Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46129 articles
Browse latest View live

KIWANDA CHA KUZALISHA HOJA NI WATENDAJI WA HALMASHAURI; DKT NCHIMBI.

0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza katika baraza maalumu la madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakati wa kujadili hoja za Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu na Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally Mwanga.
 Watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi katika baraza maalumu la madiwani la kujadili hoja za Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Rustika Turuka akizungumza katika baraza maalumu la madiwani la kujadili hoja za Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi katika baraza maalumu la madiwani la kujadili hoja za Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.

BARABARA YA UYOVU-BWANGA-BIHARAMULO KUKAMILIKA MWISHONI MWA MWAKA

0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema mradi wa ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga-Biharamulo yenye urefu wa KM 112 inayojengwa na mkandarasi wa Kampuni ya Synohydro Corporation itakamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Prof. Mbarawa amezungumza hayo mkoani Kagera, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo na kumtaka mkandarasi aongeze kasi ili barabara hiyo iweze kukamilika kwa wakati.

“Hakikisheni mnaongeza kasi ya ujenzi ili muweze kukamilisha ujenzi huu kwa wakati iwezekanavyo”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.Amemsisitiza mkandarasi kuzingatia viwango vilivyopo katika mkataba kwani mwisho wa siku lazima watanzania wapate barabara inayokidhi mahitaji yao na ubora wake.

Amewapongeza wasimamizi wa barabara hiyo ambao ni kutoka kwa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kupitia kitengo chake maalum cha wahandisi washauri wazawa (TECU), kwa kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi M/S Sinohydro Corporation kwa ukaribu.

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Geita Eng. Harun Senkuku amemueleza Waziri Prof. Mbarawa kuwa changamoto ya fidia iliyokuwa inawakabili sasa imemalizika na kiasi cha shilingi milioni 700 zimetumika kukamilisha ulipaji fidia kwa wakazi wote.

Amemhakikishia Waziri kuwa TANROADS itaendelea kumsimamia mkandarasi huyo ili kuhakikisha thamani halisi ya fedha ya Serikali inapatikana.Mradi wa ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga-Biharamulo KM 112 umehusisha ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa KM 45 na barabara ya Bwanga-Biharamulo yenye urefu wa KM 67.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Sinohydro Corporation Ltd anayejenga barabara ya Uyovu-Bwanga KM 45 kwa kiwango cha lami, mkoani Geita. 

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Bwanga-Biharamulo yenye urefu wa KM 67, mkoani Geita. 
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Geita Eng. Harun Senkuku akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, kuhusu maendeleo yaliyofikiwa ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa KM 45, mkoani Geita. 

Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma yatumia Tehama kuboresha utoaji wa huduma kwa umma

0
0

Je unajua jinsi TEHAMA inavyoboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma katika Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. Usikose kuangalia kipindi hiki uone jinsi ambavyo TEHAMA inasaidia kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma katrina taasisi hiyo

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA KAGOMA-BIHARAMULO-LUSAHUNGA YENYE UREFU WA KILOMETA 154

0
0
 Rais Dkt John pombe Magufuli mapema leo amefungua barabara ya Kagoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa Kilometa 154. Barabara hii ni muhimu kwa uchumi wa mikoa ya kanda ziwa, kanda ya kati na kanda ya magharibi. Inaunganisha mikoa ya Kagera, Geita, Kigoma, Mwanza, Shinyanga na nchi jirani za Burundi, Uganda na Rwanda
 Rais Dkt John pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya akina Mama waliofika kushuhudia hafla fupi ya ufunguzi wa barabara ya Kagoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa Kilometa 154. Barabara hii ni muhimu kwa uchumi wa mikoa ya kanda ziwa, kanda ya kati na kanda ya magharibi. Inaunganisha mikoa ya Kagera, Geita, Kigoma, Mwanza, Shinyanga na nchi jirani za Burundi, Uganda na Rwanda.

HABARI ZAIDI TUTAWALETEA BAADAE KIDOGO.

