Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1329 | 1330 | (Page 1331) | 1332 | 1333 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Meneja Mauzo Kampuni ya Tigo Mkoa wa Mtwara, Lilian Mwalongo akionesha simu mpya ya Tecno R6 kwa baadhi ya wananchii waliofika katika banda la Tigo katika maonesho ya Kilimo ya Nane Nane yanayoendelea Mkoa wa Lindi.
  .Moja ya kikundi cha Timu ya Mauzo Tigo wakiwa katika picha ya pamoja katika maonesho ya Kilimo yanayoendelea Mkoani Lindi.
  Meneja Mauzo Kampuni ya Tigo Mkoa wa Mtwara, Lilian Mwalongo akionesha simu mpya ya Tecno R6 kwa baadhi ya wananchii waliofika katika banda la Tigo katika maonesho ya Kilimo ya Nane Nane yanayoendelea Mkoa wa Lindi. · 

  Wakati maadhimisho haya yanafanyika mkoani Lindi kitaifa, Tigo inashiriki kikamilifu katika maadhimisho ya Nanenane katika mikoa ya Morogoro, Mbeya, Dodoma, Arusha, Mwanza na Tabora.

  Pia kama ilivyo kawaida yetu ya kuwajali wateja na wananchi kwa ujumla kupitia bidhaa na Huduma zetu bora, kupitia msimu huu wa Nanenane tunatoa ofa kabambe kuhakikisha wananchi wanaendelea kufurahia maisha ya kidigitali. Ofa hizi ni kwa simu za kijanja aina ya Tecno S1 kwa bei ya TZS 99,000/- na Tecno R6 kwa bei ya TZS 195,000 tu. Unaponunua simu hizi unapata mpaka GB 3 za kuperuzi na mtandao ulioboreshwa zaidi Tanzania. ·

   Hii ni sababu tosha kwa wakazi wote wa Lindi na mikoa mingine ambapo maonyesho haya ya Nanenane yanaendelea kuwahi katika banda la Tigo na kujinyakulia simu ili kupata nafasi ya kujishindis Zawadi tulizozitaja.

  Hayo yalisemwa na Meneja Mauzo wa Tigo mkoa wa Mtwara, Lilian Mwalongo kwenye maonesho hayo jana

  0 0

  Na Mathias Canal, Lindi

  Wizara ya Nishati na Madini imetambua kadhia iliyokuwa inawakumba wananchi kupata taarifa sahihi na za uhakika kuhusu masuala ya nishati jadidifu hapa nchini na hatimaye kuanzisha mfumo rahisishi wa taarifa unaojulikana kama Tanzania Renewable Energy Information Management System (TREIMS).

  Mfumno huu utasaidia kuhakikisha kwamba taarifa sahihi za masuala ya nishati jadidifu zinapatikana ambapo pindi taarifa zinapopatikana zitakuwa zinahakikiwa kabla ya kuwafikia watumiaji.

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Greyson Lwenge (Mb) amesifu mfumo huo kuwa utapunguza muda wa wadau unaotumika kutafuta taarifa zinazohusu nishati jadidifu sambamba na kufuatilia kwa urahisi maenedeleo ya miradi ya nishati jadidifu inayotekelezwa hapa nchini.

  Mhe Lwenge alisema kuwa kulikuwepo na upatikanaji hafifu wa taarifa za masuala ya nishati jadidifu hapa nchini tatizo ambalo lilichangia kuwa na maendeleo kidogo katika sekta ndogo ya nishati jadidifu.

  Alisema serikali isingeweza kufikia malengo kwa uduni wa taarifa lakini hatua ambao imefikiwa sasa na Wizara ya nishati na madini itakuwa mbadala wa mafanikio kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

  Mfumo huu unajumuisha taarifa zihusuzo sera, sheria na mifumo mingine ya kisheria inayohusika na usimamizi na uendeleaji wa sekta ndogo ya nishati jadidifu.

  Mhandisi Lwenge pia amesifu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvvuvi kwa kurejesha tena Maonesho hayo na Nanenane katika Mkoa wa Lindi ikiwa ni mara ya nne mfululizo huku akieleza kufurahishwa jinsi wananchi wanavyoendelea kujitokeza kupata elimu ya Kilimo Mifugo na Uvuvi.

  Alisema kuwa kauli mbiu ya maonesho ya Nanenane kwa mwaka 2017 inayosema“Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati” inaakisi mafanikio na fursa kwa kila mwananchi kupata mbinu bora za kilimo mifugo na uvuvi.

  Sikukuu ya wakulima inayofahamika kuwa Nanenane ina sherekewa nchini kote tarehe 8 Agosti kila mwaka. Sherehe hiyo inatayarishwa na kuratibiwa na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kuhusisha Taasisi, Wizara na mtu mmoja mmoja wanaoshughulika na kilimo. 
  MWISHO.

  Mgeni rasmi Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Greyson Lwenge (Mb) alipotembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini wakati wa Maonesho ya Nanenane ambayo kitaifa yanafanyika Katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
  Mgeni rasmi Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Greyson Lwenge (Mb) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini wakati wa Maonesho ya Nanenane ambayo kitaifa yanafanyika Katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

  0 0


  Na Mwamvua Mwinyi,Pwani 

  JESHI la Polisi Mkoani Pwani ,linamshikilia mfanyabiashara anaedaiwa kuwasafirisha wahamiaji haramu 72 raia kutoka nchini Ethiopia,Rajabu Hitaji (30)mkazi wa Vigwaza ,Bagamoyo .
  Aidha jeshi hilo linawashikilia pia wahamiaji haramu hao kwa kosa la kuingia nchini bila kibali . 

  Akitolea ufafanuzi juu ya tukio hilo ,kamanda wa Polisi mkoani Pwani(ACP) Jonathan Shanna ,alisema uchunguzi unaendelea na watafikishwa ofisi za uhamiaji kwa hatua nyingine stahiki. 

