Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1340 | 1341 | (Page 1342) | 1343 | 1344 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara, Thobias Andengenye


  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .

  Taasisi ya Wajibu imezindua Ripoti ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) na maoni yake katika ukaguzi wa 2016 katika maeneo ambayo ni muhimu kwa kila mtanzania kuweza kujua ripoti hiyo kwa mstakabali wa maendeleo ya taifa. 

  Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kabla ya uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji Taasisi hiyo, Lodovick Utouh amesema kuwa ripoti hiyo imeangalia maeneo matatu ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) na maoni yake katika ukaguzi wa 2016  ambayo  ni Serikali Kuu, serikali za Mitaa pamoja na Mashirika ya Umma.

  Amesema kuwa katika ripoti hiyo kwa deni la taifa linatakiwa kwa serikali kuongeza vyanzo vya mapato ili kuweza kulipa na shughuli zingine za maendeleo ziendelee bila kuongeza mapato na kulipa deni kutafanya shughuli hizo za maendeleo kukwama.

  Utouh amesema katika ripoti hiyo agizo la serikali kwa Halmashauri kutenga asilimia 10 ya kuwawezesha vijana na wanawake inatakiwa kuwa ni mikopo wanayopata inatakwa kuwa katika mzunguko na  kuweza kila mtu kumfikia mkopo huo.
   Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Wajibu, Ludovick Utouh akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa ripoti ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesababu za serikali na maoni yake iliyoangalia maeneo matatu ya ripoti hiyo leo.
   Mkuu wa Program ya uwajibikaji wa masuala ya fedha Tanzania wa Shirika la Maendeleo ya Ujerumani, Dk. Annette Mumert akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa ripoti ya Taasisi ya  wajibu. 
   Mkuu wa Program ya uwajibikaji wa masuala ya fedha Tanzania wa Shirika la Maendeleo ya Ujerumani, Dk. Annette Mumert akizindua ripoti ya taasisi ya wajibu  leo jijini Dar es Salaam.
  Picha pamoja Mkuu wa Program ya uwajibikaji wa masuala ya fedha Tanzania wa Shirika la Maendeleo ya Ujerumani, Dk. Annette Mumert, Watendaji wa Taasisi ya wajibu pamoja na wadau mbalimbali.

  0 0

  Delegation of Presidency for Turks Abroad and Related Communities (YTB) meets Prof. Rai (right) in his office at SUZA main Campus. Others from left are Mr. Mustafa Efe - the Advisor to YTB President, Mr. Mehmet Kose – YTB President and Mr. Nevzat Ceylan -  a Turkish government member of Parliament and Vice President of Turkey-Tanzania Friendship Committee.
  Conversation between Turkish YTB delegation and SUZA officials in progress

  The Republic of Turkey pledged to strengthen her relationship with the State University of Zanzibar (SUZA) in matters related to higher education field, this was clarified by Mr. Mehmet Kose, the Head of Presidency for Turks Abroad and Related Communities (YTB) during his visit at SUZA main campus with his delegation on 14th August, 2017. They were hosted by Prof. Idris Rai, the SUZA Vice Chancellor and his Management team.

  The delegation was very much pleased by their visiting in Zanzibar and Tanzania in totality where Mr. Nevzat Ceylan who is a Turkish government member of Parliament and Vice President of Turkey-Tanzania Friendship Committee stated that their visit is a clear testimony that their historical relationship with Zanzibar is still influential. “Our presence here today will enhance this historical relationship between us”, he added.

  Turkey through this mission has shown interest to work in partnership and promised to establish higher learning exchange programmes and expertise in various disciplines with SUZA, also aims to initiate cooperation in teaching languages spoken in these two nations.

  Prof. Idris Rai informed his visitors that Zanzibar has significantly benefited from having relationship with Turkey through the enjoyment of various educational opportunities which are offered by Turkey; he said that Zanzibar has a variety of experts in diverse fields who obtained their education from that country.

  He notified the delegation that there are already over twenty Turkish higher learning institutions which have shown interest to collaborate with SUZA in certain development programmes among which have reached agreement to sign memoranda of understanding (MoUs) which are now in process being dealt by the concerned authorities in Zanzibar.

  Prof. Rai mentioned priority areas of the State University of Zanzibar some of them being Oceanography and Natural Resources, Environmental Sciences, Mobile Computing, Oil and Gas, Medicine and Engineering saying that it will be prudent if these priorities get inspiration from highly developed stakeholders like Turkey.

  He explained that SUZA needs to strengthen the capacity building of its academic staff in masters and doctoral levels so as to be able to stand by its own and eventually develop its goals as defined by the university mission and vision.

  The delegation which also included Mr. Mustafa Efe who is the Advisor to YTB President vowed to help SUZA in building its capacity.

  Before visiting SUZA the delegation visited Tanzania mainland where it met up with the Turkish Tanzanian alumni including Honourable Hussein Mwinyi, the Minister of Defense and National Service. 

  Also while in Zanzibar it was expected to meet Dr. Ali Mohamed Shein, the President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council as well as the management of the Ministry of Education and Vocational Training and the Zanzibaris who had studied in Turkey.

  0 0

  Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mheshimiwa Balozi Benedict Mashiba wakati alipokutana naye Ofisini kwake Magogoni jijini Dar es salaam leo Jumatano,( Agosti 16, 2017).

  …………………………………………
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mheshimiwa Balozi Benedict Mashiba, ambapo amemtaka kuimarisha mahusiano baina ya nchi zote mbili.

  Amekutana na Balozi Mashiba leo (Jumatano, Agosti 16, 2017) katika makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam, ambapo amemtaka balozi huyo kuhakikisha anaboresha shughuli za Kidiplomasia kati ya Tanzania na Malawi.

  Pia Waziri Mkuu amemtaka Balozi huyo kuhakikisha anatangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, ukiwemo mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama pamoja na fursa za uwekezaji zilizopo nchini hususan katika sekta ya viwanda.

  Waziri Mkuu amesema licha ya kutangaza fursa za uwekezaji na vivutio vya utalii pia amemtaka kuboresha biashara baina ya Tanzania na Malawi kwa kutumia meli mbili za mizigo za Mv. Ruvuma na Mv. Njombe alizozizindua hivi karibuni.

  Hata hivyo, Waziri Mkuu amemtaka Balozi Mashiba kukutana na kufanya mazungumzo na Watanzania waishio nchini Malawi na kuwasisiza kuishi kwa kuzingatia sheria za nchi husika. Pia kuwaunganisha pamoja na kuwashauri waje kuwekeza nchini.

  Kwa upande wake Balozi Mashiba amesema atahakikisha anayafanyia kazi maelekezo yote aliyopewa ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama pamoja na kuboresha ushirikiano baina ya Tanzania na Malawi.

