Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live

ZAMBI APIGIA DEBE UWEZESHAJI WA KILIMO CHA UFUTA NA MIHOGO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi akizungumza na ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania wakati walipomtembelea ofisini kwake mjini Lindi. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) akitambulisha msafara wake kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi (hayupo pichani) wakati walipomtembelea ofisini kwake mjini Lindi. Kushoto ni Meneja Mikopo, Bw. Samuel Mshote na  Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (katikati).
Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (aliyesimama) akiwasilisha mada juu ya fursa za mikopo zinazotolewa na Benki ya Kilimo kwa Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Na Mwandishi wetu, Lindi .

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi ameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kukopesha wakulima wa mazao ya ufuta na mihogo ili waweze kulima kilimo cha kisasa na cha kibiashara hasa kwa wakulima wadogo wadogo wa mkoani humo.

Bw. Zambi alitoa wito huo wakati wa mkutano wa Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Bw. Zambi alisema kuwa mkoa wa Lindi ni mkoa uliojaaliwa katika kuzalisha mazao ya ufuta na mihogo lakini changamoto kubwa ni mtaji wa kulima kibiashara ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.

“Wakulima wa mkoa wa Lindi wapo tayari kushiriki katika kuleta mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara lakini kwa sasa suala la mtaji wa kilimo cha kibiashara ni changamoto kubwa,” alisema Bw. Zambi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema kuwa Benki ya kilimo ipo tayari kutoa mikopo kwa wakulima wadogo wadogo waliokuwa kwenye vikundi ili waweze kukopeshwa.

Bw. Assenga aliongeza kuwa Benki ya Kilimo pia ipo tayari kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo ya Kilimo kwa kuipatia mikopo yenye riba nafuu zilizo chini ya viwango vya kibiashara kwenye soko.

“Kwa kutambua umuhimu wa wakulima wadogo wadogo nchini TADB imedhamiria na kujizatiti kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika  kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa kusaidia upatikanaji na utoaji wa fedha ikiwa ni pamoja sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini,” alisema.

Naye, Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Chacha alisema kuwa TADB inalenga kuongeza upatikanaji wa huduma zisizo za kifedha kwa wakulima kama vile kujengewa uwezo juu ya uandaaji wa andiko la miradi ya Kilimo, pamoja na upatikanaji wa taarifa za masoko, usimamizi wa biashara, mafunzo juu ya miradi ya Kilimo na mbinu za majadiliano ya mikataba.

 “Tupo tayari kutoa mikopo kwa ajili ya kuwanyanyua wakulima kama ilivyolengwa na Serikali kupitia mikopo ya pembejeo kuongeza tija kwenye uzalishaji, miundo mbinu ya umwagiliaji na ununuzi wa zana za kilimo,” alisema.

Bw. Chacha aliongeza kuwa kwa upande wa mikoa ya kusini Benki ya Kilimo imejipanga kueendeleza miundombinu ya umwagiliaji na maghala pamoja na uzalishaji wa mbegu bora za mazao ya korosho na mihogo na kuimarisha viwanda vya kubangua mazao ya korosho, na kusindika ufuta, mihogo.
Bw. Chacha aliongeza kuwa Benki imejipanga kuwezesha uanzishaji wa mashamba mapya na ya kisasa ya mihogo, korosho na ufuta mkoani Lindi.

MWANZA: MTU MMOJA AMEUAWA NA KUNDI LA WATU WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA KOSA LA WIZI WA KUKU WILAYANI KWIMBA.

$
0
0
KWAMBA TAREHE 21/08/2017 MAJIRA YA 08:45HRS ASUBUHI KATIKA KITONGOJI CHA BUSULWA KATA YA NGULLA WILAYA YA KWIMBA MKOA WA MWANZA, LEONARD MATHIAS MIAKA 23, MKAZI WA KIJIJI CHA NGULLA, ALIUAWA NA KUNDI LA WATU WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA KUPIGWA FIMBO NA MAWE SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE KISHA BAADAE KUCHOMWA MOTO HADI KUPOTEZA MAISHA KWA KOSA LA WIZI WA KUKU WATANO MALI YA ESTER ROBERT, MKAZI WA KIJIJI CHA NGULLA, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.

INASEMEKANA KUWA MAREHEMU ALIIBA KUKU WATANO NYUMBANI KWA BI ESTER ROBERT KIJIJINI NGULLA KISHA ALIKIMBILIA KIJIJI CHA JIRANI CHA MWABOMBA. INADAIWA KUWA  WANANCHI WA KIJIJI CHA MWABOMBA WALIPOMUONA MAREHEMU AKIWA NA KUKU HAO WALIPATA MASHAKA KISHA WALIMKAMATA NA BAADAE WALITOA TAARIFA KIJIJI CHA NGULLA NDIPO MWENYE KUKU BI ESTER ROBERT ALIFIKA NA KUKABIDHIWA KUKU WAKE.

INADAIWA KUWA BAADA YA MAREHEMU KUKABIDHI KUKU KWA MWENYE MALI, WANANCHI WALIMCHUKUA NA KWENDA NAE KITUO CHA POLISI LAKINI WAKIWA NJIANI WALIANZA KUMSHAMBULIA KWA KUMPIGA FIMBO NA MAWE SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA BAADAE KUMCHOMA MOTO. POLISI WALIPATA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA NDIPO WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO NA TUKIO NA KUFANIKIWA KUKAMATA WATU SABA AMBAO WANADAIWA KUHUSIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA MAUAJI HAYO.

POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO WATUHUMIWA SABA WALIOKAMATWA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA KISHA IKITHIBITIKA WATUHUMIWA WALIHUSIKA KATIKA MAUAJI HAYO WATAFIKISHWA MAHAKAMANI. AIDHA UPELELEZI NA MSAKO WA KUWATAFUTA WATU WENGINE WALIOHUSIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA MAUAJI HAYO BADO UNAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KOSA LA JINAI, BALI PINDI WANAPOMKAMATA WAHALIFU AU MHALIFU WAMPELEKE KWENYE KITUO CHA POLISI ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAKE. PIA ANAOMBA WANANCHI WAENDELEE KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA WAHALIFU NA UHALIFU ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.

IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

SHULE YA GENIUS KINGS YAJIPANGA KUWA SHULE BORA KITAALUMA TANZANIA

$
0
0

Wanafunzi wa shule ya Genius Kings Nursery and Primary School iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam, wakifundishwa somo la kompyuta.
Wanafunzi wa darasa la tano wakimsikiliza kwa makini mwalimu wa taaluma.
Wanafunzi wa darasa la sita na la saba katika wa shule ya Genius Kings wakiwa katika chumba cha maabara wakijifunza somo la sayansi kwa vitendo.


Wanafunzi wa darasa la sita na la saba katika wa shule ya Genius Kings wakiwa katika chumba cha maabara wakijifunza somo la sayansi kwa vitendo wakitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Shule hiyo Bw. Machage Kisyeri.
Mkurugenzi wa Shule hiyo Bw. Machage Kisyeri akiwa ofisini kwake. Shule ya awali na ya msingi ya Genius Kings iliyopo Tabata-Segerea jijini Dar es Salaam imejizatiti kuhakikisha inakuwa shule bora na ya mfano kitaaluma ikiwa ni mwendelezo wa mafanikio ambayo imeyapata katika kipindi cha miaka 10 tangia kuanzishwa kwake. 
 
Akiongea jijini Dar es Salaam kuhusiana na maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake ambayo yameanza kusherehekewa mapema wiki na kutarajia kumalizika mapema mwezi Desemba mwaka huu,Mkuu wa shule hiyo,Bw.Aloyce Siame,alisema licha ya kwamba mwanzo huwa ni mgumu kwa mradi wowote ule, shule imeweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta ya elimu na kuweza kuchomoza kuwa miongoni mwa shule zinazofanya vizuri mkoani Dar es Salaam na kwa ngazi ya kitaifa. 
 
Bw.Siame alisema kuwa katika kipindi cha miaka 10 shule imeweza kushikilia rekodi ya kufanya vizuri kwa kufaulisha wanafunzi wa darasa la saba na la nne kwa kiwango cha juu na kuingia katika shule tano bora wilayani Ilala na shule bora 20 mkoani Dar es Salaam mfululizo hali ambayo imewajengea hari ya kuzidi kufanya vizuri kwa mwaka huu na miaka ijayo. 
 
