Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

MAHAKAMA YAIMARISHA HAKI ZA WATOTO KWA VITENDO

$
0
0
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akikata utepe kuzindua Mahakama ya Watoto (Juvenile Court) leo jijini Mbeya. Hii ni Mahakama ya Pili ya Watoto nchini Tanzania baada ya ile iliyoko Kisutu Jijini Dar es salaam. Mahakama hii imejengwa kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF).
Mwakilishiwa UNICEF nchini, Stephanie Shanler akizungumza wakati wa Hafla ya uzinduzi wa Mahakama hiyo.
KaimuJajiMkuuwa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim JumaakifunguaPaziakuashiriauzinduziwa Mahakamaya Watoto (Juvenile Court) leojijiniMbeya. KatikatiniMwakilishiwa UNICEF nchini, Stephanie ShanlernakushotoniJajiKiongoziwaMahakamaKuuya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali.


……………………………………






Na Lydia Churi-Mahakama

Mahakama ni moja kati ya Mihimili mitatu ya dola wenye jukumu la msingi la kutoa haki sawa kwa wote na kwa wakati. Mhimili huu hufanya kazi ya kutafsiri Sheria mbalimbali zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwapatia wananchi haki. Kupitia Mpango Mkakati wake wa miaka mitano, Mahakama ya Tanzania imeendelea kusimamia haki za Watoto kama zilivyo haki nyingine wanazostahili kuzipata wananchi wa Tanzania.

UtekelezwajiwahakizaWatoto zilizoainishwakatika mikatabambalimbali yakikandana Kimataifa na kupewa nguvu ya kisheria kupitia Sheria ya Mtoto namba 21yamwaka2009,kunahitajiushirikianobainayaTaasisina wadau wa haki za watoto. Katika kulinda haki za watoto wa Tanzania, hivi karibuni, Mahakama ya Tanzania ilizindua Mahakama ya Watoto (Juvenile Court) katika jiji la Mbeya na kufanya idadi ya Mahakama hizo kufikia mbili hapa nchini. Mahakama nyingine ya Watoto iko Kisutu jijini Dar es salaam.

Maendeleo Endelevu hupatikana kwakuzingatia misingi ya hakiza Watoto

Kwa kutambua umuhimu wa watoto kuwa ni uhai wa taifa lolote,Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) ilichukua hatua za makusudi kuhakikisha haki za kisheria za watoto zinalindwa kwa kujenga jengo la Mahakama ya Watoto jijini Mbeya. Jengo hili linakuwa ni la pili maalum kujengwa kwa shughuli za Mahakama ya watoto pekee kwa Tanzania bara. Akizindua jengo hilo hivi karibuni, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alisema endapo haki za Watoto zitadharauliwa kwa mapanayakesasa,basi azmayamaendeleo endelevu ya nchi hapo baadaye, itakuwa hatarini.

AkinukuuandikolaShirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), kuwa“Maendeleo Endelevu yanaanza na kukamilika kwamisingi ya watoto kuwa salama,wawe ni wenye afyabora na waliopata elimu bora” (Sustainable Development starts and ends with safe, healthy and well-educated children- UNICEF, May 2013). Katika nenolakelautangulizikatikaandikohilo, AnthonyLake,Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF aliandika kuwa:Hakizawatotona afya yaonjema, lazimaipewe kipaumbele katika maandalizi ya ajendayamaendeleoendelevuya baadayamwaka2015. Uwekezaji kwa manufaa ya watoto ni njiaborayakufutaumaskini,kuongezakasiyakuchanua kwa manufaa kwa wote.” Alisema andiko hilolinatukumbusha kuwa ustawi wa Watanzania unaanza na Ustawi wawatoto.

Ustawi wa watanzania unaanza na ustawi wa watoto

Kaimu Jaji Mkuu aliendelea kusema kuwa maana ya ustawi wa watanzania unaanza na ustawi wa watoto ni kwamba tayari Katiba imetamka kuwa lengo kuu na jukumu la Serikali ni ustawi wa wananchi na ustawi huo wa wananchini lazimaujengewe misingi imara ya ustawi wa watoto wa leo.

Alisema jamii ya watanzania bado inayo mengi ya kufanya ili kuendeleza asilimia 50 ya wananchi wake ambao wana umri wa miaka 18 na chini ya miaka hiyo. Alisema,kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwezi Agosti mwaka 2012, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikuwa na idadi ya watu milioni 44,928,923 na kati ya hao, watoto wenye umri wa kuanzia miaka 0 hadi 17ni asilimia 50.1

Mikataba ya Haki za Watoto iliyoridhiwa na Tanzania 

Kutungwa kwa Sheria ya Mtoto namba 21 ya mwaka 2009 nchini Tanzania kunatokana na mikataba mbalimbali ya kimataifa inayotambua na kulinda haki za Watoto ambayo Tanzania iliridhia. Baadhi ya Mikataba hiyo ni Mkataba wa KimataifawaHakizaMtoto (UNConvention on the Rights of the Child -UNCRC), Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto (African Charter on the Rights andWelfareoftheChild-ACRWWC). Mikataba mingine ni ule wa United Nations Standard Minimum Rules for theAdministration of Juvenile Justice (Beijing Rules) na United Nations Guidelines for the Prevention of JuvenileDelinquency (The Riyadh Guidelines).

Matokeo Ya Kutungwa Kwa Sheria Ya Mtoto ya mwaka 2009

Tanzania ilitunga Sheria ya Mtoto Namba 21 ya 2009 kwa ajiliya haki, ulinzi na ustawi wa mtoto. Aidha, Sheria hii imekusanya mapendekezo yoteya ndani yanchi, ya kikanda naya kimataifa kuhusumaboreshoyahaki na maslahi mapana ya mtoto na kutoa nguvu yakisheria. Baada yakutungwakwaSheria hii, mihimili yadolaimepewa majukumu ya kutekeleza na kuwajibika. Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania anasema kwa upande wa mhimiliwaMahakama,inategemewaMahakamayaWatotoisaidiekuwajibikanakutekelezaSheriayaMtoto.
Alisema kunamaeneokadhaakatikaSheriayaMtotoambayo yanasimamiwanamamlakanyingine.Pamojana ukweli huo,badoMahakamaya Watotoinawezakutoa ushirikianokwamamlakahizoauamrizamahakamazikasaidiautendajiwa mamlaka hizo, kwa mfano; mazingira mbalimbali ambayo yameainishwa na SheriaNamba 21 ya 2009 kuwa ni hatarishi kwa mtoto kama vile uyatima, kutelekezwa, kuteswa, kuzurura, kukinzanana sheria ambapo alisema Mahakama ya Watoto inaweza kutoa tafsiri nakupanua wigo wa “mazingira hatarishi”. Mahakama ya Watoto inaweza kutoa tafsiri nakupanuawigowaUlinzina wajibuwawazazikwamatunzo ya mtoto,matibabu na elimu, sifa za mtu kuwa mlezi na uasili wa mtoto; namna gani Mahakama itawasilisha taarifa mbali mbali aukutumia rejista ya watoto walioasiliwa kwa Msajili waVizazi na Vifo pamoja na uzuiaji wa kazi za udhalilishaji kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka18.

rof. Juma alisemaMahakamaya Watoto inaweza kutakiwa kutoa miongozokuhusu mafunzo ya kazi (apprenticeship) kwa watoto chiniya miaka 18 na kuchunguza mikataba ya mafunzo ya kaziambayo ni kandamizi au yasiyozingatia maslahi ya mtoto. MahakamayaWatoto pia inawezakutoamaamuziambayo yatazikumbushaSerikali zaMitaa wajibuwaowakuboresha ustawi wa watotowaliondani ya mamlakazaSerikali ya Mtaa husika. Mahakama inaweza kuitahadharisha Serikali Kuu naSerikali za Mitaa na Halmashauri wajenge shule maalumza watoto za kutosha. Hii itasaidia Mahakama ya Watotokuwa,badala yaadhabuyavifungogerezani,watotowaliopatikana na hatia watapelekwa. Kwakuanzisha nakuendesha Shule, Mihimili mingine nayo itakuwa inaisaidiaMahakama na Magereza kutekeleza wajibu wao kwamujibu wa Sheria Namba 21 ya 2009.