  Alieleza ,mtuhumiwa Hitaji ambae ni mfanyabiashara alikamatwa jana, saa 3.30 asubuhi huko maeneo ya pori la ranchi ya Taifa Narco ,Vigwaza wilaya ya kipolisi Chalinze . 

  “Kufuatia msako mkali ulioendeshwa na makachero wetu baada ya kupata taarifa juu ya uwepo wa raia walioingia nchini pasipo kufuata taratibu za uhamiaji na raia hao baada ya kugundua kuna gari la polisi linawafuatilia “
  “Waliingia kwenye hifadhi hiyo kwa lengo la kujificha lakini askari wetu waliweza kubaini mahali walipo kufuatia msako mkali uliokuwa ukiendeshwa katika ranchi hiyo ” alisema kamanda Shanna . 

  Alisema askari hao walifanikiwa kuwakamata kundi la kwanza la wahamiaji haramu 63 wakiwa mahali ambapo gari halifikiki . 

  Kamanda Shanna ,alielezea kwamba ,licha ya kukamatwa kundi hilo askari waliendelea na msako na kufanikiwa kukamata kundi jingine la wahamiaji haramu Tisa ,waliokuwa wakitafuta njia ya kutoroka katika ranchi ya taifa ya Narco . 

  Wakati huo huo ,MTU mmoja na watoto wawili wamefariki dunia baada ya mtumbwi waliokuwa wakitumia kuvuka mto Ruvu kuzama.
  Mtumbwi huo walikuwa wakiutumia kutoka upande wa Vigwaza kwenda upande wa Mlandizi katika mto huo wilaya ya kipolisi Chalinze Mkoani Pwani. 

  Kamanda Shanna alisema ,tukio hilo limetokea majira ya saa kumi alfariji usiku wa kuamkia agost 6. 

  Aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Sikuzani Mussa(41)ambae mwili wake bado haujapatikana na jitihada za kuutafuta zinaendelea.
  Kamanda Shanna, alisema watoto waliopoteza maisha kwenye tukio hilo ni pamoja na Nusurat Haji mwenye miezi minne na Fesali Hamza mwenye mwaka mmoja . 

  Aidha katika tukio hilo watu wawili waliweza kuokolewa wakiwa hai ambao ni Zuwena Ramadhani (29)na Tero Mziray (20).
  “Dereva wa mtumbwi huo haijajulikana alipo na inaaminika ya kwamba yeye hajafa maji .”alisema . 

  Kamanda Shanna, alieleza chanzo cha mtumbwi huo kuzama maji bado kinachunguzwa na miili ya marehemu imeshafanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu zao kwa ajili ya mazishi .


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kufungua rasmi  kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro maeneo ya Maweni jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Mwijage wakifunua kitambaa kama ishara ya kuweka jiwe la msingi upanuzi wa kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh  maeneo ya Kange jijini Tanga leo Agosti 6, 2017


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wafanyakazi wa kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro alipowasili kukizindua maeneo ya Maweni jijini Tanga leo Agosti 6, 2017

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na mwandishi wa habari wa TBC Bi. Vumilia Mwasha baada ya kuweka jiwe la msingi upanuzi wa kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh  maeneo ya Kange jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakicheza ngoma ya Baikoko wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi wa matanki ya kuhifadhia mafuta ya kampuni ya GBP yenye ujazo wa lita 300,000 eneo la Raskazone jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakikata utepe kwenye sherehe za  uwekaji wa jiwe la msingi wa matanki ya kuhifadhia mafuta ya kampuni ya GBP yenye ujazo wa lita 300,000 eneo la Raskazone jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga  ngoma ya Baikoko wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi wa matanki ya kuhifadhia mafuta ya kampuni ya GBP yenye
  ujazo wa lita 300,000 eneo la Raskazone jijini Tanga leo Agosti 6, 2017  0 0

  KATIKA kuongeza ufanisi kwenye utendaji, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amefanya mabadiliko ya baadhi ya watendaji kwenye wizara na idara zilizo chini ya wizara hiyo.

  Mabadiliko hayo madogo yamegusa Chuo Cha Taifa cha Utalii, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) na Idara ya Utalii kwenye makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

  Akitangaza mabadiliko hayo mwishoni mwa wiki mjini Dodoma, Waziri Maghembe alimtaja Deogratius Mdamu kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Zahoro Kimwaga TAWA kukaimu nafasi ya Mkuu wa Shughuli za Utaliiwa Picha.

  Profesa Maghembe alisema pia amemteua Phillip Chitaunga, kuwa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Maendeleo ya Utalii kwenye makao makuu ya wizara, ili kujaza nafasi iliyoachwa na Uzeeli Kiangi aliyestaafu utumishi kwa mujibu wa sheria.

  "Kwenye Chuo chetu cha Taifa Utalii, ninamteua Dk. Shogo Mlozi kuwa Kaimu Mkuu wa Chuo ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Utalii na Ukarimu kwenye Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT)," alisema.

  Pamoja na hao, Waziri huyo alimtaja Stephen Madenge kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha Taifa cha Utalii ambaye anabadilishana nafasi na Martina Hagwet, anayekwenda kushika wadhifa wa Kaimu Meneja wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Kampasi ya Temeke.

  Aidha, Waziri Maghembe alisema kwenye Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori, amemteua Dk. James Wakibara kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu nafasi iliyoachwa wazi na Martin Loibooki anayerejeshwa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), kupangiwa kazi nyingine.

  Uteuzi zaidi kwenye mamlaka hiyo, umefanywa kwa Imani Nkuwi, kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Biashara na Utalii kuchukua nafasi ya Mzamilu Kaita, anayerejeshwa Wizarani kupangiwa kazi nyingine.

  "Wa mwisho kwenye mabadiliko haya ni Mabula Misungwi, tunayemteua kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Himasheria yaani Protection ili kuchukua nafasi ya Faustine Masalu atakayepangiwa kazi nyingine hapo baadaye," alisema.