“Moja ya mtazamo wa shule hii ni kuifanya kuwa shule bora ya mfano inayotoa elimu bora nchini kuanzia shule ya awali na shule ya msingi.Tumejipanga kuhakikisha lengo hili linatimia na tunatoa shukrani kwa serikali,wazazi na wadau wote ambao wameonyesha kutuunga mkono katika kipindi hiki cha awamu ya kwanza ya mwanzo ya miaka 10 na kuwezesha mafanikio haya kupatikana”.Alisema. 
 
Aliongeza kuwa mbali na kufundisha masomo ya darasani kwa nadharia na vitendo na ujuzi wa kutumia kompyuta kupata maarifa ya kielimu shule inatoa mafunzo ya kuwajengea wanafunzi uwezo wa kuwa wabunifu,Sanaa,michezo mbalimbali,kuwajengea uwezo wa kujiamini kuongea mbele ya hadhara na kufanya mijadala ya kuchambua masuala yanayohusiana na elimu na nyanja nyinginezo hususani masuala yanayoendelea hapa nchini na nje ya nchi bila kusahau kuibua na kukuza vipaji vya wanafunzi. 
 
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa shule hiyo,Bw.Machage Kisyeri,alisema anajivunia kwa mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka 10 na kuahidi kuwa uongozi umejipanga kuhakikisha kitaalamu shule inazidi kupanda zaidi na kuimarisha mafunzo ya shule ya awali kwa ajili ya kuwaandaa wanafunzi wadogo kupata elimu bora zaidi kwa kutumia nyenzo mbalimbali za kisasa,kuimarisha miundombinu na kuongeza walimu wenye ujuzi mkubwa wa kufundisha madarasa ya chini ya watoto wadogo kwa kuwa msingi mzuri kielimu ndio unawezesha watoto kuendelea kufanya vizuri katika masomo yao. 
 
Kuhusiana na changamoto wanazokabiliana nazo alisema kuwa zipo changamoto za kawaida kinachotakiwa ni ushirikiano baina ya wazazi,walimu,na wadau wanaosimamia elimu ili kuhakikisha mafanikio yanapatikana na elimu ya Tanzania inazidi kupanda “Walimu wakiwezeshwa vizuri na kupewa ushirikiano wa kutosha naamini shule nyingi za Tanzania zitatoa elimu bora kwa kuwa tunao walimu wengi wazuri ambao wakitumiwa ipasavyo tutasonga mbele”.Alisema.
 
 Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake,Mwanafunzi John Magongo anayesoma darasa la saba shuleni hapa alisema kuwa wanawezeshwa kupatiwa elimu ya kuwajengea uwezo wa kufanya vizuri kitaaluma ,nidhamu, kujiamini na kujituma kiasi kwamba popote watakapokwenda wanaamini watazidi kung’ara kutokana na elimu inayotolewa shuleni hapo. 
 
Shule ya Genius Kings ilianzishwa mnamo mwaka 2008 na vijana wa kitanzania wenye taaluma mbalimbali ambapo waliweza kupata walimu wazuri ambao kwa kipindi chote hiki wamewezesha kupatikana mafanikio ya shule kuwanoa wanafunzi vizuri kitaaluma na kuwa miongoni mwa shule bora mkoani Dar es Salaam ,pia uwekezaji wa shule hii umewezesha kupunguza tatizo la ajira kwa kuwa mbali na kuajiri walimu imeajiri wafanyakazi katika vitengo vyake mbalimbali vya uendeshaji.

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YATEMBELA MIRADI YA UMEME WA GESI YA KINYEREZI II NA ULE WA UPANUZI KINYEREZI I

$
0
0
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (Mb), wapili kulia, akiwaongoza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, kutembelea mradi wa umeme wa Kinyerezi II na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I jijini Dar es Salaam, Agosti 21, 2018. Kamati hiyo pia ilitembelea kituo cha kupkea gesi asili kilicho jirani na Miradi hiyo.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KAMATI ya Bunge ya Bajeti, imetembelea miradi ya kuzalisha umeme wa gesi ya Kinyerezi II, na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I unaoendeshwa na Serikali kupitia Shrika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo.
Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Mtwara vijijini Mhe. Hawa Ghasia, pia ilitembelea kituo cha kupokea gesi asili inayotumika kuzalisha umeme kilichoko jirani na miradi hiyo.
Katika ziara hiyo, mwenyeji wa Kamati hiyo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, (Mb), Mhe.Dkt.Medard Kalemani, aliwahakikishia wajumbe wa Kamati hiyo kuwa miradi hiyo inaendelea kama ambavyo Serikali ilitarajia na kwamba Watanzania wategemee ongezeko kubwa la upatikanaji wa umeme pindi miradi hiyo itakapokamilika. “Mhe. Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Kamati, miradi hii kunzia ule wa Kinyerezi I unaopanuliwa ambapo kutakuwa na ongezeko la umeme Megawati 35 na hivyo kufanya jumla ya Megawati 185 zitakazozalishwa kutoka Kinyerezi I, na huu wa Kinyerezi II utakapokamilika Agosti mwakani (2018) utatupatia Megawati 240 na ukijumlisha na miradi mingine itakayofuatia ya Kinyerezi III na VI, tutakuwa na jumla ya Megawati 1175.” Alifafanua Mhe. Dkt. Kalemani.
Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephene Manda aliwaambia wajumbe wa kamati hiyo kuwa mradi huo utakuwa na jumla ya mashine 8 ambazo zitafua umeme na tayari ufungaji wa mashine hizo umeanza na unaendelea na kuongeza kuwa kuanzia Desemba Mosi mwaka huu, TANESCO itaingiza megawati 30 kwenye gridi ya taifa na kufanya hivyo kila baada ya mwezi mmoja kadri kazi ya ufungaji wa mashine hizo utakavyokuwa unakamilika.
Alisema gharama za mradi wa Kinyerezi II ni dola milioni 344.

Wajumbe wa Kamati hiyo pian walipata fursa yua kujionea kazi ya utandazaji wa mabomba makubwa ya kupitisha gesi kutoka kituo cha kupkea gesi kuelekea kwenye eneo la miradi hiyo.


“Niwapongeze sana kwa kazi nzuri mnayoifanya na haya ndio matarajio ya wabunge kuona kuwa miradi hii ambayo inagharimu fedha nyingi za walipa kodi inakamilika kwa wakati ili hatimaye serikali iweze kutekeleza mipango yake ya ujenzi wa uchumi wa viwanda kama ilivyoahidi wananchi.”Alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Hawa Ghasia. Baada ya kumaliza ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi hiyo ya umeme wa gesi asilia.

 Dkt. Kalemani (katikati mbele), akiwaongoza wajumbe hao baada ya kutembelea eneo la mradi wa upanuzi Kinyerezi I
 Hili ndio eneo la upanuzi wa mradi wa umeme Kinyerezi II
 Mtandao wa mabomba ya kusafirisha gesi asilia kutoka kituo cha kupokea gesi hiyo kuelekea eneo la miradi hiyo.
 Mafundi wa TPDC wakiwa wamesimama kwenye eneo la utandazaji wa mabomba hayo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Hawa Ghasia, (wapili kushoto), akizungumza jambo wakati akiongozana na Naibu Waziri Dkt. Kalemani (kushoto) na wajumbe wa kamati.
 Mhe. Hawa Ghasia akiwa tayari kuanza ziara.
 Dkt. Kalemani akiongea wakati wa ziara hiyo.
Mhe. Hawa Ghasia, akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, wakati wajumbe wa Kamati walipowasili eneo la Miradi.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, (TPDC), Mhandisi  Kapuulya Musomba(kulia), akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania, (TANSCO), Dkt. Alex Kyaruzi, (katikati), na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi Dkt. James M. Nzagi.
  Mhe. Hawa Ghasia, akisalimiana na Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James

 Mhe. Hawa Ghasia, akisalimiana na Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji umeme (Generation), Mhandisi Abdallah O. Ikwasa
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania, (TANSCO), Dkt. Alex Kyaruzi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (wakwanza kulia) na Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James wakiwasili eneo la mradi.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (kulia), akiwaonyesha kitu, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (wapili kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Pallangyo, (kushoto) na Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya BajetiJerome Dismas Bwanausi


 Mhe. Hawa Ghasia akizungumza baada ya ziara ya kutembelea kituo cha kupokea gesi asilia kinachosimamiwa na TPDC.
 Wajumbe wa Kamati wakipita pembezoni mwa moja ya mashine kubwa (genereta), kati ya 8 zinazofungwa kwenye mradi wa Kinyerezi II
Mhandisi Manda, (waliyenyoosha mkono), ambaye ni Meneja Mradi wa Kinyerezi II, akwapatia maelezo wajumbe wa Kamati akiwemo Naibu Waziri Dkt. Kalemani.

