Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1344 | 1345 | (Page 1346) | 1347 | 1348 | .... | 1904 | newer

  0 0

  Waziri wa Afya Ummy Mealimu akiongea na mmoja wa wagonjwa waliofika kupata matibabu kwenye kituo cha afya cha Mazwi kilichopo Manispaa ya Sumbawanga

  Waziri Ummy mwalimu akimuuliza mmoja wa mama aliyefika kupata matibabu ya nje kwenye kituo cha afya cha Mazwi kama amefika muda mrefu na hajapata matibabu,waziri huyo yupo mkoani Rukwa kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kukagua huduma za afya zinazotolewa kwenye vituo vya huduma nchini
  Waziri Ummy Mwalimu akiongea na mama mjamzito aliyelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Rukwa.Waziri Ummy alisisitiza watoa huduma kuhakikisha awatoa huduma wa afya wanajitahidi kuepusha vifo vianavyoweka kuepukika kutokana na uzazi

  Waziri wa Afya akiongea na akina mama wajawazito waliolazwa kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Rukwa
  Waziri akimjulia hali mama mjamzito aliyelezwa kwenye kituo cha afya katika manispaa ya Sumbawanga  Moja ya kipaumbele cha wizara ya afya katika kuokoa vifo vya akina mama wajawazito wakati wa kujifungua ni Damu Salama,Waziri wa Afya akiangalia akikagua bank ya damu salama iliyopo kwenye hospitali ya rufaa ya Mkoa  Baadhi ya watumishi wa sekta ya afya wa manispaa na mkoa wa Rukwa wakimsikiliza waziri wa afya(hayupo pichani) wakati wa kuongea na watumishi hao ambao walitoa changamoto zao zinazowakabili katika utendaji kazi zao za kila siku 
  Mmoja wa watumishi wa kada ya afya akiulizwa swali wakati wa mkutano wa majumuisho ya ziara ya waziri huyo.Waziri wa afya yupo mkoani Rukwa  kikazi ambapo aliweza kutembelea vituo vya afya na hospitali zilizopo wilaya za Nkasi,Kalambo ,Manispaa ya Sumbawanga na hospitali ya Mkoa ya Rukwa(picha zote na Wizara ya afya)

  ………………………………………………………………


  WAMJW- Rukwa 


  Manispaa ya Sumbawanga imeelekezwa kuongeza kujenga vituo vya afya kulingana na jiografia ilivyo ili hospitali ya Rufaa ya mkoa ibaki kutoa huduma za kibingwa mkoani hapa.

  Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea na watumishi wa sekta ya afya wa Mkoa na Wilaya kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wakati wa majumuisho ya ziara ya siku mbili ya kikazi

  Alisema Serikali inaboresha hospitali za Rufaa za Mkoa kwa ajili ya huduma za kibingwa hivyo hospitali hizo ziweze hutoa huduma za kimatibabu ya kibingwa hasa kwa watu wenye huitaji huo,”lakini wananchi wanapaswa kufuata utaratibu wa sera unavyosema kwenda kupata matibabu katika hospitali za Rufaa ni lazima mgonjwa aandikiwe rufaa na sio kila mtu anaenda moja kwa moja kwenye hospitali hizo”

  Waziri Ummy alisema kulingana na kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini ni vyema na mkoa kwa ujumla ni vyema kujenga vituo hivyo vitakavyoweza kutoa huduma kwa wananchi waliopo maeneo husika kuliko kujenga hospitali ya Wilaya ambayo wananchi waliopo maeneo ya mbali wapate huduma za afya huko huko karibu na huduma hizo ziwe bora.

  “Fanyeni maamuzi yenye manufaa kwa wananchi wa wilaya yenu ili muwasogezee huduma watu wenu,alisema kwa Wilaya ya Nkasi wao wanatakiwa kujenga hospitali ya wilaya ya serikali ambapo Wizara yake itasaidia kutoa milioni 350 kati ya 650 ambayo itajenga wodi ya wazazi,maabara pamoja na nyumba moja ya mtumishi

  Aidha,kwa Wilaya ya Kalambo alisema wanatakiwa kuboresha kituo cha afya Bimbwi kwa kujenga chumba cha dharura cha upasuaji ambacho kitasaidia kumtoa mtoto salama.

  Hata hivyo waziri Ummy alizitaka hospitali za DDH na CDH ambazo zinamilikiwa na mashirika ya dini kufanya kazi kwa kuzingatia sera na miongozo ya afya na kufanya kazi kwa pamoja na Serikali kwani hospitali hizo zimeingia ubia na serikali hivyo watoe huduma kama inavyoelekezwa na serikali ikiwemo huduma bure kwa akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano pamoja na wzee wasio na uwezo

  Kwa upande wa watumishi Waziri huyo alikiri Rukwa kuwa na idadi ndogo ya watumishi wa kada ya afya hivyo ameahidi katika kibali kijacho cha ajira atawapa kipaumbele “ila nawataka mtoe mahitaji sahihi ili tuweze kuondoa changamoto hizo, ila kwa sasa mnaweza kuwatawanya baadhi ya watumishi kwenye uhaba zaidi ili muweze kuongeza nguvu kwenye vituo vya kutolea huduma ili kuokoa maisha ya watanzania”


  Waziri wa Afya aliwasihi watumishi wa sekta yake kuacha kufanya kazi kwa mazoea,wanatakiwa kujituma na kuwa waadilifu kwani mambo yamebadilika hivyo kuweka mifumo rahisi nay a kirafiki kwa wananchi ya kutoa malalamiko


  “Wakuu wa Wilaya kama kuna Daktari ama Muuguzi amekosa tuleteeni watumishi hao tuwapeleke kwenye mabaraza ya kitaaluma ,na hivi sasa tumeanza kuwafutia leseni baadhui ya watumishi wa kada ya afya ambao hawatotimiza wajibu wao katika sehemu ya kazi

  0 0  Na Tiganya Vincent-RS –TABORA

  SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imeiagiza Kampuni ya Jossam & co Ltd kuhakikisha inakamilisha barabara ilizopewa za Uledi na Mwenge katika Manispaa ya Tabora hadi kufikia mwishoni mwa Mwezi Septemba mwaka huu.

