Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1365 | 1366 | (Page 1367) | 1368 | 1369 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Rasi, Tamisemi Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa wataalam wa maji.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rasi, Tamisemi Selemani Jafo akisikiliza taarifa ya mradi wa maji Mkoyo.
  Baadhi ya wajumbe wa kijiji cha Mkoyo pamoja na wataalam wa maji wa manispaa ya Dodoma wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo.
  jenerata ya mradi wa maji Mkoyo.  NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amesikitishwa na baadhi ya wakandarasi washauri wanaosimamia miradi ya maji katika halmashauri mbalimbali hapa nchini kwa kutofanya kazi yao kwa umakini na hivyo kuruhusu wakandarasi wa ujenzi wa miradi ya maji kujenga miradi hiyo chini ya kiwango.

  Jafo alitoa kauli hiyo alipotembelea mradi wa maji katika kijiji cha Mkoyo ndani ya Manispaa ya Dodoma, ambapo amebaini mkandarasi mshauri wa mradi huo O&A Co LTD hakuwa makini wakati wa utekelezaji wa mradi huo kwani imeonekana mradi huo ukiwa na changamoto kadhaa licha fedha nyingi kutumika zaidi ya milioni 430 kati ya milioni 480 zilizipangwa kwa mradi huo.

  Amesema wakandarasi hao wamekuwa wakisababisha miradi kujengwa chini ya kiwango na kusababisha kushindwa kuwapatia maji wananchi kama ilivyotarajiwa. Aidha amebaini kampuni hiyo mshauri huyo ndiye yule yule aliyesimamia mradi kijiji cha Itiso ambao

  aliutembelea mradi huo mwezi Agosti mwaka huu na kukumbana na changamoto nyingi.Kufuatia hali hiyo, Jafo amemuagiza Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Rais Tamisemi Mhandisi Enock kwa shirikiana na wahandisi wa maji wa halmashauri za mkoa wa Dodoma kufanya tathmini ya miradi yote ya maji inayosimamiwa na mshauri huyo ili Ofisi ya Tamisemi ifanye maamuzi sahihi.

  Aidha amesema serikali haitaweza kuvumilia endapo ikibainika mshauri wa miradi hiyo ameshindwa kuisaidia serikali katika miradi ya maji anayoisimamia.

  Naibu waziri Jafo amezitaka kampuni zote za washauri waelekezi kutimiza wajibu wao katika kusimamia miradi ya maji kwani wananchi wamekuwa wakitaabika sana kutokana na kero ya maji ilihali wao wamechukua dhamana ya kusimamia miradi hiyo ya serikali.

  0 0

  Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (TAHLISO) limesema linaunga mkono juhudi kubwa zinazoonyeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli kupigania na kuzilinda rasilimali za nchi kwa maslahi ya Taifa jambo ambalo litasaidia kuchangia kwa kasi harakati za kimaendeleo.

  Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Tahliso, Stanslaus Kadugalize katika taarifa yake kwa vyombo vya habari nchini ambapo alisema tokea Serikali ya awamu ya tano iingie madaraka inakaribia kutimiza miaka miwili lakini ndani ya kipindi hicho watanzania wameona mambo mengi makubwa yakifanywa kwa ajili ya kuipa nchi maendeleo.

  Alisema moja kati ya mambo makubwa ni suala la kiongozi huyo kupamaba na vita dhidi ya dawa za kulevya,kuondoa watumishi hewa serikalini pamoja na wenye vyeti feki, Vita dhidi ya ufisadi na uhujumu uchumi,kufufua shirika letu la Ndege(ATC) kwa kununua ndege ambazo hivi sasa watanzania wanajivunia kuwa ni mali yao.

  Mwenyekiti huyo alisema pia mambo mengine ni Ujenzi wa Reli ya kisasa, Ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi katika Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM), utoaji wa ajira zaidi ya 50,000 kwa vijana wahitimu, Kuimarisha utumishi wenye nidhamu na uwajibikaji serikalini, Kuinua kwa kasi uchumi wa nchi yetu kimataifa, Kuboresha sekta ya afya pamoja na kupunguza bei za madawa ya binadamu nchini na mengine mengi yaliyoleta maendeleo ya nchi yetu

  Alisema pamoja na hayo lakini Rais Magufuli alionyesha ujasiri mkubwa kwa kuzuia mchanga wa madini ya dhahabu (Makinikia) na kuunda tume ili ichunguze namna nchi ilivyokuwa inapoteza mapatoambayo ilionyesha jinsi watu walivyoibiwa mapato ya Taifa kwa kipindi kirefu.

  “Lakini hakuishia hapo Juzi Rais Magufuli amekabidhiwa ripoti ya uchunguzi dhidi ya Madini ya Almas na Tanzanite iliyochunguzwa na kamati mbili zilizoundwa na Mhe. Spika Jobu Ndugai ripoti ambayo imeonyesha jinsi watanzania tulivyoibiwa kwa kipindi kirefu, Mhe. Rais hakusita kuwachukulia hatua wale wote waliohusika katika kupelekea Taifa kupoteza mapato”Alisema 

  Alisema sambamba na hayo suala la ukamataji wa madini ya Almas kwenye uwanja wa Ndege yaliyokua yameripotiwa kuwa na thamani ya 31.4bn tofauti na uhalisia wake ambapo kitaalamu almas ile ina thamani ya 64bn hii ni hatua kubwa sana ya kiukombozi wa nchi yetu ambayo iligeuka kuwa shamba la bibi kila mtu anajifanyia anavyotaka wazungu wanatuibia wanapeleka mali zetu kwao huku wakituachia mashimo makubwa bila kunufaika na rasilimali zetu.

  “Kutokana na hayo tuna kila sababu ya kumpongeza Rais Magufuli kwa kuwa ameonyesha uzalendo wa hali ya juu bila kumuonea mtu haya bila kujali cheo cha mtu ameonyesha namna anavyokerwa na vitendo viovu dhidi ya rasilimali za Taifa na pia kaonyesha uchungu mkubwa wa kuzijali rasilimali za Taifa letu kwa vitendo huku akituonyesha mfano unaopaswa kuigwa na kila Mtanzania katika vita hii kubwa ya kuzilinda”Alisema na kuongeza kila mtanzania anapaswa kuwa mlinzi wa rasilimali hizo kwenye mahali alipo.