RIDHIWANI AKABIDHI ZAWADI YA MCHEZAJI BORA SPORTS EXTRA

$
0
0
 Mpiga picha bora wa Michuano ya Ndondo Cup , Rachel Palangyo akiwa na Tunzo yake mara baadaya kukabidhiwa
 Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani  Kikwete akizungumza na familia ya Wanamichezo wakati wautoaji wa Tunzo za Mchezaji borawa michuano ya Ndondo Cup inayoandaliw ana kampuni ya CloudsMedia Group kupitia kipindi chake cha Sports Extra.
  Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani  Kikwete, akikabidhi tunzo ya Mchezaji bora kwa kocha wa timu ya Misosi FcYenye maskani  yake Manzese.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA),Mulamu Nghambi akikabidhi zwadi kwa Refalii borawa michuano ya Ndondo Cup.
 Mkurugenzi wa Vipindi wa kituo cha Televisheni na Radio ya Clouds , Shafii Dauda akikabidhi Zawadi ya Mwandishi bora wa Michuano ya Ndondo  Cup Charles Abel wa Mwananchi.
 Dogo Janja akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi zawadi kwa shabiki bora wa michuano ya Ndondo Cup.
 Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha DRFA , Almas Kasongo akikabidhi zawadi ya heshima kwa Dr JJ Mwaka.

 Dj Sinyorita kutoka kipindi cha XXL cha Clouds Fm akifanya yake katika utoaji wa Tunzo za watu waliofanya vizuri katika Michuano ya Ndondo Cup
 Mtangazaji wa kipindi cha Sports Extra , Mbwiga wa Mbwiguke akifanya yake ya kizaramo jukwaani
   Mbunge wa Chalinze Ridhiwani  Kikwete akimtunza Msanii wa Singeli Msaga Sumu
 Msanii wa Muziki wa SINGELI nchini Msaga Sumu akifanya yake Jukwaani
 
 Wadau wa mpira walioshiriki hafla hiyo ya utoaji Tunzo katika michuano ya Ndondo Cup.
 Wadau wa mpira walioshiriki hafla hiyo ya utoaji Tunzo katika michuano ya Ndondo Cup.

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK SHEN AHITIMISHA ZIARA YAKE MKOA WA MJINI MAGHARIBI

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Akijadiliana Jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh Ayoub Mahamud Mohamed  alipofika kutembelea Ujenzi wa barabara ya Kwamata -Kinuni mpaka Kijito upele  inayojengwa na Mkandarasi wa kampuni ya Mecco,Rais akiwa katika ziara yake ya kutembelea maendeleo ya Miradi ya Maendeleo Wilaya ya Magharibi”B” katika Mkoa wa Mjini Magharibi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Wananchi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wa Kinuni na Magogoni leo alipofanya ziara ya kutembelea Ujenzi wa barabara ya Kwamata -Kinuni mpaka Kijito upele inayojengwa na Mkandarasi wa kampuni ya Mecco, katika ziara yake ya kutembelea maendeleo ya Miradi ya maendeleo Wilaya ya Magharibi”B” katika Mkoa wa Mjini Magharibi,(kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZMhe.Haji Omar Kheir na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud
Baadhi ya Wananchi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wa Kinuni na Magogoni wakiwa katika shamra shamra wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani ) alipofika kutembelea Ujenzi wa barabara ya Kwamata -Kinuni mpaka Kijito upele leo inayojengwa na Mkandarasi wa kampuni ya Mecco,Rais akiwa katika ziara yake ya kutembelea maendeleo ya Miradi ya maendeleo Wilaya ya Magharibi”B” katika Mkoa wa Mjini Magharibi
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh Ayoub Mahamud Mohamed Akieleza Machache Namna kampeni ya Mimi na wewe ilivyoweza kuleta Mapinduzi Makubwa Kwenye Wilaya ya Magharibi B Ambapo wamefanikiwa Kujenga Madarasa Matatu na Maabara  kwa Muda wa Siku kumi na Moja,Rais Shein Amempongeza Mkuu waMkoa huyo kwa Juhudi kwabwa Anazojitolea kuwaletea Maendeleoa Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Akiwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko  Fumba wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara  kuangalia ujenzi wa nyumba hizo zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group,(kushoto ) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibu Nd,Ayoub Mohamed Mahmoud.

  
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibu Nd,Ayoub Mohamed Mahmoud Akimkabidhi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Moja ya zawadi zilizotolewa na Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakati wa Majumuisho ya Ziara ya Siku tatu Aliofanya kwenye Mkoa wa Mjini Magharibi Kukagua Shuguli za Maendeleo


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Akiwa Ameambatana na Viongozi Mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar baada ya Kuhitimisha Ziara ya Siku tatu kwenye Mkoa wa Mjini Magharibi

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Ashiriki Ujenzi wa Taifa wa Skuli ya Msingi Uzi Ngambwa

$
0
0
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akiwa na Wananchi wa jimbo lake katika kisiwa cha uzi ngambwa wakishangilia wakati wa ujenzi wa Taifa wa kujenga madarasa saba ya Skuli ya Msingi  katika Kijiji cha Ngambwa kutowa elimu kwa watoto wa kijiji hicho kupata elimu ya msingi karibu na makaazi yao. Madarasa hayo yanajengwa kwa nguvu za Mwakilishi na Mbunge kwa Wananchi wa Jimbo lao.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akizungumza na wananchi wa Kisiwa cha Uzi Ngambwa wakati wa ujenzi wa madarasa ya Skuli ya Msingi Ngambwa Uzi inayojengwa na Mbunge na Mwakilishi na nguvu Wananchi wa kijiji hicho. 
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akiwahutubia wananchi wa kisiwa cha Uzi Ngambwa jimbo lake wakati wa ujenzi wa Taifa wa madarasa ya Skuli ya Msingi Ngambwa. 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ramadhani Abdallah akizungumza na wananchi wa kisiwa cha Uzi Ngambw wakati wa ujenzi wa Skuli ya Msingi ya Ngambwa. inayojengwa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo la Tunguu na Nguvu za Wananchi wa Kijiji hicho.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akishiriki katika ujenzi wa skuli ya msingi uzi ngambwa. 
Wananchi wa Ngambwa wakiwa katika ujenzi wa Skuli yao ya Msingi.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar akishiriki katika ujenzi huo wa Skuli ya Msingi Ngambwa Uzi.
Mwananchi wakishiriki katika ujenzi huo wa skuli ya msingi katika kisiwa cha Uzi kijiji cha Ngambwa.
Wananchi wa kijiji cha Ngambwa wakifuatilia hafla hiyo ya ujenzi wa Skuli yao mpya ya msinga katika kijiji chao. 
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohamed Said akiwa na bero likiwa na mchanga akishiriki katika ujenzi wa Skuli ya Msingi Ngambwa katika kisiwa cha Uzi Wilaya ya Kati Unguja.
Jengo la madarasa ya Skuli ya Msingi Ngambwa likiendelea na ujenzi wake.
Wananchi wa kijiji cha Ngambwa Uzi wakishiriki katika ujenzi wa madarasa katika kijiji hicho.
Wananchi wa kijiji cha Ngambwa kisiwa cha Uzi wakiwa katika ujenzi wa madarasa ya Skuli ya Msingi Ngambwa inayojengwa kwa nguvu na Mbunge na Mwakilishi kwa kushirikiana na Wananchi wa Kijiji hicho.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu ZanzibarMhe. Simai Mohamed Said akizungumza na Mwananchi wa jimbo lake mkaazi wa Ngabwa Uzi Bi. Mwanaacha Khatib mkulima wa mwani wakati wa hafla ya ujenzi taifa wa skuli ya msingi ngambwa kisiwani humo.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.com
Zanzines.com.
othmanmaulid@gmail.com.

