Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1371 | 1372 | (Page 1373) | 1374 | 1375 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO. 

  Chama cha Wazazi na Watoto wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo,Akili na Viungo Tanzania (CHAWAUMAVITA) kitafanya maadhimisho ya siku ya mtindio wa ubongo duniani kwa lengo la kuipa jamii uelewa juu ya changamoto wanazozipata watoto wenye matatizo hayo na kuwaleta pamoja familia zinazolea watoto hao ili wabadilishane uzoefu.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa chama hicho, Hilali Said alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo.

  “Kwa kawaida Siku ya Mtindio wa Ubongo duniani huadhimishwa kila Jumatano ya kwanza ya mwezi Oktoba lakini kwa mwaka huu itaadhimishwa tarehe 6, ambapo yanategemewa kufanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mjimwema vilivyopo wilaya ya Kigamboni na tunategemea mgeni rasmi wa maadhimisho hayo atakuwa Mkuu wa Wilaya hiyo”, alisema Said.

  Said ameongeza kuwa nchi mbalimbali Duniani huadhimisha siku hiyo kwa kutoa elimu ya ulemavu wa aina hiyo kwa wananchi ili kupunguza athari zinazojitokeza kwa wazazi na watoto wenyewe pamoja na kuwasaidia wanachama kutetea na kupata haki zao kwa mujibu wa sheria.

  Ameelezea mambo sita ambayo yamegundulika kuwa ni changamoto zitokanazo na matatizo hayo duniani kuwa ni fursa za matibabu kwa watoto hao, ukosefu wa dawa, ufahamu mdogo kwa jamii, ukosefu wa elimu, hali halisi ya kimaisha pamoja na mchango wao katika nchi kama binadamu wengine.

  Aidha, Said amefafanua kuwa chama hicho kwa sasa kinafanya kazi Jijini Dar es Salaam pekee ambapo kuna jumla ya vituo kumi vinavyowasaidia watoto wenye matatizo hayo kupata huduma ya mazoezi ya viungo vilivyoathirika mara moja kwa wiki.

  Alivitaja vituo hivyo kuwa vipo katika manispaa za Ilala, Kinondoni, Kigamboni, Ubungo na Temeke jijini Dar es salaam.

  Kwa upande wake mweka hazina wa chama hicho, Jane Kim ameiomba Serikali kuwasaidia watoto hao kwa kuwapatia mazingira mazuri ya kusomea pamoja na walimu wa kutosha wenye elimu stahiki ikiwa ni pamoja na kuwapatia ulinzi wa kutosha wanapokuwa shuleni ili nao waweze kupata elimu na kutimiza ndoto zao kama watoto wengine.

  “Watoto wenye mtindio wa ubongo wana haki sawa na watoto wengine hivyo wanatakiwa kupata haki zote wanazopatiwa watoto wasio na tatizo hilo zikiwemo za mazingira mazuri ya kusomea pamoja na viwanja vya michezo vinavyolingana na hali zao”,alisema Jane.

  Chama hicho cha kilisajiliwa mwezi Machi, 2013 kupitia Msajili wa Vyama vya Kiraia, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kinawahusisha na wazazi wenye watoto walio na mtindio wa ubongo ambao wanafanya mazoezi tiba katika vituo vilivyopo Jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wa Watoto Wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo Tanzania (CHAMAUMAVITA) Bw. Hilally Said (katikati), akisisitiza jambo mbele ya Waaandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya maadhimisho ya Watoto wenye Mtindio wa Ubongo yatakayofanyika tarehe 6 oktoba mwaka huu leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa CHAMAUMAVITA Taifa, Bi. Mwanahamis Hussein, na Mweka Hazina wa CHAMAUMAVITA Taifa Bi. Jane Kim.
  Katibu wa Chama cha Wazazi wa Watoto Wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo Tanzania (CHAMAUMAVITA) Taifa, Bi. Mwanahamis Hussein (katikati) akizungumza mbele ya waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya maadhimisho ya watoto wenye Mtindio wa Ubongo yatakayofanyika tarehe 6, Oktoba mwaka huu leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa CHAMAUMAVITA Bw. Hilali Said na Mweka Hazina wa CHAMAUMAVITA Taifa Bi. Jane Kim.
  Mweka Hazina wa Chama cha Wazazi wa Watoto Wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo Tanzania (CHAMAUMAVITA), Bi. Jane Kim akielezea maadhimisho ya Watoto wenye Mtindio wa Ubongo yatakayofanyika tarehe 6, Oktoba mwaka huu mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani, Kushoto ni Mwenyekiti wa CHAMAUMAVITA Bw. Hilali Said. Picha zote na Thobias Robert, MAELEZO.

  0 0


  Na. Neema Mathias-MAELEZO.

  Askofu wa kanisa la Good News For All, Dkt. Charles Gadi ametoa wito kwa wananchi na serikali kuyatunza mazingira na uoto wa asili ili kuchangia uwepo wa hali nzuri ya hewa.

  Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Askofu Gadi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo aliongoza maombi maalum kwa lengo la kuombea tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa juu ya uwezekano wa kutokea kwa upungufu mkubwa wa mvua za vuli katika mikoa mingi hapa nchini.

  Askofu Gadi amesema kuwa wananchi wote wanapaswa kulinda mazingira ikiwemo kupiga vita ukataji ovyo wa miti na badala yake wapande miti kwa bidii ili kuilinda mazingira kutokana na uharibifu unaosababisha ukame unaotokana na ukosefu wa mvua.

  Aidha askofu huyo amesema kuwa wao kama viongozi wa dini wanakubaliana na utabiri wa kisayansi uliotolewa ambao mara nyingi umekuwa ukifanikiwa, lakini haitokuwa sawa kusubiri hadi hali hiyo ya ukame itakapotokea wakati Mungu amewapa Imani na mamlaka ya kuomba dhidi ya majanga kama hayo.

  “Good News for All kwa kushirikiana na madhehebu mbalimbali tumekuwa tukiendesha mikutano ya kuiombea nchi dhidi ya ukame tangu mwaka 2006 ambapo ni zaidi ya miaka 11 sasa tunamshukuru na Mungu amekuwa akijibu maombi yetu,” alisema Askofu Gadi.

  Pia, Askofu Gadi amesema kuwa kutokana na uzoefu walionao wanatoa wito kwa viongozi wengine wa dini kufanya maombi ili ukame huo usitokee.“Ukame ni jambo baya kwa uchumi, ni baya kwa afya ya watu na baya kwa viumbe hai wote wakiwemo wanyama na mimea hivyo tuungane kwa pamoja katika kuliombea jambo hili,” alifafanua Askofu Gadi.

  Aidha, Askofu gadi amesema “jambo la kufurahisha ni kwamba mvua ni hazina nzuri ya Mungu, tena ndicho kitu cha thamani ambacho alikiacha duniani kwaajili ya kuendesha uhai aliouumba hususani kwa viumbe hai.

  Vilevile Askofu Gadi amefafanua kuwa maandiko matakatifu katika Biblia yanaonyesha kuwa mvua ni mali ya Mungu na ameahidi pasipo shaka kwamba tukimwomba atatupatia, ndiyo maana wana Imani na ujasiri kuomba dhidi ya ukame na majanga mengine kila mara na Mungu amekuwa mwaminifu kwa neno lake kwa kujibu maombi. 

  “Katika kitabu cha Matendo ya mitume 14:17, lakini hakujiacha pasipo ushuhuda, kwa kuwa alitenda mema akiwapeni mvua kutoka mbinguni, na nyakati za mavuno akiwashibisha mioyo yenu chakula na furaha,” alieleza Askofu Gadi.
  Mwenyekiti wa Kanisa la Good News For All Ministry Askofu Dkt. Charles Gadi (katikati) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati akifanya maombi maalumu ya kuombe mvua mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu wa kanisa hilo Mchungaji Palemo Massawe na kushoto ni Mchungaji wa kanisa hili Andrew Thomas.
  Mwenyekiti wa Kanisa la Good News For All Ministry Askofu Dkt. Charles Gadi (wa pili toka kulia) pamoja na wachungaji wa kanisa hilo wakifanya maombi maalumu ya kuombe mvua mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kanisa la Good News For All Ministry Askofu Dkt. Charles Gadi wakati akifanya maombi maalumu ya kuombe mvua mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

  Picha na Eliphace Marwa – Maelezo.

  0 0


  Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd imezindua Mradi mkubwa wa ufugaji kuku unaosimamiwa na Kikundi cha Ujasiriamali cha Shinyanga,Kishapu na Kahama (SHIKIKA) uliopo katika mtaa wa Sanjo kata ya Chamaguha katika manispaa ya Shinyanga.

  Uzinduzi wa mradi huo umefanyika leo Jumatatu Septemba 18,2017 katika mtaa wa Sanjo kata ya Chamaguha manispaa ya Shinyanga.Kikundi cha SHIKIKA kinachotekeleza mradi huo,kilianzishwa Machi 16,2017 baada ya kampuni ya Namaingo Business Agency Co.Ltd kuwaelekeza wanachama wake kuunda vikundi vya wanachama hamsini hamsini ili wakubaliane kuendesha mradi wanaoupenda.

  Wanakikundi hao waliamua kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku wa kienyeji ndipo kampuni hiyo ikawachangia vifaranga 200,wakaanza ufugaji tarehe 9.6.2017 na mpaka sasa kikundi kina kuku zaidi ya 1300.Akizungumza wakati wa kuzindua mradi huo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim aliwapongeza wanakikundi hao kwa kuchangishana fedha shilingi milioni 8 na kuamua kuanzisha mradi huo.

  “Ndugu zangu jambo hili mlilofanya na mlilolitekeleza kwanza ni jambo la kitaifa kwa sababu wananchi wakiwa na uchumi mzuri serikali nayo inapata kodi lakini pia tunakuwa tumetengeneza ajira”,alisema Ibrahim.

