Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1327 | 1328 | (Page 1329) | 1330 | 1331 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Naibu Waziri wa   Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na watumishi wa Kitengo cha Jeshi la Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati alipofanya ziara katika kitengo hicho kilichopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, ambapo aliwaagiza kuhakikisha wanapambana na uingizwaji wa dawa hizo kupitia bandari bubu na mianya yote ya uingizwaji na usambazaji.
   Naibu Kamishna wa Kitengo cha Jeshi la Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, DCP Mkonyi, akitoa taarifa fupi ya hali ya uzuiaji wa Dawa za Kulevya mbele ya Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani   ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,  alipofanya ziara katika kitengo hicho kilichopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, ambapo aliwaagiza kuhakikisha wanapambana na uingizaji wa dawa hizo kupitia bandari bubu na mianya yote ya uingizwaji na usambazaji.
   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisomewa takwimu za matukio ya ukamataji wa Dawa za Kulevya na mmoja wa afisa wa  Kitengo cha Jeshi la Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya  wakati alipofanya ziara katika kitengo hicho kilichopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, ambapo aliwaagiza kuhakikisha wanapambana na uingizwaji wa dawa hizo kupitia bandari bubu na mianya yote ya uingzwaji na usambazaji.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiongozana na Naibu Kamishna wa Polisi, DCP Mkonyi, wakati alipotembelea  Kitengo cha Jeshi la Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya kilichopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, ambapo aliwaagiza kuhakikisha wanapambana na uingizwaji wa dawa hizo kupitia bandari bubu na mianya yote ya uingzwaji na usambazaji. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Makamanda wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Lindi wamewataka wananchi kutunza vizuri fedha zao ili kupunguza uharibifu unaoliongezea taifa gharama za kutengeneza fedha zingine.

  Aidha, viongozi hao wameelezea umuhimu wa wananchi kutambua alama za usalama wa noti zetu ili kuepuka kuangukia mikononi mwa matapeli na kupata hasara.

  Viongozi hao, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, SACP Renatha Mzinga, Mkuu wa Magereza wa Mkoa, Bw. R. Nyange, na Mkuu wa Usalama wa Taifa wa Mkoa wa Lindi, Bw. Nsiima Wema walisema hayo baada ya kutembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika maonesho ya Wakulima kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi. 

  RPC Mzinga alisema taifa linaingia hasara kubwa kutengeneza noti zinazotokana na uharibifu unaofanywa mara kwa mara na wananchi.

  “Mimi nilikuwa najua pesa chafu zinarudishwa Benki Kuu na kufanyiwa recycling na kurudishwa kwenye mzunguko; kumbe tunapata hasara. Kwa elimu hii niliyoipata, nawashauri wananchi kwa ujumla watunze fedha zetu, kwa sababu zinapoharibika ni hasara kwa taifa,”alisema RPC Mzinga.

  Mkuu wa Usalama wa Taifa mkoani Lindi, Bw. Wema alieleza kwamba amefurahishwa sana kwa kupata elimu kuhusu alama za usalama za noti zetu na kuahidi kutumia elimu hiyo kuwafundisha wengine.

  “Kikubwa zaidi kilichonivutia ni namna ya kutambua pesa halali na pesa zisizo halali. Kwa ajili ya kukosa uelewa wananchi wengi wanalizwa kila siku kwa kupewa pesa zisizo halali kwa kuwa hawajui kuzitambua. Elimu niliyoipata itanisaidia niwaambie na wenzangu mtaani kwamba pesa halali iko hivi na isiyo halali iko hivi,” alisema Bw. Wema.

  Mkuu wa Magereza wa Mkoa, Bw. Nyange, aliwashauri wananchi wanapofikia umri wa kustaafu wajiepushe kuwekeza katika biashara wasizozijua ili kuepuka hasara na badala yake wawekeze katika dhamana za serikali zinazotoa faida ya uhakika bila wasiwasi wowote wa kuingia hasara.

  “Watu wanapostaafu mara nyingi wanajiingiza kwenye miradi mbalimbali…ambayo hawana ujuzi nayo; hawajui hata hasara zake, ili mradi wanaona mtu fulani ana biashara ya magari, ana mabasi, basi naye anajiingiza huko matokeo yake anapata hasara au mwingine anajiingiza kwenye mashamba na wakati mwingine jua mwaka huo linakuwa kali, moja kwa moja mazao yanakufa, inafikia hatua mtu anaweza hata kujiua…kumbe fedha ile unaweza ukawekeza kwenye dhamana za serikali, ukaendelea kupata faida na pesa yako ikabaki kuwa salama,” alisema.

  Viongozi hao wa vikosi vya ulinzi na usalama mkoani Lindi walitumia takriban saa nzima wakipata elimu ya kazi mbalimbali zinazofanywa na Benki Kuu na jinsi zinavyoendana na Kauli Mbio ya Maonesho ya Wakulima ya mwaka huu isemayo: Zalisha kwa tija mazao na bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati.

  Maonesho ya Nane Nane kitaifa mwaka huu yalifunguliwa na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Bw. George Simbachawene tarehe 1 Agosti, 2017, ambaye pamoja na mambo mengine aliwataka wakulima, wafugaji na wavuvi kuongeza tija kwa kuzalisha mazao na bidhaa kwa njia za kisasa.

  Waziri Simbachawene alihimiza kilimo na ufugaji wa kisasa na kuwataka wavuvi kuanzisha ufugaji wa kisasa kwa kujenga mabwawa badala ya kutegemea mitego katika mito, maziwa na bahari, ambako hakuna uhakika wowote wa kipato.Maonesho kama haya pia yanafanyika katika ngazi ya kanda katika kanda za Mashariki, Kati, Ziwa, Nyanda za Juu Kusini na Kaskazini.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani kimesema kuwa ajali za barabarani zinaweza kupungua kwa madereva  kufuata sheria za usalama barabarani.

  Hayo ameyasema Kamanda wa Polisi wa  Kikosi cha Usalama Barabarani  kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi(SACP) Fortunatus Musilim wakati akizindua uwekaji wa namba maalum za simu katika mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani leo katika kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam.

  Amesema kuwa namba za simu katika mabasi hayo zitatumika kwa abiria kutoa taarifa ya dereva anaendesha bila kufuata sheria za usalama barabarani ikiwemo mwendo kasi.Kamanda Muslim  amesema kuwa namba hizo ni bure na kwa abiria, dereva au kondakta atakaeng’oa namba hizo atachukuliwa hatua ikiwemo kunyanganywa leseni.