TAASISI YA THPS YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA KUSAIDIA MIFUMO YA AFYA 2016-2020

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mpango Mkakati wa kusaidia mifumo ya afya wa miaka mitano ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016-2020 na Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS). Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA MMG/KAJUNASON.

Wageni na wafanyakazi wa taasisi ya THPS waliohudhuria katika Uzinduzi wa Mpango Mkakati wa kusaidia mifumo ya afya wa miaka mitano ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016-2020 na Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS). Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) Dkt. Augustine Massawe akizungumza katika uzinduzi wa Mpango Mkakati wa kusaidia mifumo ya afya wa miaka mitano ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016- 2020. Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS), Dkt. Redempta Mbatia akizungumza juu ya uzinduzi wa Mpango Mkakati ya kusaidia mifumo ya afya na kuelezea malengo ya taasisi hiyo kwa miaka ijayo kati ya mwaka 2016-2020. Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam.  
 Mmoja ya vijana waelimisha Rika kutoka Zanzibara akitoa somo jinsi ya kujitambua.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akizindua Mpango Mkakati wa kwanza wa kusaidia mifumo ya afya wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016-2020. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Redempta Mbatia na wadau wengine. Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya (wa nne toka Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Redempta Mbatia (wa tako kutoka kushoto) pamoja na wadau wa afya wakionyesha chapisho la Mpango Mkakati wa kwanza wa kusaidia mifumo ya afya wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016-2020.



Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) inayosaidia Wizara za afya Tanzania Bara na Zanzibar kutoa kinga ya Virusi vya Ukimwi (VVU), huduma, matibabu na msaada kwa kuimarisha mifumo ya afya imezindua mpango mkakati wa kwanza wa miaka mitano.

Akizungumza katika uzinduzi huo wa mpango mkakati uliofanyika Jijini Dar es salaam leo. Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi wa THPS, Dkt. Augustine Massawe alisema mpango mkakati wa kwanza wa taasisi hiyo ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016 mpaka 2020 umelenga kusaidia juhudi za Wizara ya afya, Serikali za mitaa, Washiriki wengine na Wadau kuhakikisha huduma bora za afya zinazoshugulikia afya ya umma ikiwemo magonjwa yanayoambukizwa na yasiyoambukizwa ili kuboresha matokeo ya afya kiujumla katika jamii.

 Dkt. Massawe alisema anatarajia mpango mkakati utazingatia mawazo kati ya wadau muhimu wa THPS na kujenga uamuzi wa pamoja wenye matokeo mazuri. “tunataka kugusa maisha ya Watanzania wengi kwa kuathiri ubora wa huduma za afya na kujenga taifa huru la VVU/UKIMWI. Nina matumaini kuwa mpango mkakati uliofikiriwa utakuwa kama chombo cha usimamizi wa taasisi katika kuweka vipaumbele, kuzingatia nishati na rasilimali, kuimarisha shughuli mbalimbali na kuhakikisha wafanyakazi na wadau wengine wanafanya kazi kwa malengo.

 Akizungumzia juu ya uzinduzi wa mpango mkakati, Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia alielezea malengo ya taasisi kwa miaka ijayo ni kutazamia mbali VVU/ UKIMWI na kushughulika na magonjwa mengine yenye vitisho katika jamii, kulenga katika uhamasishaji wa rasilimali na kuchunguza ushirikiano wa pamoja na sekta binafsi ili kuendelea kutoa huduma zake. “Mpango mkakati huu umekuja wakati muafaka ili kuhakikisha tunafikia idadi kubwa ya watu wenye mahitaji, wakati huo huo tukikuza na kuendeleza taasisi.

 Tunataka kuendelea kuzingatia maeneo muhimu ikiwa ni pamoja na huduma bora za afya, uwezo endelevu wa kifedha, utawala bora na uwajibikaji wa pamoja na wafanyakazi wenye uwezo na kujitolea. Kama taasisi mpya nchini Tanzania tunathamini sana Imani, msaada na fursa ya kutumikia watanzania inayotolewa na serikali kuu, serikali za mtaa, wafadhili, washirika watekejezaji na wadau wengine muhimu kutoka pande zote mbili za jamhuri. Mwisho kabla ya kumaliza tunashukuru kwa msaada endelevu wa kifedha na kiufundi kutoka kwa wafadhili wetu: 

Watu wa Marekani kupitia PEPFAR/ CDC na taasisi ya taifa ya afya Marekani (NHI) , UNAIDS , Chuo kikuu cha Harvard, Chuo kikuu cha Colombia na taasisi ya mfuko wa uwekezaji kwa watoto uliopo Uingereza”. Aidha Dkt. Mbatia alisisitiza kuwa mwelekeo wa mpango mkakati kwa miaka mitano ni kufaidika kwa njia ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja kwa mamilioni ya Watanzania. Mpango huo umesimama kama nguzo ya kuongeza na kubuni ufumbuzi wa afya bora ya kupambana na VVU na UKIMWI, mifumo ya utoaji afya na changamoto nyingine za afya zinazoathiri Watanzania.

Viwanda 42 Zaidi Kuunganishwa Mfumo wa Gesi

$
0
0

Na Said Ameir-MAELEZO

Serikali imesema kuwa viwanda vingine 42 vitaunganishwa na mfumo wa matumizi wa matunizi ya gesi asilia katika kipindi cha miaka miwili ili kuongeza tija tofauti viwanda 37 vya sasa ambavyo tayari vinatumia gesi hiyo.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani aliiambia Kamati ya Fedha ya Bunge jana kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa changamoto zinazokwaza zoezi la kuvipatia viwanda nishati hiyo zinatatuliwa haraka.

“Tuna gesi ya kutosha futi za ujazo trilioni 57.25 ambapo hadi sasa tunatumia wastani wa futi za ujazo milioni 70 ikiwa ni kama asilimia kumi tu hivi” alieleza Waziri Kalemani.Kwa hivyo alisema azma ya Serikali ni kuona viwanda vinatumia gesi katika uzalishaji na kubanisha kuwa Tanzania inaongoza kwa kuwa na nishati hiyo katika Afrika Mashariki. 

Waziri Kalemani aliieleza kamati hiyo kuwa hivi sasa wateja wakubwa wa gesi hiyo ni viwanda lakini Serikali ipo mbioni kutekeleza mkakati wa kusambaza gesi hiyo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Katika maelezo yake kwa kamati hiyo ambayo ilitembelea kituo cha kupokelea gesi asilia huko Kinyerezi na miradi ya uzalishaji umeme kwa kutumia gesi hiyo ya Kinyerezi I na Kinyerezi II, Naibu Waziri huyo alidokeza kuwa Serikali ina mpango wa kuanzisha kiwanda cha kusindika gesi asilia ili iweze kusafirishwa nchi za nje.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Bunge Hawa Ghasia ameitaka TPDC kutayarisha mpango maalum kwa kuainisha na kutenga maeneo maalum ambayo yatawekewa miundombinu ya gesi ili uwekezaji wa viwanda uzingatie ramani hiyo.

“Tungetengeneza kanda maalum tukaziandaa kwa ajili ya viwanda kwa kuziwekea miundombinu ya gesi tofauti na sasa ambapo serikali inalazimika kuvifuata viwanda viliko kuvipelekea nishati hiyo” alishauri Mwenyekiti huyo.Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti huyo alieleza kuwa shirika hilo lina nafasi ya pekee katika kuifanya Tanzania kufikia lengo lake la kuwa nchi ya viwanda kama itatekeleza vyema miradi ya matumizi ya gesi viwandani.

Aliueleza uongozi wa TPDC na waandishi wa habari walioambatana katika ziara hiyo kuwa madhumuni ya ziara ya kamati yake katika miradi hiyo ni kuangalia utayari wa shirika hilo katika kuchangia maendeleo ya uchumi wa viwanda bila ya vikwazo.

Mwenyekiti huyo alieleza kuwa kamati yake imeridhika na kazi inayofanyika hadi sasa na kueleza matumiani ya kamati yake kuwa miradi ya Kinyerezi I na Kinyerezi II itamalizika kwa wakati na kufikia malengo yaliyowekwa. Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC Mhandisi Kapulya Musomba mpango wa shirika lake sasa ni kutekeleza programu yake ya kusambza gesi nchi nzima kwa kuanzia na mikoa ya Arusha, Mbeya, Mwanza na Tanga.

