Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1339 | 1340 | (Page 1341) | 1342 | 1343 | .... | 1904 | newer

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, alipofanya ziara ya kikazi bandarini hapo, jijini Dar es Salaam.
   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto), akitoa maelekezo kwa Mkururgenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko wakati akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka hiyo wakati alipofanya ziara ya kikazi, jijini Dar es Salaam. 
   Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Meli kutoka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Kapteni Abdullah Mwingano, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (wa tatu kushoto), kuhusu utaratibu wa upakuaji wa mafuta bandarini wakati alipofanya ziara ya kikazi katika Bandari ya Dar es Salaam.
   Meneja Msaidizi wa Mifumo ya ukaguzi wa mizigo (Scanner), Bandari ya Dar es Salaam Bw. Jackson Paul, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, namna mifumo hiyo inavyofanya kazi wakati wa ziara yake ya kikazi bandarini hapo. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (katikati), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati wa ziara ya kikazi katika Bandari ya Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko. Kulia ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Freddy Liundi.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jaap Frederiks  ambaye alifika Ikulu kwa lengo la kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.

  Makamu wa Rais alimhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itazidi kuimarisha uhusiano wake na nchi ya Uholanzi hasa katika sekta  ya kilimo, elimu na uboreshwaji  wa  mazingira ya uwekezaji ili  kufikia lengo la Tanzania ya Viwanda.

  Aidha, Mhe.Balozi aliahidi kuwa mjumbe mzuri wa Tanzania na atarejea mara kwa mara kuja kutembea kwani Tanzania ina watu wema na vivutio vingi vya utalii.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jaap Frederiks  ambaye alifika Ikulu kwa lengo la kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jaap Frederiks  ambaye alifika Ikulu kwa lengo la kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jaap Frederiks  ambaye alifika Ikulu kwa lengo la kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.

  0 0

  Nahodha wa timu ya Mchenga Mohamed Yusuph (jezi 10) akiwa amerusha mpira ulioleleka langoni mwa timu ya TMT katika mchezo wa kwanza wa fainali ya Michuano ya Sprite BBall King.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Timu ya mpira wa kikapu ya Mchenga Bball Stars imeanza vyema katika mchezo wa kwanza wa fainali ya Sprite BBall kings kwa kuweza kuibuka na ushindi wa alama 101 dhidi ya 71 vya TMT.

  Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Don Bosco Oysterbay ulikuwa wa kasi kwa kila upande kwa timu ya TMT Kuonekana kuwabana na kuwalinda Mchenga Bball stars.

  Katika mchezo huo wa kwanza wa fainali ya michuano ya Sprite BBall Kings,Mchenga wameweza kuibuka na ushindi wa alama 101 ambapo katika robo ya kwanza na ya pili walionekana kupewa ulinzi mkali na timu ya TMT lakini utulivu, umakini na nidhamu ya wachezaji wa Mchenga uliweza kubadili matokeo katika robo ya tatu na ya nne.
  Nahodha wa timu ya TMT Isihaka Masoud amesema kuwa wamepoteza mchezo wao wa kwanza wa fainali ila bado kuna mechi zingine zinazoweza kuamua matokeo na zaidi wanaenda kuangalia wapi wamekosea ili katika mchezo wa pili wa fainali waweze kuibuka kushinda.

  "Tunaenda kuangalia wapi tumekosea, turekebishe na katika mchezo wa pili wa fainali tunataka kuhakikisha tunatoka na ushindi kwani mecho moja haiwezi kuamua matokeo ya mechi zilizobaki," amesema Isihaka.

  Fainali hiyo inayoendelea katika viwanja vya Don Bosco iliweza kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali kwa ajili ya kushuhudia mtanange huo pamoja na kutoa Burdani kwa mashabiki wa mpira wa kikapu waliojitokeza kushabikia timu hizi mbili za Mchenga BBall Stars na TMT zote zikitokea Upanga.

  Baadhi ya wasanii waliohudhuria ni pamoja na Young D, Lulu diva, Tammy the baddest, Country Boy ,Kajala, DJ choka na wengine wengi.

  Mchezo wa pili wa  fainali utapigwa tena Kesho, Jumatano katika Viwanja vya Don Bosco ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia kiasi cha milion 10, mshindi wa pili milioni 3 na mchezaji bora wa michuano (MVP) atajinyakulia milioni 2.

  0 0

   Msanii  Mkongwe wa Muziki Bongo Fleva Juma Nature akiongoza kundi la Wanaume Family katika  katika Tamasha la Miaka 40 ya Bia ya Safari Lager lililofanyika katika Viwanja vya Readers Club Jijini Dar es Salaam
   Msanii  Mkongwe wa Muziki Bongo Fleva Juma Nature akiongoza kundi la Wanaume Family katika  katika Tamasha la Miaka 40 ya Bia ya Safari Lager lililofanyika katika Viwanja vya Readers Club Jijini Dar es Salaam
   Msanii wa Bongofleva Barnaba akiimba kwa kutumia Live band katika Tamasha la Miaka 40 ya Bia ya Safari Lager lililofanyika katika Viwanja vya Readers Club Jijini Dar es Salaam
  Msanii Mkongwe wa Muziki wa Bongo Fleva , Rehema Chalamila (Ray C) akitoa Burudani katika Tamasha la Miaka 40 ya Bia ya Safari Lager lililofanyika katika Viwanja vya Readers Club Jijini Dar es Salaam

   Msanii wa Muziki wa dansi nchini, Ally Choki  akiimba katika Tamasha la Miaka 40 ya Bia ya Safari Lager lililofanyika katika Viwanja vya Readers Club Jijini Dar es Salaam
   Msanii wa Bongo Fleva Prince Dully Sykes  akitumbuiza nyimbo zake za  Zamani katika Tamasha la Miaka 40 ya Bia ya Safari Lager lililofanyika katika Viwanja vya Readers Club Jijini Dar es Salaam
   Dj Maharufu kutoka kituo cha Radio cha Clouds Fm Dj Zero akionyesha ufundi wa kuchezea Santuri katika Tamasha la Miaka 40 ya Bia ya Safari Lager lililofanyika katika Viwanja vya Readers Club Jijini Dar es Salaam
   Dj Mkongwe katika uchezeshaji wa Santuri, John Dilinga (DJ JD) Akionyesha ufundi wa kuchezesha Santuri kwa kupiga nyimbo za Zamani katika Tamasha la Miaka 40 ya Bia ya Safari Lager lililofanyika katika Viwanja vya Readers Club Jijini Dar es Salaam
   Msanii kutoka kundi la Wanaume Family ,Rich One akitumbuiza katika Tamasha la Miaka 40 ya Bia ya Safari Lager lililofanyika katika Viwanja vya Readers Club Jijini Dar es Salaam
   Mashabiki walifurika katika Tamasha la Miaka 40 ya Bia ya Safari Lager lililofanyika katika Viwanja vya Readers Club Jijini Dar es Salaam
  Mashabiki walifurika katika Tamasha la Miaka 40 ya Bia ya Safari Lager lililofanyika katika Viwanja vya Readers Club Jijini Dar es Salaam

  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi wakati wa nyimbo za mataifa mawili zikipigwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA). Rais huyo wa Misri ameondoka mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi wakati akielekea kupanda ndege mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza nyimbo za kikundi cha matarumbeta kilichokuwa kikitumbuiza katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya kumsindikiza mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi ambaye ameondoka mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Japan Ichiro Aisawa aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mbunge na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Japan Ichiro Aisawa Ikulu jijini Dar es Salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mbunge na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Japan Ichiro Aisawa mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

  0 0

  The culture of secrecy is still embedded in public officials especially in the central government as opposed to Local Government despite improvement in service delivery and access to information, a recent study has revealed.

