Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1342 | 1343 | (Page 1344) | 1345 | 1346 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dodoma Asia Abdulkarim Halamga ameongea na viongozi wa Mashina, Matawi na Kata huko Buigiri Wilayani Chamwino ikiwa ni sehemu ya semina ya mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wapya waliochaguliwa hivi karibuni waweze kutambua majukumu yao, wafanye kazi bila kuingiliana kwa maslahi ya Chama na serikali.

  Ameyasema hayo ikiwa ni mpango maalum wa vijana wa Chama cha Mapinduzi kuwapiga msasa viongozi wake ili waweze kuisimamia serikali katika kutekeleza majukumu yake.

  Asia Halamga amewataka viongozi hao kufanya kazi kwa juhudi na uadilifu mkubwa ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na serikali kwa ujumla lakini pia kubuni miradi itakayowawezesha kujitegemea kiuchumi kwani wao ndiyo taswira ya Chama hivyo wanapaswa kuwa mfano bora kwa jamii.

  Sambamba na mafunzo hayo pia ametoa kadi 252 za umoja wa vijana UVCCM pamoja na kanuni katika matawi ya Makulu, Buigiri, Mwegamile na Chinangali II ambapo kila tawi limepata kadi 63 kwa lengo la kuongeza wanachama wa UVCCM na sehemu ya malipo yake itumike kutunisha mifuko ya matawi yao.

  Naye Diwani wa Kata hiyo Mheshimiwa Kenneth Yindi aliahidi kufanyia kazi Agizo la Katibu wa UVCCM mkoa wa Dodoma la kutatua changamoto ya kutokuwepo kwa ofisi ya Kata kwa kujenga ofisi, Ambapo ujenzi huo unaanza kufanyika mwezi tisa mwaka huu kwa kushirikiana uongozi wa umoja wa vijana na wanachama wake katika Kata ya Buigiri, ambapo Katibu wa UVCCM Mkoa aliahidi mara watakapokuwa tayari atawaunga mkono katika ujenzi wa Ofisi hiyo. 

  Pia Diwani alipokea Agizo la kuzitafutia mashamba Jumuiya tatu za Vijana, Wazazi na Wanawake watakayoyatumia kujiingizia kipato ili waweze kujitegea kiuchumi.
    Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dodoma Asia Abdulkarim Halamga akimkabidhi mmoja wa viongozi wa matawi kadi za UVCCM
   Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dodoma Asia Abdulkarim Halamga ameongea na viongozi wa Mashina, Matawi na Kata huko Buigiri Wilayani Chamwino ikiwa ni sehemu ya semina ya mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wapya waliochaguliwa hivi karibuni waweze kutambua majukumu yao, wafanye kazi bila kuingiliana kwa maslahi ya Chama na serikali.

  0 0  0 0


  Meneja matukio wa Dimba Music Concert, Mwani Nyangassa, akizungumza na waandishi wa Habari jana kutambulisha wanamuziki watakaoshiriki katika tamasha hilo, litakalofanyika Septemba 2 kwenye ukumbi wa Travertine, Hotel Magomeni. Kushoto ni Mhariri wa Dimba Jimmy Chika na kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya New Habari (2006) LTD Michael Budigila.
  Baadhi ya wanamuziki watakaoshiriki Dimba Music Concert, wakiwa na Kamati ya Maandalizi jana mbele ya waandishi wa habari katika Ofisi za New Habari (2006) LTD.
  Wanamuziki Juma Kakere, Ally Choki, Hussein Jumbe na Juma Katundu, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutambulishwa kutumbuiza katika Tamasha hilo Septemba 2.
  Mhariri wa Dimba, Jimmy Chika, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanamuziki na wajumbe wa kamati ya maandalizi ya Dimba Concert .

  ********************************************

  Kampuni ya New Habari (2006) LTD kupitia gazeti lake la DIMBA, imeandaa onesho maalum la muziki wa dansi DIMBA Music Concert litakaofanyika Septemba 2 mwaka huu katika Ukumbi wa Traventine Magomeni jijini Dar es Salaam.

  Onesho hilo lina lengo la kuukuza na kupromoto muziki wa dansi, ambao umekuwa ukielekea kupotea kila kukicha.

  Katika onesho hilo kutakuwepo na mpambano wa wanamuziki wa dansi, ambapo bendi ya Msondo Ngoma Music (Baba wa Muziki), itachuana na mastaa mbalimbali wa muziki huo kutoka bendi mbalimbali nchini.

  Kundi la mastaa ambao tumewapa jina la ‘Timu ya Taifa ya Muziki wa Dansi,’ litakalochuana na Msondo Ngoma, litaundwa na wanamuziki kama Kikumbi Mwanza Mpango' King Kiki', Hassan Rehani Bitchuka 'Stereo', Karama Regesu, Ally Choky, Juma Kakere, Nyoshi El-Saadat ‘Sauti ya Simba’ na Muumini Mwinjuma.

  Kwa upande wa vyombo, watakuwepo wapiga vyombo Saadi Ally 'Machine' kwenye dramu, gitaa la solo likitekenywa na Aldofu Mbinga wakati besi litangurumishwa na Hosea Mhogachi.

  Aidha, kinanda kitatekenywa Juma Jerry wakati tumba zitakung'utwa Salum Chakuku 'Kuku Tumba', ambapo ala za upepo watakuwepo Ally Yahaya, Hamis Mnyupe Tarumbeta na Shaabani Lendi kwenye Saksafoni.