Alisema shirika lake lipo tayari kukipatia kiwanda au mwekezaji nishati hiyo katika sehemu yeyote ambayo bomba la gesi hiyo limepita na kwamba ingependeza kuona Tanzania ina viwanda vingi ili gesi yote iweze kutumika humu nchini pasi na kusafirishwa nchi za nje. Mapema akijibu maswali kutoka kwa wajumbe wa Kamati hiyo, Mhandisi Musomba alisema shirika lake linatumia mifumo miwili ya usalama wa bomba lenye urefu wa kilomita 551 linalosafirisha gesi kutoka Mtwara hadi eneo hilo.

Aliitaja kuwa ni mfumo unaojitegemea wa bomba hilo ambapo zinapotokea hitilafu hujizima na wataalamu hufuatilia kuelewa hitilafu iliopo na mfumo wa pili ni ulinzi shirikishi ambao wanawatumia wananchi kulinda bomba hilo.

Mbali na viwanda 37 kuunganishwa katika mfumo wa matumizi ya gesi, shirika hilo pia limeziunganisha familia 70 katika mfumo wa matumizi ya gesi hiyo katika maeneo ya Mikocheni jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani

NAIBU WAZIRI MPINA AKUTANA NA KAMATI YA ARDHI NA MAWASILIANO YA BARAZA LA WAWAKILISHI KUTOKA ZANZIBAR

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Luhaga Mpina akiongea wakati wa ziara ya Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar, iliyomtembelea Ofisini kwake jijini Dar Es Salaam wa kwanza kulia nia Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh. Hamza Hassan Juma na wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar wakimsilikiza Naibu  Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Luhaga Mpina(hayupo pichani) wakati wa ziara yao Ofisini kwa Waziri huyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Luhaga Mpina akisiliza kwa makini hoja zilizokua zikitolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh. Hamza Hassan Juma(kulia) wakati wa ziara hiyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Luhaga Mpina akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar, iliyomtembelea Ofisini kwake jijini Dar Es Salaam

NAIBU WAZIRI MPINA AKUTANA NA KAMATI YA ARDHI NA MAWASILIANO YA BARAZA LA WAWAKILISHI KUTOKA ZANZIBAR

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Luhaga Mpina akiongea wakati wa ziara ya Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar, iliyomtembelea Ofisini kwake jijini Dar Es Salaam wa kwanza kulia nia Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh. Hamza Hassan Juma na wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar wakimsilikiza Naibu  Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Luhaga Mpina(hayupo pichani) wakati wa ziara yao Ofisini kwa Waziri huyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Luhaga Mpina akisiliza kwa makini hoja zilizokua zikitolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh. Hamza Hassan Juma(kulia) wakati wa ziara hiyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Luhaga Mpina akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar, iliyomtembelea Ofisini kwake jijini Dar Es Salaam

BALOZI, ADADI NA BITEKO WAKUTANA NA WAJUMBE WA CHAMA CHA MABUNGE YA JUMUIYA YA MADOLA TAWI LA CANADA.

$
0
0
 Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Mbunge wa Muheza, Mhe. Balozi Adadi Rajabu (kulia) akizungumza pale ujumbe wa Wabunge kutoka Bunge la Canada ambao ni Wajumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ulipotembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  leo Mjini Dodoma, ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi baina ya Mabunge hayo. Ujumbe huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge, Ndg. Yasmin Ratansi (wa pili kushoto), kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge, Ndg. Kerry Diotte na wa pili kulia, ni Katibu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada Ndg. Remi Bourgault.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge, Mhe. Yasmin Ratansi (wa pili kushoto) akizungumza pale ujumbe wa Wabunge kutoka Bunge la Canada ambao ni Wajumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ulipotembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  leo Mjini Dodoma, ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi baina ya Mabunge hayo, kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Mhe. Dotto Biteko, anaefuta ni Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Mbunge wa Muheza, Mhe. Balozi Adadi Rajabu , kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge, Mhe. Kerry Diotte na katikati ni Katibu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada Ndg. Remi Bourgault.
Ujumbe wa Wabunge kutoka Bungela Canada ambao ni Wajumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada walipotembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Mhe.Yasmin Ratansi (watatu kushoto), Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Mbunge wa Muheza, Mhe. Balozi Adadi Rajabu (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Mhe. Dotto Biteko (wanne kushoto) na Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah (wa tatu kulia). Ujumbe ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi baina ya Mabunge hayo.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Mtandao wa kwanza wa Mawasiliano kutoa huduma ya mtandao wa 4G Pemba

$
0
0

 Wateja wa Zantel sasa wataendelea kufurahia huduma zenye ubora wa hali ya juu kwenye upigaji wa simu na kunufaika na matumizi ya data yenye kasi. Zantel imekuwa kampuni ambayo imepiga hatua kwa kuboresha huduma yake ya mtandao na kuahidi kuendelea kuleta mabadiliko kwenye sekta ya mawasiliano ili kuendelea kubadili maisha ya mamilioni ya watu nchini Tanzania.

Ofisa Mkuu wa Masuala ya Ufundi na Teknolojia Zantel, Larry Arthur alisema, “ Tumeanza kuboresha mtandao wetu tangu Septemba ya mwaka 2016 na tulikuwa na lengo la kukamilisha kazi yetu mwezi Juni mwaka huu, lakini kutokana na mvua kubwa zilizonyesha kipindi cha hivi karibuni, ukamilishaji wa kazi hii umechelewa kufanyika kwa wakati”.

Mchakato wa kuboresha mifumo yetu ya mtandao Zanzibar na Tanzania Bara kwa sasa inakaribia kukamilika na tunafurahi kuwaeleza wateja wetu kwamba tayari tumeshaanza kufurahia matunda ya ubora wa usikivu katika kupiga simu na huduma za data kupitia mtandao wa 4G wa Zantel wenye kasi zaidi.

Kuboresha mfumo wetu wa mtandao kumeimarisha mfumo wa mtandao wa Zantel na kufika maeneo mengi zaidi pia watumiaji wa intaneti wamenufaika na huduma ya haraka ya 4G inayopatikana kwa sasa.

Zantel imekamilisha awamu ya kwanza ya uboreshaji wa mtandao Kisiwani Pemba na Mkoa wa Magharibi Unguja kuweka mfumo wa mtandao wa kisasa. Baada ya kukamilisha awamu hii, inayofuata itakuwa ni kuimarisha miundombinu ya Zantel eneo la Kaskazini na Kusini mwa Unguja.

Awamu ya pili inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu na mara itakapokamilika kwa maeneo yote, Zanzibar na Tanzania Bara zitanufaika na huduma bora za intaneti na ubora kwenye upigaji simu.

Kwa jumla mradi wote unatarajiwa kukamilika kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 10 na tayari zimeanza kutumika katika maeneo yote mjini Zanzibar, huku kukiwa tayari kumefungwa teknolojia ya kisasa pamoja kwenye vituo vilivyopo Zanzibar na Tanzania Bara.

Washirika wetu wameanza utekelezaji kwa haraka ili kuhakikisha kwamba mtandao wa Zantel unaenea katika maeneo mengi nchini. Hii inamaanisha kwamba Zantel itaweza kutoa huduma nzuri ya upigaji simu wenye usikivu mzuri pamoja na data kwa watumiaji wake huku ikiwa ni kampuni inayotoa huduma ya mtandao kwa zaidi ya asilimia 85 kwa jamii ya Watanzania huku ikiwa ni Kampuni inayotoa huduma bora ya intaneti kupitia mtandao wake wenye kasi zaidi wa 4G.

“Wakati tukiendelea kufanyia kazi maeneo yaliyosalia kwa Unguja , tunaendelea kuzingatia ubora wa mifumo yetu kupitia taarifa tunazozipata kutoka kwa wateja wetu kwa njia ya mawasiliano tuliyoweka pamoja na vituo maalumu vya kupokea taarifa ambavyo kwa kiasi kikubwa vimekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha ubora wa mtandao na huduma ya mtandao,” alisema.

