Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

KAMATI YA KUZUIA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU WAKUTANA NA WADAU KUJADILI NAMNA YA KUPAMBANA NA BIASHARA HIYO.

$
0
0


Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu , Seperatus Fella, akizungumza na  wadau kutoka taasisi  zinazojihusisha na kupambana na biashara hiyo waliokutana katika jijini Dar es Salaam leo, ili kujadili mikakati ya kutokomeza biashaara hiyo nchini. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX.2
Afisa uchunguzi Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu, Ahmed Mwendadi, akifafanua jambo kwa wadau kutoka Taasisi  zinazopambana  na biashara hiyo waliokutana  jijini Dar es Salaam, ili kujadili mikakati ya kutokomeza biashaara hiyo. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX.3
Mkurugenzi Mtendaji wa ANPPCAN Tanzania, Wilbert Muchunguzi, akieleza jambo juu ya shughuli wanazofanya katika kupambana na Biashara Haramu ya Kuzuia Usafirishaji Binadamu nchini. Kushoto ni Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Seperatus Fella. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX.4
Mkurugenzi wa kituo cha C-sema, Michael Kehongoh, akieleza jambo juu ya shughuli wanazofanya katika kituo hicho kuunga mkono harakati za kupambana na Biashara Haramu ya Kuzuia Usafirishaji Binadamu nchini. Kushoto ni Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu , Seperatus Fella. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Serikali Haitavumilia Kuona Taasisi Zinajiendesha kwa Hasara

$
0
0


Mkurugenzi wa Huduma za Kimenejimenti wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Mihale Mwakabinga akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Msajili wa Hazina, Bodi na Wizara Mama katika usimamzi wa Mashirika na Taasisi za Umma katika kikao kazi kikao kazi cha uhamasishaji wa sheria mbalimbali za Ofisi ya Msajili wa Hazina, wajibu na majukumu kilichowakutanisha na Wenyeviti wa Bodi za Wakurugenzi,Watendaji Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara leo Jijini Dar es Salaam.
PIX1b
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Umma kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina akielezea jambo wakati akiwasilisha mada kuhusu maana ya Mashirika ya Umma katika kikao kazi kikao kazi cha uhamasishaji wa sheria mbalimbali za Ofisi ya Msajili wa Hazina, wajibu na majukumu kilichowakutanisha Wenyeviti wa Bodi za Wakurugenzi, Watendaji Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Msajili wa Hazina Dkt. Oswaid J. Mashindano na Mkurugenzi wa Huduma za Kimenejimenti wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Mihale Mwakabinga.
PIX2
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Samwel Mwita Nyantahe akichangia hoja wakati wa kikao kazi baina ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na Wenyeviti wa Bodi za Wakurugenzi, Watendaji Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara leo Jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimefanyika kwa lengo la kuhamasisha sheria mbalimbali za Ofisi ya Msajili wa Hazina, wajibu na majukumu yao.
PIX3
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)  akichangia mada wakati wa kikao kazi baina ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na Wenyeviti wa Bodi za Wakurugenzi, Watendaji Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara leo Jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimefanyika kwa lengo la kuhamasisha sheria mbalimbali za Ofisi ya Msajili wa Hazina, wajibu na majukumu yao.
PIX4a
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha uhamasishaji wa sheria mbalimbali za Ofisi ya Msajili wa Hazina, wajibu na majukumu ya Wenyeviti wa Bodi za Wakurugenzi, Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara  leo Jijini Dar es Salaam.
PIX5
Msajili wa Hazina Dkt. Oswald J. Mashindano akifurahia jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Bima ya Maisha na Mafao kutoka Shirika la Taifa la Bima (NIC) Bw. Michael Mowo walipokutana katika kikao kazi cha uhamasishaji wa sheria mbalimbali za Ofisi ya Msajili wa Hazina, wajibu na majukumu kilichowakutanisha Wenyeviti wa Bodi za Wakurugenzi, Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara  leo Jijini Dar es Salaam.
PIX6
Msajili wa Hazina Dkt. Oswald J. Mashindano akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wenyeviti wa Bodi za Wakurugenzi wa Taasisi na Mashirika ya Umma mara baada ya kumaliza kikao kazi cha uhamasishaji wa sheria mbalimbali za Ofisi ya Msajili wa Hazina, wajibu na majukumu yao leo Jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimewakutanisha Wenyeviti wa Bodi za Wakurugenzi, Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara.  
PIX0
Msajili wa Hazina Dkt. Oswaid J. Mashindano akifafanua jambo katika kikao kazi cha uhamasishaji wa sheria mbalimbali za Ofisi ya Msajili wa Hazina, wajibu na majukumu mbele ya Wenyeviti wa Bodi, Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara  leo Jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Kimenejimenti kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Mihale Mwakabinga na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Umma wa OMH, Bw. Maftah Bunini.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO

RAIS AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI KWA NAIBU KAMISHNA WA UHAMIAJI *Ni baada ya kutoa vibali vya uraia kwa Wasomali 50

$
0
0
RAIS Dkt. John Magufuli amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumsimamisha kazi Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Bi. Grace Hokororo asimamishwe kazi kwa tuhuma za kuingiza nchini raia 50 wa Somalia na kuwapa vibali vya kuishi kinyume cha taratibu.

Kauli hiyo imetolewa leo (Ijumaa, Julai 28, 2017), na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza kikao na Makamishna wa uhamiaji. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.

Pia Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba kuunda tume ya uchunguzi kuhusu utoaji wa vibali uraia nchini.

Amesema haiwezekani raia wa kigeni wanaingizwa nchini na wanapewa vibali vya kuishi bila ya kufanyiwa uchunguzi wa kina. “Idara ya Uhamiaji tunaitegemea kusimamia mipaka yetu na kuziba mianya ya watu kuingia bila ya kufuata taratibu lakini kwa mapenzi yake Ofisa huyu ameruhusu Wasomali kuingia bila kufuata taratibu.”

Waziri Mkuu amesema ni lazima uchunguzi ufanyike ili kubaini “Tulidhani ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa Wasomali hao ambao hawakuwepo nchini wameingia na kupewa vibali moja kwa moja kwa mapenzi yake tu sasa hii ni dosari hatuwezi kuivumilia.”

Amesema Serikali inaitegemea Idara ya Uhamiaji kwa kuzuia mianya ya uingiaji raia mbalimbali kutoka nje ya nchi bila ya kufuata taratibu, hivyo Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ameagiza Ofisa huyo asimamishwe kazi na uchunguzi ufanyike ili kubaini malengo yake.

"Hawa Wasomali aliowapa vibali vya kuishi wala hawakuwa wanaishi nchini wameingia tu na kupewa vibali, hivyo Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli ameagiza ofisa huyo akae pembeni na achunguzwe ni kujua ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa raia hao."

