Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

MPIRA WA KIKAPU MKOA WA DAR ES SALAAM WAPATA WADHAMINI

$
0
0
 Mwenyekiti wa Mpira wa kikapu mkoa wa Dar es Salaam Bw. Okare Emesi (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu udhamini waliopata toka kampuni ya Startimes na Sibuka mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa chama hicho Bw. Peter Mpangala na kushoto ni Afisa Mahusiano toka Startimes Bw. Samwel Gisayi.
Mkurugenzi wa Masoko wa chama hicho Bw. Peter Mpangala (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu udhamini waliopata toka kampuni ya Startimes na Sibuka mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Okare Emesi na kushoto ni Afisa Mahusiano toka Startimes Bw. Samwel Gisayi.

Picha Eliphace Marwa - Maelezo


RC TABORA –LIMINE ALIZETI KWA WINGI WAWEKEZAJI WALETE VIWANDA HAPA.

$
0
0
Na Tiganya Vincent-RS-TABORA

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri ameagiza kuanzia msimu ujao wa kilimo kila mtu mwenye uwezo wa kufanyakazi ni lazima alime heka mbili za alizeti kwa ajili ya kuvutia wawekezaji kujenga Viwanda vya kusindika na kuzalisha mafuta hayo kuanza ujenzi mkoani humo.

Bw. Mwanri alitoa kauli hiyo jana wakati wa ufunguzi wa maonesho ya nanenane kwa Kanda ya mikoa ya Magharibi yaliyofanyika mkoani Tabora.

Alisema zao la alizeti katika mkoani Tabora linastawi sana na ikiwa wakazi wake watalima kwa wingi Kampuni mbalimbali zitajitokeza kwa wingi kuja kujenga viwanda vya kuzalisha mafuta hayo.

Bw.Mwanri alisisitiza kuwa wawekezaji wengi wamekuwa wanashindwa kuja kujenga viwanda vya usindikaji wa mafuta hayo kwa sababu siku za nyuma zao hilo limekuwa halitiliwi mkazo na kufanya uzalishaji kuwa wa chini sana , lakini hivi sasa hiyo itakuwa ajenda ya Mkoa kama mkakati mojawapo wa kuwavutia watu kuja kujenga viwanda.

“Ndugu zangu Wakuu wote wa Wilaya na Wakurugenzi kuanzia sasa akili yetu na agenda yetu kubwa iko katika kuhakikisha kuwa kila mkazi wa Tabora analima heka mbili za alizeti kuanzia msimu ujao wa kilimo ili tuwe na malighafi nyingi kwa ajili ya kulisha viwanda vitakavyoanzishwa kwa mwaka mzima” alisema Mkuu huyo Mkoa.

Katika kutekeleza agizo hilo aliwaagiza Maafisa Ugani wote mkoani hapa kuhakikisha wanawatembelea wakulima vijijini kwa ajili ya kuwaelimisha juu ulimaji bora na mbegu bora za zao hilo kwa ajili kuwafanya wakulima kuanza mara moja kilimo hicho pindi mvua za masika zitakapoanza.

Katika hatua nyingine aliwaagiza Wakurugenzi Watendaji wote na Maofisa Ugani wote kuhakikisha kuwa wanaanza wanawahimiza wakazi wa maeneo mbalimbali ya Mkoa huo kuanza kilimo cha zao la uwele , mtama, viazi na mihogo ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa chakula kwa sababu ya mvua kuendelea kunyesha chini ya kiwango.

Alisema tabia ya baadhi ya wananchi kuendelea kung’ang’ania mazao yanatumia miezi mingi kukomaa kusababisha wakazi hao kuendelea kukabiliwa na upungufu wa chakula wakati wakilima mazao yanayostahimili ukame tatizo haliwezi kuwapata.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nzega alisema kuwa wao tayari wameshaanza maandalizi kwa kuwa na shamba la mfano la heka 10 ambapo tayari wameshazalisha alizeti na kutoa mafuta.

Alisema kinachofuata ni kuongeza wigo wa kilimo hicho wa kuwashirikisha wananachi wengi kwa kuwaelimisha juu ya kilimo bora cha zao hilo ili waweze kuzalisha kwa wingi na kutoa fursa kwa wamiliki wa viwanda kupata malighafi ya kutoa kwa ajili ya uzalishaji mafuta.

Naye Mkazi wa Ipuli mkoani Tabora Juma Elia aliunga mkono agizo la Mkuu wa Mkoa wa Tabora la kuhamasisha wakulima kuanza kulima alizeti ambalo ni rafiki na mazingira kwa sababu halihitaji kuni kukauka kama ilivyo tumbaku.

Aliongeza kuwa zao hilo litasaidia kutoa ajira kwa njia ya vijana kushiriki kilimo na wengine kuajiriwa katika viwanda vya kusindika mafuta ya alizeti vitakavyoanzishwa.

MKUU WA WILAYA YA MKURANGA FILBERTO SANGA AAGIZA SHUGHULI ZOTE ZA UPIMAJI WA ARDHI USIMAMISHWE WA SASA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga ameagiza shughuli zote za upimaji wa ardhi kusimama kwa sasa mpaka watakapotoa kibali cha upimaji.

Mkuu Wilaya alitoa agizo katika mkutano na wananchi wa wilaya kuhusiana na mgogoro wa ardhi, ambapo vijiji vinne vinavyodaiwa kuvamia shamba la familia ya Rajwani mwenye asili ya kihindi lenye ukubwa wa ekari 2472.

Vijiji hivyo vinne ni Mwambaya,Lunzando,Mipeko na mlamleni vilivyopo kwenye Kata ya mipeko na Tambani.

Sanga amesema kuwa kwa sasa hakuna mtu kutoka Halmashauri wala maafisa mipango miji kupima ardhi mpaka awe na kibali kutoka wilayani na kuongeza kuwa Madiwani na Wenyeviti wa vitongoji kutoruhusu mtu kupima ardhi mpaka awaoneshe kibali kutoka wilayani.

Aidha amewataka wananchi wa vijiji hivyo kifanya kazi zao kwa Uhuru bila hofu yeyote kwani wilaya hiyo ipo salama."tumejipanga vizuri Mimi mwenyewe ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama na wahakikisheni mupo salama,msiache kwenda mashambani,msiache mazao shambani kavuneni mazao yenu hakina wakuwabigudhi.alisema Sanga.

Wakati huohuo ametoa wito kwa madereva wabodaboda wilayani humo wametakiwa kuvaa kofia ngumu pindi wanapoendesha pikipiki na kuacha kupakia watu wawili kwa pikipiki moja ‘Mishakaki’.

Naye Mbunge wa jimbo la mkuranga Abdalah Ulega amewatoa hofu wananchi hao kwa kuwa suala lao linashughulikiwa na wamempa notisi ya siku 90 ya kujieleza kuhusiana na eneo hilo.

