Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

Ruth Maeda aibuka Mshindi wa Tatu Mzuka jackpot kwa kujinyakulia milioni 20

$
0
0
 Mshindi wa Jackpot ya Tatu Mzuka iliyofanyika Jumapili hii Bi Ruth Rodgers Maeda akikabidhiwa hundi ya shilingi Milioni 20 aliyojishindia kutoka kwa balozi wa Mchezo wa Tatu Mzuka, Mussa Hussein. Mchezo wa Tatu Mzuka umefanikiwa kujizoelea umaarufu kwa kutoa washindi kila saa. Jackpot hiyo inaendelea jumapili hii kwa mshindi kujishindia shilingi milioni 80.
Mshindi wa Jackpot ya Tatu Mzuka iliyofanyika Jumapili hii Bi Ruth Rodgers Maeda (wa pili kutoa kulia) akishangilia pamoja na familia yake ushindi wake wa zawadi ya shilingi Milioni 20. Mchezo wa Tatu Mzuka umefanikiwa kujizoelea umaarufu kwa kutoa washindi kila saa. Jackpot hiyo inaendelea jumapili hii kwa mshindi kujishindia shilingi milioni 80.

Tigo Yazindua Promosheni Kabambe ya ‘Nunua Simu na Ushinde’

$
0
0
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akizungumza na waandishi wa habari wakati wa  uzinduzi wa promosheni ya 'nunua na ushinde' ambayo inawapa wateja nafasi ya kujishindia pikipiki na TV za kisasa kwa kununua simu mpya aina ya Tecno S1 na Tecno R6 kutoka kwenye maduka ya Tigo nchi nzima. Kushoto ni Meneja mawasiliano wa Tecno, Eric Mkomoya.

Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akfafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya 'nunua na ushinde' ambayo inawapa wateja nafasi ya kujishindia pikipiki na TV za kisasa kwa kununua simu mpya aina ya Tecno S1 na Tecno R6 kutoka kwenye maduka ya Tigo nchi nzima. Kushoto ni Meneja mawasiliano wa Tecno, Eric Mkomoya.

Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akiwa amepanda pikipiki mbele ya waandishi wa habri mara baada ya kuzindua promosheni mpya ya 'nunua na ushinde' ambayo inawapa wateja nafasi ya kujishindia pikipiki na TV za kisasa kwa kununua simu mpya aina ya Tecno S1 na Tecno R6 kutoka kwenye maduka ya Tigo nchi nzima. Pembeni ni Meneja  mawasiliano wa Tecno, Eric Mkomoya.

Wateja kushinda zawadi murua ikiwemo pikipiki na TV za kisasa kwa kununua simu za Tecno S1 na Tecno R6 kutoka maduka ya Tigo nchi nzima.

Dar es Salaam,  Agosti 17, 2017- Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidigitali, Tigo Tanzania imezidi kuwaneemesha wateja wake baada ya kuzindua promosheni kabambe ambayo inawapa wateja nafasi ya kushinda pikipiki na TV za kisasa kwa manunuzi ya simu mpya aina ya Tecno S1 na Tecno R6 kutoka kwa maduka ya Tigo nchi nzima.
Akizungumza katika uzinduzi wa promosheni hiyo murua iliyofanyika katika makao makuu ya Tigo jijini Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa kupitia promosheni hii Tigo inahakikisha kuwa kila mtu sasa ana nafasi ya kumiliki simu bora ya kisasa kwa bei nafuu. Ikiwa ni muendelezo wa juhudi za Tigo kukuza mabadiliko ya dijitali nchini..
Pamoja na hayo, kwa manunuzi ya simu aina ya Tecno S1 na Tecno R6 kutoka maduka yote ya Tigo nchini, wateja wataingizwa kwenye droo itayowapa nafasi ya kushinda mojawapo ya pikipiki 20 na televisheni 20 za kisasa zinazoshindaniwa katika promosheni hii.
Shisael aliongeza kuwa kila mteja atakaponunua simu aina ya Tecno S1 na Tecno R6 kutoka maduka ya Tigo, wafanyakazi wa Tigo watanakili namba maalum ya utambulisho ya simu (IMEI) pamoja na jina na namba ya simu ya mteja husika aliyenunua simu. Namba hizi zitaingizwa katika droo za kila wiki ambapo kila wiki, wateja watapata nafasi ya kujishindia mojawapo ya pikipiki mbili na TV mbili zitakazoshindaniwa katika droo za wiki.
‘Promosheni hii ya Tecno S1 na Tecno R6 inahusu tu wale wateja watakaonunua simu za aina hii kutoka kwa maduka yetu ya Tigo nchini kote. Simu ya Tecno S1 ni ya mfumo wa 3G na itapatikana kwa bei ya shilingi 99,000/- tu. Simu ya Tecno R6 ni ya mfumo wa 4G na itapatikana kwa bei ya shilingi 195,000/- tu. Simu zote mbili ni za kisasa na zina uwezo wa kutumia mfumo wa data, kwa hiyo wateja wataweza kutumia huduma bora za data za 3G na 4G kutoka Tigo, hii ikiwa inalingana na aina ya simu watakayonunua’ alifafanua.
‘Tigo inawaelewa na kuwathamini wateja wake kwa ushirikiano mkubwa wanaotupatia. Daima tupo mstari wa mbele kuwarudishia shukrani kwa wateja wetu kwa imani kubwa wanayotuonesha siku hadi siku. Kwa hiyo leo tuna furaha kubwa tena kuwapa wateja wetu nafasi ya kumiliki simu hizi mbili za kisasa zinazopatikana katika maduka yote ya Tigo nchini kote. Pia tunawapa nafasi ya kujishindia zawadi hizi kemkem za pikipiki na TV za kisasa zitakazoboresha maisha yao. Tunaamini kuwa hii itawawezesha wateja wetu kuendelea kufurahia huduma zetu bora zinazobadilisha maisha yao ya kidigitali siku hadi siku,’ Shisaeli alimaliza.

Balozi wa Tanzania nchini Uturuki awasilisha Hati za Utambulisho

$
0
0

Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo, Balozi Mteule wa Tanzania nchini Uturuki akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mheshimiwa Recep Tayyip Erdoǧan, Rais wa Jamhuri ya Uturuki.
Mhe. Balozi Kiondo akiagana na Mheshimiwa Rais Erdoǧan, baada ya kufanya mazungumzo kuhusu mahusiano ya Tanzania na Uturuki.
Picha ya pamoja.
 


