Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46200 articles
Browse latest View live

Vito vya Thamani vyapitishwa kimagendo Rukwa

0
0

RC Rukwa Amezionya Halmashauri Dhidi ya Matumizi Mabovu ya Mashine za EFD

0
0


RC Rukwa  Mh. Zelote Stephen akiwaonesha waheshimiwa madiwani   (hawapo pichani)risiti ambazo tayari zimeshakatwa kabla ya kutumiwa. 
P_20170731_160828_vHDR_Auto
RC Rukwa akiwaonesha waheshimiwa madiwani   (hawapo pichani) kitabu cha hoja za mthibiti na mkaguzi wa serikali kwa  Manispaa ya Sumbawanga.
P_20170731_162142_vHDR_Auto
RC Rukwa akitoa ufafanuzi. 
…………………………….
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amezionya halmashauri zote mkoani Rukwa kuhakikisha wanazitumia vizuri manshine za EFD kwa kuongeza mapato katika halmashauri zao.

Ametoa onyo hilo kwenye kikao maalum cha kujibu hoja za ukaguzi wa hesabu za serikali kwa madiwani wa  Manispaa ya Sumbawanga katika kumalizia ziara yake maalum kwa halmashauri zote mkoani humo kujua namna Halmashauri zilivyojipanga ili hoja hizo zisijirudie miaka inayofuata.  
Akiongea huku akionesha risiti alizozikamata katika maeneo mbalimbali ya mauzo alisema kuwa serikali inafanya kila liwezalo katika kuhakikisha inakusanya maopato lakini bado kuna watumishi wanatafuta namna ya kuiskosesha serikali mapato hayo.

“katika kila sehemu za mauzo lazima mashine hizi ziwepo na kuwepo sio mtindo huu (akionesha msururu wa risiti zilizokatwa tayari kwa matumizi) hizi nimezikamata maeneo anajua Mkurugenzi, asubuhi watu wanagawana, ndio mchezo uliopo, pamoja na jitihada tunazofanya bado watu wanatafuta mbinu za kuiba, hii sio kwamba nimeleta iwe mfano, hapana, nimezikamata na mfahamu kuwa mimi ni mtaalamu wa kukamata,”Alisema

Katika Kusisitiza suala la uwazi wa matumizi ya fedha za halmashauri kwa waheshimiwa madiwani Mh. Zelote alitaja majukumu kadhaa ya Mkurugenzi wa Halmashauri na kusema kuwa moja ya kazi za Mkurugenzi ni kuhakikisha kuwa madiwani wanapata taarifa za fedha za halmashauri.
“Hapa mmezungumza na mmenionyesha kwa kiasi kikubwa kwamba hamnazo taarifa na nikiangalia kazi moja wapo ya waheshimkwa madiwani ni kiusimamia matumizi ya fedha za halmashauri zao sasa mtasimamiaje ikiwa hamna taarifa,” Alisema.

Na kukumbusha kuwa Mkurugenzi ndio katibu wa kamati ya fedha ya halmashauri lakini na kuonya kuwa kamati hiyo ibebe sura ya halmashauri na sio sura ya kamati na kuwasisitiza kufuata taratibu nyingine za ikiwa kurudisha mrejesho kwa wengine juu ya mipango na maazimio yaliyofikiwa.
Katika kikao hicho Mh. Zelote alimtambulisha mtaalamu wa TEHAMA ili awaelezee waheshimiwa madiwani namna mifumo ya fedha inavyofanya kazi ili nao wawe na uelewa mpana katika kufuatilia mapato na matumizi ya halmashauri.

“Suala la kukusanya mapato limekuwa likiimbwa asubuhi, mchana na usiku, kuwa tuhakikishe tunajipanga vyema kukusanya mapato ya halmashauri kwa kupitia utaratibu uliopo, suala la kutumia hizi mashine sio la kuhoji tena mwisho ulikuwa mwezi wa tatu ndio agizo lililopo kwa wakurugenzi kuwa mashine hizi ziwepo na zinafanya kazi,” Alisema.

Na katika kuhakikisha kuwa vitabu hivyo havipati nafasi Mh. Zelote alitoa siku saba vitabu hivyo kurudishwa maghalani na kuongeza kuwa watumishi wanaokiuka miiko ya kazi zao kuwajibishwa kulingana na madhara waliyosababisha na kuwaasa kujenga uaminifu katika utumishi ndani ya halmashauri.

“Sitaki kusikia tena kuwa kwenye mkoa wangu kuna halmashauri inanyooshewa kidole, mmeshanyooshewa kidole mara moja sitaki kuona tena hicho kidole,” alimalizia.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya nSumbawanga Mh. Julieth Binyura alishanngazwa na wataalamu hao kushindwa kudhiti hoja na hatimae wao kuwa chanzo kikuu cha kuzalisha hoja.

“Mtu kama unaitwa mtaalamu na serikali imekuamini kwanini tena unaizalishia serikali hoja, na suala la fedha ni suala nyeti sana hivyo linahitaji umakini wa haloi ya juu ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma inayostahili na si vinguinevyo,” Alisema.

Akifunga kikao hicho Mstahiki meya wa Manispaa ya Sumbwanga Mh. Justin Malisawa alimuahidi Mkuu wa Mkoa kusimamia yale yote aliyoyaelekeza na kuomba msaada wake pindi pale watakapokwama. 

NAIBU WAZIRI WA MALISILI NA UTALII,MHANDISI RAMO MAKANI AZUNGUMZA NA WAKAZI WA KIJIJI CHA MSHIRI WILAYANI MOSHI KUHUSU ENEO LA NUSU MAILI

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kippi Warioba akiongozana na Naibu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani walipotembelea kijiji cha Mshiri katika wilaya ya Moshi kusikiliza Changamoto zinazo wakabili wananchi waishio kando ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro .
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akiwa na Mbunge wa Jimbo la Vunjo,James Mbatia katika mkutano wa wananchi katka kijiji cha Mshiri wilayani Moshi uliohusu Zaidi changamoto iliyopo katika eneo la Nusu Maili katka Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro .
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Mshiri wilayani Moshi waishio kando ya Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro waliofika kwa ajili ya kumueleza Naibu Waziri wa Malisli na Utalii,Mhandisi Ramo Makani changamoto zinazowakabili hususani eneo la Nusu Maili.
Niabu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mshiri wilayani Moshi ,alipotembelea kijiji hicho kusikiliza Changamoto zinazo wakabili hususani katika eneo la Nusu Maili lililopo chini ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Mshiri wilayani Moshi wakimsikiiza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani (Haupo pichani ) alipozungumza nao.
Mbunge wa jimbo la Vunjo ilipo kijiji cha Mshiri ,James Mbatia akizungumza katika mkutano huo kuhusu Changaoto mbalimbali zinazowakabili wananchi kaika kijiji hicho.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mshiri wilani Moshi.
Mku wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba akizungumza katika mkutano huo.
Baadhi ya viongozi kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) walioongozana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani kutembelea kijiji cha Mshiri,kutoka kulia ni Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete,Meneja Utalii wa Tanapa.Bw Manase na Mhifadhi Ujirani Mwema KINAPA,Bi Hobokela Mwamjengwa.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifdhi za Taifa (TANAPA) Mtango Mtahiko akiwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibook katika mkutano wa Naibu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani na wananchi katika kijiji cha Mshiri.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi wa TANAPA,Mtango Mtahiko akitoa salamu katika mkutano huo.
Baadhi ya Wananchi katika kijiji cha Mshiri.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibook akizungumza jambo katika mkutano huo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini

The first leg of the 2017 Seeds for the Future program in China kicked off.

