Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1363 | 1364 | (Page 1365) | 1366 | 1367 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na ujumbe kutoka Malawi ambao umetembelea hospitali hiyo LEO ili kujifunza jinsi inavyoboresha huduma za afya. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya nchini Malawi, Dk. Dan Namarika.
  Ujumbe kutoka Malawi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Museru.
  Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Muhimbili, Dk Julieth Magandi akieleza muundo wa hospitali kwa ujumbe wa Malawi.
  Wakurugenzi wa Muhimbili wakiwamo watalaamu wengine wa afya wakimsikiliza Dk Magandi leo.
  Ujumbe wa Malawi ikiongozwa na wenyeji wao wakiwa katika Jengo la Watoto leo. 
  Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali (EMD), Dk Juma Mfinga akitoa ufafanuzi kuhusu huduma zinazotolewa na idara hiyo.
  Ujumbe kutoka Malawi ukiwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU).Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea ujumbe wa wataalamu wa Afya kutoka Wizara ya Afya ya nchini Malawi.

  Ujumbe huo umeongozwa na Katibu wa Afya nchini humo , Dk. Dan Namarika umehusisha Madaktari , viongozi pamoja na wataalam mbalimbali kutoka katika Wizara hiyo pamoja na taasisi nyingine za afya .

  Akizungumza baada ya kupokea ujumbe huo , Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru amesema ujio wa watalaamu hao unatoa fursa ya kujifunza na kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi.

  Naye Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Juliethi Magandi amesema katika mwaka wa Fedha 2016-2017 Hospitali imehudumia wagonjwa wa nje Laki Nne , Thelathini na Sita Elfu na Miatatu Tisini na Nne wakati wagonjwa wa ndani waliohudumiwa ni Hamsini na Tisa Elfu na Miatano Hamsini na Tano.

  Akizungumzia lengo la ujio wao , Katibu wa Afya wa nchi hiyo Dk. Dan Namarika amesema wamekuja kujifunza jinsi ambavyo MNH inafanya kazi na kutekeleza mipango yake .

  Lengo la serikali ya Malawi na Wizara ya Afya kwa ujumla ni kuhakikisha inaboresha utoaji wa huduma hususani katika Hospitali za Umma nchini humo.Ujumbe usema kuwa umefurahishwa jinsi Muhimbili inavyotoa huduma za kibingwa na kusomesha wataalamu wa afya nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa mafunzo.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Fedha na Mipango wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip I.Mpango mara alipowasili Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi katika Ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,uliofanyika leo.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  Dkt. Khalid Salum Mohamed mara alipowasili Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi katika Ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,uliofanyika leo.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi mbali mbali wajkati wimbo wa Taifa Ukipigwa katika  Ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,uliofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
   Washiriki wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,kutoka Nchini South Afrika wakiwa  katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
   Washiriki wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,kutoka Nchini SWAZILAND wakiwa  katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
   Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,wakiwa  katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
   Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,wakiwa  katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
   Washiriki wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,kutoka Zanzibar Nchini Tanzania wakiwa  katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
   Washiriki wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba ya ufunguzi wa Mkutano huo leo  katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitoa hutuba yake ya  Ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,uliofanyika leo  katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akitoa hutuba yake ya  Ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Nchi za Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Udhibiti wa Biashara ya Fedha Haramu,uliofanyika leo  katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel Mbweni Nje ya Mji wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi (Picha na Ikulu)

  0 0  Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye ni mwanasheria mkuu wa CHADEMA na rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

  0 0

  KAMATI ya Utendaji ya Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), iliyokutana Dar es Salaam jana Septemba 7, 2017, imepanga Uchaguzi Mkuu wa chama hicho ufanyike Novemba 5, mwaka huu.

  Uchaguzi huo utafanyika Dar es Salaam katika ukumbi ambao utatangazwa na tayari kamati imeaigiza sekreterieti ya TASWA, ifanye maandalizi kuhusu uchaguzi huo, ikiwa ni pamoja na kulishirikisha Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa ajili ya usimamizi wa karibu.

  Kikao kimekubaliana watakaoshiriki uchaguzi huo ni wanachama wote wa TASWA waliopo katika leja kuanzia Juni mwaka 2007 hadi Juni mwaka 2017, wakiwemo walioingia uanachama wakati wa semina ya waandishi chipukizi iliyofanyika Dar es Salaam Agosti mwaka 2015 na sharti kubwa ni kila mwanachama kulipia ada ya mwaka mmoja.