Ulega aliwaahidi wananchi hao kuwachangia kiasi cha shilingi milioni moja kama sehemu ya mchango wake katika kusaidia kutatua tatizo hilo.
 .Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga akizungumza na wananchi wa vijiji vinne ambavyo vina mgogoro wa ardhi katika mkutano uliofanyika Mwanambaya .
 Mbunge wa jimbo la Mkuranga , Abdalah  Ulega akizungumza na wapiga kura wake juu ya mgogoro wa shamba lenye ekari 90 katika kijiji cha Mkuranga.
 .Sehemu ya wananchi wakimsikiza mkuu wa wilaya juu ya mgogoro unao wakabili

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, MHANDISI RAMO MAKANI AKAGUA SHUGHULI ZA UTALII NA MFUMO WA UKUSANYAJI MAPATO KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA MLIMA KILIMANJARO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kushoto) akizungumza na watalii kutoka Marekani wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame ndani ya Hifadhi ya Taifa Mlima Kilimanjaro jana. Alipowauliza watalii hao ni wapi walipata habari za mlima huo, walijibu kuwa kila mtu anajua kuhusu mlima Kilimanjaro!. 
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa nne kushoto) akizungumza na watalii kutoka Marekani wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame ndani ya Hifadhi ya Taifa Mlima Kilimanjaro jana. Alipowauliza watalii hao ni wapi walipata habari za mlima huo, walijibu kuwa kila mtu anajua kuhusu mlima Kilimanjaro!. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba, Mhifadhi Mkuu wa KINAPA, Betrita Loibooki na nyuma yake ni Mbunge wa Vunjo, James Mbatia.

Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhifadhi wa KINAPA, Steven Moshi (wa pili kulia) namna mfumo wa ukusanyaji mapato unavyofanya kazi katika Hifadhi ya Taifa Mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana. Kulia anayeshuhudia ni Mbunge wa jimbo la Vunjo, James Mbatia.
 Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (katikati) akipanda mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana. Kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo, James Mbatia, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba (kulia kwake), Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Zahoro Kimwaga (kushoto) na Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu (kulia).
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa nne kulia) akipanda mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana. Wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo James Mbatia (wa tatu kulia), Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Zahoro Kimwaga (kushoto), Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu TANAPA, Mtango Mtahiko (kulia), Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu (wa pili kulia) na Mhifadhi wa KINAPA, Steven Moshi.  
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kulia) akipanda mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana. Wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo James Mbatia (wa nne kulia), Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba (kulia), Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu TANAPA, Mtango Mtahiko (kushoto), Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu (wa pili kushoto) na Mhifadhi wa KINAPA, Steven Moshi (wa pili kulia).  
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia) akipanda mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana. Wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo, James Mbatia (kulia) na Mhifadhi wa KINAPA, Steven Moshi.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia) akisikiliza na kujibu kero mbalimbali za wapagazi wanaopandisha mizigo ya watalii katika mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana
 Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro, Betrita Loibook (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na mtalii (katikati) pamoja na mhifadhi wa hifadhi hiyo wakati wa ziara hiyo.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro, Betrita Loibook akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wahifadhi, mtalii na waongoza watalii. (PICHA NA HAMZA TEMBA - WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)

TAASISI ZA KIFEDHA ZASHAURIWA KUWA NA MASHARTI NAFUU YA UTOAJI MIKOPO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akinunua moja ya mkoba uliotengenezwa na kikundi cha Jauki kwenye banda la Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akimtazama mnyama aina ya kakakuona wakati wa Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akitembelea mabanda mbalimbali ya wajasiriamali wakati wa Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi
Baadhi ya Wajasiliamali wakimsubiri Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi kutembelea katika banda lao wakati wa Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akionyesha Dawa aina ya Mlonge inayotibu magonjwa mbalimbali wakati wa Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akikagua baadhi ya viatu vilivyotengenezwa na wajasiriamali wakati wa Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akikagua banda la Wakala wa vipimo wakati wa Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Viwanda, Biashara na Uwekezaji wakati wa  Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi


Na Mathias Canal, Lindi

Taasisi mbalimbali za fedha nchini zimeshauriwa kuwa na masharti nafuu ya utoaji mikopo ili kuwarahisishia wajasiriamali kuwa na fursa rahisi ya kupata mitaji kwa minajili ya kuendeleza biashara zao.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi.

Katika Maonesho hayo yenye kauli mbiu ya “Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati” wananchi watapata fursa yatawasaidia wananchi kupata wananchi watapata elimu ya matumizi ya teknolojia mbalimbali kwa muda mfupi lakini pia wadau kujionea na kujifunza huduma zitolewazo na serikali, mashirika ya umma na binafsi

Mhe Zambi alisema kuwa miongoni mwa changamoto ambazo zimekuwa mwiba mcvhungu kwa wajasiriamali ni pamoja na namna ya kupata mitaji kutoka katika taasisi mbalimbali za fedha jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya biashara. 

Alisema mikopo kutoka benki inatolewa kwa masharti makubwa na riba kubwa jambo ambalo ni kikwazo kwa wajasiriamali ambao wana mitaji midogo lakini inarudisha nyuma ufanisi wa wao na taifa kwa ujumla wake.

Alisema kuwa Sera ya nchi inaruhusu sekta binafsi kuendesha uchumi kupitia kampuni ndogo, za kati, na wajasilimali, hivyo mitaji kwa wajasiriamali ni jambo ambalo haliepukiki.

Zambi alisema kuwa wajasiriamali wakipatiwa huduma za fedha na kukuza mitaji yao, wana nafasi kubwa ya kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Zambi amesifu maandalizi mzuri ya Sherehe hiyo inatayarishwa na kuratibiwa na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kuhusisha Taasisi, Wizara na mtu mmoja mmoja kwa wote wanaoshughulika na kilimo.


Maonesho ya sikukuu ya wakulima Nanenane yanahusisha shughuli za wakulima, wafugaji wa mifugo, wafugaji wa nyuki, wavuvi, wanamazingira, wasindikaji wa bidhaa za mazao ya kilimo na mifugo, wizara taasisi/makampuni ya umma, makampuni binafsi, mabenki, Taasisi za umma na binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Pia uzalishaji bora wa mazao ya nafaka, ubunifu wa teknolojia rahisi za kutotoa mayai, Kuongeza thamani ya mazao ya mifugo, Makampuni ya mawasiliano, ambapo Taasisi za elimu zitaonyesha ubunifu wa kumsaidia mfugaji, Tiba za asili, Wasindikaji wakubwa na wadogo wa mazao ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Asali, na Nta.

WASANII WA BONGO FLEVA WAASWA KUZINGATIA MATUMIZI YA LUGHA.

$
0
0
Wasanii wa Bongo Freva  hapa nchini wameaswa kuzingatia matumizi ya Lugha pamoja na mavazi  ili kuepusha fungia fungia ya kazi zao za sanaa.

Hayo yamesemwa leo wakati wa mkutano wa  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe na wasanii wa nyimbo za bongo Freva pamoja na wadau mbalimbali na sanaa hapa nchini jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wasanii wa nyimbo za Bongo Freva hapa nchini kuhusu maswala mbalimbali yanayowahusu wasanii hao, pia wameshauliwa kujiunga kusajili kazi zao pamoja na kulipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kupata miongozo mbali mbali COSOTA pamoja na BASATA.
 Baadhi ya wasanii wa Nyimbo za Bongo Freva  hapanchini kutoka kulia ni Wastara Thomasi, msanii wa Bongo Fleva, Khadija Shaban (Keisha) na Witnes Mwajaga wakiwa katika Mkutano wa wasanii wa Bongo freva na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe jijini Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea saa ya ukutani ikiwa ni Rambirambi kutoka kwa wasanii wa Mziki wa Bongo Freva  kama pole kufiwa na Mkewe.
                   Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii. 