  “Pamoja na jitihada hizi mlizochukua kwa muda mfupi,Tunatamani kuona kila mtu anakuwa na kuku walau 1000 kwenye banda lake,najua changamoto kubwa iliyopo ni mitaji na riba kubwa kwenye mikopo lakini kuna fedha kwa ajili ya maendeleo ya akina mama na vijana zenye riba ndogo sana zipo kwenye benki mbalimbali,serikali inafanyia kazi suala la mikopo hiyo”,aliongeza.

  Aidha Ibrahim aliwataka wananchi kuwa na maamuzi ya kutoka katika hali walizonazo kwa kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa na kuilaumu serikali.“Hakuna haja ya kuilaumu serikali bali unapaswa kujiajiri ili kubadilisha maisha yako,hakuna maisha mazuri kama mtu ukijiajiri,hata hao waliojiriwa wakistaafu huwa wanarudi kujiajiri hivyo kujiajiri ndiyo kila kitu katika maisha yako”,aliongeza Ibrahim.

  “Sisi Namaingo Bussiness Agency Co. Ltd kazi yetu ni kuwabadilisha kiakili ili muweze kubadilika kimawazo kwani fursa za kubadili maisha yenu,zipo nyingi,kufanikiwa kwa mtu ni maamuzi ya mtu mwenyewe”,alisema.Akisoma risala, Katibu Msaidizi wa SHIKIKA,Beatrice Nangale alisema gharama za kuanzisha mradi huo ni shilingi milioni 8 lakini mpaka sasa umegharimu shilingi milioni 20 ambazo ni michango ya wanachama.Alisema ili kufikia malengo yao,kundi hilo linahitaji eneo kubwa la ekari 3000 kwa ajili kupanua mradi wa kuku,kuwa na mashine za kutotolea,kutengeneza chakula cha kuku,kuchakata minofu ya kukuna ufugaji wa nyuki wa asali.

  “Pia tunataka kufuga samaki,mbuzi,sungura na ng’ombe kisha kusindika nyama zao,kulima mboga mboga na matunda kama vile mapapai,kupanda miti na kujenga nyumba kwa ajili ya makazi”,alifafanua Nangale.

  Hata hivyo alizitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa ni ukosefu wa chakula na dawa za kuku mjini Shinyanga,masharti magumu ya benki za utoaji mikopo,ukosefu wa wataalam wa masuala ya mifugo pamoja na kukosa wahisani na misaada ya wahisani kutokana na hali ngumu za kiuchumi za wanakikundi.Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Chamaguha Deo Masalu alisema mradi huo utatumika kama shamba darasa na kuahidi serikali kuwapa ushirikiano wanachama wa kikundi ili kuhakikisha wanafikia malengo yao.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim akijiandaa kukata utepe kwa ajili ya kuzindua mradi wa kuku unaosimamiwa na Kikundi cha Ujasiriamali kutoka Shinyanga,Kishapu na Kahama (SHIKIKA) leo Septemba 18,2017.Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim akikata utepe.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim akishikana mkono na Katibu wa SHIKIKA,Gelard Egwaga baada ya kukata utepe.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim akiangalia kuku wenye umri wa miezi miwili katika moja ya mabanda ya kundi la SHIKIKA.

  Viongozi wa kundi la SHIKIKA wakimwongoza Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim kuangalia kuku hao.

  Ndani ya banda la kuku,mgeni rasmi Biubwa Ibrahi na waangalizi wa kuku (vijana watatu kulia).

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim akiwa amebeba jogoo mwenye umri wa miezi minne katika banda la kuku.
  Kuku wakiwa katika banda.
  Katibu wa SHIKIKA,Gelard Egwaga akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wao wa ufugaji kuku unaosimamiwa na SHIKIKA.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuku unaosimamiwa na SHIKIKA.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim akisisitiza umuhimu wa kujiari badala ya kutegemea kuajiriwa na serikali.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim akizungumza.
  Mwenyekiti wa SHIKIKA,Kiyungi Mohamed Kiyungi akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo.

  Wanachama wa SHIKIKA wakiwa eneo la tukio.
  Wanachama wa SHIKIKA wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea.

  Uzinduzi wa mradi unaendelea.

  Mratibu wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd mkoa wa Shinyanga,Vaileth Kyando akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa ufugaji kuku.

  Katibu Msaidizi wa SHIKIKA,Beatrice Nangale akisoma risala kwa niaba ya wanachama wa SHIKIKA.

  Wa kwanza kushoto ni Afisa Mtendaji wa kata ya Chamaguha,Deo Masalu,Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Co. Ltd,Biubwa Ibrahim na Katibu wa SHIKIKA,Gelard Egwaga wakifuatilia kwa umakini risala kutoka kwa Katibu Msaidizi wa SHIKIKA,Beatrice Nangale.

  Makamu mwenyekiti wa SHIKIKA,Aneth Muro akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa ufugaji wa kuku.

  Afisa Mtendaji wa kata ya Chamaguha,Deo Masalu akizungumza wakati uzinduzi wa mradi wa ufugaji kuku unaotekelezwa katika kata yake.Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori akizungumza wakati wa uzindulizi mradi wa usambazaji majisafi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), katika eneo la Kilungule B. Zaidi ya wakazi 5000 wanatarajia kunufaika na mradi huo. Kutoka kushoto ni Meneja wa DAWASCO - Kimara, Paschal Fumbuka na Kulia kwa Mkuu wa Wilaya ni Diwani wa Kata ya Kimara, Paschal Manota.  Diwani wa Kimara, Paschal Manota akizungumza wakati wa uzindulizi mradi wa usambazaji majisafi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), katika eneo la Kilungule B. Zaidi ya wakazi 5000 wanatarajia kunufaika na mradi huo. Kutoka kushoto ni Meneja wa DAWASCO - Kimara, Paschal Fumbuka na Kulia kwa Mkuu wa Wilaya ni Diwani wa Kata ya Kimara, Paschal Manota.
  Meneja wa DAWASCO - Kimara, Paschal Fumbuka akitoa ufafanuzi juu ya mradi huo ambao umezinduliwa leo eneo la Kilungule B, ambapo walikuwa hawakuwahi kuipata huduma hiyo kwa miaka 20. Aliongeza kuwa utekelezaji wa mradi huo ni moja ya hatua zinazofanywa na Dawasco Mkoa wa Kimara katika kuondoa kero ya ukosefu wa huduma ya Maji katika maeneo yasiyo kuwa na huduma hiyo kwenye Mkoa huo.
  Wananchi waliohudhuria uzinduzi huo wakifuatilia kwa makini.
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori akiwa ameongozana na Diwani wa Kimara, Paschal Manota na Meneja wa Dawasco - Kimara, Paschal Fumbuka pamoja na wananchi wa eneo la Kilungule B kuelekea kuzindua mradi huo.
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori pamoja na Diwani wa Kimara, Paschal Manota  wakizindua mradi wa usambazaji majisafi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), katika eneo la Kilungule B. Zaidi ya wakazi 5000 wanatarajia kunufaika na mradi huo.
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori pamoja na Diwani wa Kimara, Paschal Manota wakifurahia.
  Majiiiiiiiiiiiiiiiiii hayo...
  Akina mama wakifurahi maji.
  Maneja akitoa neno la shukrani mara baada ya uzinduzi wa mradi huo.
  Wakazi wa Kilungule B wakichota maji mara baada ya zoezi la uzinduzi kufanyika.
  Wananchi wakijiandisha ili waweze kupimiwa maeneo yao wapatiwe maji.

  0 0


  Baadhi ya Maofisa wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia kwa makini, mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango na Uongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mchumi Mkuu wa wizara, Dionisia Mjema.(Picha zote na Bw. Elia Madulesi).
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akiwa na Kamishina wa Sera, Bw. Mgonya Benedicto wasikiliza taarifa za Shirika la Posta kupitia kwa Postamasta Mkuu Bw. Deo Kwiyukwa (hayuko pichani), wakati wa ziara hiyo leo.
  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Sera Bw. Mgonya Benedicto, wakati alipokuwa anazungumza na uongozi wa Shirika la Posta, ulipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali mstaafu, Dkt. Harun Kondo (kushoto), akimweleza jambo Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati Uongozi wa shirika hilo, ulipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali mstaafu, Dkt. Harun Kondo (kushoto), akimweleza jambo Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati Uongozi wa shirika hilo, ulipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu, Bw. Deo Kwiyukwa na kulia ni Mkurgenzi wa Sera wa wizara hiyo, Bw. Mgonya Benedicto.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali mstaafu, Dkt. Harun Kondo (kushoto), akimweleza jambo Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati Uongozi wa shirika hilo, ulipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu, Bw. Deo Kwiyukwa.
  Picha ya pamoja ya uongozi wa Shirika la Posta wakiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango(wa pili kushoto) baada ya ujumbe huo kumtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali mstaafu, Dkt. Harun Kondo (wa pili kulia), akimshukuru Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, mara baada uongozi huo, kumtembelea ofisini kwake na kufanya naye mazungumzo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu, Bw. Deo Kwiyukwa na kulia ni Meneja Mkuu Rasilimali za shirika, Bw. Macrice Mbodo.  UONGOZI wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), leo umefanya ziara Wizara ya Fedha na Mipango na kufanya mazungumzo na Waziri wa wizara hiyo, Dkt. Philip Mpango, Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

  Ujumbe huo wa Shirika la Posta uliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Kanal Mstaafu Dkt. Harun Kondo, akiwa na Kaimu Postamasta Mkuu Bw. Deogratius Kwiyukwa,Kaimu Meneja Mkuu wa Rasilimali za shirika, Bw. Macrice Mbodo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Bw. Elia Madulesi.

  Katika mazungumzo hayo, ujumbe kutoka Shirika la Posta ulimweleza Waziri hali halisi ya Shirika, zikiwemo changamoto , mafanikio na maendeleo ambayo shirika limeyapata tangu lilipoanzishwa mwaka 1994 baada ya kutenganishwa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na Benki ya Posta ambao kwa sasa ni taasisi zinazojitegemea kama ilivyo Shirika la Posta.

  Mwenyekiti alieleza juu ya hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Shirika katika kulifanyia mabadiliko makubwa ya kimuundo na kiutendaji ili liweze kukabiliana na changomoto za ushindani wa huduma na biashara kwa jumla.Pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Harun Kondo, alimwomba Waziri Mpango, alisaidie Shirika katika kutatua changamoto mbali mbali.