  0 0


  Raymond Msenga ambaye ni mchekeshaji wa mitandaoni akikabidhiwa simu na meneja wa masoko mtandaoni Chen Bo simu mpya aina ya TECNO SPARK.
  Afisa mahusiano wa TECNO Mobile Eric Mkomoya (wa pili kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kampeni ya WashaCheche ns kumkabidhi Raymond Msenga (Jay Mond) wa pili kutoka kushoto zawadi ya simu toleo lao jipya kabisa la simu aina ya TECNO SPARK, kutokana na kampeni iliyopewa kuifanya wiki mbili zilizopita.


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  KAMPUNI ya simu za TECNO imemzawadia zawadi ya simu mchekeshaji Raymond Msenga maarufu kama JayMondy ikiwa ni toleo lao jipya kabisa la simu aina ya TECNO SPARK, kutokana na kampeni aliyopewa kuifanya wiki mbili zilizopita.

  Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Afisa Mahusiano wa kampuni hiyo Eric Mkomoya alisema “nia na madhumuni ya kampuni yetu ni kuinua vipaji vya vijana wa kitanzania kupitia simu hii mpya, vijana wanaotaka kufanikiwa wanapitia vikwazo vingi, ila Tecno inataka kuwasaidia kupitia washa cheche.”

  Raymond Msenga ambaye ni mchekeshaji wa mitandaoni aliomba simu kutoka Tecno Mobile kupitia video zake ili aweze kurekodi kwa ubora mzuri. Tecno Mobile walisikia kilio chake na kumpa zawadi ya simu mwaka mzima kwa kila toleo.

  “Nimefurahi kupata zawadi ya simu hii, na kikubwa na ni nafasi ya kupata mfululizo wa matoleo yote mapya ya simu zao, nawasihii vijana wenzangu wenye vipaji wawashe cheche zao na wanaweza kupata msaada kutoka Tecno Mobile.” Alisema Raymond Msenga maarufu kama Jaymond.

  Meneja wa masoko mitandaoni wa TECNO, Kelvin Boniface alisema “Namna ya kushiriki katika kampeni hii ni rahisi, Upload video au picha Kwenye mitandao ya kijamii ukitumia hashtag #WashaCheche bila kusahau kutuTag “Tecno Mobile Tanzania kwenye mitandao yetu ya kijamii ya twitter, Facebook na Instagram” alisema

  Kampeni hii itasukumwa na simu yao mpya aina ya TECNO SPARK (TECNO CHECHE) ili kuhamasisha vijana kutumia vipaji vyao kujiletea maendeleo na kujikwamua kimaisha.

  Afisa mahusiano wa TECNO Mobile Eric Mkomoya akiwaonyesha waandishi wa habari toleo jipya la simu zao kabla ya kumkabidhi Raymond Msenga ambaye ni mchekeshaji wa mitandaoni.

  0 0


  ¨       MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUMFANYIA UKATILI MTOTO WAKE WA KUMPAKA MAVI YA MBUZI KWENYE MAJERAHA ALIYOUNGUA NA  MOTO WILAYANI NYAMAGANA.

  KWAMBA TAREHE 15.08.2017 MAJIRA YA SAA 16:30HRS JIONI KATIKA MTAA WA CHAKECHAKE – MKUYUNI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, SOSPETER RAJABU MIAKA 42, MVUVI NA MKAZI WA MTAA WA CHAKECHAKE – MKUYUNI, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUMFANYIA UKATILI MTOTO WAKE AITWAYE NEEMA SOSPETER MIAKA 10, MWANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA, WA KUMPAKA MAVI YA MBUZI KWENYE MAJERAHA YA MOTO ALIYOUNGUA MAENEO YA MAPAJA YA MIGUU YOTE MIWILI KWA MUDA WA WIKI MBILI NA KUPELEKEA MAJERUHI KUWA NA HALI MBAYA KIAFYA, KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA.

  INADAIWA KUWA TUKIO HILO LA AJALI YA MOTO DHIDI YA MTOTO LILITOKEA TAREHE 04.08.2017 MAJIRA YA SAA 19:45HRS USIKU, KATIKA MTAA WA KITANGIRI WILAYANI ILEMELA AMBAPO MAJERUHI ALIKUWA AKIISHI NA MAMA YAKE KWANI WAZAZI WAKE WALITENGANA KWA MUDA MREFU . INASEMEKANA AJALI HIYO YA MOTO ILITOKEA BAADA YA MAJERUHI KUMWAGIKIWA NA MAFUTA YA TAA PINDI ALIPOKUWA AKIWEKA KWENYE TAA YA KIBATARI NDIPO ALIPOWASHA MOTO NA NJITI YA KIBIRITI MOTO ULILIPUKA NA KUMUUNGUZA KWENYE MAENEO HAYO. 

  INASEMEKANA KUWA BAADA YA MAMA WA MWENYE MTOTO KUKOSA FEDHA ZA MATIBABU ALIAMUA KUMPELEKA MTOTO KWA BABA YAKE MTAA WA CHAKECHAKE – MKUYUNI ALIPOKUA AKIISHI NA MKE MWINGINE ILI AMSAIDIE MTOTO APATE MATIBABU, LAKINI INADAIWA KUWA BAADA YA MTOTO KUFIKISHWA KWA BABA YAKE HAKUPELEKWA HOSPITALI BADALA YAKE ALIKUWA AKIPAKWA MAVI YA MBUZI NA KUPELEKEA HALI YAKE KUZIDI KUWA MBAYA.

  WANANCHI WALITOA TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, AMBAPO ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI MAENEO HAYO NA KUFANIKIWA KUMKUTA MTOTO  AKIWA KWENYE HALI NGUMU.  ASKARI KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI WALIMCHUKUA MTOTO HUYO NA KUMKIMBIZA HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU TOURE KUPATIWA MATIBABU HUKU BABA WA MTOTO SOSPETER RAJABU AKITIWA NGUVUNI.

  POLISI WAPO KWENYE UPELELEZI NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA DHIDI YA UKATILI ALIYOKUWA AKIMTENDEA MWANAE, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI. 

  MAJERUHI AMELAZWA HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU TOURE AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI.
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI WA MKOA WA MWANZA, KUWA PALE AMBAPO KUNATOKEA MTOTO AU MTU YEYOTE ANAPATA MAJERAHA AU KUUNGUA NI VIZURI WAKAWAONE MADAKTARI KATIKA HOSPITALI AMBAPO WANAWEZA KUPATA HUDUMA BORA NA STAHIKI ZA MATIBABU KULIKO KUTUMIA NJIA ZA KIENYEJI ZISIZOFAA AMBAZO HAZINA UBORA/USAHIHI, KWANI KUFUATA NJIA AMBAZO SI SAHIHI NA BORA KUNAWEZA KUPELEKEA KIFO KWA MGONJWA.
  IMETOLEWA NA;
  DCP: AHMED MSANGI
  KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.


