ya kuanza kikao hicho
Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini (CCM) Hawa Ghasia akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Mlalo (CCM) Rashidi Shangazi wakati wa kikao hicho mapema leo ambao ulifunguliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa 
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Steven Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akisalimia na Mbunge wa Jimbo la Chalinze (CCM) Ridhiwani Kikwete wakati wa kikao hicho
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto ,Ummy Mwalimu akisaliana na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku kabla ya kuanza mkutano huo


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira na Muungano Januari Makamba akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Chalinze (CCM) Ridhiwani Kikwete

Sehemu wa washiriki wa mkutano huo wakifuatilia matukio mbalimbali
Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso akifuatilia kwa umakini mkutano huo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa umakini 
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,Mathew Mtigumu katikati akimsikiliza kwa umakini Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi wakati wa kikao hicho kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano Mazingira,Januari Makamba

Baadhi ya washiriki wakiendena na mkutano 








Sehemu ya washirki wakifuatilia mkutano huo leo






Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa katika akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo leo

Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

MARUFUKU VIONGOZI WA SERIKALI KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA KOROSHO-MAJALIWA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Viongozi wa Serikali wasiokuwa na mashamba ya mikorosho kutojihusisha na biashara ya uuzaji wa zao hilo.

“Kama huna shamba, huwezi kuwa na korosho, unauza umepata wapi. Jukumu lenu ni kufuatilia, kukemea na kuchukua hatua stahiki penye udhaifu na si vinginevyo.”

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Septemba 17, 2017), wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa korosho uliofanyika mkoani Tanga.
Amesema kama viongozi hao wanahitaji kuuza korosho watumie muda huu ambao Serikali inahamasisha watu wafungue mashamba mapya nao watumie fursa hiyo na kulima.

Amesema ni vema kila mdau akahahakikisha anatimiza wajibu wake ipasavyo kama ni mkulima alime kwa kuzingatia stadi za kilimo na mnunuzi azingatie taratibu zilizopo.Waziri Mkuu amesema Bodi ya Korosho inatakiwa kuhakikisha inaimarisha zao hilo na kuishauri vizuri Serikali kuhusu namna bora ya kuliendeleza.

Amesema Serikali inaamini kuwa iwapo kila mdau wa zao la korosho atatimiza wajibu wake kikamilifu katika kuliendeleza zao hilo kila upande utanufaika kikamilifu.Hivyo, ni vizuri kila mdau ajitathmini kama anatimiza wajibu wake kikamilifu, huku akiwaagizaviongozi wa Ushirika waendeshe Ushirika kwa uadilifu mkubwa.

Waziri Mkuu amesema Serikali haitakuwa tayari kusikia mkulima yeyote akilalamika kuhusu malipo iwe kwa kupunjwa, kuchelewa ama kutolipwa.
Amesema katika msimu huu wa biashara ya korosho Serikali haitarajii kusikia mambo ambayo yalikwaza ufanisi katika misimu iliyopita kama wakulima kukatwa unyaufu kwa namna yoyote.

“Sheria ya unyaufu ni miezi sita kutoka korosho inapoanza kuvunwa hadi kuuzwa na korosho haifiki miezi sita, hivyo wakulima hawahusiki unyaufu kwa namna yoyote ile na tusisikie tena.”Amesema hali hiyo ikitokea hawatasita kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika. “Nawaagiza viongozi wa ngazi zote kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa jambo hili.”

Pia amepiga marufuku Bodi ya Maghala kutoza ushuru wa kuhifadhi mazao kwani hilo si jukumu lao bali ni la mpangaji wa ghala na wao washughulikie utoaji wa leseni tu.Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa maghala ya kuhifadhia korosho kutowazuia Viongozi wa Serikali kuyakagua kabla na wakati wa biashara.

Amesema viongozi hao wanatakiwa wasizuiwe kuyakagua maghala hayo hata baada ya minada ili kujiridhisha na mwenendo sahihi wa uhifadhi wa mazao.Pia ameagiza kukamatwa na kutaifishwa kwa korosho zote zitakazonunuliwa kwa njia ya kangomba. Korosho zitaendelea kuuzwa kupitia mfumo wa stakabadhi gharani.

Awali, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage amesema korosho ya Tanzania inaongoza kwa ubora duniani, hivyo wazalishaji wahakikisha sifa na ubora wa zao hilo katika soko la dunia haushuki.Amesema Serikali inaendelea kuwakaribisha wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza katika viwanda vya kubangulia korosho ili kuiongezea thamani kabla ya kuisafirisha nje ya nchi.

Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Mwijage, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Bw. January Makamba.

Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Bi. Anna Abdallah, Wakurugenzi wa Bodi ya Korosho, Wakuu wa mikoa na wilaya zinayolima korosho, Wabunge wanaotoka katika mikoa inayolima korosho, wanunuzi, wasafirishaji na wenye viwanda vya ubanguaji.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMAPILI, SEPTEMBA 17, 2017. 

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akifungua mkutano wa wadau mahususi wa korosho katika hotel ya Tanga Beach mjini Tanga unaolenga kutoa muongozo wa ununuzi wa korosho ghafi kwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza 0ctober 01, 2017 ambapo mkutano huo ulihusisha wakuu wa mikoa inayolima zao la Korosho,wilaya na Halmashauri.