  A study which was conducted by the Media Institute of Southern Africa (MISA) Tanzania Chapter with support from the Collaboration on International ICT Policy for East and Southern Africa (CIPESA) aimed at looking at Access to Information in Local Government Authorities (LGAs) and Central Government offices in Tanzania. The LGAs were represented by the City and Municipal Councils and the Central Government was represented by the Regional Commissioners’ Offices.

  This study wished to find out how central government and local government authorities are transparent and accountable to citizens. The study also strived to find out how the general public do/can access information in public offices.

  Practical experience from Journalists who conducted the study shows that there is an improvement in service delivery and access to information in some of the public offices especially in Local Government as opposed to Central Government.

  However, they say laxity among public servants is still a big problem in public service. “If you received someone’s documents, while would you say you can’t see them just a week later?” questions Haika Kimaro, Mwananchi Correspondent in Mtwara. 

  Similar sentiments were echoed by George Binagi, a Radio Journalist in Mwanza. “I submitted my questions in writing to the Regional Commissioner’s Office. I went back 10 days after and yet I did not get the answers , they looked for my letter and they never saw it” .

  “At Kigoma Ujiji Municipal Council they received the letter but they did not reply and even after going there for follow up, the Secretary claimed to have misplaced the letter”, says Rhoda Ezekiel, Uhuru Newspaper Correspondent in Kigoma Region.

  Jacquline Jones, Mass Communication graduate and intern at MISA Tanzania offices says she went to the Dar es Salaam Regional Commissioner’s office posing as a student researcher. But because she didn’t have the letter from her university they refused to offer her the information she requested, saying their work procedures don’t allow them to do so regardless of the information she wanted.

  “Their customer service is awful and the people at the registry department they were quite harsh and rude. One of them actually shouted at me for insisting on getting my answers in a written form”, says Ms Jones.

  She also submitted a similar request (but with different questions) to the Dar es Salaam City Council, which, according to the Information Officer it needed at least four different Heads of Sections, who gladly availed to her all the information she wanted.

  One of the questions that were asked to those who did the study was, “Did you experience good customer care among those who receive visitors/respond to telephone calls?”  According to Zulfa Musa, Mwananchi Newspaper Correspondent in Arusha, there are telephones in the City Council’s offices which are received by their assistants, but the Director and his secretary have private phones that they both receive and call personally. 

  She says that while at the office she witnessed different people receiving good service and direction and if the person in charge was not around, they were told that the person will be informed when she/he gets back.

  As previously said, the study used journalists as researchers. According to the findings, it was very interesting to see how people who usually seek information from these public offices are treated in some offices. The question that researchers ask themselves is how ordinary citizens would be treated in some of these very same offices if people with proper identification like them face those challenges.

  In its concluding remarks, the study tells that it is hard to deny the fact that free and easier access to government-held information is key to development of any democracy. It is an important aspect in promoting transparency and accountability.

  According to Information experts, access to quality and timely information by everyone, and most importantly to rural population, is crucial in facilitating informed dialogue, monitoring and evaluation of development issues at the local level and to enhance governance and accountability for improved delivery of service and implementation of projects.

  “There was an Access to Information Act that was passed in 2016. The only challenge I see for now is that both public servants and the general public are unaware of this Law. There is a need for sensitization of the law among public servants. It is in public offices where most of the information is generated. It is important they know what the law entails”, says 

  Sengiyumva Gasirigwa, Information and Research Officer at MISA Tanzania.
  He adds that there is a need for specialized trainings/seminars/workshops for public officials on Freedom of Information (FOI) issues and the public’s Right to Know (Access to public-held information) vis-à-vis its importance to country’s development.

  0 0

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (katikati), akipatiwa maelezo na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo, wakati alipotembelea vitengo mbalimbali vya shirika hilo, kuongoea na Uongozi pamoja na wafanyakazi, Dar es Salaam leo. Wa tatu ni Kaimu Katibu wa Shirika, Zuhura Pinde.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (katikati), akipatiwa maelezo na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo kuhusu utendaji kazi wa kitengo cha utumaji na upokeaji wa fedha cha Western Union, katika ziara hiyo. 
  Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo (kulia), akimpatia maelezo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani kuhusu idara mbalimbali za Posta Kuu, wakati alipotembelea sehemu hiyo katika ziara hiyo. Kushoto ni Meneja wa Posta, Mkoa wa Dar es Salaam, Margret Mlyomi.
  Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo, akizungumza wakati akimkaribisha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (kushoto kwake), kuzungumza na Uongozi wa shirika hilo, wakati wa ziara hiyo. Kulia ni Meneja Mkuu Uendeshaji wa shirika, Hassan Mwang'ombe.
  Baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, wakati alipokuwa akizungumza nao katika ziara hiyo, leo jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, akizungumza na uongozi wa Shirika la Posta katika ziara hiyo. Kulia kwake ni Kaimu Postamasta Mkuu wa shirikahilo, Macrice Mbodo, kushoto ni Kaimu Katibu wa Shirika, Zuhura Pinde na kulia ni Meneja Mkuu Uendeshaji wa shirika, Hassan Mwang'ombe.
  Baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, alipokuwa akizungumza nao leo jijini Dar es Salaam.    
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (katikati), akizungumza na uongozi wa Shirika la Posta katika ziara hiyo.
  Baadhi ya waandishi wa habari, wakisikiliza na kuchukua habari, wakati Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani alipokuwa akizungumza na uongozi wa Shirika la Posta leo jijini Dar es Salaam. 
  Baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, alipokuwa akizungumza nao leo jijini Dar es Salaam. 
  Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo, akimshukuru Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (kushoto kwake), mara baada ya kumaliza kuzungumza na Uongozi wa shirika hilo, katika ziara hiyo. 
  Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta wakiwa kwenye mkutano wao na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, alipofika kwenye taasisi hiyo, kukagua sehemu mbalimbali za shirika, kuzungumza na Uongozi pamoja na wafanyakazi.
  Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo, akizungumza wakati akimkaribisha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia), kuzungumza na wafanyakazi wa shirika hilo, wakati wa ziara hiyo. 
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Posta, wakati alipowataka kueleza matatizo yao yanayowakabili katika kazi zao kwenye shirika hilo. 
  Mmoja wa wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, Joyce Kagose akimuelezea Naibu Waziri Mhandisi Ngonyani, matatizo mbalimbali yanayowakabili kama wafanyakazi pia ya shirika hilo katika kujikwamua kimaendeleo.  
  Naibu Waziri Mhandisi Ngonyani, akisikiliza kero za wafanyakazi wakati wa mkutano huo. 
  Mfanyakazi wa shirika hilo, Ahmed Kaumo akimuelezea Naibu Waziri Mhandisi Ngonyani, matatizo yanayowakabili pamoja na yanayolikabili shirika kwa jumla.  
  Naibu Waziri Mhandisi Ngonyani, akitaka ufafanuzi wakati mmoja wa wafanyakazi alipokuwa akielezea matatizo yanayowakabili katika kazi zao za kila siku kwenye shirika hilo. 
  Mfanyakazi Jasson Kalile akimuelezea Naibu Waziri Mhandisi Ngonyani, jinsi shirika hilo, linavyokabiliwa na matatizo mbalimbali yanayolikwamisha kupiga hatu za haraka za kimaendeleo.
  Zainab Matollah, mfanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, akimuelezea Naibu Waziri Mhandisi Ngonyani, matatizo mbalimbali yanayowakabili katika kazi zao. 
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, akizungumza na wafanyakazi mara baada ya kusikiliza matatizo yao yanayowakabili katika utendaji wao wa kazi kwenye shirika hilo, la Posta.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, akizungumza na wafanyakazi.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, akisalimiana na kuagana na wafanyakazi mara baada ya kumaliza kuzungumza nao, leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  MSHINDI wa tatu wa Mbio za Dunia za London Marathon mwaka huu, Felix Simbu amesema kuwa ushindi huo alioupata si wapeke yake bali wa wanariadha wote ambao walienda kushiriki kutokana walijitoa muhanga hadi kufanya vizuri.

