Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

BANDARI YA TANGA YANG’ARA KILIMANJARO CUP

$
0
0
Mchezaji wa timu ya Bandari Tanga akiruka juu kuwania mpira wakati wa mchezo wa Mashindano ya Kilimanjaro Cup yanayoendelea kwenye viwanja wa KCMC na Baptist ambapo mechi hiyo ilikwisha kwa Bandari Tanga kuibuka na ushindi wa vikapu 64 dhidi ya 57 
Wachezaji wa timu za Bandari Tanga na Baptist wakiwania mpira wakati wa mchezo wa Mashindano ya Kilimanjaro Cup yanayoendelea kwenye viwanja wa KCMC na Baptist ambapo mechi hiyo ilikwisha kwa Bandari Tanga kuibuka na ushindi wa vikapu 64 dhidi ya 57 
Kocha wa timu ya Bandari Tanga Mohamed Fazal akitoa maelekezo kwa timu hiyo wakati wa mapumzikokulia ni PRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu 
Kocha wa timu ya Bandari Tanga,Mohamed Fazal akitoa mawaidha kwa timu hiyo wakati wa mapumziko kulia ni PRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu 
Kikosi cha timu ya Mpira wa Kikapu ya Bandari Tanga 


TIMU ya Mpira wa Kikapu ya Bandari Tanga ambayo inashikilia Ubingwa wa Mashindano ya Kilimanjaro Cup mwaka jana inashiriki tena Mashindano hayo kutetea ubingwa huo mwaka huu katika mashindano yanayoendelea kwenye viwanja KCMC mjini Moshi.

Kitendo cha timu hiyo kuendelea kufanya vizuri katika mashindano hayo kwa mara nyengine kinaonyesha namna kinavyotumia vema fursa hiyo kuitangaza Bandari ya Tanga.

Katika kuhakikisha suala hilo linakwenda kwa vitendo leo timu ya Bandari Tanga wameibuka na ushindi wa vikapu 64-57 dhidi ya timu ya Baptist katika mechi iliyokuwa na upinzani mkubwa huku Bandari Tanga ikipambana ili kuhakikisha inatetea Ubingwa wake na kuondoka na ushindi huo.

Awali akizungumza wakati akizundua mashindano hayo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwira amezitaka timu shiriki kutumia fursa ya mashindano hayo kutangaza utalii wa nchi ikiwemo mlima Kilimanjaro.“Baada ya mashindano haya timu zote shiriki zitakwenda kupanda mlima Kilimanjaro ili kuweza kuhamasisha wanamichezo na wananchi wengine kuweza kutalii mlima huo “Alisema Mkuu huyo wa mkoa.

Mkuu huyo wa mkoa alitumia nafasi hiyo kuwataka vijana kuchangia damu kwa wahitaji ambapo katika viwanja hivyo sehemu iliyotengwa kwa ajili ya kuchangia damu kwa hiari.Mashindano hayo yanaendelea kwa wiki nzima katika viwanja vya Baptist na KCMC Mkoani Kilimanjaro.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

MAHAKAMA YARUHUSU MANJI NA WENZAKE KUHOJIWA NA JESHI LA POLISI.

$
0
0

Na Karama Keyunko,Blogu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, imeruhusu mfanyabiashara Yusuf Manji na wenzake watatu kupelekwa polisi na kuhojiwa dhidi ya kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili ili kukamilisha upelelezi.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi kufuatia barua ya maombi kutoka kwa Mkuu wa upelelezi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, (ZCO), ndipo akaandika hati ya kuwatoa washtakiwa mahabusu (remove order) ili kuwafanyia mahojiano katika kesi namba 33/2017

Amesema hawawezi kukataa maombi hayo ya polisi kwani kufanya hivyo ni sawa na kupingana na kauli ya mahakama ya kukamilisha upelelezi, na ndio maana ikatolewa hati ya kuwatoa mahabusu kwa ajili ya mahojiano. “Hii sio mara ya kwanza kuwatoa washitakiwa kwa upelelezi," alisema Hakimu Shaidi.

Aidha amewaagiza polisi kuhakikisha washtakiwa wanatendewa ikiwemo kuzingatia afya zao kwani wanawakabidhi wakiwa na afya nzuri na kama watahitaji uwakilishi wa mawakili wao wapate uhuru wa kuwakilishwa kwenye jambo lolote na isiwe kificho.

Hakimu Shahidi amesema, "Namkabidhi Koplo Dotto kama barua inavyoelekeza kuwa nimkabidhi Sajenti Mkombozi au Doto lakini kwa kuwa Mkombozi hayupo basi namkabidhi Doto ila washitakiwa warudishwe kesho ndani ya muda wa kazi.

Mbali na Manji, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Quality Group Ltd, Deogratius Kisinda (28), Mtunza stoo, Abdallah Sangey (46) na Thobias Fwere (43)  mkazi wa Chanika wanakabiliwa na mashitaka ya uhujumu uchumi.

Mapema, akiwasilisha maombi hayo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi aliiomba mahakama iruhusu washitakiwa waweze kukabidhiwa kwa Polisi ili kutimiza matakwa ya upelelezi ambapo amedai kifungu
Cha 59 cha CPA kinawapa mamlaka Polisi kufanya upelelezi.

Hata hivyo, wakili wa utetezi Hudson Ndusyepo alipinga watuhumiwa kwenda kuhojiwa kwa madai kuwa, mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa amri hiyo sababu DPP hajatoa Kibali kwa mahakama hiyo kusikiliza kesi hiyo zaidi ya kutaja tarehe, alidai mahakama hiyo imefungwa mikono ya kutoa amri dhidi ya maombi hayo au yoyote yale.

Naye wakili Hajra Mungula aliiomba mahakama kukataa ombi hilo kwa madai kuwa washitakiwa hao wako chini ya ulinzi na kwamba upande wa mashitaka uliwashitaki washitakiwa kwa mbwembwe na kuwasilisha hati ya kuwazuia dhamana huku wakijua kwamba hawajakamilisha upelelezi

Hata hivyo, Wakili Kishenyi alidai mahakama imekuwa ikisisitiza kukamilisha upelelezi na kwamba wanachofanya ni sehemu ya kukamilisha upelelezi.
Pia alidai washitakiwa hao wanahaki ya kuwakilishwa hivyo maombi yao yakubaliwe.

Washtakiwa hao wanadaiwa kukutwa na sare za na vifaa mbali mbali vya jeshi.
Mfanyabiashara Yusuph Manji, akitoka Mahakamani baada ya Hakimu Mkazi, Huruma Shahidi kuruhusu yeye na wenzake watatu wanaokabiliwa na tuhuma za uhujumu uchumi kupelekwa polisi kuhojiwa ili kukamilisha upelelezi.

KAMPENI YA UZALENDO KWANZA YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR,KUHAMASISHWA NCHI NZIMA

$
0
0

Mwenyekiti wa Kampeni ya Uzalendo Kwanza, Steven Mengele almaarufu kwa jina la kisanii Steven Nyerere, akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar kuhusina na uzinduzi wa kampeni yao itakayojulikana kwa jina la UZALENDO KWANZA. Pichani kulia ni Msanii wa Filamu Wastara na kulia kwake ni Misayo Ndumbagwe.

kampeni hiyo imezinduliwa rasmi leo, ikiwa na lengo la kuunga mkono jitihada na juhudi zinazofanywa na Rais Dkt John Pombe Magufuli katika suala zima la kuhakikisha Tanzania inasonga mbele kimaendeleo ambapo wasanii wa muziki na filamu wapatao 250 wameshirkishwa pamoja na wachezaji wa mpira.

Steve amesema kuwa, ni wakati sasa kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kuvienzi na kuvipenda vitu vyao kwa namna moja ama nyingine katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa sababu nchi ni Yetu,rasimali zilizopo ni zetu,madini ni yetu,mbuga za wanyama ni vya kwetu, hivyo ni muhimu Watanzania wakaamka sasa na kuonesha uzalendo wao halisi kama ambavyo Rais Dkt John Pombe Magufuli amekuwa akionesha kwa vitendo na kusisitiza suala zima la Uzalendo ndani ya nchi yetu.

