Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1343 | 1344 | (Page 1345) | 1346 | 1347 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nnje wa CUBA Bibi Ana Teresa mara baada ya kuwasili jana August 17/2017 katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Havana kwa ajili ya ziara ya kikazi Nchini Cuba .
  Waziri Mkuu Kassim Majliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakipata makaribisho Nchini Cuba jana August 17/2017 kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nnje wa CUBA Bibi Ana Teresa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Havana kwa ziara ya kikazi Nchini Cuba .Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli inayatambua na kuyathamini mahusiano mazuri ya kidiplomasia yaliyojengwa na awamu zilizotangulia baina ya Tanzania na mataifa mbalimbali ikiwemo Jamuhuri ya Cuba na kwamba itayaendelea.

  Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Agosti 17, 2017), alipozungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Bi Anna Teressa mara baada ya kuwasili nchini Cuba kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la kudumisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

  “Tanzania na Cuba zina historia ya kutosha. Tunatambua mahusiano mazuri yaliyopo kati nchi zote mbili, ambayo yalikuwepo kuanzia Serikali ya Awamu ya kwanza chini ya uongozi wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere.”

  Amesema katika ziara yake hiyo anatarajia kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali ya Cuba kwa lengo la kukuza ushirikiano katika sekta za Afya, Elimu, Utalii na Kilimo.

  Waziri Mkuu amesema Cuba ni mojawapo kati ya nchi zenye ushirikano wa muda mrefu na Tanzania kisiasa, kijamii, kiafya na kiuchumi.”Mfano katika Sekta ya Afya, madaktari wengi kutoka Cuba walikuwa wanakuja Tanzania kutibu wagonja waliokuwa na maradhi makubwa.”

  Pia Waziri Mkuu amesema katika ziara hiyo anatarajia kukutana na Jumuya ya Wafanyabiashara wa Cuba ili kuwaelezea fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania hususan katika Sekta ya Viwanda pamoja na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

  Kwa upande wake Bi. Anna ambaye alimpokea Waziri Mkuu kwa niaba ya Serikali ya Cuba alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea ushirikiano mzuri baina ya nchi hizo mbili, hivyo alimuhakikishia kwamba wataendelea kuudumisha.

  Pia Bi. Anna ametumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa namna inavyopambana na rushwa, ufisadi, kuhimiza uwajibikaji pamoja na kutetea wanyonge.  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  IJUMAA, AGOSTI 18, 201

  0 0  Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akiwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto) na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Temesa, Mhandisi Sylvester Simfukwe (kulia), wakati Mwenyekiti huyo alipokuwa anatoka kuiangalia Karakana ya Utengenezaji wa Magari iliyopo katika ofisi za Temesa, Keko, jijini Dar es Salaam. Masauni alisema lengo kubwa la ziara yake, kuangalia jinsi gani Baraza lake linaweza kufanikisha Utekelezaji wa Mapendezo ya Kamati iliyoundwa na Baraza hilo ili kukabiliana ajali za barabarani nchini
  PIX 2.
  Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyekaa), akimsikiliza rubani Edger Mcha (kulia) wa Chuo cha Usafirishaji nchini (NIT) kilichopo jijini Dar es Salaam, wakati alipokua anamuonyesha jinsi ya kuongoza ndege inapotaka kuruka na kutua kutoka katika kiwanja cha ndege. Mwenyekiti huyo alipata maelezo hayo wakati alipokua katika darasa la kufundishia marubani chuoni hapo. Masauni alifanya ziara katika chuo hicho na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kwa lengo la kuangalia jinsi gani Baraza lake linaweza kufanikisha Utekelezaji wa Mapendezo ya Kamati iliyoundwa na Baraza hilo ili kukabiliana ajali za barabarani nchini. Akiwa chuoni hapo aliangalia ukaguzi wa magari na pia kupata mipango mbalimbali waliyonayo kuhusiana na elimu wanayoitoa ya kuhusiana na usalama barabarani. Aliyevaa koti ni Mkuu wa Chuo hicho, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza hilo, Profesa Zakaria Mganilwa
  PIX 3
  Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiangalia mashine ya kukagua magari kwa njia ya umeme iliyokua inaonyeshwa na Mhandisi Yakubu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA. Katikati ni Meneja wa Karakana ya kutengeneza magari na mitambo mbalimbali ya Serikali, Julius Humbe. Masauni alifanya ziara katika ofisi hiyo iliyopo Keko, jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuangalia jinsi gani Baraza lake linaweza kufanikisha Utekelezaji wa Mapendezo ya Kamati iliyoundwa na Baraza hilo ili kukabiliana ajali za barabarani nchini
  PIX 4.
  Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiiongoza ndege katika darasa la kufundishia marubani katika Chuo cha Usafirishaji nchini (NIT) kilichopo jijini Dar es Salaam. Masauni alifanya ziara chuoni hapo kwa lengo la kuangalia jinsi gani Baraza lake linaweza kufanikisha Utekelezaji wa Mapendezo ya Kamati iliyoundwa na Baraza hilo ili kukabiliana ajali za barabarani nchini. Akiwa chuoni hapo aliangalia ukaguzi wa magari na pia kupata mipango mbalimbali waliyonayo kuhusiana na elimu wanayoitoa hasa katika upande wa usalama barabarani. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza hilo, Profesa Zakaria Mganilwa.
  PIX 5.
  Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji nchini (NIT), Profesa Zakaria Mganilwa (katikati) alipokua anatoa historia ya chuo hicho pamoja na kozi mbalimbali zinazofundishwa katika chuo hicho, kilichopo Mabibo jijini Dar es Salaam. Masauni alifanya ziara chuoni hapo kwa lengo la kuangalia jinsi gani Baraza lake linaweza kufanikisha Utekelezaji wa Mapendezo ya Kamati iliyoundwa na Baraza hilo ili kukabiliana ajali za barabarani nchini. Kulia ni Naibu Mkuu wa Chuo hicho kwa upande wa Taaluma Utafiti na Ushauri, Dk. Prosper Mgaya.
  PIX 6
  Mkuu wa Idara ya Teknolojia ya Usafirishaji wa Chuo cha Usafirishaji nchini (NIT), kilichopo Mabibo, jijini Dar es Salaam, Amon Mwasandube, akimuonyesha Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), jinsi gari linavyokaguliwa linapokuja katika Kituo cha Ukaguzi wa Magari chuoni hapo. Masauni alifanya ziara chuoni hapo kwa lengo la kuangalia jinsi gani Baraza lake linaweza kufanikisha Utekelezaji wa Mapendezo ya Kamati iliyoundwa na Baraza hilo ili kukabiliana ajali za barabarani nchini. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Zakaria Mganilwa.
  PIX 7
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto), akimpokea Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati Mwenyekiti huyo alipofanya ziara katika ofisi hizo zilizopo Keko Mwanga, jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuangalia jinsi gani Baraza lake linaweza kufanikisha Utekelezaji wa Mapendezo ya Kamati iliyoundwa na Baraza hilo ili kukabiliana ajali za barabarani nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Na Mathias Canal, Kaskazini Pemba

  Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM umelaani vikali ubaguzi uliofanywa na baadhi ya Wanachama wasikuwa CCM kwa kuwazuia wanachama wa CCM kuswali pomoja katika misikiti kwenye baadhi ya maeneo Mbalimbali visiwani Pemba.