  Simbu alishika nafasi ya tatu katika mbio za Km 42 na kuitoa kimasomaso Tanzania ambayo ilikuwa haijafanya vizuri katika mashindano hayo kwa miaka mingi.

  Akizingumza mara baada ya kutua akitokea nchini Uingereza ambapo alipokelewa na mamia ya mashabiki, Simbu alisema haikuwa kazi rahisi kupata medali hiyo imetokana na wao kujitoa muhanga.

  "Ushindi huu si wangu peke yangu bali ni wa wetu sote kutokana tulikuwa na umoja."Huu ni ushindi wa wote, hivyo umoja wetu utazidi kujitahidi kufanya vizuri zaidi hapo baadae," alisema.

  Alisema, aliona kama maajabu kwa ushindi huo baada ya kuona bendera ya Tanzania inapandishwa kuashiria ushindi wake.Awali, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harryson Mwakyembe alisema ushindi huo umewafanya Watanzania wawe na furaha kutokana hawakuwa na imani ya kufanya vizuri.

  Alisema ni wakati sasa wa kuwekeza katika mchezo huo ili uweze kupiga hatua zaidi.Simbu aliwasilia saa 12:20 jioni kutokana na kuchelewa kufika ambapo awali aliyatarajiwa kufika saa 6:05 mchana.

  Kufika kwake alipokelewa na vikundi mbalimbali vya ngoma, wasanii ambao waliongozwa Khadija Kopa na Riyama Ally.

  0 0

  Meneja wa Huduma za Rejareja wa Kampuni ya Samsung Leilatu Jetwa akimkabidhi Rajab Mchatta mshindi wa jumla wa promosheni ijukalinayo kama ’Nunua Sajili na Ushinde’ zawadi za Friji, Microwave na Luninga wakati wa hafla ya kumkabidhi iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.


  Rajab Mchatta mshindi wa jumla wa promosheni ijukalinayo kama ’Nunua Sajili na Ushinde’ akikagua Friji, Microwave na Luninga zawadi alizokabidhiwa na Meneja wa Huduma za Rejareja wa Kampuni ya Samsung Leilatu Jetwa akimkabidhi wakati wa hafla ya kumkabidhi iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

  Rajab Mchatta mshindi wa jumla wa promosheni ijukalinayo kama ’Nunua Sajili na Ushinde’ akimshukuru Meneja wa Huduma za Rejareja wa Kampuni ya Samsung Leilatu Jetwa baada ya kumkimkabidhi Friji, Microwave na Luninga zawadi alipewa baada ya kuibuka mshindi wa jumla jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

  Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Majumbani wa Kampuni ya Samsung Tanzania, Rayton Kwembe akimpongeza Rajab Mchatta (wa pili kushoto) mshindi wa jumla wa promosheni ijukalinayo kama ’Nunua Sajili na Ushinde’  wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Meneja Bidhaa za nyumbani wa Kampuni hiyo, Eliasi Mushi na Meneja wa Huduma za Rejareja wa Kampuni ya Samsung Leilatu Jetwa. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogspot)

  0 0


  0 0

  Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani katikati (aliyevaa suti) akimsikiliza Mkuu wa Kivuko/ Magogoni Kigamboni Mhandisi Lukombe King’ombe wakati akimpa taarifa ndani ya chumba cha kuongozea kivuko cha MV. KAZI alipotembelea kujionea utendaji kazi wake, wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu .


  Baadhi ya Wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Makao makuu wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Dk. Mussa Mgwatu wakati akisoma taarifa fupi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani aliyetembelea ofisi za wakala huo kujionea utendaji kazi na kusikiliza changamoto zinazoukabili wakala huo
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu katikati akitoa ufafanuzi wakati alipokua akisoma taarifa ya wakala huo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani wa kwanza kushoto. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa wakala huo Hans Lyimo. Mheshimiwa Ngonyani alitembelea ofisi za wakala huo kujionea utendaji kazi na kusikiliza changamoto zinazoukabili wakala huo.
  Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani katikati akimsikiliza Meneja wa Karakana ya Mt Depot Mhandisi Moses Humbe wa kwanza kushoto alipokua akimuelezea kuhusu utendaji kazi wa karakana hiyo. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu.


  Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani katikati mara baada ya kushuka kutoka kivuko cha MV.KAZI alipotembelea kivuko hicho kukagua utendaji kazi wake. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu na kulia ni Mkuu wa Kivuko/ Magogoni Kigamboni Mhandisi Lukombe King’ombe .


  Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani katikati (aliyevaa suti) akipewa ufafanuzi kuhusu eneo panapojengwa chumba kipya cha kukatia tiketi eneo la Kigamboni na Mkuu wa Kivuko/ Magogoni Kigamboni Mhandisi Lukombe King’ombe (wa pili kushoto aliyenyoosha mkono). Wa pili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu anayesikiliza kwa makini.
  Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (wa pili kulia) akishuka kutoka kwenye kivuko cha MV. KIGAMBONI mara baada ya kukagua utendaji kazi wake, kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu.

  0 0

  Na fredy Mgunda, Iringa.

  Watanzania wametakiwa kuanza kuutumia mtandao wa simu wa TTCL kwa kuwa umeboreshwa kwa kiwango kikubwa na huduma zao zinazingatia wateja wake ili kuendelea kiinufaisha serikali kwa kuwa mtandao huo unamilikiwa na serikali.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa TTCL 4G mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah alisema kuwa wananchi wanapaswa kuunga mkono mtandao huu wa kizalendo ambao unahuduma nyingi nzuri.

  “Ukiangalia utagundua kuwa mtandao wa TTCL inahuduma ya pesa ambazo zina makato madogo sana kulinganisha mitandao mingine hivyo nawasiii wananchi wa mkoa wa iringa kuanza kutumia huduma za mtandao huu wa kizalendo” alisema Abdallah

  Abdallah aliwataka wananchi kuanza kuvithamini vitu vya wazawa kwanza ili kuleta maendeleo ya maendeleo kwenye kampuni na taasisi za kizalendo  ndio maana mkuu wa mkoa wa Iringa na wakuu wa wilaya wote wa mkoa huu wameamua kujiunga na mtandao huu wa TTCL.

  “Mimi,mkuu wa mkoa ,mkuu wa wilaya Richard Kasesela  na viongozi wengine wamejiunga na mtandao huu wa TTCL 4G ambao unakasi kubwa kwenye upande wa internet na huduma nyingine ziboreshwa na zimekuwa bora sana” alisema Abdallah

  Aidha Abdallah alisema kuwa kampuni hii ya kizalendo imekuwa ikihudumia jamii kwa njia tofautitofauti za kimaendeleo hasa kwa kuunga mkono kwenye michezo mbalimbali hapa nchini.

  “Kama unakumbuka hivi karibuni kulikuwa na mshindano ya Ritta kabati challenge cup ambapo kampuni hii ya kizalendo ilichangia zaidi ya milioni mbili kufanikisha kuendesha mashindano hayo hivyo utagundua kuwa TTCL imekuwa ikirudisha faida kwa wananchi”alisema Abdallah

  Abdallah alisema kuwa TTCL wana bando kuwa kwa gharama nafuu hivyo naomba wananchi wanaopenda kutumia mitandao ya kijamii wanapaswa kujiunda na mtandao huu kwa kuwa unagharama nafuu na internet yake inakasi nzuri kulingana na mitandao mingine.

  Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya TTCL nchini Waziri Kandamba alisema kuwa TTCL imekuja kuboresha maisha ya watanzania wanaopenda kutmia mitandao ya simu kwa kuwa wamejipanga kufanya kazi kishindani tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

  “Leo tumefanya uzinduzi wa mtandao wenye kasi kubwa 4G LTE ambao utakuwa unakata kiu kwa wanaopenda kutumia mitandao ya kijamii kwa kuwa tumeboresha huduma zetu zote katika mtandao huu” alisema kandamba

  Kandamba aliwataka watanzania kuvitumia na kuvithamini vitu vya kwao kama makampuni ya wazao  ndio maana TTCL ilirudi kuwatumikia watanzania kwa kuboresha huduma zetu zote.

  “Wewe jaribu kutumia mtandao wetu wa TTCL utapata jibu zuri kwa kiasi gani tumeboresha huduma hii ambayo watanzania wengi waliikosa kwa muda mrefu hivyo nawaomba watanzania kujiunga na mtandao wetu wa TTCL wenye huduma bora” alisema Kandamba.
   Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akizungumza wakati wa uzinduzi wa mitandao wa TTCL 4G LTE katika Mkoa wa Iringa eneo la ofisi za kampuni hiyo.
   Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akizindua huduma ya mtandao wa simu wa TTCL kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa bi Amina Masenza
  Picha ya Pamoja.


  0 0

  Shirika la Rafiki Social Development Organization – SDO la mkoani Shinyanga leo Jumanne Agosti 15,2017 limezindua Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili katika kata 30 kwenye halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Shinyanga Vijijini na Kahama Mji.

  Uzinduzi wa mradi huo umefanyika katika ukumbi wa Ibanza Hotel Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro. 

  Akizungumza wakati wa kuzindua mradi huo,Matiro alilitaka shirika hil0 kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa jadi la sungusungu,serikali,viongozi wa dini,kimila na wananchi. “Niwapongeze sana Rafiki SDO kwa kupata mradi huu muhimu kwa ajili ya ulinzi wa watoto,sote tunatambua kuwa vitendo vya ukatili wa watoto vimekithiri katika jamii,serikali pekee haiwezi kumaliza vitendo hivi,lazima tushirikiane ili watoto wetu wawe salama”,alisema Matiro. 

  “Natamani kusikia mashirika yanajitokeza kuanzisha miradi kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ulawiti wanavyofanyiwa watoto wetu,taarifa nilizo nazo ni kwamba baadhi ya watoto wa kiume waliopo katika shule za msingi wanafanyiwa mchezo mbaya wa kulawitiwa,tena wanafanyiwa na watu wazima,hili halikubaliki lazima tushirikiane kumaliza tatizo hili”,aliongeza Matiro. 

  “Naomba mashirika yanayojihusisha na masuala ya watoto yajitokeze na kuanzisha miradi ya kusaidia watoto wanaolawitiwa,tunapaswa kuwalinda watoto hawa,kinachotakiwa ni ushirikiano japo changamoto katika kesi za ukatili ni wazazi na walezi kumaliza kesi kienyeji”,alisema Matiro. 

  Katika hatua nyingine aliwataka wazazi na walezi kutoa ushirikiano katika vyombo vya dola pale panapotokea watoto wamefanyiwa vitendo vya kikatili na kunyimwa haki zao. 

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Mkurugenzi wa Shirika la RAFIKI SDO,Gelard Ng’ong’a alisema mradi huo unatekelezwa na Shirika la Rafiki SDO kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la kuhudumia watoto “Save The Children International” kwa hisani ya shirika la Maendeleo la nchini Sweeden – SIDA. 

  Ng’ong’a Mradi huo unalenga kumlinda mtoto na kuhakikisha watoto wanapata haki zao pamoja na kuwajengea uwezo wa kupaza sauti zao ili kuhoji haki hizo kutoka kwa wazazi, viongozi na wadau wengine wanaohusika. 

  “Kupitia mradi huu,tunaamini vitendo vya ukiukwaji wa haki za watoto vilivyokithiri mkoani Shinyanga vitapungua kwa asilimia 20% katika kata 30 za Manispaa ya Shinyanga, Shinyanga vijijini na Mji wa Kahama ifikapo mwezi wa Novemba mwaka 2018”,alisema Ng’ong’a. 

  Aidha alisema mradi huo utasaidia kuongeza utumiaji wa mifumo rasmi kama vile ofisi za ustawi wa jamii, dawati la jinsia na watoto pamoja na vituo vya huduma viliyowekwa na serikali na wadau wengine katika kumlinda mtoto na haki zake. 

  “Tunatarajia pia ongezeko la ushiriki wa watoto katika kutoa maamuzi, kuhoji na kudai haki zao kutoka kwa wazazi na wadau wengine wanaopaswa kuwahudumia watoto”,aliongeza Ng’ong’a. 

  Kwa upande wake Meneja Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala kutoka shirika la Rafiki SDO,Shangwe Kimath alisema ili kufanikisha mradi huo ipasavyo wamejipanga kutoa mafunzo na kuongeza uelewa wa ulinzi wa mtoto kwa jamii, kuhamasisha ushirikishwaji wa mtoto na uragbishi na ushawishi. 

  “Pamoja na mambo mengine tumeandaa kampeni za kuhusisha wanaume katika malezi na makuzi ya watoto na kuwajengea uwezo viongozi na watendaji wa serekali za mitaa, wazazi, waalimu na kamati za ulinzi wa mtoto juu ya ulinzi wa mtoto na utawala wa haki za watoto”,alieleza Kimath. 

  Naye Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima alisema mradi huo unatekelezwa katika mikoa mitatu nchini Tanzania,ambayo ni Shinyanga,Dar es salaam na Songwe. “Tunaishukuru serikali kwa kuendelea kushirikiana nasi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali,tunampongeza mkuu wa wilaya Josephine Matiro kwa ushirikiano wa kutosha ambao amekuwa akitupatia,suala la ulinzi wa motto linahitaji ushirikiano wa wadau wote”,aliongeza Malima. 

  Mradi huo utatekelezwa katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kwenye kata ya Ngokolo, Ndembezi , Masekelo Ndala, Kambarage, Ibinzamata Chamaguha, Chibe, Lubaga na Old Shinyanga na katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ni kwenye kata ya Salawe, Lyamidati, Mwenge, Mwantini, Tinde, Didia, Solwa, Iselamagazi Lyabusalu na Lyabukande. 

