Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

Asilimia 53 ya Watanzania Wasema Usalama Umeimarika Nchini- Twaweza

$
0
0

Na Alex Mathias

Zaidi ya nusu ya Watanzania wamesema kuwa hali ya usalama nchini imeimarika ikilinganishwa na miaka takriban miwili iliyopita na kuwafanya wananchi waishi kwa utulivu na amani.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la Kiserikali lijulikanalo kama Twaweza, Bw. Aidan Eyakuze wakati akiwasilisha matokeo utafiti wa “Hapa Usalama Tu: Usalama, Polisi na Haki nchini Tanzania” kupitia sauti za wananchi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Bw. Eyakuze alisema kuwa takwimu zilizo kusanywa na sauti za wananchi kwa mwaka huu zimeonesha kuimarika kwa usalama kwa wananchi wa Tanzania Bara ikilinganishwa na miaka iliyopita.
“Tumeongea na watu 1805 kuwauliza hali ya usalama katika maeneo wanayoishi na asilimia 53 ambayo ni sawa na nusu ya Watanzania Bara wamesema hali ya usalama imeimarika na inaridhisha” alisema Bw.Eyakuze.

Bw.Eyakuze amesisitiza kuwa wamekusanya taarifa kutoka kwa wananchi wenyewe, kupitia simu zao za mikononi ambapo wameona kuwa watanzania wengi wapo kwenye hali ya usalama na hii inamewapa taswira tofauti na taarifa zinazotolewa na vyombo vya habari.
Aidha, Bw.Eyakuze amesema kuwa asilimia 47 ya wananchi wanaridhishwa na utendaji kazi wa jeshi la Polisi nchini kutokana na kuzuia na kutatua uhalifu na kuwajali wananchi.

Ripoti hiyo imeonyesha kuwa wananchi wanapata pia ulinzi kutoka kwa polisi jamii, maarufu kama sungusungu na asilimia 41 ya wananchi wamesema wana vikundi vya sungusungu katika maeneo yao na wanaridhika na huduma zinazotolewa.
Utafiti huu ulifanyika mnamo Aprili 2017 ukihusisha mikoa yote ya Tanzania Bara na wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumuia simu za mkononi.

SERIKALI YAWATAKA VIONGOZI WA CHAMA CHA WAFUGAJI NCHINI KUONDOA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

$
0
0

Katibu Tawala Wilaya ya Arusha David Mwakiposa akizungumza leo katika warsha ya siku tatu jijini Arusha iliyowakutanisha watetezi wa haki za wafugaji nchini , mafunzo hayo yanalengo lakuwajengea uwezo watetezi hao ili waweze kuondoa migogoro inayojitokeza katika jamii(Habari Picha na Pamela Mollel Arusha).
Mratibu wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu,THRDC Onesmo Ole Ngurumo alisema kuwa ni vizuri watetezi hao wakajengewa uwezo katika sera ,sheria na mifumo ya utoaji haki katika taifa hili na nje ya Nchi ili waweze kutetea vizuri wafugaji.
Katibu mkuu chama cha wafugaji Tanzania Maghembe Makoye alisema kuwa Tanzania inamifugo na wafugaji wengi hivyo ni muhimu sana sekta hiyo kujengewa uelewa na kujielekeza kuunda mabaraza ya usuluishi katika ngazi ya vijiji,kata,tarafa hadi wilaya ili kuhakikisha kundi hilo haligombani

Makamu Mwenyekiti Taifa Esther Laban Alimuomba Rais Magufuli kuangalia namna ya kuwaelimisha zaidi Washiriki wa semina hiyo wakiwa katika picha ya pamoja leo jijini Arusha kwa semina ya siku tatu



Na Pamela Mollel,Arusha

Serikali imewaomba viongozi wa chama cha wafugaji Tanzania pamojana watetezi wahaki za wafugaji kuhakikisha wanaondoa migogoro ya wafugaji na wakulima ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara Nchini hali ambayo imekuwa ikirUdisha maendeleo nyuma

Akizungumza jijini hapa katika ufunguzi wa warsha ya siku tatu iliyowakutanisha watetezi wa haki za wafugaji nchini ,Katibu Tawala Wilaya ya Arusha David Mwakiposa alisema kuwa lengo la mafunzo hayo nikuwajengea uwezo hao watetezi ili waweze kuondoa migogoro inayojitokeza katika jamii

“Serikali tunaomba sana watetetezi wa haki za wafugaji kuangalia kwa uzito wa kipekee kuondoa migogoro ya wafugaji na wakulima na wahamasishe uwanzishwaji wa viwanda vya kuchakata bidhaa za mifugo ili kumuunga mkono Raisi Magufuli katika sera ya viwanda”Alisema Mwakiposa

Aidha alisema kuwa sekta ya wafugaji na kilimo inaajiri watanzania walio wengi zaidia asilimia 70 na ndio sekta pekee ambayo haiitaji elimu kubwa tofauti na ajira za viwandani na sehemu nyingine hivyo ni muhimu kujengwa uwezo ili kutimiza sera ya viwanda hapa nchini

Kwa upande wake mratibu wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu,THRDC Onesmo Ole Ngurumo alisema kuwa ni vizuri wakajengewa uwezo katika sera ,sheria na mifumo ya utoaji haki katika taifa hili na nje ya Nchi ili waweze kutetea vizuri wafugaji

“Tunaamini kuwa watetezi hawa wakifahamu vizu sera na sheria wataweza kuangalia mifumo ya utoaji haki kama haitendeki kwa wafugaji wataweza kutumia fursa hiyo kuwatetea vizuri”

Katibu mkuu chama cha wafugaji Tanzania Maghembe Makoye alisema kuwa Tanzania inamifugo na wafugaji wengi hivyo ni muhimu sana sekta hiyo kujengewa uelewa na kujielekeza kuunda mabaraza ya usuluishi katika ngazi ya vijiji,kata,tarafa hadi wilaya ili kuhakikisha kundi hilo haligombani

“Nivizuri tukihamasishana kufuga kisasa ili kujiongezea tija katika uzalishaji wa bidhaa za wafugaji sanjari na kupata masoko ndani na nje ya nchi “

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO NA VYOMBO VYA HABARI NCHINI