Mhe. Prof. Elizabeth K. KIONDO, Balozi wa Kwanza Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uturuki Jumatano ya tarehe 16 Agosti 2017, amewasilisha Hati zake za Utambulisho pamoja na zile za Kukoma kwa Muda wa Mtangulizi wake kwa Mheshimiwa Recep Tayyip Erdoǧan, Rais wa Jamhuri ya Uturuki. Kitendo hicho kinamfanya Mhe. Kiondo kuwa Balozi wa kwanza mkaazi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini humo.

Katika hafla hiyo Mhe. Balozi Kiondo alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Rais Erdoǧan kuhusu namna ya kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili katika maeneo ya uwekezaji, biashara, afya, Elimu, na mengineyo. Aidha, Mhe. Balozi Kiondo alimfahamisha Mheshimiwa Rais Erdoǧan kuwa Ubalozi utakuwa kiungo muhimu katika kuongeza kasi ya utekelezaji wa makubaliano mbalimbali yaliyofikiwa wakati wa ziara yake nchini Tanzania mwezi Januari 2017 ambapo mikataba na makubaliano yapatayo tisa yalisainiwa.

Kufunguliwa kwa Ubalozi mpya wa Tanzania nchini Uturuki na kuanza kufanya kazi kunatoa fursa muhimu kwa wananchi wa mataifa hayo mawili kuongeza shughuli za kiuchumi hususan biashara kwa manufaa ya pande zote mbili.

Mhe. Balozi anatoa rai kwa Watanzania kujipanga vizuri na kuchangamkia fursa mbalimbali hususan za kibiashara zinazotokana na kuendelea kuimarika kwa mahusiano kati ya Tanzania na uturuki.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 17 Agosti 2017.

Sao HILL yaanza kufanya utafiti wa kugema utovu wa miti ya misindano

$
0
0
Shamba la miti Sao Hill likishirikiana na Kampuni ya Art International limeanza utafiti wa kugema utomvu wa miti ya Misindano kama njia ya kujiongezea kipato kutokana utomvu huo kuuzwa kwa sh. 750 kwa kilo. 

Akizungumza na kamati ya Bunge ya Maliasili na Mabadiliko ya Tabia Nchi ya Malawi,Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill, Salehe Beleko  amesema katika kuongeza vyanzo vya Mapato wameingia mkataba na kampuni hiyo kufanya utafiti ni ikibainika kwamba haitaathiri Ukuaji wala Ubora wa miti wataidhinisha kuwa chanzo kipya cha mapato. 
Beleko amesema kwa kuwa ni utafitiwameanza kwanza na kwa miti iliyokuwa tayari kuvunwa wakiona hakuna Madhara wataendelea kwenye Miti michache yenye umri mdogo na matokeo ya utafiti huo yatapelekea ama kukuza ama kukataza kabisa zoezi hilo. 

Naye Mtaalam wa Kampuni ya China amesema Taasisi yake imefuata taratibu zote za ugemaji na usafirishaji wa utomvu huo na amefafanua kwamba kampuni yake inahitaji Miti Milioni 2 kwa mwaka ili kupata ujazo wa Utomvu wanaouhitaji. 
Akijibu swali la Mke wa Rais wa Zamani Bi Patricia Muluzi ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo ambaye alitaka kujua matumizi ya Utomvu huo Mtaalam huyo amesema Baada ya kuchakatwa na kuchanganywa na kemikali mbalimbali utomvu huo hutumika kutengeneza dawa mbali mbali Bazoka (chewing gum), pamoja na Gel. 
 Rashid Pemba Msusa, mjumbe wa Kamati hiyo amesema kwa Mara ya kwanza wameshuhudia matumizi mapya kabisa ya zao la mti Teknolojia ambayo hawajawahi kuiona nchini kwao Malawi. Hata hivyo ameahidi kufuatilia matokeo ya utafiti huo ili ukifaa wauhamishie Malawi.

TPB YASHIRIKI KONGAMANO LA BIASHARA JIJINI TANGA

$
0
0


Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Benki Sabasaba Mashingi akizungumza katika Kongamano la Biashara la Jijini Tanga leo
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Benki Sabasaba Mashingi wa pili kutoka kushoto akifurahia jambo na mmoja wa washiriki wa Kongamo hilo la Biashara.

AFISA Mtendaji Mkuu wa TPB Benki Sabasaba Mashingi amewahimiza wafanyabiashara mkoani Tanga kutumia huduma wanazozitoa hususani za mikopo ili waweze kukuza mitaji yao na kutanua wigo wa biashara zao.

Moshingi aliyasema hayo leo wakati akiwasilisha mada katika kongamano la biashara lililofanyika katika Hotel ya Regal Naivera Jijini Tanga na kufunguliwa na Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo,Dokta Harrison Mwakyembe.

Kongamano hilo la biashara ambalo limeandaliwa na Tanzania Standard Newspaper (TSN) katika mkoa wa Tanga lilijumuisha wadau kutoka kwenye taasisi binafsi na za serikali,wafanyabiashara wakubwa na wadogo,vijana na wasomi.

“Niwaambie tu huduma hizo zinatolewa na benki yetu kwa ajili ya wafanyabiashara wa aina mbalimbali lakini pia niwapongeze uongozi wa TSN kwa kuandaa kongamano hilo kwa mara nyengine tena katika mkoa wa Tanga”Alisema.

“Lakini pia nawakaribisha wafanyabiashara wote kutembelea tawi letu la hapa mkoani Tanga lililopo mtaa wa Taifa ili muweze kufaidika na huduma mbalimbali tunazozitoa.

“Kwani Benki yetu ya TPB imejikita kumsaidia mtanzania wa kawaida kuweza kuinua shughuli zake za kiuchumi na hatimaye kukuza uchumi wan chi yetu kwa ujumla “Alisema Moshingi.

Aidha pia alisema wanaunga mkono juhudi kubwa zinazochukuliwa na serikali ya awamu ta tano kuipeleka nchi kwenye uchumi wa viwanda ikiwemo jitihada za kufufua viwanda vilivyokufa vikiwemo vya mkoani Tanga.

Hata hivyo alisisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kutumia fursa za mradi wa bomba la mafuta uliozinduliwa na Rais John Magufuli hivi karibuni kuinua biashara zao kwani wao kama benki wapo tayari kuwasaidia kufikia mafanikio hayo.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI NCHINI AFRIKA KUMUWAKILISHA RAIS DKT MAGUFULI MKUTANO WA 37 WA SADC

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Afrika ya Kusini tayari kwa kuhudhuria Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC unaoaanza tarehe 19 na 20 ambapo kesho tarehe 18 atahudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC Double Troika Summit).

Mheshimiwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Waziri wa Mawasiliano wa Afrika Kusini Mhe. Ayanda Dlodlo.
akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli.

Akizungumza mara baada ya kuwasili kwa Makamu wa Rais, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augastine Mahiga amesema Mkutano huo utapokea na kujadili ajenda mbalimbali ikiwemo uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa SADC na Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama; Hali ya Michango mbalimbali ya Nchi Wanachama na Kupokea taarifa ya Mwenyekiti anayeondoka wa SADC Organ.

Pia Mkutano utapokea taarifa ya Katibu Mtendaji wa SADC; Kupitia hali ya kiuchumi katika Kanda ya SADC; Kuwasilisha Kaulimbiu ya Mkutano wa SADC; Taarifa kuhusu Mfuko wa Maendeleo wa SADC; Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Viwanda; Kuwezesha Chuo cha Elimu ya Sayansi na Teknolojia; Maombi ya Serikali ya Comoro na Serikali ya Burundi kujiunga na SADC; Utekelezaji wa Mabadiliko ya Kitaasisi ya Umoja wa Afrika na Mkutano wa Mshikamano kati ya SADC na Saharawi ya Magharibi.

Dkt. Mahiga amesema katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC Double Troika Summit) Tanzania itakabidhi nafasi ya Uenyekiti kwa Mwenyekiti mpya.

Double Troika inahusisha nchi wanachama sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji. Katika mkutano huo Mfalme Mswati III wa Swaziland atakuwa ndiye Mwenyekiti. Ajenda kuu katika Mkutano huu ni kupokea na kujadili taarifa kuhusu hali ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama katika Kanda na hasa nchini DR Congo na Lesotho.

Uzinduzi wa Mkutano wa Sita wa Watafiti barani Afrika wafanyika jijini Dar

$
0
0
Na Agness Francis,Blogu ya jamii.

Katika kuelekea Tanzania ya viwanda awamu ya tano ipo fursa ya kushirikiana na nchi mbali mbali ili  kuongeza wigo katika  uchumi wa viwanda nchini.

 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira,  Antony Mavunde amesema hayo katika uzinduzi wa sita wa kokangamano  la  utafiti  barani Afrika(ARCA) kwa kushirikiana na chuo cha biashara (CBE),wakala wa vipimo (WMA) na shirika La viwango Tanzania (TBS)

Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa  chuo cha biashara (CBE) katika kuelezea umuhimu wa tafiti hizo  na kuleta maendeleo zaidi ya kiuchumi nchini.

Naibu Waziri Mavunde amesema kuwa serikali amewekeza fedha za kutosha  vyuoni ili kuweza kufanya utafiti na nchi mbalimbali  duniani, ili  kukuza uchumi wa viwanda na kuweza kutoa huduma bora na bidhaa bora hapa nchini.

Awali Naibu Waziri Mavunde amesema  kuwa  kuwepo kwa ongezeko la viwanda nchini itasaidia kuondoa changamoto za ajira kwa vijana na kuongeza pato la  taifa nchini.

Nae mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara  (CBE) Profesa Emanuel Mjema, amesema ili kuwa na mahusiano mazuri na mataifa mbalimbali lazima kuwepo na vigezo vya kupima viwango bora ili kuweza kujua takwimu sahihi  kuwa ni watu wangapi wamepata huduma.

Hata hivyo  Mkuregenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Prof. Egid Mubofu amesema kuwa tunajivunia nchi yetu kwa kukidhi vigezo  vya TBS na viwango bora  kulingana na  viwango   vyote  duniani.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Antony Mavunde akifafanua jambo kwa watafiti mbalimbali barani Afrika wakati akifungua mkutano wa sita wa watafiti barani Afrika mapema hii jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Antony Mavunde (katikati) akikata utepe kuzindua ripoti ya sita ya utafiti barani Afrika mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sayansi toka taasisi ya Applied Research Conference in Africa (ARCA) Prof. Joseph Mojekwu na kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Biashara Prof. Emanuel Mjema.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Antony Mavunde (katikati) akionesha ripoti ya sita ya utafiti barani Afrika mara baada ya kuizindua, kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sayansi toka taasisi ya Applied Research Conference in Africa (ARCA)  Prof. Joseph Mojekwu na kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Biashara Prof. Emanuel Mjema.
 Mkuu wa Chuo cha Biashara Prof. Emanuel Mjema akitoa neno la utangulizi wakati wa mkutano wa sita wa watafiti barani Afrika mapema hii jijini Dar es Salaam.
 Mkuregenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Prof. Egid Mubofu akitoa mada kwa baadhi ya watafiti wa barani Afrika (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa sita wa watafiti hao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa sita wa watafiti barani Afrika wakiendelea na mkutano mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha na Eliphace Marwa - Maelezo

OLE WAKE MGOMBEA ATAKAE ENDA KINYUME NA SHERIA YA UCHAGUZI-DKT DALLO

$
0
0

Na Woinde Shizza,Arusha 

Wagombea wa nafasi mbalimbali za ungozi ndani ya chama cha mapinduzi wilaya wa Arusha wametakiwa kufuata kanuni na sheria za zilizowekwa na chama hicho.

Hayo yamebainishwa na katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Arusha Dr, Ramathani Dallo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na tuhuma za kuwepo na baadhi ya wagombea kuja kwenye usahili na watu wanaodaiwa sio wagombea bali ni waganga wa kienyeji

Alisema kuwa ni muhimu sana wagombea wakifuata kanuni taratibu na sheria zilizowekwa katika uchaguzi kwa mujibu wa kanuni ya muongozo wa uchaguzi ya mwaka 2010.

Alisema kuwa yeye binafsi hajawaona watu hao wanaodaiwa ni Waganga wa kienyeji na usahili ulienda vizuri katika kipindi hiki uchaguzi unaendelea vyema ,huku akibainisha kuwa iwapo kutakuwa na mgombea yeyote ambae atakwenda kinyume na sheria ya uchaguzi atamuaonea huruma bali atuakali zidi yake itachukuliwa .

