Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

Wadau Sekta ya Mafuta na Gesi Washauriwa Kujiunga na ATOGS

$
0
0

 Mkurugenzi wa mifuko ya Uwezeshaji toka Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bw. Edwin Chrissant akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) fursa zilizopo za uwekezaji kupitia mifuko ya hifadhi, katikati ni Mwanzilishi na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi watoa huduma ya mafuta na gesi nchini Abdulsamad Abdulrahim na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo.
Picha na Eliphace Marwa – Maelezo
Pix 03
Mkurugenzi wa Taasisi ya sekta binafsi Dkt. Godfrey Simbeye akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu fursa mbalimbali zilizopo katika ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Tanzania hadi Uganda, kulia ni Mwanzilishi na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi watoa huduma ya mafuta na gesi nchini Abdulsamad Abdulrahim na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo.
Pix 02
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo (kushoto) akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)  fursa mbalimbali zilizopo katika ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Tanzania hadi Uganda, katikati ni Mwanzilishi na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi watoa huduma ya mafuta na gesi nchini Abdulsamad Abdulrahim na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya sekta binafsi Dkt. Godfrey Simbeye.
Pix 01
Mwanzilishi na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya watoa huduma ya mafuta na gesi nchini Abdulsamad Abdulrahim akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu fursa mbalimbali zilizopo katika ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Tanzania hadi Uganda, kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya sekta binafsi Dkt. Godfrey Simbeye na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Juliana Pallangyo.
………………………………………………………………….
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Wadau wa Sekta ya Mafuta na Gesi wameshauriwa kujiunga na Jumuiya ya Watoa Huduma wa Sekta ya Mafuta na Gesi (ATOGS) ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali kwa urahisi.

Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Dkt. Julia Pallangyo aliopokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu umuhimu wa Jumuiya hiyo.
Mhandisi Dkt. Julia amesema kuwa Sera ya Taifa ya Nishati ya mwaka 2015 inahamasisha ushiriki wa Watanzania katika Sekta ya Mafuta na Gesi asilia hivyo uanzishwaji wa ATOGS umekua msaada mkubwa katika utekelezaji wa Sera hiyo pamoja na kuimarisha ushiriki wa Watanzania katika Sekta hiyo.

“Natoa wito kwa watoa huduma kujiunga na ATAGOS kwa kuwa kufanya hivyo kutawawezesha kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mradi huo ambao utatoa fursa mbalimbali” Dkt. Julia alisema.

Alizitaja fursa hizo kuwa ni pamoja na ujenzi, uhandisi, manunuzi na uwezeshaji pamoja na huduma za kifedha na kibenki, huduma za bima, huduma kisheria, ulinzi pamoja na chakula.

Kwa upande mwingine, Naibu Katibu Mkuu amewakaribisha wananchi wa Tanga na wa mikoa ya pembezoni kufika katika eneo la Chongoleani Jumamosi tarehe 5 Agosti mwaka huu kushuhudia uwekwaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania. 

Akimuwakilisha Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Mkurugenzi wa Mifuko ya Uwezeshaji wa NEEC. Edwin Chrissant amesema kazi moja wapo ya Baraza ni kusimamia, kuratibu na kufuatilia shughuli zote za kiuchumi ikiwemo ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji hivyo mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ni fursa kubwa ambayo Watanzania wanaihitaji.

“Ujenzi wa mradi huu ni moja ya miradi mikubwa kufanyika nchini ambao utagharimu jumla ya shilingi trilioni 8 na bomba hili litakuwa na urefu wa Kilomita 1445 kati ya hizo kilomita 1149 sawa na asilimia 80 ziko Tanzania hivyo watanzania wakiwemo wale walio karibu na sehemu za ujenzi huo wanahamasishwa kujiunga na ATOGS ili kujengewa uwezo wa jinsi ya kutumia fursa hizo ”alisema Chrissant.

Chrissant alifafanua kuwa bomba hilo ambalo litapita katika mikoa nane ikiwemo ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara pamoja na Tang,ujenzi wake utachukua kati ya miezi 24 hadi 36 hadi kukamilika.

Nae, Makamu Mwenyekiti wa ATOGS, Abdulsamad Abdulrahim ameihakikishia Serikali kuwa watoa huduma waliopo nchini wameonesha uwezo na utayari wa kutoa huduma nyingi za kitaalam na nyinginezo zilizopo katika mnyororo wa ongezeko la thamani zitakazohitajika wakati wa ujenzi wa bomba la mafuta.

”Inatia moyo kwamba ushiriki wa watoa huduma wa Tanzania katika Sekta hiyo unapewa nguvu kisheria pia tunaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuthibitisha msimamo wake wa kutaka kuona Watanzania wananufaika na fursa za sekta hii jambo linaloleta matumaini mapya kwa jumuiya yetu,” alisema Abdulrahim.

ATOGS ilianzishwa kama chombo cha juu nchini kinachowakilisha na kusimamia maslahi ya wadau na makampuni yanayotoa huduma katika sekta ya mafuta na gesi nchini.

Uanzishwaji wa Jumuiya hiyo ulizingatia uwepo wa fursa zitokanazo na rasilimali za mafuta na gesi zikiwemo za ujenzi wa bomba la kusafirishia mafuta pamoja na mipango iliyopo ya kusambaza gesi katika miji mikubwa nchini.

RC MAKONDA APOKEA KOMPYUTA NYINGINE ZA KISASA 100, ZENYE THAMANI YA SHILLINGI MILLION 210

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda jana  amepokea Jumla ya kompyuta  za kisasa 100 zenye thamani ya Shillingi Million 210 kutoka kiwanda cha utengenezaji wa nguo zitokanazo na pamba ya Tanzania cha NIDA Textile Ltd.