  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimkaribisha Balozi wa Qatar hapa nchini Abdulla Jassim Al-Maadad,  ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo
   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimsalimia msaidizi wa  Balozi wa Qatar hapa nchini Abdulla Jassim Al-Maadad,  ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam
    Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwa na Balozi wa Qatar hapa nchini Abdulla Jassim Al-Maadad,  ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam
    Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi wa Qatar hapa nchini Abdulla Jassim Al-Maadad,  ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam        
  MAZUNGUMZO YAKIENDELEA
  🔻
   ZAWADI YA NGAO
  🔻
    Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akikabidhiwa zawadi ya ngao na Balozi wa Qatar hapa nchini Abdulla Jassim Al-Maadad, baada ya mazungumzo yao,  ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam
   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimshukuru Balozi wa Qatar hapa nchini Abdulla Jassim Al-Maadad, wakati akipokea zawadi hiyo
   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimsindikiza Balozi wa Qatar hapa nchini Abdulla Jassim Al-Maadad, baada ya mazungumzo yao,  ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam
   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimsindikiza Balozi wa Qatar hapa nchini Abdulla Jassim Al-Maadad, baada ya mazungumzo yao,  ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam
   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimsindikiza Balozi wa Qatar hapa nchini Abdulla Jassim Al-Maadad, baada ya mazungumzo yao,  ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa wa Itifaki katika Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Makao Makuu ya CCM, Frank Uhahula
   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimsindikiza hadi nje, Balozi wa Qatar hapa nchini Abdulla Jassim Al-Maadad, baada ya mazungumzo yao,  ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam
   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiagana na Balozi wa Qatar hapa nchini Abdulla Jassim Al-Maadad, baada ya mazungumzo yao,  ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam
   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiagana na Balozi wa Qatar hapa nchini Abdulla Jassim Al-Maadad, baada ya mazungumzo yao,  ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO. PICHA ZAIDI/>BOFYA HAPA

  0 0

   WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Jumatano, Agosti 16, 2017) kuelekea nchini Cuba kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la kudumisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

  Akiwa nchini Cuba Waziri Mkuu anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi waandamizi wa Cuba kwa lengo la kukuza ushirikiano katika sekta za afya, elimu utalii na Kilimo.

  Aidha, nchi ya Cuba ni mojawapo ya nchi zenye ushirikano wa muda mrefu na Tanzania Kisiasa, Kijamii na Kiuchumi.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATANO, AGOSTI 16, 2017.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke ,Felex Jackson katika Uwanja wa Ndege wa Julias Nyerere Dar es salaam leo August,16/2017 akiwa anaelekea Nchini Cuba Kwa ziara ya kikazi.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
   

  0 0

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akipokea moja ya kitabu chenye kumbukumbu ya historia ya Afrika ikiwemo Tanzania kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa UNESCO nchini Tanzania Bibi. Zulmira Rodrigues wakati wa kikao na watendaji wa Wizara pamoja na UNESCO kujadili mashirikiano yaliyopo katika kuhifadhi historia ya nchi leo Jijini Dar es Salaam .

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa UNESCO nchini Tanzania Bibi. Zulmira Rodrigues wakati wa kikao na watendaji wa Wizara pamoja na UNESCO kujadili mashirikiano yaliyopo katika kuhifadhi historia ya nchi leo Jijini Dar es Salaam
  Mwakilishi Mkazi wa UNESCO nchini Tanzania Bibi. Zulmira Rodrigues (wapili kushoto) akizungumza wakati wa kikao na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) pamoja na watendaji wa Wizara kujadili mashirikiano yaliyopo katika kuhifadhi historia ya nchi leo Jijini Dar es Salaam
  Mkurugenzi Msaidizi Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Benard Lubogo (katikati) akichangia mada wakati wa kikao na watendaji kutoka UNESCO kujadili mashirikiano yaliyopo katika kuhifadhi historia ya nchi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bibi. Martha Swai 


  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara yake na watendaji kutoka UNESCO baada ya kikao na watendaji hao kujadili mashirikiano yaliyopo katika kuhifadhi historia ya nchi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa UNESCO nchini Tanzania Bibi. Zulmira Rodrigues na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bibi. Martha Swai

  Picha na: Genofeva Matemu -WHUSM

  0 0


  Na Agness Francis, Blogu ya jamii.

  Kampuni ya  Startimes Tanzania imezindua uoneshaji wa ligi ya  Bundesliga  mwaka 2017/2018 ambayo itarushwa mubashara kupitia  vipindi vya startimes  kwa wapenzi wa soka hapa  nchini

  Uzinduzi huo umefanyika  leo jijini Dar es Salaam lengo ni kuwa  kuwafahamisha wapenzi  wa mpira kununua ving’amuzi na   kujiunga na vifurushi  ili kuburudika na mechi hizo ambazo ligi hiyo itakuwa ikiionyeshwa moja kwa moja na startimes.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif  amesema kuwa ipo fursa kwa waandishi wa habari za michezo  kufanya mashindano ya  uandishi wa mechi  hiyo na kwa mshindi  wa shindano hilo atagharamiwa safari zote za ti ya ndege  kwenda moja kwa moja Ujerumani.

  Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Suluhu nae amesema wana mahusiano mazuri na bundesliga  kwa kuwa na mkataba wa miaka mitano na hadi sasa ni mwaka wa tatu kuonyesha ligi hiyo.

  Meneja Uwendeshaji  Startimes, Gaspa Ngowi  amesema kuwa  huduma mpya ya  malipo kwa wale wenye hali ya chini  wanaweza  kulipia siku moja king’amuzi  cha Startimes  kwa gharama ya bei ya shilingi 1000, ambapo kwa wiki utalipia elfu 4000.

  Hata hivyo mhariri mkuu wa gazeti la Championi , Salehe Jembe amesema  kuwa  ligi ya Bundesliga  ina ubora na kuburudisha zaidi kulinga na  ligi zingine duniani  kwa kuwa na wachezaji bora 

  Nae Meneja mahusiano wa Tabibu TV, Kaki Mwaigomole ametoa shukrani kwa kampuni ya  startimes kwa kuwapa fursa ya kuweza kuonyesha mubashara  mtanange huo ambao utaanza rasmi tarehe  18-27 Agosti mwaka huu
  Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa kuonesha ligi ya Bundesliga kwa msimu wa mwaka 2017/18 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura Hanif(wa pili kutoka kushoto) akikata utepe pamoja na wadau mbalimbali wa mpira hapa nchini. 
  Baadhi ya wafanyakazi wa StarTimes Tanzania wakfuatilia yaliyokuwa yanajiri kwenye uzinduzi huo
  Mtangazaji wa kipindi cha michezo Radio Clouds 'Sports Extra' na Clouds Tv 'Sports Bar', Shaffih Dauda akitoa uchambuzi pamoja na kubashiri ligi hiyo itakavyokuwa kwenye msimu wa mwaka 2017/2018.
   Mhariri mkuu wa gazeti la Championi, Salehe Jembe akitolea ufafanuzi kuhusu ligi ya Bundesliga ya nchini Ujerumani itakavyokuwa kwa msimu wa mwaka 2017/18 kwenye uzinduzi wa kuonesha ligi hiyo kwa mwaka wa tatu kupitia kwenye king’amuzi cha Startames.
   Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Suluhu akizungumza kuhusu kampuni hiyo wanavyoshirikiana kuonesha ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga
  Picha ya Pamoja 