"Sisi kama Wasanii, kwa moyo mmoja tumeamua kushikamana kwa pamoja na baraka zote tunazo kushikamana na kuiunga mkono kauli mbiu ya Rais Dkt Joh Pombe Magufuli ya UZALENDO KWANZA kuwa na harakati za kuifanya Tanzania yetu na Watanzania wenyewe kuwa Wazalendo kwa nchi yao",alisema Steve Nyerere na kuongeza kuwa kauli mbiu hiyo sio kwa ajili ya Dar Es Salaam tu bali,ni kwa ajili ya Tanzania nzima.
Wasanii wa mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya UZALENDO KWANZA.
Mwenyekiti wa Kampeni ya Uzalendo Kwanza Steven Mengele almaarufu kwa jina la kisanii Steven Nyerere akitoa ufafanuzi zaidi kuhusina na kampeni hiyo ya UZALENDO KWANZA mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar,kampeni hiyo inatarajia kuhamasishwa mikoa mbalimbali nchini .Pichani kushoto ni Msanii wa Filamu ni Misayo Ndumbagwe pamoja na Kemmy .
Baadhi ya Wasanii mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya UZALENDO KWANZA,itakayosambazwa nchi nzima kuhakikisha wananchi wanaelewa dhana nzima ya kuwa mzalendo na nchi yako.
Mkutano ukiendelea mapema leo wa uzinduzi wa kampeni ya UZALENDO KWANZA.
Msanii wa Filamu Wastara Juma akiwahimiza Watanzania kuwa WAZALENDO KWANZA katika mambo mbalimbali ikiwemo kuvithamini vya vyumbani,pia amewaomba Watanzania kuwaunga mkono Wasanii wao kwa kununu kazi zao zilizo halisi na halali ili kuhakikisha dhama nzima ya UZALENDO KWANZA inatimia.
Baadhi ya Wasanii wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi wa kampeni ya UZALENDO KWANZA,itakayopita mikoa mbalimbali kuwahamasisha wananchi kuwa Wazalendo na nchi yao na pia kumuunga mkono Rais Dkt John Pombe Magufuli katika suala zima la kuhakikisha Tanzania inasonga mbele kimaendeleo.

MCHENGA BBALL STARS MABINGWA WAPYA WA SPRITE BBALL KINGS 2017

$
0
0
Mabingwa wa Michuano ya Sprite BBall Kings  Mchenga BBall Stars wakiwa pamoja na Afisa Masoko msaidizi wa kampuni ya Coca-Cola Pamela Lugenge (aliyevaa t-shirt ya kijani) baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya kiasi cha Shilingi Milioni 10 sambamba na kukabidhiwa kikomne baada ya kushinda katika mchezo wa fainali uliomalizika kwa Mchenga kushinda kwa pointi 104-94 dhidi ya TMT..


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

TIMU ya Mchenga BBall Stars wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Sprite BBall Kings 2017 baada ya kuibugiza wapinzani wao TMT kwa pointi 104-94 katika fainali ya mwisho iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii kwenye Viwanja vya Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es salaam.

Mchenga wanakuwa mabingwa wa Kwanza wa michuano hiyo wakijinyakulia kitita cha shilingi Milioni 10 sambamba na kombe huku TMT ikijinyakulia milioni tatu baada ya kushika nafasi ya pili.

Katika mchezo wa kwanza hadi wanne TMT walifanikiwa kushinda mara mbili sawa na Mchenga na kupelekea mchezo wa tano kuwa wa kasi na ushindani huku kila upande akijaribu kutokufanya makosa na kuibuka kidedea.

Pamoja na hayo, mechi ya leo iliweze kuonyesha utofauti na ufundi mkubwa kutokana na timu zote mbili kupania kuwa bingwa jambo ambalo lilipelekea timu hizo kujikuta zikitoka sare ya pointi 84-84 kwa mara ya kwanza na kupelekea waamuzi kulazimika kuongeza dakika nyingine tano ili aweze kupatikana mshindi wa mashindano hayo na ndipo Mchenga BBall Stars alipomchapa TMT jumla ya pointi 102-94
Timu ya TMT ikiwa imeshikilia mfano wa hundi yenye thamani ya Milioni tatu baada ya kushinda nafasi ya pili michuano ya Sprite BBall Kings 2017.

Kwa upande mwingine, mchezaji Rwahabura Munyagi kutoka timu ya Mchenga BBall Stars ameweza kushinda nafasi ya mchezaji bora 'MVP' kwa kuweza kuipigania timu yake kushinda mchezo wa leo.

 Afisa Masoko msaidizi wa kampuni ya Coca-Cola Pamela Lugenge aliweza kuwakabidhi mabingwa hao wapya wa Sprite BBall Kings 2017 mfano wa hundi ya kiasi cha Milioni 10 pamona na kombe, aliweza pia kuwakabidhi Timu ya TMT na mchezaji bora wa mashindano hayo 'MVP' Rwahabura Munyagi kutoka Mchenga.

Mratibu wa Mashindano hayo, Basilisa Biseko ameweza kuipongeza timu ya Mchenga kwa ushindi huo walioupata wakiwa ndio mabingwa wa kwanza wa Sprite BBall Kings na kuwataka wawe mabalozi wazuri wa mpira wa kikapu mtaani ili kuweza kuhamasisha watoto na vijana kuupenda mchezo huo na kurejesha thamani ya Mpira wa Kikapu.

Amesema Mwitikio mkubwa wa watu umeonekana katika mashindano hayo hasa katika michezo iliyokuwa inachezwa kwenye Viwanja vya Don Bosco na anaamini mwakani yatakuwa na hamasa zaidi tofauti na mwaka huu.

Mashindano hayo yalianza rasmi mwezi Mei mwaka huu kwa kuanza kufanya usaili kwa timu 54 katika Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam zikianza kwa mtoano kwenye Viwanja mbalimbali na kuhitimishwa wikiendi hii ya Septemba 02.
 Mchezaji bora 'MVP' wa michuano ya Sprite BBall Kings kwa mwaka 2017. Rwahabura Munyagi akiwa ameshikilia kikombe chake sambamba na kupata kiasi cha shilingi Milioni 2.