  "Utakua ni usiku wa mastaa wa dansi kuionyesha kazi Msondo Ngoma, kwani miaka ya hivi karibuni imekua ikikosa mbabe katika kila bendi inayoshindanishwa nayo lakini safari hii tumeamua tuwaonyeshe kazi."
  Kiingilio katika onesho hilo litakaloanza kuanzia saa 2:00 usiku hadi majogoo, kitakuwa ni shilingi 10,000 kwa wote na 20,000/- kwa VIP.


  IMETOLEWA NA MENEJA WA TUKIO ‘DIMBA MUSIC CONCERT’ MWANI NYANGASSA

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wa mtoto ya Wilaya ya Mufindi alipotembelea Mkoani Iringa.
  Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wa mtoto ya Wilaya ya Mufindi wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga(hayupo pichani) wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea Mkoani Iringa.
  Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William akisistiza jambo wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wa mtoto ya Wilaya ya Mufindi wakati Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga alipotembelea Mkoani Iringa.
  Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi akieleza jambo kwa na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wa mtoto ya Wilaya ya Mufindi wakati Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga alipotembelea mkoani Iringa.
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wa mtoto ya Wilaya ya Mufindi wakati Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga alipotembelea Mkoani Iringa.
  Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mufindi Mhe. Maua Rashid akifafanua jambo la kisheria kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga alipotembelea Wilayani hapo na kuzungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wa mtoto ya Wilaya.
  Mjumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mtoto ya Wilaya ya Mufindi Inspecta akielezea masuala mbalimbali ya kesi zilizoripotiwa polisi kutokana na ukatili dhidi ya kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga alipotembelea Wilayani hapo.
  Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mufindi Abechi Masanga akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga zilizoripotiwa Polisi kuhusu ukatili dhidi ya watoto wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea mkoani Iringa.
  Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mufindi Abechi Masanga(katikati) akielezea jinsi Dawati la Jinsia na watoto kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga linavyofanya kazi yake wakati alipotembelea Wilayani hapo.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba akitoka katika Ofisi ya Dawati la Jinsia na watoto katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Mufindi kujionea shughuli zinazofanyika katika dawati hilo.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na usalama wa mtoto na watendaji wa Dawati la Jinsia na watoto Wilaya Mufindi Mkoani Iringa.

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga akiwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mufundi wakati alipotembelea Mkoani Iringa.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mufundi wakati alipotembelea mkoani Iringa.
   
   Picha na Erasto Ching’oro WAMJW
   

  0 0


  Na. Jeshi la Polisi.

  Makamishna wastaafu wa Polisi Paul Chagonja, Hamdan Omar Makame na Kenneth Kaseke wametakiwa kuendeleza elimu ya Polisi jamii pamoja na kutoa msaada wowote utakaohitajika kwa Jeshi la Polisi pindi wanapokuwa katika maisha ya uraia baada ya kustaafu utumishi wa Jeshi la Polisi ili kuhakikisha kuwa wahalifu hawapati nafasi ya kutamba hapa nchini.

  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro wakati wa sherehe zilizoambatana na Gwaride maalumu la kuwaaga wastaafu hao lililofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Polisi Dar Es Salaam ambapo wastaafu hao walisukumwa kwenye gari maalumu na Makamishna Wasaidizi Waandamizi sita ikiwa ni utaratibu wa Jeshi hilo katika kuwaaga maofisa wakuu.

  IGP Sirro alisema kazi waliyofanya wastaafu hao ni kubwa lakini kustaafu kwao siyo mwisho wa kutumika katika kazi za Polisi na hivyo waendelee kuwa tayari wakati wowote kwa kuwa sasa Jeshi la Polisi linaendelea kushirikisha jamii kukabiliana na uhalifu.

  “Upolisi ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine hivyo utaalamu hauzeeki na kwetu sisi tunaondelea kubaki Jeshini tutaendelea kufuata yale yote mazuri mliyofanya na nyie mnapokuwa nje ya utumishi endeleeni kutusaidia kwa mawazo na milango yetu ipo wazi ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa salama” Alisema IGP Sirro

  Akizungumza baada ya kuagwa rasmi Jeshini Kamishna Paul Chagonja ambaye alikuwa Kamishna wa Oparesheni na mafunzo kwa muda mrefu amewaasa Maofisa na Askari kuendeleza tamaduni na maadili ya Polisi pamoja na kufanya kazi kwa weledi.

  Chagonja amesema nidhamu ndio msingi wa Askari Polisi popote pale wafanyapo kazi zao hivyo amewaomba kuendelea kusimamia sheria bila ya kumuonea muhali mhalifu yeyote.

  Kwa upande wake Aliyekuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame amewashukuru wananchi wote hususani wa Visiwani kwa ushirikiano waliompatia kipindi chote hali ambayo imesababisha Zanzibar kuendelea kuwa shwari.