0
0
The first leg of the 2017 Seeds for the Future program in China kicked off.
Beijing, 31 July, 2017: The best 10 ICT students, who were selected to join the second phase of the Seeds for the Future program from Tanzania, have started their first leg of their study trip in Beijing, China.

Apart from having a well designated cultural training that have started this Monday, the Tanzanian’s university students had an opportunity to visit various tourist attractions in the Beijing Capital such as Forbidden City and Great Wall and experience Chinese traditional and cultural things.

During their trip in Beijing, students also have started their language and cultural training program, the session will be one of its kind designated to help them learn more about Chinese culture and gain cross-cultural work experience in a global business environment.

Speaking during the tour at the Great Wall of China, one of the students Ms Inviolata Rimisho, student from University of Dodoma (UDOM) said it was a really great experience to climb up the Great Wall. Despite the high temperatures and the large crowd students enjoyed the day.

She said the Great Wall of China is one of the greatest sights in the world. It’s an ancient defensive architecture in the Chinese kingdom.

“This historic preservation of a country like the Great Wall tells the story of its past and make the country distinct from other countries. I would like to urge Tanzania to a preserve well the physical reminders of our past because they create a sense of place and a country’s pride. They also provide economic benefit through tourist activities,” she said.

Historically, the Great Wall of China is a series of fortifications made of stone, brick, tamped earth, wood and other materials, generally built along an east-to-west line across the historical northern borders of China to protect the Chinese states and empires against the raids and invasions of the various nomadic groups of the Eurasian Steppe.

Ms Rimisho said through this training opportunity they had received, they will learn more about the culture and experience traditional culture of the Chinese people as well as to get knowledge from the advanced world while they are in Shenzhen at Huawei headquarter.

Another UDOM student, Mr Anatory Mcharo said “I am one of the participants of the 2017 ‘Seeds for the Future’ program and on my first day I visited the Forbidden City. It was extremely great to visit the Forbidden City, as our tour guide provided us with information on it.

He said that this city is a China museum of the Imperial Royal Palace of the Ming and Qing dynasties which was built in 1420 AD about 600 years ago, after being home to twenty-four emperors, fourteen of the Ming Dynasty and ten of the Qing Dynasty, the Forbidden City ceased to be the political Centre of China in 1912 and it was declared a world cultural heritage by UNESCO in 1987.
 
“It was very interesting to walk through the Forbidden City. It was really crowded but I enjoyed the visit as I saw various building, structures and artifacts of 600 years ago being nicely and clearly visible,” he said.

Mcharo further said that the preservation of cultural heritage is a challenge in many part of the world but here in china they saw a very unique attitude in preservation the cultural heritage.

“Despite various challenges the Forbidden City encountered from when it was started to be used as a museum which include Japanese invasion, destruction of the throne in the Harmony hall, the Chinese authority has with greater success preserved this cultural heritage,” he said. 

Adding “I would like to urge my beloved country Tanzania to impart such an altitude to its authorities in order to preserve our cultural heritage for the benefit of present and future generation.”

Through the Seeds for the Future program, each year Huawei provide opportunity for Tanzania students to explore all beautiful Chinese palatial architecture and through this it had influence us to encourage our country and the government at large to preserve and develop our cultural and architectural in our nation and elsewhere.

This year, Huawei had offered 2-week educational experience, language training, exposure to Chinese culture and the experience of processes in Huawei’s dynamic global business environment in China.

Gazeti la Mwanahalisi latakiwa kuiomba radhi Tume ya Taifa ya Uchaguzi

0
0

Waziri Jenista Mhagama akutana na Balozi wa Vietnam Bw. Nguyen Kim Doanh

0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira  na Watu Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na Balozi wa Vietnam Bw. Nguyen Kim Doanh kuhusu ushirikiano baina ya nchi ya Vietnam na Tanzania ofisini kwake, Jijini Dar es Salaam Agosti 2, 2017. Kulia ni Msaidizi wa Balozi Bw. Ton Ho Tri Dzung. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Kazi, Vijana Ajira na Watu Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama (Mb) akisisitiza jambo pamoja na Balozi wa Vietnam Bw. Nguyen Kim Doanh ofisini kwake, Jijini Dar es Salaam Agosti 2, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Vietnam Bw. Nguyen Kim Doanh baada ya mazungumzo yao, ofisini kwake Jijini Dar es Salaam Agosti 2, 2017.

VETA NA AIRTEL YATHIBITISHA KUHUDUMIA WANAOTAKA KUJIFUNZA UFUNDI WALIKO

0
0
 Afisa Matukio wa Airtel Tanzania akikabidhi simu maalum zitakazotumika kuendesha mradi wa VSOMO kwa Msajili Mkuu Veta Kipawa(Registry), Bw,   Harold Mganga, (kushoto), akishuhudiwa na Mratibu wa Miradi na Kozi fupi. (Project and Short Course Coordinator)Veta Kipawa Gosbert Kakiziba (katikati) simu hizo zimetolewa kwa  kwaajili  ya mradi wa VSOMO. VSOMO ni applikesheni maalum inayotoa mafunzo ya ufundi stadi ya VETA kwa njia ya mtandao inayodhaminiwa na Airtel Tanzania.
Afisa Matukio wa Airtel Dangio Kaniki (kulia) akimuonyesha applikesheni ya VSOMO  Mkuu wa Usajili Veta Kipawa (Registry) Bw,   Harold Mganga  (katikati) pamoja na Mratibu wa Miradi na Kozi fupi. (Project and Short Course Coordinator) Veta Kipaw bw, Gosbert Kakiziba (kulia).  hafla fupi ya makabidhiano ya simu hizo yaliyofanyika  Veta Kipawa. Aplikesheni ya VSOMO inatoa mafunzo ya ufundi stadi ya VETA kwa njia ya mtandao inayodhaminiwa na Airtel Tanzania.

Mamlaka ya elimu ya ufundi Tanzania (VETA) kwa kupitia mfumo wa mafunzo kwa mtandao wa VSOMO unaodhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imebainisha kuwa iko tayari kuhudumia vikundi au jamii ya wanaotaka kujifunza ufundi stadi kwa kupeleka timu yao ya mafunzo kwa vitendo popote ili kuhakikisha dhana ya uchumi wa viwanda inakamilika kwa kuwa na mafundi wazuri waliohitimu ufundi katika chuo maalumu nchini

Hayo yamebainishwa na mkuu wa chuo cha veta kipawa ambae pia ni msimamizi wa mradi wa mafunzo kwa njia ya simu unaodhaminiwa a Airtel kwa lengo la kutoa FURSA kwa vijana wegi mjini kupata ujuzi na kujiajiri Mhandisi Lucius Luteganya.

VETA tuko tayari kuwafuata wanafunzi wetu endapo watajiandikisha na kuhamasihana kwa kikundi kusoma kwa njia ya mtandao wa VSOMO , ikiwa watakuwa vijana kuanzia 15-20 na wakipenda kupata mafunzo waliko basi sisi tutawafuata waliko ili kuhakikisha wanahudumiwa na mobile trainers wetu”

“sasa hivi kupitia mtandao wa Vsomo tunakozi 12, wanafunzi wanaweza wakajisomea wawapo popote mara baada ya kupakua App yetu ya VSOMO na kulipia kozi anayotaka” alisisitiza Luteganya.