Makonda amesema kmpyuta hizo atazitoa kwa Vituo vya Polisi 20 kwa ajili ya kufungwa mfumo wa kisasa wa kuripoti taarifa za uhalifu zilizoripotiwa kwenye Vituo vya Polisi kila siku (Crime Statistic Management Information System) kupambana na uhalifu.

Faida za Mfumo ni kumsaidia Mwananchi kupata taarifa za ndugu yake aliepotea pasipokujua yupo wapi kwa kumuangalia kwenye mfumo kama anashikiliwa kwenye Kituo cha Polisi mfumo utaonyesha taarifa zake kwa wakati kwenye kila Kituo.

Aidha mfumo utasaidia viongozi kupata taarifa za uhalifu zinazoripotiwa katika vituo vya Polisi kwa wakati na kupunguza uhalifu kwani taarifa zote za wahalifu zitaonekana kuanzia ngazi ya Mkuu wa Mkoa, Kamanda wa Mkoa,Wilaya na Mkuu wa kituo hivyo kusaidia viongozi kufanya maamuzi.

Mfumo pia utaondoa Rushwa na matukio ya Wananchi kubambikiziwa kesi kwani kila atakaefikishwa kituo cha Polisi viongozi wote akiwemo Mheshiniwa Makonda atapata atajua.

Mfumo pia utamuwezesha kiongozi kujua idadi na aina ya uhalifu unaofanyika kwa siku,eneo ambapo matukio hujirudia mara kwa mara sanjari na mhalifu ambae matukio matukio yake ya uhalifu yamekuwa yakijirudia maeneo mbalimbali.

“Tunaachana na kuandika taarifa kwenye makaratasi na makaunta au madaftari kwenye Vituo vya Polisi ambayo baada ya muda mfupi yanapotea na kumuacha Mwananchi hajui kesi yake imeishia wapi, huu mfumo ni ukombozi na mwonekano mpya wa Jeshi la Polisi na hata Wananchi wataachana na matatizo ya rushwa na watu kubambikiziwa kesi” Alisema Makonda.

Mfumo wa CSMIS utachukuwa taarifa za Mhalifu kuanzia anapoingia kituo cha polisi CRO, Jina la Mhalifu, Aina ya kesi,jina la Mpelelezi, Hakimu, Mahakama anayopelekwa na kama amehukumiwa kulipa faini au kifungo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda cha NIDA Bwana Mohamed Hamza amesema kampuni yao imeamua kuunga mkono jitiada za Mheshimiwa Makonda katika dhamira yake ya kufanya Mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam. 
 Baadhi ya Kompyuta hizo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ,Paul Makonda(wakwanza kulia) akikabidhiwa  Computer za kisasa 100 zenye thamani ya Shillingi Million 210 na  Mkurugenzi wa Kiwanda cha NIDA Bwana Mohamed Hamza.

 

DC HAPI AMALIZA MGOGORO SUGU WA ARDHI NAKASANGWE

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi ametoa miezi mitatu kwa kampuni ya upimaji wa ardhi ya Afro Map kuhakikisha wanamaliza upimaji wa ardhi kwa eneo la Nakelekwe, Mtaa wa Nakasangwe Kata ya Wazo ambalo limekuwa na mgogoro wa ardhi kwa muda wa miaka 13 tangu mwaka 2004 baina ya wakazi wa eneo hilo na wamiliki wa mashamba.

DC Hapi amesema chanzo cha mgogoro wa eneo hilo ni kutokupimwa, hivyo atahakikisha maeneo yote katika wilaya yake yanapimwa ili migogoro ya ardhi iwe historia kwa wanakinondoni.

Vilevile DC Hapi ameeleza kuwa serikali haiwezi kuacha wakazi 3900 wakipoteza maeneo kisa uwepo wa mashamba, ndiyo maana ameamua kuzikutanisha pande zote mbili ili waweze kutatua migogoro hiyo, na upimaji utakapofanyika vitapatikana viwanja 6000 ambapo pande zote mbili zitanufaika bila kubagua na maeneo mengine yatatengwa kwaajili ya huduma za jamii ikiwemo zahanati, shule na miundombinu ya barabara.

DC Hapi ameongeza kuwa wananchi wa maeneo hayo wasiyauze maeneo hayo mpaka upimaji utakapo fanyika, na wale ambao maeneo yao hayo kuwa katika mgogoro wafanye hivyohivyo.

Pia DC Hapi amewataka viongozi wa kisiasa kuacha kuchochea migogoro ya ardhi kwa maslahi yao ya kisiasa na endapo wakiendelea kufanya hivyo atachukua hatua stahiki dhidi yao.

Kwa upande wao wakazi wa eneo hilo na wamiliki wa mashamba wamepongeza jitihada za serikali kwa kutatua mgogoro huo na kuhaidi kufuata utaratibu ulioelekezwa.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi leo amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa maeneo ya Nakasangwe, Nakalekwa na kuwapa ujumbe kuwa mgogoro wa ardhi uliodumu eneo hilo kwa miaka 13 kiasi cha kusababisha vifo sasa suluhu yake imepatikana.

Hapi amesema kuwa ikiwa ni muendelezo wa utatuzi wa migogoro ya ardhi wilayani Kinondoni ofisi yake ilizikutanisha pande mbili za wenye mashamba na wakazi ambazo kwa miaka kadhaa zimekua kwenye mgogoro mkubwa na kufanya nao mazungumzo yaliyoweka msingi mzuri wa kumaliza mgogoro huo.

Hapi amewahakikishia wananchi hao kutokuwa na wasiwasi na kwamba serikali wilayani Kinondoni imeamua kutumia falsafa ya

"pata kidogo poteza kidogo" (win win)ili kumaliza mgogoro huo baina ya pande mbili na kurejesha hali ya amani kayila eneo hilo.