Aidha Serikali za Mitaa na Serikali Kuu zitakapoanzisha vituo vya kutunzia na kulelea watoto wenye shida ya malezi na Bunge kutoa fedha za kutosha kuendesha vituo hivyo zitaisadia Mahakama kwa kiasi kikubwa, alisema Kaimu Jaji Mkuu na kuongeza kuwa MahakamazaWatotopia zinawezakugunduamapungufukatikaSheriana kupendekezakuwa Waziri mwenyedhamana ya watoto atunge kanuni stahiki.


Sheria ya Mtoto Shirikishi nainataka Ushirikiano

Akizungumzia ushiriki na ushirikishwaji wa Sheria ya Mtoto, Kaimu Jaji Mkuu alisema Sheria kuwa sheria hii imesimamakatika misingi ya ushirikiano baina ya mihimili yote, ushirikianona wadau mbali mbali kama UNICEF na NGOs, taasisi ambazo zinashughulika na masuala ya haki za watoto. Alisema, Sheria hii pia inaitaka Mahakama ichukue uongozi, na kunamasuala ambayo mihimili mingine imepewa nafasi ya uongozi hivyo Mahakama inayo nafasi nzuri ya kuipa uhai sheria hii kwa kuwa kwanza, haki zote stahili zilizoainishwa ndani ya Sheriahii zinamfaidisha mtoto, pili, Sheria hii inapotafsiriwa,paleambapo wanaona kuna “kutofahamika, “utata” wawena ujasiri wa kuielekeza sheria kufikia malengo mazuriyaliyowekwa na Mikataba ya Kikanda na Kimataifa kuhusuhaki ya watoto.

Mahakama pia inayo nafasi nzuri ya kuipa uhai Sheria hii kwa sababu Mahakimu katika Mahakama ya Watotowatakuwa na nafasi ya karibu kabisa kuona namnavifungu mbali mbali vya Sheria hii vinavyofanyakazi, hivyo Kaimu Jaji Mkuu aliwaagiza Mahakama wanaosikiliza kesi za Watoto kuorodheshamapungufu ya Sheriahiina kuhyawasilisha kwenye kamati ya Kanuni ya Jaji Mkuu kwa ajili ya kupendekezakwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu mabadiliko yaSheria.

Akisisitiza juu ya kulinda haki za Watoto, kaimu Jaji Mkuu aliwataka mahakamu wanaosikiliza kesi za Watoto wasome taarifa za Utekelezaji zinazowasilishwa na Tanzania na pia zile zinazowasilishwa na mataifa mengine kuhusu Tanzania ili waweze kugundua mapungufu yetu ya kiutekekezaji ili tuweze kupanga namna ya kuboresha utekekezaji. Mahakimu hao pia wametakiwa kufuatilia haki za Watoto pindi wanapofanya ukaguzi kwenye Magereza.


Ujenzi wa Jengo la Mahakama ya Watoto Mbeya 

Jengo la Mahakama ya Watoto jijini Mbeya lililojengwa kwa ushirikiano kati ya

Mahakama ya Tanzania na UNICEF limegharimu kiasi cha shilingi za kitanzania

Milioni 415 ambapo Mahakama imechangia kiasi cha shilingi milioni 214 na UNICEF shilingi milioni 201. Jengo hili lilianza kutumika April 18, 2017 na linaofisi mbili za Hakimu, Ofisi ya Wakili wa Serikali, ofisi ya Afisa Ustawi wa Jamii na chumba cha Mawakili wa Kujitegemea.

Sababu za Mahakama kujengwa Mbeya 

Jengo hili ambalo ni la pili la Mahakama ya Watoto nchini limejengwa jijini Mbeya kwa kuzingatia upatikanaji wa wadau na huduma zote muhimu za haki kwa mtoto. Huduma hizo ni pamoja na uwepo wa shule ya maadilisho (approved school) ikiwa ni pekee nchini, kuwepo kwa Mahabusu ya watoto mkoani humo, na kuwepo kwa dawati la jinsia la watoto lenye viwango vinavyotambulika lililoanzishwa na Jeshi la polisi. Mahakama hii pia ilianzishwa kutukana na uwepo wa timu ya ulinzi na usalama wa mtoto (child protection team) na kuwepo kwa mfumo wa marekebisho ya tabia kwa watoto (community rehabilitation programme).

Ushirikiano wa Mahakama na UNICEF katika masuala ya haki ya Mtoto

Katika kipindi cha takribani miaka mitano yaani tangu mwaka 2012, UNICEF na Mahakama walishirikiana katika kutengeneza kanuni za Mahakama yaWatoto ikiwa ni matakwa ya kifungu cha 99(1) cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 ambacho kinamtaka Jaji Mkuu kutengeneza kanuni za kutumika katika uendeshaji wa kesi katika Mahakama za Watoto.

UNICEF ilitoa msaada wa kitaaluma (technical support) na fedha katika kuandaa kanuni ambazo zilitangazwa katika Gazeti la Serikali No 182/2016. Uandaaji wa kanuni hizo ulihusisha wadau mbalimbali wa haki za watoto kama Majaji, Mahakimu, Mawakili wa Serikali, Maafisa Ustawi wa Jamii, na Mashirika yasiyo ya kiserikali vinayotoa msaada wa kisheria na vyombo vingine vinavyohusika na masuala ya mtoto.

Aidha, UNICEF imeshirikiana na Mahakama katika kuandaa mafunzo kwa wakufunzi (TOT) juu ya uendeshaji wa kesi za watoto kwa mujibu wa Sheria na kanuni za watoto.Wakufunzi walitoka Mahakamani, Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Idara ya Ustawi wa Jamii.

UNICEF pia imeshirikiana na Mahakama kutoa mafunzo kwa Mahakimu, Mawakili, wa Serikali na Waendesha Mashtaka, Maafisa Ustawi wa Jamii, taasisi zinazotoa msaada wa kisheria na Taasisi zisizo za Kiserikali katika Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani, Mbeya, na Iringa. Aidha mafunzo kwa wadau wote yanaendelea kufanyika katika wilaya mbalimbali kwa kutumia wakufunzi waliopata mafunzo yaliyotolewa na UNICEF na Mahakama.

Kwasasa Mahakama na UNICEF watashirikana katika kutengeneza rejista za maalum mashauri ya watoto, kupitia mwongozo wa mafunzo (Training Manual) kwa kushirikiana na Chuo cha Mahakama Lushoto na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa vitendo (Law School of Tanzania).

Sambamba na hilo kwa mwaka huu wa fedha UNICEF wataendelea kushirkiana na Mahakama katika mpango endelevu wa kutoa mafunzo kwa wadau wote wa haki za Watoto. Pia UNICEF imeonyesha nia ya kushirikiana na Mahakama katika ukarabati mdogo wa Mahakama ili kuziweka katika mazingira rafiki kwa watoto.

Hata hivyo, bado iko haja ya kuongeza idadi ya Mahakama za watoto nchini kutokana na kuwepo kwa kesi za watoto na nyingine ambazo kwa namna moja au nyingine zinawahusisha watoto katika mikoa mbalimbali nchini ili kutekeleza azma ya kulinda na kutetea haki za Mtoto.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mahakama ya watoto jijini Mbeya, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali aliiomba UNICEF kuangalia uwezekano wa kujenga majengo mengine manne ya Mahakama za watoto katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Dodoma na Tabora ili kuwapatia Mahakimu fursa ya kujifunza kwa vitendo namna Mahakama za watoto zinavyofanya kazi.