  Alisema watanzania wamefika hapa walipo kwa sababu ya baadhi ya watu waliopewa dhamana na serikali katika nyadhifa mbalimbali kukosa maadili ya uongozi kwa makusudi ama kwa bahati mbaya (uzembe) ambao umeligharimu Taifa lna kulisababishia kupoteza fedha nyingi ambazo zingeweza kuisaidia serikali yetu kutuboreshea maisha yetu, upatikanaji wa Maji, ujenzi wa barabara, Utoaji elimu bure hadi Chuo Kikuu, huduma za afya nk.

  “Hata hivyo sisi kama TAHLISO Tunawataka ndugu zetu waliopewa dhamana na serikali hii ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. John Pombe Joseph Magufuli kwa nyadhifa mbalimbali wafanye kazi kwa bidii na kuzingatia maadili na miiko ya kazi zao”Alisema

  Lakini pia wakitangulize uzalendo wa nchi yetu kwa maslahi ya Taifa letu bila kuangalia maslahi yao binafsi huku wakitambua kuwa wamesomeshwa na kodi za wanachi wa Tanzania ili kuwatumikia Watanzania kwa moyo safi na weredi mkubwa.

  Katika hatua nyengine Mwenyekiti huyo wa Tahaliso aliwataka vijana kuacha kukata tamaa tusikate tamaa wala kukatishwa tamaa na mtu kwa haya yaliyofanyika huko nyuma badala yake wajipe moyo na kumuunga mkono Rais wa nchi ambaye amejitolea kwa nia dhati kurudishia Tanzania Mpya itakayokuwa na kasi kubwa ya kiuchumi.

  “Lakini pamoja na hayo tusiache kumuombea kwa mungu ili aweze kumlinbda na kumpa afya njema katika kipindi chake cha uongozi kutokana na dhamira ya kipekee aliyokuwa nayo kulinda rasilimaliza za nchi “Alisema.

  0 0


  .Msanii Alli Kiba akiwaongoza mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, Naibu waziri wa Ajira,Kazi na Vijana, Athony Mavunde, Goodluck Charles na Henry Kinambo kutoka Tigo kucheza pamoja kwenye jukwaa la Tigo Fiesta 2017 mkoani Arusha usiku wa kuamkia juzi.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo kanda ya kaskazini, Henry Kinabo akizungumza na waandishi wa habari kwenye wa tamasha la Tigo Fiesta2017 mkoani Arusha
  Alicia akiendelea kushamyulia jukwaa la Tigo fiesta Jijini Arusha mapema mwishoni wa wiki iliyopita.
  Msanii wa Ben Pol akitumbuiza kwenye jukwaa la Tigo Fiesta 2017 jijini Arusha tamasha llilofanyika uwanja wa sheikh Amri Abeid usikuwa kuamkia jana
  Aslay akitumbuiza kwenye jukwaa la Tigo Fiesta 2017 jijini Arusha tamsha llilofanyika uwanja wa sheikh Amri Abeid usikuwa kuamkia jana

  Umati wa wakazi wa Arusha wakiwa katika kushuhudia burudani ya Tigo Fiesta
  Shangwe za Tigo fiesta zikiendelea
  Vanesa Mdee akitumbuiza kwenye jukwaa la Tigo Fiesta 2017 jijini Arusha tamsha llilofanyika uwanja wa sheikh Amri Abeid usikuwa kuamkia jana

  Jux akilishambulia jukwaas la Tigo Fiesta  Maya Sama akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta
  Msaga sumu akitumbuiza katika jukwaa la tigo Fiesta.


  Young D akishambulia jukwaa la Tigo fiesta usiku wa kuamkia juzi Jijini Arusha.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Dkt. James Wakibara (wa tatu kushoto, mstari wa mbele ) akiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka hiyo, Imani Nkuwi (kushoto kweke) na viongozi pamoja wafanyakazi wa Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU) Kanda ya Kaskazini Mkoani Arusha. Lengo la ziara hiyo ilikua kuona na kukagua shughuli zinazofanywa na kikosi hicho kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wake.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Dkt. James Wakibara (katikati) akisikiliza hoja mbalimbali kutoka kwa watumishi wa KDU alipotembelea ofisi zao hivi karibuni. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi wa Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka hiyo, Imani Nkuwi (kulia) na Mkuu wa Kikosi hicho Kanda ya Kaskazini, Ndugu Mkeni (kushoto). 
   Askari wa KDU Kanda ya Kaskazini wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TAWA, Dkt. James Wakibara wakati akitoa maelekezo mbalimbali ya kuboresha utendaji kazi wa kikosi hicho.
  Baadhi ya watumishi na Askari wa KDU Kanda ya Kaskazini wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TAWA (hayupo pichani).
  Wafanyakazi na Askari wa KDU Kanda ya Kaskazini wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TAWA, Dkt. James Wakibara wakati wa mkutano huo. (PICHA NA TAWA)

  0 0

  NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

  WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto imepokea shilingi Bilioni 227.76 kutoka kwenye mfuko wa pamoja (Health Basket Fund) kwa ajili ya kufadhili shughuli mbalimbali za sekta ya afya nchini.

  Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wakati wa kupokea fedha hizo , Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa fedha hizo zitaelekezwa katika uboreshaji wa huduma za afya nchini.“Fedha hizi zitasaidia pia kutoa huduma za chanjo kwani ni afua muhimu kwa wananchi hususan katika kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano nchini” alisema Dkt. Ulisubisya.

  Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa kwa mara ya kwanza wameamua kupeleka fedha hizo moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kuepuka changamoto za vituo hivyo kukosa dawa muhimu mara kwa mara.Mbali na hayo Dkt. Ulisubisya alisema kuwa asilimia 90 ya fedha hizo zinaenda moja kwa moja kwenye vituo vinavyotolea huduma za afya vya ngazi ya Halmashauri na asilimia 10 inatumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za usimamizi wa kisera katika sekta ya afya nchini. 

  Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa fedha hizo pia zitasaidia katika kuimarisha miundombinu katika vituo vya afya na zahanati ili viweze kutoa huduma za upasuaji wa dharura kwa ajili ya akina mama wajawazito wanaokabiliwa na uzazi pingamizi.

  Kwa upande wake Balozi wa Denmark nchini Tanzania Bw. Einar Jensen kwea niaba ya wadau wa mfuko huo amesema kuwa mbali na Fedha hizo kushughulikia maswala ya afya nchini hapa pia zitakuwa na shughuli mbalimbali za maendeleo .

  “Mbali na kushughulikia masuala ya afya pia napendekeza fedha hizi zihusike katika kuhudumia wakimbizi wanaongia Tanzania hasa katika maeneo ya Kigoma na Kibondo” alisema Bw. Jensen.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya.

  0 0


  Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Siloamu, Mpaka Mafuta akimfanyia maombi rasmi ya kumbariki Kuhani wa kanisa hilo nchini Kenya Agatha Mtindi, kwenye Ibada ya Mungu Baba, iliyofanyika jana katika Kanisa hilo, Mbezi Makonde jijini Dar es Salaam. Agatha alifanyiwa maombi hayo maalum ya kumbariki kufuatia kuteuliwa kwake kuwa Mbunge kwenye Akaunti ya Machakosi nchini Kenya katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika hivi karibuni.Zifuatazo ni picha za tukio hilo, tangu mwanzo hadi mwisho wa ibada. Picha zote na Bashir Nkoromo  0 0


  Na Jumia Travel Tanzania

  Miongoni mwa majengo yake mengi yakiwa yamejengwa mnamo karne ya 18 na 19, Mji Mkongwe wa Zanzibar bado haujapoteza taswira yake halisi mpaka hivi leo. Na kutokana na muonekano huo, kutembea na kuvinjari mitaa na majengo mbalimbali kunakufanya ujihisi kama kweli ulikuwepo kipindi cha nyuma pindi inajengwa.

  Kati ya majengo maarufu ambayo Jumia Travel inakuhakikishia utayaona pindi utakapoingia kwenye mji huu ni pamoja na Ngome Kongwe iliyojengwa kwenye eneo la mwanzo la Kanisa la Wareno; nyumba ya maajabu; kasri kubwa iliyojengwa na Sultan Barghash; zahanati ya kale; Kanisa Kuu Katoliki la Mtakatifu Joseph; Kanisa Kuu la Kristu la Waanglikana likiwa limejengwa kukumbuka kazi ya David Livingstone katika kukomesha biashara ya utumwa na kujengwa eneo lilipo kuwepo soko la watumwa; makazi ya aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa watumwa Tippu Tip; Msikiti wa Malindi Bamnara; jengo la Jamat Khan lililojengwa kwa ajili ya dhehebu la Ismailia; eneo la makaburi ya Kifalme; na mabafu ya Kiajemi.

  Kwa pamoja, mitaa na barabara nyembamba zikiwa na kona nyingi, na majengo makubwa yanayotazamana na bahari ndyo yanaufanya mji huu kuwa wa kipekee ukiakisi shughuli za muda mrefu za kibiashara kati ya Waafrika na Waarabu. Kwa ujumla, Mji Mkongwe unatambulika kama sehemu ambayo hatimaye biashara ya utumwa ilikomeshwa.

  Kutokana na upekee na umaarufu wake mamia ya maelfu ya watalii kutoka kona mbalimbali za dunia husafiri kuja kujionea vivutio vya kila aina vinavyopatikana kwenye mji huu mkongwe wa Zanzibar.

  Kwa ufupi takribani kila kitu ndani ya Mji Mkongwe kina historia ya kuvutia na kusisimua. Kuanzia mila na tamaduni za watu wake, shughuli wanazozifanya, vyakula vyao na majengo ni utalii tosha ambao hauwezi kupatikana sehemu yoyote duniani.

  Huchukua muda wa saa moja na nusu kusafiri kwa kutumia boti kutoka Dar es Salaam mpaka kufika Zanzibar na usafiri huanzia saa moja asubuhi mpaka saa 12 za jioni. Hivyo basi kumbe inawezekana kwa mtu kutokea jijini Dar es Salaam akaenda kule, akatalii na kurudi siku hiyo hiyo. Na kama una mpango wa kuufaidi zaidi mji huo pia inawezekana kwani vyakula na malazi vya gharama nafuu kabisa ambayo kila mtu anaweza akamudu.

  Uzuri wa Mji Mkongwe ni kwamba ni rahisi kuuzunguka kwani mitaa yote inapitika kwa urahisi kabisa aidha kwa kutumia ramani ya karatasi au simu (google map) au muongozaji wa kitalii utayempata. Ni vizuri kuwa na muongozaji mzuri kama ni mara yako kwanza kufika kule ili iwe rahisi na pia kutembelea sehemu nyingi zaidi ambazo hauzifahamu.

  Kikubwa cha kushangaza zaidi ni namna majengo yalivyojengwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia vifaa mbalimbali kama vile chokaa, matumbawe na miti. Na cha kuvutia zaidi ni umri wa majengo hayo ambayo yamekuwepo karne na karne bila ya kupoteza uhalisia wake. 
   
  Pongezi kubwa ziende kwa serikali na shirika la Umoja wa Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kuweka jitihada kubwa na sheria za kuulinda mjii huu. Kutokana na jitihada hizo mnamo mwaka 2000 UNESCO liliutangaza Mji Mkongwe wa Zanzibar kama eneo la urithi wa dunia.

  Utakuwa haujaufaidi Mji Mkongwe endapo hautopata fursa ya kula vyakula mbalimbali (vya baharini) vinavyopatikana katika migahawa tofauti. Eneo maarufu ambalo unaweza kuvipata vyakula vya aina hiyo kwa pamoja ni kwenye bustani ya Forodhani. Litakuwa jambo la ajabu kama umefika Zanzibar na hukuenda kutembelea eneo hili.
   
   Umaarufu wa bustani ya Forodhani umetokana na mkusanyiko wake wa aina lukuki za vyakula vya baharini vinavyopatikana pale kila siku kuanzia jioni. Na ni eneo ambalo huwakutanisha watu kutokea sehemu mbalimbali za visiwa vya Zanzibar, hivyo inawezekana kukutana na watu ambao mlikuwa mkipishana mchana kutwa.