  Agizo hilo limetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri baada ya kutembelea ujenzi wa barabara hizo zinazojengwa katika Kata ya Uledi na Isevya ili kujionea maendeleo na kuhakikisha kama mjezni amezingatia upana na urefu ullioandikwa katika makubaliano ya mkataba.

  Alisema kuwa kiasi cha shilingi milioni 700 zilizopangwa na Manispaa ya Tabora kutumika kukamilisha mradi huo ni fedha nyingi ni vema Mkandarasi anayejenga mradi huo akahakikisha anajenga katika kiwango bora na kwa upana na urefu uliomo katika mkataba ili thamani ya pesa ionekane.

  Mkuu huyo wa Mkoa aliwaagiza Watendaji wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha wanasimamia kwa karibu ujenzi wa barabara hizo unazingatia matakwa yaliyoelezwa katika Mkataba wa Ujenzi ili barabara hizo ziweze kutumika kwa muda mrefu bila kuharibika.

  Awali Mhandisi Msaidizi kutoka Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Tabora Stephen Warioba alisema kuwa ujenzi wa barabara hizo unahusisha njia za waenda kwa miguu na ipaswa inamalize katika kipindi kilichoelezwa katika Mkataba.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mwl. Queen Mlozi alimwakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa atafuatilia kwa karibu ili kuhakikisha kuwa kazi inayofanyika katika eneo husika inazingatia mambo yote yaliyomo katika Mkataba na sio nje ya hapo.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Bosco Ndunguru alisema kuwa baada ya ujenzi wa Mradi huu kukamilika kutakuwepo na zoezi la upandaji wa miti na maua kando kando ya barabara.

  0 0

  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka akiagana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kumaliza ziara ya siku nne ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Visiwani Pemba.
  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka akiagana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kumaliza ziara ya siku nne ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Visiwani Pemba. 
  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka akiagana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kumaliza ziara ya siku nne ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Visiwani Pemba. 


  Na Mathias Canal, Pemba

  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka amehitimisha ziara ya siku nne ya kikazi Kisiwani Pemba-Zanzibar kwa kuzuru katika Mikoa yote miwili ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba na Wilaya zake zote za Wete, Mkoani, Chakechake na Micheweni.

  Katika ziara hiyo pamoja na mambo mengi alikagua na kushiriki kufanya kazi za kijamii ikiwa ni pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM 2015-2020, kushiriki kuona shughuli mbali mbali za uzalishaji Mali kupitia makundi ya vijana na kuwasaidia kwa kuwaunga mkono ili kuongeza mtaji wa miradi yao.

  Alitumia ziara hiyo kuzungumza na makundi ya vijana kwa nyakati tofauti, viongozi wa CCM, jumuiya za CCM Pamoja na kushiriki shughuli zingine mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kisiasa na kuwaasa kukaa maskani pekee pasina kufanya kazi za uzalishaji mali jambo ambalo litapeleka mbele maendeleo katika jamii.

  Katika maeneo yote aliyozuru Kaimu Katibu Mkuu huyo alitilia zaidi msisitizo kwa vijana kujiunga na vikundi mbalimbali vya kijamii ili kupatiwa mikopo ya vijana inayotolewa na serikali kwa asilimia 5 kila mwezi.


  SALAMU KWA MALIM SEIF 

  Katika hatua nyingine Shaka alimtumia salaamu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF aliyesimamishwa uongozi Maalim Seif Shariff Hamad kwa kumtaka kuacha kueneza chuki kwa wananchi dhidi ya serikali yao kwani kuhubiri siasa za mgawanyiko ni utaratibu wa kiongozi asiyekuwa mweledi kwani maendeleo hayahitaji ubaguzi dhidi ya wananchi.

  "Juhudi za SMZ na SMT katika kuwatumikia wananchi hazitadumazwa kwa maneno ya wapinzani badala yake zitaendeleza mikakati yake ya kutekeleza ilani ya uchaguzi ya ccm ya mwaka" Alisema Shaka

  Alisema ni Siasa uchwara kuhubiri mgawanyiko katika jamii na kutumia nasaba na asili ili kusaka madaraka, kiongozi ambaye atajiegemeza katika siasa chafu milele hawezi kupata ridhaa ya wananchi.

  "Nimeshiriki ujenzi wa shina hili nikiwa na furaha kwenye mtima wangu, Msisahau kumpelekea salamu Maalim Seif Shariff Hamad mwambieni asichoke kueneza siasa za mgawanyiko CCM na serikali zake haizitaacha kabisa kuwapelekea maendeleo wananchi bila kuwabagua" Alisema Shaka 

  Shaka alisema kuwa Kiongozi au mwanasiasa anayekusudia kupata imani na amana ya wananchi hawezi kushiriki kuwagawa watu bali huwa kiranja wa kuwaunganisha na kuwataka wawe wamoja huku wakiishi kwa maelewano na mshikamano.

  Alisema kuwa Wakati dunia, vyama vya siasa makini, wanaharakati na mashirika ya kimataifa yakihubiri uwepo wa amani, maelewano na kukataa mgawanyiko, itashangaza kumsikia mtu anayejiita kiongozi akihubiri siasa chafu za mgaanyiko na mifarakano.

  "Tunamsubiri tena Seif Sharif Hamad mwaka 2020 tumpige mara ya saba, sijui atawania Urais kwa CUF ipi, ile ya Profesa Lipumba haimtaki, yake yeye haitambuliwi na Msajili wala hana Bodi ya Wadhamini, akija tutamgaragaza ili aje kupumzika Mtambwe " Alisema Shaka

  Ziara ya Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka imeacha gumzo kubwa kwa wananchi kufunguka kiakili na kumualika tena kwa mara nyingine kwani tayari wamewelewa namna wanavyopotoshwa na viongozi wa vyama vya upinzani.

