Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1358 | 1359 | (Page 1360) | 1361 | 1362 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa ya mwenendo wa mchakato wa uchaguzi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) na kusema kuwa yoyote atakaye jihusisha na vitendo vya Rushwa asitegemee nafasi ndani ya jumuiya hiyo au chama
   Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka, akisisitiza jambo kwa Waandishi wa habari juu ya mwenendo wa Jumuiya hiyo nchini na mafanikio waliyoyapata ndani ya miaka mitatu
   Waandishi wa  Habari walioshiriki mkutano huo wakifuatilia hotuba ya Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shakha Hamdu Shakha.


  Ndugu Waandishi wa habari;

  Kwa mara nyingine tena tunawakaribisha kwa mikono miwili katika mkutano huu muhimu. Karibuni sana huku nikiwaomba  mjione mko huru na mko nyumbani .

  Dhana ya Demokrasia ni jambo muhimu linalohitaji kuheshimiwa na kuenziwa ndani ya Chama na  Jumuiya zake. Kiongozi wa UVCCM mahali popote pale huchaguliwa kwa kufanyika uchaguzi huru na wa  haki unaozingatia Kanuni na Taratibu za Uchaguzi kama zilivyoagizwa na vikao husika bila ya kukiuka, kupuuzwa au kuvunjwa.

  Nia ya UVCCM ni kujenga na kudumisha haiba  njema ya kuendelea kuheshimu misingi ya demorasia ya kweli , yenye kuchunga  adabu na kufuata nidhamu, miiko na maadili kwa kila mwanachama anayetaka kutumia haki ya kuchagua au kuchaguliwa.

  April Mwaka 2017 Chama Cha Mapinduzi kilianza mchakato wa Uchaguzi ndani ya Chama na Jumuiya zake. Kufuatia mabadiliko ya Kanuni ya UVCCM yaliyofanyika mwezi Machi, 2017 tulianza Uchaguzi katika ngazi za Matawi ambapo hadi leo jumla ya Matawi 23,529  sawa na Asilimia 99.4% kati ya Matawi  23,670 sawa na Asilimia 0.59% yamekamilisha uchaguzi.
  Ngazi za   Kata  3,913 sawa na Asilimia 96.59% kati ya Kata 4,051 sawa na asilimia 3.4% zimekamilisha uchaguzi .Kwa upande wa majimbo ya  Zanzibar majimbo 54 sawa na Asilimia 100%, wamekamilisha uchaguzi.  

  Ngazi ya Wilaya na Mkoa  mchakato wa uchujaji wa  majina kwa Vijana waliomba nafasi mbali mbali ndani ya Jumuiya yetu , umeanza na  unaendelea vizuri huku jumla ya Vijana 7,606 wamejitokeza kuchuka fomu za kugombea nafasi mbali mbali katka Jumuiya yetu, hali inayoonyesha kumekupo kwa mabadiliko  na msisimko wa kisiasa ukilinganisha na chaguzi zilizopita.

  Kwa upande wa ngazi ya Taifa Vijana 350 wamejitokeza kuomba nafasi za uongozi ndani ya UVCCM kama ifuatavyo:-
  (i) Nafasi ya Mwenyekiti 113 Walioomba
  (ii) Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa 24 Walioomba
  (iii) Nafasi 5 za Wajumbe wa H/Kuu 103 Walioomba
  (iv) Nafasi  5 za Wajumbe wa B/Kuu Taifa 81 Walioomba
  (v) Nafasi 1 Wawakilishi UWT 14 Walioomba
  (vi) Nafasi 1 Wawakilishi Wazazi 15 Walioomba
  Maandalizi kwa ajili ya Mikutano Mikuu ya Wilaya hadi Taifa yanaendelea vyema ambapo chaguzi zote ndani ya UVCCM zinategemewa kukamilika Novemba 2017.
  Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tunaendelea kusisitiza kuwa sifa na wasifu wa kila mgombea aliyeomba kuteuliwa kwa kadri alivyojaza kwenye fomu yake, utaandaliwa na kuandikwa vizuri katika kitabu maalum cha wagombea wote ambacho watapatiwa wajumbe wa Mkutano siku ya uchaguzi husika.

  Kila mgombea atapata nafasi ya kujieleza na kutoa wasifu wake, kutaja dhamira na malengo yake mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu husika baada ya taratibu za vikao vya uteuzi kukamilika si kinyume na hivyo.Tunaendelea kuwakumbusha kuwa ni mwiko kwa mgombea kuanza kampeni mapema  au wapambe wake kufanya ushabiki wa kisiasa kumnadi, kumpigia debe, au kujipitisha na kuelezea nafasi anayogombea. Ukiukaji huo wa Kanuni na taratibu utampotezea sifa za kuteuliwa.

  Aidha tunaendelea kuwasisitiza kuwa ni marufuku na hairuhusiwi kabisa walioomba nafasi mbali mbali kuanza kufanya kampeni za kihuni , kutumia lugha chafu, siasa za maji taka kuchafuana, matusi, dharau kinyume na ubinadamu.

  Kuyaacha hayo yote yafanyike bila ya kuyadhibiti, kuyaasa na kuyakemea ni mwanzo wa kukaribisha mvurugano, mgawanyiko hatimaye  kujipenyeza kwa adui rushwa. Hivyo basi  tunaendelea kuwaagiza watendaji wote wa ngazi husika kusimamia matakwa ya Kimaadili, Kikanuni na Kikatiba.

  Aidha  tunaendelea kuviomba vyombo vinavyohusika katika ngazi zote hasa TAKUKURU kuendelea na  kufuatilia kwa karibu nyendo za wagombea na wapiga kura ili kubaini kuwadhibiti na kuwachukulia hatua za kisheria. Mgombea au mpiga kura yoyote atakayethibitika kutoa au kupokea Rushwa, hatua za kimaadili na kisheria tunaelekeza zichukuliwe ili kulinda heshima ya taasisi yetu.

  Tunaendelea kusisitiza kuwa uchaguzi wa UVCCM katika ngazi zilizobakia zitafanyika kwa misingi ile ile ya uhuru na uwazi huku kila mgombea akipitishwa na vikao vya kikanuni na kikatiba baada ya kukidhi mashariti ya uchaguzi kwa mujiba kanuni na katiba.

  Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na malumbano yenye kupandikiza chuki na kupalilia mifarakano isio na ulazima huku baadhi wa watu wakiwachafua wenzao kwenye mitandao ya kijamii na wakati mwingine wapo wanaothubutu kuwatukana wenzao matusi ya nguoni kinyume na ustaarabu, ubinadamu na misingi na Maadili ya Chama Cha Mapinduzi.
  Wapo baadhi yao hujivika kofia ya Jumuiya wakitumia  njia hatari na batili, wamekuwa wakikebehi, kutuhumu wenzao kinyume na utaratibu huku baadhi yao hata kufikia kutoa madai  yanayovuka mipaka na   kubeba taswira ya  Jinai au  madai. 

  Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi umestushwa na  hali hiyo inayoonekana kutaka kuibua migogoro na kujenga mazingira yanayotaka kuonyesha kana kwamba ndani ya Jumuiya kuna mvurugano au  kuporomoka kwa mshikamano wetu wakati mambo nayo  hayapo. 

  Kimsingi  yote yanayofanyika ni kinyume na utamaduni wa Chama Cha Mapinduzi Kikatiba na Kikanuni na Kimaadili. CCM si genge la wahuni bali ni Chama makini  cha Siasa kinacho heshimu  utu wa mtu, taratibu na miongozo iliyojiwekea katika kushughulikia mambo yake.
  Kwa miaka yote wanajumuiya na viongozi wamekuwa wakiishi kwa kuzingatia misingi ya Umoja, Upendo, mashauriano na kudumisha Maelewano.