"Tumeamua sasa eneo hili lote lipimwe viwanja, ili wakazi wote mliohakikiwa kila mmoja apate kipande cha ardhi cha kuishi na familia yake na viwanja vinavyobaki wapate wenye mashamba. Hii ndiyo njia pekee ya kuweza kuwafanya muishi kwa amani katika mji uliopimwa na kupangwa vizuri."Alisema DC Hapi

Aidha, Hapi aliwaeleza wananchi hao kuwa katika eneo hilo zaidi ya viwanja 6000 vitapatikana na hivyo kuwatoa shaka kuwa wakazi wote zaidi ya 3000 waliohakikiwa kila mmoja atapata ardhi iliyopimwa huku wenye mashamba nao wakipata viwanja vitakavyobakia ili waweze kuviendeleza au kuviuza vikiwa na hati miliki.

DC Hapi amesema kazi ya upimaji wa ardhi katika eneo hilo inatarajiwa kuanza haraka na kumalizika ndani ya kipindi cha miezi mitatu chini ya kampuni ya Afro Map ambayo pande mbili zimeichagua kufanye kazi hiyo.

"Nawapa kampuni hii miezi mitatu tu, kazi ya upimaji iwe imekamilika eneo hili ili wananchi wangu waishi kwa amani wakijua serikali yao ipo kuwasaidia." Alisema DC.

Mgogoro wa Nakasangwe ulianza mwaka 2004 na hivyo kudumu kwa miaka 13 kipindi ambacho kilitawaliwa na chuki, uhasama na uadui mkubwa baina ya wenye mashamba na wananchi waliovamia mashamba hayo. Watu kadhaa walipoteza maisha katika mgogoro huo.

Wananchi wote wanaounda pande mbili za mgogoro wamemshukuru DC Hapi na kushikana mikono kama ishara ya mwisho wa mgogoro huo na mwanzo mpya.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi akizungumza jana mbele ya wananchi  wa Mtaa wa Nasarangwe, Kata ya Wazo   juu   ya kampuni ya Afro Map imepewa kazi upimaji wa viwanja  itakayokamilika  ndani ya miezi mitatu badala ya miezi nne iliyokuwa ikifahamika hapo awali.
 Diwani wa Kata ya Wazo Joel Mwakalebela akizungumza leo na wananchi wa juu ya kutoa ushirikiano katika kuchangia gharama za upimaji wa viwanja ili zoezi hilo lisikwame.
 Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi

VIJUSO VYA MAGAZETI YA ALHAMIS LEO AUG 3, 2017

Dkt.SUBI: MFUMO MPYA WA KUANDAA BAJETI UMELENGA KURAHISISHA KAZI

BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA-AfDB YAKUNWA NA VIWANGO VYA UJENZI WA BARABARA MTWARA

$
0
0
Benny Mwaipaja, WFM, Mtwara

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), imeelezea kuridhishwa na kasi pamoja na viwango vya miradi ya ujenzi ya barabara inayofadhiliwa na benki hiyo katika Ukanda wa Kusini, na kuahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa na wananchi wake.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo anayesimamia Kanda wa Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, baada ya kutembelea na kukagua barabara ya Tunduru-Nangaka-Mtambaswala, mkoani Mtwara, yenye urefu wa kilometa 202.2.

Barabara hiyo yenye vipande vitatu imejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 180 kupitia ufadhili wa benki hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) na Serikali ya Tanzania.

Dkt. Weggoro amesema kuwa barabara hiyo ambayo upande mmoja inaunganisha Tanzania na Msumbiji, itachochea maendeleo ya wananchi kutoka pande hizo mbili kwa kusafirisha watu na bidhaa kwa urahisi zaidi.

“Nimeona mabadiliko makubwa sana, si tu kwa barabara, lakini maisha ya watu, mabadiliko ambayo ni dhahiri yanatokana na hii miradi ya barabara ambayo imefungua fursa nyingi za maendeleo, watu wanafanyabiashara lakini pia wanatembeleana!” alisema Dkt. Weggoro.

Alitoa wito kwa Watanzania kuchangamkia fursa ya uwepo wa barabara hizo kujiletea maendeleo kwa kufanyabiashara hivyo kujikwamua kiuchumi.

Mhandisi Heldaus Jerome kutoka Wakala wa Barabara -Tanroads, Makao Makuu, alisema kuwa barabara hiyo ya Tunduru-Mangaka-Mtambaswala, ina vipande vitatu, kutoka Mangaka – Nakapanya (km 70.5), Nakapanya – Tunduru (66.5) na Mangaka – Mtambaswala (km 65.5)

Alifafanua kuwa gharama za ujenzi wa mradi huo, kiasi cha Dola milioni 210, kimetolewa na AfDB (64.79%), Shirika la Maendeleo la Japan-JICA (32.83%) na Serikali ya Tanzania (2.38%) na kwamba Wadau hao pia wanafadhili ujenzi wa barabara kutoka Dodoma-Babati yenye urefu wa kilometa 180.53.

Baadhi ya wakazi wa mji wa Mangaka wilayani Masasi mkoani Mtwara, wameishukuru Serikali kwa kufanikisha ujenzi wa barabara hiyo muhimu kwa uchumi na maisha yao kwa ujumla kwa kurahisisha usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo ndani na nje ya nchi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilimanihewa, Bw. Abbas Muhidin Mwira, alisema kuwa maeneo ya Mangaka yamechangamka kibiashara na vijana wengi wamejiajiri wenyewe kwa kufanyabiashara zinazowaingizia kipato huku huduma za usafiri zikiboreshwa baada ya mabasi ya abiria yaendayo mikoani pamoja na malori yanayobeba saruji kutoka Kiwanda cha Saruji cha Dangote-Mtwara kuanza kupita njia hiyo na kusisimua biashara zao.