“Nasema kwakweli ili suala na mgombea wa UWT kuja na mganga wa kienyeji kwenye usaili sijaliona, ila ukweli napenda kuchukua nafasi hii kuwasihi iwapo tutamkamata mgombea yeyote yule anaekwenda kinyume na sheria tutamchukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuita kikao kama jambo ni gumu sana, pia itatulazimu tumkate jina lake na asiwepo kwenye kinyanganyiro chochote”alisema Dkt Dallo.

Alizitaja baadhi ya kanuni kuwa ni pamoja na kutofanya kampeni ,kukusanya watu kufanya mikutano isioyo rasmi kichama pamoja na nyingi 
Aidha akiongelea baadhi za uchaguzi zilizopita alisema kwa upande wa uchaguzi wa kata ,mitaaa umemalizika vizuri sasa ivi ndio wanaendelea na maeneo mengine yaliyobaki.

Awali baadhi ya wagombea ambao hawakutaka majina yao yaandikwe walisema kuwa kuna mmoja wa mgombea mwenza sik u ya usahili alikuja akiwa na mganga wa kienyeji kitu ambacho ni kinyume na sheria ya uchaguzi

MTOTO ALIYEUNGUA MIKONO SASA KUREJEA DARASANI

$
0
0
Mtoto aliyeungua na kushindwa kuendelea na masomo mkoani Mtwara ametibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na sasa anaweza kuendelea na masomo pamoja na kufanya shughuli zake za kawaida.

Mtoto huyo aliungua moto baada ya kusukumwa na mwenzake shuleni na hivyo kuungua mikono yote miwili na kusababisha vidole kujikunja na kushikamana.Baada ya kufikishwa Muhimbili madaktari bingwa walifanyia upasuaji na sasa amepona.

Daktari Bingwa wa Upasuaji, Ibrahimu Mkoma amesema mtoto Mwanahidi Hamisi aliungua miaka saba iliyopita na mikono yake kuadhirika na kushindwa kufanya kazi yoyote.

Amesema mwaka 2015 mtoto huyo alifanyiwa upasuaji mkono wake wa kulia katika Hospitali ya CCBRT na kwamba sasa anaendelea vizuri.Dk Mkoma amesema Juni 7, 2017 Muhimbili ilimpokea mtoto huyo na baada ya kufanyia uchunguzi walimfanyia upasuaji mkono wa kushoto na kunyoosha viungo katika vidole vyake ambavyo vilikuwa vimejikunja.

“Baada ya kuungua moto vidole vyake vilishikana na viungo kujikunja, lakini tumefanikiwa kuvinyoosha viungo hivyo na sasa Mwanahidi anaendelea vizuri na matibabu,” amesema Dk Mkoma.Amesema mtoto huyo sasa anaweza kufanya kazi mbalimbali kama kufua na kwamba anaweza kundelea na shule tofauti na awali baada ya kuungua.

Mama wa mtoto huyo, Amina Mohamed Mkadengile ameambiwa kwamba anapaswa kumfanyia mazoezi mtoto wake ili aimarike zaidi.“Daktari amenielekeza jinsi ya kumfanyia mtoto mazoezi, nitakuwa nafanyia mazoezi katika Hospitali ya Mkoa ya Ligula mkoani Mtwara. Nawashukuru san

ZIARA YA RAIS DK.SHEIN WILAYA YA KUSINI UNGUJA, LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akiangalia Tungule wakati alipotembelea Biashara za Kilimo za Ushirika wa Mtule AMCOS leo pamoja na Viongozi wengine wakati alipotembelea katika Ofisi ya Ushirika huo kupata maelezo akiwa katika ziara ya kutembelea Miradi mbali mbali ya Wananchi wa Wilaya ya Kusini Unguja,(kulia) Mwenyekiti wa Ushirika wa Mtule AMCOS Bw.Mgana Khamis Zidi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akiangalia Mabilingani wakati alipotembelea Biashara za Kilimo za Ushirika wa Mtule AMCOS leo pamoja na Viongozi wengine wakati alipotembelea katika Ofisi ya Ushirika huo kupata maelezo akiwa katika ziara ya kutembelea Miradi mbali mbali ya Wananchi wa Wilaya ya Kusini Unguja,(wa pili kulia) Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja pia kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) alipokuwa akiuliza jambo wakati alipotembelea Biashara za Kilimo za Ushirika wa Mtule AMCOS leo pamoja na Viongozi wengine (Pichani) matikiti yaliyouzwa kati ya Shilingi za Kitanzania Elfu tano Mpaka Elfu Nne wakati alipotembelea katika Ofisi ya Ushirika huo kupata maelezo akiwa katika ziara ya kutembelea Miradi mbali mbali ya Wananchi wa Wilaya ya Kusini Unguja. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akifuatana na Mwenyekiti wa Ushirika wa Mtule AMCOS Bw.Mgana Khamis Zidi (katikati) pamoja na Viongozi wengine wakifuatana mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Ushirika huo leo na kupata maelezo akiwa katika ziara ya kutembelea Miradi mbali mbali ya Wananchi wa Wilaya ya Kusini Unguja. Baadhi ya Akina Mama wa Ushirika wa Mtule AMCOS walipokuwa wakimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipotembelea katika Ofisi ya Ushirika huo iliyopo Mtule Kandahar wakati alipokuwa katika ziara ya kutembelea Miradi ya maendeleo ya wananchi Wilaya ya Kusini Unguja leo. Mjumbe wa Kamati ya Mikopo katika Ushirika wa Mtule AMCOS Nd,Haji Juma Haji (kushoto) alipokuwa akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) wakati alipotembelea katika Ofisi ya Ushirika huo iliyopo Mtule Kandahar wakati alipokuwa katika ziara ya kutembelea Miradi ya maendeleo ya wananchi Wilaya ya Kusini Unguja leo (katikati) Mwenyekiti wa Ushirika wa Mtule AMCOS Bw.Mgana Khamis Zidi

Mjumbe wa Kamati ya Mikopo katika Ushirika wa Mtule AMCOS Nd,Haji Juma Haji (kushoto) alipokuwa akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) wakati alipotembelea katika Ofisi ya Ushirika huo iliyopo Mtule Kandahar wakati alipokuwa katika ziara ya kutembelea Miradi ya maendeleo ya wananchi Wilaya ya Kusini Unguja leo (katikati) Mwenyekiti wa Ushirika wa Mtule AMCOS Bw.Mgana Khamis Zidi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika Picha ya Pamoja na Wanaushirika wa Mtule AMCOS leo wakati alipotembelea katikaOfisi ya Ushirika huo kuangalia maendeleo waliofikia wananchi hao akiwa katika ziara ya kutembelea maendeleo katika Wilaya ya Kusini Unguja