Eng Luteganja alitaja kozi hizo kuwa ni “Tunampango waongeza kozi zingine 15 hivi karibuni lakini kwa sasa zilizopo tayari kwenye mtandao ni Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo ya kompyuta, umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani , Umeme wa magari, Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi wa simu za mkononi, Ufundi Alluminium, Utaalamu wa maswala ya urembo pamoja ma Ufundi wa kuchomea vyuma.

Tangu VETA na Airtel walipozindua mfumo huu wa mafunzo kwa njia ya mtandao waVSOMO mwezi wa Juni 2016 Mfumo huu wa VSOMO sasani umepata umaarufu mkubwa kwa vijana ambapo takwimu zinaonyesha zaidi ya vijana 30,000 tayari wamepakua application ya VSOMO, 8000 wamejiandikisha na kati yao 50 wameshasoma kozi mbalimbali na kupata vyeti vyao vya ufundi stadi kutoka VETA.

kujiandikisha katika mojawapo ya kozi 12 zinazopatikana katika application ya VSOMO mwanafunzi atalipia kwa simu yake gharama ndogo ya shilingi 120,000 tu kupitia huduma ya Airtel Money kwa kupiga *150*60#. na kufanya malipo ambazo gharama hizi zitamuwezesha kuja kupata mafunzo kwa vitendo bila malipo ya ziada.

Vitu ambavyo hauruhusiwi kusafiri navyo kwenye ndege

0
0

Na Jumia Travel Tanzania

Kama umeshawahi kusafiri kwa ndege naamini utakuwa unafahamu ni kitu gani cha kubeba kwenye begi lako na kipi sio. Endapo haujawahi au unatarajia kufanya hivyo kwa siku za hivi karibuni basi usafiri huo una masharti na taratibu zake ambazo ni lazima zifuatwe vinginevyo hautoweza kuutumia.

Tofauti na usafiri wa kawaida kama vile mabasi ambayo watanzania wengi tunayatumia ambapo ni mara chache kukuta kunakuwa na upekuzi mkali wa abiria mbali na tiketi zao, Jumia Travel ingependa kukufahamisha kwamba kusafiri kwa kutumia ndege kuna masharti na taratibu ambazo kila abiria ni lazima azifuate na kuzizingatia ndipo aruhusiwe kuingia ndani.  

Vifaa vyenye ncha kali. Hairuhusiwi kabisa kubeba vitu vyenye ncha kali kama vile kisu, wembe, mkasi, bisibisi au panga kwenye begi lako la kusafiria labda iwe kwenye mzigo tofauti ambao utapekuliwa na kupewa kibali. Kwa ufupi kama unadhani utahitajika kuvibeba ni vema kuviweka kwenye mzigo tofauti ili vifanyiwe upekuzi ndipo uruhusiwe. Tofauti na hapo ili kuepuka usumbufu au kuchelewa safari yako basi unashauriwa kuwasiliana mapema na shirika la ndege utakalosafiri nalo kwa msaada zaidi.      

Silaha za moto. Hakuna silaha inayoruhusiwa kubebwa kwenye begi lako la kusafiria kwa sababu za usalama wako na abiria wengine kwenye ndege. Ingawa taratibu hutofautiana baina ya nchi au mashirika ya ndege lakini asilimia kubwa vitu hivyo huwa haviruhisiwi kabisa labda kuwa na sababu na kibali maalumu.   

Vitu vinavyoweza kulipuka. Kuna baadhi ya bidhaa tunazitumia ambazo ndani yake zina kemikali ambazo hulipuka kwa urahisi bila ya kujua. Kwa mfano, takribani marashi yote ya kujipulizia mwilini (body spray) au vibiriti vya gesi huwa na kemikali ambazo zinaweza kulipuka kwa urahisi na ndiyo maana huwekwa alama ya moto (inflamable). Hivyo basi ni vema kulijua hilo ili unaposafiri usibebe maana utaishia kwenda kuyaacha mahala pa ukaguzi kabla ya kupanda ndege.

Vifaa vya michezo. Kuna baadhi ya vifaa vya michezo vinachukuliwa kama silaha. Kwa mfano, vifaa vya kuchezea gofu, tenesi, mpira wa magongo, upinde na mkuki na kadhalika. Kwa mfano, timu nyingi za michezo mbalimbali zinaposafiri vifaa hivi huwekwa kwenye mizigo tofauti na ile ya wachezaji kwa ajili ya ukaguzi ili kuepusha usumbufu.

Vifaa vya kazi. Inawezekana ukawa ni fundi mzuri na una wateja takribani kila kona ya nchi hivyo ukahitajika kusafiri kwenda kufanya kazi. Itakuwa ni jambo la busara ukafahamu mapema kwamba kusafiri kwenye begi lako na vifaa vyako vya kazi kama vile nyundo, msumeno, patasi au bisibisi itakuwa ngumu. Utaweza kufanya hivyo pale tu utakapovifungasha kwenye mzigo wake tofauti ili ukaguliwe kwa ajili ya usalama wako.   

Dawa za binadamu. Kuna wakati unaweza ukawa na matatizo ya kiafya lakini ukahitajika kusafiri hivyo ni vema kujua pia kuna taratibu za kusafiri na dawa zako za matibabu. Iwe unasafiri ndani au nje ya nchi vitu muhimu vya kuzingatia ni pamoja na barua au maelezo ya daktari kuhusu ugonjwa wako pamoja na dawa alizopendekeza kuzitumia na kubeba. Kwa hiyo ili kuepuka kuzuiwa kusafiri na dawa wakati mwingine itakuwa vizuri hata ukawasiliana na shirika la ndege utalosafiri nalo ili ujue taratibu zao zikoje.

Vimiminika. Unaweza ukashangaa kwanini hautoruhusiwa kusafiri na maji yako ya kunywa ambayo umeyabeba kwenye begi lako. Ingawa sheria hutofautiana kwa baadhi ya nchi ambazo huruhusu kiwango fulani kwa hapa Tanzania hali ni tofauti. kwenye kundi hili maziwa ya chupa na madawa hayaingii kwenye kundi hili ingawa ni lazima yaambatinishwe na maelezo au kibali maalum.     

Bangi. Nadhani hili linaeleweka miongoni mwa watu wengi kwamba Tanzania kilevi hicho ni marufuku kukitumia kwa hiyo kukutwa nacho tu ni uvunjaji wa sheria. Kuna baadhi ya nchi zinaruhusu aina ya kilevi hicho kana kwamba mpaka madaktari hutoa vibali kabisa kwa wagonjwa wao kutumia. Ila kwa nchi ya Tanzania bangi ni marufuku na ukikutwa nayo utachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa kawaida mtu wa kawaida anaposafiri kwa kutumia ndege kunakuwa hakuna vitu vingi vya kuhofia kwani ni mara chache vitu hivyo huhitajika kubebwa. Mbali na hapo utajitafutia matatizo au kuhatarisha usalama wa abiria wenzako. Jumia Travel imeona ni vema kukutahadhirisha kwamba kutokana na kuongezeka kwa matukio ya kutishia usalama kupitia usafiri huo, hatua kali zimekuwa zikichukuliwa na nchi mbalimbali duniani.