DEATH ANNOUNCEMENT: MUGANYIZI MUTTA

$
0
0
We are devastated to inform our clients, partners and stakeholders of the death of our very own, Muganyizi Mutta, who was our Public Relations Director. 

Mutta passed away on Saturday afternoon, September 16, 2017 at Mwananyamala Hospital in Dar es Salaam after a sudden illness. We have not only lost a member of Aggrey & Clifford family, but also a friend. Always in suits, Mutta was gregarious, charismatic and a hard worker with a big heart. Mutta joined Aggrey & Clifford, Tanzania in January 2016 until his sudden passing. 

We will always remember and treasure the time that we have had the pleasure of knowing and working with him. May his soul rest in eternal peace.

CUTHBERT MIDALA AFUNGA NDOA NA CATHERINE, JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Hayawi hayawi mwisho huwa. Ofisa wa Makao Makuu ya CCM, Cuthbert Midala na Mkewe Catherine, wakionyesha pete zao vidoleni, baada ya kufunga ndoa mubashara, katika Kanisa la ECWC, Kimara kwa Msuguri, Dar es Salaam, jana, Jumamosi Septemba 16, 2017. Baadaye walihitimsha kwa mnuso mkali uliokutanisha Wazazi, Ndugu, Marafiki na Jamaa, katika Ukumbi wa Msasani Beach Club, pia Dar es Salaam. Zifuatazo ni picha kem kem za tukio hilo, tafadhali, endelea...

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 18, 2017

KAMISHNA MKUU TRA AFANYA ZIARA YA KIKAZI TBL

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group, Roberto Jarrin (kulia) akimkaribisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere wakati alipoongoza ujumbe wa Maofisa Waandamizi wa taasisi hiyo katika ziara ya kikazi katika kiwanda cha Bia cha Tanzania Breweries Limited, kilichopo Ilala jijini Dar e Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group, Roberto Jarrin (aliyesimama) akielezea ujumbe wa Kamishna Mkuu wa TRA utendaji kazi wa kampuni hiyo. Meneja wa Afya na Usalama sehemuya kazi wa TBL Group, Renatus Nyanda (kushoto) akimweleza Kamishna Mkuu wa TRA (Kulia) na ujumbe wake utekelezaji wa kanuni za usalama wa kampuni kabla ya kuanza ziara ya kutembelea kiwanda ,wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL,Roberto Jarrin. Kamishna Mkuu wa TRA na ujumbe wake wakipata maelezo ya mchakato wa kutengeneza bia kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha TBL cha Ilala-Calvin Martin. Mtaalam wa kuonja bia wa TBLGroup, Rebecca Semoka, (kushoto) akimweleza Kamishna Mkuu wa TRA na ujumbe wake mchakato wa kuonja ubora wa radha ya bia kabla ya kuingia kwenye masoko. Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group,Roberto Jarrin ( wa nne kulia) na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya MapatoTanzania (TRA) Charles Kichere ( wa tatu kushoto ) wakiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Waandamizi wa TBL na TRA wakazi wa ziara ya kikazi ya watendaji wa TRA katika kiwanda hicho.

ANSAF YATOA DIRA YA KUTATUA CHANGAMOTO ZA KILIMO

$
0
0
Mkuu wa idara ya miradi ya ANSAF, Edna Lugano akizungumza wakati wa mkutano na Wadau wa kilimo na wakulima wa mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma wamenufaika utafiti uliofanywa na ANSAF kwa kushirikia na Alliance for Green Revolution of Africa (AGRA) ambao una lengo la kutatua changamoto za wakulima wadogo wadogo kufikia kuwa wakulima wa kati ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi na kuelewa vigezo vinavyochangia katika upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima. 
Baadhi ya washiriki walioshiriki mkutano wa kutambulisha utafiti uliofanywa na ANSAF kwa kushirikia na Alliance for Green Revolution of Africa (AGRA) uliokuwa na lengo la Kutambua na kuelewa vigezo vinavyochangia katika upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima.



Na Fredy Mgunda,Iringa.

Wadau wa kilimo na wakulima wa mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma wamenufaika utafiti uliofanywa na ANSAF kwa kushirikia na Alliance for Green Revolution of Africa (AGRA) uliokuwa na lengo la Kutambua na kuelewa vigezo vinavyochangia katika upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima wadogo na kutathimini mfumo wa kikanuni/ kisheria wa udhibiti wa pembejeo.

Akizungumza wakati wa mkutano huo mkuu wa idara ya miradi ya ANSAF, Edna Lugano alisema kuwa waliamua kufanya utafiti kwa lengo la kumkomboa mkuliwa mdogo kuondokana na changamoto zinazomrudisha nyuma kimaendeleo.

“tunatekeleza mradi wa miaka miwili unaolenga uimarishaji utekelezaji wa sera wezeshi za kilimo na uratibu unawezesha upatikanaji wa pembejeo (mbegu, mbolea na viuatilifu) kudhibiti soko na kuhamasisha upatikanaji wake kwa wakulima wadogo” alisema Lugano.

Lugano alisema kuwa utafiti ulilenga kutazama mahitaji ya pembejeo na kiwango cha usambazaji kwa kutazama aina chache za mazao, Ufanisi wa mfumo wa kudhibiti ubora wa pembejeo za kilimo na jitihada zinazofanywa na serikali pamoja na wadau wengine katika kudhibiti biashara ya pembejeo zisizo na ubora.