  0 0
  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akisalimiana Viongozi mbali mbali wakati alipowasili katika viwanja vya Skuli ya msingi Kihinani Jimbo la Mfenesini kuweka jiwe la msingi Jengo jipya la Skuli hiyo leo akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo
  DSC_9852
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akifungua pazia kama ishara ya   kuweka jiwe la Msingi Jengo jipya la Skuli ya msingi Kihinani leo akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo
  DSC_9886
  Baadhi ya wananchi na Wazee wa Wanafunzi wa Skuli ya msingi Kihinani jimbo la Mfenesini wakiwa katika sherehe za ufunguzi wa Jengo jipya la Skuli hiyo leo iliyowekwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani )akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,
  DSC_9918
  Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Kihinani walipokuwa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani ) alipokuwa akizungumza na Wanafunzi hao pamoja na Wazee wakati wa Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo jipya katika Skuli hiyo leo,akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo
  DSC_9919
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akizungumza na Wananchi,Wazee na Wanafunzi   wakati wa Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo jipya katika Skuli ya msingi Kihinani jimbo la Mfenesini  leo,akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,(kulia) Waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma na (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud
  DSC_9933
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akizungumza na Wananchi,Wazee na Wanafunzi   wakati wa Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo jipya katika Skuli ya msingi Kihinani jimbo la Mfenesini  leo,akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,
  DSC_9964
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipofika kutembelea Ofisi ya Walimu mara baada ya kuweka  Jiwe la Msingi Jengo jipya katika Skuli ya msingi Kihinani jimbo la Mfenesini  leo,akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,(kulia) Waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma na (kushoto) Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo  Bi.Mafunda Juma Khamis,
  DSC_0022
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A” Nd,Mwinyiussi (katikati) wakati alipofika kutembelea Mradi wa Visima vya Maji Safi na salama katika Shehia ya Bumbwisudi leo alipofanya ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,(kulia) Waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira Mhe.Salama Aboud Talib,
  DSC_0036
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipofuatana na Viongozi mbali mbali  wakati alipofika kutembelea Mradi wa Visima vya Maji Safi na salama katika Shehia ya Bumbwisudi leo alipofanya ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,
  DSC_0073
  Waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira Mhe.Salama Aboud Talib alipokuwa akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) wakati alipotembelea Mradi wa Visima vya Maji Safi na salama katika Shehia ya Bumbwisudi leo alipofanya ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo
  Picha na Ikulu.20/08/2017

  0 0

    Mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Arusha Mkaguzi wa Polisi Happyness Temu akitoa elimu juu ya wajibu wa wazazi wa kiume katika malezi ya mtoto katika kikao cha wazazi kilichofanyika jana kwenye shule ya Saint Monica iliyopo jijini Arusha (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
   Mwalimu Mkuu wa shule ya Saint Monica Sister Pauline Etyang Nasike akitoa shukrani zake kwa Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto mara baada ya Mkuu wa kitengo hicho kutoa elimu kwa wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo juu ya malezi ya watoto wao. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
  Wazazi wa wanafunzi wa shule ya Saint Monica waliohudhuria kikao hicho wakionekana wakimsikiliza kwa umakini mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Arusha Mkaguzi wa Polisi Happyness Temu alipokuwa akitoa elimu juu ya umuhimu wa wazazi wa kiume kuwa karibu na watoto wao. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)


  WAKINA BABA WATAKIWA KUTOA TAARIFA ZA MAENDELEO YA WATOTO KWA WENZA WAO


  Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

  Kumekuwa na tabia iliyojengeka kwa baadhi ya jamii zetu kwamba taarifa za maendeleo ya masomo au ukatili na unyanyasaji wa watoto lazima zitoke kwa mzazi wa kike kwenda kwa mzazi wa kiume.

  kufuatia hali hiyo Kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto mkoani hapa kimetoa ushauri kwa wazazi wa kiume kurudi nyumbani mapema pia kuwa na muda wa kuongea au kukaa na watoto wao na kuwa wa kwanza kutoa taarifa za maendeleo ya watoto kwa wake zao badala ya hali hiyo kufanywa na wenza wao pekee kama ilivyo sasa.

  Akizungumza jana Jumamosi katika kikao cha wazazi wa wanafunzi ya Saint Monica iliyopo maeneo ya Moshono jijini hapa, Mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia na watoto mkoa wa Arusha Mkaguzi wa Polisi Happyness Temu alisema kwamba, imekuwa kawaida kwa baadhi ya wazazi wa kiume kutokuwa na muda wa kukaa na watoto kwa kile tunachokiita uwajibikaji katika utafutaji na kushindwa kujua matatizo ya watoto wao.

  Alisema mara nyingi wazazi wengi wa kiume wamekuwa wakijiweka pembeni katika kuwasikiliza watoto wao kwa masuala madogo madogo na kudhani kwamba wenzi wao pekee ndio wanapaswa kujua masuala hayo na kufikiri wao huwa wanatatua shida kubwa kama vile chakula, mavazi na ulipaji wa ada.

  Alisema vitendo vya ukatili na unyanyasaji hasa ubakaji na ulawiti vinavyowakumba watoto vinatokana na wazazi kutokuwa na muda wa kuongea na watoto wao na hivyo kusababisha watoto hao kushindwa kutoa duku duku lao kwa watu wao wa karibu katika wakati sahihi.

  Alisema wakati umefika sasa kwa baadhi ya wazazi wa kiume pamoja na kutimiza mahitaji mbalimbali ya nyumbani lakini wanatakiwa kutenga muda wa kukaa na watoto, kuwadadisi mambo mbalimbali, kuwasikiliza lakini pia kufuatilia nyendo zao badala ya kuwaachia wazazi wa kike pekee.

  Alisema kama wazazi wote watasaidiana katika malezi ya watoto hasa kuwa nao karibu na kuwasikiliza itasaidia kwa kiasi kikubwa kugundua maendeleo yao lakini pia matatizo yao ambayo pengine walishindwa kuyaeleza kwa watu wengine.

  Wakichangia katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na wazazi 580 miongoni mwa wazazi waliohudhuria kikao hicho Bw. Felix Mwetha alisema amevutiwa na elimu hiyo iliyotolewa na kitengo hicho lakini pia aliwataka wazazi wenzake wawe wanafanya maombi ili watoto wao wasikumbwe na vitendo hivyo.