RAIS DKT MAGUFULI AMWANDALIA RAIS MUSEVENI WA UGANDA DHIFA YA KITAIFA JIJINI TANGA

$
0
0



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wakati wa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga.  Pamoja nao meza kuu ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Mama Janeth Magufuli. Hii ikiwa ni bado masaa machache kabla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa  mradi mkubwa wa usafirishaji wa Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga.
2
Sehemu ya mawaziri na manaibu waziri wa Tanzania na Uganda wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa za nchi hizo mbili na wa Afrika Mashariki kwenye dhifa ya Taifa aliyoandaa Rais Dkt. Magufuli kwa heshima ya mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda Ikulu ndogo jijini Tanga Ijumaa usiku
3
  Sehemu ya viongozi mbalimbali wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa za nchi hizo mbili na wa Afrika Mashariki kwenye dhifa ya Taifa aliyoandaa Rais Dkt. Magufuli kwa heshima ya mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda Ikulu ndogo jijini Tanga Ijumaa usiku.
4
Sehemu ya wageni waalikwa wa mataifa mbalimbali wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa za nchi hizo mbili na wa Afrika Mashariki kwenye dhifa ya Taifa aliyoandaa Rais Dkt. Magufuli kwa heshima ya mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda Ikulu ndogo jijini Tanga Ijumaa usiku
5
Wakuu wa Mikoa wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa za nchi hizo mbili na wa Afrika Mashariki kwenye dhifa ya Taifa aliyoandaa Rais Dkt. Magufuli kwa heshima ya mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda Ikulu ndogo jijini Tanga Ijumaa usiku
6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wakiongea  kwenye dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga.  Pamoja nao meza kuu ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Mama Janeth Magufuli.
7
 Baadhi ya wasanii wa Kizazi kipywa wakiwa kwenye dhifa ya Taifa aliyoandaa Rais Dkt. Magufuli kwa heshima ya mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda Ikulu ndogo jijini Tanga Ijumaa usiku
8
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni  baada ya dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga. 
9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kwa  mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumalizika kwa  dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga. 
10
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana  kwa  mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumalizika kwa  dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga. 

11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi  kwa  mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumalizika kwa  dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga. 
12
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na  mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wakiagwa kwa saluti na Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kumalizika kwa  dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga.  
13
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitakiana usiku mwema na  mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni baada ya dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga.  Pamoja nao ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Mama Janeth Magufuli.
Picha na IKULU

NEC YAPONGEZWA KWA USIMAMIZI NA MATUMIZI BORA YA RASILIMALI ZA SERIKALI

$
0
0

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani (Kulia) akimweleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) alipotembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi eneo la kuhifadhia Mashine za BVR. Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akitazama moja ya Daftari la Wapiga Kura alipotembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani na Kushoto ni Afisa TEHAMA wa Tume Bi. Mwamvita Solo.

Afisa TEHAMA wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Julius Kobelsiki akitoa ufafanuzi kuhusu Mashine ya kuandikisha Wapiga Kura ya BVR kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea Ofisi za Tume jijini Dar es salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya watendaji na watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mara baada ya kuhitimisha ziara yake katika Ofisi za Tume jijini Dar es salaam. Kulia kwake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi na Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani (kulia).


Na. Aron Msigwa - Dar es slaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye UlemavuMhe. Jenista Mhagama ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kuendelea kusimamia matumizi bora ya rasilimali inazopewa na Serikali na kuzitaka taasisi nyingine za Serikali kuiga mfano huo.


Mhe. Muhagama ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuangalia utekelezaji wa maagizo ya Bunge kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Bora iliyoridhia Bunge lipitishe fedha kiasi cha shilingi bilioni 10 kuiwezesha Tume kufanya maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini .


Akizungumza na watendaji na baadhi ya watumishi wa Tume amesema kuwa ameridhishwa na utendaji kazi wao na namna Tume ilivyojipanga kutekeleza jukumu la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kuelekea uchaguzi ujao wa mwaka 2020 kwa kuwa na mpango Kazi, unaochambua na kubainisha mahitaji muhimu yanayotakiwa, lini na wapi ili kazi hiyo iweze kufanyika kwa umakini. 


“ Naipongeza sana Tume kwa kuendelea kufanya vizuri , nimegundua kuwa imejipanga vizuri kutekeleza majukumu yake ambayo yameainishwa Katika Katiba,  kwa niaba ya Waziri Mkuu nimekuja hapa na timu ya watendaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kuangalia utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Bora walioridhia Bunge lipitishe fedha shilingi Bilioni 10 ili kuiwezesha kufanya maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura” Amesema.

DKT. TIZEBA ATEMBELEA BANDA LA BUNGE KATIKA MAONYESHO YA NANE NANE YANAYOENDELEA LEO MJINI DODOMA.

$
0
0


Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Charles Tizeba akisalimiana na Katibu Msaidizi wa Bunge, Ndg. Bakari kishoma wakati alipotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya Nane nane yanayoendelea  kwenye Viwanja vya Nzunguni, Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
IMGL8670
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Charles Tizeba (katikati)akimsikiliza  Afisa Habari wa Bunge Ndg. Patson Sobha (kushoto) wakati alipotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya Nane nane yanayoendelea  kwenye Viwanja vya Nzunguni, Mjini Dodoma. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Ndg. Deogratius Ndejembi
IMGL8673
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Charles Tizeba akiuliza swali baada kutembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya Nane nane yanayoendelea kwenye Viwanja vya Nzunguni, Mjini Dodoma. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Ndg. Deogratius Ndejembi na kulia ni Afisa Habari wa Bunge Ndg. Patson Sobha

UN YAZUNGUMZA NA VIJANA WA TEMEKE KUHUSU MALENGO YA MILENIA

$
0
0
--


 Ofisa kutoka Idara ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa Tanzania ,Didi Nafisa akizungumza na Vijana wa Mtandao wa Vijana Temeke(TEYODEN), Juu ya Malengo ya Milenia kwa vijana na mambo yaliyopewa vipaumbele katika malengo hayo
 Katibu mkuu wa Mtandao wa Vijana Temeke(TEYODEN),Yusufu Kutegwa akizungumza juu ya namna Mtandao huo unavyofanya kazi kusaidia Vijana
 Baadhi ya Vijana walioshiriki Mkutano Huo wakisikiliza kinachozungumzwa kutoka kwa watoa mada
 Balozi wa Malengo ya Dunia kwa Vijana kutoka chuo cha Uhasibu Arusha ,Gloria Nassary akizungumza na Vijana wa Temeke juu ya Vipaumbele vitano vya Kibinadamu katika Malengo ya Milenia
  Balozi wa Malengo ya Dunia kwa Vijana kutoka chuo cha Mtakatifu Agustino ,Julius Kitingati akieleza namna Vijana wanavyoweza kufanikisha malengo hayo kwa Sera ya Viwanda hapa nchini
Sehemu ya Viana walioshiriki katika mkutano huo ulioandaliwa na TEYODEN  Kwa kushirikiana na umoja wa Mataifa

NMB YATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI 10 KUFANIKISHA TAMASHA LA USALAMA BARABARANI AGOSTI 12 MWAKA HUU

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi , Mhandisi Ahmad Masauni akizungumza na Waandishi wa Habari Mapema jijini Dar es Salaam juu ya Tamasha la Usalama barabarani linalotaraji kufanyika Agosti 12 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kushirikisha makundi mbalimbali ya Wasanii watu maharufu na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi , Mhandisi Ahmad Masauni,akipokea jezi kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Wateja Binafsi na Mauzo ,Omary Mtiga NMB imetoa Vifaa Vyenye Thamani ya Shilingi Milioni 10 kwa ajili ya Kufanikisha Tamasha la Usalama Barabarani Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi , Mhandisi Ahmad Masauni,akipokea jezi kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Wateja Binafsi na Mauzo ,Omary Mtiga NMB imetoa Vifaa Vyenye Thamani ya Shilingi Milioni 10 kwa ajili ya Kufanikisha Tamasha la Usalama Barabarani Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi , Mhandisi Ahmad Masauni Akipokea Fulana kutoka kwa Meneja Masoko wa Azam Omary Kuwe
Meneja wa Mwanamuziki Mahiri wa Bongo Fleva Diamond Platnum, Salam Mendez akizungumza juu ya uwepo wa mwanamuziki huyo katika Tamasha la Usalama Barabarani la Twenzetu Taifa.
Msanii Mkongwe wa Maigizo nchini , Suzan Lewis Mharufu kama Natasha akizungumza jambo juu ya masuala ya usalama barabarani kuelekea tamasha hilo agosti 12.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi , Mhandisi Ahmad Masauni,akipokea jezi kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Mauzo wa Kampuni ya Binslum ya hapa nchini Tanzania
Sehemu ya Wanahabari na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani wakifatilia mkutano huo kwa makini juu ya Tamasha la Twenzetu Tifa katika masuala ya usalama barabarani