  0 0


  0 0

  Katibu Tawala wa Wilaya, Shadrack Kengese akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha shughuli za kilimo na elimu kwa wananchi.
  Ofisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika katika halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Godwin Everygist akifafanua jambo kwa wananchi wakati wa uhamasishaji wa shughuli za kilimo.
  Ofisa Elimu Sekondari halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Cleophas akihamasisha wananchi kushiriki shughuli za elimu.
  Ofisa Elimu Msingi halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Moshi Balele akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji elimu na kilimo kwa wananchi.
  Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kijiji cha Malwilo kata ya Somagedi wilayani Kishapu.

  …………………….

  Na Mwandishi Maalumu, Kishapu

  Halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imezindua kampeni kabambe ya kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za kilimo na elimu.

  Imezindua kampeni hiyo katika kijiji cha Malwilo kata ya Somagedi ambayo itashirikisha wananchi katika vijiji vyote vya wilaya hiyo ili kuinua hali za wananchi kiuchumi na kielimu.

  Akizindua kampeni hiyo wa niaba ya Mkuu wilaya hiyo, Nyabaganga Taraba, Katibu Tawala wa Wilaya, Shadrack Kengese alisema kila mwananchi ana wajibu wa kutumia fursa ya ardhi kujiletea maendeleo.

  Kengese alimiza wananchi kulima mazao yanayostahimili hali ya ukame kutokana na hali ya hewa ya wilaya hiyo ambayo hupata mvua chini ya wastani unaotakiwa.

  Alisema halmashauri ya wilaya hiyo kwa kutambua hali ya hewa ilitunga sheria ndogo mwaka 2008 ya kilimo cha mazao yanayostahimili ukame na hifadhi ya chakula cha kutosha kwa kaya.

  “Sheria hii imemtaka kila mkazi wa wilaya ya Kishapu kulima mazao yanayostahimili ukame ikiwa ni pamoja na kuhifadhi chakula cha kutosheleza mahitaji ya familia angalau miaka miwili au zaidi.

  “Aidha sheria hii ilitungwa ili kutuhakikishia usalama wa chakula muda wote hivyo ni rai yangu kuwa wananchi wote tutashiriki katika shughuli za kilimo kwa kulima mazao yanayostahimili ukame,” alisisitiza.

  Aidha, Kengese aliongeza kuwa sheria imetaja adhabu kwa mtu atakayekadi adhabu yake ni kifungo kisichozi miezi 12 au kulipa faini isiyozidi sh. laki tatu au adhabu zote mbili.

  Pia aliwataka maofisa kilimo waisimamie sheria hiyo kikamilifu na kuwa yeyote atakayekaidi afikishwe kwenye vyombo vya sheria kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anaondoka nchini leo kwenda Pretoria Africa ya Kusini ambako atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika utakaofanyika Pretoria, Afrika Kusini tarehe 19 na 20 Agosti, 2017. 

  Mkutano huo utapokea na kujadili ajenda mbalimbali ikiwemo uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa SADC na Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama; Hali ya Michango mbalimbali ya Nchi Wanachama na Kupokea taarifa ya Mwenyekiti anayeondoka wa SADC Organ.  


  Pia Mkutano utapokea taarifa ya Katibu Mtendaji wa SADC; Kupitia hali ya kiuchumi katika Kanda ya SADC; Kuwasilisha Kaulimbiu ya Mkutano wa SADC; Taarifa kuhusu Mfuko wa Maendeleo wa SADC; Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Viwanda; Kuwezesha Chuo cha Elimu ya Sayansi na Teknolojia; Maombi ya Serikali ya Comoro na Serikali ya Burundi kujiunga na SADC; Utekelezaji wa Mabadiliko ya Kitaasisi ya Umoja wa Afrika na Mkutano wa Mshikamano kati ya SADC na Saharawi ya Magharibi. 

  Mkutano huo utatanguliwa na Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC Double Troika Summit) tarehe 18 Agosti, 2017 ambao Tanzania itakabidhi nafasi ya  uenyekiti kwa mwenyekiti mpya. Double Troika inahusisha nchi wanachama sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji. Katika mkutano huo Mfalme Mswati III wa Swaziland atakuwa ndiye Mwenyekiti. Ajenda kuu katika Mkutano huu ni kupokea na kujadili taarifa kuhusu hali ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama katika Kanda na hasa nchini DR Congo na Lesotho.

  Makamu wa Rais amefuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa AfrikaMashariki, Mhe. Balozi Dkt Augustine Mahiga, Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijange, Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Ashatu Kijaji na watendaji wengine waandamizi Serikalini

  Makamu wa Rais na ujumbe wake anatarajia kurudi nchini Agosti 21, 2017.

  Imetolewa na
  Ofisi ya Makamu wa Rais
  Dar es salaam
  17/8/2017
   
   
   Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke ,Felex Jackson katika Uwanja wa Ndege wa Julias Nyerere Dar es salaam leo Agosti ,17/2017 akielekea Nchini  Pretoria Africa ya Kusini ambako atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika utakaofanyika Pretoria, Afrika Kusini tarehe 19 na 20 Agosti, 2017.
   Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza ambo na Mkuu wa Wilaya ya Temeke ,Felex Jackson katika Uwanja wa Ndege wa Julias Nyerere Dar es salaam leo Agosti ,17/2017 akielekea Nchini  Pretoria Africa ya Kusini ambako atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika utakaofanyika Pretoria, Afrika Kusini tarehe 19 na 20 Agosti, 2017.
   

