Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

ZANZIBAR KUWABANA KISHERIA WAVUTAJI SIGARA HADHARANI

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Ali Abdallah akizungumza na walikwa katika uzinduzi wa kanuni ya udhibiti wa tumbaku uliofanyika ukumbi wa Wizara ya Afya Zanzibar. Kulia mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani Dr. Matthieu Kamwa.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Bi. Harusi Said Suleiman akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha kanuni ya kuzibiti matumizi ya tumbaku Zanzibar (kushoto alieshika kitabu) ni Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani Dr. Matthieu Kamwa.

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Bi. Harisi Said Suleiman na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani Dr. Matthieu Kamwa wakionyesha Kitabu cha kanuni ya kuzibiti matumizi ya tumbaku Zanzibar kilichozinduliwa leo Wizara ya Afya.

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Bi. Harusi Said Suleiman wa (katikati) katika picha ya pamoja na viongozi wa WHO pamoja na watendaji wa Wizara ya Afya Zanzibar.

Picha na Makame Mshenga.

……………………………………………………………………

Na Mwashungi Tahir – Maelezo

Wizara ya Afya imezindua kanuni ya udhibiti wa matumizi ya Tumbaku ikiwa ni mkakati wa kupambana na ongezeko la Matumizi ya Tumbaku kwa jamii ya Zanzibar.

Hafla ya uzinduzi huo imefanywa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Harusi Saidi Suleiman huko Wizara ya Afya mnazi mmoja.

Akizungumza katika hafla hiyo Naibu huyo amesema jamii ya kizanzibari inakabiliwa na changamoto kubwa ya matumizi ya tumbaku ikiwemo uvutaji wa sigara.

Amesema Sigara ni bidhaa halali inayoingizia Serikali mapato kupitia kodi, hata hivyo mbali na mapato yanayopatikana , matumizi yake yamethibitika kuwa ni athari kubwa mno kwa mtumiaji pamoja na wanaomzunguka .

“Ifahamike kuwa tumbaku ina aina nyingi ya sumu ikiwemo NIKOTIN ambayo inasababisha uraibu na husafirishwa kwa njia ya mzunguko wa damu na kuathiri sehemu mbali mbali za mwilini” alisema Naibu huyo.

Alisema tafiti zilizofanywa ulimwenguni zinafahamisha kuwa matumizi ya tumbaku ikiwemo uvutaji wa sigara hupelekea kupata maradhi yasiyoambukiza ikiwemo Saratani za mapafu, kinywa, shingo ya kizazi , ugonjwa wa shinikizo la damu na kisukari .

Aliongeza kuwa matumizi yake huathiri pia mfumo mzima wa mishipa ya damu, maradhi sugu ya kuziba njia ya hewa kusababisha maradhi ya kiharusi.

Akielezea kuhusu Utafiti uliofanyika Zanzibar mwaka 2011 Naibu huyo alisema asilimia 7.3 ya watu katika jamii ni watumiaji wa Sigara na bidhaa zitokanazo na tumbaku, na kwa upande wa wanafunzi tafiti ndogo zilizofanyika imebainika skuli zaidi ya nane zilizomo wilaya ya mjini asilimia 9.5 ya wanafunzi wanatumia bidhaa zitokanazo na tumbaku ikiwemo sigara.

Akizitaja changamoto katika jamii alisema ni matumizi holela ya tumbaku hususan uvutaji wa sigara katika maeneo ya uwazi kama vile majengo yanayotoa huduma za kijamii, maeneo ya burudani, sokoni, viwanja vya mpira.

Naibu huyo alieleza kuwa Zanzibar inashuhudia watoto chini ya umri wa miaka 18 wakishirikishwa kwa njia moja au nyengine katika matumizi hayo na kwamba ipo haja wazazi na walezi kuwa na hadhari kwa watoto wao.

Ameviomba vyombo vya habari na vyombo vya sheria kuzipitia na kuzisimamia kanuni hizo ili kuweza kukabiliana na changamoto za matumizi hayo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mtu atakayeuza bidhaa ya tumbaku ikiwemo sigara lazima bidhaa hiyo iambatane na onyo la afya liililochapishwa kwa wino mwekundu na inayosomeka vizuri.

Kanuni hizo pia zinakataza mtu yeyote chini ya umri wa miaka 18 kutoruhusiwa kujishughulisha na kuuza sigara au kushiriki katika bidhaa ya tumbaku na kanuni inakataza kudhamini na kuhamasisha bidhaa hii ikiwa nchini au nje ya nchi kupitia vyombo vya habari na matangazo yanayohamasisha matumizi ya tumbaku.

Nae Mwakilishi wa Shirika la Afya duniani (WHO) Dr. Matthieu Kamwa amesema tumbaku ni miongoni mwa bidhaa zinazoongoza kusababisha vifo kwa watumiaji wake ambapo zaidi ya watu million saba hufariki duniani kote kutokana na matumizi yake.

Mwakilishi huyo amesema Tumbaku ni janga kubwa ambalo linagharimu uchumi wa dunia ambapo takriban dola za Marekani Tirion 1.2 hutumika kwa ajili ya matibabu ya watumiaji wa tumbaku.

Ameongeza kuwa Shirika la afya ulimwenguni litaendelea na mashirikiano yake na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kutengeneza kanuni zake dhidi yamatumizi ya tumbaku .

“Malengo endelevu ya dunia ni kuona dunia iko salama dhidi ya matumizi ya tumbaku ifikapo 2030 na ni jambo linalohitaji mashirikiano ya kila mdau katika kuhakikisha wanaepukana na matumizi hayo” alisema Kamwa.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa wizara ya Afya Asha Ali Abdullah akizungumza katika uzinduzi huo alisema tumbaku ni miongoni mwa Madawa ya kulevya hivyo ameomba elimu itolewe ili watumiaji waelewe athari zake hasa kwa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa la kesho.

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AZINDUA MFUMO WA BIOMETRICS NA KAMERA ZA CCTV KATIKA HOSPITAL YA RUFAA MKOA WA DODOMA

$
0
0
Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde,akizungumza na wafanyakazi wa Hospital ya Mkoa wa Dodoma hii leo.
Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde,akizungumza na wafanyakazi wa Hospital ya Mkoa wa Dodoma hii leo,wakati wa uzinduzi mfumo wa Biometrics na kamera za CCTV katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo.
Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde,akibonyeza kitufe wakati wa kuzindua matumizi ya mfumo wa Biometrics na kamera za CCTV katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
MBUNGE wa Dodoma mjini Anthony Mavunde ameendelea kutatua kero katika sekta ya Afya jimboni humo ambapo leo amezindua matumizi ya mfumo wa Biometrics na kamera za CCTV katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma,kufuatia hali hiyo wagonjwa wengi waliokuwepo hospital hapo walionekana wenye furaha na kuunga mkono jitihada za mbunge wao katika kusaidia kuboresha huduma za Afya katika hospital hiyo.

