Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

SERIKALI ZA TANZANIA NA KENYA ZAMALIZA MZOZO WA VIKWAZO VYA BIASHARA BAINA YA MATAIFA HAYO.

$
0
0
Baadhi ya Maafisa Waandimizi wa Serikali, Wafanyabiashara na Wazalishaji wa bidhaa za Kilimo kutoka wakulima kutoka Tanzania na Kenya wakifuatilia taarifa mbalimbali zilizotolewa na Wenyeviti wa Mkutano huo uliojadili changamoto na utatuzi wa vikwazo vya biashara na uwekezaji katika Mataifa hayo.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. Pindi Chana akitoa taarifa ya majadiliano ya mkutano baina ya Watendaji Wakuu wa Serikali ya Tanzania na Kenya uliojadili changamoto na utatuzi wa vikwazo vya biashara na uwekezaji katika Mataifa. Mkutano huo ulifanyika jana Septemba 8 Jijini Dar es Salaam. Wengine katika Picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Tanzania, Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Kenya Dkt. Chris Kiptoo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Baishara na Uwekezaji), Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Watendaji Wakuu wa Serikali, Wafanyabiashara na Wazalishaji wa bidhaa za kilimo katika Mataifa hayo. Mkutano huo ulifanyika jana Septemba 8 Jijini Dar es Salaam. Wengine katika Picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Tanzania, Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Kenya Dkt. Chris Kiptoo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Ushirikiano wa Kenya, Dkt. Chris Kiptoo akizungumza na Watendaji Wakuu wa Serikali, Wafanyabiashara na Wazalishaji wa bidhaa za kilimo katika Mataifa hayo. Mkutano huo ulifanyika jana Septemba 8 Jijini Dar es Salaam. Wengine katika Picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Tanzania, Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Kenya Dkt. Chris Kiptoo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Uwekezaji na Ushirikiano wa Kenya, Dkt. Chris Kiptoo na Mwenjeji wake Prof. Adolf Mkenda wakionyesha Sera ya Taifa ya Biashara ya Kenya wakati mkutano baina ya Watendaji Wakuu wa Serikali, Wafanyabiashara na Wazalishaji wa bidhaa za kilimo katika Mataifa hayo uliojadili changamoto na utatuzi wa vikwazo vya biashara na uwekezaji katika Mataifa hayo. Mkutano huo ulifanyika jana Septemba 8 Jijini Dar es Salaam.(PICHA NA ELIPHACE MARWA-MAELEZO)



Na Ismail Ngayonga-MAELEZO-DAR ES SALAAM

SERIKALI za Tanzania na Kenya zimekubaliana kwa pamoja kumaliza vikwazo vya kibiashara katika usafirishaji na uingizaji wa bidhaa katika mipaka baina ya nchi hizo mbili hatua inayokusudia kuimarisha ushirikiano wa biashara na uwekezaji katika Mataifa hayo.

Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Wizara, Biashara na Uwekezaji (Biashara na Uwekezaji) Prof. Adolf Mkenda mara baaada ya kumalizika kwa mkutano wa pamoja yao ulioshirikisha Viongozi Waandamizi wa Serikali hizo, Wafanyabiashara na Wakulima kutoka Mataifa hayo.

Anasema katika mkutano huo Serikali ya Tanzania iliwasilisha mapendekezo 15 kwa Serikali ya Kenya yanayopaswa kupatiwa ufumbuzi, ambapo kwa upande wa Kenya waliwasilisha mapendekezo 16 ambapo kwa kiasi kikubwa hoja hizo zimekubaliwa na kupatiwa majibu yake katika mkutano huo.

Prof. Mkenda alisema kupatikana kwa mwafaka wa majadiliano hayo ni maelekezo ya Viongozi Wakuu wa Mataifa hayo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa Tanzania na Uhurru Kenyatta wa Kenya kwa kuwa Viongozi hao wametaka suala hilo lipatiwe mwafaka wa haraka ili kuweza kuendeleza ushirikiano na uhusiano katika nyanja mbalimbali baina ya nchi hizo.

Kwa mujibu wa Prof. Mkenda alisema mkutano huo uliofanyika kwa muda wa siku tatu ulilenga kumaliza changamoto za biashara zinazojitokeza kwa Wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya, ambapo Timu za Wataalam wa Serikali hizo ambapo hoja hizo zimeweza kujadiliwa na kupatiwa ufumbuzi wa pamoja, hatua inayolenga kufungua upya milango ya ushiriakiano baina ya Wafanyabiashara na Wakulima wa Tanzania na Kenya. 

“Katika majadiliano yetu tumekubaliana kuwa sasa bidhaa ya gesi ya kupikia na ungano wa ngano ambazo zilizuliwa kuingia Kenya sasa zitaruhusiwa kuingia nchini humo, na sisi kwa upande wetu Tanzania tumeruhusu maziwa na sigara kutoka Kenya zianze kuingia nchini” alisema Prof. Mkenda.

Akifafanua zaidi Mkenda anasema Mkutano huo pia uliwashirikisha Wafanyabiashara na Kampuni za uzalishaji wa bidhaa za ngano ikiwemo kampuni ya Azam Bakhressa ambayo huzalisha na kusambaza ngano hapa nchini pamoja na nchi jirani ikiwemo Kenya pamoja na wakulima wa zao hilo kutoka mikoa ya Sumbawanga, Iringa na Manyara.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Ushirikiano ya Kenya, Dkt. Chris Kiptoo alisema Serikali ya Kenya itayachulia kwa uzito unaostahili mwafaka wa majadiliano hayo, kwa kuzingatia kuwa Serikali ya Tanzania na Kenya zina uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu katika masuala ya biashara na uwekezaji.

Alisema kuwa Serikali ya Kenya imewekeza jumla Dola Bilioni 1.5 katika sekta ya viwanda, ambapo hadi sasa vimeweza kuajiri jumla ya watu 50,000 na pia msingi wa biashara ya Kenya katika Tanzania imeweza kuongeza kutoka Tsh. Bilioni 17 mwaka 2004 hadi kufikia Dola Bilioni 34 mwaka 2015.

Dkt. Kiptoo anasema mara baada ya mkutano huo, Viongozi wa Serikali hizo pamoja na Wafanyabiashara kutoka upande za Tanzania na Kenya wanatarajia kukutana kwa mara ya mwisho Mombasa nchini Kenya kwa ajili ya kuhitimisha makubaliano ya pamoja ya uingizaji na usafirishaji wa bidhaa.

Akifafanua zaidi Dkt. Kiptoo anasema katika majadiliano hayo Idara muhimu zinazohusika na masuala ya biashara na uwekezaji kutoka Serikali za Tanzania na Kenya zilishiriki katika mkutano huo, ikiwemo Maafisa wa Idara za forodha, kodi na ushuru.

Tarehe 3 Agosti mwaka huu, Viongozi Waandamizi wa Serikali za Tanzania na Kenya walikutana katika Mpaka wa Namanga kwa ajili ya kikao cha majadiliano ya pamoja kilicholenga kumaliza mzozo wa kuzuiwa kwa Wafanyabiashara ya Ngano nchini kuingiza bidhaa hiyo nchini Kenya.