RAIS DKT MAGUFULI AWAPANDISHA NA KUWATEUA MAAFISA WAWILI WA ZIMAMOTO KUWA MAKAMISHNA

0
0

MTANDAO WA ELIMU TANZANIA, (TenMet), WAKUTANA NA BLOGGERS JIJINI DARES SALAAM

0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said.
BINADAMU ili aweze kuyakabili mazingira yake, moja ya nyenzo muhimu ni elimu, na kwa kutambua umuhimu wa elimu, wadau mbalimbali wamekuwa wakifanya juhudi kubwa katika kusaidiana na serikali ili kufikia lengo la kuwapatia elimu Wananchi wa Tanzania.
Mtandao wa Elimu Tanzania, kwa kifupi TenMet, ni moja ya taasisi zinazifanywa juhudi kub wa katika kuhakikisha malengo yaliyotajwa hapo juu yanafikiwa.
TenMet ambayo iliasisiwa miaka 18 iliyopita ikiunganisha taasisi nyingine 39 wakati huo, kwa sasa mtandao huo umepanuka na kufikia jumla ya taasisi 181 zilizojikita katika swala la kuhakikisha watanzania wanapatiwa haki yao ya elimu, lakini sio tu kupatiwa elimu bali pia elimu iliyo bora.
Ili kufikisha ujumbe kwa wahusika (jamii) TenMet hufikisha ujumbe kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na makongamano, semina na vyombo vya habari vikiwemo vile vya kisasa (social media kama vile Blogs).
Agosti 2, 2017, Maafisa wa TenMet waliwaalika bloggers ili kuangalia namna gani wanavyoweza kushirikiana katika kutekeleza malengo yaliyoanishwa hapo juu ya kusambaza taarifa mbalimbali zinazohusu masuala ya elimu.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Meneja Programu wa TenMet, Bw.Nicodemus Shauri Eatlawe, alisema, lengo la mkutano huo ni kuimarisha ushirikiano wa kikazi baina ya taasisi yake na vyombo vya habari vya kimtandao kwani anaamini taarifa zitawafikia wadau wengi zaidi.

“Lakini pia tunaamini ushirikiano huu utatusaidia katika kuibua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu nchini, kwa kuhabarisha umma, hivyo tunayo furaha kubwa kukutana nanyi leo hii.”Alifafanua.
Kwa upande wake, Afisa Programu wa TenMet, Bi. Alistidia Kamugisha, amefafanua kuwa, TenMet kama ambavyo malengo yake yalivyoainishwa, imekuwa ikifanya tafiti mbalimbali kuhusu elimu hapa nchini, lakini pia kwa kushirikiana na taassi nyingine za kimataifa ikiwa ni pamoja na kuratibu mikutano, maonesho na semina kuhusu masuala ya elimu.
Afisa Programu wa Mtandao wa Elimu Tanzania, (TenMet), Bi. Alistidia Kamugisha, akizungumza wakati wa kikao cha kujenga ushirikiano baina ya taasisi hiyo na Bloggers kilichofanyika makao makuu ya TenMet, Sinza jijini Dar es Salaam, leo Agosti 2, 2017.
Meneja Programu wa TenMet, Bw.Nicodemus Shauri Eatlawe, (katikati), akifafanua jambo wakati wa kikao hicho. Kulia ni Bi. Alistidia Kamugisha, na Afisa Programu wa taasisi hiyo, Bw. David Sizya.
 Mmoja wa washiriki wa kikao hicho, akitoa maoni yake.
 Afisa wa TenMet, Bw. Dominic Dogani, akitoa ufafanuaiz wa masuala mbalimbali yatakayojadiliwa kwenye kikao hicho.
 Majadiliano yakiendelea.

 Mmoja wa washiriki wa kikao akitoa maoni yake.
 Baadhi ya washiriki wa kikao hicho wakinakili yaliyokuwa yakijadiliwa kupitia vitendea kazi vyao.
 Mwenyekiti wa Mtandao wa Bloggers Tanzania, (TBN), Bw. Joachim Mushi, akiwa makini na yaliyokuwa yakijadiliwa.
 Mmiliki wa blog ya Jiachie, Bw. Ahmad Michuzi (kulia) akifuatilia mjadala. Kushoto ni Bw. Mushi.
 Bi. Kamugisha akiweka sawa vitabu vyenye taarifa za TenMet.
 Bw. Sizya, (kulia), akimpatia nakala ya vitabu vya TenMet mwandishi wa Mo Blog, Bw. Rabif Humwe.
Picha ya pamoja

Milioni 20 za Biko zamfikia Moses Matagili wa Goba

0
0

BAHATI Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, droo ya 28 imefanyika leo, huku mkazi wa Goba, jijini Dar es Salaam, Moses Matagili, akifanikiwa kuibuka kidedea kwa kushinda Sh Milioni 20.
Kajala Masanja Balozi wa Biko Tanzania.
Droo hiyo iliyofanyika jana, ilichezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa kushirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo.

Akizungumza baada ya kumpata mshindi huyo, Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema sasa ni wakati wa kuchangamkia fursa ya kuibuka na mamilioni kwa kucheza Biko inayotoa ushindi wenye fursa ya kiuchumi.

Alisema kwamba droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 20 inafanyika Jumatano na Jumapili, huku Jumatano hii ikienda kwa Matagili, ambaye ni mkazi wa Goba, sanjari na washiriki kuvuna zawadi mbalimbali za fedha taslimu kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja.

“Tunampongeza mshindi wetu wa droo ya 28, Matagili kwa kuvuna donge nono la Sh Milioni 20 kutoka Biko, hivyo tunawaomba Watanzania wengine waendelee kucheza Biko ili waweze kujipatia zawadi mbalimbali kutoka kwetu.

“Jinsi ya kucheza ni rahisi maana bahati nasibu yetu inachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, Mpesa na Airtel Money, ambapo namba yetu ya kampuni ni 505050 na kumbukumbu ni 2456,”Alisema.

Naye mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo, alisema mchezo wa Biko unachezwa kwa kufuata sheria zilizowekwa, jambo linaloongeza ufanisi kwa Watanzania wote kucheza na kushinda zawadi za Biko.

“Tunawakumbusha Watanzania kuwa Biko ni mchezo rahisi na ambao unachezeshwa kwa uangalizi mkubwa wa bodi yetu, hivyo kwa wale wanaocheza waelewe kuwa huu ni mhcezo salama,” Alisema.

Wakati Matagili akiibuka kidedea kwa kuzoa Sh Milioni 20 kutoka Biko huku akitarajiwakukabidhiwa fedha zake mapema iwezekanavyo, tayari mshindi wa droo ya 27, Viane Kundi wa Irnga, akiwa ameshapokea fedha zake Jumatatu iliyopita.