Akizungumza katika uzinduzi wa matumizi ya vifaa hivyo, Mavunde amesema ufungaji wa mifumo hiyo ni miongoni mwa jitihada zake za kuhakikisha huduma za afya katika jimbo hilo zinatolewa ipasavyo.

Mavunde ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira na Vijana amesema mfumo huo umefungwa na Ofisi ya Mbunge wa Dodoma na amelazimika kufunga vifaa hivyo kutokana na malalamiko ya muda mrefu ya wagonjwa kuwa wamekuwa wakitolewa lugha chafu na wauguzi.

Amesema pamoja na kamera hizo, pia umefungwa mfumo wa Biometrics(uchukuaji alama za dole gumba) ili kudhibiti watumishi ambao wamekuwa wakiondoka kabla ya muda na kuchelewa kuingia kazini.

“Kamera hizi zinarekodi sauti na kuchukua video ili kuondokana na malalamiko yaliyotolewa na wananchi na itakuwa ni rahisi kumbaini mtu atakayelalamikiwa na mgonjwa,”amesema Mavunde

Mavunde amesema fedha alizotumia kununulia Kamera hizo na mfumo wa Biometrics amezipata kwa kujibana katika mshahara wake lengo likiwa ni kutekeleza ahadi yake aliyowaahidi wananchi wakati wa Kampeni kutatua kero za afya.

Aidha amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza kasi ya utoaji huduma kwa wananchi hasa ukizingatia kwasasa Dodoma kuna ongezeko la watu kutokana na serikali kuhamia mkoani humo.

“Baadaye pia tutaweka mfumo wa kuhifadhi mafaili, hii yote ni kurahisisha utendaji kazi katika hospitali hii ili wananchi wetu waweze kupata huduma za afya ipasavyo.pia nimeomba vifaa mbalimbali vya kisasa Ujerumani kwa ajili ya hospitali hii tukipatiwa itasaidia sana utoaji huduma za afya,”amesisitiza Mavunde

Amesema ameahidi kutatua changamoto katika sekta ya afya ambapo mbali na ufungaji vifaa hivyo alishakabidhi vitanda katika Zahanati na Vituo vya afya 35

“Nimetoa madawa kwenye kituo cha afya cha Makole yenye thamani ya Sh. Milioni 15,nimefunga umeme wa jua katika vituo vya Afya 17 pamoja na huduma za macho kwa watu 7000 na watu 3000 walipata huduma za upasuaji bure,”amesema

Naye, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Caroline Damiani amemshukuru Mbunge huyo huku akidai kuwa matunda ya ufungaji wa kamera yameanza kuonekana kwa watumishi kufanya kazi zao kwa ufanisi wa hali ya juu tofauti na awali.

“Kumekuwa na kero nyingi kutoka kwa wagonjwa sasa Kamera za CCTV zitatusaidia kutatua kero hizi na kudhibiti wale wanaotoka kabla ya muda wa kazi kuisha au kuchelewa kazini,”amesema Mganga huyo

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni ya Entersoft Limited,Keneth Yindi amesema wamefunga Kamera 4 pamoja na mfumo wa Biometrics katika hospitali hiyo na ina uwezo wa kurekodi matukio kwa miezi tisa mfululizo.

WAZIRI MKUU AMTAKA MKURUGENZI HALMASHAURI YA SONGWE KUTOA USHIRIKIANO

Tumieni fursa zilizopo kuanzisha viwanda kukuza uchumi

$
0
0
Watanzania wametakiwa kutumia fursa zinazoendelea kuwekwa na serikali ya awamu ya tano kujikita katika ujasiriamali na kuanzisha viwanda kwa ajili ya kujenga uchumi viwanda ili kufikia uchumi kati na kuboresha ustawi wa jamii hapa nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,Profesa Adolf Mkenda alisema hayo wakati wa mkutano wa wadau uliokuwa ukijadili rasimu ya mapendekezo ya kuwa na mkakati wa kitaifa kuendeleza ujasiriamali hapa nchini, kuwa wakati wa watanzania kujikita katika ujasiriamali na kuwekeza katika viwanda umewadia.

“Wakati wa watanzania kuanzisha viwanda kuzalisha bidhaa zinazotokana na mali ghafi za hapa nchini umewadia,” na hakuna wakati mzuri zaidi kuliko kipindi hiki ambacho serikali imweka kipaumbele zaidi katika hili, aliongeza kusema Profesa Mkenda.

Mkakati huo wa kitaifa wa kuendeleza ujasiriamali umeandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali likiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa Linalojihusisha na Maendeleo ya Biashara (UNCTAD).

Profesa Mkenda alifafanua kwamba serikali imeamua kuja na rasimu hiyo kupata mkakati wa uendelezaji ujasiriamali huku ikitambua uchumi wa Tanzania utajengwa na watanzania na wawekezaji wa nje kuja kuongezea tu.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng’I Issa alisema Baraza lake linasimamia sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi na suala la uasiriamali ni nguzo muhimu katika uwezeshaji wananchi.

“Pendekezo la mkakati huu wa kuendeleza ujasirimali umeandaliwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na leo ni siku ya pekee kwa wataalaam kutoa maoni yenu ili kupata mkakati wa kitaifa,” na aliwaomba watalaamu hao kutoa maoni yao kukamilisha upatakanaji wake, alisema, Bi. Issa 

  Alisema jukumu la kuaandaa mkakati wa kitaifa wa kuongoza ujasiriamali kufikia uchumi wa kati na wa viwanda ni muhimu kwa vile utawezesha kupata wajasiriamali wenye mafanikio walioongozwa vyema.

Alisema uandaaji wa rasimu hiyo umeangalia mapungufu yaliyopo katika nchi na umekuja na majibu ambayo ni rafiki kwa wajasiriamali.

Alisema hadi kufikia Agosti mwezi ujao maoni yote ya wadau yatakuwa yameingizwa na matarajio yaliyopo ni kwamba mkakati huo utaweza kuwa tayari Octoba 2017 kwa ajili ya kuendeleza ujasiriamali.

Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Linalojihusisha na Maendeleo ya Biashara (UNCTAD),Bw. Lorenzo Tosini alisema shirika hilo limeweka suala la uendelezaji ujasirimali katika ajenda kuu na Tanzania inapofanya hivyo inaendana na ajenda hiyo.

“Katika kukuza ujasiriamali kuna changamoto mbalimbali ambazo nchi nyingi za Afrika zinakabiliana nazo na kuwepo kwa mkakati huo nchini Tanzania itasaidia katika hili,” na kuongeza mkakati huo pia usaidie kuja na sera inayoleta usawa kwa wajasiriamali.