SINGIDA UNITED YAZIDI KUJIIMARISHA, YAINGIA MKATABA WA MILIONI 250 NA KAMPUNI YA YARA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya Singida United Festo Sanga  (kushoto) na  Mkurugenzi Mkuu  wa kampuni ya YARA Alexander Macedo wakibadilishana nyaraka za mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja wenye thamani ya kiasi cha Milioni 250.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Timu ya Singida United imeingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya kiasi cha Milioni 250  na kampuni ya uzalishaji mbolea ya YARA ikiwa ni katika mikakati ya kuongeza vyanzo vya mapato ya timu hiyo.

Mkataba huo umesainiwa leo mbele ya waandishi wa habari ukishuhudiwa na kocha mkuu wa timu ya Singida United Hans Van De Pluijm.

Akizungumza kabka ya utiaji saini wa Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya Singida United Festo Sanga amesema kuwa mkataba huu wa mwaka mmoja utaizidi kmuimarisha timu yao katika masuala ya kifedha na zaidi wataendelea kuwakaribisha makampuni mengine kwa ajili ya kufanya nao kazi.

Sanga amesema kuwa, katika moja ya makubaliano yaop wameshapata shamba la ekari 10000 kwa ajili ya kilimo cha Mahindi na zitasimamiwa na kamouni ya YARA ikiwemo uwekezaji wa mazao hayo ndani na nje ya nchi.

Pia mbali na hilo, Singida United wameingua makubaliano ya kibiashara ya kusambaza bidhaa za YARA ndani ya nchi ikiwemo na kuzitangaza.

Kwa upande wa kampuni ya YARA,  Mkurugenzi Mkuu Alexander Macedo amesema kuwa wameamua kuidhamini timu ya Singida United kwani wameona ni timu nzuri na hata nembo ya timu yao ina ua la Alizeti ambalo linatumika sana kwa ajili ya utengenezaji mafuta hayo.

Macedo mwenyeji wa Brazili amesema watashirikiana na timu yya Singida ili waweze kuendeleza kilimo cha Mahindi nchini pampja na kuhakikisha wanawapatia wataalamu wazui wa soka kwa ajili ya mafunzo mbalimbali.
 Mkurugenzi Mkuu  wa kampuni ya YARA Alexander Macedo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya udhamini wa mwaka mmoja kwa timu ya Singida United wenye thamani ya kiasi cha Milioni 250.
  Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya Singida United Festo Sanga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya udhamini wa mwaka mmoja kwa timu ya Singida United wenye thamani ya kiasi cha Milioni 250.

Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya Singida United Festo Sanga  (kushoto) na  Mkurugenzi Mkuu  wa kampuni ya YARA Alexander Macedo wakitia saini karatasi ya makubaliano ya udhamini wa timu ya Singida wenye thamani ya Milioni 250.
Wachezaji wa Simgida United wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya YARA Alexande Macedo (kulia)
kocha mkuu wa timu ya Singida United Hans Van De Pluijm (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Singida United Festo Sanga wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya udhamini wa mwaka mmoja kwa timu ya Singida United wenye thamani ya kiasi cha Milioni 250.

Moses Matagili akabidhiwa Milioni 20 zake

$
0
0

WAENDESHAJI wa bahati nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, leo wamemkabidhi jumla ya Sh Milioni 20, mshindi wao wa droo ya 28, Moses Matagili, mkazi wa Goba, aliyetangazwa jana Jumatano, jijini Dar es Salaam.
oses Matagili mshindi wa Biko wa Milioni 20 mkazi wa Goba, katikati akipokea fedha zake kutoka kwa Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles kulia, huku akishuhudiwa na afisa wa NMB, tawi na Bank House, jijini Dar es Salaam leo mchana.

Matagili anakuwa mshindi wa droo ya 28 ya Biko, inayochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money kuanzia Sh 1,000 na kuendelea, huku namba ya kampuni ikiwa ni 505050 na kumbukumbu ni 2456.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha zake, Matagili anayejishughulisha na kazi za ujenzi wa nyumba, alisema amepokea ushindi wake kwa furaha, baada ya kuuwazia kwa muda mrefu na kuamua kuwa mchezaji mzuri wa Biko. Mshindi wa droo ya 28 ya Biko, Moses Matagili, kushoto akipokea fedha zake jumla ya Shilingi Milioni 20 kutoka kwa Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles kulia katika benki ya NMB leo jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa Biko wa Milioni 20, Moses Matagili akiwa anafurahia fedha zake saa chache baada ya kukabidhiwa leo katika benki ya NMB, jijini Dar es Salaam.

Alisema makabidhiano hayo ya fedha yamefanyika haraka, tofauti na matarajio yake, ikiwa ni siku moja baada ya kupigiwa simu ya ushindi na Balozi wa Biko, Kajala Masanja.

“Nashukuru kwa kushinda na kukabidhiwa fedha zangu mapema, nikiamini kuwa nitapiga hatua kubwa kiuchumi kwa namna moja ama nyingine, ukizingatia kuwa ndio matarajio yangu.

“Nawaomba Watanzania wote waendelee kucheza Biko mara nyingi zaidi na wasikate tamaa, kwa sababu kushinda kwangu kumeniongezea imani kubwa kwa waendeshaji wa Biko,” Alisema.

Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema Biko inaendelea kutoa fedha mbalimbali kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazolipwa papo hapo kupitia simu za washiriki waliocheza Biko.