WAZIRI WA FEDHA AKAGUA NA KUTOA MAAGIZO KUHUSU MADINI YA ALMASI YALIYOKAMATWA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MWALIMU JULIUS NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango (katikati) akiwa na viongozi wengine wa Serikali, Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) Biswalo Mganga (kushoto), Kamishna Mkuu wa  Mamlaka ya Mapato nchini TRA Charles Kichere(kulia) Naibu Kamishna Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo wakiangalia Mzigo wa Almasi uliokamatwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango akisoma maelezo ya mzigo huo ambayo yalikuwa tofauti kabisa na uhalisia mara baada ya kuhakikiwa na timu ya  Wataalamu wa Kitanzania wazalendo.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango akipata maelezo ya mzigo huo ambayo yalikuwa tofauti kabisa na uhalisia mara baada ya kuhakikiwa na timu ya  Wataalamu wa Kitanzania wazalendo.
 Sehemu ya Mzigo huuo wa Almasi uliokamatwa katika uwanja wa Ndege ambao thamani yake ni zaidi ya Tsh. Bilioni 65.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango akizungumza wakati akipokea Ripoti ya Uchunguzi wa Madini hayo ya Almasi jijini Dar es Salaam.
Profesa Abdulkarim Mruma akiwasilisha Taarifa yake ya Uchunguzi wa Madini yaliyokamatwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Mpiga Picha Maalum.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiongea na wanahabari baada ya kufanya  ziara ya kushtukiza, kufuatilia Almasi iliyokamatwa ikisafirishwa kwenda nje ya nchi huku ikiwa imethaminiwa chini ya kiwango katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Naibu Kamishna Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo, Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Kichere na Kushoto kwake ni Kamishna wa Madini Tanzania Mhandisi Benjamini Mchwampaka Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano na kulia kabisa ni Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Bw. John Biswalo. 



Dare es Salaam, 09 Septemba, 2017: Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), ameviagiza vyombo vinavyohusika kuchukua hatua za kisheria dhidi ya kampuni ya Williamson Diamond Ltd na wote waliohusika kuidhinisha usafirishaji wa madini ya almasi kutoka migodi ya kampuni hiyo na kudanganya thamani halisi ya madini hayo kwa lengo la kuisababishia hasara Serikali. 
Dkt. Mpango ametoa agizo hilo leo tarehe 09 Septemba, 2017 baada ya kukagua madini ya almasi yaliyokamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam yakisafirishwa kupelekwa nchini Ubelgiji. 
Miongoni mwa hatua za kisheria ni pamoja na kutaifisha madini yote ya almasi yaliyokamatwa baada ya kubainika udanganyifu wa thamani yake halisi, kuwakamata na kuwachunguza wote waliohusika katika udanganyifu huo wakiwemo wajumbe wa bodi zilizomaliza muda wake na wafanyakazi waliopo na waliostaafu. 
Almasi hiyo ilikamatwa tarehe 31 Agosti, 2017 muda mfupi kabla ya kupakizwa kwenye ndege ili isafirishwe kwenda nchini Ubelgiji, na ilipochunguzwa ilibainika kuwa nyaraka za kampuni ya Williamson Diamond Ltd zimeonesha kuwa almasi hiyo ina thamani ya Dola za Marekani Milioni 14.798 sawa na Shilingi Bilioni 33 za Tanzania wakati thamani yake halisi ni Dola za Marekani Milioni 29.5 sawa na Shilingi Bilioni 65 za Tanzania. 
Kabla ya kukagua almasi hiyo Waziri Mpango amepokea taarifa ya timu ya wataalamu iliyofanya tathmini ya thamani halisi ya madini hayo ambapo kiongozi wa timu hiyo Prof. Abdulkarim Mruma amesema pamoja na kubaini upotevu mkubwa wa fedha, kuna dosari nyingine zikiwemo kukosekana kwa vifaa ya kupimia madini hayo, almasi kusafirishwa na kuuzwa sokoni bila uwepo wa mwakilishi wa Serikali na ameshauri hatua za udhibiti huo zifanyike katika madini yote yanayochimbwa hapa nchini.

Pamoja na kuipongeza timu iliyofanya tathmini hiyo na vyombo vya dola vilivyokamata madini hayo Waziri Mpango amesema Serikali itatekeleza ushauri wote uliotolewa na timu ya Prof. Mruma na kwamba kuanzia sasa almasi inayozalishwa hapa nchini itasindikizwa na maafisa wa Serikali hadi sokoni na inataka kuanza kupokea gawio halali kutoka mgodi huo. 

Waziri Mpango ametoa maagizo hayo mbele ya viongozi wa vyombo mbalimbli wakiwemo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Bw. Biswalo Mganga, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Julius Mbungo, Kamishna wa Madini Tanzania Mhandisi Benjamin Mchwampaka na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP - Lazaro Mambosasa. 

Imetolewa na Benny Mwaipaja
MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

WAKUU WA MIKOA 10 WAAGIZWA KUSIMAMIA PAMBA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wakuu wa Mikoa inayolima zao la pamba nchini kwenye makazi yake mjini Dodoma Septemba 9, 2017. Kulia kwake ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba, watatu kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo na wanne kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Maimuna Tarishi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa mikoa 10 inayolima pamba nchini wasimamie zao hilo kwa karibu ili kuinua uzalishaji wake na kuwaongezea kipato wananchi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni (Ijumaa, Septemba 8, 2017) wakati akizungumza na wakuu hao wa mikoa kwenye kikao alichokitiisha mjini Dodoma kujadili mbinu za kufufua zao hilo. Wakuu wa mikoa walioitwa kwenye kikao hicho ni kutoka mikoa ya Shinyanga, Singida, Kagera, Tabora, Morogoro, Mara, Mwanza, Simiyu, Katavi na Geita.

“Serikali imeamua kufufua mazao makuu matano ya biashara ambayo ni pamba, chai, kahawa, korosho na tumbaku na leo nimetaka nianze na ninyi wakuu wa mikoa ili mwende mkawasimamie watu wenu tunapokaribia kuanza msimu mpya,” alisema.

Waziri Mkuu alisema Serikali imeamua kusimamia kilimo cha pamba kuanzia maandalizi ya shamba, kupanda, matumizi ya pembejeo na dawa, kuvuna na kutafuta masoko na akawataka wasimamie katika maeneo yao ili kilimo cha zao hilo kiweze kubadilika.

“Kuna maafisa kilimo kwa kila Halmashauri iliyoko kwenye mikoa yenu. Maafisa kilimo hawa lazima wahusike kikamilifu. Moja ya majukumu yake kwa cheo chake, kazi kubwa aliyonayo ni kusimamia zao la pamba. Kama hajafanya kazi hiyo, usiridhike kuwa na afisa kilimo wa aina hiyo,” alisema.

“Ni lazima kila mmoja awe na mpango kazi, ausimamie na atoe matokeo ya kuwa zao hili limefanikiwa katika eneo lake. Tunataka zao hili lichukue nafasi yake ya namba moja. Heshima ya “Dhahabu Nyeupe” lazima irudi lakini pia ni vema mkumbuke kuwa zao la pamba ni uchumi, zao la pamba ni siasa katika mikoa yenu,” alisisitiza. 

Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba; Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI; Bw. Suleiman Jafo, Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Kilimo, Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Dkt. Tito Haule na Mkurugenzi Msaidizi wa Uhamasishaji Mazao, Bw. Beatus Malema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
40480 DODOMA, 

JUMAMOSI, SEPTEMBA 9, 2017.

