Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1360 | 1361 | (Page 1362) | 1363 | 1364 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Kata ya Dutwa(hawapo pichani) Wilayani Bariadi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Igaganulwa wakati wa ziara yake aliyofanya kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
  Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa Kata ya Dutwa (hawapo pichani)katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Igaganulwa wakati wa ziara Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka aliyofanya Wilayani humo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
  Diwani wa Kata ya Dutwa Wilayani Bariadi, Mhe.Mapolu Nunde Mkingwa akizungumza na wananchi wa Kata hiyo (hawapo pichani)katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Igaganulwa wakati wa ziara Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka aliyofanya Wilayani humo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Igaganulwa Kata ya Dutwa (hawapo pichani) Wilayani Bariadi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Kijijini hapo wakati wa ziara yake aliyofanya kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
  Diwani wa Kata ya Sapiwi, Mhe. James Kibuga Wilayani Bariadi akizungumza na wananchi wa Kata ya Dutwa (hawapo pichani)katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Igaganulwa wakati wa ziara Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka aliyofanya Wilayani humo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
  Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi akifafanua jambo katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Igaganulwa wakati wa ziara Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka aliyofanya Wilayani humo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

  ……………………………..

  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amepiga marufuku Halmashauri zote Mkoani humo kutoza ushuru wa biashara ndogondogo zinazofanywa na wananchi kwa kutandika na kupanga bidhaa zao chini au kuuzwa katika mabeseni maarufu kama matandiko.  Mtaka ametoa agizo hilo baada ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Igaganulwa, Mhe.Nhandi Masaka Kachala na baadhi ya wananchi kutoa malalamiko yao kuhusu ushuru huo, wakati wa ziara yake wilayani Bariadi yenye lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi .  Amesema suala hilo lilishatolewa maelekezo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, hivyo Halmashauri zinapaswa kubuni vyanzo vipya vya mapato vyenye tija kwa Halmashauri na wananchi badala ya kutegemea kutoza ushuru unaowakwaza wananchi.  “Kama kuna Halmashauri bado inatoza ushuru wa matandiko wamechelewa sana, kuanzia kesho hamna huo ushuru, kama ninyi mnafikiri mapato ni kutoza tandiko la nyanya, dagaa, mchicha na ninyi kama wakuu wa idara hiki ndicho chanzo mnachokifikiria kichwani hiyo kazi haiwafai, mkatafute kazi nyingine ya kufanya” alisema Mtaka.

  “Halmashauri lazima ibuni chanzo cha mapato chenye tija kwenye Halmashauri na watu. Sasa mtu anahangaika na beseni lake la nyanya wewe unamtoza ushuru, umechangia nini, beseni si lako nyanya si zako” alisema Mtaka.

  Aidha, ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kuhakikisha kuwa inarejesha asilimia Kumi ya mapato yanayokusanywa inayokusanywa kutoka katika vijiji vyote kwenye kila robo mwaka ili Vijiji hivyo viweze kutekeleza mipango ya maendeleo iliyowekwa.

  Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewahamasisha wananchi kuendelea kulima pamba kwa kuwa Serikali imekusudia kujenga kiwanda cha bidhaa ya Afya zitokanazo na zao la pamba mkoani humo na wataalam wanaofanya upembuzi yakinifu wanatarajia kufika Mkoani Simiyu Septemba 20 mwaka huu kuja kuona eneo kitakapojengwa kiwanda.

  Amesema wananchi wasikate tamaa kulima pamba kwa sababu ya matatizo ya kihistoria na kuwaeleza kuwa, Serikali ya Mkoa imepanga mikakati madhubuti ya kuirudisha pamba kuwa dhahabu, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata mbegu bora, dawa, pembejeo zote na suala la bei ya pamba itaanza kujadiliwa mapema.

  Ameongeza kuwa wananchi wasiache kulima mazao jamii ya mikunde hususani choroko na dengu kwa kuwa Serikali inashughulikia suala la upatikanaji wa soko la uhakiki pamoja na kupunguza au kuondoa kabisa madalali katika biashara ya mazao hayo ili wananchi wanufaike kupitia kilimo.

  Akitolea ufafanuzi hoja ya Diwani wa Kata ya Ikungulyabashashi Mhe.Bupi Maduhu Litunga ya kupimiwa maeneo, Mkuu wa Mkoa huyo wa Mkoa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Bariadi kupitia Idara ya Ardhi, kuitisha mikutano katika Vijiji vyote ambavyo wananchi wanahitaji kupimiwa maeneo na baadae awasilishe mihutasari ya vikao hivyo Ofisini kwake tarehe 13/09/2017.

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amekamilisha ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ambapo amesikiliza na kutatua kero za wananchi katika sekta ya Elimu,Afya, Kilimo, Mifugo, Ardhi, Ujenzi, Biashara na Uchumi pamoja na suala la utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA) ambazo amezitolea maelekezo na ameahidi kufuatilia utekelezaji wake.

  0 0


  Na Adili Mhina.

  Taasisi ya Kimataifa ya Kupunguza Umaskini China (IPRCC) imeahidi kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano baina yake na Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Tume ya Mipango kwa lengo la kuongeza kasi ya maendeleo na kupunguza umaskini nchini.

  Uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha wataalamu kutoka Wiraza ya Fedha na Mipango kupitia Tume ya Mipango wakiongozwa na Kaimu Katibu Mtendaji Bw. Maduka Kessy na ujumbe kutoka taasisi hiyo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza katika kikao hicho kiongozi wa ujumbe kutoka China Bw. Xia Gengsheng alieleza kuwa maeneo mapya yanayotarajiwa ni pamoja na kuanzisha vituo vingingine vya mfano vya kilimo katika vijiji mbalimbali hapa nchini.

  Bw. Xia alieleza kuwa wameamua kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano kutokana na mafanikio yaliyojitokeza katika juhudi za kupambana na umaskini nchini hususan katika kutoa elimu ya kilimo kwa wakulima kupitia kuanzishwa kwa Kijiji cha mfano cha Peapea Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.

  “Ndugu Kaimu Katibu Mtendaji naomba nikuhakikishie kwamba tutaanzisha vijiji vingine vya mfano kama kile cha Peapea na kutoa fursa kwa wananchi wengi zaidi kujifunza mbinu bora za kilimo ili waweze kuendesha kilimo chenye tija na waondokane na umaskini,” alieleza Bw. Xia.

  Eneo jingine la ushirikiano litakalo anzishwa ni masuala ya utafiti ambapo IPRCC kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Tume ya Mipango na taasisi zingine itawezesha kufanyika kwa tafifi katika kuchochea maendeleo na kutafuta mbinu mbalimbali za kupunguza kasi ya umaskini.

  Kwa upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Maduka Kessy alieleza kuwa ushirikiano kati ya Tume ya Mipango na Taasisi ya IPRCC ambao umedumu kwa zaidi ya miaka sita umekuwa na faida kubwa katika kukabiliana na umaskini kwa watanzania.

  Alielezea kuwa kwa kipindi hicho Tume ya Mipango na IPRCC wamefanikiwa kuendesha programu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuratibu mazungumzo ya kisera juu ya mageuzi ya kilimo vijijini na kupunguza umaskini, kuanzishwa kwa kituo cha mfano katika kupunguza umaskini kwa wakulima wadogo Kilosa Mkoani morogoro.