  0 0

   Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akisalimiana na viongozi wa chama mkoa wa kaskazini unguja akiwa katika ziara ya kikazi  visiwani pemba.
   Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akipokelewa na viongozi ofisi za CCM wilaya ya micheweni  katika ziara ya kikazi  visiwani pemba.
   vijana wakiburudisha kwa kupiga dufu wakati wa mapokezi ya  Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shakaalipowasili ofisi za CCM wilaya ya micheweni  katika ziara ya kikazi  visiwani pemba.
   Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka wa pili kulia pamoja na mkuu wa idara ya Uchumi uwezeshwaji na fedha (UVCCM)Dorice Obedi wakisain Vitabu vya wageni walipowasili wasili katika ofisi za CCM Wilaya ya micheweni ziara ya kikazi  visiwani pemba.
   Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza jambo pamoja na mwl,Ally khatibu Hassan Mkuu wa shule ya msingi Michekweni wakati akikagua jengo la Ujenzi wa maktaba pamoja na madarasa ya Shule ya Msingi Micheweni. wakati wa ziara ya kikazi  visiwani pemba.
   Wanafunzi wa Darasa la kwanza Issa Haji (wa kwanza kulia) pamoja na Abdulwahid abdallah wakisalimiana na  Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka wakati  alipokwenda kukagua jengo la Ujenzi wa maktaba pamoja na madarasa ya Shule ya Msingi Micheweni.
    Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akimfunga Vifungo vya shati Mwanafunzi wa Darasa la kwanza Shule ya Msingi Micheweni Abdulwahid abdallah wakati  alipokwenda kukagua jengo la Ujenzi wa maktaba pamoja na madarasa ya Shule ya Msingi Micheweni.
   Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akiwa Shumba mjini akikagua sehemu itakayo jengwa jeti
   Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akigagua ujenzi wa ofisi ya ccm tawi la njuguni inayojengwa na mwakilishi Jimbo
   Afisa mipango wa halmashauri ya konde (pili kushoto)akitolea ufafanuzi juu ya ujenzi wa soko la mboga mboga la samaki pamoja na mbogamboga kwa Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akiwa katika ziara ya kikazi  visiwani pemba.
    Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza na Viongozi na wanachama wa CCM na Jumuiya zake Tawi la kuiyu Mbuyuni akiwa katika Ziara ya Kikazi Mkoa wa Kaskazini pemba .
   Wanachama Wa CCM na Jumuiya zake wakishangilia katika mkutano wa ndani uliofanyika Skuli ya Michekweni.Mkoa wa Kaskazini Pemba.
   Ustadh,Abdul mohammed akifungua kwa Kusoma quran Tukufu katika ukumbi wa Skuli ya Michekweni  Mkoa wa Kaskazini Pemba.
    Mkuu wa Idara ya Uchumi Uwezeshaji na Fedha (UVCCM) ndg:Dorice Obed akizungumza katika Mkutano wa ndani  wa Wanachama na Viongozi wa CCM na Jumuiya zake Wilaya ya Michekweni Mkoa wa Kaskazin pemba.
   Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mhe:Abeid Juma Ally akizungumza
    Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza katika Mkutano wa ndani  wa Wanachama na Viongozi wa CCM na Jumuiya zake Wilaya ya Michekweni Mkoa wa Kaskazin pemba.
   Wanachama na Viongozi wa CCM na Jumuiya zake Wilaya ya Michekweni wakifuatilia kwa Umakini mkutano huo.
   Mkuu wa Idara ya Uchumi Uwezeshaji na Fedha ndg:Dorice Obed akicheza nyimbo ya CCM pamoja na wanachama na Viongozi wa CCM na Jumuiya zake Wilaya ya MichekweniMkoa wa Kaskazin Pemba

  ''Shaka ni kijana jasiri mwenye kujenga hoja na kushambulia wapinzani kwa Vielelezo hamofii Seif,Sumaye Lowasa na wengine,wala kingunge,anwajibu kwa ushahidi na Vielelezo''Alisema Dady faki Dady msaidizi wa Rais SIASA Pemba wakati akizungumza katika mkutano wa ndani uliofanyika Skuli ya Michekweni.Mkoa wa Kaskazini Pemba.(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)

  ...................................................................................................................................................................
  Na Mathias Canal, Kaskazini Pemba

  Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema kuwa Jukumu la kuleta maendeleo ya kiuchumi katika jamii ni la kila mwananchi sio jukumu la serikali pekee.

  UVCCM imesema kuwa jukumu la serikali ni kuwaonyesha wananchi fursa zilipo na namna bora ya kuzichanganua ikiwa ni pamoja na kufanya kazi ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla wake sambamba na kuwezeshwa kupata mikopo katika vikundi vyao vya ujasiriamali.

  Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka leo Agosti 16, 2017 alipokuwa akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

  Alisema kuwa vijana ni nguvu kazi ya Taifa hivyo wanapaswa kutumia nguvu zao vizuri kwa kufanya kazi ili kujikwamua kiuchumi katika familia zao badala ya kukaa maskani kujadili mambo yasiyokuwa na tija kwao.

  Aliongeza kuwa UVCCM inaunga mkono vijana kukaa maskani kwa maslahi mapana ya mjadala wa Maendeleo yatakayopelekea kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kujiunga katika vikundi mbalimbali vya ujasiriamali.

  Shaka alisema kuwa  Kila mwananchi kwa nafasi yake anatakiwa kuwajibika kwa nafasi aliyonayo ndani ya chama ama serikali kwani wananchi wanataka maendeleo ya uchumi wao sio ahadi hewa za majukwaani.

  Aidha, alisema kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ipo pamoja na watanzania wote ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ama wale ambao sio wanachama wa vyama vya siasa kwani mchakato wa maendeleo hauangalii itikadi za vyama vya siasa.

  Alisema wananchi wanatakiwa kutumia Tunu ya amani, umoja na mshikamano uliopo nchini kufanya shughuli za maendeleo na kujiepusha na maneno ambayo yataleta chokochoko za kuondoa mshikamano katika jamii.

  Shaka alisema kuwa vijana wanatakiwa kujiajiri katika ujasiriamali kwa kuchukua hatua za makusudi za kujiajiri kwani kusubiri ajira za serikali zitawachelewesha na pengine kufikia hatua ya uzee pasina kuajiriwa kutokana na uchache wa ajira serikalini na wingi wa vijana.

  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana UVCCM ameanza ziara ya kikazi jana Agosti 15, 2017 visiwani Pemba ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya ushindi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020.