AFYABANDO KAMPENI KUWAKOMBOA WATANZANIA

$
0
0

 Mtaalam Mwelekezi wa Afyabando-Nordic Foundation Tanzania, Dkt. Respicius Salvatory akiongea na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Septemba 3 2017, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kujishindia kadi ya bima ya Afya ijulikanayo kama ‘AfyaBando’. Kulia ni Afisa Mwandamizi Mipango na Utawala wa Taasisi ya Nordic, Maria Nimrod na Afisa Tehama wa Taasisi hiyo, Dickson Leonard.
 Afisa Mwandamizi Mipango na Utawala wa Taasisi ya Nordic, Maria Nimrod akifafanua jambo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kujishindia kadi ya bima ya Afya ijulikanayo kama ‘AfyaBando’. Pamoja naye ni Mtaalam Mwelekezi wa Afyabando-Nordic Foundation TanzaniaDkt. Respicius Salvatory (wa pili kulia) , Afisa Tehama wa Taasis hiyo, Dicson Leonard Afisa Afya na Teddy Uledi. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogspot) 
HOTUBA   YA MTAALAM MUELEKEZI WA MRADI WA AFYABANDO. DKT. RESPICIUS SALVATORY KATIKA UZINDUZI WA KAMPENI YA KUAMASISHA WATANZANIA KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA KUPITIA KAMPENI YA AFYABANDO INAYORATIBIWA NA TAASISI YA NORDIC FOUNDATION TANZANIA LEO TAREHE 03/08/2017 KEBB’Y HOTEL.
Ndugu Waandishi wa habari
Napenda kuchukua nafasi hii kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kufika mahali hapa. Pia mimi kama mtumishi wa umma kwenye sekta ya afya napenda kuwashukuru sana Waandishi wa habari kwa kuitikia wito wetu huu kwani kampeni tunayoizindua leo yaani Afyabando ni muhimu sana kwa kila Mtanzania.
Mimi napenda kujikita kwenye mambo muhimu ambayo napenda watanzania waweze kuyajua na kuyafanyia kazi.  Kwanza kabisa mimi naongea kwa uzoefu wa miaka mingi ya kazi katika jiji letu hili kama sehemu ya Tanzania.  Kwa siku tunapokea wagonjwa wengi sana tena sana. Kwa kutokana na uzoefu huo pamoja na kupokea wagonjwa wengi nimekuja hapa ndugu Waandishi kuwaomba na kutoa Elimu kwa Watanzania umuhimu wa Bima ya afya. Ndugu zangu si utani tena, Bima ya afya ni muhimu sana, hivyo inabidi tusaidiane kuondoa changamoto  zifuatazo ili watu wengi wapate kujiunga.
  1. KUONDOA MTIZAMO HASI/MTIZAMO FINYU KUHUSU BIMA YA AFYA.
Ndugu Waandishi ni muhimu tushirikiane kutoa elimu kwa umma ili kuondoa mtizamo hasi dhidi ya bima ya afya. Nadharia ya Bima ni jambo ambalo halijazoeleka kwa jamii zetu hivyo ni jukumu la kila mtu kutoa elimu na kumuamasisha mwenzake umuhimu wa kuijunga na bima. Ugonjwa haupigi hodi hivyo ni vizuri kuacha kuwa na mtizamo hasi kuhusu Bima. Ni jambo la kushangaza watanzania wanapenda sana kuchangia misiba na kwa pesa nyingi lakini hawana utamaduni wa kuchangia wapendwa wao kupata Bima ya afya. Ni jambo la kushangaza watanzania wanapenda sana kuchangia harusi, kitchen party , birthday party na mambo mengi lakini watanzania hawana utamaduni wa kumchangia ndugu kuwa na Bima ya afya.
Ndugu Waandishi wa habari ninawaomba kupitia hadhara hii kuwajulisha Watanzania kuwa huu sasa ni wakati wa kubadilika na kutumia umoja wetu kuanza kuchangia ndugu na jamaa kadi za bima. Ni vizuri tuanze kuamasishana hivyo. Sisi watumishi wa hospitali za umma mnatupatia wakati mgumu sana, anafika mgonjwa hana bima wala pesa za matibabuhata chakula. Ndugu na jamaa ndipo wanaanza kuanza kuchanga tena kwa shida na inabidi mgonjwa tumpokee na kumuandika madeni. Naomba watanzania waache kusubiri kuchangia misiba waanze kampeni za kifamilia, kijamii na maeneo yao ya shughuli za kazi hasa hasa sekta binafsi kuanza kuchangia kadi ya bima. Tuanze kukumbushana na kuulizana je wewe una kadi ya bima. Watanzania tuache tabia ya kuchangia pesa nyingi harusi lakini bila kuchangia kadi ya Bima.
Tunaomba waandishi wa habari tusaidieni sana kufikisha elimu hii ili tuweze kuwa na mwamko wa kuchangia Bima zetu za afya kwa nguvu na hari mpya. Ni kwa msingi huu sasa watanzania wachamkie fursa hii yah ii kampeni ya Afyabando kwa kucheza hii bahati nasibu ya kijamii yenye uhakika kwani washindi ni wengi na hata kwa shilingi mia tano mtu anapata Bima ya afya. Naomba Waandishi na nyinyi changamkia hii fursa ya kupata Bima kwa kujiunga na Afyabando tusipende kuchangia misiba bali tupende kuchangia kuboresha afya zetu kupitia Bima ya afya.
  1. TABIA YA MATIBABU YA MAZOEA NA HOLELA KWA KUKOSA BIMA YA AFYA
Ndugu Waandishi wa habari  napenda  kusisitiza kuwa kumekuwa na tabia yakufanya matibabu ya mazoea kwa mtindo wetu wa mila yaani kufanya matibabu pasipo vipimo. Watu wengi wanashindwa kwenda kupima afpya zao na kufanya uchunguzi kwa sababu hawana Bima ya afya na kutoa pesa kufanya hivyo ni mpaka mtu awe mgonjwa. Hata akiwa mgonjwa wengi wanafanya matibabu ya mazoea ya kwenda kwenye maduka ya dawa mitaani na kununua dawa kwa kufanya hisia mbali mbali za magonjwa yanayowakabili. Matokeo yake wengine wanameza dawa zenye mathara makubwa kwenye miili yao na kupelekea vifo au magonjwa kuwa sugu. Ndugu waandishi wa habari na ndugu watanzania tuache hii tabia ya matibabu holela ni hatari sana kwa afya zetu ni wengi chazo kikubwa ni kukosa bima ya afya. Hivyo tuchangamkie Afyabando ili tuweze kuepuka matibabu holela nay a mazoea.
  1. TUWE NA MTIZAMO CHANYA KWAMBA BIMA YA AFYA NI KINGA KWA WAGONJWA
Ndugu Waandishi wa habari, Bima ya afya ni kimbilio la wagonjwa na ni muhimu sana kila Mtanzania kuwa nayo. Ni jambo la kushangaza kuwa bado kuna Watanzania wengi hawana Bima ya afya. Tafiti za hivi karibuni zinaonyesha zaidi ya watanzania asilimia 73% hawana bima. Hili ni jambo la hatari kwa kuzingatia kuwa gharama za maisha zimepanda sana. Hivyo kuna watanzania wenzetu wengi sana hawana Bima ya afya. Ili tuweze kuokoa maisha yao ni jambo la maana  sana kujenga mtizamo chanya kuhusu bima.  Napenda kupitia kwenu kutoa wito huu kwani kuna watu wengi wanapoteza maisha na kuzidiwa na magonjwa kwa kukosa matibabu sahihi. Wengi wanatumia njia za mkato na za kubabaisha kwa sababu hawana pesa wala bima hivyo kujikuta wanachelewa kupata matibabu hivyo kusababisha ugonjwa kuwa mkubwa na matokeo kupelekea vifo ambavyo vingweza kudhuhirika (Preventive death) . Sasa tunachamgamkie fursa ya Afyabando. Tuamasishane kwa kila mtanzania aweze kupata Bima ya afya.
  1. CHANGAMOTO YA IMANI POTOFU/  TIBA MBADALA
Ndugu Waandishi wa habari kuna napenda kuwaomba watanzania kujua kuwa magonjwa yapo tusitafute njia ya mkato ya kuyakabili kwa kutumia imani zetu na wengine kwenda kwenye tiba mbadala hata kwa magonjwa yanahitaji huduma ya kisayansi.
Sasa niombe watanzania tumie makundi yenu ya kijamii kutafuta bima ya afya kama vile makanisani, vyama vya familia, ukoo, vyama za saccos, vicoba na vikundi vyote hivi vijikite katika kuamasisha umuhimu wa bima. Tuache tabia ya kupenda njia za mkato kwenye tiba mbadala hata kwa magonjwa ambayo siyo ya mchezo mchezo.
UFAHAMU SAHIHI WA NADHARIA YA BIMA KUWA NI RAHISI KULIKO KULIPA KWA PESA TASILIMU.
Ndugu waandishi wa habari matibabu kwa njia ya Bima ya afya ni kwamba mgonjwa anakuwa amechangiwa na watu wengi sana na wengine hawapati maradhi. Lakini mgonjwa anayetumia pesa inabidi atumie pesa nyingi kwa sababu anajigharamia mwenyewe hata waswahili wanasema umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Na jambo hili napenda kusisitiza kwamba kuna magonjwa ambayo gharama zake ni kubwa sana kwa mtu wa kawaida hata mtumishi wa umma au binafsi ni gharama sana kumudu. Mfano kwa sasa kuna watanzania wengi wenye matatizo ya figo wanaenda clinic mara tatu kwa wiki ambapo gharama za siku si chini ya laki tatu au nne. Clinic ya figo yaani Dialysis ni gharama sana kwa mtu binafsi kugharimia na hii ndiyo kazi ya bima duniani kote hivyo nawaomba waandishi wa habari tusaidiane kuwaelimisha watanzania ili tuokoe maisha yao. Mfano mwingine, miaka ya siku hizi magonjwa ya moyo nayo yameongezeka sana hivyo kuna wagonjwa wengi sana. Magonjwa haya pia matibabu yake ni gharama sana kwa mtu wa kawaida kumudu. Sasa changamoto ni kwamba mtu ukiugua inakuwa vigumu sana baadhi ya kampuni za bima kukubali maana wanaona wewe ni mzigo kabla ya kuchangia. Kwa sasabu hizi za kisayansi ni lazima kila mtanzania kuchangimkia bima ya afya.
Tafadhali waandishi tuwaelimishe watanzania wajiunge na bima ya afya kwani gharama za matibabu kwa magonjwa niliyotaja hapo juu ni kubwa mno. Fikiria asilimia 73% ya watanzania hawana bima hivyo lazima wapo wengi wanateseka na wengine wanauza mali zao zote kwa matibabu ambapo wangekuwa na bima wasingeweza kuwa kwenye matatizo. Ndugu zangu wanahabari , nrudiaa tena na tena, watanzania tujiunge na bima ya afya na sasa niwashukuru sana Nordic Foundation Tanzania kwa kuja na kampeni hii ya Afyabando na  kweli, hii ni mkombozi kwa wanyonge na watu wengi wasio na bima ya afya.
HITIMISHO
Napenda kuwashukuru ndugu zangu waandishi wa habari, pia nawashukuru viongozi wa Taasisi ya Nordic Foundation Tanzania na pia nawashukuru sana nyote mliohudhuria shughuli hii ya kuzindua kampeni hii kwa watanzania. Narudia watanzania tuchangamkie bima ya afya na kwa sasa naomba tujiunge na Afyabando kwani nimejulishwa kuwa droo ya kwanza ya bahati nasibu hii ya afayabando ni wiki ijayo jumapili ambapo kadi kumi za bima zitatolewa zenye uwezo wa kuwapatia bima familia ya watu sita, mke na mme na watoto wane. Hivyo nunua ticket yako kwa shilingi 500/= tu ili uweze kupata bima ya mwaka mzima. Kwanza bahati nasibu hii ni ya kijamii siyo biashara ndiyo maana washindi ni wengi sana kwani kwa washindi kumi ni fursa kubwa kwa wengi kupata. Na pia wale ambao hawakupata droo ya kwanza wanaweza kupata droo ya pili au  ya tatu. Hakuna kupoteza kwenye Afyabando kwani husipopata wewe anapata jirani yako au ndugu yako au mtanzania mwenzako.
Asante kwa kunisikiliza
Dkt. Respicius Salvatory
Mtaalam Mwelekezi Afyabando-Nordic Foundation Tanzania