Alisema vikwazo vikuu katika mataifa haya katika ujasiriamali na biashara ni pamoja na vikwazo vya kisheria, upatakanaji wa mitaji kutoka taasisi za kiedha, na uhafifu wa teknolojia na mawasiliano .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,Profesa Adolf Mkenda (katikati) akifuatilia mada iliyokuwa inatolewa na Mwezeshaji, Dkt Donath Olomi hayupo pichani wakati wa mkutano wa wadau uliokuwa ukijadili rasimu ya mapendekezo ya kuwa na mkakati wa kitaifa kuendeleza ujasiriamali hapa nchini, wapili kushoto Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng’I Issa, kushoto ni Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Linalojihusisha na Maendeleo ya Biashara (UNCTAD),Bw. Lorenzo Tosini, wa pili kuli ni Mkurugenzi Msaidizi Mazingira ya Biashara Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Christopher Mramba na kulia ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa baraza hilo, Bi. Anna Dominick.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,Profesa Adolf Mkenda (katikati) akiteta jambo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng’I Issa, wakati wa mkutano wa wadau uliokuwa ukijadili rasimu ya mapendekezo ya kuwa na mkakati wa kitaifa kuendeleza ujasiriamali hapa nchini, na kulia ni Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Linalojihusisha na Maendeleo ya Biashara (UNCTAD),Bw. Lorenzo Tosini.
Wadau kutoka taasisi mbalimbali wakiwa katika makundi wakati wa mkutano uliokuwa ukijadili rasimu ya mapendekezo ya kuwa na mkakati wa kitaifa wa kuendeleza ujasiriamali hapa nchini, aliyesimama ni mwezeshaji wa mkutano huo, Dkt. Donath Olomi.

WADAU WA KILIMO WAJA MBINU YA KUSAIDIA WAKULIMA WADOGO KUPATA MASOKO YA UHAKIKA

$
0
0
Mkurugenzi Mkazi wa Farm Africa, Steve Ball akizungumza kuhusu umuhimu wa wakulima kupata taarifa za uhakika kuhusu mwenendo wa masoko, wakati wa warsha ya wadau wa mazao ya nafaka iliyofanyika  jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
Mpango mpya unaohamasishwa na wadau wa sekta ya kilimo hatimaye utawapa wakulima wadogo nchini kote fursa ya kupata masoko ya uhakika na endelevu kwa kuepuka madalali wa mazao yao.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Farm Africa jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkazi wa Tanzania wa Farm Africa,  Steve Ball alisema kuwa warsha hiyo ililenga kuwafudisha wakulima namna bora kuingia kwenye mfumo rasmi wa biashara ya nafaka.

Alisema kuwa jukwaa hilo la wadau kwenye sekta hiyo linaunganisha biashara nzima ya nafaka kutoka kwenye shamba hadi sokoni  na inashirikisha mkusanyiko wa programu zinazoruhusu watumiaji kusimamia hesabu, mazao ya biashara, soko endelevu na kupata mikopo kutoa kwenye taasisi za fedha.

"Tuko hapa kuzungumza juu ya njia bora ya kuwasaidia wakulima wadogo ili kuepuka madalali wakati wa kutafuta masoko ya mazao yao na ili waweze kupata kwa bei bora zaidi baada ya kupata taarifa sahihi na kwa wakati muafaka juu ya mwenendo wa soko,” alisema.

Aliongeza pia kwamba wadau katika sekta hiyo wana matumaini kwamba wakulima watakusanya nguvu kwa pamoja na kutengeneza maghala yao ya kuhifadhi mazao yao na kuuza kwa pamoja ili kupata bei nzri zaidi.

Alibainisha kuwa kwa njia ya G-Soko, wakulima wanaweza kuunganisha mavuno yao kupitia ghala lao na kuthibitishwa na kupata huduma za kifedha kwa kutumia nafaka zao kama dhamana. Jukwaa pia hutoa programu ya malipo ya huduma na ukusanyaji wa data wa wakulima.

Alifafanua kamba wadau wanajua kwamba zuio la serikali kuuza chakula ni kudhibiti hali ya uchumi wa nchini na vile vile kuzuia kununua unga, mchele kutoka nje baada ya wakulima kuuza mahindi na mtama lakini aliongeza ni muhimu kwa serikali kuwajengea wakulima uwezo ili kuanzisha viwanda vya kusindika vyakula hapa hapa nchini.

Kwa upande wake, Mshauri wa Sera kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Revelian Ngaiza alisema kuwa serikali inatafuta njia bora ya kupunguza gharama za shughuli za kilimo kwa mkulima mdogo kwa kuboresha mfumo wa miundombinu, usafiri na usambazaji.

"Kuboresha upatikanaji wa habari kwa wakulima wadogo juu ya bei ya soko na mahitaji ya walaji na kuwezesha ushirikiano na sekta binafsi na serikali katika kumuinua mkulima mdogo vijijini,’ alisema.

Alisema serikali ina nia ya kuanzisha mikakati na sera mbalimbali za kubadilisha kilimo ili kuendeleza utendaji bora na uboreshaji ulioimarishwa na ukuaji wa uchumi.

"Katika Tanzania peke yake, karibu asilimia  40 nafaka hupotea kutokana na uhifadhi duni na mabadiliko ya hali ya hewa kila mwaka, kwa gharama ya dola za Kimarekani milioni 332 na kuacha wakulima wa nafaka kwenye hasara kubwa," alisisitiza

Shirika lisilo kuwa la kiserikali la Mipango ya Maendeleo Mjini na Vijijini (RUDI), Afisa Mtendaji Mkuu wake, Lameck Kikoka ana matumaini kuwa kuingilia kati kwa wadau hao wa kilimo nchini na mashirika ya kimataifa ya kilimo kutasaidia wakulima zaidi ya 30,000 nchini Tanzania pekee kupata masoko zaidi, hivyo kupambana na umaskini na kuboresha ustawi wa wakulima.

Alisema kuwa zamani changamoto za wakulima zilikuwa kubwa gharama kubwa za pembejeo kama vile mbegu zilizoboreshwa na mbolea na wengi walikuwa hawana mahali pa kuhifadhi mazao yao wakati wanasubiri bei bora kwenye soko.

"Lakini kuingilia kati kwa serikali na kuanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani kutaendelea kuwahahikishia wakulima bei bora na usalama wa mazao yao na soko endelevu kwa mazao yao wakati na kuongeza uwezo wao wa kuhifadhi kwa kuendelea kujenga maghala yao wenyewe yatakayo thibitishwa na serikali,” alifafanua.