  Kutembelea, kuogelea na kutazama jua likizama kwenye fukwe ya bahari ya Hindi ukiwa Zanzibar nazo ni miongoni mwa shughuli ambazo watalii wengi hufurahia. Baadhi ya hoteli ambazo ukiwa kwenye Mji Mkongwe unaweza kuyafanya hayo ni kama vile Mizingani Seafront Hotel, Africa House Hotel na Seyyida Hotel & Spa.

  Kwa kumbukumbu zako itakuwa ni vema zaidi ukibeba kamera kwa ajili ya kupiga picha matukio mbalimbali unayoyaona njiani. Kwa majengo inakuwa ni rahisi zaidi ila kwa watu itakuwa ni busara ukaomba ruhusa ili kuepuka matatizo kwani sio wote watakuwa tayari kufanya hivyo. Zanzibar ni kubwa na ina maeneo mengi ya kutembelea ila kwa leo Jumia Travel inaamini angalau utakuwa umeipata picha ya Mji Mkongwe wa Zanzibar na shughuli za kufanya na kufurahia ukiwa kule.

  0 0

  NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

  WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto imepokea shilingi Bilioni 227.76 kutoka kwenye mfuko wa pamoja (Health Basket Fund) kwa ajili ya kufadhili shughuli mbalimbali za sekta ya afya nchini.

  Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wakati wa kupokea fedha hizo , Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa fedha hizo zitaelekezwa katika uboreshaji wa huduma za afya nchini.“Fedha hizi zitasaidia pia kutoa huduma za chanjo kwani ni afua muhimu kwa wananchi hususan katika kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano nchini” alisema Dkt. Ulisubisya.

  Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa kwa mara ya kwanza wameamua kupeleka fedha hizo moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kuepuka changamoto za vituo hivyo kukosa dawa muhimu mara kwa mara.Mbali na hayo Dkt. Ulisubisya alisema kuwa asilimia 90 ya fedha hizo zinaenda moja kwa moja kwenye vituo vinavyotolea huduma za afya vya ngazi ya Halmashauri na asilimia 10 inatumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za usimamizi wa kisera katika sekta ya afya nchini. 

  Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa fedha hizo pia zitasaidia katika kuimarisha miundombinu katika vituo vya afya na zahanati ili viweze kutoa huduma za upasuaji wa dharura kwa ajili ya akina mama wajawazito wanaokabiliwa na uzazi pingamizi.

  Kwa upande wake Balozi wa Denmark nchini Tanzania Bw. Einar Jensen kwea niaba ya wadau wa mfuko huo amesema kuwa mbali na Fedha hizo kushughulikia maswala ya afya nchini hapa pia zitakuwa na shughuli mbalimbali za maendeleo .

  “Mbali na kushughulikia masuala ya afya pia napendekeza fedha hizi zihusike katika kuhudumia wakimbizi wanaongia Tanzania hasa katika maeneo ya Kigoma na Kibondo” alisema Bw. Jensen.
  Picha ya Pamoja ya makabidhiano ya mkataba wa mfuko wa pamoja (Health Basket Fund) kwa ajili ya kufadhili shughuli mbalimbali za sekta ya afya nchini ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Mh. Dotto James na Balozi wa Denmark nchini Tanzania Bw. Einar katika kikao kilichofanyika ofisi ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam,wakwanza kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya 

  Balozi wa Denmark nchini Tanzania Bw. Einar Jensen akisisitiza jambo katika kikao cha makabidhiano ya mkataba wa mfuko wa pamoja (Health Basket Fund), kilichofanyika mapema leo katika ofisi ndogo za Wizaraya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam. 
  Watumishi wa Serikali wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakifuatilia kwa karibu majadiliano katika kikao cha makabidhiano ya mkataba wa mfuko wa pamoja (Health Basket Fund) kwa ajili ya kufadhili shughuli mbalimbali za sekta ya afya nchini.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akisaini mkataba wa mfuko wa pamoja (Health Basket  Fund) kwa ajili ya kufadhili shughuli mbalimbali za sekta ya afya nchini, tukio lililofanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango leo jijini Dar es salaam. 

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Udhibiti wa Ubora wa Mbolea Tanzania(TFRA) Bw. Lazaro Kitandu (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari wakati zoezi la upakuaji wa mbolea ya kupandia ukiendelea katika bandari ya Dar es Salaam mapema hii leo. 
  Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari nchini wakiendelea na zoezi la upakiaji wa mbolea ya kupandia tani elfu 23 tayari kwenda kwa wakulima mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari nchini wakiendelea na zoezi la kufunga mbolea ya kupandia katika mifuko tayari kwa kupakiwa na kusafirishwa kwenda kwa wakulima.Picha na Eliphace Marwa - Maelezo


  Na. Eliphace Marwa - Maelezo

  Serikali imeingiza nchini jumla ya tani elfu 32 za mbolea ya kukuzia pamoja na tani elfu 23 za mbolea ya kupandia kupitia mfumo mpya wa uagizaji wa mbolea kwa pamoja, lengo likiwa ni kudhibiti bei kwa kuzingatia bei elekezi.

  Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam wakati zoezi la upakuaji wa mbolea hiyo likiendelea Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Udhibiti wa Ubora wa Mbolea Tanzania(TFRA) Bw. Lazaro Kitandu amesema kuwa mpaka sasa jumla ya tani elfu 55 za mbolea zimewasili nchini.

  Hii ni awamu ya kwanza ya kuingiza mbolea nchini kupitia mfumo mpya ya uagizaji mbolea kwapamoja ambapo kampuni ya OCP S.A ya nchini Morocco imeingiza jumla ya tani elfu 23 za mbolea ya kupandia na Kampuni ya Premium Agro Chem imeingiza tani elfu 32 za mbolea ya kukuzia.

  “Mpaka sasa zoezi la kupakua mbolea ya kupandia (DAP) tani elfu 23 linaendelea vizuri na mara baada ya kumaliza kupakua mbolea hii tutaanza zoezi la kupakua mbolea ya kukuzia (UREA) ambayo ni tani elfu 32,” alisema Bw. Kitandu.