RAIS DKT MAGUFULI ATOA POLE KATIKA MSIBA WA MHADHIRI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM DKT STEPHEN JUMA MDACHI

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapa pole wana familia wa Marehemu Dkt. Stephen Juma Mdachi aliyefariki Jumanne Agosti 1, 2017 katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Marehemu ambaye alikuwa ni mhadhiri katikl idara ya Kemia, ameacha mjane na watoto watatu.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapa pole wana 
familia wa Marehemu Dkt. Stephen Juma Mdachi aliyefariki Jumanne Agosti 1, 2017 katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Marehemu ambaye alikuwa ni mhadhiri katikl idara ya Kemia, ameacha mjane na watoto watatu.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapa pole wana 
familia wa Marehemu Dkt. Stephen Juma Mdachi aliyefariki Jumanne Agosti 1, 2017 katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Marehemu ambaye alikuwa ni mhadhiri katikl idara ya Kemia, ameacha mjane na watoto watatu.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka sini katika kitabu cha maombolezi nyumbani kwa Marehemu Dkt. Stephen Juma Mdachi aliyefariki Jumanne Agosti 1, 2017 katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Marehemu ambaye alikuwa ni mhadhiri katikl idara ya Kemia, ameacha mjane na watoto watatu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji Mama Mary Mdachi, mjane wa Marehemu  Dkt. Stephen Juma Mdachi aliyefariki Jumanne Agosti 1, 2017 katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Picha na IKULU

Benki ya FINCA Microfinance yazindua kampeni ya FikaNaFINCA

0
0

Meneja wa Masoko wa Benki ya Finca Microfinance Bw. Nicholous John, Benki ya FINCA Microfinance Bwana Nicholous John akionyesha mfano wa tiketi ya ndege itakayotumika katika kampeni yao iliyopewa jina la FikaNaFINCA iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Afisa Mawasiliano wa Shirika la ndege la Tanzania ATCL Bi. Lilian Fungamtama

Kutoka kushoto ni Meneja usafirishaji wa kampuni ya Super Feo Bw Masumbuko akifuatiwa na Meneja wa Masoko wa Benki ya Finca Microfinance Bw. Nicholous John, Afisa Mawasiliano wa Shirika la ndege la Tanzania ATCL Bi. Lilian Fungamtama Bi. Lilian Fungamtama na Mtaalamu wa Masoko wa Benki ya FINCA Bw. Noel Mulumba wakionyesha mifano ya tiketi za usafirishaji ambazo wateja watapaswa kupiga picha na kushirikisha wafuasi wako katika mitandao ya kijamii ili kujishindia tiketi ya bure katika kampeni iliyopewa jina la FikanaFINCA


Moja ya Benki inayokua kwa kasi nchini, Benki ya FINCA Microfinance, leo imetangaza kampeni ya miezi miwili inayofahamika kama 'FikaNaFINCA' Kampeni hii itampa fursa anayefwatilia kurasa za kijamii ya benki hiyo nafasi ya kujishindia tiketi ya kwenda na kurudi bure baada ya kuposti picha ya bahasha ya tiketi yenye nembo ya FIKA NA FINCA na pia kupendwa na watu wengi.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari katika makao makuu ya benki jijini Dar es Salaam, Meneja wa Masoko wa Benki ya Finca Microfinance, Nicholus John alisema kuwa washindi watakuwa na nafasi ya kupata tiketi za usafiri wa anga na barabara ya kwenda na kurudi kutoka mashirika ya usafiri wa anga ya ndani ya Air Tanzania (ATCL) na Auric Air na pia kwa mabasi yanayoenda bara yakiwemo mabasi ya kampuni za Ngorika, New Force na Isamilo.

"FINCA inathamini wateja wake na jamii kwa ujumla, katika kuonyesha hilo, ndo maana tumeleta kampeni hii itakayoenda kwa miezi miwili huku mshindi kutangazwa kila wiki. Jinsi ya kushinda ni rahisi sana, piga picha tiketi yako yenye nembo ya FIKA NA FINCA, posti kwenye kurasa ya Facebook na Instagram ukiweka #FikaNaFINCA kwenye caption, alafu aalike ndugu jamaa na marafiki kuipenda."alisema John.

John aliongeza: "Ninatoa wito kwa Watanzania kuchukua fursa hii ya kipekee na kushiriki kwa wingi ili kushinda ofa hii ya kusafiri bure".

Kwa upande wao, Air Tanzania, Lilian Fungamtama ambaye ni Afisa Mawasiliano wa ATCL aliipongeza benki hiyo kwa kuwaunganisha pamoja ili kuwapatia abiria wao safari za bure ambayo wanaamini itaimarisha uhususiano mzuri na wateja wao.

Benki ya FINCA Microfinance, inafurahia kuwa na matawi zaidi ya ishirini pamoja na mawakala zaidi ya mia nchi nzima. Benki hiyo pia inajivunia huduma zake za kuweka akiba na kutoa mikopo yenye riba nafuu.

Benki hiyo inaamini huduma zake zinasaidia wateja wao kufikia malengo chini ya msaada na usimamizi wao na ndo sababu ya msingi ya kuja na kampeni hii ya FikaNaFINCA.

WFP YATAMBULISHA MIKAKATI YA KUTOKOMEZA NJAA NCHINI

0
0
 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Dunford akielezea kwa undani namna shirika hilo litakavyoweza kufanya kazi nchini Tanzania na kuitaja mikakati mitano waliyo iweka kwa ajili ya Shirika hilo.
 Mmoja wa Blogger Bw. Bethuel Kinyori ambaye ni Mmiliki wa mtandao wa Dailypulse24.com akiuliza swali wakati wa Mkutano huo ulio fanyika katika Hotel ya New Africa Jijini Dar es salaam leo.
 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Dunford akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na waandishi wa Habari za Mtandaoni.
Mmoja wa wafanyakazi wa WFP Bw. Masasa Makwasa akielezea namna Programu ya ‘Farm to Market Alliance’ inavyofanya kazi na inavyowasaidia wakulima katika shughuli zao za Kilimo.
 Mtaalam wa mambo ya usimamizi wa Fedha ambaye pia ni Blogger Bi. Monica Joseph akiuliza swali linalohusiana na maswala ya fedha hasa kwa wakulima ambao WFP wanaofanyanao kazi.
 Bi. Alice Maro kutoka WFP akielezea mambo zaidi kuhusu Shirika hilo
 Bw. Krantz Mwantepele ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Koncept na Mmiliki wa mtandao wa Mwanaharakati Mzalendo akiuliza swali wakati wa Mkutano huo.
 Baadhi ya Bloggers wakiwa katika mkutano huo
 Baadhi ya watumishi wa WFP wakiwa katika Mkutano huo uliowahusisha waandishi wa Habari za Mtandanaoni (Bloggers)
 Bw. Masasa Makwasa kutoka WFP akijibu baadhi ya Maswali yaliyoulizwa na Bloggers
Picha ya Pamoja ya watumishi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) pamoja na waandishi wa Habari za Mtandaoni (Bloggers)
Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa Tanzania
 Habari na Michuzi Media na Mo BlogShirika la chakula Duniani (WFP) limetambulisha mikakati yake mitano ya
kutokomeza njaa nchini itakayofanyika ndani ya miaka minne kuanzia
mwaka huu hadi 2021.
Akizungumza katika warsha iliyowakutanisha WFP na waandishi wa Habari za mtandaoni, mkurugenzi wa WFP Tanzania,Michael Danford ameitaja mikakati hiyo kuwa, ni kuwasaidia wakimbizi na jamii zao, kutoa msaada wa lishe hasa katika maeneo ya Dodoma na Singida.
Aidha alitaja mikakati mingine kuwa ni, kuimarisha mfumo wa chakula Serikalini na ubunifu wa namna ya kupata chakula cha ziada.
Akifafanua namna ya utekelezaji wa mikakati hiyo, amesema, watatoa
msaada wa fedha kwa wakimbizi wapatao 400,000 kwa ajili ya kuwawezesha kupata mahitaji yao wanayotaka pia kuiongezea serikali kipato.
“Kuna faida zaidi ya kutumia fedha kuliko chakula kwa wakimbizi kwani
kila dola moja iyakayotumika inaweza kuimarisha uchumi wa nchi sababu
fedha zitakazoingia zitakuwa za kigeni”.
Aidha ameongeza, WFP kwa kushirikiana na wadau wengine watatoa elimu kwa wakulima wadogo juu ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kuwaunganisha kwenye masoko ya uhakika.
” Tangu Tanzania ipate Uhuru, WFP ndio iliyosaidia wakulima kwa Mara ya
kwanza kupata mikopo kutoka benki, tulikaa na taasisi za fedha
tukawashawishi kuwaamini wakulima na kuanza kuwapa mikopo,” amesema.

