Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live

Tigo, Clouds Wazindua Msimu wa ‘Tigo Fiesta 2017 – Tumekusoma’

$
0
0
 Kaimu Meneja wa Masoko Tigo, William Mpinga(katikati) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2017 'Tumekusomaa' leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Tigo Fiesta, Sebastian Maganga na mwakilishi toka Basata, Mrisho Mrisho.
 Kaimu Meneja wa Masoko Tigo, William Mpinga(katikati) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2017 'Tumekusomaa' leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Tigo Fiesta, Sebastian Maganga na mwakilishi toka Basata, Mrisho Mrisho.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Tigo Fiesta 2017, Sebastian Maganga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa Tigo Fiesta 'Tumekusomaa' leo jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Kaimu Meneja wa Masoko Tigo, William Mpinga na mwakilishi toka Basata, Mrisho Mrisho.
Mwakilishi toka Basata, Mrisho Mrisho akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2017 'Tumekusomaa' leo jijini Dar es salaam. Wengine toka kushoto niMwenyekiti wa kamati ya maandalizi Tigo Fiesta 2017, Sebastian Maganga na Kaimu Meneja wa Masoko Tigo, William Mpinga.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Tigo Fiesta 2017, Sebastian Maganga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa Tigo Fiesta 'Tumekusomaa' leo jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Kaimu Meneja wa Masoko Tigo, William Mpinga na mwakilishi toka Basata, Mrisho Mrisho.

‘Tigo Fiesta 2017 – Tumekusoma’ kurindima katika mikoa 15 nchini


Dar es Salaam, Agosti 17, 2017- Msimu mkubwa zaidi wa shamrashamra za kitamaduni katika kanda ya Afrika  Mashariki na Kati, Tigo Fiesta 2017 – Tumekusoma sasa upo tayari kurindima kwa mziki wa kusisimua, ofa murwa na mabadikilo makubwa ya kidigitali nchini kote.

Hii inafuatia uzinduzi mkubwa wa makubaliano kati ya Tigo Tanzania – kampuni inayoongoza katika mabadiliko ya kidigitali nchini na Clouds Entertainment Group. Makubaliano haya yanayoipa Tigo haki miliki za jina Tigo Fiesta 2017 – Tumekusoma yatawezesha mzimu huu wa utamaduni ukifikia mikoa 15 nchini.

Wakitangaza makubaliano hayo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugrenzi wa Masoko wa Tigo, William Mpinga aliahidi kuwa Tigo Fiesta 2017 – Tumekusoma litakuwa tamasha  kubwa na la kusisimua zaidi katika historia ya miaka 16 ya tamasha hilo la kitamaduni katika ukanda huu wa Afrika.

‘Kauli mbiu ya Tigo Fiesta 2017 ni Tumekusoma, ikionesha sifa kuu ya Tigo kama mtandao unaoelewa zaidi mahitaji ya wateja wake nchini kote,’ Mpinga alisema.

‘Ushirikiano huu unamaanisha kuwa pamoja na kuwa mtandao unaoongza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo sasa pia ndio mtandao unaosisimua zaidi nchini. Tutawaletea wasanii wenye hadhi ya kimataifa na waliojizolea sifa ndani na nje ya nchi katika msimu wa miezi mitatu iliyojaa ofa kabambe kutoka Tigo zitakazoendana na shamrashamra za furaha na kumbukumbu za muziki murwa.

‘Kupitia Tigo Fiesta 2017- Tumekusoma, Tigo imejikita kuinua vipaji vya wasanii wa Kitanzania kama njia mojawapo ya kukuza sanaa nchini. Kama tunavyojua, sanaa imekuwa mojawapo ya nafasi kubwa za ajira kwa vijana wetu na baaadhi ya wasanii wetu pia wamepata nafasi ya kuperusha bendera ya nchi katika nchi za kigeni, kwa hiyo kusaidia kuitangaza nchi yetu.  Tuna imani kuwa kupitia ushirikiano huu tutaweza kuwakutanisha wasanii wetu na mashabiki wao, kuwajengea uwezo na hivyo kuwasaidia wasanii wengi zaidi kufikia viwango vya kimataifa,’ alisema.  

Kwa upande wake, Mratibu Mkuu wa Kamati ya Maandilizi ya Tigo Fiesta 2017 – Tumekusoma, Sebastian Maganga alisema kuwa msimu huu wa Tigo Fiesta 2017 – Tumekusoma utajumuisha mikoa ya Arusha Kahama, Musoma, Mwanza, Tabora na Dodoma. Mikoa mingine itakayohusishwa ni Iringa, Songea na Njombe pamoja na Sumbawanga, Morogoro, Tanga, Moshi na Mtwara .

‘Kama ilivyokuwa kawaida yetu, hatma ya Tigo Fiesta 2017 – Tumekusoma itafanyika Dar es Salaam,’ Sebastian alisema, huku akibainisha kuwa tarehe za tamasha, maeneo husika pamoja na wasanii na matukio yataoendana na msimu huu yatatangazwa hivi karibuni.

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) YATEUA MADIWANI 12 WANAWAKE WA VITI MAALUM

RAIS DKT. MAGUFULI AMTEUA BRIGEDIA JENERALI JOHN JULIUS MBUNGO KUWA NAIBU MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU

SERIKALI KUTUMIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI KUDHIBITI AJALI BARABARANI

$
0
0
 Serikali imetoa mwezi mmoja kwa Mamlaka zinazohusika na masuala ya usalama barabarani kuhakikisha zinakamilisha uboreshaji wa mfumo wa kielektroniki wa uwekaji wa vifaa vya kufuatilia udhibiti mwendo barabarani ikiwa lengo ni kushughulikia matatizo ya kiusalama barabarani kupitia vyombo vya usafiri.
Akizungumza hayo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amesema kuwa mfumo huo uendane na utengenezaji wa mpango wa Taifa wa kufuatilia masuala ya kiusalama barabarani utakaohusisha wataalam kutoka Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) na Wataalam wa Idara ya Usalama na Mazingira (Sekta ya Ujenzi).

"Shirikianeni kutengeneza mfumo ambao utasaidia kutambua matatizo mbalimbali yanayoweza kujitokeza barabarani ili kubaini mwenendo wa mabasi na malori mwanzo hadi mwisho wa safari zake",  amesema Naibu Waziri Ngonyani.

Amesisitiza kuwa mfumo ambao utaandaliwa na wataalam hao unatakiwa kukidhi mahitaji ya kila mmoja ili kuleta matokeo chanya kwa manufaa ya nchi yatakayosaidia kupunguza ajali za barabarani zinazotokana na mwendo kasi, kupambana na uhalifu na kulinda usalama wa abiria.