  Baadhi ya changamoto alizozitaja katika mazungumzo hayo ni pamoja na;

  Shirika la Posta kuwekwa kwenye orodha ya Mashirika yanayotarajiwa kurekebishwa au kubinafsishwa hatua iliyolidhoofisha Shirika. pamoja kikwazo hicho shirika la posta linabeba mzigo mkubwa wa kuwalipa watumishi wake mishahara na marupurupu yao bila kuitegemea Serikali ikizingatiwa kwamba Shirika halikupewa mtaji na haliruhisiwa kukopa kwa ajili ya kujiendesha.

  Mwenyekiti wa Bodi alimkumbusha Waziri kuwa Shirika la Posta ni mali ya Serikali kwa asilimia mia moja (100%) na sheria namba 19 ya mwaka 1993 iliyoanzisha Shirika la Posta inatamka wazi kuwa Serikali kupitia Waziri wa Fedha atakaa na Waziri mwemye dhamana ya Posta ili kubaini mtaji utakaowezesha Shirika kujiendesha, hadi sasa mtaji huo haujaweza kutolewa ili kuliwezesha Shirika kujiendesha.

  Pia Mwenyekiti amemwomba Waziri ili Shirika lirejeshewe fedha kiasi cha shilingi 3,977,000,000/= ambazo Shirika lilizitumia kulipa Pensheni ya wastaafu wa lililokuwa Shirika la Posta na Simu la Jumuia ya Afrika Mashariki.

  Vilevile alimuomba Waziri kuhamisha jukumu la kuwalipa wastaafu hao kwenye Mifuko ya hifadhi ya jamii.Serikali iangalie uwezekano wa kuchukua mzigo wa riba na tozo (Interest and Penalty) na malimbikizo ya kodi ya shilingi 29,000,833,757/= ambayo kati ya hizo, tozo na riba ni shilingi 22,013 701,414.28.

  Mwenyekiti alimweleza Mheshimiwa Waziri kuwa haya yote yakifanyika kwa wakati Shirika litaweza kujiendesha kwa faida na kutoa gawio kwa mwenye mali (Serikali) kama ilivyokusudiwa.

  Pia alieleza kuwa kwa sasa Shirika linafanya mabadiliko makubwa ya kimfumo na ya kimuundo ambapo linahitaji fedha kwa ajili ya kuboresha huduma zake, kuanzisha miradi mipya na kuimarisha zile zilizoko.

  Mwisho, Waziri Dkt. Mpango aliahidi kuyafanyia kazi maombi hayo kwa karibu na kuangalia namna ya kutatua changamoto hizo kwa kushirikiana na Wizara inayosimamia Shirika la Posta liweze kutoa huduma bora katika vituo yake, kujiendesha kwa faida na hatimaye kuweza kutoa gawio kwa Serikali.

  0 0  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania,Anna Abdallah katikati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Tanga leo kuhusu bei elekezi ya korosho msimu wa 2017/2018 kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo,Maokola Majogo 
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martin Shigella akizungumza katika mkutano huo kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania,Anna Abdallah kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT)Hassani Jarufu 
  Sehemu ya wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia 
  Waandishi wa habari mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo kushoto ni Mbaruku Yusuph wa Gazet la Tanzania Daima,Amina Kingazi wa Gazeti la The Guardian mkoani Tanga,Burhan Yakub wa Mwananchi
  Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo kulia ni Sussan Uhinga wa gazeti la Mtanzania Tanga,Pamela wa Tanga One Blog wakifuatilia
  Mwandishi wa gazeti la Habari Leo mkoani Tanga Anna Makange akiuliza swali kwenye mkutano huo
  Mwandishi wa Clouds TV Mkoani Tanga Gift Kika akiuliza swali kwenye mkutano huo kulia ni Amina Omari wa gazeti la Mtanzania


  BODI ya Korosho Tanzania imetangaza bei elekezi kwa msimu 2017/2018 kwa kilo moja ya Korosho ghafi daraja la kwanza (Standard Grade) kitakuwa ni sh.1,450 huku kilo moja ya daraja la pili itakuwa ikiuzwa kiasi cha sh.1,160.

  Hayo yalisemwa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Anna Abdallah wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga kuhusu ufunguzi rasmi wa soko la Korosho msimu wa mwaka 2017/2018.

  "Niseme tu bei hii elekezi ya korosho imetangazwa na bodi hiyo kwa mamlaka waliopewa chini ya kifungu cha 5(3)(d) ambapo bei hiyo imefikiwa baada ya utafiti wa kupata gharama halisi za kuzalisha kilo moja ya korosho ghafi na kuongeza asilimia 20 kama faida ya mkulima "Alisema.

  Alisema kwa msimu huu gharama ya kuzalisha kilo moja ya korosho ghafi ni 1,208.39 na asilimia 20 ya faida kwa kilo ni sh.241.68 .

  Aidha alisema katika mjengeko wa bei ya korosho ghafi msimu wa 2017/2018 ambapo magunia na kamba vitatolewa na serikali kupitia CBT huku chama cha msingi kikipata sh.90.00,Halmashauri ya wilaya ikipata asilimia 3 ya sh.43.50,mfuko wa wakfu ukipata sh.10.00 ambapo jumla ya gharama ni 143.50 wakati bei elekezi ikiwa ni 1,450.00 na mjengeko wa bei ukiwa ni tsh.1,593.50.

  Aliongeza kuwa katika msimu wa ununuzi wa korosho 2017/2018 utafunguliwa rasmi Octoba Mosi mwaka huu huku akiwahimiza wadau wote wanaohusika na uuzaji na ununuzi wa zao la korosho kukamilisha maandalizi ya msimu kabla ya ununuzi kuanza.

  "Wadau hao ni pamoja na Sekretarieti za mikoa,halmashauri za wilaya,Wakulima,Vyama vya Ushirika vya Msingi,Vyama Vikuu vya Ushirika,Wakala wa Vipimo,Bodi ya Leseni za Maghala,Waendesha Maghala,Wasafirishaji,Wanunuzi,Mamlaka ya Bandari,Mabenki na wengine ambao wanahusika kwa namna moja au nyengine"Alisema.

  Akizungumzia suala la utoaji wa leseni za ununuzi wa korosho, Mwenyekiti huyo alisema bodi hiyo inatumia fursa hiyo kuwahamasisha wanunuzi wa zao hilo wa ndani na nje kuomba leseni ya ununuzi kwa ajili ya msimu wa 2017/2018.

  "Leseni hii itatolewa bila malipo yeyote,Fomu namba 2 ya maombi ya leseni za ununuzi wa korosho ghafi inapatikana kwenye tovuti ya bodi ya korosho Tanzania (www.cashew.go.tz) na kwenye ofisi zake zilizopo Mtwara(Makao Makuu) na kwenye matawi yake ya Dar es Salaam,Tanga na Tunduru "Alisema

  Hata hiyo alisisitiza umuhimu wa wauzaji,wanunuzi na wadau wa korosho kufuata mfumo wa stakabadhi ghalani wa kuuza na kununua korosho huku akitoa wito kwa yeyote atakayekiuka sheria,kanuni na mwongozo namba 1 wa mwaka 2017/2018 wa mauzo ya korosho,atachukuliwa hatua kali ikiw ni pamoja na kutaifishwa korosho.Habari kwa hisani ya Blog ya Kijami ya Tanga Raha

  0 0

   Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (wakwanza kulia), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, (wakwanza kushoto), na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo anayeshughulikia Miradi, Mhandisi Khalid James, (watatu kushoto), wakimsikiliza Meneja Mradi wa TEDAP, Mhandisi Emmanuel Manirabona, (aliyenyoosha mkono), wakati Naibu Waziri na uongpozi wa TANESCO, ulipotembelea mradi wa TEDAP wa Gongolamboto jijini Dar es Salaam, Septemba 18, 2017. Mradi huo unahusu upanuzi na uendelezaji wa mradi wa kusafirisha umeme wa 132kv.
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  SERIKALI kupitia Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), imeahidi kusimamia miradi ya umeme Kituo cha Tipper-Kigamboni,  Mbagala na Kurasini ili kuhakikisha inakamilika kwa haraka na kwa wakati na hatimaye wananchi wa maeneo hayo wanaondokana na adha ya kukatika kwa umeme mara kwa mara.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, mwishoni mwa ziara yake ya kufuatilia uboreshaji wa vituo vya kupoza na kusambaza umeme pamoja na ujenzi wa kituo kipya cha kufua na kusambaza umeme huko Kimbiji  wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam Septemba 18, 2017.

  Waziri pia amekagua ujenzi wa mradi wa maendeleo ya upanuzi na upatikanaji nishati (TEDAP), wa kusafirisha umeme wa 132kv ulioko Gongolamboto nje kidogo ya jiji.

  “Wananchi wanataka umeme, hawahitaji kujua  nguzo za umeme zimepatikana wapi, au upembuzi yakinifu utakamilika lini, nimeagiza baada ya siku tano kuanzia leo (Septemba 18), fanyeni kazi usiku na mchana walau vituo viwili vya kupoza na kusambaza umeme viwe vimekamilika ili wananchi wa Mbagala na Kigamboni wapate umeme wa kutosha.” Alisema Dkt. 

  Kalemani mbele ya Mbunge wa Kigamboni Dkt. Faustine Ndungulile, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mhe. Hashim Mgandila na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, Dkt. Tito Mwinuka na viongizi wengine wa Tanesco.

  Dkt. Kalemani alisema, miradi hiyo imechukua muda mrefu, na kwamba hakuna muda zaidi utakaoongezwa kuikamilisha.Serikali kupitia TANESCO, inatekeleza miradi mitano ya kuongeza kiasi cha umeme kwenye maeneo ya Mbagala na maeeno kadhaa ya wilaya ya Temeke, Kurasini na Kigamboni ili kukabiliana na ongezeko la kasi la watu na shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo.
  Aidha Naibu Waziri aliipongeza TANESCO, kwa kutekeleza agizo lake la kuhakikisha wakazi 3,500 wa Kigamboni waliolipia ili kuunganishiwa umeme, wawe wameunganishiwa ifikapo Septemba 15, 2017 ikiwa ni pamoja na kupeleka nguzo za umeme zaidi ya 1,000 maagizo ambayo yametekelezwa.