  Kitandu aliongeza kuwa Mheshimiwa Waziri wa kilimo juzi alipokuwa anaongea na waandishi wa habari mjini Dodoma na akasisitiza bei ambazo zimetolewa zisimamiwe na kila ngazi kwasababu taasisi peke yake haiwezi kuwa na watu kila mahali hivyo Tawala za mikoa, Serikali za mitaa mpaka Kijiji zitasaidia kusimamia bei ambazo zimetolewa. 

  Pia Kitandu aliongeza kuwa kuhusiana suala la bei ya mbolea hiyo itatangazwa kupitia vyombo vya habari kama vile magazeti na televisheni na hivyo kutoa onyo kwa mawakala kujipangia bei kwa kuuza mbolea nje ya bei elekezi ya Serikali kwamba watachukuliwa hatua za kisheria kama kunyang’anywa leseni, kufungwa, faini au vyote kwa pamoja.

  Aidha Kitandu alisisitiza kuwa mbolea hizi siyo mbolea za ruzuku kwani wakulima wengi wamekuwa wakichanganya mbolea hizi na mbolea za ruzuku na amefafanua kuwa mbolea hii imefanyiwa utaratibu wa kudhibiti toka kule inapotoka na hivyo serikali itahakikisha mbolea hii inauzwa kwa kulingana na bei ya soko la dunia.

  Aidha Bw. Kitandu aliwahakikishia wakulima kuwa mbolea itasafirishwa mpaka vijijini kwa kutumia treni na malori kwa sehemu ambapo treni haiwezi kufika, na amewatoa hofu wakulima kuwa msimu unaoanza mwezi huu wameingiza tani 23,000 kwa mbolea ya kupandia (DAP) na tani 32,000 kwa mbolea ya kukuzia (UREA) ambapo watakuwa wanaagiza kwa awamu kwa miezi miwili miwili.

  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimwangalia Profesa Ibrahim Hamis Juma akitia sahihi hati ya kiapo baada ya kumuapisha kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka sahihi hati ya kiapo baada ya kumuapisha Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyezo za kazi baada ya kumuapisha Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea baada ya kumuapisha Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika Job Ndugai, Profesa Ibrahim Hamis Juma, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba kabudi na Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman katika picha ya kumbukumbu baada ya Rais kumuapisha Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika Job Ndugai, Profesa Ibrahim Hamis Juma, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba kabudi na Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman katika picha ya kumbukumbu na Majaji wa Mahakama ya Rufaa na wa Mahakama kuu baada ya Rais kumuapisha Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017.

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Hamis Juma, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman katika picha ya kumbukumbu na Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama baada ya Rais kumuapisha Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Hamis Juma, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman katika picha ya kumbukumbu na watendaji waandamizi Serikalini baada ya Rais kumuapisha Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Hamis Juma, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman katika picha ya kumbukumbu na watendaji waandamizi wa Mahakama kuu  baada ya Rais kumuapisha Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Hamis Juma, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman katika picha ya kumbukumbu na Majaji wastaafu  baada ya Rais kumuapisha Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Hamis Juma, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman katika picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya Mkoa huo Lazaro Mambosasa baada ya Rais kumuapisha Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Jaji Mkuu mpya Profesa Ibrahim Hamis Juma na mkewe Mama Marina P. Juma na wajukuu wao baada ya Rais kumuapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Jaji Mkuu mpya Profesa Ibrahim Hamis Juma na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia Mhe. job Ndugai baada ya Rais Kumuapisha Profesa Juma Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpatia Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh abubakary Zubeiry Ally wakati wa hafla ya kumuapisha Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 11, 2017


  0 0

  Na Beatrice Lyimo- MAELEZO DODOMA.

  Serikali  imepanga kuongeza idadi ya Maafisa Ugani wenye ujuzi katika kila Kata na Kijiji ili kuleta mapinduzi ya kilimo Nchini.

  Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. William Ole Nasha wakati akijibu swali lililohusu mkakati wa Serikali wa kuhakikisha inafanya mapinduzi ya kilimo kwa kuwa na wataalamu wa kutosha, leo Bungeni mjini Dodoma.

  Naibu Waziri huyo amesema kuwa Serikali inatambua kuwa Sekta ya Kilimo ni muhimu na ndiyo yenye kuajiri watanzania wengi hivyo mapinduzi ya kilimo yatachangiwa na uwepo wa wataalam wa kutosha wenye taaluma na ujuzi stahiki ili waweze kushauri matumizi ya teknolojia na kanuni bora za kilimo.

  " Hadi kufikia mwaka 2016/2017 Serikali imeajiri maafisa ugani 8,756 sawa na asilimia 43 ya mahitaji ya maafisa ugani 20,374 katika ngazi ya Kijiji, Kata na Wilaya" amefafanua Naibu Waziri Ole Nasha.

  Aidha, Naibu Waziri Ole Nasha aliongeza kuwa Serikali inaendelea kuboresha na kuwezesha vituo vya kilimo na vituo vya Rasilimali za kilimo za kata (WARCs) kwa ajili ya kufundishia teknolojia mbalimbali za kilimo.

  Vilevile alisema kuwa Serikali itaendelea kutoa ushauri wa kitaalam na kuandaa miongozo na mafunzo ya huduma za ugani, ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa kazi za Ugani na kuboresha usambazaji wa teknolojia za kilimo bora kwa wakulima nchini.Mbali na hayo Serikali inaendelea kusomesha vijana na kuwaajiri kulingana na upatikanaji wa rasilimali fedha.
  Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. William Ole Nasha

  0 0

  Wanajopo walioshiriki mjadala huo kutoka kushoto ni Viola Julius mratibu wa tovuti ya iSwapMyBooks, Given Edward toka mtandao wa MyElimu,Kiya JK wa taasisi ya SEMA na  Irene Kiwia wa TWA network
  Mmoja wa wachangiaji Bw. Yeriko Nyerere  akichangia jambo wakati wa siku hiyo
   Bw. Paschal Masalu kutoka Elimika Wikiendi akiendelea ku Tweet wakati wa Siku hiyo ya kisomo
  Baadhi ya wadau mbalimbali wa Elimu wakiwa katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Kisomo

  Wadau mbalimbali wa elimu wamekutana kuadhimisha siku ya kimataifa ya kisomo ambayo hufanyika Septemba 8 kila mwaka. Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na taasisi ya iSwapMyBooks kwa kushirikiana na SOMA pia Elimika Wikiendi ulihusisha mjadala wa namna ambavyo Tanzania inaweza kutumia faida ya uwepo wa nyenzo za kidigitali katika kusaidia watoto na watu wazima kujifunza.

