Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1369 | 1370 | (Page 1371) | 1372 | 1373 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,akionyesha eneo la mradi litakapozalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Dam),ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawatts 2,100 za umeme.(Picha na Mwamvua Mwinyi )
  Eneo la mradi litakapozalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Dam),ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawatts 2,100 za umeme,linavyoonekana .
  Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mloka kilicho karibu na pori la akiba la Selou .

  Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,na ujumbe wake wakikagua eneo la mto huo.(Picha na Mwamvua Mwinyi )  Na Mwamvua Mwinyi ,Rufiji

  Wakazi wa wilaya ya Rufiji ,Mkoani Pwani pamoja na watanzania kijumla wanatarajia kunufaika na mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (stiegler’s gorge hydropower dam project),ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawatts 2,100 .

  Mradi huo utazalishwa kutoka chanzo hicho , katika pori la akiba la Selou Kanda ya Kaskazini (Matambwe ).Kwasasa nchi inazalisha megawatts 1,450 lakini Stiegler’s gorge itazalisha megawatts 2,100 hali itakayoleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi .

  Akizungumza mara baada ya kwenda kukagua na kujiridhisha eneo utakapozalishwa mradi huo kabla ya utekelezaji kuanza,Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo, alisema tangazo rasmi limeshatolewa na wizara ya nishati na madini tangu august 30 mwaka huu.

  Aidha alifafanua ,tangazo hilo linawapa nafasi kwa makampuni ya ujenzi wa mabwawa ya maji ya kuzalisha umeme .Mhandisi Ndikilo,alibainisha kampuni yoyote iwe ya ndani ama nje ya nchi ikikidhidhi vigezo itatangazwa .
  Alieleza endapo mradi utakamilika utawezesha kuwepo kwa umeme wa uhakika na kuvutia wawekezaji kwa wingi.Mhandisi Ndikilo ,alisema wilaya ya Kisarawe na baadhi ya maeneo ya wilaya ya Kibiti na Rufiji umeme ukatikakatika hivyo kuna changamoto ya upungufu wa umeme hali inayokwamisha jitihada za kuinua sekta ya uwekezaji na viwanda .

  “Tatizo la umeme bado ni kubwa mkoani hapa licha ya mkoa huu kusheheni viwanda “Mradi umekuja muda muafaka ambapo mkoa huo umejipanga kuwa ukanda wa viwanda ” alifafanua .

  Faida moja wapo ya mradi ni kuwa na maji mengi ya kunywa na viwandani kwa mikoa ya Pwani ,Dar es salaam na Morogoro ,utaliii ,maji kwa ajili ya wanyama pori na kilimo .

  Mhandisi Ndikilo alieleza ,mradi umekuja muda muafaka na umefika mahala pake ,ambapo Mkoa huo umejipanga kuwa ukanda wa viwanda .“Ni nia ya serikali ya awamu ya tano kuhakikisha mawazo ya baba wa taifa hayati mwl .Julius Nyerere ya tangu mwaka 1980 juu ya kuzalisha umeme kutoka katika maporomoko ya mto huo yanatekelezwa kwa haraka iwezekanavyo “alisema mhandisi Ndikilo .

  Baada ya kutembelea eneo la mradi mhandisi Ndikilo ,alipata fursa ya kwenda kuzungumza na wakazi wa kijiji cha Mloka kilicho mpakani na pori la akiba la Selou .Mhandisi Ndikilo, alisema ujenzi wa mradi huo utafungua milango ya kiuchumi na ujasiriamali na kibiashara .

  Kwa upande wa wakazi wa Mloka ,Ikwiriri na Kibiti waliliridhia na kuonyesha kukubali maendeleo wanayosogezewa .Mkazi wa Mloka ,mzee Mbonde ,alisema alikuwepo enzi za hayati baba wa taifa mradi ulipofanyiwa tathmini na wa Norway.

  Mzee Mbonde na bibi Fatuma Majengo walimpongeza mh rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli kwa kubeba mzigo .Walisema kwa mwanzo huu ,Dk.Magufuli atatatua tatizo la uhaba wa umeme.

  Eneo litakalotumika kujenga mradi ni kilometa za mraba 1,350 ambalo ni sawa na asilimia tatu pekee ya eneo lote la pori la akiba la Selou yenye ukubwa wa km za mraba 50,000 .

  Mkuu wa pori hilo la akiba la Selou kanda ya kaskazini (Matambwe)Lawrence Okode ,alisema katika historia jina la Stiegler’s gorge limetokana na mjerumani aliyefariki katika eneo hilo aliyejulikana kwa jina la Stiegler’s baada ya boti yake kugonga jiwe kubwa na kusababisha umauti wake .

  0 0

  Afisa wa Ubalozi wa Marekani anayeshughulikia masuala ya umma Bi. Brinille Ellis aliwakaribisha wanafunzi, wazazi na walimu zaidi ya 100 katika Shule ya JOMAK School iliyopo huko  Bahari Beach katika mahafali ya washiriki wa programu ya mafunzo ya Kiingereza inayofadhiliwa na Ubalozi iitwayo “English Access Microscholarship Program”.  
  Wanafunzi wapatao 25 wa vidato vya tatu, nne na tano walianza kuhudhuria mafunzo yao ya Kiingereza baada ya masomo ya kawaida shuleni katika shule ya JOMAK hapo mwezi Septemba mwaka 2015.  Hawa watakuwa kundi la kwanza la wahitimu wa programu hii jijini Dar es Salaam. Serikali ya Marekani inafadhili madarasa mengine matatu hapa nchini chini ya programu hii.  Hii ni pamoja na darasa la pili katika shule ya JOMAK na madarasa mawili mjini Moshi yanayoendeshwa na taasisi iitwayo Kilimanjaro Information Technology. Inatarajiwa kuwa madarasa mengine yataanza mwezi Januari 2018 katika miji ya Mwanza, Tanga and Zanzibar. 

  Bi. Ellis aliwapongeza wanafunzi wa programu hii kwa kujitoa kwao kwa dhati na kushiriki kikamilifu katika mafunzo yao: “Kwa kupitia programu ya Access mmepata mambo mengi zaidi ya ujuzi wa lugha ya Kiingereza. Mmekuwa viongozi wa jamii na mfano wa kuigwa katika jamii zenu.” Wakati wa hafla hii, wanafunzi walifanya maonyesho na kutambulisha kwa Kiingereza miradi na kazi mbalimbali za kuhudumia jamii walizozifanya wakati wa mafunzo yao katika programu hii. 

  Programu ya Access hutoa mafunzo ya msingi ya lugha ya Kiingereza kwa watoto na vijana wenye vipaji wa kuanzia miaka 13 hadi 20 kutoka jamii zenye hali duni kiuchumi kupitia madarasa yanayoendeshwa baada ya muda wa shule na yanayotoa mafunzo ya kina.  Programu ya Access huwapatia washiriki wake stadi za lugha ya Kiingereza jambo ambalo huwapa fursa zaidi za kielimu na ajira.  Toka mwaka 2004, zaidi ya wanafunzi 200 kutoka Tanzania na 100,000 kutoka zaidi ya nchi  85 wameshiriki katika programu hii.

  0 0

  0 0

  Sehemu ya vijana wa Kijiji cha Manghungu, Kata ya Vinghawe Halmashauri ya Mpwapwa mkoani Dodoma wakishiriki kazi ya kuchimba Lambo kwa kutumia nguvu zao wenyewe. 
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akishiriki kuchimbua eneo la Lambo la Kijiji cha Manghungu, Kata ya Vinghawe Halmashauri ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Bw. Mohamed Maje akiweka mchanga kwenye ndoo katika zoezi la uchimbaji wa Lambo Kijijini cha Manghungu.
  Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Manghungu, kata ya Vinghawe Halmashauri ya Mpwapwa mkoani Dodoma wakishiriki kazi ya kuchimba Lambo kwa kutumia nguvu zao wenyewe.
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akikabidhi nyundo nzito kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Manghungu, kata ya Vinghawe Halmashauri ya Mpwapwa mkoani Dodoma Bw. Sospeter G. Nyaombo kuwezesha kazi ya uchimbaji wa Lambo.
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akikabidhi jembe kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Manghungu, Kata ya Vinghawe Halmashauri ya Mpwapwa mkoani Dodoma Bw. Sospeter G. Nyaombo kuwezesha kazi ya kuchimba Lambo la maji kijijini hapo.
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akikabidhi chepeo kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Manghungu, Kata ya Vinghawe Halmashauri ya Mpwapwa mkoani Dodoma Bw. Sospeter G. Nyaombo wakati wa kushiriki uchimbaji wa lambo kijijini hapo. 
  Afisa Mtendaji wa Kijiji cha cha Manghungu, Kata ya Vinghawe Halmashauri ya Mpwapwa mkoani Dodoma Bw. Sospeter G. Nyaombo akionesha moja ya ndoo zilizotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jmaii, Jinsia Wazee na watoto kuwezesha kazi ya uchimbaji wa Lambo. 
  Mratibu wa masuala ya Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI Bibi Mwajina Lipinga akijumuika na akinamama kuimba wimbo wa kuhamsha ari ya kuchimba Lambo la maji ya kunywa wakati alipotembelea Kijiji cha Manghungu ,Kata ya Vinghawe Halmashauri ya Mpwapwa mkoani Dodoma.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW  Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

  Serikali imeadhimia kuwa Sera ya Maendeleo ya Jamii ya mwaka 1996, inatekelezwa kikamilifu na inafuatilia utekelezaji wa Sera hiyo katika ngazi ya mikoa, Wilaya, Kata na Vijiji mbalimbali hapa nchini.