  Huku Bw. Mhando Bamara alisema kutokana na umuhimu wa elimu hiyo alilishauri jeshi la Polisi kuandaa programu maalum ambayo itatengeneza vipindi vya uelimishaji kupitia kitengo hicho ili watu wengi wafahamu badala ya kuishia kwenye vikao pekee.

  Naye Sister Pauline Etyang Nasike ambaye ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, ambayo inamilikiwa na Augustinian Missionary Sisters alilishukuru Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto kwa kutoa elimu kwa wazazi pamoja na walezi lakini pia aliahidi kuandaa kikao kingine kitakachotoa fursa kwa kitengo hicho kutoa elimu kwa wanafunzi.

  Imekuwa kawaida wanafunzi hasa wa shule za msingi kujitokeza kwa wingi na kuelezea matatizo yao mara baada ya Kitengo hicho cha Dawati la Jinsia na Watoto kutembelea shule hizo na kutoa elimu juu ya masuala ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji, hali inayojidhihirisha baadhi ya wazazi hawatoi nafasi ya kuwasikiliza watoto wao mara kwa mara.

  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akisaini kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika kituo cha Television cha Jiji la Tanga (Tanga TV) akiwa na wajumbe wa kamati ya Mfuko wa Jimbo kuangalia fedha za mfuko wa Jimbo zilivyotumika kulia ni Meneja wa kituo hicho,Mussa Labani
   Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kulia akimsikiliza Afisa Mipango na Uchumi wa Jiji la Tanga ambaye pia ni Katibu wa Mfuko wa Jimbo,Ramadhani Possi mara baada ya kusaini kitabu hicho
   Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akiwa na wajumbe wa kamati hiyo wakiorozesha baadhi ya vitu wakati wa ziara hiyo
   Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku katika akimsikiliza Meneja wa kituo hicho,Mussa Labani kushoto
   Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku wa pili kutoka kushoro akipewa maelekezo na Meneja wa Kituo cha Tanga TV Mussa Labani 
   Afisa Mipango na Uchumi wa Jiji la Tanga ambaye pia ni Katibu wa Mfuko wa Jimbo,Ramadhani Possi wa pili kutoka kushoto akimuonyesha jambo  Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku
  Picha ya pamoja baada ya kumaliza ziara hiyo 
  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Mhe.Miraji Mtaturu (wa tatu waliokaa), leo Agosti 20,2017 ameongoza uzinduzi wa albamu ya injili ya mwimbaji Elineeema Babu (wa tatu kushoto) uliofanyika kwenye uwanja wa Stendi Mpya ya Ikungi.

  Katika uzinduzi huo, Mhe.Mtaturu ameendesha zoezi la uuzaji wa albamu hiyo iitwayo TARATIBU NITAFIKA na kusaidia upatikanaji wa zaidi ya shilingi Milioni Tatu ikiwa ni fedha taslimu pamoja na ahadi.

  Mhe.Mtaturu amewahimiza waimbaji wa nyimbo za injili wilayani humo kutumia vyema fursa waliyonayo kwa kuimba nyimbo zenye kuhamasisha amani na upendo nchini, akitolea mfano kwaya ya AIC Makongoro ya Jijini Mwanza iliyoimba wimbo uitwao AMANI kwa ajili ya kuhamasisha amani nchini.

  Mwimbaji Elineema Babu ameachia albabu ya tatu iitwayo "Taratibu Nitafika" yenye nyimbo nane ambapo amewasihi wadau wengine kumsaidia kwa kununua albamu hiyo (Audio) ili aweze kupata shilingi Milioni Sita zinazohitaji ili aweze kurekodi video ya albamu hiyo. Taratibu Nitafika ni albamu ya tatu baada ya kutanguliwa na albamu mbili ambazo ni Nitumie pamoja na Fanya Kazi ya Bwana.
  Mwimbaji Elirehema Babu akitumbuiza kwenye uzinduzi huo hii leo
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Mhe.Miraji Mtaturu akizungumza kwenye uzinduzi huo ambapo alikuwa mgeni rasmi
  DC Ikungi akizindua albamu hiyo
  DC Ikungi akionesha albamu iliyozinduliwa leo
  Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Mhe.Miraji Mtaturu (kushoto), akimkabidhi CD Katibu wa CCM wilayani humo (kulia) kwenye uzinduzi wa albamu ya mwimbaji Elineema Babu
  Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Mhe.Miraji Mtaturu (kushoto), akimkabidhi CD Baba Askofu wa Jimbo la Singida Dkt.Paul Samweli
  BMG Habari

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa. Makame Mbarawa akipanda juu ya Barabara ya Juu (Tazara Flyover) inayoendelea kujengwa katika eneo la Tazara Jijini Dar es Salaam wakati wa Ziara ya Rais wa Shirika la Maendeleo Kimataifa la Japan (JICA Dkt. Shinichi Kitaoka aliyewasili nchini leo.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa. Makame Mbarawa akimuelezea jambo Rais wa Shirika la Maendeleo Kimataifa la Japan (JICA) Dkt. Shinichi Kitaoka (kushoto) alipotembelea kukagua maendeleo ujenzi wa Barabara ya Juu (Tazara Flyover) inayoendelea kujengwa katika eneo la Tazara Jijini Dar es Salaam leo.
  Rais wa Shirika la Maendeleo Kimataifa la Japan (JICA) Dkt. Shinichi Kitaoka akimuelezea jambo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia) alipotembelea kukagua maendeleo ujenzi wa Barabara ya Juu (Tazara Flyover) inayoendelea kujengwa katika eneo la Tazara Jijini Dar es Salaam leo.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa. Makame Mbarawa akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wataalamu wa Kampuni ya Ujenzi ya Sumitomo Mitsui wakati wa ziara ya Rais wa Shirika la Maendeleo Kimataifa la Japan (JICA) Dkt. Shinichi Kitaoka (watatu kushoto) alipotembelea kukagua maendeleo ujenzi wa Barabara ya Juu (Tazara Flyover) inayoendelea kujengwa katika eneo la Tazara Jijini Dar es Salaam leo.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa. Makame Mbarawa akitazama mchoro wa mradi wa ujenzi wa Barabara ya Juu (Tazara Flyover) wakati wa ziara ya Rais wa Shirika la Maendeleo Kimataifa la Japan (JICA) Dkt. Shinichi Kitaoka (kushoto kwake) alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Barabara hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mmoja wa wataalamu wa Kampuni ya Ujenzi ya Sumitomo Mitsui ambayo ndiyo mkandarasi wa mradi huo
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa na Rais wa Shirika la Maendeleo Kimataifa la Japan (JICA) Dkt. Shinichi Kitaoka wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa TANROADS, na wataalamu wa Ujenzi mara baada ya kumaliza ziara ya kukagua maendeleo ujenzi wa Barabara ya Juu (Tazara Flyover) inayoendelea kujengwa katika eneo la Tazara Jijini Dar es Salaam leo.
  Muonekano wa Juu na Pembeni mwa bararaba ya Juu (Tazara Flyover) ambao ujenzi wake umekamiklika kwa asilimia 53 na unatarajiwa kukamilika mapema mwezi wa kumi mwakani.