Hafla ya Uzinduzi wa Tawi la NMB Haydom Mkoa wa Manyara

0
0
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Sara Msafiri Ally ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Hanang akizindua jengo la tawi la NMB lililopo katika mji mdogo wa Haydom. Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Sara Msafiri Ally ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Hanang (wa tatu kulia) kikata utepe kuashiria uzindua wa jengo la tawi la NMB lililopo katika mji mdogo wa Haydom. Wa pili kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Straton Chilongola.

KILIO cha wakazi wa jimbo la Haydom wilaya ya Mbulu mkoani Manyara cha kukosa huduma za kibenki toka Tanzania ipate uhuru,kimepata ufumbuzi wa kudumu baada ya NMB benki, kufungua tawi katika mji mdogo wa Haydom. Kwa mujibu wa mbunge wa jimbo la Haydom, Flatei Massay, katika kipindi chote hicho, wananchi wa jimbo hilo wamekuwa wakilazimika kufuata huduma za kibenki Mbulu mjini, umbali wa zaidi ya kilometa 90. Mbunge Massy alisema kitendo cha kufuata huduma za kibenki umbali mrefu kiasi hicho, kumekuwa na madhara mengi na makubwa, ikiwemo gharama kubwa ya usafiri na pia usalama wa fedha.

 “Umbali huo umesababisha wakulima, wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla, kutunza fedha zao majumbani. Miaka ya nyuma majambazi yalitumia bomu kubomoa kasiri (sefu) la kutunzia fedha mali ya hospitali ya rufaa ya misioni Haydom na yalifanikiwa kuiba fedha, Pia fedha nyingi ziliungua kwa moto wa bomu”, alisema na kuongeza; “Zipo hisia kwamba majambazi hayo yalihisi hospitali hiyo haipeleki fedha benki kwa wakati kutokana na umbali mrefu benki ilipo, kwa hali hiyo yalitarajia kupata fedha za kutosha”. 

Mbunge huyo alisema kufunguliwa kwa benki hiyo yenye mashine mbili za kutolea fedha, wananchi na wafanyabiashara, wanapaswa kuitumia kikamilifu, ili kupanua kilimo na biashara zao. Kwa upande wake mgeni rasmi katika ufunguzi huo, kaimu mkuu wa mkoa wa Manyara, Sara Msafiri Ally, ameihimiza benki ya NMB kuongeza juhudi zaidi katika kuendelea kutoa mikopo na huduma zingine kwa wakazi wa vitongoji vyote mkoani Manyara. Alisema serikali ya awamu ya tano imeweka mikakati mizuri ya kupunguza umaskini, hivyo mikopo inayotolewa na mabenki ikiwemo NMB, itasaidia kuendeleza kukuza uchumi na kuongeza ajira.

 Ameongeza kwa kuwahimiza wananchi wa Haydom, kuchangamkia uwepo wa benki ya NMB, ili kutumia huduma zao za kibenki kupata maendeleo yao binafsi, wilaya ya Mbulu na mkoa wa Manyara kwa ujumla. “Serikali inawapongeza NMB kwa kutambua umuhimu wa kusaidia jamii. Ni ulweli usiofichika kuwa faida mnayopata katika huduma zenu za kibenki, inatokana na wananchi. 

Hivyo kusaidia jamii ni njia nzuri ya kurudisha shukrani kwa waliosaidia mkapata faida”, alifafanua Sara. Awali meneja wa NMB kanda ya kati, Straton Chilongola, alisema NMB tawi la Haydom, litahudumia vijiji na viitongoji vya Maghani, Labai, Maritadu, Endamilayi, Getanyamba na Dongobeshi. Aidha, alisema benki hiyo imeendelea kubuni bidhaa mbalimbali na zenye kuzingatia mahitaji halisi ya soko kwa wakati husika. “Moja ya bidhaa hizo, ni kampeni ya ‘FANIKIWA’ akaunti ambayo ni mahususi kabisa kwa wajasiriamali wadogo wadogo. 

Wajasiriamali hao ni pamoja na baba/mama lishe, wauza chipis, wenye maduka ya biashara yakiwemo ya nguo”, alifafanua Chilongola. Akifafanua zaidi,alisema akaunti hiyo inampa fursa mteja kupata mkopo wa shilingi laki tano hadi shilingi 30 milioni. Pia meneja huyo, alisema wanayo akaunti nyingine ya ‘Wajibu’ ambayo ni mahususi kwa ajili ya watoto wenye umri wa miaka 0-18.

 “Kwa upande wa teknolojia, tuna akaunti ya ‘Chap Chap’. Akaunti hii mteja anaweza kufungua akaunti kwa muda mfupi na papo hapo kupata kadi yake ya ATM, na kuanza kufanya miamala wo wote”, alisema Chilongola. Benki ya NMB, ina matawi zaidi ya 200 na mashine za kutolea fedha zaidi ya 700 nchi nzima.Ina wateja zaidi ya milioni mbili jambo linaloifanya kuwa benki pekee nchini yenye hazina ya wateja wengi kuliko benki zingine zilizopo nchini.
Burudani zikiendelea.
Meneja wa NMB kanda ya kati, Straton Chilongola, akitoa taarifa yake kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi la NMB Haydom mkoani Manyara. Hafla hiyo imefanyika katika mji mdogo wa Haydom. Baadhi ya wakazi wa mji mdogo wa Haydom,waliohudhuria uzinduzi wa tawi la NMB katika mji mdogo wa Haydom wilaya ya Mbulu mkoani Manyara juzi. Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Sara Msafiri Ally ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Hanang akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi la NMB tawi la Haydom wilaya ya Mbulu uliofanyika juzi katika mji mdogo wa Haydom.Wa kwanza kushoto (waliokaa) ni meneja NMB kanda ya kati, Straton Chilongola na mbunge wa jimbo la Haydom, Flatei Massy.

WAZIRI MWIJAGE, WAZIRI TIZEBA WAFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI MKUU WA VIETNAM

0
0
Leo tarehe 2 Agosti, 2017, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yao nchini Vietnam, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage pamoja na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba, wamekutana kwa mazungumzo na Waziri Mkuu wa Vietnam, Mhe. NGUYEN XUAN PHUC, ambapo walijadili namna ya kuimarisha mahusiano na ushirikiano wa kiuchumi na biashara baina ya nchi hizo mbili. Mazungumzo hayo yalifanyika baada ya kukamilisha kongamano la tatu la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Vietnam lililofanyika siku hiyo hiyo ya tatu ya ziara yao.