  Akiongea na wananchi wa Kijiji cha Manghangu, kilichoko Kata ya Vinghawe Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike amesema Sera hiyo imeweka wazi kuwa wananchi ndiyo kitovu cha maendeleo maana ushiriki wao unatoa dhamana thabiti ya maendeleo na ustawi wa wananchi katika ngazi mbalimbali.

  Bw. Patrick Golwike ametanabaisha kuwa lengo la kufika katika Kijiji hicho ni kushirikiana na wananchi kufanya kazi za maendeleo kwa vitendo.

  “Kazi ya kuhamsha ari iliyobuniwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inalenga kuhamasisha wananchi kushiriki katika kuibua miradi, kupanga, kutekeleza na kusimamia shughuli za maendeleo kwa kutumia rasilimali zilipo katika mazingira yao ili kujiletea maendeleo yao” alisema Bw. Golwike.

  Kwa upande wake Mratibu wa masuala ya Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI Bibi Mwajina Lipinga, alisema kuwa mradi wa ujenzi wa lambo la maji, na ushiriki wa wananchi katika kazi za kujitolea utakuwa chachu kwa vijana kuhamsha ari ya kujitolea na kuchangia maendeleo ya vijiji na Taifa.

  “Kazi hii inayofanyika naomba iwe chachu kwa mikoa mingine ipende kuhamsha ari na kwa kufanya kazi kama kipimo cha heshima na utu wa mtu” alisema Bibi Lipinga.

  Aliongeza kuwa, wananchi wanapoona Serikali na wadau wanajitokeza kusaidia kufanya kazi fulani, jamii nayo inawajibu wa kujitokeza katika kushughulikia changamoto zilizopo ili kupata majawabu yenye ufumbuzi wa matatizo hayo kwa manufaa ya wanachi wote.

  Akiongea katika zoezi la uchimbaji wa lambo hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpwapwa Bw. Mohamed A. Maje ameahidi kuendeleza kazi ya kushirikiana na jamii katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kutumia nguvu za wananchi.

  “Nitaandaa matukio mengine mawili ya kuamsha ari ya wananchi kufanya kazi za maendeleo yao ambayo yatasimamiwa na Halmashauri ili kurejesha ushiriki wa wananchi katika kazi za kujitolea” alisema Bw. Maje.

  Naye Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Manghangu Bw. Sospeter G. Nyaombo alishukuru Wizara kwa kufika kijijini na kutoa msaada wa vifaa vya uchimbaji wa Lambo pamoja na kushirikiana kazi kwa vitendo.

  “Kufika kwenu katika kijiji chetu kumekuwa chachu ya kuchangia maendeleo katika kijiji chetu na maeneo mengine nchini” alisema Bw.Nyaombo.

  Vifaa vilivyotolewa na Wizara ni pamoja na majembe 27, chepeo 5, nyundo 3, na ndoo 10.

  Mradi wa uchimbaji wa Lambo la maji safi umekadiriwa kukamilika katika kipindi cha siku 15. Chanzo hiki cha maji kitanufaisha kaya zipatazo 538, wananchi 2297, kati yao wanaume wakiwa 983 na wanawake 1314.

  0 0

  Askari Pilisi wakiwa tayari kwa kazi katika moja ya magari 18 yaliyokamilika kwa ukarabati kati ya magari 26 yaliyopelekwa kwenye Gereji la RSA mjini Moshi na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda kwa matengenezo makubwa wakati alipoyakagua leo mkoani Kilimanjaro.
  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akikagua moja ya magari 18 kati ya 26 ya polisi Dar es salaam yaliyopelekwa mjini Moshi katika Gereji ya RSA kwa matengenezo makubwa Mkuu wa mkoa huya ameyakagua magari hayo na atakabidhiwa magari 18 ambayo yamekamilika.
  Baadhi ya magari ambayo tayari yamekamilika kwa matengenezo.  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda jana  ametembelea na kukagua Ukarabati wa Magari 26 ya Polisi yaliyopelekwa Mkoani Kilimanjaro yakiwa Mabovu kwaajili ya kukarabatiwa na kubadilishwa Mwonekano ambapo hadi sasa Magari 18 yapo hatua ya mwisho kukamilika.

  Magari hayo ambayo yalipelekwa Moshi yakiwa Chakavu kwa sasa baadhi yanatembea ambapo yamepakwa Rangi huku yakifungwa vifaa mbalimbali ikiwemo Magurudumu Mapya, Taa,Vioo,Bodi, Side Mirrow na vifaa vingine muhimu.

  Makonda amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa na kusema kuwa atakabidhiwa Magari hayo mwanzoni mwa mwezi October ili ayakabidhi kwa Jeshi la Polis.Amesema Magari hayo yenye mwonekano kama yale ya UN yatakuwa na uwezo wa kubeba Askari Tisa nyuma wakiwa wamekaa ambapo Watatu watakuwa wakitazama Nyuma, Watatu Kushoto, Watatu Kulia na Mmoja Mbele wote wakiwa wamebeba silaha.

  Aidha Makonda amesema kupatikana kwa Magari hayo yatasaidia kupunguza vitendo vya Uhalifu kwa Wananchi.RC Makonda amesema kuwa lengo lake ni kuona hakuna Mwananchi yoyote anaeibiwa au kuporwa kitu.

  Hata hivyo amesema Baadhi ya Askari walikuwa wakipoteza maisha na kuporwa Silaha kutokana na aina ya Magari waliyokuwa wakitumia kutowapa uwezo wa kukabiliana na wahalifu hivyo Magari hayo yatamaliza matukio hayo.

  Ameishukuru kampuni ya RSA Limited kwa kumuunga mkono kwa kujitolea kukarabati Magari 56 ya Jeshi la Polisi kwa kuyafanya kuwa ya kisasa na Mapya.Sanjari na hayo amesema Magari hayo yataenda kufanya Doria kwa masaa 24.

  Nae Mkurugenzi wa Kampuni ya RSA Bwana Manmohan Bhamra amesema kwa sasa Magari hayo ni sawa na Mapya kwakuwa yamewekwa vifaa vipya.
  Amesema Magari yote watayakabidhi kwa wakati iliyakaongeze tija katika kuimarisha Ulinzi na Usalama kwa Wananchi.

  0 0

  KAMPENI ya Uzalendo Kwanza iliyoanzishwa na Wasanii wa Filamu nchini, a.k.a Bongo Muvi inazidi kupanua wigo wake baada ya kuongeza matawi yake kwa mikoa yote ya Tanzania huku ikipata wanachama wakongwe waliowahi kutamba ndani ya Soka hapa nchini. 

  Akizungumza na wanahabari wakati akiwapokea wanachama wapya, Mwenyekiti wa Chama hicho, Steve Mengele 'Steve Nyerere' amesema kuwa, lengo la Chama hicho ni kuwafikia Watanzania wote kufahamu umhimu wa uzalendo, kuipenda nchi yako ikiwa ni pamoja na kushirikiana kikamilifu na Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt John Pombe Magufuli katika kumuunga mkono wa kizalendo katika kuhakikisha Tanzania inasonga mbele kimaendeleo. 

  "Taifa la wazalendo linaanzia darasani, tunawaomba walimu wote wawe wazalendo kufundisha darasani, manesi na madakatari wawe wazalendo kutoa huduma zao, uzalendo pia ni mhimu kusapoti vilabu vyetu vya soka na Timu ya Taifa,na Wasanii wetu wa muziki ni lazima wawe wazalendo kwa kuitangaza nchi yao kwa mambo ya Kizalendo," alisema Nyerere. 

  Wacheza soka ambao wamejiunga na Uzalendo Kwanza ni; Mwanamtwa Kihwelo, Monja Liseki, Abdallah Kaburu, Dotto Mokili na wengine.Aidha Nyerere amewaasa wanachama hao na Watanzania wote kuunganisha nguvu ya pamoja ili kulinda kazi zao za sanaa sambamba na kuwafanya Watanzania kupenda vilvivyo vyao mfano, kazi za wasanii wa ndani ili kukuza kipato chao na kuinua uchumi wa nchi. 