  Kwa wanachama wengine wapya wanaotaka kujiunga, watafanya hivyo baada ya uongozi mpya kuingia madarakani na kupewa utaratibu kulingana na Katiba ya chama inavyoeleza na pia kwa kadri uongozi mpya utakaoingia madarakani utakavyoona inafaa.Kutokana na hali hiyo wanachama wote wenye sifa hizo, wanatakiwa kulipia ada zao kwa Mhazini Msaidizi, Zena Chande kuanzia leo hadi Septemba 30, mwaka huu.

  Uongozi wa sasa wa TASWA uliingia madarakani mwaka 2014, ambapo Juma Pinto alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Egbert Mkoko (Makamu Mwenyekiti), Amir Mhando (Katibu Mkuu), Grace Hoka (Katibu Mkuu Msaidizi), Shija Richard (Mhazini) na Zena Chande (Mhazini Msaidizi).

  Wajumbe ni Rehure Nyaulawa, Chacha Maginga, Mussa Juma, Mwani Nyangassa, Mroki Mroki, Ibrahim Bakari na Majuto Omary anayeingia kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa TASWA FC.

  Juma Pinto
  Mwenyekiti TASWA
  08/09/2017

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru (katikati) akiwa meza kuu na Viongozi wa TRA na CTI wakiongoza Mkutano wa Msamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Wadau wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini CTI, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, jana. Mkutano huo ulikuwa na lengo la majadiliano kuhusu namna ya kutatua changamoto mbalimbali ili kufikia Uchumi wa Viwanda wa Kati pamoja na vikwazo vya ulipaji na ukusanyaji Kodi nchini. 
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru, akizungumza wakati wa Mkutano wa Msamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Wadau wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini CTI, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo. Mkutano huo ulikuwa na lengo la majadiliano kuhusu namna ya kutatua changamoto mbalimbali ili kufikia Uchumi wa Viwanda wa Kati pamoja na vikwazo vya ulipaji na ukusanyaji Kodi nchini. 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru, akizungumza wakati wa Mkutano wa Msamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Wadau wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini CTI, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo. Mkutano huo ulikuwa na lengo la majadiliano kuhusu namna ya kutatua changamoto mbalimbali ili kufikia Uchumi wa Viwanda wa Kati pamoja na vikwazo vya ulipaji na ukusanyaji Kodi nchini. 
  Kamishina Mkuu wa TRA, Charles Kichele, akizungumza wakati wa Mkutano wa Msamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Wadau wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini CTI, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo. Mkutano huo ulikuwa na lengo la majadiliano kuhusu namna ya kutatua changamoto mbalimbali ili kufikia Uchumi wa Viwanda wa Kati pamoja na vikwazo vya ulipaji na ukusanyaji Kodi nchini. 
  Mkurugezni Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini, Leodger Tenga, akizungumza wakati wa Mkutano wa Msamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Wadau wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini CTI, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo. Mkutano huo ulikuwa na lengo la majadiliano kuhusu namna ya kutatua changamoto mbalimbali ili kufikia Uchumi wa Viwanda wa Kati pamoja na vikwazo vya ulipaji na ukusanyaji Kodi nchini. 
  Mwenyekiti wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini,Dkt. Samuel Nyantahe, akizungumza wakati wa Mkutano wa Msamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Wadau wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini CTI, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo. Mkutano huo ulikuwa na lengo la majadiliano kuhusu namna ya kutatua changamoto mbalimbali ili kufikia Uchumi wa Viwanda wa Kati pamoja na vikwazo vya ulipaji na ukusanyaji Kodi nchini. 
  Wadau wa mkutano huo wakisikiliza na kuweka kumbukumbu wakati viongozi wakiwasilisha majadiliano.
  Baadhi ya waandishi wakiwa bize kuandika kinachizungumzwa ukumbini hapo
  Umakini wa kusikiliza
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru, akipongezwa na Kamishina Mkuu wa TRA.Charles Kichele, baada ya hotuba yake.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru, akipongezwa na Mkurugezni Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini, Leodger Tenga baada ya kumaliza kuhutubia katika Mkutano wa Msamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Wadau wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini CTI, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, jana. Mkutano huo ulikuwa na lengo la majadiliano kuhusu namna ya kutatua changamoto mbalimbali ili kufikia Uchumi wa Viwanda wa Kati pamoja na vikwazo vya ulipaji na ukusanyaji Kodi nchini. 
  Kamishina Mkuu wa TRA, Charles Kichele, akizungumza wakati wa Mkutano wa Msamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Wadau wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini CTI, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo. Mkutano huo ulikuwa na lengo la majadiliano kuhusu namna ya kutatua changamoto mbalimbali ili kufikia Uchumi wa Viwanda wa Kati pamoja na vikwazo vya ulipaji na ukusanyaji Kodi nchini. 
  Wadau wakinyoosha mikono kuuliza maswali.....
  Wadau wakiuliza maswali....
  Viongozi wakinakili maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wadau
  wadau wakiuliza maswali....
  Wadau wakiuliza maswali....
  Kamishina mkuu wa TRA. Charles Kichele, akijibu maswali ya wadau
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru, akijibu maswali ya wadau
   Mfanyakazi wa Kampuni ya Montage Ltd, Happy Mbuya, akipokea cheti cha shukrani kwa kufanikisha mkutano huo kutoka kwa Katibu Mkuu, Dkt.Mero.
   Picha ya pamoja kwa kumbukumbu
  Picha ya pamoja kwa kumbukumbu