  Jumuiya yetu imekuwa ikifanya kazi zake kwa uwazi na umakini mkubwa. Tusingependa kuona ikitiwa nyufa au kukumbwa na athari za kutengenezwa na watu wachache. Nasema tena hatutasita kuchukua hatua stahili kwa mujibu wa kanuni Katiba ya Chama na ikibidi hata kisheria ili kukomesha vitendo hivyo vyenye nia ya kuondosha haiba nzuri ya Chama na Jumuiya katika kufanya mambo yake ya msingi.

  Tumeanza kuwafatilia kwa karibu mno na kuanza kuwatambua wote ambao wanafanya au kushiriki vitendo hivyo vya aibu aidha iwe kwenye Jumuiya au ndani ya Chama chetu  .Chama Cha Mapinduzi na  Jumuiya zake  hujadili mambo yake aidha yakiwa magumu au mepesi kwa mujibu  wa ajenda na njia za majadiliano kupitia vikao halali hatimaye  maamuzi hutolewa baada ya kujiridhisha.  

  Kimsingi utaratibu wa kushughulikia mambo mbali mbali ndani ya chama na Jumuiya zake uko wazi.Yeyote mwenye madai, tuhuma au shutuma anatakiwa atumie vikao halali vya kikanuni na kikatiba   ama kuyafikisha kwa viongozi husika kwa kufuata utaratibu si kinyume na hivyo. 

  Kwa kila mwana jumuiya muadilifu, msemakweli, mpenda Umoja na Mshikamano, siku zote huheshimu kanuni, taratibu, katiba na maelekezo yanayotolewa na viongozi wetu.Nachukua nafasi hii kuwaasa na kuwonya wale wote ambao pengine watakuwa wameteleza na kujikuta wakijielekeza katika kushiriki vitendo hivyo vyenye muoneekano wa uasi , tunawataka wajiepushe navyo hasa kipindi hiki ambacho tunaelekea katika Demokrasia ya kweli ndani ya Jumuiya.

  Narejea tena wapo tunaowajua wakishiriki kufanya vitendo hivyo  na kadri itakavyothibitika kwa kukusanya ushahidi na vielelezo , hatua za kikanuni, kikatiba na pale itakapobidi hatutasita kuchukua hatua za kisheria ili liwe funzo kwa wengine.

  Tusingependa kuona watu wanajitwika na kubeba agenda binafsi au kufikiria kumchafua mtu ndio kupata cheo ndani ya Jumuiya yetu hakuna utamaduni huo haki na usawa itasimamiwa muda wote . Mtu yeyote atayendeleza kufanya hivyo kwa kisingizio cha Uchaguzi wa Chama na Jumuiya zake, mambo hayo hayakubaliki na hayatavumiliwa tena. i

  Uchaguzi ni kipimo cha kupevuka na kielelezo cha ukomavu wa demokrasia ya kweli bila mizengwe au hila ndani ya chama na Jumuiya kwa lengo la kusimamia shabaha na misingi sahihi itokanayo na miongozo, maelekezo na kuheshimu utaratibu unaohimizwa na Chama Cha Mapinduzi .

  Ili kuonyesha  kutii na kufuata maelekezo yanayotolewa mara kwa mara na Mwenyekiti wetu wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli kila mwanachama anapaswa kujitambua, kujiheshimu, kufuata misingi ya katiba na kulinda kwa nguvu zake zote heshima ya Chama Cha Mapinduzi.

  0 0

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb) akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017. Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Mifuko ya Jamii ya PPF na NSSF limeingia ubia katika mradi huo wa uchumi wa viwanda chini ya Kampuni ya MKULAZI.

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb) akiangalia mbegu za miwa kabla ya kuzipanda katika eneo la Shamba la miwa alipowasili Gereza Mbigiri katika ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama.

  Shamba la miwa katika mradi wa Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa – MKULAZI katika eneo la Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro likiwa limestawi kama inavyoonekana katika picha.

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akitoa hotuba fupi kwa Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza Mkoani Morogoro, Watendaji wa Kampuni ya MKULAZI pamoja na Wananchi wanaoishi jirani na Gereza Mbigiri katika ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017.

  Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim(hayupo pichani) namna Jeshi hilo lilivyojipanga katika kuhakikisha kuwa ufufuaji wa Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro unakamilika kama ilivyopangwa ambapo matarijio ni kuwa Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha sukari tani 50,000 kwa mwaka.
  Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Mkoani Morogoro wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017.

  Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kyaharara akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017.
  Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage(kulia) mara baada ya ziara ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambapo amekagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017.

  Mkurugenzi Mkuu wa PPF William Erio akitoa neno la shukurani mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017.

  Ujenzi wa maghala ya kuhifadhia sukari katika mradi wa Kiwanda cha Sukari cha MKULAZI kilichopo Gereza Mbigiri ukiendelea katika hatua mbalimbali kama inavyoonekana katika picha

  Wataalam wazalendo ambao wanajitolea katika ujenzi wa mradi wa Kiwanda cha Sukari – MKULAZI Mbigiri wakitambulishwa mbele ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa(hayupo pichani(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
  Maafisa Waandamizi wa PPF na NSSF wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa(hayupo pichani).

  0 0

  Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akipokea zawadi ya kumbumbu kutoka kwa Balozi wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem.
  Balozi wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Zanzibar.
  Balozi wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem akimkabidhi mabeseni 300 ya vifaa tiba vya mama mjamzito Waziri wa Afya wa Zanzibar , Mahmoud Thabit Kombo(wapili kulia) katika hafla ilifanyika katika Hospitali ya mnazi mmoja.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Watoto,Bi Sihaba Nkinga akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa watoto ulioandaliwa na taasisi ya REPSSI yenye makao yake nchini Afrika Kusini kutoka mataifa zaidi ya 30 barani Afrika unaofanyika jijini
  Arusha,mkutano huo pamoja na mambo mengine unalenga kuwawezesha watoto sauti zao kusikika na kuwajenga kisaikolojia.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi ya REPSSI,Noreen Huni ambaye ni raia wa
  Zimbabwe akizungumza katika mkutano huo wa kimataifa jijini Arusha leo.
  Watoto kutoka mataifa mbalimbali wakifatilia mada kwenye mkutano huo.
  Watoto  kutoka mataifa mbalimbali wakiwa kwenye mkutano ambao unawapa fursa ya
  kuwasilisha taarifa za matukio ambayo ni changamoto kwao.
  Watoto wakiwa kwenye mkutano ambao unawapa fursa ya kuwasilisha taarifa za matukio ambayo ni
  changamoto kwa mamlaka husika na kutafutiwa ufumbuzi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Watoto,Bi Sihaba Nkinga(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa baraza la watoto nchini,Joel
  Festo(kushoto) na Mwenyekiti wa baraza la watoto nchini Kenya,Brian Musyoka katika mkutano wa kimataifa wa watoto ulioandaliwa na taasisi ya REPSSI yenye makao yake nchini Afrika Kusini .
  Mmoja wa washiriki akifatilia kwa makini.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Watoto,Bi Sihaba Nkinga(katikati)akiagana na viongozi wa watoto mara baada ya kufungua mkutano huo jijini Arusha

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo amekutana na kufanya mazungumzo na chama cha Wamiliki wa Malori ya Usafirishaji wa Mchanga ambao wamemuunga mkono kwenye kampeni ya ujenzi wa ofisi za walimu kwa kujitolea kusafirisha mchanga wote utakaohitajika. 

  Wamiliki hao kwa kauli moja wamemwambia Makonda kuwa suala la kusafirisha mchanga wa kujenga ofisi zote 402 watalibeba hao hivyo yeye aendelee na majukumu mengine. 

  Makonda ameshukuru chama hicho kwa kutambua thamani na mchango wa mwalimu. 

  Amesema Walimu wakiboreshewa Mazingira ya kufanyia kazi itawawezesha kufanya kazi yao kwa ufanisi na kuwapatia Wanafunzi Elimu bora itakayosaidia Taifa kuwa na wataalamu wa kutosha na kupunguza utegemezi wa wataalamu kutoka nje ya nchi. 