Rais Dkt Magufuli awapatanisha Ruge na Makonda jukwaani

Wajumbe wa Bodi Mkula wasekwa lupango kwa kushindwa kusimamia Mkopo

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (aliyesimama) akizungumza katika mkutano wa pamoja na wanachama wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula,iliyopo katika kijiji cha Mkula wilaya ya Kilombero.
DSC_0051
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (aliyesimama) akihimiza jambo wakati akizungumzia kukamatwa kwa wajumbe wa Bodi ya Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula ambao wamezembea kusimamia mkopo wa TADB.
DSC_0052
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Adam Kamanda (kushoto) akiongea kwa uchungu kitendo cha wajumbe wa Bodi ya Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula ambao wamezembea kusimamia mkopo wa zaidi ya shilingi milioni 790 zilizotolewa TADB.
DSC_0053
Baadhi ya wanachama na wanakijiji wa kijiji cha Mkula wakifuatilia mazungumzo wakati wa kikao cha pamoja kati ya Mkuu wa Wilaya hiyo, wawakilishi wa Benki ya Kilimo na wanachama wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula.
DSC_0054
Baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha Mkula wakitoa maoni yao kuhusu kutoridhishwa na kitendo cha kucheleweshwa marejesho ya mkopo wa TADB.
DSC_0055DSC_0056
Zoezi la kukamata wajumbe likiendelea.
DSC_0057DSC_0058
Zoezi la kukamata wajumbe likiendelea.
………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu.

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo ameagiza kukamatwa kwa wajumbe wa bodi ya Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula kufuatia kuchelewesha kwa makusudi malipo ya mkopo walioupata kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).

Akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na wanachama wa Skimu hiyo, Bw. Ihunyo alisema kuwa uzembe wa Bodi hiyo umepelekea kuchelewesha marejesho ya mkopo wa takribani shilingi milioni 790.

Mkuu huyo wa wilaya aliongeza pia kitendo cha Bodi hiyo inarudisha nyuma juhudi za serikali katika kupambana na umaskini nchini.“Lengo la mikopo hiyo ni kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania, hivyo kuchelewesha mikopo hiyo kwa makusudi ni kurudisha nyuma juhudi hizi,” Bw. Ihunyo alisema.

Bw. Ihunyo aliongeza kuwa kuchelewesha kurudisha mikopo hiyo kunakosesha wakulima wengine kuchelewa kupata fursa hizo za mikopo hiyo nafuu inayotolewa na TADB ambayo imelenga kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Adam Kamanda alisema kuwa tangu wapatiwe mkopo huo, baadhi ya wakulima wa skimu hiyo wamekuwa wakichelewesha kwa makusudi kurejesha mkopo huo licha ya jitahada za kuwahimiza kurejesha mkopo huo.

Bw. Kamanda alisema kuwa vitendo hivyo ni kwenda kinyume na malengo ya
“Mheshimiwa Rais anahimiza watu kufanya kazi kwa bidii sasa vitendo hivi ni kukaidi maagizo hayo hivyo kupingana na dhana ya hapa kazi tu inayochagiza kufanya kazi kwa bidii,” alisema.
Bw. Kamanda aliongeza kuwa Benki ya kilimo imejipanga kuhakikisha inatekeleza maelekezo ya serikali ya kuwawezesha wakulima nchini kwa kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika  kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa kusaidia upatikanaji na utoaji wa fedha ikiwa ni pamoja sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini.
Mwakilishi huyo wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji alisema kuwa TADB imedhamiria na kujizatiti kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika  kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa kusaidia upatikanaji na utoaji wa fedha ikiwa ni pamoja sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini.
 “Tuna dira ya Kuwa benki ya mfano na ya kisasa katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania kutoka kilimo cha kujikimu kwenda katika kilimo cha kibiashara na uzalishaji wenye tija katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini,” alisema.

WANAFUNZI WAKIPATIWA ELIMU KUHUSU BUNGE KATIKA MAONYESHO YA NANE NANE MJINI DODOMA.

$
0
0

Afisa Habari (Itifaki) wa Bunge, Ndg. Patson Sobha (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Miyuji walipotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya Nane nane yanayoendelea Mjini Dodoma.
IMGL8535
Afisa Habari (Itifaki) wa Bunge, Ndg. Patson Sobha akizungumza na wageni Mbali mbali waliotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya Nane nane yanayoendelea Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
IMGL8611

BALOZI KAMALA ATEMBELEA KATA KITOBO NA KUZINDUA MRADI WA DARAJA LA KYANKOKO

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala siku ya jana alitembelea Kata ya Kitobo Wilayani Missenyi na  kuzindua  Daraja la Kyankoko lenye sehemu tatu zilizowekewa Kalavati ,mrasdi uliopewa jina la la Novati Rutegaruka Memorial Bridge ambalo ni jina la muasisi na mwanasiasa mkongwe ambaye aliangaingia eneo hilo katika kipindi cha Uhai wake.
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala pichani wakati akizindua Daraja hilo lililogharimu kiasi cha shilingi milioni  kumi na nne za kitanzania (Tsh 14,000,0000)kulia pichani ni Diwani wa Kata ya Kitobo Mh.Willy Mtayoba.
 Muonekano wa Daraja la Kyankoko lililopewa jina la Novati Rutegaruka Memorial Bridge Daraja linalovikutanisha Vijiji vya Msibuka na Kayanga katika Kata ya Kitobo Wilayani Missenyi
 Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (pichani) akiongea na wananchi wa Kijiji cha Kashasha kata Kitobo  waliohudhuria katika mkutano wake wa hadhara,Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala ameweza kuchangia miradi ya maendeleo inayoendelea katika kata hiyo na pamoja na kuahidi kuzifanyia kazi kero mbalimbali kama Uhaba wa wauguzi katika Zahanati na vituo vya Afya,Utaratibu wa Bima ya Afya kwa Wazee na watu wenye Ulemavu kwa kuwapunguzia changamoto wanazokutana
 Sehemu ya wananchi wakifatilia kwa umakini wakati mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiendelea kuwahutubia na kufanya majumuhisho ya changamoto alizozibaini katika ziara yake ya Siku 17 Jimboni Mwake.
 Baadhi ya wananchi waliohudhurio mkutano wameweza kupata nafasi ya kuelezea Kero zinazowakabili licha ya kuwepo mafanikio katika utatuzi wa baadhi ya kero kupitia kwa Mbunge wao Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala
 Baadhi ya wananchi waliohudhurio mkutano wameweza kupata nafasi ya kuelezea Kero zinazowakabili licha ya kuwepo mafanikio katika utatuzi wa baadhi ya kero kupitia kwa Mbunge wao Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala
Wananchi wakifurahia jambo katika mkutano huo uliofanyika Jana katika Kijiji cha Kashasha kata Kitobo Wilayani Missenyi,Picha kwa hisani ya #bukobawadaumedia
Afisa Maendeleo Kata Kitobo  Saudi Crispian wakati akisoma taarifa ya maendeleo ya kata kwa Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Balozi Dr. Diodorus Buberwa alipotembelea kata hiyo, Balozi Dr.Kamala amehitisha ziara yake  kwa kutembelea maeneo mbalimbali kwa kukagua miradi ya maendeleo na kubaini namna miradi mingi ya Maji Wilayani Missenyi ilivyotekelezwa chini ya kiwango.Picha kwa hisani ya #bukobawadaumedia