KINANA AWASILI TANGA KUSHIRIKI UZINDUZI WA UJENZI WA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA UGANDA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Henry Shekifu baada ya kuwasli kwenye mkutano wa hadhara wa Rais Dk. John Magufuli uliofanyika katika Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, leo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya hiyo Mwanasha Tumbo
 Mbunge wa  Viti Maalum mkoa wa Tanga, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Ummy Mwalimu akisalimia wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Henry Shekifu akisalimia wakati wa mkutano huo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akienda jukwaani kusalimia wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Rais Dk Magufuli
 Katbu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza alipoalikuwa kuzungumza wakati wa mkutano huo.
 Katbu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza alipoalikuwa kuzungumza wakati wa mkutano huo.
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo
 Mke wa Rais Mama Janet Magufuli akisalimia kwenye mkutano huo
 Rais Dk John Magufuli na viongozi wengine wa meza kuu akiwemo Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo
 mamia ya watu wakiwa wamefurika kwenye mkutano huo
 Mbunge wa Muheza Adadi Rajab akizungumza wakati wa mkutano huo mbele ya Rais Dk Magufuli
 Rais Dk Magufuli akizungumza wakati wa mkutano huo

 Kinana akifuatana na viongozi wa CCm mkoa wa Tanga kumsikiliza Rais Nagufuli alipozungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake katika eneo la Pongwe
 Kinana na baadhi ya viongozi wa CCM wakimsikiliza Rais Magufuli katika eneo la Pongwe
 Rais akizungumza na wananchi katika eneo la Pongwe PICHA ZAIDI/> BOFYA HAPA

COSTECH YATOA MAFUNZO YA KILIMO CHENYE TIJA KWA WAKULIMA KATIKA MAONYESHO YA NANENANE MKOANI LINDI

$
0
0

Mwezeshaji kutoka Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold Mneney (kulia), akitoa mafunzo ya siku moja ya kilimo chenye tija  kwa wakulima wa Mkoa wa Lindi kwenye Maonyesho ya Kitaifa ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Ngongo mkoani hapa leo.
Wakulima wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Usikivu katika mafunzo hayo yaliyofanyika Ukumbi wa Mikutano katika Jengo la Halmshauri ya Wilaya ya Kilwa lililopo katika viwanja hivyo vya Ngongo.
Mafunzo yakiendelea.
Mkulima kutoka Wilaya ya Kilwa, Omari Kijuwile akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Dadi Uredi Chibwana mkulima kutoka Kijiji cha Kiwalala Lindi Vijijini akielezea changamoto mbalimbali walizonazo wakulima katika mkoa huo.
Mkulima Zarafi Mahamudu kutoka Manispaa ya Lindi, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Anastazia Benjamin Lai kutoka Wilaya ya Kilwa akitoa shukurani kwa COSTECH kwa kuwapelekea mafunzo hayo.
Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Philbert Nyinondi ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro (SUA), akiwaelezea wakulima hao umuhimu wa matumizi ya MB katika siku zao katika kuinua kilimo na utafutaji wa masoko katika maeneo mengine ya ndani na nje ya nchi.

Na Dotto Mwaibale, Lindi

TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imetoa mafunzo ya siku moja kwa wakulima wa Mkoa wa Lindi yenye lengo la kuwasaidia kulima kilimo chenye tija.

Mafunzo hayo yametolewa na mwezeshaji kutoka Jukwaa la Bioteknolojia kwa maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk. Hamalord Mneney katika maonyesho ya kitaifa ya wakulima Nanenane yanayoendelea Viwanja vya Ngongo mkoani hapa leo.

Akizungumza kuhusu mafunzo hayo Dk. Mneney alisema Serikali imeona itoe mafunzo kwa wakulima hao ili wajifunze kilimo cha kisayansi chenye tija badala ya kuendelea na kilimo cha mazoea.

"Serikali siku zote inawajali wakulima ndio maana tukaona ni vizuri kuleta mafunzo haya kwa hawa wakulima ili kuondoa changamoto wanazokabiliana nazo katika shughuli zao za kilimo" alisema Dk.Mneney.

Wakulima walionufaika na mafunzo hayo ni kutoka wilaya za Lindi, Lindi vijijini, Rwanga, Kilwa na Nachingwea ambapo kulikuwa na washiriki zaidi ya 20.

Wakizungumza katika mafunzo hayo wakulima hao walisema changamoto kubwa waliyonayo  ni mabadiliko ya tabia nchi na ukame unaotokana na mvua kutopatikana kwa wakati pamoja na pembejeo za kilimo kutowafikia kwa wakati.

Walitaja changamoto nyingine kuwa ni mazao ya chakula kushambuliwa na wadudu waharibifu, kukosekana kwa masoko ya mazao yao na magonjwa kama batobato na michirizi kahawia yanayoshambulia mihogo pamoja na mbegu bora.

Mkulima Omari Kijuwile kutoka Wilaya ya Kilwa alisema wakulima wana ari ya kulima lakini wanakosa mtaji baada ya taasisi za kifedha kushindwa kuwakopesha kwa kuwa hawana kitu cha kuweka dhamana ambapo aliomba umilikishwaji wa mashamba yao kwa hati za kimila ambazo zitatambuliwa na taasisi hizo ili waweze kupata mikopo hiyo.

"Tunaomba tumilikishwe mashamba yetu kwa hati za kimila ili tuweze kuaminika na kupata mikopo kutoka taasisi za kifedha" alisema Kijuwile.

Mkulima Dadi Uredi Chibwana kutoka Kijiji cha Kiwalala Lindi vijijini ni vizuri wakulima wakajenga tabia ya kufuata ushauri wa maofisa ugani kuhusu kilimo badala ya kutegemea kilimo cha mazoea.

Zarafi Mahamudu mkulima wa Manispaa ya Lindi alisema wakulima wamekuwa wakijitahidi lakini masoko yamekuwa ni changamoto kubwa kwao hivyo aliiomba serikali kuangalia jambo hilo kwa undani zaidi.

Mkulima kutoka Wilaya ya Kilwa Anastazia Lai aliomba serikali na wadau wengine itoe msaada wa kukabiliana na wadudu waharibifu wa mazo badala ya kuacha nguvu zao kupotea bure kutokana na wadudu hao.

Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Philbert Nyinondi ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro (SUA), aliwataka wakulima hao kutumia simu zao kutafuta masoko badala ya kutumia kwa matumizi yasiyo na tija.

"Wenzenu wa nchi zingine wamekuwa wakitumia MB katika simu zao kuwasiliana na wakulima wa nchi zingine katika masuala ya kilimo na kutafuta masoko ya mazo yao badilikeni nanyi mnaweza kufanya hivyo" alisema Dk. Nyinondi.


SSRA YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE YANAYOENDELEA VIWANJA VYA NZUNGUNI MKOANI DODOMA

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde Msika akifafanua jambo wakati wa Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kikanda  katika viwanja vya Nanenane Mkoani Dodoma.
Afisa wa SSRA, Bi. Aminah Kisisa akigawa vipeperushi kwa moja ya wadau waliotembelea Banda la SSRA kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati.
Afisa wa Uhusiano na Uhamasishaji, SSRA Bw, Ally Masaninga akifafanua kwa mmoja ya wadau waliotembelea banda la Mamlaka hiyo wakati wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati.
Timu ya SSRA katika picha ya pamoja wakati wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati yanayofanyika katika Viwanja vya Nanenane Mkoani Dodoma.
Sehemu ya wafanyakazi wa SSRA wakati wa Maonesho ya Nanenane.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA Bi Sarah Kibonde Msika, akimkabidhi mfuko wa SSRA pamoja na Vipeperushi Mratibu wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati Bw, Mwinuka, Maonesho hayo yanaendelea Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde Msika akiwa na wadau waliotembelea Banda la SSRA wakati wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati.