  Ametoa wito kwa Jamii kuendelea kuchangia Kampeni ya ujenzi wa Ofisi za Walimu ili Walimu wasifanyekazi kwenye mazingira Magumu. 

  Kwa Upande wake Mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa Malori ya Kusafirisha Mchanga Bwana Emmanuel Moshi amesema kuwa wameamua kuunga mkono kutokana na juhudi za Makonda na kutambua thamani ya Mwalimu huku akieleza kuwa wataendelea kumuunga mkono.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo kuwachukulia hatua wakandarasi wa magari ya taka ambao wamekuwa hawatimizi wajibu wao wa kuzoa taka.
  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, kata ya Kiwalani DC Mjema alifikia hatua ya kutoa agizo hilo baada ya wakazi wa eneo hilo kulalamika kuwa wiki ya pili imepita mkandarasi anae husika na uzoaji taka eneo hilo kutokufanya kazi hiyo na kupelekea taka kuzagaa maeneo mbalimbali ya eneo hilo jambo ambalo ni hatari kwa afya.
  " Watu wa namna hii Mkurugenzi inabidi wachukuliwe hatuaq kwa kukamatwa na kupelekwa mahakamani kwa kufanya mambo yaliyo nje ya makubaliano" Alieleza DC Mjema.
  Pia DC Mjema amemuagiza Mkurugenzi huyo ndugu Msongela Palela kuhakikisha kuwa hakuna mradi wowote unafanyika katika kata husika bila ya ushirikishwaji wa wananchi ili baadae zisije kutokea sintofahamu na kwa pamoja wakubaliane bei za tozo za ada ya uzoaji taka katika maeneo hayo.
  Katika hatua nyingine DC Mjema amewataka wananchi wa eneo hilo kwenda ofisi ya Mkurugenzi ili maeneo yao yapimwe kama yapo ndani ya hifadhi ya reli ili wajiandae mapema kabla ya bomoabomoa haijawafikia.
  "Hili swala la bomoabomoa lipo nje ya uwezo wangu kwa wale wananchi ambao nyumba zao zipo kwenye hifadhi ya reli kati ya mita 30 na 50 waende ofisi ya Mkurugenzi kwa uhakiki" Alieleza DC Mjema.
  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Palela amewataka watendaji wa mitaa kutowatoza wananchi tozo ya huduma wananchi pindi wanapokwenda katika ofisi zao, vinginevyo atawachukulia hatua, na kuwataka wananchi watoe taarifa kwa mtendaji wa kata, ikishindikana wakamuone yeye ofisini kwake.

  0 0

  WANAFUNZI wa shule ya Msingi ya Tusiime ya Tabata jijini Dar es Salaam, wametoa msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kwa watu wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha Mama Teresa cha Mburahati, Dar es Salaam.

   Msaada huo ambao umetokana na michango ya wanafunzi wa shule hiyo ni pamoja na unga, mchele, mafuta ya kupikia na vinywaji vya aina mbalimbali.Akizungumza punde tu baada ya kukabidhi msaada huo, mmoja wa wanafunzi wa Tusiime, Agnes Heke  amesema walianza kuchangishana wenyewe kwa wenyewe muda mrefu lengo ikiwa ni kusaidia watu wanaolelewa kwenye kituo hicho.

  Alisema dhamira ya kusaidia wenzao wa kituo hicho inatokana na mafundisho ya upendo wanayofundishwa wakiwa shuleni Tusiime.“Tumekuwa tukifundishwa kuwajali wenye shida na kwa kweli tulianza kuchangishana muda na leo hii tumeona hiki tulichopata tuwape wenzetu, huu ni mwanzo maana kadri tutakavyokuwa tunapata tutarudi kuwasaidia,” alisema Agnes.

  Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo, Mkuu wa Taaluma wa shule hiyo, Maxon Wilson amesema  msaada uliotolewa na wanafunzi hao ni sehemu tu na wameahidi kuendelea na moyo huo wa upendo kwa wenzao.Alisema msaada uliotolewa na wanafunzi hao unadhihirisha kuwa mafunzo ya maadili na kuwapenda wenzao wanayoyafundisha yamewaingia vema na wanayazingatia kwa dhati.

  Mmoja wa wazee wanaolelewa na kituo hicho, Elizabeth Daudi, aliishukuru shule ya Tusiime kwa namna ambavyo imewafundisha wanafunzi wake kuwa na upendo kiasi cha kuamua kuchanga kwa ajili yao.“Msaada huu ni ishara kwanza mafunzo ya upendo mnayoyapata shuleni yamefanyakazi, hatukutarajia kupata msaada kama huu tunawashukuru na Mungu awazidishie,” alisema kwa niaba ya wenzake.

  Alishukuru msaada huo wa wanafunzi wa Tusiime kwani umekuja wakati muafaka kwani huwa wanaishiwa na vyakula mara kwa mara.“hatuna maneno ya kutosha kuelezea furaha yetu , tunaomba watu wengine waige mfano wa Tusiime, waone watu  wanaolelewa hapa ni wajamii nzima,” alisema.
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi  Tusiime, ya Tabata Dar es Salaam, Agnes Heke na Ibrahim Shaban wakikabidhi vyakula mbalimbali kwa Bi. Elizabethi Daudi asiyeona ambaye ni mmoja wa watu wasiojiweza wanaolelewa kwenye kituo cha Mama Teresa Mburahati jijini Dar es Salaam.Msaada huo umetokana na michango ya wanafunzi wenyewe.
   Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya  Tusiime ya Tabata wakiwa wamebeba vyakula mbalimbali na sabuni kwa ajili ya kutoa msaada kwenye kituo cha watu wasiojiweza wanaolelewa kwenye kituo cha Mama Teresa Mburahati jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetokana na michango ya wanafunzi wenyewe.      
                   

  0 0


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN akiangalia kofia iliofumwa kwa mikono wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Coco Blue Jambiani.

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa Mkoa wa Kusini Unguja liliofanyika jana kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa Mkoa wa Kusini Unguja liliofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani.

  0 0


  Wakimbizi wa Burundi waliokimbia machafuko nchini kwao wataanza kurejea nchini kwao ifikapo Septemba 7 hadi Desemba 31, mwaka huu mara baada ya pande tatu ikiwemo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), kutiliana saini Mpango wa Kuwarejesha wakimbizi baada ya mkutano uliochukua takribani siku tatu katika kuandaa mpango huo.

  Wakitiliana saini makubaliano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki,Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo kutoka nchini Burundi, Pascal Barandagiye na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini Tanzania, Chansa Kapaya, mwishoni mwa wiki wote walikubaliana kutekeleza vipengele vilivyopo katika makubaliano hayo yakiwa na lengo la kuwarudisha wakimbizi walioomba kurejea nchini Burundi, baada ya hali ya Amani na utulivu kurejea.

  Akizungumza baada ya kutiliana saini makubaliano hayo Waziri Mwigulu, alisema umefika wakati wa wakimbizi wa Burundi kurudi nchini kwao kuungana na familia zao na ndugu waliobaki ili kusaidia kujenga uchumi wa nchi yao baada ya kuwa katika machafuko yaliyosababisha kukimbia nchi yao kwa muda mrefu.

  “Mimi kama mwanauchumi ninaona madai yao ya kurudi nchini Burundi kujishughulisha na shughuli za kilimo ni maamuzi mazuri huku pia wakisisitiza kurejea kwa Amani na Utulivu nchini kwao kuwa ni sababu ya msingi ya kufikia kuomba kurejea, sisi kama Serikali tutahakikisha zoezi hilo la urejeaji nchini kwao linaenda salama tukishirikiana na Serikali ya Burundi kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchini Burundi,” alisema Mwigulu.