SERIKALI YAOMBWA KUDHIBITI KONOKONO WAHARIBIFU WA MAZAO MKOANI LINDI

$
0
0
Mwezeshaji kutoka Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold Mneney (kulia), akitoa mafunzo ya siku moja ya kilimo  kwa wakulima wa Mkoa wa Lindi kwenye Maonyesho ya Kitaifa ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Ngongo mkoani hapa jana. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)
Wakulima wakiwa kwenye mafunzo hayo
Utambulisho ukifanyika.
Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa Wilaya ya Kilwa, John Ignas Mkinga, akifungua mafunzo hayo.
Wakulima wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mkulima Jakazi Ali kutoka Kilwa akielezea masoko ya kuuza mazao yao yalivyo na changamoto.
Mkulima Rashid Hassan kutoka Lindi vijijini akielezea jinsi konokono wanavyoathiri mazao yao.
Mkulima Saada Makota kutoka Wilaya ya Nachingwea akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Betty Milanzi mkulima kutoka Wilaya ya Nachingwea akielezea changamoto za kilimo wanazokumbana nazo.
Mkulima Mwanajumbe Nchuwa kutoka Kilwa akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk. Philbert Nyinondi ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro (SUA), akiwaeleza wakulima hao umuhimu wa kutumia simu zao kupata masoko ya mazao yao na kuwasiliana na wakulima wenzao katika masuala ya kilimo.



Na Dotto Mwaibale, Lindi

WAKULIMA wa Mkoa wa Lindi wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka ili kudhibiti konokono ambao wametajwa kuwa ni tishio kwa uharibifu wa mazao ya chakula na biashara mkoani humo.

Ombi hilo walilitoa katika mafunzo ya siku moja ya kilimo yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) katika maonyesho ya kitaifa ya wakulima Nanenane yanayoendelea viwanja vya Ngongo mkoani hapa jana.

"Tunachangamoto nyingi katika kilimo lakini kubwa zaidi ni konokono ambao wapo katika mashamba yetu ambao wanashambulia mimea ikiwa michanga na hata tukiwaua wamekuwa wakiongezeka jambo ambalo linatukatisha tamaa" alisema Rashid Hassan mkulima kutoka wilaya ya Lindi vijijini.

Alisema hawajui konokono hao wanatoka wapi na wafanyeje ili kumaliza changamoto hiyo ambayo imekuwa ni kilio kikubwa kwa wakulima wa mkoa huo kwani konokono hao wamekuwa wakila majani ya mmea ambayo ni machanga.

Mkulima Saada Makota kutoka Wilaya ya Nachingwea alisema changamoto waliyo nayo kucheleweshewa kufika kwa pembejeo za kilimo kwa wakati na ugonjwa wa kutu unaoshambulia mikorosho na kuifanya ikauke majani yake kwa juu.

"Pembejeo za kilimo tunaletewa mwezi wa tatu wakati mvua zimeanza kunyesha badala ya mwezi wa Desemba jambo ili linaturudisha nyuma wakulima" alisema Makota.

Mwanajumbe Nchuwa mkulima kutoka Kijiji cha Luato wilayani Kilwa alilamikia bei ya ufuta kushushwa na walanguzi kutoka sh.2000 kwa kilo hadi 1500 kwa mtindo wa choma choma.

Mkulima Betty Milanzi kutoka Kijiji cha Nammanga Nachingwea alisema changamoto nyingine waliyonayo ni wanyama waharibifu wa mazao yao kama nyati, tembo, nguruwe hivyo wakaomba serikali kupitia idara ya wanyapori iwasaidia kumaliza changamoto hiyo.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Jukwaa la Bioteknolojia kwa maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk. Hamalord Mneney aliwataka wakulima hao kubadilika na kulima kilimo chenye tija na kufuata maelekezo ya wataalamu badala ya kuendelea na kilimo ambacho hakina manufaa kwao.

Alisema lengo la mafunzo hayo ni kubadilishana uzoefu na kuona ni jinsi gani sayansi na teknolojia inavyoweza kutumika katika kilimo cha kisasa katika mazao yote ya chakula na biashara yanayolimwa katika mkoa huo.

Mkulima Saada Makota aliomba muda wa mafunzo hayo uongezwe ili waweze kupata fursa zaidi ya kujifunza na kupeleka elimu hiyo kwa wakulima waliowengi katika maeneo yao.

Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Philbert Nyinondi ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro (SUA), aliwataka wakulima hao kutumia simu zao kutafuta masoko ya mazao yao na kupeana taarifa mbalimbali ili kukabiliana na changamoto wanazo kabiliana nazo katika kilimo.

WAZIRI SIMBACHAWENE ATOA MAAGIZO KWA WAKUU WA MIKOA

WAKULIMA WAHIMIZWA KUTUMIA RASILIMALI ZA NCHI KWA KULIMA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg Methew J. Mtigumwe akisoma na kupata maelezo mbalimbali kuhusu ufanisi katika Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg Methew J. Mtigumwe akisikiliza maelezo ya namna ya ufyatuaji matofali yanayotumika kujengea nyumba za NHC mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg Methew J. Mtigumwe (Kushoto) akisikiliz akwa makini maelezo kuhusu ufanyaji kazi katika banda la TAMISEMI mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi. Mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Mhe Rukia Muwango.
Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi idara kuu ya kilimo Ndg Twahir Nzallawahe akisikiliza maelezo mbalimbali katika banda la Nanyamba mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi idara kuu ya kilimo Ndg Twahir Nzallawahe akisikiliza maelezo mbalimbali katika banda la Nanyamba mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi. Mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi.

Na Mathias Canal, Lindi

Pamoja na mazao mbalimbali yanayolimwa na wakulima nchini Tanzania lakini wametakiwa kujikita zaidi na kilimo cha mazao yanayostahimili ukame ikiwemo kuanzisha kilimo cha umwagiliaji hususani katika maeneo yaliyopo pembezoni mwa Bahari ya Hindi katika Mikoa ya Mtwara na Lindi.

Kufanya hivyo ni kutumia vizuri rasilimali za nchi ikiwemo maji na maeneo oevu katika kilimo chenye tija jambo ambalo linatoa fursa kwa wakulima wadogo kuwa na kipato kikubwa na kutafsiri ipasavyo kipato cha nchi na mtu mmoja mmoja.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi idara kuu ya kilimo Ndg Twahir Nzallawahe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg Methew J. Mtigumwe mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Nzallawahe alisema kuwa katika mikoa ya Mtwara na Lindi serikali tayari imeanzisha kanda ya umwagiliaji ambapo kuna mradi wa Kitele huku akisema kuwa jitihada zaidi za kuwa na miradi ya umwagiliaji katika mikoa yote nchini zinaendelea.

Alisema kuwa pamoja na mbinu bora za Kilimo Mifugo na Uvuvi wanazopatiwa wananchi lakini pia Maonesho ya Nanenane kwa mwaka huu 2017 yamezidi kuwa bora zaidi ukilinganisha na Maonesho ya kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Aliongeza kuwa wananchi wanapaswa kutembelea katika Maonesho hayo ili kujifunza mbinu mbalimbali za Kilimo Mifugo na Uvuvi huku akiwasisitiza zaidi kununua bidhaa zinazotengenezwa na kuzalishwa ndani ya nchi kwani kufanya hivyo watarahisisha kipato cha wakulima nchini ikiwemo pia kurahisisha kasi ya ukuaji wa kilimo.

Aidha amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya nchini hususani kuwapatia wananchi maeneo kwa ajili ya kilimo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Mhe Rukia Muwango alisema kuwa Katika Maonesho haya wakulima watajifunza mbinu bora za kisasa za kilimo zitakazowawezesha kupata mazao mengi na kuinua kipato chao.

Aidha ametoa  wito kwa wakulima na mashirika kujitokeza katika maonesho hayo kwa sababu watapata fursa ya kujifunza mambo mengi na kubadilishana uzoefu na wataalamu mbalimbali wa kilimo.

RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA RAIS MUSEVENI WA UGANDA WAWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA HOIMA UGANDA MPAKA BANDARI YA TANGA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake, Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga huku viongozi mbalimbali wa Tanzania na Uganda wakishuhudia. Shughuli hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake, Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga huku viongozi mbalimbali wa Tanzania na Uganda wakishuhudia. Shughuli hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono wa pongezi na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga huku Viongozi mbalimbali wa Tanzania na Uganda wakishuhudia. Shughuli hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mbalimbali waliohudhuria shughuli ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga katika kijiji cha Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Chongoleani kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka nchini Uganda hadi Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono pamoja na mke wake Mama Janeth Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wakiagana na Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika uwanja wa ndege wa Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza ngoma ya msanja na Mama Janeth Magufuli pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kumsindikiza Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika uwanja wa ndege wa Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika viwanja vya Chongoleani kabla ya tukio la uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta.
Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimpa mkono Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumaliza kuhutubia katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela akiongea wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania ambapo aliwaahidi Rais Magufuli na Rais Museveni kuwa wataulinda mradi huo kwa faida ya nchi hivi mbili na Afika Mashariki kwa Ujumla.
Baadhi ya wananchi wakifurahia jambo wakati wa hotuba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la Mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimueleza jambo Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la Mradi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika viwanja vya Chongoleani kabla ya tukio la uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati wakielekea kuweka jiwe hilo la msingi.
Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika sherehe hizo za uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa bomba la mafuta.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii mbalimbali mara baada ya kutumbuiza.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni akihutubia katika viwanja vya Chongoleani nje kidogo ya jiji la Tanga. PICHA NA IKULU

AfDB YASISITIZA WELEDI KWA WANAFUNZI WANAOFADHILIWA NA BENKI HIYO CHUO KIKUU CHA NELSON MANDELA

$
0
0
--
Benny Mwaipaja-WFM, Arusha

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, amewataka wanafunzi 45 kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na Ethiopia, wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia kilichoko mkoani Arusha, kusoma kwa bidii na maarifa ili waweze kuzisaidia nchi zao kuinua sekta ya viwanda kwa njia ya utafiti na ubunifu wa teknolojia mbalimbali

Dkt. Weggoro ametoa rai hiyo alipotembelea Chuoni hapo ili kuangalia utekelezaji wa programu ya miaka mitano ya kuboresha masuala ya rasilimali watu inayofadhiliwa na Benki yake kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 8.2

Alisema kuwa Benki yake imeamua kuwekeza fedha nyingi katika eneo la Sekta ya elimu ya juu katika nyanja ya ufundi ili kuwapata vijana wa kutosha watakaoziba pengo lililopo na kuweka misingi mizuri ya maendeleo ya baadae hasa katika matumizi ya teknolojia na sayansi.

 “Nimefurahi sana kuona wanafunzi wanasoma na wana ari kubwa na kwamba fedha tulizozitoa zinatumika vizuri, tunadhani hata baada ya mradi huu wa  miaka 5 kukamilika, Benki itaweza kusaidia zaidi ufadhili wa fedha na vifaa” Alisema Dkt. Weggoro.

Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, Prof. Joram Buza, ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB kwa ufadhili huo, hatua iliyoongeza udahili wa wanafunzi katika chuo hicho.

“Mwaka wa masomo wa 2014/2015, Chuo kilidahili wanafunzi 7 pekee kutokana na changamoto wafadhili lakini baada ya ufadhili wa AfDB na Benki ya Dunia, wanafunzi wameongezeka hadi kufikia 135 jambo linalotia matumaini” alisema Pro. Buza.

Bi. Mwanaisha Mkangara na Bw. Alexander Mzura, wanaosomea shahada ya uzamivu katika masuala ya uhandisi na mifugo, kupitia ufadhili wa AfDB, wamesema kuwa masomo yao yatawaongezea ujuzi wa namna ya kufanya utafiti wa kihandisi na kuvumbua chanjo mbalimbali za mifugo.

AfDB inafadhili wanafunzi 45 ambapo 42 kati yao wanatoka Tanzania, huku Uganda, Kenya na Ethipia zikitoa mwanafunzi mmoja mmoja. 

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro akizungumza kuhusu umuhimu wa vijana wenye weledi wa kitaaluma katika kukuza uchumi, alipokutana na wanafunzi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha (hawapo pichani) wanaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB)




Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro (kulia) akiwa na Mkutano na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha Prof. Joram Buza, alipotembelea chuo hicho kuangalia mradi wa kuwafadhili wanafunzi unaotekelezwa na Benki yake.


 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha wanaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro (hayupo pichani) alipotembelea Chuo hicho, ambapo aliwasisitiza kusoma kwa bidii ili kuhimili ushindani katika soko la ajira.


 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro (kulia), na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha Prof. Joram Buza wakizungumza jambo baada ya kumalizika kwa mkutano na wanafunzi wa chuo hicho wanaofadhiliwa na AfDB.
 Afisa wa Idara ya Fedha za Nje anayeshughulikia Dawati la AfDB kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Said Nyenge (kulia) na Meneja wa Mradi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) wa ufadhili wa wanafunzi katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, Arusha, Bw. Julius Lenguyana (kushoto), wakibadilishana mawazo baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao kuhusu ufadhili wa AfDB katika mradi wa miaka 5 kwa baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho.
 Meneja wa Mradi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha, Julius Lenguyana (kulia) akimuongoza Mkurugenzi Mtendaji wa AfDB Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro (kushoto) alipowasili chuoni hapo kuangalia utekelezaji wa mradi wa ufadhili wa wanafunzi unaotekelezwa na Benki yake kwa miaka mitano katika Chuo hicho.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro (mbele wa pili kushoto),  Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha Prof. Joram Buza (kulia kwake), Mshauri wa Mkurugenzi huyo Bw. Amos Kipronoh Cheptoo (kushoto kwake) na Afisa Mwandamizi wa Idara ya Fedha za Nje anayeshughulikia Dawati la AfDB kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Said Nyenge (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na  wanafunzi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha wanaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) kwa ngazi ya shahada ya uzamili na uzamivu.

Mradi wa Bomba la Mafuta Waurejesha Mkoa wa Tanga Katika Historia

$
0
0
Na: Judith Mhina – MAELEZO

Hakika historia imejirudia, mkoa wa Tanga ni kati ya mikoa mashuhuri nchini Tanzania kabla ya uhuru wa Tanganyika katika kupigania uhuru, kwa kuwa ni mkoa uliokuwa na wasomi wengi kuliko mikoa mingine wakati huo.

Hii ilitokana na uwepo wa shule za wamisionari wa kanisa la Anglikana (UMCA) ambalo ni la kwanza kuingia katika Pwani ya Afrika Mashariki mwaka 1878 na waliojenga shule za Magila na Kiwanda Muheza, Korogwe misheni, Kideleko Handeni (Shule za Kati) na Saint Andrew Minaki Pwani (shule ya Sekondari).

Hata baada ya uhuru chini ya Serikali ya Awamu ya Kwanza na ya Pili ya uongozi wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere na Rais Msataafu Ali Hassan Mwinyi, mkoa wa Tanga ulikuwa maarufu kutokana na uwepo wa viwanda vingi, njia za reli na Bandari yenye kina kirefu yenye uwezo wa kuingiza meli kubwa za mizigo za Kitaifa na Kimataifa.

Viwanda ambavyo vilijengwa katika mkoa wa Tanga ni pamoja na vya chuma, mbolea, saruji, maziwa, kamba za katani na mazulia, amboni plastic, mbao, sabuni maarufu ya mbuni, gardenia, foma na mafuta ya nazi.

Historia hii sasa inajirudia katika mkoa wa Tanga baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli, kupigania kwa nguvu zote Mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda kuja nchini Tanzania ambalo litaishia katika kijiji cha Chongoleani.

Wananchi wote wa Tanzania wana kila sababu ya kujivunia ujenzi wa bomba hilo la mafuta ambalo litawapatia ajira Watanzania hususan wananchi wa mkoa wa Tanga. Pongezi kubwa ziende kwa Rais wetu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa juhudi zake za kuhakikisha kwamba Mradi huu unakuja Tanzania. Wananchi wa mkoa wa Tanga na Tanzania kwa ujumla wana kila sababu ya kulinda heshima ya nchi yetu kwa kuhakikisha kuwa kunakuwepo na ulinzi mkali wa Bomba hilo kila mahali lilikopita.