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Radio ya Efm Bw. Francis Ciza wakati wa ziara yake  kutembelea chombo hicho cha habari leo Jijini Dar es Salaam.
Pix 2
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na watumishi wa Radio ya Efm (hawapo katika picha) alipofanya ziara ya kutembelea chombo hicho cha habari leo Jijini Dar es Salaam.
Pix 3
Watumishi wa Radio ya Efm wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo katika picha) alipotembelea chombo hicho cha habari leo Jijini Dar es Salaam.
Pix 4
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Radio ya Efm pamoja na watendaji wa Wizara ya Habari wakati wa ziara yake leo Jijini Dar es Salaam
Pix 5
Katibu Mkuu Wizara Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akiongea na Viongozi wa  Radio One na ITV  alipofanya ziara yake IPP Media  leo Jijini Dar es Salaam kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji Radio One na ITV Bi. Joyce Mhaville.
Pix 6
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa ITV/Capital Tv Bw. Koigi Wacharia  wakati wa ziara yake kutembelea Chombo hicho cha Habari leo Jijini Dar es Salaam.
Pix 7
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyekaa) pamoja na watendaji wa Wizara ya Habari wakiangalia namna mfumo wa urushwaji wa habari unavyofanya kazi katika studio za ITV wakati wa ziara yake leo Jijini Dar es Salaam.
Pix 8
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyekaa kushoto ) akiwa katika picha ya  pamoja na viongozi wa Radio One/ITV na  watendaji wa Wizara ya Habari  wakati wa ziara yake leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Genofeva Matemu – MAELEZO
…………………………
Na Lorietha Laurence-WHUSM
Serikali imeeleza kuwa inathamini na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Vyombo vya Habari nchini katika kuhakikisha kuwa jamii inapata taarifa sahihi na kwa wakati.
Akizungumza katika ziari yake alipotembelea vyombo vya habari vya Radio EFM na Radio One/ ITV leo Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema kuwa lengo kubwa la Serikali ni kuwepo kwa ushirikiano mzuri na sekta ya habari nchini.
“Lengo la ziara hii ni kuimarisha uhusiano baina ya Serikali na vyombo vya habari pamoja na kufahamu utendaji wenu wa kazi na namna mnavyosimamia maudhui ya vipindi vyenu mnavyoviandaa” amesema Prof. Gabriel
Aidha aliongeza kuwa ni jambo jema linalofanywa na watanzania wazawa kuwekeza katika sekta ya habari kwa kuwa dunia ya sasa imetawaliwa na utandawazi kupitia taarifa mbalimbali zinazotolewa zenye lengo la kuhabarisha na kujenga taifa letu. 
Kwa upande mwingine Prof. Gabriel amewataka watumishi wa vyombo hivyo vya habari kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, weledi na uzalendo ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Pia amewataka watumishi wa vyombo hivyo vya habari kujenga utamaduni  wa kufanya kazi kwa kujituma ili kupata matokeo chanya katika soko la ushindani na kuifikia jamii kubwa zaidi katika kutoa habari za uhakikia na zenye usahihi.
Sambamba na hilo Prof. Gabriel amevitaka vyombo hivyo vya habari kuzingatia maudhui yanayoendana na jamii ya kitanzania pale wanapoandaa vipindi mbalimbali ili kujenga jamii yenye utamaduni mzuri ikiwemo kufanya kazi kimkakati.
Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Redio  Efm, Bw. Denis Ssebo amesema kuwa uongozi wa radio yake upo tayari kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na Serikali lengo likiwa ni kuhakikisha wanafuata sheria na kanuni za utangazaji ili kufanya kazi kwa kiwango chenye ubora .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Radio One/ITV Bibi. Joyce Mhaville ameishukuru serikali kupitia wizara ya Habari kwa kuonyesha ushirikiano mzuri na vyombo vya habari ikiwemo kufanya kazi kwa karibu na  kuviwezesha vyombo hivyo  kupata habari zenye ukweli na uhakika.

WANAHABARI WAJADILI UMUHIMU WA UHIFADHI NA UJIRANI MWEMA JIJINI TANGA

$
0
0
--
 Mkurugenzi wa Utalii na Masoko  kutoka Hifadhi za Taifa Tanzania, Ibrahim  Mussa akizungumza wakati wa Mjadala juu ya uhifadhi katika Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'. 
 Mtaalam na Mtafiti wa Tembo,Dk Alfred Kikoti  akizungumza na Wahariri na Waandishi Waandamizi wa Vyombo  mbalimbali vya habari nchini  kuhusu Ikolojia ya tembo katika hifadhi nchini katika Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'. 

 Mwenyekiti wa MisaTan , Salome Kitomari  akichangia jambo katika moja ya mada katika Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'. 
 Ofisa anaeshughulikia masuala ya Ujirani mwema kutoka TANAPA, Ibrahim Ninga akitoa somo kwa Wanahabari nini Mamlaka yake imefanya katika kuakikisha hakuna migogoro baina ya hifadhi na Majirani
 Sehemu ya Wahariri na Waandishi Waandishi waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari  ambao wameshiriki mkutano wa Mwaka wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Nchini Jijini Tanga
Mhariri wa MwanaHalisi ,Jabir Idrissa akiuliza swali kwa wawezeshaji wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) Jijini Tanga.
 Katibu wa Jukwaa la Wahariri , Neville Meena  akinyosha Mkono kwa ajili ya kuhitaji kuchangia juu ya nini kifanyike hili Waandishi wa habari waweze kuripoti habari za utalii wa hapa nchini katika nyanja ya kimataifa.
 Mwenyekiti wa MisaTan , Salome Kitomari  akichangia jambo katika moja ya mada katika Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'. 
 Ofisa anaeshughulikia masuala ya Ujirani mwema kutoka TANAPA, Ibrahim Ninga akitoa somo kwa Wanahabari nini Mamlaka yake imefanya katika kuakikisha hakuna migogoro baina ya hifadhi na Majirani
 Mhariri wa gazeti la Jamhuri ,Jackton Manyerere akichangia juu ya umuhimu wa wadau wa utalii sasa kutumia mkoa wa mara ambao upo jirani na Hifadhi ya serengeti utumike kama kituo cha kupokelea Watalii kuliko Arusha hivi sasa
 Mdau Lilian Timbuka na Sara Kibonde wakaijadili jambo mara baada ya kukutana kwenye mkutano wa Wahariri na waandishi waandamizi.
 Mratibu wa mradi Misitu ya Hifadhi ya Mazingira  Asilia Tanzania, Gerald Kamwenda akiteta jambo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania(TFS) ,Prof Dos Santos Silayowakati wa Mkutano wa Mwaka wa Wahariri na Waandishi Waandamizi Jijini Tanga ulioandaliwa na Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA)
Washiriki wengine wakifatilia Mada katika Mkutano wa Mwaka  wa Wahariri wa Waandishi Waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya Habari ulioandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA).

JAFO AFURAHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI IHUNGO.

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akifanya ukaguzi wa miundombinu inayojengwa katika Shule ya Sekondari Ihungo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika ukaguzi wa ujenzi wa madarasa na mabweni katika Shule ya Sekondari Ihungo.
Jengo la bweni linalojengwa katika shule ya Sekondari Ihungo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akikagua majengo yanayojengwa katika Shule ya Sekondari Ihungo.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya Sekondari ya Omumwani wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo

………………………………..