  Hata hivyo naibu Waziri alimueleza Mheshimiwa Mbunge wa Kigamboni na Mkuu wa Wilaya hiyo kuwa tiba mahsusi ya upungufu wa umeme kwenye wilaya hiyo ni kukamilika kwa ujenzi wa kituo kipya cha kupoza na kusambaza umeme cha Kimbiji.

  “Tiba kubwa ya matatizo ya umeme kwa watu wa Kigamboni, na Mbagala ni hapa Kimbiji(kituo kipya), vile vituo vingine vitapunguza tu matatizo lakini naomba Mheshimiwa Mbunge, uwafikishie ujumbe wananchi kuwa Serikali ya awamu ya Tano inayo dhamira ya kweli ya kuhakikisha inawapatia umeme wa uhakika sio tu wananchi wa Kigamboni bali watanzania wote kwa ujumla.” Alifafanua Dkt. Kalemani.

  Naibu Waziri ameshuhudia hatua mbalimbali za ukamilishaji wa miradi hiyo zikiwa zimefikiwa ambapo katika kituo maeneo yote aliyotembelea.
  Kuhusu ujenzi wa kituo kipya cha Kimbiji, Dkt. Kalemani amemuagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANSCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, kuwaleta mafundi wa TANESCO wealiotekeleza kwa muda mfupi ujenzi wa mradi wa kituo cha kupoza na ksuambaza umeme kule Mtwara ili waje kuongeza nguvu.
  Mbunge wa Kigamboni Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile, (kushoto), akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani ambaye alifuatana naye kwenye ziara hiyo.
  Sakafu ya kufungia transfoma mpya ya umeme wa 15mva kituo cha Tipper-Kigamboni, ikijengwa Septemba 18, 2017
  Mshine mpya kwenye kituo cha Mbagala
  Kituo cha Kurasini ambacho nacho kitakuwa tayari baada ya siku tano.
  Dkt. Kalemani, (katikati), Dkt. Ndungulile (wapili kushoto) na Dkt. Mwinuka, (wakwanza kushoto), wakiwa na Meneja wa Mradi wa TADEP, Mhandisi Emmanuel Manirabona, (kulia), baada ya kujionea moja ya mashine mpya ikiwa bado imefunikwa ili kuzuia vumbi kwenye kituo cha Kurasini.
  Fundi akiwa kazini kwenye kituo cha Kurasini.
  Naibu Waziri Dkt. Kalemani, na Mbunge wa Kigamboni Dkt. Ndungulile, wakiwa na furaha baada ya kutembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mbagala, ambacho ujenzi wake umekamilika
  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mhe. Hashim Mgandila, akizungumza mwishoni mwa ziara ya Naibu Waziri, Dkt. Kalemani huko Kimbiji.
  Naibu Waziri Dkt. Kalemani na Mhandisi Khalid James.
  Msafara wa Naibu Waziri ukiwa kwenye eneo la mradi wa TEDAP. Gongolombaoto.
  Mkandarasi anayejenga mradi wa TEDAP, Gongolamboto, akizunguzma.
  Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia usambazaji umeme na huduma kwa wateja mama Joyce Ngahyoma, akielezea hatua zilizochukuliwa na TANESCO katika kuhakikisha wateja 3,500 wa TANESCO Kigamboni waliolipia gharama za kuunganishiwa umeme, wanapatiwa huduma hiyo ikiwa ni pamoja na kupelekwa kwa nguzo zaidi ya 1,000 kwenye eneo la Kigamboni. Anayemsikiliza ni Naibu Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani.
  Kituo cha Mbagala
  Dkt. Kalemani, (kushoto), akimsikiliza Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke, Mhandisi Jahulula akielezea hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Tipper-Kigamboni.
  Dkt. Kalemani, (wapili kushoto), akizungumza jambo na Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, walipowasili eneo la Kimbiji ambako kunatarajiwa kujengwa kituo kipya cha kupoza na kusambaza umeme kitakachohudumia wakazi wa Kigamboni, Kurasini na Mbagala. Wakwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO nayeshughulikia Miradi, Mhandisi Khalid James.

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa majengo ya shule Manispaa ya Dodoma
  Moja ya nyumba ya walimu iliyojengwa katika shule ya msingi Nzasa.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Ihumwa alipokuwa akikagua ujenzi wa madarasa na vyoo.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Ihumwa.


  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amezitaka halmashauri zote kukamilisha miradi ya ujenzi wa madarasa, mabweni, vyoo, maabara, na miundombinu mingine ya shule za msingi na sekondari kabla tarehe 30 Novemba mwaka huu.

  Jafo aliyasema hayo leo hii alipokuwa akifanya ukaguzi wa miradi hiyo katika shule ya Nzasa na Ihumwa zilizopo katika manispaa ya Dodoma. 

  Mnamo mwezi Juni serikali ilitoa fedha kupitia mpango wa lipa kwa matokeo (P4R) sh.bilioni 16 kwa ajili ya miundo mbalimbali kwa shule 63 za sekondari na shule 56 za msingi katika halmashauri mbalimbali ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

  Hata hivyo bado kuna halmashauri chache zinasuasua kukamilisha ujenzi huo hali iliyomlazimu Naibu Waziri huyo kuagiza halmashauri zote hapa nchini kukamilisha miradi iliyo pangwa katika maeneo yao kabla tarehe hiyo.

  Jafo amesema kwamba hataki kusikia au kuona halmashauri yeyote ambayo itakuwa haijakamilisha miradi hiyo kwa kipindi kilichopangwa.“Hatua kali itachukuliwa kwa yeyote atakayefanya uzembe ambao utasababisha ujenzi huo kutokamilika,”amesema Jafo

  Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Jafo amelipongeza sana jeshi la wananchi kutoka kikosi cha Ihumwa kwa kushirikiana na manispaa ya Dodoma kwa kufanikisha ujenzi katika shule ya Nzasa na Ihumwa na ameviomba vikosi vingine hapa nchini kuiga mfano huo mzuri ambao umewezesha kukamilisha miundombinu hiyo kwa gharama ndogo.

  Jafo anaendelea na ziara zake za kikazi za kukagua miradi ya maendeleo katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

  0 0
  0 0

  Na HAMZA TEMBA - WMU
  -----------------------------------------------------------
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ameliagiza Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kupitia Hifadhi ya Taifa ya Arusha kuhakikisha kuwa wananchi wote waliolima ndani ya eneo la hifadhi hiyo kinyume cha sheria wanaondoa mazao yao pamoja na kusitisha kabisa shughuli zozote za kibinadamu ndani ya hifadhi hiyo.  

  Prof. Maghembe ametoa agizo hilo jana wakati akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku moja katika hifadhi hiyo iliyopo wilaya ya Arumeru mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na hifadhi hiyo ikiwemo maeneo yenye mgogoro kwa ajili ya kuyatafutia ufumbuzi.

  "Naagiza, kuanzia leo ni marufuku mtu yeyote kuonekana akilima katika eneo hili, wekeni askari hapa, atakayeonekana piga pingu, hatuwezi kushuhudia watu wanalima ndani ya hifadhi tukae kimya, ni lazima tuchukue hatua. Watangaziwe na wapewe muda wa kuondoa mazao yao, ndani ya siku 30 au 40 wawe wameshaondoka", alisisitiza Prof. Maghembe baada ya kukagua eneo hilo.

  Awali akiwasilisha taarifa ya hifadhi hiyo kwa Waziri Maghembe, Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo, Steria Ndaga alisema eneo hilo ambalo pia linajulikana kama shamba namba 40 na 41 limekuwa na mgogoro tangu mwaka 1990 baada wananchi wa Kijiji cha Olkung'wado kuvamia eneo hilo huku wakitoa hoja kadhaa ikiwemo madai kuwa shamba hilo ni maeneo yao ya asili waliyokuwa wakimiliki tangu zamani.

  Alisema hoja nyingine wanazozitoa ni kuwa walipewa mashamba hayo na Serikali wakati wa operesheni ya uanzishwaji wa vijiji mwaka 1975 na 1976, Aidha, hoja nyingine ni kuwa hawakushirikishwa kwenye mchakato wakati wa ugawaji wa mashamba hayo na kwamba TANAPA pia haina hati miliki ya mashamba hayo.

  Ngada alisema hoja zote hizo zilikinzana na ukweli ya kwamba shamba hilo lilimilikishwa kwa TANAPA tangu mwaka 1980 baada ya kutolewa tangazo kwa wadau wanaoweza kuliendeleza kufuatia muwekezaji wa awali, James Preston Mallory kushindwa kuliendeleza na hivyo kufutiwa hati miliki na Mhe. Rais mnamo mwaka 1979.

  “Wadau mbalimbali waliomba umiliki wake ikiwemo Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro na Halmashauri ya Kijiji cha Olkung'wado, lakini Kamati ya Ushauri ya Ardhi ya Mkoa wa Arusha ikaishauri Serikali mashamba hayo yamilikiwe na TANAPA na hivyo tukaandikiwa barua rasmi ya kukubaliwa kupewa shamba na Idara ya Ardhi Mkoa” alisema Ndaga.

  Alisema TANAPA ilinunua eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 966 kwa lengo la kupanua hifadhi ya Taifa ya Arusha ambapo baada kupewa shamba hilo, iliagizwa kulipa fidia ya mali zilizokuwepo, mwaka 1983 tathmini ikafanyika na malipo yakalipwa Serikalini hatimaye TANAPA ikapewa barua ya kumiliki ardhi mwaka 1988. Alisema kwa upande wa Kijiji hicho cha Olkung'wado hakuna nyaraka yeyote inayoonesha shamba hilo kupewa kijiji hicho. 