  0 0  Mkuu wa Wilaya ya Mbeya,William Paul Ntinika akitoa hotuba ya uzinduzi wa huduma mpya ya mawasiliano ya 4G inayotolewa na kampuni ya simu Tanzania ya TTCL kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu Tanzania (TTCL)Waziri Kindamba akielezea umuhimu ya kuzindua mfumo mpya wa mawasiliano wa 4G kwa Mkoa wa Mbeya katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika Ofisi za TTCL mkoa wa Mbeya.Mkuu wa Wilaya ya Mbeya William Paul Ntinika akisaidiana na Afisa Mtendaji mkuu wa TTCL Waziri Kindamba kutoa kitambaa kuashiria kuzindua huduma ya 4G mkoani Mbeya.Afisa mtendaji mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba akimkabidhi zawadi Mkuu wa Wilaya ya Mbeya William Paul Ntinika baada ya kuzindua huduma ya 4G LTE mkoani MbeyaMkuu wa Wilaya ya Mbeya William Paul Ntinika akisaidiana na Afisa Mtendaji mkuu wa TTCL Waziri Kindamba kuonesha bango kuashiria kuzindua huduma ya 4G mkoani Mbeya.Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Mbeya pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi wa 4G LTE mkoani Mbeya.Baadhi ya Wageni waalikwa na wateja wa huduma ya simu ya TTCL wakifuatilia uzinduzi wa huduma ya 4G LTEBaadhi ya Watumishi wa Kampuni ya Simu ya TTCL Mkoa wa Mbeya wakiwa kwenye uzinduzi wa huduma ya 4G LTE mkoani MbeyaMkuu wa Wilaya ya Mbeya William Paul Ntinika akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Kapuni ya Simu ya TTCL Mkoa wa Mbeya,Afisa wa TTCL akitoa maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na TTCL ikiwemo huduma ya TTCL PESA iliyozinduliwa hivi karibuni.
  KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imezindua huduma mpya ya mawasiliano ya 4G LTE pamoja na kutambulisha huduma nyingine ya TTCL PESA.

  Hata hivyo katika uzinduzi huo imeelezwa kuwa mawasiliano bora yanahitajika ili kuendelea kuimarisha shughuli za kiuchumi mkoani Mbeya ikiwa ni pamoja na kuongeza urahisi wa upatikanaji wa taarifa za masoko na bei nzuri kwa wazalishaji na Wakulima.

  Hayo yalielezwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla wakati akizindua huduma mpya ya kampuni ya Simu ya TTCL ya 4G LTE katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntika katika ofisi za Kampuni hiyo zilizopo jijini Mbeya.

  Alisema mawasiliano bora yanamchango mkubwa katika ukuaji wa sekta za Elimu, Afya, Miundombinu, Biashara, utalii, huduma za jamii na sekta zingine mtambuka hivyo kitendo cha TTCL kuibuka upya kutasaidia kuchochea maendeleo katika Mkoa wa Mbeya na Taifa kwa ujumla.

  Aliongeza kuwa mbali na Mawasiliano kusaidia kukuza uchumi pia Wafanyakazi wa Sekta binafsi na sekta za umma wanahitaji mawasiliano bora ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na utekelezaji wa majukumu yao katika maeneo yao ya kazi.

  Aidha alitoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya kuchangamkia fursa za kibiashara zinazotolewa na TTCL kama vile kuwa wakala wa kuuza vocha, Laini na kuwa Wakala wa huduma mpya ya kifedha ya TTCL Pesa kwani kufanya hivyo kutasaidia kuongeza ajira na vipato vyao.

  Hata hivyo Makalla alitoa wito kwa Kampuni ya TTCL kupanua wigo wa utoaji huduma kwa kuhakikisha huduma hiyo inasambaa kote nchini hususani vijijini ambako watumiaji ni wengi ambao pia wanahitaji huduma zenye gharama nafuu kama zinazotolewa na kampuni ya TTCL.

  Awali Afisa mtendaji mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba katika hotuba yake alisema Kampuni ya TTCL ni kampuni ya kizalendo inayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 hivyo inatekeleza mpango mkakati wa biashara wa miaka mitatu kuanzia 2016 hadi 2018 unaolenga kuboresha na kutoa huduma mpya katika soko la mawasiliano nchini.

  Kindamba alisema malengo mengine ya mkakati huo ni pamoja na kuongeza tija na uwajibikaji ili kutoa huduma bora kwa wateja wa mawasiliano ambapo hivi sasa wameweza kufanya mabadiliko mengi yaliyowezesha Kampuni hiyo kurejea kwa kishindo katika soko la mawasiliano.

  Alisema mbali na kuzindua huduma mpya ya mawasiliano ya 4GLTE pia ni kutambulisha huduma mpya ya kifedha kwa njia ya mtandao ijulikanayo kama TTCL Pesa ambayo ilizinduliwa Julai mwaka huu na Makam wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu.

  Alisema huduma hiyo ya kifedha itawezesha wananchi kupata huduma mbalimbali kama kutuma fedha, kulipia Ankara za maji, umeme, ving’amuzi na kununua vifurushi vya TTCL huku huduma zingine zikiendelea kuongezwa ikiwemo kulipia kodi TRA.

  Aliongeza kuwa lengo la kuzindua huduma hizo mkoani Mbeya linatokana na kuwa ni Mkoa wenye kibiashara na utajiri mkubwa wa idadi ya watu na uwepo wa shughuli za kiuchumi zinazogusa sekta nyingi na kuwa kitovu cha kilimo cha kibiashara, tegemeo la chakula nchini na kuwa kituo kikubwa cha kibiashara kutokana na kupakana na Nchi jirani za Malawi na Zambia hivyo TTCL kutumia fursa hiyo ya kiuchumi.

  0 0

  Na Vero Ignatus, Arusha. 

  Mwanamke mmoja mkazi wa Levolosi Arusha bi Rehema Juma Kishena (40) anawaomba watanzania wenye mapenzi mema kumsaidia kupata fedha ya matibabu kutokana na tatizo la uvimbe linalomsumbua katika shavu lake la kulia ambalo limezunguka taktibani robo tatu ya uso wake . 

  Mwanamke huyo ambae ni mama wa watoto (4) amesema kuwa tatizo hilo lilimuanza kwa jino kuumua ,akachukua hatua ya kwenda hospitalini kuling’oa , mwaka 2001 uvimbe ulijitokeza katika jino alilong’olewa, na kupelekea kufanyiwa upasuaji, baada ya miaka mitatu uvimbe ulirudi tena kama awali. ‘’Jino lilikuwa linaniuma nikaenda hospitalini kuling’oa, ndipo ukaanza uvimbe kwenye jino nililongoa nikarudi hospitalini wakaniambia nifanyiwe upasuaji ili kuondoa uvimbe ,baada ya miaka mitatu tatizo hilo likajirudia kama lilivyokuwa mwanzo “alisema Bi. Rehema.

  Amesema kuwa kwa sasa hana msaada wowote kwani wazazi wake ni wazee, hawana mwezo wa kumsaidia,yeye mwenyewe hana mume kwani alimkimbia wati alipoona tatizo linaendelea kuwa kubwa. “Nawaombeni msaada ili niweze kujitibu kwani hali yangu kama mnavyoiona nipo kwa dada yangu hapa ,sina msaada wowote” alisema Bi. Rehema. 

  Kwa upande wake dada yake ( Rehema )Aziza Bakari Muyai amewaomba watanzania kushirikiana nae katika kumsaidia mdogo wake ili aweze kupatiwa matibabu kwani hali yake inazidi kuwa mbaya kadri siku zinavyozidi kwenda. Ameomba kwa yeyote aliyepo tayari kumsaidia atumie mawasiliano kwa namba 0653179373.
   Bi. Rehema Juma Kishena akiwa na mtoto wake Sophia Dastan Mandia pamoja na dada yake bi Aziza Bakari Muyai nyumbani kwake Levolosi Mkoani Arusha. 