  Umoja huo umesema kuwa kuzuia watu kuswali kisa itikadi za dini zao ni dhambi kwa Mwenyezi Mungu kwani kufanya hivyo ni kupiga amri ya Mwenyezi Mungu anayetoa onyo Kali katika Quran kwa wale wanaothubutu kuwazuia waini wengine kuswali.

  Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mpinduzi UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka Wakati akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake Wakati alipotembelea Msikiti wa Masjid Lmuhajiriina uliopo Eneo la Kiungoni Kimango Wilayani Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

  Alisema kuwa Imani ya dini yoyote nchini haibagui wala kuchagua watu kuswali kutokana na Itikadi zao za kisiasa ama kikabila kwani dini Ni ibada ya Imani kwa kila mwananchi.

  Shaka Alisema kuzuia watu kuabudu Ni makosa kwa mujibu wa taratibu za nchi lakini pia ni Dhambi kwa Mwenyezi Mungu kwani hakuna maandiko yanazuia watu kushiriki katika ibada.

  Mnamo Mwaka Mwaka 2016 baada ya kura ya marejeo kikundo Cha watu wachache katika baadhi ya maeneo walianza kuwashawishi Wananchi kususia kuswali na Wanachama wanaotokana na CCM ambapo kwa kiasi kikubwa waliwaunga mkono Jambo lililopelekea waumini was kiislamu watokanao na CCM kuanza kusali majumbani mwao.
  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mpinduzi UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka akizungumzia kadhia ya kuzuiwa kuswali waumini wa dini ya kiislamu ambao ni wanachama cha chama cha mapinduzi ccm. (Picha Na Fahad Siraj)
  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mpinduzi UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka akisikiliza taarifa ya kadhia ya kuzuiwa kuswali waumini wa dini ya kiislamu ambao ni wanachama cha chama cha mapinduzi ccm. (Picha Na Fahad Siraj)
   Wanachama wakimlaki Kaimu katibu mkuu mara baada ya kuwasili kuzungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

  0 0

  Waziri wa Maliasli na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amesema serikali imefanikiwa kukamata jumla ya meno ya tembo 28 katika ghala moja lililopo Mbezi Beach jijini Dar es salaam, yenye uzito wa takribani kilo 376. 

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri Maghembe amesema meno hayo yaliyokamatwa tarehe 13 na 14 mwezi wa nane mwaka huu yanaonekana ni ya tembo waliouawa miaka ya nyuma ikikadiriwa kuuawa miaka ya 2013 au 2014 na wahalifu hao kuyaweka majumbani mwao huku wakiendelea kutafuta masoko.

  Waziri Maghembe amesema tayari hadi hivi sasa watuhumiwa sita wa ujangili wameshakamtwa akiwemo Mohamedi Yahya Mohamed, almaarufu Mpemba, Aboubakar Zuberi Seguni mkazi wa Mbezi Beach ambaye pia ni mwenyekiti wa serikali za mtaa na imamu wa msikiti wa Huda uliopo Mbezi, Juma Saleh Jebo mkazi wa Manzese jijini Dar es salaam, Hamisi Rashid Omary mkazi wa Mbezi, Amir Bakari Shelukindo Mkazi wa Gairo Morogoro na Ahmed Shabani Bakari mkazi wa Mkuranga.

  Wakati akiwataja watuhumiwa hao, Waziri Maghembe alisema vita dhidi ya ujangili ni ngumu kwa vile hata baadhi ya watu wasiotegemewa katika jamii kujihusisha nayo nao wamo, akitolea mfano wa mtuhumiwa, Bakari Zuberi Seguni mkazi wa Mbezi Beach ambaye pia ni mwenyekiti wa serikali za mtaa na imamu wa msikiti wa Huda uliopo Mbezi kuwa yeye ni mfano katika jamii kwa kuwa ni kiongozi wa kiserikali lakini pia ni mtu wa Mungu ambaye ni ngumu kufikiria ni miongoni mwa washirika wa biashara hiyo haramu.

  Aliongeza kuwa, Tanzania kupitia Wizara yake inataka kufuta kabisa biashara ya meno ya tembo kama China walivyofanya licha ya kuwa uuzaji wa meno ya tembo kwa sasa mara baada ya kufuta soko la wazi imekuwa ikiendelea kwa njia ya mtandao.

  Katika hatua nyingine , Waziri Maghemba alipaza sauti kwa mataifa kama vile Vietnam na Thailand kuacha kujihusisha na biashara hiyo na kuiomba jumuiya ya Kimataifa kuingilia ili tembo waendelee kuwepo kwa faida ya kizazi kijacho na badae na dunia kwa ujumla.

  Aidha, Waziri Maghembe amesema Tanzania na Dunia kwa ujumla imepata pigo kubwa baada ya kutokea kwa mauaji ya Mkurugenzi wa Palm Foundation, Wayne Lotter raia wa Afrika Kusini yaliyotokea usiku wa jana Masaki jijini Dar es Salaam kwa kuwa alikuwa mstari wa mbele katika kuisaidia serikali katika vita dhidi ya Ujangili.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Mghembe akizungumza na waandishi wa habari wakati alipokuwa akiwaonesha jumla ya meno ya tembo 28 yakiwa na takribani kilo 376 yaliyokamatwa kwenye ghala katika eneo la Mbezi Beach hivi karibuni. Jumla ya watuhumiwa wa ujangili wapatao 6 tayari wameshakamatwa akiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa na Imam wa msikiti wa Huda wa Mbezi Beach, Aboubakar Zuberi Segumi ( Picha na Lusungu Helela- WMU)
  Baadhi ya meno ya tembo yaliyokamtwa hivi karibuni katika ghala moja lililopo Mbezi Beach jijini Dar es salaam, yenye uzito wa takribani kilo 376.

  0 0

  Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza katika Mkutano wa ndani na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba. (Picha na Fahad Siraji)
  Wanachama na Viongozi wa CCM na Jumuiya zake Wilaya ya Wete wakimsikiliza Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka

  Na Mathias Canal, Kaskazini Pemba

  Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mpinduzi UVCCM umewasihi Vijana kote nchini wanapaswa kutumia Maskani zao kwa hamasa ya shughuli za Maendeleo yao na kukuza uchumi katika Jamii.

  Umoja huo umeonya Vijana kutumia Maskani kwa kupiga sogo za kisiasa pasina kufanya kazi Jambo ambalo linapelekea kwa Wakati wote kuilaumu Serikali ilihali walipaswa kutumia weledi wao kuanzisha vikundi Mbalimbali vya kijamii ambavyo vingewaongezea kipato. 

  Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mpinduzi UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka Wakati alipotembelea na kuwasalimu Vijana wa Maskani ya Subira yavuta kheri iliyopo eneo la Mgogoni Wilayani Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba Ili kubaini changamoto zao na kushirikiana namna ya kutatua.

  Alisema kuwa kuanzisha Maskani Ni jambo zuri Kama Vijana watashauriana namna ya kujikwamua kimaisha kwa kufanya shughuli zao Mbalimbali za kijamii zitakazoshika kipato ikiwa Ni pamoja na Kujiunga na vikundi vya ujasiriamali.

  Pia aliwasihi Vijana hao kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli sambamba na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe Dkt Ali Mohamed Shein kwani wana dhamira ya dhati ya kuwatumikia wanachi kwa weledi Mkubwa.