Aidha, Eng. Ngonyani amefafanua kuwa katika juhudi za kuhakikisha serikali inapunguza ajali za barabarani wizara yake kupitia Idara ya Usalama na Mazingira tayari imesaini mkataba wa kufunga kamera za udhibiti mwendo kasi katika barabara kuu ya TANZAM (Dar es Salaam - Tunduma), ambapo sehemu ya majaribio ya mradi huo imefanyika katika maeneo ya
Dar es Salaam - Chalinze - Morogoro.


Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Eng. Hamad Masauni, amesema kuwa taratibu za kutengeneza mfumo huo zinatakiwa kukamilika haraka ili kusaidia Jeshi la Polisi kutumia mfumo huo kuweza kupambana na uhalifu katika maeneo mbalimbali ya nchi. 


Ametanabaisha kuwa Serikali itamchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote atakaejaribu kuhujumu mfumo huo kwani serikali itatumia fedha nyingi kuutekeleza kwa lengo la kuhakikisha usalama wa raia unalindwa ipasavyo.


Naye Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Gilliard Ngewe, ameeleza manufaa ya mfumo huo kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri wa magari ya abiria na mizigo kuwa ni itasaidia kupunguza matumizi ya mafuta, uharibifu wa matairi ya magari mara kwa mara na kupunguza gharama za matengenezo ya magari.

Mfumo huo wa kieletroniki wa usalama barabarani ni moja ya mbinu zinazotumiwa na Serikali katika kuhakikisha matumizi ya usalama barabarani yanazingatiwa kwa mujibu wa Sheria, Taratibu na Kanuni.

 Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akizungumza na wataalam wa mfumo wa kieletroniki wa usalama barabarani katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Eng. Hamad Masauni.

 Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Eng. Hamad Masauni, akichangia mada katika kikao kazi na wataalam wa mfumo wa kieletroniki wa usalama barabarani, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu Mweyekiti wa Baraza hilo ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani.

 Kamanda wa Usalama Barabarani, Jeshi la Polisi Tanzania Fortunatus Muslim, akifafanua jambo kwa watalaam wa mfumo wa kieletroniki wa usalama barabarani katika kikao kazi kilichofanyika, jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Julius Chambo akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha watalaam wa mfumo wa kieletroniki wa usalama barabarani kilichofanyika, jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), Godfrey Nsato, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Eng. Hamad Masauni (hawapo pichani), namna mfumo wa kieletroniki wa kudhibiti mwenendo wa magari ya abiria na mizigo inavyofanya kazi, jijini Dar es Salaam. 

WADAU WA NGO’s WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUANZA UHAKIKI WA NGO’s NCHINI

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO BIBI SIHABA NKINGA AZINDUA MPANGO WA UHAKIKI WA NGO’S NCHINI.

MATUKIO YA WIKI YALIYOTIKISA MKOA WA RUVUMA NA NJE YA MKOA WA RUVUMA

$
0
0
Tumekusogezea matukio ya wiki yaliyojili mkoani Ruvuma kuanzia Tarehe 14 August hadi August 20 , 2017 kama ilivyo kawaida yetu.  

Daktari ‘feki’ wa Muhimbili, anaswa tena Hospitali ya Amana leo

$
0
0
Mkaazi  wa  jiji la Dar es Salaam, Abdallah Juma aliyewahi kukamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akidaiwa kujifanya daktari amenaswa tena katika Hospitali ya Rufaa ya Amana kwa kufanya kazi katika hospitali hiyo wakati sifa za udaktari hana. Juma amenaswa leo ndani ya Hospitali ya Amana, majira ya mchana, akijifanya daktari, baada ya kuwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo.

Kukamatwa kwa Juma  kunakuja ikiwa ni miezi mitatu tu imepita tokea Juni 19 mwaka huu alipo kamatwa katika hospitali ya Muhimbili kwa kujifanya daktari. Katika hospitali ya Muhimbili kijana huyo alijifanya kutoa huduma katika maabara kuu  huku uongozi ukiwa hauna taarifa ya kuwepo kwa huduma aliyokuwa akiitoa kitu ambacho kilisababisha kushtukiwa na kukamatwa.

Baada ya kukamatwa Uongozi wa hospitali hiyo ulifanya uchunguzi na kubaini kuwa kijana huyo hakuwa daktari bali daktari feki kama alivyokuwa akijitambulisha na kwamba amekamatwa mara baada ya kuwekewa mtego na askari wa hospitali hiyo. Daktari wa Kitengo cha Watu wanaoishi na Virusi  vya Ukimwi (WAVIU),    Shani Mwaruka alikiri kukamatwa kwa  kwa mtuhumiwa huyo.

Amesema, Juma alinaswa baada ya uongozi kupata malalamiko kutoka kwa  watu waliokuwa wakihitaji huduma  katika hospitalini hiyo. Amesema tayari hospitali hiyo iliweka mtego imara wa maofisa wake, ambapo Juma aliingia bila hofu yeyote na kukutana na watu ambao alitaka wampe fedha ili awahudumie ndipo aliponaswa.

Baadhi ya watu waliodaiwa kuombwa fedha na  daktari huyo feki, wamesema aliahidi kuwatafutia kazi mbalimbali katika hospitali hiyo.

Nae mwananchi aliyekwenda kupata huduma hospitali ya Amana Cecilia amesema  Agosti 9 mwaka huu, kijana  huyo aliwaeleza kuwa kuna kazi  katika hospitali ya Amana na yeye kama daktari bingwa anayefanya kazi hapo anaweza kuwasaidia.

“Alituambia kuwa  fomu zinatolewa katika  hospitali ya muhimbili sh. 150,000 lakini kwakuwa wao ni madakatari atatufanyia kwa sh. 100,000 tu. Tulichanga fedha hiyo na ilifikia 800,000 tukampatia,”alieza Cecilia. Ameongeza,Juni  19 mwaka huu aliwaita katika hospitali ya Amana ili kufanyiwa usahili lakini hakutokea na simu akawa hapokei.

“Tuliamua kuuliza kwa madakatari kama wanamfahamu lakini hakuna aliyemfahamu ndipo tulipobaini kwamba tumetapeliwa na kuamua kufanya mtego kwa kushirikiana na uongozi uliofanikisha kumnasa  leo ,”alieleza.
Daktari wa Kitengo cha Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) wa Hospitali ya Amana, Dkt. Shani Mwaruka akizungumza na waandishi wa habari juu ya kumnasa Daktari ‘feki’ katika hospitali hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Daktari ‘feki’ Abdallah Juma akiwa chini ya ulinzi wa Askari waliofika katika hospitali hiyo mara baada ya kupata taarifa.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Amana,Zainab Hoti akizungumza waandishi habari juu wananchi kuacha njia ya mkato katika kupata huduma katika hospitali ya Amana.picha na Emmanuel Massaka.