  0 0

   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akimvisha taji la Miss Garden Route 2017/2018 la Afrika Kusini Mtanzania Mlimbwende Witness Teddy Kavumo leo mjini Dodoma.
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akimpongeza Mtanzania Mlimbwende Witness Teddy Kavumo kwa ushindi wa taji la Miss Garden Route 2017/2018 la Afrika Kusini leo mjini Dodoma.
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akipokea nyaraka za ushindi wa taji la Miss Garden Route 2017/2018 la Afrika Kusini kutoka kwa mshindi wa taji hilo Mtanzania Mlimbwende Witness Teddy Kavumo leo mjini Dodoma.
   Mshindi wa taji la Miss Garden Route 2017/2018 la Afrika Kusini Mtanzania Mlimbwende Witness Teddy Kavumo akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mjini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura. 
  Mshindi wa taji la Miss Garden Route 2017/2018 la Afrika Kusini Mtanzania Mlimbwende Witness Teddy Kavumo. (Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma)

  Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma.

  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura amewataka vijana nchini kutumia muda vizuri na mazingira yanayowazunguka ili kufikia azma ya malengo waliojiwekea katika kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

  Naibu Waziri Wambura ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma alipokuwa akimpongeza Mlimbwende Witness Teddy Kavumo ambaye ni Mtanzania anayeishi Afrika Kusini kwa kushinda taji la Miss Garden Route 2017/2018  Mei 6 mwaka huu nchini humo katika mji wa George.

  Mlimbwnde Witness aliibuka mshindi wa Miss Garden Route 2017/2018 akiwa ni miongoni mwa washindani 14 walioingia fainali baada ya mchujo wa awali wa washiriki 600.“Ni dhahiri umetumia ujuzi, ubunifu, sanaa, imani, bidii, desturi, maadili, na sheria ambavyo umevipata  kutoka kwa familia, jamii ya Kitanzania na pia kwa jamii ya watu wa  Afrika Kusini” amesema Naibu Waziri Wambura.

  “Vijana wa Kitanzania, Mlimbwende Witness Mshindi wa taji la Miss Garden Route 2017 la Afrika Kusini amewaonesha njia, mjenge utamaduni wa kupambana na mazingira ili kufikia azma mnazojiwekea” alisistiza Naibu Waziri Wambura.

  Aidha, Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa Bi Witness ameonesha uzalendo kwa nchi yake kwa kuamua kuja Dodoma na kutoa taarifa ya mafanikio yake kama Mtanzania kwa ushindi alioupata katika mashindano ya ubunifu mavazi huko Afrika ya Kusini.

  Hatua hiyo inaonesha Mlimbwende huyo ameumeuthamini Utanzania wake na kuonesha kujali kutumia muda wa ziada kwa masuala ya fani ya urembo licha ya kwamba jukumu lake la msingi nchini humo ni la Kimasomo.
  Zaidi ya hayo Naibu Waziri Wambura amesema kuwa fani ya ubunifu na mitindo inatambulisha utamaduni, kuongeza kipato, kuinua uchumi na kukuza utalii kwa kuongeza juhudi, maarifa na kufanya kazi kwa bidii hatua nambayo inaleta matokeo mazuri yenye tija.

  Aidha, Naibu Waziri Wambura amemshauri Witness, kutumia bidhaa zenye asili ya Tanzania katika fani yake, ili kuzitangaza katika soko la ndani na la nje, kuvutia utalii, kuingiza kipato na  kukuza uchumi katika ngazi zote za mnyororo wa thamani katika sekta ya ubunifu wa mavazi na mitindo kwake yeye binafsi na kwa Taifa.