TANZANIA IS RATED THE BEST SAFARI COUNTRY OF 2017 IN AFRICA

0
0

THE NETHERLANDS– SafariBookings.com has conducted an in-depth analysis of reviews from safari tourists and acclaimed Africa experts to determine the continent’s best country for safaris. And the winner? TANZANIA came out on top – the country is the clear winner and has been awarded our best safari country for 2017.

More than 2,500 reviews were used in this comprehensive research. Contributions came from safari-goers all over the world. And 22 reputable guidebook authors – working for Lonely Planet, Rough Guides, Frommer’s, Bradt and Footprint, who make-up the SafariBookings expert panel – also contributed reviews.

Tanzania with its teeming wildlife and astounding natural beauty on average had the highest scores. The country won only by a slim margin though from Zambia. Interestingly, when the results are broken down, members of the expert panel rated Tanzania the highest while safari tourists had a preference for Zambia.

In 2013 SafariBookings conducted its first-ever review analysis to determine the best country for safaris in Africa. Tanzania won that contest clearly. However, because things change so rapidly in Africa we conducted another analysis in 2017, using new reviews from safari tourists and from the guidebook authors on our expert panel. One thing that hasn’t changed is Tanzania’s popularity, once again voted the best safari country in Africa.

Best country for wildlife

SafariBookings analysis also determined that Tanzania was the best country in Africa for spotting wildlife. Given the exceptional wildlife-viewing opportunities in parks such as the superlative Serengeti and the wildlife-rich Ngorogoro Conservation area, this was unsurprising.


Recently, Tanzania has received a good number of famous superstars from around the Globe visiting her tourist attractions. Those visitors includes the former Israel Prime Minister, Ehud Barak, football superstars such as David Beckham, Morgan Schneiderlin, Mamadou Sakho, Victor Wanyama, Christian Erikssen, Wayne Rooney and Everton Football Club. Others who fall under the category of Musician and Actors includes Will Smith, Usher Raymond, Harrison Ford and Sanjay Dutt of India.


Indeed, Tanzania is the Africa Tourist Destination.


WELCOME/KARIBU ! #visittanzania The land of #kilimanjaro#zanzibar and the #serengeti

YOU MAY ALSO REFFER THE NEWS FROM SAFARIBOOKINGS BY CLICKING THE LINK BELOW: https://www.safaribookings.com/blog/best-safari-country-2017

JUMIA TRAVEL YAZINDUA YAUNGANISHA MFUMO WA HUDUMA KWA WATEJA NA FACEBOOK MESSENGER

0
0

Kampuni inayoongoza kwa uwakala wa huduma za kusafiri mtandaoni Afrika, Jumia Travel imezindua mfumo mpya wa huduma kwa wateja kupitia ‘Facebook Messenger’ kwa kushirikiana na Salesforce (Kampuni kinara kwenye Usimamizi wa Huduma kwa Wateja)

Na Jumia Travel

KATIKA kuboresha utoaji wa huduma Jumia Travel imeuunganisha mfumo wake wa kuwasiliana na wateja kupitia Facebook Messenger. Kuunganishwa kwa ‘Messenger’ kwenye mfumo wa utoaji wa huduma wa Jumia Travel ni ishara ya mapinduzi makubwa kwenye kuwapatia wateja uzoefu, kwani unatoa fursa ya kuwasiliana moja kwa moja kwenye Facebook messenger. 
Njia hiyo pia inaweza kutumika kuomba huduma ya chumba hotelini papo hapo, ambapo wataalamu wa masuala ya kusafiri wa kampuni watakuwa wakitoa ushauri juu ya machaguo bora zaidi ya malazi pamoja na kufanya huduma.

Ikiwa ni kampuni ya kwanza barani Afrika kuunganisha huduma ya Facebook Messenger kwenye mfumo wake wa utoaji huduma, Estelle Verdier, Afisa Mkuu wa Oparesheni na Mwasisi-mwenza wa Jumia Travel amesema kuwa, “hii ni hatua katika kuonyesha namna tulivyojipanga siku zote kuwaletea wateja wetu teknolojia za kisasa na huduma zenye ubora wa hali juu.”