VIKWAZO VYA KIBIASHARA VILIVYOPO KATI YA TANZANIA NA KENYA VYAONDOLEWA.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Biashara wa Kenya, Dr Chris Kiptoo akizungumza makubaliano waliyokubaliana kati ya Kenya na Tanzania kuhusiana kuondoa vikwazo vilivyopo katika biashara ya nchi mbili.
Katibu Mkuu wa biashara na uwekezaji nchini Tanzania, Adolph Mkenda akizungumza wakati wa majadiliano ya kibiashara kati ya Tanzania na Kenya na kuondoa vikwazo vilivyopo vya kibiashara kati ya nchi hizi mbili. Majadiliano hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa biashara wa Kenya, Dr Chris Kiptoo akimkabidhi repoti za kibiashara za nchini kwenya Katibu Mkuu wa biashara na uwekezaji nchini Tanzania, Adolph Mkendajijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kuondoa vikwazo vilivyopo vya kibiashara.
kibiashara
 Baadhi ya Wadau wa Biashara kutoka Tanzania na Kenya wakiwa katika mkutano wa majadiliano ya kuondoa vikwazo vya kibiashara kati ya nchi hizi mbili.
 Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. Pindi Chana akizungumza na wadau wa biashara kati ya Kenya na Tanzania jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Nchi za Tanzania na Kenya zimetimiza agizo la maraisi wake na kukubaliana kuondoa vikwazo vya biashara katika bidhaa za unga wa ngano na gesi ya kupikia kutoka Kenya na zile za Maziwa na Sigara kutoka Tanzania.
Aidha masuala mengine 15 kutoka Tanzania na 16 ya Kenya bado yako mezani na majadiliano yanaendelea.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakati wa kuhitimisha mazungumzo ya kibishara baina ya nchi hizo ya Siku mbili, Katibu Mkuu wa biashara na uwekezaji nchini Tanzania Adolph Mkenda amesema wamefikia makubaliano hayo ya kibiashara ili kuhakikisha wanatimiza matakwa ya viongozi  wakuu, Rais John Pombe Magufuli na Uhuru Kenyata, yaliyoyowataka wafanye kazi na kuondoa vikwazo vya  biashara mara moja katika nchi hizoi mbili kubwa ndani ya jimuiya ya Africa Mashariki,

Amesema, baada ya maagizo yao, kwa kushirikia na Katibu Mkuu wa biashara wa Kenya, Dr Chris Kiptoo walianza kuwasiliana kwa karibu ambapo kwa kuanzia walifanya mkutano katika mpaka wa Namanga kuangalia biashara inavyokwenda na vikwazo vilivyopo katika nchi hizo ambavyo vilitatuliwa baada ya kupitia masuala mbali mbali,

 Aidha amesema kupitia majadiliano hayo, wameweza kupatia ufumbuzi mambo mengi ikiwemo biashara ya ngano, ambapo amesema wamekubaliana kifungua biashara ya ngano katika nchi hizi na kuhahakikisha wanaiboresha zaidi ikiwamo kutoa kipaumbele kwa wakulima wa zao hilo.

"Tulipata fursa ya kukaa na wadau wa biashara ya unga na ngano yenyewe kutoka nchi hizi mbili, wakiwemo wadau wenye viwanda vya kusaga ngano, wakulima na maafisa wa wizara za kilimo kutoka nchi zote ambao tumekubakiana kufungua biashara ya unga wa ngano kati ya Kenya na Tanzania, na sasa hivi unga wa ngano unapita unavuka mpaka bila vikwazo vyovyote." Amesema Mkenda

Kenya sasa hivi inazalisha ngano nyingi kuliko Tanzania na Tanzania ina uwezo mkubwa wa kuzalisha ngano kuliko Kenya hivyo tukiunganisha biashara na uwezeshaji,ngano ya Kenya itaongezeka na maeneo mengi Tanzania ambayo yanauwezo wa kuzalisha ngano yataongeza uzalishaji wa ngano

Aidha alisema wamekubaliana na wenye viwanda waanze kutumia ngano za kutoka nchini kabla kuagiza kutoka nje ya nchi hizi mbili na waonyeshe nia nzuri ya kujenga ushirikiano Wa jumuiya hii ya Africa Mashariki..

Kwa upande wake, katibu Mkuu Wa Kenya, Dr Chris's Kaptoo amesema, Kenya imewekeza zaidi dola bilioni moja na nusu nchini Tanzania kwa ajili ya masuala mbali mbali ya kibiashara na viwanda ambapo watu zaidi ya elfu 50 wameajiriwa.

 Ameogeza katika kuendeleza biashara katika nchi hizi mbili, watatumia Uchumi na Nakumati supermarket na kuhakikisha zinafanya kazi inavyopaswa na wale wanaopeleka bidhaa zao wanalipwa kwa wakati.
"Tunafanya bidii kuona Uchumi Supermarket inaimarika, tunataka matawi yake yote yaliyokuwepo Tanzania yanaendelea kama yalivyokuwa awali na pia wale wote watakao kuwa wanapeleka bidhaa zao huko wanalipwa kwa wakati" amesema Dr Kiptoo"

Amesema, siyo wajibu wake yeye katibu kuingilia biashara za watu binafsi kama Nakumat na Uchumi lakini kwa umuhimu wa biashara wanaingilia kati kuhakikisha iko salama na inatimiza matakwa ya nchi.

MAHAFALI YA 44 SHULE YA MSINGI YA WATOTO WENYE ULEMAVU YA JESHI LA WAOKOVU JIJINI DAR ES SALAM LEO.

$
0
0
Watoto wenye ulemavu wakitoa burudani mbele ya Mgeni rasmi pamoja na wazazi wa watoto hao waliohudhuria katika mahafali ya wanafunzi wa Darsa la saba 2017 jijini Dar es Salaam leo.
VIFIJO na ndelemo vilivyochangamana na majozi kwa wanafunzi wanaohitimu masomo yao ya shule ya msingi katika shule ya watoto wenye ulemavu ya Jeshi la Wokovu jijini Dar es Salaam leo.

Furaha iliyoje kwa watoto waliohitimu masomo ya msingi na majozi kwa waliobakia, ikiwa risala ya wahitimu imetoa changamoto mbalimbali kwa watoto wenye ulemavu ikiwemo vifaa visaidizi kwa watoto hao pamoja na mafuta ya kupaka kwa watoto wenye ulemvu wa ngozi(Albino).

Akizungumza katika mahafali hayo jijini Dar es Salaam leo, Mwalimu wa Michezo katika shule ya Msingi Jeshi la Wokovu, Emmanuel Ibrahim ameiomba serikali kuwaruhusu watoto hao wenye ulemavu na wanavipaji mbalimbali washiriki mashindano ya Kitaifa pamoja na ya kimataifa kama watoto wengine.

Pia wameomba kuongezewa Madaktari watakaotoa huduma ya afya kwa watoto hao wenye ulemavu ilikukidhi mahitaji ya watoto wenyeulemavu shuleni hapo.
Mkurugenzi wa shule ya msingi ya Jeshi la wokovu iliyopo Tameke jijini Dar es Salaam, Luteni Thomas Sinana akisoma risala ya shule hiyo kwa mgeni rasmi na kutaja changamoto mbalimbali zinazoikabiri shule hiyo inayohudumia watoto walemavu katika hafla ya mahafali ya wanafunzi wanao hitimu masomo yao ya shule ya msingi jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi wa shule ya msingi ya Jeshi la wokovu iliyopo Tameke jijini Dar es Salaam, Luteni Thomas Sinana akimkabidhi Mgeni Rasmi katika mahafali ya shule ya msingi ya watoto wenye ulemavu mbalimbali, Kamishina wa ustawi wa Jamii, Rabikira Mushi katika hafla ya wanafunzi wa Darsasa la Saba 2017 jijini Dar es Salaam leo.
Mgeni Rasmi katika mahafali ya shule ya msingi ya watoto wenye ulemavu mbalimbali, Kamishina wa ustawi wa Jamii, Rabikira Mushi akizungumza na watoto pamoja na wazazi katika hafla ya wanafunzi wa Darsasa la Saba 2017 jijini Dar es Salaam leo. Pia amesema changamoto mbalimbali zilizotajwa kati Risala ya watoto hanaohitimu zitashughulikiwa.
 Katibu  wa Kanisa la Jeshi la waokovu, Luteni Kanali Samweli Mkami akizungumza na wahitimu pamoja na wazazi wenye watoto walemavu wasiwafiche waende katika shule ya jeshi la wokovu ili kujipatia malezi mazuri pamoja na elimu katika shule hiyo.
wahitimu wa shule ya msingi Jeshi la Wokovu na Watoto wenye ulemavu tofauti tofauti wakitumbuiza ngojera mbele ya mgeni rasmi zilizokuwa na mahusia mazuri kwa wazazi wenye watoto wenye ulemavu pamoja na kuwashuru walezi na walimu wao kwa kuwalea tangu walipokuwa Darsa la kwanza mapaka sasa wanahitimu masomo yao ya shule ya msingi.
 Wahitimu wa Shule ya Msingi Jeshi la wokovu wakimsiliziza mgeni rasmi jijini Dar es Salaam leo wakati wa mahafali ya kuwaaga.
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya msingi  ya watoto wenye ulemavu ya Jeshi la wokovu iliyopo Temeke Jijini Dar es Salaam, Neema Urio akizungumza kwa niaba ya Kamati ya shule na kuwashukuru walezi wa watoto wenye ulemavu katika shule hiyo jijini Dar es Salaam leo katika mahafari ya kuhitimu Msomo ya Shule ya Msingi ya wanafunzi 24 .
 Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya msingi  ya watoto wenye ulemavu ya Jeshi la wokovu iliyopo Temeke Jijini Dar es Salaam, Neema Urio akiwa na Mwalimu wa Mazoezi katika shule ya Msini Jeshi la Wokovu, Emmanuel Ibrahim katika mahafari ya Wanafunzi wa Darasa la saba wanao hitimu masomo yao ya shule ya msingi.