“Kumekuwa na malalamiko mengi yanayohusu uwepo wa mbegu na mbolea zisizo na ubora zinazowasababishia hasara kubwa wakulima wadogo wadogo ili kutatua changamoto hizo tumekuja na huu utafiti unaoweka mambo mengi wazi na jinsi gani ya kutatua kero hizo” alisema Lugano.

Aidha Lugano alisema kuwa utafiti huo umefanywa kwenye mikoa 10 ilichaguliwa kutoka katika kanda za kilimo na kuzingatia minyororo ya thamani pamoja wilaya mbili kila mkoa zilichaguliwa kwa kuzingatia umbali kutoka makao makuu ya mkoa ili kuwezesha kulinganisha uhusiano wa umbali na upatikanaji wa pembejeo.

“Mikoa ambayo tumefanya utafiti ni pamoja Ruvuma, Kagera, Mbeya, Morogoro, Manyara, Rukwa, Iringa, Shinyanga na Simiyu hii ndio tuliona sahihi kufanyia utafiti kwakuwa ipo katika kanda za kilimo na kuzingatia minyororo ya thamani” alisema Lugano

Lugano alisema kuwa upatikanaji wa mbegu bora kimekuwa kikwazo moja wapo kwa wakulima wadogo wadogo hasa wale ambao hawana elimu ya kilimo na kusababisha hasa kwa wakulima na wengine kukata tamaa ya kilimo.

“Mahitaji ya mbegu kwa mwaka nchini inakadiriwa kuwa tani 120,000. Kati ya hizo, 25% (tani 30,000) huzalishwa na sekta rasmi, kiasi kinachosalia huagizwa kutoka nje ya nchi na makapuni za kibiashara” alisema Lugano

Lugano alisema kuwa makisilio ya mahitaji na upatikanaji ya viuatilifu kwa mwaka ni changamoto kutokana na kuwa usambazaji hivyo hutegemea mahitaji mahsusi kwa eneo maalum lenye uhitaji kwa wakati maalum

“Mahitaji ya viatilifu huongozwa na Mfumo wa ‘Integrated Pesticides Management (IPM)’ Sera ya taifa ya kilimo (2013) inahimiza menejiment sahihi ya viuatilifu ambao unazingatia kanuni za kilimo bora zinazozingatia usalama na uhifadhi wa mazingira takriban viuatilifu vyote vinavyotumika nchini huagizwa kutoka nje ya nchi” alisema Lugano

Naye afisa kilimo wa manispaa ya Iringa Gerlad Mwamila aliupongeza utafiti uliofanywa na jukwa la kilimo la ANSAF kwa kazi kubwa waliyofanya kwa kuweza kuyafumbua maeneo yenye changamoto na jinsi gani ya kuzitatua kwa kutuwekea wazi mapendekezo yake.

"ukiangalia utafiti huu umewakusa sana wakulima na unamanufa kwa wakulima hivyo sisi viongozi ambao tupo serikalini tunapaswa kufikisha elimu hii kwa viongozi wetu wa juu pamoja na wakulima ili kukuza kilimo cha wakulima wadogo" alisema Mwamila

Mwamila alisema kuwa serikali inatakiwa kujipanga kufanikisha zoezi la upimaji ardhi ili kuwasaidia wakulima wadogo kulima kwa uhakika na sio kulima kwa kubahatisha kama ambavyo saizi wanavyolima.

"kwa kweli halmashauri zetu hazina pesa za kutosha kufanikisha zoezi la upimaji ardhi kwa wakulima wote,lakini kama halmashuri zikifanya kazi sambamba na taasisi binafsi tunaweza kufanikisha lengo la kumkomboa mkulima mdogo" alisema Mwamila

Kwa upande wake afisa kilimo wa halmashuri yawilaya ya Iringa Merry Mushi alisema kumekuwa na changamoto kwa wakulima kuuziwa pembejeo ambazo hazina ubora hivyo halmashauri imejipanga kutatua tatizo hilo.

"mara kwa mara tumekuwa tutoa elimu kwa wakulima juu ya kutumia pembejeo zisizo na ubora hivyo wakulima wameanza kuelewa na kufikisha malalamiko yake kwenye ofisi za kilimo za wilaya hiyo ni hatua kubwa sana kwetu"alisema Mushi

Mwakilishi na Mbunge wa Jimbo la Tunguu Wakabidhi Fedha Kwa Vikundi 13 Vya Ushirika Shehia za Unguja Ukuu

$
0
0
Mwakilishi wa Jimbo Tunguu Zanzibar Mhe, Simai Mohammed Said akizungumza na wananchi wa Jimbo lake katika Tawi la CCM Unguja Ukuu Kae Pwani Wilaya ya Kati Unguja wakati wa hafla ya kukabidhi fedha Vikundi 13 vya Ushirika vya Wananchi wa Kae Pwani Unguja. Mchango huo umetolewa na Mbunge na Mqwakilishi kuchangia vikundi hivyo kwa ajili ya kutunisha mifuko ya vikundi vya vinavyojishughulisha na ujasiriamali wa kutengeneza bidhaa na kilimo na kukupeshana, hafla hiyo imefanyika katika Tawi la CCM Ungua Ukuu Kae Pwani.