  Akifungua maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya SOMA Bi. Demere Kitunga alieleza namna ambavyo kwa miaka ya karibuni Tanzania imekuwa ikipiga hatua katika matumizi ya nyenzo za kiditali kutokana na usambaaji wa matumizi ya vifaa vilivyounganishwa na mtandao wa intaneti hivyo kupelekea uhitaji katika kutumia nyenzo hizi katika kuboresha namna ambavyo watoto wanaweza kujifunza masomo.

  Wanajopo walioshiriki mjadala huo Irene Kiwia wa TWA network, Given Edward toka mtandao wa MyElimu, Kiya JK wa taasisi ya SEMA na Viola Julius mratibu wa tovuti ya iSwapMyBooks walielezea namna ambavyo taasisi zao zimekuwa zikitumia njia za kidigitali kuwahamasisha watoto na vijana  kujifunza kwa kubadilishana ujuzi kupitia mtandaoni.

  Washiriki wengine kwa namna tofauti walionyesha wasiwasi kwa namna ambavyo utaratibu wa watu kujisomea unaendelea kutoweka na hasa kwa wazazi ambao wamekuwa hawana utaratibu wa kuwanunulia watoto vitabu badala yake kuwapa simu za mkononi ambazo wamekuwa wakizitumia kwa mambo yasiyofaa.

   Akijibu wasiwasi huo, Mkurugenzi wa taasisi ya SEMA ndugu Kiiya JK alisema ni wakati mitaala ya masomo ibadilike kuendana na hali halisi. “Tunalazimika kama Watanzania kutengeneza vitabu vinavyoendana na hali halisi ya maisha yetu kwa sasa, wenzetu wamegundua hilo na wamekuwa mstari wa mbele kuwekeza katika kuchapisha vitu vinavyowafaa watoto wetu”.

  Siku ya kimataifa ya kisomo ilianzishwa na shirika la UNESCO miaka 50 iliyopita ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ilikuwa “Kisomo Katika Ulimwengu wa Kidigitali”.

  0 0


  Na Binagi Media Group.

  Utafiti mpya uliofanywa na Taasisi ya Taifa Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini (NIMR) umebaini kwamba magonjwa ya Malaria, Ukimwi, Moyo, Mfumo wa Upumuaji pamoja na Upungufu wa Damu yanayongoza kwa kusababisha vifo vya hospitalini.


  Aidha utafiti huo ambao uliofanyika mwaka jana kwa kutumia takwimu za kuanzia mwaka 2006 hadi 2015 katika hospitali 39 nchini ambazo ni pamoja na hospitali ya Taifa, hospitali za Kanda, Hospitali za mikoa na wilaya umeonyesha kwamba vifo vya ajali vimeongezeka kwa asilimia 16, saratani asilimia 24, kiharusi asilimia 27 na kisukari asilimia 11.


  Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza hii leo Jijini Mwanza kwenye uwasilishaji wa matokeo ya utafiti huo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na Kanda ya Magharibi, Mganga Mkuu mkoani Mwanza Dkt.Leonard Subi amesema hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa kwa kutumia utafiti huo ili kudhibiti vifo hivyo.


  Mtafiti Mkuu Kiongozi kutoka NIMR, Dkt.Leonard Mboera amesema utafiti huo pia ulilenga kuangalia upatikanaji wa takwimu za vifo katika hospitali nchini Tanzania ambapo ilibainika kuwepo changamoto katika ukusanyaji, uchanganuzi na matumizi ya takwimu katika hospitali.


  Taasisi ya NIMR ilifanya utafiti ili kubaini sababu na vyanzo vya vifo katika hospitali nchini Tanzania na kubaini kwamba ugonjwa wa Malaria unaongoza kwa kusababisha vifo kwa asilimia 12.8, Mfumo wa upumuaji kwa asilimia 10.1, Ukimwi asilimia 8.0, upungufu wa damu asilimia 7.8, magonjwa ya moyo na mfumo wa damu asilimia 6.3 huku mikoa ya Dar es salaam, Mwanza na Morogoro ikiongoza kwa vifo katika hospitali nchini.

  Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonard Subi akizungumza kwenye warsha hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella. Warsha hiyo imejumuisha washiriki kutoka mikoa ya Kigoma, Kagera, Geita, Tabora, Shinyanga, Mara, Simiyu na Mwanza.
  Dkt.Changalucha John ambaye ni Mkurugenzi Mkuu NIMR kituo cha Mwanza akizungumza kwenye warsha hiyo
  Mtafiti Mkuu Kiongozi kutoka NIMR, Dkt.Leonard Mboera, akizumza na wanahabari nje ya warsha hiyo.
  Dkt.Omari Gamuya akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Mganga Mkuu mkoani Mara
  Mmoja wa watafiti kutoka NIMR akifafanua jambo mbele ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuhusu utafiti huo
  Washiriki wa warsha hiyo
  Baadhi ya washiriki
  Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Leonard Subi (wa tatu waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi pamoja na washiriki mbalimbali wa warsha hiyo.
  Picha ya pamoja