Pia Waziri Mkuu ameiagiza idara ya Uhamiaji wadhibiti kitengo cha utoaji hati za kusafiria za Kibalozi na kwa wanaomaliza muda wasipewe tena. " Lazima hati hizo zikaguliwe katika mipaka yote na maeneo yote ya usafiri ili kujua kama huyo anayeitumia bado anahadhi hiyo na msiporidhika ichukuweni kwani kuna watu wanazitumia vibaya."

Hata hivyo Waziri Mkuu ameagiza uchungilzi wa kina ufanyike kwa watu wote walioomba hati za kusafiria pamoja na vibali vya makazi kama wanakidhi matakwa ya kisheria kabla ya kuwakabidhi.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

IJUMAA, JULAI 28, 2017

TEF YALAANI WAANDISHI WA HABARI WA TBC KUFUKUZWA KWENYE MKUTANO WA CHADEMA

WATOTO WA KIKE WAASWA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI

$
0
0
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano na Mazingira January Makamba (kulia) akimsikiliza Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini Tanzania(ERB) Mhandisi Patrick Balozi (kushoto) akitoa neno la utangulizi wakati wa uzinduzi wa kongamano la tatu la wahandisi wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano na Mazingira January Makamba (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wahandisi Wanawake nchini Mhandisi Alice Isibike akielezea changamoto wanazokutana nazo wahandisi wanawake mapema hii leo wakati wa uzinduzi wa kongamano la tatu la wahandisi wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano na Mazingira January Makamba akizungumza na wahandisi wanawake nchini wakati akizindua kongamano la tatu la wahandisi wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wahandisi wanawake wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano na Mazingira January Makamba wakati akizindua kongamano la tatu la wahandisi wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa – Maelezo


Na. Paschal Dotto- MAELEZO


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. Janauary Makamba amewaasa watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi ambayo yatawawezesha kupata utaalamu katika fani ya uhandisi.

Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais katika Tamasha la Wahandisi wanawake(TAWECE) lililofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salamu Mhe. Makamba amesema kuwa katika juhudi za kujenga taifa la viwanda fani ya uhandisi ni muhimu hivyo watoto wakike hawana budi kuweka kipaumbele katika masomo ya sayansi.

“katika hali ya kawaida wahandisi wa kike ni wachache kulinganisha na wahandisi wa kiume hii ni kutoka na kuwepo kwa imani kuwa masomo katika kada hii ni ya wanaume na si wanawake kama watoto wengi wanavyojua,watoto wa kike onyesheni tofauti someni masomo ya sayansi muweze kutoa mchango kwa taifa “ Alisema Waziri Makamba.

Pia Waziri Mhe. Makamba ameishukuru Serikali ya Norway kwa kutoa nafasi kwa masomo kwa watoto wa kike kusomea uhandisi kwani hali hii imesaidia kuongeza idadi ya wahandisi wa kike kutoka 96 kwa mwaka 2010 hadi kufikia wahandisi 379 kwa mwaka huu.

Naye Mwenyekiti wa chama hicho Mhandisi Alice Sibike ameishauri Serikali ya Tanzania kuwawezesha watoto wa kike katika kuwapa fursa kwa kuwapa mikopo elimu ya juu ili kusaidia kuongeza idadi ya watoto wa kike wanaosoma fani uhandisi.

Katika kutekeleza kwa vitendo mpango huo chama hicho kimeanza kutembelea shule mbalimbali na kutoa elimu kwa watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi ambapo mpaka sasa wameshatembelea shule za Azania, Feza girls na Tambaza zote za jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa usajili wahandisi Mhandisi Patrick Balozi amesema ipo haja ya watoto wa kike na jamii kwa ujumla kuhamasika kuweka kipaumbele cha masomo ya sayansi kwa watoto wa ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuwa na uchumi wa viwanda.

Tanzania ina jumla ya wahandisi 19,164 ambao kati yao wanawake ni 1,763 huku wahandisi 4831 wako mafunzoni baada ya kumaliza masomo na kati yao wa kike ni 372.

“tunahitaji wahandisi 80000 ili kukidhi mahitaji ya kujenga nchi ya viwanda lakini watoke katika jinsia zote ili kuweka mfumo sawa katika kutenda kazi”, Alisema Mhandisi Balozi

Tamasha la chama hicho lilianza rasmi mwaka 2015 na lengo ni kuwakutanisha wahandishi wote wa kike ili kubadilishana ujuzi na pia kuwawezesha watoto wa kike kujifunza kutoka kwa wahandisi wenye uzoefu

KIWANDA CHA NONDO CHA UNIQUE STEEL CHAJIPANGA KATIKA UWEKEZAJI KUHUDUMIA BOMBA LA MAFUTA

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Kiwanda cha uzalishaji wa nondo cha Unique Steel Rolling Mills kilichopo Tanga kimesema kimejipanga kufanya uwekezaji mkubwa,Ili kutumia fursa ya uwepo wa ujenzi wa Bomba la gesi kutoka Tanga mpaka Uganda kutumia malighafi kutoka kiwandani hapo.

Hayo yamebainishwa na Mhasibu Mkuu wa kiwanda hicho, Sikander Omar alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari waliotembelea kiwanda hicho Jijini Tanga.Omar amesema kuwa Wakati Serikali ikipambana kuhakikisha viwanda vinakua nchini, baadhi ya viwanda vilivyopo vimekuwa vikikumbana na changamoto mbalimbali zinazozuia uzalishaji kwa wakati."Moja ya changamoto hizo ni kukatika katika kwa umeme bila taarifa jambo linalotia hasara wakati wa uzalishaji. 

Mbali na hilo upatikanaji wa mikopo kwa ajili ya kuwekeza zaidi imekuwa ni changamoto kwao,anapambana kukiboresha kiwanda hicho lakini umeme kutokuwa wa uhakika imekuwa changamoto".Amesema Omar.Amesema kwa sasa wanazalisha hadi tani 60 za nondo ambazo nyingi huuzwa mkoa wa Arusha.

Akizungumzia changamoto zilizopo msimamizi wa kiwanda hicho, Jagjeet Singh alisema umeme unapokatika wakati wa uzalishaji inakuwa ni hasara kwao kwa kuwa mtambo wa kuyeyusha chuma hupoa na vyuma vilivyokuwa vinayeyuka ili kutoa nondo huganda.