Vikundi vilivyokabidhiwa fedha hizo ni Tushikamane,Hatutaki Shari, Nia Njema,Aso Mtu Ana Mungu,Siri Moyoni, Tuwe Nao,Pita na Zako,Hatutaki Kero,Hapa Kazi Tu, Mkorofi Sio Mwezetu,Hawavumi, Imani Moja na Wajibu Wetu.
Baadhi wa Viongozi wa Vikundi vya Ushirika katika Shehia za Kae Pwani Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja wakati wa hafla hiyo. 
Sheha wa Shehia ya Kae Pwani Ndg. Khamis Ibrahim akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi fedha kwa Vikundi vya Ushirika vua Shehia hiyo zilizotolewa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo la Tunguu Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika Tawi la CCM Unguja Ukuu Kae Pwani.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohamrd Said akimkabidhi fedha Mwenyekiti wa Kikundi cha Tushikamano wakati wa hafla hizo kukabidhi fedha hizo zilizotolewa na Mbunge na Mwakilishi kutunisha Mfuko wa Kikundi Chao.. 
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohamrd Said akimkabidhi fedha Mwenyekiti wa Kikundi cha Aso Mtu Ana Mungu, wakati wa hafla hizo kukabidhi fedha hizo zilizotolewa na Mbunge na Mwakilishi kutunisha Mfuko wa Kikundi Chao.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohamrd Said akimkabidhi fedha Mwenyekiti wa Kikundi cha Tuwe Nao,wakati wa hafla hizo kukabidhi fedha hizo zilizotolewa na Mbunge na Mwakilishi kutunisha Mfuko wa Kikundi Chao.
Baadhi ya Viongozi wa Vikundi vya Ushirika wakifuatilia hafla hiyo. ya kukabidhiwa fedha kutunisha mfuko wa vikundi vya jumla ya vikundi 13 vimekabidhiwa fedha taslim zilizotolewa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo lao la Tunguu Zanzibar. Vikundi vilivyokabidhiwa fedha hizo ni Tushikamane,Hatutaki Shari, Nia Njema,Aso Mtu Ana Mungu,Siri Moyoni, Tuwe Nao,Pita na Zako,Hatutaki Kero,Hapa Kazi Tu, Mkorofi Sio Mwezetu,Hawavumi, Imani Moja na Wajibu Wetu.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Wilaya ya Kati Unguja Mkoa wa Kusini Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza baada ya kukabidhi fedha kwa Vikundi vya Ushirika vya Kae Pwani Unguja Ukuu Unguja fedha hizo zimetolewa kwa pomoja yeye na Mbunge wake kwa ajili ya Wananchi wa Jimbo lao kukuza Mtaji wa Vikundi vyao vya ushiriki vinavyojishughulisha na kilimo cha mboga mbogo, kuweka na kukopa na vikundi vya Ujasiriamali, hafla hiyo imefanyika katika Tawi la CCM uNGUJA Ukuu Kae Pwani.
Baadhi ya Viongozi wa Vikundi vya Ushirika wakifuatilia hafla hiyo. ya kukabidhiwa fedha kutunisha mfuko wa vikundi vya jumla ya vikundi 13 vimekabidhiwa fedha taslim zilizotolewa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo lao la Tunguu Zanzibar. Vikundi vilivyokabidhiwa fedha hizo ni Tushikamane,Hatutaki Shari, Nia Njema,Aso Mtu Ana Mungu,Siri Moyoni, Tuwe Nao,Pita na Zako,Hatutaki Kero,Hapa Kazi Tu, Mkorofi Sio Mwezetu,Hawavumi, Imani Moja na Wajibu Wetu.
Mwenyekiti wa Tawi la CCM Kae Pwani Ndg.Ali Muhidini akizungumza na kutoa nasaha zake kwa Wananchi wa Vikundi vya Ushiriki kushikamano na kuvikuza vikundi vya katika kujiletea maendeleo ya kipato kupitia katika vikundi vyao.
Katibu wa CCM Tawi la CCM Kae Pwani Ndg. Daruweshi Ali akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi fedha Vikundi 13 vya Ushirika katika Shehia ya Kae Pwani.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe. Simai Mohammed Said akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa CCM Tawi la Kae Pwani na Viongozi wa Vikundi vya Ushirika vya Shehia hizo mbili za Kae Pwani.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe. Simai Mohammed Said akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa CCM Tawi la Kae Pwani na Viongozi wa Vikundi vya Ushirika vya Shehia hizo mbili za Kae Pwani
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe. Simai Mohammed Said akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa CCM Tawi la Kae Pwani na Viongozi wa Vikundi vya Ushirika vya Shehia hizo mbili za Kae Pwani
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akimsalimia Mtoto Mulhat Ai Ramadhani wakati alipofanya ziara kutembelea Wananchi wa Jimbo lake la Tunguu na kukabidhi fedha kwa vikundi 13 ili kutunisha mfuko wa vikundi vyao, katika shehia ya Kae Pwani Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja.