 Burudani ikiendelea kati ya wazazi na watoto wenye ulemavu katika mahafali ya shule ya Msingi Jeshi la Wokovu jijini Dar es Salaam leo.
 Mmoja ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi akimsaidia mwenzake Mwenye ulemavu wa Viungo katika Mahafali ya Wahitimu wa Darasa la saba 2017 katika shule ya Msingi Jeshi la wokovu Jijini Dar es Salaam.
 Wahitimu wa Masomo ya Shule ya Msingi katika shule ya Jeshi la wokovu jijjini Dar es Salaam wakisoma risala mbele ya Mgeni rasmi.


 Wahitimu 24 katika shule ya Msingi Jeshi la Wokovu wakitumbuiza katika mahafari yao ya Kuhitimu Masomo ya Shule ya Msingi jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya walimu na walezi wa wanafunzi walemavu wa shule ya msingi Jeshi la waokovu wakiwa katika mahafali ya wanafunzi 24 waliohitimu masomo yao ya shule ya Msingi.
 
 Bendi ya Jeshi ikitumbuiza katika mahafili ya wanafunzi wanaohitimu masomo yao ya shule ya msingi jijini Dar es Salaam leo.
 Wahitimu wa masomo ya Darasa la Saba katika shule ya Msingi Jeshi la Wokovu wakitoa zawadi kwa waliimu wao pamoja na walezi wao kwa kuwajua sauti zao pamoja na matendo ambayo huwafanyia watoto hao pia kwa kuwaita kwa kuigiza sauti zao.













 Mgeni Rsmi akipokea zawadi kutoka kwa wahitimu wa Darsa la saba katika shule ya Msingi Jeshi la Wokovu jijini Dar es Salaam leo.

 Wakati  kutoa zawadi na vyeti kwa wahitimu wa shule ya Msingi Jeshi la waokovu jijini Dar es Salaam leo.





















Picha zote na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

TANZIA: KAMISHNA MSTAAFU WA OPERESHENI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KUAGWA KESHO JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini – Thobias Andengenye, ataongoza Maafisa na Askari katika zoezi la kuuaga mwili wa Marehemu na kutoa heshima za mwisho (Kwa Paredi Maalum), kwa aliyekuwa Kamishna Mstaafu wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CF (OPS) Rogatius Peter Kipali, ambaye alifariki dunia Semptemba 7, 2017 akiwa nyumbani kwake Mombasa, Ukonga Jijini Dar es Salaam.

Zoezi la kuuaga mwili wa Marehemu litafanyika kesho Semptemba 10, 2017 kuanzia saa 3:00 asubuhi katika viwanja vya Kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala eneo la (FIRE) Jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anapenda kuvitaarifu Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Maafisa, Askari na Watumishi wote wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, , familia ya Marehemu na wale wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine kujitokeza kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho.


IFUATAYO NI RATIBA NZIMA YA MSIBA

Bwana alitoa na bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe

Amina.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI.

WANANCHI WAENDELEA KUMIMINIKA KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA KUPIMA AFYA

$
0
0
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk.Grace Magembe akitoa maelekezo kwa wananchi waliofika katika upimaji wa afya kwenye  viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam.
 Wazazi na walezi wakiendelea kumiminika kusajili watoto wao na bima ya afya ya Toto Afya Kadi  kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa ni kampeni ya Afya Mkoa wa DSM. Pichani watumishi wa NHIF wakiendelea na uandikishaji .
 Maafisa wa NHIF wakitoa maelekezo kwa wazazi namna ya kujaza fomu za bima ya Toto Afya Kadi, leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Masoko wa Tanga Fresh Ltd, Ally Sechonge akigawa maziwa kwa wananchi  waliofika katika upimaji wa afya ndani ya viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wananchi waliofika katika upimaji wa afya ndani ya viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

MAKONDA AWEKA JIWE MSINGI LAUJENZI WA VIWANDA VIDOGO VIDOGO KATIKA KARAKANA YA JIJI LA DAR ES SALAAM.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es`Salaam Paul Makonda akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa viwanda vidogo vidogo katika karakana ya jiji la Dar es Salaam iliyopo Mwananyamala leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya majengo ya mradi wa viwanda vidogo vidogo katika karakana ya jiji iliyopo Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China ,Dk. Lu Youqing akipiga mpira katika uwanja bandari wakati makabidhiano ya uwanja huo na Mkuu wa Dar es Salaam, Paul Makonda. 
Monekano wa Uwanja wa Bandari uliokarabatiwa na Ubalozi wa China leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amezitaka Manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam zitengeneze mazingira rafiki kwa wajasiriamali wadogo ili kuwawezesha na fursa mbalimbali za biashara . 

Makonda ameyasema hayo leo wakati wa kuweka jiwe la msingi katika uzinduzi wa viwanda vidogovidogo katika Karakana ya Jiji iliyopo Mwananyamala Jijini Dar es Salaam, amesema kuweka mazingira rafiki ya viwanda kutasaidia wajasiriamali kujitokeza na kuyatumia na nchi kuweza kupata maendeleo pamoja na kukuza uchumi wa kufikia uchumi wa kati. 

"Niwapongeze kwa kazi mnayoifanya kwa manispaa lakini pia kuunga mkono jitihada za wajasiriamali kwa kuwapa mikopo kupitia vikundi vyao na nitoe wito pia kwa watendaji msitoe mikopo holela itakuwa kazi kuzirejesha" Amesema RC Makonda. 

Aidha amesema kuwa Halmashauri ya Jiji imejenga mazingira rafiki kwa kuanza kutoa Ruzuku kwa manispaa ambapo ilikuwa hafanyi hivyo katika miaka iliyopopita.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,Sipora ya Liana amesema kuwa kupitia mradi huo Jiji la Dar es Salaam limeendelea kutoa kipaumbele kwa wanawake, vijana na walemavu wanaopata mikopo kutoka Halmashauri ya Jiji kwa kuona mazingira wanayofanyia kazi sio rafiki na wanahangaika sana kupata masoko.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMAPILI LEO SEPT 10, 2017

RC MASENZA: MARUFUKU WENYEVITI WA MITAA NA VIJIJI KUJIHUSISHA NA UUZAJI WA ARDHI

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akizungumza na wadau mbalimbali wa wilaya ya mufindi wakati wa kutambulisha mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa Mafinga uliokuwa na lengo la kuonyesha dira ya miaka ya hamsini (50) ya maendeleo ya mji wa Mafinga ambapo inasemeka ni moja kati ya miji inayokuwa kwa kasi .

hawa ni baadhi ya wadau waliojitokeza katika ukumbu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya mufindi kushuhudia utambulisho wa mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa mafinga.