Kiwanda hicho ambacho kilikuwa cha Serikali na kuzinduliwa Julai 21, 1971 kilisimama na kuanza uzalishaji tena hivi karibuni baada ya kuchukuliwa na  mwekezaji huyo. Omar amesema hivi sasa wako katika mchakato wa kutafuta mkopo ili kukiongezea nguvu kiweze kuzalisha zaidi na kutoa huduma katika mikoa zaidi ya Tanga na Arusha ambalo ndilo soko kubwa lao lilipo kwa sasa.
Mhasibu Mkuu wa kiwanda cha Nondo cha Unique Steel Rolling Mills kilichopo Tanga, Sikander Omar akizungumza na Wandishi wa Habari waliotembelea kiwanda chake kungalia hali ya uzalishaji
Watendaji wa kiwanda cha Unique Steel Rolling Mills kilichopo Tanga wakiwaonesha waaandishi wa habari sehemu ya kuzalishia Nondo ambayo imesimama kutokana na matatizo ya Umeme
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi Boniface Meena akiangalia moja ya Nondo zinazozalishwa na Kiwanda cha Unique Steel Rolling Mills kilichopo Tanga

CHANJO YA HOMA YA INI KUPATIKANA KWA WANANCHI WOTE MPAKA KUFIKIA 2020

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiwahutubia waandishi nwa habari (Hawapo kwenye picha) katika kilele cha maazimisho ya siku ya Homa ya Ini Duniani yaliyofanyika leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mganga mkuu wa Serikali Pro Muhamad Bakari kambi na Kulia ni Afisa kutoka kitengo cha magonjwa ya Mlipuko Dkt. Azma Simba.

Waandishi wa habari kutoka vyombo tofauti wakifuatilia kwa ukaribu tamko la kilele cha maadhimisho ya Homa ya Ini Duniani lililotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (Hayupo kwenye picha) leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akijadiliana kwa ukaribu na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Muhamad Bakari Kambi wakati akitoa tamko kuhusu Homa ya Ini Duniani katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakifuatilia kwa umakini tamko lilitolewa na Mh. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.

……………………………..

NA WAMJW –DAR ES SALAAM.

CHANJO ya homa ya Ini inatarajiwa kupatikana kwa wananchi wote bila kujali kigezo cha umri wala uwezo wa kifedha kwa wananchi wenye hatari au ugonjwa wa ini kwa bei nafuu mpaka kufikia mwaka 2020 kutoka mwaka wa fedha 2018/2019.

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya ugonjwa wa homa ya ini duniani.

“Katika kuadhimisha siku ya ugonjwa wa homa ya ini duniani tumedhamiria kuhakikisha chanjo ya ugonjwa huu inapatikana kwa watu wote nchini ambao wana hatari ya kupata maambukizi ya homa ya ini au tayari wamepata ugonjwa huo kwa bei nafuu kwa mswaka wa bajeti 2018/2019” alisema Waziri Ummy.

Aidha waziri Ummy amesema kuwa chanjo ya homa ya Ini kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano inapatikana hapa nchini kwenye vituo vya huduma ya afya vya Serikali na watu binafsi.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa ili kujilinda na maambukizi ya ugonjwa wa homa ya ini mpango wa damu salama unatakiwa kuhakikisha wanapima damu zote za wachangiaji kabla ya kuwawekea wagonjwa wanaohitaji huduma ya damu.

Waziri Ummy ameongeza kuwa ugonjwa wa homa ya ini unaua idadi kubwa ya watu duniani kwa taratibu ikiwa katika watu 100 watu 8 wana maambukizi ya ugonjwa huo na kutoonyesha dalili mapema.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa asilimia 50 ya wanaotumia madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano wana maambukizi ya ugonjwa wa homa ya ini hivyo kuwataka watanzania kutojihususha na matumizi hayo na kuepuka ngono zembe.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohamad Bakari Kambi amesema kuwa virusi vikubwa vya ugonjwa wa ini ni A,B na C ambapo vimelea A huletwa na mtu asiye na maambukizi kula chakula kisicho salama na kunnywa maji yasiyo salama.

Aidha Prof. Kambi amesema kuwa virusi B na C vya ugonjwa wa homa ya ini husababishwa pale mtu asiye na maambukizi kugusa majimaji au damu kutoka kwa mgonjwa mwenye ugonjwa wa homa ya ini.

Maadhimisho ya ugonjwa wa homa ya Ini huadhimishwa Julai 28 kila mwaka Duniani na mwaka huu imebeba kauli mbiu isemayo “TOKOMEZA HOMA YA INI” ambapo hapa nchini imeadhimishwa jijini Dar es salaam.

PROFESA MBARAWA ASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO WA PAMOJA WA USAFIRSHAJI.

$
0
0


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akipitia mkataba wa makubaliano katika mkutano wa kwanza wa Mawaziri wa usafirishaji na uchukuzi mkoani Kigoma,kuhusu kushirikiana katika miradi ya maendeleo ya pamoja kati ya nchi ya Tanzania, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akisaini mkataba wa makubaliano mkoani Kigoma, kuhusu kushirikiana katika miradi ya maendeleo ya pamoja kati ya nchi ya Tanzania, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na waandishi wa habari mkoani Kigoma, katika mkutano wa kwanza uliohusisha Mawaziri wa uchukuzi kutoka nchi ya Tanzania, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Mkutano huo umejadili ushirikiano katika miradi ya maendeleo ya pamoja baina ya nchi hizo.
…………………….
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesaini mkataba wa ushirikiano katika miradi ya pamoja inayohusu masuala ya usafirishaji na uchukuzi, lengo likiwa ni kuleta maendeleo na kukuza uchumi katika nchi wanachama.

Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo mkoani Kigoma, Waziri Mbarawa amesema kuwa mkataba huo ambao unahusisha nchi ya Tanzania, Uganda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), unalenga kuhuisha fursa za kiuchumi katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika.

Amesema pamoja na mambo mengine, Mawaziri wa Muungano wa Uchukuzi na Usafirishaji wa Nchi za Ukanda wa Ziwa Tanganyika (LTITS), wamepokea ripoti ya wataalam inayooelekeza utekelezaji wa miradi kwa nchi wananchama ili kufikia malengo yanayotarajiwa.

“Tumeelekeza Sekretarieti ya ukanda huu kuunganisha pamoja rasilimali kutoka nchi wanachama, sekta binafsi na wadau wa maendeleo ili miradi inayotekelezwa kwa pamoja iweze kukabiliana na changamoto za usafirishaji zilizopo katika ukanda wa Ziwa Tanganyika”, amesema Profesa Mbarawa.

Mawaziri hao Bagiire Aggrey Henry kutoka Uganda, Eng. Jean Bosco Ntunzwenimana kutoka Burundi na Katibu wa Sekretarieti wa Ukanda huo Capt. Dieudonne Dukundane kwa pamoja  wamepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania hususan katika ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge), na uboreshaji wa huduma katika Mamlaka ya Bandari Tanzania ambavyo kwa pamoja vitaunganisha Ukanda huo.