“Biko tunaendelea kulipa fedha mbalimbali za papo kwa hapo pamoja na droo kubwa ya Jumatano na Jmapili ambayo ni Sh Milioni 20, kama tulizompa leo mshindi wetu wa Goba,” Alisema Melles huku akiwataka Watanzania waendelee kucheza Biko ili waibuke na zawadi mbalimbali.

Wakati mshindi huyo akipokea fedha zake, tayari mshindi wa droo ya 27, Viane Kundi, mkazi wa Iringa Mjini naye akiwa ameshapokea fedha zake Jumatatu iliyopita, huku pia mwezi Mei na Juni pekee Biko wakiwa wameshatoa zawadi zaidi ya Sh Bilioni moja.

MAKALA - MASWALI NA MAJIBU KUHUSU UTEUZI WA WABUNGE 8 WA VITI MAALUM WA CHAMA CHA CUF

NAIBU WAZIRI WA MALISILI NA UTALII,MHANDISI RAMO MAKANI AKUTANA NA WATUMISHI WA HIFADHI YA TAIFA YA MLIMA KILIMANJARO (KINAPA).

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akizungumza jambo wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Mtango Mtahiko akimueleza jambo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani wakati wa kikao cha uwasilishaji wa taarifa ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA).
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA) Betrita Loibook pamoja na Mhifadhi Ikolojia KINAPA,Iman Kikoti wakifanya maandalizi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA).
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibook akifanya uwasilishaji wa taarifa kuhusu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro kwa Naibu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani.
Madiwani kutoka kata mbalimbali za jimbo la Vunjo pamoja na Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia pia wameshiriki katika kikao hicho kilichofanyika makao makuu ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makini akifuatilia kwa makini uwasilishaji wa taarifa ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) uliokuwa ukifanywa na Mkuu wa Hifadhi hiyo Betrita Loibook.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Betrita Loibook akitoa ufafanuzi wa mambo kadhaa yaliyoulizwa wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA).
Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadi za Taifa (TANAPA) Mtango Mtahiko akitoa ufafanuzi na majawabu ya maswali yaliyoibuka wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA).
Mbunge wa Jimbo la Vunjo,James Mbatia ,akichangia jambo katika kikao hicho .
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akichangia jambo katika kikao hicho.
Mhifadi Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilmanjaro (KINAPA) Hobokela akieleza namna ambavyo Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA) inavyoshughulikia changamoto za wananchi wanaosihi kando ya hifadhi hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATEMBELEA BANDA LA COSTECH VIWANJA VYA NANENANE NGONGO MKOANI LINDI

$
0
0
Mtafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),  Bestina Daniel (kushoto), akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhandisi Mathew Mtigumwe (kulia), kuhusu ushiriki wa COSTECH katika maonyesho hayo, alipotembelea banda la COSTECH , lililopo chini ya Wizara hiyo katika Maonyesho ya Kitaifa ya Wakulima yanayoendelea Viwanja vya Nane Nane vya Ngongo mkoani Lindi jana.
Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Mikocheni (MARI), Ismail Ngolinda, akitoa maelezo Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhandisi Mathew Mtigumwe (kushoto), alipotembelea banda hilo. Katikati ni  Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, HusseinMansour.
Watafiti wakijadiliana jambo kwenye maonesho hayo. Kutoka kulia ni Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB), Filbert Nyinondi, Bestina Daniel, mdau wa kilimo, Flaviana, Dk. Emmarold Mneney, Ismail Ngolinda kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga Kilosa mkoani Morogoro na Christina Kidulile
Taswira ya banda hilo katika maonyesho hayo.

MAKALA ZIARA YA NAIBU WAZIRI DKT.KIGWANGALLA KATIKA SHULE YA MSINGI BUHANGIJA- SHINYANGA

IDARA YA UHAMIAJI:MGOMBEA URAIS WA TFF WALLACE KARIA NI RAIA HALALI WA TANZANIA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Idara ya Uhamiaji Nchini imethibitisha kuwa  Kaimu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Wallace John Karia ambaye ni Mgombea Urais wa TFF  katika uchaguzi unatarajia kufanyika August 12  mwaka huu ni Raia halali wa Tanzania.
 Akizungumza na waandishi habari leo makao makuu ya Idara ya Uhamiaji, Msemaji Mkuu wa Idara hiyo  Ally Mtanga amesema kuwa mmoja wa wagombea wa Urais wa TFF alimkatia rufaa mgombea mwenzake Wallace Karia kuwa si raia wa Tanzania .
 "Wallace Karia ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa chini ya kifungu cha 5(1) na (2) cha sheria ya uraia ya Tanzania sura ya 357(Rejeo la 2002) na kanuni zake, wakati huo huo akiwa raia wa Somalia kwa kurithi"
Mtanga amesisitiza  utambuzi wa uraia upo kisheria sura ya 357 (rejeo la 2002) uraia hauangaliwi Rangi, kabila wala dini.
 Idara hiyo imevitaka vilabu vyote na taasisi za michezo kuhakikisha wafanyakazi wote na wachezaji ambao raia wa kigeni wanatimiza taratibu zote za kisheria za kukaa nchini  bila kufanya hivyo sheria itashukua mkondo wake .
 Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanga akizungumza na waandishi wa habari juu ya utata wa mgombea Urais, Wallace Karia  leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanga leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

SERIKALI YAONGEZA UZALISHAJI KATIKA MAZAO MAKUU YA CHAKULA JAMBO LINALOPELEKEA KUJITOSHELEZA KWA CHAKULA NCHINI KWA ASILIMIA 100

$
0
0

Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe William Tate Ole Nasha (Mb) akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tizeba wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, jana tarehe 1/8/2017. (Picha zote na Mathias Canal)










Na Mathias Canal, Lindi

Serikali imeongeza uzalishaji katika mazao makuu ya chakula hususani mahindi, mchele, mtama, uwele, na mikunde jambo linalopelekea kujitosheleza kwa chakula kwa wastani wa asilimia 100. Aidha, Uzalishaji mwingine umeongezeka kwenye mazao ya jamii ya mizizi kama muhogo, ndizi, viazi vitamu na mviringo.