  Aliongeza kuwa ushirikiano kati ya Tume ya Mipango na IPRCC umefanikisha uratibu wa programu za kuwajengea uwezo watanzania kwa kutoa udhamini wa masomo katika ngazi za uzamili na uzamivu katika fani za maendeleo vijijini pamoja na kuandaa mafunzo mbalimbali yanayohusu mageuzi ya kilimo kwa maafisa kilimo pamoja na wakulima wenyewe.

  Pamoja na mambo mengine, Taasisi ya Kimataifa ya Kupunguza Umaskini ya China imekuwa ikisaidia kutoa msaada wa kitaaalamu ambapo wataalamu wa kilimo kutoka China wamekuwa wakitoa mafuzo kwa wakulima mkoani Morogoro.
   Kaimu Katibu Mtendaji, Wizara ya Fedha na Mipango – Tume ya Mipango Bw. Maduka Kessy (wa tatu kutoka kushoto, mwenye tai nyekundu) na kiongozi wa ujumbe kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Kupunguza Umaskini China, Bw. Xia Gengsheng (wanne kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka China na viongozi wa Tume ya Mipango.
  Wataalamu kutoa Tume ya Mipango wakiwa katika kikao na Ujumbe kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Kupunguza Umaskini China (hawapo pichani).
  Ujumbe kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Kupunguza Umaskini China wakiwa katika kikao na wataalamu wa Wizara ya Fedha na Mipango – Tume ya Mipango (hawapo pichani) katika ofisi za Tume ya Mipango, jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Katibu Mtendaji, Wizara ya Fedha na Mipango – Tume ya Mipango Bw. Maduka Kessy (katikati), Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi Bw. Paul Sangawe (kulia) na Kaimu Naibu Katibu Mtendaji anayesimamia Klasta ya Huduma za Jamii na Idai ya Watu, Tume ya Mipango, Bw. Ibrahim Kalengo (kushoto) wakimsikiliza mjumbe (hayupo pichani) kutoka China wakatika wa kikao.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na wasimamizi wa miradi ya kutoa ajira za muda kwa wanufaika wa mpango wa Tasaf kutoka halmashauri na manispaa ya Singida wakati akifungua mafunzo ya uwezeshaji wa kusimamia miradi hiyo.
  Wasimamizi wa miradi ya kutoa ajira za muda kwa wanufaika wa mpango wa Tasaf kutoka halmashauri na manispaa ya Singida wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Singida (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya uwezeshaji wa kusimamia miradi hiyo.
  Mratibu wa Tasaf Mkoa wa Singida Patrick Girigo Kasango akiwa na Afisa Ufuatiliaji kutoka Tasaf Sinith Haule wakifurahia jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uwezeshaji wa kusimamia miradi ya ajira za muda kwa wasimamizi wa kutoka halmashauri na manispaa ya Singida.
  Ramadhani Alute kutoka kata ya Minga manispaa ya Singida akiandika baadhi ya mambo katika mafunzo ya uwezeshaji wa kusimamia miradi ya ajira za muda kwa wasimamizi wa kutoka halmashauri na manispaa ya Singida.


  …………….

  Wanufaika wa mpango wa Kunusuru kaya masikini Tasaf, Mkoa wa Singida wametakiwa kupanda mikorosho ili waweze kutunza mazingira pamoja na kujiongezea kipato kutokana na zao la korosho.

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ametoa rai hiyo wakati akifungua mafunzo ya uwezeshaji kwa wasimamizi 67 wa miradi ya kutoa ajira za muda kwa wanufaika wa mpango wa Tasaf kutoka halmashauri na manispaa ya Singida.

  Dkt Nchimbi amesema kutokana na kuwa ajira za muda kwa awamu hii zimelenga katika utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti hivyo amewataka Tasaf mkoa wa Singida kuwasiliana na Bodi ya Korosho waweze kupatiwa mbegu ili isipandwe miti mingine bali mikorosho.

  Amesema kwa kufanya hivyo mkoa wa Singida utaweza kuwa mzalishaji mkubwa wa Korosho huku ajira hiyo ya muda ya kutunza mazingira kwa kupanda mikorosho, ikiwa imewatengenezea wanufaika hao ajira yao ya kudumu.

  “Tukiweza kupanda mikorosho kwa zoezi hili la ajira za muda baada ya muda wanufaika hawa wataweza kuwa na kipato kikubwa kwa kuweza kuuza korosho zao, hii itakuwa ndio maana halisi ya mpango wa kunusuru kaya masikini ambapo zinatakiwa pia zishiriki katika kukuza uchumi”, amesema na kuongeza kuwa,

  “Katika kuelekea Tanzania ya uchumi wa kati wa viwanda haimaanishi kila mtu afungue kiwanda bali kila mwananchi asiachwe nyuma katika kufanikisha uwepo wa viwanda, kwa maana hiyo hawa wanufaika watasaidia uwepo wa viwanda kutokana na malighafi ya korosho watakayoilima”, amefafanua.

  Dkt Nchimbi ameongeza kuwa miradi ya ajira za muda itafanikiwa endapo itaweza kuwajengea uwezo wanufaika hao wa kutambua fursa za kujiajiri na sio kupokea fedha na kuzitumia kisha kurudi katika umasikini ule ule.

  Aidha amewataka watumishi wa umma wasiwafundishe wanufaika hao kulalamika kuwa fedha ni ndogo kama ambavyo wao wamekuwa wakilalamikia mishahara, bali wajifunze kwa wanufaika ambao wameweza kuanzisha miradi kama ufugaji kuku, kilimo cha bustani kutokana na fedha ndogo wanayopata.

  Kwa upande wake Mratibu wa Tasaf Mkoa wa Singida Patrick Girigo Kasango amesema mpango wa ajira za muda kupitia Tasaf unafanyika katika halmashauri nne kati ya saba kwa Mkoa wa Singida ambazo ni halmashauri ya Singida, manispaa ya Singida, Malakama na Iramba.

  Kasango amesema kwa awamu hii ajira za muda zimelenga katika kutunza mazingira kwa kupanda miti, kutengeneza mabwawa ya maji na kuzuia mmomonyoko wa udongo.

  Ameongeza kuwa ajira hizo hufanyika kipindi ambacho si cha kilimo pia wanufaika hao watafanya kazi kwa muda wa masaa manne kwa muda wa siku sitini ambapo watakuwa wanalipwa kiasi cha shilingi 2300 kwa masaa hayo.

  Girigo amesema wasimamizi 27 kwa Manispaa ya Singida, 40 halmashauri ya Singida, 41 Mkalama na 42 Iramba watapewa mafunzo kwa siku sita pamoja na mafunzo kwa vitendo yatakayowawezesha kusimamia vema ajira za muda.

  Naye mmoja wa washiriki amesema mara baada ya mafunzo hayo wasimamizi hao wakatoe mafunzo kwa wanufaika waweze kutumia fursa ya ajira za muda na fedha watazopata kwa kujiendeleza kiuchumi.