Na Fredy Mgunda, Iringa

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ametaka wenyeviti wa vijiji au wa mitaa kutojihusisha na uuzaji wa ardhi ili kuondoa migogoro ambayo imekuwa ikisababishwa na viongozi hao.

Akizungumza wakati wa utambulisho wa mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa Mafinga, Masenza alisema kuwa kumekuwa na migogoro ambayo inasababishwa na wenyeviti wa serkali za vijiji au mtaa hivyo ni marufuku viongozi hao kujihusisha na swala hilo.

“Sipendi kusikia mwenyekiti wa mtaa au mwenyekiti wa kijiji akihusisha kuwa shahidi wa uuzwaji wa ardhi kwa kuwa hilo sio jukumu lao waichie mamlaka ya ardhi kufanya kazi kwa utaalamu wao”alisema Masenza

Aidha Masenza alimtaka wakurugenzi wote wa mkoa wa iringa kuwaambia ukweli viongozi juu ya sheria ya uuzaji wa ardhi ili kuondoa migogoro inayosababisha maumivu kwa upande unaonewa na kudhurumiwa haki yao ya msingi na kusababisha kumrudisha nyuma kimaendeleo.

“Wakurugenzi waambieni vijana wetu waache ujanja ujanja wa kupokea,kuchora,kuonyesha na kuelekeza swala lolote linalohusu uuzwaji wa ardhi ili hii mipango kabambe ya halmashuri ziende vizuri kama serikali inavyopanga”alisema Masenza

Masenza alisema kuwa acheni kufanya kazi kwa ujanja ujanja maana serikali ya uwamu ya tano chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe maguli haitaki wananchi na viongozi kuishi kwa mazoea.

Sixbet Kayombo ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Balali katika halmashauri ya mji wa Mafinga alisema kuwa tamko la mkuu wa mkoa lianukweli ndani yake kwa kuwa kuna wenyeviti wengi wamekuwa wakisababisha migogoro isiyokuwa na maana kwa uroho wa kupokea pesa.

“Lakini ukiangalia kwa undani utagundua kuwa haiwezekani wananchi kuuza ardhi bila kuwepo ushaidi wa serikali ya mtaa hivyo tunamuomba mkuu wa mkoa kutafuta njia mbadala ili mwananchi asiwe na ukakasi wowte wakati wa uuzaji wa ardhi yake” alisema Kayombo

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Amani kata ya Upendo Merikioni Ndelwa alisema kuwa tatizo hilo limekuwa kubwa hasa vijijini kwa kuwa viongozi wengi bado hawana elimu ya mwisho wa madaraka yaho hivyo tunamuomba mkuu wa mkao kutoka elimu wa wenyeviti ili kuepusha migogoro ya ardhi.

SHAKA AMTEMBELEA WAZIRI MKUU MSTAAFU JOHN MALECELA NYUMBANI KWAKE MJINI DODOMA.

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela akizungumza na Kaimu Katibu wa umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka (kushoto) wakati alipomtembelea, nyumbani kwake mjini Dodoma

Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela akimwonyesha kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka kinyango chenye uzito wa tani 1 wakati alipomtembelea, nyumbani kwake mjini Dodoma
Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela akimwelezea kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka picha iliochorwa na Mwanafinzi wa darasa la saba Mwaka 1982 wakati wa hali ngumu ya uchumi nchini.
Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela akimwelezea kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka picha iliyochorwa na mjuu wake ikimuonesha yeye na Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

 Picha ya pamoja Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela na Kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka picha
 kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM ) Shaka Hamdu Shaka  akimuaga  Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela alipomtembelea nyumbani kwake Mtaa wa Kilimani Mjini Dodoma(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)..

CHINA KUONGEZA NGUVU ZOEZI LA UPIMAJI AFYA BURE DSM

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akiongeza na Balozi wa China Nchini Tanzania Dr.Lu Youqing na ujumbe wake katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo zoezi la upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa Dar es Salaam limeingia siku ya Nne. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akizunguza na wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Mnazi Mmooja kwa ajili ya kupima afya


Balozi wa Jamhuri ya watu wa China anaemaliza Muda wake nchini amemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo zoezi la upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa Dar es Salaam limeingia siku ya Nne.

Mhe Balozi wa China akiwa ameambatana na Maofisa wa Ubalozi huo hapa nchini Ameshangazwa na UBUNIFU wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda wa kuwasaidia wananchi wengi wa Mkoa kwa WAKATI MMOJA hususani ni wenye vipato vya Chini ambao idadi kubwa hawawezi kumudu Gharama za matibabu nje ya mifumo rasmi iliyowekwa na Serikali mfano wa Bima ya Afya.

Kutokana na Mkusanyiko huo wa Maelfu ya wananchi Mhe Balozi wa China amesema Serikali ya Jamhuri ya watu wa China imeamua KUUNGA mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda na kuanzia sasa na kuendelea serikali ya ya Jamhuri ya watu wa China itaungana na Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam katika kusaidia zoezi upimaji Afya BURE kwa kufanya yafuatayo :-

1. Serikali ya China italeta Madaktari Bingwa kutoka China ambao wataungana na Madaktari wa Timu maalum ya Mhe Makonda ambao wamekuwa wakitoa huduma za upimaji Afya Bure hivyo Madaktari wa Tanzania wataungana na Madaktari wa China katoka kuendesha huduma ya Utoaji wa Afya Bure Mkoa wa Dar es Salaam. 

2. Serikali ya China itatoa vifaa vya kisasa vya UPIMAJI ambazo vitasaidia kuongeza kasi ya upimaji kwa watu wengi zaidi. 

3. Serikali ya China ITAGHARAMIA dawa kwa watu wasio na UWEZO wa kumudu Gharama za ununuaji dawa mara baada ya kupimwa na kuandikiwa dawa.

Mhe Balozi wa China amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kumuunga mkono Mhe Makonda hatua ambayo imeishawishi serikali ya China kusaidia katika zoezi hilo zuri lenye Malengo ya kutoa huduma bora za Afya kwa Wananchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda AMEMSHUKURU balozi wa China kwa Niaba ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kukubali kuunga mkono Jitihada za kuboresha Afya za wananchi wake, ambapo amesema wazo hilo la kutoa HUDUMA ZA upimaji bure wa Afya alilianza tangu akiwa Mkuu wa Wilaya ya KINONDONI, na kumuhakikisha balozi huyo kuwa hilo litakuwa zoezi ENDELEVU kwa Mkoa wa Dar es Salaam likiwa na Malengo makubwa matatu ambayo ni :-

1. Kuongeza UELEWA kwa Wananchi kuhusu umuhimu wa Upimaji wa Afya hata kama hawaumwi. 

2. Kuwawezesha wananchi WANYONGE kupata huduma za AWALI za upimaji wa Afya ili kuwasaidia mapema katika hatua za AWALI kugundua matatizo yao. 

3. Kubaini magonjwa ambayo husababisha VIFO katika hatua za AWALI.

Mhe Makonda amesema kwa ujumla hatua anazozifanya Katia Sekta ya Afya zinalenga kuunga mkono jitihada na kipaumbele cha Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika masuala ya Afya, na ni kwa sababu hiyo ameamua kuendelea kupambana na changamoto zilizoko kwenye Sekta ya Afya pasipo kusubiria fedha za Bajeti ambazo hata hivyo hazitoshelezi mahitaji halisi ya Afya kwa Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam.