WAFANYAKAZI WA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) WAAGANA NA MADAKTARI BINGWA WA MOYO KUTOKA NCHINI CHINA

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya  Magonjwa ya Moyo ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akimkabidhi zawadi Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka China Sun Long wakati wa hafla fupi ya kuwaaga madaktari hao iliyofanyika hivi karibuni. Serikali ya China kila baada ya miaka miwili inatuma madaktari wake kwa ajili ya kufanya kazi ya Matibabu ya Moyo katika Taasisi hiyo.  
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya  Moyo ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akimkabidhi zawadi Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka China Qu Xianfeng wakati wa hafla fupi ya kuwaaga madaktari hao iliyofanyika hivi karibuni. Serikali ya China kila baada ya miaka miwili inatuma madaktari wake kwa ajili ya kufanya kazi ya Matibabu ya Moyo katika Taasisi hiyo.  
 Madaktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka China wakiwa katika picha ya pamoja na  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya  Moyo ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge mara baada ya kuwakabidhi  zawadi wakati wa hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika hivi karibuni. Serikali ya China kila baada ya miaka miwili inatuma madaktari wake kwa ajili ya kufanya kazi ya Matibabu ya Moyo katika Taasisi hiyo.  
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya  Moyo ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akimkabidhi zawadi Daktari Bingwa wa chumba cha wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU) kutoka China Xie Weifeng  wakati wa hafla fupi ya kuwaaga madaktari hao iliyofanyika hivi karibuni. Serikali ya China kila baada ya miaka miwili inatuma madaktari wake kwa ajili ya kufanya kazi ya Matibabu ya Moyo katika Taasisi hiyo.  
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka China Qu Xianfeng (hayupo pichani) wakati akizungumza katika hafla fupi ya kuwaaga madaktari hao iliyofanyika hivi karibuni. Serikali ya China kila baada ya miaka miwili inatuma madaktari wake kwa ajili ya kufanya kazi ya Matibabu ya Moyo katika Taasisi hiyo.  

Picha na JKCI

SPIKA NDUGAI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI LEO MJINI DODOMA.

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati)akiongoza kikao cha kamati ya uongozi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma, ikiwa ni Maandalizi kabla ya kuanza Mkutano wa 8 wa Bunge la 11 unaoendelea kesho tarehe 5 Septemba, 2017 Mjini Dodoma.
 Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati ya uongozi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma, ikiwa ni Maandalizi kabla ya kuanza Mkutano wa 8 wa Bunge la 11 unaoendelea kesho tarehe 5 Septemba, 2017 Mjini Dodoma. kushoto ni Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas kashililah.
Wajumbe wa kamati ya uongozi wakiwa katika kikao cha pamoja kilichoongozwa  na Spika wa Bunge katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma, ikiwa ni Maandalizi kabla ya kuanza Mkutano wa 8 wa Bunge la 11 unaoendelea kesho tarehe 5 Septemba, 2017 Mjini Dodoma.  kulia ni Mhe. Andrew Chenge, Mhe. Stanslaus Nyongo (katikati) na Mhe. Christine Ishengoma (kushoto).

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

BASATA yatoa cheti cha utambuzi kwa Tasnia ya Injili nchini

$
0
0
Na Agness Francis , Globu ya Jamii.
Mtandao wa wasanii wote  wa tasnia ya injili  na maadili ya Utaifa, Tanzania Gospel  Artists Nertwork (TAGOANE) wamekabidhiwa  cheti kilicho sajiriwa  kisheria  kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia chombo chenye dhamana BASATA  na kupewa namba ya usajiri  BST/00020 kwa mujibu wa sheria Na.23 ya mwaka 1984.
Zoezi hilo limeongozwa na  Katibu Mtendaji BASATA, Godfrey Mngereza  ambaye ndiye amekabidhi  cheti hicho leo  katika ofisi zake zilizoko BASATA  Ilala Sharif Shamba  Jijijni Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji BASATA, Godfrey Mngereza amesema kuwa maadili mema  huleta amani kwa wananchi na amewapongeza  wasanii hao kwa hatua waaliofikia  hadi sasa kwa kutembelea mikoa tofauti tofauti nchini  kwa lengo la kuwaunganisha na fursa mbalimbali ulimwenguni  katika kukuza huduma na kukua kiuchumi .
 Hata hivyo Rais wa TAGOANE , Godwine  Maimu Nnyaka ametanabaisha kuwa watashirikiana na Seriakali  katika kukuza pato la taifa kwa kudhibiti wauzaji haramu, wanyonyaji  na matapeli wa kazi za wasanii  kwa kuchukuliwa hatua za kisheria  kwa dhumuni la kuongezea kipato Taifa na kwa wasanii pia.
Nae Katibu mkuu TAGOANE,  Mchungaji Lucy Wilson ametoa wito kwa wakidada na wakinakaka wajitokeze kwa wingi  kujiunga na  mtandao huo  wa wasanii wote wa tasnia ya injili na maadili ya utaifa na waichukulie sanaa ya injili kama kazi zingine.
Rais wa TAGOANE , Godwine  Maimu Nnyaka akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu kuwaunganisha wasanii wote wa Tasnia ya Injili ili kuwa na sauti moja na lugha moja ili kufikia malengo yao kiroho na kimwili leo walipokuwa wakikabidhiwa cheti na BASATA cha kutambua umuhimu wa wasanii wa sanaa ya tasnia ya Injili.
  Katibu Mtendaji BASATA, Godfrey Mngereza  akimkabidhi  cheti cha kutambua umuhimu wa wasanii wa sanaa ya tasnia ya Injili kwa Rais wa TAGOANE , Godwine  Maimu Nnyaka leo jkatika ofisi za BASATA jijini Dar.
 Katibu Mtendaji BASATA, Godfrey Mngereza akiwapongeza Viongozi wa wasanii wote wa Tasnia ya Injili kwa hatua waliofikia kwa kutembelea baadhi ya mikoa mbalimbali hapa nchini  kwa lengo la kuwaunganisha na fursa mbalimbali ulimwenguni  katika kukuza huduma na kukua kiuchumi 
Baadhi ya viongozi wa wasanii wote wa Tasnia ya Injili pamoja na wasaii wakiwa kwenye picha ya pamoja.

NEEMA YA UPIMAJI AFYA BURE KUTOLEWA KWA WANA DAR ES SALAAM

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda anawatangazia Wananchi wote wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi kwenye Kampeni ya Upimaji wa Afya Bure kuanzia siku ya Jumatano ya Septembe 06 -10 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Zoezi hilo litaendeshwa na Madaktari bingwa na Wauguzi zaidi ya 200 kutoka Hospital za Umma, Jeshi na za Watu Binafsi zilizomuunga mkono RC Makonda.

Makonda amesema kuwa hatopenda kuona Mwananchi anapoteza maisha kwa kukosa huduma ya Afya ndio maana ameamua kuendesha zoezi la upimaji wa Afya Bure ili Wananchi wapate fursa ya kujua Afya zao na kuwa na utaratibu wa kupima Afya zao mara kwa mara.