Benki ya CRDB yaendeleza juhudi zake za kutoa huduma bora kwa wateja, kwa kuendelea kuwajengea uwezo zaidi mawakala wake

$
0
0
Mawakala wa Benki ya CRDB maarufu kama Fahari Huduma Wakala mjini Songea, wakifuatilia kwa makini mafunzo ya uborosheji wa huduma kwa wateja yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB. Pichani Ofisa wa benki hiyo, Willy Kamwela, akifafanua jambo kuhusu mafunzo hayo.
Mawakala wa benki ya CRDB maarufu kama Fahari Huduma Wakala mjini Songea, wakiwa katika mafunzo ya uborosheji wa huduma kwa wateja yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB.

Ofisa wa Benki ya CRDB, Tom Mwaisenye, akitoa mafunzo kwa Fahari Huduma Wakala-Mjini Songea kuhusu namna bora ya uendeshaji na usimamizi wa biashara ya Uwakala wa Benki ya CRDB.

Ofisa wa Benki ya CRDB, Hemed Kiluvia, akitoa mafunzo kwa Mawakala wa Fahari Huduma mjini Songea kuhusu namna bora ya kuzingatia taratibu za Uwakala.
Mawakala wakiwa katika majadiliano na maofisa wa Benki ya CRDB.
Mawakala wa benki ya CRDB maarufu kama Fahari Huduma Wakala mjini Songea, wakiwa katika mafunzo ya uborosheji wa huduma kwa wateja yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB.
Meneja wa Benki ya CRDB, tawi la Mbinga, Bi. Efronsina Mwanja akifungua semina ya kuwajengea uwezo Mawakala wa Benki ya CRDB katika kutoa Huduma kwa Wateja.
Ofisa wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela, akitoa mfunzo kwa Mawakala wa Benki hiyo kuhusu uboreshaji Huduma kwa Wateja iliyofanyika wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.
Baadhi ya Mawakala wa Benki ya CRDB wilayani Mbinga wakimsikiliza Ofisa wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela (hayupo pichani), wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kutoa huduma bora kwa wateja.
Mawakala wa Benki ya CRDB, Mjini Mbinga wakifuatilia mafunzo ya kuboresha Huduma kwa Wateja.
Baadhi ya Mawakala wa Benki ya CRDB wilayani Mbinga wakimsikiliza Ofisa wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela, wakati wa mafunzo ya Uborosheji wa Huduma kwa Wateja yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB.
Meneja wa Benki ya CRDB, tawi la Mbinga, Bi. Efronsina Mwanja na maofisa wengine wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja na Mawakala wa Benki ya CRDB mjini Songea baada ya kuhitimisha mafunzo ya siku moja.
Mawakala wa mjini Songea wakiwa katika picha ya pamoja naa maofisa wa Benki ya CRDB.

DKT KIGWANGALLA KUFUNGUA KONGAMANO LA CCCB

$
0
0

Mratibu wa Kongamano la CCCB,Shabani Yusuph (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu
ufunguzi wa kongamano hilo litakalo fanyika Septemba 19-20 mwaka huu katika hoteli ya Ramada Mbezi Beach jijini Dar es Salaam,a,ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Hamis Kigwangalla.kushoto ni Mkufunzi wa Vijana,Hamza Jabir
Mkufunzi wa Vijana,Hamza Jabir akifafanua jambo kwenye mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.

PROF. MBARAWA MAWASILIANO YA SIMU YAPATIKANE WAKATI WOTE

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto), akikagua jenereta linalowezesha mnara wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), katika eneo la eneo la Gairo Hill,wilayani Gairo, Mkoani Morogoro. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bibi. Siriel Mchembe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bibi. Siriel Mchembe, kabla ya kuzungumza na wananchi wa kata ya Leshata, wilayani Gairo, Mkoani Morogoro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto), akimsikiliza Mtendaji mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF), Mhandisi Peter Ulanga (kulia) alipokagua minara ya simu wilayani Gairo, Mkoani Morogoro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto), akitoa maelekezo kwa Wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania mara baada ya kufungua mnara wao katika kijiji cha Chakwale wilayani Gairo, Mkoani Morogoro.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameyataka makampuni ya simu nchini kuhakikisha mawasiliano ya simu yanapatikana wakati wote katika ubora unaotakiwa ili kuwawezesha wananchi kupata huduma inayowiana na thamani ya fedha wanayolipa.

Akikagua na kuzindua minara ya simu ya kampuni za TTCL, VODACOM, HALOTEL, na TIGO katika Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro, Profesa Mbarawa amesema Serikali itaendelea kushirikiana na kampuni za simu kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF ili katika kipindi cha miaka mitatu ijayo sehemu zote za Tanzania ziwe zimefikiwa na huduma ya mawasiliano ya simu ya uhakika.

“Tumieni mawasiliano ya simu kufanya biashara, kuboresha huduma za jamii kama elimu na habari ili kukuza ustawi wa maisha yenu”, amesema Profesa Mbarawa.Waziri Prof. Mbarawa amewaonya wananchi kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao ya simu kwani ipo sheria kali inayodhibiti matumizi mabaya ya simu.

Amezungumzia umuhimu wa kampuni za simu kujenga minara katika maeneo mapya na kukarabati minara ya zamani ili kuwezesha mawasiliano kuwa katika ubora maeneo yote ya nchi.Amewataka wakazi wa vijiji vya Letugunya, Leshata na Chakwale kutumia fursa ya upatikanaji wa mawasiliano kuongeza uzalishaji wa mazao na kuyauza kwa bei nzuri na hivyo kukuza uchumi wao.