  Sherehe hizo zimehudhuriwa na Viongozi mbalimbali kutoka vyombo vya ulinzi na usalama, Mkurugenzi wa Takukuru Kamishna Valentino Mlowola, IGP Mstaafu Said Mwema, DCI Mstaafu Robert Manumba na Kamishna Mstaafu wa Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam Suleiman Kova pamoja na maofisa na Askari Polisi.
   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Kamishna Mstaafu Paul Chagonja wakati wa sherehe zilizoambatana na Gwaride maalumu la kuwaaga makamishna wastaafu watatu, gwaride lililofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Polisi Dar Es Salaam ambapo wastaafu hao walisukumwa kwenye gari maalumu na Makamishna Wasaidizi Waandamizi sita ikiwa ni utaratibu wa Jeshi hilo katika kuwaaga maofisa wakuu. Kulia ni Kamishna Mstaafu Hamdani Makame.
  Kamishna Mstaafu Paul Chagonja akikagua gwaride maalum lililoandaliwa kwaajili ya sherehe ya kuwaaga makamishna wastaafu watatu akiwemo kamishna Chagonja, Kmaishna Paul Chagonja na Kamishna Kenneth Kaseke. Gwaride hilo lilifanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Polisi Dar Es Salaam ambapo wastaafu hao walisukumwa kwenye gari maalumu na Makamishna Wasaidizi Waandamizi sita ikiwa ni utaratibu wa Jeshi hilo katika kuwaaga maofisa wakuu.
  Makamishna wastaafu Paul Chagonja (kushoto) na Hamdani makame wakisukumwa kwenye gari na Makamishna Wasaidizi Waandamizi sita ikiwa ni utaratibu wa Jeshi la Polisi katika kuwaaga maofisa wakuu. Makamishna hao wamestaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria na waliandaliwa Gwaride maalum la kuwaaga lililofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Polisi Dar Es Salaam.Picha kwa hisani ya Jeshi la Polisi

  0 0

  Mkurugenzi wa Mkuu wa TIB Corporate Bank,Frank Nyabundege akizungumza wakati wa Jukwaa la Biashara lililofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Regal Naivera Jijini Tanga 
  Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano ya Benki ya TIB Corporate ,Theresia Soka akizungumza wakati wa Jukwaa hilo 
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Dokta Harrison Mwakyembe kulia akilakiwa na wajumbe wa Jukwaa hilo wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa TSN Dokta Jimmy Yonazi wanne kushoto ni MD wa TIB Corporate Bank,Frank Nyabundege na wakwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa. 

  TIB Corporate Bank (TIB CBL) wameshiriki katika Jukwaa la Biashara ,Jukwaa hili linakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo ili kujadili na kuona namna gani Kila mmoja anawezesha mkoa wa Tanga Katika kuleta maendeleo.

  TIB Corporate Bank ni benki ya Biashara na inatoa Huduma zote za kibenki. Kwa kutambua fursa mbalimbali KTK Mkoa wa tanga, benki inajiweka sawa ili kuhakikisha huduma za kibenki zinawafikia wana Tanga.tunambua Kuwa maendeleo yoyote Yale ya kibiashara na viwanda yanahitaji uwezeshwaji wa kifedha (bank facilities).

  TIB Corporate Bank inatoa Huduma mbalimbali kutokana na mahitaji ya Mteja.Baadhi ya Huduma hizo ni pamoja na akaunti mbalimbali za kwa makampuni na Watu binafsi,mikopo ya aina mbalimbali ya muda mfupi na muda wa kati,dhamana za kibenki( bank guarantee),ununuaji na uuzaji wa fedha za kigeni,uwekezaji katika hati fungani,( treasury bills & Bonds), ukusanyaji wa fedha na kuwezesha malipo ya jumla kwa makampuni (cash management ) pamoja na ulipaji wa mishahara kwa Njia rahisi na haraka

  Huduma zetu hutolewa kwa umahiri na ufanisi mkubwa ili kuhakikisha Mteja anafurahia mahusiano yake na benki.Pia Huduma ya Premier Banking kwa wateja wanaopenda kujitofautisha zaidi.

  Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

  Na Rhoda James

  Wizara ya Nishati na Madini imekutana na Kampuni ya Hyundai E & C ya Korea Kusini ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika vyanzo vipya vya nishati nchini.

  Kampuni hiyo na Wizara wamekutana jijini Dar es Salaam ambapo kikao hicho pia kimehudhuriwa na taasisi zilizo chini ya Wizara likiwemo Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Madini ya Taifa (STAMICO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

  Akizungumzia kuhusu uwekezaji huo, Kamishna wa Nishati anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati, James Andilile amesema kuwa Serikali inakaribisha wawekezaji zaidi kuwekeza nchini hususan katika vyanzo vipya vya umeme ikiwemo Makaa ya Mawe, miradi inayotumia nguvu za maji, pamoja na miradi ambayo bado haijaanza kutekelezwa.

  Andilile ameeleza kuhusu miradi mikubwa ya nishati inayoendelea kutekelezwa nchini kwa sasa ikiwemo ile ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia na kuitaja kuwa ni pamoja na Mradi wa Kinyerezi II wa Megawati 240, Kinyerezi I Extension Megawati 185.

  “Ipo miradi ambayo inahitaji ufadhili au Serikali inahitaji kuingia ubia na Kampuni za ndani na nje ili kuifanikisha, mojawapo wa miradi hiyo ni Kiwira ambao Serikali ingependa kuona unaanza haraka,” amesisitiza Andilile.

  Kwa upande wake Mwakilishi wa Kampuni ya Hyundai E & C, Dongil Chang amesema kuwa, kampuni hiyo inayo nia ya kuwekeza Tanzania kwa kuwa inao uzoefu mkubwa katika masuala ya Nishati.Ameongeza kuwa, kampuni hiyo ni ya 13 kwa ukubwa Duniani hivyo inavyo vigezo na uwezo wa kutekeleza miradi mbalimbali.

  “Tupo tayari kuwekeza Tanzania katika sekta ya Nishati. Mara baada ya kupata taarifa zote muhimu kwa ajili ya uwekezaji bila shaka tutaanza majadiliano mara moja.” ameongeza Chang.
   Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (mbele), Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati, James Andilile (wa kwanza kulia mstari wa mbele) ambaye ameeleza kuhusu uwekezaji katika masuala ya umeme kwa kutumia makaa ya mawe. Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 18 Agosti, 2017 katika ukumbi wa Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni wajumbe kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara.

  Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (mbele) akieleza jambo mbele ya wajumbe walioshiriki kikao baina ya Wizara na Wawekezaji wa Kampuni ya Hyundai E & C.

  Wajumbe kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Madini ya Taifa (STAMICO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakifatilia mada katika kikao baina ya Wizara na Kampuni ya Hyundai E & C.

  Kamishna wa Biashara nchini kutoka Ubalozi wa Korea, Jeon, Heesu (anayetoa maelezo) akielezea uzoefu wa Kampuni ya E & C katika masuala ya Nishati katika kikao kilichofanyika Wizara ya Nishati. Wengine katika picha ni Ujumbe kutoka Kampuni ya Hyundai E & C pamoja na Wawakilisha kutoka Benki ya Exim nchini.

  0 0

   Mbunge wa Ubungo,Saed Kubenea akizungumza na Wanafunziwa Darasa la Tatu wa Shule ya Msingi Makuburi wakati alipokwenda kukagua ukarabati wa Madarasa wa shule hiyo unaotokana na mfuko wa jimbo na fedha za Halmashauri ambapo jumla ya fedha zaidi ya Milioni 88 zimetolewa na Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya ubungo na Milioni 17 Kutoka Mfuko wa Jimbo wa  mbunge huyo
   Mbunge wa Ubungo,Saed Kubenea akizungumza na Wanafunziwa Darasa la Tatu wa Shule ya Msingi Makuburi wakati alipokwenda kukagua ukarabati wa Madarasa wa shule hiyo unaotokana na mfuko wa jimbo na fedha za Halmashauri ambapo jumla ya fedha zaidi ya Milioni 88 zimetolewa na Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya ubungo na Milioni 17 Kutoka Mfuko wa Jimbo wa  mbunge huyo
   Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaaa wa Mwongozo , James Gointamile (CCM)   akimuonesha Mbunge wa Ubungo , Saed Kubenea (CHADEMA), Baadhi ya Vigae ambavyo vilikuwa vinavuja katika madarasa matatu ya Shule ya Msingi Makuburi mara baada ya Mbunge Huyo kutoa Milioni 17 kwa ajili ya kununua bati mpya za kisasa kuezeka shule hiyo.
   Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akionesha Sehemu ya Paa ambayo inavuja, inatarajiwa kuzibwa hivi karibuni na Mabati amabyo yametolewa kwenye fedha za mfuko wa Jimbo
   Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akiangalia sehemu ya Shimo la choo cha Matundu 12 kinachotaraji kujengwa na fedha za Halmashauri ya Manispaa ya ubungo mara baada ya Choo cha shule hiyo kutokuwa katika hali nzuri
   Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akizungumza na Watendaji wa Mtaa na Diwani wa kata ya Makubuli, Hanifa Chiwili kwenye darasa ambalo liko juu ya chemba ya kuhifadhia maji ya mvua ya shule hiyo hili kuzuia Mmong'onyoko kwa Madarasa Mengine
   Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akizungumza na Walimu wa shule ya Msingi Makuburi mara baada ya kutembelea chumba cha Walimu.
   Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea Akiwa katika korido za shule msingi Makuburi
   Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akiagana na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Makuburi

  0 0

  UCSAF imesaini makubaliano na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel pamoja na makampuni mengine ya simu nchini kwa lengo la kuhakikisha mawasiliano ya simu yanawafikia watanzania wote hadi vijijini. Hafla ma makubaliano hayo imefanyika leo kwenye makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam,

  "mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano Mallya alisema "Airtel tunasaini mkataba huu kwa lengo lakuendelea kutimiza mawasiliano kwa wote nchini

  Singano alisema kuwa "uwepo wa mawasiliano haya vijijini utasaidia hata kutimiza malengo mbalimbali ambayo serikali imejiwekea katika kupanua uchumi wa nchi kwa ujumla, elimu, afya, uboreshwaji wa kilimo pamoja na huduma za kibenki kwa maeneo ambayo yako pembezoni.
  Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Malya wakisaini mkataba wa Mradi wa sita wa kupeleka mawasiliano kwa wote. UCSAF imesaini makubaliano na makampuni yote ya simu nchini yenye lengo la kuhakikisha mawasiliano ya simu yanawafikia watanzania wote hadi vijijini na hafla hiyo imefanyika kwenye makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam, Agosti 18, 2017.
   Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice Suingano Malya, wakibadilishana hati baada ya kusaini mkataba wa sita wa kepeleka mawasiliano ya simu kwa wote. UCSAF imesaini makubaliano na makampuni yote ya simu nchini yenye lengo la kuhakikisha mawasiliano ya simu yanawafikia watanzania wote hadi vijijini na hafla hiyo imefanyika kwenye makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam, Agosti 18, 2017.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, (kulia), akimpongeza Mwakilsh wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Malya, mara baada ya Airtel kusaini mkataba wa sita wa Mradi wa kupeleka mawasiliano ya simu kwa wote na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, (UCAF), jijini Dar es Salaam, Agosti 18, 2017.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (Katikati) akiwashuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Le Van Dai kwa Pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF) Mhandisi. Peter Ulanga wakitia saini Mkataba wa kuboresha Mawasiliano vijijini baina ya kampuni hiyo na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF). Katika hafla hiyo kampuni ya Halotel itajenga minara mipya 47 sawa na asilimia 59 ya tenda iliyotolewa kwa makampuni yote ya simu.
  Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (Katikati) akiwashuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Le Van Dai kwa Pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF) Mhandisi. Peter Ulanga wakitia saini Mkataba wa kuboresha Mawasiliano vijijini baina ya kampuni hiyo na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF). Katika hafla hiyo kampuni ya Halotel itajenga minara mipya 47 sawa na asilimia 59 ya tenda iliyotolewa kwa makampuni yote ya simu.
  Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai, kabla ya kuanza kwa hafla ya kutiliana saini Mkataba wa kuboresha Mawasiliano vijijini baina ya kampuni hiyo na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF). Katika hafla hiyo kampuni ya Halotel itajenga minara mipya 47 sawa na asilimia 59 ya tenda iliyotolewa kwa makampuni yote ya simu. Pamoja naokatika picha ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (USCAF) Mhandisi. Peter Ulanga.