“Kukamilika kwa reli ya Kati ya kisasa hadi Uvinza- Msongati kutawezesha reli hiyo kuunganisha vizuri nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi na hivyo kuchochea maendeleo katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika”, amesisitiza Waziri wa Uchukuzi wa Burundi, Eng. Jean Bosco Ntunzwenimana.

Mawaziri hao wameelezea umuhimu wa uboreshaji wa huduma za uchukuzi katika Bandari ya Ziwa Tanganyika ili iwe na viwango vya kimataifa na kuunganisha vizuri ukanda huo.

Mkutano huo ni mkakati wa nchi za Ukanda wa Ziwa Tanganyika wenye lengo la kuboresha huduma za usafirishaji na uchukuzi katika nchi hizo ili kukuza uchumi na kurahisisha huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

NAIBU WAZIRI UTALII NA MALIASILI INJINIA RAMO MAKANI AFUNGA RASMI MKUTANO WA SITA WA TANAPA KWA WAHARIRI NA WANAHABARI WAANDAMIZI MKOANI TANGA

$
0
0

Naibu Waziri Maliasili na Utalii Injinia  Ramo Makani akimkabidhi
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006)Ltd, Absalom Kibanda cheti cha ushiriki wa Mkutano wa Mwaka na Wahariri na Wanahabari Waandamizi nchini uliohitimishwa jioni ya leo jijini Tanga.Katika hatua hiyo ya kukabidhiwa vyeti,washiriki wote walikabidhiwa vyeti vya ushiriki wao kwa ukamilifu katika mkutano huo.

Mgeni rasmi,Naibu Waziri Maliasili na Utalii Injinia  Ramo Makani(wanne kulia) akiwa katika picha ya pmoja na washiriki wa Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika jana kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'. 
Naibu Waziri Maliasili na Utalii Injinia Ramo Makani leo akizungumza jambo wakati akifunga rasmi Mkutano wa Mwaka na Wahariri na Wanahabari Waandamizi nchini jijini Tanga.

Sehemu ya Meza kuu,kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF),Theophil Makunga,Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO),Dkt.Hassan Abbas,Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa TANAPA,Bwa.Ibrahim Mussa ,Mgeni rasmi-Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Ramo Makani,Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Mhe.Thobis Mwilapa.

Baadhii ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo kabla ya kufungwa rasmi jioni ya leo.
Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa TANAPA,Bwa.Ibrahim Mussa akiwashukuru washiriki wa Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika jana kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga ,na kuhitimishwa rasmi jioni ya leo na Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Ramo Makani .
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mh.Thobias Mwilapa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh.Martin Shigella wakati wa kutoa salamu za shukurani kabla ya kufungwa rasmi kwa Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika jana kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.

 Meneja Mahusiano wa TANAPA,Pascal Shelutete akizungumza jambo kabla ya mgeni rasmi kufunga Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika jana kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga.

WASICHANA WAISHUKURU TGGA KUFANIKISHA ZIARA YA MAFUNZO NJE YA NCHI

$
0
0
 Wasichana wanachama wa Tanzania Girl Guides wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, wakitokea kwenye ziara ya programu ya miezi sita ya mafunzo ya kubadilisha uzoefu katika masuala ya utamaduni, uongozi na maadili. Kutoka kushoto ni Ummy Mwabondo alikwenda Zambia, Edna Chembele (Zimbabwe), Elizabeth Betha (Madagascar) na Farida Mjoge aliyekuwa Uganda. PICHA, HABARI NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

WASICHANA wanne wanachama wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA) wamerejea nchini kutoka kwenye programu ya mafunzo ya miezi sita katika nchi mbalimbali za Afrika.

Wasichana hao waliokuwa kwenye mafunzo ya kubadilishana uzoefu katika mambo ya utamaduni, uongozi na maadili katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Madagascar na Uganda wameipongeza TGGA kwa kufanikisha ziara hiyo yenye mafanikio makubwa katika maisha yao.

Walipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana kwa ndege ya Kenya Airways, walilakiwa na Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba, ndugu jamaa na marafiki huku wengine wakivishwa mashada na kupatiwa zawadi mbalimbali. Wasichana waliokwenda kwenye mafunzo hayo ni; Ummy Mwabondo, Elizabeth Betha, Edna Chembele na Farida Mjoge ambao kila mmoja anaeleza jinsi alivyonufaika na ziara hiyo.

Elizabeth Betha ambaye programu yake aliifanyia Madagascar, anaeleza kuwa Wananchi wa Kisiwa hicho utamaduni wao ni tofauti kabisa na wa Tanzania na  maeneo mengine ya Afrika, ambapo mara nyingi hutumia lugha yao ya asili na  kifaransa kama Lugha yao ya Taifa, ni wakarimu sana na wana upendo.

Anasema kuwa licha ya kuwafundisha mambo mengi ya Tanzania ikiwemo utamaduni, mapishi ya vyakula mbalimbali, lugha ya kiswahili na vivutio mbalimbali vya kitalii pia wakiwa huko walipanda  miti, kufundishana kwa uwazi masuala ya hedhi salama, kuzuia ukatili wa kijinsia pamoja na kuwapa stamina ya kujiamini na kujithamini.

Edna Chembele, ambaye alikwenda  Zimbabwe, anasema akiwa huko alijifunza kuhusu uendeshaji wa Guides, kuishi maisha ya kawaida mashuleni na mitaani, mambo ya kimila na kiutamaduni, msichana kujiamini na kujithamini.  Pia walitembelea maeneo mbalimbali maarufu nchini humo. kuwaeleza wasichana kwamba nao wana  uwezo kufanya kazi zinazofanywa na wanaume.

Farida Njope yeye alipelekwa Uganda ambako anaelezea kuwa alijifunza mambo mengi kuhusu  Utamaduni, mavazi, mapishi ya aina mbalimbali za vyakula kama vile matoke chakula kinachotokana na ndizi zilizopondwa pondwa.

Naye aliwafundisha Girl Guides wa huko, kujiamini na kujielewa kwa kuthamini usichana wao katika jamii, pia aliona tofauti ya matumizi ya Lugha ambapo Tanzania lugha ya Taifa ni Kiswahili na Uganda Lugha yao ya Taifa ni Kiingereza ambayo alidai inawasaidia sana kujieleza kirahisi katika mambo mbalimbali yakiwemo ya kimataifa.

Alishauri Serikali ya Tanzania kubadilisha mitaala Kiingereza kitiliwe mkazo kwa kuwa somo la lazima kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu akidai lugha hiyo ni muhimu sana kwa mawasiliano kimataifa.

"Naishukuru sana TGGA kunipepeleka Uganda nimejifunza mengi. imenijenga kiakili na kuishi na watu wa aina mbalimbali nikiwa  mbali na wazazi wangu jambo ambalo sitolisahau kati maisha yangu."Alisema kwa msisitizo.