  Mhifadhi huyo alisema baada ya mgogoro wa muda mrefu, wataalam wa TANAPA walifanya survey katika shamba hilo ili kubaini maeneo yaliyo na shughuli nyingi za kibinadamu na yale yenye umuhimu zaidi kiikolojia, mapendekezo yalitolewa kuwa maeneo yenye shughuli nyingi za kibinadamu yaachwe kwa wananchi na yale yenye umuhimu kiikolojia yaendelee kuhifadhiwa, Bodi ya TANAPA iliridhia ekari 366 zipewe wananchi na ekari 600 ziendelee kuhifadhiwa.

  “Baada ya kikao cha wadau wa uhifadhi kilichoitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru tarehe 11 Mei, 2017 ambacho kilijumuisha Madiwani, mwakilishi wa Mbunge, katibu tarafa, watendaji wa kata, wenyeviti na watendaji wa vijiji, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na wataalam wa halmashauri, ilifikiwa maazimio ambapo wajumbe waliridhia maamuzi ya Bodi ya Wadhamini ya TANAPA kuwapa wananchi ekari 366 ya shamba hilo na kubakiwa na ekari 600” alisema Ndaga.

  Aliongeza “Kikao hicho pia kiliridhia TANAPA kuweka vigingi vya mpaka katika shamba hilo ambapo tarehe 14 Mei, mwaka huu, 2017 zoezi hilo lilianza na jumla ya vigingi 26 viliwekwa”.

  Alisema hata hivyo kumekuwepo na taarifa kuwa baadhi ya wanakijiji wa Kitongoji cha Momella walifungua kesi mahakamani wakidai wakidai kuwa kijiji cha Olkung'wado kimenyang'anywa ardhi yao na TANAPA, hata hivyo Serikali hiyo ya Kijiji imekana kwa maandishi kuhisika na ufunguzi wa kesi hiyo wakidai imefunguliwa na mtu binafsi na sio Serikali ya Kijiji hicho.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Dkt. Alan Kijazi alimuhakikishia Waziri Maghembe kuwa maagizo yote aliyoyatoa ya kusitisha shughuli za kibinadamu ndani ya eneo hilo yatafanyiwa kazi na atapewa mrejesho wa utekelezaji wake.

  Hifadhi ya Taifa ya Arusha ilianzishwa mwaka 1960 wakati huo ikiitwa Ngurdoto na ina ukubwa wa kilomita za mraba 322. Hifadhi hiyo ni maarufu kwa utalii wa magari, kutembea kwa miguu, kupanda milima (mlima Meru), utalii wa farasi, mitumbwi ya kuogelea, baiskeli na wa utalii wa kutumia farasi. Katika mwaka wa fedha uliopita 2016/2017 hifadhi hiyo ilivunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato kwa asilimia 12 ambapo ilikusanya Shilingi bil. 5.4.
  Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akiingia kwenye ofisi kuu ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha jana Mkoani Arusha katika ziara yake ya kikazi ya siku moja katika hifadhi hiyo iliyolenga kukagua shughuli za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuitafutia ufumbuzi. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Dkt. Alan Kijazi.
   Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akisalimiana na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha, Steria Ndaga alipowasili katika ofisi kuu ya hifadhi hiyo jana Mkoani Arusha kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja iliyolenga kukagua shughuli za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuitafutia ufumbuzi. 
   Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha, Steria Ndaga (wa pili kulia) akiwasilisha taarifa ya hifadhi hiyo kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja katika hifadhi hiyo jana ambayo ililenga kukagua shughuli za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuitafutia ufumbuzi.
  Prof. Maghembe akizungumza kwenye kikao hicho.
  Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Dkt. Alan Kijazi (kushoto) akizungumza kutambulisha viongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha kwa Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja katika hifadhi hiyo jana Mkoani Arusha ambapo ililenga kukagua shughuli za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuitafutia ufumbuzi. 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) na wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia taarifa kuhusu Hifadhi ya Taifa ya Arusha ambayo iliwasilishwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Steria Ndaga.
   Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akiongea na viongozi wa TANAPA kuhusu eneo lililolimwa na wananchi ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha kinyume cha sheria wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja katika hifadhi hiyo iliyolenga kukagua shughuli za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuitafutia ufumbuzi, aliagiza wananchi hao waondolewe ndani ya siku 40. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Dkt. Alan Kijazi na Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo, Steria Ndaga (kulia). 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia) akisikiliza ufafanuzi wa jambo kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha, Steria Ndaga (kushoto) wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja katika hifadhi hiyo jana ambayo ililenga kukagua shughuli za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuitafutia ufumbuzi. 
   Baadhi ya wanyamapori (Twiga na Pundamilia) wakionekana wakijivinjari ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ya Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe katika hifadhi hiyo jana ambayo ililenga kukagua shughuli za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuitafutia ufumbuzi. 

  0 0

   Msaidizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Kanali Mkeremy akibidhi Rambirambi(kwa niaba ya Mhe. Rais) kwa Mufti wa Tanzania Shekhe Aboubakar Zubeir ambaye amefiwa na Kaka yake Shekhe Saad Zubeiry Ally ambaye amefariki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. 
   Msaidizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Kanali Mkeremy akizungumza jambo na Mufti wa Tanzania Shekhe Aboubakar Zubeir ambaye amefiwa na Kaka yake Shekhe Saad Zubeiry nyumbani kwa Marehemu Kinondoni Mtaa wa Ufipa jijini Dar es Salaam. Wakwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu.
  Msaidizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Kanali Mkeremy akiagana na Shekhe wa mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum mara baada ya kuwasilisha Rambirambi kwa niaba ya Mhe. Rais katika msiba huo uliopo Kinondoni mtaa wa Ufipa jijini Dar es Salaam. 
  PICHA NA IKULU

  0 0

   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mchungaji Kelvin Ngaeje wa kanisa la Anglican baada ya kualikwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Kongamano la Mtandao wa wanamaombi Tanzania (APN) uliofanyika leo katika ukumbi wa Chuo kikuu cha St. John kilichopo Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kushoto)akizungumza wakati akifungua Kongamano la Mtandao wa wanamaombi Tanzania (APN) lililofanyika leo katika ukumbi wa Chuo kikuu cha St. John kilichopo Mjini Dodoma. kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Emmanuel Mbennah, Askofu Dudly Magon (wa pili kulia) na Mchungaji Can Ruwa (kulia).
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akisaini kitabu cha wageni kabla ya kufungua  Kongamano la Mtandao wa wanamaombi Tanzania (APN) lililofanyika leo katika ukumbi wa Chuo kikuu cha St. John kilichopo Mjini Dodoma.
  Wanamaombi wa Mtandao Tanzania (APN) wakimsikiliza Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (hayupo kwenye picha) wakati akifungua Kongamano la Mtandao wa wanamaombi Tanzania (APN)uliofanyika leo katika ukumbi wa Chuo kikuu cha St. John kilichopo Mjini Dodoma.

  (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0

  Miongoni mwa mitumbwi iliyokuwa imezagaa katika mwambao wa ziwa Tanganhyika Kijiji cha Wampembe ambayo mingi haikuwa na usajili na kuipotezea serikali mapato katika sekta ya uvuvi.

  Mmoja wa maafisa wa Sumatra (mwenye overoli la bluu) akitoa ufafanuzi mbele ya Mh. Zelote (mwenye kaunda suti0 pamoja na maafisa mbalimbali walioambatana katika ziara hiyo kwenye kijiji cha Wampembe, Wilayani Nkasi.

  Mkuu wa mkoa wa Rukwa kamishna Mstaafu zelote Stephen (kushoto) akimuonesha Afisa Uvuvi wa Kata Godfrey kashengebi (kulia) nyavu zilizobainika kutokidhi vipimo vilivyokubalika na serikali katika shughuli za uvuvi na kuagiza kukamatwa kwa kokoro hizo zilizokuwa zikiendela kutumiaka bila ya kukaguliwa na afisa huyo.


  vijana wakiwa wamebeba kokoro zilizoagizwa kukamatwa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa na kufikishwa ofisi ya kata. 

  ……………………

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna Mstaafu Zelote Stephen ametoa siku saba kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, Kalambo pamoja na Mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) kumpatia orodha kamili ya vyombo vyote vya majini vinavyofanya shughuli zake katika mwambao wa ziwa Tanganyika katika Wilaya za Nkasi na Kalmbo za Mkoa wa Rukwa.

  Ametoa agizo hilo alipotembelea mwambao wa Ziwa Tanganyika katika Kijiji cha Wampembe, Kata ya Wampembe Wilaya ya Nkasi na kubaini mitumbwi kadhaa iliyokuwa ikizagaa kwenye mwambao huo ikiwa haijafanyiwa usajili na kusababisha upotevu wa mapato ya serikali kupitia sekta hiyo ya uvuvi.

  “Halmashauri zimekuwa zikilalamika hazina mapato ya kutosha wakati naona pesa zikielea tu hapa na Hakuna chochote kinachoendelea, sasa natoa siku saba kwa Halmashauri na SUMATRA nipate orodha kamili ya vyombo vyote vya usafiri wa majini, usajili wao na leseni zao zinazowaruhusu kufanya shughuli za uvuvi katika mwambao huo.” Amesema.

  Pamoja na hayo agizo hilo pia limekuja baada ya wiki moja iliyopita boti ambayo mmiliki wake hakujulikani kuzama ziwa Tanganyika ikitokea katika Kijiji cha Kalila, Kata ya kabwe, tarafa ya Kirando, Wilayani Nkasi kuelekea Kijiji cha Kyala Mkoani Kigoma na kupelekea kifo cha mtoto mmoja na watoto wengine wawili kuhofiwa kufa maji huku watu 11 wakiokolewa. Na wafanyakazi wawili wa boti hiyo kukimbia.

  Katika kuhakikisha usalama wa Kijiji cha Wampembe unaimarika Mh. Zelote aliagiza kuhamishwa kwa watumishi wawili, Afisa Mtendaji wa kata ya Wampembe Faustine Wakulichamba pamoja na Afisa uvuvi wa Kata Godfrey Kashengebi kwa makosa mbalimbali moja ikiwa kutosimamia makusanyo ya mapato ya uvuvi jambo lililopelekea kudorora kwa makusanyo ya mapato pamoja na kuwepo kwenye kata hiyo kwa miaka zaidi ya sita jambo ambalo linapunguza ufanisi wao wa kazi.