  Mabadiliko hayo alisema ni ya kawaida na kwamba utekelezaji wake unaanza mara moja ambapo Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi aliyathibitisha kwa barua rasmi iliyoandikwa Agosti 3, mwaka huu.


  0 0

  Mheshimiwa Spika Job Ndugai leo amemtembelea Ikulu na kufanya mazungumzo na Rais wa Iran alieapishwa jana,Mhe Hassan Rouhani ambapo Mheshimiwa Spika amempongeza kuteuliwa kwake kwa mara ya pili na kumuahidi ushirikiano wa karibu baina ya Bunge la Tanzania na la Iran. Mheshimiwa Spika alikuwa ni miongoni mwa wageni mashuhuri walioalikwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais Rouhani katika sherehe zilizofanyika kwenye Bunge la Iran mjini Tehran.
   

  0 0

  Dodoma: Ikiwa zimebaki siku mbili kufika kikomo cha Maonyesho ya Kilimo na Mifugo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga amewataka wadau wa misitu nchini kuzalisha kwa tija mazao na bidhaa za mazao ya misitu na nyuki ili kufikia uchumi wa kati.

  Akizungumza na wadau hao jana mara baada ya kutembelea Banda la Maliasili na Utalii katika Uwanja vya Maonyesho ya Kilimo Nzuguni - Dodoma alisema serikali imekusudia kuhakikisha inawawezesha wajasiliamari kufungua viwanda vidogo vidogo vitakavyozalisha kwa tija mazao na bidhaa mbalimbali ili kufikia uchumi wa kati.

  Odunga alisema katika Mkoa wa Dodoma kuna eneo lililotengwa kwa ajili ya viwanda na kuwataka wadau wa misitu na nyuki kujiunga kwenye vikundi ili serikali iweze kuwasaidia kufungua viwanda vitakavyowawezesha kuzalisha bidhaa zenye ubora.

  " Nimetumia muda mwingi kwenye mabanda ya wadau wa sekta ya misitu na nyuki kwa kuwa katika sera zetu tunataka kuona jinsi gani wananchi wanaweza kutumia misitu kwa kuzingatia matumizi endelevu ikiwa ni kutekeleza sera ya misitu na wakati huo huo kutekeleza sera ya viwanda kwa kuzalisha viwanda vinavyotumia malighafi za misitu," alisema Odunga.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Christina Mdeme alisema licha ya kuzalisha kwa tija mazao na bidhaa za misitu na nyuki, wajitangaze na kama bajeti ni tatizo watumie mitandao ya kijamii.

  Mdau kutoka kampuni ya Arti Energy Limited ya Dar es Salaam, Abdalah Shehushi alisema kupiti ufadhili wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wameweza kushiriki maonyesho mbalimbali nchini kuonyesha teknologia, kufundisha na kutoa vitendea kazi vya kutengenezea mkaa mbadala kwa kutumia mimea mikavu, nyasi, mabua na malanda.

  “Mheshimiwa naomba nikuhakikishie kuwa tunaweza kutengeneza mkaa bila kukata mti na kuharibu misitu huku tukitekeleza sera ya viwanda kwa vitendo, Arti Energy inafadhiliwa na serikalini na taasisi mbalimbali kuhakikisha wadau wa misitu wanazalisha kwa tija mkaa mbadala bila kukata mti na kuharibu.

  Shehushi alisema katika kuhakikisha wakazi wa Kanda ya Kati Dodoma wanazalisha kwa tija mkaa mbadala baada ya maonesho ya mwaka huu, watakaa chini na Kaimu Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa wilaya ya Chemba kuona jinsi gani wananchi wake wanaweza kunufaika na teknologia ya Arti Enegy.

  Naye Mwenyekiti wa Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Charles Ngatigwa aliwataka wananchi kufika kwa wingi kwenye Banda la Wizara kupata fursa za utalii, misitu na nyuki zitakazowawezesha kujikwamua kiuchumi.

  Maonesho ya Kilimo (NaneNane) yalianza Agosti 1, 2017 kote nchini kwa ngazi mbalimbali za kanda huku Maonesho hayo Kitaifa yakifanyika Mkoani Lindi huku Maandalizi na maonesho ya Ki-Kanda yanaratibiwa na uongozi wa mikoa husika.

  Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane yatafanyika kwa siku 8 yalianza Agosti 1, 2017 kote nchini kwa ngazi mbalimbali za kanda ambapo Kitaifa yatafika ukomo jioni ya Agosti 8, 2017 katika Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.

  Kauli mbiu ya mwaka huh ni "Zalisha kwa tija mazao na bidhaa za kilimo/mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati.

  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Chemba-Dodoma, Simon Odunga (katikati) akipewa maelezo ya bidhaa zilizotengenezwa na malighafi za misitu (vinyago) na mdau wa Wakala wa Huduma za Misitu kutoka kampuni ya Kasana Artist kutoka Kijiji cha Makumbusho Dar es Salaam, Bi. Rukia Katembo (mwenye sweta) katika Banda la Maliasili na Utalii Kwenye maonyesho ya Nane Nane Kanda ya Kati yanayofanyika Katika uwanja wa Nzuguni Dodoma kuanzia tarehe 01/08 hadi 08/08/2017 na kutoa wito kwa wananchi kutembelea banda hilo ili kuweza kujionea faida mbalimbali za uhifadhi wa misitu hususan katika kumuinua mwananchi kutoka uchumi wa kawaida hadi wa kati. Wa Mwisho kushoto ni mdau mwingine Angel Msangi.

  Mdau wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzaniakutoka kampuni ya Jem Herbarist kutoka Bukoba inayozalisha bidhaa zake kwa kutumi mti wa Mlonge na Mshana, Bi. Janerose Mtayoba (mama mwenye kofia) akiwaeleza wananchi (wanaosoma maelezo ya dawa) waliotembelea Maonyesho ya Kilimo/Mifugo na Sherehe za Nane Nane Kanda ya Kati Dodoma matumizi ya dawa anazozalisha, kulia ni Katibu wa Chama cha Waganga na Wakunga wa Jadi Tanzania, Tabibu Issah Mkombozi akisikiliza maelezo hayo.