  Kwa upande wake Miss Garden Route 2017/2018 Mlimbwende Witness amesema kuwa anajivunia kuwa Mtanzania na kuonesha uzalendo kwa nchi yake na amewashauri Watanzania kusimama kwa kujiamini na kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

  Mashindano ya Miss Garden Route 2017/2018 yaliandaliwa na ‘The RoleModels Foundation” kwa kushirikiana na Wakala wengine akiwemo “Gemini Modelling Agency” iliyopo Mossel Bay  Afrika Kusini.

  0 0

   Mkurugenzi wa bodi ya Utalii nchini, Tanzania Devotha Mdachi  akikabidhiwa bendera Msanii wa mitindo, Jocktan Makeke.
  Msanii wa mitindo inayohusu utamaduni wa Mwafrika Jocktan Makeke / MAKEKE INTERNATIONAL anatarajia kwenda Abuja Nigeria kwa ajili ya maonesho makubwa ya utamaduni ya FACE OF CULTURE NIGERIA, ambapo ataonesha mavazi yenye ubunifu wa hali ya juu ambayo yanakwenda kwa jina la #OTOSIM2017

  Tamasha hilo litafanyika siku ya tarehe 09/09/2017 katika ukumbi wa Sheraton Hotel ya mjini Abuja.Aidha maonesho hayo yataambatana na utoaji wa tuzo kwa watu mbalimbali ambao wamefanya vizuri kwenye mambo ya utamaduni.

  0 0

  Na Mathias Canal, Dodoma

  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Septemba 7, 2017 Amezindua Programu maalumu kwa Vijana wa CCM katika ushiriki wa shughuli za miradi ya Kimaendeleo, Kiuchumi na Kijamii katika ukumbi wa CCM (NEC) Mjini Dodoma.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Shaka alisema Wazo hilo limeibuliwa wakati muafaka huku serikali ya CCM awamu ya tano chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ikiweka mkazo na vipaumbele kadhaa vinavyomtaka kila mtanzania hususani vijana kujituma, kufanya kazi kwa bidii na kuzalisha Mali.
   
  Alisema dhana ya kufanya kazi kwa bidii, malengo na shabaha si ngeni lakini kwa wakati huu inahubiriwa kwa nguvu kulingana na changamoto nyingi zilizopo, fursa, ushirikishwaji kwa kuzingatia mahitaji halisi kutokana na mabadiliko ya dunia Kiuchumi na Kimaendeleo.

  Aliwasisitiza Vijana kutambua wajibu wa kukuza shughuli za kazi na maisha zikiongozwa na nguvu ya uzalendo, kujali utaifa na kutambua dhamana iliyopo ya kudumisha amani, Umoja, Mshikamano na Maendeleo."Ili kusihi yote hayo hatimaye Vijana waweze kuyafanikisha tunapaswa kuwa na mioyo isiyopwaya au kukosa rutuba ya kutodumisha uzalendo, tunalazimika kwa pamoja kutambua mpango wowote wa kuyafikia maendeleo ya kweli utabaki ni hadithi na ndoto Kama hatutaongozwa na shime ya uzalendo au kutothamini utaifa wetu Kama ambavyo viongozi wanatuhimiza siku Hadi siku" Alisema Shaka.

  Shaka aliwaeleza Vijana kuwa pamoja na kuwepo juhudi kubwa za mara kwa mara kuchukuliwa na serikali, mashirika hiari ya Kijamii na yasiyokuwa ya kiserikali, kuelimisha juu ya dhana ya ushirikishwaji na ushiriki wa Vijana katika miradi ya Kiuchumi na Kijamii wanapaswa kuwa na utayari, uthubutu, uzalendo, na Utaifa.

  Alisema kuwa Vijana wanapaswa kukubali kujadiliana na wenzao juu ya mpango wa maendeleo na hatma ya Taifa na mustakabali wake kwani ndiyo njia pekee ya kukuza uzalendo kwa Taifa.Alisema mataifa yaliyoendelea yametokana na watu wake kukubali kufanya kazi kwani Ndiko kuliko yakomboa mataifa hayo yaliyoendelea kutoka katika uchumi duni na kuhamia katika uchumi wa Kati na Sasa wakionekana kuwa na uchumi wa maendeleo ya viwanda.

  "Mafanikio hayakuja Kama zawadi kwenye kisahani Cha Chai ama kutokea kwa bahati mbaya Kama mtende unavyoota jangwani ni lazima kukubali kwa pamoja kufanya kazi ili kupambana na adui umasikini""Wakati huu ambao serikali imebeba mzigo wa kutoa elimu bure toka msingi Hadi sekondari ni lazima Vijana tuwe na muktadha mmoja wa kujenga mtazamo wa pamoja kwa kujitambua na kukubali kufanya kazi bila kusukumwa" Alisema Shaka.