Aidha amezipongeza Hospital na zilizomuumga mkono ikiwemo Muhimbili, Ocean Road, Amana, Temeke, Mwananyamala, Muhimbili, TMJ, Sanitas, Agha Khan, Regency, Kairuki, TANCDA, IMMI Life, APHTA, CCP Medicine, MDA, NHIF, Wandile wa kaya, P Consult, Besta Diagnestics, Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete, Jamii Bora na Damu salama.

Makonda amesema watakaopimwa na kubainika kuwa na matatizo ya kiafya watapelekwa Hospital na kupatiwa matibabu Bure.

Hata hivyo amesema kuwa kutakuwepo na vifaa tiba vya kisasa, Magari ya kubeba Wagonjwa, Vyoo, Sehemu za watoa huduma na Sehemu za kupumzika wakati wa kusubiri huduma.

WANANCHI WA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA WAHIMIZWA KUJIUNGA NA JUMUIYA YAO.

$
0
0
Na Miza Kona, MAELEZO .

MAKAMU wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, ameitaka Jumuiya ya Maendeleo ya Mkoa wa Kaskazini Unguja kuzidisha mshikamano  ili kuweza kubadilika kielimu na kuleta maendeleo mazuri mkoani humo.

Balozi Seif ameyasema hayo katika ukumbi wa  zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni mjini Zanzibar katika mkutano wa Jumuiya hiyo.
Alisema vijana wengi wa mkoa huo wanakosa kuingia katika ushindani wa soko la ajira kutokana na kukosa sifa zinazohitajika.

Balozi Seif alisema jumuiya inaweza kuleta mafanikio makubwa  kwa kushirikana  pamoja na kuzidisha mshikamano katika dhamira ya kuibadilisha jamii ya mkoa huo kielimu.Alifahamisha kuwa elimu ndio silaha pekee inayoweza kuwakomboa vijana na kuwawezesha kukubalika katika ajira mbalimbali na hivyo kuondokana na umasikini.

“Ni wakati sasa wa kubadilika kwa kuwekeza katika elimu ya watoto wetu ili kuwainua vijana na kuwawezesha kuhimili ushindani kwa kuwa na sifa zitakazoweza kuajiriwa au kujiajiri,” alifahamisha Balozi Seif.
Alieleza vijana wengi wa mkoa huo hawana mwamko wa kusoma, jambo linachangia mkoa wa Kaskazini kuwa nyuma kielimu na kimaendeleo ikilinganishwa na mikoa mingine nchini.

Amehimiza kuwepo ushirikiano wa pamoja baina ya viongozi na wana jumuiya katika kuishajiisha jamii ili iweze kubadilika kiuchumi na kuacha kuingiza itikadi za siasa katika suala la kuleta maendeleo.
Balozi Seif alisema jumuiya ina nia ya kuimarisha umoja na kuleta maendeleo katika mkoa huo.

Aidha Makamu wa Pili  wa Rais amewasisitiza viongozi wa majimbo na serikali katika mkoa huo kudumisha ushirikiano na kuwasaidia vijana wasio na uwezo wa kujikimu kwa kuwapa msukumo wa kimaendeleo pamoja na kuishajiisha jamii kujiunga jumuiya hiyo.

Jumuiya Maendeleo ya Mkoa wa Kaskazini Unguja (NUDO), imeasisiwa mwezi Aprili 2016, na sasa ina zaidi ya wanachama zaidi ya 1000.
Lengo la kuanzishwa kwake ni kuendeleza, kuwezesha na kuijengea uwezo jamii ya mkoa huo katika kuinua ustawi wake kiuchumi, kijamii na mazingira.
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi akifungua mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Mkoa Kaskazini Unguja katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni.
 Mjumbe wa Kamati ya Uongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Mkoa Kaskazini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud akieleza mafanikio ya Jumuiya tokea ilipoasisiwa mwaka jana katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Mkoa Kaskazini Unguja Ali Juma Ali akiwaeleza wananchama wa Jumuiya hiyo mikakati na mipango ya kuiendeleza ili kufikia malengo yake katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni.
aadhi ya wajumbe wa mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Mkoa Kaskazini Unguja wakifuatilia mkutano huo uliofanyika Baraza l a Wawakilishi la zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Mkoa Kaskazini Unguja Ali Juma Ali akiagana na Makamu wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi baada ya mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika Ukumbi wa Baraza la wawakilishi la zamani Kikwajuni.Picha na Makame Mshenga.

MKUTANO WA NANE WA BUNGE KUANZA KESHO MJINI DODOMA

WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA UGAWAJI WA VITAMBULISHO VYA TIBA KWA WAZEE MANISPAA YA UBUNGO

$
0
0

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 amezindua Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika Viwanja vya TP Sinza E Waziri Ummy alipongeza uongozi wa Wilaya ya Ubungo kwa kutambua umuhimu wa kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya serikali ya kuwatambua Wazee katika Halmashauri na kuwapatia vitambulisho vitakavyo wawezesha kupata Huduma za matibabu bila vikwao.

Alisema kuwa Wazee ni asilimia 5.6 ya wananchi wote wa Tanzania idadi ambayo kwa kiasi kikubwa inaleta msukumo wa nchi kuweka mifumo madhubuti ya kuhudumia Wazee ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa Huduma katika matibabu.

Alisema kuwa Jambo hilo ni kuzingatia ukweli kwamba Wazee wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazosababishwa na umri mkubwa na mtazamo wa Jamii ambao umekuwa ukichangia ukiukwaji wa haki na maslahi ya Wazee katika ngazi mbalimbali.

Alisema Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeingia kwenye rekodi kwa kuwatambua Wazee wasio na uwezo kwani watapatiwa vitambulisho vitakavyo wawezesha kupata Huduma za matibabu Bure.

Mhe Ummy alisema kuwa Halmashauri zingine kote nchini zinapaswa kuanzisha haraka zoezi la kuwathamini Wazee kwa kuwapatia Huduma Bora za afya kabla ya kutoa Huduma za matibabu kwa Wazee kote nchini kwa kuanzisha dirisha maalumu na wataalamu wa kuwahudumia Wazee.

Alitoa Rai kwa watoa Huduma wa Afya kuviheshimu vitambulisho wakati wote Wazee wanapoenda navyo kupatiwa matibabu huku akiwasihi Wazee kutumia vitambulisho hivyo kwa kuzingatia maelekezo sio kwa kuwapa watu wengine wasiohusika navyo.

Aidha waziri Ummy ameahidi bima ya afya kwa watoto 100 wenye umri chini ya miaka 18 wanaoishi kwenye mazingira magumu wilaya ya Ubungo na uandikishwaji utaanza leo pia ameahidi kujenga wodi ya wazazi, watoto na maabara ya damu kwenye kituo kimoja cha afya wilaya ya ubungo mara baada ya kusikia hotuba ya kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Ubungo.

Muheshimiwa waziri ameiomba jamii kujiunga na bima za afya za gharama nafuu ili kupunguza mzigo kwa halmashauri na kulinda afya za wananchi.Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori alisema kuwa lengo la uzinduzi huo wa ugawaji wa vitambulisho ni kuonesha umma kuwa Wilaya ya Ubungo inawajali Wazee ikiwa ni Sehemu ya utekelezaji wa ilani ya ushindi ya Chama Cha Mapinduzi katika kipindi Cha mwaka 2015-2020, sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 na sera ya Afya ya Mwaka 2007.

Mhe Makori alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha Wazee wote nchini wanapata Huduma Bora za afya bila vikwao hivyo Wilaya ya Ubungo imeanza na utoaji vitambulisho kea Wazee 7296 waliojiandikisha na zoezi hilo litakuwa endelevu.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza na mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com mara baada ya uzinduzi wa ugawaji wa vitambulisho vya Tiba kwa Wazee alisema kuwa Manispaa ya Ubungo imetekeleza agizo la serikali lililotolewa na Waziri Mkuu kwenye maadhimisho ya siku ya Wazee Octoba 1, 2009 kuwa Hospitali zote na Vituo vya Afya vya Umma kutenga dirisha na watumishi maalumu wa Afya kwa ajili ya kutoa Huduma za matibabu bure kwa Wazee.

Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa Manispaa ya Ubungo ina jumla ya Vituo 19 vya kutolea Huduma za afya ikiwa ni pamoja na Hospitali moja, Vituo vya afya vitatu, Zahanati 15, na Kliniki Moja ya Mama na Mtoto hivyo Vituo hivyo vyote vitaanza kutoa Huduma za matibabu kwa Wazee wasio na uwezo bila malipo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu akizungumza wakati wa uzindua wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu (Wa Tatu Kushoto) akionyesha vitambulisho vya Wazee akiwa na viongozi wengine wa Chama na serikali Wilaya ya Ubungo wakati wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisalimiana na baadhi ya Wazee walioshiriki uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
 Kaimu Mganga Mkuu Wilaya ya Ubungo Bi Maria Maliwa akisoma taarifa ya huduma za afya, Ustawi wa jamii na Msamaha kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo katika uzinduzi wa vitambulisho vya msamaha kwa wazee wa Manispaa ya Ubungo. 
 Zoezi la Uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu akimpatia Mzee Ferooz Kafuru kitambulisho Cha matibabu wakati wa uzindua wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wazee wa Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo wakishuhudia zoezi la Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee. Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo Ndg Salum A. Kalli akitoa salamu za CCM wakati wa uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.Kalli amepongeza uongozi wa serikali Wilaya ya Ubungo kwa kutekeleza ilani ya CCM ya ushindi yenye mkataba na wananchi kwa kipindi cha miaka mitano 2015-2020 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu akiteta Jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo mara baada ya kuzindua Huduma ya Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Walaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisalimiana na Wazee waliofika kushuhudia zoezi la uzinduzi wa vitambulisho kwa Wazee wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo lilifanywa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu akimpatia Bi Theresia Mbimbo kitambulisho Cha matibabu wakati wa uzindua wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wazee wa Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo wakishuhudia zoezi la Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee. Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 .
Baadhi ya Wazee wa Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo wakishuhudia zoezi la Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee. Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 
Baadhi ya Wazee wa Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo wakishuhudia zoezi la Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee. Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 
Madiwani wa Manispaa wakishuhudia zoezi la Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee. Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, M

RATIBA YA MAZISHI YA MAREHEMU MUHINGO RWEYAMAMU.

$
0
0

Leo Jumanne,Septemba 5,2017

Asubuhi Saa 2:00 -300: Chai nyumbani kwa Marehemu, Mbezi Msigani.

Asubuhi Saa 3:00- 5:00:Ibaada Kanisa la KKT Mbezi Luisi,lilipo Kibanda cha Mkaa,Mbezi.

Saa 5:00-6:00:Msafara kwenda Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Mchana Saa 6:00-8:00: Hafla ya kuaga mwili Mnazi Mmoja

Mchana Saa 8:00-8:20:Kuelekea Kinondoni Makaburini

Mchana Saa 8:20-9:00:Maziko Kinondoni Makaburini.

Jioni Saa 9:00-10:00:Kurejea nyumbani kwa Marehemu Mbezi Msigani

Kwa Mawasiliano zaidi:

Stella Nyemenohi 0758295529
Joyce Mmasi 0714233929
 Sanduku lenye mwili wa Marehemu Muhingo Rweyamamu,nyumbani kwake tayari kwa ratiba ya kuagwa mapema leo katika viwanja vya Mnazi mmoja na baadae maziko yake kufanyika katika makaburi ya Kinondoni,jijini Dar Es Salaam
Pichani kulia Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Mh.Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na ndugu wa marehemu jana usiku nyumbani kwa marehemu Muhingo kwa ajili ya kufariji wafiwa.
  Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Mh.Dkt Harrison Mwakyembe akisaini kitabu cha maombolozo jana usiku nyumbani kwa marehemu Muhingo.

WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE WAHITIMU MAFUNZO YA JKT

$
0
0
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa wamejipanga kusubiri sherehe za mahafali ya kumaliza mafunzo ya JKT kuanza. Mafunzo hayo yalifanyika Kambi ya JKT ya Oljoro mkoani Arusha kwa kipindi cha wiki sita kuanzia tarehe 24 Julai hadi 04 Septemba 2017. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima ambaye alikuwa Mgeni Rasmi wa mahafali hayo akiwa katika jukwaa kwa ajili ya kupokea heshima kutoka kikosi cha Vijana cha Operesheni Viwanda (hakipo pichani) ambacho kimejumuisha watumishi 30 wa Wizara ya Mambo ya Nje. 
Mgeni Rasmi, Balozi Mlima akikagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa heshima yake na kikosi kilichohitimu mafunzo ya JKT ambacho kilijumuisha watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje
Mgeni Rasmi, Balozi Aziz Mlima wakiwa wamesimama pamoja na Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (kulia) na Kamanda wa Kambi ya Oljoro kwa ajili kuangalia vikosi vikipita mbele yao katika mwendo wa pole na kasi
Kikosi kikipita mbele ya Mgeni Rasmi kwa mwendo wa pole 
Kikosi kikipita mbele ya Mgeni Rasmi kwa mwendo wa kasi 
Mgeni Rasmi akikabidhi zawadi kwa waliofanya vizuri zaidi. 
Bi. Khadija Othman akipokea zawadi yake 
Bw. Graison Ishengoma akipokea zawadi yake kutoka kwa Mgeni Rasmi 
Bw. Edward Komba akipokea zawadi yake. 
AWahitimu wa mafunzo ya JKT kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakila kiapo cha utii 
Risala kwa Mgeni Rasmi. katika risala hiyo waliahidi kuyafanyia kazi mafunzo yote waliyoyapata watakaporejea katika kituo chao cha kazi. Walijifunza uzalendo, utii, ustahamilivu, ukakamavu na mengine mengi. 
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje ambao nao washapitia mafunzo hayo katika awamu ya kwanza wakiwashuhudia wenzao wakihitimu mafunzo ya JKT katika awamu ya pili. 
Burdani ilikuwepo siku ya mahafali. Hapo bendi ya Jeshi ikitumbwiza. 
Onesho la Makamandoo hapo mmoja wao amebeba ndoo za maji kwa kutumia meno yake. 
Mkuu wa Kambi ya Oljoro akiongea machache kabla ya kumkaribisha Mwakilishi wa Mkuu wa JKT ili amkaribishe Mgeni Rasmi 
Mwakilishi wa Mkuu wa JKT akimkaribisha Mgeni Rasmi atoe hotuba ya kufunga mafunzo hayo. Kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi alisisitiza umuhimu wa taasisi nyingine za umma kuiga Wizara ya Mambo ya Nje kwa kupeleka watumishi wao ili kupata mafunzo ya JKT ambayo ni muhimu kwa kujenga uzalendo, nidhamu na umoja. 
Mgeni Rasmi akisoma hotuba yake. Alitoa ushuhuda kuwa watumishi walioshiriki mafunzo hayo katika awamu ya kwanza wameonesha umahiri mkubwa katika kutekeleza majukumu yao na ndio sababu amepeleka kundi lingine katika awamu ya pili. Aliahidi atawapeleka watumishi wa Wizara yake wenye sifa ikiwemo ya umri (chini ya miaka 40) hatua kwa hatua hadi watakapomalizika. 
Wahitimu wa mafunzo ya JKT wakisikiliza hotuba ya Mgeni Rasmi
Baadhi ya wageni waliohudhuria mahafali hayo. Hapo afande anateta na Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Bw. Othman Rashid.
Mkurugenzi wa Utawala katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Nigel Msangi akimpongeza Bw. Wambura kwa kuhitimu mafunzo ya JKT. 
Tumemaliza salama, shukran kwa Wizara kwa kutuandalia mafunzo haya yenye tija kubwa kwetu. 

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala; Bi. Ngusekela Nyerere na Mwalimu wa somo la Uzalendo ambaye alikuwa Msadizi wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.
Furaha tumemaliza mafunzo, Kutoka kushoto ni Felista Rugambwa, Teodos Komba na Rose Mbilinyi. 
Wakiwa katika pose baada ya kumaliza mafunzo. 
Wanaimba nyimbo za jeshi. 
Picha ya pamoja kati ya Mgeni Rasmi na wahitimu wa JKT.

Muda wa Maongezi, SMS na Data za Bure kwa Wanunuzi wa Tiketi za ‘Tigo Fiesta 2017 - Tumekusomaa’

$
0
0

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Masoko Tigo, William Mpinga(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jana wakati wa kutangaza ofa maalum za vifurushi zitazotolewa ununuapo tiketi ya tamasha la Tigo Fiesta kwa njia ya Tigo pesa. Pembeni ni Afisa Biashara wa Tigo, Edwin Mgoa

Tigo inatoa dakika 100 za muda wa maongezi, SMS  100 SMS na and 100 Mbs za data kwa manunuzi yote ya tiketi kupitia TigoPesa


Dar es Salaam, Jumatatu 4 Septemba, 2017- Huku ikiwa imebakia siku chache tu kabla ya onesho la kwanza la msimu wa Tigo Fiesta 2017 – Tumekusomaa kufanyika jijini Arusha, wadhamini wakuu kampuni ya Tigo inazidi kutoa ofa kabambe kwa wateja wote wa Tigo watakaonunua tiketi zao za awali kupitia huduma ya TigoPesa.