  0 0

   Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Mhandisi, Cecil Nkomola Francis (kulia)na Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Mhandisi  Peter Ulanga(Kushoto) wakisaini mkataba wa kupeleka mawasiliano vijijini, na kushuhudiwa na Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, katika hafla iliyofanyika ofisi za UCSAF, Kijitonyama, Dar es salaam 
   Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Mhandisi, Cecil Nkomola Francis (kulia)na Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF Mhandisi , Peter Ulanga(Kushoto) wakibadilishana hati za mkataba wa kupeleka mawasiliano vijijini. 
    Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano akitoa hotuba katika hafla ya kusaini mkataba kwa Makampuni ya Simu kupeleka mawasiliano vijijini.  
  Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Mhandisi Peter Ulanga akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba na makampuni ya simu kupeleka mawasiliano vijijini, katika hafla iliyofanyika ofisi za UCSAF, Kijitonyama, Dar es salaam

  0 0

  TACAIDS has commended the work done by Jhpiego, a non-governmental organization leading the Sauti Project with EngenderHealth, Pact, and NIMR-Mwanza, in leading the fight against HIV in Shinyanga by implementing innovative combination prevention interventions.

  Briefing the media on how they are fighting HIV/AIDS in Shinyanga, the Regional AIDS Coordinators for TACAIDS Mr. Nassibu Rashidi Ngoya says the government through TACAIDS in partnership with non government partners like Jhpiego are working tirelessly to fight this pandemic by targeting key and vulnerable populations such as out-of-school adolescent girls and young women aged 15-24yrs.

  Mr. Ngoya says “The DREAMS Initiative activities under Sauti Project have been astonishing in helping to bring hopes to young girls in Shinyanga as it has specific components that deal with behavior change communication to build risk reduction skills and self-efficacy among them and empower them economically." Giving the overview of the HIV prevalence, Mr. Ngoya, explained that Shinyanga has a prevalence rate of 7.4% which is higher compared to other surrounding regions, and DREAMS interventions are being rolled out in four councils of Kahama Town, Ushetu, Msalala, and Shinyanga Municipality.Outlining how the USAID-funded Sauti

  Project's DREAMS Initiative interventions work, Miss. Esther Majani, the Senior Technical Adviser for Adolescent and Youth Sexual Reproductive Health, says that everything is aimed at creating determined, resilient, empowered, AIDS-free, mentored and safe young women--objective components which also make up the acronym DREAMS.

  “Apart from education on gender and sexual reproductive health, we provided them with economic empowerment training through which they gained entrepreneurial skills and they are now able to form peer groups, contribute and raise enough money for potential capital. Everyone who is given a loan is mentored to ensure that their business is sustainable,” she added. When in groups, the girls also get access to free, adolescent-friendly and nonjudgmental Voluntary Counselling and Testing services, family planning methods, and screenings for gender-based violence.

  The DREAMS Initiative in Tanzania is funded by the US Government through PEPFAR, which has provided $18 million to support a combination of age-appropriate and evidence-based interventions targeting vulnerable 10-14 year olds who are in-school and 15-24 years old adolescent girls and young women who are out-of-school as part of targeted, innovative and multisectoral efforts to curb new HIV infections.
   Young Adolescent Girls in Shinyanga Region in a joyful mood after a successful skills learning sessions on how to prevent risky HIV behaviors as part of the DREAMS initiatives activities which aim to empower them with multifaceted skills to live healthier lives and achieve their Dreams. The DREAMS Initiative in Tanzania is funded by the US Government through PEPFAR and Jhpiego's SAUTI project is a community prevention implementing partner.
   Young Adolescent Girls in Shinyanga Region in a joyful mood after a successful skills learning sessions on how to prevent risky HIV behaviors as part of the DREAMS initiatives activities which aim to empower them with multifaceted skills to live healthier lives and achieve their Dreams. The DREAMS Initiative in Tanzania is funded by the US Government through PEPFAR and Jhpiego's SAUTI project is a community prevention implementing partner.

   Young Adolescent Girls in Shinyanga Region in a joyful mood after a successful skills learning sessions on how to prevent risky HIV behaviors as part of the DREAMS initiatives activities which aim to empower them with multifaceted skills to live healthier lives and achieve their Dreams. The DREAMS Initiative in Tanzania is funded by the US Government through PEPFAR and Jhpiego's SAUTI project is a community prevention implementing partner.
   

  0 0

  Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Jasem Al-Najem (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto wanaoishi wanaoishi katika magumu cha Eco Village mkoa wa Pwani baada ya kuwakibidhi zawadi mbalimbali.

  Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasem Al-Najem ametembelea Kijiji cha Eco-Village kilichopo Kisemvule Mkoa wa Pwani. Eco-village ni eneo la kulelea na kuhudumia mayatima ambapo ndani yake kunafanyika shughuli za kilimo,ufugaji wanyama hasa kuku na ng'ombe, na hutegemea umeme wa jua kama chanzo cha nishati.

  Katika ziara hiyo Mhe. Jasem  alikabidhi msaada wa vyakula unga wa ngano,mchele,maharage,mafuta ya kula,majani ya chai na sukari kwa ajili ya watoto mayatima msaada ambao utatosheleza kwa kipindi cha miezi miwili.