  Aliongeza kuwa kazi ya Vijana siku zote na kila wakati inapaswa kuwa ni kufikiri, kupambanua, kubuni na kujadiliana ili kumaliza changamoto, vikwazo, fursa na matumizi ya nafasi husika katika Jamii.Aidha, kupitia kusanyiko hilo aliwaagiza na kuwataka makatibu wote wa Umoja wa Vijana wa CCM wa mikoa na Wilaya nchini kila mmoja kuhakikisha programu hiyo inaanzishwa katika mikoa na Wilaya zake na kusisitiza kuhitajika matokeo makubwa kwani ataandaa utaratibu wa kuthamini programu hiyo kila kipindi Cha robo mwaka.

  Sambamba na hayo pia Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Shaka Hamdu Shaka alishiriki ujenzi wa shule ya Msingi Mizengo Pinda iliyopo katika Kijiji Cha Chinangali 2 Kata ya Bwigili Wilayani Chamwino.Pamoja na kushiriki shughuli ya uchimbaji msingi, ufyatuaji tofali na matengenezo ya tungilizi kwa ajili ya upauaji wa majengo ya shule hiyo pia Shaka alichangia mifiko 20 ya saruji kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za wananchi walizozianza kwa kujitolea nguvu, muda na rasilimali zao.

  0 0

  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Balozi wa Vietnam nchini Tanzania, Nguyen Doanh pale ugeni kutoka Vietnam ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
    Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Balozi wa Vietnam nchini Tanzania, Nguyen Doanh pale ugeni kutoka Vietnam ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa kazi pamoja na kuboresha urafiki baina ya nchi hizi mbili.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Vietnam nchini Tanzania, Nguyen Doanh pale ugeni kutoka Vietnam ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa kazi pamoja na kuboresha urafiki baina ya nchi hizi mbili.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akiwa katika picha ya pamoja​ na ugeni kutoka Vietnam uliomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa kazi pamoja na kuboresha urafiki baina ya nchi hizi mbili. Katikati ni Balozi wa Vietnam nchini Tanzania, Nguyen Doanh na kushoto ni katibu wa Balozi huyo, Ndg. Nguyen Binh.(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0

   Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Epharaim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Epharaim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusianaMfumuko wa bei wa Mwezi Agosti Mwaka huu(2017) kwa kipimo cha Mwezi umepungua kwa asilimia 0.4
  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Epharaim Kwesigabo  jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na mfumuko wa bei kwa mwezi Agosti Mwaka huu.Kulia ni Kaimu Meneja wa Ajira na Takwimu za Bei Ruth Minja

  MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Agosti 2017 umepungua zaidi hadi kufikia asilimia 5.0 ikilinganishwa na asilimia 5.2 ilivyokuwa mwezi Julai2017.

  Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Amesema hii inamanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2017 imepungua zaidi ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Julai,2017.

  Kwesigabo alisema Mfumuko wa Bei wa Bidhaa za Vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Agosti, 2017 umepungua hadi asilimia 8.6 kutoka asilimia 8.9 ilivyokuwa mwezi Julai, 2017.
  "Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 108.46 mwezi Agosti, 2017 kutoka 103.28 mwezi Agosti, 2016" alisema Kwesigabo.

  Akizungumzia mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani kwa mwezi Agosti,2017 umepungua hadi asimilia 9.1 kutoka asilimia 9.3 mwezi Julai 2017. Ambapo badiliko la Fahirisi za bei zisizo za vyakula umebaki kuwa asilimia 3.1 mwezi Agosti, 2017 kama ilivyokuwa mwezi Julai, 2017.

  Kwesigabo ameongeza kuwa mfumuko wa bei ambao haujumuishi vyakula na nishati kwa mwezi Agosti, 2017 umepungua hadi asilimia 1.8 kutoka asilimia 2.2 Julai, 2017.

  Fahirisi inayotumika kukokota aina hii ya mfumuko wa bei haijumuishi vyakula vinavyoliwa nyumbani na migahawani, vinywaji baridi, petroli, dizeli, gesi ya kupikia, mafuta ya taa, mkaa kuni na umeme.

  Amesema vyakula na bidhaa za nishati vinasifa ya kuwa na bei ambazo hubadilika mara kwa mara, hivyo vikiondolewa kwenye fahirisi ya bidhaa na huduma zote hubakia fahirisi ambayo ina mwelekeo imara kwa watunga sera.