  Mbali na hao, msanii wa Bongo Fleva, atambulikae kwa jina la Ruby pia amejiunga na kampen ya Uzalendo Kwanza,Msanii huyo amepewa jukumu la kutunga nyimbo za Uzalendo na video zake ili kufikisha ujumbe kwa wananchi wote.

  Katika hatua nyingine,Uongozi wa Uzalendo kwanza umetoa msaada wa vyakula mbalimbali na kiasi cha fedha tasilimu Laki tano kwa aliyewahi kuwa mpiga picha wa Magazeti ya Serikali (Habari Leo &Daily News),Athuman Hamis ambaye alipata ulemavu wa kudumu kufuatia ajali aliyoipata akiwa kwenye majuku yake ya Kazi ikiwa yapata miaka kumi sasa tangu kutokea kwa tukio hilo.

  Steve Nyerere amemaliza kwa kuwaasa Wasanii wenzake kuendelea kuwa Wazalendo na kuwakumbusha kujiunga katika mifuko ya hifadhi ya kijamii,amesema kuwa mfuko wa hifadhi ya Jamii PPF wameanza kwa kuidhamini kampeni yao ya Uzalendo Kwanza,huku wakionesha utayari mkubwa wa kuwasaidia iwapo wataamua kuendelea kujiunga katika mfuko huo na ukawa mkombozi kwao.
  Mmoja wa Mabalozi wa Kampeni ya Uzalendo Kwanza akiwasili kwenye mkutano,Athuman Hamis aliyewahi kuwa mpiga picha wa Magazeti ya Serikali (Habari Leo &Daily News), ambaye alipata ulemavu wa kudumu kufuatia ajali aliyoipata akiwa kwenye majuku yake ya Kazi ikiwa yapata miaka kumi sasa tangu kutokea kwa tukio hilo.
  Mwenyekiti wa kampeni ya Uzalendo kwanza Steve Mengele almaarufu kwa jina la Steve Nyerere akimkabidhi bahasha yenye kiasi cha fedha shilingi laki tano pamoja na msaada wa vyakula mbalimbali kwa aliyewahi kuwa mpiga picha wa Magazeti ya Serikali (Habari Leo &Daily News),Athuman Hamis ambaye alipata ulemavu wa kudumu kufuatia ajali aliyoipata akiwa kwenye majuku yake ya Kazi ikiwa yapata miaka kumi sasa tangu kutokea kwa tukio hilo.
   Mwenyekiti wa kampeni ya Uzalendo kwanza Steve Mengele almaarufu kwa jina la Steve Nyerere akimnyanyua Mzee Rajab Shabani mkazi wa Mburahati ambaye ni mlemavu wa miguu (kwa miaka mitano sasa),kumkalisha kwenye kiti cha matairi matatu (Wheel chair),ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na Wadau wa kampeni hiyo wakishirikiana na uongozi wa kampeni ya Uzalendo kwanza. 
  Pichani kati ni Mwenyekiti wa kampeni ya Uzalendo Kwanza , Steve Mengele 'Steve Nyerere' akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini dar,wakati akiwapokea wanachama wapya walioamua kujinga na kampeni hiyo.Pichani kulia ni Mjumbe Halima Yahya na kushoto ni Misayo Ndumbagwe. 
  Pichani kati (njano) Mwenyekiti wa kampeni ya Uzalendo Kwanza , Steve Mengele 'Steve Nyerere' akiwatambulisha wanamichezo wazalendo wa zamani katika Soka na Waigizaji wengie mahiri mbele ya Waandishi wa habari mapema leo jijini dar,walioamua kujiunga na kampeni hiyo ya Uzalendo Kwanza.
  Pichani Kati ni Msanii wa bongofleva Hellen Majeshi a.k.a Ruby ambaye pia ametangazwa kujiunga na kampeni hiyo ya Uzalendo Kwanza. 
  Baadhi ya Wasanii mbalimbali wa Bongo movie wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo na Waandishi wa Habari uliofanyika mapema leo,jijini Dar.

  Baadhi ya Wasanii mbalimbali wa Bongo movie wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo na Waandishi wa Habari uliofanyika mapema leo,jijini Dar.

  0 0


  Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Roma Mkatoliki na Stamina(Rostam) wakitumbuiza kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma Mkoa wa Mara,kwenye tamsha la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana.


  Meneja wa Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi Tigo kanda ya Ziwa Edgar Mapande,akizungumza na waandishi wa habari, kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma Mkoa wa Mara,kwenye uzinduzi wa tamsha la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana .
  Fareed Kubanda "Fid q akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta katika uwanja wa Karume mkoani Mara.
  Jux akitumbuiza maelfu ya wakazi wa Musoma Katinka jukwaa la Tigo Fiesta
  Mr Blue naye alikuwa katika list ya wasanii walitoa burudani katika jukwaa la Tigo Fiesta .
  Nandy akitumbuiza kaaika jukwaa la Tigo Fiesta mapema jana katika uwanja wa karume Mkoani Mara.
  Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa(aliyevaa koti la suti) akizindua tamasha la Tigo Fiesta, kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma Mkoani humo usiku wa kuamkia jana .
  Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa(aliyevaa koti la suti) akicheza mziki wakati wa uzinduzi wa tamasha la Tigo Fiesta, kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma Mkoani humo usiku wa kuamkia jana .
  Msanii wa nyimbo za kitamaduni Saida Karoli, akitumbuiza kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma Mkoa wa Mara,kwenye tamsha la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana .


  Msanii wa nyimbo za kitamaduni Saida Karoli, akitumbuiza kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma Mkoa wa Mara,kwenye tamsha la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana  Weusi wakitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta
  Chege akilishambulia jukwaa la tigo Fiesta usiku wa kuamkia leo mjini Musoma

  Wakazi wa Musoma mjini na maeneo ya jirani wakifurahia burudani ya tamasha la Tigo Fiesta, kwenye uwanja wa Karume mkoani Mara usiku wa kuamkia jana.

  0 0


  Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation,Ernest Sungura akikabidhi tuzo Tuzo ya Uandishi wa Kishujaa na Ulitukuka ya Daudi Mwangosi mwaka 2017 kwa Afisa Mahusiano kutoka Clouds Media Group Simalenga Simon leo Jumamosi Septemba 16,2017 mkoani Tanga-Habari/Picha na Oscar Assenga na Kadama Malunde.

  Jopo la Majaji Tuzo ya Uandishi wa Kishujaa na Ulitukuka ya Daudi Mwangosi mwaka 2017 limeitangaza Clouds Media Group kuwa mshindi wa Tuzo hiyo kwa mwaka 2017. Tuzo hiyo imetolewa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC wakati wa mkutano wake mkuu wa unaofanyika katika ukumbi wa Tanga Beach Resort mkoani Tanga.

  Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa uongozi wa Clouds Media Group na Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation,Ernest Sungura. Mbali na kupewa tuzo hiyo,pia Clouds fm imekabidhiwa hundi ya shilingi milioni 10 kama pole kwa changamoto waliyopitia baada ya kituo cha matangazo kuvamiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda aliyekuwa ameambatana na askari polisi.

  Mwenyekiti wa Jopo la Majaji Tuzo ya Uandishi wa Kishujaa na Ulitukuka ya Daudi Mwangosi mwaka 2017,Jenerali Ulimwengu alisema madhumuni ya tuzo ya mwangosi ni kumuenzi na kumkumbuka kwa kumpa mwanahabari au chombo cha habari tuzo yenye jina lake.

  “Jopo la majaji mwaka huu tunaitangaza Clouds Fm kuwa mshindi wa tuzo ya Daudi Mwangosi mwaka 2017 kwa sababu tarehe 17,Machi,2017 wanahabari wa Clouds walivamiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam akiwa na askari polisi akiwataka kutangaza habari ambayo hawakuitaka lakini wafanyakazi hao wakakataa kutangaza habari hiyo,huu ni ushujaa kwani hawakukubali kutii amri ambazo zilikuwa kinyume na kazi waliyofundishwa na uandishi wa habari”,alisema Ulimwengu.

  “Lengo la tuzo hii iliyoanzishwa mwaka 2013 na UTPC ni kupinga vitendo viovu wanavyofanyiwa waandishi wa habari , hutolewa kwa mwandishi wa habari anayefanya kazi nchini aliyekutana na madhila katika utendaji kazi wake ama chombo cha habari ambacho kimekutana na madhila”,alieleza Ulimwengu.