  Pembezoni mwa ziara Mhe. Balozi alipanda mti ikiwa ni ishara ya kuunga mkoni juhudi za Eco-village ambacho ni kituo kinachoendesha mambo yake kisasa. 
   Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Jasem Al-Najem  akipanda mti katika kituo cha watotot wanaoishi wanaoishi katika magumu cha Eco Village mkoa wa Pwani  alipikwenda kutembelea kituo hicho na kutoa msaada wa vitu mbalimbali.

  0 0

  Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza na kikundi cha wajasiliamali kikundi cha ushoni Mchanga mdogo Mkoa wa Kaskazini pemba wilaya Wete.
  Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka(wa kwanza kushoto) akishiriki ujenzi wa Jengo la maskani Mtambwe Wilayani wete.
  wanachama wakimlaki Kaimu katibu mkuu mara baada ya kuwasili kuzungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
  Wanachama na Viongozi wa CCM na Jumuiya zake Wilaya ya Wete wakifuatilia kwa Umakini mkutano huo.
  Kaimu katibu wa Idara ya Uchumi Uwezeshaji na Fedha (UVCCM) ndg:Dorice Obed akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
  Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Pemba Khadija Nassoro Ally akizungumza katika Mkutano wa ndani akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
  Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza katika Mkutano wa ndani akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
  Wanachama na Viongozi wa CCM na Jumuiya zake Wilaya ya Wete wakimsikiliza  Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI).  Na Mathias Canal, Kaskazini Pemba

  Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Umeipongeza serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi Visiwani Pemba.

  UVCCM imesema kuwa RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko makubwa ya kimaendeleo ikiwemo kuundwa kwa Mamlaka ya Viwanja vya ndege vya Zanzibar jambo ambalo litaongeza mapato kwa serikali na vipato kwa wananchi.

  Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka leo Agosti 17, 2017 alipokuwa akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

  Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya muundo wa Umoja wa Kitaifa (SKU) imepata mafanikio makubwa katika kipindi cha uongozi wa miaka saba cha Dkt Shein.Alisema kuwa kuwepo kwa Serikali hiyo kumeweza kuleta maelewano ya kisiasa pamoja na kuvishirikisha vyama vingine katika uwezeshaji wa serikali.

  Alisema kuwa sekta ya elimu imeimarika kwa kiasi kikubwa jambo ambalo linazidi kurahisisha upatikanaji wa elimu bora ikiwemo kuimarika kwa mishahara ya wafanyakazi Visiwani Zanzibar.

  Alisema kuwa uvumilivu wa kisiasa na kuheshimu Katiba na sheria ndio siri ya mafanikio ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwemo kuheshimu katiba, utawala bora, kupinga udhalilishaji kwa watoto na wanawake.

  Awali akizungumza na vijana wa Maskani ya Subira yavuta kheri iliyopo eneo la Mgogoni, Shaka alisema kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF aliyesimamishwa uongozi Maalim Seif Shariff Hamad anapaswa kupumzika na kuacha siasa za kuwagawa wananchi badala yake amemtaka awe kuungo katika kujenga umoja na mahusiano.

  Shaka yupo ziarani Kisiwani Pemba ambapo atatembelea mikoa yote miwili ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba ambapo pia atazuru katika Wilaya zote nne ikiwa ni pamoja na Wilaya ya Wete, Micheweni, Mkoani na Chakechake kwa kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020.


  0 0

  Hyasinta Kissima-Njombe.

  Shirika la kulinda na kutetea haki za watoto dunia UNICEF limetoa vifaa vya aina mbalimbali vyenye thamani ya Shilingi Milioni 4,591,000/= kwa makundi matatu ya watoto wenye mahitaji maalumu katika Halmashauri ya Mji Njombe.

   Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda amesema kuwa anaipongeza UNICEF kwani wamekuwa wadau wakubwa wa maendeleo katika halmashauri yake sio kwa upande wa lishe kwa watoto bali hata kujali makundi ya watoto wenye mahitaji maalumu.

  Aidha Mkurugenzi huyo amevipongeza vyombo vya habari kwa kuandika habari mbalimbali za kijamii kwani kupitia habari za shughuli za kijamii zilizokuwa zinaandikwa na vyombo vya habari shirika la UNICEF liliguswa na kuona ni vyema kuunga mkono jitihada hizo.

  “Ninaamini kabisa Kwa jitihada za waandishi wa habari kutangaza habari ambazo huwa tunatoa misaada kidogo kidogo ile ya Halmashauri kila robo ya mwaka kwa vituo mbalimbali vya kulelea watoto habari ziliwafikia wenzetu wa UNICEF nao wakaona ni vizuri wakatuunga mkono”Alisema Mwenda.

  Farida Mgeni ni mzazi ambaye mtoto  wake wa umri wa miaka sita anaulemavu wa akili ambaye yeye ameishukuru UNICEF kwa kupokea msaada wa  godoro, mashuka, blanket na vifaa vya kuchezea mtoto wake na amesema vifaa hivyo vitamsaidia sana mtoto wake alikua hana malazi na vifaa vya michezo vitaendelea kuimarisha akili na kuongeza uchangamfu kwa mtoto wake.

  Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Hosea Yusto amesema kuwa miongoni mwa changamoto wanazokumbana nazo katika kutambua uwepo wa watoto wenye mahitaji maalumu ni pamoja na wazazi kutokuwa na uelewa kuwa licha ya mtoto kuwa na ulemavu bado anahaki ya kupata mahitaji yake yote ya msingi na hivyo kupelekea watoto kufichwa ndani bila kupatiwa huduma kama elimu na afya na amewataka wazazi kuachana na tabia hiyo na kuhakikisha watoto hao wanatambuliwa ili waweze kupatiwa huduma wanazostahili. 