  Shaka Alisema kuwa Ni vyema kuwasaidia Vijana waliojiunga na vikundi mbalimbali kupata mikopo serikalini lakini busara zaidi Ni kuwasaidia kwa kuwapatia ujuzi katika nyanja Mbalimbali ikiwa Ni pamoja na Kujifunza mbinu Bora za Ufugaji na Kilimo sambamba na namna ya kuwa na nidhamu ya fedha ili kupitia ujasiriamali wawe na mafanikio makubwa.

  Alisema kuwa ili kuwa na Vijana makini katika Jamii UVCCM imeamua kukifufua Chuo Cha Siasa Uongozi, Itikadi na Ujasiriamali kilichopita Kijiji cha Ihemi Mkoani Iringa ambapo Vijana Mbalimbali watapata fursa ya kujifunza mambo muhimu na muhimili katika Jamii.

  MWISHO.

  0 0

  Msafara huo wakiangalia jengo la maabara(halipo pichani) wakati wa ukaguzi wa majengo yaliyopo kituo cha afya Matai Kushoto ni waziri Ummy Mwalimu,katikati ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt.Boniface Kasulu na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Julieth Binyura(Picha zote na Wizara ya Afya) .
  Waziri Ummy Mwalimu akiongea na baadhi ya akina mama waliofika kupata huduma kwenye kituo hicho cha afya
  Mkuu wa Wilaya ya ya Kalambo Julieth Binyuru akisalimiana na akina mama hao waliokuwa wakisubiri kuwajulia hali wagonjwa wao waliolazwa kwenye kituo vha afya cha Matai
  Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akimjulia hali mama aliyejifungua kwenye wodi ya wazazi kituoni hapo


  -Baadhi ya Watumishi wa Kituo cha afya cha Matai wakimsikiliza Waziri huyo wakati aluipofanya ziara kwenye kituo cha afya kwa ajili ya kujione hali ya utoaji huduma za afya Mkoani Rukwa
  Afisa Muuguzi Msaidizi Darous Bakari akisoma taarifa ya kituo cha afya cha Matai Wilayni Kalambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Afya alipokuwa akizungumza na watumishi wa kituo hicho.
  …………………………………………………….


  Na.WAMJW-Kalambo

  Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka watoa huduma za afya katika kituo cha afya cha Matai wilayani Kalambo kutoa huduma bora kwa wanawake wajawazito

  Rai hiyo imetolewa jana na Waziri huyo alipokuwa kwenye ziara ya kikazi wilayani hapo na kutembelea hospitali hiyo pamoja na kuongea na watumishi wa sekta ya afya kujua changamoto zinazowakabili

  Alisema wajawazito wanapaswa kupata huduma bora kila wanapofika kliniki kila mwezi kwa kuangaliwa mfano dalili za kifafa cha mimba ,wigi wa proteini pamoja na viatarishi vingine vinavyoweza kusababisha uzazi pingamizi na hivyo kupelekea vifo kwa mama au mtoto wakatiwa kujifungua

  “Nawapongeza sana kwa kutenga dirisha la wazee ila kusiwepo tu dirisha bali muwape dawa wazee wasio kuwa na uwezo,hivyo kama kuwakatia mfuko wa bima ya jamii (CHF)ni gharama basi wapatieni vitambulisho vya matibabu bure ili wazee wakija kwenye matibabu wasije na barua za watendaji wa vijiji”

  Kwa upande wa madawa Waziri Ummy amewaambia watendaji hao hakuna masharti magumu ya ununuzi wa madawa na vifaa tiba kwa kutumia pesa za CHF“nimeshawaambia MSD ndani ya masaa ishirini na nne umeagiza vitu MSD hana,ndani ya masaa hayo kama hana unaruhusiwa kwenda kununua unapotaka kwenda”hivyo ni vyema wakapitisha wadhaburi watakaokuwa wananunua.

  “Tangu serikali hii iingie madarakani imefanya mabadiliko makubwa katika upatikanaji wa dawa kwa kuongezwa bajeti ya dawa kwa asilimia kubwa,hizi changamoto ndogondogo zipo ila mwisho wa siku wananchi wanahitaji dawa,hivyo kuhakikisha dawa zile muhimu zinapatikana wakati wote.

  Hata hivyo amewataka kuwapa kipaumbele wale wanaotumia bima ya afya,nataka kuona mnaongeza wananchi watakaotumia bima ya afya kwenye matibabu ili kuweza kutatua changamoto za sekta ya afya

  Upande wa Malaria Waziri Ummy vipimo vya haraka vya malaria vya MRTD ni bure pamoja na dawa ya kutibu Malaria’ALU’ ni bure”asije kuwaambia mtu kipimo hicho utoe pesa,sindano kama mtu amezidiwa na maralia kali ni bure”alisisitiza Waziri Ummy

  Akiongelea ugonjwa wa Kifua Kikuu”TB” Waziri huyo alisema ni wakati wa kuwaambiwa watu Tb inatibika kwani katika kila watu mia moja wanaoumwa kifua kikuu na kutumia dawa watu tisini wanapona kabisa na wanaendelea na shughuli zao.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitambulishwa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 37 wa SADC kwenye ukumbi wa OR Tambo mjini Pretoria, Afrika ya Kusini. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.
   Rais wa Zambia Mhe. Edgar Lungu akiwashukuru washiriki wa mkutano huo wakati wa Utambulisho kwenye ufunguzi wa mkutano wa 37 wa SADC kwenye ukumbi wa OR Tambo mjini Pretoria, Afrika ya Kusini.# Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

  Mkutano huo wa 37  wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC Double Troika Summit),unawakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia Dkt John Pombe Magufuli.Katika mkutano huo Tanzania itakabidhi nafasi ya  Uenyekiti kwa Mwenyekiti mpya.

  Double Troika inahusisha nchi wanachama sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji. Katika mkutano huo Mfalme Mswati III wa Swaziland atakuwa ndiye Mwenyekiti. Ajenda kuu katika Mkutano huu ni kupokea na kujadili taarifa kuhusu hali ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama katika Kanda na hasa nchini DR Congo na Lesotho.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Kuelekea Ndanda Day kesho, Timu ya Soka ya Ndanda inatarajia kushuka dimbani kuumana na Kikosi cha Azam katika kuadhimisha siku hiyo kwenye Uwanja wa Chamazi, Jijini Dar es salaam.

  Mchezo huo utakaoanza sa 10 alasiri utatanguliwa na burudani mbalimbali ikiwemo muziki kutoka kwa wasanii wa bongo flava wenye asili ya Mkoani Mtwara.

  Akizungumza kuelekea maadhimisho ya siku hiyo, Afisa habari wa Ndanda Idrisa Bandari amesema kuwa katika siku ya kesho wataanza asubuhi kwa kwenda kutoa huduma za kijamii hospitali ya Temeke wodi ya wazazi na kisha kufuatiwa na burudani kutoka kwa wasanii wa muziki wa bongo Flava. 
  Bandari amesema, wasanii hao Wenye asili ya mkoani Mtwara Jay Mo, Amini, TID, Msaga Sumu na Juma Nature anayetokea Mkoa wa Pwani ambapo watatanguliza shughuli hiyo inayofanyika kwa mara ya nne ambapo mwaka huu itakuwa Mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni mara ya kwanza.

  Kwa upande wa Mshauri Masoko wa Ndanda, Peter Simon amesema kuwa kwa mwaka huu Ndanda Day itafanyika mara mbili kwani wameamua kuifanya na Dar es salaam kwani wanaamini kuna mashabiki wengi sana ndani ya Mkoa huu pia ili kuwapa fursa mashabiki wao kuiona Ndanda mpya iliyo chini ya Kocha Ramadhan Nsanzalwino mwenye asilia ya Burundi.