  Amesema uwekaji wa namba maalumu kwenye mabasi unafanyika nchi nzima ikiwa yote nikulinda maisha ya abiria katika kuwa na uhakika wa safari zao.

  Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Mkoa wa Kinondoni, Solomon Mwangamilo amesema kuwa watasimamia maagizo ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro ambapo yamekaziwa na Kamanda wa Polisi wa  Kikosi cha Usalama Barabarani  kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi(SACP) Fortunatus Musilim.

  Mkuu wa Usalama Barabarani Kituo cha Ubungo Ibrahim Samwix amesema kuwa kila siku wanafanya ukaguzi na gari ambayo ina kasoro haiwezi kufanya safari zake.Amesema watahakikisha kuwa kila basi linalondoka katika kituo cha ubungo linakuwa na namba maalum za simu  katika kila basi..
   Kamanda wa Polisi wa  Kikosi cha Usalama Barabarani kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi(SACP) Fortunatus Musilim akizungumza na waandishi habari katika uzinduzi wa uwekaji wa namba maalum za simu katika mabasi yaendayo Mikoani na Nchi jirani katika kituo Kikuu Cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
   Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni, Solomon Mwangamilo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkazo na maagizo ya Ukaguzi wa magari katika kituo Kikuu Cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Usalama Barabarani Kituo cha Ubungo Ibrahim Samwix (katikati) akizungumza na waandishi  habari kuhusu ukaguzi magari yanayotoka kituo Kikuu Cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
   Kamanda wa Polisi wa  Kikosi cha Usalama Barabarani  kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi(SACP) Fortunatus Musilim akiweka namba maalmu za simu katika basi itakayotumika kupiga kwa  abiria kwa dereva atakaye kiuka sheria za usalama barabani .
    Askari wa Usalama barabani  wakiwa katika ukaguzi mbalimbali wa mabasi katika kituo Kikuu cha Mabasi  Ubungo.
   Muonekano wa Mabasi yakiwa katika kituo Kikuu cha Ubungo leo asubuhi  0 0

  Mbunge wa Ubungo ,Saed Kubenea akihutubia wakazi wa Kimara kata ya Kilungule wakati wa mkutano wa hadhara mara baada ya kumaliza kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo katika eneo hilo na kuwashukuru wapiga kura wake kupitia mkutano huo,ambapo aliahidi kutoa Milioni 20 za Mfuko wa jimbo kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati katika kata hiyo.
  Wananchi wa kata ya Kilungule Kimara jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Ubungo Saed Kubenea katika mkutano wake wa hadhara
  Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Saed Kubenea akizungumza na mmoja wa wazee Maarufu wa kata ya Kilungule mara baada ya kumaliza kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo katika eneo hilo
  Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Saed Kubenea akifurahi na wakazi wa kata ya Kilungule mara baada ya kumaliza kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo katika eneo hilo
  Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Saed Kubenea akifurahi na wakazi wa kata ya Kilungule mara baada ya kumaliza kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo katika eneo hilo
  Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob akifuatilia mkutano wa Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea Kimara Kilungule.

  0 0

  MWENYEKITI wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi amezitaka Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kushirikiana katika kutumia utajiri wake mkubwa wa raslimali kunufaika kiuchumi. Ushirikiano huo ni pamoja na kuzindeleza raslimali hizo na kutumia nembo moja ya kibiashara ili kuzalisha mabilionea wakubwa duniani. 

  Mwenyekiti huyo alisema hayo katika mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili.  Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi akizungumza wakati akifungua mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam.

   Pamoja na kutoa wito huo Dk Mengi pia amempongeza Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli pamoja na serikali yake kwa kuwa mstari wa mbele kuboresha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Kenya. Aidha alisema dhamira yake ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda itasaidia kuwakwamua Watanzania kutoka katika umaskini. Katika mazungumzo hayo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania –TPSF Dr Reginald Mengi na Ujumbe wa Kenya umeongozwa na Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor. Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor akimpongeza Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi kwa kutoa risala nzuri ya ufunguzi wa mkutano huo.

  Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye amesema mkutano huo umeitishwa kutokana na kujitokeza vikwazo vya kufanya biashara baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya, jambo linalokwamisha malengo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kujenga uchumi unaoongozwa na sekta Binafsi. Kwa upande wake Kiongozi wa Ujumbe wa KEPSA Bw. George Owuor amesema Wafanyabiashara wa Kenya wanapenda sana kushirikiana kibiashara na wenzao wa Tanzania, na wangependa kuona vikwazo vinavyokwamisha mahusiano ya kibiashara vinaondolewa. Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor akiwasilisha mada kuhusu kupunguza pengo la biashara kati ya Tanzania na Kenya na kutumia fursa zilizopo na kutanua biashara nje ya mipaka katika mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam. Meneja anayeshughulikia Utafiti, Uchambuzi na Sera wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA, Victor Ogalo (kushoto) akitoa mada kuhusu changamoto za kisera za Tanzania na Kenya katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia walioketi ni Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor na Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi wakifuatilia kwa umakini mada hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Alaska Tanzania, Jennifer Bash wakifuatilia mada mbalimbali zikizokuwa zikiwasilishwa ukumbini hapo katika mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam. Pichani juu na chini ujumbe wa Tanzania na Kenya ulioshiriki mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam.   Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor na mwenyeji wake Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi katika mkutano huo. Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye akijibu maswali kwa waandishi wa habari (hawapo pichani). Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi.

  0 0

  Mgeni rasmi, Flora Kimaro ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Taasisi ya MOI akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliofanyika Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili leo. Pamoja na maadhimisho hayo Chama cha Wakunga Nchini (TAMA) kimepongezwa kwa kutoa huduma za afya ambapo watu wanapima afya leo katika hospitali hiyo. Siku ya Wakunga Duniani huadhimishwa Mei 5, kila mwaka, lakini TAMA tawi la Muhimbili imeamua kuadhimisha siku hii katika wiki ya unyonyeshaji duniani.

  Baadhi ya wananchi waliofika katika siku ya maadhimisho hayo wakimsikiliza mgeni rasmi,
  Mgeni rasmi akikakata utepe akiashiria kuanza kwa shughuli za maadhimisho hayo ikiwa ni pamoja na kupima watu mbalimbali afya
  Mmoja wa wauguzi, Gladisia Kessy akimpima afya mmoja wa watu waliofika Muhimbili leo kwa ajili ya kushuhudia maadhimisho hayo.
  Mgeni rasmi pamoja na baadhi ya maofisa wa Muhimbili wakiwamo wakunga wakielekea meza kuu leo.
  Baadhi ya watu wakifuatilia maadhimisho hay oleo.
  Maofisa wa Muhimbili wakiwamo wakunga wakiwa katika picha pamoja leo.