  Kwa upande wa halmashauri ya Mji wa Kahama mradi utatekelezwa kwenye kata ya Mwendakulima, Nyihogo, Kagongwa, Nyasubi, Majengo, Kahama mjini, Mhongolo Zungomela, Nyandekwa na Busoka. 
  Wa kwanza kushoto ni Afisa Ustawi wa jamii Manispaa ya Shinyanga John Nhabi,akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,Mkurugenzi wa Shirika la RAFIKI SDO,Gelard Ng’ong’a na Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima (wa kwanza kulia) wakiwa katika ukumbi wa Ibanza Hotel Mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala utakaotekelezwa na Shirika la Rafiki SDO kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la kuhudumia watoto “Save The Children International” kwa hisani ya shirika la Maendeleo la nchini Sweeden – SIDA. 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza ukumbini. 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo. 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini. 
  Wadau wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa mradi huo. 
  Wadau mbalimbali wa masuala ya watoto kutoka kata 30 za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini,Manispaa ya Shinyanga na Kahama Mji ambako mradi huo utatakelezwa 
  wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini. 
  Mkurugenzi wa Shirika la RAFIKI SDO,Gelard Ng’ong’a akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala. 
  Mkurugenzi wa Shirika la RAFIKI SDO,Gelard Ng’ong’a akieleza namna mradi huo utakavyosaidia kupunguza vitendo vya kikatili dhidi ya watoto. 
  Mkurugenzi wa Shirika la RAFIKI SDO,Gelard Ng’ong’a akizungumza ukumbini ambapo alisema ili kufanikisha mradi huo pia panahitajika bajeti kutoka serikalini kwa ajili ya watoto. 
  Wadau wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini. 
  Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akieleza namna wanavyoshirikiana na serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika jamii. 
  Wadau wakiwa ukumbini. 
  Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akisisitiza jambo. 
  Afisa Ustawi wa jamii Manispaa ya Shinyanga John Nhabi akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo ambapo alisema jitihada za maksudi zinahitajika ili kukabiliana na tatizo la watoto wa kiume kulawitiwa na watu wazima lakini pia wao kwa wao. 
  Maafisa watendaji wa kata wakiwa ukumbini. 
  Meneja Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala kutoka shirika la Rafiki SDO,Shangwe Kimath akitambulisha mradi huo ukumbini. 
  Mratibu wa Masuala ya Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka shirika la Rafiki SDO,Alex Enock akichangia hoja ukumbini 
  Diwani wa kata ya Lubaga,Mchungaji Obeid Jilala (Chadema) akichangia hoja ukumbini ambapo alihamasisha mashirika yanayotekeleza miradi katika jamii kushirikiana na viongozi wa maeneo husika ipasavyo. 
  Diwani wa kata ya Ndembezi,David Nkulila (CCM) akichangia hoja kuhusu namna ya kulinda haki za watoto ambapo alisema Mikopo imekuwa ikiwanyima haki watoto pale panapotokea wazazi/wakopaji kufirisiwa mali nyumbani huku akisisitiza suala la umiliki wa mali katika familia linahusu pia watoto,hivyo wazazi wanapofirisiwa watoto wanapoteza haki zao.
  Diwani wa kata ya Kambarage,Hassan Mwendapole ( CCM) akichangia hoja ukumbini ambapo aliwataka wazazi na walezi kuwajali watoto wao kwa kuwapatia mahitaji muhimu ili kuwaepusha kutojiingiza katika vitendo viovu. Mwendapole aliwataka wazazi kuwanunulia watoto wao nguo za ndani 'Chupi' kwani kutokana na kujisahau kwao kunasababisha watu wenye tabia mbaya kutumia mwanya huo kuwarubuni watoto matokeo yake wanajiingiza katika mahusiano ya kimapenzi wangali wadogo hatimaye wanapata ujauzito na hata kuambukizwa magonjwa ya yanayotokana na ngono. 
  Diwani wa kata ya Ngokolo,Emmanuel Ntobi akichangia hoja ukumbini ambapo alisisitiza serikali kutenga bajeti kwa ajili ya watoto,huku akibainisha kuwa halmashauri ya wilaya imekuwa ikidai kutenga bajeti lakini haiwafikii walengwa. 
  Mwanafunzi Zuhura Juma kutoka shule ya msingi Ushirika katika manispaa ya Shinyanga akizungumzia umuhimu wa watoto kupewa haki zao. 
  Mwanafunzi Jenifa Maganga kutoka shule ya Msingi Bugoyi A katika manispaa ya Shinyanga akichangia hoja ukumbini ambapo alisisitiza umuhimu wa wazazi kujali watoto wao na kuwasikiliza. 
  Mwanafunzi,Faraja Kichele kutoka shule ya Msingi Ushirika katika manispaa ya Shinyanga akichangia hoja ukumbini. 
  Mwalimu Faustina Mram kutoka shule ya msingi Bugoyi A akichangia hoja ukumbini kuhusu namna ya kuwalinda watoto. 
  Afisa Maendeleo manispaa ya Shinyanga,Mwanamsiu Dossy akichangia hoja ukumbini. 
  Kaimu Afisa Elimu Msingi wilaya ya Shinyanga,Beatrice Mbonea akichangia hoja ukumbini. 
  Diwani wa kata ya Kizumbi Reuben Kitinya akizungumza wakati uzinduzi wa mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala. Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

  0 0

  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza na Viongozi Mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake Mara baada ya kuzuru katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akisaini kitabu cha wageni Mara baada ya kuzuru katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
  Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akionyesha ilani ilani ya CCM mwaka 2015-2020 na maelekezo ya namna ya utekelezaji wakati akizungumza na Viongozi Mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake Mara baada ya kuzuru katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
  Katibu Tawala wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba Ndg Abdallah Rashid Ali akielezea namna Ofisi ya Mkuu wa Wilaya inavyotekeleza ilani ya CCM mbele ya Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Mara baada ya kuzuru katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.

  Na Mathias Canal, Kusini Pemba

  Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kwa kauli moja Umewataka watumishi wa Umma kote nchini Kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015-2020 kwa kutenganisha Siasa na shughuli za maendeleo. 

  Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 15, 2017 na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) alipokuwa akizungumza na Viongozi Mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake Mara baada ya kuzuru katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.

  Shaka ametilia mkazo zaidi kwa kuwataka Watumishi wa Serikali kutenganisha siasa na Majukumu ya kazi kwa Wananchi ili kuwaletea maendeleo pasina kuwabagua kwa dini, kabila ama utofauti wa itikadi za vyama vya kisiasa.

  Alisema kuwa litakuwa Jambo la aibu tena lisilovumilika kwa Viongozi wa Umma kushughulika na Mambo ya siasa kwani hizo Ni kazi za vyama vya siasa ambavyo hata vyama vya siasa vina mipaka katika kufanya siasa.

  Shaka Alisema kuwa watumishi wa Umma wamepewa dhamana kubwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli hivyo Ni matarajio ya Chama Cha Mapinduzi CCM na Serikali, watumishi wote Kusimamia na kuwajibika ili Kutekeleza imara ilani kwa utayari.

  Alisema kuwa ilani ya CCM imeielekeza Serikali kufanya Mambo mengi ya Maendeleo ambayo kwa asilimia kubwa tayari yameanza kutekelezwa kwa usimamizi mzuri wa Rais Magufuli.

  Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo chini ya CCM hivyo kila kiongozi aliyeajiriwa na Serikali Ana jukumu moja kubwa la Kutekeleza ilani kwa umakini mkubwa kwa maslahi mapana ya Taifa.

  "Kama kuna mtumishi asiyefanya hivyo basi ni wazi kuwa hastahili kuendelea kuwa kwenye nafasi yake"

  "Tunakuwa na mipango mingi lakini utekelezaji wake unasuasua kwa kisingizio Cha bajeti ndugu zangu ifike Wakati tuwe na bajeti inayotekelezwa na itekelezwe kwa umakini, uangalifu na weledi Mkubwa" Alisema Shaka

  Alisema kuwa watumishi wa serikalini wanapaswa kubainisha vyema Mipango ya muda mfupi na muda mrefu kwa manufaa ya Wananchi pasina kuwabagua zaidi ni kukubali kuwa wawajibikaji wazuri.

  Katika Hatua nyingine UVCCM Taifa imempongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe Dkt Ali Mohed Shein kwa maendeleo endelevu aliyoyafanya katika kipindi Chake tangu amekuwa Rais wa Zanzibar kwa kuimarisha Huduma za uwanja wa Ndege, uchumi wa Pemba umeimarika, fursa za uwekezaji sio Kama kipindi kilichopita.

  Umoja huo umesisitiza kuwa Ni vyema wasaidizi wa Rais kumsaidia kwa vitendo sio maneno kwani Ni Lazima Viongozi kuwa na uthubutu na uwajibikaji.

  MWISHO.