Kwenye ripoti waliyoizindua hivi karibuni juu ya sekta ya utalii Tanzania, Jumia Travel imebainisha kuwa 65% ya utafutwaji wa huduma za hoteli kwenye mtandao wao hufanyika kupitia simu za mkononi huku 35% ndiyo wanaofanya huduma. Ukulinganisha na wateja wanaoutumia kompyuta 40% hutumia kwa kutafuta huduma wakati 60% ndio wanaofanya huduma.

“Kwa upande wa Afrika, kupenya kwa matumizi ya barua pepe (e-mail) kumekuwa ni kwa kusuasua kutokana na njia hiyo kutotoa fursa ya mazungumzo ya mara kwa mara na haisawiri kwa kiasi kikubwa kwenye simu za mkononi.
 
Kwa kuunganisha utoaji wa huduma na Messenger, tumewaletea wateja wetu njia ya papo kwa papo na rahisi ya kuwasiliana nasi kwenye simu za mkononi kupitia Facebook. Tuna imani kwamba Facebook Messenger itakuwa ni njia kuu kwa miaka ijayo, na kipengele hiki kipya kwetu kitaturuhusu kuongeza namna ya kuwasiliana na wateja wetu kupitia Messenger,” alisema Stanislas Dinechin, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Jumia Travel Kimataifa.

“Kwetu sisi hii ni fursa kubwa kwa kuweza kuunganisha mfumo wetu wa huduma kwa wateja na Facebook Messenger kwa sababu watanzania wengi wanaipata kupitia simu zao za mkononi. Tunatumaini wateja wataupokea mfumo huu mpya na kuutumia vizuri katika kufurahia huduma zetu,” alithibitisha Fatema Dharsee, Meneja Mkazi wa Jumia Travel Tanzania.

Njia hii pia itakuwa ikitumika kushughulikia masuala na maombi mbalimbali ya wateja kama vile huduma ya usafiri kutoka uwanja wa ndege pamoja na kubadili huduma ya malazi iliyokwishafanyika. Afrika ikiwa na watumiaji wengi wa simu za mkononi, Facebook Messenger inatoa fursa kubwa ya kuwafikia watu wengi ukijumuisha na wa kwenye mitandao mingine ya kijamii ukilinganisha na wanaotokana na kumtembelea mtandaoni.

Milioni 20 za Biko zakimbiza homa ya Marianus wa Chanika

0
0
AWADI nono ya Sh Milioni 20 zinazotolewa na Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, zimekimbiza homa ya mshindi wa droo ya 24 ya Biko, iliyotangazwa leo jijini Dar es Salaam, huku akiipata mkazi wa Chanika, jijini Dar es Salaam, Enos Marianus.

Akizungumza kwa njia ya simu wakati anapewa taarifa za ushindi wake na Balozi wa Biko, Kajala Masanja, Marianus alisema kwamba amekuwa mchezaji mzuri wa Biko, huku habari za ushindi wake zikiikimbiza homa iliyokuwa inamsumbua kwa wiki moja sasa.

Marianus alisema kwamba ushindi wa Sh Milioni 20 aliyotangazwa na Biko utakuwa muafaka kwake kutokana na kujihusisha na biashara ndogo ndogo kwa ajili ya kusukuma mbele gudurumu la maisha yake.

“Nashukuru sana kwa kunitangaza mimi kuwa ni mshindi wa droo ya 24 ya Biko, hivyo hapa hata homa inayonisumbua imeondoka na nimepona kabisa kwa sababu ya habari zenu nzuri, nikiamini kwamba nikipata fedha hizo nitapiga hatua kubwa kiuchumi hususan katika biashara zangu,” Alisema Marianus.

Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba droo ya Jumatano imekwenda kwa mfanyabiashara mdogo wa Chanika, huku akiwataka wengine waendelee kucheza kwa ajili ya kuvuna donge nono la Sh Milioni 20 kwa Jumatano na Jumapili, pamoja na zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja.

“Biko ni mchezo rahisi kushinda na unaweza kubadilisha maisha ya Watanzania, hivyo endeleeni kucheza kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kuanzia Sh 1,000 na kuendelea, huku kiasi cha fedha cha Sh 1000 kikitoa nafasi mbili za ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa za Sh Milioni 20 za Jumatano na Jumapili, namba ya kampuni ikiwa ni 505050 na kumbukumbu ni 2456,” Alisema.

Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed, alisema mchezo wa Biko unachezeshwa kwa kufuata sheria zote za michezo ya kubahatisha, huku akiwataka Watanzania kuuamini na kutumia fursa za ushindi kwa ajili ya maisha yao.

Biko ni mchezo wa kubahatisha unaotikisa katika viunga mbalimbali vya Tanzania, huku mwezi Mei na Juni pekee ukitoa zaidi ya Sh Bilioni moja kwa washindi wake walioshinda zawadi mbalimbali kutoka kwenye bahati nasibu hiyo, huku mshindi wa droo ya 24 akitarajiwa kukabidhiwa fedha zake haraka iwezekanavyo.


Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akizungumza kwa simu na mshindi wa droo ya 24 ya Biko , Enos Marianus, aliyejizolea jumla ya Sh Milioni 20 atakazokabidhiwa haraka wiki hii. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed, akiandika dondoo za mshindi huyo wakati anazungumza kwa njia ya simu mara baada ya namba yake kuibuka kidedea katika droo hiyo ya 24. Picha na Mpigapicha Wetu.

SERIKALI HAIJAFUTA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA UMMA

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akipokewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Mhe. Charles Kwiyeko alipofanya ziara ya kikazi katika Manispaa hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema akitoa hotuba ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuzungumza na watumishi wa umma katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Manispaa hiyo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Bw, Msongela Palela akiwasilisha taarifa ya manispaa anayoiongoza kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika Manispaa hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala alipofanya ziara ya kikazi  katika Manispaa hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (Hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mthibiti Mkuu Ubora wa Shule – Manispaa ya Ilala, Bi. Juliana Mhonyiwa akiwasilisha hoja wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha watumishi wa umma Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) leo Jijini Dar es Salaam.

Serikali haijafuta mafunzo kwa watumishi wa umma ambapo Taasisi za Serikali zimeelekezwa kuandaa Mpango wa Mafunzo kwa watumishi kwa njia ya uwazi na shirikishi ili kuepuka malalamiko kutoka kwa baadhi ya watumishi wa umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Kairuki amesema mwajiri anapoandaa Mpango wa Mafunzo kwa watumishi wake ni vyema mpango huo ukawa shirikisha kwa watumishi wote ili kujua mpangilio wake, ikiwa ni pamoja na kuandaa orodha ya ziada ya watumishi watakaochukua nafasi za wale waliopangwa kushiriki mafunzo lakini wakashindwa.

“Napokea malalamiko mengi sana kuhusiana na upendeleo katika suala la mafunzo, napenda kuwasisitiza waajiri tuandae Mpango wa Mafunzo ambao ni shirikishi kwa watumishi wote kuepuka haya, wengine wanapangwa na hawashiriki mafunzo,” Mhe. Kairuki amesema na kuongeza baadhi ya watumishi wa umma wanapangwa kushiriki mafunzo na hawaendi kwa sababu mbalimbali, lakini fursa ya nafasi hizo hawapangiwi wengine ili kuendana na mpango.

Mhe. Kairuki ameongeza kuwa Mpango wa Mafunzo shirikishi pamoja na kuondoa malalamiko, utasaidia pia kutorudisha fedha zilizobaki kwa watumishi wa umma ambao walipangwa lakini wakashindwa kuhudhuria mafunzo kwa sababu mbalimbali.

Aidha, Mhe. Kairuki amesema kwa sababu ya kutoshirikishwa wapo wanaopotosha kuwa Serikali imefuta Mpango wa Mafunzo. “Napenda kuwaambia kuwa Serikali haijafuta mafunzo, ili mtumishi wa umma aweze kufanya kazi zake kwa weledi ni lazima ahudhurie mafunzo,” Mhe. Kairuki amesema na kusisitiza Serikali inajali mafunzo kwa rasilimaliwatu kwa matokeo bora.

Mhe. Kairuki yupo katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Dar es salaama ambapo leo ni siku ya nane akiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kukutana na watumishi wa umma wa kada zote katika vikao kazi.