  0 0

  Niabu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mshiri wilayani Moshi ,alipotembelea kijiji hicho kusikiliza Changamoto zinazo wakabili hususani katika eneo la Nusu Maili lililopo chini ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.

  NA HAMZA TEMBA -WMU
  ...............................................................................

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo makani amesema  jukumu la uhifadhi wa Maliasili za taifa sio la Serikali pekee kwakua Maliasili hizo ni urithi wa taifa na kila mwananchi anapaswa  kujua kuwa ana jukumu la kulinda urithi huo kutokana na umuhimu wake kwa taifa na jamii kwa ujumla.

  Makani amesema hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mshiri, Jimbo la Vunjo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro katika ziara yake ya siku mbili mkoani humo kwa ajili kuona changamoto za uhifadhi na kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo yaliyohifadhiwa.

  Alisema askari pekee na mitutu ya bunduki haitoshi kulinda maliasili hizo kutokana na ukubwa wa maeneo yaliyopo ukilinganisha na rasilimali zilizopo. "Maliasili hizi zipo kwa faida ya kila mwananchi, tunawaomba muendelee kuiunga mkono Serikali katika kulinda Maliasili tulizonazo, tunahitaji kufanya uhifadhi shirikishi, utalii uimarike na nchi yetu ipate mapato zaidi tuweze kufikia uchumi wa kati", alisema Makani.

  Akitaja miongoni mwa faida hizo, Makani alisema maliasili za misitu husaidia upatikanaji wa mvua, kuweka mazingira bora kwa ajili ya kilimo na upatikanaji wa hewa safi. Kwa upande wa faida za kiuchumi alisema sekta hiyo kupitia utalii inachangia asilimia 17.2 ya pato la taifa na asilimi 25 ya mapato yote ya fedha za kigeni.

  Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro, Betrita Loibooki alisema hifadhi hiyo imejenga mahusiano mazuri na wananchi wa vijiji jirani na kwa kiasi kikubwa imefanikiwa kukabiliana na ujangili ambapo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita hakuna tukio lolote la ujangili wa tembo lililoripotiwa katika hifadhi hiyo.

  Betrita alisema katika kutekeleza agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la uwekaji wa vigingi vya mipaka kwenye maeneo ya hifadhi ili kuepuka migogoro na wananchi alisema jumla vigingi 290 vimewekwa kwa ushirikiano na wananchi kuzunguka hifadhi hiyo kwa urefu kwa kilomita 123 sawa na asilimia 100 ya lengo lililokusudiwa.

  Kwa upande wa Wananchi wa kijiji hicho cha Mshiri ambacho kinapakana na Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro waliiomba Serikali iwalegezee masharti waweze kuingia na waume zao pamoja na vijana wao wa kiume katika eneo la Nusu Maili lililopo ndani ya hifadhi hiyo waweze kusaidiana kazi ya kukata majani ya mifugo na kuokota kuni.

  Akitoa ombi hilo mbele ya Mhandisi Makani, mkazi wa kijiji hicho, Theresia Mtui alisema wanawake wa vijiji jirani na hifadhi hiyo wanaruhusiwa kuingia ndani ya eneo hilo kwa ajili ya kukata majani ya mifugo na kuokota kuni kavu lakini wanaume hawaruhusiwi.

  Alisema wapo tayari kuhifadhi na kulinda mlima huo “Tunaomba mturuhusu na mtupe angalao miaka miwili au mitatu ya majaribio muone tutakavyolinda msitu huu”, alisema Mtui.

  Mkazi mwingine wa kijiji hicho, Estomi Benjamin Moshi alisema “Ombi letu turuhusiwe kuingia na kukata majani tu katika eneo hili, tupo tayari kuilinda hifadhi hii kwa taratibu tutakazopewa”.

  Akijibu ombi hilo Naibu Waziri Makani alisema, ombi hilo litaenda kufanyiwa kazi kwa ushirikiano kati Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Wakuu wa Wilaya zinazozunguka eneo hilo la hifadhi ambazo ni Moshi, Rombo, Hai na Siha, Wizara ya Maliasili na Utalii na TANAPA ambapo wananchi watapewa mrejesho wa ombi lao hilo.

  Sheria za uhifadhi zinakataza mtu yeyote kuingia na kulisha mifugo kwenye maeneo yaliyohifadhiwa kisheria ikiwa ni pamoja na shughuli nyingine za kibinadamu, kutokana na umuhimu wa eneo hilo kwa wananchi wanaolizunguka na katika jitihada za Serikali kujenga uhifadhi shirikishi, Mwaka 2014 Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kilimanjaro iliruhusu wanawake pekee kuingia ndani ya eneo hilo umbali wa mita 800 kutoka kwenye mpaka wa hifadhi hiyo kwa ajili ya kukata majani ya mifugo na kuokota kuni, wanaume walizuiliwa kutokana na kujihusisha na uharibifu wa eneo hilo. 

  Nae mbunge wa Jimbo la Vunjo, James Mbatia alisema ili uhifadhi uimarike ni lazima uwepo ushirikiano wenye tija kwa Serikali, Wananchi na Hifadhi huku akitoa rai ushirikiano huo uimarishwe kwa maslahi ya pande zote.

  0 0

   Mkuu wa Kitengo cha Biashara, Steve Kimea wa ZOLA akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya uzinduzi wa duka hilo ambalo watakuwa wanatoa huduma pamoja na kuuza vifaa mbalimbali vitakavyotumika kupata umeme wa ZOLA.
  DUKA jipya linalouza vifaa na kutoa hudumaza umeme wa ZOLA lazinduliwa Mwenge jijini Dar es Salaam leo. Akizungumza wakati uzinduzi wa Duka hilo Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa ZOLA, Steve Kimea ametoa wito kwa Taasisi za Serikali ambazo hazina huduma za umeme hasa vijijini kushirikiana nao ili kuwafikia watu wengi zaidi hasa kwenye vituo vya afya ili kuwasaidia wagojwa pamoja na kinamama wajawazito.
    
  Amesema kuwa kampuni hiyo inayotoa umeme wa ZOLA hapa nchini imeshatoa huduma hiyo kwenye vituo vya Polisi pamoja na vituo vya huduma za afya na umeme upo vizuri.