  Ramadhani Alute kutoka kata ya Minga manispaa ya Singida amesema watajitahidi kuwaelekeza vizuri wanufaika hao ili wasizitumie vibaya fedha hizo bali wawekeze hicho watakachopata kwa manufaa ya baadaye.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

  Baada ya jeshi la Polisi kumaliza mahojiano yao dhidi ya mshtakiwa  Yusuf Manji na wenzake watatu juu ya tuhuma zinazowakabili za uhujumu uchumi, mapema leo wamemkabidhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kama ilivyoamriwa Jana.

  Mbali na Manji ambaye ni mfanyabiashara maarufu nchini, washitakiwa wengine waliokabidhiwa ni Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Quality Group Ltd, Deogratius Kisinda, Mtunza stoo, Abdallah Sangey na Thobias Fwere.
   
  Akiwakabidhi watuhimiwa hao, wakili wa serikali mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa washtakiwa hao wamerudishwa mahakamani kama ilivyoamuriwa, baada ya polisi kumaliza kuwahoji.
  Baada ya washtakiwa kukabidhiwa wakiwa salama na afya zao nzuri, Hakimu Shaidi alisema kesi hiyo itaendelea na utaratibu kama ulivyokuwa awali, ambapo itatajwa September 8/2017.

  Jana mchana mahakama hiyo iliruhusu Manji na wenzake kwenda kuhojiwa na Polisi  ili kukamilisha upelelezi katika kesi ya uhujumu uchumi.

  0 0

   Uzinduzi huu wa viatu vya SULTAN klabu ya GENTLEMAN ya Jack Daniel ulibarikiwa na viongozi wa serikali, wanamzuziki, wanamitindo, wabunifu, waigizaji na watu wengi mashuhuri.
   Mshindiwa Big brother Afrika 2014 Idris Sultan amezindua viatu vyake viitwavyo SULTAN by FOREMEN akiwa pamoja na klabu ya GENTLEMAN ya Jack Daniel. Uzinduzi huu ulifanyika pamoja kama namna ya kuwaunganisha wanaume wa Tanzania kuwa sehemu ya viatu hivi maalum na umoja endelevu.
   SULTAN by FORMEN ni chapa ya viatu iliyotengenezwa kwa kuzingatia unadhifu, ubora, starehe (comfort) na hadhi ya uzito wa viatu vya mwanaume wa kitanzania.
  “Tumetengeneza dizaini tofauti zit akazoingia sokoni kubadilisha ulimwengu wa fasheni katika usafi, unadhifu, furahanauchangamfu. Aina hii ya viatu inawakilisha mwanaume wa kitanzania anayefanya kazi zake kwa bidii, kwa ubunifu akiwa na muonekano wa tofauti unaopendeza” asema Idris.
   Chapa hii ya SULTAN by FOREMEN ni mafanikio mapya kwa Idris ukiacha mafanikio yake mengine aliyoyapata hivi karibuni kama kuchaguliwa kuigiza katika movie ya Hollywood marekani itakayogharimu takribani dola million 5. 
  Idris ambaye alifanikiwa kukonga nyoyo za mashabiki wa filamu Tanzania baada ya kushiriki katika filamu ya KIUMENI ambayo imeshinda tunzo mbili katika tamasha la filamu la ZIFF
  Idris ni mchekeshaji na kijana maarufu anayependa kuvaa vizuri na kwenda na wakati hivyo atauza viatu hivi kwa bei nafuu ilikila mtanzania aweze kuvimudu.


  0 0


  Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, hati ya mashtaka ya kesi ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo dhidi ya mfanyabiashara Yusuf Alli maarufu kama mpemba wa Magufuli’ inatarajiwa kupelekwa Mahakama ya mafisadi.

  Hayo yameelezwa na wakili wa serikali, Elia Athanas mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa. "Mheshimwa, jalada la kesi hii limekamilika, hivyo naomba muda ili wapeleke hati ya mashtaka Mahaka Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi 'Mahakama ya Mafisadi'.

  Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi September 19/2017.

  Yusuf anashtakiwa pamoja na Charles Mrutu, mkazi wa Mlimba, Morogoro, Benedict Kungwa, mkazi wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima, mkazi wa Mbezi, Ahmed Nyagongo, dereva na Pius Kulagwa, wanakabiliwa na mashitaka manne ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh.milioni 785.6.

  Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari, 2014 na Oktoba, mwaka huu wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, walijihusisha na mtandao wa ujangili kwa kukusanya na kuuza nyara za serikali ambazo ni

  vipande 50 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Dola za Marekani 180,000 sawa na Sh milioni 392.8 bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.
  Watuhumiwa hao wakiwa katika viunga vya Mahakama ya Kisutu,mapema leo kwenye kesi yao ya kudaiwa  kujihusisha na biashara ya meno ya tembo,ambayo kwa sasa inatarajiwa kupelekwa Mahakama ya mafisadi.

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa salaamu za pole za Serikali na Wizara yake leo Jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga mwili wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa heshima za mwisho leo Jijini Dar es Salaam kwa mwili wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.

  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akitoa heshima za mwisho leo Jijini Dar es Salaam kwa mwili wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.

  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bibi Sophia Mjema akitoa heshima za mwisho leo Jijini Dar es Salaam kwa mwili wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.  Mkuu wa Wilaya ya Handeni Bw.Godwin Gondwe akizungumza wakati wa kuaga mwili wa mkuu wa wilaya mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.
  Mtoto wa marehemu Muhingo Rweyemamu Bw. Emmanuel Muhingo akisoma wasifu wa baba yake aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan wakati wa kuagwa leo Jijini Dar es Salaam .
  Baadhi ya waombolezaji wakifuatilia tukio la kuaga mwili wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.


  …………………..


  Na Shamimu Nyaki-WHUSM


  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe ameongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari, marehemu Muhingo Rweyemamu aliyefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.


  Akitoa salamu za pole kwa niaba ya Serikali na Wizara yake leo Jijini Dar es Salaam, Mhe. Mwakyembe amemuelezea marehemu Rweyemamu kuwa alikua mtumishi mzuri katika Serikali hasa katika wadhifa wake wa Ukuu wa Wilaya na mara zote alihakikisha Wananchi anaowaongoza wanakuwa wachapakazi kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.


  “Serikali inatoa pole sana kwa familia na wanatasnia ya habari kwani marehemu Rweyemamu ameacha pengo kubwa kwa familia yake na wanahabari kutokana na uhodari wake katika uandishi lakini pia Serikali inakumbuka uchapakazi wake alipokua Serikalini. Tunaomba Mungu awape faraja na uvumilivu wafiwa wote”. Alisema Mhe. Mwakyembe.


  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe amemuelezea marehemu kuwa alikuwa mchapakazi hodari wakati alipokuwa Mkuu wa Wilaya hiyo na Wananchi wa Handeni watamkumbuka katika jitihada zake za kuhimiza watoto wa kike kupenda shule ambapo alianzisha kampeni iliyoitwa “niache nisome” lengo likiwa ni kuelimisha umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike.