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo amefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa shule ya wavulana ya kidato cha tano na sita ya Ihungo ambayo majengo yake yalibomoka kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea mwaka Jana.

Kutokana na kubomoka kwa majengo hayo, Serikali iliamua kuijenga upya kwa kutumia wakala wa majengo Tanzania (TBA). Akiwa katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali mkoani Kagera, Jafo alitembelea shuleni hapo kukagua ujenzi wake.

Naibu Waziri Jafo aliwapongeza wakandarasi kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya ambapo kazi hiyo inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Agosti. Akizungumza na wananchi waliokuwepo katika eneo hilo, Jafo alisema serikali imeamua kuijenga sekondari hiyo kisasa zaidi. Alisema sekondari hiyo inatarajiwa kuwa sekondari ya mfano ndani ya Tanzania kwa kuwa na majengo ya kisasa zaidi kuliko sekondari zote hapa nchini.

Hata hivyo, Jafo alitoa angalizo kwa sekondari hiyo kubaki kuwa sekondari ya wavulana kwani kutokana na uzuri wa miundombinu ya kisasa inayojengwa isije baadae wakaja watu na kubadilisha mawazo kuwa Chuo kikuu jambo ambalo sio sahihi.

Alibainisha serikali imejipanga kuimarisha ubora wa elimu ya sekondari kwasasa. Katika ziara hiyo, Jafo pia alitembelea shule ya Omumwani ambayo imeanza kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano ambao ni wasichana kwa mwaka huu. Alitoa maagizo kwa manispaa ya Bukoba kumalizia ukarabati wa maabara ndani ya wiki mbili zijazo ili kuwawezesha wanafunzi kufanya vyema zaidi katika masomo yao kivitendo.

PROF. MAGHEMBE ATAMBUA MCHANGO WA VYOMBO VYA HABARI KATIKA VITA DHIDI YA UJANGILI NCHINI

$
0
0
NA HAMZA TEMBA - WMU

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amevipongeza vyombo vya habari nchini kwa mchango wake katika vita dhidi ya ujangili huku akitoa rai kwa vyombo hivyo kuongeza bidii katika kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa uhifadhi endelevu wa maliasili za taifa kwa faida ya jamii iliyopo na vizazi vijavyo.

Prof. Maghembe ametoa pongezi na rai hiyo leo wakati akifungua mkutano wa sita wa mwaka wa wahariri na wanahabari waandamizi wa vyombo vyote vya habari nchini ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) jijini Tanga huku kaulimbiu ya mkutano huo ikiwa UTALII WA TANZANIA YA UCHUMI WA VIWANDA.

"Ujangili bado upo, Majangili tumepambana nao kweli kweli, na ninyi wanahabari mmetusaidia sana katika kuhabarisha jamii juu ya matukio ya kukamatwa kwao na hukumu wanazozipata, jambo ambalo limesaidia kujenga uoga kwa watu kushiriki katika vitendo hivyo", alisema Maghembe.
Alisema hofu hiyo pamoja na jitihada za Serikali za kupambana na ujangili imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matukio ya ujangili nchini hasa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita ambapo mizoga ya tembo inayotokana na ujangili imeonekana kupungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha ni miaka iliyopita.

Akizungumzia changamoto ya mifugo kwenye maeneo ya hifadhi nchini amesema sheria za uhifadhi zinakataza watu kuingiza mifugo kwenye maeneo yaliyohifadhiwa kisheria, hivyo ni wajibu kwa wanahabari kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kutii sheria hizo.  "Ni vema wanahabari wakatumia kalamu zao vizuri kuelimisha jamii juu ya athari za muingiliano wa binadamu, mifugo na wanyamapori".

Alisema wanyamapori wanabeba virusi vya magonjwa mbalimbali ikiwemo homa ya bonde la ufa, ndigana, kifua kikuu, homa za vipindi (brucolosis) na kimeta, Magonjwa ambayo yanaweza pia kuambukiza mifugo na binaadamu wanaoishi karibu na wanyamapori. Alisema kuwa endapo muingiliano huo utaendelea kuwepo kwa muda mrefu unaweza kusababisha mlipuko mkubwa wa magonjwa hayo kwa binaadamu na mifugo hivyo kusababisha vifo vingi kwa wakati mmoja.

Prof. Maghembe alisema kumekuwepo na kisingizio cha kumega maeneo ya hifadhi nchini kwa ajili ya matumizi ya kawaida kutokana na ongezeko la wananchi jambo ambalo sio sahihi na kwamba njia pekee na salama ni kubadili mfumo wa matumizi ya rasilimali zilizopo ikiwepo ya ardhi kwa kutumia sayansi na teknolojia na kuweka matumizi bora ya ardhi kwa kulenga matokeo chanya.

Akizungumzia sekta ya utalii, Prof. Maghembe alisema wanahabari wanapaswa kuwa sehemu ya kukuza uchumi wa nchi kwa kushiriki moja kwa moja katika utoaji wa taarifa sahihi kwa Watanzania na wageni kuhusu sekta hiyo bila ubaguzi wa aina yeyote.

"Tuipende nchi yetu, tuitangaze na kuilinda, na katika habari hizi za uchumi tuweke itikadi zetu pembeni tuandike habari za kujenga nchi yetu", alisema Prof. Maghembe.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa, Alan Kijazi amesema sekta ya utalii inachangia asilimia 17.2 ya pato la taifa na asilimia 25 ya mapato yote ya fedha za kigeni. Alisema asilimia 80 ya wageni wanaokuja nchini wanatembelea hifadhi za Taifa hususan za ukanda wa Kaskazini jambo ambalo linaweka msukumo wa kuendeleza na kutangaza hifadhi za nyanda zingine ili kuongeza idadi ya watalii na pato la taifa.

Akizungumzia mchango wa TANAPA katika uchumi wa taifa, Kijazi alisema mchango huo umeongezeka ambapo katika mwaka 2015/2016 shirika hilo lilichangia Shilingi bilioni 27 katika mfuko mkuu wa Serikali na mwaka 2016/2017 likachangia bilioni 34 sawa na ongezeko la bilioni saba.

Pamoja na mafanikio hayo alisema jukumu la kuendeleza uhifadhi nchini haliwezi kufanikiwa kwa jitihada za Serikali pekee bila kushirikisha wananchi kupitia vyombo vya habari, Hivyo akatoa rai kwa wanahabari kuiunga mkono Serikali katika kunadi sera za uhifdhi endelevu kwa maslahi ya taifa.