  Hata hivyo amesema kuwa utakapo nunua  mtambo wa umeme waZOLA  utatengenezewa mfumo wa umeme katika nyumba yako kwa bei nafuu na wengine kwani huduma zao zinalingana na maisha ya Mtanzania.

  Amesema kuwa umeme wa ZOLA unaweza kutumika katika vifaa mbalimbali kama kuchaji simu, mashine za kunyolea, televisheni pamoja na kuwasha taa sita za ndani. 
  Pia ukinunua vifaa vya ZOLA utapata dhamana(Warrant) ya miaka mitano endapo kifaa chochote kitaharibika mteja utatengenezewa bila gharama yeyote ile. 
  Katikati ni Meneja Masoko  wa ZOLA Tanzania, Irene Mbowe akikata utepe kuzindua Duka linalouza  na kutoa huduma za ZOLA lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam leo, kulia ni Mkuu wa kitengo cha mauzo wa ZOLA, John Amach na Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa ZOLA, Steve Kimea wakishrikiana kukata utepe kuzindua duka hilo.
   Duka la ZOLA lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
   Meneja Masoko  wa ZOLA Tanzania, Irene Mbowe akipata maelekezo na Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa ZOLA, Steve Kimealeo katika uzinduzi wa Duka jipya ambalo linatoa huduma mbalimbali za umeme wa ZOLA jijini Dar es Salaam leo.
   Mfanyakazi wa kampuni inayotoa huduma ya umeme wa ZOLA akitoa maelekezo kwa baadhi ya wateja waliofika dukani hapo Mwenge  jijini Dar esSalaam leo wakati wa uzindu wa duka hilo.

  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo,(kushoto) amezungumzia umuhimu wa taasisi za umma zilizo chini ya mradi wa Benki ya Dunia kuhakikisha mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), iliyofungwa inafanyakazi mara moja ili kuongeza tija na ufanisi katika kuhudumia wananchi.

  Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua ufanisi wa matumizi ya TEHAMA katika hospitali ya rufaa ya Dodoma na Halmashauri ya Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Dkt. Sasabo  amewataka viongozi wa taasisi hizo kuhakikisha mifumo hiyo inakamilika na kuanza kazi mara moja.

  “Hakikisheni ifikapo mwezi Septemba mawasiliano yenu na huduma zenu zilizounganishwa kwenye mifumo ya TEHAMA inafanyakazi ili kurahisisha utendaji na kuiongezea Serikali mapato”, amesema Dkt. Sasabo.

  Dkt. Sasabo amemtaka Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya rufaa ya Dodoma Dkt. Samweli Seseja, kuhakikisha hospitali hiyo inakuwa na mfumo maalum wa mawasiliano utakaowezesha kuboresha huduma katika hospitali hiyo na kumudu ongezeko la watu katika Manispaa ya Dodoma.

  Akiwa wilayani Bahi, Katibu Mkuu huyo wa mawasiliano  amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya  wilaya ya Bahi Bi, Rachel Chuwa kuhakikisha mifumo ya Tehama iliyofungwa  katika ofisi za halmashauri hiyo na katika shule za sekondari wilayani humo inafanyakazi mara moja ili kuendana na malengo ya serikali katika utoaji wa huduma bora, za kisasa na kwa wakati kwa wananchi wake na hivyo kuiwezesha Tanzania kufikia malengo ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

  Serikali imekuwa ikihamasisha matumizi ya TEHAMA katika taasisi zake zikiwemo ofisi, shule, hospitali na vituo vya polisi  ili kuboresha huduma na kuwezesha uwazi katika ukusanyaji wa mapato na hivyo kuhamasisha wananchi kuchangia huduma kwa hiari.
  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0

  Na Agness Moshi- MAELEZO,

  Ni takribani mwaka mmoja sasa tangu taarifa za kujengwa kwa Mradi wa Bomba la Mafuta litakaloanzia Hoima Nchini Uganda mpaka Tanzania kwenye bandari ya Tanga kuenea kwenye vyombo vya habari ,mitandao ya kijamii na kwa wakazi wa Mkoa wa Tanga ambao ndio wahusika wakuu kwenye mradi huu japo unajengwa kwa manufaa ya mataifa haya mawili kwa ujumla.

  Mradi huu ni moja kati ya miradi mikubwa ambayo Nchi imeweza kutekeleza na utagharimu kiasi cha dola za Kimarekani Billioni 3.5 ambazo ni sawa na Tsh Trillioni 8 kwa fedha za kitanzania. Bomba hili linategemewa kuwa na urefu wa kilometa 1,445 likiwa na uwezo wa kusafirisha mapipa ya mafuta takribani 2,016,000 kwa siku na kutoa ajira zaidi ya 1,000 na vibarua zaidi ya 30,000.

  Taarifa hizo zilianza kuwa rasmi, mnamo tarehe 14 marchi 2016 ambapo Makamu wa Rais wa kampuni ya Total Afrika Mashariki Bw.Javier Rielo alimhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kuanza kwa ujenzi wa Mradi huo.

  Nyota njema ya Mradi huu ilianza kuonekana Aprili 24 ya mwaka jana, baada ya aliyekua Waziri wa Nishati na Madini Prof.Sospeter Muhongo kurejea Nchini kutoka Uganda, kuongea na waandishi wa habari kuhusu makubaliano yaliyofikiwa kwa mradi huo.

  Bwana Muhongo alisema kuwa, kulikua na mjadala mkubwa wa kuchagua wapi Mradi huo ujengwe na wapinzani wakubwa kwa Tanzania walikua Kenya lakini kutokana na ubora wa bandari ya Tanga ukilinganisha na bandari nyingine Tanzania ilichaguliwa kunufaika na mradi huu.

  “Bandari ya Tanga ni bora kwa sababu ina kina kirefu ambacho ni zaidi ya mita 23 ambayo ndicho kinayotakiwa Kimataifa kwasababu hiyo kinaweza kufanya kazi mwaka mzima”, alisema Prof. Muhongo.

  Chagizo la kuanza kwa mradi huu lilipamba moto Marchi 28 mwaka huu, baada ya Rais Magufuli kukutana na Mawaziri wa Nishati na Madini wa Serikali zote mbili katika Ukumbi wa Baraza la Mawaziri Ikulu, Jijini Dar es Salaam ili kujadili Maendeleo ya Mradi huo.