Kwa upande wake Mtendaji mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote Mhandisi Peter Ulanga amemhakikishia Waziri Profesa Mbarawa kuwa mfuko huo umejipanga kukamilisha miradi yote kwa wakati na kufanya uhakiki wa takwimu za mawasiliano nchi nzima ili kubaini maeneo ambayo yana changamoto kubwa ya mawasiliano na kuyatatua.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo Siriel Mchembe amemshukuru Waziri Mbarawa kwa kuboresha huduma za mawasiliano katika Wilaya hiyo na kumhakikishia wananchi watailinda miundombinu hiyo ili idumu kwa muda mrefu.

SERIKALI YALITAKA GAZETI LA MWANAHALISI KUJIELEZA KWA KUDAIWA KUKIUKA MAADILI YA UANDISHI WA HABARI

KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM ZANZIBAR YAKUTANA LEO

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa  Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja
Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakiwa katika kikao cha siku moja cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo katika Ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani)
 Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakifuatilia kwa makini taarifa zilizotolewa katika kikao hicho kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Juma Abdalla Juma (Mabodi) wakiimba wimbo wa Chama mara walipoingia katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja katika  kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo,
  Baadhi ya wajumbe kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakiimba wimbo wa Chama kumkaribisha  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika kikao cha Siku moja  kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja, [Picha na Ikulu.] 18/09/2017.
  Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakifuatilia kwa makini taarifa zilizotolewa katika kikao hicho kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Juma Abdalla Juma (Mabodi) alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) kuzungumza na Wajumbe wa kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 18/09/2017.

UJERUMANI YAISAIDIA TANZANIA BILIONI 521 KUIMARISHA SEKTA MBALIMBALI ZA KIUCHUMI NA KIJAMII

$
0
0
 Wajumbe kutoka Ujerumani waliohudhuria Mkutano wa Mashauriano ya Maendeleo kati ya Tanzania na nchi hiyo wakisikiliza kwa makini maelezo ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (hayupo pichani) akieleza mafanikio ya msaada wa nchi hiyo katika Nyanja za Afya, Maji, Nishati na Utawala wa Fedha, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Maafisa waandamizi kutoka Tanzania wakifuatilia kwa makini Mkutano wa Mashauriano ya Kimaendeleo kati ya Tanzania na Ujerumani yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Dkt. Detlef Wachter (wa pili kushoto) akizungumza kuhusu nia ya nchi yake kuisaidia Tanzania katika miradi ya Nishati, Maji, Utawala wa Fedha na Afya kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kuanzia mwaka 2018, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto) na Naibu Mkuu wa Ushirikiano wa kiuchumi Kanda ya Afrika Mashariki kutoka Ujerumani Bw. Georg Rademacher wakibadilishana kumbukumbu za Mkutano wa Mashauriano baada ya kusainiwa katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (wa nne kushoto) na Naibu Mkuu wa Ushirikiano wa kiuchumi Kanda ya Afrika Mashariki kutoka Ujerumani Bw. Georg Rademacher (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa waandamizi kutoka Ujerumani na Tanzania baada ya kusainiwa kwa kumbukumbu za Mkutano wa Mashauriano, katika ofisi za  Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

 Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mamelta Mutagwaba akipeana mkono na Naibu Mkuu wa Ushirikiano wa Kiuchumi Kanda ya Afrika Mashariki kutoka Ujerumani Bw. Georg Rademacher (kushoto) baada ya kusainiwa kumbukumbu za Mkutano wa Mashauriano ya Maendeleo kati ya nchi hizo mbili Jijini Dares Salaam.
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mamelta Mutagwaba akisalimiana na Wajumbe wa Mkutano wa Mashauriano ya Maendeleo kati ya Tanzania na Ujerumani, katika viunga vya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).

Ujerumani imeipatia Tanzania kiasi cha Euro milioni 198.5 sawa na Sh. Bilioni 520.86 zilizotumika kufadhili miradi mbalimbali ikiwemo ya Maliasili na Mazingira, Afya, Maji, Nishati, Udhibiti wa Fedha za Umma (Good Financial Governance) na Kusaidia Huduma za Wakimbizi katika mkoa wa Kigoma, katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban wakati wa tukio la Tanzania na Ujerumani kusaini kumbukumbu za Mkutano wa Mashauriano ya Kimaendeleo (Bilateral Development Consultations) ambapo Ujerumani imeonesha nia ya kuendelea kuisaidia Tanzania katika Sekta hizo kuanzia mwaka 2018 hadi 2021.

Kumbukumbu za Mashauriano hayo zimesainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Naibu Mkuu wa Idara ya Kanda ya Afrika Mashariki katika Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani Bw. Georg Rademacher kwa niaba ya Serikali ya Ujerumani. 

Mkutano huo ni maandalizi ya mkutano wa Majadiliano ya Kimaendeleo (Bilateral Negotiations) kati ya nchi hizi mbili unaotarajiwa kufanyika mwaka 2018 ambapo Serikali ya Ujerumani itatangaza kiasi cha fedha watakazotoa kama msaada kwa ajili ya kufadhili Sekta zilizoainishwa katika kumbukumbu zilizosainiwa.