BARAZA LA MADIWANI KISHAPU MKOANI SHINYANGA WAPONGEZWA KWA HATUA YA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO KWA UFANISI PAMOJA NA CHANGAMOTO ZA UHABA WA FEDHA

$
0
0
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Boniphace Butondo akizungumza wakati akifungua kikao cha Baraza la Madiwani la kupokea na kujadili tarifa za kata za robo ya nne ya mwaka. Wengine pichani kushoto ni Makamu mwenyekiti wa halmashauri, Edward Shigela na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Stephen Magoiga.

Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza wakati wa kikao hicho. Wengine pichani kuanzia kushoto ni Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kangese, Makamu mwenyekiti wa halmshauri, Edward Shigela na Mwenyekiti Boniphace Butondo.

Madiwani na wataalamu kutoka halmashauri hiyo wakifuatilia kikao hicho cha kupokea na kujadili tarifa za maendeleo ya kata.

Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akizungumza neno wakati wa kikao hicho.

Makamu mwenyekiti wa halmshauri, Edward Shigela akizungumza wakati akifunga kikao hicho.

Madiwani na wataalamu kutoka halmashauri hiyo wakifuatilia kikao hicho cha kupokea na kujadili tarifa za maendeleo ya kata.


………………………………


Na Robert Hokororo

Halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imepongezwa kwa hatua yake ya utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo kwa ufanisi pamoja na changamoto za uhaba wa fedha.

Pongezi hizo zimetolewa leo na mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Boniphace Butondo wakati akifungua kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi kupokea taarifa za kata kwa kipindi cha robo ya nne ya mwaka.Butondo alisema miradi hiyo imetekelezwa kwa kiwango kizuri pamoja na changamoto ya uhaba wa fedha iliyoikabili halmashauri hiyo kwa kipindi hicho.

Alisema ushirikianoa baina ya madiwani na wataalamu kutoka halmashauri hiyo ndiyo siri ya mafanikio hayo ambayo ni tija kwa wananchi wanaowahudumia.Aidha, aliwapongeza wataalamu hao kutoka idara mbalimbali kwa kuwa na usimamizi mzuri ikiwemo wa fedha na maeneo ambayo miradi hiyo inatekelezwa na kuwataka waendelee kushikamana.

“Naomba niwapongeze wote kwa ushirikiano mkubwa mnaounesha najua kuna changamoto ya kuwa na mapato kidogo kutokana na hali ya hewa na hivyo kuchangia kutopata pamba kwa wingi ambayo inaingiza mapato halmashauri,” alisema.

Mwenyekiti huyo ambaye pia ni diwani wa kata ya lagana aliishukuru ofisi ya mkuu wa wilaya kwa ushirikiano mkubwa kwa halmashauri na hivyo kuchangia mafanikio hayo.

Tayari miradi mbalilimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa, zahanati, barabara na maji imetekelezwa katika kata mbalimbali za halmashauri ya wilaya hiyo.

DC Babati awataka wakulima kuunga mkono jitihada za watafiti wa mbegu

$
0
0


Mratibu wa Mradi wa WEMA, na Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti Ilonga, Dk. Justin Ringo (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Babati, Raymond Mushi (kulia) juu ya shamba la majaribio ya mbegu chotara za mahindi zinazostahimili magonjwa na ukame (WEMA), katika moja ya shamba la utafiti shirikishi lililopo Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati walipotembelea Mtafiti wa Mradi wa WEMA, Ismail Ngolinda (kulia) akimtembeza mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Babati, Raymond Mushi (kushoto) ndani ya shamba la majaribio katika moja ya shamba la utafiti shirikishi lililopo Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati walipotembelea. Mkuu wa Wilaya ya Babati, Raymond Mushi akitembelea shamba la majaribio ya mbegu chotara za mahindi zinazostahimili magonjwa na ukame (WEMA), katika moja ya shamba la utafiti shirikishi lililopo Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati walipotembelea. Mtafiti wa Mradi wa WEMA, Ismail Ngolinda (kwa kwanza kulia) akijibu maswali ya baadhi ya wakulima ndani ya shamba la utafiti shirikishi lililopo Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati walipotembelea Mahindi ndani ya shamba la utafiti shirikishi na wakulima la Mradi wa WEMA lililopo Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati.
Mjumbe wa Kamati ya Mawasiliano na uratibu Mradi wa WEMA, Bw. Temu akizungumza kwenye maadhimisho hayo. Mratibu wa Mradi wa WEMA, na Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti Ilonga, Dk. Justin Ringo akijibu maswali ya wakulima (hawapo pichani) mara baada ya kutembelea shamba la utafiti shirikishi wa mbegu chotara za mahindi zinazostahimili ukame na magonjwa (WEMA) Katibu Tawala wa Wilaya ya Babati, Cade Mshamu (wa pili kulia) akizungumza na wakulima na watafiti wa Mradi wa utafiti mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame na magonjwa (WEMA), katika maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati. Baadhi ya wakulima na wageni anuai wakiwa katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati Mkulima akiuliza swali kwa watafiti katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati. Mkuu wa Wilaya ya Babati, Raymond Mushi (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Maendeleo ya Utafiti kutoka Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Jackson Nkuba (kulia) kwenye hafla hiyo Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Shabaan Husein (kulia) akizungumza kwenye hafla hiyo.[/caption] Na Joachim Mushi, Babati MKUU wa Wilaya ya Babati, Raimond Mushi amewataka wakulima kufuata maelekezo ya wataalamu wa kilimo wakiwemo watafiti wa mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame, magonjwa (WEMA) ili waweze kuendesha kilimo chenye tija na kuachana na kilimo cha kujikimu ambacho hakiwezi kuwapa maendeleo.


Mkuu wa Wilaya ya Babati, Raymond Mushi akizungumza na wakulima na watafiti wa Mradi wa utafiti mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame na magonjwa (WEMA), katika maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini, wilayani Babati
 
 Alisema kilimo cha sasa kinapaswa kuendeshwa kisayansi na kufuata ushauri wa kitaalamu, ambapo ni pamoja na kutumia mbegu bora zilizofanyiwa utafiti kulingana na mahitaji ya maeneo ya wakulima. Mh. Mushi ametoa ushauri huo mjini Babati alipokuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Wakulima wilayani Babati ambapo pia alitembelea shamba la utafiti shirikishi wa mbegu za mahindi unaotekelezwa na watafiti kutoka Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kwa ushirikiano na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia mradi wa utafiti wa mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame na magonjwa (WEMA). 
 