BODI YA CHAKULA DAWA NA VIPODOZI YAANGAMIZA CHAKULA AINA YA SOSEJI ZILIZOKWISHA MUDA WAKE KIBELE WILAYA YA KUSINI UNGUJA.

$
0
0
Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi wakiteremsha boksi za Chakula aina ya Soseji zilizokwisha muda wake kwa ajili ya kuangamizwa baada ya kugundulika katika Ghala la chakula linalomilikiwa na Kampuni ya Best Inmport Maruhubi na wakaguzi ,Kibele Wilaya ya Kusini Unguja.
Chakula aina ya Soseji zilizokwisha muda wake zikiwa zimekusanya kwa ajili ya kuangamizwa baada ya kugundulika katika Ghala la chakula linalomilikiwa na Kampuni ya Best Inmport Maruhubi na wakaguzi ,Kibele Wilaya ya Kusini Unguja.
Mkuu wa kitengo cha Ufatiliaji madhara ya Chakula Aisha Suleiman akizungumza na Waandishi wa Habari katika zoezi la kuangamiza Chakula aina ya Soseji zilizokwisha muda wake na kwamba hazifai kutumiwa na maisha ya Binaadamu ,Kibele Wilaya ya Kusini Unguja.
Mkaguzi wa Chakula Bi Amina Ramadhan Salim akizungumza na Waandishi wa Habari katika zoezi la kuangamiza Chakula aina ya Soseji zilizokwisha muda wake na kwamba hazifai kutumiwa na maisha ya Binaadamu ,Kibele Wilaya ya Kusini Unguja.
Chakula aina ya Soseji zilizokwisha muda wake zikisangwa na baadae kufukiwa baada ya kugundulika kua hazifai kutumiwa na maisha ya Binaadamu ,Kibele Wilaya ya Kusini Unguja.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Wanachama TEN/MET watoa hoja nzito kwa Kamati ya Kudumu ya Huduma za Jamii

$
0
0
Mwanachama wa TEN/MET toka taasisi ya FAWETZ, Bi. Neema Katundu (kulia) akiwasilisha hoja mbalimbali kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii jana mjini Dodoma juu ya maboresho katika sekta ya elimu. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba (kushoto) na katibu wake kulia wakizungumza na wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) jana mjini Dodoma.


Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MTANDAO wa Elimu Tanzania (TEN/MET) umekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii na kuwasilisha hoja mbalimbali za kufanyiwa kazi na Serikali kupitia sekta ya elimu lengo likiwa ni kuhakikisha elimu bora inapatikana nchini Tanzania.

Akiwasilisha hoja hizo mahususi 14 mjini Dodoma, Mwanachama wa TEN/MET toka taasisi ya FAWETZ, Bi. Neema Katundu alisema hii ni mara ya pili kuwasilisha hoja na lengo la msingi ni kuitaka serikali kuingiza katika utekelezaji.

Bi. Katundu alisema wanaikumbusha Serikali kuhakikisha inatenga hadi asilimia 20 ya bajeti ya taifa kwenye sekta ya elimu na pia kuwekeza zaidi katika kuziba mianya ya upotevu wa mapato na matumizi mabaya ya fedha toka mapato ya ndani ili iweze kutumika uboreshaji elimu ya msingi nchini.

Alisema hoja zingine walizowasilisha Serikalini ni pamoja na kutaka utoaji wa ruzuku shuleni hali halisi ya mahitaji ya sasa na kuhakikisha mchakato wa kuanzishwa kwa Bodi ya Taaluma ya uwalimu itakayoongeza tija na kulinda maslahi ya walimu katika sekta hiyo.

Aidha, hoja zingine walizowasilisha kwa kamati hiyo ni kutaka kuimarishwa kwa idara ya kudhibiti ubora (ukaguzi) na ipewe mamlaka na vitendea kazi kiuhalisia ili iweze kufanya kazi yake kiufasaha, uzingatiwaji wa haki za watoto na pia kuundwa kwa chombo maalumu cha usimamizi, utungaji na utekelezaji wa sera ya elimu.

Walishauri Serikali kutoa kipaumbele cha bajeti kwa sekta ya elimu kama ilivyofanywa kwa sekta ya miundombinu miaka miwili iliyopita, Serikali za mitaa kutunga na kusimamia sheria ndogondogo zitakazo wabana wazazi wanaowanyima watoto haki ya elimu, huku wakiomba fedha za mikopo ya elimu ya juu kutenganishwa na fedha za maendeleo ya wizara ya elimu.

Kilio kingine kilichofikishwa katika kamati hiyo ya Bunge ya Huduma za Jamii, ni pamoja na kutaka kuhimarishwa kwa kamati za shule, kuhamashishwa kwa wazazi kuchangia maendeleo ya watoto wao kielimu, kuingiza kipengele cha elimu ya mlipa kodi katika mitaala ya elimu na pia serikali kupunguza vigezo katika upatikanaji wa mikopo ya elimu ya juu na kuongeza bajeti eneo hilo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba aliwashukuru wanachama wa TEN/MET kwa kuwa wazalendo kuipigania elimu nchini, hivyo kuwataka watoe muda kwa kamati hiyo ili iweze kuzifanyia kazi hoja hizo kwa maendeleo ya taifa. 
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii ikiwa katika kikao na Wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET). 
Afisa Programu toka HakiElimu, Makuba Mwemezi (kushoto) ambaye pia ni mwanachama wa TEN/MET akichangia hoja katika kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii. 
Kikao hicho kikiendelea jana mjini Dodoma.

Rais Dkt Magufuli amteua Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania

$
0
0
Prof. Ibrahim Hamis Juma alieteuliwa na Rais kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania



MWANRI ATOA MWEZI MMOJA KWA WAMILIKI WA KIWANDA CHA MANOGA KUHAKIKISHA KINAANZA KAZI.

$
0
0
Baadhi ya mitambo ya Kiwanda cha Pamba cha Manonga wilayani Igunga ambayo ilikuwa ikutumika kuchambua Pamba na kuzalisha mafuta yake ambayo hafanyi kazi kwa kipindi kirefu baada ya wamiliki wake kusimamisha uzalishaji. Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri( hayupo katika picha) jana ametoa mwezi mmoja mitambo hiyo ianze kufanya kazi.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (aliye mbele) akiangalia mmoja wa mitambo baaya kutembelea Kiwanda cha Pamba cha Manonga jana wilayani Igunga kwa ajili ya kujionea hali halisi kilivyo hivi na mahitaji yake ili kianze upya uzalishaji.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kulia) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU) Robert Mayongela Jongera (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo (kulia) baada viongozi mbalimbali kutembelea Kiwanda cha Pamba cha Manonga jana wilayani Igunga kwa ajili ya kujionea hali halisi kilivyo hivi na mahitaji yake ili kianze upya uzalishaji.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kulia) akiwasisitiza wamiliki wa Kiwanda cha Pamba cha Manonga kilichopo wilayani Igunga kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja mitambo ya kiwanda hicho iwe imeshaanza kazi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo. Mkuu wa Mkoa alitoa maelezo hayo jana alikwenda kutafuta sababu za kwanini hakiendelei na uzalishaji kwa zaidi ya miaka 20.

Na Tiganya Vincent-RS-Tabora.

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imetoa mwezi mmoja kwa wamiliki wa Kiwanda cha Pamba cha Manonga kuhakikisha wamekikarabati ili kiweze kuanza tena uzalishaji wa mafuta ya pamba na uchambuzi wa Pamba na kutengeneza ajira kwa vijana mkoani hapo.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri jana wilayani Igunga wakati alipokwenda kujionea hali halisi ya kiwanda hicho ambacho kwa maika zaidi ya 20 hakifanyi kazi.