  0 0  0 0

   Mhe. Dkt. Tizeba akisisitiza umuhimu wa taarifa za hali ya hewa kwa wakulima alipotembelea banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), anayezungumza nae ni Mkurugenzi wa utafiti na matumizi ya taarifa za hali ya hewa Dkt. Ladislaus Chang'a
   Mkurugenzi wa utafiti na matumizi ya taarifa za hali ya hewa Dkt. Ladislaus Chang'a akitoa maelezo ya umuhimu wa matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa kwa waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi
    Baadhi ya wageni mbalimbali wanaoendelea kutembelea banda ili upata elimu juu ya umuhimu wa taarifa za hali ya hewa na jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa
  Mhe. Dkt Tizeba akiteta jambo na Mkurugenzi wa utafiti na matumizi ya taarifa za hali ya hewa Dkt. Ladislaus Chang'a na Meneja wa Kanda ya Kusini  wa TMA Bw. Amas Daudi


  0 0

  Picha ikimuonesha Mkandarasi kutoka Kampuni ya Caberisa Co.Ltd Bernad Mgohamwende, ambaye anajenga barabara kwa kiwango cha changarawe yenye urefu  wa kilomita 36, eneo la barabara ya mbauda ,Osunyai Mkoani Arusha iko katika hatua za mwisho kukabidhi (Picha na Pamela Mollel)

  Wakandarasi nchini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upitaji wamagari makubwa bila ya kuwa na vipimo maalum ambapo hali hiyo imekuwa ikiharibu miundombinu ya barabara ambapo wamekuwa wakitumia gharama kubwa ya kufanya marekebisho mbalimbali ya kabla ya kukabidhi barabara hizo kwa Serikali.

  Hayo yameelezwa leo na mmoja wakandarasi kutoka Kampuni ya Caberisa Co.Ltd Bernad Mgohamwende am,bae anajenga barabara kwa kiwango cha changalawe yenye ukubwa wa kilomita 36 eneo la barabara ya mbauda ,Osunyai iko katika kiwango cha changarawe ambapo yuko katika hatua za mwisho kukabidhi ambapo iko katika wilaya ya Arusha,Mkoa wa Arusha.

  ALiongeza kuwa katika kutekelezaji wa kujenga barabara hizo ,Serikali itaweka utaratibu wa kupima magari hayo itawasaidia kuweza kutunza barabara hizo na kuweza kutotumia gharama kubwa kwa wakandarasi .

  Kwani Serikali italazimika kutoa pesa za mara kwa mara kuwalipa wakandarasi kwa ajili ya kufanya marekebisho ambapo hali hiyo inawatia hasara Serikali na kuwa na matumizi mabaya ya pesa hizo.

  Hata hivyo ameitaka Serikali kuweza kutenga maeneomaalumu ya kuweza kupatikana kwa madini ya udongo na mchanga ili kuwezwsha wkandarsi kupata madini hayo kwa urahisi kwani hivi sasa wanapata changamoto kubwa katika udongo huo..

  Aliongeza kuwa hivi sasa wananunua udongo huo kwa wananchi ambapo wamekuwa wakiwauzia kwa gharama kubwa hali ambayo imekuwa ikiwagharimu pesa nyingi ukilinganisha na hali halisi..

  Kwa upande wake meneja wa Tanroad Mkoa wa Arusha Mhandisi John Edward Kalupale alisema kuwa kuhusu suala hilo la upitaji wa magari makubwa katika barabara inayijengwa ya Mbauda Osunyai ambapo alisema kuwa kisheria hawaruhusiwi kuweka mizani kutokana na kuwa na barabara hiyo kutokuwa na lami. ambayo hivi sasa iko kiwango cha changalawe.

  Aliongeza kuwa wasafirishaji ni waharibifu lakini wapende nchi yao na kuwa makini katika kutumia barabara zinzoboreshwa kwa viwango vyote kuanzia changarawe mpaka lami kwani maendeleo yoyote yale yanaletwa na uboreshaji wa miundo mbinu ya barabara zote.

  Ambapo katika barabara hiyo ya osunyai mbauda wamekuwa yakipita magari makubwa ambayo yanajaza michanga na udongo kupita kiasi na pia wanachanganya watu na michanga hhiyo hali ambayo imekuwa ikiharibu barabara hiyo badala yake amewataka madereva wawe wazalendo katika kutumia barabara hizo ili kuweza kuleta manufaa zaidi kwa watumiaji wote ili kuweza kuzitunza na kuepusha serikjali kuweza kutumia pesa nyingi katika kujenga barabara hizo.

  Mhandisi John alisema kuwa arusha bado kunakabiliwa na changamoto kubwa ya ardhi lakini wanafata taratibu za kuwezesha kupatikana kwa ardhi ilikuweza kuepuka kupata madini udongo pindi wakandarasi hao wanapohitaji kupata malighafi ya kutekeleza miradi wanyopewa na serikali.

  Katika kuweza kupata ufumbuzi wakudumu wapo katika hatua za awali ambapo upembuzio yakinifu wa kina unaendelea katika mhandisi mshauri unaendelea.

  Ambapo wanatarajia kuweka lami kilomita 400 kuanzia barabara ya Arusha,osunyai .olkesimate mpaka dosidosi Kongwa ili kuweza kumaliza changamoto mbalimbali zilizoko .
  Kwa upande wake dereva wa daladala kutoka mbauda mpaka Olkesimati Erasto Msuya alisema kuwa marekebisho hayo ya barabara yasmewarahisishia sana katika kupeleka abiria hao katika maeneo hayo kwa kabla ya marekebisho hayo walikuwa wanapata tabu na changamoto kubwa sana katika kuweza kutumia na kupelekja abiria eneo hilo.