Alisema wakulima wakitaka kufanya kilimo cha manufaa hawana budi kutumia mbegu zilizofanyiwa utafiti na kupendekezwa na wataalamu wa kilimo kutumika katika maeneo yao. "...Tuwe macho na mbegu tunazonunua ili tuweze kuvuna mazao ya kutosha, wakulima sasa lazima tubadilike tusiendeshe kilimo cha kujikimu tu...mkulima huwezi kuendelea kwa kufanya kilimo cha kujikimu, tunataka ulime upate chakula na ziada kisha uuze mazao kukuza uchumi wako na ubaki na akiba," alisema Raimond Mushi. 
 
Alisema serikali ya awamu ya nne imedhamiria kufanya uchumi wa viwanda hivyo wakulima wanakila sababu ya kufanyia kazi ushauri wa wataalamu wa kilimo ili waweze kuzalisha mazao ya kutosha yatakayotumika kama mazao ghafi kwenye viwanda na kunufaika zaidi. "Tunapolima sasa tulime kisayansi na kwa malengo, tutumie maeneo yetu vizuri ili tuweze kuzalisha mazao ya kutosha," alisisitiza Mkuu wa Wilaya, Raimond Mushi na kuongeza eneo la kilimo kwa sasa linapungua kutokana na ongezeko la idadi ya watu nchini hivyo kuna kila sababu ya kutumia eneo dogo linaloleta matokeo makubwa na manufaa kwa mkulima.
 
 Alisema serikali imedhamiria kuleta mabadiliko kwa wakulima ndio maana inawawezesha wataalamu kama WEMA na kuwaunga mkono shughuli za utafiti kwa maendeleo ya wananchi hawa wakulima. "Sisi hapa Babati tunangoja kwa hamu matokeo ya utafiti ili tuweze kuyafanyia kazi...tuleteeni mapema tutasimamia na kuhamasisha wakulima wetu kutumia mbegu za WEMA," alisema. 
 
Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Maendeleo ya Utafiti kutoka Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Jackson Nkuba alisema Serikali ipo tayari kushirikiana na makampuni yatakayojitokeza kuzalisha mbegu za WEMA na zingine bora zinazofanyiwa utafiti ili wakulima wazipate kirahisi, hivyo kutoa rai kujitokeza kwa wingi. Awali Mkuu wa Wilaya ya Babati, Bw. Mushi, viongozi mbalimbali katika tukio hilo wakiwemo wakulima kwa pamoja walitembelea shamba la utafiti shirikishi wa mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame na magonjwa (WEMA) lililopo Mtaa wa Maisala Kata ya Babati Mjini na kujionea mbegu zilizofanyiwa utafiti wa WEMA na kujionea matokeo ya utafiti.

VIDEO: Harmonize – Sina

Bagumako: Mamilioni ya Biko nimeyavulia kofia

$
0
0
Mratibu wa Matukio na Mawasiliano, Hassan Melles kulia akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wao wa droo ya 26 ya Biko, Leonard Bagumako wa pili kutoka kulia. Wengine pichani ni baba mlezi wa Bagumako, Gerlad Madaraka kushoto pamoja na mtumishi wa NMB, Tawi la Bank House, jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSHINDI wa Sh Milioni 20 kutoka Bahati Nasibu ya Biko, Leonard Bagumako, amesema ameyavulia kofia mamilioni ya Biko, baada ya kukabidhiwa huku akiwa hakufahamu lolote kwamba yeye angeweza kuyatwaa.

Bagumako aliyasema hayo jana wakati anakabidhiwa fedha zake jumla ya Sh Milioni 20, katika benki ya NMB, jijini Dar es Salaam, huku akiwa kijana mwenye umri wa miaka 21 tu anayefanya shughuli za uuzaji wa duka Kigamboni.

Mratibu wa Matukio na Mawasiliano, Hassan Melles kulia akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wao wa droo ya 26 ya Biko, Leonard Bagumako katikati. Kushoto ni baba mlezi wa Bagumako, Gerlad Madaraka. Picha na Mpigapicha wetu.

Akizungumzia fedha hizo, Bagumako alisema awali aliamini kuwa mchezo wa Biko unahusu watu matajiri, lakini baada ya kukabidhiwa fedha hizo, ameamini kila Mtanzania bila kuangalia wapi anaishi na uchumi wake anaweza kuibuka kidedea kwa kupata ushindi.

“Biko nimewavulia kofia kwa sababu kumbe hata sisi mafukara tunaweza kushinda zawadi mbalimbali za biko kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja za papo kwa hapo, bila kusahau ushindi mnono wa Sh Milioni 20 kama niliyoupata mimi,” Alisema.

Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema baada ya kumkabidhi Bagumako fedha zake, wanashauku kubwa ya kumkabidhi mtu mwingine Milioni 20 atakayetokana na droo ya 27 itakayofanyika Jumapili, jijini Dar es Salaam.

“Bagumako ameshapata fedha zake na mwingine atapokea kutoka droo kubwa ya Jumapili, ambapo Biko tunaamini yoyote anaweza kuibuka na ushindi huo mnono kwa kucheza biko kwa mitandao ya simu Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kwa kufanya miamala kuanzia Sh 1,000 na kuendelea ambapo namba yetu ya kampuni ni 505050 na kumbukumbu ni 2456.

“Namna ya kucheza ni rahisi kwa sababu mshiriki atafanya muamala kulingana na matakwa ya mtandao wake, huku kiasi cha Sh 1,000 kikiwa na nafasi mbili, ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 20 inayofanyika Jumapili na Jumatano,” Alisema.

Kwa kipindi cha miezi miwili ya Mei na Juni, tayari bahati nasibu ya Biko, wameshatoa zaidi ya Sh Bilioni moja kwa washindi wa papo kwa hapo na donge nono la Sh Milioni 20 linalotoka kila Jumatano na Jumapili.