  Vifaa vilivyokakabidhiwa ni pamoja na magodoro, mashuka, blanket, vifaa maalumu vya kujifunzia na vifaa vya michezo Halmashauri ya Mji Njombe inajumla ya vituo vitatu vyenye waalimu waliopatiwa elimu maalumu ya jinsi ya kuwafundisha watoto wenye ulemavu.
   Mkurugenzi wa Halmasahuri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda (wa kwanza kushoto) akisoma taarifa ya vifaa vilivyokabiidhiwa kutoka UNICEF
   Sehemu ya watoto  wenye mahitaji maalumu kutoka shule ya Msingi Ramadhani, Kibena na Kituo cha Kulelea watoto Yatima cha Compassion waliofika kwenye makabidhiano hayo
   Msaada wa Vifaa kwa watoto wenye mahitaji maalumu kutoka UNICEF
  Mtoto mwenye ulemavu wa macho Timoth  Mwageni akitoa shukrani zake kwa UNICEF mara baada ya kupokea misaada hiyo.

  0 0

  Hyasinta Kissima-Njombe.

  Shirika la kulinda na kutetea haki za watoto dunia UNICEF limetoa vifaa vya aina mbalimbali vyenye thamani ya Shilingi Milioni 4,591,000/= kwa makundi matatu ya watoto wenye mahitaji maalumu katika Halmashauri ya Mji Njombe.

   Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda amesema kuwa anaipongeza UNICEF kwani wamekuwa wadau wakubwa wa maendeleo katika halmashauri yake sio kwa upande wa lishe kwa watoto bali hata kujali makundi ya watoto wenye mahitaji maalumu.

  Aidha Mkurugenzi huyo amevipongeza vyombo vya habari kwa kuandika habari mbalimbali za kijamii kwani kupitia habari za shughuli za kijamii zilizokuwa zinaandikwa na vyombo vya habari shirika la UNICEF liliguswa na kuona ni vyema kuunga mkono jitihada hizo.

  “Ninaamini kabisa Kwa jitihada za waandishi wa habari kutangaza habari ambazo huwa tunatoa misaada kidogo kidogo ile ya Halmashauri kila robo ya mwaka kwa vituo mbalimbali vya kulelea watoto habari ziliwafikia wenzetu wa UNICEF nao wakaona ni vizuri wakatuunga mkono”Alisema Mwenda.

  Farida Mgeni ni mzazi ambaye mtoto  wake wa umri wa miaka sita anaulemavu wa akili ambaye yeye ameishukuru UNICEF kwa kupokea msaada wa  godoro, mashuka, blanket na vifaa vya kuchezea mtoto wake na amesema vifaa hivyo vitamsaidia sana mtoto wake alikua hana malazi na vifaa vya michezo vitaendelea kuimarisha akili na kuongeza uchangamfu kwa mtoto wake.

  Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Hosea Yusto amesema kuwa miongoni mwa changamoto wanazokumbana nazo katika kutambua uwepo wa watoto wenye mahitaji maalumu ni pamoja na wazazi kutokuwa na uelewa kuwa licha ya mtoto kuwa na ulemavu bado anahaki ya kupata mahitaji yake yote ya msingi na hivyo kupelekea watoto kufichwa ndani bila kupatiwa huduma kama elimu na afya na amewataka wazazi kuachana na tabia hiyo na kuhakikisha watoto hao wanatambuliwa ili waweze kupatiwa huduma wanazostahili. 

  Vifaa vilivyokakabidhiwa ni pamoja na magodoro, mashuka, blanket, vifaa maalumu vya kujifunzia na vifaa vya michezo Halmashauri ya Mji Njombe inajumla ya vituo vitatu vyenye waalimu waliopatiwa elimu maalumu ya jinsi ya kuwafundisha watoto wenye ulemavu.
   Mkurugenzi wa Halmasahuri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda (wa kwanza kushoto) akisoma taarifa ya vifaa vilivyokabiidhiwa kutoka UNICEF
   Sehemu ya watoto  wenye mahitaji maalumu kutoka shule ya Msingi Ramadhani, Kibena na Kituo cha Kulelea watoto Yatima cha Compassion waliofika kwenye makabidhiano hayo
   Msaada wa Vifaa kwa watoto wenye mahitaji maalumu kutoka UNICEF
  Mtoto mwenye ulemavu wa macho Timoth  Mwageni akitoa shukrani zake kwa UNICEF mara baada ya kupokea misaada hiyo.

  0 0  0 0

  Mbunge wa mkuranga ,Abdallah Ulega akizindua madarasa yaliyojengwa kwa ushirikiano na familia ya Ghulam Hussein pamoja na mdau wa maendeleo na balozi wa heshima kutoka visiwa vya Seychelles Maria Van Pool (aliyevaa nguo nyekundu).

   Mbunge wa Mkuranga  Abdallah Ulega amefanikiwa kuzindua madarasa mawili katika shule ya msingi Muongozo kijiji cha Mwarusembe yaliyojengwa kwa hisani ya familia ya Ghulam Hussein ikiwa ni kuitikia ombi la Mbunge la kushirikiana na wadau mbalimbali katika  kuijenga Mkuranga.

  Familia hii imeunganishwa na mdau wa maendeleo na balozi wa heshima kutoka visiwa vya Seychelles Maria Van Pool na Katika uzinduzi huo  Ulega aliwasisitiza wazazi kusimamia vyema maendeleo ya elimu ya watoto kwa kushirikiana na walimu.