Zantel inamkaribisha kila mmoja kujaribu na kufurahia huduma ya mtandao wa 4G kutumia data mahali popote nchini Tanzania, huduma za kifedha kwa njia ya simu, huduma za kibiashara na huduma za kibenki nchi nzima.
Mkuu wa masuala ya Teknolojia na Ufundi Zantel, Larry Arthur (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kisiwani Zanzibar hivi karibuni kuhusu uboreshwaji wa mtandao wa Zantel baada ya Kampuni hiyo kupokea vifaa vipya kutoka Ericsson na Huawei Technologies vitakavyotumika kuboresha mtandao huo. Wengine kutoka kushoto ni William Cheng (Wei) wa Huawei Technologies, Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Khamis Mussa (Baucha) na Mwakilishi wa Kampuni ya Ericsson, Frode Dyrdal.
 

Mashirika ya ndege, TTB wakubaliana

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bibi Devota Mdachi na Meneja Mkazi Shirika la Ndege la Ethiopian Airlines, Bwana Dahlak Teferi wakibadilishana hati za makubaliano ya kufanikisha maonyesho ya utalii ‘Swahili International Tourism Expo,’ jijini Dar es Salaam jana, maonyesho hayo yatakayofanyika Oktoba 13-15 mwaka huu.
Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya utalii Bi Devota Mdachi akizungumza katika hafla ya kutia saini ushirikiano wa kufanikisha maonyesho ya utalii ‘Swahili International Tourism Expo,’ jijini Dar es Salaam jana, maonyesho hayo yatakayofanyika Oktoba 13-15 mwaka huu, (kushoto) Mhandisi Ladislaus Matindi Mkurugenzi mtendaji Air Tanzania wapili( kulia) Bwana Dahlak Teferi Meneja wa Ethiopian Airlines, (kulia) Lima Silva Mwakilishi wa mauzo mwandamizi Shirika la ndege la Ethiopia, Ethiopian Airlines.
Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devotha Mdachi akiwa kwenye picha ya pamoja na Wadau wa Utalii mda mfupi baada ya hafla ya kutia saini ushirikiano wa kufanikisha maonyesho ya utalii ‘Swahili International Tourism Expo’ iliyofanyika Jijini Dar es Salaam jana’ wa tatu (kulia) Mhandisi Ladislaus Matindi Mkurugenzi Mtendaji Air Tanzania wa pili (kushoto) Dahlak Teferi Meneja wa Shirika la Ndege la Ethiopia, Ethiopian Airlines. Ends

TCAA KUNUNUA RADA NNE ZA KISASA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) imeingia makubaliano  ya manunuzi ya rada Nne na kampuni ya Thales ya nchini Ufaransa  zenye thamani ya sh.bilioni 61.3.

Akizungumza leo na waandishi wa habari kabla ya kusaini makubaliano ya manunuzi ya rada hizo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,  Profesa  Makame Mnyaa Mbarawa amesema kuwa kampuni hiyo ifunge kwa viwango vilivyoainishwa katika mkataba na watakaosimamia mradi huo wanatakiwa kuwa na uadilifu kutokana fedha hiyo ni nyingi kutolewa na serikali.

Amesema kuwa kufungwa kwa rada hizo kutasaidia serikali kupata mapato ya sh. bilioni moja, kuongeza idadi ya ndege kutumia anga ya Tanzania pamoja na kuongeza idadi ya wataalii kutokana na anga kuwa salama.

Profesa Mbarawa amesema kuwa TCAA imetumia fedha zake pamoja na serikali kuepukana na mkopo ambapo wameweza kuokoa  sh. bilioni 10 ambazo zingetokana ulipaji mkopo katika taasisi ya fedha.

Amesema kuwa TCAA wameweza kujibana hadi kufikia ununuzi wa rada hizo na kutaka taasisi zilizo chini ya wizara kutumia vyanzo mapato vyao katika miradi mbalimbali kuliko kuangalia kukopa katika taasisi fedha  benki.

Nae, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari  amesema kuwa rada hizo zitafungwa katika viwanja vya ndege vya Dar es Salaam , Kilimanjaro, Songwe -Mbeya  pamoja na Mwanza.

Amesema kuwa TCAA kwa kufungwa rada hizo inakwenda kimataifa kutokana na huduma zinazotolewa na mamlaka hizo kuzingatia viwango vya kimataifa vilivyowekwa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO).

Aidha amesema kuwa rada hizo ni matokeo ya  serikali ya awamu ya tano katika kufikia uchumi wa kati kufikia 2025 unaoendana na pamoja na usafiri wa anga.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi wa TCAA, Profesa Longinus Rutasitara amesema kuwa TCAA imejibana katika vyanzo vyake na kuweza kununua rada hizo.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akizungumza  wakati wa hafla ya utiaji wa saini ya mkataba  wa ufungaji wa mitambo minne  ya Rada ya kuongozea ndege  baina ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na Kampuni ya Thales  Air System  ya nchini Ufaransa. Hafla hiyo pia imeambatana na uzinduzi wa nembo ya mpya ya TCAA  leo jijini Dar es Salaam. Wengine kwenye picha ni Makamu Mwenyekiti Bodi ya TCAA, Prof. Longinus Rutasitara, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari na Meneja Masoko wa Kanda wa Kampuni ya Thales  Air System, Bwana  Abel Curr. 
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa(wapili kushoto aliyesimama), akishuhudia  utiaji wa saini ya mkataba  wa ufungaji wa mitambo minne  ya Rada ya kuongozea ndege  baina ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kupitia Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza S. Johari (Kushoto) na Meneja Masoko wa Kanda wa Kampuni ya Thales Air System ya nchini Ufaransa, Abel Curr .wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa( katikati), akishuhudia Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza S. Johari (Kushoto) na Meneja Masoko wa Kanda wa Kampuni ya Thales Air System Abel Curr wakibadilishana nyaraka baada ya kutia saini ya mkataba wa ununuzi wa rada nne za kuongozea ndege. wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa(katikati)  akikata utepe kuashiria uzinduzi wa nembo mpya ya TCAA  huku akishuhudiwa na makamu  Mwenyekiti Bodi ya TCCA, Prof. Longinus Rutasitara,(kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hamza S. Johari.(kushoto) wakati wa hafla ya utiaji wa saini ya mkataba  wa ufungaji wa mitambo minne  ya Rada ya kuongozea ndege  baina ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na Kampuni ya Thales  Air System  ya nchini Ufaransa leo jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa(kulia)  na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hamza S. Johari. (Kushoto) wakishangilia mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa nembo mpya ya TCAA, wakati wa hafla ya utiaji wa saini ya mkataba  wa ufungaji wa mitambo minne  ya Rada ya kuongozea ndege  baina ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na Kampuni ya Thales  Air System  ya nchini Ufaransa leo jijini Dar es Salaam.

NANI MBABE NGAO YA JAMII KESHO? YANGA KUENDELEZA UBABE AU SIMBA KULIPIZA KISASI?

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KUELEKEA mtanange wa kumaliza ubishi baina ya mahasimu wawili Simb ana Yanga huku kila upande ukijinasibu kufanya vizuri kwenye mchezo huo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa kesho kuanzia majira ya saa 11 jioni Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Ni mechi ya watani wa jadi inayozungumzwa sana midomoni mwa watu, kila mmoja akijinasibu kumfunga mwenzake kwa idadi kubwa ya magoli na na kuinyakua Ngao ya Jamii.

Simba ikiwa imefanya usajili mkubwa sana na wagharama, wakiwajumuisha nyota wanne kutoka Azam Fc John Bocco, Shomari Kapombe, Aishi Manula na Erasto Nyoni pamoja na Kiungo Mnyarwanda kutoka Yanga aliyekipiga kwa misimu kadhaa Haruna Niyonzima.
Mbali na hao, wamemsajili golikipa wa Timu ya Taifa akitokea Mtibwa Sugar Said Dunda na Emanuel Mseja kutoka Mbao Fc, beki wa kulia Shomary Ally, beki wa kati kutoka Toto Africa Yusuf Mlipili, Salim Mbonde kutoka Mtibwa na Mshambuliaji Emanuel Okwi kutoka Sc Villa ya Nchini Uganda. Nicolaus Gyan kutoka Nchini Ghana na beki wa kushoto kutoka Mbao Jamal Mwambeleko 


Kwa upande wa Yanga, wameweza kufanya usajili kwa kuwasajili Ibrahim Ajib kutoka Simba, Raphael Daud kutoka Mbeya City, Pius Buswita kutoka Mbao Fc, Gadiel Michael kutoka Azam, Papii Kabamba Tshishimbi wa Mbabane Swallows na wameweza kuwapanisha vijana wao kutoka timu B Said Musa, Maka Edward ili kuja kuziba nafasi zilizoachwa wazi na wachezaji walioachwa pamoja na wale waliosajiliwa na timu zingine.