“ Tunaishukuru Ujerumani kwa kuwa miongoni mwa washirika wa muda mrefu wanaotoa misaada mikubwa ya kimaendeleo kwa Tanzania na sisi tunaahidi kuendeleza ushirikiano huo kwa faida ya pande zote mbili” alisema Bi. Amina Khamis Shaaban.

Kwa upande wake Bw. Georg Rademacher kwa niaba ya Serikali ya Ujerumani amesema kwamba Tanzania imekuwa na sifa njema nchini Ujerumani hasa kwa sababu ya amani iliyopo, jinsi ambavyo imehifadhi maliasili zake na kuifanya kuwa nchi yenye vivutio vya kipekee vya utalii.

Bwana Rademacher aliongeza kwamba kwa sasa nchi ya Tanzania imepiga hatua kubwa sana katika kupambana na ubadhirifu wa mali za Umma na kwamba Ujerumani itaendelea kuisaidia Tanzania ili kuweza kuleta maendeleo kwa watu wake na kuondoa umaskini.

Imetolewa na;
Benny Mwaipaja

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kwa Ndg. Gregory Teu kufuatia vifo vya wanafamilia 13

Shangwe zatawala wanafunzi wakipokea vitabu kutoka CanEducate

$
0
0

Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia umetoa msaada wa vitabu vya ziada 285 kwa wanafunzi 200 wa Shule ya Sekondari Bugisha, ikiwa ni sehemu ya jitihada za mgodi huo kusaidia maendeleo ya elimu nchini.Msaada huo ni sehemu ya ufadhili ndani ya programu ya CanEducate inayoendeshwa na kampuni hiyo.

CanEducate ilianzishwa mwaka 2010 lengo kuu likiwa ni kudhamini wanafunzi wa shule za sekondari kutoka katika familia maskini. Chini ya programu hiyo, wafanyakazi huchangisha fedha chini ya mfuko maalumu na kisha kampuni ya Acacia hutoa kiwango sawa na kile kilichochangishwa. Fedha hutumika kulipa ada za shule, kununua sare, vitabu na vifaa vya shule kwa wanafunzi.

Wakati wa kuanzishwa kwake, mpango huo uliwasaidia wanafunzi 158 walio karibu na Mgodi wa Dhahabu ya Bulyanhulu. Hata hivyo, kutokana muitikio mkubwa kutoka kwa wafanyakazi na makandarasi wa Acacia, programu imeweza kukua zaidi na kuwafikia zaidi ya wanafunzi 800 kutoka shule zinazoizunguka Buzwagi.

Moja ya sababu ambazo zinachangia kufanya vibaya kwa wanafunzi katika mitihani yao ya kidato cha nne na cha sita, ni ukosefu wa vitabu mashuleni, na gharama za vitabu ni kubwa ukilinganisha na uwezo wa kifedha wa wazazi na walezi.
Katika eneo la Buzwagi, mpango huo unahusisha shule tatu za sekondari; Shule ya Sekondari ya Bugisha, Shule ya Sekondari ya Mwendakulima, na Shule ya Sekondari ya Nyasubi ambazo zimetoa wanafunzi bora katika mitihani ya kidato cha nne na kidato cha sita.

Msaada uliotolewa kwa Shule ya Sekondari ya Bugisha ulisimamiwa na maafisa mahusiano ya jamii wa mgodi wa Buzwagi, Yunia Wangoya na Antonia Kiondo.

Msaada huo ulitolewa mbele ya walimu, wazazi na wanafunzi ambao kwa pamoja walitoa shukrani zao za dhati kwa kampuni ya Acacia kwa kuwezesha upatikanaji wa msaada huo mkubwa.

TCAA KUKUTANISHA WADAU SEKTA YA USAFIRI WA ANGA KESHO JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) kwa kushirikiana na sekta wa usafiri wa anga wameandaa kongamano usafiri huo kwa lengo kujadili namna ya kuinua na koboresha zaidi sekta ya usafiri wa anga katika uchumi wa taifa.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hamza Johari amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kutokana na sekta ya Usafiri wa Anga katika kufikia uchumi wa kati 2025.

Amesema kuwa katika mada watakazo jadili ni  kupungua kwa shehena zinazosafiri kupitia viwanja vya ndege ikiwemo Samaki zinazovuliwa katika Ziwa Vicktoria kutumia kiwanja cha ndege cha Entebe  cha nchini Uganda na Maua ya Mkoa wa  Kilimanjaro na Arusha   kutumia uwanja wa ndege wa Mombasa nchini Kenya.

Hamza amesema mkutano huo ndio utatadhimini hali ya usafiri  ili kuboresha masuala mbalimbali ya usafiri wa anga katika kufanya uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere  kiunganisha  kwa safari za ndege.

Amesema  kuwa mkutano huo unafanyika mara mbili kwa mwaka ili kuangalia masuala mbalimbali ya usafiri wa anga kutokana na umuhimu wa sekta hiyo katika ukuaji wa uchumi.

Mgeni Rasmi katika Mkutano huo atakuwa ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi , Profesa Makame Mnyaa Mbarawa  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi- Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho.