Lengo la kukutana na watumishi wa umma ni kusikiliza malalamiko, ushauri na changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili kuweza kuzifanyia kazi na kuleta mabadiliko katika Utumishi wa Umma nchini ili kufikia malengo yaliyopangwa na Serikali.

EngenderHealth WATOA MSAADA WA VIFA TIBA KWA MKOA WA KIGOMA

0
0
Na Editha Karlo -Globu ya jamii-Kigoma

SHIRIKA la Kimataifa lisilo la kiserikali la EngenderHealth limetoa msaada wa vifaa tiba chini ya ufadhili wa Bloomberg kwa Mkoa wa Kigoma ili kuboresha huduma za afya ya uzazi.

Akiongea wakati wakukabidhi vifaa hivyo muwakilishi wa shirika la EngenderHealth kutoka makao makuu Dar es Salaam Dkt.Godson Maro alisema kuwa lengo lao ni kuendelea kuboresha huduma za uzazi,ikiwa ni sambamba na kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Dkt Maro alivitaja vifaa walivyotoa msaada kuwa ni pamoja na vitanda vya kujifungulia,mashine za kupima mapigo ya moyo ya mtoto,mzani wa kupima uzito,vitanda vya kupumzikia akina mama baada ya kujifungu,mashine ya kupima mapigo ya moyo ya mtoto akiwa tumboni na drip stand vyote vina thamani ya zaidi ya shilingi milioni 374.

"Vifaa hivi vitapelekwa katika zahanati mbalimbali zilizopo Mkoani hapa zenye upungufu wa vifaa tiba pia tutaendelea kushirikiana na serekali kuboresha huduma za afya ili kufikia malengo makubwa ya kupunguza vifo vya mama na mtoto"alisema

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt Paul Chawote alishukuru kwa msaada huo wa vifaa tiba kwani utawasaidia kutatua changamoto mbalimbali walizokuwa wanakutana nazo katika utoaji wa huduma.

Dkt Chawote alisema kuwa vifaa hivyo watavitunza vizuri ili visaidie wananchi wengi na kudumu kwa muda mrefu.

Alisema Mkoa wa Kigoma unachangamoto ya watumishi katika zahanati nyingi na sababu kubwa ni mbiundombinu hasa ya. barabara hali inayofanya watumishi wengi wakipangiwa kazi huwa hawafiki.

Muwakilishi wa shirika la kimataifa lisilo la kiserekali la EngenderHealth Dkt Godson Maro kutoka makao makuu Dar es Salaam akimkabidhi Mganga mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt Paul Chawote vifaa tiba vilivyotolewa na shirika hilo ili kuboresha huduma ya uzazi kwa mama na mtoto

Kikosi cha wafanyakazi wa shirika lisilo la kiserekali la kimataifa la EngenderHealth kutoka Dar es salaam na Kigomawakiwa katika picha ya pamoja baada ya makabidhino ya vifaa tiba.

RAIS DKT MAGUFULI KUFANYA ZIARA YA SIKU TATU YA KIKAZI MKOANI KIGOMA.

0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

RAIS Dkt John Pombe Magufuli anatarajia kuanza ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani Kigoma ambapo pamoja na mambo mengine atazindua barabara zenye kiwango cha lami na mradi wa maji.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga alisema kuwa Rais atawasili mkoani Kigoma kupitia Wilaya ya Kakonko tarehe July 21 akitokea Mkoani Kagera ambapo atafanya uzinduzi wa barabara iliyojengwa kwa kiwango cha lami kutokea Nyakanazi hadi Kibondo yenye kilometa 50.

Mkuu wa Mkoa alisema pia siku hiyo Rais atafanya mkutano wa hadhara na wananchi katika Wilaya ya Kakonko ili kusikiliza kero zao mbali mbali,pia Rais ataelekea Wilayani Kasulu ambapo pia atazindua barabara kidahwe mpaka kasulu iliyojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 63.

Maganga alisema July 22 Rais ataweka jiwe la msingi mradi wa maji uliopo Manispaa ya Kigoma Ujiji na kisha atafanya mkutano wa hadhara na wananchi katika uwanja wa Lake Tanganyika.