  Meneja Mkuu wa Masoko wa Mitsun Group ambao ni wadhamini wa Ndanda, Erhad Mlyansi amewaahidi uongozi wa Ndanda kuwapatia bidhaa kutoka kampuni yao ya Sayona kwa ajili ya kuwapelea wagonjwa siku ya kesho.
  Nao Wasanii wamewataka mashabiki wa Ndanda kujitokeza kwa wingi siku ya kesho kwa ajili ya kuishuhudia timu yaon na kwa mwaka huu wanaamini kutokana na udhamini walioupata basi timu yao ya Mkoani Mtwara itafanya vizuri huku wakiahidi kutoa burudani ya kutosha.
  Afisa habari wa Ndanda, Idrisa Bandari akizungumza na wanahabari kuelekea Ndanda Day itakayoadhimishwa kesho katika Uwanja wa Chamazi wakicheza na timu ya Azam Fc ikiwa ni mara ya nne kufanyika kwa Tamasha hilo na likisindikizwa na burudani kutoka kwa wasanii wa Bongo Flava wenye Asili ya Mkoani Mtwara pamoja na kutoa huduma za kijamii katika Wodi ya wazazi Hospital ya Temeke. Kushoto ni mshauri wa Masoko wa Ndanda Peter Simon akifuatiwa na wasanii wa Bongo Flava Jay Mo, Richie One na Amini.
  Meneja Mkuu wa Masoko wa Mitsuni Group,Erhard Mlyansi amewaahidi Ndanda kuwapatia bidhaa zinazopatikana kutoka kampuni ya Sayona kwa ajili ya kuwapelekea wakinamama kwenye Wodi ya wazazi Temeke Hospital siku ya Kesho
  Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Khaleed maarufu kama Top In Dar 'TID' akihamasisha mashabiki wa wana Mtwara kujitokeza kwa wingi siku ya kesho Kuadhimisha Ndanda Day akiwa sambamba na wasanii wenzake Jay Mo, Richie One na Amini.

  0 0

   Meneja mkuu wa Redio ya Efm Ndugu, Denis Busulwa akiwapa vipande wapinzani wake katika mtanange kati ya timu ya E.Fm Redio na timu ya Viongozi wa Serikali katika mchezo ulio chezwa hii leo katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini mbeya ambapo Timu Ya EFm iliongoza kwa kuibugiza Timu ya Viongozi wa Serikali Gori 6-1.

  Efm redio 103.3 imekuja Mbeya rasmi, ambapo kwa wiki  nzima imekua ikitoa mafuta ya LAKE OIL kwa vyombo vya moto wenye  stika ya 103.3 Efm Mbeya.kila pikipiki, bajaji na magari iliwekewa mafuta full tank. ikiwa ni Shamra shamra za ujio wa kituo hicho cha redio kuingia rasmi na kusikika kwa kishindo mkoani mbeya kupitia mawimbi ya 103.3 fM.
   Kutoka kulia ni Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya Mohamed Mpinga akizungumza jambo kwa wachezaji wa Timu ya Efm Redio Pamoja na Timu ya Viongozi wa serikali hawapo pichani kabla ya mchezo kuanza.
  Kutoka kushoto ni  Meneja mkuu wa Redio ya E.fm Ndugu, Denis Busulwa akipokea zawadi ya Tsheti kutoka kwa wadau na wasikilizaji wa 103.3 Efm Redio Mbeya
  Vile vile siku ya Leo kulikua na jogging club asubuhi na wakazi wa Mbeya kwa lengo la kuhamasisha mazoezi kwa wakazi wa mbeya ili kujijenga kimwili na kiafya kama ambavyo Efm Redio imekuwa ikifanya mazoezi hayo kila siku jijini Dar es salaam.
  madereva wa pikipiki wakisubiri zawadi ya mafuta kutoka Efm redio 103.3 , ambapo kwa wiki  nzima imekua ikitoa mafuta ya LAKE OIL kwa vyombo vya moto vilivyoweka stika ya 103.3 Efm Mbeya. Kila pikipiki na bajaj iliopata fursa hiyo iliwekewa mafuta full tank. 
  PICHA NA MR.PENGO - MBEYA.


  0 0

  THE NETHERLANDS – SafariBookings.com has conducted an in-depth analysis of reviews from safari tourists and acclaimed Africa experts to determine the continent’s best country for safaris. And the winner? Tanzania came out on top – the country is the clear winner and has been awarded our best safari country for 2017.
  More than 2,500 reviews were used in this comprehensive research. Contributions came from safari-goers all over the world. And 22 reputable guidebook authors – working for Lonely Planet, Rough Guides, Frommer’s, Bradt and Footprint, who make-up the SafariBookings expert panel – also contributed reviews.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akifungua pazia kufungua  Tawi la CCM Muembe Matarumbeta Jimbo la Jang’ombe Mjini Unguja leo akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Mjini kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,[Picha na Ikulu.] 19/08/2017. 
  DSC_9278
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)alipokuwa akipokea risala ya Tawi la CCM Muembe Matarumbeta Jimbo la Jang’ombe Mjini Unguja leo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdalla Juma Abdalla (Mabodi) baada ya kulifungua rasmi Tawi hilo akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Mjini kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,[Picha na Ikulu.] 19/08/2017. 
  DSC_9407
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)alipokuwa akizungumza na Viongozi mbali mbali na Wananchi wa Chama cha Mapinduzi wakati wa ufunguzi wa Tawi la CCM Muembe Matarumbeta Jimbo la Jang’ombe Mjini Unguja leo  akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Mjini kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,[Picha na Ikulu.] 19/08/2017. 
  DSC_9686
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)alipokuwa akiwasalimia Watoto wa maeneo ya Muembe Matarumbeta Jimbo la Jang’ombe Mjini Unguja leo baada ya kumalizika shamra shamra za ufunguzi wa Tawi la CCM  la Muembe Matarumbeta  akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Mjini kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,[Picha na Ikulu.] 19/08/2017. 
  DSC_9691
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)alipokuwa akiwapungia mkono wanachama wa CCM na Wananchi mbali mbali waliohudhuria katika ufunguzi wa Tawi la CCM la Muembe Matarumbeta Jimbo la Jang’ombe Mjini Unguja leo baada ya kumalizika kwa shamra shamra za ufunguzi wa Tawi la hilo  akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Mjini kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,[Picha na Ikulu.] 19/08/2017.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitambulishwa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 37 wa SADC kwenye ukumbi wa OR Tambo mjini Pretoria, Afrika ya Kusini. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.
  Rais wa Zambia Mhe. Edgar Lungu akiwashukuru washiriki wa mkutano huo wakati wa Utambulisho kwenye ufunguzi wa mkutano wa 37 wa SADC kwenye ukumbi wa OR Tambo mjini Pretoria, Afrika ya Kusini.# Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais. 
  Mkutano huo wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC Double Troika Summit),unawakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia Dkt John Pombe Magufuli.Katika mkutano huo Tanzania itakabidhi nafasi ya Uenyekiti kwa Mwenyekiti mpya.