  Naye Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo kutoka nchini Burundi, Pascal Barandagiye, amesema anaishukuru Serikali ya Tanzania na Watanzania wanaoishi kwenye maeneo yaliyotumika kuwahifadhi wakimbizi kwa ukarimu wao walioonyesha muda wote kwa raia kutoka nchini Burundi huku akisisitiza kurejea kwa hali ya Amani na utulivu ambao hapo mwanzoni ilitoweka.

  “Nawaomba wananchi wetu warejee nchini ili tuweze kuijenga Burundi yetu ambayo hivi sasa kuna Amani na utulivu, pia naishukuru Serikali ya Tanzania na Watanzania ambao wamekua wakiwaonyesha ukarimu wakimbizi kutoka Burundi na kuwapa hifadhi nchini hapa,”alisema Barandagiye.

  Kwa upande wao Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) kupitia kwa Mwakilishi wao nchini,Chansa Kapaya, wameahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuhakikisha wakimbizi wa Burundi 6,800 walioomba kurejea nchini kwao wanasahiliwa na kurejeshwa kwao katika hali ya utu na usalama huku shirika hilo likizishukuru Serikali za Tanzania na Burundi kwa msaada wao walioupata katika kushughulikia masuala ya wakimbizi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba,akibadilishana nyaraka na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini Tanzania,Chansa Kapaya(kulia) zenye makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa mkoani Kigoma.Makubaliano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki, Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo kutoka nchini Burundi, Pascal Barandagiye, akibadilishana nyaraka na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini Tanzania, Chansa Kapaya (kulia) zenye makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa mkoani Kigoma.Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.Makubaliano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki, Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Wajumbe kutoka Serikali ya Burundi wakiongozwa na Balozi wa Burundi nchini Tanzania,Gervais Abayeho wakiwa katika Mkutano wamakubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa mkoani Kigoma.Makubaliano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki,Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Wajumbe kutoka Mashirika mbalimbali ya kimataifa wakiwa katika Mkutano wa makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa mkoani Kigoma.Makubaliano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki, Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0


  Na. Benedict Liwenga-WHUSM.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa pongezi za dhati kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu Youking kutokana na utendaji kazi wake uliotukuka katika kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na China hususani katika nyanja za masuala ya habari, utamaduni, sanaa na michezo.

  Pongezi hizo amezitoa hivi karibuni wakati wa hafla ya kumuaga balozi huyo iliyowakutanisha baadhi ya Viongozi wa Chama cha Ushirikiano wa Rafiki wa Tanzania na China wakiwemo Waandishi wa habari.

  Moja ya mambo makubwa muhimu yaliyofanyika chini wakati wa kipindi cha Balozi Lu Youking ni tukio la utiaji saini mwezi Machi mwaka huu ambapo Serikali ya Tanzania na China zilitiliana saini Mkataba wa Ushirikiano wa Kiutamaduni wa Miaka mitatu ambao utawapa fursa vijana 200 kutoka Tanzania kila mmoja kwenda China kwa ajili ya kupata mafunzo katika nyanja mbalimbali za habari, sanaa na utamaduni.

  “Balozi Lu Youking umetuachia zawadi kubwa sana sisi Wanahabari wa Tanzania, sasa hivi mimi na wenzangiu Wizarani tunakamilisha utaratibu wa utekelezaji wa Mkataba huu ili tuanze kuutekeleza mapema iwezekenavyo”, alisema Dkt. Mwakyembe.

  Aliongeza kuwa, Balozi Lu Youking hivi karibuni ameshirikiana na Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Balozi Mbelwa Kairuki katika kuhakikisha kwamba Waandishi wa habari 10 kutoka Tanzania wanaondoka mwezi ujao kuelekea nchini China kwa ajili ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya habari.

  Kwa upande wake Balozi Lu Youking alisema kwamba, urafiki kati ya Tanzania na China umekuwa wa afya na imara zaidi ya nusu karne akikumbushia kuwa, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake aliwahi kusema kwamba, Tanzania ina marafiki wengi, lakini China ni zaidi ndiyo maana Rais wa China, Mhe. Xi Jinping alichagua Tanzania kuwa kituo chake cha kwanza Afrika wakati wa ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu kuwa mkuu wa nchi.

  Aliongeza kuwa, kila mwaka zaidi ya Wanafunzi 700 kutoka Tanzania huenda China kwa ajili ya masomo zaidi na kutokana na hilo, matokeo ya ushirikiano wa China na Tanzania umekuwa wa manufaa katika maeneo yote ya uchumi wa Tanzania na maendeleo ya jamii na kwa kila maisha ya Mtanzania.

  “Uhusiano wa China na Tanzania umetoa mwongozo kwa Ushirikiano wa Kusini na Kusini yaani South-South Cooperation, hivyo kutokana na maendeleo ya ushirikiano huu katika uwezo wa uzalishaji kati ya China na Tanzania na mpango wa Ukanda mmoja njia moja, tunaamini ushirikiano huu utakuwa na matunda zaidi”, alisema Balozi Youking.

  Urafiki baina ya Tanzania na China ulianzishwa na Waasisi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Kikomunisti cha China, Bw. Mao Tse-Tung (Mao Zedong) ambapo uhusiano baina wa nchi hizi mbili kwa sasa umekuwa kwa kasi na kuleta maendeleo baina ya pande zote mbili.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe(kulia) akimpongeza Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu Youking wakati alipowasili kwa ajili ya kushiriki hafla ya kumuaga balozi huyo iliyofanyika katika mgahawa wa Great Wall Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na wageni waalikwa pamoja na Viongozi mbalimbali waliohudhulia hafla ya kumuaga balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu Youking iliyofanyika katika mgahawa wa Great Wall Jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu Youking akiongea na wageni waalikwa pamoja na Viongozi mbalimbali waliohudhulia hafla ya kuagwa kwake iliyofanyika katika mgahawa wa Great Wall Jijini Dar es Salaam
  Mwenyekiti wa Chama cha Ushirikiano wa Urafiki baina ya Tanzania na China, Dkt. Salim Ahmed Salim (kushoto) akimpongeza Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu Youking mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kumuaga balozi huyo iliyofanyika katika mgahawa wa Great Wall Jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)

  0 0

  SERIKALI imesema hivi sasa inatoa sh. bilioni 22.2 kila mwezi ili kuboresha elimu ya msingi na sekondari hapa nchini.

  Kauli hiyo imetolewa jana (Jumamosi, Septemba 2, 2017) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bw. George Simbachawene wakati akizungumza na wahitimu 166 wa darasa la saba wa shule ya msingi ya Martin Luther, kwenye sherehe za mahafali ya 10 zilizofanyika shuleni hapo katika Manispaa ya Dodoma.

  Waziri Simbachawene ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alisema Serikali itaendelea kuboresha elimu ya sekondari kwa kuajiri walimu wengi zaidi wa masomo ya sayansi.

  “Wazazi wa wanafunzi wanaohitimu tunawakaribisha kwenye shule za sekondari kwa sababu zote zina walimu wa kutosha, madawati na vifaa vya kufundishia. Kila mwezi tunatenga sh. bilioni 22.2 kuendesha shule za msingi na za sekondari hadi kidato cha nne,” alisema.Alisema hivi sasa, baadhi ya shule zinakabiliwa na changamoto ndogo ya upungufu wa walimu wa sayansi lakini nayo itatuliwa hivi karibuni kwa sababu vibali vya ajira vimeanza kutolewa.

  “Tunaendelea kuziboresha na tumeshuhudia miaka ya karibuni wanafunzi bora kitaifa wakitoka katika shule za Serikali ambazo wengi wamezoea kuziita ni shule za kata. Hakuna shule za kata. Zote ni zimejengwa na Serikali,” alisisitiza.“Ukienda vyuo vikuu, wanafunzi na ufaulu wa juu wengi wao ni wale waliotoka kwenye shule za Serikali,” aliongeza.