DKT. PHILIP MPANGO ABAINI BAADHI YA WAFANYABIASHARA DODOMA HAWATUMII IPASAVYO EFDs

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akikagua mashine ya EFD na risiti ya kieletroniki aliyopewa baada ya kununua bidhaa kwenye moja ya maduka mjini Dodoma, alipofanya ziara ya kushitukiza kukagua kama wafanyabiashara wa mji huo wanatumia ipasavyo mashine hizo.
Kiongozi wa Timu Maalumu ya Ukaguzi wa Mashine za EFD’s kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Dodoma, Bw. Godfrey Patrick (wa pili kushoto) akifafanua jambo wakati wa ziara ya kushitukiza iliyofanywa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), kwenye maduka mjini Dodoma.
Mfanyabiashara wa duka la rejareja mjini Dodoma, Bw. Donald Chami, akimwonesha mashine ya kieletroniki ambayo imeharibika, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), baada ya kufanyaziara ya kushitukiza kwenye duka lake na kubaini kuwa hatoi risiti za kielektroniki kwa wateja wake.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akipitia kwa makini fomu ya makadirio ya kodi iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika moja ya duka la vipodozi mjini Dodoma wakati alipofanya ukaguzi wa matumizi ya mashine za EFD’s katika baadhi ya maduka yaliyopo mjini humo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akimuonya mfanyabishara wa mjini Dodoma, Bw. Isdori Shirima, baada ya kukuta akiuza bidhaa bila kutoa risiti za kielektroniki kwa wateja wake inavyotakiwa na kuagiza Mamlaka ya Mapato mkoani humo kufanya ukaguzi wa kina ili kubaini kiwango cha ukwepaji kodi cha mfanyabiashara huyo na kumchukulia hatua za kisheria.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akikagua risiti ya mteja aliyenunua tanki la kuhifadhia maji katika moja ya duka linalouza vifaa vya ujenzi mjini Dodoma, na kutoa wito kwa wananchi kukagua risiti zao ili kubaini kama kiwango kilichoandikwa kinalingana na kiasi kilichoandikwa kwenye risiti.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akimwelekeza mwananke mmoja aliyemkuta dukani akague risiti yake baada ya kufanya manunuzi kwenye duka moja la vifaa vya ujenzi mjini Dodoma, alipofanyaziara ya kushitukiza ili kubaini namna wafanyabiashara wa maduka mjini humo wanavyotumia mashine za kielektroniki za kutolea risiti. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akimuagiza Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Dodoma, Bw. Ngaka Magere, kumkutanisha na mawakala wanaosambaza mashine za kieletroniki za kutolea risiti mkoani humo baada ya kutoridhishwa na huduma zao.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akisikiliza maelezo ya matumizi ya mashine za kielektroniki kutoka kwa mfanyakazi wa Kituo kimoja cha Mafuta mjini Dodoma, alipofanyaziara ya kushitukiza kituoni hapo kuangalia matumizi ya mashine hizo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akikagua risiti na kupata maelezo kutoka kwa mhudumu wa Kituo cha Mafuta cha ORYX mjini Dodoma, Bi. Hanifa Shaldin, alipofanya ziara ya kushitukiza kuangalia kama vituo vya mafuta mjini humo vimefungwa mashine za kielektroniki za kutolea risiti kwa wateja wao. (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM).

SHUGHULI MBALIMBALI ZA UVUVI WA SAMAKI PWANI YA TANGA MAPEMA LEO.

$
0
0
 Wachuuzi wa Samaki  wakiwa wanaelekea ndani ya Maji kwa ajili ya kununua Samaki maarufu kwa jina la Uono, ambao unapendwa sana katika mji wa Tanga kwa ajili ya kulia Ugali na kutafuna wakati wa chai asubuhi
 Wachuuzi wa Samaki wakichangamkia Samaki katika moja ya jahazi lililoingia na mzigo kutoka  katika kina kirefu mara baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu
 Mchuuzi wa Samaki akingia katika maji kwa ajili ya kununua Samaki katika Majahazi yaliyofika katika ufukwe wa Sahare
 Mchuuzi wa Samaki akingi katika maji kwa ajili ya kununua Samaki katika Majahazi yaliyofika katika ufukwe wa Sahare
 Wavuvi wakiondoka kwenda kuvua mapema leo Asubuhi katika pwani ya Jiji la Tanga
 Mchuuzi wa Samaki akingi katika maji kwa ajili ya kununua Samaki katika Majahazi yaliyofika katika ufukwe wa Sahare
 Mkazi wa Jiji la Tanga akichagua Samaki kutoka wauzaji wa soko la Sahare jijini Tanga












HIZI NDIZO SABABU KWANINI BAADHI YA VIVUTIO VYA UTALII HATUVITANGAZI -TANAPA

$
0
0
Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa TANAPA,Bwa.Ibrahim Mussa akifafanua mambo mbalimbali ukiwemo moja ya mjadala kuwa ni kwanini Tanzania ina vivutio vingi lakini havitangazwi,Mkurugenzi huyo ameyazungumza mapema leo kwenye Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika jana kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.  

NIC YATOA ELIMU YA BIMA KWENYE MAONYESHO YA 12 YA TCU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Baadhi ya wakazi wa jijini Dar es Salaam, wakipewa maelezo na Afisa Mwanadamizi wa Shirikala Bima la Taifa(NIC) Konjeta Mwaipopo juu ya namna ya kujiunga na huduma za bima wakati walipotemblea banda la Shirika hilo, kwenye maonesho ya 12 ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkazi wa Dar es Salaam, ambaye ni mjasiriamali Manoko Marikishua (kushoto) akipewa maelezo na Afisa Bima wa shirika la Bima la Taifa (NIC)) juu ya bima ya mazao wakati alipofika kwenye banda la Shirika hilo, kwenye maonesho ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam,wakipata maelezo juu ya huduma za bima toka kwa Afisa Bima wa Shirikala Bima la Taifa (NIC)) wakati walipofika kwenye banda la Shirika hilo, kwenye maonesho ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam









TIMU YA RIADHA CHINI YA MIAKA 17 YAREJEA NCHINI NA MEDALI YA SHABA.

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akimpongeza mwanariadha Francis Damas leo katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa kupata ushindi wa medali ya shaba baada ya kushinda mbio za mita 3000 katika mashindano ya Jumuiya ya madola chini ya miaka 17 yaliyomalizika hivi karibuni huko nchini India.
  Katibu Mkuu chama cha Riadha nchini Bw. Filbert Bayi (aliyesimama) akizungumza  na wanariadha na wadau wa mchezo huo mara baada ya timu ya riadha ya vijana chini ya miaka 17 kurejea nchini na medali ya shaba katika mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyoalizika hivi karibuni huko  chini India.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea Bendera ya Tanzania kutoka kwa  mwanariadha  Regina Mpigachai mara baada ya kurejea nchini na ushindi wa medali ya shaba katika mashindano ya Jumuiya ya madola chini ya miaka 17 yaliyomalizika hivi karibuni huko nchini India.Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi msaidizi wa maendeleo ya michezo wa Wizara hiyo Bw. Alex Nkenyenge.
Mkuu wa Msafara na mwalimu wa wanariadha Bibi Mwinga Mwanjala akitoa neno la shukrani  mara baada ya kurejea nchini na  ushindi wa medali ya shaba katika mashindano ya Jumuiya ya madola chini ya miaka 17 yaliyomalizika hivi karibuni huko nchini India.

Na Shamimu Nyaki –WHUSM.
Timu ya riadha ya vijana chini ya miaka 17 imeleta heshima kubwa kwa nchi yetu baada ya kurejea na medali ya shaba aliyoshinda kijana Francis Damasi katika  mbio za mita 3000 kwenye mashindano ya  Jumiya ya Madola yaliyomalizika hivi  karibuni huko nchini India.