"Ili kusaidia wakulima kufaidika na fursa hizi, Farm Africa na washirika wa ushirika (RUDI) sasa wanataka kusaidia wadogo wa Tanzania na Uganda kushika mchele, mazao na maharage ya ziada."

"Tunapaswa kulima  na kuvuna zaidi baada y kupata uelewa wa mfumo rasmi wa biashara ya nafaka na uelewa wa kupata soko la uhakika bila madalali ," alisema Emerita Singaile.  Mwenyekiti wa Umoja wa wakulima wa Makalali kutoka mkoani Iringa

AMSHA AMSHA YA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA ZA SOKO LA EAC YASHIKA KASI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (The Foundation for Civil Society- FCS), Bw. Francis Kiwanga akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa katika Kongamano la siku moja la kuwahamasisha vijana kuchangamkia fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Kongamano hilo lilifanyika kwenye ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza tarehe 19 Julai 2017. 
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Mary Onesmo Tesha ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella akisoma hotuba ya ufunguzi kwenye kongmano la kuwhamasisha vijana kufanya biashara za kuvuka mipaka ya nchi za EAC. Mhe. Tesha aliwasihi vijana waondoe hofu na wajiunge katika vikundi ili waweza kufanya biashara kwa urahisi. Aliahidi kutoa milioni moja kwa kikundi kilichoundwa hapohapo kwa uratibu wa Mwkilishi wa Cloud Media, Bw. Samsonight Odera 
Bi. Tesha akiendelea na hotuba yake. 
Mchumi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw, Justin Kisoka akiwaeleza vijana wa Mwanza waliofurika kwenye ukumbi wa Rock City Mall sheria, kanuni na taratibu za kufuata kwa yeyote anayetaka kuanza biashara ya kuvuka mipaka ya nchi za EAC. 
Mtaalamu wa Msauala ya EAC, Bw. Abel Maganya akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu kufanya biashara ndani ya Jumuiya ya EAC ikiwemo namna ya kupata cheti cha uasili na hati za kusafiria. 
Mbinu mbalimbali zilitumika kufikisha ujumbe wa umuhimu wa kufanya biashara katika nchi za EAC. Hapa vijana wa Vipaji Foundation wakionesha kwa kutumia igizo baaadhi ya bidhaa zinazoweza kuuzwa katika nchi za EAC. 
Mjasiriamali aliyefanikiwa ambaye pia ni maaruku wa kutoa mihadhara ya mbinu za kufanya biashara, Bw. James Mwang'amba akiwasilisha mada kuhusu mbinu za kuanza biashara na kuiendesha hadi ikakua kubwa. 
Sehemu ya umati wa watu walioshiriki kongamano.


BABATI, MANYARA 

Msafara ulipokuwa unatokea Mwanza kwenda Arusha, ulisimama kwa muda Babati na kuongea na Wanababati namna ya kufanya biashara katika nchi za EAC. 
Mkazi wa Babati akiuliza swali ili apate ufafanuzi kabla ya kuanza kupeleka bidhaa zake nchini Kenya 
Vijana wa Vipaji Foundation wakitoa somo kwa Wanababati kupitia sanaa. 

Wanababati wakisikiliza kwa makini ujumbe wa namna ya kufanya biashara ya kuvuka mipaka. 

VIJUSO VYA MAGAZETI YA IJUMAA LEO JULAI 21,2017

Wahalifu wengine wawili wauawa tena IKWIRIRI, mmoja atambulika.

$
0
0
Na Tamimu Adam - Jeshi la Polisi. 

Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika Kanda maalumu ya kipolisi Rufiji ambapo mmoja kati ya watu hao ametambulika kwa jina la Abdallah Ally Ngande Makeo ambaye alikuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa muda mrefu kutokana na kushiriki kwake katika matukio ya mauaji maeneo ya Ikwiriri, Kibiti pamoja na uvamizi wa kituo cha Polisi Ikwiriri. 
Akielezea tukio hilo, Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 19, julai, 2017 saa mbili usiku katika eneo la Utende kata ya Ikwiriri, wilaya Rufiji kanda maalum ya Polisi Rufiji. 
“ Askari Polisi wa doria waliwatilia mashaka watu wanaokadiliwa kuwa watano ambapo walianza kuwafutilia ndipo walianza kukimbia huku wakiwashambulia askari kwa risasi, askari nao kwa ujasiri walijibu mashambulizi na kufanikiwa kuwajeruhi wahalifu wawili miongonio mwao ambao baadaye walifariki wakipelekwa Hospitali ya Taifa ya muhimbili kutokana na kuvuja damu iliyosababisishwa na majeraha ya risasi waliyoyapata” alisema Sabas. 
Aliongeza kuwa katika eneo hilo la tukio ilipatikana silaha moja aina ya rifle 375 ambayo ilikutwa imekatwa kitako na mtutu ikiwa na risasi mbili (2). Aidha, Miili ya marehemu wote wamehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Taifa ya muhimbili. 
Kamanda sabas ameendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa wahalifu wengine waliosalia na kwamba opereheni hiyo ya kuwasaka wahalifu katika Kanda hiyo ya kipolisi Rufiji ni endelevu na hakuna atakaye baki. 
Mkuu wa Operesheni Maalun za Jeshi la Polisi, Naibu kamishina wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas akiwa katika eneo la tukio akizungumzia namna Jeshi la Polisi lilivyofanikiwa kuuawa watu wawili awanaosadikiwa kuwa ni miongoni mwa wahalifu wanaojihusisha na mauaji watu katika Ikwiriri na kibiti. (Kushoto kwake ) ni Kamanda wa Kanda maalum ya Kipolisi Rufiji, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Onesmo Lyanga akiwa ameshika silaha aina ya Rifle 375 iliyokutwa katika eneo la tukio. Picha na Tamimu Adam.

Tigo imekabidhi darasa lenye thamani ya Tsh milioni 8.5 kwa shule ya msingi Hachwi wilayani Kondoa.

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Sezaria Makutta akikata utepe kuashiria kupokea darasa lenye thamani ya shilingi milioni 8.5 lililojengwa na kampuni ya Tigo kwa shule ya msingi Hachwi wilayani Kondoa, wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata, Mkuu wa kitengo cha usimamizi na mahusiano na serikali kutoka Tigo, Sylvia Balwire na Meneja wa mahusiano na huduma za Jamii kutoka Tigo, Halima Okash(mwenye kilemba) makabidhiano hayo yalifanyika jana.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Sezaria Makutta akiingia katika darasa lenye thamani ya shilingi milioni 8.5 lililojengwa na kampuni ya Tigo kwa shule ya msingi Hachwi wilayani Kondoa, wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata, Mkuu wa kitengo cha usimamizi na mahusiano na serikali kutoka Tigo, Sylvia Balwire na Meneja wa mahusiano na huduma za Jamii kutoka Tigo, Halima Okash(mwenye kilemba) makabidhiano hayo yalifanyika jana.
Darasa lenye thamani ya shilingi milioni 8.5 lililojengwa na kampuni ya Tigo kwa shule ya msingi Hachwi wilayani Kondoa,
Wazazi wakishudia makabidhiano ya darasa lenye thamani ya Milion 8.5 kwa shule ya msingi Hachwi wilayani Kondoa.