VIJUSO VYA MAGAZETI YA IJUMAA LEO AGOSTI 18,2017

VIJUSO VYA MAGAZETI YA IJUMAA LEO AGOSTI 18,2017

VIJUSO VYA MAGAZETI YA IJUMAA LEO AGOSTI 18,2017

Baraza la Hifadhi ya Mazingira lampongeza mshindi wa Biko

$
0
0
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Tanzania, (NEMC), limpongeza mshindi wa droo ya 32 ya Bahati Nasibu ya Biko nchini Tanzania, Edward Gama, mkazi wa Tabata, aliyefanikiwa kunyakua jumla ya Sh Milioni 20 inayotolewa na Biko, huku akitwaa zawadi hiyo katika droo ya Jumatano iliyopita na kumtaka ajihusishe na masuala ya mazingira na ufugaji wa nyuki.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Baraza hilo, Dr Vedast Makota, wakati Gama anapokea hundi yake ya Sh Milioni 20, saa chache kabla ya kukabidhiwa rasmi fedha zake katika benki ya NMB, Tawi la Bank House, Posta, jijini Dar es Salaam leo (jana).

Akizungumzia ushindi huo wa mwanafunzi anayesubiri ajira, Dr Makota, alisema ni furaha kubwa kwa kijana wao kuibuka na ushindi huo wa Sh Milioni 20 ambapo amekabidhiwa, huku akisema ni fursa kubwa zaidi kama Gama atajihusisha pia na masuala ya mazingira kulingana na taaluma yao.

“Ni furaha kubwa kuona kijana wetu amefanikiwa kuibuka na ushindi huu mnono, hivyo namtaka azitumie vizuri fedha zake pamoja na kuwekeza pia katika sekta ya mazingira ikiwamo ufugaji wa nyuki ambao ni biashara nzuri sana,” Alisema.

Naye Gama aliwapongeza Biko kwa kumkabidhi fedha zake haraka, huku akisema wakati anapokea simu ya Kajala Masanja na Mujuni Sylvester ‘Mpoki’, hakuamini kabisa kulingana na bahati nasibu hiyo inavyohusisha watu wengi wanaocheza Biko kila siku.

“Nashukuru kwa kukabidhiwa fedha zangu ambazo nimezipata baada ya kuingiza namba 505050 na kumbukumbu namba 2456, ambapo kabla mbali na kunyakua fedha za droo kubwa, pia watu wanashinda zawadi nyingi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja inayolipwa moja kwa moja kwenye simu za Tigo Pesa, M-PESA na Airtel Money,” Alisema Gama.

Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema mbali na watu kushinda donge nono la Sh Milioni 20 kila Jumatano na Jumapili, pia kuna zawadi nyingi za papo hapo pamoja na bonasi zinazolipwa kwa wingi, huku akiwataka Watanzania wote kuendelea kucheza Biko ili wajipatie fedha za kupanua uchumi wao kwa kutumia bahati nasibu yao inayochezwa kwa kufanya miamala kwenye simu za Vodacom, Tigo na Airtel kuanzia Sh 1,000 na kuendelea.

Msanii nyota wa vichekesho Tanzania, Mpoki, aliwataka Watanzania kuacha kucheza michezo migumu, badala yake watumie uwapo wa Biko ili waweze kujipatia fursa za kukuza uchumi wao, ukizingatia kuwa tayari zimeshalipwa zaidi ya Sh Bilioni mbili kwa mwezi Mei, Juni na Julai.

WAZIRI MHAGAMA AZITAKA HIFADHI ZA TAIFA KUTUMIA WASANII KATIKA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII

$
0
0
 
Na Pamela Mollel,Arusha

WAZIRI wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Jenista Mhagama
amezitaka hifadhi za taifa nchini kuendelea kuwatumia wasanii nchini
katika kutangaza vivutio mbalimbali vinavyopatikana huku akiipongeza
Mamlaka ya hifadhi za taifa Ngorongoro inavyotangaza vivutio vyake
kupitia msanii Mrisho Mpoto.

Kauli hiyo aliitoa hivi karibuni jijini Arusha alipotembelea banda la Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro katika maonesho ya Nanenane.

Alisema kuwa wasanii wananafasi kubwa ya kuutangaza utalii wa ndani na
kuendelea kuitangaza Tanzania endapo watatumiwa kama mabalozi kupitia
umaarufu wao jambo ambalo litasaidia pia kuiingizia nchi kipato kupitia
watalii.

Naye Balozi wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Mrisho Mpoto aliwapongeza watanzania kuwa na mwitikio mkubwa wa kutembelea hifadhi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwapeleka watoto wao katika maonesho hayo ili kujifunza na kuona shughuli zinazofanywa na mamlaka hiyo hivyo kuwaandaa watoto hao kuwa wahifadhi kwa baadae.

“Mfano mzuri ni hili la punguzo la shilingi elfu 50 lililotolewa ili
watanzania waweze kutembelea hifadhi ya Ngorongoro tumeona watu
walivyochangamkia na kwenda kutembelea Ngorongoro hivyo ni jambo zuri
na la kupongezwa kwa watanzania na ninaomba waendelee kutembelea
hifadhi zetu”alisema Mpoto.

Kwa upande wake Ofisa Utalii wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Peter
Makutian aliwashukuru watanzania kuendelea kuhamasika kutembelea hifadhi hiyo tofauti na awali na kusema kuwa idadi ya wageni toka nje ya nchi wanaotembelea hifadhi hiyo kwasasa ipo sawa na watanzania.

Aidha aliwaomba watanzania wengine kuendelea kutembelea vivutio vya Tanzania ikiwemo Ngorongoro kwakuwa gharama wanazotoza ni ndogo kwao ukilinganisha na wageni toka nje ya nchi hivyo ni fursa nzuri kwao
kuitumia na kuwa mabalozi wa hifadhi kwa wengine.
WAZIRI wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akiwa anamsikiliza Balozi wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Mrisho Mpoto mara baada ya kuwasili katika banda hilo hivi karibuni jijini Arusha katika maadhimisho ya sikukuu ya nane nane 

Ofisa Utalii wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Peter Makutian aliwashukuru watanzania kuendelea kuhamasika kutembelea hifadhi hiyo tofauti na awali na kusema kuwa idadi ya wageni toka nje ya nchi wanaotembelea hifadhi hiyo kwasasa ipo sawa
na watanzania. 