Hayo yamesemwa jana tarehe 01/08/2017 na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. Wiliam Tate Ole Nasha (Mb) wakati akizungumza na wakulima wadau wa kilimo Mifugo na Uvuvi na wananchi kwa ujumla wakati wa uzinduzi wa sikukuu ya wakulima – nane nane, Maonesho yenye kauli mbiu ya “Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati” yanayofanyika Kitaifa kwenye uwanja wa maonesho ya kilimo wa Ngongo Mkoani Lindi.

Alisema kuwa Katika mwaka 2015/2016 Sekta ya Kilimo ilichangia asilimia 29.1 ya Pato la Taifa ikilinganishwa na asilimia 29.0 mwaka 2014/2015. Mchango mkubwa katika Pato la Taifa ulitokana na Sekta ya Kilimo, ikifuatiwa na Sekta nyingine za kiuchumi.

Mchango huo mkubwa ni Kwa kuwa asilimia kubwa ya Watanzania wanashiriki katika shughuli za kilimo, hivyo kilimo kinachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza kipato na kupunguza umaskini.
Mhe Nasha Alisema kuwa uzalishaji wa mazao, mifugo na uvuvi umeimarisha zaidi usalama wa chakula na lishe nchini, ambapo katika mwaka 2015/2016 uzalishaji wa chakula ulikuwa ni tani milioni 16.2 ikiwa ni ongezeko la tani milioni 0.7 (sawa na 4.5%) ikilinganishwa na tani milioni 15.5 mwaka 2014/2015.

Uzalishaji wa mazao ya nafaka umeongezeka kutoka tani milioni 8.9 mwaka 2014/ 2015 hadi tani milioni 9.5 mwaka 2015/ 2016 ikiwa ni ongezeko la tani milioni 0.6 (sawa na 6.7%). Uzalishaji wa mahindi umeongezeka kutoka tani milioni 5.9 mwaka 2014/2015 hadi tani milioni 6.1 mwaka 2015/2016 sawa na ongezeko la tani milioni 0.2 (sawa na 3.4%). Uzalishaji wa mchele uliongezeka kutoka tani milioni 1.9 mwaka 2014/ 2015 hadi tani milioni 2.2 mwaka 2016 sawa na ongezeko la tani milioni 0.3 (sawa na 15.8%).

Vilevile, uzalishaji wa mazao ya chakula yasiyo nafaka umeongezeka hadi kufikia tani milioni 6.7 ikilinganishwa na tani milioni 6.6 kwa mwaka 2014/ 2015 ikiwa ni sawa na ongezeko la tani milioni 0.1 (sawa na 1.5%).

Kwa ujumla uzalishaji wa mazao ya chakula ukilinganishwa na mahitaji ya tani milioni 13.2 ya chakula na matumizi mengineyo katika mwaka 2016/2017 unaonesha kuwepo kwa ziada ya tani milioni 3.0 za chakula. Kutokana na hali hiyo Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa asilimia 123 ambayo ni ongezeko la asilimia 3 ikilinganishwa na asilimia 120 ya mwaka 2015.

Katika mwaka 2016/2017 idadi ya mifugo nchini imefikia ng’ombe milioni 28.44, mbuzi milioni 16.67 na kondoo milioni 5.01. Pia, wapo kuku wa asili milioni 37.43, kuku wa kisasa milioni 34.5, nguruwe milioni 1.85 na punda wapatao 572,357. jumla ya mitamba 634 ilizalishwa kutoka mashamba ya Serikali na Kampuni ya Ranchi za Taifa - NARCO ikilinganishwa na mitamba 646 iliyozalishwa mwaka 2015/2016. Aidha, jumla ya mitamba 10,820 ilizalishwa na Sekta binafsi na kusambazwa kwa wafugaji wadogo nchini ikilinganishwa na mitamba 10,803 iliyozalishwa mwaka 2015/2016.

Mhe Nasha alisema kuwa Vituo vya Kanda vimeendelea kuimarishwa kwa kupatiwa vitendeakazi, ukarabati wa miundombinu na mitambo ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya uhimilishaji wakati wote.

Jumla ya dozi 100,000 za mbegu bora za mifugo zilizalishwa ikilinganishwa na dozi 80,000 mwaka 2015/2016. Pia, ng’ombe waliohimilishwa wameongezeka kutoka 221,390 mwaka 2015/2016 hadi ng’ombe 457,557 mwaka 2016/2017.

Soga za Diaspora Episode 2


BOMBA LA MAFUTA TANGA: WANANCHI 365 KUFIDIWA CHONGOLEANI

$
0
0


Wananchi 365 wa kijiji cha Chongoleani watafidiwa shilingi bilioni 3,035 kwa ajili ya kutoa maeneo yao, ili kupisha ujenzi wa bomba la mafuta linalojengwa kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Tanga.

Hayo yamesemwa na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Usimamizi wa Bandari Tanzania TPATanga, Bibi Janeth Rwuzangi katika mahojiano maalum na  Idara ya Habari (MAELEZO) leo.

Bi Ruzangi amesema kuwa  kwa hapa Chongoleani mradi una ukubwa wa hekta 200 zikiwemo hekta 100 zitakazotumiwa kuweka miundombinu ya mafuta ghafi. Hekta 100 zilizosalia zitatumika kwa ajili ya shughuli za TPA) kuwekeza miundombinu ya kupokea mafuta yaliyosafishwa. Vile vile eneo hili limezingatia maendeleo endelevu ya biashara ya mafuta na gesi katika siku zijazo.