  Anapongeza sana Serikali ya awamu ya tano katika kujenga miundombinu ya barabara na kuboresha maeneo ya barabara mbalimbali nchini.

  0 0

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (wa pili kushoto) akimkabidhi ufunguo wa pikipiki mshindi wa kwanza kilometa 200 (wanaume), Hamisi Hussein kutoka Arusha katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi (kulia) ni Mkurugenzi Kampuni ya Jambo Food Products ambayo ni mdhamini, Mhe.Salum Khamis akimpongeza Mshindi huyo 

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (mwenye bendera nyeupe kulia) akifungua mashindano ya Mbio za Baiskeli Mkoa wa Simiyu(Simiyu Jambo Festival) kwa kuruhusu washiri kuanza mashindano hayo Mjini Bariadi. 

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (mwenye baiskeli wa pili kulia) akiwa na viongozi wa Mkoa na baadhi ya Wabunge wa Mkoa wa Simiyu na Viti Maalum kutoka nje ya Mkoa kwa ajili ya kufungua mashindano ya baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi. 


  Mkurugenzi Kampuni ya Jambo Food Products, Mhe.Salum Hamis ambaye ndio mdhamini wa mashindano ya baiskeli na ngoma za asili akimkabidhi Mshindi wa kwanza mbio za Kilometa 80 (wanawake) Raulensia Luzuba kutoka mkoani Mwanza zawadi ya shilingi laki tano taslimu. 

  Rais wa Chama cha Baiskeli Taifa, Godfrey Mhagama akimkabidhi mshindi wa kwanza katika mbio za kilometa 10 (walemavu) katika mashindano ya Baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) yaliyofanyika Mjini Bariadi Simiyu. 

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akimkabidhi ufunguo wa pikipiki mshindi wa kwanza (wanaume) katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi kilometa 200, Hamisi Hussein kutoka Arusha 

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu wa mbio za Kilometa 10 (walemavu) na viongozi wa Mkoa wa Simiyu na baadhi kutoka nje ya mkoa wa Simiyu, mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya baiskeli na Ngoma za Asili(Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi. 

  Mshindi wa tatu mbio za baiskeli kilometa 80(wanawake), Vumilia Mwinakila kutoka Mkoa wa Simiyu akicheza wimbo wa Kisukuma pamoja na  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson baada ya kupokea kitita cha shilingi laki tatu. 

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu wa mbio za Kilometa 80(wanawake) na viongozi wa Mkoa wa Simiyu na baadhi kutoka nje ya mkoa wa Simiyu, mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya baiskeli na Ngoma za Asili(Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi. 

  Washiriki wa mashindano ya mbio za Baiskeli kilometa 200(wanaume) wakiendelea kuchuana vikali kushindania pikipiki na fedha taslimu 

  mshindi wa kwanza kilometa 200 (wanaume), Hamisi Hussein kutoka Arusha akipanda kwenye pikipiki yake aliyokabidhiwa baada ya kuibuka mshindi dhidi ya wenzake katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi Mkoani Simiyu. 

  Wa pili kutoka kushoto Katibu Tawala mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini, Mbunge wa Busega, Mhe.Raphael Chegeni , Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson wakiwa wamembeba nyoka wa kikundi cha wasanii wa ngoma ya asili ya Kisukuma. 

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akimpongeza Bibi.Tatu Malulu kutoka Mwanza kwa kuwa mshindi wa pili mbio za kilometa 80 (wanawake) katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mkoani Simiyu. 

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalum mara baada ya kuwapokea washiriki wa mashindano ya mbio za baiskeli wa makundi yote(wanaume, wanawake na walemavu) yaliyofanyika Bariadi Mkoani Simiyu. 

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthny Mtaka akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalum mara baada ya kuwapokea washiriki wa mashindano ya mbio za baiskeli wa makundi yote(wanaume, wanawake na walemavu) yaliyofanyika Bariadi Mkoani Simiyu. 

  Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kilometa 200 (wanaume), Hamisi Hussein kutoka Arusha(mwenye pikipiki) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na washindi wenzake, mshindi wa pili Masunga Duba kutoa Simiyu(wa tatu kushoto mstari wa pili) na wa tatu Richard Laizer (wa pili kulia mstari wa pili). 

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson(wa nne kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na mamanju wa vikundi viwili vya ngoma za asili kimoja kinachochocheza na fisi na kingine knacheza na fisi mara baada ya mashindano ya baiskeli na ngoma za asili kumalizika Mjini Bariadi. 

  Kikundi cha ngoma ya asili cha Wagalu kikitoa burudani kwa wananchi na viongozi waliofika kushuhudia mashindano ya baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi Mkoani Simiyu. 

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na mamanju wa vikundi vya Wagika na Wagalu Mkoani Simiyu, mara baada ya mashindano ya baiskeli na ngoma za asili kumalizika Mjini Bariadi. 

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson(kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kushoto wakiteta jambo wakati wakiwasubiri washiriki wa mashindano ya mbio za baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi, kufika katika kituo cha mwisho. 


  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson(wa tatu kushoto) akicheza pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na waimbaji kutoka Kata ya Bumela Wilayani Itilima wakati wa kuhitimisha mashindano ya baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi. 

  Baadhi ya wasanii wa Kikundi cha ngoma ya asili cha Wagika wakitoa burudani kwa wananchi na viongozi waliofika kushuhudia mashindano ya baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi Mkoani Simiyu. 

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson(wa nne kulia) akicheza pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Msanii Elizabeth Maliganya(wa tatu kulia) kutoka Bariadi wakati wa kuhitimisha mashindano ya baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi. 

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kuhitimishwa kwa mashindano ya mbio za baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi. 

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akisalimia na Katibu Tawala Wilaya ya Bariadi, Albert Rutaihwa ara baada ya kuwasilis kwa ajili ya kufungua mashindano ya baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu. 