  0 0

  KAMPENI ya kuhakikisha vijiji vyote nchini vinapatiwa umeme, imeendelea jana (Agosti 16, 2017), mkoani Ruvuma, ambapo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, amezindua mradi huo kwenye kijiji cha Litapaswi, wilaya ya Songea vijijini mkoani Ruvuma, kwa kugawa vifaa vijulikanavyo kama umeme tayari (Ready Board) kwa wanakijiji.

  Katika hafla ya uzinduzi huo, uliofanywa kwa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Watu Wenye Ulemavu), Mheshimiwa Jenista Mhagama, Wanakijiji walipatiwa vifaa hivyo vinavyowezesha umeme kuwaka mara moja bila ya kuhitaji (mtandao wa waya kwenye nyumba- (Wiring).

  “Kifaa hiki ni maalum kwa matumizi ya nyumba isiyozidi vyumba viwili na mwanakijiji analipia shilingi elfu 36,000 tu kupata kifaa hiki.” Amefafanua Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji ambaye anafuatana na Naibu Waziri kwenye ziara hiyo.

  Hali kadhalika alisema, kifaa hicho kwa sasa kinapatikana kwenye ofisi zote za TANESCO za Mikoa na Wilaya kwenye mikoa ambayop tayari mradi huo umezinduliwa.Alisema, tayari Naibu Waziri amekwishazindua mradi kama huo kwenye mikoa yote ya Tanzania bara isipokuwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, na Katavi.

  “Jambo la kufurahisha sana ni kwamba mradi huu wa REA III, unafadhiliwa na Serikali yetu kupitia Wakala wa Nishati Vijijini na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO)” alifafanua Bi. Muhaji.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe.Jenista Mhagama, akikabidhi kifaa kijulikanacho kama umeme tayari(Ready Board) kikichobuniwa na Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), kwa mwanakijiji wa kijiji cha Litapwasi, Peramiho, Mkoani Ruvuma wakati wa uzinduzi wa mradi wa Usambazaji umeme vijijini unaoratibiwa kwa pamoja na Wakala wa Umeme Vijijini REA na Shirika la Umeem Tanzania , (TANESCO), ambapo uzinduzi huo ni awamu ya tatu. Uzinduzi huo ni mwendelezo wa kazi kama hiyo ulioanzishwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medad Kalemani(aliyeshika vipaaza sauti) kwenye mikoa mbalimbali nchini.  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

  TAARIFA KWA UMMA

  Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngorongoro, kwa kushirikisha Hifadhi ya Taifa Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, inaendesha zoezi la kuondoa mifugo na makazi ndani ya hifadhi ya Taifa Serengeti na kwenye mpaka wa Pori Tengefu Loliondo.

  Zoezi hilo lililoanza tarehe 10  Agosti 2017  litadumu kwa siku kumi na nne na linashirikisha Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ngorongoro, Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Hifadhi ya Taifa Serengeti na Hifadhi ya eneo la Ngorongoro.

  Zoezi hilo linalenga kunusuru uhifadhi ndani ya hifadhi, ndani ya Pori Tengefu Loliondo, na ndani ya mfumo ikolojia wa Serengeti na pia kunusuru utalii katika mfumo ikolojia huo.

  Aidha, hatua hii ya kuondoa makazi na mifugo kutoka katika maeneo ya mipaka ya Pori Tengefu Loliondo kutaongeza uhakika wa kupatikana malisho ya mifugo wakati wa kiangazi kwa kuwa hakutakuwepo na makazi ndani ya Hifadhi na ufugaji holela.

  kimsingi zoezi hili linaendana na wito wa Serikali wa kuondoa mifugo ndani ya maeneo yote yaliyohifadhiwa nchini.

  Katika kutekeleza zoezi hili, Mkuu wa Wilaya  Ngorongoro, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ngorongoro Bwana Rashidi Taka, alitoa maelekezo yafuatayo:

  1. Zoezi litafanyika ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti na kwenye mpaka wa Pori Tengefu Loliondo. Kwa upande wa mpaka wa Pori Tengefu Loliondo zoezi litaanzia kaskazini hadi kusini urefu wa kilometa 90, na upana wake utakuwa kilometa 5. Kwa ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti litafanyika upande wa mashariki kuanzia milima ya Kuka (kaskazini) hadi kigingi na. SNP 9 (kusini); 

  2. Maboma yatakayokutwa ndani ya hifadhi yatateketezwa kwa moto na watu watakaokutwa na mifugo watachukuliwa hatua za kisheria, ikiwemo kupelekwa mahakamani;

  3.  Maboma yaliyoko ndani ya mpaka wa Pori Tengefu Loliondo -  kwenye mpaka na ndani ya kilometa tano - wataondolewa ili warudi vijijini. Eneo hilo litabaki kwa ajili ya malisho na si kwa ajili ya makazi.  Uwepo wa makazi kwenye mpaka wa Hifadhi ya Taifa Serengeti umekuwa kichocheo kikubwa cha mifugo kuingizwa hifadhini.

  Zoezi hili linalenga kuondoa changamoto kubwa ya mifugo kuingizwa Hifadhi ya Taifa Serengeti na kwenye mpaka wa Pori Tengefu Loliondo, kupambana na uvamizi mkubwa uliofanywa na wahamiaji haramu kutoka nchi jirani na kunusuru vyanzo vya maji kutokana na mifugo kulishwa kwenye vyanzo vya maji na hivyo kusababisha vyanzo hivyo kuharibika na kukosekana kwa maji kwa ajili ya mifugo na wanyamapori.

  Hadi sasa zoezi hili la kuondoa mifugo na makazi ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti na kwenye mpaka wa Pori Tengefu Loliondo linaendelea vizuri likihusisha kuchoma moto maboma yote yaliyoachwa na wafugaji walioondoka wakati wa zoezi.

  Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuufahamisha umma kuwa hakuna watu wanaopigwa katika zoezi hili.

  Pia, Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuutaarifu umma kuwa habari zinazosambazwa mitandaoni ni upotoshaji wa ukweli wenye nia ovu ya kujenga chuki dhidi ya Serikali  kwa wananchi wa Loliondo na maeneo yanayopitiwa na zoezi hilo.

  Aidha, Wizara ya Maliasili na Utalii, inapenda kuweka bayana kuwa, taarifa za kupigwa risasi Pormoson Losso mwenye umri wa miaka 23, mkazi wa Ololosokwan zilitolewa tarehe 8 Agosti 2017 na hazihusiani na zoezi tajwa kwani tukio hilo  lilitokea siku tano kabla ya kuanza zoezi la kuondoa mifugo na makazi ndani ya hifadhi wakati zoezi hili lilianza kutekelezwa Jumapili tarehe 13 Agosti 2017.