  “Wananchi wa handeni wamesikitishwa sana na kifo hiki kwani wanakumbuka uhodari wake katika kuwatumikia alipokuwa mkuu wa Wilaya yao hasa juhudi zake za kuhimiza jamii kupeleka watoto shule kwa manufaa yao ya baadae”. Alisema Mhe. Gondwe”.


  Naye mwakilishi kutoka vyombo vya habari Bw. Absolum Kibanda amesema kuwa marehemu alikuwa mwalimu na mshauri mzuri katika tasnia ya habari na alikuwa anaipenda kazi yake na kufanya waandishi wengi kuiga na kujifunza kutoka kwake uandishi wa habari za uchunguzi na makala.


  Marehemu Muhigo Ryeyemamu amewahi kufanya kazi katika magazeti ya mbalimbali hapa nchini ikiwemo Mtanzania, Mwananchi, Rai, The Citizen akitumikia nyadhifa mbalimbali kama mhariri na mwandishi. Marehemu amezikwa leo katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam na ameacha mke,watoto wanne na mjukuu mmoja.

  0 0

   Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (kushoto) akizungumza na Wenyeviti wa Bodi za Mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali pamoja Watendaji Wakuu wa taasisi hizo (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kuweka saini mkataba wa utendaji kazi kwa taasisi hizo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
   Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda (wa pili kulia) wakiweka saini katika mkataba wa utendaji kazi mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu toka Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Michael John na kulia ni Kaimu Meneja wa Sheria toka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi. Martha Charles.
   Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (wa pili kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda (wa pili kulia) mkataba wa utendaji kazi mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu toka Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Michael John na kulia ni Kaimu Meneja wa Sheria toka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi. Martha Charles.
   Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Bi. Gaudensia Kabaka (kulia) wakiweka saini katika mkataba wa utendaji kazi mapema hii leo jijini Dar es Salaam. 
  Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Bi. Gaudensia Kabaka (kulia) mkataba wa utendaji kazi mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Wenyeviti wa Bodi za Mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali pamoja Watendaji Wakuu wa taasisi hizo wakimsikiliza Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuweka saini mikataba ya utendaji kazi kwa taasisi na Mashirika ya Umma mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

  Na.Bushiri Matenda-MAELEZO
  Ofisi ya Msajili wa Hazina inasema kuwa Taasisi na Mashirika ya Umma sasa rasmi kutekeleza mkakati wa utendaji kazi ili kujiendesha na kutoa gawio kwa Serikali yenye lengo la kuchochea maendeleo kwa taifa na kuendelea kuboresha huduma bora za kijamii.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Msajili Mkuu wa Hazina Dkt.Oswad Mashindano wakati wa hafla ya kutia saini mkataba wa utendaji kazi baina  ya Msajili wa Hazina na baadhi ya Wenyeviti wa bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma nchini. 
  “Ofisi ya Hazina inasimamia Taasisi mbalimbali takribani 265, ni vyema Taasisi hizo kwa kushirikiana kwa pamoja zikasimamiwa vizuri ili kutoa huduma endelevu na kuchangia katika uwekezaji wenye tija kwa taifa”,alisema Dkt.Mashindano.

  Aidha alisema kuwa mwaka 2014-2015 Ofisi ya msajili wa hazina walifunga mkataba naTaasisi na Mashirika ya Umma 71 kati ya 265 ambapo mkataba huo ulilenga katika maeneo  manne ya kiutendaji ambayo ni usimamizi katika rasilimali fedha , watu, utawala bora na huduma kwa wateja.

  Dkt. Mashindano aliongeza kuwa Katika tathmini ya mkataba uliopita kupitia nyaraka  mbalimbali , uchambuzi umeonyesha kuwa  zipo baadhi ya dosari katika utekelezaji wa makubaliano  ya awali  ambazo alizitaja kuwa asilimia 25 ya mpango mkakati  waliojiwekea Taasisi na Mashirika hayaendani na  bajeti  waliojiwekea.

  Pili malengo yaliyobainishwa na Taasisis hizo  hayaendani na mpango kazi , maeneo ya ya usimamizi wa rasilimali watu na utawala bado kuna changamoto, eneo la ukusanyaji mapato katika baadhi ya Taasisi bado ni ndogo pamoja na  eneo la Huduma kwa wateja linahitaji kusimamiwa ipasavyo na kuwepo kwa baadhi ya Taasisi na Mashirika ya Umma kujaza matokeo ya kazi ambazo hazipo kwenye utekelezaji wa mapango kazi.

  “Katika utiaji wa  sahihi, mkataba huu unaohusisha zaidi ya Taasisi na Mashirika 30  naamini tutazingatia kutatua changamoto zilizopo na kuweka mpango wa maendeleo endelevu”, alisisitiza Dkt. Mashindano.

  Naye spika wa bunge mstaafu ambaye pia ni mwenyekiti wa Bodi wa Mfuko wa bima wa afya Bi. Anna Makinda  alitoa neno kwa niaba ya wenyeviti wa Bodi wa Taasisi na Mashirika ya Umma alisema  ni vizuri tukatatua changamoto zilizojitokeza katika uendeshaji wa mashirika ya Umma ili yajiendeshe kwa tija na maslahi ya Taifa.

  “Watendaji wakuu wa Taasisi za Umma na wenyeviti wa Bodi tunawajibishwa na makubaliano haya, tunategemewa sana katika kuwaletea maendeleo wananchi na Taifa kwa ujumla”, alisema Bi. Makinda. 
  Aliongeza kuwa Taasisi za vyuo vikuu vilivyoingia makubaliano haya watawajibika katika kuwatayarisha vijana katika kuliletea Taifa maendeleo.  
  Wenyeviti wa Bodi na watendaji wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma wanatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia miongozo iliyopo taratibu na Sheria zilizopo kwa kushirikiana na Ofisi ya Hazina ili kuleta tija kwa watumishi wengine katika Taasisi za Umma. 
  Mbali na majukumu iliyonayo Ofisi ya Msajili wa Hazina pia inasimamia katika masuala yote ya uwekezaji nchini, mitaji, malipo mbalimbali ikiwemo mishahara kwa watumishi wa Umma.

  0 0

   Mgeni rasmi katika uzinduzi wa huduma mpya ya HaloYako ya Kampuni ya Simu ya Halopesa kwa kushurikiania na Finca Microfinance Bank, Kamishna  wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, John Rubuga (katikati) akiwa pamoja na Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Halotel Tanzania, Le Van Dai (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Finca Microfinance Bank, Issa Ngwegwe wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo, uliofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena, Jijini Dar es salaam Septemba 5, 2017.

  Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo, Mgeni rasmi ambaye alimuwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, John Rubuga amesema kuwa serikali imeendelea kutengeneza mazingira rafiki ya uwekezaji kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo ili kurahisisha huduma na kutatua changamoto zinazowakabili Watanzania hususan katika maendeleo ya kiuchumi.