Naye Ummy Mwabondo ambaye programu ya kubadilisha uzoefu alifanyia Zambia, anasema alijifunza mambo mengi ikiwemo  
Jinsi ya kushirikiana na watu na kuongea nao hivyo kuimarisha uwezo wake wa kuzungumza jambo ambalo awali hakuwa nalo, alishiriki pia kupanda miti katika mikoa mbalimbali ya nchi hiyo.

Anasema alipata wasaa wa kuwafundisha wasichana kuwa wakakamavu na kujiamini kutenda mambo mbalimbali katika jamii ikiwemo kupinga ukandamizaji, unyanyasaji dhidi ya watoto wa kike pamoja na kutoa elimu ya hedhi salama kwa wasichana kwa kuwafanya wasiogope kuwa kwenye hali hiyo kwani jambo hilo ni la maumbile ya kibailojia.


 Girl Guides wakiwasili na mizigo yao
 Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba  (kushoto) akiwalaki Girl Guides Uwanja wa Ndege Dar es Salaam
 Ni furaha iliyoje
 Grace Shaba akiwa na Girl Guides wanaoonesha moja ya alama za TGGA
 Elizabeth na Farida wakilakiwa na ndugu zao uwanja wa ndege
 Edna Chembele akilia kwa furaha alipowaona ndugu zake waliofika kumpokea Uwanja wa Ndege Dar es Salaam
 Ummy akivishwa shada la maua na dadake
 Farida akikubatiana kwa furaha na dadake Grace Mjoge aliyefika kumlaki
 Farida Mjoge (wa pili kuli) akikata keki kwa furaha aliyoletewa na ndugu zake kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa
 Farida Mjoge akilishwa keki na dadake Grace
 Katibu Mkuu, Grace Shaba akiwa na Girl Guides hao
 Shaba akiwa na Girl Guide pamoja na ndugu waliofika kuwalaki
Farida Mjoge akimlisha keki Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba.

WADAU WA MAENDELEO WAIMWAGIA TANZANIA MSAADA WA BILIONI 101 KUJENGA BARABARA YA KIDATU HADI IFAKARA KWA KIWANGO CHA LAMI

$
0
0




Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (wa pili kulia) na Mkandarasi kutoka Kampuni ya Ujenzi ya Reynolds, Bw. Dan Yzhak Shahn (kushoto) wakisaini mkataba wa Sh. Bilioni 101 kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ya Kidatu- Ifakara yenye urefu wa Kilometa 66.9, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kulia) na Mkandarasi kutoka Kampuni ya Ujenzi ya Reynolds, Bw. Dan Yzhak Shahn (kushoto) wakibadilishana mkataba wa Sh. bilioni 101 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Kidatu – Ifakara yenye urefu wa Kilometa 66.9, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto) akizungumza kuhusu umuhimu wa barabara ya Kidatu – Ifakara kwa kiwango cha lami kwa maendeleo ya Kilimo baada ya kutiliana saini mkandarasi atakayejenga barabara hiyo, hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania, Roeland van de Geer akizungumza kwa niaba ya EU, UK-AID na USAID, kuhusu mpango wao wa kuendelea kuisaidia Tanzania katika ujenzi wa miundombinu baada ya kuwekwa saini mkataba wa Sh. bilioni 101 kwa ajili ya Ujenzi wa barabara ya Kidatu – Ifakara, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria hafla ya kuwekwa saini mkataba wa Sh. bilioni 101 kwa ajili ya Ujenzi wa barabara ya Kidatu – Ifakara wakifuatilia nyaraka za mkataba huo kabla ya kusainiwa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

…………………………………………………………………………………..

Benny Mwaipaja, WFM

Wizara ya Fedha na Mipango imetiliana saini na Kampuni ya ujenzi wa barabara ya Reynolds kandarasi ya ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara mkoani Morogoro, yenye urefu wa kilometa 67 kwa kiwango cha lami utakaojengwa kwa shilingi bilioni 101, kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya, Marekani na Uingereza.

Mkataba huo umesainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Shaaban kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Bw. Dan Yzhak Shahn, Bw. Benjamin Arbit ambaye ni Mkandarasi kutoka Kampuni ya Ujenzi ya Reynolds.

Kiasi hicho cha fedha ni sawa na Euro milioni 40.4 ambapo Euro milioni 29.6 zimetolewa kwa ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Shirika la Misaada la Uingereza-UK-AID, huku kiasi kinachobaki cha Euro milioni 10.8 kikitolewa na Shirika la Misaada la watu wa Marekani- USAID.

Akizungumza mara baada ya kutiwa saini kwa kandarasi hiyo, Bi. Amina Khamis Shaaban, amesema ujenzi wa barabara hiyo utakaohusisha pia ujenzi wa daraja katika Mto Ruaha Mkuu, utasaidia wakulima wadogo kupitia Program ya Uendelezaji Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania-SAGCOT, walioko katika Bonde la Mto Kilombero, kuyafikia masoko ya uhakika ya mazao yao.

“Kuimarika kwa kipande hiki cha barabara kutaongeza uzalishaji wa nafaka na bidhaa nyingine hatimaye kupunguza gharama za chakula na umasikini wa wananchi” aliongeza Bi. Shaaban

Bi Shaaban amewashukuru wadau hao wa maendeleo kwa msaada huo utakao fungua milango ya kiuchumi kwa Watanzania kupitia Program hiyo ya kuendeleza Kilimo katika Ukanda huo wa Kusini-SAGCOT, unaohusisha pia kuboresha masuala ya nishati ya umeme.

“Ujenzi wa miundombinu unalengo la kuchochea maendeleo ya kilimo cha kibiashara kwa kuwa itasaidia kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara na wakulima”. Aliongeza Bi Shaaban.

Aidha amesema uboreshwaji wa miundombinu utachochea uwekezaji ambao ndio chachu ya maendeleo ya biashara za watu wa chini, hivyo kuinua kiwango cha maisha yao.

“Barabara ya Kidatu hadi Ifakara ndiyo inayounganisha Wilaya za Kilombero na Ulanga na ni barabara kuu itokayo Bandari ya Dar es Salaam kwenda Zambia, Malawi na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) hivyo kuwa na tija katika kuharakisha maendeleo ya kiuchumi jambo ambalo ndio lengo kubwa la Wahisani hao”. alifafanua Bi Shaaban.

Kwa upande wake Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa nchini, Roeland van de Geer ameahidi kuwa EU, UKAID na USAID, zitaendelea kushirikiana kwa kiwango cha juu na Serikali ya Tanzania katika kuboresha Sekta ya ujenzi na miundombinu kwa ujumla lakini pia atahakikisha wanachangia katika kupata soko la uhakika la mazao ya kilimo.