Leo tarehe 19 Julai 2017, Kondoa Dodoma – Kampuni ya maisha ya kidigitali inayoongoza Tanzania Tigo, leo imekabidhi darasa lenye thamani ya shilingi milioni 8.5 kwa shule ya msingi Hachwi iliyoko wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma katika juhudi za kusaidia ukuaji wa kiwango cha elimu wilayani humo.

Akiongea katika sherehe ya makabidhiano iliyofanyika shuleni hapo, Mkurugenzi wa Tigo wa Kanda ya Kaskazini George Lugata alisema kwamba mchango huo ulikuwa ni sehemu ya juhudi za wafanyakazi wa Kampuni kujitolea na jukumu la kampuni kusaidia maendeleo ya jamii (CSR) katika kusaidia elimu Tanzania.

“Tigo ina sera nzuri ya (CSR) ambayo inasisitiza katika kutoa kwa ajili ya kusaidia Jamii ambako kampuni inaendesha shughuli zake. Tunaamini kwamba kupitia mchango huu, Tigo itakuwa imechangia kwa mara nyingine katika kutengeneza mazingira kwa ajili ya ukuaji wa wataalamu wa baadae kwa ajili ya maendeleo ya haraka ya nchi”, alisema Lugata.

Katika nafasi yake Meneja wa CSR wa Tigo, Bi Halima Okash, aligusia vipaumbele vya kampuni vya uwekezaji katika jamii, akisema kwamba Tigo ilikuwa tayari kushirikiana na wadau wengine wenye fikra kama hizo katika juhudi zake za kusaidia maendeleo ya jamii.

Kupitia mpango wetu wa uwekezaji katika jamii, Tigo imekuwa katika mstari wa mbele kuinua sekta ya elimu nchini ambapo tumeshatoa komputa na kuunganisha shule 60 za sekondari kwenye mtandao wa intaneti wenye kasi zaidi kupitia mradi wetu wa e-school pamoja na kuchangia zaidi ya madawati 7,000 kwa shule za msingi nchini kote”alisema Okash. Mgeni rasmi katika sherehe, Mkuu wa mkoa wa wilaya ya Kondoa, Sezeria Makutta aliishukuru Tigo kwa mchango wake, akibainisha kwamba itasaidia sana katika kupunguza msongamano wa wanafunzi katika darasa moja, ambapo itatengeneza mazingira mazuri ya kujifunzia shuleni.

“Tunawashukuru sana Tigo kwa msaada wao”, alisema Makutta, akiongeza kwamba; “Tunawaomba watu wengine wenye moyo wa kujitolea kujitokeza na kuongeza nguvu katika kuondoa upungufu wa madarasa katika wilaya yetu”.

WATAALAM WA USAFIRI WA ANGA WAJENGEWA UWEZO KUHUSU NAMNA YA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA WATUMIAJI WA USAFIRI WA ANGA

$
0
0
Wataalam wa Usafiri wa Anga  nchini wamekutana katika semina ya siku tatu ya kuwajengea uwezo kuhusu namna bora ya kushughulikia malalamiko na kero za watumiaji wa usafiri wa anga nchini katika semina iliyofanyika mjini Morogoro kuanzia  Julai 20, 2017. 

Semina hiyo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA)  nchini imewakutanisha wajumbe wa kitengo cha Kushughulikia Malalamiko ya Watumiaji wa Usafiri wa Anga cha TCAA(TCAA-CCU), Watendaji wa Baraza la Watumiaji wa Usafiri wa Anga(TCAA-CCC), wanasheria wa Mamlaka na maafisa  kutoka idara ya udhibiti masuala ya Kiuchumi ya TCAA ambayo inajukumu la kulinda maslahi ya watumiaji wa usafiri  wa anga .

Miongoni mwa mada zilizotolewa kwenye semina hiyo ni pamoja na  wajibu wa  kampuni za ndege kwa abiria, iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa  TCAA, Hamza S. Johari, majukumu ya kitengo cha kushughulikia malalamiko ya watumiaji wa usafiri wa anga na  nyezo za kushughulikia malalamiko ya watumiaji wa usafiri wa anga.

Semina hii ni sehemu ya mkakati wa usafiri wa anga wa kuboresha huduma zinazotolewa kwa watumiaji wa usafiri wa anga na kukuza sekta ya usafiri wa anga Tanzania
 Mkurugenzi  Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S. Johari, akitoa mada kuhusu wajibu wa Mashirika ya Ndege kwa Abiria Kwa Washiriki wa Semina ya Siku Tatu Kuhusu Namna ya Kushughulikia Malalamiko ya Watumiaji wa Usafiri wa Anga Nchini Iliyofanyika Morogoro, Kuanzia Julai 20, 2017. 
 Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza S. Johari(Kulia) na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Kudhibiti Masuala ya Kiuchumi, Dan Malanga wakifuatilia mada kwenye semina kuhusu namna ya kushughulikia Malalamiko ya Watumiaji wa Usafiri wa Anga iliyofanyika Morogoro Mwezi July 20, 2017.
 Washiriki wa Semina kuhusu namna ya kushughulikia malalamiko ya matumiaji wa Usafiri wa Anga wakifuatilia mada ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza S. Johari.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Watumiaji wa Usafiri wa Anga(TCAA-CCC) Elias Mwashiuya, akiwasilisha mada kwa Washiriki wa Semina ya Siku Tatu kuhusu namna ya kushughulikia malalamiko ya watumiaji wa Usafiri wa Anga iliyofanyika Morogoro Julai 20, 2017.

ZITTO KABWE AUSHUKURU UBALOZI WA CHINA NCHIN

$
0
0
Kwa niaba ya Manispaa ya Kigoma Ujiji naomba kuchukua fursa hii kuushukuru Ubalozi wa China nchini, Balozi pamoja na Timu ya Wawekezaji kutoka China waliokuwa wageni wetu hapa Ujiji kwa muda wa siku 3. 