WAZIRI MKUU AWATAKA WATANZANIA KUIMARISHA UZALENDO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati) akizungumza na wanafunzi wanaosomea fani ya Udaktari nchini Cuba, alipokutana nao katika Hotel ya Nacional de Cuba, jana Agosti 20, 2017. kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi Cuba, Goodchance Tarimo na kulia ni Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Canada na Cuba, Leonce Bilauri. Waziri Mkuu yupo Havana Cuba kwa Ziara ya Kikazi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akisalimiana na wanafunzi wa Kitanzania anaye Soma fani ya Udaktari nchini Cuba, Eshe Hemed Rashid pamoja na Nasra Sheikhan, alipokutana nao katika Hoteli ya Nacional de Cuba, jana Agosti 20, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi Wakitanzania wanao someafani ya Udaktari nchini Cuba.
 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wote wahakikishe wanaboresha mshikamano wao pamoja na kuimarisha uzalendo kwa Taifa lao.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumapili, Agosti 20, 2017) wakati akizungumza na wanafunzi wa Kitanzania wanaosomea udaktari nchini Cuba.

Waziri Mkuu yuko nchini Cuba kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la kudumisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Alisema uzalendo kwa Taifa ni jambo muhimu.

 “Uzalendo ni muhimu sana kwa sababu tumekosa fursa nyingi za kimaendeleo kutokana na baadhi ya wananchi kutokuwa wazalendo kwa Taifa lao.”

Kutokana na hali hiyo Serikali inawasisitiza Wananchi kuwa wazalendo na washirikiane kuhakikisha fursa za kimaendeleo zilizoko nchini zinaendelezwa.

Alisema Serikali inatekeleza miradi mingi kwa lengo la kukuza uchumi kutoka wa chini kwenda wa kati, ni vema wananchi wakashirikiana nayo ili kufanikisha adhma hiyo.

Pia Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwasihi wanafunzi hao kuzingatia sheria za nchini waliyoko pamoja na kukumbuka kurudi nyumbani mara wamalizapo masomo yao.

Alisema Serikali inatambua uwepo wao wa kimasomo nchini Cuba na kwamba inatarajia kupata mchango mkubwa kutoka kwao punde wamalizapo masomo yao.

 “Nawaomba msome kwa bidii na mfaulu mitihani yenu. Elimu yenu iwasaidie katika ajira na muweze kurejesha mikopo mliyopewa na Serikali ili iwanufaishe wengine.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwataka Mabalozi wote wanaoiwakilisha Tanzania katika mataifa mbalimbali kuhakikisha wanatangaza vivutio vya utalii.

Alisema Tanzania imejaaliwa kuwa na vivutio vingi vya utalii, hivyo ni vema Mabalozi wakavitangaza jambo ambalo litasaidia kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini.

Miongoni mwa vivutio vya utalii vilivyoko nchini ni pamoja na mlima Kilimanjaro, visiwa vya Zanzibar, mbuga mbalimbali zenye wanyama wa aina tofauti tofauti.

Awali Mwenyekiti wa wanafunzi hao, Bw. Goodchance Tarimo alimuhakikishia Waziri Mkuu kwamba watarejea nyumbani mara baada ya kumaliza masomo yao nchini humo.

Alisema wao wanaimani kubwa na Serikali na wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na viongozi wa Taifa kwa lengo la kuboresha maendeleo pamoja na kukuza uchumi.

“Tunapongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika  kujenga uchumi wa viwanda, mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi na ujenzi wa miundombinu ya kisasa.”

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMATATU, AGOSTI 21, 2017.

BENKI YA KILIMO YAWAASA WAKULIMA WA KOROSHO

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (aliyesimama) akifungua Warsha ya Siku Mbili ya Wadau wa Vyama vya Ushirika inayoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Benki Kuu Tawi la Mtwara, Bw. Lucas Mwimo (kushoto) na Kaimu Katibu Tawala Msaidizi – Uchumi na Uzalishaji, Bw. Amani Rusake (kulia).

Na Mwandishi wetu, Mtwara

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imewaasa wakulima wa korosho nchini kuongeza uzalishaji wa korosho ili kuchangamkia fursa za masoko ya zao hilo linalohitajika zaidi katika masoko ya Marekani, Vietnam na India.

Wito huo umetolewa jana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga wakati akifungua Warsha ya Siku Mbili ya Wadau wa Vyama vya Ushirika inayoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Bw. Assenga alisema kuwa mahitaji ya korosho ni makubwa sana katika soko la dunia hivyo wakulima wa zao hilo hawana budi kujizatiti ili kuhakikisha wanazalisha kiasi kikubwa cha korosho ili kufikia au kuzidi malengo ya mavuno kwa msimu ujao ambayo yanakadiriwa kufikia kati ya tani laki tatu (3) hadi laki nne (4) ukilinganisha na takribani tani laki mbili na nusu kwa msimu uliopita.
Mkurugenzi wa Biashara wa Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha akiwasilisha mada kuhusu mchango wa TADB katika mapinduzi ya kilimo nchini.

Bw. Assenga alisema kuwa korosho ni zao la kimkakati ambalo likiwekezwa kwa usahihi linaweza kunyanyua uchumi na kipato kwa wakulima wa mikoa ya kusini na pwani ambao niyo ni wazalishaji wakuu wa zao hilo.
“Nawaasa mujitahidi kulima kisasa ili kuweza kufikia au kuvuka malengo ya mavuno ya msimu huu hali itakayowaongezea kipato hivyo kufikia malengo ya serikali ya kuwanyanyua wakulima nchini,” alisema.

Kaimu Mkurugenzi huyo wa TADB aliongeza kuwa Benki yake imejipanga kusaidia mfumo wa Stakabadhi ya maghala ili kuhakikisha kuwa malengo ya mavuno ya korosho kwa msimu huu yanafikiwa.
“TADB iko tayari kuratibu mfumo wa malipo ya fedha zitokanazo na mauzo ya korosho kwa njia ya TEHAMA, pia kwa kushiriakiana na soko la mazao (TMX), kusimamia ununuzi wa mazao kwa njia ya mtandao (electronic auction),” aliongeza.
Mwakilishi wa Mrajis wa Vyama vya Ushirika Nchini, Bw. Nerei Kyara akizungumza na Wadau wa Vyama vya Ushirika wakati wa Warsha ya Siku Mbili ya Wadau inayoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara. Wengine pichani ni Kaimu Katibu Tawala Msaidizi – Uchumi na Uzalishaji, Bw. Amani Rusake (kushoto) na Mkuu wa Kilimo na Fedha Vijijini wa Mfuko wa Kukuza Sekta ya Fedha, Bw. Mwombeki Baregu.