UNESCO YAKABIDHI VIFAA VYA RADIO ZA KIJAMII VYA MAMILIONI

$
0
0
SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limekabidhi vifaa vya radio kwa radio za jamii nne vyenye thamani ya mamilioni ya shilingi. Unesco imesema kwamba utoaji wa vifaa hivyo umelenga kuongeza usikivu wa mawimbi ya radio katika maeneo ya vijijini. Shughuli ya kukabidhiana imefanyika Agosti 17 mwaka huu.

 Akizungumza wakati wakukabidhiana vifaa hivyo Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues alisema kwamba UNESCO inatambua kazi nzuri zinazofanywa na radio hizo za jamii za kuwafikia wananchi wengi zaidi. Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akikabidhi hati ya makubaliano na moja kati ya vifaa hivyo kwa Ofisa Utawala na Rasilimali Watu wa Radio Jamii ya Pangani FM, Rehema Kilapilo wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano Unesco Dar es Salaam. Picha juu na chini ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na Meneja wa radio ya Jamii ya Baloha FM ya Kahama, Samada Maduhu kwa pamoja wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa hivyo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za UNESCO jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano UNESCO Dar es Salaam. Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akikabidhi hati ya makubaliano na moja kati ya vifaa hivyo kwa Meneja wa radio ya Jamii ya Baloha FM ya Kahama, Samada Maduhu wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam. Picha juu na chini ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa Radio Jamii Uvinza FM, Ayubu Kalufya kwa pamoja wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa hivyo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za UNESCO jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano UNESCO. Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akikabidhi hati ya makubaliano na moja kati ya vifaa hivyo kwa Mkurugenzi wa Radio Jamii Uvinza FM, Ayubu Kalufya wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam. Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akigonga 'cheers' na wawakilishi wa redio jamii zilizopokea vifaa hivyo kwenye hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo Unesco jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kushoto) akizungumza jambo wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya radio jamii iliyofanyika katika ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.[/caption] Aidha alisema ni muhimu sana kwa radio hizo za jamii kujiangalia na kujitunza zenyewe ili wasiingie katika matata na kuchapisha au kutangaza stori baada ya kukamilika kwake.

 Alisema ipo haja kwa vyombo vya habari kufanyakazi kwa mujibu wa taratibu zao na kuhakikisha kwamba hawachapishi habari ambazo zinahatarisha uwapo wa uandishi unaozingatia maadili. Meneja wa radio ya Jamii ya Baloha FM, Samada Maduhu aliishukuru UNESCO kwa kusaidia kituo chake na kwamba wanatarajia kufikia wilaya tano. Meneja wa radio ya Jamii ya Baloha FM ya Kahama, Samada Maduhu, akitoa neno la shukrani kwa ofisi za Unesco wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo yaliyofanyika katika ofisi za Shirika hilo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa mtaalamu wa Mawasiliano Unesco, Nancy Kaizilege Angulo.

Alishukuru UNESCO kwa kuwawezesha kufika katika wilaya tano na kwamba kwa msaada huo wataokoa shilingi laki saba kwa mwezi kuazima transmita. “Radio yetu inawafikia watu 500,000 lakini kwa kupatiwa hivi vifaa tutaweza kufikia watu milioni 1 katika wilaya zaidi ya tano za Kahama, Shinyanga Vijijini, Nyang’wale na Mbogwe mkoani Geita na pia Nzega na Uyui mkoani Tabora ,” alisema meneja huyo . Kwa mujibu wa Maduhu, kama wasingelipata transmita hiyo wangelikuwa wanatumia sh milioni 8.4 kwa mwaka. Ofisa Utawala na Rasilimali Watu wa Radio Jamii ya Pangani FM, Rehema Kilapilo akitoa shukrani kwa uongozi wa Unesco wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya redio iliyofanyika katika ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.[/caption] Kwa upande wake, Ayubu Kalufya wa radio ya jamii Uvinza alisema kwamba kituo chake kilikuwa kinakodisha transmita kwash laki tano na kufanya kwa mwaka mzima kutumia sh milioni 6.

 Alisema kwa kupata vifaa hivyo walikuwa wanaachama na ukodishaji huo. Kwa mujibu wa Kalufya, transmita hiyo mpya itawafikisha mbali zaidi katika pwani za Ziwa Tanganyika na hivyo kuleta mabadiliko yanayokusudiwa. Kalufya alisema wananchi wakisikia mambo mbalimbali ya kuwaelimisha na wao wakapata nafasi ya kutoa maneno yao haki za binadamu zitakuwa zimeheshimiwa sana nchini. Mkurugenzi wa Radio Jamii Uvinza FM, Ayubu Kalufya (kulia) akitoa neno la shukrani kwa hivyo Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kushoto) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa vya radio hizo yaliyofanyika kwenye ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam.

Aliishukuru Unesco kwa kuendelea kuwasaidia na kusema kama si kwa msaada wa UNESCO jamii zilizopo pembezoni zisingepata nafasi ya kutoa madukuduku yao. Radio nyingine zilizonufaika na msaada huo ni Pangani FM. Radio hiyo sasa inaweza kusikika Tanga nzima badala ya Pangani pekee. Katika orodha ya redio zilizopatiwa vifaa ipo pia Mkoani FM ya kutoka Zanzibar.  Picha juu na chini ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na Ofisa Utawala na Rasilimali Watu wa Radio Jamii ya Pangani FM, Rehema Kilapilo wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za UNESCO jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano UNESCO.

CHUO CHA UFUNDI ARUSHA CHAZINDUA MTAALA MPYA WA GESI NA MAFUTA

$
0
0
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo akizungumza wakati wa ufunguzi wa kozi ya ufundi bomba,mafuta na gesi katika chuo
cha Ufundi Arusha(ATC) jijini Arusha,kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Camosun nchini Canada,Sherri Bell na kulia ni Mkuu wa Chuo cha ATC,Dk Richard Masika. 
Afisa wa kitengo cha biashara katika ubalozi wa Canada nchini,Anita
Kundy akisoma hotuba yake,kushoto ni Mshauri wa ufundi kutoka nchini Canada,Dk Alan Copeland. 
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo akionesha nakala ya mtaala mpya wa kozi ya ufundi bomba,mafuta na gesi uliozinduliwa
katika chuo cha Ufundi Arusha(ATC) 
Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi nchini(TVET)Wizara ya Elimu,Sayansi na
Teknolojia,Mhandisi Thomas Katebalirwe akizungumza jambo katika hafla ya uzinduzi huo. 
Baadhi ya wanafunzi wa mwanzo wa kozi ya ufundi bomba na utaalamu wa gesi na mafuta katika Chuo cha ufundi Arusha 

Mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo(wa tatu kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na wageni kutoka Chuo cha
Camosun,Victoria nchini Canada na Chuo cha ATC. 

Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo amekipongeza Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) kwa uamuzi wake wa kushirikiana na Chuo cha Camosun cha nchini Canada kuandaa mtaala wa ufundi bomba,gesi na mafuta katika ngazi ya Diploma.

Akizindua mtaala huo ambao ni kwanza na aina yake nchini alisema utaisadia serikali kuwapata vijana wengi wenye utaalamu wa sekta ya mafuta na gesi nchini katika ngazi hiyo ambayo imenekana kuna pengo kubwa nchini.

“Mafunzo haya yatasaidia sana kuwapata wataalamu wetu na itaipunguzia serikali mzigo wa kuwaajili wataalamu wa kigeni ambao ulipwa fedha nyingi za kigeni,”alisema

Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha,Dk Richard Masika amesema baada ya kutambua mahitaji makubwa ya wataalamu wa fani hiyo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita walikua wakiaanda mtaala kwa ushirikiano na Chuo cha Camosun na mafanikio yamepatikana.

Alisema kozi hiyo ni nyumbufu itakayowawezesha wanafunzi kufanya kazi baada ya kumaliza mwaka wa kwanza na baadaye kuendelea na masomo jambo ambalo litakua likiwapa maarifa kwa vitendo zaidi badala ya nadharia pekee.

Mmoja wa wanafunzi wanaosoma kozi hiyo ambayo imegharamiwa na serikali ya Tanzania,Latifa Mkombo amesema wanaishukuru serikali kwa kutoa ufadhili huo na kuahidi kusoma kwa bidii kwaajili kuingia katika ajira za gesi na mafuta.

Ukomo wa kushughulikia maombi ya muda mrefu ya kuunganisha Umeme ni Agosti 30- Dkt Kalemani

$
0
0
Na Teresia Mhagama

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani ameeleza kuwa ukomo wa kuunganishia umeme wateja walioomba kuunganishiwa huduma hiyo kwa muda mrefu ni Agosti 30, 2017 na Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) atakayeshindwa kutimiza agizo hilo atashushwa cheo.

Dkt. Kalemani aliyasema hayo kwa nyakati tofauti akiwa katika ziara ya kuzindua mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu katika mikoa ya Rukwa, Ruvuma na Mtwara.

"Unakuta kuna wateja wameomba kuunganishiwa umeme miezi kadhaa iliyopita lakini mpaka sasa hawajaunganishwa wakati vifaa vipo, kwa hili lazima tuchukue hatua kwa Meneja kama ni wa wilaya, mkoa, Kanda au Mkurugenzi atayechelewa kuunganishia wateja Umeme," alisema Dkt. Kalemani.

Dkt. Kalemani alisema kuwa muda wa kumuunganishia mteja Umeme mara anapolipia huduma hiyo ni Siku Saba na si vinginevyo."Natambua kuna maeneo ambayo TANESCO mnafanya kazi vizuri lakini katika hili tutawajibishana," alisisitiza Dkt. Kalemani.

Wakati huohuo. Dkt. Kalemani aliwaagiza watendaji wa TANESCO kuhakikisha kuwa watu wote wanaofanya kazi ya kutandaza nyaya za umeme ndani ya nyumba wawe wanatambulika na Shirika hilo ili kuondoa tatizo la vishoka kufanya kazi hiyo pasipo ufanisi na baadaye kuleta madhafa kama ya moto.

Vilevile aliwataka watendaji hao kutokukaa maofisini na badala yake wawafuate wananchi sehemu walipo, suala ambalo litafanya Shirika hilo kuongeza idadi ya wateja na kuwaondolea wananchi kero ya kutembea kwa umbali mrefu kufuata huduma TANESCO.

Kuhusu usimamizi wa mradi wa usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu ambao umeshaanza kutekelezwa nchini, Dkt Kalemani aliwataka watendaji wa TANESCO kuhakikisha kuwa wanawasimamia wakandarasi wanaofanya kazi hiyo usiku na mchana ili mradi ukamilike ndani muda uliopangwa.

Aidha Dkt. Kalemani alitoa maagizo mbalimbali ambayo yanapaswa kutekelezwa na wakandarasi wote waliopewa kazi ya kusambaza umeme vijijini katika Mradi wa Awamu ya Tatu.

Naibu Waziri aliwaagiza Wakandarasi hao kutoajiri wakandarasi wasaidizi wanaotoka nje ya eneo lao la kazi ili wananchi wanaotoka katika maeneo hayo wapate ajira na kutoa huduma mbalimbali kwa wakandarasi hao na hivyo kujiongezea kipato.

Pia aliwataka wakandarasi hao kutokuruka kijiji, kitongoji, sehemu zinazotoa huduma muhimu kama mitambo ya maji, Shule, vituo vya afya na sehemu za biashara, na nyumba ambazo tayari zimeshafanyiwa malipo ya kuunganishwa na huduma ya umeme.

" nisingependa kusikia Kituo cha Afya, Shule au Mitambo ya Maji imerukwa na haijawekewa Umeme hivyo nichukue nafasi hii kuwashauri watendaji wa Halmashauri nchini kutenga fedha kwenye Bajeti zao kwa ajili ya kutandaza nyaya za Umeme kwenye sehemu hizo ili wakandarasi waweze kuingiza Umeme," alisema Dkt. Kalemani.

Vilevile, Dkt. Kalemani aliwataka wakandarasi hao kutoa malipo kwa wakandarasi wadogo ndani ya wakati ili kuepusha mradi huo kusuasua na kuwacheleweshea huduma wananchi.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mradi wa kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika mkoa wa Ruvuma.

JAFO AAGIZA MKANDARASI WA MRADI WA MAJI ITISO ASAKWE

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amemwagiza Mkurugenzi wa halmashauri ya Chamwino Athumani Masasi kumtafuta mkandarasi wa mradi wa maji Itiso ili akamilishe mradi huo haraka kabla ya kuchukuliwa hatua.