  Aliwataka wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani yao Septemba 6 na 7, wasiwe na hofu kwani kufanya hivyo ni chanzo cha kuwafanya wachanganye mambo na kisha kufeli.Kwa upande wake, Mkurugenzi wa shule hiyo, Bw. Rabbiely Mmanga aliwaasa wazazi na kuwaomba wasiwaingize watoto kwenye migogoro kwani matendo hayo yanawajisi watoto na kuwaathiri kisaikolojia hata wawapo shuleni.

  “Ninawaomba sana wazazi, tofauti zenu ziishie chumbani na zisifike masikioni mwa watoto kwa sababu zinawasumbua kisaikolojia na kuwaharibia concentration yao kimasomo. Tumewahoji baadhi na wamesema wanaumia kwa kukumbuka adha ambayo mama anaipata kutoka kwa baba, au baba anaipata kutoka kwa mama,” alisema.

  Katika mahafali hayo, wanafunzi mbalimbali walipewa vyeti kwa kufanya vizuri kwenye masomo mbalimbali huku Ismail Milambo na Nise-Magreth Malila wakiibuka kidedea kwenye masomo yote (best academic performers). Tuzo za nidhamu bora (discipline) zilichukuliwa na Michael Nyalusi na Sayuni Kampuni.

  Wanafunzi wengine waliopata tuzo na masomo yao kwenye mabano ni Ismail Milambo (Hisabati), William Terry William (Kiingereza), Majaliwa K. Majaliwa (Sayansi), Nise Malira (Kiswahili), Clinton Dotto (Social Studies) na Justin Kilimali (Kompyuta).

  Wengine walipewa tuzo kwenye vipengele vya michezo, uchoraji na sanaa, usafi, uongozi shuleni, uimbaji na uongozi wa ibada.Katika risala yao, wanafunzi wanaohitimu walisema wanaamini misingi ya elimu walioipata kwenye shule ya Martin luther haitapotea bure na wakaahidi kufanya mitihani yao kwa umakini ili watoke na ufaulu wa hali ya juu.

  Wanafunzi wa darasa la saba kote nchini, wanatarajiwa kufanya mitihani yao ya kitaifa Septemba 6 na 7, mwaka huu.

  0 0

                                         
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watendaji katika mikoa yote nchini kuhakikisha wanafuatilia maendeleo ya viwanda mbalimbali katika maeneo yao.

  Amesema mpango wa Serikali wa kujenga uchumi wa viwanda unalenga kuinua uchumi wa Taifa kutoka wa chini kwenda wa kati, hivyo ni muhimu kuvifuatilia.Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Jumamosi, Septemba 2, 2017) alipozungumza na watendaji na wananchi wa mkoa wa Morogoro alipofanya ziara katika kiwanda cha Moproco.

  Alisema licha ya kukuza uchumi wa Taifa, viwanda vitasaidia katika kutatua tatizo la ukosefu wa ajira hususani kwa vijana kwani vinauwezo wa kuajiri watu wengi.“Viwanda hivi vinatupa uhakika wa ajira nchini kwa sababu vinauwezo wa kuajiri watu wengi na wa kada mbalimbali, hivyo ni muhimu tukafuatilia utendaji wake.”

  Waziri Mkuu aliongeza kuwa mbali na kutoa ajira nyingi, pia viwanda vitawezesha wakulima kupata soko la uhakika la mazao yao na kukifanya kilimo kuwa na tija.Alisema kwa muda mrefu sekta ya viwanda nchini ilikuwa haifanyi vizuri jambo ambalo lilisababisha kuongezeka kwa tatizo la ajira na mazao yalikosa soko.

  Hata hivyo Waziri Mkuu alitoa wito kwa wafanyakazi walioajiriwa katika viwanda mbalimbali kuwa waaminifu ili kuviwezesha viwanda hivyo kuendelea na uzalishaji.Pia aliwataka wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali ili kuviwezesha viwanda kuwa na uhakika wa upatikanaji wa malighafi ndani ya chini.

  Awali Meneja Mkuu wa kiwanda cha Moproco, Bw. Arif Abood aliiomba Serikali kuongeza kodi kwa mafuta yanayotoka nje ya nchi ili kulinda viwanda vya ndani.Alisema uingizwaji wa mafuta kutoka nje ya nchi kwa kiasi kukubwa ulichangia kufungwa kwa viwanda vya ndani vya mafuta kutokana na kukosa soko.

  Katika ziara hiyo Waziri Mkuu aliambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mheshimiwa Charles Mwijage pamoja na maofisa wengine wa Serikali.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S.L.P 980,
  40480-DODOMA 
  JUMAPILI, SEPTEMBA 3, 2017.


  Waziri Mkuu. Kassim Majaliwa akishiriki kupanda mbegu za miwa katika Shamba la Gereza Mbigiri kwa ajili ya maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro jana Septemba 2, 2017.Picha na ofisi ya Waziri Mkuu


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amezindua zoezi la Ulipaji wa fidia kwa Wakazi wanaopitiwa na Mradi wa uboreshaji wa Barabara kwa maeneo yasiyopangwa DMDP,ambao wataanza kulipwa Fedha zao kuanzia kesho sambamba na kufanya ziara ya ukaguzi wa Miundombinu ya Barabara.

  Mradi huo utahusisha  uboreshaji wa Barabara,Mabonde ya Mito, Ujenzi wa Mitaro ya Maji, Taa za Barabarani, Njia za watembea kwa Miguu, Vizimba vya taka, alama za Barabarani na Soko la Mwananyamala ambapo unagharimu kiasi cha Shilingi Billion 230.

  Miongoni mwa Barabara zitakazojengwa kwa kiwango cha lami ni Barabara inayoanzia Morocco hotel hadi Sinza Kijiweni Km 5, Barabara ya Tandale Kisiwani kuelekea Mwananyamala na Barabara za Makumbusho, , TANESCO Msasani, Simu200, Kilungule na MMK.

  Makonda amesema mradi huo utafanya jiji la Dar es Salaam kuendelea kuwa la kisasa na kufikia azma yake ya Dar Mpya.Amewataka wananchi watakaolipwa fidia kuhakikisha wanazitumia fedha hizo vizuri kwa kutafuta makazi bora sehemu nzuri zaidi na pia kufanyia shughuli zingine za kimaendeleo zitakazo waingizia kipato.

  Aidha Makonda amesema kuwa Kata za Tandale, Mburahati na Mwananyamala zitaingizwa kwenye idadi ya Kata 14 zinazopandishwa viwango kwa kuwa Barabara za kisasa maana ya kuwa na Lami,Taa na Mitaro ya Maji.Hata hivyo amesema Mto Ng’ombe pia utatengenezwa kwa kiwango cha kisasa urefu wa Km 7.5 ili kuwezesha Maji kwenda moja kwa moja hadi Baharini kupitia eneo la Jangwani kutakapojengwa mfumo wa kusafirisha maji taka.

  Makonda amempongeza Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta na Manispaa hiyo na kuwataka kuhakikisha kila anaestahili kulipwa fidia analipwa kile anachostahili bila usumbufu.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akipata maelezo mafupi kutoka kwa baadhi ya Wananchi kuhusu maeneo ambayo miundombinu yake imekuwa kero kwa wananchi,ikiwemo makaravati yaliyoziba na mitaro 
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa ameambatana na Watendaji wa wilaya ya Kinonondi akizungumza na baadhi ya wananchi walioko kwenye kituo cha daladala cha Simu 2000 
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa ameambatana na Watendaji wa wilaya ya Kinonondi wakikagua miondombnu mingine ikiwemo madaraja na makaravati yaliyoziba,ambayo yanahitaji kufanyiwa marekebisho 
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa ameambatana na Watendaji wa wilaya ya Kinonondi wakikagua barabara ya Makumbusho mapema leo jijini Dar.Picha na Emmnanuel Masaka-Globu ya Jamii.


  0 0  0 0


  Na Beatrice Lyimo- MAELEZO,
  DODOMA.