   “Serikali iko tayari kushirikiana na kampuni mbalimbali zenye malengo ya kuondoa umaskini kwa watanzania kwa kukuza kipato chao ili kuboresha maisha. Tunaamini pia kupitia huduma hii ya Haloyako Watanzania wengi zaidi ambao hawatumii huduma za benki wanaweza kutumia ili kuweza kufanikisha malengo yao ya kifedha,” alisema na kuongeza kuwa “Halotel na FINCA wana malengo sawa, ambayo wanalenga kuwasaidia watanzania wenye hali ya chini na wakati ambao wengi wao wako maeneo ya vijijini, ni Imani yetu kuwa ushirikiano huu utakuwa na manufaa makubwa kwa jamii ya Watanzania na tutajenga utamaduni wa kujiwekea akiba”.
  Aidha, amezitaka kampuni hizo kuhakikisha zinatoa elimu ya kutosha ili Watanzania waweze kuelewa umuhimu wa huduma hiyo na kuweza kuitumia vyema huku akitoa wito kwa jamii ya Watanzania kuepuka kuhifadhi hela ndani na kujenga utamaduni ya kujiwekea akiba.

  Kwa upande wa Halotel, Mkurugenzi Mtendaji wake, Le Van Dai alisema “Tunashukuru sana kwa uhusiano huu ambao tumeujenga kati yetu na FINCA ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakitoa huduma za kifedha kwa jamii ya Watanzania, Kwa uapnde wetu sisi hii ni hatua kubwa sana katika kuhakikisha tunatatua changamoto ya huduma za kifedha kwa Watanzania, Tumejitahidi kwa kiasi kikubwa kuhakikisha hatuishii kuwa tu kampuni ya Mawasiliano ila tunataka kuwa kampuni inayoishi maisha ya Watanzania”

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Finca, Issa Ngwegwe Aliongeza kuwa lengo kubwa ya FINCA ni kutoa suluhisho la kutokomeza umaskini kwa kusaidia watu kujenga mitaji, kutengeneza ajira na kuboresha maisha.

  “Haloyako sio tu huduma ya kifedha kupitia simu ya mkononi bali ni akaunti ya akiba ya malengo ambayo itakuwa jibu kwa Watanzania ambao wanataka huduma za kifedha ili kuweza kuweka akiba kutimiza mahitaji yao ya kifedha kama vile kulipa karo, kodi ya nyumba, kuwekeza, kulipia huduma za afya na pia kusafiri, Kupitia Haloyako mteja anaweza kuweka mipango na kuanza kuweka akiba ili kutimiza lengo lake na hivyo kuepuka madeni au kushindwa kukidhi mahitaji ya kifedha ya familia.  Alihitimisha Ngwegwe.

  Huduma ya HALOYAKO inapatikana kupitia huduma ya HALOPESA inayotolewa na kampuni ya mawasiliano ya Halotel ambayo ni huduma ya kifedha inayomwezesha mteja kutuma na kupokea fedha kwa urahisi na kwa usalama.
  Mgeni rasmi katika uzinduzi wa huduma mpya ya HaloYako ya Kampuni ya Simu ya Halopesa kwa kushurikiania na Finca Microfinance Bank, Kamishna  wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, John Rubuga (katikati) akiwa pamoja na Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Halotel Tanzania, Le Van Dai (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Finca Microfinance Bank, Issa Ngwegwe wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo, uliofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena, Jijini Dar es salaam Septemba 5, 2017.
  Picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi
  Picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Kampuni ya ya Halotel na Finca Microfinance Bank.

  0 0

   Mshindiwa Big brother Afrika 2014 Idris Sultan amezindua viatu vyake viitwavyo SULTAN by FOREMEN akiwa pamoja na klabu ya GENTLEMAN ya Jack Daniel. Uzinduzi huu ulifanyika pamoja kama namna ya kuwaunganisha wanaume wa Tanzania kuwa sehemu ya viatu hivi maalum na umoja endelevu.
   SULTAN by FORMEN ni chapa ya viatu iliyotengenezwa kwa kuzingatia unadhifu, ubora, starehe (comfort) na hadhi ya uzito wa viatu vya mwanaume wa kitanzania.
  “Tumetengeneza dizaini tofauti zit akazoingia sokoni kubadilisha ulimwengu wa fasheni katika usafi, unadhifu, furahanauchangamfu. Aina hii ya viatu inawakilisha mwanaume wa kitanzania anayefanya kazi zake kwa bidii, kwa ubunifu akiwa na muonekano wa tofauti unaopendeza” asema Idris.
   Chapa hii ya SULTAN by FOREMEN ni mafanikio mapya kwa Idris ukiacha mafanikio yake mengine aliyoyapata hivi karibuni kama kuchaguliwa kuigiza katika movie ya Hollywood marekani itakayogharimu takribani dola million 5. 
  Idris ambaye alifanikiwa kukonga nyoyo za mashabiki wa filamu Tanzania baada ya kushiriki katika filamu ya KIUMENI ambayo imeshinda tunzo mbili katika tamasha la filamu la ZIFF
  Idris ni mchekeshaji na kijana maarufu anayependa kuvaa vizuri na kwenda na wakati hivyo atauza viatu hivi kwa bei nafuu ilikila mtanzania aweze kuvimudu.
   Uzinduzi huu wa viatu vya SULTAN klabu ya GENTLEMAN ya Jack Daniel ulibarikiwa na viongozi wa serikali, wanamzuziki, wanamitindo, wabunifu, waigizaji na watu wengi mashuhuri.


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Jinsia linalofanyika kwenye viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao Dkt. Vicensia Shule (kushoto) wakati wa sherehe za uzinduzi wa Tamasha la Jinsia lililoandaliwa na TGNP Mtandao. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea tuzo ya Uongozi kwa kuwa Makamu wa Rais wa Kwanza Mwanamke na kutambua mchango wake katika kusimamia na kuhamasisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake kutoka kwa mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao Dkt. Vicensia Shule (kushoto) wakati wa sherehe za uzinduzi wa Tamasha la Jinsia lililoandaliwa na TGNP Mtandao.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amezindua Tamasha la 14 la Jinsia lililoandaliwa na TGNP Mtandao 

  Makamu wa Rais amesema Serikali imechukua hatua mbali mbali ili kumuwezesha mwananke kujikomboa kiuchumi, ikiwa pamoja na kuanzisha Benki ya Wanawake Tanzania, kuanzisha mifuko mbali mbali ya uwezeshaji ukiwemo mfuko wa Maendeleo ya Wanawake pamoja na kuhamasisha uanzishwaji wa SACCOS na VICOBA na vikundi vingine vya kiuchumi pia serikali iliagiza Asilimia 30 ya zabuni za serikali zipewe wanawake, vile vile iliagiza halmashauri zote kutenga asilimia 5 ya mapato kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya wanawake.

  Alisema “ Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua na kuthamini umuhimu wa uzingatiaji wa masuala ya jinsia katika kuchangia na kuharakisha  maendeleo ya nchi”.

  Mhe. Samia alitoa wito kwa wadau wa maendeleo  kushirikiana katika kuhakikisha Tanzania kama nchi tunafikia lengo namba 5 la ajenda ya Maendeleo Endelevu na Ajenda ya mwaka 2063 ya Afrika ya kuhakikisha Mwanamke ana haki sawa na mwanaume katika Nyanja zote za kijamii na haachwi nyuma kwenye maendeleo.

  Makamu wa Rais alisisitiza ni muhimu kwa Wizara, Idara na Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuzingatia vipaumbele vya kijinsia kwenye mipango yake ya bajeti.