  0 0

  Meneja wa Maendeleo ya Wakulima Wadogo wa TADB, Bw. Joseph Mabula (kulia)akizungumzia nafasi ya Benki hiyo katika kuwawezesha wakulima wadogo kulima kibiashara. Wanaomsikiliza ni  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (katikati) na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa Benki, Bw. Augustino Matutu Chacha (wapili kushoto) kwa mbali kushoto ni Afisa habari Mwandamizi wa Idara ya Habari, Bw. Jonas Kamaleki.
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (katikati) akisisitiza jambo wakati akiongea na wanahabari kuhusu kutimiza miaka miwili ya kutoa huduma kwa wakulima wa Tanzania na mkakati wa TADB wa kujitanua kupitia kongani. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa Benki, Bw. Augustino Matutu Chacha (kushoto) na Meneja wa Maendeleo ya Wakulima Wadogo wa TADB, Bw. Joseph Mabula (kulia).
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (wapili kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa Benki, Bw. Augustino Matutu Chacha (wapili kushoto) wakati wa Mkutano wao na Wanahabari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo. Kushoto ni  Afisa habari Mwandamizi wa Idara ya Habari, Bw. Jonas Kamaleki na kulia ni Meneja wa Maendeleo ya Wakulima Wadogo wa TADB, Bw. Joseph Mabula.
   Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa Benki, Bw. Augustino Matutu Chacha (kushoto) akizungumzia mafanikio ya Benki hiyo katika kukopesha wakulima wadogo nchini. Wanaomsikiliza ni  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (katikati) na Meneja wa Maendeleo ya Wakulima Wadogo wa TADB, Bw. Joseph Mabula (kulia).

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Theresia Mhongo wa pili kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu wa kwanza kushoto, Makamu Mwenyekiti Charles Ngereza wa tatu kutoka kushoto na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu Bw. Mourice wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa APC 2017 uliofanyika ukumbi wa KKK Karatu.(Picha na PamelaMollel Arusha).
  Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa APC wakisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mhongo(hayuko pichani),
  Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mhongo akielekea kupiga picha ya pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kufungua mkutano mkuu wa APC 2017 katika ukumbi wa KKKT Lutherani Karatu
  Mjumbe wa mkutano mkuu wa APC, Nerbert Mramba katikati akichangia mada kwenye mkutano Mkuu wa APC 2017 katika ukumbi wa KKKT Lutheran.
  Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa APC waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbalimbali nchini wakiwa katika picha ya pamoja katika lango la kuingilia hifadhi ya Taifa Tarangire
  Viongozi wa APC kutoka kushoto Pamela Mollel (Mwekahazina), Claud Gwandu (Mwenyekiti), na Charles Ngereza (Makamu Mwenyekiti) wakisikiliza wajumbe wa mkutano mkuu wa APC uliokuwa ukiendelea katika ukumbi wa KKKT Karatu.

  0 0

   Mhifadhi katika hifadhi ya Taifa ya Tarangire Beatrice Ntambi akizungumza na waandishi wa chama cha waandishi mkoani Arusha(APC)waliokwenda kutembelea  hifadhi hiyo kwa lengo la kujifunza na kutangaza utalii wa ndani
   Sehemu ya waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini
   Mratibu wa Arusha Press Club Seif Mangwangi akiorodhesha majina ya waandishi wanaoingia katika hifadhi ya Tarangire katika ziara ya mafunzo pamoja na kutangaza utalii wa ndani
   Picha ikionyesha fuvu la mnyama aina ya Tembo
   Sehemu ya makundi makubwa ya tembo wanaopatikana katika hifadhi ya Taifa ya Tarangire
   Twiga wakionekana vizuri katika hifadhi ya Tarangire
   Tembo wakizunguka ndani ya hifadhi ya Tarangire
   Katika hifadhi hii utakuta  aina ya miti mikubwa ya mibuyu inayosadikika kuishi mamia ama maelfu ya miaka ambayo pia ni kivutio kikubwa katika hifadhi ya Tarangire
   Wanahabari wakichukua taswira katika hifadhi ya Tarangire
   Wanahabari wakichukua Selfiee kabla ya kuanza safari keelekea kujionea vivutio ndani ya hifadhi ya Tarangire


   Makundi ya Tembo yakiwa katika hifadhi ya Tarangire
  Baadhi ya wanachama wa Arusha Press Club wakiwa katika picha ya pamoja katika lango la kuingilia katika hifadhi ya Taifa Tarangire.(Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa wadau wa Mafuta na Gesi ambapo wadau wa Gesi na Mafuta watapata nafasi ya kujadili Fursa zilizopo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt. Medard Kalemani wakati wa  mkutano wa siku mbili wa wadau wa Mafuta na Gesi uliofanyika kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.   0 0

   Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo akizungumza  katika hafla ya kufungua mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi  katika Ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma leo.
   Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt. Zainabu Chaula akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Prof. Joseph Semboja  akiwasilisha taarifa ya awali kwa Mgeni Rasmi na Washirki wakati wa  kufungua mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi  katika Ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma leo.
   Baadhi wa wa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa walioshiriki kwenye mafunzo ya uongozi yanayoendeshwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa ushirikiano na Taasisi ya Uongozi.
  Naibu Waziri wa OR-Tamisemi Mhe. Selemani Jafo (mbele katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Tamisemi Dkt. Zainabu Chaula (mbele kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja (mbele kulia) pamoja na baadhi wa wafanyakazi wa Taasisi ya Uongozi walioandaa mafuno haya.

  Nteghenjwa Hosseah, Tamisemi – Dodoma.

  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala  za Mikoa  na Serikali za Mitaa  Mhe. Selemani Jafo amewataka Wakuu wa Wilaya  na Wakurugenzi wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi  ili kutimiza matarajio  ya watanzania  ambao wanaitegemea Wizara hii kama chachu ya  mabadiliko  katika utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya Tano. 

  Mhe.Jafo ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mikoa ya Dar es Salaam, Shinyanga, Mbeya, Songwe, Rukwa, Ruvuma, Iringa na Njombe yanayoendeshwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa ushirikiano na Taasisi ya Uongozi.

  Akiungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo  Mhe.Jafo amewataka viongozi hao kutumikia Wananchi kwa kuzingatia Taratibu, Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma huku wakizingatia mipaka yao ya Utawala, kuboresha mahusiano katika maeneo ya kazi na  kuhakikisha hakuna muingiliano wa majukumu baina ya viongozi wa Wilaya na Halmashauri. 

  “Nafahamu baadhi viongozi  mlitokea katika sekta binafsi na humkuwa mnafahamu vizuri utendaji kazi wa shughuli za Serikali hata hivyo mmefanikiwa  kwa kipindi chote kutenda kwa kadiri ya maelekezo ya Serikali,vipaumbele na miongozo mbalimbali  iliyotolewa pia mmejitahidi kutoa huduma bora ukiachilia mbali mapungufu madogo madogo ambayo tumeyabaina na kuyashuhudia katika baadhi ya maeneo” alisema Jafo.