Mwakyembe Ataka Kuanzishwa kwa Mfuko wa Wasanii

$
0
0


 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na wadau wa sanaa ya muziki kupitia Chama cha Wanamuziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa TUMA Bw. Bryton Kibwana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo. Mkutano huo umeratibiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa lengo la kuwakutanisha wasanii hao na Mhe. Waziri ili kujadilia changamoto zao.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Bw. Onesmo Kayanda akizungumza wakati wa mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe(hayupo pichani) na wadau wa sanaa ya muziki kupitia Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA) leo Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Joyce Hagu akielezea jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani). Mkutano huo umewakutanisha wasanii mbalimbali kupitia Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA) leo Jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA) Bw. Samwel Mbwana (Bryton) akielezea jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani). Mkutano huo umewakutanisha wasanii mbalimbali kupitia Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA) leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiteta jambo na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Bw. Onesmo Kayanda wakati wa mkutano baina ya Waziri Mwakyembe na wadau wa sanaa ya muziki kupitia Chama cha Wanamuziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA) leo Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akiteta jambo na Katibu wa Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA) Bw. Samwel Mbwana (Bryton) wakati wa mkutano baina ya Waziri Mwakyembe na wadau wa sanaa ya muziki kupitia Chama cha Wanamuziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA) leo Jijini Dar es Salaam.

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Jeff Mduma akitumbuiza wakati wa mkutano wa mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye kofia) na wadau wa sanaa ya muziki leo Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umeratibiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) na kuwakutanisha wasanii mbalimbali kupitia Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA).

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) pamoja na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (kushoto) na Kaimu wakipokea zawadi ya Saa ya Ukutani kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya (TUMA) Bw. Samwel Mbwana (Bryton) ikiwa ni kutambua mchango wa Serikali katika kushughulikia changamoto za wasanii leo Jijini Dar es Salaam katika mkutano uliowakutanisha wadau wa sanaa ya muziki kupitia Chama cha Wanamuziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA). Kulia kushoto kwa Waziri ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Bw. Onesmo Kayanda na Msanii Witness Mwijage.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiwapongeza baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya waliochaguliwa kuwawakilisha wenzao katika kamati itakayoundwa na Serikali kwa ajili ya kupitia Sera na Sheria za sekta ya sanaa hapa nchini wakati wa mkutano na wadau wa sanaa ya muziki kupitia Chama cha Wanamuziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Witness Mwijage, Azma Mponda, Taji Liundi na Nikki wa Pili.

…………………………


Na. Neema Mathias na Thobias Robert- MAELEZO

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewahamasisha Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya nchini kuanzisha mfuko wa wasanii kwa lengo la kutatua changamoto ya udhamini inayowakabili.

Waziri Mwakyembe ametoa wito huo leo Jijini Dar es Salaam katika kikao kazi na Wasanii hao kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) ambacho kilijadili changamoto mbalimbali zinazowakabili Wasanii na namna ya kukabiliana nazo.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Mwakyembe alisema kuwa kutokana na malalamiko na changamoto mbalimbali zinazowakabili Wasanii, ambazo nyingi zinasababishwa na mikataba inayowanyonya Wasanii katika kazi zao, ni vema sasa Wasanii hao kupitia Chama chao cha Tanzania Urban Music Association (TUMA) kuanzisha mfuko ambao utakua unatoa mikopo kwa Wasanii ili kuwezesha utendaji wa kazi zao pasipo kutegemea wadhamini.

“Ninafikiri dawa tunayohitaji ni kuanzishe mfuko wa Wasanii ambapo kila Msanii atatakiwa kuchangia fedha. Jambo ambalo litawavutia wadau wengine kuchangia mfuko huo na kuwaondoa katika dhana ya utumwa, na mfuko huo utamsaidia msanii aliyejisajili kupata mkopo bila kutozwa riba yoyote,” alielezea Waziri Mwakyembe.

Waziri Mwakyembe alisema kuwa Tasnia ya Sanaa ina mchango mkubwa katika kuongeza pato taifa hivyo ametaka tasnia hiyo kurasimishwa ili kupunguza tatizo la ajira na pia kutumika kama chombo maalumu cha kuielimisha jamii kwani kupitia Sanaa wananchi hupata ujumbe kwa urahisi.

Aidha, Waziri Mwakyembe ameunda Kamati ya kushughulikia masuala yanayowakabili Wasanii ikiwemo sera na sheria ili kuboresha maslahi ya Msanii. Wasanii wanaounda Kamati hiyo ni Azma Mponda, Niki wa Pili pamoja na Witness Mwaijanga.

Katika hatua nyingine Waziri Mwakyembe amelitaka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kufanyia mabadiliko sera ya Sanaa pamoja na baadhi ya vipengele vya sheria ya Sanaa ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia.

“Tunahitaji mabadiliko ya sheria ya sanaa haraka. Katika sheria hiyo ni marufuku mmiliki wa vyombo vya habari kulipwa na Msanii ili kupiga wimbo wake, hakuna nchi katika dunia hii ambayo Msanii anatozwa fedha ili wimbo wake upigwe,” alisisitiza.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Onesmo Kayanda amesema kuwa, ili kuboresha na kukuza tasnia ya muziki nchini ni lazima kuwepo na soko la uhakika la kazi hizo pamoja na tuzo mbalimbali ambazo zitatumika kutia hamasa kwa wasanii.

Hata hivyo Bw. Kayanda ameongeza kuwa sera, sheria na miongozo ya baraza hilo ihuishwe ili kulinda kazi mbaimbali za Wasanii ikiwa ni pamoja na kuanzisha mfumo wa kielektoniki wa kujisajili ili Serikali iweze kupata mapato halisi kupitia biashara ya muziki.

Kikao hicho ni cha kwanza kufanyika tangu Waziri Mwakyembe ateuliwe katika Wizara hiyo ambapo ameeleza kuwa kikao kazi kitakuwa kikifanyika mara kwa mara na atakuwa akikutana na wasanii wa vikundi mbalimbali ili kujadili mambo yanayohusu Wasanii hao.

Simbachawene Ahamasisha Teknolojia ya Kilimo Kihamishiwe kwa Wakulima

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,George Simbachawene akifungua maonesho ya wakulima na wafugaji Kanda ya Kaskazini(Taso) kwenye viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,George Simbachawene(wa pili kushoto)akitembelea maonesho kwenye vipando vya kampuni ya mbegu ya Seed Co kabla ya kufungua maonesho ya wakulima na wafugaji Kanda ya Kaskazini(Taso) kwenye viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha,kushoto ni Mtaalamu wa ardhi na mimea wa kampuni hiyo,Philemon Mushi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,George Simbachawene(wa pili kushoto)akitembelea maonesho kwenye vipando vya kampuni ya mbegu ya Seed Co kabla ya kufungua maonesho ya wakulima na wafugaji Kanda ya Kaskazini(Taso) kwenye viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha,kushoto ni Mtaalamu wa ardhi na mimea wa kampuni hiyo,Philemon Mushi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,George Simbachawene(kulia)akipewa maelezo ya namna ya kulima bila kutumia udongo na Mtalaamu wa kilimo wa kampuni ya Rijk Zwaan alipotembelea maonesho kwenye vipando vya kampuni ya mbegu hiyo kwenye viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha,kushoto ni Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,George Simbachawene(wa pili kushoto)akiangalia namna kikundi cha Nronga Women Dairy cha wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro kinavyojishughulisha na uuzaji wa maziwa kwenye banda la halmashauri ya Hai kwenye viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha,kushoto ni Mkuu wa Hai,Gelasius Byakanwa.
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akizungumza kwenye maoenesho ya 24 ya wakulima na wafugaji kanda ya kaskazini .