Sekta ya kilimo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania mbapo zaidi asilimia 70 ya wakazi wake hutegemea kilimo na kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza uzalishaji, kipato na kukuza ajira, hususan kwa wanawake na vijana ikiwa miundombinu inayochangia ukuaji wa Sekta hiyo itazidi kuimarika.

RAIS AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI KWA NAIBU KAMISHNA WA UHAMIAJI

$
0
0

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamishna Uhamiaji, mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, Temeke alipotembelea Idara hiyo leo mchana.
PMO_6104
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiongea na Makamishna mbalimbali wa Uhamiaji ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa  Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, Temeke alipotembelea Idara hiyo leo mchana
PMO_6113
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiongea na Makamishna mbalimbali wa Uhamiaji ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa  Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, Temeke alipotembelea Idara hiyo leo mchana.
PMO_6127
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akitoa maelekezo kwa  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala wakati wa ziara yake alipotembelea Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, Temeke leo mchana wanaosikiliza ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Meja Jenerali Projest Rwegasira;  Kamishna wa Pasipoti na Uraia, Gerald Kihinga na Mkurugenzi Mkuu Idara ya Wakimbizi,Harrison Mseke.
PMO_6138
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akitoa maelekezo kwa  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala wakati wa ziara yake alipotembelea Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, Temeke leo mchana wanaosikiliza ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Meja Jenerali Projest Rwegasira;  Kamishna wa Pasipoti na Uraia, Gerald Kihinga na Mkurugenzi Mkuu Idara ya Wakimbizi,Harrison Mseke.
PMO_6146
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi pamoja na Menejimenti ya Idara ya Uhamiaji alipotembelea  Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, Temeke leo mchana.
PMO_6148
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akimwelekeza jambo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala wakati wa ziara yake alipotembelea Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, Temeke leo mchana. Nyuma kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Meja Jenerali Projest Rwegasira.

NMB YATOA SHILINGI 25M/= KUSAIDIA DUKA LA DAWA KWA JAMII MSD

$
0
0
 Ofisa Mkuu wa Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Richard Makungwa (wa kwanza kushoto) akimkabidhi mfano wa hudi ya shilingi milioni 25 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Madawa Tanzania (MSD), Bw. Laurean Bwanakunu zilizotolewa na benki hiyo kusaidia uboreshaji na uendelezaji wa ujenzi wa maduka ya madawa kwa jamii ya MSD katika mikoa tofauti. Hafla hiyo ilifanyika katika ofisi za MSD zilizopo jijini Dar es Salaam. Ofisa Mkuu wa Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Richard Makungwa (wa kwanza kushoto) akizungumza kabla ya kukabidhi mfano wa hudi ya shilingi milioni 25 zilizotolewa na benki hiyo kusaidia uboreshaji na uendelezaji wa ujenzi wa maduka ya madawa kwa jamii ya MSD katika mikoa tofauti. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Madawa Tanzania (MSD), Bw. Laurean Bwanakunu. Hafla hiyo ilifanyika katika ofisi za MSD zilizopo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Madawa Tanzania (MSD), Bw. Laurean Bwanakunu akitoa shukrani kwa Benki ya NMB baada ya kupokea mfano wa hudi ya shilingi milioni 25 zilizotolewa na Benki ya NMB kusaidia uboreshaji na uendelezaji wa ujenzi wa maduka ya madawa kwa jamii ya MSD katika mikoa tofauti. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Richard Makungwa.
 
BENKI ya NMB imekabidhi kiasi cha sh. Milioni 25 kusaidia Bohari Kuu ya Dawa (Medical Stores Department) katika kuboresha uendeshaji wa maduka na uendelezaji wa ujenzi wa maduka katika mikoa tofauti. Hundi hiyo ilikabidhiwa katika ofisi za MSD zilizopo jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa wateja wakubwa wa NMB Richard Makungwa, alisema msaasa huo ni muendelezo wa mahusiano yao na Bohari ya Dawa (MSD). 
 
Ujenzi wa bohari hiyo ya dawa itasaidia kupunguza adha ya upatikanaji wa dawa hasa kwa wananchi wa Rukwa kwani kulikuwa na umbali mkubwa kufikia huduma hiyo. Sekta ya afya ni moja kati ya kipaumbele kikubwa sana kwa benki ya NMB ikiwa ni njia ya mojawapo ya kujali jamii inayotuzunguka. Naye Mkurugenzi Mkuu wa (MSD) Laurean Bwanakunu ameishukuru benki ya NMB kwa kuwa karibu nao hasa katika suala zima la kusaidia maendeleo ya jamii. 
 
Mpaka sasa kuna vituo saba ambavyo ni pamoja na kilichopo nje ya Hospitali ya Taifa (MNH), Sekoture Mwanza, Mount Meru Arusha, nje ya Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Katavi, Ruangwa iliyopo mkoa wa Lindi na Chato Geita.

NGO'S ZAPEWA SOMO KUFANYA KAZI KWA WELEDI

SERIKALI YADHAMIRIA KUBORESHA HALI YA WAZEE NCHINI.


NAIBU WAZIRI DKT. KIGWANGALAA AMPONGEZA KATIBU MKUU BI.SIHABA NKINGA KWA UBORESHAJI WA MAKAZI YA WAZEE NCHINI

WAZIRI MKUU AZINDUA MELI MBILI ZILIZONUNULIWA NA SERIKALI ITUNGI KYELA MKOANI MBEYA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua meli mbili zilizonunuliwa na serikali ili zihudumie wananchi katika ziwa Nyasa . Uzinduzi huo ulifanyika kwenye bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited. Wapili kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu na Kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla. (PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ndani ya moja kati ya meli mbili alizozizindua kwenye badari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimenunuliwa na serikali ili ziwahudumie wananchi katika ziwa Nyasa na zimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chumba cha kulala cha mabaharia wa moja kati ya meli mbili alizozizindua kwenye bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimenunuliwa na serikali na zimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited ili ziwahudumie wananchi katika ziwa Nyasa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika chumba cha mitambo ya moja ya meli mbili alizozizindua katika bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimenunuliwa na serikali na kujengwa na kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited ili ziwahudumie wananchi katika ziwa Nyasa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika chumba cha nahodha wa moja kati ya meli mbili zilizonunuliwa na serikali ili zihudumie wananchi katika ziwa Nyasa, baada ya kuzindua meli hizo kwenye bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017.Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Moja kati ya meli mbili zilizonunuliwa na serikali na kujengwa na Kampuni ya Songoro Marine Transport Limited ikiondoka kwenye gati la bandari Kiwira wialyani Kyela baada ya kuzinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Julai 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya wananchi wakimshangilia Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa.