Aliongeza kuwa Benki ipo tayari kusimamia uuzaji wa mazao kwa mifumo ya salama ya kimataifa ya malipo kama vile dhamana ya malipo.

Naye Mkurugenzi wa Biashara wa Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha alisema kuwa Benki ya Kilimo ipo tayari kutoa mikopo kwa ajili ya uendelezaji wa miundombinu ya umwagiliaji na maghala na uzalishaji wa mbegu bora za mazao ya korosho na mihogo.

SOMA ZAIDI HAPA

Maendeleo ya miundombinu: Nguzo ya uwezeshaji katika kufikia uchumi imara

$
0
0
Mkurungezi Mtendaji wa Buzwagi Gold Mine Bw; Stewart Hamilton akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi wa Uwanja wa ndege wa Buzwagi na pembeni yake ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu ambao kwa kwa kiasi kikubwa ACACIA wamewekeza katika kuboresha uwanja huo.
Wananchi wa Kahama wakishuhudia uzinduzi wa safari za ndege za shirika la Precision Air katika uwanja wa ndege wa Buzwagi.


Mazingira mazuri ya kukuza uchumi yanahitaji miundombinu bora inayowezesha uchukuzi huku ikiboresha uzalishaji na ufanisi. Hivi karibuni, wakazi wa Kahama na Shinyanga watafurahia safari za ndege kati ya Kahama na Dar es Salam. Haya ni matokeo ya ushirikiano wa Acacia Mining ulioanza toka mwaka 2008, ilipoanza uzalishaji katika mgodi wake wa Buzwagi; huku wakiendelea kuwekeza katika kiwanja cha ndege cha Kahama, wakihakikisha kiwanja kinatunzwa na kufanya kazi. 

Ushirikiano wa karibu kati ya Mkuu wa Wilaya Mh. Fadhil Nkurlu na Mgodi umewezesha kuanzishwa kwa safari za ndege za moja kwa moja. Safari za shirika la ndege la Precision zitapunguza adha ya usafiri ya wakazi wa Kahama na Shinyanga waliotakiwa kusafiri hadi Mwanza ili kupata usafiri wa ndege kuelekea Dar es Salaam.

 ‘Hii itasaidia sana kuongeza ufanisi katika muda na fedha zinazotumika katika usafiri,’ alisema mfanyabiashara Bw. Charles Thomas akiongeza kuwa safari ya barabara hadi Mwanza ingeweza kuchukuwa hadi masaa 6. Kufuatia mafanikio ya safari ya majaribio mwezi uliyopita, Meneja Mahusiano wa Kampuni wa shirika la ndege la Precision, Bw. Hillary Mremi alisifia hali ya kiwanja akisema, ‘njia ya ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Buzwagi ipo katika hali nzuri na matunzo yake ni mazuri; hii ni nzuri kwa usalama wa abiria na ndege zetu. 


Tunashukuru Acacia kwa kuwekeza katika kuboresha, kiwanja kidogo cha Buzwagi; hatua iliyoturuhusu kuanza safari kuelekea Kahama, zitakazo anza 5 September, 2017, tukiwa na safari tatu kwa wiki, na safari zikiongezeka zikitegemea mahitaji ya wasafiri. Hatua ya kutatua shida ya miundombinu ni moja itakayoleta matokeo chanya kwa biashara mkoani Shinyanga kwa kupunguza gharama za kuendesha biashara; huku ikiongeza faida.

Japokuwa Acacia imefanya uwekezaji wenye tija katika kuendeleza na kurekebisha kiwanja hiki kidogo cha ndege, ni muhimu kukumbuka kwamba kiwanja hiki ni mali ya Serekali chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). Uwekezaji katika kiwanja hiki kidogo inaonyesha nia ya Acacia kuendelea kusaidia jamii na taasisi zinazozunguka migodi yake.

TTB yapigia chapuo safari za ndege moja kwa moja kwenda China

$
0
0
BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imeridhishwa na idadi kubwa ya watii kutoka nchini China na kuelezea kuwa endapo kutakuwa na safari za ndege za moja kwa moja kutoka Tanzania kutasaidia kupunguza gharama za safari na pia kuchochea utalii.

Mwenyekiti wa Bodi ya TTB Jaji Mstaafu Thomas Mihayo aliwaambia waandishi wa habari jijini hapa juzi kuwa endapo kutakuwepo na ndege ya moja kwa moja kutoka Tanzania mpaka China, idadi kubwa ya watilii kutoka nchi hiyo itaongezeka na pia mataifa mengine, hivyo sekta ya utalii uchangia zaidi mapato ya serikali.

akizungumza mara baada ya kumaliza ziara ya kuwatembeza waandishi waandamizi wa habari kutoka nchini China katika hifadhi za Ngorongoro Crater na Manyara,Jaji Mihayo alisema vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini ni tunu kubwa kwa taifa na pia vinawaleta watalii kutoka sehemu mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii(TTB) Bi.Devota Mdachi(wanne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja waandishi Waandamizi wa habari kutoka China walipotembelea hifadhi ya Ngorongoro Crater na Ziwa Manyara na kujionea fahari ya Tanzania. Lengo la ziara ya waandishi hao ni kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kwenda kuvitangaza kupitia makala na machapisho ili kuvutia wachina wengi kutembelea Tanzania.

“Ujio wa wanahabari hawa ni fursa kwetu kwani watakwenda kuwa mabalozi wazuri kwa kutoa machapisho na habari nchini kwao juu ya vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania,” alisema na kutoa wito kwa waandishi wa ndani kuunga mkono jitihada hizo.

Alisema waandishi hao kutoka China wameonyesha nia ya dhati ya kuvitangaza vivutio vyetu na hivyo kutokana na urafiki wa kihistoria uliopo kati ya China na Tanzania, zoezi hilo litakuwa la mafanikio makubwa.

Aliongezea kuwa China ni nchini yenye watu wengi Dunia hivyo kupitia waandishi hawa watakwenda kuwafikia wananchi wengi wa nchi hiyo kupitia makala na machapisho mbalimbali kuhusiana na vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof.Jumanne Maghembe(kushoto) akizungumza na waandishi waandamizi wa habari kutoka China mara baada ya kumaliza ziara yao ya kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro Crater na Ziwa Manyara. Lengo la ziara ya waandishi hao ni kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kwenda kuvitangaza kupitia makala na machapisho ili kuvutia wachina wengi kutembelea Tanzania.