……………………………

Nteghenjwa Hosseah – Arusha

Nane nane ni miongoni mwa maonyesho maarufu Nchini Tanzania ambayo huwagusa na kuwakutanisha wakulima, wafugaji, wavuvi wa Mjini na Vijijini, Taasisi za Serikali na binafsi zinahusika na sekta hiyo zilizopo ndani na nje ya Nchi pamoja na Wadau wa Kilimo.

Maonyesho ya Nane nane hutoa fursa kwa wadau wote wa sekta ya Kilimo kuonyesha bidhaa mbalimbali za Kilimo, kuuza bidhaa hizo, kubadilishana uzoefu na kujifunza teknolojia mbalimbali zia kuboresha Sekta ya Kilimo ili kuondokana na Kilimo cha kufa na kupona na kuwa Kilimo chenye Tija kinanachofaa kwa biashara na kutosheleza kwa chakula.

Katika historia ya maonyesho haya ambayo wakulima kutoka Halmashauri mbalimbali Nchini hushiriki ili kujifunza teknolojia hizo mpya za Kilimo kumekuwa na mabadiliko kidogo katika eneo la utekelezaji wa Teknolojia hizo katika maeneo yao.

Huenda tatizo likawa ni uelewa mdogo wa wakulima wetu wanaoshiriki katika maonyesho hayo, kutokujifunza kwa umakini kuhusu mbinu hizo za kisasa au kukosekana kwa uwezeshaji wa wananchi katika kutekeleza mbinu hizo kwenye maeneo yao au kutokuwa na usimamiza wa maafisa Ugani katika maeneo mengi ya Kilimo Nchini.

Ushiriki wa mazoea katika Maonyesho haya unaelekea kufika mwisho baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene kufungua Maonyesho ya 24 Kanda ya Kaskazini yaliyofanyiika Mkoani Arusha katika viwanja wa Themi – Njiro.

Wakati wa Ufunguzi wa Maonyesho hayo Waziri Simbachawene alikagua mabanda mbalimbali ya Kili mo na Mifugo ya Halmashauri za Kanda ya Kaskazini, Sekta binafsi za Kuzalisha Mbegu bora, Pembejeo, Zana za Kilimo viwatilifu pamoja na dawa za Mifugo na kujionea teknolojia bora na za kisasa zinazoweza kumsaidia Mkulima na Mfugaji kuachana na kilimo cha kujitaftia chakula na kuhamia kwenye biashara njia itakayoweza kumuo ngezea kipato na kumwinua kiuchumi.

Akifungua Maonyesho hayo Mhe. Simbachawene amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauro zote Nchini sambamba na Maafisa Ugani kujifunza Teknolojia mbalimbali zilizopo kwenye maonyesho haya na kwenda kuwafundisha wananchi na kuwawezesha kuzitekeleza katika maeneo hayo.

Amesema kuanzia mwaka huu nataka maonyesho haya yanalete mabadiliko kwa wananchi wetu kwa kuwawezesha kulima kwa Tija kwa kutumia eneo dogo na kuweza kupata mazao mengi, kufunga kisasa kwa kuwa na mifugo bora na michache lakini yenye faida kubwa pamoja na kuanzisha ufugaji bora wa samaki katika maeneo mengi Nchini.

“Kuanzia mwakani tutaanza kufanya tathmini ya namna ambavyo maonyesho haya yamebadilisha maisha ya wakulima wetu katika Halmashauri na sio kila mwaka Halmashauri zinashiriki lakini hamuondoki na kitu kipya wala hamuwasaidii wakulima wa kule vijijini ambao huenda hawapati fursa ya kuja kuona mapinduzi haya katika Kilimo”.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya maonyesho haya Kanda ya Kaskazini amesema katika mara hii ya kwanza ambapo maonyesho haya yametoka kwenye Chama cha Wakulima na Wafugaji (TASO) na kuratibiwa na Serikali wamejitahidi kushirikisha wadau mbalimbali wenye teknolojia tofauti tofauti ili kuweza kutoa wigo mpana kwa wakulima na wafugaji kujifunza zaidi.

Pia aliongeza kuwa ameunda kamati ambayo itaongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro kuchunguza namna ambavyo TASO walivyokuwa wanafanya kazi, Mali zinazomilikiwa na Taso, Mapato yaliyopatikana wakati wa uratibu wao na namna ambavyo yalitumika na mgawanyo wa kazi zao na kuja na usahuri wa kitaalam juu ya nini kifanyike katika kuboresha zaidi usimamizi wa maonyesho hayo.

Waziri Simbachawene amefungua maonyesho haya ikiwa ni ya Pili tangu maadhimisho ya Sherehe hizi yalipoanza na alifungua Kitaifa katika Viwanja vya Ngongo – Lindi na atafunga maoneysho katika viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya.

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI AWAAPISHA MAKAMISHNA WAPYA

$
0
0

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimvisha cheo Kamishna wa Divisheni ya Operesheni Billy Mwakatage,wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimvisha cheo Kamishna wa Divisheni ya Usalama dhidi ya Moto, Jesuald Ikonkowakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimsikiliza Msemaji wa Jeshi hilo Mrakibu Msaidizi Puyo Nzalayaimisi,akitoa utambulisho mfupi wa Makamishna wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Divisheni ya Oparesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage, akila kiapo cha Utii mbele yaKamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye,wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Divisheni ya Usalama dhidi ya Moto wa Jeshi la Zimamoto na, Jesuald Ikonko, akila kiapo cha Utii mbele ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye(watatukulia), akiwa katika picha na Kamishna wa Utawala na Fedha, Michael Shija (wapili kulia), Kamishna wa Oparesheni Billy Mwakatage (kushoto) na Kamishna wa Usalama dhidi ya Moto, Jesuald Ikonko (kulia) wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI, MAKAO MAKUU

RAIS DKT MAGUFULI APOKEWA KWA NDEREMO MKOANI TANGA

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia  maelfu ya wananchi wa Mkata  akiwasili mkoani Tanga
 Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkata wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
 Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkata wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
 Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkata wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
 Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkata wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
 Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkata wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
 Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkata wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
 Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkata wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
 Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkata wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi Mkata
 Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkata wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaga baada ya kuongea na wananchi wa Mkata
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa aliposimama kuongea na wananchi eneo la Komkonga
  Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama kuongea nao eneo la Komkonga
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi aliposimama eneo la Komkonga
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi aliposimama eneo la Komkonga
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe akimshangilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akiongea na wananchi aliposimama eneo la Komkonga
 Wananchi wakiwa na furaha kumuona Rais wao

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza kwa kazi nzuri na ya mfano  katika kuendeleza elimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mhe. Robet Gabriel 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza kwa kazi nzuri na ya mfano  katika kuendeleza elimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mhe. Robet Gabriel 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe akiongea jambo na  Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mhe. Robet Gabriel 
 Wananchi wa Hale wakimsikiliza Rais
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi wa Michungwani