  Aliongeza kuwa tuzo hiyo inalenga kuwafanya wadau wa habari ikiwemo serikali kutambua kazi ya waandishi wa habari.

  “Daudi Mwangosi alikuwa mwenyekiti Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa,aliuawa Tarehe 2 mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo mkoani humo,akitekeleza majukumu yake,ni mwandishi wa habari wa kwanza nchini Tanzania kuuawa akiwa kazini, kifo chake kilishtua na kusikitisha watu wengi duniani”,alieleza.

  Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation,Ernest Sungura akikabidhi tuzo Tuzo ya Uandishi wa Kishujaa na Ulitukuka ya Daudi Mwangosi mwaka 2017 kwa Afisa Mahusiano kutoka Clouds Media Group Simalenga Simon
  Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation,Ernest Sungura cheti cha ushindi kwa Afisa Mahusiano kutoka Clouds Media Group Simalenga Simon
  Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation,Ernest Sungura akikabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kwa Afisa Mahusiano kutoka Clouds Media Group Simalenga Simon. Habari/Picha na Oscar Assenga na Kadama Malunde

  0 0

  Ilikuwa ni siku ya furaha mno kwa wananchi wa jamii ya wafugaji kitongoji cha Endevesi, kata ya Njoro, Wilayani Same. Ambapo Septemba 12, 2017 wakati Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule akipokea majengo ya Shule ya msingi kwa niaba ya serikali. Pamoja Na mradi wa Maji kwa ajili ya wananchi hao wasiopungua 6,000. Shule hiyo yenye madarasa 6, ofisi za walimu, vyoo Na nyumbani za walimu. Imejengwa kwa ushirikiano wa masista wa Grail, Joy of faith Na Korea Hope Foundation. 
   
  Jamii hii ya Endevesi walikuwa wakipata Huduma hizi umbali wa km. Zaidi ya 5 Na kupelekea watoto wengi kuwa watoro. "Shule tumejengewa, serikali tutahakikisha tunapanga walimu Na shule hii inaanza 2018. Wananchi wakikishe wanaleta watoto shuleni. Nasi tutawachukulia hatua wote watakaokuwa watoro." Aliwashukuru pia kwa kuunga mkono juhudi za Mh. Rais wa Tanzania katika kuhimiza elimu. Miradi hiyo imegharimu zaidi ya Tshs. 800M.
  Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule akiongea mara baada ya kupokea majengo yaliyojengwa kwa ushirikiano wa masista wa Grail, Joy of faith na Korea Hope Foundation.
  Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemary Senyamule akipanda mti wa kumbukumbu.  
   Mkuu wa wilaya na kiongozi wa Korea Hope Foundation wakinawa mikono katima bomba ambalo ni moja ya mradi waliokabidhiwa.

  0 0

  Ndugu, jamaa, marafiki na wadau wa sanaa na haki za watoto Tanzania.

  Kamati ya Maandalizi ya Msiba inapenda kutoa Tangazo rasmi la shughuli ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa mpendwa wetu marehemu Sister Jean Pruitt itakayofanyika siku ya Jumatano tarehe 20/09/2017.


  Shughuli hii itafanyika katika Ukumbi wa Karimjee uliopo Posta, Mtaa wa Sokoine, mkabala jijini Dar es salaam. Wadau wote tunaombwa kuwasili mapema kwa ajili ya kutoa

  heshima zetu za mwisho na kuaga mwili saa 3:30 asubuhi siku hiyo.

  Baada ya hapo Mwili utasindikizwa kwenda kanisa la Mt. Joseph kwa ajili ya misa itakayoanza saa 9 Alasiri siku hiyo ya Jumatano.


  Tunawaomba tuzidi kumwombea mama yetu Sista Jean Pruitt apumzike kwa Amani. Raha ya milele umpe eh Bwana na mwanga wa milele umwangazie,
  apumzike kwa Amani - Amina

  Kamati ya Maandalizi ya Msiba


  0 0


  0 0

  Tupokigwe Abnery Mwampondele amezaliwa,Seronera - Serengeti mkoani Mara.Alisomea shahada ya Isimu ya lugha ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Kwa sasa ni mwalimu wa somo la Kiswahili katika shule ya Sekondari ya Wasichana Precious blood iliyopo mkoani Arusha-Tanzania.
   
   N’je na kazi ya uwalimu Tupokigwe Abnery ni mtunzi wa vitabu vya hadithi, mbunifu wa mavazi ya kiasili, mjasiriamali na mwandishi wa gazeti tando (blogger) inayoitwa Sinyati Blog.

  Tupokigwe Abnery alikuwa na kawaida ya kupenda kujibembeleza au kujifariji akiwa anatembea kwa kutengeneza hadithi katika fikra zake ili kuweza kulala au kufika anakoelekea bila kuchoka,ndipo siku moja baada ya kushiriki shindano la uandishi wa Riwaya fupi kwa wanafunzi wa shule ya msingi,sekondari na vyuo vikuu Tanzania kwa ajili ya Tuzo ya mama Salma Kikwete iliyoandaliwa na TASAKI(Tamasha la Sauti ya Kiswahili) aliibuka mshindi wa pili wa riwaya fupi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania.

  Hivyo hiki kitabu ni muendelezo wa Riwaya aliyopatia Tuzo.Soma kitabu hiki uweze kujionea ubunifu wa hali ya juu wa fani pamoja na mshikamano wa maudhui uliyopo ndani ya kitabu hiki. 

  Mapenzi Kaburini ni kitabu chenye mtazamo yakinifu,ni kitabu ambacho maudhui yake yamezitazama nchi za Afrika Mashariki na changamoto zilizopo katika nchi kwa upande wa viongozi pamoja na wananchi.Kimebeba maudhui yanayowalenga wananchi wote bila kujali utabaka.Kwa upande wa fani kimetumia majina ya halisi na kubuni hasa kwa upande wa maeneo ya miji mfano kuna miji kama Kinyonga,kupe,chatu ambayo ni majina yaliyopo katika nchi ya Simba.Nchi hii ya Simba ni nchi inayosimamia nchi zilizopo Afrika Mashariki.

  Mbali na hilo pia visa na matukio vimepewa majina ya hifadhi za Taifa zilizopo katika nchi ya Tanzania.Mfano hifadhi ya Ruaha,Sanane,Manyara na kitulo kama ukisoma kitabu hiki utagundua kuwa sifa ya hifadhi inaendana na visa na matukio yaliyopo katika sehemu hiyo iliyoandikwa kwa jina la hifadhi.Mfano hifadhi ya Kitulo inasifika kwa kuwa na maua,kama tujuavyo maua huashiria sifa nyingi moja wapo hapo ni upendo,watu wengi hutumia maua katika kuwapa wapenzi wao,mfano kuomba msamaha,kumfariji mtu,hata kuonesha upendo kwa mtu unayempenda.

  Utakaposoma kitabu hiki utaburudika na kufundishwa baadhi ya mambo kama Kukuza imani yako kwa Mungu,uaminifu katika ndoa,uzalendo katika nchi yako na Madhara ya kujihusisha katika mahusiano na mtu usiye mjua.
  Nitakupatia kionjo kidogo katika sura ya kwanza ili kuweza kuona mwanzo tu wa hadithi hii ambayo hutapenda kuacha kuifuatilia:

  Sura ya kwanza 

  Hifadhi ya Sanane 
  Ilikuwa siku ya Jumatatu katika ghorofa la tajiri mmoja, mmiliki wa hoteli maarufu katika nchi ya Simba. Tajiri huyo alifahamika sana kwa kuwa alikuwa akijitolea sana kwa wananchi wasiojiweza, katika miji mbalimbali ya nchi hiyo.Watu husemamfadhili punda kuliko mwanadamu vilevile tenda wema kisha nenda zako baraka utazipata kwa Mungu,usisubiri hisani za wanadamu.

  Pamoja na misaada aliyoitoa kwa watu mbalimbali lakini wananchi wa Simba hawakujali misaada yake, walimteta kila kona kuwa anatumia nguvu za giza na amekwisha toa kafara ndugu, jamaa na hata watoto wake ili kujipatia utajiri mkubwa alionao. Siku hiyo ya Jumatatu katika pagala la tajiri huyo aliyefamika kwa jina la Pesa nyingi.

  katika moja ya chumba cha ghorofa hilo kulikuwa na mwanamke mrembo na mzuri sana wa sura, mrefu mithili ya twiga, mwenye umbo zuri la kiafrika, chini alikuwa amevaa suruali ya chupa huku akiwa amevaa blauzi tatu juu zenye rangi tofauti na nywele timutimu zikiwa zime nakishiwa na vitu vya jaani kama vichana,visude, rasta chakavu na kufungwa kitambaa cha kitenge aina ya makenzi ,uso wake ulikuwa kama paka mwenye madoa kutokana na kujipamba kwa majivu na masizi ya mkaa wa jaani. Pembeni ya ua hilo alikuwepo mnyama mwenye maringo 

  mbugani kuliko wote, sio mwingine bali ni kijana mtanashati aliyekwenda hewaani, rangi ya ngozi yake nyeusi ya kung’aa. Tabasamu la mwanaume huyo lililokuwa likimfariji mtoto mzuri, lili mvutia sana Savannah. Ghafla ilisikika sauti ya mwanamke huyo ikiita kwa sauti ya chini iliyojaaa simanzi na mateso ya muda mrefu,ilisema “John naumia mume wangu, hali yangu kila kukicha afadhali ya jana”. 