“changamoto kubwa waliyoiona ni gharama ya usafari wa ndege ni kubwa kutokana na kutokuwepo kwa ndege za moja kwa moja,” alisema Jaji Mihayo na kuongezea kuwa usafiri wa anga utakapo imarishwa utachochea idadi kubwa ya watalii kutoka China. Alisema tayari Rais Magufuli alishaahidi kuleta ndege Kubwa itakayofanya safari ndefu hivyo itasaidia kupata soko la watalii kutoka china kuongezeka na itasaidia kuongeza mapato katika sekta ya utalii.

Alisema pia Halmashauri na wawekezaji katika hoteli mbalimbali zilizopo katika maeneno ya vivutio vya utalii waunganishe nguvu ili kutatua changamoto za barabara kwani imekuwa ni kero kwa wageni. Miundombinu ya barabara kuelekezea maeneo ya hotel pia katika vivutio ni mbovu hivyo Serikali kushirikiana na sekta binafsi wajipange kuboresha miundombinu ili iwe rafiki na kuvutia watalii zaidi alisema Jaji Mihayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof.Jumanne Maghembe(kushoto) akimkabidhi zawadi kwa Mhariri Msaidizi kutoka China Daily Media Group, Bw. Kang Bing(kulia) mara baada ya kumaliza ziara yao ya kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro Crater na Ziwa Manyara. Lengo la ziara ya waandishi hao ni kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kwenda kuvitangaza kupitia makala na machapisho ili kuvutia wachina wengi kutembelea Tanzania. ziara hiyo iliwajumuisha wahariri sita kutoka vyombo mbalimbali vya nchini China.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TTB, Bibi Devota Mdachi alisema ujio wa wanahabari hawa ni mwendelezo wa juhudi za TTB katika kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania ili kufanya idadi ya watalii kuongezeka. “ tumepokea jumla ya waandishi sita kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya Nchini China ikiwa ni njia mojawapo ya kuendeleza juhudi za kutangaza vivutio vya utalii katika nchi hiyo,” alisema Bi.Mdachi Alisema tumejipanga kukuza soko la utalii kwa kuongeza idadi ya watilii kutoka china kwani ni moja ya nchi yenye watu wengi duniani hivyo kwa njia ya kuwatumia waandishi wa habari itasaidia kuvitangaza vivutio vyetu kwa urahisi zaidi.

Aliongezea kuwa pamoja na kuvitangaza vivutio vyetu ni lazima kuboresha miundombinu hususani barabara katika maeneno ya vivutio ili kuwapa urahisi watalii kufika katika maeneo ya hifadhi. “Wamevutiwa sana na vivutio vyetu na wameahidi kuwa mabalozi wetu nchini kwao wa kuvitangaza vivutio vyetu,”alisema Bi Mdachi Alisema matumaini yetu kupitia ujio huu ni kupata watalii wengi kutoka nchini China na njia hii ya kutumia waandishi wa habari tutaendelea kuitumia kwa nchi nyingine ili nao wawemabalozi katika nchi zao na hatimae kukuza sekta ya utalii nchini.

Akiongea kwa niaba ya watalii wengine Mhariri Msaidizi kutoka China Daily Media Group Bw. Kang Bing alisema wamefurahi kuona vivutio vilivyopo Tanzania pamoja na ukarimu wa watanzania. “Tulitembelea maeneo mbalimbali kama Ngorongoro na ziwa Manyara na kuona wanyama na ndege mandhari nzuri na hili limekuwa somo jipya kwetu,” alisema Bw. Bing Alisema tutakwenda kuwa mabalozi wa kutangaza maeneo ya vivutio vya utalii kupitia machapisho na makala mbalimbali ili kuchochea idadi ya watalii kutoka china kuongezeka.

Changamoto kubwa ni kuboresha miundombinu ya barabara katika maeneo ya hifadhi na pia kuwekeza kwenye usafiri wa anga kwa kuwa na safari za moja kwa moja. Jumla ya waandishi sita kutoka Beijing Press Group, China Daily, International Liaison Drpartment, English news service na China Radio International walitembelea hifadhi ya Ziwa Manyara na Ngorongoro Crater.

UCHANGIAJI WA MIGUU BANDIA KWA WATU 1,000

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo ametangaza kuanza kwa Kampeni ya Uchangiaji wa Miguu Bandia kwaajili ya Wananchi 1,000 wenye uhitaji wa Miguu hiyo ili kuwawezesha kutembea na kufanya shughuli zao.

Katika zoezi hilo Wananchi wataweza kutoa Michango yao kwa njia ya Simu, Bank au kufika Ofisi za Mkuu wa Mkoa na kuwasilisha michango yao.

Hatua hii inakuja baada ya wenye uhitaji wa Miguu Bandia*kuwa kubwa tofauti na ile iliyokusudiwa na Mkuu wa Mkoa ya watu 200 ambapo awamu ya kwanza jumla ya watu *650 walichukuliwa vipimo.

Makonda amesema bado uhitaji wa Miguu hiyo ni mkubwa hivyo amewaomba wadau ikiwemo Makampuni, Taasisi na Watu Binafsi kujitokeze kuchangia ili kutimiza dhamira yake ya kuwafanya walemavu kutembea.

Hadi sasa Wadau mbalimbali ikiwemo CCBRT wamechangia Miguu 25 kwaajili ya Miguu ya watu wenye Ugomjwa wa Kisukari,Msanii Mrisho Mpoto miguu mitatu huku Taasisi za MOI, Ajma Othopedics Medical Service wakiunga mkono zoezi hilo.

Baada ya kuona uhitaji ni mkubwa wa Wananchi Kituo cha Utangazaji cha EFM na TV E wameamua kumuunga mkono RC Makonda kwa kuibeba Kampeni hiyo kwa kuhamasisha uchangiaji kupitia vipindi mbalimbali.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumzana na waandishi wa habari leo juu ya  Kampeni ya Uchangiaji wa Miguu Bandia kwaajili ya Wananchi 1,000 wenye uhitaji wa Miguu hiyo
 Meneja Mkuu wa EFM Radio na Tv E , Denis Busulwa (SEBO), (kulia) kizungumza na Waandishi wa Habari juu ya  kumuunga mkono RC Makonda kwa kuibeba Kampeni hiyo kwa kuhamasisha uchangiaji kupitia vipindi mbalimbali Tv na Radio. Picha na Emmanuel  Massaka,Globu ya Jamii

RC SHINYANGA AFANYA MKUTANO WA HADHARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI MJINI SHINYANGA

$
0
0

Leo Jumatatu Agosti 21,2017,Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack (aliyesimama pichani) amefanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Zimamoto karibu na soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga kusikiliza kero za wananchi.

Mkuu huyo wa mkoa wa Shinyanga aliyekuwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa,na watumishi mbalimbali wa serikali alisikiliza kisha kujibu kero za wananchi huku pia akitoa nafasi kwa watumishi kutoka idara mbalimbali kujibu hoja na kero za wananchi.