Timu hiyo iliyorejea nchini leo imepokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ambapo  ameeleza kufurahishwa na matokeo hayo mazuri waliyopata wanariadha hao ambao wameitangaza vyema Tanzania.

“Vijana mmefanya vizuri sana katika mashindano haya Serikali tunawapongeza sana  kwa kuitangaza nchi yetu lakini pia kwa kuonyesha uzalendo wa hali ya juu katika mashindano haya nawaahidi kuendelea kushirikiana na uongozi na wadau wa riadha nchini ili tufike mbali zaidi” Alisema Prof. Elisante Ole Gabriel.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa chama cha riadha nchini Bw. Filbert Bayi  amesema kuwa mchezo wa riadha kwa sasa ni mchezo ambao umeitangaza Tanzania kwa kiasi kikubwa kutokana na kushiriki  mashindano mengi ya Kimataifa hivyo ni vyema wadau wakajitokeza kwa wingi kuwekeza katika mchezo huo ambao umeendelea kuletea heshima Taifa.

“Riadha imeitangaza Tanzania na itaendelea kuitangaza hivyo wadau wanapaswa kuona fursa hii na kuwekeza katika mchezo huu ili ufike mbali,kila mtu katika eneo lake aone fursa hii na aitumie kwa manufaa ya kizazi hiki na kitakachokuja” Alisema Bw. Bayi.

Naye Kijana Francis Damian aliyepata medali hiyo baada kushinda mbio za mita 3000 ameeleza kufurahishwa na ushindi huo kwani alijiandaa na alizingatia maelekezo ya walimu wake yaliyompelekea kupata ushindi huo na ameshauri vijana kama yeye kuthubutu na kuamini kuwa wanaweza kwani mchezo huo ni mzuri na una mafanikio makubwa.

Medali ya shaba katika mahindano ya riadha  iliyoletwa na kijana Francis imerejea tena baada ya miaka 19 tangu Tanzania ilivoshinda medali hiyo mwaka 2008.

SIMIYU KUNUFAIKA NA MRADI MKUBWA WA MAJI KUTOKA ZIWA VICTORIA KWA UFADHILI WA MFUKO WA MABADILIKO YA TABIANCHI

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora akifungua mkutano wa wadau wa Utekelezaji wa Mradi wa Maji Simuyu. Mradi huo mkubwa uko katika hatua za mwisho kabla ya kuanza kutekelezwa. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Eng. Emmanuel Kalobelo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Eng. Emmanuel Kalobelo akifunga kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora.
Katibu Mkuu Prof. Faustin Kamuzora (watatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi wanaohusika na utekelezaji wa Mradi wa maji wa Simiyu mara baada ya ufunguzi wa kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma.

Na Lulu Mussa, Dodoma.

Serikali ya Tanzania kupitia Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi (Green Climate Fund) imepata fedha za kutekeleza mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi Mkoa wa Simiyu ambapo fedha za Mradi huo zitapitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW).

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora wakati wa kikao kazi kilichojumuisha wadau wanaohusika na utekelezaji wa Mradi wa maji wa Simiyu, mradi unaofadhiliwa na Mfuko wa mabadiliko ya tabianchi ambapo imebainika kuwa utekelezaji wake utaanza mara moja.

Aidha, Prof. Kamuzora amesema kuwa fedha hizo zinapitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani kutokana na sababu kwamba Serikali ya Ujerumani imekua ikifadhili miradi mbalimbali ya maji hapa nchini. “Ili kupata fedha kutoka katika mfuko huu ni lazima zipite kwenye taasisi ambayo imethibitishwa “accredited entity”alisisitiza Profesa Kamuzora.

Prof. Kamuzora amesema kuwa huu ni mradi mkubwa sana na wenye manufaa kwa wakazi wa Simiyu ambapo Mfuko wa Mabadiliko ya tabianchi umetoa kiasi cha 102,700,000 EURO, Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) itachangia 25,900,000 EURO na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itagharamia kiasi cha 13,100,000 EURO. Vilevile jamii inayozunguka mradi itachangia kiasi cha 1,500,000EURO, hivyo mradi wote unatarajiwa kugharimu kiasi cha EURO 143,000,000 na utatekelezwa ndani ya kipindi cha miaka mitano.

Mradi huo pia una lengo la kuimarisha afya za wakazi hao, kuhimiza uzalishaji endelevu na maendeleo ya jamii inayozunguka kwa kuwapatia maji safi na salama kwa miji na vijiji ambapo mradi utapita pamoja na kuhimili mabadiliko ya tabianchi hususan kwa wakulima wa Mkoa wa Simiyu.

Akitoa maelezo ya awali juu ya Mradi huo Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mabadiliko ya Tabia Nchi anayeiwakilisha Afrika Bw. Richard Muyungi, amesema kuwa ni mradi mkubwa sana na wa kwanza duniani kupatiwa fedha kupitia mfuko huo ambazo si mkopo. “Ni fedha zisizo za mkopo, ni msaada hivyo katika awamu ya kwanza takriban watu 395,000 katika Wilaya ya Busega, Bariadi na Itilima watanufaika na mradi huo”

Kupatikana kwa mradi huu na utekelezaji wake utasaidia sana changamoto zitokanazo kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya tabianchi ikiwa ni pamoja na ukame uliokithiri na utasaidia kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi katika Wilaya husika.

Kikao cha Wadau  cha kujadili utekelezaji wa Mradi wa maji wa Simiyu, kimeratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais  ambao ni Wasimamizi wa Fedha za Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi hapa nchini na wanadhamana ya kuhakikisaha fedha za Mfuko huo zinatumika ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuendana na mipango nchi iliyojiwekea.

MAJALIWA AKUTANA NA MKUU WA MAJESHI WA INDIA NA KUFANYA MAZUNGUMZO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Majeshi wa India, Admiral  Sunil Lanba Ofisini kwake jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kulia ni Mkuu wa Majeshi, Jeneral Venance Mabeyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Majeshi wa India , Admiral Sunil Lanba  (kulia kwake) pamoja na ujumbe wake, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Majeshi, Jeneral Venace Mabeyo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na  Mkuu wa Majeshi wa India Admiral Sunil Lanba  (wapili Kushoto) na Mkuu wa Majeshi nchini, Jeneral Venance Mabeyo (kushoto) baada ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kushoto ni Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na  Mkuu wa Majeshi wa India Admiral Sunil Lanba  (kulia kwake ) na Mkuu wa Majeshi nchini, Jeneral Venance mabeyo (kushoto kwake ) baada ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kushoto ni Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo  na Mkuu wa Majeshi wa India, Admiral  Sunil Lanba (kulia) baada ya mazungumzo yao Ofisini kwa  Waziri Mkuu  jijini Dar es salaam Julai 28, 2017 . Wapili kulia ni Mkuu wa Majeshi Nchini, Jeneral Venance Mabeyo na kushoto ni Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya.v


TANZANIA KUENDELEZA USHIRIKIANO NA INDIA-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania itaendeleza ushirikiano na Serikali ya India katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya ulinzi.