  Makamu wa Rais alisema ili kufikia usawa wa kijinsia lazima mwanamke apewe mbinu za kumuezesha kiuchumi na lazima alindwe  na vitendo vya ukatili wa kijinsia ili aweze kusimama imara kwenye majukumu yake mbali mbali.

  Makamu wa R­­ais alihimiza pia Wanawake kusaidiana na kuinuana ili kufikia malengo .
  Mwisho Makamu wa Rais aliwapongeza TGNP na Kamati ya Kitaifa ya kuweka kumbukumbu za wanawake kwa ajili ya kuwatambua, kuwaenzi na kuweka kumbukumbu za michango ya wanawake katika nyanza mbali mbali za maendeleo.


  0 0

  Timu ya JKT mlale inayoshiriki ligi daraja la kwanza kutoka mkoa wa ruvuma watamba kufanya vizuri kwenye kundi lake latika msimu huu wa ligi. hii inatokana baada ya kumfunga majimaji bao moja kwa bila katika mchezo wa kirafiki uwanja wa majimaji mjini SONGEA.

  0 0

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma

  Serikali imewataka watumishi wa Mikoa, Halmashauri na vituo vya kutolea huduma na kutoa taarifa za mapato na matumizi kwa wakati kwa wananchi katika maeneo yao.
  Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa wakati akizindua Mfumo wa Kielektroniki wa Kuandaa Mipango, Bajeti na Ripoti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) iliyoboreshwa na Mfumo Mpya wa Uhasibu na Utoaji Taarifa (FFARS) leo mjini Dodoma.

  “Ukamilishaji wa mifumo hii utasaidia kuongeza uwazi, uwajibikaji kwa watumshi hasa katika eneo la mapokezi na matumzi ya fedha za umma kuanzia katika vituo vya kutolea huduma mpaka ngazi ya Halmashauri”.

  “Kuanzia sasa sitegemei kuona kituo chochote cha kutolea huduma kilichopo chini ya Halmashauri kinakuwa na matumizi yasiozingatia taratibu na kanuni za fedha au kubadilisha matumizi ya fedha bila kuwasiliana na Mamlaka husika” amesisitiza Waziri Mkuu.

  Aidha, alisema kuwa lengo la matumizi ya mifumo ya TEHAMA ni kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utendaji kazi wa shughuli za Serikali na zisitumike kukwamisha shughuli na utaratibu wa kazi za Serikali.

  Vilevile, Waziri Mkuu alisema kuwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa kipindi kirefu imekuwa ikitumia gharama kubwa, muda mwingi katika kukamilisha zoezi zima la uandaaji wa Mipango, Bajeti. Hivyo kupitia mfumo changamoto hizo zimetatuliwa.

  Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI George Simbachawene amesema kuwa kupitia mfumo huo umeweza kuokoa zaidi ya Shilingi Bilioni nne gharama ya Serikali zilizokuwa zikitumika kila mwaka kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kuandaa bajeti.

  “Mifumo hii itasaidia kutaleta ufanisi na uwajibikaji katika utekelezaji wa huduma kwa wananchi, utasaidia kupunguza muda na kuleta maendeleo kwa kasi na pia utasaidia kutunza taarifa ya mapato yote katika ngazi ya Halmashauri” ameongeza George Simbachawene.

  Naye Kaimu Balozi wa Marekani nchini Imni Patterson amesema kuwa pamoja mifumo hiyo itaongeza ufanisi na kuboresha usimamizi wa fedha na kuwezesha Serikali ya Tanzania kutoa fedha kwa malengo yaliyokusudiwa na mahitaji ya wananchi kwa ufasaha.

  “Marekani inajivunia kushirikiana na Tanzania, mnapofanya kazi kwa malengo ya kuwa na Serikali yenye uwazi, maendeleo endelevu na ustawi wa pamoja” amesema Kaimu Balozi wa Marekani nchini.

  Akitoa salamu, Mkurugenzi wa Mradi wa PS3 Dkt. Emmanuel Malangalila amesmea kuwa mifumo hiyo imeundwa na kutengenezwa na vijana wa Kitanzania kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI wakishirikiana na watumishi wa mradi wa uimarishaji wa mifumo ya sekta ya umma (PS3).

  “Mifumo hii miwili itaimarisha uwazi, uwajibikaji na ufanisi wa matumizi ya fedha katika Halmshauri na ngazi za vituo vya kutolea huduma na hivyo utoaji wa huduma kwa wananchi kuboreka zaidi” amesema Dkt. Malangalila.

  Mradi wa uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) ni mradi wa miaka mitano ulioanza Julai 2015 na kumalizika 2020 na unafanya kazi katika Halmashauri 93 katika mikoa 13 Tanzania Bara ikiwa na lengo la kutoa msaada wa kitaalamu kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Serikali katika ngazi ya Taifa na Halmashauri ili kuboresha utoaji wa huduma za jamii.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo ametembelewa Ofisini kwake na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zuber na kufanya Mazungumzo.

  Katika Mazungumzo hayo Mufti amemtia Moyo Makonda na kumsihi asikate tamaa sababu kazi anayoifanya ni Njema na inagusa watu wa makundi  yote hususani Wanyonge.

  Aidha Mufti amemuunga mkono RC Makonda kwa kumletea mdau atakaejenga Ofisi za Walimu kwenye Shule tatu.

  "Nimeona nisikae kimya ndio maana nimeona niunge mkono Kampeni yako ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu kwa kutafuta mdau ambae atajenga Ofisi kwenye Shule Tatu ili Walimu wafanye kazi kwenye mazingira mazuri" Alisema Mufti.

  Makonda amemshukuru Mufti kwa kumtembelea na kusema kuwa ataendelea na jitiada zake za kufanya kazi kwa bidii ilikutatua changamoto za Wakazi wa Dar es salaam.

  Aidha Makonda amewaomba Viongozi wa Dini na Vyama vya Siasa kujitoa kwa pamoja ili kuijenga Dar es Salaam

  0 0


  José Graziano da Silva mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula Dunia (FAO) akiongea na wenyeji wake baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam leo kwa ziara ya kikazi. Kushoto ni Mwenyeji wake Mwakilishi mkazi wa FAO, Fred Kafeero. (Imreandaliwa na Robert Okanda Blogspot)

  José Graziano da Silva Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Dunia (FAO) akitambulishwa kwa Katibu wa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Joseph Rubiro baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam leo kwa ziara ya kikazi. Anayetoa utambulisho ni ni Mwenyeji wake Mwakilishi mkazi wa FAO, Fred Kafeero.

  José Graziano da Silva mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula Dunia (FAO) akiongea na wenyeji wake baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam leo kwa ziara ya kikazi. Kushoto ni Mwenyeji wake Mwakilishi mkazi wa FAO, Fred Kafeero.

  José Graziano da Silva mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula Dunia (FAO) akisalimiana na Mratibu mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa UNDP, Alvero Rodriguez, baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam leo kwa ziara ya kikazi. Katikati ni Mwenyeji wake Mwakilishi mkazi wa FAO, Fred Kafeero.