  0 0

  Natoa pole kwa wote walioathirika na janga la moto kwa wafanyabiashara soko la Sido. SOKO la sido lilianza kuungua saa 21.32 Hrs jana usiku na kuteketeza mali za wafanyabiashara wa soko la sido.

  Pamoja na kutoa pole niwashukuru wananchi, vyombo vya ulinzi kwa ushirikiano na kazi kubwa YA kudhibiti moto usiendelee kuleta madhara makubwa zaidi.

  Serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Mbeya imeunda kamati  ya kufanya tathmini ya kujua hasara na chanzo cha Moto huo .

  Tunaomba wananchi waendelee kuwa watulivu na watoe ushirikiano kwa kamati hiyo ili tuweze kujua chanzo cha moto na hasara iliyopatikana
  Aidha vyombo vya ulinzi vinaendelea kuchunguza kujua kama moto huo utakuwa umesababishwa na mtu/ watu uchunguzi huo bado unaendelea
  Nirudie tena kuwapa pole wote walioathirika na janga na mungu awatie nguvu ktk kipindi hiki Kigumu
   
  Amos G.Makalla
  Mkuu wa mkoa wa Mbeya

  0 0

  Na Robert Hokororo, Kishapu DC.

  Wananchi wametakiwa kujiunga na Mfuko wa Afya (CHF) iliyoboreshwa ili wapate huduma na kuboresha afya zao na hivyo kuweza kushiriki shughuli mbalimbali za uzalishaji.

  Wito huo ulitolewa jana na Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese wakati akizindua kampeni ya uhamasishaji shughuli za afya wilayani hapa.

  Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo katika kijiji cha Malwilo, Mheshimiwa Nyabaganga Taraba, Kangese aliwataka viongozi wa serikali za vijiji kuonesha mfano kwa kujiunga na mfuko huo mapema.Kangese pia aliwataka viongozi hao kuhamasisha kaya zingine zijiunge ifikapo Oktoba mwaka huu wakiwemo walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF). 

  Alisema huduma hiyo ni muhimu kwa wananchi wasiojiweza na wenye kipato cha chini ambapo kwa sh. 10,000 humuwezesha kuhudumiwa yeye na watu wengine sita katika kaya kwa mwaka mzima.

  Alisema Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya kwa kutengeneza miundombinu, kutoa vifaa tiba na kuongeza wataalamu wa sekta hiyo ili waweze kuhudumia wananchi kwa ufanisi.Katibu Tawala huyo aliongeza kuwa utekelezaji wa mradi wa CHF iliyoboreshwa ulianza rasmi Machi 2016 kwa kuimarisha mfumo wa fedha na uoreshaji dawa na vifaa tiba.

  Aidha, alisema katika wilaya hiyo ni kaya 10,756 zimeandikishwa huku lengo likiwa ni kaya 42,000 ambapo kila mwananchama anapata kadi na matibabu mwaka mzima.Aliwataka watumishi wa afya pamoja na changamoto ya uchache waendelee kuhudumia wananchi kwa kufuata sheria, taratibu na miongozo iliyopo wakati Serikali inaendelea na michakato ya kuongeza wengine.

  Kwa upande wake, mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Dk. Josephat Shani aliwataka wajawazito kuhudhuria kliniki ili kujifungua salama.Alisisitiza umuhimu kwa wanawake kujifungulia katika hosptali ili kupata huduma stahiki pamoja na mtoto na kuwa katika hali ya usalama tofaui na nyumbani.

  Dk. Shani ambaye pia ni mganga mkuu wa wilaya pia aliwataka kufuata maelekezo ya watoa huduma za afya ili kuepuka kupata matatizo yanayoweza kutokea wakati wa kujifungua. 
   Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akizungumza wakati wa kampeni ya afya aliyoizindua kijiji cha Malwilo kata ya Somagedi.
   Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Dk. Josephat Shani ambaye pia mganga mkuu wa wilaya akizunguza wakati wa uzinduzi huo.
   Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Maguja Daniel akitoa neno wakati wa uzinduzi huo. 
   Mratibu wa Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) mkoa wa Shinyanga, Haruni Kasale akizungumzia umuhimu kwa wananchi kujiuna na mfuko wa CHF iliyoboreshwa.
   Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Malwilo wakifuatilia uzinduzi wa kampeni ya afya.
   Ofisa Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wilaya ya Kishapu, Jacob akitoa ufafanuzi kuhusu mradi huo wa CHF.
   Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akizungumza na wananchi katika kijiji cha Malwilo wakati wa uzinduzi wa kamnpeni hiyo ya afya.
  Wananchi wakifuatilia matukio hayo.

  0 0

   

  Raisi wa Mahakama akitambulisha Jaji Matusse kwa Raisi was Guinea Bissau Ikulu. Kushoto wa pili ni Makamu wa Raisi wa Mahakama Jaji Ben Kioko.
   
   Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau Mheshimiwa Jose Mario Vaz ameahidi kuwa, nchi yake itaridhia itifaki iliyoanzisha mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu (AfCHPR) mapema iwezekanavyo .

  Akizungumza na ujumbe wa mahakama hiyo ulioko katika ziara ya kikazi nchini Guinea Bissau, Rais Vaz alisema hatua hiyo inatokana na ukweli kwamba Guinea Bissau ilikuwa miongoni mwa nchi za mwanzo za umoja wa Afrika kutia saini itifaki iliyoanzisha AfCHPR mwaka 1998.

  Katika mazungumzo yake na ujumbe huo ulioongozwa na rais wa AfCHPR mheshimiwa Jaji Sylvain Ore kiongozi huyo wa Guinea Bissau alielezea kuridhishwa kwake na madhumuni ya kuanzishwa kwa mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu na kuongeza kuwa masuala ya haki za binadamu yana umuhimu mkubwa katika kufikiwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi za Afrika na kuwaondoa wananchi wake katika lindi la umaskini na ufukara.

  “Ahadi yangu ni kuhakikisha kuwepo kwa haki za binadamu katika nchi yangu” alisisitiza Rais Vaz.

  Ujumbe wa AfCHPR pia ulikutana na waziri mkuu wa Guinea Bissau Mheshimiwa Umario Sissoco Embalo ambaye alisema mamlaka husika za nchi yake zitaandaa nyaraka zinazohitajika ili kuzipeleka katika bunge la taifa nchini humo kwa lengo la kuridhia itifaki iliyoanzisha mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu.

  “Mimi ni muumini mkubwa wa umajumui wa Afrika (Pan-Africanism) na nitafanya kila linalowezekana kuimarisha taasisi za umoja wa afrika” alisisitiza waziri mkuu huyo.

  Rais wa AfCHPR jaji Ore na ujumbe wake ambao umejumuisha Makamu wa rais wa mahakama hiyo Mheshimiwa Jaji Ben Kioko, Mheshimwa Jaji Angelo Matusse na baadhi ya maafisa wa ofisi ya msajili wa AfCHPR pia ulikutana na Jaji Mkuu, waziri wa masuala ya jamii na pia kamisheni ya haki za binadamu ya Guinea Bissau.

  Jaji Ore alisema ilikufanikisha malengo ya mahakama na pia kuimarisha mfumo wa haki za binadamu barani Afrika nchi nyingi za umoja wa afrika hazina budi kuridhia itifaki iliyounda AfCHPR kwa mujibu wa kifungu cha 34(6) na kutoa tako rasmi la kutambua na kukubali a mamlaka ya mahakama kuweza kupokea kesi za watu binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs)

  Hadi sasa ni Nchi 30 tu kati ya nchi 55 wanachama wa AU ndio zimeridhia itifaki husika.

  AfCHPR yenye makao yake makuu jijini Arusha iko nchini Guinea Bissau kwa ziara ya kikazi ya siku 2 ili kukutana na viongozi na wadau mbalimbali kwa lengo la kuitangaza mahakama hiyo.