Miongoni mwa kero zilizoibuka eneo la mkutano huo ni pamoja na ardhi ambapo baadhi ya wananchi walieleza kutoridhishwa namna ardhi inavyotolewa na jinsi migogoro ya ardhi inavyotatuliwa.

Kero nyingine ni ukosefu wa maadili kwa baadhi ya askari polisi waliodaiwa kutowajali wananchi wanaofika katika kituo cha polisi huku askari polisi wakiendelea kufanya mambo yao ikiwemo kuchat kwenye mitandao ya kijamii badala ya kuhudumia wananchi wanaofika kituoni.

Suala la vumbi katika barabara ambazo ujenzi wake haukamiliki mjini Shinyanga nalo likiibuka kwamba afya zao ziko hatarini kutokana na vumbi hilo. Pia wananchi wakaomba kuwekewa taa za barabarani pamoja na askari wa usalama barabarani katika eneo la Japanese Corner mjini Shinyanga ambapo panadaiwa kutokea ajali za mara kwa mara.

Kero ya bei kubwa ya maji nayo haikusahaulika,wananchi walieleza kuwa bei ya maji inayotozwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika manispaa ya Shinyanga (SHUWASA). Hali kadhalika wananchi wakaomba kuwekewa sehemu ya kupumzikia walau wawekewe mwamvuli katika mahakama ya Mwanzo mjini Shinyanga. Wananchi pia waliomba kuongezwa kwa waganga katika kituo cha afya Kambarage ambacho kinadaiwa kuzidiwa na idadi ya wagonjwa wanaofika kupata huduma.

Wazee nao wakatoa kilio chao cha kutaka huduma bora ya afya wakiomba kuingizwa kwenye bima ya afya badala ya kupewa tu dawa bure. kijibu hoja mbalimbali za wananchi,Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack aliwataka watumishi wa umma kuzingatia maadili yao ya kazi katika kuwatumikia wananchi huku akiwasisitiza kutatua kero za wananchi kwa wakati.

Telack alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kutoa taarifa pale inapotokea mkandarasi anayejenga barabara mjini hajamwaga maji kwenye barabara kwani wamemwagiza kuwa anamwaga maji ili kuepusha vumbi. Aidha baada kusikiliza kero za wananchi,mkuu huyo wa mkoa aliagiza kupewa taarifa ya utekelezaji wa mambo mbalimbali waliyokubaliana wakati wa mkutano huowa hadhara ifikapo Septemba 15,2017 ili kuhakikisha kero za wananchi zinapungua.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara kusikiliza kero za wananchi leo mjini Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akizungumza

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akiendelea kuzungumza na wananchi.
Viongozi mbalimbali wakiwa eneo la mkutano,kushoto ni Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akifuatiwa na kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,Simon Haule na mkuu wa upelelezi mkoa wa Shinyanga

Mkazi wa Shinyanga mjini Ndyamkama Venant akieleza kero zake kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga.

Mkutano unaendelea,viongozi wakiandika dondoo muhimu/maswali ya wananchi

Mwananchi akieleza kero zake

Mkazi wa Shinyanga akieleza kero yake

Mwananchi akieleza kero yake

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akisikiliza kero za wananchi

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,Simon Haule akijibu kero za wananchi kuhusu jeshi la polisi





Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,Simon Haule akizungumza





Afisa Ardhi wa manispaa ya Shinyanga,Alex Rutailwa akijibu hoja za wananchi kuhusu migogoro ya ardhi.





Viongozi mbalimbali wakiwa eneo la mkutano





Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika manispaa ya Shinyanga (SHUWASA),Injinia Sylivester Mahole akijibu hoja za wananchi kuhusu maji.





Mkutano unaendelea





Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi akijibu hoja za wananchi





Mkutano unaendelea





Mwananchi akieleza kero zake





Katibu tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akijibu hoja za wananchi





Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea





Mwananchi akiuliza swali wakati wa mkutano huo





Mkutano unaendelea





Wananchi wakiwa katika mkutano huo





Mwananchi akieleza kero yake




Mwananchi akieleza kero yake

Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dk. Rashid Mfaume akijibu hoja za wananchi
Mkazi wa Shinyanga Mjini,Mohammed Diwani Mkambala akieleza kero yake kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga

Wananchi wakiwa katika foleni wakiuliza maswali na kueleza kero zao

Mwananchi akieleza kero yake.


Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Waziri Maghembe 'kuibeba' Rock City Marathon

$
0
0
Dar es Salaam;WAZIRI wa Maliasili na Utalii Prof Jumanne Maghembe mwishoni mwa wiki hii alizindua rasmi usajili wa msimu wa nane wa mbio za Rock City Marathon huku akiahidi kushirikiana na waandaaji wa mbio hizo katika kuhakikisha kuwa zinatumika vema kuutangaza utalii wa ndani.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa mchezo huo wakiwemo viongozi wa serikali pamoja na wadhamini mbalimbali wa mbio hizo, Waziri Maghembe alisema azma yake hiyo inasukumwa na malengo ya mbio hizo ambayo ni kutumia mchezo wa riadha katika kutangaza utalii hususani katika Ukanda wa Ziwa.

"Kwa kuzingatia uzito wa malengo ya mbio hizo nitamke bayana kuwa nipo tayari kushirikiana na waandaaji wa mbio hizi kuhakikisha kwamba kuanzia mwaka huu mbio hizi zinafana na zinavutia washiriki wengi zaidi hususani wa kimataifa,'' alisema Waziri Maghembe ambae pia alithibitisha ushiriki wake kwenye mbio hizo zinazoratarajiwa kufanyika Octoba 29, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na kupita katika barabara mbalimbali za jiji hilo kabla hazijamalizikia katika uwanja huo.

Mbali na ushiriki wake,Waziri Maghembe alitoa wito kwa mashirika mbalimbali yaliyo chini ya wizara yake ikiwemo la Hifadhi za Taifa(Tanapa), Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori (TAWA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Makumbusho ya Taifa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kufanikisha mbio hizo.

"Ukanda wa Ziwa una vivutio vingi ambavyo pia kama Wizara yenye dhamana ya utalii lazima tuvigeukie na kuvitangaza kwa nguvu na kwa njia tofauti ikiwemo michezo,'' alisema Waziri Maghembe huku akivitaja baadhi ya vivutio hivyo kuwa ni pamoja na Kisiwa cha Saanane, Makumbusho ya kabila la Wasukuma pamoja na tamaduni za makabila ya wakazi wa Kanda ya Ziwa.