  José Graziano da Silva mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula Dunia (FAO) akielekea kupanda gari tayari kuanza kwa msafara wake baada ya baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam leo kwa ziaraya kikazi. Pamoja nao ni Mratibu mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa UNDP, Alvero Rodriguez (wa pili kushoto) Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Jestus Nyamanga na Mwambata wa FAO kutoka Roma Italia, Meshack Malo (kulia).

  José Graziano da Silva Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Dunia (FAO) akitambulishwa Msaidizi wa Mwakilishi wa FAO Tanzania (Utawala) na Msaidizi Mwenza (Programu) Charles Tulahi baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam leo kwa ziara ya kikazi. Anayetoa utambulisho ni ni Mwenyeji wake Mwakilishi mkazi wa FAO, Fred Kafeero.

  0 0

  Mkoa wa Ruvuma umefikia lengo ya ununuzi wa mahindi waliyopanga kununua katika msimu huu wa mavuno kwa vituo vyote ambayo viliteuliwa rasmi na hifadhi ya chakula ya mkoa.

  0 0

  Mkurugenzi wa Barabara toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi John Ngowi akielezea jambo wakati wa kongamano la pili la majadiliano kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya EcomResearch ambayo ndio mshauri mwelekezi wa uanzishwaji wa taasisi hiyo Profesa Godwin Mjema na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala toka wizara hiyo Bw. Stephen Mushi.
  Mwenyekiti wa Kampuni ya EcomResearch ambayo ndio mshauri mwelekezi wa uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), Profesa Godwin Mjema akifafanua jambo wakati wa kongamano la pili la majadiliano kuhusu uanzishwaji wa taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Barabara toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi John Ngowi na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala toka wizara hiyo Bw. Stephen Mushi.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Bi. Segolena Francis akifafanua jambo wakati wa kongamano la pili la majadiliano kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) leo Jijini Dar es Salaam.
  Mtaalamu wa Utafiti kutoka Kampuni ya EcomResearch ambayo ndio mshauri mwelekezi wa uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT),akifafanua jambo wakati wa kongamano la pili la majadiliano kuhusu uanzishwaji wa taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Barabara toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi John Ngowi (wanne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya ujenzi mara baada ya kufungua kongamano la pili la majadiliano kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) leo Jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Mafundi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakifunga taa za kuongozea magari (traffic lights) katika makutano ya barabara za Taifa na Pangani jijini Tanga. Mradi huo wa kwanza kufanyika jijini Tanga unahusiha taa za kuongozea magari na waenda kwa miguu katika makutano ya barabara za Taifa na Pangani pamoja na makutano ya barabara za Swahili, Uhuru na ile ya Hospital ya Bombo. Taa hizo zitatumia nishati ya umeme jua.

  Na Theresia Mwami – TEMESA TANGA.

  Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) inatekeleza miradi miwili ya taa za kuongozea magari na abiria (traffic lights) jijini Tanga katika makutano ya barabara za Taifa na Pangani, pamoja na makutano ya barabara za Swahili, Uhuru na ile inayoelekea hospitali ya Bombo. Ifahamike kuwa mji wa Tanga haujawahi kuwa na taa za kuongozea magari na waenda kwa miguu hapo kabla, zaidi ya kuwa na vipita shoto kwenye baadhi ya barabara zake.

  Akiongea na Waandishi wa Habari Meneja wa Kikosi cha Umeme TEMESA Mhandisi Pongeza Semakuwa alisema miradi hii miwili ya taa za barabarani hapa Tanga inahusisha taa za kuongozea magari pamoja na zile za kuongoza waenda kwa miguu kuvuka makutano hayo ya barabara. Taa hizo zitakuwa zikitumia umeme jua, nishati ambayo itaziwezesha kufanya kazi muda wote hata pale umeme wa TANESCO unapokuwa na hitilafu.

  Nae Mbunge wa Jimbo la Tanga mjini Mheshimiwa Alhaj Mussa Mbaruku  ambae alipita katika eneo la mradi la makutano ya Barabara ya Pangani na Taifa maarufu kama “Taifa/Ring Junction” kujionea utekelezaji huo wa mradi wa Serikali, alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutapunguza ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikitokea kwenye makutano ya barabara hizo na vile vile kuufanya mji wa Tanga kuwa wa kisasa zaidi.


  Kwa upande wake Meneja wa TEMESA Tanga Mhandisi Margareth Gina alisema kuwa miradi hiyo ya usimikaji wa taa za kuongozea magari na waenda kwa miguu jijini Tanga imeiingizia TEMESA jumla ya shilingi za kitanzania milioni 434 fedha za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitakazolipwa kwa TEMESA kupitia ofisi ya Mkurugenzi wa jiji la Tanga. Aliongeza kuwa miradi yote miwili iko mbioni kukamilika mapema mwezi huu.
   Mafundi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakifunga mabomba ya chuma kwa ajili ya kusimika mfumo wa taa za kuongozea magari katika makutano ya barabara za Taifa na Pangani jijini Tanga. Mradi huo wa kwanza kufanyika jijini Tanga unahusiha taa za kuongozea magari na waenda kwa miguu (traffic lights) katika makutano ya barabara za Taifa na Pangani pamoja na makutano ya barabara za Swahili, Uhuru na ile ya Hospital ya Bombo na utatumia umeme jua.
   Mafundi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakiunganisha nyaya kwenye “Panel za Solar” zitakazotumika katika mfumo wa taa za kuongozea magari na abiria (traffic lights) katika makutano ya barabara za Taifa na Pangani Jijini Tanga. Mradi huo wa kwanza kufanyika jijini Tanga unahusiha taa za kuongozea magari na waenda kwa miguu katika makutano ya barabara za Taifa na Pangani pamoja na makutano ya barabara za Swahili, Uhuru na ile ya Hospital ya Bombo. Taa hizo zitatumia nishati umeme jua.
  Mbunge wa Tanga Mjini Mhe. Alhaj Mussa Mbaruku akiongea na watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) alipofika katika eneo la mradi wa kusimika taa za barabarani katika makutano ya barabara za Taifa na Pangani jijini Tanga. Mradi huo wa kwanza kufanyika jijini Tanga unahusiha taa za kuongozea magari na waenda kwa miguu katika makutano ya barabara za Taifa na pangazi pamoja na makutano ya barabara za Swahili, Uhuru na ile ya Hospital ya Bombo. Taa hizo zitatumia nishati ya umeme jua. kutoka kushoto ni Mhandisi Zuhura Semboja, Mhandisi Pongeza Semakuwa pamoja na Mhandisi Margaret Gina. Picha zote na Theresia Mwami - TEMESA

  0 0


  Balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Xiaowu na Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo wakitia saini makubaliano mapya ya china kuendelea kuleta madaktari na kutumika kwa mwaka mmoja badala ya miwili, wanaoshuhudia Mwanasheria wa Wizara ya Afya Amina Moh’d na Mkuu wa kitengo cha uchumi na fedha wa ubalozi wa China Zanzibar Chen LI hafla hiyo ilimefanyika Wizara ya Afya.
  Balozi Xie Xiaowu na Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo wakibadilishana hati za makubaliano ambapo China itaendelea kuleta madaktari Zanzibar na kufanyakazi kwa kipindi cha mwaka mmoja.Picha na Makame Mshenga.