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuzindua mfumo wa kielektoniki wa kuandaa Mipango , Bajeti na Ripoti kwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa(PlanRep) na Mfumo wa Uhasibu wa Utoaji wa Taarifa za Fedha kwenye Vituo vya Kutolea Taarifa(FFARS).

  Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma, Mkurugenzi msaidizi anayeshughulikia masuala ya TEHAMA Ofisi ya Rais – TAMISEMI Baltazar Kibola amesema kuwa mifumo hiyo inatarajiwa kuzinduliwa Septemba 5, 2017 katika ukumbi wa LAPF Mkoani Dodoma.

  Akifafanua Bw. Kibola alisema kuwa lengo la mifumo hiyo ni kusaidia kuja na mfumo mmoja wa kitaifa utakaowezesha kuwa na utaratibu wa kuandaa mpango na bajeti ambapo utasaidia Hamlashauri zote nchini kuwa na muundo mmoja wa uandaaji wa mipango na Bajeti za Serikali.

  Aidha alisema kuwa lengo la Mradi wa uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) ni kushirikiana na Serikali katika kuimarisha mfumo ili kusaidia uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa katika ngazi ya kila kituo husika.

  Kwa upande wake Mkuu wa Timu ya Rasilimali Fedha kutoka Mradi wa uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Dkt. Gemin Mtei alisema kuwa lengo la mradi huo ni kufanya maboresho ya mifumo katika Sekta za Umma ili kuongeza ufanisi.

  “Mradi huu unalenga kufanya maboresho katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la Utawala Bora, Rasilimali watu, Rasilimali Fedha na pia katika maeneo ya TEHAMA ambapo utasaidia ni namna gani mifumo inawezeshwa kufanya kazi kwa urahisi” amesema Dkt. Mtei.

  Aidha Dkt. Mtei amebainisha baadhi ya maeneo yaliyolengwa kufanyiwa maboresho ikiwemo utoaji wa huduma, kutambua watoa huduma na pia kuwekeza kwa watoa huduma ili kuwezesha wananchi kuweza kunufaika na huduma hizo.

  Vile vile Dkt. Meti alisema kuwa Mfumo wa kielektroniki (PlanRep) iliyoboreshwa na Mfumo wa Uhasibu wa Utoaji wa Taarifa za Fedha kwenye Vituo vya Kutolea Taarifa(FFARS) Mradi wa (PS3) ikiwa ni mradi wa miaka mitano (2015 – 2020) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa (USAID) kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania.

  Naye Mtaalamu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Elisa Rwamiago amesema kuwa mfumo umeundwa kwa kuzingatia Ubora, Usimamizi wa fedha, ufanisi katika utendaji kazi wa umma, kupunguza gharama za usimamizi na utendaji wa kazi.

  “Mfumo uliokuwa ukitumika awali ulitumia gharama nyingi, muda mwingi na pia ulihusisha watu wengi kukaa kusafiri kukaa pamoja sehemu moja, ila mfumo huu ulioboreshwa umerahisisha utendaji kazi na kupunguza gharama iliyokuwa ikitumika awali” amesema Rwamiago

  Akibainisha faida za mifumo hiyo kwa Serikali Rwamiago amesema kuwa itawezesha ufuatiliaji kuanzia ngazi za vituo vya Afya, Zahanati na shule hivyo utawezesha upatikanaji wa taarifa kutoka katika kila kituo kwa wakati.

  Vilevile amesema kuwa mifumo hiyo ina manufaa katika ngazi zote za utendaji hivyo itasidia uunganishaji wa Taarifa kuhusu fedha za Serikali kutoka katika ngazi ya vituo hadi Halmashauri mpaka ngazi ya Taifa.

  “Mifumo hiyo imeandaliwa katika ubora kwa kuzingatia changamoto zilizokuwepo awali kwa lengo la kuleta ufanisi katika utekelezaji wa kazi za Serikali” alifafanua Rwamiago.

  Mradi wa uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) ni mradi uliounganisha Mikoa yote ya Tanzania na Halmashauri zake ambapo wataalamu wa masuala ya Mipango, Bajeti,Waganga wakuu wa Wilaya, Makatibu Afya, Mweka Hazina kutoka katika kila Halmashauri wamepatiwa mafunzo kuhusu Mifumo hiyo.
  Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya TEHAMA toka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Baltazar Kibola akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma kuhusu uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa kuandaa Mipango,Bajeti na kutoa Ripoti za Malaka ya Serikali za Mitaa utakaozinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Septemba 5,2017 mjini Dodoma kulia ni Mkuu wa Timu ya Rasilimali Fedha kutoka mradi wa PS3 Dkt. Gemini Mtei na kushoto ni Mtaalamu kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Elisa Rwamiago.
  Mkuu wa Timu ya Rasilimali Fedha kutoka mradi wa PS3 Dkt. Gemini Mtei akizungumzia faida za mfumo huo wakati wa mkutano na vyombo vya habari leo mjini Dodoma. Kushoto ni.Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya TEHAMA toka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Baltazar Kibola.
  Mmoja wa Wataalamu kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI bw. Elisa Rwamiago akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo mjini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya TEHAMA toka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Baltazar Kibola.(Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo ,Dodoma

  0 0

  Kitengo cha Usajili wa Hati na Nyaraka katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kimefanya maboresho katika upatikanaji wa Hati na Nyaraka kwa muda mfupi zaidi na ilivyokuwa hapo awali.

  Akizungumza wizarani hivi karibuni; Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Hati; Bwn. Kastor Ngonyani alisema; Katika zoezi la usajili wa Hati mpya zilizokuwa zikiandaliwa kwa muda wa miezi mitatu toka tarehe ya kuwasilishwa kwa Msajili, sasa zoezi hilo linachukua wiki mbili tu. Ameeleza utaratibu huo umerahisishwa kwa kutumia mfumo wa Kielektroniki.

  Aidha, Bwn. Ngonyani alisema kwa nyaraka nyingine zinazohusu Ardhi, kama zile za Uhamisho, Mikopo na zile zisizohusu Ardhi/za mali zinazohamishika zinatumia wiki moja tu kuwa tayari kutoka tarehe ambapo nyaraka husika iliwasilishwa kwa Msajili wa Hati.

  Vile vile, Msajili alisema kwamba utoaji wa taarifa nyingine za upekuzi/ Search ambazo huhusisha taarifa mbalimbali kama vile; Kujua kiwanja ni cha matumizi gani, kina Hati au hakina, Mmiliki wake ni nani na taarifa zinazofanana na hizo kuhusu Historia ya kiwanja husika; " Sasa taarifa hizo zinapatikana kwa siku mbili tu, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo zoezi hilo lilikuwa linachukua wiki mbili, mwezi mzima au hata zaidi," alisema Bwn. Ngonyani.

  Bwn. Ngonyani alieleza jinsi ambavyo ofisi yake imekuwa na Hati na nyaraka mbalimbali za Wananchi ambao bado hawajafika kuchukua Hati na Nyaraka hizo, licha ya nyaraka hizo kuwa tayari kwa muda mrefu uliopita. Bwn. Ngonyani alitoa rai kwa Wananchi wote ambao walishafika katika ofisi yake kwa ajili ya kupatiwa huduma hizo wafike kuchukua Hati na Nyaraka hizo muhimu kwao.

  Ofisi ya Kitengo cha Msajili wa Hati ipo kisheria . Sheria zinazoainisha uwepo wake sambamba na majukumu yake ni ; Sheria ya Usajili wa Ardhi , Sura ya 334 ya Sheria za Nchi; Sheria ya Usajili wa Nyaraka, Sura 117 ya Sheria za Nchi; Sheria ya Uhamisho wa Mali/Usajili wa Mali zinazohamishika, Sura 210 ya Sheria za Nchi na Sheria za Usajili wa Majengo ( Unit Tittle Act).