Alisema kuwa baada mwezi mmoja huo kukamilika atafanya ziara Kiwandani hapo ili kuhakikisha kama ukarabati umeshakamilika na mitambo imeshaanza kufanya kazi na kinyume cha hapo atalazimika kumwandikia Waziri wenye dhamana na viwanda ili wamiliki wake wanyang’anye kwa ajili ya kumpa mwekezaji mwingine.

Mwanri aliwaagiza Wamiliki wa Kiwanda hicho ambao ni Rajani pamoja na Chama Kikuu cha Ushirika cha Igembensabo kupanga ratiba ya mpango kazi wa utekelezaji shughuli zitakazoonyesha mipango ya ufufuaji na muda wa ukamilishaji kwa ajili kufanikisha zoezi hilo ndani ya muda ulipangwa , vinginevyo watashindwa.

“Tengenezeni ratiba itakayowasaidia katika upangaji wa mambo yenu,Mfano siku fulani mnakwenda TANESCO kwa ajili ya kuomba umeme three phase ili kuachana na ule single phase ambao mnasemaje hauwezi kuwasaidia katika uendeshaji wa kiwanda chenu…kisha mnapanga siku ya kufuatilia upatikanaji wa maji kiwandani mtaona mambo yanakwenda mbamumbamu na ukarabati ukamika kwa wakati” alisisitiza Mwanri.

“Nataka nikirudi hapa nikute mitambo inaunguruma…vingine nitamwita Mheshimiwa Mwijage aje hapa kuchukua kiwanda hiki…sitaki mambo yafike huko fanye kazi ili kiwanda kianze uzalishaji na vijana wetu wapate ajira” alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Mmoja wa Wabia katika Umikili wa Kiwanda cha Pamba cha Manonga Urveshi Rajani alisema kuwa watahakikisha kuwa ndani ya mwezi mmoja Kiwanda hicho kinakuwa tayari kwa ajili ya uzalishaji wa mafuta ya pamba na uchambaji wa zao hilo.

Alitoa wito kwa viongozi kuhakikisha wanahamasisha wakulima kulima pamba kwa wingi ili Kiwanda cha kiwe na malighafi za kosha kwa ajili ya uzalishaji wa mafuta na uchambuzi wa zao hilo.

Naye Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) Jospeh Mihangwa alisema kuwa mitambo ya Kiwanda cha Pamba cha Mananga ni mizuri na inasaidia kuchamba pamba bila kukatakata na hivyo kuwa na soko kubwa duniani.

Alisema kuwa kwa sababu ya ubora wa kiwanda hicho wao kama majirani na Mkoa wa Tabora wako tayari kushirikiana na wamiliki wake kama watahitaji msaada wa mafundi wa kusaidia kukarabati mitambo ili kianze tena uzalishaji kwa sababu kiwanda hicho ni muhimu sana katika uchambuzi wa pamba.

“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kiwanda hiki ni kizuri sana kina mitambo ya Platt Lumus ambacho wakati wa uchambuaji wa pamba haikati nyuzi na kufanya pamba inachambua hapa iwe na bei kubwa katika soko la dunia…sisi kama watahiji msaada wa mafundi wa kusaidia kufufua tuko tayari kuwasaidia” alisema Meneja huyo Mkuu wa SHIRECU.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Revocatus Kuuli aliwahakikishia Wamiliki wa Kiwanda cha Pamba cha Manongo wasiwe na wasiwasi kuhusu upatikanaji malighafi ya kutosha kwa ajili ya kiwanda hicho,kwani uongozi umeshajipanga kuhakikisha msimu ujao wananchi walima Pamba kwa wingi na wanavuna pamba nyingi kuliko ya msimu uliopita.

Alisema pamoja na jitihada kuwa za muda mfupi msimu uliopita Wakulima katika Wilaya ya Igunga walifanikiwa kuzalisha kilo 10, 700,000 ,msimu ujao wanatarajia mavuno kuwa mara mbili ya kilo hizo na hivyo kuwa malighafi nyingi kwa ajili ya viwanda..

Kiwanda hicho kinamilikiwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Igembensabo kwa asilimia 20 na M/S Rajani Metals and Machinery Ltd mwenyewe anamikili asilimia 80.

Kiwanda cha Manonga ambacho kilijengwa mwaka 1958 na Kampuni ya wafanyabiashara binafsi na mnamo mwaka 1962 Serikali ilikitaifisha na kuipatia Kampuni ya Wakulima wa Kahama na Nzega (KANZECO) kina miaka zaidi ya ishirini bila kufanya kazi.

Twende App kuwawezesha wasafiri kupata huduma ya usafiri kupitia simu za mkononi.

$
0
0

Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) na Mkurugenzi wa Twende App Justin Kashaigili (kulia) wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma mpya ya simu za mkononi ijulikanayo kama Twende App inayiowawezesha wasari kupata huduma ya haraka na usalama ya usafiri wa umma wa Taxi, pikipiki za bodaboda na pikipiki za magurudumu matatu kwa kutumia simu za mkononi.

 Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania imeungana na kampni inayotoa huduma za usafiri Twende App kuzindua huduma mpya itakayowezehsa wasafiri kupata huduma bora, ya haraka na uhakika zaidi kupitia mfumo wa simu za mkononi unaojulikana kama Twende App.

TwendeApp ni mfumo wa kidigitali wa simu za mkononi unaowezesha wasafiri kutafuta na kupata usafiri wa taxi, pikipiki za magurudumu mawili (bodaboda) na zile za magurudumu matatu kupitia simu zao za mkononi kwa uhakika zaidi na kwa bei nafuu.

Twende App ambayo, tayari inatumika katika jiji la Dar es salaam, sasa imepanua wigo wake na kufikia miji ya Arusha, Morogoro, Mwanza, Kilimanjaro, Dodoma Iringa na Mbeya. Kuna mipango ya kusambaza huduma hiyo kwenda Zanzibar, Tanga na Mtwara.

Akizungumza katika uzinduzi wa Wende App jijini Arusha leo, Meneja Uhusiano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa Twende App inatumia teknologia ya GPS kwa kutegemea mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo. Hii inawahakikishia watumiaji huduma ya uhakika, haraka na yenye usalama wa hali ya juu.

‘Kwa sasa magari mengi ya usafiri wa taxi na bodaboda yamepaki kwenye vijiwe wakisubiri wateja. Twende App itawaunganisha madereva na wasafiri kwa muda na sehemu sahihi na inayohitajika. Kwa kupakua mfumio wa Twende App kwenye simu zao za mkononi, wasafiri wataweza kuwasiliana kwa haraka na madereva wa vyombo vya usafiri wa umma ambao wapo karibu zaidi na eneo husika ambapo usafiri wenyewe unahitajika. 
 
Hii inaondoa adha ya kutembea kutafuta usafiri na pia inapunguza muda wa kusubiri usafiri kwani mteja anawasiliana kwa haraka na chombo cha usafiri kilichokuwa karibu zaidi naye. Kwa upande wa madereva, Twende App itawaokolea muda, kuwaongezea wateja na kuongeza mapato kwa kuwa hawahitaji tena kushinda kijiweni wakisubiri wateja,’ alisema.

‘Wateja wanaohitaji usafiri wanaweza kuona eneo ambalo madereva wapo kwa kutumia teknologia ya GPS na mfumo wa Google maps. Baada ya hapa watatuma ombi la kupata usafiri na moja kwa moja, mtandao huu wa Twende App utamjulisha dereva aliye karibu zaidi kuhusu ombi hili la usafiri na eneo ambalo msafiri yupo,’aliongeza.