  ………………………………………………………………

  Na Ramadhani Ali – Maelezo


  Serikali ya Watu wa China imetiliana saini na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar makubaliano mapya ambapo China itaendelea kuleta madaktari kutoa huduma Zanzibar na kuanzia sasa watakuepo nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja.

  Hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo zilifanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja ambapo Zanzibar iliwakilishwa na Waziri Mahmoud Thabit Kombo na China iliwakilishwa na Balozi wake mdogo aliepo Zanzibar Xie Xiaowu.

  Akizungumza katika hafla hiyo Waziri Mahmoud alisema kundi la kwanza la madaktari 21 watakaofanyakazi kwa utaratibu mpya wa mwaka mmoja limeanza kazi mwezi Julai ambapo madaktari 12 wapo Unguja na tisa Pemba.

  Waziri wa Afya aliwatoa wasi wasi wananchi juu ya utaratibu wa sasa wa madaktari hao kufanyakazi mwaka mmoja na kuondoka kwavile ni wamajaribio na ukionekana unaleta usumbufu utaratibu wa zamani wa miaka miwili unaweza kurejeshwa.

  Wakati huo huo Waziri wa Afya alisema Madaktari bingwa watano wa maradhi ya Saratani, wakiwa na vifaa vya kisasa, kutoka Hospitali ya Nanjing China wanatarajiwa kuwasili Zanzibar mwisho wa wiki hii kuungana na madaktari wazalendo katika kampeni maalum ya uchunguzi wa maradhi ya saratani ya shingo ya kizazi.

  Alisema kampeni hiyo itaanza rasmi tarehe 10 hadi tarehe 23 mwezi huu katika Hospitali za Unguja na Pemba na amewahimiza akinamama waliofikia miaka 18 kuitumia fursa hiyo kuchungaza afya zao.

  Alisema uamuzi huo unafuatia uchunguzi uliofanywa kwa akinamama wanaojifungua baadhi yao kubainika kuwa na chembe chembe za maradhi ya saratani ya shingo ya kizazi

  Waziri Mahmoud alikumbusha kuwa maradhi ya saratani sio rahisi kugundulika bila ya kufanyiwa uchunguzi na dawa kubwa ya maradhi hayo ni kugundulika mapema na kupatiwa tiba katika hatua ya awali.

  Nae balozi Xie Xiaowu aliahidi kuwa Serikali ya Watu wa China itaendeleza uhusiano wa kihistoria wa kuisaidia Zanzibar katika sekta mbali mbali za maendeleo ikiwemo kuimarisha huduma za Afya.

  China ilianzisha makubaliano na Zanzibar kuleta madaktari kutoa huduma katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja na Abdalla Mzee Mkoani tokea mwaka 1964 baada ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  0 0

  Mwenyekitiwa Chama cha Wanawake katika Utalii Tanzania (AWOTTA),Mary Kalikawe (katikati) akisisitiza jambo kwa wanachama (hawapo pichani) wakati wa mkutano mkuu wa mwaka ulioambatana na sherehe za kutimiza miaka sita ya chama hicho zilizofanyi jijini Dar es Slaam leo.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Devotha Mdachi na Katibu wa chama hicho, Agnes Rwegasira .

  Katibu Mkuu wa Chama cha Wanawake katika Utalii Tanzania (AWOTTA) , Agnes Rwegasira akisisitiza jambo kwenye semina hiyo. iliyofanyika katika ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania ( TTB) jijini Dar es Salaam
  Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Utalii (TTB) Bi. Fatma s. Mchumo(kushoto) akitoa mchango kwenye semina hiyo

  Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wanawake nchini Tanzania Bi. Jacqueline Maleko. (TWCC ) kulia, akiongea wakati wa semina hiyo

  Mkuu wa idara , Sera na Mpingo wa Wizara ya Maliasili naUtalii Tanzania, Dorothea Masawe (katikati) Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake katika Utalii Tanzania (AWOTTA) Mary Kalikawe (wapilikushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Devotha Mdachi (wa tatu kutoka kulia) wakikata keki ya kuadhimisha miaka 6 ya AWOTTA.

  Baadhi ya wanachama na wafanyakazi wa chama cha Chama cha Wanawake katika Utalii Tanzania (AWOTTA) wakiwa kwenye mkutano Mkuu wa Mwaka uliaoambatana na sherehe za kutimiza miaka sita tangu kuanzishwa kwa chama hicho. Wakati wa hafla na semina iliyofanyika katika ofisi za TTB jijini Dar es salaam


  ………………………….

  Wakati serikali ya awamu ya tano imejipanga kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati na kuimarisha zaidi sekta ya viwanda,Wanawake wanaojishughulisha na utalii kupitia umoja wao unaojulikana kama Association of Women in Tourism Tanzania (AWOTTA) umeweka mikakati mikubwa ya kuhakikisha inatumia fursa zilizopo kukuza sekta ya utalii.

  Akiongea wakati wa mkutano wa mkuu wa mwaka, hafla ya kuadhimisha miaka 6 ya umoja huo sambamba na semina ya kujadili changamoto na kuweka mikakati iliyofanyika jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa AWOTTA,Mary Kalikawe,aliipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais,Dk.John Magufuli,kwa jitihada inazofanya kukuza uchumi kwa nchi kupitia sekta mbalimbali.

  Kalikawe alisema kuwa katika kipindi cha miaka 6 tangu ianzishwe AWOTTA imefanikiwa kwa kuwaunganisha wanawake wanaofanya biashara ya utalii hapa nchini kwa upande wa bara na visiwani na aliwataka akina wanawake wengi kujitokeza kujiunga na umoja huu kwa kuwa umoja ni nguvu katika kukabiliana na changamoto mbalimbali kisekta.

  Alibainisha baadhi ya changamoto zinazokwamisha wanawake kuendesha shughuli za utalii ni kutokuwa na mitaji ya kutosha,kodi nyingi na kubwa zinazotozwa na serikali katika sekta hiyo,na wananchi na wadau wengi kutokuwa na ufahamu kuhusiana na sekta hii japokuwa inachangia pato la taifa kwa kiasi kikubwa na aliiomba serikali kusaidia kukabiliana na changamoto hizo hili sera ya Tanzania ya viwanda iende sambamba na fursa za kukuza utalii nchini.

  Kwa upande wake,Afisa Mwandamizi kutoka kitengo cha sera na Mipango, Dorothea Masawe ambaye alimwakilisha Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Mh.Ramo Makani katika maadhimisho hayo aliipongeza AWOTTA kwa kazi nzuri inayofanya ya kuunga mkono jitihada za serikali za kukuza sekta ya utalii na aliahidi kuwa serikali itafanya kazi kwa kushirikiana na taasisi hiyo “Serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na AWOTTA katika kukuza utalii nchini,inawapongeza kwa kutimiza miaka 6 na itaendelea kufanya kazi nanyi bega kwa bega”.Alisisitiza.

older | 1 | .... | 1360 | 1361 | (Page 1362) | 1363 | 1364 | .... | 1897 | newer