  Katika doria hiyo Mh. Zelote pia alikamata kokoro na nyavu kadhaa zilizokuwa hazikukidhi vipimo vya serikali katika matumizi yake jambo ambalo maafisa hao walifumbia macho na kuisababishia serikali upotevu wa mapato.

  Kwa mujibu wa sheria za halmashauri mtumbwi wenye urefu wa mita 4 hulipiwa dola 4 kwa mwaka kama ada ya usajili.

  0 0

   

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akishiriki wa Ufyatuaji wa Matofali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za kisasa 402  za Walimu, leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanel Massaka,Globu ya Jamii.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizugumza leo katika uzinduzi wa Ufyatuaji wa Matofali kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Shule katika Mkoa wa Dar es Salaam.


  Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu Kanali Charles Mbuge akizungumza katika uzinduzi wa ufyatuaji tofali za ujenzi wa ofisi za shule katika mkoa wa Dar es Salaam.

  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amezindua rasmi wa Ufyatuaji wa Matofali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za kisasa 402 za Walimu, ambapo amewaomba Wadau na Wananchi mbalimbali kuunga Mkono jitihada hizo.

  Katika uzinduzi huo RC Makonda pamoja na kushiriki shughuli hiyo pia amebainisha kuwa la Ujenzi wa Ofisi hizo ni kuboresha Mazingira ya kufanya kazi kwa walimu ili waweze kutoa Elimu bora kwa Wanafunzi na kuongeza ufaulu.

  Amesema wapo wengi waliopanga kufanya ujenzi wa Ofisi za Walimu lakini mipango hiyo iliishia kubaki kwenye makarabrasha maofisini lakini kupitia juhudi zake na Kamati aliyoiunda wameweza kuleta matokeo chanya.

  RC Makonda ametoa wito kwa Wananchi na Wadau kuchangia Mabati, Saruji, Kokoto,Mchanga, Nondo au Nguvu kazi ilikuwawezesha walimu kufanyakazi katika mazingira bora.

  Amesema ataki kuona kwenye Mkoa wake Walimu wanadhalilika kwa kukosa Ofisi na Vyoo hali inayopelekea kujisaidia kwa Majirani,Bar au Vichakani.

  Aidha amesema hadi sasa amefanikiwa kupata mifuko zaidi ya 10,000 ya Saruji Mashine za kufyatulia Matofali,Gurdoza na vifaa vingine ambapo ataendelea kugonga hodi kwa Wadau ili waweze kuchangia ujenzi huo.

  Amewaomba Wananchi kuwa na uzalendo kwa kujitoa katika ujenzi huo iwe kwa mtu binafsi au Vikundi vya Joaging,Timu za Mpira na vikundi vya maendeleo.

  Ameipongeza Kamati ya ujenzi wa Ofisi za walimu,JKT,Jeshi la Magereza, Jeshi la Polisi,NHC, TBA,Channel Ten na Umoja wa Wamiliki wa Malori na wengine kwa namna wanavyojitoa kusaidia katika zoezi hilo.

  Katika hatua nyingine RC Makonda amesema atatoa TV 30 kwa Magereza ya Ukonga, Segerea na Keko ili wafungwa wapate fursa za kutazama hotuba za Rais Dk. John Pombe Magufuli ili wajue maendeleo yanayofanyika uraiani.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu Canal Charles Mbuge amesema hadi sasa kiasi cha fedha kilichotumika ni zaidi ya Million 200 ambapo watahakikisha ujenzi huo unakamilik

  0 0


  Waziri mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo,wakati alipowasili katika kiwanda cha kutengeneza sabuni cha KEDS kilichopo Pichandege Kibaha Mjini.
  Waziri mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mkurugenzi wa viwanda vya kutengeneza sabuni cha KEDS Pichandege Kibaha Mjini ambae pia ni mkurugenzi wa kiwanda cha kutengeneza vigae cha Twyford kilichopo Pingo Chalinze,Jack Feng.Picha na Mwamvua Mwinyi  Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

  WAZIRI mkuu,Kassim Majaliwa amezitaka serikali za vijiji na ngazi nyingine mkoani Pwani,kujikita kuimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya viwanda ili kulinda mali na usalama wa wawekezaji na watanzania kijumla.

  Amesema haijajulikana hadi sasa nia na dhamira ya watu wasiojulikana wanaojihusisha kupoteza maisha ya watu ,na ni hatari endapo watajiingiza katika maeneo ya uwekezaji kwani hakuna mwenye uhakika wa azma yao.

  Aidha Majaliwa ,ametoa wiki mbili kwa waziri wa maji kutathmini matokeo ya mwenendo wa mradi wa maji wa WAMI ,ili kutoa utaratibu na kama sheria inaruhusu kuvunja mkataba ikiwa mkandarasi ameshafikia kiwango cha asimilia 50 ya utekelezaji.

  Waziri huyo ,pia ameziagiza halmashauri nchini kuona umuhimu wa kutenga fedha kwa ajili ya kununua magari ya zimamoto yatakayosaidia kudhibiti majanga ya moto yanapotokea hususan kwenye maeneo ya uzalishaji na viwanda.

  Katika hatua nyingine amelitaka shirika la umeme Tanesco,Dawasco kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya umeme na maji katika maeneo yenye uwekezaji ili kuvutia wawekezaji.

  Alitoa rai hiyo,wakati wa ziara yake ya siku moja ,aliyoifanya mkoani Pwani kutembelea kiwanda cha kutengeneza sabuni cha KEDS kilichopo Kibaha,na cha kutengeneza vigae Twyford Ceramics Ltd/Pingo,Chalinze ,Bagamoyo.

  Majaliwa ,alieleza kuwa ni lazima raia mmoja mmoja na jukumu la kila mmoja kusimamia kulinda nchi kuanzia maeneo wanayoishi .

  Alisema serikali imejipanga kuendelea kusimamia amani na utulivu,ambapo amewataka wananchi waiunge mkono serikali kupambana na wahalifu wasio na nia njema na serikali.

  “Hatuna uhakika kwa watu hawa wanaofanya vitendo vya ovyo,watanzan ia waungane na serikali,kupambana ili wasije kuingia kwa wawekezaji na kupoteza ndoto za serikali za kupata wawekezaji “alisema Majaliwa.

  Akizungumzia tatizo la uhaba wa maji ,alisema mradi wa WAMI ulikuwa ukamilike tangu mwezi July mwaka huu.

  Alisema alitembelea mradi huo mwezi juni mwaka huu ukiwa chini ya asilimia 38 na kusema mkandarasi akiendelea kusuasua watamfukuza na kutoa agizo ikifika mwezi huu wafikie asimilia 80.

  “Nilitaka kuja mwezi huu lakini nikaambiwa speed ni ndogo na bado hali hairidhishi,na mkandarasi hajamaliza”mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete amekuwa akiuliza juu ya kukwama kwa mradi huo” ;”Nimetoa wiki mbili kwa waziri aangalie dhamana ya kampuni kwenye ubalozi wao wa India na kuangalia sheria namna ya kufanya ama kukamilisha mradi kwa muda mfupi uliobaki”alifafanua.

  Kuhusu nishati ya umeme Majaliwa,alisema serikali ipo mbioni kutekeleza mradi mkubwa wa umeme stiegler’s gorge katika chanzo cha mto Rufiji, utakaozalisha megawatts 2,100 zitakazoondoa kama si kumaliza upungufu wa umeme uliopo.

  Aliitaka halmashauri ya Chalinze,ijipange kwa matumizi bora ya ardhi ili kuondoa migogoro na kuondoa usumbufu kwa wawekezaji.

  Kuhusu suala la zimamoto ,Majaliwa alisema mkoa huo kwasasa una viwanda vikubwa hivyo wakati serikali ikipokea changamoto ya uhaba wa vifaa na magari ya zimamoto ,halmashauri ijipange kupitia bajeti zao.

  “Viwanda hivi ni vikubwa vinajengwa ,kiwanda hiki cha KEDS kina jengo hilo hapo lenye urefu wa mita 30 juu,tuombe mungu moto usitokee ,unawezaje kuzima moto kwa maji ya kwenye ndoo ,ipo haja ya kuangalia namna ya kutatua changamoto hii”

  “Dar es salaam ambako ni mji wa kibiashara serikali itasaidia katika kununua mitambo ya kusaidia kuzima moto kutegemea ukubwa wa majengo yaliyopo”aliongeza Majaliwa.

  Kwa upande wa miundombinu ya barabara,alitoa rai kwa halmashauri ya Mji wa Kibaha kuboresha barabara zilizopita mitaani na kuhakikisha mitaa yote iwe na barabara bora kwa kufumua zisizofaa na kuchonga barabara zenye viwango.

  Pamoja na hayo ,Majaliwa alibainisha uwekezaji kama huu unaendana na dhana ya Rais Dk John Magufuli wa kuifanya nchi kuwa ya Viwanda ambapo itaongeza pato la nchi na itazalisha ajira kwa wingi.

  Aliwasihi vijana ambao tayari wana ajira kwenye viwanda hivyo kutumia nafasi walizozipata kwa kuchapa kazi .

  Majaliwa aliwaomba vijana hao kuchapa kazi na kuwathibitishia wawekezaji kuwa watanzania ni wachapazi na wana uwezo wa kufanyakazi viwandani na hakuna haja ya kuleta watumishi nje ya nchi.

  Nae mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo,alimwambia waziri mkuu ,kwamba mkoa huo unakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya barabara isiyo ya kuridhisha kwa wawekezaji.

  Alitaja changamoto nyingine kuwa ni upungufu wa nishati ya umeme isiyokidhi mahitaji kwani kwasasa mahitaji ni megawatts 73.2 na uliopo ni megawatts 40 ambao bado hautoshelezi.