  0 0

   Wakala wa wauzaji wa Vifaa Vya kuunganishia mabomba yanayotoka nchini Marekani, David Robert Mwamsojo akionyesha waandishi wa habari moja ya kiunganishi cha  mabomba yanayotengenezwa na kampuni ya GroovJoint ya nchini Marekani katika mkutano wa kuitambulisha kampuni ya GroovJoint ya nchini Marekani iliyoleta nchini Tanzania teknolojia mpya ambayo itasaidia kuokoa miundo mbinu ya maji. Pembeni ni Makamu wa Rais wa Kampuni ya GroovJoint ya nchini Marekani iliyokuja kuwekeza nchini Tanzania katika sekta ya viwanda.Picha na Kajunason/MMG.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye akitoa shukrani zake za pekee kwa kampuni ya GroovJoint iliyokuja nchini Tanzania kuwekeza upande wa viunganishi vya mabomba ambapo alisema kuwa wameamua kuwapokea kwa mikono miwili kampuni hiyo kwa vile viunganishi vitasaidia wananchi kupata maji safi na salama. Pembeni ni Makamu wa Rais wa Kampuni ya GroovJoint ya nchini Marekani iliyokuja kuwekeza nchini Tanzania katika sekta ya viwanda na Wakala wa wauzaji wa Vifaa Vya kuunganishia mabomba yanayotoka nchini Marekani, David Robert Mwamsojo. Makamu wa Rais wa Kampuni ya GroovJoint ya nchini Marekani, David Newman iliyokuja kuwekeza nchini Tanzania katika sekta ya viwanda kwa kuleta viunganishi vya mabomba.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye akimshukuru Makamu wa Rais wa Kampuni ya GroovJoint ya nchini Marekani, David Newman mara baada ya mkutano na waandishi wa habari kuelezea malengo ya kampuni yao. Pembeni ni Wakala wa wauzaji wa Vifaa Vya kuunganishia mabomba yanayotoka nchini Marekani, David Robert Mwamsojo.

  0 0


  0 0


  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akimkabidhi simu aina ya Tecno S1 mmoja kati ya washindi 120 waliojishindia simu kwenye promosheni ya mwisho ya Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi , Brigitta Mbuya, jumla ya washindi 720 wamejishindia simu nchi nzima . Hafla hiyo ilifanyika Duka la Tigo Manzese jijini Dar Es Salaam leo.
  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akimkabidhi simu aina ya Tecno S1 mmoja kati ya washindi 120 waliojishindia simu kwenye promosheni ya mwisho ya Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi , Ibrahim Hassan mkazi wa Goga, jumla ya washindi 720 wamejishindia simu nchi nzima . Hafla hiyo ilifanyika Duka la Tigo Manzese jijini Dar Es Salaam leo.
  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akimkabidhi simu aina ya Tecno S1 mmoja kati ya washindi 120 waliojishindia simu kwenye promosheni ya mwisho ya Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi , Cecilia Paul mkazi wa Kimara, jumla ya washindi 720 wamejishindia simu nchi nzima . Hafla hiyo ilifanyika Duka la Tigo Manzese jijini Dar Es Salaam jana.
  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akimkabidhi simu aina ya Tecno S1 mmoja kati ya washindi 120 waliojishindia simu kwenye promosheni ya mwisho ya Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi , Aisha Hamisi mkazi wa Magomeni, jumla ya washindi 720 wamejishindia simu nchi nzima . Hafla hiyo ilifanyika Duka la Tigo Manzese jijini Dar Es Salaam leo.
  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akimkabidhi simu aina ya Tecno S1 mmoja kati ya washindi 120 waliojishindia simu kwenye promosheni ya mwisho ya Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi , Sarah Lema mkazi wa Tabata, jumla ya washindi 720 wamejishindia simu nchi nzima . Hafla hiyo ilifanyika Duka la Tigo Manzese jijini Dar Es Salaam leo.
  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akimkabidhi simu aina ya Tecno S1 mmoja kati ya washindi 120 waliojishindia simu kwenye promosheni ya mwisho ya Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi , Goodluck Mayanja, jumla ya washindi 720 wamejishindia simu nchi nzima . Hafla hiyo ilifanyika Duka la Tigo Manzese jijini Dar Es Salaam leo.

  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akimkabidhi simu aina ya Tecno S1 mmoja kati ya washindi 120 waliojishindia simu kwenye promosheni ya mwisho ya Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi , Amour Haji mkazi wa Mbagala, jumla ya washindi 720 wamejishindia simu nchi nzima . Hafla hiyo ilifanyika Duka la Tigo Manzese jijini Dar Es Salaam leo.
  Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washindi walioshinda simu aina ya Tecno S1 zilikuwa zinatolewa kwenye promosheni ya Jaza ujazwe Ujaziwe zaidi leo .