Katika mazungumzo yao, Waziri Mkuu wa Vietnam aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua nzuri za kiuchumi inazoendelea kupiga kwa kuzingatia kwamba Tanzania ni kati ya nchi kumi duniani ambazo uchumi wake unakua kwa kasi na ni ya kwanza kwa Afrika Mashariki. Aliishukuru pia serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuisaidia kampuni ya Halotel katika utoaji wa huduma zake za mawasiliano na hasa vijijini. 
Aliwakikishia Mawaziri hao kuwa Vietnam itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zinafikia malengo ya biashara yaliyowekwa na Marais wa nchi hizi hapo mwaka 2016 nchini Tanzania.

Kwa upande wake Waziri Mwijage alieleza kuwa Serikali ya Tanzania inatambua na kuenzi urafiki na ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi hizi mbili. Alieleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kuendeleza mikakati ya kutekeleza maelekezo ya viongozi wa nchi hizo mbili kwamba ifikapo mwaka 2020 biashara kati ya nchi hizi ifikie dola za marekanii bilioni 1. 


Hivyo, kongamano la uwekezaji lililofanyika hapo mjini Hanoi, limeweza kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania wapatao 30 na wafanyabiashara wa Vietnam zaidi ya 200. Aidha, kutokana na kongamano hilo, changamoto mbalimbali zilielezwa ambazo zinarudisha nyuma jitihada za wafanyabiasha. 
Alieleza kuwa tayari amekutana na Waziri wa Biashara na Biwanda wa Vietnam na wamekubaliana timu ya wataalmu ikutane Dar es Salaam mwezi Septemba kuanza kufanyia kazi mapungufu hayo kwa pande za nchi zote. Nae Waziri Dkt.  Tizeba alimshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa nafasi aliyowapa ya kukutana pamoja na kuwa ana majukumu mengi. 

Alieleza kuwa changaoto nyingi zilizoelezwa na wafanyabiashara katika kongamano la biashara zingeweza kutatuliwa iwapo hati za makubaliano zilizopendekezwa na nchi hizo zingekuwa zimekamilishwa na kuwekwa saini. 
Hivyo, alimuomba Mheshimiwa Waziri Mkuu asaidie kwa upande wa Serikali ya Vietnam ili hati za makubaliano ya ushirikiano kati ya taasisi mbali mbali za Tanzania na Vietnam zikamilishe na kurahisisha biashara.

.WATAKAOBADILISHA MATUMIZI YA FEDHA KUCHUKULIWA HATUA KALI.

0
0
Wakulima mkoani RUVUMA wametakiwa kuzalisha mazao yeye tija ili kukuza sekta ya kilimo na kupanua uzalishaji ili kuifanya nchi ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ambapo mkoa wa ruvuma ni kati ya mikoa inayozalisha chakula kwa wingi hapa nchini Tanzania.

Tigo yatoa msaada kompyuta 47 Chuo Kikuu cha Dodoma

0
0

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dodoma, Prof. Idris Kikula akipokea moja kati ya komputa 47 za thamani ya shilingi milioni 71/- toka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Simon Karikari.Wengine kutoka kushoto Makamu Msaidizi Mkuu wa Chuo, Utawala, Mipango na Fedha, Prof. Ahmed Amme, Makamu Mkuu Msaidizi Chuo Kikuu Udom, Prof. Peter Msofe, Meneja huduma kwa jamii Tigo, Halima Okash(mwenye kilemba) na Meneja mawasiliano Tigo, Woinde Shisael. Hafla iliyofanyika jana chuoni hapo.

Meneja Mawasiliano Tigo, Woinde Shisael akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya kukabidhi komputa .
Baadhi ya wafanyakazi wa chuo kikuu Dodoma (UDOM)wakifutilia makabidhiano


 Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali, Tigo Tanzania leo imetoa msaada wa kompyuta 47 za thamani ya shilingi milioni 71 kwa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ili kuimarisha juhudi za taasisi hiyo za kutoa elimu ya juu nchini.

Wakati akikabidhi kompyuta hizo kwa chuo hicho Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema kuwa kupitia sera ya kampuni ya uwajibikaji kampuni hiyo imejikita katika kuwawezesha vijana na jamii kwa ujumla kufikia taarifa za kimataifa na uelewa, ambapo watajifunza, kupanua ubunifu wao na kushirikiana na wenzao duniani kote.

Alifafanua zaidi kuwa kupitia mchango huo, Tigo imeunga mkono Serikali ya Tanzania katika mtazamo wake wa kubadilisha nchi kuwa na uchumi unaoegemea katika uelewa ifikapo mwaka 2025 na kuthibitisha kujitoa kwa kampuni hiyo katika kuunga mkono jitihada za wizara husika ya kubadilisha elimu nchini kwa kupitia kujumuishwa kwake katika uwanja wa kidijitali.

"Kupitia uwekezaji wetu wa kijamii, Tigo imekuwa mstari wa mbele katika kukuza sekta ya elimu nchini. Hatufanyi kazi tu na taasisi za elimu ya juu, bali pia tumeshatoa kompyuta na kuunganisha zaidi ya shule 60 za sekondari kwa mtandao wa intaneti wenye kasi kupitia Mradi wetu wa Shule-elektroniki. Hali kadhalika, Tigo imetoa msaada wa madawati zaidi ya 7,100 ambayo yamewanufaisha wanafunzi wa shule za msingi zaidi ya 21,000 kote nchini ", alisema Karikari.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Makamu Mkuu wa Chuo cha UDOM, Prof. Idriss Kikula alishukuru Tigo kwa mchango huo akisema; "Ni kupitia ushirikiano huu kwamba tutaweza kutoa stadi za kisasa za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) pamoja na maarifa kwa kizazi cha wataalamu, ili nchi iweze kukidhi mahitaji ya taarifa zinazovbadilika na mtiririko wa kidijitali katika jamii na uchumi wa dunia."

"Ninashukuru Tigo kwa utayari wake katika kushirikiana na chuo chetu ili kuongeza kiwango cha ueledi katika elimu ya kidijitali. Nakaribisha ushiriki wa wadau wengine katika utengemano wa teknolojia katika kujifunza, " alisema Kikula.

Msaada huo unafuatia mkataba wa makubaliano uliosainiwa kati ya Tigo na Chuo Kikuu cha Dodoma mwanzoni mwa mwaka huu, ambapo kampuni hiyo pia imejitolea kutoa kompyuta kwa taasisi hiyo ili iweze kutoa urahisi wa kufikiwa kwa bidhaa za mtindo wa maisha ya kidijitali za kampuni hiyo.

KAMPUNI YA BIMA JUBILEE ZANZIBAR YAADHIMISHA MIAKA 80 KWA KUKARABATI SKULI

0
0
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud akikata utepe kuashiria uzinduzi wa madarasa sita yaliyofanyiwa ukarabati na kampuni ya Jubilee katika skuli ya Jang’ombe ‘B’. Wa kwanza kushoto ni Kamishna wa mamlaka ya usimamizi wa Bima Zanzibar Mohammed Ameir, akifuatiwa na Meneja wa Bima Jubilee Zanzibar Abdulrauf Suleiman pamoja na Mwenyekiti wa kamati ya skuli ya Jang’ombe ‘B’ Taifani Vuai Makame.
Meneja wa Kampuni ya Bima Jubilee Zanzibar Abdulrauf Suleiman (katikati) katika picha maalum na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud pamoja na Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Jang’ombe ‘B’ Bi. Salila Adam Sadik.
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud akimtunuku cheti Meneja wa kampuni ya Bima Jubilee Zanzibar Abdulrauf Suleiman kwa kuthamini mchango wake wa kampeni ya mimi na wewe katika hafla iliyofanyika skuli ya msingi Jang’ombe mjini Zanzibar.