  Na kitengo cha Mawasiliano Serikalini -Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi .


  Msajili wa Kitengo cha Hati; Bwn. Kastor Ngonyani akizungumzia Maboresho yaliyofanyika katika ofisi yake.

  Afisa katika Kitengo cha Hati akimhudumia mteja aliyefika katika dawati lake.

  Maafisa mbalimbali katika Kitengo cha Hati. Na wengine wa Idara mbalimbali za Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiendelea kuhudumia Wananchi katika Kituo cha Huduma kwa Mteja Wizarani hapo.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva, Jumanne wiki hii ataanza ziara rasmi nchini Tanzania ambapo anategemewa kufanya mikutano na mazungumzo na maofisa waandamizi wa serikali na wadau. 

  Bw. Graziano da Silva anategemewa kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.

  Mkurugenzi Mkuu wa FAO amepanga kufanya mikutano na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Tanzania Bara), Dkt. Charles Tizeba, na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed.

  Ziara hii ya Mkurugenzi Mkuu inakuta wakati FAO ikiadhimisha miaka 40 toka kuanza shughuli zake hapa Tanzania. Wakati wa ziara hii, Bw. Graziano da Silva atakutana na uongozi na wafanyakazi wa FAO hapa Tanzania kabla ya kuhudhuria hafla maalum hapa Dar es Salaam kusherehekea maadimisho hayo. Hafla hiyo itahudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan. 

  Mwakilishi Mkazi wa FAO hapa nchini, Bw. Fred Kafeero, amethibitisha kuwa Bw. Graziano da Silva atakuwa hapa nchini kufuatia mwaliko wa Serikali ya Tanzania. “Mkurugenzi Mkuu wa FAO atabadilishana mawazo na Serikali ya Muungano wa Tanzania kwenye masuala makuu yanayohusiana na uhakika wa chakula na maendeleo ya kilimo, ikijumuisha juhudi za FAO kitaifa na kikanda,” alisema. Bw. Graziano da Silva pia atajadili mambo mengine yanayohusiana na ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na FAO, pia masuala mengine ya umuhimu kati ya pande hizo mbili, aliongeza. Mbali ya Maafisa wa Serikali, Mkurugenzi Mkuu atakutana na wadau wengine wa FAO hapa nchini wakiwa ni pamoja na asasi za kiraia, taasisi za elimu, na taasisi za utafiti. 

  Baadae Mkurugenzi Mkuu ataenda Zanzibar ambapo, miongoni mwa mambo mengine, anategemewa kuweka jiwe la msingi katika jingo la Mradi wa Kuzalisha vifaranga vya samaki unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Korea kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa KOICA. Pia Bw. Graziano da Silva atapata fursa ya kutembelea mradi wa kilimo cha mwani na pia kuona maonesho ya bidhaa mbali mbali zilizotengenezwa na wanawake wanaojihusisha na kilimo cha mwani. 

  Tanzania ilijiunga na FAO mwaka 1962, na mwaka 1977 FAO ilifungua ofisi zake hapa Tanzania. Katika miaka 40 ya uwepo wake, FAO imeisadia Serikali ya Tanzania katika kupanga na kutekeleza sera, mikakati na mipango ya kilimo hapa nchini. Kazi ya FAO imejikita katika kuboresha usalama wa chakula na lishe pamoja na maisha ya wakulima wadogo na hivyo kuwa chachu ya kukua kwa uchumi kupitia sekta ya kilimo.

  0 0

  NA HAMZA TEMBA - WMU.

  Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii imeunga mkono uamuzi uliofikiwa na kamati maalum iliyoundwa na Serikali ya Wilaya ya Bagamoyo kwa ajili ya kutafuta suluhu ya kumaliza mgogoro wa ardhi baina ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan na wananchi wa kitongoji cha Uvinje walioanzisha makazi ya kudumu ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadan kinyume cha sheria.

  Kamati hiyo iliyoundwa na wajumbe watatu ambao ni Serikali ya Wilaya ya Bagamoyo, Uongozi wa Kitongoji cha Uvinje na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) kupitia Hifadhi ya Taifa ya Saadan ilifikia maazimio kuwa wananchi wa kitongoji hicho walioanzisha makazi ndani hifadhi hiyo waondolewe kwa utaratibu wa kulipwa fidia ili kumaliza mgogoro huo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana Wilayani Bagamoyo, Mwenyekii wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta Ndetiye alisema baada ya kutembelea eneo hilo wamejiridhisha kuwa Kitongoji hicho cha Uvinje kimeanzishwa ndani ya eneo la hifadhi ambapo ni kinyume cha sheria. 

  "Kiuhalisia tumeona kuna kitongoji ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadan, tumewasikiliza wananchi, tumesikiliza upande wa Serikali, kwa mujibu wa taratibu na sheria wale wananchi wanapaswa watoe ushirikiano, tunaamini kuna taratibu za Kiserikali zinafanywa kuhakikisha wale wananchi wanalipwa ili waondoke kwa usalama" alisema Ndetiye.

  Aliongeza, "tumeona jinsi ambavyo baadhi ya wananchi hawako tayari kulipwa, lakini nadhani wakieleweshwa vizuri wataelewa kuwa ile ni hifadhi ya Taifa, na kama ni hifadhi ya Taifa basi inahusu maslahi ya Taifa, hivyo kila mwananchi anatakiwa atoe ushirikiano ili angalao Serikali ifanye uwekezaji wa kueleweka"

  Ndetiye alisema kamati hiyo imeshaweka maazimio kwa ajili ya kushauri Bunge ili liazimie ni nini kifanywe na Serikali kumaliza mgogoro huo. Alisema, "Kwa udharura wake na kutokana na maelezo ya mkuu wa Wilaya, kwa ujumla kamati inakubaliana nayo kwasababu ameeleza vitu ambavyo tumeona vina tija zaidi kwa watanzania na tunaenda kulishauri Bunge na Serikali haraka iwezekanavyo ili hatua ziweze kuchukuliwa kumaliza mgogoro huo".

  Awali akielezea kuhusu mgogoro huo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga alisema baada ya maazimio ya kamati iliyoundwa na Serikali ya wilaya kumaliza mgogoro huo baadhi ya wananchi walikubali maazimio yaliyowekwa ya kulipwa fidia huku wengine wakikaidi kuondoka akiwemo muwekezaji aliyeshikilia sehemu ya eneo hilo kwa zaidi ya miaka tisa bila kuwekeza mradi uliokusudiwa ambapo wamepewa kipindi cha mwezi mmoja waondoke kwa hiari kabla ya nguvu kutumika kuwaondoa.

  Mwenyekiti wa Kitongoji cha Uvinje,  Hussein Akida alisema kitongoji hicho kilianzishwa ndani ya kijiji cha Saadan katika Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani zaidi ya miaka 100 iliyopita huku kikiwa na ukubwa hekta 3,000 na mpaka sasa Kitongoji hicho kina wakazi wasiopungua 72. Aliiomba Serikali kutambua mipaka ya kitongoji hicho pamoja na kuwasogezea wananchi  huduma za kijamii.

  Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walitilia mashaka uwiano wa kimahesabu wa taarifa hiyo na uhalisia ambapo walihoji iweje kitongoji chenye miaka mingi kiasi hicho kiwe bado hakijapewa hati ya kuwa kijiji kamili pamoja na idadi ndogo ya wananchi wasiongezeka ndani ya muda mrefu wa miaka zaidi ya 100 toka kuanzishwa kwa Kitongoji hicho.