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda jana amekabidhi Pikipiki za Traffic 10, Computer 100 na Baiskel za kisasa 200 kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi wa Jeshi la Polis Dar es Salaam na kulifanya kuwa la kisasa.

  Kupatikana kwa Vitendeakazi hivyo ni matokeo ya jitihada binafsi za RC Makonda kutafuta Wahisani.Makonda amesema amedhamiria kuleta Mapinduzi Makubwa kwa Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha Askari wanakuwa na Vifaa vya kutosha ikiwemo Magari, Pikipiki za kawaida na zile za Traffic,Baiskeli za Doria,Silaha na Computer ilikuwafanya kufanya kazi katika Mazingira mazuri.
  Amesema amechoka kuona Askari wakipoteza Maisha wakitekeleza majukumu yao kwa kuvamiwa na Majambazi na kuporwa Silaha ndio maana anapambana kutafuta vitendeakazi ili Askari wake wajivunie kufanya kazi katika Mkoa wake.Aidha amesema Pikipiki za Traffic zitaenda kusaidia kwenye Misafara ya Viongozi, Misiba na kuwahisha wagonjwa Hospital.
  Kuhusu Computer 100 alizotoa amesema zitagawanywa kwenye Vituo vya Polisi 20 na kufungwa mfumo wa kisasa wa kupokea taarifa za Uhalifu, kubainisha maeneo yaliyoshamiri Uhalifu, kutambua wahalifu Sugu ambapo mfumo huo utatoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa,Kamanda wa Mkoa,Wilaya na Mkuu wa kituo ili kuwezesha Viongozi kufanya maamuzi.
  Amesema Baiskeli 200 alizozitoa zitaendelea kuimarisha Doria mitaani na kuongeza kuwa Baiskeli nyingine za kisasa 1,000 zipo Nchini China zikifanyiwa Maboresho ambapo zikikamilika zitakuja kuongeza nguvu kupambana na Uhalifu.Sanjari na hayo amesema Magari Mabovu 15 ya Polisi kati ya 26 yaliyopelekwa Kilimanjaro kufanyiwa marekebisho yamekamilika ambapo yatakuwa na Mwonekano wa kisasa kama ilivyo kwa Magari ya Jeshi ya UN.
  Pamoja na kuligusa Jeshi la Polisi kama Taasisi ameona pia aguse maisha ya Askari mmoja mmoja kwa kuwatafutia Mkopo wa Viwanja sababu gharama ya Viwanja ni kubwa hivyo kufanya Askari kushindwa kumudu gharama hali inayosababisha baadhi yao kustaafu wakiwa hawana makazi na kuishi kwa tabu.

  Viwanja hivyo vilikuwa vikiunzwa kwa Tsh 20,000/= kwa Square meter lakini RC Makonda amepambana hadi kufikia Tsh 5,000/= kwa Square Meter ambapo Askari watakuwa wakilipa mkopo huo kidogokidogo kwa muda wa Miaka Mitano na wataruhusiwa kujenga hata kama hawajamaliza mkopo wao.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa vyerehani 25 kutoka katika Taasisi ya African Releaf Organization ya nchini Kuwait.

  Amepokea msaada huo leo (Ijumaa, Septemba 9, 2017) kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Ruangwa.

  Waziri Mkuu ameishukuru taasisi hiyo kwa msaada huo wa vyerehani ambavyo vitagawiwa kwenye vikundi mbalimbali vya wajasiriamali wilayani Ruangwa.Amesema vyerehani hivyo vitawawezesha wajasiriamali wanaojishughulisha na ushonaji kupata vitendeakazi vitakavyotumika kama njia ya kujiongezea kipato.

  Waziri Mkuu amesema mbali na kutoa msaada huo wa vyerehani pia taasisi hiyo inajenga Zahanati katika kijiji cha Mbecha kata ya Nanganga wilayani Ruangwa.“Taasisi hii ni rafiki na Halmashauri yetu na Wanaruangwa wamefarijika kwa kupata zahanati na vyerehani vitakavyotumika kama njia ya kujiongezea kipato.”

  Awali, Mkurugenzi wa Miradi wa Taasisi ya African Releaf Organization, Bw. Khamis Mkanachi alishukuru kwa ushirikiano wanaoupa kutoka Halmashauri ya Ruangwa.Pia Bw. Mkanachi amesema taasisi yao itaendelea kuvisaidia vikundi mbalimbali vya ujasiriamali katika Halmashauri hiyo kwa lengo la kuvikwamua kiuchumi.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alimtembelea na kumpa pole mbunge wa jimbo la Newala Vijijini, Bw. Rashidi Akbar aliyelazwa katika Taasisi Moyo ya Jakaya Kikwete.Kwa upande wake Bw. Akbar alimshukuru Waziri Mkuu kwa kumtembelea hospitalini hapo na kwamba hali yake kwa sasa inaendelea vizuri ukilinganisha na alivyofikishwa.