 Wananchi wakimshangilia Rais Magufuli
 Rais akisalimiana na wananchi wa Kabuku 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia vazi la mwananchi
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia vazi la mwananchi 
 Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukisimamishwa na maelfu ya wananchi kila alipopita 
 Wenyeji kwa wageni wakifurahia ujio wa Rais Magufuli
 Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukisimamishwa na maelfu ya wananchi kila alipopita 
 Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukisimamishwa na maelfu ya wananchi kila alipopita 
 Rais Magufuli akiongea na wananchi eneo la Hale
 Wananchi wenye furaha wakimsikiliza Rais Magufuli
 Wengi walitumia simu zao za mkononi kumrekodi Rais Magufuli
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe January Makamba akiongea 
 Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akilakiwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo alipowasili wilayani humo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mbunge wa Muheza Mhe. Adadi Rajabu
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa kwa shangwe na wananchi wa Muheza
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma mabango alipowasili wailayani Muheza
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndg. Abdulrahmana Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Mhe. Henry Shekifu wakati wa mkutano wa hadhara wilayani Muheza
  Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndg. Abdulrahmana Kinana akiongea katika  mkutano wa hadhara wilayani Muheza
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitambulishwa kwa wananchi wakati wa mkutano wa hadhara wilayani Muheza
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimia  wananchi wakati wa mkutano wa hadhara wilayani Muheza
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa meza kuu na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigella wakati wa mkutano wa hadhara wilayani Muheza

 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndg. Abdulrahmana Kinana katika  mkutano wa hadhara wilayani Muheza
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndg. Abdulrahmana Kinana akiongea na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe January Makamba  katika  mkutano wa hadhara wilayani Muheza

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi wa Muheza
 Wananchi wa Muheza wakimsikiliza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Mhe. Stephen Ngonyani aka 'Profesa Maji Marefu' akisalimia wananchi
 Mbunge wa Pangani Jumaa Aweso akisalimia wananchi
  Mbunge wa Korogwe Mjini Mhe. Mary Chatanda akisalimia wananchi
 Mbunge akisalimia wananchi
 Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini Mhe Omari Kigoda akisalimia wananchi
 Mbunge wa Muheza Mhe. Adadi Rajabu akisalimia wananchi
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha na baadhi ya viongozi wa Muheza
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Profesa Maji Marefu
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha na baadhi ya watoto waliokuwepo kwenye mkutano wake wa hadhara Muheza
 Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukielekea mkoani Tanga ambako katika ziara yake ya siku tano ataungana na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda kesho Jumamosi katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la kuanza kwa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima hadi bandari ya Tanga
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Tanga pamoja na maelfu ya wananchi wa Mkata wakati akiwasili mkoani Tanga
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Tanga pamoja na maelfu ya wananchi wa Mkata wakati akiwasili mkoani Tanga

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza diwani wa Pongwe Mhe. Mbaraka Saadi Mbaraka akimuelezea changamoto za eneo lake

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza  diwani wa Pongwe Mhe. Mbaraka Saadi Mbaraka aliyemuelezea kwa ufasaha changamoto za eneo lake 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsifia  diwani wa Pongwe Mhe. Mbaraka Saadi Mbaraka kwa kumuelezea changamoto za eneo lake. 

 Wananchi na diwani wa Pongwe Mhe. Mbaraka Saadi Mbaraka wakifurahia umauzi wa Rais wa kujengwa kituo cha mabasi eneo lao 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekeza eneo la Pongwe lijengwe kituo cha mabasi na kuitwa jina la diwani wa Pongwe Mhe. Mbaraka Saadi Mbaraka baada ya  kufurahishwa na jinsi alivyomuelezea kwa ufasaha  changamoto mbalimbali za eneo lake. Picha zote na IKULU

Mahojiano ya Mubelwa Bandio na Maduhu Emmanuel ndani ya Kilimanjaro Studios

$
0
0
Emmanuel Maduhu ni mtangazaji wa Morning Star Radio na Televisheni jijini Dar Es Salaam.Mwezi Julai 2017 alifanya ziara ya kikazi nchini Marekani, ambapo alitembelea majimbo kadhaa.Mwishoni mwa ziara yake, alipata fursa kuketi na Mubelwa Bandio wa Kwanza Production ndani ya Kilimanjaro Studios na kujadili mambo mbalimbali kuhusu kazi, ziara, maisha nk Karibu ujiunge nasi

Mkuu wa Wilaya Mkalama, Awataka Bodaboda kuchangamkia Fursa NMB

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, Eng.Jackson Makata akizindua rasmi tawi la NMB wilayani humo. Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, Eng. Jackson Makata (mwenye miwani) pamoja na maofisa wa NMB wakifurahia mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa Tawi la Benki ya NMB Mkalama.

MKUU wa Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, Eng. Jackson Jonasi Masaka, amewaagiza madereva wa boda boda kuanzisha na kusajili vikundi vya ujasiriamali, ili kujijengea mazingira mazuri kupata mikopo toka tawi la NMB benki, lililozinduliwa wilayani humo. Eng. Masaka ametoa agizo hilo juzi wakati akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa tawi la NMB tawi la Mkalama, lililopo katika makao makuu ya wilaya hiyo, Nduguti.

Alisema kufunguliwa kwa tawi hilo kumesogeza karibu zaidi huduma mbalimbali ikiwemo ya mikopo zinazotolewa na NMB benki, kwa wakazi wa wilaya hiyo. Akifafanua, alisema huko nyuma wakazi wa wilaya hiyo pamoja na watumishi wa umma, iliwabidi kufuata huduma za kibenki Singida mjini, umbali wa kilometa 140 kwenda na kurundi.

“Kwa hiyo ninyi madereva wa bodaboda, NMB imesongeza huduma…huu ni wakati muafaka kuboresha shughuli zenu. Msilale changamkeni, jiungeni kwenye vikundi vilivyosajiliwa muweze kupata mikopo itakayokuza mitaji yenu. Mjue tu kwamba dereva mmoja mmoja ni ngumu mno kupata mkopo kwenye taasisi za kifedha”, alisema mkuu huyo wa wilaya. Eng. Makata pia ametumia fursa hiyo kuwahamasisha baba/mama lishe, wauza chips na wajasiriamali mbalimbali wakiwemo wadogo, kuchangamkia mikopo kupitia akaunti ya ‘FANIKIWA’.

“Niipongeze NMB benki kwa kubuni bidhaa hii ya akaunti ya FANIKIWA. Kupitia akaunti hii ya FANIKIWA, wajasiriamali niliowataja hapo juu, wataweza kupata mikopo kati ya shilingi laki tano na milioni 30. Nasisitiza tumieni fursa hizi zilizosongewa karibu zaidi na NMB, ili mkuze mitaji yenu iweze kukidhi mahitaji ya wakati wa sasa,” alisema.

Katika hatua nyingine, mkuu huyo wa wilaya ameishukru na kuipongeza NMB benki kwa msaada wake wa vitanda 15, magodoro 15, vitanda viwili vya kujifungulia akina mama wajawazito na mashine mbili za kupimia mapigo ya moyo.

“Msaada huu wenye thamani ya shilingi milioni 10 ambao umetolewa kwa kituo cha afya, vitunzwe na kulindwa vizuri ili viweze kutumika kwa kipindi kirefu,” alisema Eng. Makata. Awali meneja wa uhusiano wa biashara kati ya serikali na benki NMB kanda ya kati, Yasin Mfinanga, alisema msaada huo ni mwendelezo wa NMB katika kumuunga mkono Rais Dk. Magufuki kuboresha sekta ya afya.