…………………………………………………………………………….

*Ameonya zisitumike kuvushia wahamiaji haramu na dawa za kulevya

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua meli mbili za mizigo za Mv Njombe na Mv Ruvuma zitakazotumika katika kusafirishia mizigo kwenye ziwa Nyasa na kuonya kwamba zisitumike kama eneo la kuvushia wahamiaji haramu na dawa za kulevya.

Amesema kukamilika kwa ujenzi wa meli hizo zilizogharimu sh. bilioni 11.253 ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Magufuli alizozitoa katika ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 kwa lengo la kutatua changamoto ya usafiri wa abiria na mizigo katika ziwa Nyasa.

Amesema ni jambo la faraja na la kujivunia kwa Serikali na wananchi kwa pamoja kushuhudia meli zilizotengenezwa na Mtanzania, zikiwa zimekamilika tayari kwa kuanza kazi ya kuwahudumia wananchi, ambapo awali suala hilo lilikuwa likifanywa na raia wa kigeni.

Waziri Mkuu amezindua meli hizo zilizojengwa na kampuni ya Kitanzania ya M/S Songoro Marine Transport leo (Jumamosi, Julai 29, 2017) katika bandari ya Kiwira wilayani Kyela akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mbeya.

Amesisitiza kwamba meli hizo zitumike katika kukuza uchumi wa wananchi kwa kusafirisha mizigo na biashara halali kati ya nchi za Tanzania na Malawi na zisitumike kama eneo la kuingiza wahamiaji haramu pamoja na dawa za kulevya nchini.

Waziri Mkuu amewataka wananchi wa maeneo hayo kuwa walinzi na kuhakikisha meli hizo zifanya shughuli halali za kiuchumi ambazo zitawaletea tija wao na Taifa kwa ujumla na kamwe wasikubali zikatumika kama kichaka cha uhalifu.

“Changamoto ya usafiri wa mizigo katika ziwa Nyasa itakuwa historia kwani meli hizi zitarahisisha usafiri na kupanua wigo wa biashara kati ya Tanzania nan chi za Malawi na Msumbiji, hivyo tunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa kutoa ahadi hii ambayo leo utekelezaji wake umekamilika.”

Awali,Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Karim Mataka alisema ujenzi wa meli hizo ulianza Juni 2015 zina uwezo wa kubeba tani 1,000 za mizigo kwa kila moja.

Mhandisi huyo alisema mbali na kukamilika kwa mradi huo pia TPA imeingia mkataba na kampuni ya M/S Songoro Marine Transport Ltd kwa ajili ya ujenzi wa meli ya abiria yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 300 za mizigo. Mradi huo ambao upo katika hatua za mwisho kamilika utagharimu sh. bilioni 9.12.

DC HAPI ASHUSHA PRESHA KWA WANANCHI KUNDUCHI, AHITIMISHA MGOGORO WA ARDHI WA MUDA MREFU

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi amefanya maamuzi magumu leo Jijini Dar es Salaam Kata ya Kunduchi Mjimwema baada ya kuumaliza mgogoro uliokuwepo kati ya wachimbaji wa kokoto na wananchi wapatao 3000 wa eneo hilo, mgogoro ambao umedumu kwa muda wa zaidi ya miaka 20.
DC Hapi ameagiza wananchi wa eneo hilo kuendelea kukaa maeneo hayo baada ya leseni ya uchimbaji kokoto eneo hilo kufutwa kutokana na uharibifu wa miundombinu.
"Hatuwezi kuhatarisha maisha ya wananchi 3000, tutawapeleka wapi, kwani wao siyo wanakinondoni, kwani wao siyo watanzania" Alisema DC Hapi.
DC Hapi ametoa maagizo kwa watendaji kuhakikisha kuwa wananchi hao wanamilikishwa maeneo hayo kwao kufuata taratibu na sheria ambapo itabidi maeneo hayo yapimwe na wananchi hao wawe wavumilivu maana kuna baadhi ya maeneo yatatengwa kwa huduma za kijamii, ikiwemo vituo vya Afya, Polisi na barabara.
Hata hivyo DC Hapi amewatoa hofu wananchi wa maeneo hayo kuhusu kulipia gharama za upimaji wa ardhi ambazo itabidi wachangie, huku akieleza kuwa wataiandikia barua mamlaka ya chuo cha Ardhi ili waweze kutoa baadhi ya wanafunzi ambao watafanya upimaji katika eneo hilo bure na kuwaondolea wananchi gharama za ziada.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitta amesisitiza kuwa serikali itakuwa bega kwa bega na wananchi wanyonge kuhakikisha haki yao haipotei, huku Diwani wa Kata hiyo akihimiza ushirikiano katika shughuli za maendeleo kwani maendeleo hayana chama, hvyo ni vyema kuondoa itikadi.
Wananchi wa maeneo hayo wameonesha kuridhishwa na uamuzi huo wa serikali na kuhaidi kutoa ushirikiano wa hali na mali, huku wakimpongeza Rais Magufuli kwa serikali yake kujali maslahi ya wanyonge.





Mkuu wa Wilaya ya Kindoni Mhe Ally Hapi akishangiliwa na wananchi mara baada ya kuzungumza nao na kumaliza mgogoro wa muda mrefu wa ardhi katika eneo la Kunduchi Mecco na mji mpya Kata ya Kunduchi ambao hapo mwanza ilidaiwa na Manispaa ya Kinondoni kuwa wamevamia kwakuwa eneo hilo lilikuwa limepangwa kwa ajili ya Machimbo ya Kokoto.


Mkuu wa Wilaya ya Kindoni Mhe Ally Hapi leo ametangaza msimamo wa serikali ya wilaya ya Kinondoni kuwa wananchi wa Kunduchi Mecco na mji mpya Kata ya Kunduchi waliokuwa na hofu ya kuondolewa kuwa hawataondolewa na kwamba badala yake makazi yao yatapimiwa viwanja na watamilikishwa rasmi.

Uamuzi huo umekuja baada ya mvutano wa miaka mingi baina ya manispaa ya Kinondoni na wananchi hao waliovamia eneo hilo ambalo awali lilitengwa kwa ajili ya machimbo ya kokoto. Katika mvutano huo ulioibua kesi mbili zilizoendeshwa kwa muda mrefu na hatimaye manispaa kushinda kesi hizo, uamuzi umefikiwa kuwa Manispaa ya Kinondoni haitawavunjia na kuwaondoa wananchi hao wapatao zaidi ya 3000 waliojenga eneo hilo. Badala yake eneo hilo litapimwa ili kupanga vema mji na kuruhusu maeneo ya huduma za msingi za jamii kama barabara, shule, afya na zahanati kutengewa maeneo.