  ………………………… 

  Na Stella Kalinga, Simiyu 

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amefungua Mashindano ya Mbio za Baiskeli na Ngoma za Asili Mjini Bariadi(Simiyu Jambo Festival) ambayo yamehudhuriwa na Maelfu ya  Wananchi wa Mkoa wa Simiyu. 


  Mashindano hayo ya mbio za baiskeli yamehusisha kilometa 200 wanaume, kilomita 80 wanawake ambapo pia walemavu waliweza kushindania katika umbali wa kilomita tano. 

  Akizungumza baada ya kufungua mashindano hayo Dkt.Tulia pamoja na kuupongeza Mkoa wa Simiyu kuandaa mashindano hayo amesema, ipo michezo nchini haijapewa kipaumbele lakini ikitumiwa vizuri inaweza kutoa ajira ukiwemo mchezo wa mbio za baiskeli; ambapo ametoa wito kwa viongozi wa mikoa mingine pia kuwekeza katika michezo mbalimbali ili kuwasaidia wananchi kupata kipato. 

  “Lililofanyika Simiyu ni jambo jema sasa watu watakuwa wanajua kuwa wakijifua vizuri kwenye baiskeli na ngoma za jadi wanakuja kushiriki mashindano ya Baiskeli Simiyu, nitoe wito kwa viongozi wengine kufikiria mambo mengine yanayoweza kuwasaidia wananchi katika maeneo yao kupata ajira na kujipatia kipato” alisema. 

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema mkakati wa mkoa huo ni kurasimisha tamaduni zote za Mkoa wa Simiyu na kuhusianisha na shughuli za Utalii ndani ya mkoa huo. 

  “Position(Nafasi) ya Mkoa wa Simiyu kwenye nchi ni kukuza tamaduni na sanaa zetu kama moja ya eneo litakalotuunganisha na sekta ya Utalii, tumezungukwa na mapori ya akiba na mbuga za wanyama, tungehitaji watalii wanapokuja kwenye maeneo hayo wapate ladha ya tofauti kiwemo utamaduni wa Mtanzania” 

  Mtaka ameongeza kuwa wasanii wote watatambuliwa na baadae kujengewa uwezo kupitia watalaam wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(Kitivo cha sanaa),Chuo cha Sanaa Bagamoyo na vyuo vya michezo ili waweze kufanya kazi zao kibiashara na kuimarisha uchumi wao. 

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products,Mhe.Salum Khamis ambaye ndio Mdhamini wa mashindano ya Baiskeli na ngoma za Asili (Simiyu Jambo Festival) amesema ataendelea kudhamini mashindano kama hayo Mkoani Simiyu ili kuwaweseha wananchi kuinua kipato kupitia vipaji vyao. 

  Naye mshindi wa kwanza mbio za kilometa 80 (wanawake) Raulensia Luzuba kutoka Mwanza ameomba mashirika na makampuni mbalimbali kuwadhamini ili waweze kujengewa uwezo na kuandaliwa kushiriki katika mashindano ya Kimataifa. 

  Masunga Duba mshindi wa mbio za kilometa 200(wanaume)kutoka Simiyu amesema pamoja na wafadhili kudhamini mashindano ameomba pia wawasaidie wachezaji kupata baiskeli za kisasa zitakazowasaidia kwenda kwa kasi inayotakiwa. 

  Mashindano ya baiskeli Mkoani Simiyu yameshirikisha wachezaji kutoka mikoa ya Simiyu, Mwanza, Shinyanga,Arusha na Mbeya ambapo ushindi kwa upande wa wanaume umechukuliwa na Hamisi Hussein(Arusha) ambaye amejishindia pikipiki, wa pili ni Masunga Duba(Simiyu) kitita cha shilingi 1,000,000/= wa tatu Richard Laizer .shilingi 500,000/= na zawadi nyingine zimetolewa kwa mshindi wa nne mpaka wa 15. 

  Kwa upande wa wanawake mshindi wa kwanza Raulensia Luzuba kutoka Mwanza amejipatia shilingi 500,000/=, mshindi wa pili Tatu Malulu(Mwanza) shilingi 400,000/= na wa tatu ni Vumilia Mwinamila(Simiyu) shilingi 300,000/= na zawadi nyingine zimetolewa kwa mshindi wa nne mpaka wa 10. 

  Walemavu mshindi wa kwanza Emmanuel Mtemi amejipatia shilingi 200,000/= wa pili Masunga Sendama shilingi 150,000/= na wa tatu Saguda Sospeter shilingi 100,000/=wote kutoka mkoa wa Simiyu na zawadi nyingine zimetolewa kwa mshindi wa nne na wa tano.

  0 0


  ·         787 Dreamliner features Etihad Airways’ industry-leading, award-winning cabins
  ·         Popular route approaching millionth passenger milestone

  Etihad Airways has introduced the Boeing 787-9 on its scheduled daily service from Abu Dhabi, the capital of the United Arab Emirates (UAE), to Seoul. The aircraft touched down this morning at the South Korean capital’s space-age Incheon International Airport.

  The new two-class 787 Dreamliner service replaces the Airbus A340-600 aircraft previously operated on the route, and features Etihad Airways’ next-generation Business and Economy Class cabins, configured with 299 seats - 28 Business Studios and 271 Economy Smart Seats.


  “There has been a steady increase in the number of business and leisure travellers flying to South Korea from Abu Dhabi and the GCC region, and vice versa. The UAE government’s initiatives to develop the already strong trade ties between our two countries has allowed many Korean companies to operate successfully here, contributing to the success of Etihad Airways’ Seoul Incheon service. Furthermore, many of our customers on the route transit onwards through Abu Dhabi to major destinations on the Etihad network across Europe, the Middle East and Africa.

  “The addition of more 787 Dreamliners into our fleet has allowed us to upgrade the Seoul service so our customers can enjoy the unique Etihad experience available on this incredible aircraft, and ensuring that we maintain the competitive edge with the innovative cabin and seating designs featured onboard.”