  Mhandisi Ndikilo,alieleza tatizo la uhaba wa vifaa,vitendea kazi na magari kwa idara ya zimamoto na kuhofia endapo janga la moto likitokea kushindwa kuzima moto kwa wakati na kusababisha athari kubwa.

  Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ,alilalamikia uzembe na uvivu uliokubuhu katika utekelezaji wa mradi wa maji Chalinze (CHALIWASA).

  Alielezea kuwa,tatizo la maji limedumu kwa takribani miaka 13 sasa hali inayosababisha adha kwa wawekezaji na wananchi kijumla.

  Ridhiwani alisema ,haridhishwi na mwenendo wa mkandarasi wa ujenzi wa miundombinu ya maji katika mradi huo kutokana na kasi yake kuwa ni ndogo na haiendani na maagizo aliyoyatoa waziri mkuu hapo awali.

  Akiwa kiwanda cha KEDS ,mbunge wa jimbo la Mji wa Kibaha ,Silvestry Koka ,alimuomba Majaliwa kuangalia kwa jicho la tatu kero ya miundombinu isiyo rafiki kwa wawekezaji.

  Koka alisema wawekezaji wengi wanakimbilia kuwekeza mji wa Kibaha na mji huo upo usoni mwa barabara kuu ya Morogoro-Dar es salaam lakini bado kuna tatizo la barabara mbovu.

  Wakati huo huo ,mkurugenzi mkuu wa kiwanda cha KEDS na Twyford ,Jack Feng alisema asilimia 95 ya malighafi itakuwa inatoka hapa nchini .

  Alisema katika kiwanda cha KEDS wameshaajiri watu 200 huku wakitarajia kuajiri wafanyakazi 2,000 katika kiwanda hicho .

  ‘Ndani ya ujenzi huu kuna kiwanda kingine kikubwa ambacho tutazalisha bidhaa ya pempars na kiwanda kingine tutatengeneza misumali”alieleza Feng.

  Alisema hatua ya ujenzi ni nzuri imefikia asilimia 90 na wanategemea kuanza uzalishaji mwezi ujao,na utagharimu dola mil.200 hadi utakapokamilika.

  Feng alifafanua,kwenye kiwanda cha Twyford watarajia kuajiri wafanyakazi 4,000 hadi 6,000 mara watakapoanza kuzalisha mwezi Nov mwaka huu,sasa kuna wafanyakazi 1,200.

  Mkurugenzi huyo ,alieleza gharama ya mradi wa ujenzi wa kiwanda cha Twyford ni dola mil. 56 sawa na bilioni 120 na watauza vigae ndani ya nchi hadi nje ya nchi Zambia, Uganda, Rwanda na Burundi.

  0 0

  Madaktari Bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Evarist Nyawawa (kulia) na mwenzake Ajay Kaul (kushoto) wa  Hospitali ya BLK ya nchini India wakimfanyia mgonjwa leo upasuaji wa kuziba tundu la moyo.theater 2
  Madaktari Bingwa wa usingizi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anjela Muhozya na Sameer  Arora wa BLK  Hospitali ya nchini India wakizungumza jambo wakati wakimsubiri mgonjwa aandaliwe kwaajili  kuingia katika chumba cha upasuaji wa Moyo.theater 3
  Madaktari Bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya BLK ya nchini India wakimfanyia mgonjwa leo upasuaji wa kuziba tundu la moyo.theater 4
  Kazi ya upasuaji wa moyo kwa ajili ya kuziba tundu lililopo katika vyumba vya chini ya moyo ikiendelea.Picha na JKCI

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizngumza baada ya kutembelea kiwanda cha Sabuni cha KEDS wilayani  Kibaha September 19, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi, Evarest Ndikilo  na Kushoto  kwake ni Mkurugenzi Mtenaji wa kiwanda hicho, Jack Fen. Kulia ni Mbunge wa Kibaha Mjini Silyvestry Koka.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mifuko ya Sabuni ya unga aina ya Kleesoft wakati alipotembelea kiwand ia cha sabuni cha KEDS mjini Kibaha Septemba 19, 2017. Kulia kwakie ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo na kushoto kwake ni  Mkurugenzi Mtendaji wa  kiwanda hicho, Jack Fen. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha sabuni cha  KEDS wilayani  KIbaha  Sptemba 19, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi  Evarest Ndikilo na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Jack Fen. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha sabuni cha KEDS wilayani Kibaha, Bw. Jack Feni (Kushoto  kwake) kuhushu  mitambo ya  kiwanda hicho   hicho  wakati alipokitembela September 19, 2017.  Kulia kwake ni. Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mahandisi Evarest Ndikilo na kulia ni Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyvestry Koka.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) Dkt. Stephen Nindi (aliyesimama)akitoa maneno ya utangulizi kwa wadau wa Korido ya Mngeta na ukanda wa Magombela-Selous-Udzungwa wilayani Kilombero juu ya utafiti uliofanywa na wataalam kutoka Tume hiyo wakishirikiana na Asasi ya kiraia ya African Wildlife Foundation uliolenga maeneo ya uhifadhi wa Mazingira,Matumizi bora ya Ardhi, Hati miliki za Kimira na Bioanuai katika Korido ya Mngeta na ukanda wa Udzungwa-Mgombela-Selous, iliyofanyika Wilayani Kilombero.
   Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero (DAS)  Mh.Robert Selasela(aliyesimama) akifungua mkutano huo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Kilombero uliohusu uhifadhi wa Mazingira,Matumizi bora ya Ardhi, Hati miliki za Kimira na Bioanuai katika Korido ya Mngeta na ukanda wa Udzungwa-Mgombela-Selous
  Bw. Eugine Cylilo mtaalam kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi akitoa tathimini ya tafiti iliyofanywa na wataalamu kutoka Tume wakishirikiana na African Wildlife Foundation(AWF) ambayo ilionesha hali halisi ya usimamizi wa mipango ya Ardhi katika Korido ya Mngeta na ukanda wa Udzungwa-Mgombela-Selous juu ya,utunzaji wa Mazingira na Bioanuai,Mipango ya matumizi ya Ardhi na hati miliki za kimila na migogoro ya ardhi.
   Wadau wakimsikiliza Bw. Eugine Cylilo mtaalam kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi akiwasilisha utafiti huo.
   Bi. Jane Mkinga Afisa mradi wa jumuiko la maliasili Tanzania akichangia maswala juu ya maliasili
   Diwani wa kata ya Mngeta Mh. Flora Kigawa akitaka kupata ufafanuzi  wa changamoto za kutatua migogoro kati ya vijiji na pia kutaka kufahamu idadi ya wanawake wangapi wanamiliki ardhi katika wilayani Kilombero.
   Diwani wa Kata ya Chita Mh. Chelele John akiuliza maswala mbalimbali yahusuyo Ardhi.
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bi. Albina Burra akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali yaliyoulizwa na wadau kuhusu utunzaji wa Mazingira na Bioanuai,Mipango ya matumizi ya Ardhi na hati miliki za kimila na migogoro ya ardhi.
   Bw. Pastor Magingi Meneja wa Programu wa  asasi yakiraia ya African Wildlife Foundation akieleza namna walivyoshirikiana  NLUPC katika utafiti wa uhifadhi wa Mazingira,Matumizi bora ya Ardhi, Hati miliki za Kimira na Bioanuai katika Korido ya Mngeta na ukanda wa Udzungwa-Mgombela-Selous
   Muwezeshaji wa Mkutano huo Bw. Geofrey Siima akiendelea kutoa Muongozo wakati wa warsha hiyo.
   Afisa Miradi kutoka asasi ya Kiraia ya Solidardad Bi. Maria Sengelela akitoa maelezo ya namna wanavyoshirikiana na NLUPC katika swala zima la matumizi bora ya Ardhi.
  Afisa Sheria wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi Bi. Devotha Salukele akijibu Maswala mbali mbali yahusuyo sheria yaliyoulizwa na wananchi kuhusu Ardhi.
  Afisa Ardhi Mteule kutoka Wilaya  Kilombero Bi. Syabumi Mwaipopo akifafanua na  kujibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wadau wakati wa mkutano huo.
   Afisa Mipango wa Wilaya ya Kilombero Bw. Ludwing Ngakoka akizungumza jambo wakati wa Mkutano huo
   Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Mh. David Lugazio akitoa neno la Shukurani baada ya Mkutano huo kumalizika.
  Wajumbe mbalimbali wakiendelea kufuatilia mkutano huo
  Picha ya pamoja 


  Katika kuhakikisha kuwa kuna mipango na matumizi bora ya ardhi nchini Tanzania, Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi kwa kushirikiana na Asasi ya Kiraia ya African Wildlife Foundation (AWF) walifanya utafiti wa uhifadhi wa Mazingira,Matumizi bora ya Ardhi, Hati miliki za Kimila na Bioanuai katika korido ya Mngeta na ukanda wa Udzungwa-Mgombela-Selous Wilayani Kilombero.

  Akizungumza wakati wa kuwasilisha utafiti huo kwa Madiwani, Watendaji Wilaya, Tarafa na Kata, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya matumizi ya Ardhi (NLUPC) Dkt. Stephen Nindi alisema kuwa Tume ilifanya utafiti katika ushoroba wa Mngeta pamoja na ukanda wa Udzungwa-Magombela-Selous lengo likiwa ni kuangalia mambo mbalimbali yanayohusu matumizi bora ya Ardhi, umiliki wa ardhi, uhifadhi ya mazingira na Bioanoai katika maeneo hayo.

  Mkurugenzi Mkuu alidokeza kuwa Wilaya ya Kilombero ni moja ya Wilaya tajiri katika nchi ya Tanzania ambayo ina ardhi yenye rotuba kubwa inayofaa kwa kilimo cha aina mbalimbali pamoja na uoto wa aina mbalimbali “Kuna matumizi ya aina mbalimbali ya ardhi katika Wilaya hii, tuna wakulima, wawekezaji wakubwa katika kilimo, wawekezaji wakubwa katika misitu, hifadhi ya wanyama pori, kilomo cha kati na kilimo cha wakulima wadogo wadogo, wafugaji, wavuvi, wafanya biashara ambao kwa umoja wanatengeneza ubia mbalimbali katika matumizi ya Ardhi” alisema Dkt. Nindi.