  Picha na: Idara ya Habari – MAELEZO

  0 0

  Makamau wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka saini moja ya makubaliano katika mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika wakati wa kuhitimishwa kwa mkutano huo mjini Pretoria. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Dkt. Stergomena Tax akila kiapo mara baada ya kuteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa SADC .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
  Makamau wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka saini moja ya makubaliano katika mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika wakati wa kuhitimishwa kwa mkutano huo mjini Pretoria. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) .
  Dkt. Stergomena Tax mara baada ya kuteuliwa na kula kiapo kuwa Katibu Mtendaji wa SADC .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais


  Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC umemalizika leo tarehe 20 Agosti 2017 katika mji wa Pretoria Afrika Kusini ambapo Wakuu wa nchi na Serikali wa SADC kwa kauli moja wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake katika Asasi ya Ushirikiano wa siasa , Ulinzi na Usalama Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi cha uongozi wake akiwa Mwenyekiti wa Asasi hiyo.

  Tanzania imemaliza kipindi chake cha Uenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama tarehe 19 Agosti, 2017 wakati wa Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa SADC ambao umefanyikia hapa Pretoria, Afrika Kusini kuanzia tarehe 19 na 20 Agosti, 2017.

  Akizungumzia mambo muhimu yaliyojadiliwa katika mkutano huo wa 37 wa SADC, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema pamoja na mambo mengine SADC imetambua na kuthamini mchango wa Tanzania katika kipindi cha Uongozi wa Asasi ya Saisa , Ulinzi na Usalama iliyokuwa chini ya Rais Dkt. John Pombe magufuli.

  Amesema Tanzania imeshakuwa Mwenyekiti wa Asasi hiyo mara tatu, kwa nyakati tofauti ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni kipindi cha 2006/2007 na mara ya pili ilikuwa ni 2012/2013 na mara ya tatu katika kipindi cha Agosti 2016 hadi Agosti 2017 chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo alikabidhiwa kijiti cha uongozi huo kutoka kwa Jamhuri ya Msumbiji wakati wa Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika Falme ya Swaziland tarehe 30 Agosti, 2016.

  Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana wakati wa Uenyekiti wa Tanzania katika Asasi hiyo ni kusimamia uchaguzi wa Bungenchini Seychelles ambao ulifanyika mwezi Septemba, 2016.

  Aidha katika kipindi cha Uongozi wa Tanzania ulisaidia kurejesha hali ya amani na utulivu nchini Lesotho ambayo kwa muda mrefu tangu 2014 imekuwa kwenye mgogoro wa kisiasa pamoja na kushughulikia matatizo ya Uchaguzi nchini DR Congo.

  Mkutano wa 37 wa SADC pia umemuongezea muda mwingine Mtanzania Dkt. Stergomena Taxi kuendelea na wadhifa aliokuwa nao wa Katibu Mtendaji wa SADC kwa kipindi cha miaka minne mingine ambapo atatumikia nafasi hiyo hadi mwaka 2021.

  Dkt. Tax amethibitishwa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi uliomaliza leo na kuapishwa rasmi kushika nafasi hiyo.

  Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC) umehitimishwa kwa kutolewa Tamko (Communique) kuelezea yaliyojiri katika Kikao cha Wakuu wa Nchi na Serikali ikiwa ni pamoja na mkutano wa 38 kufanyika nchini Namibia

  Imetolewa na ;
  Ofisi ya Makamu wa Rais
  Pretoria, Afrika Kusini
  20 Agosti, 2017.

  0 0

   
  WANACHAMA wa Coastal Union ya Tanga wameazimia kurudisha umoja kwenye klabu ili kuhakikisha timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza inarejea Ligi Kuu ya Tanzania Bara.


  Akizungumza na mwandishi wetu baada ya kuisha mkutano wa wanachama kutoka Tanga, msemaji wa klabu hiyo maarufu Wagosi wa Kaya, Hafidh Kido alisema kwa mipango iliyokuwepo hakuna sababu ya kuifanya timu hiyo kongwe nchini kushindwa kurejea ligi kuu msimu ujao.

  “Mkutano ulikuwa na ajenda nyingi lakini kubwa ilikuwa ni kuleta umoja na kubainisha mikakati ya kushiriki vema ligi daraja la kwanza msimu huu.
  “Tumefanya usajili wa nguvu, wachezaji wengi waliokuwa wakishiriki ligi kuu msimu uliopita tumewanaka na tayari wamesharipoti kambini,” alisema Hafidh Kido na kuongeza:

  “Hii ni Coastal Union mpya, wapenzi na wanachama wote uliokuwa ukiwajua wamerejea kwa ajili ya kuongeza nguvu. Sasa hivi Coastal Union ni wali ng’ombe hakuna njaa.”