Ametoa kauli leo (Ijumaa, Julai 28 , 2017) alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Majeshi wa India, Bw. Admiral Sunil Lanba jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema Tanzania na India ni nchini ambazo zina uhusiano mzuri na wa muda mrefu, ambapo ameahidi kwamba Serikali itaendelea kuudumisha.

 “Ushirikiano wa Tanzania na India ni wa kihistoria, hivyo tutauendeleza na kuudumisha. India tunashrikiana nao katika sekta za uchumi, afya, elimu na ulinzi.”

Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya India kwa ufadhili walioutoa kwa Tanzania  katika kuimarisha miradi ya maji kwenye mikoa mbalimbali nchini.

Pia Waziri Mkuu amewakaribisha raia wa India kuja kutembelea maeneo ya  utalii nchini ukiwemo mlima wa Kilimanjaro, mbuga za wanyama na visiwa vya Zanzibar.

Kwa upande wake, Mkuu wa Majeshi wa India, Bw. Lanba ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano inaoutoa kwa Serikali ya India hususan katika masuala ya ulinzi.

Amesema wamefanya kikao na Mkuu wa Majeshi nchini Generali Venance Mabeyo ambapo katika mazungumzo yao wameweka mikakati ya kushirikiana katika kuimarisha ulinzi hususan maeneo ya mipakani pamoja na masuala ya mafunzo.

WANAHABARI WAHAMASISHWA KUANDIKA HABARI ZA KUUTANGAZA UTALII WETU NA UHIFADHI NCHINI

$
0
0
Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Dkt.Hassan Abbas akiwasilisha mada katika Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika jana  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'. .

Akiwasilisha mada ya Wajibu wa Wanahabari katika kutangaza Utalii nchini,Dkt Abbas alisema kuwa Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wana wajibu wa kuwashirikisha Wanahabari kwa kuwapatia taarifa sahihi,Ili jamii nayo ielimishwe habari zenye usahihi katika nyanja mbalimbali za Utalii.

"Tuwafadhili Waandishi wa habari kufanya stadi muhimu kama habari za Takwimu (data Journalism) na za uchunguzi (investigative journalism) kwa habari zenye maslahi kwa Taifa kama vile kufichua mitandao ya Waharifu wa mazingira au Majangili",alisema Dkt Abbas.

Dkt.Abbas amewataka Wanahabari kuandika habari za Utalii kwa wingi katika suala zima la kuutangaza Utalii wa nchi yetu,ambao ukitangazwa vizuri itasaidia kukuza uchumi wetu na hatimae kuongeza pato la Taifa,akaongeza kuwa pia na jamii inayozunguka katika suala zima la utalii itanufaika kwa namna moja ama nyingine.
Pichani kati ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Utangazaji Tanzania (TBC),Dkt Ayub Rioba akiwa sambamba na Meneja Mahusiano wa TANAPA,Pascal Shelutete na wadau wengine wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Dkt.Hassan Abbas alipokuwa akiwasilisha mada katika Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika jana  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'. 
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri ,Theophil  Makunga  akiwa na Wajumbe wengine katika Mkutano wa Wahariri na Waandishi waandamizi  ulioandaliwa na Tanapa
Wahariri na Waandishi waandamizi wa Habari walioshiriki katika Mkutano Maalum wa Mwaka ulioandaliwa TANAPA juu ya Utalii na Tanzania ya Viwanda 
Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Mkoa wa Morogoro Lilian Lucas  akipitia jarida la Mamlaka ya Hifadhi ya  Ngorongoro wakati wakati somo la umuhimu wa kuhifadhi na kutangaza utalii wa eneo hilo.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006)Ltd, Absalom Kibanda  akichangia jambo kwenye mada iliyohusu Wajibu wa Wanahabari katika kutangaza Utalii nchini, wakati wa mkutano wa Wahariri na Waandishi wa Habari Waandamizi juu ya Utalii na Tanzania ya Viwanda.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri ,Theophil  Makunga  akiuliza moja ya swali kwenye mada iliyohusu Wajibu wa Wanahabari katika kutangaza Utalii nchini,katika mkutano wa Wahariri na Waandishi wa Habari Waandamizi juu ya Utalii na Tanzania ya Viwanda.

ZIMAMOTO WAKUTANA NA WADAU WA VIFAA VYA USALAMA DHIDI YA MAJANGA YA MOTO (TAFEDA) JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (Katikati), akizungumza na Wadau wa Vifaa vya Usalama dhidi ya majanga ya moto (TAFEDA), walipokutana na kufanya kikao katika ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Jeshi hilo, leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Wadau wa Vifaa vya Usalama dhidi ya majanga ya moto (TAFEDA), Mohamed Kaumbwa akitoa utambulisho wa wajumbe aliombatana nao, walipokutana na kufanya kikao katika ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, leo jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, akiwa kwenye picha ya pamoja na Wadau wa Vifaa vya Usalama dhidi ya majanga ya moto, leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

MANTRACK TANZANIA YAONESHA MAPINDUZI MAPYA KATIKA SEKTA YA UJENZI NCHINI.

$
0
0
Katika kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya kuleta maendeleo kwa wananchi kampuni ya magari ya Mantrack Tanzania jana imeendesha warsha fupi yenye lengo la kutambulisha vifaa na teknolojia mpya itakayoongeza ufanisi wa kazi hasa katika sekta ya ujenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari, mwakilishi wa kampuni ya Mantrack Tanzania alisema kuwa wameleta vifaa vipya vitakavyoendana na kasi ya maendeleo ya Serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha Tanzania mpya inajengwa na uchumi bora na yenye miundombinu bora.

“Vifaa hivi ni imara na vinatumia teknolojia mpya na ya kisasa inayosaidia utendakaji wa shughuli za ujenzi kuwa rahisi. Tumeamua kuja na kasi ya serikali mpya ya kutenda vitu kwa urahisi na kwa ufanisi wa hali ya juu”.

Tuna wakaribisha wadau wa ujenzi wafike kujionea wenye tunachosema. Alisema. Warsha hiyo imefanyika katika karakana ya Mantrack Tanzania iliyopo karibu na jengo la Quality Plaza barabara ya Nyerere na ilihudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka makampuni mbalimbali ya ujenzi hapa nchini waliofika kushuhudia vifaa hivyo vinavyofanya kazi.



Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images