  Double Troika inahusisha nchi wanachama sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji. Katika mkutano huo Mfalme Mswati III wa Swaziland atakuwa ndiye Mwenyekiti. Ajenda kuu katika Mkutano huu ni kupokea na kujadili taarifa kuhusu hali ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama katika Kanda na hasa nchini DR Congo na Lesotho.
  Mwenyekiti wa SADC aliyemaliza muda wake Mfalme Mswati III akimkabidhi Uenyekiti Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika mjini Pretoria, Afrika ya Kusini ambapo Tanzania iliwakilishwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   
  Viongozi wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika mjini Pretoria, Afrika ya Kusini .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  …………………………………………………………………………..

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 19 Agosti 2017, amehudhuria ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC mjiniPretoria Afrika Kusini akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.

  John Pombe Magufuli.

  Mhe. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa taarifa fupi kuhusu majukumu ya SADC Organ kwa kipindi cha Agosti 2016 – Agosti 2017 kwa niaba ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa SADC Organ anayemaliza muda wake.

  Makamu wa Rais amewasilisha kwa Wakuu wa Nchi na Serikali taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya SADC Organ kwa kipindi cha Agosti 2016 hadi Agosti 2017 kwa niaba ya Mwenyekiti wa SADC Organ anayemaliza muda wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

  Taarifa hiyo inaelezea hali ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama katika Kanda katika kipindi tajwa hususan katika Nchi za DRC, Madagascar na Lesotho.Aidha taarifa hiyo pia imetoa mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto zinazoendelea kuikabili Kanda katika maeneo ya siasa, ulinzi na usalama.

  Taarifa hiyo pia imeelezea hali ya demokrasia na chaguzi zilizofanyika kwa kipindi cha 2016/2017 kwa nchi wanachama.Katika Mkutano huu Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amekabidhi Uenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama kwa Angola, baada ya Tanzania kukamilisha kipindi cha Uongozi wake chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

  Mkutano huu wa SADC uliofunguliwa rasmi leo na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ambaye ni Mwenyeji wa Mkutano wa 37 wa SADC, ulitanguliwa na mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili uliofanyika tarehe18 Agosti, 2017

  Mkutano wa Troika Mbiliumefanyika kwa kuzingatia mapendekezo ya Mkutano wa Mawaziri wa Kamati ya Asasi ya Ushirikiano wa Siasa,Ulinzi na Usalama (SADC MCO) uliofanyika Dar es Salaam tarehe 20 na 21 Julai, 2017 ambapo Mawaziri waliona ipo haja ya kuitisha Double Troika pembezoni mwa Mkutano huu wa 37 ili kujadili pamoja na mambo mengine, hali ya ulinzi na usalama.

  Troika Mbili inahusisha nchi wanachama sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji.Serikali ya Afrika Kusini ambayo ni mwenyeji wa Mkutano huu wa 37 wa SADC na Mwenyekiti imependekeza kuwakaulimbiu ya Mkutano wa 37 iwe ni Kushirikiana na Sekta Binafsi katika kuendeleza Viwanda na Kuongeza Thamani ya Bidhaa.

  Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Uenyekiti wa SADC kutoka kwa Mfalme Mswati III, Rais wa Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma amesisitiza nchi wananchama kutekeleza kwa vitendo Kauli Mbiu ya Mkutano wa 37 wa SADC juu ya kushirikiana na Sekta Binafsi katika kuendeleza Viwanda na Kuongeza Thamani ya Bidhaa kuwa ndio njia pekee ya nchi za Jumuiya hiyo kupiga hatua kimaendeleo.

  Rais Zuma amesisitiza nchi za Afrika kufanyakazi kwa bidii na kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kwa faida ya maendeleo yay a kweli.

  Wakuu wa Nchi na Serikali wamepokea taarifa ya utekelezaji wa Mkakati wa Maendeleo ya Viwanda wa SADC 2015 – 2063 ambao ulipitishwa katika Mkutano wa Dharura uliofanyika tarehe 29 Aprili, 2015 mjini Harare, Zimbawe.

  Mkakati huu unalenga kuzifanya nchi za SADC kuwa na uchumi wa viwanda na kushiriki zaidi katika mnyororo wa thamani kikanda na kimataifa na hivyo kuongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi wake.

  Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC) utahitimishwa hapo kesho Jumapili tarehe 20 Agosti 2017, kwa kutolewa Tamko (Communique) litakaloelezea yaliyojiri katika Kikao cha Wakuu wa Nchi na Serikali.

  Imetolewa na ;
  Ofisi ya Makamu wa Rais
  Pretoria, Afrika Kusini

  9 Agosti, 2017.

  0 0


  ZAWA1
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari – MAELEZO, Bibi. Zamaradi Kawawa akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusiana na taarifa za kuzuiwa kwa ndege ya Serikali aina ya Bombadier ambayo inatengenezwa nchini Canada.  (Picha na: Idara ya Habari – MAELEZO)
  ZAWA2
  Serikali imethibitisha na kuwahakikishia Watanzania kuwa ujio wa ndege mpya ya tatu aina ya Bombardier Q400-Dash 8 upo pale pale licha ya baadhi ya wanasiasa wasio wazalendo kutumia kila njia kukwamisha ujio huo.

  Kauli ya kuthibitisha ujio wa ndege hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Bi. Zamaradi Kawawa wakati akiongea na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.

  Alieleza kuwa kuchelewa kwa ndege hiyo ambayo ilitakiwa kuwasili mwezi Julai mwaka huu kumetokana na majadiliano yanayoendelea ambayo kimsingi yamechangiwa na baadhi ya wanasiasa wasio wazalendo kushiriki kwao moja kwa moja kuweka zuio mpaka pale majadiliano yatakapo kamilika.

  “Kuna baadhi ya Watanzania wenzetu wenye maslahi binafsi wanapiga vita ndege hii kuletwa nchini lakini Serikali inawahakikishia wananchi kuwa ndege itakuja na hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi”, alisisitiza Zamaradi.
  Alieleza kuwa Serikali iliishapata fununu kuwa kuna kuna baadhi ya viongozi wa chama cha siasa wana mpango wa kukwamisha juhudi za ujio wa ndege mpya na kwamba bila hata chembe ya uzalendo, watu hao wamejidhihilisha wenyewe hadharani kwamba wapo nyuma ya pazia la kuhujumu jitihada za Serikali kwa maslahi yao binafsi.

  “Serikali imesikitishwa sana kwa hujuma zinazofanywa waziwazi na kwa ushabiki wa hali ya juu na baadhi ya viongozi wa kisiasa kupingana na mwelekeo mzuri wa Rais wa kuleta maendeleo”, alieleza Zamaradi.

  Aidha alisema kuwa Serikali imeanza kuchukua hatua za diplomasia na za kisheria kwa wote wanaoshabikia na kutengeneza migogoro na hujuma mbalimbali dhidi ya maendeleo ya nchi yetu.

  Kwa mujibu wa Zamaradi, kuna wanasiasa waliokwenda kufungua madai kwamba Serikali ya Tanzania inadaiwa na kwamba ndege hiyo ishikiliwe hawana uhalali wowote wa kufanya hivyo na ni vibaraka waliotumwa na wapiga dili wasioitakia mema Tanzania.