  Hata hivyo Serikali inawapongeza wananchi wengi miongoni mwa wafugaji kwa kuunga mkono zoezi hili na kwa ushirikiano wanaotoa.
  Serikali inatoa onyo kwa yeyote anayejihusisha na upotoshaji wa ukweli kuhusu zoezi hili lenye nia njema linalolenga kunusuru hifadhi, kuacha mara moja ili kujiepusha na hatua za kisheria zitakazochukuliwa pindi atakapobainika.

  Imetolewa na;

  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

  17/08/2017

  0 0

  Barabara ya lami ya Kia-Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ambayo imeshakabidhiwa kwa Serikali, inaendelea kuwa kwenye kipindi cha matazamio kwa muda wa mwaka mmoja. 

  Mradi huo wa barabara uliokabidhiwa serikali Mei 31 mwaka huu, mkandarasi wake anaendelea na kazi ndogo ndogo za ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua, vivuko na vituo vya basi hasa eneo la Kairo. 

  Meneja wa wakala wa barabara nchini (Tanroads) mkoa wa Manyara, mhandisi Bashiri Rwesingisa aliyasema hayo wakati akisoma taarifa ya mradi huo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi) mhandisi Joseph Nyamhanga alipotembelea eneo hilo. 

  Mhandisi Rwesingisa alisema barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 27 iliyojengwa na kampuni ya China Henan International Cooperation Group (Chico) kwa gharama ya sh32.2 milioni, chini ya usimamizi wa ujenzi mhandisi mshauri M/s LEA International Ltd ya India kwa ushirikiano na kampuni ya DOCH Tanzania Ltd. 

  Alisema kazi zilizotekelezwa ni ujenzi wa kiwango cha lami urefu wa kilometa 27 ikijumuisha Kia hadi Mirerani, Mirerani hadi eneo la uwekezaji la (EPZ), barabara ielekeayo Arusha inayopitia Mbuguni, barabara ya kuingia na kutoka kituo cha mabasi Mirerani na mzunguko kiwanda cha TanzaniteOne. 

  "Ujenzi wa barabara hii umehusisha pia kujenga mifereji ya pembezoni mwa barabara kwenye maeneo ya mji, sehemu za kuvuka mifugo na sehemu za kuvushia huduma muhimu kama waya za simu na umeme," alisema mhandisi Rwesingisa.

  Alisema mradi huo umekuwa na changamoto za migomo ya wafanyakazi, wananchi kugoma kuondoa mali zao ndani ya hifadhi ya barabara. 

  Alisema mipango ya baadaye ni kujenga kilometa 114 barabara kwa kiwango cha lami itakayounganisha eneo la EPZ na mji mdogo wa Orkesumet, makao makuu ya wilaya ya Simanjiro, kama ilivyoainishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015. 

  Akizungumza baada ya kukagua mradi huo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia ujenzi, mhandisi Joseph Nyamhanga alipongeza jitihada zilizofanyika kwa pande zote hadi barabara hiyo ikamalizika. 

  Mhandisi Nyamhanga alisema wakati wanasubiri barabara hiyo kuzinduliwa wakati inaendelea kutumika, watumiaji wanapaswa kufuata masharti ya matumizi ya barabara hiyo ili waitunze. 

  Aliitaka jamii ya eneo hilo ambao kwa muda mrefu walikuwa wanalilia utengenezwaji wa barabara na ndiyo wanufaika wa mradi huo, kuutunza vizuri kwani ni kwa ajili ya faida yao na vizazi vijavyo. 
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi) mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati) akizungumza na viongozi wa wakala wa barabara nchini (Tanroads) Mkoa wa Manyara, alipotembelea eneo la mji mdogo wa Mirerani, (kushoto) ni meneja wa Tanroads Mkoani Manyara, mhandisi Bashiri Rwesingisa
  Meneja wa Tanroads Mkoa wa Manyara, mhandisi Bashiri Rwesingisa (aliyevaa shati la maua) akimwelezea Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi) Joseph Nyamhanga (kushoto kwake) juu ya barabara ya lami ya Kia - Mirerani, ambayo imemalizika inasubiri kufunguliwa.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho na Bushiri 
  Matenda - MAELEZO.

  Serikali imewapiga marufuku mawakala wa forodha wanaogushi nyaraka kwa ajili ya kuingiza kemikali kwani ni kinyume cha Sheria na pia wanaipotezea Serikali mapato. 

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Prof. Samwel Manyele alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uingizaji wa kemikali nchini kutoka nje ya nchi.

  Prof. Manyele amesema kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Kemikali nchini kila anayeingiza kemikali anatakiwa awe amesajiliwa na kupewa hati ya usajili huo vile vile anatakiwa kupata idhini ya wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kabla ya kuagiza mzigo wa kemikali nchini.

  “Natoa onyo kwa mawakala wote wa forodha wasiofuata taratibu zilizowekwa na Serikali hasa wanaogushi nyaraka zenye lengo la kukwepesha Sheria na kukwepa kulipa kodi na tozo mbalimbali za Serikali hivyo watakaokaidi hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,” alisema Prof. Manyele.

  Prof. Manyele amesisitiza kuwa kuanzia Leo Agosti 17, 2017 hakuna mtu atakayeruhusiwa kujishughulisha na shughuli za kemikali bila kuwa na hati ya usajili wa shughuli anayoifanya pia hakuna atakayeruhusiwa kuagiza mizigo ya kemikali bila kuwa na kibali. 

  Aidha, Prof. Manyele alifafanua lugha elekezi zinazotakiwa kutumika katika kuweka lebo za kemikali husika kuwa ni Kiswahili na Kingereza tu hivyo hakuna kemikali itakayoruhusiwa kuingia nchini ikiwa imendikwa kwa lugha tofauti na hizo.Vile vile hakuna mdau atakayeruhusiwa kushiriki tenda za ununuzi kwa ajili ya kuuza kemikali bila kuwa na usajili kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

  Ofisi ya Mkemia Mkuu inaendelea kukabiliana na changamoto za wadau wa kemikali kwa kuendelea kuwaelimisha wadau kuhusiana na matakwa ya Sheria na Kanuni za uingizaji wa kemikali nchini, kuchukua hatua za kisheria kwa wale wanaokiuka matakwa ya Sheria na kanuni zake, kuboresha mifumo, vifaa na sehemu za kufanyia kazi pia wakala inaendelea kufanya kazi kwa masaa 24 katika siku saba za wiki.

older | 1 | .... | 1340 | 1341 | (Page 1342) | 1343 | 1344 | .... | 1897 | newer