  Wahenga walisema “Hata Mbuyu ulianza kama Mchicha” wakiwa na maana kila kitu kikubwa kilianza kikiwa kidogo vivyo hivyo Mradi huu ulianza kwa ahadi, makubaliano na hatimaye utekelezaji.

  Mei 21 mwaka huu, Rais Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni walitia rasmi saini ya tamko la pamoja ili kukamilisha majadiliano ya vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi huo.

  Wakazi wa Mkoa wa Tanga, wanahesabu miezi miwili tangu kusainiwa rasmi kwa mkataba wa mradi huo utakaowapeleka kwenye mafanikio mbalimbali ikiwemo fursa za ajira , ukuaji wa kasi wa maendeleo , na kuurudishia umaarufu uliopotea wa mji huo.

  Ikumbukwe Mkoa huo, ulikua maarufu miaka ya 1960 na 1970 kutokana uwepo wa viwanda mbalimbali ikiwemo vya uzalishaji katani ambalo ni zao kuu la biashara mkoani humo .Lakini umaarufu huo ulipotea baada ya viwanda hivyo kushindwa kuendelea kuzalisha bidhaa za kutosha kama vile kiwanda cha saruji Tanga.

  Licha ya mji huu kupoteza umaarufu bado ni kivutio kikubwa cha Utalii kwani kuna Mapango ya Amboni ambayo yamekua yakiupamba mji huo wenye kilomita za mraba 27,348 na Wilaya 10 ambazo ni Handeni Vijijini, Handeni Mjini, Kilindi, Korogwe Vijijini, Korogwe Mjini, Lushoto, Mkinga, Muheza, Pangani na Tanga Mjini pamoja na majimbo 11 ya uchaguzi ambayo ni Tanga Mjini, Pangani, Handeni, Korogwe Mjini, Korogwe Vijijini, Lushoto, Bumbuli, Mlalo, Kilindi Mkinga na Muheza.

  Miaka , na miezi ilipita hatimaye, Mkoa huo umefufua umaarufu wake kupitia Kata ya Chongoleani inayopatikana katika moja ya Wilaya mkoani humo, yenye wakazi wapatao 4,737 , kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2012 ,ambao pia karibu nusu ya wakazi wake ni wanufaika wa huduma ya umeme tangu mwaka 2015 kufuatia mpango wa serikali wa usambazaji umeme vijijini.

  Agosti 5 mwaka huu (kesho), Tanga inatarajia kurudisha sifa na umaarufu uliopotea kwa zaidi ya miaka takribani 60 kufuatia shughuli za uwekwaji wa jiwe la msingi la Mradi itakayofanywa na Rais Magufuli na Museveni ambao utapelekea Nchi zote mbili kwenye mapinduzi ya kiuchumi kwa Nchi na wakazi wa Mkoa huo kupitia fursa mbalimbali hususani kwenye upatikanaji wa Ajira, biashara, chakula ,malazi, bima na huduma za kifedha.

  Kwa Upande wake, Mkurugenzi Wa Mawasialiano Ikulu Bw.Gerson Msigwa ametoa wito kwa Watanzania wanaoishi mbali na Mkoa huo kufuatilia matangazo na machapisho mbalimbali yanayotolewa ili kupata taarifa kuhusiana na shughuli hiyo na kwa upande wa wakazi wa Mkoa huo amewasihi kuhudhuria ili waweze kushuhudia tukio hilo la kihistoria.

  Ifike wakati Watanzania tujivunie na tumpongeze Rais Magufuli kwa juhudi anazozifanya ili kuinua kipato kwa Wananchi kuanzia ngazi ya chini kwa kutengeneza fursa mbalimbali za ajira, miundo mbinu ili kurahisha shughuli za biashara na Afya kwa ujumla badala ya kushabikia mambo yasiyo na tija kwa maendeleo.

  Kwa wakazi Mkoa Tanga, Serikali imetekeleza ahadi iliyotolewa hivyo basi ni wajibu wao kuunga mkono Mradi huu kwa kutoa ushirikiano hususani katika kufanya kazi kwa bidii, kulinda ili kuzuia uharibifu au kukwamisha shughuli hizo kwa namna yoyote.

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpokea Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere Dar es Salaam tayari kuelekea jijini Tanga kwa Sherehe za Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi toka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania utakaofanyika kesho Agosti 5, 2017 katika eneo la Chongoleani.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpokea Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere Dar es Salaam tayari kuelekea jijini Tanga kwa Sherehe za Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi toka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania utakaofanyika tarehe 5 Agosti 2017 katika eneo la Chongoleani.Pichani kulia ni Naibu Spika wa Bunge Mh.Dkt. Dkt Tulia Ackson Mwansasu

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira,Bodi ya Kamisheni ya Ardhi na Uongozi wa Kamisheni ya Ardhi katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambacho kimejadili mambo mbali mbali ya kiutendaji,
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira,Bodi ya Kamisheni ya Ardhi na Uongozi wa Kamisheni ya Ardhi katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambacho kimejadili mambo mbali mbali ya kiutendaji
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira,Bodi ya Kamisheni ya Ardhi na Uongozi wa Kamisheni ya Ardhi katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambacho kimejadili mambo mbali mbali ya kiutendaji,(kuchoto) Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,

  0 0

   Mhe. Spika Job Ndugai  leo amekutana na Spika wa Bunge  la Iran, Mhe. Dkt. Ali  Larijani na kufanya nae mazungumzo yenye lengo la kuimarisha mahusiano ya kibunge baina ya Bunge la Tanzania na Iran.

  0 0

  Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma Dkt. Samwel Seseja (Wa Pili kushoto), akitoa taarifa ya namna mfumo wa TEHAMA unavyofanya kazi katika hospitali hiyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo (kushoto), alipokagua matumizi ya TEHAMA katika hospitali hiyo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo (Wa Pili kulia), akiwasili katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma kukagua utendaji wa mifumo ya TEHAMA katika hospitali hiyo. Wa Kwanza kushoto ni Afisa TEHAMA wa hospitali hiyo ni Bi. Sylivia Urio.
  Muonekano wa mifumo ya TEHAMA iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma ambayo itawezesha hospitali hiyo kutoa huduma kwa njia ya kisasa na kwa urahisi.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bi. Rachel Chuwa, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo (kushoto).

  ………………………

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo, amezungumzia umuhimu wa taasisi za umma zilizo chini ya mradi wa Benki ya Dunia kuhakikisha mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), iliyofungwa inafanyakazi mara moja ili kuongeza tija na ufanisi katika kuhudumia wananchi.

  Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua ufanisi wa matumizi ya TEHAMA katika hospitali ya rufaa ya Dodoma na Halmashauri ya Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Dkt. Sasabo amewataka viongozi wa taasisi hizo kuhakikisha mifumo hiyo inakamilika na kuanza kazi mara moja.


  “Hakikisheni ifikapo mwezi Septemba mawasiliano yenu na huduma zenu zilizounganishwa kwenye mifumo ya TEHAMA inafanyakazi ili kurahisisha utendaji na kuiongezea Serikali mapato”, amesema Dkt. Sasabo.


  Dkt. Sasabo amemtaka Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya rufaa ya Dodoma Dkt. Samweli Seseja, kuhakikisha hospitali hiyo inakuwa na mfumo maalum wa mawasiliano utakaowezesha kuboresha huduma katika hospitali hiyo na kumudu ongezeko la watu katika Manispaa ya Dodoma.


  Akiwa wilayani Bahi, Katibu Mkuu huyo wa mawasiliano amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi Bi, Rachel Chuwa kuhakikisha mifumo ya Tehama iliyofungwa katika ofisi za halmashauri hiyo na katika shule za sekondari wilayani humo inafanyakazi mara moja ili kuendana na malengo ya serikali katika utoaji wa huduma bora, za kisasa na kwa wakati kwa wananchi wake na hivyo kuiwezesha Tanzania kufikia malengo ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.


  Serikali imekuwa ikihamasisha matumizi ya TEHAMA katika taasisi zake zikiwemo ofisi, shule, hospitali na vituo vya polisi ili kuboresha huduma na kuwezesha uwazi katika ukusanyaji wa mapato na hivyo kuhamasisha wananchi kuchangia huduma kwa hiari.


  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0

  Na Estom Sanga-TASAF 

  Vikundi vya baadhi ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF kutoka mikoa ya Dodoma, Pwani Manyara na Singida vinashiriki kwenye maonyesho ya nane nane yaliyoanza mwanzoni mwa wiki hii mjini Dodoma. 

  Vikundi hivyo vilivyoko kwenye banda la Ofisi ya Rais kwenye eneo la maonyesho la Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma, vinaonyesha bidhaa zilizotengenezwa na vikundi hivyo baada ya kuwezeshwa na TASAF ikiwa ni njia mojawapo ya kuinua shughuli za uzalishaji mali na kuongeza mapato ya walengwa wa Mpango huo wenye lengo la kusaidia jitihada za serikali za kuwapunguzia wananchi kero ya umasikini. 

  Bidhaa zinazotengenezwa na vikundi hivyo na ambazo zimeletwa kwenye maonyesho hayo ni pamoja na sabuni na mafuta ya manukato ambavyo vimetengenezwa kwa kutumia mmea wa mwani ambao humea kwenye maeneo ya baharini. 

  Bidhaa nyingine ambazo zimezalishwa na vikundi hivyo vya walengwa wa TASAF ni pamoja na asali,ubuyu,mafuta ya alizeti na mifuko bora ya kuhifadhia nafaka ambavyo vimetokana na kazi za mikono ya walengwa hao ikiwa ni maojawapo ya sharti la kuzifanya kuinua uchumi na kujiongezea kipato kwa njia ya vikundi. 

  Walengwa hao wamepongeza hatua ya serikali kupitia TASAF kuwashirikisha kwenye maonyesho hayo kwani hatua hiyo inasaidia kutangaza shughuli za uzalishaji mali zinzofanywa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini ambao wanahitaji masoko ya bidhaa wanazozizalisha ili kukuza uchumi wao. 

  “hii ni hatua muhimu katika kutangaza vikundi vya uzalishaji mali ambavyo kimsingi havina uwezo wa kutangaza bidhaa kupitia vyombo vya habari kutokana na gharama zake”amesema mwenyekiti wa kikundi cha uzalishaji asali cha Juhudi kutoka Kongwa mkoani Dodoma bwana Augen Lekas Makanda. 

  Katika maonyesho hayo yaliyofunguliwa na Mkuu wa mkoa wa Singida, Dokta Rehema Nchimbi,TASAF pamoja na mambo mengine imekuwa ikitoa ufafanuzi wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini pamoja na matumizi ya malipo kwa walengwa na kutumia utaratibu wa kielektroniki kama njia mojawapo ya kuboresha huduma zake kwa walengwa. 

  Zifuatazo ni baadhi ya picha za wananachi wanaotembelea banda ya maonyesho la TASAF lililoko kwenye jengo la ya Ofisi ya Rais kwenye viwanja vya Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma.
   Baadhi ya maafisa wa TASAF wakitoa maelezo kwa wanafunzi waliotembelea banda la maonyesho la TASAF kwenye viwanja vya nane nane ,Nzuguni nje kidogo ya mji wa Doodoma.
   Mmoja wa walengwa wa TASAF kutoka kikundi cha Wakulima wa Mwani Msichoke cha Bagamoyo akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la TASAF. Kikundi hicho kimewezeshwa na TASAF na sasa kinatengeza sabuni na mafuta kutokana na zao la mwani kama njia ya kujiongezea kipato.
  Mtaalam wa Mawasiliano wa TASAF Bi. Zuhura Mdungi akitoa maelezo kwa baadhi ya watu waliotembelea banda la maonyesho la TASAF lililoko kwenye jingo la Ofisi ya Rais kwenye eneo la Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma.

   Mmoja wa maafisa wa TASAF, Bi. Grace Kibonde akitoa maelezo kwa baadhi ya watu waliotembelea banda la TASAF kwenye maonyesho ya nane nane  kwenye eneo la Nzuguni  nje kidogo ya mjini Dodoma
   Mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya Nane Nane kanda ya kati  Bi.Tabu Ally Likoko akipata maelezo kutoka kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini ambao wameunda kikundi cha kuzalisha sabuni na mafuta kwa kuwezeshwa na TASAF .
   Baadhi ya wanafunzi wakipata maelezo ya namna shughuli za TASAF zinazvyotekelezwa kutoka kwa watumishi  wa taasisi hiyo inayotekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji Baraza la Wafanyakazi ambacho kimefanyika leo katika hospitali hiyo. Kikao hicho kinajadili jinsi ya kuboresha huduma za afya zinazotolewa na MNH.
  0002
  Baadhi ya wafanyakazi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Museru.
  0003
  Mkurugenzi wa Fedha na Mipango, Gerald Jeremia  akieleza mikakati ya kuboresha huduma za afya katika kurugenzi ya upasuaji pamoja na huduma nyingine.
  0004
  Baadhi ya wafanyakazi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Fedha na Mipango leo.
  0005
  Mshauri Mwelekezi katika Masuala ya Mawasiliano, Dk. Henry Mambo akieleza mkakati wa mawasiliano ambao umeandaliwa kwa ajili ya kufikia malengo ya kutoa huduma bora.
  0006

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga akiwa ameongozana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (haonekani pichani) na kupokewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa tayari kwa Sherehe za Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi toka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania utakaofanyika Agosti 5 2017 katika eneo la Chongoleani.
  Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga akiwa ameongozana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kupokewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa tayari kwa Sherehe za Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi toka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania utakaofanyika Agosti 5 2017 katika eneo la Chongoleani.