  Katika siku za hivi karibuni kumeibuka baadhi ya wanasiasa Watanzania ambao wamekuwa wakitoa kauli zenye lengo la kuhujumu maendeleo ya nchi ikiwemo kushawishi wafadhili kuinyima misaada Tanzania lakini pamoja na jitihada hizo, washirika wa maendeleo wameendelea kuongeza misaada kwa Tanzania kutokana na kuridhishwa na hatua mbalimbali za Serikali katika kupambana na rushwa na ufisadi na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

  0 0
 • 08/19/17--12:16: TAARIFA KWA UMMA

 • 0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christian Mndeme akizungumza alipokuwa akifungua warsha ya siku mojo ya Klabu ya wafanyabiashara wavBenki ya NMB Mkoa wa Dodoma iliyowajengea uwezo wa kibiashara wafanyabiashara.
  Ofisa Mkuu Kitengo cha Mikopo Benki ya NMB, Tom Borghols akizungumza na wafanyabishara wa jiji la Arusha namna ya benki hiyo ilivyosongeza huduma kwao katika mkutano na wajasiriamali toka Klabu ya Biashara ya NMB jijini humo.
  Wajasiriamali wa jijini Arusha wakimsikiliza Ofisa Mkuu Kitengo cha Mikopo Benki ya NMB, Tom Borghol wakati akizungumza nao namna ya benki hiyo ilivyosongeza huduma kwao katika mkutano uliofanya.
  Wajasiriamali wa jijini Arusha wakimsikiliza Ofisa Mkuu Kitengo cha Mikopo Benki ya NMB, Tom Borghol wakati akizungumza nao namna ya benki hiyo ilivyosongeza huduma kwao katika mkutano uliofanya.

  Wajasiriamali wa jijini Arusha wakimsikiliza Ofisa Mkuu Kitengo cha Mikopo Benki ya NMB, Tom Borghol wakati akizungumza nao namna ya benki hiyo ilivyosongeza huduma kwao katika mkutano uliofanya.

  Warsha ikiendelea.
  Mgeni Rasimi kwenye Washa ya Klabu ya wafanyabiashara wadogowadogo na mawakala wa Benki ya NMB Mkoa wa Kilimanjaro, Sebastian Masanja Katibu tawala msaidizi toka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, akizungumza na washiriki wa warsha hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Kuringe Mjini Moshi.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mikopo wa Benki ya NMB Tanzania Tom Borghols, akizungumza na washiriki wa Warsha ya Klabu ya wafanyabiashara wadowadogo na mawakala wa NMB Mkoa wa Kilimanjaro, warsha hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Kuringe Holl Mjini Moshi.
  Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Straton Chilongola akitoa taarifa ya lengo la Benki ya NMB kuwakutanisha wafanyabiashara Mkoa wa Dodoma kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua warsha hiyo.
  Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Straton Chilongola (kulia) akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christian Mndeme alipowasili katika hafla hiyo.
  Baadhi ya wafanyabishara wa jiji la Arusha wakiwa katika mkutano huo.

  0 0  Na Jumia Travel Tanzania

  Inawezekana usiamini kwamba kuna sehemu zinagharimu zaidi ya shilingi milioni 22 za kitanzania kulala kwa usiku mmoja tu! Amini au usiamini sehemu hizo zipo, tena hapa hapa nchini kwetu Tanzania.
  Jumia Travel ingependa kukujulisha kwamba kupitia shughuli za kitalii, hakuna kinachoshindikana. Linapokuja suala la kujionea mazingira adimu na ya kuvutia au wanyama wa aina mbalimbali, gharama au umbali wa kuyafanikisha hayo huwa siyo masuala ya msingi.
  Thanda, ni sehemu kwa ajili ya mapumziko iliyotengenezwa na mtu binafsi katika eneo la kisiwa cha Shungimbili kilichomo Wilaya ya Kisiwa cha Mafia. Kisiwa hiki kina ukubwa wa takribani hekari 20 ambamo ndani yake imejengwa nyumba moja. Nyumba hiyo ina vyumba vya kulala vitano na vibanda viwili pembezoni mwa ufukwe wa bahari ya Hindi kusini mwa Tanzania ambapo familia ya watu mpaka 10 inaweza kuishi.
  Ili kuweza kuishi kwenye kisiwa hiki, wamiliki hutoza wageni kiasi cha dola za kimarekani 10,000 kwa usiku mmoja ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 22 za kitanzania. Mazingira ya kuvutia, utulivu wa hali ya juu na namna eneo hili lilivyotengenezwa ndivyo vinavyowafanya watalii kulipia gharama hizo lisiwe ni jambo la kushangaza. Ni jambo la kawaida ukiwa mapumzikoni kisiwani humo kuwaona au kuogelea pamoja na viumbe wa baharini kama vile pomboo (dolphin), papa wakubwa (whale sharks) na kobe wa majini.

  Wamiliki wa kisiwa hiki binafsi cha mapumziko, wanandoa Bw. Dan na Bi. Christin Olofsson ambao asili yao ni Sweden walipata wazo la kutengeneza sehemu hii ikiwa ni kwa ajili ya kupumzikia pamoja na watoto wao watatu na wajukuu nane. Kikubwa kilichowasukuma kufanya hivyo ni katika jitihada za kubadili mazingira hususani hali ya hewa ukizingatia nchi za Scandinavia wanapotea hukumbwa na baridi kali kwa vipindi virefu vya majira ya mwaka. Walianza kwa kuwekeza Afrika ya Kusini kutokana na kuvutiwa na wanyama na uoto wa asili kabla ya kuja nchini Tanzania.  
  Miongoni mwa masuala ambayo yalizingatiwa kabla ya uwekezaji katika kisiwa hiki ni pamoja na kulinda vivutio vya kitalii na kuhifadhi viumbe wa baharini katika eneo hilo. Kwa kushirikiana na Mamlaka ya Uhifadhi wa Baharini ya Kisiwa cha Shungimbili, wamiliki wa Kisiwa cha Thanda wanashirikiana kwa ukaribu kuhakikisha jitihada za kulinda na kuendeleza uhifadhi wa vivutio vyake unazingatiwa.
  Mbali na hayo, Kisiwa cha Thanda kinahakikisha kwamba jamii ya wakazi wanaoishi karibu na sehemu hiyo ambapo ni Kisiwa cha Mafia, wanafaidika na uwekezaji huo. Wakazi wake wananufaika kupitia ajira, uchangiaji kwenye shughuli za maendeleo ya elimu pamoja na uhifadhi wa viumbe wa baharini ambalo ndio kipaumbele kubwa.    
  Tanzania inazo fursa nyingi za kitalii ambazo watu kutoka mataifa ya nje wanaziona na kuzitumia ipasavyo. Jumia Travel inaamini kwamba kupitia makala haya utakuwa umejifunza mambo mengi kuhusu Kisiwa cha Thanda ambayo hukuyajua hapo awali. Ni fursa kwako kuendelea kutafuta na kujifunza vivutio vinavyopotikana sehemu nyingine za nchi.  


  0 0


  0 0

  Mgeni rasmi, Katibu Tawala mkoa wa Singida Dkt.Angeline Lutambi, akizungumza kwenye ufunguzi wa michuano ya soka ya "Ikungi Elimu Cup 2017" kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo Dkt.Rehema Nchimbi.

  Michuano hiyo ilizinduliwa jana kwenye uwanja wa shule ya sekondari Ikungi, lengo ikiwa ni kuhamasisha wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa elimu kusaidia kutatua baadhi ya changamoto za elimu wilayani Ikungi ikiwemo ujenzi wa madarasa, maabara, nyumba za waalimu pamoja na vyoo.

  Wazo hilo liliibuwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Miraji Mtaturu ambaye ni mlezi wa mfuko wa elimu Ikungi ulioanzishwa ulioanzishwa kwa ajili ya kusaidia utatuzi wa changamoto za kielimu wilayani humo.