Amesema katika ukaguzi wa Shirika la Usafiri wa Anga (ICAO)  kwa Mamlaka hiyo  imepata asilimia 64.4  katika mwaka huu  kutoka asilimia 37. 5  mwaka 2013.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA), Hamza Johari akizungumza  leo na  waandishi wa habari juu ya mkutano wa wadau wa usafiri  anga utaofanyika Septemba 18 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Wandishi wa habari wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA), Hamza Johari wakati akitangaza mkutano wa wadau utaoanza kesho, jijini Dar es Salaam

MKAZI WA MWANZA IMANI MAKUNDI ATUSUA TSH 15M ZA VODACOM TANZANIA PLC

$
0
0
 Mshindi wa Sh 15 Milioni kupitia  promosheni ya Tusua Mapene inayoendeshwa na Vodacom Tanzania PLC,Bw. Imani Makundi, akifurahia kwenye duka la kampuni hiyo lililopo PPF jijini Mwanza jana baada ya kukabidhiwa kitita chake.
 Meneja Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Mkoa wa Mwanza Victoria Chale(kulia) akimakabidhi pesa zake Mshindi wa Sh 15 Milioni ya promosheni ya Tusua Mapene Imani Makundi, kwenye hafla iliyofanyika jijii Mwanza jana.
Imani Makundi ambaye ni Mshindi wa Sh 15 Milioni kupitia  promosheni ya Tusua Mapene inayoendeshwa na Vodacom Tanzania PLC, Akiondoka na kitita chake huku akifurahia jambo na wateja wa Vodacom Tanzania  kwenye duka la kampuni hiyo lililopo PPF jijini Mwanza jana baada ya kukabidhiwa kitita chake na Meneja Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Mkoa wa Mwanza Victoria Chale(Hayupo pichani) .


UNA Tanzania yazijengea uwezo asasi za vijana za Tanzania Bara na Visiwani

$
0
0
Mkufunzi Nuria Mshare akitoa mada kuhusu ushawishi na utetezi kwa maafisa miradi wa asasi za vijana kuhusu namna ya kufanya shughuli ushawishi, utetezi na ufuatiliaji wa haki za vijana katika ngazi ya serikali za mitaa, kitaifa na kimataifa kwenye mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Saddam Khalfan (Afisa wa Program - UNA Tanzania) akielezea kuhusu sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 na mchakato wa kupitia upya sera hiyo na mchakato wa kukusanya maoni ya sera ya maendeleo ya vijana kwenye mkutano uliowakutanisha asasi mbalimbali za vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani chini ya ufadhili wa The Foundation for Civil Society ili kuwajengea uwezo katika ushawishi na utetezi na ufuatiliaji wa haki za Vijana.
Rais Wa Chama ca Walimu wenye Uziwi(CWUT), Theresia Nkwera(kulia) akipata ufafanuzi wa mafunzo kwa vitendo kutoka kwa Bi Eliza William wakati wa uwasilishwaji wa mada  kuhusu usashwishi na utetezi kwa maafisa miradi wa asasi za vijana kuhusu namna ya kichambua sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 na mchakato wa kupitia upya sera.
 Baadhi ya maafisa miradi wa asasi za vijana wakichangia mada kuhusu sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 kwenye mkutano uliowakutanisha ili kujadili namna ya kufanya kazi kwa pamoja ili kuwa na sauti moja kwenye sera ya vijana. 
 Baadhi ya  maafisa miradi wa asasi za vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani wakifuatilia mada kuhusu sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 na mchakato wa kupitia upya sera hiyo na mchakato wa kukusanya maoni ya sera ya maendeleo ya vijana.
Mkufunzi Nuria Mshare akitoa mada kuhusu ushawishi na utetezi kwa maafisa miradi wa asasi za vijana kuhusu namna ya kufanya shughuli ushawishi, utetezi na ufuatiliaji wa haki za vijana katika ngazi ya serikali za mitaa, kitaifa na kimataifa kwenye mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Saddam Khalfan (Afisa wa Program - UNA Tanzania) akielezea kuhusu sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 na mchakato wa kupitia upya sera hiyo na mchakato wa kukusanya maoni ya sera ya maendeleo ya vijana kwenye mkutano uliowakutanisha asasi mbalimbali za vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani chini ya ufadhili wa The Foundation for Civil Society ili kuwajengea uwezo katika ushawishi na utetezi na ufuatiliaji wa haki za Vijana.
Rais Wa Chama ca Walimu wenye Uziwi(CWUT), Theresia Nkwera(kulia) akipata ufafanuzi wa mafunzo kwa vitendo kutoka kwa Bi Eliza William wakati wa uwasilishwaji wa mada  kuhusu usashwishi na utetezi kwa maafisa miradi wa asasi za vijana kuhusu namna ya kichambua sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 na mchakato wa kupitia upya sera.
 Baadhi ya maafisa miradi wa asasi za vijana wakichangia mada kuhusu sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 kwenye mkutano uliowakutanisha ili kujadili namna ya kufanya kazi kwa pamoja ili kuwa na sauti moja kwenye sera ya vijana. 
 Baadhi ya  maafisa miradi wa asasi za vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani wakifuatilia mada kuhusu sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 na mchakato wa kupitia upya sera hiyo na mchakato wa kukusanya maoni ya sera ya maendeleo ya vijana.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images