Aliongeza kuwa TPA itakuwa na wajibu wa kuhudumia meli, kuhakikisha usalama wa bidhaa, vyombo na watu pamoja na kusimamia masuala ya afya bandarini. Aidha, Majukumu la TPA yanatarijiwakujikita katika shughuli za uendeshaji wa majini ikiwemo kuwa na vyombo na boti maalumu kwa ajili ya kuongozea meli wakati wa kuingia na kutoka kwenye gati la mafuta ghafi.

Akitoa ufafanuzi, Bi Ruzangi amesema vile vile, TPA ina jukumu la kuhakikisha inahudumia shehena ya vifaa vyote vya ujenzi katika Bandari ya Tanga kwa kushirikiana na Bandari Kuu ya Dar es Salaam. Shughuli nyingine ni pamoja na ulinzi wa miundombinu ya majini pamoja na usalama wa eneo la Bandari ambalo limegawanyika katika sehemu kuu mbili; ardhini kwenye gati la mafuta na majini kwenye lango la kuingilia meli na nangani.

Kwa upande wa ajira za TPA Ruzangi amesemawafanyakazi ambao wataajiriwa ni pamoja na mabaharia, wahandisi, mafundi, wahasibu, wachumi, watakwimu, vibarua mbalimbali kwa ajili ya nguvu kazi n.k. Sehemu ya wafanyakazi hawa watatokana na waliopo sasa kwenye Bandari watakaopangiwa kazi hizo. Hata hivyo TPA inatarajia kuajiri wengine ambao watalazimika kufanya kazi hizo kulingana na taratibu za ajira za TPA.

Pamoja na kuwa na bomba la mafuta,  kijiji cha Chongoleani kitafaidika na ujenzi wa barabara ya kilometa 8 itakayounganisha bandari na barabara kuu ya Horohoro – Tanga, ambapo kwa kiasi kikubwa itainua uchumi wa wananchi wanaoishi maeneo hayo kusafirisha mazao, samaki na bidhaa nyingine kwa urahisi.

Akifafanua uwekaji wa jiwe la msingi Ruzangi amesemakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli na Mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wanatarajia kuweka jiwe la msingi la Mradi wa Bomba la Mafuta tarehe 05 Agosti 2017.

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Chongoleani, Bw. Mbwana Nondo amesema; “Kwa moyo wa dhati kabisa, naomba nimshukuru sana sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kwa kutujali wananchi wake na kutuletea neema ya Mradi wa Bomba la Mafuta, katika maisha yetu wanachongoleani, hatutaweza kumsahau kwa kizazi hiki kinachoshuhudia mradi huu na vizazi vijavyo”.
Nondo alisema kuwa anamuhakikishia Mhe. Rais kuwa  kuwa wote watakaopata fursa kwenye mradi wa Bomba la Mafuta, watafanyakazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa  kwa ujumla.
Bomba la Mafuta la kutoka Hoima Uganda mpaka Tanga Chongoleani lina urefu wa Kilometa 1445 ambapo kwa upande wa Tanzania itakuwa na jumla ya kilometa 1115 na Uganda  330. Aidha, Mradi utatarajia kusafirisha mapipa laki mbili na kumi na sita  elfu (216,000) kwa siku .

Kijiji cha Chongoleani ndio kituo cha mwisho ambapo mitambo mikubwa itasimikwa katika eneo hili kwa ajili ya kusukuma mafuta eneo la baharini ili,  kuweka kwenye vyombo vya usafirishaji kusafirisha maeneo mbalimbali duniani ambayo Uganda watakuwa wamepata soko.

Tanzania itafaidika na mradi huu kutokana na kodi, tozo na mrahaba  wa bomba la mafuta, itakayofanywa moja kwa moja na mradi huo. Faida nyingine ambazo, sio za moja kwa moja ni  ajira, fursa za kufanya biashara na uwezekano wa mikoa 8 ambayo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Morogoro na Tanga.


MWISHO

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA MSATA, KABUKU, HALE NA MUHEZA WAKATI AKIELEKEA TANGA MJINI LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mkata wakati alipokuwa njiani kuelekea mkoani Tanga kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Mkata waliosimama pembeni ya barabara kuu ya Chalinze- Segera (hawaonekani pichani) mara baada ya kumaliza kuhutubia katika kijiji cha Mkata mkoani Tanga.
Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Tanga akiwemo Wabunge na wakuu wa Wilaya wakipiga makofi wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia Mkata mkoani Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa waliosimama pembeni ya barabara kuu ya Chalinze Segera katika eneo la Kwa mkonga wakati akiwa njiani kuelekea Tanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Kabuku mara baada ya kumaliza kuwahutubia wakati akielekea mkoani Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Kabuku Handeni mkoani Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela kabla ya kuwahutubia wananchi wa Hale mkoani Tanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Hale mkoani Tanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja ya wakazi wa Hale mkoani Tanga mara baada ya kuhutubia katika eneo hilo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Hadija Juma mara baada ya kusoma ujumbe ulioandikwa kwenye sare aliyovaa mama huyo.

Wananchi wa Muheza wakimpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kufika katika eneo hilo la mjini akiwa njiani kuelekea Tanga. PICHA NA IKULU.