Picha na Makame Mshenga.

……………………….

Na Miza Kona-MAELEZO ZANZIBAR

Mkuu wa Mkoa Mjini magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, ameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuweka mpango maalum wa kuyafanyia matengenezo madarasa na madawati pale yanapoharika ili kuepusha hasara.

Ameyasema hayo huko Skuli ya Msingi Jang’ombe katika hafla ya Uzinduzi wa Madarasa sita yaliyofanyiwa matengenezo na Kampuni ya Bima ya Jubilee katika kusheherekea miaka 80 tangu kuanzishwa kwake.

Alisema mpango huo mbadala utasaidia kupunguza gharama za matengenezo na kuweka majengo katika mazingira mazuri yatayomwezesha mwanafunzi kusoma katika hali ya kuridhisha.

Alisema kuwepo utaratibu wa kuwatoza fidia kwa mwanafunzi au raia yeyote atakaharibu kitu ili kuweza kudhibiti majengo na vifaa vya skuli na kuiepushia serikali hasara ya kuyafanyia matengenezo kwa gharama kubwa.

Alieleza kuwa serikali inachukua jitihada ili kuhakikisha skuli zote zake zote zinapatiwa madawati ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

“Tatizo la madawati katika skuli litafikia ukomo wake mwishoni mwa mwaka huu,” alifahamisha Mhe. Ayoub.

Mkuu huyo wa Mkoa amewaomba wazazi na walezi kujiunga na bima ya elimu kwa ajili ya watoto wao ili kuwekeza katika elimu na kuwajengea mazingira mazuri ya maisha yao ya baadae.

Aidha alieleza kuwa kuna changamoto nyingi katika jamii hasa kwenye sekta ya elimu na afya, hivyo jamii inatakiwa kushirikiana ili kuzipatia ufumbuzi wa pamoja kasoro zinazojitokeza.

Ayoub pia ameipongeza kampuni ya Bima ya Jubilee kwa mchango wake huo wa kiunga mkono serikali katika sekta ya elimu na kuwataka wadau wengine kutoa michango yao katika huduma za kijamii ili kuleta maendeleo nchini.

Alikabidhi cheti kampuni hiyo kwa kuwa mdau mkuu wa kutoa mchango katika huduma za jamii na kuunga mkono kampeni ya Mimi na Wewe.

Akisoma risala, Meneja wa kampuni ya Bima Jubilee Zanzibar Abdulrauf Suleiman alisema kampuni yake imejitolea kukarabati madarasa sita katika sehemu zilizobomoka, sakafu pamoja na kuta, kuweka madirisha, milango na kupaka rangi ndani na nje ili kuwaondoshea watoto kero zinazowakabili na kujali afya zao wakati wa masomo.

Aidha ameitaka jamii kuzitunza mali za serikali kwa kuzingatia kwamba skuli ni mali ya jamii hivyo ni wajibu kuzienzi na kuzilinda ili ziweze kunufaisha vizazi vya sasa na vijavyo.

Mapema akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Kamati ya skuli ya Jang’ombe Taifani Vuai Makame, alisema tatizo kubwa la skuli hiyo ni kuvuja kwa paa lake wakati wa mvua, hali inayofanya wanafunzi wasiweze kuendelea na masomo.

Article 15

0
0

DAIMA NITAKUWA NAWE

Nina kila sababu ya kuendelea kumuunga mkono Rais wangu mpendwa Dk. John Pombe Magufuli kwenye kila hatua anayopiga anapoiongoza nchi yetu ya Tanzania, Nina kila sababu ya kubaki na Rais Magufuli.

Rais Magufuli tangu uingine nimekuwa shuhuda wa namna gani unavyotimiza ahadi yako ya kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari. Elimu hii bure hugharimu pesa nyingi, kiasi cha Tsh. Bilioni 18.77 kila mwezi ambazo Serikali ya Rais Magufuli imekuwa ikizitoa ili Mimi, Wewe na yule tuwe wanufaika wa kumuangamiza adui ujinga.

Nimekuwa shuhuda namna Serikali ya Rais Magufuli inavyotoa mikopo ya elimu ya juu. Kwa mwaka 2017/18 Serikali ilitoa mikopo ya Tsh. Bilioni 483 kutoka mikopo ya Tsh. Bilioni 341 kwa mwaka 2015 wakati Serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani. Ongezeko hili la fedha limeongeza pia idadi ya Wanafunzi wanufaika wa mikopo hiyo. Kwanini nisimuunge mkono Rais Magufuli?

Serikali ya Rais Magufuli imefanikiwa kuula "mfupa mgumu" kwa kuhakikisha shule zinakuwa na madawati, maktaba pamoja na maabara.

Rais Magufuli amefanikiwa kupunguza kiwango cha rushwa nchini na kuongeza kiwango cha nidhamu na uwajijikaji kwa Watumishi wa umma maeneo ya kazi.

Rais Magufuli tangu aingie madarakani sioni tena yale manyanyaso ya mgambo kwa Wamachinga na Mama Ntilie wanaofanya biashara halali, sehemu halali.

Serikali ya Rais imefanikiwa kufufua mashirika ya umma yaliyokuwa shimoni ama yaliyokuwa njia moja kuelekea shimoni. Rais Magufuli amefufua Shirika la ndege la ATCL kwa kununua ndege 4 mpya, amefufua shirika la simu TTCL kwa kununua hisa zote na sasa linamilikiwa na Serikali na ufufukaji wake unaonekana.

Rais Magufuli ameendelea kukiboresha kilimo hapa nchini kwa kuhakikisha pembejeo zinapatikana kwa wakati, amefuta kodi kero na mzigo kwa Wakulima. Nina kila sababu ya kuendelea kumuunga mkono Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameendelea kudhibiti mfumuko wa bei hadi kufikia asilimia 5.4 kwa mwezi Juni kutoka asilimia 6.7 mwaka 2015.

Hali hiyo imesababisha uchumi wa nchi kukua hadi kufikia asilimia 7.2 ambao ni ukuaji wa juu  kabisa ukanda wa Afrika Mashariki.

Rais Magufuli tangu aingie madarakani madawa yamekuwa yakipatikana hospitali tena kwa bei nafuu. Vipimo, vifaa tiba na operesheni nzito zimekuwa zikifanyika hapa hapa nchini.

Utawala wa Rais Magufuli umeendelea na ujenzi wa miundo mbinu kama vile Barabara, viwanja vya ndege, madaraja, vivuko na reli. Mathalani upande wa reli kuna ujenzi wa reli ya kisasa kwa ujenzi wa standard gauge kuanzia Dar mpaka Moro kwa awamu ya kwanza. Reli hii ikikamilika itakuwa na kasi ya ajabu ya spidi 160 kwa saa. Nani kama Magufuli?

Ndio maana nazidi kusisitiza, daima nitakuunga mkono, daima nitakuwa nawe, daima nitabaki nawe Rais wangu mpendwa Dk. John Pombe Joseph Magufuli

Na Emmanuel J. Shilatu
0767488622
Viewing all 46200 articles
Browse latest View live




Latest Images