  John alijibu “usijali Savannah nipo hapa mke wangu kwa ajili yako utapona tu tutakwenda hospitali,subiri nikuandalie chakula ule, kisha nikupeleke hospitali malikia wangu”. Basi baada ya John kumfariji Savannah aliamka na kuelekea jikoni pembeni ya sehemu aliyokuwa amelala mpenzi wake. 

  Watu hawa walipendana sana ni vile tu hali yao haikuwa nzuri kifedha waliishi kwa kuhangaika, kuomba msaada na wakati mwingine walifukuzwa na walimwengu pale walipokuwa wakiomba msaada, watu waliwapita kama mbwa waliokosa matunzo. 

  Wapenzi hao Walizoea maisha ya kuokota vyakula jalalani na kukimbilia magari ya taka sambamba na kusubiria mabaki ya chakula katika migahawa mbalimbali. Wakati huo John alikuwa akitimiza ahadi aliyo mhahidi malikia wake alimuandalia chakula walicho kiokota katika soko kuu la mji huo wa Chatu. John alimuinua Savannah pale alipokuwa amelala kwenye kanga chakavu akiwa amejifunika magunia yalionekana ni ya mpunga. John alimlisha Savannah chakula kile ambacho hawakujua kilipikwa lini na kutupwa na nani na lini. Savannah alisikika akisema “asante mume wangu hata 

  mwanangu anafurahi sasa naona napata nafuu, nahisi ni njaa ilikuwa inaniuma”. Mwanangu nisamehe mama kakushindisha njaa, nakupenda sana najua wewe utakuwa mrembo zaidi yangu mwanangu hata baba yako anakupenda”. John alikuwa anapenda sana utani alicheka na kusema “atakuwa mrembo kama wewe kweli mke wangu lakini rangi ya ngozi yake itakuwa kama yangu, yako iko kama ya nguruwe hahahaaaa!” Savannah alikuwa mweupe kama Nguruwe, ingawa alivyokuwa anaonekana ni kama mtu mwenye ngozi ya rangi ya maji ya kunde kutokana na ugumu wa maisha. 

  Wawili hao walifurahi pamoja na kusahau shida walizokuwa nazo.Walipomaliza kula wapenzi hao waliamua kutoka nje baada ya kukaa ndani ya paghala hilo kwa muda wa wiki moja, Dikidiki hao walikuwa na kaida ya kufanya hivyo wanapotafuta riziki na kujilimbikizia ndani ya paghala lao kisha wana kaa kwa muda huo bila kutoka. Usilolijua ni kama usiku wa kiza, basi Savannah na John walipotoka wakiwa n’je ya mgahawa mmoja uliokuwa unapendwa sana na wananchi wa mji huo wa Chatu zilisikika sauti za wanawake wakisema: 

  “haya jamani sasa ni ule wakati wa Pesa nyingi kuingiza hela sasa wenzi wametoka fungate”. Waliamini kuwa Pesa nyingi alikuwa anawatumia Dikidiki hao kama misukule inayotoka na kurudi ndani na wanapotoka basi mzee Pesa nyingi huingiza hela nyingi sana. Kwakuwa wenzi hao walikuwa hawaelewi kinachoongelewa waliendelea kuomba msaada kwa wateja waliokuwepo hapo mgahawani. Wanapokosa waliamua kucheza baadhi ya nyimbo zilizokuwa 

  zikipigwa katika mgahawa huo, wakicheza hupewa chakula na fedha ambazo hutoka katika mifuko ya wateja. John alikuwa anapenda sana kucheza,wakiwa wamekaa chini walisikia wimbo wa mwanamuziki maarufu Tanzania Diamond unaosema Je, Utanipendaga? John alimuinua Savannah aliyeonekana kachoka na mimba yake. Savannah aliamka na kucheza na mpenzi wake ,walicheza kwa miondoko ya kihindi, machozi yalisafisha uso wa Savannah huku yakiosha kifua cha John kilichokuwa kimejaa kama mlima na mikono iliyokuwa na miinuko ya kupanda na kushuka ilizunguka juu ya kifua cha Savannah na kumfanya ahisi kazungukwa na jeshi kubwa la malaika wa ulinzi.

  Baada ya kumaliza kucheza savannah alikuwa amechoka sana, kitendo cha kucheza kilimsababishia kuchokoza maumivu na kupelekea kupata uchungu katika kizazi chake. Baada ya kuona hivyo John aliinama na kuchukua zawadi walizozipata kutoka kwa hadhira iliyokuwa ikiwatazama huku baadhi ya hadhira wakibubujikwa na machozi walimpelekea hela na chakula John katika kapu lake la kukusanyia riziki. Watu waliokuwa wakiwatazama Savannah na John hawakujali maumivu ya mwanamke yule na kuona kawaida. 

  Wapo waliosikika wakisema hawa vichaa wana akili, wengine walisema hawa si vichaa, vichaa gani wana akili ya kutafuta hela hivi, wamekusanya umati mkubwa hivi na kuwafanya watu kutoa kile walichonacho. Mama mmoja mwenye busara anayeuza katika mgahawa huo aliyefahamika kwa jina la mama ndaga akasema“Jamani mimi nawafahamu hawa vichaa kwanza hawakuwa wakitembea hivi pamoja kama Dikidiki, huyo kaka unayemuona alikuwa..........pata mwendelezo kwa kujipatia kitabu hiki.


  Nicheki kwa mawasiliano haya:+255756377940
  Instagram: @sinyatiblog
  Facebook:Tupokigwe Abnery 

  0 0


  Afisa TEHAMA wa Taasisi ya NORDIC, Dickson Leonard akiongea na wanahabari kumtambulisha Hilary Daudi ‘Zembwela’ kuwa Balozi wa Nordic Foundation Tanzania Dar es Salaam Septemba 15 2017. Balozi Zembwela atafanya kampeni ijulikanayo kama ‘AfyaBando’. Kushoto ni Mtaalam Mwelekezi wa Afyabando-Nordic Foundation Tanzania, Dkt. Resipicius Salvatory. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogspot)
  Balozi Zembwela akionesha namba ya kampuni na kumbukumbu kwa ajili ya kushiriki bahati nasibu ya kucheza 'Afyabando' ili kupata kadi ya Bima ya afya kwa shilingi 500.

  0 0


   Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Renata Mzinga (kushoto), akiwavisha beji miongoni mwa wanafunzi 230 waliojiunga na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), katika hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi Mjini.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG. 
   Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Macha akiwavisha beji miongoni mwa wanafunzi 230 waliojiunga na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), katika hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi Mjini. 

  Na Richard Mwaikenda,Lindi
   JESHI la Polisi limeahidi kushirikiana na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), kuwakamata wanaowanyanyasa na kuwabaka Watoto wa Kike.

  Kauli hiyo ilitolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Renata Mzinga 

  katika hafla ya kuwaapisha wanafunzi wa kike 230 waliojiunga na TGGA mkoani Lindi jana.

  Hilo siyo ombi bali ni wajibu wa jeshi la Polisi kushirikiana na chama hicho pamoja na jamii kuhakikisha wale wote 

  wanaowatendea vitendo vibaya watoto wa kike wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali  za kisheria.

  "Msiombe msaada kwetu, bali sisi tunahitaji sana msaada mkubwa kutoka kwenu, kwani huku kwetu watoto wa kike 

  wanakuja wakiwa wameharibikiwa, ushauri wenu kwao umesaidia sana," alisema Kamanda Mzinga na kuwataka 

  waendelee kutoa elimu hiyo kwenye Tarafa, Kata, Kijiji na vitongoji ili kumkoboa mtoto wa kike.

  Kamanda Mzinga, aliipongeza TGGA kwa kitendo cha kuwapatia mafunzo takribani wasichana 1200 ya jinsi ya 

  kuepukana na vitendo vibaya vya kubakwa na kupewa mimba, magonja kama vile Ukimwi na ndoa za utotoni.