  0 0
  0 0

  Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Kupoozea Umeme cha Njiro Mkoani Arusha, Mhandisi Lembrice Mollel, akitoa maelezo kuhusu mitambo ya Kituo hicho kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt Nyamajeje Weggoro (kulia) alipotembelea Kituo hicho kukagua mradi wa kusambaza umeme uliofadhiliwa na AfDB, uliogharimu Dola milioni 4.2, Jijini Arusha
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt Nyamajeje Weggoro (wa pili kulia) akipewa maelekezo ya namna mitambo ya usambazaji umeme katika Kituo cha Njiro Jijini Arusha inavyoendeshwa kwa mfumo wa Kidigitali. Mitambo hiyo imefadhiliwa na Benki ya AfDB ukiwa ni mkopo wenye masharti nafuu.
  Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Umeme cha Njiro Mkoani Arusha, Mhandisi Lembrice Mollel (kulia) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki Dkt Nyamajeje Weggoro (katikati) alopotembelea Kituo cha kusambaza umeme cha Njiro Jijini Arusha. Mitambo hiyo imefadhiliwa na Benki ya AfDB. Kushoto ni Meneja wa Mradi wa umeme wa AfDB Mhandisi Florence Gwang’ombe.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro (kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa wataalamu wa Kituo cha Kupoozea Umeme cha Njiro, Mkoani Arusha, kuhusu usalama wa mitambo kutakapo tokea dharula. Mitambo hiyo imefadhiliwa na Benki ya AfDB, ikiwa ni mkopo wenye masharti nafuu.
  Muonekano wa mitambo iliyofadhiliwa na Benki ya Maedeleo ya Afrika (AfDB), katika kituo cha kusambaza umeme cha Njiro, Mkoani Arusha. Mitambo hiyo imesaidia kupatikana kwa umeme wa ziada wa Megawati 70.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt Nyamajeje Weggoro akizungumza na Msimamizi wa Kituo cha usambazaji umeme cha Njiro-Arusha, Mhandisi Lembrice Mollel na wengine (hawapo pichani) baada ya kutembelea mradi huo na kuridhishwa na matokeo ya mradi huo kwa wakazi wa Arusha.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt Nyamajeje Weggoro (kushoto) na Mshauri wake Amos Cheptoo wakionesha kufurahishwa na ufanisi wa mradi wa kusambaza umeme wa Njiro Jijini Arusha baada ya kukagua na kujiridhisha na thamani ya mradi huo uliofadhiliwa na Benki yake kwa gharama Dola milioni 4.2.

  (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

  ……………………….

  Na Benny Mwaipaja, WFM-Arusha

  WAKAZI wa Jiji la Arusha wameondokana na na adha ya umeme kukatika mara kwa mara baada ya kukamilika kwa mradi wa umeme katika Kituo cha kupoozea umeme cha Njiro kilichoko Mkoani Arusha chenye uwezo wa kuzalisha megawati 130.

  Hali hiyo inatokana na Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB kuwekeza kiasi cha Dola milioni 4.2, ukiwa ni mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili kuongeza uwezo wa Kituo hicho kuzalisha umeme unaotumika kwa ajili ya makazi ya watu, maeneo ya biashara na viwanda.

  Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Usambazaji umeme cha Njiro Mhandisi Lembrice Mollel amesema mradi huo umesaidia kuongeza Megawati 130 za umeme ambao umekidhi mahitaji ya Jiji la Arusha linalo hitaji Megawati 60 hivyo kubakiwa na Umeme wa ziada kiasi cha Megawati 70.

  Alisema kuwa tatizo la kukatika katika kwa umeme katika mji huo wa kitalii na kibiashara litakuwa historia na kwamba umeme unaozalishwa kituoni hapo unasafirishwa kwenye maeneo mengine yenye uhitaji ikiwemo mikoa ya Kilimanjaro na Tanga.

  Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Umeme wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Mhandisi Frorence Gwang’ombe amesema kuwa lengo la mradi lilikuwa kupatikana kwa umeme wa uhakika na kuimarisha miundombinu ya usambazaji na kupooza umeme jambo ambalo limefikiwa kikamilifu.

  Alisema kuwa uboreshaji wa Kituo hicho cha kupoozea Umeme cha Njiro ni sehemu ya utekelezaji wa uboreshaji wa Sekta ya Umeme nchini kupitia mradi ujulikana kama Electricity V, uliofadhiliwa na AfDB kupitia mkopo nafuu wa kiasi cha Dola milioni 8, ukihusisha pia mkoa wa Dar es Salaam, Vituo vya kupooza umeme vya Sokoine na Ilala.

  “Mradio huu umelenga kuwahudumia wananchi takribani 8,400 hivyo kukamilika kwa mradi huo ni neema kwa wananchi wengi kwa kuwa utasaidia kuimarisha uwezo wao wa kibiashara ndani ya Jiji la Arusha na maeneo mengine ya nchi” alisema Mhandisi Gwang’ombe

  Alifafanua kuwa uboreshaji wa mradi wa Kituo cha Kupooza Umeme cha Njiro umehusisha ufungaji wa transfoma mpya 2 zenye uwezo wa kufua megawati 50 kila moja na nyingine 2 zenye uwezo wa kubeba megawati 15 kila moja, hatua iliyosaidia kuongeza kiwango hicho cha umeme.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), anayehudumia Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, ameelezea kuridhishwa na utekelezaji pamoja na manufaa ya mradi huo utakaosaidia kukuza biashara na kusisimua uwekezaji wa viwanda katika mkoa wa Arusha.