  Mbunge Ulega alisisitiza pia kutunzwa kwa miundombinu ya elimu ili iweze kudumu kwa mda mrefu na kuwanufaisha waTanzania walio wengi                       
    Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi katika hafla ya uzinduzi wa madarasa mawili katika shule ya msingi Muongozo kijiji cha Mwarusembe, Madarasa hayo yamejengwa kwa hisani ya familia ya Ghulam Hussein.                        
  Muonekano wa nje wa madarasa hayo, pamoja na Mbunge wa mkuranga ,Abdallah Ulega akiwa pamoja na  familia ya Ghulam Hussein pamoja na mdau wa maendeleo na balozi wa heshima kutoka visiwa vya Seychelles Maria Van Pool na wanafunzi wa shule wakiwa wamekaa katika madawati ndani ya madarasa hayo.
   Mbunge wa mkuranga ,Abdallah Ulega akisalimiana na wazazi na  wanafunzi  katika hafla ya uzinduzi wa madara mawili katika shule ya msingi Muongozo kijiji cha Mwarusembe, Madarasa hayo yamejengwa kwa hisani ya familia ya Ghulam Hussein


  0 0

   Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akikiwasilisha mada katika mkutano wa wadau katika kuchangia ushiriki wa Tanzania katika Tamasha la Utamaduni la Afrika Mashariki (Jamafest) leo Jijini Dar es Salaam. Tanzania inatarajiwa kuwakilishwa na wasanii takribani 240. 
   Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bibi. Leah Kihimbi akizungumza kwa niaba ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe katika mkutano wa wadau katika kuchangia ushiriki wa Tanzania katika Tamasha la Utamaduni la Afrika Mashariki (Jamafest) leo Jijini Dar es Salaam. Tanzania inatarajiwa kuwakilishwa na wasanii takribani 240. 
   Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group (CMG), Bw. Ruge Mutahaba akichangia mada wakati wa kikao cha wanakamati ya maandalizi ya kufanikisha ushiriki wa Tanzania katika Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Jamafest) litakalofanyika Jijini Kampala, Uganda, leo Jijini Dar es Salaam. Tanzania inatarajiwa kuwakilishwa na wasanii takribani 240. 
   Mwakilishi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Bw. Nelson Madirisha akisisitiza jambo wakati wa kikao cha wadau kufanyikisha ushiriki wa Tanzania katika Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Jamafest) litakalofanyika Jijini Kampala, Uganda, leo Jijini Dar es Salaam. Tanzania inatarajiwa kuwakilishwa na wasanii takribani 240. 
  Picha ikionyesha namba zinazotumika kupokea michango kutoka kwa wadau kwa ajili ya kusaidia ushiriki wa wasanii kutoka Tanzania katika Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Jamafest) itakayofanyika Jijini Kampala Uganda mapema mwezi Septemba.
   Mmoja wa wadau wa Sanaa na Utamaduni Bi. Esther Baruti akielezea jambo wakati wa kikao cha wadau kufanyikisha ushiriki wa Tanzania katika Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Jamafest) litakalofanyika Jijini Kampala, Uganda, leo Jijini Dar es Salaam. Tanzania inatarajiwa kuwakilishwa na wasanii takribani 240.
  Mmoja wa wadau wa Sanaa na Utamaduni akijaza fomu baada ya kutoa ahadi ya kuchangia fedha kwa ajili ya kufanikisha ushiriki wa Tanzania katika Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Jamafest) litakalofanyika Jijini Kampala, Uganda, katika mkutano uliowakutanisha wanakamati walioteuliwa na Mhe. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) leo Jijini Dar es Salaam. Tanzania inatarajiwa kuwakilishwa na wasanii takribani 240.
   Baadhi ya wadau waliofika kwenye mkutano huo uliowakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi ili kuchangia fedha kwa ajili ya kufanikisha ushiriki wa Tanzania katika Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Jamafest) litakalofanyika Jijini Kampala, Uganda, katika mkutano uliowakutanisha wanakamati walioteuliwa na Mhe. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) leo Jijini Dar es Salaam. Tanzania inatarajiwa kuwakilishwa na wasanii takribani 240.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassana , leo tarehe 18 Agosti 2017 amehudhuria Mkutano wa Troika Mbili za Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC na Troika ya SADC kwa ajili ya kujadili hali ya Siasa , Ulinzi na Usalama katika Kanda.

  Mkutano huu umejadili zaidi hali ya Siasa nchini Lesotho na namna ya kuisaidia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo inatarajiwa kufanya Uchaguzi Mkuu.

  Taarifa kamili ya Mkutano huu itawasilishwa kesho Jumamosi tarehe 19 Agosti 2017, katika Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC.

  Double Troika inahusisha nchi wanachama Sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji.

  Imetolewa na
  Ofisi ya Makamu wa Rais
  Pretoria, Afrika Kusini
  18 Agosti, 2017.
   
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) kabla ya Mkutano wa Troika Mbili za Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  SADC na Troika ya SADC kwa ajili ya kujadili hali ya Siasa , Ulinzi na Usalama katika Kanda.
  Mkutano huo unafanyika mjini Pretoria, Afrika Kusini.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye ukumbi wa OR Thambo mjini Pretoia,Afrika ya Kusini tayari kuhudhuria Mkutano wa Troika Mbili za Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  SADC na Troika ya SADC kwa ajili ya kujadili hali ya Siasa , Ulinzi na Usalama katika Kanda

older | 1 | .... | 1342 | 1343 | (Page 1344) | 1345 | 1346 | .... | 1897 | newer