Ujio wao ni jambo lenye faraja kwetu kwamba juhudi zetu za kuainisha fursa za uwekezaji hapa  Kigoma (kupitia mwongozo wa Uwekezaji Kigoma Ujiji - Kigoma Ujiji Investor's Guide) zimeanza kuzaa matunda na kuvutia uwekezaji kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Ziara ya Balozi Lu Youqing na timu yake imewezesha makubaliano kwenye maeneo matano (5) ya uwekezaji:

1. Ujenzi wa Kiwanda cha kuchakata Samaki na mazao ya Samaki katika mji wa Katonga, Kata ya Bangwe.

2. Ujenzi wa Kituo cha Biashara Ujiji (Ujiji City - The Great Lakes Trade and Logistics Center) katika kata ya Kitongoni na Kasimbu.

3. Uwekezaji Wa Kiwanda cha kusindika mazao ya michikichi.

4. Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Vijana eneo la Mwanga Community Center.

5. Ukarabati wa Soko la Ujiji na jengo la watumwa na ujenzi wa barabara ya watumwa ili kukuza Utalii na Ujenzi Mwalo wa Katonga.

Ziara ilikuwa ya mafanikio makubwa sana, ikitufikisha hata katika maeneo ambayo ni nadra mabalozi kufika (kama pichani tukivuka mto Luiche), ninaamini kuwa wananchi wa Kigoma watafanikiwa na miradi hii inayotokana na mahusiano mazuri kati ya nchi yetu na Jamhuri ya watu wa China. 

Ni dhamira yetu kuhakikisha tunautumia muda wa dhamana yetu tuliyopewa na wananchi kushirikiana nao kuleta maendeleo na kuipeleka mbele Kigoma Ujiji.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Mbunge, Kigoma Mjini - ACT Wazalendo 
Kigoma

MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI LA NYUMBA ZA HALMASHAURI YA MOMBA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mwanachuo wa Chuo cha DIT, Grolia Shoo kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba zinazojengwa na Shirika la Taifa la Nyumba katika eneo la Chitete wialyani Momba Julai 21, 2017. Gloria anafanya kazi kwa muda akijifunza katika shirika hilo. Kushoto kwake ni mkewe Mary na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa, NHC, Blandina Nyoni. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la ujenzi wa nyumba 20 za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba katika eneo la Chitete akiwa katika ziara ya mkoa wa Songwe Julai 21, 2017. Wapili kulia ni mkewe Mary na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linalojenga nyumba hizo, Blandina Nyoni. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Mwenyekiti wa CHADEMA wa kata ya Kangwa wilayani Songwe ,Keneth Nzowa ambaye pamoja na wenzake walitangaza kukihama Chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa michezo wa Mkwajuni wilayani Songwe Julai 20, 2017.
Wananchi wa Songwe wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadahara katika uwanja wa michezo wa Songwe Julai 20, 2017.(picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Chief Mwibongo wa Ivungu baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa michezo wa Mkwajuni wilayani Songwe Julai 20, 2017.

WAZIRI SIMBACHAWENE AFANYA ZIARA YA KIKAZI JIMBONI KWAKE KIBAKWE-MPWAPWA

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, Kibakwe.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tamisemi Mhe. George Simbachawene amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote Nchini kuandaa mazingira rafiki kwa watumishi wapya wanaopangiwa katika Halmashauri zao.

Simbachawene ameyasema hayo ikiwa ni wiki moja tangu kutangaza ajira mpya za Walimu wa Masomo ya Hisabati na Sayansi wapatao 3,081 wa ngazi ya Shahada na Stashahada ambao wamepangiwa kwenye Halmashauri mbalimbali Nchini.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msangambuya wakati wa Ziara yake ya Kikazi Wilayani Mpwapwa katika Jimbo la Kibakwe Mhe. Simbachawene amesema watumishi wengi wapya wanakatishwa tamaa na mazingira mabovu wanayoyakuta katika Halmashauri zao na hali hiyo huwatia hofu ya kuendelea kukaa katika maeneo hao.

Unakuta mtumishi anafika Halmashauri malipo yake hayajaandaliwa zaidi ya mwezi mzima, kisha anapangiwa kwenye Kata mbayo hata hajawahi kuifahamu hapo awali na hapewi hata maelekezo ya ziada ya namna ya kufika katika Kituo chake na unakuta wenyeji wake katika Kata na Shule hawana taarifa za ujio wa mtumishi huyo hivyo mtumishi anahangaika mpaka anakosa ari ya kufanya kazi katika kituo chake kipya alisema Simbachawene.

“Ninahitaji Kila Halmashauri kuandaa Malipo stahiki kwa ajili ya walimu wanaoendelea kuripoti hivi sasa katika maeneo mbalimbali, Usafiri wa kuwapeleka katika vituo vyao vya Kazi, mapokezi stahiki kwa uongozi wa Kata pamoja Shule sambamba na kuhakikisha anapata makazi bora ya kuishi katika eneo lake jipya la Kazi”.

Sitaelewa Halmashauri ambayo itashindwa kuzingatia maagizo haya kwa namna yeyeote ile na ntaendelea kufuatilia mazingira ya mapokezi ya watumishi hawa, sitaki mtumishi yeyote ashindwe kufanya kazi yake kwa ufanisi kwa sababu ya mazingira magumu anayokutana nayo wakati wa kuripoti kazini, Aliongeza.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpwapwa Bi. Eliachi Macha alisema Halmashauri imeandaa mazingira mazuri kwa ajili ya mapokezi ya walimu wapya na pia watahakikisha wanatekeleza Maagizo yote ili watumishi wote waweza kufanya kazi za ujenzi wa Taifa na kuleta matokeo chanya.

Naye Diwani wa Kata ya Mtera Mhe. Amon Kodi ambaye alishiriki katika ziara hii alimpongeza Waziri Simbachawene kwa kazi kubwa anayoendelea kufanya katika Kata yao, Jimbo la Kibakwe na Taifa kwa Ujumla na kumshkuru kwa kufanikisha utekelezaji wa Miradi ya ujenzi wa bweni la Mtera Sekondari, ukarabati wa zahanati ya kisima pamoja na ukarabati wa matundu ya vyoo vya Shule vya Msingi Msangambuya.

Mhe. Simbachawene yupo katika ziara ya Kikazi Wilayani Mpwapwa, Jimbo la Kibakwe na ametembelea Kijiji cha Msangambuya, Chamsisili pamoja na Chinoje.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tamisemi Mhe. George Simbachawene (kwanza Kulia) akisalimiana na Wakina Mama wa Kijiji cha Msangambuye wakati wa Ziara yake Wilayani Mpwapwa katika Jimbo la Kibakwe.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tamisemi Mhe. George Simbachawene(mbele) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msangambue, Kata ya Mtera Tarafa ya Rudi wakati wa Ziara yake Katika Jimbo la Kibakwe.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tamisemi Mhe. George Simbachawene(mbele) akitoa maelekezo kwa Wazee wa Kijiji cha Msangambuye wakati wa Ziara ya Kikazi Jimboni Kibwakwe.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tamisemi Mhe. George Simbachawene(mbele) akizungumza na mwanafunzi wa darasa la kwanza Yusta Mwanshinga katika shule ya Msingi Msangambuya alipopita kuwasalimia wanafunzi wa shule hiyo wakati wa ziara yake.