  ‘Arusha ni mji wa Kitalii hivyo unahitaji kuwa na umeme wa kutosha utakaosaidia katika uwekezaji na ufanisi wa biashara, upatikanaji wa umeme wa uhakika utachochea shughuli za Kilimo na viwanda kwa kasi kubwa’, aliongeza Dkt. Weggoro.

  Amewataka wakazi Arusha na Watanzania kwa ujumla kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazotokana na kuboreshwa kwa miundombinu ya umeme ili kwenda sambamba na Sera ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

  Baadhi ya wakazi wa Mji wa Arusha, wakiwemo Bw. Jackson William na Bw. Steven Chitara wamekiri kuwa maisha yao yamebadilika kiuchumi kutokana na kuimarika kwa upatikanaji wa umeme ikilinganishwa na hapo awali.

  Wamesema kuwa vijana wengi wamejiajiri kupitia shughuli mbalimbali za uzalishaji mali zinazotegemea uwepo wa nishati hiyo kama kuchomelea vyuma, vinyozi, ufundi wa aina mbalimbali pamoja na wafanyabiashara wakubwa kuanza kuvutiwa kuwekeza mkoani humo.

  0 0


  Na: Agness Moshi – MAELEZO.

  Ulaji wa nyama una faida lukuki kwa afya ya binadamu ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa virutubisho vya aina ya protini ambayo ni rahisi kutumika mwilini, madini mbalimbali (Calcium, Magnesium, Phosphorus, Zinc na Chuma); vitamini aina ya folic asidi, E, B na B12 ambayo inapatikana katika nyama pekee.

  Nyama pia inasaidia katika ukuaji na kuongeza afya ya mlaji kutokana na uwezo mkubwa wa kujenga mwili, kukarabati seli za mwili zilizokufa, kuzalisha chembe hai mpya, kurekebisha kinga ya mwili, kuongeza damu na kuimarisha mifupa.

  Hata hivyo faida zote hizo zinapatikana tu, kwa walaji wa nyama iliyo bora na yenye kiwango. Hivyo ni vizuri wananchi wakazingatia kanuni za ulaji wa nyama yenye kiwango ili kujiepusha na athari zinazoletwa na nyama isiyo na kiwango.

  Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Bi.Suzana Kiango amesema kuwa nyama yenye kiwango na bora huanzia kwenye utunzwaji wa mifugo wenye kuzingatia kanuni za uzalishaji bora, unenepeshaji wa mifugo yenye umri mdogo kwa kuwalisha chakula mchanganyiko kwa muda usiopungua siku 90 kabla ya kuchinja.

  Bi.Kiango amesema kuwa hatua nyingine ni katika uchinjaji ambapo inashauriwa ufanyike kwenye machinjio bora ambayo yanakidhi viwango vya usafi. Hii ni pamoja na kuwa na sakafu na kuta zinazosafishika, maji ya kutosha na sehemu za kuning’iniza wakati wa kuchuna na kupasua.

  “Kanuni za uchinjaji ni pamoja na kupumzisha mifugo ili kuipoteza fahamu na kumfanya mnyama asiogope na kuzalisha asidi nyingi inayosababisha nyama kuwa ngumu, pia iwe rahisi kutoa damu yote katika misuli. Uning’inizwaji wa chune mara baada ya kuchinjwa unasaidia kuondoa damu iliyo mwilini. Endapo damu haitatoka yote kwenye chune itasababisha nyama kuwa na rangi nyeusi na kuharibika mapema”, alisema Bi.Kiango.

  Madhara ya ulaji wa nyama isiyo na viwango na bora ni pamoja na kupata magonjwa ya tumbo, kuharisha na kutapika endapo nyama itapata vimelea vya magonjwa hayo, kuugua magonjwa ya kuvimba miguu, kifua kikuu, shinikizo la damu, kisukari na kansa.

  Hata hivyo, Bi. Kiango amesisitiza kuwa magonjwa haya yanaweza kuwatokea pia watu ambao hawatumii kabisa nyama kwa hivyo si nyama pekee ndio chanzo cha magonjwa haya japo inaweza kuwa sababu ya mtu kuugua.

  “Bodi imeendelea kutoa elimu kwa watumiaji na wachinjaji wa nyama kupitia vyombo mbalimbali vya habari kama vile, redio, televisheni na magazeti. Pia katika maonesho mbalimbali kama Saba saba na Nane nane ambapo wataalamu wa bodi hutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea mabanda ikiwa ni pamoja na kusambaza vipeperushi” amesema Bi.Kiango.

  Namna nyingine ya kutoa elimu ni pamoja na kutumia matamasha ya nyama choma, wiki ya mayai na maonesho ya kuku, wiki ya chakula salama na siku ya chakula duniani. Wakati wa shughuli hizi wanashiriki hupatiwa elimu kuhusu faida na athari za kula nyama isiyo na viwango ili kunusuru afya zao.

  Aidha walaji huelekezwa maeneo mbalimbali wanayoweza kupata nyama hiyo, na kwa upande wa wafanyabiashara wa nyama hupewa maelekezo ya kuboresha miundombinu ya kuzalisha, kuchinja na kuuza kwa kuzingatia viwango vya ubora na usalama.

  Kutokana na baadhi ya wafanyabiashara ya nyama kuendelea kuwauzia walaji nyama isiyo na viwango kwa kujua au kutojua madhara ya nyama hizo, Bi.Kiango alisema kuwa Bodi inachukua hatua za kuhakikisha wafanyabiashara hao wanapata uelewa wa kutosha.

  “Bodi imeanza kutoa mafunzo kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ambao watashiriki katika kutekeleza majukumu ya Bodi ikiwa ni pamoja na kusimamia uzalishaji wa nyama na kuelimisha wachinjaji ,walaji na wadau wengine wanaojishughulisha na uzalishaji wa nyama”alifafanua Bi.Kiango.

  Aliendelea kusema mafunzo hayo yameshatolewa kwa vitendo kwa watumishi wanne kutoka katika kila Mamlaka za Serikali za Mitaa za mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Dodoma ambapo hadi sasa jumla ya wadau 490 katika maeneo tajwa wamekwisha patiwa elimu hiyo. Pia mafunzo yanatolewa na wadau wengine ambao ni Chuo cha nyama cha VETA, Dodoma na Kampuni ya nyama ya jijini Arusha.

older | 1 | .... | 1327 | 1328 | (Page 1329) | 1330 | 1331 | .... | 1897 | newer