Yanga walifanikiwa kuwabakisha wachezaji muhimu kama Donald Ngoma, Thaban Kamosoku na Amisi Tambwe waliokuwa wamemaliza mikataba ya kuitumikia klabu hiyo ya Yanga.

Michuano hii ya Ngao ya Jamii, kwa kawaida huwa ni ‘Super Cup’, kwa maana ya kukutani­sha mabingwa wa michuano miwili to­fauti  bingwa wa FA dhidi ya  mshindi wa pili wa ligi kama bingwa wa ligi na FA.

Safari hii kuna uhalisia zaidi, watu wataona nani mkali kati ya bingwa wa ligi kuu ambaye ni Yanga na bingwa wa  Kombe la FA Simba na kwa mwaka 2017 inakuwa ni mechi ya mara ya 10 toka kuanzishwa mwaka  2001, kusimama na kurudi tena mwaka 2009.

YANGA 

Yanga imewezza kucheza   jumla ya mechi nane ambazo ambapo katika hizo mechi 3 wamecheza  dhidi ya Simba , Mtibwa  ni mara 1 na Azam mara  4 aambapo ndiyo timu ambayo imecheza mechi nyingi zaidi za Ngao ya Jamii tangu ilivyoanzishwa mwa­ka 2001 kati ya timu nne ambazo zime­wahi kucheza mechi hiyo.

SIMBA.

Simba imecheza Ngao ya Jamii  mara nne ikiwa dhidi ya mahasimu wao Yanga mara (3) , Azam mara (1) na kuchukua mara 2  kisha  kupotea na kuwaacha Azam wakicheza mfululizo ndani ya miaka 5 na kulinyakua mara moja msimu wa 2016/17.

YANGA 5, SIM­BA 4

Yanga imefanikiwa kui­funga Simba jumla ya mabao matano katika Ngao ya Jamii pindi ili­pokutana katika miaka tofauti ambapo mwaka 2001, Wa­najangwani hao waliibuka na ush­indi wa mabao 2-1 na mwaka 2010 waliifunga penalti 3-1. Lakini Simba imewafunga wapinzani wao hao jumla ya ma­bao manne yakiwemo mawili kwenye ushindi wa 2-0 mwaka 2011.

WAFUNGAJI SIM­BA, YANGA ZILI­VYOKUTANA

Yanga 2-1 Simba (2001)

Mabao ya Yanga yali­fungwa na Edibily Lunyam­ila na Ally Yusuph ‘Tigana’ la Simba lilifungwa na Steven Ma­punda.

Simba 1-3 Yanga (2010) penalti

Penalti ya Simba ilifungwa na Mohamed Banka huku Emmanuel Okwi na Uhuru Seleman wakikosa penalty, na kwa upande wa Yanga zilipigwa na Godfrey Bonny, Stephano Mwasyika na Isack Boakye.

Simba 2- 0 Yanga (2011)

Wafungaji Haruna Moshi ‘Boban na Felix Sunzu.

AZAM MECHI 5, IME­CHUKUA MA R A MOJA

Azam ndiyo timu yenye historia ya kucheza Ngao ya Jamii mara nyingi zaidi na kushindwa kuchukua kombe hilo . Azam wa­mecheza mara tano kwenye mechi hizo na ku­fanikiwa kushinda mara moja pekee.

Nimefunga mjadala wa Rambirambi-RC Gambo

$
0
0
Hatimaye utata uliokuwa umeenea wa kuwepo kwa ufujaji na matumizi mabaya ya fedha kiasi cha milioni 285.49 zilizokuwa zimechangwa na wadau  pamoja na serikali kwa ajili ya rambi rambi ya vifo vya ajali ya basi la wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent umekwisha baada ya mkuu wa mkoa wa  Arusha Mrisho Gambo kukabidhi milioni 23.27 kwa wazazi wa watoto walionusurika katika ajali hiyo.

Akikabidhi fedha hizo mbele ya waandishi wa habari ambapo kila mzazi amepata Milioni 7.75, Bw. Gambo amesema fedha hizo zilikuwa zimebaki baada ya matumizi ya shughuli za mazishi kwa watoto 32 walimu wawili na dereva waliokuwa wamekufa katika ajali hiyo na matumizi mengine yakiwemo ya wazazi waliokuwa nchini marekani kwa ajili ya kuwauguza watoto wao na kwamba matumizi ya fedha hizo watapanga wao wenyewe.

Katika hatua nyingine Bw Gambo alisema Serikali imekubali kutoa wataam wa saikolojia kwa ajili ya kuendelea kuwasaidia watoto walionusurika katika ajali ya basi la wanafunzi ili kuwaweka sawa na pia kuwaandaa kufanya mtihani wa darasa la saba unaowakabili mnamo mwezi Septemba.

Aidha Bw, Gambo amesema kazi ya kutoa tiba ya kisaikolojia pia ilishafanyika kwa wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent .Wakizungumza baada ya kukabidhiwa Fedha hizo wazazi wa watoto hao wameishukuru serikali na wafadhili kutoka marekani kwa msaada mkubwa kwa watoto wao tangu mwanzo hadi sasa.

Aidha wazazi hao wamesema pamoja na watoto wao kuwa nje ya shule kwa zaidi ya miezi mitatu wako tayari kufanya mtihani na kumaliza ELIMU ya msingi unaotarajiwa kufanyika mwezi September.

Kwa mujibu wa Bw Gambo baada ya kutokea kwa AJALI hiyo MWEZI May 2017 wadau MBALIMBALI na serikali walijitolea na kuchanga fedha na kupatikana zaidi ya milioni 285.49 ambazo nbaada ya matumizi zilibaki milioni 23.27 ambazo zimekabidhiwa leo.

Na kuhusu ombi la wazazi la kutaka watoto wao wafanye mtihani wa kumaliza elimu ya msingi licha ya kuwa nje ya shule kwa miezi zaidi ya mitatu Bw Gambo alisema kama wazazi wako tayari na wanaona watoto wao wana uwezo wa kufanya mtihani hakuna kipingamizi.“Suala hili linawezekana ikiwa wazazi na watoto wataonyesha utayari wa kufanya mtihani huo,na hata mapema leo waziri wa elimu Mhe. Ndalichako ameshalizungumzia” alisema Gambo.

Kuhusu maelezo yalikuwa yameenea katika mitandao ya kijamii kuwa Bw Gambo ametakiwa kukabidhi fedha hizo kwenye mfuko wa kuendeleza watoto hao ulioanzishwa na shirika la Stemm huku wengine wakidai kuwa zipelekwe kuboresha Hosipitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount meru Gambo alisema suala la kuanzisha mfuko na kuboresha hosipitali lina taratibu zake na sio lazima lisubiri fedha za chenji ya rambirambi.

“Kama kuna mfuko wa ELIMU ni jambo jema na unaweza kuanzishwa na kuendelea ila hizo zilizopo wanakabidhiwa wazazi bila masharti yeyote.” alisisitiza Mhe Gambo.

Kuhusu madai kuwa serikali iliahidi kugharamia mazishi na baadaye yakagharamiwa na fedha za wadau Bw Gambo alisema fedha zilizotolewa na taasisi za serikali ni sawa na serikali imetoa na kwamba hayo ni masuala ya kisisasa ambayo asingependa yaingizwe kwenye masuala ya msingi yanayohusiana na maisha ya watu.

“Fedha zilizotolewa na taasisi mbalimbali za serikali mfano NSSF huwezi sema sio za serikali, nadhani ifike mahali tuache siasa nyepesi” alisema Mhe Gambo.