Akiambatana na Meya wa manispaa hiyo Benjamin Sitta pamoja na Kaimu Mkurugenzi, Mh. Hapi ameeleza kuwa serikali ya wilaya itaendelea kumaliza migogoro ya ardhi wilayani humo na kwamba wananchi waendelee kuiunga mkono na kuipa ushirikiano.Uamizi huo umepokewa kwa shangwe kubwa na wananchi wa Kunduchi walioamua kumuamuru dereva azime gari la DC HAPI na kulisukuma huku wakina mama wakilifuta vumbi kwa kanga kama ishara ya kufurahia uamuzi huo.

“Leo natangaza rasmi uamuzi wa serikali ya wilaya kuwa hamtaondolewa hapa.Badala yake mtapimiwa na kumilikishwa kihalali ili mpewe hati.”
Alisema DC Hapi.

Akishukuru kwa niaba ya wananchi wake, diwani wa kata hiyo Mh. URIO ameishukuru serikali kwa uamuzi huo na kwamba wananchi wake wataendelea kuiunga mkono.

RC RUVUMA AMEAGIZA KUTAIFISHWA KWA MAGARI YOTE YALIYOHUSIKA NA UBEBAJI WA MBAO NA MKAA KINYUME NA SHERIA.

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma dkt.Bilinith Mahenge atoa agizo kwa wiazara ya maliasili mkoa wa Ruvuma kuwachukilia hatua mara moja wale wote wanaohusika na ukataji miti ovyo na uchomaji mkaa ,rai hiyo ameitoa baada ya kukamata gari lilo beba mbao 400 zilizokuwa zinasafirishwa kunyume na sheria .HABARI KAMILI HII HAPA.

SIMBA U20 YAAGA MASHINDANO YA HISANI YA ATF YATOLEWA NA TANZANIA PRISONS KWA PENATI

$
0
0
 Beki wa Simba U20, Jacob Jalala (kulia) akichuana kuwania mpira na mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Mohamed Rashid, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Beki wa Tanzania Prisons, Michael Ismail (kushoto) akijaribu kumpita mchezaji wa Simba U20, Rashid Juma, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1.
 Beki wa Simba U20, Abdallah Rashid (kulia) akichuana kuwania mpira na mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Kassim Hamis, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka 
dakika 90 kwa sare ya 1-1.
******************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Mbeya
TIMU ya Vijana wa Simba chini ya umri wa miaka 20, jana walishinda kuungana na wenzao wa Yanga katika fainali ya Mechi za Hisani kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI baada ya kufungwa na Tanzania Prisons kwa mikwaju ya penati 6-5 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu wa Sokoine jijini Mbeya.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu zote kutoka uwanjani bila kupata bao, huku timu zote zikicheza kwa taadhari na kufanya mashambulizi ya kushitukiza.
Katika mchezo huo Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 69 kupitia kwa mshambuliaji wake, Dadi Mbarouk, baada ya kuwatoka mabeki wa Tanzania Prisons Aron Kalambo, aliyekuwa ametoka golini akijaribu kuwahi kumzuia na  kupishana na mpira uliotinga wavuni.
Bao la kusawazisha la Tanzania Prisons, lilifungwa na Kassim Hamis, kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 79, baada ya mchezaji wa Simba U20, kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari na kufanya dakika 90 kumalizika timu hizo zikiwa sare kwa kufungana 1-1.
Baada ya sare hiyo timu hizo zilikwenda katika hatua ya matuta, ambapo zilipigwa jumla ya penati 8, na Tanzania Prisonswakikosa 2 na kupata penati 6 na Simba wakikosa 3 na kupata penati 5.
Simba wameungana na wenzao Mbeya City Kikosi cha kwanza ambao walitolewa na Kikosi cha Yanga U20 kwa kukubali kichapo cha mabao 3-0 katika mechi hizo za Hisani zilizoandaliwa na Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS, na kushirikisha jumla ya timu Nne za Yanga U20 na Simba U20 kutoka jijini Dar es Salaam, Mbeya City na Tanzania Prisons vikosi vya kwanza Ligi Kuu Bara.
Mchezo wa fainali unachezwa leo jioni kwenye Uwanja huo wa Sokoine kati ya Yanga U20 na Tanzania Prisons.
Akizungumzia matokeo hayo Kocha wa Simba U20, Nico Kiondo, alisema kuwa kwa upande wao hali ya hewa ilichangia kwa kiasi kikubwa kupata matokeo hayo lakini pia maandalizi yao hayakuwa ya kutosha kwani wachezaji wengi ni wageni ndani ya Kikosi chao.
''Kwa kweli hali ya hewa imetugharimu kupoteza mchezo wa leo lakini pia hatukuwa na mazoezi ya kutosha kabla kwani wachezaji wengi ni wageni waliojiunga na timu msimu huu''. alisema Kiondo
Kwa upande wake Kocha wa Tanzania Prisons, Abdalla Mohamed, alisemakuwa timu yake imejitahidi kupata matokeo hayo japo imecheza na kikosi cha pili cha Simba kutokana na timu zote kucheza kwa uangalifu kwani hawakuwa na maandalizi ya kutosha baada ya usajili wa wachezaji wapya ambao wengi wao ndiyo walicheza ili kuwajaribu ili kuona mapungufu, huku wengine wakitarajia kucheza katika mchezo wa leo dhidi ya Yanga.
''Nimeona mapungufu kwa wachezaji wangu na hasa kwa safu ya ushambuliaji, nitayafanyia kazi ili kupata matokeo mazuri katika mechi zijazo kwani wachezaji wangu wengi ni wageni ambao tumewasajili msimu huu bado hawajazoea hali ya hewa, na wengini nitawajaribu katika mchezo wa leo dhidi ya Yanga''. alisema Mohamed
 Kipa wa Tanzania Prisons, Aron Kalambo, akiokoa moja ya hatari langoni kwake wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1.
 Wachezaji wa Tanzania Prisons, wakimdhibiti mshambuliaji wa Simba U20, Abilay Issa, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1.
 Mshambuliaji wa Simba U20, Said Hamis (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Tanzania Prisons, Sharif Shaban, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1.
 Beki wa Simba U20 Erick Costantine (kulia) akijaribu kumzuia mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Cleophace Anthony, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1.
 Kipa wa Mbeya City akidaka mpira katikati ya wachezaji wa Simba.
 Mchezaji wa Simba U20, Abilay Issa (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Tanzania Prisons, Sharif Shaba, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1.
 Wachezaji wa Simba U20 wakishangilia bao lao 
 Beki wa Simba U20, Jacob Jalala (kulia) akichuana kuwania mpira na mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Mohamed Rashid
 Bao la Simba
 Heka heka langoni kwa Simba U20
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images