Tigo inatoa dakika 100 za bure, SMS 100 za bure, na  kifurushi cha 100Mbs cha data bure kwa wateja wote wa Tigo watakaonunua tiketi zaoTigo Fiesta 2017 - Tumekusomaa kupitia huduma ya TigoPesa.

Akitangaza ofa hiyo murwa jijini Dar es Salaam jana, Mkuu Mtendaji wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga alisema kuwa ofa hii mpya ya dakika 100 za muda wa maongezi, SMS 100 na 100Mbs za  data inaenda sambamba na ofa iliyopo sasa ya punguzo ya bei asilimia 10% kwa tiketi zote za awali za Tigo Fiesta 2017 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa au huduma ya kuhamisha fedha ya mitandao mingine yote ya simu nchini.

‘Kama tulivyoahidi hapo awali, tuna furaha kuthibitisha kuwa wateja wote wa Tigo watakaonunua tiketi zao za ‘Tigo Fiesta 2017 Tumekusomaa’ kupitia Tigo Pesa, moja kwa moja watapata bonasi ya dakika 100 za muda wa maongezi, SMS 100 na 100 Mbs za data bure kutoka Tigo. Hii ni pamoja na ofa nono ya punguzo la 10% wanayopata wateja wote wa simu za mkononi wanaonunua tiketi zao za Tigo Fiesta 2017 kwa njia ya huduma ya kuhamisha fedha kwa njia ya mtandao wa simu.’

Aliongeza kuwa ofa hii inaendana na sifa kuu ya Tigo kuwa mtandao unaowaelewa na kuwajali zaidi wateja wake nchini.

Ili kununua tiketi za Tigo Fiesta 2017 kwa njia ya mtandao na kupata ofa hizi kabambe, mteja anahitaji kufuata hatua za kawaida za kutuma fedha na kutuma TZS 9,000/- kwenda namba 0678 888 888. Hapo mnunuzi atapokea ujumbe mfupi wa maneno (SMS) utakathibitisha kuhusu manunuzi yake ya tiketi pamoja na ofa za dakika 100 muda wa maongezi, SMS 100 na 100Mbs za data kutoka Tigo. 
‘Napenda kuwaambia wateja wa Tigo wakae mkao wa kufaidika katika msimu huu wa Tigo Fiesta 2017 kwa sababu kuna ofa nyingi za kusisimua ambazo tutazitanganza katika siku zijazo,’ Mpinga alisema.


Mwaka huu msimu wa Tigo Fiesta 2017 – Tumekusomaa utajumuisha mikoa ya Arusha Kahama, Musoma, Mwanza, Tabora na Dodoma. Tigo Fiesta 2017 – Tumekusomaa pia itatua katika mikoa ya Iringa, Songea, Njombe, Sumbawanga, Morogoro, Tanga, Moshi na Mtwara, kabla ya kuhitimishwa jijini Dar es Salaam.

TUVAE MAVAZI YENYE STAHA TUNAPOFUATA HUDUMA MBALIMBALI KATIKA OFISI ZA UMMA

$
0
0
Mmoja kati ya watangazaji wa Kipindi cha “LEO TENA” kinachotangazwa na kituo cha redio cha Clouds FM, Bw. Musa Hussein (aliyesimama) akiwa katika mjadala na Afisa Utumishi Mwandamizi kutoka Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bi. Leila Mavika (kushoto).
Afisa Utumishi Mwandamizi kutoka Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bi. Leila Mavika (kushoto) akishiriki mjadala kuhusu masuala ya maadili, hususan mavazi kwa watumishi wa umma na wateja wanaofuata huduma katika taasisi za umma katika kipindi cha LEO TENA kinachotangazwa na kituo cha redio cha Clouds FM.
Afisa Utumishi Mwandamizi kutoka Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bi. Leila Mavika (kushoto) akifafanua kuhusu muonekano na aina ya mavazi yanayopaswa kuvaliwa na watumishi wa umma na wateja wanaofuata huduma katika taasisi za umma katika kipindi cha LEO TENA kinachotangazwa kituo cha redio cha Clouds FM.

ZANTEL YATOA ZAWADI YA MBUZI KATIKA KUSHEHEREKEA SIKUKUU YA 'EID AL HADHA',YAWAKUMBUKA YATIMA NA WAZEE

$
0
0

Mwakilishi wa Zantel-Tanga Mansoor Ally, (kulia) akikabidhi mbuzi kwa kituo cha kulea watoto yatima cha Goodwill & Humanity Foundation kilichopo jijini Tanga wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika kituo hicho, siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita ikiwa ni moja ya hatua ya kujitolea kwa jamii kwa Kampuni hiyo. Zaidi ya mbuzi 100 walitolewa katika mikoa mbalimbali ya bara na visiwani katika kuadhimisha sikukuu ya Eid Al Adha.
Meneja wa Data na Vifaa vya Intaneti, Hamza Zuheri (kushoto) akikabidhi mbuzi kwa mwakilishi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Malaika kilichopo Kinondoni Malongwe jijini Dar, wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika makao makuu ya ofisi za Zantel jijini Dar es salaam, siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita ikiwa ni moja ya hatua ya kujitolea kwa jamii kwa Kampuni hiyo. Zaidi ya mbuzi 100 walitolewa katika mikoa mbalimbali ya bara na visiwani katika kuadhimisha sikukuu ya Eid Al Adha.
Afisa wa Zantel Abdallah Saadun (kushoto) akikabidhi mbuzi kwa Afisa rasilimali watu wa kituo cha kulea watoto yatima cha SOS-Zanzibar, Bw. Salum Abdallah Salum (wa pili kushoto) wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi kuu ya Zantel iliyopo Unguja, siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita ikiwa ni moja ya hatua ya kujitolea kwa jamii kwa Kampuni hiyo ambapo zaidi ya mbuzi 100 walitolewa katika mikoa mbalimbali ya bara na visiwani katika kuadhimisha sikukuu ya Eid Al Adha.
Meneja wa Data na Vifaa vya Intaneti, Hamza Zuheri (kushoto) akikabidhi mbuzi wawili kwa mwakilishi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Buguruni Swafaa, Zimbwe Hatibu Koja wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika makao makuu ya ofisi za Zantel jijini Dar es salaam, siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita hii ikiwa ni moja ya hatua ya kujitolea kwa jamii kwa Kampuni hiyo ambapo zaidi ya mbuzi 100 walitolewa katika mikoa mbalimbali ya bara na visiwani katika kuadhimisha sikukuu ya Eid Al Adha. Wengine kwenye picha ni maafisa wa Zantel Emmiliana Vakolawene(kushoto) na Winnes Baldwin Lyaro (wa pili kushoto).
Afisa wa Zantel Abdallah Saadun akikabidhi mbuzi kwa walezi na watoto wa kituo cha kulea watoto yatima cha Mazizini-Zanzibar wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi kuu ya Zantel iliyopo Unguja, siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita ikiwa ni moja ya hatua ya kujitolea kwa jamii kwa Kampuni hiyo ambapo zaidi ya mbuzi 100 walitolewa katika mikoa mbalimbali ya bara na visiwani katika kuadhimisha sikukuu ya Eid Al Adha. Anayeshuhudia kushoto ni Meneja Chapa na Mawasiiano wa Zantel, Rukia Mtingwa.
Afisa Masoko wa Zantel, Deus Mtena (wa pili kushoto) akikabidhi mbuzi kwa Katibu wa kituo cha kulea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo Bunju, Bw. Omari Abdu (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika makao makuu ya ofisi za Zantel jijini Dar es salaam, siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita hii ikiwa ni moja ya hatua ya kujitolea kwa jamii kwa Kampuni hiyo ambapo zaidi ya mbuzi 100 walitolewa katika mikoa mbalimbali ya bara na visiwani katika kuadhimisha sikukuu ya Eid Al Adha. Wengine katika picha ni Afisa Mawasiliano wa Zantel Winnes Baldwin Lyaro (Kushoto) na Mweka Hazina wa kituo cha Mwandaliwa Haji Mahmood Bakhulla.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA HIFADHI YA MAZINGIRA ASILIA ULUGURU NA JUMUIYA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI YA WAMI MBIKI MKOANI MOROGORO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakati wa ziara yao ya kikazi katika eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Wami Mbiki/Ushoroba mkoani Morogoro ambayo iliyolenga kubaini changamoto mbalimbali za uhifadhi kwa ajili ya kuishauri Serikali namna bora ya kukabiliana nazo.
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakimsikiliza Afisa Wanyamapori Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Leonard Mayeta (wa nne kulia) wakati akitoa maelezo kuhusu Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Wami Mbiki/Ushoroba wakati wa ziara ya kamati hiyo kwenye hifadhi hiyo ambayo ililenga kubaini changamoto mbalimbali za uhifadhi kwa ajili ya kuishauri Serikali namna bora ya kukabiliana nazo.
Kaimu Mkurugenzi wa Biashara na Utalii wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Imani Nkuwi akiwasilisha taarifa ya mamlaka hiyo kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Dkt. James Wakibara mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii baada ya kutembelea eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Wami Mbiki mkoani Morogoro. 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (wa tatu kulia) wakiongoza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kupanda mlima katika Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru mkoani Morogoro wakati wa ziara yao iliyolenga kubaini changamoto mbalimbali za uhifadhi kwa ajili ya kuishauri Serikali namna bora ya kukabiliana nazo. 
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kulia) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakati wa ziara yao ya kikazi katika Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru mkoani. 
 Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru, Cathbert Mafupa (kushoto) akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Kamati hiyo kuhusu Hifadhi hiyo. 
 Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mary Chatanda (wa tatu kushoto) akizungumza kutaka ufafanuzi wa baadhi ya mambo kuhusu Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru wakati wa ziara ya kamati kwenye hifadhi hiyo. Wengine pichani ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kulia), Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Ndetiye (wa nne kulia) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu, Prof. Dos Santos Silayo (wa pili kulia). 
 Wajumbe wa Kamati wakikagua eneo la Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru mkoani Morogoro wakati wa ziara yao ya kikazi ya kuangalia changamoto mbalimbali za uhifadhi zinazoikabili hifadhi hiyo kwa ajili ya kuishauri Serikali namna bora ya kukabiliana nazo. 
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kulia) akiongoza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kutembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru. 
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) na Wajumbe wa Kamati hiyo wakitembelea eneo la Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru. 
 Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mtango Mtahiko (kulia) ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo kwenye ziara hiyo.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kushoto) akiwasilisha taarifa ya taasisi hiyo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii baada ya kutembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru mkoani Morogoro jana wakati wa ziara ya kamati hiyo iliyolenda kubaini changamoto mbalimbali za uhifadhi katika hifadhi hiyo kwa ajili ya kuishauri Serikali namna bora ya kukabiliana nazo. 
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kushoto) akiwasilisha taarifa ya taasisi hiyo mbele ya Kamati.
PICHA ZOTE NA HAMZA TEMBA-WIZARA YA MALIASILI