“Kila mwaka baada ya kutoa gharama zote za uendeshaji, benki yetu huwa inatenga asilimia moja ya faida, kwa ajili ya kutoa misaada inayolenga sekta ya afya na elimu. Agizo la rais Magufuli la kuchangia madawati katika shule za msingi na sekondari, NMB ilishiriki kikamilifu,” alisema Mfinanga kwa kujiamini.

Mfinanga alitumia fursa hiyo kuwataka wakazi wa kanda ya kati, kuacha kabisa utamaduni wa kutunza fedha kwenye simu zao za viganjani na badala yake wazitunze kwenye mabenki ikiwemo ya NMB. Akisisitiza, alisema fedha zinazotunzwa kwenye simu za viganjani usalama wake ni mdogo mno, ikilinanishwa na zile zinazotunzwa kwenye mabenki ya kuaminika.

“Fedha hizi zilizopo kwenye simu za viganjani na wakazi wa kanda ya kati wakijitokeza kwa wingi kuweka fedha benki, hatua hiyo itachangia NMB benki kuwa na uwezo mkubwa katika kutoa mikopo. Aidha, hatua hii itachangia benki kupunguza riba zinazokatwa kwenye gharama za uendeshaji,” amesisitiza zaidi.

Wakati huo huo.mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mkalama, James Mkwega, alisema kufunguliwa kwa tawi la NMB tawi la Mkalama, pamoja na mambo mengine, kutachochea ukuaji wa uchumi. “Binafsi nimefarijika mno…na naipongeza NMB benki kufungua tawi hapa kwetu Nduguti makao makuu ya wilaya ya Mkalama. Huko nyuma tulilazimika kufuata huduma za kibenki Singida mjini kilometa 140 kwenda na kurudi. Madhara yake yalikuwa makubwa mno,” alisema na kuongeza;

“Watumishi wa umma wakiwemo walimu nao wametaabika sana katika kufuata mishahara yao New Kiomboi wilaya ya Iramba umbali wa likometa 90. Hapo ilikuwa kabla wilaya Iramba yaijagawanywa na kuzaa wilaya ya Mkalama. Nakumbuka baadhi ya walimu walikuwa wanatumia usafiri wa baiskeli, wakifika msitu wa Gumanga, walikuwa wakiporwa mishahara yao na majambazi,”

Mwenyekiti huyo ambaye ni diwani (CCM) kata ya Gumanga, alisema kuwa kwa sasa hayo yote yatabaki kuwa histori, baada ya NMB kufungua tawi hilo.

JAFO: HILI NI DAMPO LA MFANO

$
0
0
Kazi ya utupaji taka na ushindiliaji taka ikifanyika ndani ya Dampo la kisasa la Chidaye.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua eneo la Dampo la Chidaye
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza mara baada ya kukagua Dampo la Chidaye.

…………………….
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo ameipongeza Manispaa ya Dodoma kwa usimamizi mzuri wa miradi inayo tekelezwa na Ofisi ya Rais Tamisemi katika Manispaa hiyo ikiwemo kufanikisha ujenzi wa miundombinu ya barabara za Lami pamoja na ujenzi wa Dampo la kisasa.

Naibu Waziri Jafo aliimwagia sifa Halmashauri hiyo kwa usimamizi mzuri uliofanikisha ujenzi huo licha ya kuanza kutumika tangu mwezi Februari mwaka huu.

“Pamoja na kutumika tangu mwezi Februari lakini hakuna chembe ya harufu wala inzi ukilinganisha na madampo mengine hapa nchini,”amesema Jafo

Amependezwa na mfumo mzima uliotumika katika ujenzi wa Dampo hilo ambalo ni miongoni mwa madampo kadhaa yanayo jengwa na Tamisemi katika miji mbalimbali hapa nchini kwa fedha kutoka Benki ya dunia.

Jafo amewataka wataalam wengine kutoka miji mbalimbali kuja kujifunza ili maeneo yote yanapojengwa madampo hayo waige mfano mzuri wa Dodoma.

Jafo ameutaka uongozi wa jiji la Dar es salaam pamoja na manispaa zake kuja Dodoma kujiongezea maarifa wakati wanajiandaa kujenga miradi kama hiyo katika jiji hilo kupitia mradi wa Dar es salaam Metro Politant Development Project (DMDP) ulio chini ya Ofisi ya Rais Tamisemi.

Naibu Waziri Jafo amewataka wanadodoma kutunza miundombinu hiyo ambayo serikali inaingia gharama kubwa kuijenga.

Dampo hilo linatarajiwa kutumika kwa zaidi ya miaka 19 kuanzia sasa.

MPINA AAGIZA UJENZI WA CHANZO CHA MAJI CHA AJABU KUKAMILIKA MAPEMA

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira Mhe.Luhaga Mpina ambaye pia ni Mbunge wa Kisesa akiongea na wadau hawapo katika picha kuhusu utekelezaji wa mradi wa chanzo cha maji cha Igombe, Mwandoya Mkoani Simiyu.
Chanzo cha maji cha ajabu kikiwa chini ya Mchanga, ambapo juu hakuna maji yoyote yanayoonekana badala yake ni mchanga unaonekana kama mto uliyokauka maji, chanzo hiki kipokatika kijiji cha Igombe wilayani Meatu.
Jengo linaloonekana katika Picha ni sehemu ya kupokelea maji yanayotoka chini ya mchanga na kupanda bila pump katika mabomba ndani ya jengo hilo na kuja kusambazwa kwa wakazi kwa vijiji jirani kwa matumizi ya nyumbani
Jengo linaloonekana katika Picha ni sehemu ya kupokelea maji yanayotoka chini ya mchanga na kupanda bila pump katika mabomba ndani ya jengo hilo na kuja kusambazwa kwa wakazi kwa vijiji jirani kwa matumizi ya nyumbani

………………….

NA EVELYN MKOKOI – IGOBE

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ameagiza chanzo cha maji cha kipekee ambacho kinatoa maji chini ya Mchanga, kilichopo katika kijiji cha Igobe Wilayani Meatu kukamilika ifikapo mwisho wa Mwezi huu ili kusaidia utoaji na usambazaji wa huduma ya maji safi na salama katika vijiji jirani na chanzo hicho na kata ya Mwandoya kwa ujumla.

Akiendelea na ziara ya kikazi Jimboni Kisesa, Mpina ameelezwa kuwa ucheleweshwaji wa kukamilika kwa matumizi ya chanzo hicho cha maji yametokana na kucheleweshwa kwa malipo kwa mkandarasi Mbesso Constraction Company ltd. ambapo kati ya fedha za mradi shilingi milioni 502, zinazotelewa na serikali kupitia Wizara ya maji na umwagiliaji ni kiasi cha fedha cha shilingi milioni 114 tu ndizo zilitoka na kutumika mpaka sasa.

Mpina, ameagiza kufanyiwa kazi kwa kasoro zilizojitokeza katika mradi huo wenye uwezo wa kuhudumia takribani watu elfu nane katika kijiji cha Mwandoya na Igobe, ili kumuwezesha mkandarasi kukamilisha kazi hiyo wa wakati.