  Akielezea walichonufaika katika wakati wa mafunzo yaliyodumu kwa takribani siku nne, Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa 

  Lindi, alisema kuwa waischana walifaidika kwa kupata mafunzo ya ukakamavu, kujiamiini, kuepukana na vikwazo 

  mbalimbali wanavyokumbana navyo wakati wa kwenda shule na kurejea nyumbani ikiwemo kurubuniwa kwa kupewa 

  mimba za utotoni.

  Alitaja mambo mengini waliyonufaika nayo ni ujasiriamali, utunzaji wa mwili, utunzaji wa mazingira, uongozi, maadili, 

  kujitolea , kuwa na upendo na uzalendo kwa nchi yao.

  Mwenyekiti aliimpongeza Kamanda Mzinga kwa kuwapatia askari wa kike ambaye anafanya kazi nzuri ya kukutana na 

  watoto wanaoelezea matatizo yao bila woga baada ya kupata mafunzo ya TGGA, ambapo alidai baadhi ya wanafunzi 

  hao wanadiriki kusema wazi kwamba wazazi wao wana tabia ya kutaka kuwabaka.

  Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Shaba, aliwaasa wasichana waliopata mafunzo hayo, kulinda kiapo walichokipata 

  kwa kuwa watiifu na kuweka mbele uzalendo, awe na imani iliyo thabiti katika maisha yake, nchi yake na Jamii.

  "Hivyo basi msilichukulie jambo la kawaida,  libaki mioyoni mwenu mbele ya Mungu na muepukane na ulevi, kutumia 

  dawa za kulevya, matumizi mabaya ya mitandao, tunataka muwe na misimamo katika maisha yao yote."Alisema Shaba.

  Alisema TGGA ina utaratibu wa kuwaingiza uanachama kuanzia watoto wa miaka mitatu na kuendelea ambapo 

  huwapatia  mafunzo ya kujiamini, kujithamini, ujasiriamali na kuipenda nchi yao.

  Pia alitangaza  kwa wanachama wao walio likizo na waliomaliza shule wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kuomba 

  kujiunga na programu ya Yess kwenda nje ya nchi kupata mafunzo ya uongozi, utamaduni na maadili katika nchi tano 

  wanachama kwa ufadhili wa Makao Makuu ya Girl Guides ulimwenguni.

  Alisema wanachama watakaofanikiwa kwenye programu hiyo inayoendeshwa kuanzia miezi mitatu, sita au mwaka 

  mzima watafaidika kwa kujiongezea upeo wa mambo mbalimbali.   Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Macha akimkaribisha mgeni rasmi, RPC wa Lindi, Renatha Mzinga kwenye hafla hiyo.

   Baadhi ya wazazi wa Girl Guides waliokuwa wakiapishwa wakiwa katika hafla hiyo

   Timu ya soka ya wanawake mkoani Lindi wakitambulishwa katika hafla hiyo. Nao wanatarajia kujiunga na Girl Guides
   Mkufunzi Mkuu kutoka TGGA Makao Makuu Dar es Salaam, Emmiliana Stanslaus akitambulishwa wakati wa hafla hiyo
   Young Leader wa Dar es Salaam, Valentina Gonza akitambulishwa wakati wa hafla hiyo
   Makamu Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, Sharifa Mkwango akijitambulisha
  Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam, Ruth Namatanga akimvisha beji mwanachama mpya
   Girl Guides wakitumbuiza wakati wa hafla hiyo
   Mgeni rasmi, RPC Mzinga akimvisha beji mwanachama mpya wa Girl Guides
   Makamu Mwenyekiti wa TGGA Lindi, Sharifa Mkwango akimvisha beji mwanachama mpya wa Girl Guides
    Mkufunzi Mkuu wa TGGA, Emmiliana Stanslaus akimvisha beji mwanachama mpya wa Girl Guides
   Girl Guides mpya akivishwa beji
   Mkufunzi Msaidizi wa TGGA Mkoa wa Lindi, Kidawa Naheka akimvisha beji mwanachama mpya wa TGGA

   Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi akimvisha beji mwanachama mpya
   Katibu wa TGGA Mkoa wa Lindi  akimvisha beji mwanachama mpya   Girl Guides wapya wakila kiapo
   Girl Guides mpya Elvila Dickson akisoma risala 
   RPC Mzinga akihutubia wakati wa hafla hiyo
   RPC Mzinga akiwa na baadhi ya viongozi wa TGGA
   RPC Mzinga akiwa na baadhi ya Girl Guide wapya pamoja na viongozi
  RPC MZINGA AKIWAAGA BAADA YA HAFLA KUMALIZIKA

  0 0

  Na  Binagi Media Group.
  Benki ya CRDB leo imekutana na wafanyabiashara wadogo na wa kati mkoani Mwanza na kuwahakikishia kwamba itaendelea kutoa huduma bora ikiwemo mikopo ili kukuza mitaji yao.

  Akisoma hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dkt.Charles Kimei, Mkurugenzi wa CRDB tawi la Mwanza,Wambura Calystus amewahakikishia wafanyabiashara hao kwamba huduma za mikopo zitatolewa kwa wakati wote katika benki hiyo kwa kuzingatia kanuni za kibenki nchini.


  Amesema benki hiyo imeendelea kutanua na kuboresha huduma zake ikiwemo uwepo wa Matawi 20, vituo vya kutolea huduma 50, ATM 135, mawakala wa Fahari huduma zaidi ya 649 katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.


  Aidha amesema kwa mkoa wa Mwanza benki ya CRDB ina matawi manne, vituo vya huduma 13 pamoja na Mawakala wa Fahari Huduma zaidi ya 105 na hivyo kusaidia kuwafikia wateja wake kwa urahisi.


  Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mkutano huo, Agapiti Malya pamoja na Doroth Baltazari wameipongeza benki hiyo kwa namna ilivyowawezesha kwa njia ya mikopo na kuinua biashara zao ambapo wameomba benki hiyo kuendelea kuboresha zaidi huduma zake ili kuwanufaisha wafanyabiashara wengi zaidi.

  Baadhi ya wafanyabiashara (wajasiriamali) wadogo na wa kati walioshiriki mkutano ulioandaliwa na benki ya CRDB mkoani Mwanza kwa ajili ya kujadili pamoja masuala mbalimbali ya kibenki ili kusaidia kuboresha huduma zinazotolewa na benki hiyo.

  Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Mkoani Mwanza, Wambura Calystus akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huu, hii leo Jijini Mwanza
  Meneja Mwandamizi wa benki ya CRDB, kwa wateja wadogo na wa kati, Elibariki Masuka akizungumza kwenye mkutano huo Jijini Mwanza
  Meneja Biashara benki ya CRDB, Danford Muyango akizungumza kwenye mkutano huo
  Mmoja wa watoa mada kutoka benki ya CRDB akiwasilisha mada kwenye mkutano huo
  Mmoja wa watoa mada kutoka benki ya CRDB akiwasilisha mada kwenye mkutano huo
  Mmoja wa watoa mada kutoka benki ya CRDB akiwasilisha mada kwenye mkutano huo
  Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada kwenye mkutano huo
  Benki ya CRDB imeendelea kuwahakikishia wajasiriamali kwamba itaendelea kushirikiana nao kwa kuwapatia mikono yenye riba nafuu ili kukuza biashara zao
  Mjasiriamali Doroth Baltazari ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Chabati Pop Food, akiwaonyesha baadhi ya wanahabari bidhaa anazotengeneza.

  0 0

  Na ChalilaKibuda, GlobuyaJamii

  WAFANYAKAZI 17 wa Mamlaka ya Usafiriwa Anga wa Nchini Uganda wamehitimu mafunzo katika kozi mbalimbali katika Chuo cha Mamalaka ya Usafiri wa Anga wa nchini (CATC).

  Akizungumza katika mahafali ya 270 ya Chuo hicho ,MkurugenziMkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA) , Hamza Johari amesema kuwa waliohitimu mafunzo katika chuo hicho wakatumie elimu ambayo italeta mabadiliko katika usafiri wa anga.

  Amesema chuo cha CATC kinatambulika na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) hivyo mafunzo yanayotolewa ni bora kutokana nakutambulika kwa nchi mbalimbali kuleta watalaamu wao kuja kujifunza masuala ya usafiri anga nchini Tanzania.

  Hamza amesema tofauti kinachofanya kwa watalaam hao kuwa wameiva ni kuonyesha mikakati yauekelezaji kwa kile walichojifunza katika maendeleo ya nchi yao pamoja na Afrika Mashariki katika utoaji wa huduma ya usafiri wa anga.

  Amesema mikakati iliyopo kwa chuo hicho ni kuingia ubia na Chuo cha Nchini Singapore kwa ajili ya kutoa mafunzo ya usafiri wa anga kwa nchi za Afrika hali ambayo itafanya Chuo kuongeza idadi ya wanafunzi wanakuja kusoma na kuifanya Tanzania kutambulika zaidi katika utoaji wamafunzo ya usafiri wa anga.