Alliongeza kuwa serikali imeshatenga Bilion 1.9 kwa ajili ya Hosipitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru na kamwe serikali haiwezi kutumia michango hiyo kwa suala kama hilo na kuziita taarifa zilizosambaa mitandaoni kua ni za kizushi zenye nia ya kuichafua serikali.
RC Gambo akiwakabidhi wazazi wa Doreen Mshana jumla ya Shilingi Milioni 7.75 ikiwa ni bakaa ya michango ya rambirambi.
RC Gambo akiwakabidhi wazazi wa Wilson Tarimo jumla ya Shilingi Milioni 7.75 ikiwa ni bakaa ya michango ya rambirambi.
RC Gambo akimkabidhi mzazi wa Shadhia jumla ya Shilingi Milioni 7.75 ikiwa ni bakaa ya michango ya rambirambi
Kushoto ni mtoto Shadhia na Kulia ni mtoto Wilson wakitoka nje ya jengo la ofisi ya Mkuu wa mkoa
Mhe Gambo akisalimiana na mtoto Doreen Mshana

Mhe Gambo katika picha ya pamoja na manusura wa ajali ya Lucky Vincent walipotembelea ofisi yake mapema hii leo.

ASILIMIA KUBWA YA WANANCHI WAISHIO VIJIJINI HAWANA ELIMU YA KUTOSHA KUHUSU HUDUMA ZA MAWASILIANO -TCRA CCC

$
0
0
 Mjumbe wa Baraza na Mwenyekiti wa kamati ya Elimu na Uhamasishaji Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za Mawasiliano,John Njawa akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar kuhusiana na utafiti walioufanya kwa Watumiaji wa huduma za mawasiliano hivi karibuni wakishirikiana na Chuo cha Mipango cha Dododoma.Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za Mawasiliano,Mary Shao Msuya na kushoto ni Mjumbe wa Baraza na Kamati ya Elimu Uhamisishaji -Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za Mawasiliano (TCRA CCC),Nyanda Shuji
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huo
 Mjumbe wa Baraza na Mwenyekiti wa kamati ya Elimu na Uhamasishaji Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za Mawasiliano ((TCRA CCC)),John Njawa akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa Waandishi aaliyeuliza swali kuhusiana na utafiti huo walioufanya,mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar.Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za Mawasiliano,Mary Shao Msuya.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za Mawasiliano,Mary Shao Msuya pamoja na Mjumbe wa Baraza na Kamati ya Elimu Uhamisishaji -Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za Mawasiliano (TCRA CCC),Nyanda Shuji (kushoto),wakionesha vitabu vyenye utafiti uliofanywa na Baraza hilo kwa Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano,wakishirikiana na chuo cha Mipango cha Dodoma.

 Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za Mawasiliano,Mary Msuya alisema kuwa utafiti huo umefanywa ikiwa ni moja ya mipango ya baraza hilo kwa mwaka 2016/2017.

Katika utafiti huo,Mary alisema kuwa utafiti huo ulifanyika katika wilaya tano,ambazo ni Manispaa ya Dodoma (Mjini),Chamwino (vijijini),Mvomero (vijijini),Temeke Manispaa (mjini),na Kaskazini A Unguja,Zanzibar (vijijini),alisema na kuongeza kuwa watu walioshirikishwa kwenye huduma hizo za mawasiliano ni 697,umri kuanzia miaka 15,huku asilimia 50.5 wakiwa wanafunzi wa elimu ya shule ya msingi.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji na Huduma za Mawasiliano,Mary Shao Msuya akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar kuhusiana na utafiti walioufanya kwa Watumiaji wa huduma za mawasiliano hivi karibuni wakishirikiana na Chuo cha Mipango cha Dododoma.

Tigo yachimba kisima chenye thamani ya 18m/- kijiji cha Usongelani Tabora

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanry akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa kisima cha maji kilichokabidhiwa na kampuni ya Tigo chenye thamani ya Tsh 18m/-kwa kijiji cha Usongelani wilaya ya Urambo mkoani Tabora jana .
Mkuu wa mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanry akipampu maji kuzindua kisima cha maji alichokabidhiwa na kampuni ya Tigo chenye thamani ya 18m/-kwa kijiji cha Usongelani wilaya ya Urambo mkoani Tabora jana . Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya ziwa (mwenye miwani), Alli Maswanya, Diwani wa viti maalum kata ya Usoke, Aneth Msangama na Diwani wa Usoke, Said Kazimilo.

Mkuu wa mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanry akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kata ya Usoke wilayani Urambo, Nusura Swalehe mara baada ya uzinduzi wa kisima cha maji chenye thamani ya tsh 18m/-alichokabidhiwa na kampuni ya Tigo kwa kijiji cha Usongelani wilaya ya Urambo mkoani Tabora jana .
Mkuu wa mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanry akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kata ya Usoke wilayani Urambo, Rehema Maganga mara baada ya uzinduzi wa kisima cha maji chenye thamani ya tsh 18m/-alichokabidhiwa na kampuni ya Tigo kwa kijiji cha Usongelani wilaya ya Urambo mkoani Tabora jana.
-Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanry akicheza mziki na baadhi ya wakazi wa kijiji cha Usongelani wakati wa hafla fupi ya kukabidhi kisima cha maji kilichotolewa msaada na kampuni ya simu za mkononi nchini Tigo .















Ni sehemu ya msaada wa Tigo katika kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama

Tabora, Agosti 22, 2017- Tigo Tanzania imejenga kisima cha maji chenye thamani ya Sh 18m/-katika kijiji cha Usongelani katika wilaya ya Urambo, mkoani Tabora kama sehemu ya ahadi iliyotolewa na kampuni hiyo ya kuunga mkono ya kuunga mkono ustawi wa kijamii katika maeneo inamohudimia pamoja na juhudi za kuunga mkono katika kuhakikisha kuwa wananchi wote nchini wanapata maji safi na salama.

Akizungumza kwenye sherehe ya makabidhiano iliyofanyika katika Kijiji cha Usongelani mkoani Tabora, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Ally Maswanya alielezea matumaini yake kuwa kisima hicho kitachangia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo la uhaba wa maji katika eneo hilo kwa kuipatia jumuia ya eneo hilo kupata maji ya uhakika, safi na salama.

"Tumejitahidi kuboresha maisha ya jamii , sio tu kwa kuhakikisha kuwa wanafurahia huduma nzuri za mawasiliano kutoka katika mtandao wetu, bali pia kupiga hatua zaidi kuhakikisha kuwa afya zao na ustawi wao unaboreka," alisema.

Maswanya alibainisha kwamba msaada huo unafanya vijiji vilivyonufaika kufikia 21, na hivyo kuwafanya watu zaidi ya 187,000 kunufaika na kujituma huko kwa Tigo katika kuwapatia watu maji safi na salama kote nchini.

Mwaka huu, Tigo inakusudia kuchimba visima katika maeneo yaliyo na uhitaji mkubwa ambapo inatarajiwa kuwa zaidi ya watu 350,000 watafaidika na mchango wetu wa kuisaidia juhudi za za kupunguza uhaba wa maji safi na salama uliopo nchini.

Makabidhiano hayo yalishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mheshimiwa Aggrey Mwanri ambaye wakati akiwashukuru Tigo kwa msaada unaohitajika sana alisema kuwa kisima hicho kitasaidia kwa kiwango kikubwa kuimarisha afya na ustawi wa jamii kwa kusaidia kukua kiuchumi na kijamii. Aliwataka watu wengine wenye mapenzi mema kujitokeza kuunga mkono jitihada za kuondokana na tatizo la uhaba wa maji katika mkoa huo.

Tunapenda kuwashukuru Tigo kwa kutusaidia katika jitihada zetu za kuwapatia maji ya uhakika katika eneo hili kwa kutatua uhaba wa maji uliokuwepo. Tunaamini kuwa upatikanaji wa maji safi na salama karibu na makazi kutaongeza pia uzalishaji wa kiuchumi hasa kwa wasichana na wanawake ambao hawatakuwa wakitumia tena muda mwingi kutafuta maji safi mahali pengine. 
 
Hii itawapa wasichana fursa ya kuhudhuria kwa uhuru shuleni na kuwapunguzia mzigo wa kijamii hasa wanawake, hivyo kupata nafasi ya kushughulikia kwa ufanisi majukumu yao ya kila siku kwa maendeleo ya taifa, " alisema Mkuu wa Mkoa.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMATANO LEO AGOSTI 23,2017

Viewing all 46371 articles
Browse latest View live




Latest Images