  0 0

  Group CEO, United Capital Plc. Oluwatoyin Sanni (left); Founder, The Tony Elumelu Foundation, Mr. Tony Elumelu; and Director General of NAPTIP, Julie Okah-Donli during the visit of DG to the foundation in Lagos on Thursday;
  Tony Elumelu: Human Trafficking Is Evil, It Strips Our Youth Of Dignity And Denies Them Opportunity
  Tony Elumelu Foundation commits to support National Agency for the Prohibition of Trafficking in Persons (NAPTIP).

  In recognition of the growing concerns around human trafficking in Africa, The Tony Elumelu Foundation (TEF), an African founded and funded 21st century philanthropic organization committed to youth empowerment and entrepreneurship development, hosted the Director General of Nigeria’s National Agency for the Prohibition of Trafficking in Persons (NAPTIP), Julie Okah-Donli.
  According to Okah-Donli, UNESCO ranks human trafficking as the third most lucrative criminal enterprise in Nigeria. Thus, agencies like NAPTIP need good laws, sustained funding and equally important, critical support from local and global stakeholders to execute the urgent war against human trafficking.  “We can no longer wait for government alone to fight this war. 

  Many victims are on standby, anxious to be fully reintegrated into society. At the agency, we are desperate for assistance to empower and rehabilitate these millions of victims in need. Thus, we are identifying and approaching organizations like the Tony Elumelu Foundation (TEF) for support.”

  She continued: “We need to refurbish and rehabilitate our existing shelters, facilitate periodic provision of food, clothing and medical consumables and shelter for victims. We also need assistance in the development of standard skills’ acquisition centres in strategic locations for the training of vulnerable persons, as well as rescued victims.”

  In response, Mr. Tony Elumelu CON, Founder, Tony Elumelu Foundation, commended Okah-Donli for her accomplishments at the agency, including the conviction of over 325 persons, and successful rehabilitation of more than 12,000 victims. He also added that she was a former staff of leading pan-African bank, United Bank for Africa (UBA).  “She is an alumna of the United Bank for Africa (UBA), Africa’s global bank, thus we are not surprised at what she has become. We predicted that she will attain such great heights because of the passion she has always had for human trafficking,” he said
  On behalf of the Foundation, he pledged commitment to the war against human trafficking. 

  “We support what you are doing and we stand behind you. The Tony Elumelu Foundation believes in the empowerment of our youths and as we all know, they cannot be empowered if they are not free.” “We stand with you in eradicating human trafficking in Nigeria and will engage extensively with you as you work to restore dignity to mankind, protect the dignity of our youth and ensure no one can take undue advantage of them.”

  He also made an appeal to the government to increase budgetary funding to the cash-strapped agency. “I call on the Federal Government to make more resources available to support you. As private companies, we pay taxes to the Federal Government and we want to see a more judicious use of the taxes paid.”

  Elumelu also urged other private sector players to join the agency to fight human trafficking, assuring them of the credibility and competency of NAPTIP and its DG whom he could vouch for. “If she succeeds, we will all succeed. Let us come together to make sure our youth, our future leaders, are not trafficked.”

  0 0

   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) pamoja na baadhi ya Viongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakimpongeza Mwanariadha Alphonce Simbu kwa kuibuka mshindi wa tatu ambapo alijinyakulia medali ya shaba. Hafla hiyo ilikuwa ni maalum ya kumpokea yeye pamoja na wanariadha wengine wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere toka nchini Uingereza kwenye Mashindano ya Marathon ya 2017.
    Mwanariadha Alphonce Simbu akiwashukuru Viongozi mbalimbali waliokuja kumpokea na kumpongeza kwa ushindi wake katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka 2017 ambapo aliweza kujinyakulia medali ya shaba.
  Wazazi wa Mwanariadha Alphonce Simbu wakiwaonyesha Waandishi wa habari (hawapo pichani) medali ya shaba aliyoshinda mtoto wao katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka 2017. 
  Mwanariadha Alphonce Simbu akiwaonyesha Waandishi wa habari (hawapo pichani) medali ya shaba aliyoshinda katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka 2017.

  0 0

  Hivi Karibuni, Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda kwa pamoja waliweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga Tanzania. Katika Makala hii pamoja na mambo mengine Mwandishi Said Ameir wa Idara ya Habari- MAELEZO anaeleza kwani nini mradi huu ni kipimo cha utayari na ujasiri wa watanzania katika kuchangamkia fursa.

  Mradi huu unaojulikana kama Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) unatekelezwa kwa ubia kati ya washirika wa sekta binafsi na sekta za umma za nchi za Tanzania na Uganda.

  Washirika hao ni Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kampuni ya Taifa ya Petroli ya Uganda (UNOC), Kampuni ya Mafuta ya Total ya Ufaransa, Kampuni ya TULLOW yenye makao makuu yake London nchini Uingereza na Kampuni ya China National Offshore Oil Company (CNOOC).

  Bomba ambalo litagharimu dola za kimarekani 3.5 bilioni, sehemu yake kubwa yaani kilomita 1,115 kati ya kilomita 1,445 litajengwa katika ardhi ya Tanzania na kupita mikoa 8, wilaya 24 na vijiji 184.

  Kutokana na hali hiyo, inaelezwa kuwa, mradi huu wakati wa ujenzi na utakapokamilika, utatoa na fursa nyingi za kiuchumi ambazo zitasaidia sana kuchangamsha shughuli za kiuchumi hivyo kuchangia ukuaji uchumi na kuinua kiwango cha maisha ya watanzania kwa namna mbalimbali.

  Mradi huu ni mfano wa ushirikiano kati ya nchi za Tanzania na Uganda na kwa upande mwingine ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na sekta za umma katika nchi hizi. 

  Katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake, mradi huu utahitaji ushiriki wa sekta binafsi katika nchi zote mbili na wakati mwingine hata taasisi nyingine za umma ambazo zinatoa huduma zitakazohitajika na mradi.

  Kwa hiyo, wakati tukisifia kuwa ni mfano wa mradi wa ubia wa sekta ya umma na sekta binafsi katika nchi zetu, watanzania hawana budi kuelewa kuwa wana wajibu mkubwa wa kuzitumia vyema fursa za mradi huu.

  Kwa Tanzania, mradi huu unaweza kuonesha picha halisi ya ushirikiano wa sekta hizo kwa kuzingatia namna makampuni na taasisi za humu nchini zitakavyoweza kushiriki na kufanikisha mradi huu.

  Kwa maana nyingie ni mradi ambao unaweza kutumika kupima utayari, umakini, uwezo na ujasiri wa watanzania katika kuchangamkia fursa za kiuchumi.

  Kama alivyoeleza Rais Magufuli wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kuwa katika mradi huu, Serikali imesamehe mambo mengi ili uweze kutekelezwa kwa kuishirikisha Tanzania. Wataalamu wa nchi walichambua na kupembua hadi kubaini kuwa kusamehe huko kutafidiwa na fursa nyingi zitakazoletwa na mradi huu.

  Kwa maana hiyo bila ya watanzania kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha wanazitumia kadri itakavyowezekana fursa hizo uamuzi huo wa Serikali kusamehe hivyo ilivyovisamehe hautakuwa na maana yeyote.

  Kuja kwa mradi huu Tanzania, watanzania hawana budi kuipongeza Serikali chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa jitihada kubwa kwa kutumia ushawishi wa kisiasa, kidiplomasia, uchumi na ukaribu wa viongozi wa nchi hizo mbili pamoja na hoja nyingine hadi kufanikisha mradi huu kuja Tanzania.