Mbio za Rock City Marathon zilizoanzishwa miaka minane iliyopita zinazozidi kujiongezea umaarufu kila mwaka na tayari zimefanikiwa kuwavutia baadhi ya wadhamini ikiwa ni pamoja na kampuni za TIPER, PUMA, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Mwanza Hotel , Real PR Solutions Limited, Afrimax Strategic Partnerships Limited, EF Outdoor, CF Hospital na ATCL.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Bw Zenno Ngowi alitoa wito kwa washiriki wa ndani hususani wa mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na wadhamini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo ambazo kwa mwaka jana zilifanikiwa kuhusisha washiriki zaidi ya 2000 na watazamaji zaidi ya 30,000. 

Naye Mratibu wa mbio hizo zinazoandaliwa na kampuni ya Capital Plus International, Bi Adeline Ndesanjo alisema mbio za mwaka huu zinatarajiwa kuhusisha washiriki wengi zaidi kutoka kila kona ya dunia ikiwemo Afrika, Ulaya,China,Mashariki ya Kati hususani Israel na Marekani huku akitoa wito kwa washiriki wa ndani kujisajili kwa wingi ili kuthibitisha ushiriki wao kwenye mbio hizo.

Akizungumza kwa niaba ya wadhamini wengine wa mbio hizo Meneja Masoko wa Kampuni ya mafuta ya Puma, Bw Machumani Shebe alisema ushiriki wao umechagizwa zaidi na azma ya kampuni hiyo kuisaidia serikali katika kuutangaza utalii wa ndani.

"Tukiwa kama wadau muhimu katika biashara ya mafuta hususani mafuta ya ndege tunategemea sana ustawi wa sekta ya utalii katika kuongeza soko la biashara yetu na kwa kuwa mchezo wa riadha umekuwa ukitumika zaidi katika kuwavutia watalii tukaona kuna haja ya kuunga mkono ufanikishaji wa mbio hizi,'' alisema.

 WAZIRI wa Maliasili na Utalii Prof Jumanne Maghembe akizungumza na wadau mbalimbali wa mchezo wa riadha hapa nchini pamoja na waandaaji wa mbio za Rock City Marathon kwenye hafla maalumu ya uzinduzi  rasmi usajili wa msimu msimu wa nane wa mbio hizo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. 
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Bw Zenno Ngowi akizungumza kwenye hafla hiyo. Alitoa wito kwa washiriki wa ndani hususani wa mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na wadhamini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo ambazo kwa mwaka jana zilifanikiwa kuhusisha washiriki zaidi ya 2000 na watazamaji zaidi ya 30,000. 
 Mratibu wa mbio hizo zinazoandaliwa na kampuni ya Capital Plus International, Bi Adeline Ndesanjo akitoa maelezo kuhusu maandalizi ya mbio hizo kwenye hafla hiyo. Alisema mbio za mwaka huu zinatarajiwa kuhusisha washiriki wengi zaidi kutoka kila kona ya dunia ikiwemo Afrika, Ulaya,China,Mashariki ya Kati hususani Israel na Marekani . 
 Wadhamini nao hawakuwa nyuma!Meneja Masoko wa Kampuni ya mafuta ya Puma Energy, Bw Machumani Shebe alisema ushiriki wao kwenye mbio hizo umechagizwa zaidi na azma ya kampuni yake hiyo kuisaidia serikali katika kuutangaza utalii wa ndani. 
 Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Prof Jumanne Maghembe akiwa kwenye picha ya pamoja na waandaaji wa mbio hizo pamoja na wadau mbalimbali wa mchezo huo wakiwemo  viongozi wa serikali pamoja na wadhamini wa mbio hizo.


Mohamed Kivugo: Milioni 20 za Biko nitajengea nyumba

$
0
0
FUNDI magari mkazi wa Tabata, jijini Dar es Salaam, Mohamed Kivugo mwenye miaka 45, amesema kwamba fedha zake alizokabidhiwa jana baada ya kushinda kwenye Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', atazitumia kujengea nyumba ili aondokane na changamoto ya makazi.

Kivugo aliyasema hayo jana wakati anapokea zawadi ya Sh Milioni 20 za ushindi wa Biko alizokabidhiwa katika benki ya NMB, tawi la Bank House Posta, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Kivugo alisema dhamira yake kubwa ni kutatua changamoto ya makazi kwa kuzitumia fedha za Biko kujenga nyumba.

"Ingawa nimepata ushauri mzuri kutoka kwa watu wa NMB baada ya kukabidhiwa fedha zangu kutoka Biko baada ya kushinda kwenye droo ya 33 iliyochezeshwa Jumapili, lakini naamini wazo la nyumba ni zuri kwangu.

"Nawashauri Watanzania wenzangu wacheze Biko mara nyingi na wasikate tamaa ili waweze kuibuka na ushindi kama nilivyoibuka mimi, ukizingatia kuwa biko ni bahati nasibu inayotoa ushindi na kukabidhi fedha kwa Jataka, "Alisema.

Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, aliwataka Watanzania kucheza Biko ili wavune utajiri mkubwa kutoka kwenye bahati nasibu yao inayochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kuanzia Sh 1000 na kuendelea katika Tigo Pesa, MPesa na Airtel Money huku namba ya Kampuni ikiwa ni 505050 na kumbukumbu ni 2456.

"Kushinda Biko ni rahisi pamoja na kupokea zawadi mbalimbali kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh milioni moja zinazolipwa moja kwa moja kwenye simu za washindi wanazotumia kuchezea Biko bila kusahau donge nono la Sh Milioni 20 inayotoka kila Jumatano na Jumapili kama aliyoshinda mshindi wetu Kivugo wa Tabata," Alisema.

Kwa mujibu wa Melles, zaidi ya Sh Bilioni mbili zimelipwa kwa washindi katika miezi mitatu ya Mei, Juni na Julai, huku akiwataka Watanzania wacheze kwa wingi na mara nyingi ili wajiwekee mazingira mazuri ya kuibuka mamilioni ya bahati nasibu ya Biko.


Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles kulia mwenye fulana ya Biko akimkabidhi fedha zake mshindi wao wa Bahati Nasibu, Mohamed Kivugo aliyeibuka kidedea katika droo ya 33 iliyochezeshwa Jumapili. Kushoto ni Afisa wa NMB, Tawi la Bank House, Posta jijini Dar es Salaam akishuhudia makabidhiano hayo.
Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko, Mohamed Kivugo akiwa ameshika fedha zake baada ya kukabidhiwa jana katika Tawi la NMB la Bank  House, Posta, jijini Dar es Salaam tayari kwa matumizi yake ya kawaida.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI NCHINI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Kaimu Balozi wa Marekani nchini Mhe.Inmi Patterson aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam na kujitambulisha na kufanya mazungumzo kwa mara ya kwanza tangu alipowasili nchini.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Mhe. Inmi Patterson (Katikati) mara baada ya kujitambulisha ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.