  Pia Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kumjulia hali Bw. Anzigar Kambanga ambaye ni mwananchi wa wilaya ya Ruangwa aliyelazwa katika Taasisi Moyo ya Jakaya Kikwete.

  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  IJUMAA, SEPTEMBA 9, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipeana mkono na mkurugenzi wa taasisi ya African Relief Organization, Wakati akipokea cherehani ikiwa ni sehemu ya vyerehani 25 vya msaada, zilizo tolewa kwa Wananchi wa Ruangwa kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Septemba 8, 2017, (kulia) ni Mratibu wa miradi wa African Relief Organization Bw. Khamis Mkanachi.

  0 0


  0 0


  Na David John -Mwanza.

  KATIBU wa Chama cha Michezo wilaya ya Nyamagana Daddy Gilbert amewataka wanasiasa kuacha tabia ya kuitumia michezo pindi wanapotafuta nafasi za uongozi na wakishapata hawana habari.
  Amesema wanasiasa wengi wamekuwa wakitumia michezo kama tiketi yao ya kutaka uongozi na wakifanikiwa hawanahabari na michezo jambo ambalo halipendezi.

  Kiongozi huyo wa michezo ametoa dukuduku lake hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo walifika katika ofisi za chama cha soka wilaya hiyo kutaka kujua namna walivyojipanga kuendeleza michezo.
  Daddy amesema anakerwa na baadhi ya wanasiasa ambao wanatumia michezo kupata uongozi na pindi wanapofanikiwa hawajari tena.

  "unajuwa kama wezetu wanasiasa wangekuwa wanatuunga mkono naamini hata kwa hapa mwamza tungefika mbali lakini bahati mbaya wakishapata wanachokipata hawana muda tena na sisi. amesema Daddy.

  Pia bosi huyo wa chama wilaya ametoa rai kwa wananchi wa mkoa wa mwanza kujitokeza katika viwanja vya michezo hususani uwanja wa Nyamagana ambapo ligi ya Willya kutafuta timu zitakazo cheza ligi ngazi ya mkoa.

  "kama mmavyoona hapa kuna ligi ya Wilaya ambayo imeshirikisha timu 25 inaendelea lakini mwamko wa mashabiki Kama mnavyoona."amesema Daddy.
  Mwenyekiti wa Chama cha Soka wilaya ya  Nyamagana Daddy Girbat( kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mwandishi wa Habari hizi David John leo mara baada ya kumtembelea ofisini kwake ulipo uwanja wa michezo wa Nyamagana. Mkoani mwanza


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza Mwananchi wa Wilaya ya Ruangwa Bw. Anzigar Kambanga, wakati alipoenda kumjulia hali katika Taasisi ya Jakaya Kikwete, iliyopo Muhimbili Septemba 8, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimjulia hali Mbunge wa Newala Vijijini, Razak Rashid Akbar, wakati alipoenda kumjulia hali katika Taasisi ya Jakaya Kikwete, iliyopo Muhimbili Septemba 9, 2017.

  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0

  Baada ya Msanii wa Bongo Fleva, Nasib Abdul (Diamond Platinumz) kumwimba Mzee Onyango kuwa zilipendwa sasa mzee huyo ameibuka na kukana kuwa yeye sio Zilipendwa.

  Hatimaye Mzee Onyango ambaye ni Mwigizaji Mkongwe nchini Tanzania amemjibu Diamond Platinumz kwa vitendo baada ya kuachia filamu yake mpya ya iitwayo BABU THE PERFECT MAN kupitia kampuni yake ya  ONYANGOPRODUCTION.

  "Nashangaa sana kusikia Diamond Platinumz kuimba kwamba mimi na Mzee Jangala zilipendwa, mtoto huyu amenikosea sana mimi bado napendwa na mashabiki zangu bado wanaamini kuwa nina uwezo mkubwa sana wa kufanya kazi ya uigizaji bila tatizo lolote" alisema Mzee Onyango.


  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiwasilisha maelezo ya Muswada wa Sheria ya Reli wa mwaka 2017 kwa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Rashid Chuachua.
  Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiwasilisha maelezo kuhusu Muswada waSheria ya Reli wa mwaka 2017 ambao umeshasomwa Bungeni kwa mara ya kwanza.

older | 1 | .... | 1363 | 1364 | (Page 1365) | 1366 | 1367 | .... | 1898 | newer