BANDARI TANGA YAZIDI KUCHANUA KILIMANJARO CUP YAITANDIKA SCOPION YA ARUSHA VIKAPU 91-60

$
0
0
 Kikosi cha timu ya Bandari Tanga ambacho kinaendelea kung'ara kwa kuibuka na ushindi wa vikapu 91 kwa 60 kwenye mchezo uliochezwa kwenye viwanja vya KCMC Mjini Moshi       
 kikosi cha timu ya Scopion ya Arusha  kabla ya kuanza mchezo wao na Bandari Tanga ambapo Bandari Tanga iliendelea kung'ara kwa kuibuka na ushindi wa vikapu 91 kwa 60 kwenye mchezo uliochezwa kwenye viwanja vya KCMC Mjini Moshi
Wachezaji wa timu ya Bandari Tanga wakisalimiana na wa timu ya Scopion ya Arusha ambapo Bandari Tanga iliendelea kung'ara kwa kuibuka na ushindi wa vikapu 91 kwa 60 kwenye mchezo uliochezwa kwenye viwanja vya KCMC Mjini Moshi
Wachezaji wa timu ya Bandari Tanga wakisaliana na wa timu ya Scopion ya Arusha kabla ya kuanza mechi yao na michuano ya Kilimanjaro Cup ambapo Bandari Tanga iliendelea kung'ara kwa kuibuka na ushindi wa vikapu 91 kwa 60 kwenye mchezo uliochezwa kwenye viwanja vya KCMC Mjini Moshi
Wachezaji wa timu ya Bandari Tanga wakichuano na timu ya Scopion ya Arusha ambapo Bandari Tanga iliendelea kung'ara kwa kuibuka na ushindi wa vikapu 91 kwa 60 kwenye mashindano ya Kilimanjaro Cup yanayoendelea kwenye viwanja vya KCMC Mjini Moshi

 Wachezaji wa timu ya Bandari Tanga wakichuana na timu ya Scopion ya Arusha ambapo Bandari Tanga iliendelea kung'ara kwa kuibuka na ushindi wa vikapu 91 kwa 60 kwenye mchezo uliochezwa kwenye viwanja vya KCMC Mjini Moshi

 Wachezaji wa timu ya Bandari Tanga wakipewa mawaidha na Kocha Mkuu wa timu hiyo,Mohamed Fazal wakati wa mapumziko katika mchezo wa michuano ya kikapu ya Kilimanjaro Cup ambapo Bandari Tanga illibuka na ushindi wa vikapu 91 kwa 60 ambapo leo Bandari watawavaa timu ya Mtwara kushoto ni
 Benchi la timu ya Bandari wakiwa kwenye umakini mkubwa
Timu ya Scopion ya Arusha Wachezaji wa timu ya Bandari Tanga wakiwa kwenye benchi lao wakifuatilia kwa umakini mchezo baina yao na  timu ya Scopion ya Arusha ambapo Bandari Tanga iliendelea kung'ara kwa kuibuka na ushindi wa vikapu 91 kwa 60 kwenye mchezo uliochezwa kwenye viwanja vya KCMC Mjini Moshi
Mchezaji wa timu ya Bandari Tanga akihojiwa mara baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa vikapu 91-60 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa KCMC mjini Moshi . Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

SERIKALI YA AWAMU YA TANO YA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFURI IMERUDISHA IMANI KWA WANANCHI

$
0
0
Na David John Mwanza

 KADA wa   Chama cha Mapinduzi na Mwenyekiti Mstaafu wa Serikali  ya Mtaa wa kiloleli B Jijini Mwanza Joshua Mnana amesema kazi nzuri inayofanywa na Serikali inasababisha kukimarisha Chama  cha Mapinduzi CCM.

Mwenyekiti huyo mstaafu alisema kwamba hivi Sasa Makada na wanachama wa CCM wanatembea kwa kujidai na hiyo nikutokana na serikali iliyopo madarakani inafanya  vizuri ukilinganisha na huko nyuma.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini hapa Mnana alisema hata kuhairishwa kwa baadhi ya Chaguzi ambazo zinaendelea kufanyika ndani ya Chama hicho niwazi kwamba hivi watu wanakipenda chama hivyo yeye haoni Kama kasoro.

 "Unajuwa ndugu waandishi zamani kulikuwa hakuna hiyo hali nasababu ilikuwa wanachama walikuwa wanashindwa kuchukua hata fomu ya kugombea kutokana na chama kilivyokuwa."alisema Mnana

  Aliongeza kuwa kuingia madarakani kwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt.John Magufuli kumefanya watu kukubali kazi zinazofanyika na kurudisha imani kubwa kwa Chama cha Mapinduzi.

Aidha akizungumzia mtaa wake wa kiloleli alisema kihalisia eneo hilo ni la milima lakini chini ya uongozi wa Rais Magufuli hivi wamepata barabara ya kiwango cha lami ambayo pia zimewekwa na taa nakufanya eneo hilo kuwa tofauti na mitaa mingine mkoani Mwanza.

  Pia Mnana aliomba viongozi wa eneo hilo ambao wapo madarakani hivi sasa kufanya utaratibu ili barabara izinduliwe na Rais Dkt Magufuli huku akiipongeza Kampuni ya Nyanza Road kwa kazi nzuri ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha juu.

  "Binafsi nitaendelea kuwa Mwanachama mwadilifu wa Chama cha Mapinduzi ccm na naunga mkono kwa asilimia mia moja kazi nzuri inayofanywa na rais Magufuli. "alisema Mnana
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images