  Aliongeza kuwa “kupitia mafunzo haya ni imani yangu kuwa wote sasa tutakuwa na uelewa wa pamoja wa kufanya kazi Kimkakati ili kuwaletea wananchi maendeleo huku mkifahamu vyema Muundo wa Serikali na namna inavyofanya kazi kwa kuzingatia mipaka na mgawanyo wa majukumu, Itifaki, utunzaji wa Siri za Serikali na maadili ya viongozi wa Umma”.

  Aidha Mhe. Jafo aliwataka viongozi hao kuendelea kusimamia nidhamu ya watumishi, kuendeleza mapambano dhidi ya Dawa la kulevya, kulinda amani na utulivu katika maeneo yao huku  wakisimamia kwa makini mapato na matumizi ya Fedha za Serikali na kusisitiza matumizi ya mifumo ya Kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

  Akimkaribisha Mgeni rasmi katika mafunzo hayo Naibu Katibu Tamisemi anayeshughulikia Afya Dkt. Zainabu Chaula amesema kitu cha msingi kati yetu sisi watendaji ni umoja ambao kupitia huo  utatuleta Ushindi  na muongozo wa utendaji wetu uko kwenye ilani ya Chama cha Mapindui hivyo kila mmoja wetu arejee Ilani ile ili afahamu nini anachotakiwa kukifanya katika kipindi hiki cha miaka mitano.

  Awali akitoa taarifa  ya utangulizi kwa mgeni rasmi na washiriki wa mafunzo hayo Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja alisema  mafunzo haya yanatolewa na wataalamu walioboea katika masuala ya uongozi na yatafanyika kwa muda wa siku tano kwa viongozi aidi ya 72.
  Aliongeza kuwa maeneo ambayo yatajen gewa uwezo ni namna bora ya  kufanya maamuzi ya kimkakati yanayozingatia mahitaji na manufaa mapana ya Taifa, namna bora ya kuongoza watu na kusimamia Rasilimali za Taifa na pia  jinsi ya  kujijengea Sifa za kiungozi ambazo zinaleta heshima kwa jamii, kuaminika na kutegemwa katika kuleta mabadiliko.

  Mafunzo haya yamepangwa kufanyika katika awamu nne(4) ambapo awamu mbili tayari zimekwsihafanyika ziliojumuisha Wah. Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kutoka Mikoa kumi na mbili(12) ya Dodoma, Morogoro, Singida, Tabora, Kigoma, Katavi, Kagera, Mwana, Mara, Simiyu, Geita na Manyara.

  Awamu ya kwanzaya mafunzo haya ya Uongozi  yalifanyika Mwezi Mei, 2017 na  yalifunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na awamu ya mwisho inatarajiwa kufanyika kabla ya mwezi Disemba 2017.

  0 0

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Vwawa Mhe. Japhet Hasunga (CCM)

  Serikali imesema kuwa kushuka au kupanda kwa thamani ya shilingi nchini hakusababishwi na bidhaa na huduma mbalimbali kutozwa kwa dola bali kunatokana na misingi ya shughuli mbalimbali za kiuchumi (Macroeconomic fundamentals) pamoja na hali halisi ya uchumi wa nchi zinazofanya biashara na Tanzania. 

  Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Vwawa Mhe. Japhet Hasunga (CCM), aliyetaka kujua mikakati ya Serikali katika kuimarisha thamani ya shilingi ya Tanzania na kupiga marufuku matumizi ya fedha za kigeni nchini. 

  Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji aliainisha kuwa nakisi ya urari wa biashara, mfumuko wa bei na tofauti ya misimu (seasonal factors) ni sababu kuu zinazosababisha kushuka na kupanda kwa thamani ya shilingi nchini.
  Dkt. Kijaji aliliambia Bunge kuwa ili kuimarisha thamani ya shilingi Benki Kuu inaendelea kuthibiti mfumuko wa bei ili usitofautiane sana na wabia wa biashara nchini. 

  “Benki Kuu imethibiti biashara ya maoteo (speculation) katika soko la fedha za kigeni ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa miamala ya fedha za kigeni inafanywa na benki kwa ajili ya shughuli za kiuchumi tu na sio biashara ya maoteo, hali hii itasaidia upatikanaji wa fedha za kigeni katika soko la rejareja ili kupunguza shinikizo la kuporomoka kwa thamani ya shilingi.”Alisema Dkt Kijaji. 

  Dkt. Kijaji alifafanua kuwa pamoja na hatua zinazochukuliwa na Benki Kuu ufumbuzi wa kudumu wa kutengamaa kwa thamani ya shilingi nchini hutegemea zaidi kupungua kwa nakisi ya urari wa biashara ya bidhaa, huduma na uhamisho wa mali nchi za nje. 
  Imetolewa na: 

  Benny Mwaipaja
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Wizara ya Fedha na Mipango
  11/9/2017

  0 0

  Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo akikata keki kuashiria uzinduzi wa Chama cha washereheshaji (WSB) 'Wakali wa sherehe Bongo' jijini Dar es Salaam leo. Kutoka (kushoto) ni Moafisa wakuu wa Elimu kwa mlipa Kodi, Rose Mahendeka na Julius Mjenga, Mwenyekiti wa WSB, Lameck Matemba na Katibu wa chama hicho, Reuben Ndimbo.
  Mwenyekiti wa WSB, Lameck Matemba akiongea wakati wa uzinduzi huo. 
  Afisa Mkuu wa Elimu kwa mlipa Kodi, Julius Mjenga akitoa mada kwa wana WSB. 
  Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo akimpa za wadi ya diary Mwenyekiti wa WSB, Lameck Matemba 
  Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo akiwa katika picha ya pamoja na wana WSB na wageni wao. 
  Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa WSB.
  Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo
  Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo akitoa elimu kwa wanachama wa WSB. 

older | 1 | .... | 1365 | 1366 | (Page 1367) | 1368 | 1369 | .... | 1896 | newer