“ Lazima Pawepo na usimamizi madhubuti katika mradi huu ili wakazi wa maeneo jirani na mradi na mbali na hapa waweze kunufaika na kama kutajitokeza kwa uzembe wowote wahusika watawajibika kwa mamlaka.” Alisisitiza Mpina.

Katika ziara yake Naibu Waziri Mpina pia alitembelea shule ya Sekondari ya Mwandoya ambapo aliongea na walimu wa shule hiyo na kuwaeleza bila kuficha kuwa wamekuwa wakilaumiwa sana kwa kuwa na mauhusiano ya kimapenzi na wanafunzi wa shule hiyo na kuwaasa kuacha tabia hiyo inayopelekea kuwaharibia maisha vijana hao na kutoa wito kwa watu wazima katika kijiji cha Mwandoya kuachana kabisa na tabia hiyo kwani ni kinyume na sheria na maadili ya Tanzania na kuwa Serikali ya awamu ya tano ipo kazini.

Pamoja na hilo Mpina alisikiliza changamoto zinazoikabili shule hiyo na kuhaidi kutatua baadhi ya changamoto mpya, pia Mpina alikagua baadhi ya Mabweni mapya ya kisasa yaliyojengwa katika shule hiyo.

Sambamba na hilo Naibu Waziri Mpina ambaye pia ni Mbunge wa Kisesa, alikagua ujenzi wa wodi Mpya ya wazazi inayojengwa katika zahanati ya Mwandoya ambayo imefikia katika hatua ya kupauliwa.

WANANCHI WA LONGIDO WAPONGEZWA KWA KUJITOLEA KUJENGA JENGO LA POLISI WILAYA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa jengo la utawala la Polisi wilaya ya Longido, kulia kwake ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo na kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Longido Bw. Daniel Chongolo
Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wakati akifungua jiwe la msingi lililowekwa katika ujenzi wa jengo la utawala la Polisi wilaya ya Longido

Jengo jipya la utawala Polisi wilaya ya Longido ambalo lilizinduliwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo jana katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)

…………………….
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo amewashukuru na kuwapongeza wadau mbalimbali wa maendeleo ambao wamejitoa na kuhakikisha wanakamilisha jengo la utawala la Polisi wilaya ya Longido.

Akizindua jengo hilo jana, alisema kwamba litawezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa utulivu sambamba na kukabiliana vyema na masuala ya uhalifu katika wilaya hiyo, na kuongeza kuwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa anajisikia furaha na fahari kuona wadau wanashirikiana na kuagiza meneja wa Tanesco wilaya ahakikishe ameweka mita ya umeme ambapo gharama hizo aliahidi atazitoa yeye mwenyewe.

“Lazima tuimarishe mipaka na Polisi wawe na vituo vya uhakika vya kufanyia kazi ili waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali za uhalifu na Jeshi hilo litaendelea kutumia mbinu shirikishi”. Alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Bw. Gambo aliwaasa baadhi ya viongozi wa vijiji na vitongoji pamoja na wananchi kutoficha wageni ambao wanaishi nchini bila kufuata sheria na kuongeza kuwa yeyote atakayegundulika anafanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.

“Kila kiongozi anapaswa kutambua watu wote wanaoishi katika eneo lake na kuhakikisha mgeni yoyote amefuata sheria na kama akigundua (Anaishi bila utaratibu) atoe taarifa kupitia kamati za ulinzi na usalama za kata ili hatua ziweze kuchukuliwa”. Alisisitiza Bw. Gambo.

Akizungumza katika uzinduzi huo mwenyeji wa shughuli hiyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Omari Mkumbo mbali na kuwashukuru wadau hao, alisema kwamba tukio la uchangiaji na ukamilishaji wa jengo hilo limeonyesha kwamba wana Longido wana mshikamo wa hali juu.

Kamanda Mkumbo alisema kwamba wananchi waendeleze mshikamo huo ili kuweza kuimarisha kituo kingine cha Polisi kilichopo tarafa ya Kamwanga na kutaja majengo mengine ambayo yanajengwa na kukaribia kukamilika kwa hamasa ya Mkuu wa mkoa kuwa ni kituo cha Polisi cha Kwa Morombo pamoja na kituo cha Polisi cha Utalii ambacho ujenzi wake unafadhiliwa na TATO (Tanzania Tourist Operators).

“Kazi kubwa ya Jeshi la Polisi ni kuhakikisha uhalifu unakomeshwa na japokuwa takwimu za matukio ya uhalifu katika wilaya hiyo yapo chini lakini bado kuna tatizo la madawa ya kulevya aina ya Bhangi na Mirungi hivyo wananchi endeleeni kutoa ushirikiano kwa askari kwani madhara ya madawa hayo ni makubwa”. Alisema Kamanda Mkumbo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Daniel Chongolo alisema ongezeko la ukamataji wa madawa ya kulevya umetokana na udhibiti mzuri na kuahidi kuimarisha zaidi usalama kwa kutumia Polisi na vyombo vingine vya usalama huku akitoa shukrani zake kwa Kamanda wa Polisi mkoa kwa kutoa gari ambalo litasaidia kuimarisha ulinzi katika tarafa ya Kamwanga.

Awali akitoa taarifa ya uhalifu pamoja na mchakato wa ujenzi huo, Mkuu wa Polisi wilaya ya Longido Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Joswam Israel Kaijanante alisema kwamba ujenzi huo umegharimu zaidi ya Milioni 80 ambazo zilichangwa na viongozi, askari pamoja na wananchi na kuongeza kwamba bado jengo hilo halina samani na “Kompyuta , Printer” pamoja na mfumo wa maji taka ambapo gharama zake ni Milioni 16.

Mchakato wa ujenzi wa jengo hilo ambao una ofisi tatu ambazo ni za Mkuu wa Polisi wilaya, Mkuu wa Upelelezi wilaya na Mwendesha Mashtaka wa Polisi ulianza mwaka 2015 na kukamilika mwezi Julai mwaka huu uliwashirikisha kikamilifu jumla ya wadau wapatao 20 ambao pia walipewa vyeti vya shukrani.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA AUG 4,2017

TCAA YASHIRIKI MAONESHO YA NANE NANE MKOANI LINDI

$
0
0
Afisa Muongoza Ndege Mwandamizi, Godlove Longole akitoa elimu kwa wanafunzi waliotembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
 Afisa Muongoza Ndege Mwanadamizi (kulia) Godlove Longole na Afisa Habari Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Bestina Magutu wakitoa Elimu kwa watoto waliotembelea Banda la TCAA katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Mkufunzi Mwandamizi wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Kinachomilikiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Adinan Mvungi (Kulia),Adinan Mvungi Akitoa Elimu kwa Wanafunzi Waliotembelea Banda la TCAA Katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
 Afisa Habari Msaidizi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Ally Changwila  akitoa elimu kwa Mwanafunzi  aliyetembelea Banda la TCAA katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
Afisa Habari Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Bestina Magutu(wa pili kutoka kushoto) akitoa Elimu kwa wananchi waliotembelea banda la TCAA katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi. Wa kwanza kushoto ni Afisa Muongoza Ndege Mwanadamizi Godlove Longole.
Afisa Habari Msaidizi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Ally Changwila  akitoa elimu kwa Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi –Taarifa za Hali ya Hewa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini(TMA), Dkt Ladislaus Chang’a  aliyetembelea Banda la TCAA katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
 Timu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), wakiwa kwenye picha ya pamoja katika maonesho ya Nane nane 2017 katika viwanja vya Ngongo Lindi.
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images