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani alisema, mgogoro huo uko wazi na unapaswa kumalizika mara moja kwa kuwa Serikali ya Wilaya kupitia kamati iliyoundwa imeshafikia maazimio ya kuwaondoa wananchi walioanzisha makazi ndani ya eneo la hifadhi kinyume cha Sheria. Alitoa wito kwa wananchi kutii sheria za hifadhi na kuheshimu mipaka iliyowekwa kuepusha migogoro isiyo ya lazima baina ya Serikali na wananchi.
   Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kushoto) akimkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi atashasta Ndetiye kwa ajili ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadan hususan eneo lenye mgogoro wa ardhi baina ya kitongoji cha Uvinje na Hifadhi hiyo wakati wa ziara ya kamati hiyo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani jana. Wananchi wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa fidia.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta Ndetiye (wa tatu kushoto) akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Uvinje wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kuhusu mgogoro wa ardhi baina ya kitongoji hicho na Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya kamati hiyo wilayani humo jana. Wananchi wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa fidia.Wengine pichani ni Naibu Waziri,Wizara ya Maliasili, Mhandisi Ramo Makani(wa pili kulia) na  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga (kulia).
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kushoto) akiongoza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kutembelea eneo lenye mgogoro baina ya Kitongoji cha Uvinje na Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya kamati hiyo kwenye eneo hilo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani jana. Wananchi wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa fidia. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Ndetiye (wa nne kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Hemed Mwanga (wa pili kushoto).
  Wajumbe wa kamati hiyo wakijadili baadhi ya mambo waliyoyaona katika eneo hilo lenye mgogoro.
   Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mtango Mtahiko ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo  akiwasilisha taarifa ya Shirika hiyo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadan jana wilayani Bagamoyo.
  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Hemed Mwanga (kushoto) akizungumza na wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu mgogoro baina ya kitongoji cha Uvinje na Hifadhi ya Taifa ya Saadan.
  Wajumbe wa kamati wakikagua eneo hilo la mgogoro.
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA),ambaye alikuwa Muhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Saadan Dkt. James Wakibara (kulia) akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Biashara na Utalii wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Imani Nkuwi kandokando ya fukwe  za Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wilayani Bagamoyo jana.
   Baadhi ya maofisa wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wakitembelea fukwe za Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wilayani Bagamoyo jana.
   Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Paschal Shelutete (kushoto) na Katibu wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Gerald Magiri wakitembelea fukwe za Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya kamati hiyo kwenye hifadhi hiyo jana.
   Mwenyekiti wa kitongoji cha Uvinje, Hussein Akida akitoa maoni yake kuhusu mgogoro huo mbele ya kamati ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii jana. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Ndetiye.
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuri (katikati), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Dkt. James Wakibara (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Wizara hiyo, Dkt. Iddi Mfunda wakisikiliza maoni ya wananchi wa kitongoji cha Uvinje katika mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wilayani Bagamoyo jana.
   Baadhi ya wananchi wa kitongoji hicho wakitoa maoni yao mbele ya kamati.
   Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Moses Nnauye (kulia) akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Uvinje wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kuhusu mgogoro wa ardhi baina ya kitongoji hicho na Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya kamati hiyo wilayani humo jana. Wananchi hao ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo wametakiwa kuondoka katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi ambapo watalipwa fidiaNyuma yake kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Ndetiye.
   Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Moses Nnauye (kushoto) akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Uvinje wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kuhusu mgogoro wa ardhi baina ya kitongoji hicho na Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara ya kamati hiyo wilayani humo jana. Wananchi wa kitongoji hicho ambao wameweka makazi ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria wametakiwa kuondoka kwa hiari katika kipindi cha mwezi mmoja kupisha eneo la hifadhi kabda ya kuondolewa kwa nguvu ambapo watalipwa fidia.  Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Ndetiye.

  Nyumba inayodaiwa kuwa ni ya muwekezaji anaeshikilia moja ya eneo katika hifadhi ya taifa ya Saadan kwa madai kuwa alipimiwa eneo hilo na Serikali. Taarifa zilitolewa ni kuwa eneo hilo lilipimwa kiholela bila ya kufuata taratibu za kisheria. Hata hivyo licha ya muwekezaji huyo kutoka nchini Botswana kukaa katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka tisa ameonekana hajaendeleza eneo hilo kwa lengo lililokusidiwa.

  0 0

  Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu akiongoza Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi katika Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyoongozwa na Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu.
  Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu akiwapaka mafuta vijana wa Kipaimara katika Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.
  Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu akiwabariki vijana wa Kipaimara katika Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.
  Baadhi ya Vijana waliopata Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi wakiimba katika ibada .
  Kwaya ya Shirikisho ikiimba katika Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.
  Ndg. Vincent Mubali Jilala akionesha Kitabu alichokiandika kijulikanacho kama “MWANZO WA KUWA TAJIRI “ambacho kimezinduliwa leo na Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu katika Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.
  Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu  akiingia katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi ambapo aliongoza Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (mwenye shati jeupe) na Mkewe Neema Mbiha(kulia) wakifuatilia mahubiri wakati wa Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi iliyoongozwa na Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu.
  Vijana wa Kipaimara (wenye sare ya rangi nyekundu) katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi wakiingia Kanisani kwa ajili ya ibada ya Sakramenti hiyo, ambayo iliongozwa Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu.
  Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu  akizindua Kitabu cha “MWANZO WA KUWA TAJIRI” wakati wa Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi, kilichoandikwa na Muumini wa Kanisa hilo Ndg.Vincent Mabula Jilala.
  Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu (katikati), Paroko wa Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi Padre Kizito Nyanga na Mapadri wengine wakifuatilia Ujumbe wa Mkuu wa Mkoa wakati wa Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.


  …………………………


  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu amewataka Vijana kutokubali kutumiwa kuleta vurugu, chuki na mafarakano hapa nchini.


  Askofu Sangu ametoa wito huo wakati wa Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.“……Maandiko Matakatifu yanasema Vijana wana nguvu; kwa hiyo nawasihi vijana popote pale mlipo muwe chimbuko la Upendo, furaha na amani; watu wengine wasitumie nguvu zenu vijana kuleta chuki, fitina na mafarakano, muwe macho” alisema Askofu Sangu.

  Askofu Sangu amewaasa waumini wa Kanisa hilo kuishi maisha mema ambayo hayatakuwa chanzo cha mateso kwa watu wengine katika familia, jumuiya , jamii wanaoishi na Taifa kwa ujumla.Aidha, amewataka Watanzania wote kupinga na kukemea mauaji ya watu wenye ualbino kwa kuwa wanayo haki ya kuishi kama watu wengine na watu wote wameumbwa kwa mfano wa Mungu.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ametoa wito kwa Kanisa kuwa na mtazamo wa kuisaidia nchi katika kupambana na tatizo la ajira hususani kwa vijana.Ameongeza kuwa ni vema Kanisa liyavae maneno ya Mhe.Rais kuhusu Ujenzi wa Tanzania ya Uchumi wa Kati na kuona namna linavyoweza kushiriki katika kufikia Tanzania Mpya, kwa kuimarisha Idara za Kanisa na Vyama vya Kitume na kuzijenga idara na vyama hivyo katika mtazamo wa Kiujasiriamali.

  “Kanisa lione namna gani WAWATA tulionao wanakuwa WAWATA wa miradi, VIWAWA wanakuwa wa miradi, TYCS wa miradi, lakini sasa Vyama vyetu vya Kitume navyo pia vianze kujielekeza kusaidia Kanisa kwenye eneo la miradi”amesema Mtaka.

  Mtaka amesema upo umuhimu wa kufanya semina za Ujasiriamali kwa vijana, wanawake na Vyama vya Kitume katika Kanisa na waumini wote kwa ujumla ili kuwa na waumini waliojengwa kiuchumi na wanaoendana na mtazamo wa Serikali ya Awamu ya Tano ya kufikia Uchumi wa Kati.

  Akiwa katika Ziara yake Mkoani Simiyu, Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu , Jumamosi Septemba 02 alizindua Parokia mpya ya Mtakatifu Luka iliyopo Mjini BARIADI, sambamba na kutoa kipaimara na leo ametoa kipaimara kwa vijana 164, katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.

older | 1 | .... | 1358 | 1359 | (Page 1360) | 1361 | 1362 | .... | 1897 | newer