 Mama Theresia Costantine Komba (kushoto) akimshkuru Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tamisemi Mhe. George Simbachawene kuwatembelea katika Kijiji cha Chinoje.

KUTANA NA 'TYRESE' WA TANZANIA AITWAYE BANYE

$
0
0
:

Elias Banyenza nduo jina alilopewa na wazazi wake, lakini unafahamika na wengi kwa jina la Banye. Anapenda kuimba na RnB ndio muziki ana unaoupenda zaidi. Banye alianza kuimba akiwa Sunday Schools na Talent Shows lakini alivutiwa zaidi na Mwanamziki Tyrese tangu alipomuona mara ya kwanza kwenye Tangazo la Coca-Cola la mwaka 1986 na kujaribu kumfuatisha jinsi alivyoimba kila mara lile Tangazo lilipopita. 
Watu wengi wakimuona kwa mara ya kwanza huwa wanahisi kama waliwahi kumuona sehemu nahisi hii ni kwasababu waliwahi kuomuona kwenye sehemu zifuatazo:- Mwaka 2014/2015 alikuwa miongoni mwa wawashiriki 6 (Damian Soul,Grace Matata,Eli Daddy, Rogers Lucas, Myra) waliowakilisha Tanzania kwenye shindano la kuimba la Maisha Superstar nchini Kenya, kipindi hicho cha Tv kilirushwa na Maisha Magic ambapo walienda kushindana na washiriki wengine 12 kutoka nchi tofauti tofauti za Africa Mashariki, walisimamiwa na Shaa, AY(Tanzania), Jose Chameleon, Maurice Kirya (Uganda),Nameless, King Kaka(Kenya) na Music Director alikuwa Eric Wanaina. 
Mwaka 2015/2016, alikuwa kati ya washiriki 5 (Nandy, Jeff, Kechu na Zouccu) waliochagulia kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano makubwa zaidi ya Karaoke kuwahi kutokea Africa, Tecno Own The Stage Lagos nchini Nigeria, kipindi hicho kilirushwa na Africa Magic Showcase ambapo pia alishindana na waimbaji wengine 14 kutoka sehemu mbalimbali za bara la Afrika. Kwenye shindano hili walikuwa chini ya usimamizi wa Yemi Alade, MI, ID Cabasa (Nigeria), Bien Soul/Saut Sol, Anto Neosoul(Kenya) and AY (Tanzania) 
Ndoto yake kubwa alitamani atoke kimuziki kupitia Mashindano ya kuimba, lakini hakuweza kufanya vizuri huko kwa sababu alikuwa anafanya multitasking…ikiwemo Shule,Kazi na Muziki kwa wakati mmoja hivyo kumpelekea kufanya maandalizi ya zima moto.
Ukiachana na Muziki Banye amesoma Masters of Business Administration in Marketing na Bachelor in Mass Communication na kaspecilize kwenye Public Relations and Marketing. Na sasa kaamua kuingia studio na wimbo wake wa kwanza ni huo Brown Colour.

MAENDELEO PAMOJA NA WEWE

$
0
0
 Maendeleo Bank pamoja na wewe. Bank ya Maendeleo leo imezindua promosheni iitwayo Maendeleo pamoja na wewe. Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Ibrahim Mwangalaba alisema “  Leo tumekutana hapa kwa ajili ya tukio fupi tu la kuzindua rasmi promosheni tuliyoipa jina la Maendeleo Bank pamoja na wewe”.

Aliongeza kusema “Promosheni ya Maendeleo Bank pamoja na wewe ni mahususi kwa wateja waliopo au wapya. Kama mnavyojua Maendeleo Bank imeanzishwa miaka 4 iliyopita na imepiga hatua kubwa sana; Tumeongeza matawi kutoka moja hadi 3 ambayo ni Luther House, Mwenge na Kariakoo, tumebuni bidhaa nyingi, tumepata faida nzuri katika kipindi kifupi hadi kufikia Milioni 550, Amana za benki zimeongezeka hadi kufikia Bilioni 34,tumetoa mikopo inayofikia Bilioni 27 tumeajiri wafanyakazi 63, na kama tutaruhusiwa na CMSA tunatarajia kukaribisha wanahisa wapya kupitia Soko la awali yaani IPO hivyo kukuza wigo wa umiliki wa benki na mtaji wa kufanya mambo mengi zaidi”.

alimalizia kwa kusema , Sisi kama benki yenye kulenga kuwapa wateja wetu Maendeleo tunawapa wateja watakaofungua akaunti za akiba au timiza nafasi yakujishindia ; Viwanja, tani za cement, mabati au ada za shule kwa wale watakao fungua au kuweka amana kwenye Maendeleo Junior.
Promosheni hii ni ya miezi 3.

Mchakato wa Uanzishaji Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi Waanza.

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano - Sekta ya Mawasiliano, Injinia Angelina Madete amesema uanzishaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ufundi (ICoT), utasaidia kupunguza pengo lililopo sasa baina ya wahandisi, mafundi sanifu na mafundi mchundo hapa nchini.

Akifungua warsha ya wataalam washauri na wadau wa Taasisi ya Teknolojia ya Ufundi Jijini Dar es salaam leo, Mhandisi Madete amewataka wataalam hao kufanya uchambuzi wa kina ili kuwezesha taasisi hiyo mpya kukidhi mahitaji ya mafundi sanifu na mchundo na hivyo kukidhi uwiano wa kimataifa unaotaka mhandisi mmoja, fundi sanifu watano na mafundi mchundo 25.

“Tunataka kuwa nchi ya viwanda vya kati ifikapo mwaka 2025, hivyo ni lazima tuwe na wahandisi, mafundi sanifu na mafundi mchundo wa kutosha watakaofanyakazi kwa weledi na kumudu ushindani katika soko la ajira”, amebainisha Injinia Madete.

Mhandisi Madete amesema kuwa pengo la wahandisi, mafundi sanifu na mafundi mchundo limeongezeka kutokana na vyuo vingi vya kati kutoa shahada hivyo uwepo wa ICoT utakabiliana na kumaliza changamoto hiyo.

Aidha amezungumzia umuhimu wa taasisi hiyo mpya kuanzisha kozi ya waendesha mitambo ambayo mahitaji yake ni makubwa hapa nchini na kwa sasa hakuna chuo kinachotoa kozi hiyo.

Hakikisheni taasisi hii inapata ithibati ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), ili kuwawezesha wahitimu wote wa ICoT kupata fursa za kujiendeleza na elimu ya juu.