Vodacom yakabidhi vifaa kwa timu zinazoshiriki ligi kuu (VPL)

$
0
0
Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi(kulia) akimshuhudia Mwakilishi wa timu ya Yanga ambaye ni Afisa habari wa timu ya Simba, Haji Manara(kushoto) baada ya timu hiyo kukosa mwakilishi akimtania mmoja wa vijana aliyeitambulisha jezi ya Yanga itakayotumika katika msimu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2017/2018 wakati wa hafla iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ya  kukabidhi vifaa kwa timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura akipokea keki toka kwa Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi(kulia)kuashiria Uzinduzi wa msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,wakati wa hafla iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ya  kukabidhi vifaa kwa timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi(kulia)akimpongeza mmoja wa vijana aliyeitambulisha jezi ya Azam FC wakati wa hafla iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ya  kukabidhi vifaa kwa timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo jana jijini Dar es Salaam,Kutoka kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura na Mwakilishi wa Timu hiyo, Jafari Maganga.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura(kushoto)akiwashuhudia mwakilishi wa timu ya  Simba Afisa habari wa timu hiyo, Haji Manara(watatu kushoto)pamoja na Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi(kulia)wakiwapongeza vijana walioitambulisha jezi ya nyumbani na ugenini ya timu hiyo wakati wa hafla iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ya  kukabidhi vifaa kwa timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo jana jijini Dar es Salaam.

Timu zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom tanzania bara zimekabidhiwa vifaa mbalimbali na mdhamini mkuu wa ligi hiyo Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, vifaa hivyo vilivyokabidhiwa kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo vina thamani ya zaidi ya shilingi milioni 500/=

Akikabidhi vifaa hivyo jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa kampuni hiyo, Hisham Hendi, alisema kuwa  kwa mara nyingine tena katika kuhakikisha ligi ya soka nchini inaenda vizuri Vodacom inakabidhi  vifaa mbalimbali vya ligi ambavyo ni jezi mbalimbali, viatu vya mazoezi na mechi, soksi, vilinda ugoko, nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves, mabegi ya kusafiria, nguo za marefa, bendera, substitution boards  na vifaa vingine vingi vinavyohitajika. “Tunajisikia furaha  kukabidhi vifaa hivi siku ya leo tukiwa tunatekeleza  matakwa ya mkataba wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu zitakazoshiriki ligi zimejiandaa vya kutosha kwa msimu mpya wa ligi  wa 2017/2018”Alisema Hendi.

Hendi alisema Vodacom inaendelea kudhamini ligi kuu kwa sababu soka ni mchezo unaopendwa sana hapa nyumbani ukiwa na washabiki wengi hivyo inapenda kuona wananchi ambao baadhi yao ni wateja wake wanapata burudani ya mchezo waupendao pia siku zote inaamini kuwa michezo ni ajira kubwa duniani kote, ikiendelezwa inaweza kubadilisha maisha ya watu wengi na taifa kunufaika kwa mapato makubwa ya kodi kutoka katika sekta hii.

Aliwataka wadhamini wengine kujitokeza ili kuboresha  zaidi ligi ya Tanzania na kuongeza  maslahi kwa wachezaji wanaoshiriki katika ligi “Tukiunganisha nguvu timu zetu zinaweza kuwa na wachezaji wa kimataifa pia ni muhimu  kwa wadau mbalimbali kuanza kuwekeza katika timu za vijana chipukizi kwa kuwa vipaji vinaanzia ngazi ya chini ambako vinapaswa kuibuliwa na kuendelezwa ”Alisema Hendi.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi,Boniface Wambura aliishukuru hiyo,  na kuzitaka klabu zinazoshiriki ligi hiyo kuheshimu chapa ya mdhamini wakati wote wa mechi za ligi. “Ninatoa mwito kwa klabu zote kutumia jezi zenye nembo ya mdhamini mkuu katika kuhakikisha ligi inafanikiwa kama inavyotakiwa,”alisema.

Aliongeza kuwa  TFF isingependa kutumia kanuni na sheria kuadhibu klabu inayokwenda kinyume, bali kila klabu izingatie masharti ya mdhamini  kama ambavyo anavyotimiza haki yake ya kuwapatia vifaa.

Alisema ligi ya mwaka huu itakuwa bora kutokana na maandalizi yote  kukamilika mapema pia timu zitazoshiriki zimejiandaa vya kutosha kuhakikisha ligi inakuwa na msisimko na ushindani mkubwa.

KIJANA AELEZEA MKASA WA BABA YAKE MZAZI PAMOJA NA BIBI YAKE WALIVYOLIWA NA MAMBA

$
0
0
Kijana Emidio Nkoma mkazi wa kijiji cha Londo kilichopo Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma, Aelezea mkasa wa baba yake mzazi pamoja na bibi yake walivyoliwa na mamba katika Daraja la mto Rwika ambalo linaunganisha kijiji cha Londo na Ngido .

TMF NA HIVOS KENYA YAFUNGUA MAFUNZO YA MIEZI SITA YA NISHATI JADILIFU KWA WANAHABARI TANZANIA

$
0
0
 Muwezeshaji kutoka Tanzania Media Foundation Dustun Kamanzi akizungumza na Waandishi wa habari walioshiriki katika mafunzo ya uandishi Nishati Jadilifu
  Mwandishi Mwandamizi Alan Lawa  akizungumza jambo wakati wa majadala uliokuwa ukiendelea katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na TMF na Hivos Kenya
 Muwakilishi wa Hivos Kenya , Maimuna Kabatesi akizungumza juu ya Hivos  Kenya katika kusaidia masuala ya mabadiliko ya Tabia nchi
 Waandishi  walioshirikikatika mafunzo hayo wakijadili jambo wakati wa kazi za makundi.
 Mjumbe wa bodi ya Terea Godwin Msigwa akiwa pamoja mwandishi wa DW Hawa Biolga wakati wa ufundishaji wa makundi katika mafunzo hayo
 Waandishi  walioshirikikatika mafunzo hayo wakijadili jambo wakati wa kazi za makundi

Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images