MADIWANI ACHENI KUINGILIA KAZI ZA WATAALAM " DC MBINGA"

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Mbinga Cosmas Nshenye awajia juu madiwani wanaoingilia kazi za wataalam na kusababisha kurudisha nyuma maendeleo ya wilaya hiyo.

KILIMO CHA UFUTA NA MIHOGO CHA PIGIWA DEBE NA ZAMBI.

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi akizungumza na ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania wakati walipomtembelea ofisini kwake mjini Lindi.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) akitambulisha msafara wake kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi (hayupo pichani) wakati walipomtembelea ofisini kwake mjini Lindi. Kushoto ni Meneja Mikopo, Bw. Samuel Mshote na  Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (katikati).
 Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (aliyesimama) akiwasilisha mada juu ya fursa za mikopo zinazotolewa na Benki ya Kilimo kwa Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Na Mwandishi wetu, Lind.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi ameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kukopesha wakulima wa mazao ya ufuta na mihogo ili waweze kulima kilimo cha kisasa na cha kibiashara hasa kwa wakulima wadogo wadogo wa mkoani humo.
 
Bw. Zambi alitoa wito huo wakati wa mkutano wa Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Bw. Zambi alisema kuwa mkoa wa Lindi ni mkoa uliojaaliwa katika kuzalisha mazao ya ufuta na mihogo lakini changamoto kubwa ni mtaji wa kulima kibiashara ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.

“Wakulima wa mkoa wa Lindi wapo tayari kushiriki katika kuleta mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara lakini kwa sasa suala la mtaji wa kilimo cha kibiashara ni changamoto kubwa,” alisema Bw. Zambi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema kuwa Benki ya kilimo ipo tayari kutoa mikopo kwa wakulima wadogo wadogo waliokuwa kwenye vikundi ili waweze kukopeshwa.

Bw. Assenga aliongeza kuwa Benki ya Kilimo pia ipo tayari kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo ya Kilimo kwa kuipatia mikopo yenye riba nafuu zilizo chini ya viwango vya kibiashara kwenye soko.

“Kwa kutambua umuhimu wa wakulima wadogo wadogo nchini TADB imedhamiria na kujizatiti kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika  kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa kusaidia upatikanaji na utoaji wa fedha ikiwa ni pamoja sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini,” alisema.

Naye, Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Chacha alisema kuwa TADB inalenga kuongeza upatikanaji wa huduma zisizo za kifedha kwa wakulima kama vile kujengewa uwezo juu ya uandaaji wa andiko la miradi ya Kilimo, pamoja na upatikanaji wa taarifa za masoko, usimamizi wa biashara, mafunzo juu ya miradi ya Kilimo na mbinu za majadiliano ya mikataba.

 “Tupo tayari kutoa mikopo kwa ajili ya kuwanyanyua wakulima kama ilivyolengwa na Serikali kupitia mikopo ya pembejeo kuongeza tija kwenye uzalishaji, miundo mbinu ya umwagiliaji na ununuzi wa zana za kilimo,” alisema.

Bw. Chacha aliongeza kuwa kwa upande wa mikoa ya kusini Benki ya Kilimo imejipanga kueendeleza miundombinu ya umwagiliaji na maghala pamoja na uzalishaji wa mbegu bora za mazao ya korosho na mihogo na kuimarisha viwanda vya kubangua mazao ya korosho, na kusindika ufuta, mihogo.

Bw. Chacha aliongeza kuwa Benki imejipanga kuwezesha uanzishaji wa mashamba mapya na ya kisasa ya mihogo, korosho na ufuta mkoani Lindi.

RIPOTI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI YATHIBITISHA MANJI ANATUMIA DAWA ZA KULEVYA.

$
0
0

 Mfanyabiashara Maarufu nchini, Yusuph Manji akiteta jambo na Wakili wake, Hudson Ndusyepo wakati wakiwa ndani ya mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu jijini Dar es Salaam leo kabla ya kusomewa mashtaka yanayomkabili.

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

SHAHIDI wa Kwanza katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili mfanyabiashara maarufu, Yusuph Manji amedai mahakani kuwa uchunguzi Wa mkemia Mkuu umeonyesha Manji anatumia dawa za kulevya.

Shahidi huyo wa kwanza wa upande wa jamuhuri, Ramadhani Kingai ambaye no Naibu Mkuu wa upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam amedai hayo leo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Akiongozwa na Wakili Wa Jamuhuri, Timon Vitalis, Kingai amedai, February 9 mwaka huu aliambiwa kufanya uchunguzi wa suala lililoripotiwa na Mkuu wa mkoa Wa Dar es Salaam Paul Makonda  juu ya watuhumiwa wa dawa za kulevya wakiwemo Josephat Gwajima na Yusuph Manji. 

Amesema alimuelekeza Dutektivu Koplo Sospter kuwapeleka Manji ambaye alifika katika kituo cha polisi mwenyewe na Gwajima kupelekwa kwa Mkemia Mkuu kupimwa juu ya tuhuma hizo za dawa za kulevya ambapo baadae walipata taarifa kuwa Manji anatumia dawa za kulevya.
Alidai baada ya ripoti hiyo, alielekeza Manji afunguliwe jalada la kutumia dawa za kulevya kisha kwa DPP ambaye alimfungulia mashtaka

Hata hivyo shahidi Kingai alipoulizwa nani alielekeza kuwa dawa anazodaiwa kutumia Manji ni Heroine alidai, yeye alifanya upelelezi tu ila anayeandaa mashtaka in DPP.

Naye shahidi wa pili Koplo Sospeter amedai alipokea maelekezo juu ya mtuhumiwa Manji ambapo moja ya maelekezo hayo yalikuwa yakimtaka kumpeleka Manji  kwa mkemia Mkuu kwa ajili ya kupima sampuli  ya mkojo ambapo baada ya kufuata taratibu za ofisi ya mkemia na kupata namba ya maabara alimpeleka Manji msalani ambapo aliweka mkojo kwenye chupa maalumu kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.
Amedai Februari 10, mwaka huu  majibu yalitoka na akakuta yanasema mkojo wake una chembechembe za dawa za kulevya.
Kesi hiyo itaendelea kesho.
Mfanyabiashara Maarufu nchini, Yusuph Manji akiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akisubiri  kusomewa kesi ya Madawa ya Kulevya inayomkabiri.
 Mfanyabiashara Maarufu nchini, Yusuph Manji akiwa ndani ya ukumbi wa mahakama ya Hakimu Makazi Kisutu jijini Dar es Salaam akisubiri kusomewa mashtaka yanayo mkabiri.
Mazungumzo yakiendelea.Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live




Latest Images