Kurejea kwa mkoa wa tanga katika ramani ya Tanzania ya viwanda umedhihirishwa na Wananchi wa Chongoleani ambao siku ya uwekaji jiwe la msingi walikuwa wawakilishi wa Watanzania ambao hawakupata fursa ya kwenda Tanga kumshuhudia Mheshimiwa Rais na na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakifungua pazia la jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa Mradi huo.

Kutokana na tukio hilo la uwekaji wa jiwe la msingi wana Chongoleani walitoa ya moyoni kwa kuonyesha furaha yao isiyo na kifani kupitia kwa Mwenyekiti wao wa kijiji Ndugu Mbwana Nondo wakisema; “Kwa moyo wa dhati kabisa tunamshukuru sana Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutujali Wananchi wake kwa kutuletea neema ya mradi huu wa bomba la mafuta”.

Aidha, Mwenyekiti huyo aliongeza kwa kusema kwamba, katika maisha yetu Wananchi wa Chongoleani hatutaweza kumsahau Mheshimiwa Rais kwa mambo mengi anayowafanyia Watanzania na Taifa kwa ujumla na itakuwa ni kumbukumbu kwa kizazi kijacho.

“Napenda kusisitiza kwamba tunamuahidi Rais, kuwa wote watakaopata fursa kwenye Mradi huu wa Bomba la Mafuta, watafanyakazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla”. Alihitimisha Bw Nondo.

Naye Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Bibi Ummy Mwalimu, amewaomba wanawake wa Mkoa wa Tanga kuchangamkia fursa zinazojitokeza, kutokana na uwepo wa mradi wa bomba la mafuta.

Akisisitiza kuhusu ajira hizo amesema; “Kwa wale wenye ujuzi wanaweza kupata ajira za kudumu katika mradi, ila kwa wale ambao hawana ujuzi wachangamkie fursa nyingine kama mama lishe ambapo mkoa unjulikana kwa kujua kupika mapishi yanayovutia walaji wengi”

Aidha, amewaasa wakulima kuona fursa ya kulima mazao ambayo yataliwa kwa wingi kwa watumishi watakaoajiriwa Tanga katika mradi wa bomba la mafuta. Mfano matunda na mbogamboga ambavyo ni sehemu ya kuimarisha lishe za watumishi hao watakao kaa Tanga.

Mradi wa Bomba la Mafuta ni ishara njema kwa Watanzania, Serikali na Taifa kwa ujumla maana inaonyesha dhahiri kukosekana kwa fursa kama hii kwa miaka mingi katika mkoa wa Tanga ni fundisho kwa Watanzania hususan Wananchi wa mkoa wa Tanga kama waswahili wasemavyo “usichezee shilingi chooni” ikiwa na maana shilingi ikitumbukia kuipata sio rahisi.

Kila jambo jema lina fursa zake, nalo bomba la mafuta limekuja na neema zake, mfano wana Chongoleani kupata barabara ya kilometa 8 inayowaunganisha na barabara kuu ya kutoka Tanga kwenda Horohoro. Hii ina maana kubwa kwa wana chongoleani kiuchumi, maana watakuwa na wepesi wa usafiri wa mabasi na malori. Hivyo, bidhaa zitokazo chongoleani sasa zitaenda Tanga na nje ya mkoa wa Tanga kwa urahisi. Mfano samaki, mazao ya chakula na mengineyo.

Wafanyabiashara wetu wachangamkie fursa iliyojitokeza watembelee eneo husika na kudadisi kipi wanachoweza kufanya biashara kwa ajili ya kuinua kipato chao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Kama tujuavyo Taifa letu liko kwenye harakati za kuelekea katika uchumi wa viwanda, na kama ujuavyo Tanga ni Mkoa wenye kuzalisha matunda ya aina mbalimbali na mbogamboga kwa wingi, nazi, katani, mahindi, viazi, maharagwe, samaki, viungo kama tangawizi, iliki, pilipili manga, mdalasini, chai na mifugo kama ngombe mbuzi na kondoo wapo kwa makundi katika ranchi zinazotambulika na wale wanaofugwa kiasili.

Katika suala zima la bomba la mafuta ni muhimu mikoa yote ambapo bomba linapita kutambua na kujiandaa kuitumia fursa zilizopo na zitakazo jitokeza katika mikoa ya; Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma Morogoro na Tanga. Wilaya zitakazopitiwa na bomba hilo zipo 24 na vijiji zaidi ya 180, vitafahamishwa kwa usahihi hapo baadaye.

Kwa kuwa Wizara ya Nishati na Madini inahamasisha kwa pamoja na wadau mbalimbali ni vema kutumia mafunzo hayo, kujiimarisha na kuwa sehemu ya matokeo mazuri ya bomba husika.

Bomba la Mafuta la kutoka Hoima Uganda mpaka Tanga Chongoleani lina urefu wa Kilometa 1445 ambapo kwa upande wa Tanzania itakuwa na jumla ya kilometa 1115 na Uganda 330. Aidha, Mradi utatarajia kusafirisha mapipa laki mbili na kumi na sita elfu (216,000) kwa siku .

Kijiji cha Chongoleani ndio kituo cha mwisho ambapo mitambo mikubwa itasimikwa katika eneo hili kwa ajili ya kusukuma mafuta eneo la baharini ili, kuweka kwenye vyombo vya usafirishaji kusafirisha maeneo mbalimbali duniani ambayo Uganda watakuwa wamepata soko.

Tanzania itafaidika na mradi huu kutokana na kodi, tozo na mrahaba wa bomba la mafuta, itakayofanywa moja kwa moja na mradi huo. Faida nyingine ambazo, sio za moja kwa moja ni ajira, fursa za kufanya biashara katika mikoa 8 ambayo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Morogoro na Tanga.

Tusisahau unapopata fursa moja, ni vema kuitumia kwa kuimarisha na kuitangaza Tanga kimataifa kwa upande wa utalii katika machimbo ya Amboni, utalii wa samaki adimu duniani Silikanti eneo la ufukwe wa Kigombe. Samaki huyu alikuwepo duniani miaka 6000 iliyopita, ambapo alitoweka na kugundulika kuwa yupo katika pwani ya bahari ya hindi eneo la Kigombe Muheza Tanga.

Aidha, utalii wa milima ya Usanbara na Nnguu Kilindi, misitu ya asili ambayo kama vile miti ya miwati inayotengeneza nta au gundi, Tao la Mashariki misitu ya asili ya Nguu na maporomoko ya maji katika Tao la mashariki ikiwa ni pamoja na milima ya usambara, amani, maghamba, na nguu. Uoto wa asili na baridi ambayo isingedhaniwa kabisa kuwepo katika milima inayoelekea bahari ya Hindi.

Pia Hifadhi ya Taifa ya wanyamapori ya Saadani yenye kivutio cha ngiri wanaoishi katika makazi ya binadamu ambayo ni mbuga pekee iyopo pembezoni mwa bahari katika Afirka mashariki, pia mbuga ya Mkomazi na mbuga ya uwindaji wanyapori ya Nnguu, madini ya aina mbalimbali, Kasa wa pembezoni mwa ufukwe wa bahari ya Hindi na vipepeo adimu duniani wa milima ya usambara Amani. Ni vema kuwakarimu wageni kwa utamaduni wa asili wa Tanga kwa kuwaonyesha mapishi na ukarimu uliotukuka wa Watanzania wapatapo wageni. 


Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.