  Nae Mkuu wa Chuo CATC, Dk. Daniel Karenge amesema kuwa wahitimu waliohitimu chuo hicho tangu kilipoanzishwa mwaka 2000 niwahitimu 3056 katoka nchi mbalimbali zaAfrika .

  Amesema kuwa wanaopata mafunzo hayo kwa asilimia kubwa ni watu wa nje ya nchi hivyo amewasaa watanzania kutumia fursa ya kupata mafunzo ya usafiri wa anga katika chuo chao.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA) , Hamza Johari akizungum za katika mahafali 270 ya Chuo cha Usafiri wa Anga CATC yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA),jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Chuo cha Usafri wa Anga (CATC), Dk. Daniel Karenge akitoa taarifa ya Chuo hicho katika mahafali ya 270 yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA), jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari akitoa cheti kwa Mhitimu wa Kozi ya Watoa Taarifa za Usafiri wa Anga, Stella Kabagenyi katika mahafali ya Mahafali ya 270 ya Chuo cha UsafiriwaAnga Tanzania(CATC) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA, Jijini , Dar es Salaam.
  Sehemu ya wahitimu wakionesha vyeti vyao katika mahafali ya 270 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA, Jijini , Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA) , Hamza Johari akiwa katika picha pamoja na wahitimu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) katika mahafali ya 270 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA, Jijini , Dar es Salaam.

   

  0 0

  Na Jumia Travel Tanzania

  Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio lukuki takribani kila sehemu utakayoipendelea. Mji Mkongwe uliopo visiwani Zanzibar ni mojawapo ya maeneo hayo yenye utajiri wa vivutio vya watalii kama vile maisha na vyakula vya wakazi wake, biashara pamoja na majengo ambayo yanayoakisi tamaduni za mataifa tofauti kama vile Waarabu, Waajemi, Wareno, Waafrika na Waingereza ambayo yamekuwepo tangu karne za 18 na 19.
  Katika kuhakikisha maeneo hayo yanajulikana miongoni mwa watanzania na wageni wanaotembelea nchini, Jumia Travel wamezindua kampeni ambayo itakuwa ikiangazia maeneo mbalimbali. Ikiwa imejikita kwenye Mji Mkongwe wa Zanzibar, kampuni hii ambayo inajishughulisha na huduma za hoteli kwa njia ya mtandao ilifanya mahojiano na Meneja Operesheni wa Africa House Hotel, Bw. Justus Kisome na mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo.

  JT: Unaizungumziaje hoteli yako?

  Justus: Africa House Hotel ni hoteli ya nyota nne inayopatikana kwenye jengo la kihistoria linalomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lililopo katika Mji Mkongwe wa Zanzibar. Hoteli yetu ina vyumba 15 vikiwa na hadhi tofauti kukidhi haja ya wateja mbalimbali wanaotembelea hapa. Miongoni mwa vyumba hivyo 6 vinatazamana na bahari ya Hindi ambavyo huwapatia wageni fursa ya kutazama tukio nadra na kuvutia la kuzama kwa jua. Vyumba 9 vinawapatia wateja mandhari nzuri ya Mji Mkongwe wa Zanzibar ambao umebarikiwa kuwa na majengo na tamaduni za kale kwa karne kadhaa sasa.

  JT: Unadhani ni vitu gani vinaifanya hoteli yako kuwa ya kipekee?
  Justus: Naweza kusema kwamba tunajivunia hoteli yetu kuwa ndiyo pekee yenye maktaba katika Mji Mkongwe huu wa Zanzibar ambapo wageni wanayo fursa ya kujisomea masuala mbalimbali. Lakini pia ukiachana na hilo, Africa House Hoteli ndiyo hoteli pekee yenye mgahawa unaopika vyakula vya Kichina katika Mji Mkongwe wa Zanzibar. Mgahawa huu tumeujenga hivi karibuni, hakuna hoteli yoyote hapa yenye huduma kama hii, mgahawa unaendelea vizuri kwani tunapata maombi ya huduma mpaka moja kwa moja kutoka nchini China.
  JT: Je unafikiri wateja wako ni wa aina gani? Kutoka ndani au nje ya nchi?
  Justus: Naweza kusema kwamba idadi kubwa ya wateja wetu ni mchanganyiko, wengi wakiwa ni kutoka nje ya hapa Mji Mkongwe. Kwa wageni wa hapa nyumbani wengi tunaowapokea hupendekezwa na serikali na kwa wenyeji pia huwaleta au kuwaelekeza wageni wao kuja hapa.

  JT: Ni shughuli gani zinazopendelewa kufanywa au kuuliziwa zaidi na wateja pindi wanapotembelea hoteli yako?Justus: Asilimia kubwa ya wageni tunaowapokea hapa huja kwa madhumuni ya kibiashara au kikazi sio kwa mapumziko. Kwa ujumla, kama zilivyo hoteli nyingi kwenye Mji Mkongwe, hufanya sehemu hii ni kama kituo na kisha kuendelea na safari zao. Hivyo basi, mara nyingi wageni wanaofika hapa hulala kwa siku moja au mbili na kisha kuendelea na safari zao kama vile kwenda sehemu za ufukweni, uwanja wa ndege au bandarini.

  JT: Una maoni gani juu ya ukuaji wa utalii wa ndani? Je kuna mabadiliko yoyote uliyoyaona?

  Justus: Ukuaji wa utalii wa ndani kwa hapa Mji Mkongwe ni mzuri kwani wageni huongezeka mara kwa mara kadiri siku zinavyokwenda. Ingawa hatupokea wageni wengi wazawa kwenye hoteli yetu lakini kuna idadi kubwa ambao huwaleta wageni wao hapa. Hata kama hawatembelei hapa lakini kuna maeneo mengi ambayo tunawaona watalii wazawa wakitembelea na kwenye mitaa ya Mji Mkongwe.
  JT: Unaizungumziaje Zanzibar kama mojawapo ya sehemu inayopendelewa kutembelewa zaidi? Je unadhani umaarufu wake unaongezeka au kupundua kadiri miaka inavyozidi kwenda?

  Justus: Zanzibar kama kitovu cha utalii bado ni imara na kinaedelea kukua kadiri siku zinavyozidi kwenda. Wateja ni wengi na wanaendelea kuongezeka. Kwa mfano, kuanzia mwezi wa Julai, Agosti na huu wa Septemba ni vipindi ambavyo huwa tunapokea wageni wachache lakini tofauti na kipindi cha nyuma wateja ni wengi na kuna baadhi ya hoteli zimejaza vyumba na zingine zikiwa zimebakisha vichache! Hii ni ishara na dalili nzuri kwamba hali ni shwari huku Zanzibar ambapo kwa kipindi kama hiki hapo awali hakukuwa na wageni wengi kama sasa.
  JT: Unazungumziaje kuhusiana na tozo mbalimbali kwenye sekta ya utalii, ukiachana na 18% za VAT, je zinaathiri biashara yako?

  Justus: Kwa upande wangu naweza kusema kwamba Zanzibar haijaathirika na hizo tozo mbalimbali na sidhani kama zimeathiri biashara yetu. Kwa mfano, tozo ambazo zinalipwa ni zilezile na wageni kutoka nje ambao wanakuja nchini kuja kutembelea vivutio mbalimbali zikiwemo kodi na viingilio. Kama kungekuwa na athari basi tungewasikia wageni wakilalamika lakini wanaridhika na kuelewa kuwa ni taratibu ambazo ziko kama sehemu nyingine ukizingatia ni vivutio ndivyo wamekuja kuviangalia na sanasana huwashawishi na wageni wengine kuja kutembelea Zanzibar.

  JT: Una maoni gani juu ya shughuli za mitandaoni kwenye kukuza sekta ya utalii nchini Tanzania?

  Justus: Ni kweli dunia imebadilika hususani kwenye namna biashara zinavyoendeshwa siku za hivi karibuni. Kama zilivyo sehemu zingine, Zanzibar nayo imeipokea teknolojia ya mtandaoni vizuri kwa sababu idadi kubwa ya wageni tunaowapokea tunawapata kwa njia ya mtandaoni. Na kitu kizuri ni kwamba wanaiamini mitandao hiyo katika kufanya huduma zao na sisi tunajiimarisha kila kukicha kwenye Nyanja hiyo.
  JT: Kwa kuongezea, unauzungumziaje ushirikiano baina ya Jumia Travel na hoteli yako? Unadhani ni msaada katika uendeshaji wa biashara yako?
  Justus: Mahusiano na ushirikiano wetu na Jumia Travel ni mazuri kwani wanatusaidia kwa kiasi kikubwa kwenye uendeshaji wa shughuli zetu. Jumia Travel inakuja vizuri na inakua kwa sasa kwani mchango wake kwenye uendeshaji wa shughuli zetu ni mkubwa kutokana na wao kuwepo kwenye soko. 