  Etihad Airways’ modern fleet of 16 Boeing 787 aircraft feature innovative, award-winning cabin designs and products, complemented by the airline’s acclaimed service and hospitality offering. Seoul flights include Food and Beverage Managers in Business Class and a Norland approved Flying Nanny in Economy Class to provide extra specialised care for families with young children.

  The Business Studios offer direct aisle access, a fully-flat bed of up to 80.5 inches in length, and an increase of 20 per cent in personal space. Upholstered in fine Poltrona Frau Leather, the Business Studio is equipped with an in-seat massage and pneumatic cushion control system which enables guests to adjust the firmness and comfort of their seat. 

  Each Business Studio has an 18-inch personal touch-screen TV with noise-cancelling headsets. Guests can also enjoy mobile connectivity, onboard Wi-Fi and seven satellite channels of live TV.

  Economy Smart Seats provide enhanced comfort with a unique ‘fixed wing’ headrest, adjustable lumbar support, a seat width of approximately 19 inches and an 11.1” personal TV monitor on each seat. The aircraft has been designed with enhancements including humidity controls while air pressure levels are set to ensure a smoother flight, allowing guests to arrive feeling fresher.

  The airline’s Boeing 787 fleet is equipped with the latest inflight entertainment system featuring over 750 hours of movies and programmes,as well as hundreds of music choices and a selection of games for both adults and children.

  Boeing 787 schedule to Seoul, South Korea, effective 1 August 2017
  Flight
  Origin
  Departs
  Destination
  Arrives
  Frequency
  Aircraft
  EY 876
  Abu Dhabi
  22:15
  Seoul
   11:55 +1
  Daily
  Boeing 787-9
  EY 873
  Seoul
  00:55
  Abu Dhabi
  05:50
  Daily
  Boeing 787-9

  Notes: All departures and arrivals are listed in local time.


  0 0


  Mkuu wa wilaya ya Newala, Aziza Mangosongo, akitembelea banda la VETA katika maonesho ya Kilimo 2017 yanayoendelea mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo ambapo alipongeza VETA kwa kuweka fursa nyingi za mafunzo ya ujuzi kwa makundi mbalimbali ya wananchi. Aliahidi kushirikiana na VETA ilikuwa wezesha wananchi wilaya ni kwake kunufaika pia na fursa mbalimbali za mafunzo ya ufundi stadi.
  Wanafunzi wa shule ya sekondari Medi ya mkoani Mtwara wakipata maelekezo juu ya aina ya mafunzo yanayotolewa katika vyuo vya ufundi Stadi walipotembelea banda la VETA katika Maonyesho ya kilimo ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
  .Mwalimu wa Elektroniki wa Veta Kipawa, Aneth Mganga akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda la VETA Pikipiki inayoendeshwa ni lazima dereva awe amevaa kofiangumu.
  Wananchi wakipata maelezo ya jiko la mafuta ya taa ambalo limebuniwa kwa kutotumia mafuta mengi na halina moshi.

  Baadhi ya wananchi waliofika kutembelea banda la VETA ili kuweza kupata taarifa mbalimbali kuhusianana VETA pamoja na kuaangalia teknolojia mbalimbali.


  Na Chalila Kibuda,GlobuyaLindi

  Katika kukabiliana na changamoto za madhara ya ajali za pikipiki yanayosababishwa na madereva kutovaa kofiangumu (helmet), Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imebuni teknolojia ya kukabiliana na hilo.

  Mwalimu wa fani ya elektroniki kutoka VETA Kipawa, AnethMganga, amebuni mfumo wa kielektroniki unaozuia pikipiki kuwa kampaka dereva awe amevaa kofiangumu (helmet).

  Akizungumza na katika viwanja vya maonesho ya Nanenane Ngongo, mkoani Lindi, mwalimu Aneth amesema mfumo huo ukianza kutumika na madereva wa pikipiki utapunguza madhara endapo kunatokea ajali kwa kuwa bila ya kuvaa kofiangumu pikipiki haiwaki na hata ukiwa katika mwendo ikitokea ukavua kofiangumu pikipiki itazimika.

  Aidha, katika usalama barabarani inasaidia kuzuia wizi wa pikipiki kwani mwizi hatoweza kuiwasha bila kofiangumu ambayo imeunganishwa kieletroniki.

  Aneth amesema anaendelea kufanya utafiti nakuboresha zaidi ubunifu huo, lakini ameomba serikali na wadau mbalimbali kuunga mkono ili uweze kuenea, kukubalikana kutumika na waendesha pikipiki katika maeneo mbalimbali nchini.

  0 0

   Taswira za Stendi mpya na ya kisasa ya mabasi mjini Korogowe mkoani Tanga ambayo imezinduliwa asubuhi hii na Rais Dkt. John Pombe Magufuli  0 0


  Tanzanian ICT students who are in China attending the ‘Seeds for the Future’ program have completed the first week of technological training and Chinese cultural and language classes in Beijing.

  The selected students started their journey on 28th July, 2017, spent time in Beijing, where they received an introduction to Chinese culture and Mandarin. And later on, the students travelled to Huawei’s Shenzhen campus learning about the technology industry and the long-term trends in mobile, networking and cloud computing.

  Speaking during the closing ceremony for the Cultural and language trainings, Ms Asha Said Seif a student from State University of Zanzibar (SUZA) said that “Our third day in Beijing has been one of the great experience as we start taking our first Chinese language class in the School of Continuing Education of Beijing Language and Culture University.”

  She said that during their session, they were given basic introductions to the basic and fundamental things about the Chinese language, such as initials and finals, tones, the positions of tonal marks, new words, pronouncing and memorizing simple phrases, counting and so on.

  “The hardest part was pronouncing the words and phrases, and the favourite part was being able to count the numbers and sing two of the best Chinese songs by the best Chinese singers,” she said.