  Jitihada hizi ni kielelezo cha dhamira ya kweli iliyonayo Serikali ya Awamu ya Tano ya kutafuta kila aina ya fursa za kiuchumi ambazo zitasaidia kutimiza ahadi zake kwa watanzania ya kujenga Tanzania yenye uchumi imara.

  Serikali imejitwika mzigo mkubwa wa kushiriki katika kutekeleza mradi huu mkubwa wa aina yake lakini imefanya hivyo kwa kuamini kuwa watanzania wako tayari na wako imara kuupokea kwa hali na mali.

  Imeelezwa mara kwa mara kuwa mradi huu utaliingizia taifa mapato makubwa, utaleta tekinolojia na utalaamu na fursa za kiuchumi ambazo watekelezaji wake kwa kiwango kikubwa ni kutoka sekta binafsi. Kwa mnasaba huo, Serikali hapa imefanya zaidi ya wajibu wake ambao ni wa kujenga mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji.

  Wale wahenga wa Cambrigde walisema“give us the tools and lets finish the job” na hivi ndivyo ilivyofanya Serikali kwa mradi huu. Imeleta mradi na kufungua fursa tele ambazo watanzania wanapaswa kuzitumia kujenga kiuchumi wao binafsi na uchumi wa taifa.

  Haitakuwa na maana hata kidogo katika ngazi ya serikali na katika ngazi ya Mtanzania mmoja mmoja kufika wakati fursa za mradi huu kuchukuliwa na wageni kwa sababu zozote na katika mazingira yeyote yale. Ikifikia hatua hiyo watanzania watakuwa wamewaangusha viongozi wao.

  Hii kutokana na mazingira ambayo Serikali imeyaweka kuwawezesha watanzania kushiriki katika sekta ya mafuta na gesi asilia. Mbali ya kupitisha Sheria ya Local Content Act ya 2015 ambayo inasisitiza ushiriki wa watanzania lakini zaidi dhamira ya kweli ya kisiasa iliyonayo uongozi wa Serikali ya kuhakikisha kuwa watanzania wanafaidika ipasavyo na mradi huu.

  Ni jambo la kutia moyo kuona kuwa baadhi ya Taasisi za Serikali na za sekta binafsi zimeshaanza maandalizi au zimejitokeza kuwaandaa watanzania kuchangamkia fursa hizo na kuhakikisha wanazitumia vyema.

  Miongoni mwa taasisi hizo ni Jumuiya ya Watoa Huduma katika Sekta ya Mafuta na Gesi (ATOGS) ambayo inawakusanya pamoja watoa huduma katika sekta hiyo ambapo lengo lake kubwa ni kuhakikisha kuwa fursa za mradi huo zinatumika ipasavyo kwa manufaa ya muda mfupo na mrefu ya watanzania.

  ATOGS, kama taasisi nyingine zitakazoelezwa baadae, imeonesha mfano wa utayari kwa kuwa na mpango mkakati wake ambao unalenga kuwawezesha watoa huduma wa humu nchini wanapata fursa hizo kwa kuwasaidia kwa namna mbali mbali tangu hatua za awali za kuwania fursa hizo hadi utekelezaji wake.

  Makamu Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Abdulsamad Abdulrahim katika moja ya mikutano na waandishi wa habari alisema taasisi yake imejipanga kuwajengea uwezo watoa huduma na kutoa wito watoa huduma hao kwa waliokuwa bado hawajajiunga wajiunge na taasisi hii kwa minajili ya kufaidika na uwezeshaji wao.

  Halikadhalika, Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) nalo linaeleza kuwa limejidhatiti kuhakikisha kuwa watanzania watakaobahatika kupata fursa za kutoa huduma katika mradi huo hawashindwi kwa kukosa fedha za kutekeleza kandarasi zao.

  “Hatutaki kusikia mtanzania amekosa fursa hii kwa sababu ya kukosa fedha …ukibahatika njoo kwenye Baraza tutakushauri… Serikali ina mifuko 17 yenye fedha za kutosha kukuwezesha” anaeleza Mkurugnezi wa uwezeshaji wa NEEC Bwana Edwin Chrisant.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Bwana Godfrey Simbeye aliwaambia waandishi wa habari kuwa taasisi yake imejipanga kuhakikisha kuwa mikataba ya kandarasi itakayofikiwa inazingatia maslahi ya pande zote na utekelezaji wake unafanyika kulingana na vipengele vya mikataba.

  Dhamira hizi zilizoelezwa na taasisi hizi muhimu nchini, hapana shaka yoyote kuwa ni habari njema inayoashiria matumaini makubwa na kuonesha sasa watanzania wameamka na wamedhamiria kujenga Tanzania mpya kwa kila mmoja kwa nafasi yake kuyatumia mazingira yaliyopo kujenga uchumi wa taifa.

  Kama kweli taasisi hizi zitatekeleza yale ziliyojipangia ikiwemo kuwapatia watoa huduma msaada wa kitaalamu, huduma za kisheria, kifedha, viwango na vigezo katika manunuzi, utaalamu, kuwaunganisha na wabia, kuwajengea uwezo vijana wasomi ili waweze kushika nafasi zitakuwa zimetoa msaada mkubwa kwa nchi.

  Kwa hakika mradi huu kama ilivyoelezwa awali utakuwa kigezo muhimu kupima utayari, umakini na uwezo wa sekta binafsi kuchangamkia fursa zinapotokea na mafanikio ya ushiriki wa sekta hiyo huenda ukawa mwanzo mzuri wa kuupa mgongo utamaduni ulizoeleka wa watanzania kulalamika hususan kuilalamikia Serikali kuwa haiwapi fursa kama hizi.

  Wahenga walisema “shike shike na mwenyewe nyuma” kwa hili Serikali zimefanya wajibu wake sasa mpira uko kwa wadau katika sekta binafsi kuucheza kwa zitumia fursa na ni vyema kukumbuka kuwa “mso matendo hula uvundo” hivyo watanzania wachangamkie fursa wasije wakajikuta karamu imekwisha ‘wakaramba vyungu.

   Ni vyema pia kutanabahisha kuwa fursa za mradi huu haziko kwa watoa huduma kama hao pekee ambao wao ni wafanyabiashara na wataalamu ambao tayari wanajielewa, wana uwezo na wako katika sekta hiyo hivyo tunaweza kusema wana angalau uzoefu.

  Lakini ukweli hi kuwa fursa za mradi huu zimetapakaa kila mahala katika ngazi mbali mbali kuanzia wakulima wa jembe la mkono, wafugaji wadogo wadogo, mafundi mchundo, hadi vibarua wa ujenzi. Hivyo taasisi zinazohusika zinapaswa pia kuliangalia kundi hili kubwa na kuhakikisha linashiriki vyema.

  Hii ni kwa sababu, inapozungumziwa ajira elfu kumi na ajira nyingine zaidi ya elfu thelathini nyingi zinawagusa watanzania wa kundi hili. Ikumbukwe kuwa kundi hili ambalo ndilo litakalokuwa karibu na mradi ndilo litakalokuwa la kwanza kulalamika pindi litakapokosa fursa na kujikuta halina namna ya kushiriki na kufaidika.

  Utekelezaji mzuri na wenye ufanisi wa mradi huu kwa kushirikisha sekta binafsi nchini utakuwa kigezo cha kufungua milango kwa miradi mingine mikubwa ya aina hii humu nchini.

  Watanzania hawana budi kumpongeza Rais Magufuli kwa jitihada zake za kujenga Tanzania Mpya yenye matumaini mapya. Hakika Tanzania yenye uchumi wa kati na ya viwanda inawezekana, kama kila mmoja atatimiza wajibu wake.

older | 1 | .... | 1339 | 1340 | (Page 1341) | 1342 | 1343 | .... | 1904 | newer