Naye mratibu wa wataalam wa uanzishaji ICoT Profesa Peter Chonjo amesema wamejipanga kuhakikisha taasisi hiyo ya teknolojia ya ujenzi inakuwa ya mfano hapa nchini kwa kuwa itawezesha wataalam wengi wa ujenzi kuwa na weledi unaokubalika na kuibua uwezo wa ushindani katika soko la ajira na hivyo kuwezesha Tanzania kufikia malengo yake ya kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Tanzania inakadiriwa kuwa na mtandao wa barabara wenye zaidi ya kilometa elfu 87 na kati ya hizo elfu 35 ni barabara za kitaifa na elfu 52 ni barabara za Wilaya ambazo ujenzi wake unahitaji wataalam wa kutosha katika fani ya ujenzi na uendeshaji wa mitambo.

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – Sekta ya Mawasiliano Mhandisi Angelina Madete akisisitiza jambo alipokuwa akifungua warsha kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya ECOM Research Group Ltd, Profesa Godwin Daniel Mjema akifafanua jambo mbele ya wadau wa sekta ya ujenzi wakati wa warsha kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya ECOM Research Group Ltd, Profesa Godwin Daniel Mjema akifafanua jambo mbele ya wadau wa sekta ya ujenzi wakati wa warsha kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar es Salaam leo.
Mmoja wa wataalam elekezi wa uanzishaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), Profesa Beatus Kundi akifafanua jambo kwa wadau wa sekta ya ujenzi wakati wa warsha ya siku moja kuhusu uanzishaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu Mkurugenzi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – Sekta ya Ujenzi, Mhandisi John Ngowi (wa pili kulia) akifuatilia mada wakati wa warsha ya siku moja kuhusu uanzishaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – Sekta ya Mawasiliano Mhandisi Angelina Madete.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – Sekta ya Mawasiliano Mhandisi Angelina Madete(wanne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa sekta ya ujenzi mara baada ya kufungua warsha ya siku moja kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar es Salaam leo.

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAKABIDHI VIFAA VYA KUTAMBUA GESI ZINAZOHARIBU NA ZISIZOHARIBU TABAKA LA OZONI (REFRIGERANT IDENTIFIERS) KWA CHUO CHA VETA NA SHIRIKA LA VIWANGO TBS.

$
0
0
 Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi (kushoto)  akikabidhi kifaa kinachotumika kutambua gesi zinazoharibu na zisizoharibu  tabaka la ozoni (Refrigerant Identifier)  kwa Mkufunzi wa Chuo cha Ufundi stadi (VETA) Bwana Daudi Kadinda wakati wa makabidhiano Ofisini kwa Mkurugenzi huyo.
 Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi (kushoto) akikabidhi kifaa kinachotumika kutambua gesi zinazoharibu na zisizo haribu tabaka la ozoni(Refrigerant Identifier ) kwa Afisa toka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bwana Arnold Mato, wakati wa makabidhiano Ofisini kwa Mkurugenzi huyo.
 Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi akipeana mkono na Wataalamu kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  na Chuo cha ufundi Stadi VETA-Chang'ombe mara baada ya kuwakabidhi vifaa vya vinavyotumika kutambua gesi zinazoharibu na zisizoharibu  tabaka la ozoni.
 Pichani kifaa kinachotumika kutambua gesi zinazoharibu na zisizo haribu tabaka la ozoni(Refrigerant Identifier ) kinavyoonekana kwa ndani.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais  Bibi Magdalena Mtenga akijadiliana jambo na Wawakilishi toka TBS na VETA-Chang'ombe mara baada ya makabidhiano hayo.

BALOZI WA ISRAEL NCHINI AMALIZA MUDA WAKE

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Israel nchini anayemaliza muda wake Mhe. Yahel Vilan.

Balozi huyo alikutana na Makamu wa Rais na kumuaga rasmi kwani muda wake wa kutumikia nchini ulikuwa umemalizika. akamu wa Rais alisema anafurahi kuona Idadi kubwa ya Watalii kutoka Israel wanaokuja Tanzania .

“Tunawakaribisha sana Tanzania ,waje kwa wingi wao, tunawakaribisha kwa mikono miwili” na alimuhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuimarisha mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizi mbili.

Kwa upande wake Balozi Yahel alisema watalii kutoka nchini Israel wameongezeka kutokana na kuvutiwa na mazingira mazuri , amani na utulivu wa nchi.

Balozi Yahel alisema atakuwa mjumbe wa kuitangaza Tanzania popote duniani .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Israel nchini Mhe. Yahel Vilan (kushoto) ambaye muda wake wa kutumikia umemalizika na alifika kumuaga Mhe. Makamu wa Rais kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuaga .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Israel nchini Mhe. Yahel Vilan (kushoto) ambaye muda wake wa kutumikia umemalizika na alifika kumuaga Mhe. Makamu wa Rais kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuaga .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Israel nchini Mhe. Yahel Vilan (kushoto)ambaye muda wake wa kutumikia umemalizika na alifika kumuaga Mhe. Makamu wa Rais kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuaga .



 

RAIS DKT MAGUFULI AMUUNGA MKONO MLEMAVU ARON MICHAEL

$
0
0
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo  Mlemavu aitwaye Aron Michael Kipalilo ambaye ni mkazi wa kibondo mwenye ujuzi/fundi wa kushona nguo. Amekutana na Rais Magufuli na ameomba amshonee Kaunda Suti.Rais Dkt Magufuli yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya siku tatu ya kikazi
Rais Dkt John Pombe Magufuli akifurahia jambo na  mmoja wa Walemavu aitwaye Aron Michael Kipalilo ambaye ni mkazi wa kibondo mwenye ujuzi/fundi wa kushona nguo. Mlemavu huyo amekutana na Rais Dkt Magufuli amshonee Kaunda Suti.

Ujumbe Ubalozi wa Israel Watembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili Leo

$
0
0
 Ujumbe kutoka Ubalozi wa Israel nchini Kenya umetembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo. Maestro Nir Brand akipiga kinanda ili kuwaburudisha watoto wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kushoto ni Ofisa Uhusiano kutoka ubalozi huo, Angela Mogusu.  
 Watoto wanaotibiwa katika hospitali hiyo wakisikiliza moja wa wimbo uliokuwa ikiimbwa na Brand leo kwenye Jengo la watoto.
 Watoto wakicheza na Daktari Bingwa wa Watoto, Rehema Laiti leo.
  Ilala Brand akipiga makofi ikiwa ni sehemu ya kuungana wagonjwa leo.

 Dk. Shlomi Cohen akishiriki katika shughuli ya kuimba na kucheza na watoto hao leo.
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images