  Mr Ahmed Haji Abdullah who is also a student from SUZA said that given an opportunity to participate in the Huawei Seeds for the Future program, will not only help them to explore and learn the Chinese language and culture, but also will prepare them for the 21st century.

  He said that many employers and companies across the globe seeking to establish relationships and develop key business links with China; Chinese language has indeed become a very valuable and highly sought skill in today’s world.

  “Since China has become a major player in the world economy, the demand for experienced professionals with Chinese language skills has increased dramatically,” he added.

  Mr Nhendegese Martine from University of Dodoma (UDOM) said “In the afternoon session, a highly waited painting lesson was presented to the students by a Chinese teacher. With all required tools for painting, step by step students were taught on how to paint flower and bird, figure, vegetable and fruits and animal. In this skilled like session students demonstrated their paintings and wrote their Chinese names as the way to appreciate the talent,” he said.

  He said that Chinese people let the foreigners know the culture and language of their country which make feel like they are at their home country. This positive tricky should be considered by developing countries like Tanzania to attract more tourists.

  Through the Seeds for the Future program, each year Huawei provide opportunity for Tanzania students to explore all beautiful Chinese palatial architecture and through this it had influence us to encourage our country and the government at large to preserve and develop our cultural and architectural in our nation and elsewhere.

  This year, Huawei had offered 2-week educational experience, language training, exposure to Chinese culture and the experience of processes in Huawei’s dynamic global business environment in China.
  Huawei Tanzania's Public relation Officer, Frank Amani hands over a book to a Tanzanian ICT student  in Beijing, China over the weekend after successfully completing the first week training in China in Huawei's phase II Seeds for the Future Program.

   

  0 0  Baadhi ya wateja waliofurika kwenye banda la Tigo kwenye maonesho ya Nanenane mkoani Dodoma jana kupata ofa kabambe ya simu za kisasa za Tecno S1 kwa bei ya TZS 99,000/- na Tecno R6 kwa bei ya TZS 195,000 tu.
  Mtoa huduma ya mauzo wa kampuni ya Tigo, akihudumia wateja waliofika kwenye banda la Tigo maonesho ya Nane nane Dodoma jana.
  Baadhi ya wateja waliofurika kwenye banda la Tigo kwenye maonesho ya Nanenane mkoani Dodoma jana kupata ofa kabambe ya simu za kisasa za Tecno S1 kwa bei ya TZS 99,000/- na Tecno R6 kwa bei ya TZS 195,000 tu.

  Mtoa huduma ya mauzo wa kampuni ya Tigo, Sharifa Matula akihudumia wateja waliofika kwenye banda la Tigo maonesho ya Nane nane Dodoma jana.

  0 0  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Lindi mchana huu tayari kwa kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima ya Nane Nane itakayofanyika Kitaifa mkoani Lindi.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh.Nape Moses Nnauye ,mara baada ya kuwasili mkoani Lindi mchana huu tayari kwa kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima ya Nane Nane itakayofanyika Kitaifa mkoani Lindi.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali wa chama cha Mapinduzi (CCM),mara baada ya kuwasili mkoani Lindi mchana huu tayari kwa kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima ya Nane Nane itakayofanyika Kitaifa mkoani Lindi.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0

  MKAZI wa Dodoma nchini Tanzania, Innocent Nyalia, ameibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 kutoka kwa waendeshaji wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, katika droo iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam.


  Droo hiyo ilichezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo, ambaye kwa pamoja alishuhudia kupatikana kwa mshindi huyo wa droo ya 29 ya Biko.

  Akizungumza katika droo hiyo, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alimpongeza mshindi huyo wa mjini Dodoma, Nyalia na kuwataka Watanzania wote kuchangamkia fursa za mamilioni ya Biko.

  Alisema huu ni wakati wa kutajirika kwa kuvuna mamilioni ya Biko yanayoendelea kutolewa kwa wingi, ikiwa ni mwendelezo wa kuona wachezaji hao wanaotumia simu za M-Pesa, Airtel Money na Tigo Pesa kwa kuingiza namba ya kampuni 505050 na kumbukumbu 2456 wananeemeka na Biko.

  “Kama kawaida yetu ushindi wa Biko ni rahisi kupatikana na kucheza kwake  kuliko michezo mingine yoyote, hivyo tunawaomba Watanzania wasilaze damu katika mchezo wetu wa Biko unaozidi kutoa mamilioni ya fedha.

  “Mbali na ushindi mkubwa wa Sh Milioni 20 unaopatikana Jumapili na Jumatano, pia zipo zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazolipwa moja kwa moja kwa kupitia simu zao walizotumia kuchezea,” Alisema Melles.

  Naye Ngolo, mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, aliendelea kuwakumbusha Watanzania jinsi ya kutumia muda wao kwa kucheza mchezo wa Biko ili wajipatie maendeleo makubwa kutoka Biko.

  “Wakati Bodi yetu ikiwapongeza washindi wote wanaoshinda zawadi kubwa na ndogo kutoka Biko, pia nitumie muda huu kuwataka kila mmoja kuona fursa ya michezo ya kubahatisha hususan wa Biko ambao unachezwa kwa kufuata taratibu zote za nchi yetu,” Alisema.

  Kwa kutangazwa kwake mshindi, sasa mkazi huyo wa Dodoma anatarajiwa kukukabidhiwa mamilioni yake mapema wiki hii ili aziweke katika matumizi yake ya kawaida katika hali ya kukuza uchumi wake, ikiwa ni siku chache baada ya mshindi wa droo ya 28, Moses Matagili, mkazi wa Goba, kupokea fedha zake wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Kama ulipitwa na matukio ya wiki nzima yaliyojili mkoani Ruvuma kuanzia 7 July 31 hadi August 06, 2017 basi usipate tabu tumekusogezea matukio 7 ambayo ni ya wiki .

older | 1 | .... | 1329 | 1330 | (Page 1331) | 1332 | 1333 | .... | 1897 | newer