  Kwa upande wake Mwenyekiti Kamati ya Usajili na Mashindano, Hemed Hilal ‘Aurora’ alisema; “Makundi ndiyo yaliyoidhoofisha Coastal Union lakini leo nathibitisha wazi makund yamekufa na Coastal Union ni moja.”
  Alisisitiza kuwa kila mmoja atimize wajibu wake ili msimu huu mambo yanyooke na Coastal Union irudi mahali panapostahili kwa sababu kushiriki ligi daraja la kwanza si hadhi yao.

  Aidha mbali ya mambo mengine uongozi wa klabu hiyo ulitangaza jana kuwa kambi inaanza rasmi Jumatatu (leo) ambapo wachezaji wote waliosajili tayari wamesharipoti kambini.Kwa upande wake mchezaji wa zamani wa Coastal Union, Razak Yusuf 'Careca,' alisema Coastal ya mwaka huu ni moto wa kuotea mbali kinyume na watu wanavyoitazamia.

  "Tayari tumeshapata nyumba ambayo wachezaji wote watakaa, tuna wachezaji wengi walioshiriki ligi kuu msimu uliopita ikiwemo Ndanda na African Lyon."Wapo wachezaji pia kama golikipa wa zamani wa Mtibwa na Simba, Hussein Shariff 'Casilas,' Baraka Jafari aliyekua kapteni African Lyon, mchezaji wa zamani wa Yanga, Athumani Idd 'Chuji,' Rashid Roshwa mfungaji bora wa Ndondo Cup iliyoisha hivi karibuni na mchezaji mkongwe Salvatory Ntebe," alisema Careca.

  Aidha, mazoezi ya wachezaji yatafanyika asubuhi na jioni chini ya usimamizi wa Makocha Juma Mgunda na Joseph Lazaro. Asubihi yatafanyika katika uwanja mkongwe wa Mkwakwani na jioni yatafanyika katika uwanja wa Shule ya Sekondari Galanosi.

  Coastal Union iliyoanzishwa mwaka 1948 ni miongoni mwa timu chache zilizoanzisha Ligi Kuu Tanzania Bara wakati huo ikiitwa Ligi ya Taifa na imejizolea sifa nyingi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati kutokana na soka lililonyooka kaioka miaka ya 1960 hadi 1990.

  0 0

  Mti aina ya msindano ambao umegemwa utomvu katika Shamba la miti la Sao Hill lililoko Mufindi mkoani Iringa ikiwa ni utafiti unaofanywa na Kampuni ya Art International kwa kushirikiana na shamba hilo ikiwa ni njia ya kujiongezea kipato.
  Meneja wa Shamba la miti la Sao Hill, Salehe Baleko akikinga utomvu unaotoka katika mti wa msindano ambao baada ya kugemwa huchakatwa na kuchanganywa na kemikali mbalimbali ambao hutumika kutengenezea dawa mbalimbali ikiwemo bazoka (chewing gum) pamoja na gel. (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)
  Mtaalamu wa Kampuni ya Art International, Zhoung Yhoung akitoa maelezo kuhusu zoezi la ugemaji wa utomvu kwa ujumla unaofanywa na kampuni yake (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)

  ……………………………………………………………………………..

  Shamba la miti la Sao Hill likishirikiana na Kampuni ya Art International limeanza utafiti wa kugema utomvu wa miti ya msindano kama njia ya kujiongezea kipato.

  Akizungumza na Kamati ya Bunge ya Maliasili na Mabadiliko ya tabia ya nchi ya nchini Malawi iliyotembelea Shamba la Miti la Sao Hill, Meneja wa Shamba hilo Salehe Beleko amesema katika kuongeza vyanzo vya mapato wameingia mkataba na kampuni hiyo kufanya utafiti na ikibainika kwamba haitaathiri ukuaji wala ubora wa miti wataidhinisha kuwa chanzo kipya cha mapato.

  Akifafanua Salehe Baleko amesema wanatarajia kuuza kila kilo moja ya utomvu kwas h. 750.

  Beleko amesema kwa kuwa ni utafiti wameanza kwanza na miti iliyokuwa tayari kuvunwa wakiona hakuna madhara wataendelea kwenye miti michache yenye umri mdogo na matokeo ya utafiti huo yatapelekea ama kukuza ama kukataza kabisa zoezi hilo.

  Naye mtaalamu wa kampuni ya uchina, Yhoung Zhoung amesema taasisi yake imefuata taratibu zote za ugemaji na usafirishaji wa utomvu huo na amefafanua kwamba kampuni yake inahitaji miti millioni mbili kwa mwaka ilikupata ujazo wa utomvu wanauhitaji

  Akijibu swali la mke wa Rais wa zamani wa Malawi, Patricia Muluzi ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo ambaye alitaka kujua matumizi ya utomvu huo mtaalamu huyo amesema baada ya kuchakatwa na kuchanganywa na kemikali mbalimbali utomvu huo hutumika kutengenezea dawa mbalimbali bazoka (chewing gum) pamoja na gel

  Mjumbe wa Kmaati hiyo, Rashid Pemba Msusa, amesema kwa mara ya kwanza wameshuhudia matumizi mapya kabisa ya zao la mti teknolojia ambayo hawajawahi kuiona nchini kwao Malawi. Hata hivyo ameahidi kufuatilia matokeo ya utafiti huo ili ukifaa wauhamishie Malawi

  0 0

  NOA1
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikabidhi msaada wa Gari aina ya Noah, Pikipiki Tatu, Computer Tano na Camera Mbili za kisasa kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania  TBC  Bi. MARTHA SWAI .
  NOA2
  Hizi ni Pikipiki tatu zilizokabidhiwa kwa TBC ikiwa ni miongozi mwa vifaa vilivyotolewa na Mkuu wa Mkoa huyo kwa Shirika hilo.

  ………………………………………………………………………………
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo ametoa msaada wa Gari aina ya Noah, Pikipiki Tatu, Computer Tano na Camera Mbili za kisasa kwa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC ili kuongeza nguvu katika kuwafikia Wananchi.

  Mbali na Vifaa hivyo vya kisasa pia Makonda amefanikiwa kumpata mfadhili atakaepaka Rangi Jengo lote la TBC kuanzia siku ya kesho ili liwe na mwonekano wa kisasa.

  Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo MAKONDA amesema lengo ni kuwawezesha Wananchi ambao hawana uwezo wa kuita vyombo vya habari na kueleza matatizo yao waweze kufikiwa.

  Makonda ametoa msaada huo baada ya kufika Ofisi za TBC na kubaini uwepo wa changamoto za vifaa ikiwemo Usafiri, Camera na Computer ambapo kwa sasa Gari na Pikipiki hizo zitawawezesha Waandishi kufika kwenye matukio kwa uharaka huku*Compute* zikimuwezesha  Mhariri kutekeleza majukumu yake.

  Vifaa hivyo vitatumika kuongeza nguvu kwenye kipindi cha Hadubini ambacho kimekuwa kikisaidia Wananchi wanyonge kupaza sauti zao.
  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TBC  Bi. MARTHA SWAI amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwapatia msaada huo kuku Zaitun Mkwama ambae ni mtayarishaji wa kipindi cha Hadubini akieleza kuwa vifaa hivyo vitawaongezea ufanisi katika kazi yao.

  0 0

  By our Correspondent

  THE Independent Power Tanzania Limited (IPTL) and Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP) have moved the High Court (Commercial Division) to order Standard Chartered Bank Hong Kong Limited and Standard Chartered Bank Malaysia Berhard to pay about 50bn/-as security for costs.

  In an application lodged before the Dar es Salaam Court recently, the two local companies are seeking such orders for payments of 22,880,006 US dollars, pending determination of proceedings challenging enforcement a foreign judgment for payments of about 400bn/- in favour of the two banks.

  Judge Barke Sahel will hear the application that has been filed under certificate of urgency on October 10th this year. The application has been supported by seasoned Advocate Joseph Makandege, who is also the Company Secretary and Chief Counsel of IPTL and PAP.

  In the affidavit to support the application, Mr. Makandege, currently the Acting Executive Chairman and Managing Director of IPTL and PAP, states that the two banks, who are respondents, are corporate citizens of and domiciled in Hong Kong in the Peoples’ Republic of China and Malaysia, respectively.

  “None of them is registered in the country or own any property, let alone an immovable property, or asset or has a known registered establishment in Tanzania, within the local limits of the jurisdiction of this court,” reads part of the affidavit.

  He stated that as of to date none of principal officers of the respondent banks has signed or verified any document or pleading, be it in proceedings for enforcement of the impugned judgment or counter affidavits filed in opposition to the applicants proceedings to set aside registration of such judgment.

  As a result, the advocate sates, such principal officers could hardly be bound by the pleadings filed, or take charge of the consequences arising there from and critically reflected, the respondents are apparently conducting themselves with a view to eventually evade the consequences.

  Mr. Makandege states that the counsel for the respondents who drew and filed the proceedings for enforcement of the impugned judgment has not exhibited to the court or to the applicants any document instructing and authorizing him to institute and act as such for and on their behalf.

   “The countries wherein the respondents are reportedly incorporated and domiciled do not have any reciprocal arrangements with Tanzania for enforcement of decisions of their respective courts, which may guarantee recoverability of the applicants’ costs of litigating the proceedings,” he states.

   According to him, the monetary value of the claim the respondents seek to recover from the applicants being over 168,800,063.87 US dollars (about 376,424,142,274/-) is colossal, hence costly to litigate and the applicants have not obtained any legal aid or anyhow been exempted from payments of legal fees.

  It is stated in the affidavit further that the respondents are habitual forum shoppers who may at any time abandon their proceedings for enforcement of the impugned judgment and the applicants’ proceedings for setting aside registration of the judgment or any appeal that may emanate there from.

  Mr. Makandege states that given the matters deposed to in his affidavit cumulatively, the respondents’ impugned foreign judgment sought to be enforced was vitiated by a number of legal and factual considerations, hence more susceptible and vulnerable to being assailed.

  “The security sought by the applicants for their costs for litigating the proceedings for setting aside registration of the judgment or an appeal that may emanate there from are statutory and applicable in almost all commonwealth jurisdictions, hence not an impediment to access to justice,” he states.

  Even the applicants and VIP Engineering and Marketing Limited, being not British corporate citizens and not domiciled in Britain, were in 2016 ordered by the English Court at the instance of the respondents to deposit security for their costs of litigating the English proceedings.

  In their main applications, IPTL, PAP and VIP are requesting the High Court to set aside the Ex-Parte Order given by Judge Sehel on February 9, 2017, registering the foreign judgment given in favour of the two foreign Banks.

  Justice Flux of the High Court of Justice of England, Queen’s Bench Division, Commercial Court, had given such judgment after VIP, PAP and IPTL defaulted to submit to the jurisdiction of the London-based English Court.

  IPTL, PAP and VIP charge that Judge Sahel surprisingly issued the order registering such judgment in question without summoning them while they are all based within the vicinity of the High Court in Dar es Salaam, which they view as being at odds with the law and practice of the land. 

  The Judgment is highly contested on a number of grounds and fronts. The three companies, the applicants in the matter, canvases for a declaration that the foreign judgment registered following ex-parte order given by Judge Sahel, is unregistrable and unenforceable in Tanzania.

  0 0


  Siku ya jana Chama Cha Alliance for Democratic Change (ADC) chenye kaulimbiu ya Dira ya Mabadiliko kimetimiza miaka mitano tangu kupata usajili rasmi 22 Agosti 2012.
  Akizungumza katika maadhimisho ya Chama hicho Mwenyekiti wa chama hicho Hamad Rashid ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, ametoa wito kwa vyama vya siasa kuiga mfano wa ADC ambao wamekuwa wakimaliza migogoro yao kwa njia ya mazungumzo kwa kipindi hicho cha miaka mitano tofauti na vifanyavyo vyama vingine.