  Ukilinganisha na mwanzo ambapo kulikuwa na changamoto kadhaa kama vile kutokuwepo na mawasiliano ya kutosha pale kunapokuwepo na matatizo. Hivi sasa wanatutembelea na kuwasiliana mara kwa mara kujua tunafanyaje shughuli zetu. Naweza kusema wanastahili pongezi kwa hilo na naamini timu ya sasa iliyopo inafanya kazi vema na inajitambua zaidi.


  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi ya ESTL,Bi Rose Mjema akiwasilisha mada kwa washiriki wa mafunzo ya kupinga vitendo vya ukeketaji huku akitoa tahadhari juu ya madhara yatokanayo na vitendo hivyo vya ukeketaji.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).

  Shirika lisilokuwa la kiserikali la Empower Society Transform Lives (ESTL) la Mkoani Singida limesema kwamba ukeketaji wa wanawake na watoto ni tatizo kubwa Afrika,Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi 28 zinazotajwa kuendeleza mila hiyo mbaya.

  Hayo yalisemwa na Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo Mkoani Singida,Joshua Ntandu kwenye risala aliyosoma wakati wa uzinduzi wa mradi wa kutokomeza ukeketaji katika vijiji 14 vilivyopo katika kata za Itaja,Mgori,Ntonge na Ughandi,uliofadhiliwa na The Foundation For Civil Society na kufanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Singida.

  Aidha Ntandu alifafanua kwamba inakadiriwa kuwa Tanzania ina zaidi ya wanawake milioni 7.9 waliogundulika kuwa wamekeketwa huku Mkoa wa Singida ukishika nafasi tano za juu za mikoa inayoongoza kwa ukeketaji hapa nchini.

  Alisema tafiti zinaonyesha pia kwamba vitendo hivyo vinaendelea kuongezeka katika Mkoa wa Singida na sababu kubwa zinazotajwa ni pamoja na imani kwamba ukeketaji ni sehemu ya makuzi ya mtoto wa kike na kwamba humzuia mtoto wa kike asiingie katika mahusiano ya mapenzi kabla ya kuolewa.

  Hata hivyo Ntandu alisisitiza kuwa jamii pia huamini kwamba ukeketaji ni tiba ya ugonjwa unaojulikana kama lawalawa kwa watoto wa kike (Vaginal or Urinary Tract Infection (UTI).

  “Kadhalika kuna mbinu mpya ambayo imeshamiri ya ukeketaji wa watoto wachanga mara tu wanapozaliwa na kabla ya kufikia umri wa mwaka mmoja,na hii hufanywa ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria na vyombo vya dola”alisisitiza Mtendaji mkuu huyo wa ESTL.

  Akizindua mradi huo kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida,Afisa Ustawi wa jamii wa Mkoa wa Singida,Shukurani Mbago,pamoja na kusikitishwa na mbinu mpya iliyoshamiri ya ukeketaji wa watoto wachanga,alizitaja baadhi ya sababu za kuongezeka kwa vitendo hivyo kuwa ni imani kuwa ukeketaji ni sehemu ya makuzi ya mtoto wa kike na kwamba kumzuia mtoto wa kike asiingie katika mahusiano ya mapenzi kabla ya ndoa.

  “Jamii pia huamini kuwa ukeketaji ni tiba ya ugonjwa ujulikanao kwa jina la lawalawa kwa watoto wa kike mara tu wanapozaliwa na kabla ya kufikia umri wa mwaka mmoja.”alifafanua Katibu tawala huyo wa Mkoa.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya ESTL Mkoa wa Singida,Rose Mjema aliweka bayana kwamba mpaka sasa wameshaunda kamati za kutokomeza ukeketaji katika ngazi za vijiji na kata kutokana na watu waliopo katika ngazi hizo kuonyesha utayari wa kufanyakazi na wao.

  Kwa mujibu wa Mjema wajumbe waliopo katika kamati hizo ni ni vijana tu kwa ngazi ya kata na vijiji,viongozi wa jadi,wakunga wa tiba asilia na wakunga wa jadi kwa kuwaandalia vikundi vya kupiga vita masuala ya ukeketaji kwenye maeneo yao.

  Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Singida,Elia Digha akizungumza na washiriki wa semina hiyo alishauri kwamba ili kukabiliana na vitendo hivyo kuanzia ngazi za serikali za vijiji pamoja na Halmashauri waanze kuandaa sheria ndogo itakayosimamia udhibiti wa ukeketaji katika Halmashauri ya wilaya hiyo.
  Baadhi ya Mangariba na wakunga wa jadi kutoka katika Tarafa ya Mgori, wilayani Singida ambao wameamua kuachana na shughuli za kukeketa baada ya kupatiwa elimu na Shirika lisilokuwa la kiserikali la ESTL la Mkoani Singida,wakitoa ushuhuda kwenye uzinduzi wa mradi wa kutokomeza ukeketaji kwa wanawake katika Mkoa wa Singida uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Singida.

  0 0

  Afisa maendeleo ya vijana Temeke, Anna Marrica amezindua mradi wa sauti ya vijana katika Halmashauri ya wilaya ya Temeke na kuwataka vijana hao kutokata tamaa katika kutafuta maendeleo ili kujikwamua kiuchumi.

  Marrica amesema hayo katika uzinduzi wa mradi uliofanyika kwenye ukumbi wa manisapaa ya Temeke, lengo likiwa ni kutaka kuwapa moyo na kuwapongeza vijana hao kwa hatua nzuri waliofikia katika kuhakikisha wanaleta maendeleo ambapo mradi huo umelenga kuanzia ngazi ya kata ambazo ni Buza, Makangarawe, Kilakala pamoja na Tandika.

  Nae Mwenyekiti Mtendaji MYIDC, Ismae Mnikite amesema kuwa lengo pia ni kutaka kuishawishi Halmashauri ya Manispaa hiyo kufanya mchakato wa kutoa taratibu huru za wazi zinazofaa kuwaingiza vijana katika mfumo rasmi wa kutoa maamuzi ikiwemo kushirikisha hatua mbalimbali za uundwaji wa baraza la vijana kunzisha nganzi ya kata na hata hadi kiwilaya kwa mujibu wa tamko la sera ya Taifa ya maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007.

  Vile vile Mratibu wa mradi MYIDC, Kissango Mario ametanabaisha kuwa upo umuhimu wa vijana kujengewa uwezo wa kuhamasishwa, utetezi na ushiriki katika maamuzi pamoja na kuandaliwa kimaadili.

  Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi msaidizi mafunzo na maendeleo ya ujuzi kutoka ofisi ya Waziri mkuu kazi vijana ajira na wenye ulemavu, Julius Tweneshe amesema kuwa Serikali inathamini na kutambua mchango wa vijana hasa katika swala la kimaendeleo na ametoa ame toa wito kwa vijana wachangamkie fursa mbalimbali zianazojitikeza.
  Afisa maendeleo ya vijana Temeke, Anna Marrica akizungumza na vijana wa mradi wa sauti ya vijana MYIDC na kuwapongeza kwa hatua waliofikia na kuwataka wasikate tamaa katika swala la kutafuta maendeleo. Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam .
  Mwenyekiti Mtendaji MYIDC, Ismae Mnikite akizungumza na vijana wa mradi wa MYID pamoja na kudadafua zaidi lengo la uzinduzi huo ni nikulenga kuanzisha na kuendeleza majukwaa ya vijana kuanzia ngazi ya kata nne 4 ambazo ni Buza, Mkangarawe, Kilakala na Tandika, leo Jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Mkurugenzi msaidizi mafunzo na maendeleo ya ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Julius Tweneshe akizungumza na vijana wa mradi wa MYID kwa kutoa wito katika kuchangamkia fursa zinazojitokeza hapa nchini.
  Afisa Habari wa chama cha mbio za polepole Manispaa ya Temeke (Jogging) akiuliza swali kwa Mkurugenzi msaidizi mafunzo na maendeleo ya ujuzi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Julius Tweneshe.
  Vijana wa Mradi wa sauti ya vijana MYID wakisikiliza kwa makini mazungumzo ya viongozi wakati wauzinduzi wa mradi wa sauti ya vijana MYID uliofanyika katika harmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam.
  Picha ya pamoja wakiwa ni viongozi, vijana wa mradi wa sauti ya vijana MYID, wageni waalikwa pamoja na waandishi wa habari.

  0 0older | 1 | .... | 1369 | 1370 | (Page 1371) | 1372 | 1373 | .... | 1897 | newer