Woinde aliongeza kuwa mfumo huu wa kisasa unapatikana kupitia simu za kisasa za kupangusa (smartphones), kwa hiyo utaongeza matumizi ya simu za kisasa nchini ikiwemo matumizi ya mfumo wa kutumia simu za mkononi kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa mbali mbali.

‘Twende App pia inakuletea matumizi ya Tigo pesa katika biashara ya usafiri. 
 
Hii inaendana na dhana kuu ya Tigo ambayo ni kuongeza matumizi ya mfumo wa digitali nchini pamoja na kutoa huduma ambazo zinaboresha na kujibu mahitajiya wateja wake nchini kote. Tunawaasa wateja wetu kujaribu mfumo huu mpya katika kipindi hiki cha Tigo Fiesta 2017 kama njia bora ya kwenda na kutoka kwenye matamasha ya msimu huu,’ Woinde alisema.

Mkurugenzi wa Twende App, Justin Kashaigili, alisema kuwa mfumo huu unatumia madereva na magari ambayo yana leseni halali za udereva na za biashara, na waliothibitishwa kutokuwa na historia ya uhalifu. Hii inawahakikishia wasafiri usalama wao. Kwa kushirikiana na Tigo, Twende App pia inatoa simu za kisasa zaidi ya 1,000 kwa madereva wanaojisajili na Twende App ili kuwawezesha madereva kufanya biashara zao kwa umakini zaidi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva Taxi wa Arusha, Ali Mohammed, aliusifu mfumo huo mpya huku akisema kuwa utawaongezea kipato, usalama na kuwapa uhakika zaidi katika biashara zao.

‘Kwa bahati mbaya kumekuwa na matukio ya uhalifu yanayohusu madereva na hata abiria wa usafiri wa umma. Twende App itasaidia kuondoa hofu baina ya dereva na msafiri kwani wote wanakuwa wamesajiliwa katika mfumo mmoja kwa hiyo hata upotevu wa aina yoyote ukitokea, suala la ufuatiliaji linakuwa rahisi,’ alisema.

SALASALA VISIONS GROUP WAMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI KWA KUWA WAZALENDO WA KWELI

$
0
0

Uzalendo limekuwa neno kuu katika siku za karibuni. Na wengi wetu tunatafsiri kama ni kuipenda na kuiweka Nchi yako mbele. Lakini sifa nyingine muhimu sana ya uzalendo ni kujitolea kwa faida au maendeleo ya 
.
Salasala Vision Group ( SVG) iliasisiwa miaka 5 iliyopita na wakazi wachache wa Salasala Kilimahewa lengo likiwa ni kisaidia masuala ya ulinzi, mazingira, miundombinu, michezo na kuchochea maendeleo ya wanachama wake wengi.
Hadi leo SVG imepanda miti zaidi ya 10,000, imetengeneza barabara za mitaa pamoja na kurekebisha barabara kuu, imetoa msaada vitendea kazi kwa polisi, kutengeneza viwanja vya michezo na pia kununua aridhi kwa wanachama wake zaidi ya hekari 250 huko Bagamoyo.
Wiki hii kwa mwaliko wa Spika wa Bunge SVG imetembelea Bungeni na kisha kucheza mechi na timu ya Bunge na kuibuka na ushindi wa bao 2 - 1.

UFUNGUZI WA UCHUNGUZI WA KINYWA NA MENO WAFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania Dokt,Lorna Carneiro kulia akitoa hotuba ya makaribisho katikaUfunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.

Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya katika Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt,Fadhil Abdalla akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.
Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya katika Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt,Fadhil Abdalla katikati akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari kutoka Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).pamoja na madaktari wa Zanzibar katika Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.
Daktari wa Kinywa na Meno kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt,Ismail Amour akitoa Elimu ya kujikinga na maradhi hayo katika Ufunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.


Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania Dokt,Lorna Carneiro kushoto akifanya mahojiano na Muandishi wa Habari kutoka ITV Farouk Kariym pamoja na muandishi wa Habari Maelezo Zanzibar Khadija Khamis katika Ufunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.

Daktari wa Kinywa na Meno kutoka Haspitali ya Arrahma Zanzibar akimfanyia Uchunguzi wa mardhi ya Kinywa na Meno Kauthar Vuai mkaazi wa meli nne, katika Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
 

Na Khadija Khamis –Maelezo

Jamii inatakiwa kuweka utaratibu wa kupima afya ikiwemo afya ya kinywa na meno ili kupatiwa uchunguzi wa awali pamoja na elimu sahihi ya afya angalau mara mbili kwa mwaka .

Hayo aliyaeleza na Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya Dr Fadhil Mo’hd Abdalla huko katika Kituo cha Afya Rahaleo, wakati akifungua zoezi la uchunguzi wa afya ya kinywa na meno linaloendeshwa na Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno kutoka Tanzania .

Alisema afya hiyo ni muhimu kufanyika awali kabla ya madhara, kwa kupatiwa ushauri wa mapema kabla ya athari kujitokeza na kusababishwa kupoteza meno .Alifahamisha kuwa katika miaka ya nyuma elimu ya afya ya kinywa na meno zilikuwa zikitolewa katika maskuli ,wataalamu hutoa elimu kwa wanafunzi pamoja na kung’oa meno kwa wale ambao meno yao yameadhirika .

Aidha alisema mpango huo wa uimarishaji afya ya jamii iko haja kurejea utaratibu wa kizamani , wataalamu wa afya ya kinywa na meno kutoa huduma za matibabu katika maeneo mbali mbali ikiwemo maeneo ya maskuli na vijijini .

“Huu usiwe mwanzo wa kuonyesha njia kwa jamii na wala msisubiri kuumwa kila muda mujiwekee utaratibu wa kujichunguza afya zenu ikiwemo afya ya kinywa na meno pamoja na maradhi yasioambukiza ili muweze kupata ushauri mapema kwa Madaktari ,”alisema Mkurugenzi Kinga.

Alieleza kutoa elimu na uchunguzi wa afya kwa jamii itasaidia kupunguza gharama za matibabu na kuimarisha kinga ya awali na kujiepusha na matumizi ya vyakula ambavyo vinachangia kuleta madhara ikiwemo vyakula vya sukari kuchangia uozeshaji wa meno hasa kwa watoto .

Nae Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno ( TBA) Dr Lorna Carneiro alisema mara hii wamepata fursa ya kuja Zanzibar kwa kufanya uchunguzi wa afya ya kinywa na meno ili kujua wale wagonjwa  ambao wanamatatizo na kuwapatia tiba pamoja na kuwapa elimu ya afya .

Alisema Chama hicho kinahimiza umuhimu wa afya bora kwa jamii na kutoa ushauri wa maradhi mbalimbali ikiwemo ukimwi ,saratani ,Kifua kikuu,afya ya kinywa na meno pamoja na maradhi yasioambukiza kwa kuifanya jamii ipate uelewa na kujikinga na maradhi ambayo yanauwezo wa kuepukika .

“Hali ya idadi ya Wagonjwa ni kubwa wakati ya kuwa magonjwa haya yanakingika kwa haraka na kupona lakini kikwazo ni kuwa na uchache wa madaktari ,“alisema Dr Lorna .

Alifahamisha kila ifikapo tarehe 20 machi ya kila mwaka huadhimisha siku ya afya ya kinywa na meno kwa mwaka ujao wanatarajia uzinduzi wa zoezi hilo litafanyika Zanzibar .

Nae Mgonjwa BI Nargisi Uzia ambae alifika kupatiwa huduma ya matibabu katika kituo hicho alisema anaishukuru Serikali kwa kuwaletea wataalamu wa kuchunguza afya zao lakini pia iko haja ya zoezi hilo liwe endelevu kwani matatizo yako mengi yanahitaji uchunguzi.
 

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPT 11,2017

Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images