  Mwenyekiti Hamad Rashid ameuzungumzia mgogoro unaoendelea ndani ya Chama cha CUF na kueleza kuwa hatua waliyofikia ya kupelekana mahakami siyo sahihi kwani itazidi kuchochea mgogoro huo.
  "Mahakama kazi yake ni kuhukumu mmoja lazima akose na mwingine lazima apate kutokana na hukumu, ni vyema viongozi wawili wanaoonekana kutajwa katika mgogoro huo Profesa Lipumba na Maalim Seif kukaa katika meza moja ya majadiliano na kuutatua mgogoro huo" Alisema Hamad Rashid.

  Hamad Rashid amefafanua kuwa ADC ilikuwa na mgogoro na aliyekuwa mwenyekiti wa kwanza wa Chama hicho Said Miraji na wenzake wanne lakini wameumaliza mgogoro wao kwa majadiliano bila kufikishana mahakamani, hivyo ni vyema CUF wakaiga mfano huo na kuziondoa tofauti zao.

  Naye Katibu Mkuu wa Chama hicho Doyo Hassan Doyo ameeleza kuwa zuio la kufanya mikutano ya kisiasa limekwamisha utendaji kazi wa ADC kama chama kinachohitaji kujitangaza kwa wananchi.

  Vilevile Katibu Mkuu Doyo amesisitiza kuwa Chama chao kitaendelea kupinga vikali kuwatumia vijana katika kufanya vurugu na maandamano yasiyo na tija, ndoa za jinsia moja, na adhabu ya kifo.

  0 0


  0 0

  Na Tiganya Vincent-RS –TABORA

  SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imeiagiza Maafiza kuhakikisha wafanya ukaguzi katika Vyama vya Ushirika Vya Kuweka na Kukopa (SACCOS) ili kuridhisha kama fedha walizoweka wanachama zipo au hazipo iweze kuwachukulia hatua kali.

  Agizo hilo limetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri katika nyakati tofauti alipokuwa akiongea na wajumbe Jukwaa la Ushirika na wakati wa Sherehe ya kuwaaga walimu walistaafu kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma.

  Alisema kuwa amelazimika kuchukua hatua hiyo baada ya kupata malalamiko kutoka kwa watumishi wakiwemo walimu kuwa wamekuwa wakiweka fedha katika SACCOS kama sehemu ya kujiwekea akiba lakini wanapohitaji kukopa wanaambiwa fedha hazipo.

  Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora alisisitiza Mtu atakayebainika kula fedha za wanachama wa SACCOS hajiandae kufikishwa katika vyombo vya Sheria ili kujibu masharti.

  “Niwaagiza Maafisa Ushirika waende wakakague SACCOS zote…haiwezekani Serikali ifikishwe hapo na ibaki kimya”alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.

  “Ukaguzi huo ni pamoja na kuangalia Viongozi waliopo katika SACCOS wamekopa kiasi gani na wanalipa kwa mfumo gani isije ikiwa wanaonufaika ni viongozi tu” aliongeza Mwanri.

  Aliongeza kuwa baada ya ukaguzi huo Ofisi yake itayafanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua mbalimbali wale wote watakaonekana kutumia vibaya madaraka yao katika SACCOS.

  Naye Kaimu Afisa Ushirika wa Wilaya ya Urambo Hilda Boniface akisoma risala ya wanaushirika alisema kuwa baadhi ya SACCOS zimekufa kwa sababu ya viongozi wake ikiwemo Wakurugenzi Watendaji kushindwa kupeleka makato ya fedha za wanaushirika katika sehemu husika.

  Alisema kuwa hali hiyo imewakatisha baadhi ya wanaushirika na kuwafanya wasione umuhimu wa kujiunga na SACCOS katika maeneo yao.

  0 0  0 0


  Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WAMJW.

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia wazee na watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya jamii) Bibi Sihaba amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii katika halmashauri zote nchini kutekeleza wajibu wa uundaji wa Kamati za Ulinzi na Usalama wa mtoto kuanzia ngazi ya mtaa mahali walipo wananchi ili kuwa na mfumo thabiti wa kuzuia na kutoa huduma kwa watoto wanaofanyiwa ukatili.

  Ameyasema hayo mapema wiki hii wakati wa kikao cha majumuhisho kwenye kilele cha safari yake ya kikazi katika kijiji cha Tanangozi, kata ya Mseke, tarafa ya Mlolo, wilaaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa na kupokea taarifa za utetezi wa haki za watoto kutoka kwa Baraza la Watoto la Kata ya Mseke, Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto, na Timu ya malezi ya watoto wa Kata ya Mseke.

  Ameongeza kuwa mabaraza ya watoto yakianzishwa na kuimarishwa katika ngazi za vijiji na kata yatasaidia kutoa raghiba ya watoto kujitambua, kujithamini na kujilinda dhidi ya vitendo vya ukatili na pia kujiepusha na vishawishi vya mahusiano na wanaume katika umri mdogo.

  Aidha, Katibu Mkuu aliwapongeza wajumbe wa vyombo hivyo vilivyoundwa na watoto na wazazi kuendeleza wajibu wao wa kuzuia na kutokomeza ukatili na nyanyasaji wa watoto katika ngazi ya familia, jamii na shuleni ili kuongeza ubora wa jamii zetu katika utoaji wa haki za msingi za watoto wote katika jamii zetu.

  Alisema Serikali imekamilisha mwongozo wa utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza dhidi ya wanawake na watoto hapanchioni amabo utasambazwa kwa wadau ili kutoa maelekezo fasaha ya utendaji katika maeneo ya utekelezaji wa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

  Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga amesisitiza kutumia vikundi vya malezi ya watoto na sanaa katika Kata ya Msewe, Wilaya ya Iringa Vijijini kwa kujiunga pamoja na kutumia stadi na mbinu walizonazo katika kuelimu jamii kuacha vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ili kuimarisha mazingira upatikanaji wa haki na usawa kwa wototo wote.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga(kushoto) akisalimiana na mjumbe wa Kamati Kuu ya Baraza la Watoto Taifa Lulu Nziku mara baada ya kumaliza mkutano na Baraza la kata ya mseke iringa Vijijini hivi karibuni.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW.

  0 0


older | 1 | .... | 1344 | 1345 | (Page 1346) | 1347 | 1348 | .... | 1904 | newer