  BMG Habari.
  Michuano ya soka ya “Ikungi Elimu Cup 2017” imezinduliwa kwa kishindo katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida baada ya mamia ya wakazi wa wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi kushuhudia uzinduzi huo.


  Michuano hiyo iliyoandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi na kuendeshwa na Chama cha Soka wilayani Ikungi, ilizinduliwa jana Agosti 19,2017 katika uwanja wa shule ya sekondari Ikungi huku ikitarajiwa kushirikisha timu 69 wilayani humo.


  Mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala mkoa wa Singida Dkt.Angeline Lutambi, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida ambaye alipongeza wazo la kuanzishwa kwa michuano hiyo inayolenga kuhamasisha wananchi pamoja wadau mbalimbali ndani na nje ya wilaya ya Ikungi ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kutatua changamoto za elimu ikiwemo ujenzi wa madarasa, maabara, vyoo pamoja na nyumba za waalimu.


  Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe.Miraji Mtaturu ambaye ni mlezi wa mfuko wa elimu Ikungi, alisema michuano hiyo itasaidia upatikanaji wa shilingi bilioni tatu kupitia mfuko wa elimu Ikungi katika kipindi cha miaka mitatu kwa ajili ya kusaidia utatuzi wa kero za elimu wilayani huo.


  Uzinduzi wa michuano hiyo, ulikwenda sambamba na uzinduzi wa zoezi la ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara uliokwama tangu mwaka 2009 katika shule ya sekondari Ikungi hii ikiwa ni uzinduzi rasmi wa zoezi kama hilo kwenye kata zote wilayani Ikungi ambapo kila Kata imepewa jukumu la kufyatua matofali elfu kumi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na nyumba za waalimu.


  Katika zoezi hilo, walijitokeza wadau pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo madiwani, wenyeviti wa halmashauri, jeshi la polisi, Tanesco na wanachi ambao walimuunga mkono Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Mhe.Mtaturu aliyekabidhi mifuko 100 ya simenti na wao wakachangia fedha taslimu zaidi ya shilingi 800,000 na ahadi zaidi ya shilingi 1,900,000, ahadi za simenti mifuko 194 na mchanga wa moramu malori matano kutoka kwa mdau wa maendeleo wilayani Ikungi Hussein Sungita.


  Aidha mgeni rasmi aliwakabidhi shilingi laki moja kila mmoja, jumla ya wanafunzi 16 wa kidato cha sita shule ya sekondari Ikungi waliopata daraja la kwanza kwenye mtihani wao ikiwa ni ahadi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu aliyoitoa wakati wa mahafali ya wanafunzi hao huku akiwaahidi walimu shilingi milioni moja kwa kila wanafunzi 10 wenye madaraja ya kwanza.


  Nazo timu 69 zinazoshiriki michuano hiyo ya “Ikungi Elimu Cup 2017” zilipokea vifaa vya michezo ikiwemo jezi na mipira kwa ajili ya michuano hiyo ambapo jana zilipigwa mechi mbili za kirafiki, ya kwanza ikiwa ni kati ya madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Singida dhidi ya madiwani wa halmashauri ya Ikungi ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare tasa.

  Mchezo wa pili ulikuwa kati ya Ikungi United dhidi ya Puma ukimalizika kwa puma kuwashangaza Ikungi waliokuwa wanaongoza kwa bao mbili hadi kipindi cha kwanza, baada ya kusawazisha na kujipatia bao la ushindi katika kipindi cha pili na hivyo matokeo kuwa Puma 3-2 Ikungi.

  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Miraji Mtaturu akizungumza kwenye uzinduzi huo
  Mgeni rasmi akishiriki shughuli ya ufyatuaji tofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari Ikungi ikiwa ni uzinduzi wa shughuli kama hiyo katika Kata zote wilayani Ikungi ambazo zitashiriki kufyatua tofali elfu kumi kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa na nyumba za waalimu.
  Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Mhe. Miraji Mtaturu akishiriki zoezi la ufyatuaji matofali
  Matofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari Ikungi ambayo ujenzi wake ulikwama tangu mwaka 2009
  Mwenyekiti wa wa halmashauri ya Ikungi akishiriki zoezi hilo
  Zoezi la ufyatuaji matofali ukiendelea ambapo viongozi mbalimbali walishiriki
  Katibu wa CCM mkoa wa Singida akishiriki zoezi hilo
  Mkuu wa wilaya ya Ikungi (kulia) akipokea michango ya papo kwa papo kutoka kwa viongozi mbalimbali waliojitokeza kumuunga mkono katika kusaidia utatuzi wa changamoto za elimu wilayani humo kupitia mfuko wa elimu Ikungi
  Mkuu wa wilaya ya Ikungi (wa pili kushoto) Miraji Mtaturu akikabidhi mifuko 100 ya simenti aliyoahidi kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari Ikungi ambapo wadau wengine walimuunga mkono kwa kuchangia mifumo mingine 194 na hivyo jumla ikapatikana mifuko 294
  Msingi wa jengo la maabara katika shule ya sekondari Ikungi ambao ujenzi wake umekwama tangu mwaka 2009 huku mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, Mhe.Tundu Lissu akilalamikiwa kukwamisha ujenzi huo baada ya kuwazuia wananchi kutoshiriki kwenye michango mbalimbali ya maendeleo
  Mgeni rasmi akiwakabidhi wanafunzi 16 wa kidato cha sita waliopata daraja la kwanza katika shule ya sekondari Ikungi shilingi laki moja, ikiwa ni ahadi ya mkuu wa wilaya ya Ikungi aliyoitoa kwa kila mwanafunzi atakayepata daraja hilo. Wanafunzi 16 walipata daraja la kwanza kwenye mtihani wao wa kidato cha sita. Pia waalimu waliahidiwa shilingi milioni moja kwa kila wanafunzi 10 wenye daraja la kwanza.
  Mwanafunzi wa kidato cha sita shule ya sekondari Ikungi akipokea shilingi laki moja baada ya kupata daraja la kwanza kwenye mtihani wake
  Timu zote 69 zinazoshiriki michuano ya Ikungi Elimu Cup zilipatiwa vifaa vya michezo ikiwemo jezi na mipira miwili
  Timu shiriki za Ikungi Elimu Cup zikipatiwa jezi na mipira kwa ajili ya ligi
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi (kulia) na mwenyekiti wa halmashauri ya Ikungi (kushoto) wakiingia uwanjani kwenye mchezo wa kirafiki na timu ya Manispaa ya Singida
  Mkuu wa wilaya ya Ikungi akipiga penati kama ishara ya ufunguzi wa michuano ya Ikungi Elimu Cup 2017
  Go Goo Goooooooo!
  Mgeni rasmi akiwa na kikosi cha timu ya madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Singida kilichocheza na timu ya madiwani wa Halmashauri ya Ikungi kikiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Ikungi na matokeo yakawa ni suluhu ya bila kufungana
  Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na kikosi cha madiwani wa halmashauri ya Ikungi kilichocheza na kikosi cha madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Singida na matokeo yalikuwa ni suluhu ya bila kufungana
  Baadaye kuliwa na mchezo kati ya timu zinazoshiriki ligi ya Ikungi Elimu Cup ambapo Ikungi United walicheza na Puma na Ikungi wakakubali kufungwa bao 3-2.
  Ikungi United na Puma zikisalimia kabla ya kuanza kuchuana kwenye mchezo wa kirafiki kuelekea kwenye ligi ya Ikungi Elimu Cup 2017. Matoke yalikuwa ni Puma 3-2 Ikungi
  Katibu wa CCM ikungi akifurahia ngoma ya asili iliyotumbuizwa na kikundi cha Nyota Njema
  Kamanda wa polisi mkoani Singida, Debora Magirigimba aliwataka vijana kujikita kwenye michezo na kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya huku pia akiwaonya wanaowapa mimba wanafunzi na kwamba atakaebainika kujihusisha kimapenzi na mwanafunzi atachukuliwa hatua kali za kisheria
  Ikungi Elimu Cup-Changia, Boresha Elimu Ikungi
  BMG Habari