Makonda, Ruge na Tanzania All Stars wanogesha sherehe za uwekaji jiwe la msingi la mradi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga kijijini Chongolieni

$
0
0
 Wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya wanaounda kundi la Tanzania All Stars wakijiandaa kupanda jukwaani kutumbuiza kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
 Wasanii nyota wa filamu wa Bongo Movie wakiwa  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba wamalize tofauti zao na kuweka maslahi ya nchi mbele wakati alipohutubia kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
 Baada ya kupatanishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba walishuka jukwaani bega kwa bega huku wakitabasamu.
 Kisha wakaelekea kwenye jukwaa la wasanii wa Tanzania All Stars
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba wakiwa jukwaani bega kwa bega huku wakiimba na Tanzania All Stars
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba wakiwa jukwaani bega kwa bega huku wakiimba na Tanzania All Stars
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba wakiwa jukwaani bega kwa bega huku wakiimba na Tanzania All Stars
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigella  akiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
 Naibu Waziri Mkuu wa Uganda Dkt Ali Kirunda Kivenjija akiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba wakiwa jukwaani bega kwa bega huku wakiimba na Tanzania All Stars. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.  Ashatu Kijaji wakiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakisubiri  kuwapa mikono wasanii wa Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016











































VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMAPILI LEO AUG 6,2017

MPINA ALIPONGEZA JIJI LA MWANZA KWA UJENZI WA DAMPO NA MACHINJIO YA KISASA

$
0
0
Karakana za kisasa zilizojengwa katika Dampo la jiji la Mwanza.
Mwenye Kofia Nyeupe Msimamizi wa Dampo la jiji la Mwanza (Site Manager) Bw. Desderius Pole akimuonyesha Naibu Waziri Mpina tokea mbali karakana za kisasa hazipo katika picha zilizojengwa katika Dampo la jiji hilo, kulia ni wana habari kazini.
Afisa Mazingira wa jiji la Mwanza wa pili kulia Bi Lidya Nyeme, akimuelezea Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira na Ujumbe wake katika picha kuhusu machinjio ya kisasa ya Jiji la Mwanza iliyojengwa kwa ufadhili wa Bank ya Dunia kupitia Mradi wa hifadhi ya mazingira ya Ziwa Victoria (LVEMP) uliyopo chini ya Wizara ya Maji, Naibu Waziri Mpina yupo katika Ziara ya kikazi jijini Mwanza.

…………………………………………………..

NA EVELYN MKOKOI – MWANZA

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu w rais Muungano na mazingira amelipongeza jiji la mwanza kwa hatua iliyochukua ya kutunza mazingira kwa ujenzi wa Dampo na machinjio ya kisasa kwa lengo la kupunguza uharibifu na uchafuzi wa mazingira kutokana na utupaji taka ovyo.

Aidha, amelipongeza jiji hilo kwa maandalizi ya ujenzi wa miundombinu ya dampo la kisasa kama mizani ya kupimia taka, ofisi na maabara ya kemikali katika dampo hilo uliopelekea jiji hilo kufuzu kupata ufadhili kupitia Bank ya dunia licha ya kutumia mapato ya ndani.”Nikiangalia naona mmewekeza kama zaidi ya milioni 700 ambayo mumewekeza kama manispaa ya Jiji la mwanza.” Alisema Mpina.

Mpina aliongeza kwa kusema kuwa kwa jiji la mwanza kufanya hivyo ni hatua kubwa na kulitaka jiji hilo kuendelea na ari hiyo katika suala zima la hifadhi na utunzaji wa mazingira. Mpina pia aliitaka Manispaa hiyo kukamilisha kwa wakati hatua nyingine za ujenzi wa dampo hilo kama vile za Tathmini ya Athari kwa Mazingira na kulipa fidia kwa wananchi na kaya zilizobakia ili kukamilisha upanuzia wa dampo hilo, na kuepuka vipingamizi visivyo vya lazima.

Katika hatua nyingine Mpina pia aliwapongeza wahisani kwa kuiamini serikali ya awamu ya tano katika mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika suala zima la hifadhi ya mazingira. “Naamini katika mradi huu unaokuja wa zaidi ya shilingi Bilioni 19.8 miundombinu ya hapa itakuwa ni mizuri na rafiki zaidi kwa mazingira, kikubwa zaidi ni kuwekeza nguvu zetu katika mradi huu na kuhakikisha kuwa unatekelezwa kama ulivyopangwa”. Alisema Mpina.

Wakati huo huo Naibu Waziri Mpina alitembelea Machinjio ya kisasa ya jiji la Mwanza na kujionea ukarabati wa machinjio unahusisha utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mtambo wa kisasa wa kutibu majitaka yanayotoka katika machinjio hayo ambapo mtambo huo utazalisha pia biagas kwa ajili ya kuzalisha nishati ya umeme na kuzalisha mbolea. Ukarabati huo unahusisha pia ujenzi wa chumba cha kisasa cha kuhifadhia nyama kitakachowezesha wafanyabiashara ya nyama kusafirisha nje ya nchi.

Katika hali isiyo ya kawaida Naibu Waziri Mpina alitembelea kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Senrun Investment kilichopo eneo la Igoma na kusisitiza kiwanda hicho kiendelee kufungwa kutokana na kubainika kuendesha shughuli zake kinyume na Sheria kwa kutokuwa na vibali vya uchenjuaji dhahabu, cheti cha Tathmini ya athari kwa Mazingira na kibali cha matumizi ya kemikali kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali. 
 
“Nasisitiza kwamba kiwanda hiki kiendelee kufungwa kama ambavyo NEMC wamekifunga na nawataka wamiliki kuwasilisha vibali husika ndani ya siku 7 na wasiendelee na uzalishaji mpaka watakapomaliza zoezi la kufanya tathmini ya athari kwa mazingira”. Awali kiwanda hicho kilifungwa na NEMC kufuatia malalamiko ya wananchi wa maeneo hayo kwa kutiririsha maji yenye kemikali, kutoa moshi mkali kutokana na uchomaji wa taka zenye sumu na kutokuwa na vibali muhimu vya kuruhusu uendeshaji wa shughuli za uchenjuaji dhahabu.

MDAU NELSON PALLANGYO NA BI. THERESIA BYAKWAGA WAFUNGA NDOA MJINI KARATU

$
0
0
 Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini, Jimbo La Karatu, Usharika wa Karatu Mjini akiwafungisha ndoa Bw. Nelson Charles Pallangyo na Bi. Theresia Justine Byakwaga iliyofanyika Agosti 5, 2017 na baadae sherehe ikafanyika ukumbi wa Samawe Complex. PICHA ZOTE NA KAJUNASON/MMG - KARATU. 
Bwana Harusi Nelson Charles Pallangyo  akimvalisha pete mkewe Bi. Theresia Justine Byakwaga wakati wakifunga ndoa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini, Jimbo La Karatu, Usharika wa Karatu Mjini akiwafungisha nd Agosti 5, 2017. Bibi Harusi Theresia Justine Byakwaga akimvalisha pete mumewe Nelson Charles Pallangyo wakati wakifunga ndoa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini, Jimbo La Karatu, Usharika wa Karatu Mjini akiwafungisha nd Agosti 5, 2017.
Bwana Harusi Nelson Charles Pallangyo na mkewe Bi. Theresia Justine Byakwaga wakila kiapo cha uaminifu wakati wakifunga ndoa yao takatifu. Pembeni ni wasimamizi wao.
 Waumini wakifuatilia ibada.
  Mchungaji akiwagawia vyeti.
 Maharusi wakionyesha vyeti vyao mara baada ya kufunga ndoa. Pembeni ni wasimamizi wao.
 Maharusi wakitoka kanisani.
 Wazazi wa Bwana Harusi (kushoto), Charles Pallangyo na Bibi Harusi (kati mwenye shati la blue) Justine Byakwaga wakizungumza machache na mchungaji mara baada ya kufungisha ndoa ya watoto wao Nelson Charles Pallangyo na Bi. Theresia Byakwaga.
 Pongezi za ndugu, jamaa na marafiki mara baada ya kutoka kanisani.
 Pongeni na shamra shamra zikiendelea.
 Bwana Harusi Nelson Charles Pallangyo na Bibi Harusi Theresia Justine Byakwaga wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi wa pande zote mbili.
   Wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wakiwa katika picha ya pamoja na maharusi.
Maharusi wakikaribushwa nyumbani kwa shangwe na vigelegele....

Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>