  Aliongeza kuwa lengo la utafiti huu ilikuwa kuangalia wadau mbalimbali katika utumiaji, upangaji na usimamizi wa ardhi wanatekelezaje, kuangalia changamoto za mipango ya matumizi ya Ardhi, umiliki wa ardhi,uhifadhi wa mazingira na Bioanoai.

  “Tupo hapa kwa ajili ya kuwasilisha utafiti wetu kwamba namna gani mambo haya yanafanyika shughuli hizi za uhifadhi wa mazingira na Bioanoai, Shughuli za upangaji na matumizi ya Ardhi, umiliki wa Adhi pamoja na utekelezaji wake na usimamizi zinavyofanyika katika kanda hizi mbili” alisema Dkt. Nindi.

  Akiwasilisha matokeo ya utafiti huo, mtaalamu wa mazingira kutoka Tume bwana Eugen Cyrilo, alibainisha changamoto kadhaa matumizi ya ardhi, umiliki pamoja na uhifadhi wa mazingira. “Changamoto kubwa iliyobainika katika utafiti huu, ni utekelezaji wa maipango ya matumizi ya ardhi. Vijiji vingi tulivyopitia vimeandaliwa mipango ya matumizi ya ardhi, ila kwa kuwa hakuna usimamizi wa mipango hiyo kwa ngazi ya vijiji, kunakuwa hakuna utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi waliojitengea” alieleza bwana Cyrilo.

  Aidha, katika upande wa mazingira, ilibainika kuwa kumekuwa usimamizi usioridhisha hasa kwenye misitu na vyanzo vya maji kwa baadhi wanavijiji wenyewe au watu kutoka nje ya vijiji kuvamia na kuweka makazi kwenye misitu ikiwa pamoja na kukata miti bila utaratibu. “Kwenye baadhi ya maeneo, kumekuwa na uvamizi wa misitu ambapo hapo awali ilikuwa imetengwa kwa ajili ya uhifadhi, na sehemu zingine tulikuta wanavijiji wakifanya shughuli ambazo si rafiki kwa mazingira pembezoni mwa mito, hii ni tishio kubwa katika utunzaji wa mazingira” alisema bwana Cyrilo.

  Akichangia katika matokeo ya utafiti huo, Meneja wa Programu kutoka AWF bwana Pastor Magingi aliwasihi uongozi wa Wilaya kuja na suluhisho la kusimamia mipango ya matumizi ya ardhi ili kufanya kazi nguvu kubwa inayofanywa na na Tume, Wadau pamoja na Halmashauri yenyewe isipotee bure.

  Hatua hii iliwapelekea Madiwani wa Kata zilizohusika kwenye utafiti huu kupendekeza kuwapo kwa mtaalamu wa Wilaya atakayehusika moja moja na kusimamia utekelezakji  wa mipango ya matumizi ya ardhi katika Wilaya ili kutoa ripoti ya mara kwa mara juu ya usimamaizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ili kuwa endelevu na yenye manufaa kwa wananchi.

  Utafiti huo ulihusisha Kata nne za ukanda wa Udzungwa-Magombera-Selous, ambazo ni Msolwa Stesheni, Mkula, Mang'ula B na Sanje pia kulikuwa na vijiji nane vya Msolwa Stesheni, Mkula, Sonjo, Msufini,Katurukila, Kanyenja, Magombera na Sanje. Aidha katika korido ya Mngeta utafiti huo ulihusisha kata sita za Namawala, Igima, Mbingu, Mngeta, Chita na Mofu pamoja na Vijiji  vya Mofu, Ihenga, Kisegese, Vigaeni, Makutano, Igima, Mbingu, Njage, Mngeta, Mchombe na Lukolongo.

  0 0

  KAMPUNI ya Puma Enegy Tanzania, imehitimiza mashindano ya uchoraji picha za usalama barabarani kwa shule za Msingi kwa mwaka 2017 kwa kutoa kutoa zawadi ya Sh milioni 2 kwa mshindi wa kwanza. 

  Akizungumza jijini Dar e Salaam jana Mkurugenzi Mkuu wa Puma Enegy Tanzania Ltd, Philippe Corsaletti, alisema kuwa mashindano ya mwaka huu yalihusisha jumla ya shule 14 za mikoa ya Dar es Salaam na Kilimanjaro ambapo washindi hao walipatikana jana. 

  Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza aliyeibuka ni Nasri Mwema wa Shule Msingi Amani katika shindano hilo lililoshirikisha shule 14. 

  “Mshindi huyu wa kwanza atapata kikombe na cheti ambapo shule anayotoka itapata fedha Shilingi milioni 2 ambazo zitatumika kwa ajili ya kununulia vitabu. Shindano hili la usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi kwa njia ya uchoraji linalenga kusaidia kuelimisha wanafunzi wa shule za msingi katika masuala ya usalama barabarani. 

  “Mpango wetu wa usalama barabarani kwa shule hapa nchini Tanzania ulianza tangu mwaka 2013 na mpaka sasa shule za msingi zipatazo 47 zimeshashiriki zikiwa na jumla na wanafuzni 60,000 kutoka mikoa mbalimbali,” alisema Corsaletti 

  Mkurugenzi huyo wa Puma Enegy, alisema kuwa shindano hilo la usalama barabarani kwa njia ya uchoraji linalenga kumpatia kila mwanafunzi nafasi ya kushirikisha mawazo yake juu ya namna bora ya kuboresha usalama barabarani ambapo kati yao huchaguliwa washindi na kuzawadiwa. 

  “Lengo letu la muda mrefu ni kufikia shule zote hapa nchini ziweze kushiriki katika mpango huu. Kampuni ya Puma Enegy imekuwa ikishirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani pamoja na SUMATRA katika masuala mbalimbali yahusuyo usalama barabarani. 

  “Tunaamini kwamba ajali za barabarani zinaweza kupungua kwa kiasi kikubwa ikiwa pande zote zinazohusika ambazo ni pamoja na madereva, wenye magari na wasimamizi wakitekeleza wajibu wao ipasavyo. Jukumu letu pamoja linabaki kuwa wajibu shirikishi katika kutengeneza mazingira salama kwa ajili ya watoto wetu na vizazi vijavyo,” alisema alisema 

  Naye Msajili wa Hazina, Dk. Osward Mashindano, alisema kilichofanywa na Kampuni ya Puma ni jambo jema ambalo litasaidia katika kuiandaa jamii kuepuka ajali za barabarani.

  Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu (kushoto), akimwangalia Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Amani, Nasri Mwema baada ya kumkabidhi tuzo ya kuwa mshindi wa kwanza kwa kuchora vizuri picha inayoelezea athari za usalama barabarani katika hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya Uuuzaji Mafuta ya Puma Energy katika Shule ya Msingi Diamond Dar es Salaam leo. Mashindano hayo yanadhaminiwa na Puma Energy Tanzania. Kulia ni Msajiri wa Hazina, Oswald Mashindano na Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Phillipe Corsaletti. 

  Mwanafunzi Nasri Mwema akipokea tuzo kutoka kwa Msajiri wa Hazina , Oswald Mashindano (kulia),.Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Puma, Phillipe Corsaletti.
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Puma, Phillipe Corsaletti akipongezana na Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu 
  Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu na viongozi wengine wakishiriki kuteua picha bora tatu zilizochorwa na wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi Mkoa wa Dar es Salaam.
  Mwanafunzi George Jonas wa Shule ya Msingi Upendo akikabidhiwa begi na madaftari yenye alama za usalama barabarani baada ya kuwa mshindi wa tatu katika mashindano hayo
  Mshindi wa pili wa shindano la uchoraji wa picha za kuonesha athari za usalama barabarani, Rehema Mzimbili wa Shule ya Msingi Buza, Temeke, Dar es Salaam, akipokea vifaa vyake vya shule.
  Mshindi wa Kwanza Nasri Mwema akiwa katika picha ya pamoja na viongozi  baada ya kukabidhiwa zawadi ambapo pia Shule yake ya Amani ilizawadiwa  sh. mil. 2.
  Kamanda Musilimu akionesha picha iliyoshinda katika mashindano hayo
  Washindi kwakiwa katika picha ya pamoja
  Washindi wote watatu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi pa walimu wao   Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu (kushoto), akimwangalia Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Amani, Nasri Mwema baada ya kumkabidhi tuzo ya kuwa mshindi wa kwanza kwa kuchora vizuri picha inayoelezea athari za usalama barabarani katika hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya Uuuzaji Mafuta ya Puma Energy katika Shule ya Msingi Diamond Dar es Salaam leo. Mashindano hayo yanadhaminiwa na Puma Energy Tanzania. Kulia ni Msajiri wa Hazina, Oswald Mashindano na Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Phillipe Corsaletti. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA Mwanafunzi Nasri Mwema akipokea tuzo kutoka kwa Msajiri wa Hazina , Oswald Mashindano (kulia),.Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Puma, Phillipe Corsaletti. Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Puma, Phillipe Corsaletti akipongezana na Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu na viongozi wengine wakishiriki kuteua picha bora tatu zilizochorwa na wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi Mkoa wa Dar es Salaam. Mwanafunzi George Jonas wa Shule ya Msingi Upendo akikabidhiwa begi na madaftari yenye alama za usalama barabarani baada ya kuwa mshindi wa tatu katika mashindano hayo Mshindi wa pili wa shindano la uchoraji wa picha za kuonesha athari za usalama barabarani, Rehema Mzimbili wa Shule ya Msingi Buza, Temeke, Dar es Salaam, akipokea Mshindi wa Kwanza Nasri Mwema akiwa katika picha ya pamoja na viongozi baada ya kukabidhiwa zawadi ambapo pia Shule yake ya Amani ilizawadiwa sh. mil. 2. Kamanda Musilimu akionesha picha iliyoshinda katika mashindano hayo Washindi wote watatu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi pa walimu wao

  Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap

older | 1 | .... | 1371 | 1372 | (Page 1373) | 1374 | 1375 | .... | 1897 | newer