Akizungumza leo katika ziara yake ya kukagua mradi huo, Jafo amesema mkandarasi huyo kutoka kampuni ya Audancia anatakiwa kurudi eneo la mradi haraka kukamilisha kama mkataba wake unavyoelekeza.

“Mmtake arudi haraka hapa kwenye eneo la mradi au kama ikishindikana achukuliwe hatua za kisheria kwa kukamatwa na polisi na kupelekwa mahakamani kutokana na kushindwa kutekeleza mkataba,”amesema Jafo. 

Amesema Mkandarasi huyo ametoweka eneo la mradi huku akiwa amefunga mabomba yenye ubora wa chini kwenye njia kuu (Main line) kinyume cha mkataba.Ameeleza kuwa mkandarasi huyo amelaza mabomba ya Class B(PN 6) badala ya bomba za Class C(PN10) jambo ambalo 

limesababisha mradi huo kushindwa kufanyakazi kwa kuwa mabomba yaliyofungwa yameshindwa kuhimili msukumo wa maji.Kadhalika, Jafo pia ameagiza mkandarasi mshauri wa mradi huo O&A Company LTD kutafutwa kwani ameshindwa kusimamia mradi huo ipasavyo na kuruhusu kazi hiyo ifanyike kinyume cha mkataba na kuruhusu mkandarasi atoke eneo la mradi wakati vituo vinne havitoi maji kati ya vituo kumi vya mradi. 

Hata hivyo Jafo ametoa onyo kwa wakandarasi washauri na wakandarasi wa ujenzi wa maji ambao wameshindwa kutimiza wajibu wao kwamba hivi sasa kazi zilizo chini ya Ofisi ya Tamisemi watazisikia kwenye bomba.

“Tutakuwa tumebaini makampuni yote yanayofanya kazi kwa ubabaishaji na kutoyapatia kazi tena za usimamizi na ujenzi katika halmashauri zote,”amesema Naibu Waziri Jafo

Jafo ameagiza kasoro zote za mradi huo zirekebishwe na ifikapo Septemba 15, mwaka huu mradi huo uwe umekamilika.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Seleman Jafo akizungumza na wananchi nakutoa maelekezo watendaji wa Halmashauri ya Chamwino katika mmoja ya kituo cha kuchotea maji kwenye mradi wa maji Itiso. 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Seleman Jafo akizungumza na wananchi nakutoa maelekezo watendaji wa Halmashauri ya Chamwino katika mmoja ya kituo cha kuchotea maji kwenye mradi wa maji Itiso. 
Mbunge wa Chilonwa Joel Mwaka akimkaribisha Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo kuzungumza na wananchi katika mradi wa maji Itiso.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na wananchi na viongozi wa Itiso.

IKUNGI UNITED WAJINOA KUELEKEA MICHUANO YA "IKUNGI ELIMU CUP 2017" MKOANI SINGIDA.

$
0
0
Fundi akichomelea vyuma kwa ajili ya kufunga nyavu ikiwa ni marekebisho ya mwisho katika uwanja wa shule ya Sekondari Ikungi, wilaya ya Ikungi mkoani Singida kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya ligi ya mpira wa miguu ya Ikundi Elimu Cup 2017 wilayani Ikungi.Kauli mbiu katika mashindano hayo ni " Changia, Boresha Elimu Ikungi.

Na George Binagi, BMG
Mashindano hayo yatashirikisha timu mbalimbali kutoka Kata 28 wilayani Ikungi yakilenga kuhamasisha wananchi na wadau wengine wa elimu kushiriki katika kutatua changamoto za elimu ikiwemo uhaba wa madarasa, nyumba za waalimu, maabara pamoja na vyoo vya shule.

Hii ni baada ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Miraji Jumanne Mtaturu kuteuliwa kuwa mlezi wa mfuko wa elimu wilayani humo na hivyo kuamua kuanzisha michuano hiyo ili kuleta chachu kwa wananchi na wadau mbalimbali kuchangia masuala ya kielimu.

Jumamosi timu ya soka ya Ikungi United na inakuwa ikimenyana na timu ya Puma ambapo mchezo huo utatanguliwa na mchezo kati ya madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Singida dhidi ya madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.

Katika mchezo huo wa awali timu ya madiwani kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ikungi itaongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu huku timu ya madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Singida ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe.Elias Tarimo.

Ufunguzi wa mashindano hayo utatanguliwa na shughuli ya ufyatuaji matofali ambapo kila Kata wilayani Ikungi imetakiwa kufyatua matofali yasiyopungua 10,000 ili kusaidia ujenzi wa madarasa, nyumba za waalimu na vyoo vya shule.
Mwl.Seth Raban Mwakalasya ambaye ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya ligi ya ligi ya soka ya Ikungi Elimu Cup 2017 yanayotarajiwa kuanza katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Jumamosi Agosti 19 katika uwanja wa shule ya sekondari Ikungi.
Timu ya soka ya Ikungi United Sports Club ikifanya mazoezi katika uwanja wa shule ya msingi Ikungi jioni ya leo
Ikungi United Sports Club wakifanya mazoezi katika uwanja wa shule ya msingi Ikungi jioni ya leo
Ikungi United Sports Club watamenyana na timu ya Puma katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Ikungi Elimu Cup 2017
Timu ya Ikungi United Sports Club ikiwa kwenye mazoezi hii leo jioni
Nahodha wa timu ya Ikungi United Sports Club, Lazaro John Francis (pichani) amesema maandalizi yao yako vizuri na kwamba michuano ya Ikungi Elimu Cup 2017 itakuwa na ushindani mkubwa hivyo wapenzi wa soka wategemee soka la kuvutia kwenye michuano hiyo
Kocha wa timu ya soka ya Ikungi United Sports Club, Danny Ayoub amesema kikosi chake kimejipanga vyema na kwamba michuano itaweza kuiwezesha timu yake kusonga mbele kimichezo nchini ikifuata nyayo za kaka zao Singida United.
Kikosi cha Ikungi United Sports Club kikiwa kwenye tathmini fupi baada ya mazoezi ya hii leo jioni
Kocha wa kikosi cha Ikungi United Sports Club akitoa tathmini fupi baada ya mazoezi ya timu hiyo jioni ya leo ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye michuano ya Ikungi Elimu Cup 2017 katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida ambapo michuano hiyo itafunguliwa jumamosi Agosti 19,2017 huku mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Dkt.Rehema Nchimbi.
Kauli mbiu katika mashindano hayo ni " Changia, Boresha Elimu Ikungi.
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live


Latest Images