  0 0


  Afisa miradi ya elimu kwa masharika yasiyo ya kiserikali ubalozi wa Sweden nchini, Stephen Chimalo akizungumza jambo wakati wa mafunzo ya ufuatiliaji hatua ya chini ya uandaaji wa bajeti na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha katika sekta ya elimu kwa kutumia mfumo wa PETS kwa wadau kutoka asasi za elimu kwa mikoa ya Tanga, Tabora, Dodoma, Singida, Dar es Salaam na wenyeji Morogoro iliyoandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (Ten/Met).
  Afisa miradi wa Mtandao wa Elimu Tanzania (Ten/Met), Alistidia Kamugisha akizungumza jambo katika mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku tatu hoteli ya Flomi mkoani Morogoro.
  Mtaalamu wa masuala ya IT Mtandao wa elimu Tanzania, Dominic Dogani akifafanua jambo kwa wadau wa mafunzo hayo wakati wa kujadili mada kupitia vikundi.
  Mwanaidi Juma (Katikati) kutoka shirika la Morogoro Saving The Poor Organization (Mosaporg) akiwa na wadau wenzake wa elimu wakati wakiwajibika katika majukumu ya kujifunza mafunzo hayo.

  Mratibu wa shirika la Youth Movement For Change (YMC) la mkoani Singida, Fidelis Yonde kushoto akijadiliana jambo na washiriki wa mafunzo hayo.
  Mkufunzi wa masuala ya elimu, Zelote Loilang'akaki akitoa mafunzo kwa wadau wa asasi za elimu yaliyoandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (Ten/Met) ya namna ya kufuatilia hatua ya chini ya uandaaji wa bajeti na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha katika sekta ya elimu kwa kutumia mfumo wa PETS kwa mikoa ya Tanga, Tabora, Dodoma, Singida, Dar es Salaam na wenyeji Morogoro iliyoandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (Ten/Met).

  Mratibu wa shirika la Youth Movement For Change (YMC) la mkoani Singida, Fidelis Yonde akielezea jambo kuhusu masuala ya changamoto cha elimu ya Tanzania.
  Mkurugenzi Mtendaji Fair Education & Information Centre (Fadice) kutoka mkoa wa Tabora Tabora, Philimon Boyo akifafanua jambo.

  Baadhi ya wadau kutoka asasi za elimu kwa mikoa ya Tanga, Tabora, Dodoma, Singida, Dar es Salaam na wenyeji Morogoro wakifutilia mafunzo ya ufuatiliaji hatua ya chini ya uandaaji wa bajeti na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha katika sekta ya elimu kwa kutumia mfumo wa PETS yaliyoandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (Ten/Met).
  Kiongozi wa shirika la Tabora Advocacy Centre For Development (Tacede), Pai Nyanzandoba akiwalisha mada baada ya washiriki wa mafunzo hayo kujadiliana kwenye vikundi katika siku yao ya tatu ya mafunzo hayo yaliyofanyika mkoani Morogoro.
  Godbless Nkungu kutoka shirika la Youth Life Relief Foundation (YLRF) Tabora naye akiwalisha mada mara baada ya washiriki wa mafunzo hayo kujadiliana kupitia vikundi.
  Naye Mkurugenzi Mtendaji Fair Education & Information Centre (Fadice) akiwasilisha mada kupitia kundi lake wakati wa mafunzo hayo.Afisa miradi ya elimu kwa masharika yasiyo ya kiserikali ubalozi wa Sweden nchini, Stephen Chimalo wa pili kutoka (kulia mstari wa mbele waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka asasi za elimu kwa mikoa ya Tanga, Tabora, Dodoma, Singida, Dar es Salaam na wenyeji Morogoro mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo ya ufuatiliaji hatua ya chini ya uandaaji wa bajeti na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha katika sekta ya elimu kwa kutumia mfumo wa PETS kwa iliyoandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (Ten/Met).

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (wapili kushoto) akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi iliyokopeshwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wilayani humo. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (katikati) na viongozi waandamizi kutoka wilayani na Benki ya Kilimo.
  Makamu Mwenyekiti wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula, Bw. Mohamed Dadi (kushoto) akionesha maendeleo ya Skimu hiyo wakati Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (wapili kulia) pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (katikati) na viongozi waandamizi kutoka wilayani na Benki ya Kilimo walipotembelea Skimu hiyo.
  Kaimu Afisa Tarafa ya Mang’ula, Bw. Omary Said (kulia) akitoa maelezo kuhusu Mradi wa Kilimo Shadidi kinachofanyika katika Kijiji cha Msolwa Ujamaa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (kushoto) na Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (katikati). Wengine wanaosikiliza na viongozi waandamizi kutoka wilayani na Benki ya Kilimo.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa, Bw. Sebastian Sanindege (kushoto) akiongea na ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo ulioambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (kulia). Benki ya Kilimo ilifanya ya ukaguzi wa miradi iliyopatiwa mikopo ili kujionea maendeleo ya miradi wilayani Kilombero.
  Meneja Ufuatiliaji na Tathamini ya Mikopo wa TADB, Bw. Dickson Pangamwawe (wapili kushoto) akionesha maendeleo ya ukuaji wa miwa ya Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa ambao ni wanufaika wa mikopo ya Benki ya Kilimo. Wanaotazama ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (wapili kulia). Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa, Bw. Sebastian Sanindege.
  Maafisa kutoka Benki ya Kilimo na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero wakingalia Mpunga uliyo tayari kuvunwa katika Skimu ya Umwagiliaji ya Kijiji cha Msolwa Ujamaa. 
  Wakulima wa Skimu ya Umwagiliaji ya Kijiji cha Msolwa Ujamaa wakipanda mpunga kwa kutumia njia ya kilimo shadidi.

  ………………………………………………………………

  Katika kuhakikisha miradi inayopatiwa mikopo na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), uongozi wa Benki hiyo kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Bw. James Ihunyo wametembelea miradi minne iliyopo wilayani humo.

  Miradi iliyotembelewa ni Kapolo AMCOS, Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula. Nyingine ni Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa na Hope ya Kidatu.

  Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema ameridhishwa na maendeleo ya miradi hiyo hali inayochochea ari ya Benki katika kutimiza lengo la Serikali la kukopesha wakulima nchini.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo aliwaasa wakulima hao kurudisha mikopo kwa wakati ili wakulima wengine waweze kupatiwa mikopo hiyo.

  “Lengo la mikopo hiyo ni kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania, hivyo kuchelewesha mikopo hiyo kwa makusudi ni kurudisha nyuma juhudi hizi,” Bw. Ihunyo alisema.

  Zaidi ya Shilingi bilioni 2 imekopeshwa kwa wakulima wa mpunga na miwa wilayani Kilombero.

older | 1 | .... | 1343 | 1344 | (Page 1345) | 1346 | 1347 | .... | 1897 | newer