Na July 23 Rais ataelekea Wilayani Uvinza kwaajili ya kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji uliopo katika Kata ya Nguruka eneo la amani na baadae mkutano wa hadhara na wananchi.

Maganga amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais kwani hii ni ziara yake ya kwanza tokea uchaguzi Mkuu ufanyike.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia mstaafu Emanuel Maganga akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya ziara ya Rais Dkt John Pombe Magufuli Mkoani Kigoma.

SPIKA NDUGAI AONGOZA WABUNGE KATIKA MAZISHI YA MKE WAZIRI MWAKYEMBE, MAREHEMU LINAH MWAKYEMBE KYELA, JIJINI MBEYA.

0
0
 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisaini kitabu cha Maombolezo wakati wa mazishi ya Mke wa Waziri Wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Dkt Harisson Mwakyembe, Marehemu Linah Mwakyembe Wilayani Kyela, Jijini Mbeya.
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsabai Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Dkt Harisson Mwakyembe wakati mazishi ya Mke wake, Marehemu Linah Mwakyembe Wilayani Kyela, Jijini Mbeya.
 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Naibu Spika Dkt Tulia Ackson wakati wa mazishi ya Mke wa Waziri Wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Dkt Harisson Mwakyembe, Marehemu Linah Mwakyembe Wilayani Kyela, Jijini Mbeya.
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akitoa Salamu za heshima kwa mwili wa Mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Dkt Harisson Mwakyembe, Marehemu Linah Mwakyembe wakati wa mazishi yake nyumbani kwake Wilayani Kyela, Jijini Mbeya.
 Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa (wa kwanza toka kushoto)Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai, Naibu Spika Dkt Tulia Ackson wakifuatilia misa ya mazishi ya Mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Dkt Harisson Mwakyembe, Marehemu Linah Mwakyembe wakati wa mazishi yake nyumbani kwake Wilayani Kyela, Jijini Mbeya
Mweyekiti wa Wabunge wa Chuma cha Mapinduzi kutoka Mkoa wa Mbeya Mhe Victor Mwambalasu akizungumza kwa niaba ya Wabunge wa Mkoa huo wakati wa mazishi ya Mke wa Waziri Wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Dkt Harisson Mwakyembe, Marehemu Linah Mwakyembe Wilayani Kyela, Jijini Mbeya. Wengine katika picha ni Wabunge wa Chama cha Mapinduzi kutoka Mkoa wa Mbeya.

Picha na Ofisi ya Bunge

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA MAZISHI YA LINAH MWAKYEMBE

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiweka shada la Maua kwenye  kaburi la  Linah George Mwakyembe, mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe katika mazishi yaliyofanyika Kyela Julai 19, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo baada ya kuwasili nyumbani kwa Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe  kushiriki katika mazishi ya mke wa Waziri huyo, Linah George Mwakyembe yaliyofanyika Kyela Julai 19, 2017.  Kulia ni  mkewe Mary.

  Askofu, Rabison Mwakanani wa Kanisa la Evangelical Brotherhood la Mbeya akizungumza katika Ibada ya mazishi ya Linah George Mwakyembe , Mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sana na Michezo,Dkt. Harrison Mwakyembe yaliyofanyika Kyela, Julai 19, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary  (wapili kushoto) wakishiriki katika ibada ya mazishi ya Marehemu, Linah George Mwakyembe, Mke wa Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Dkt Harrison Mwakyembe katika mazishi yaliyofanyika  Kyela Julai 19, 2017.  Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya  Amos Makalla, Spika wa Bunge, Job Ndugai, Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu kulia ni Waziri wa  Kilimo na Mifugo,   Dkt . Charles Tizeba.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na viongozi wa dini walioongoza ibada ya mazishi ya Linah George Mwakyembe, mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo,  Dkt. Harrison Mwakyembe yaliyofanyika  Kyela Julai 19,2017.
 aziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu, Linah George  Mwakyembe, mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe katika mazishi yaliyofanyika Kyela, Julai 19, 2017.
 Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt.  Harisson Mwakyembe pamoja na familia yake wakiwa pamoja na waombolezaji wakati wa Ibada ya ya mazishi ya mkewe, Linah George Mwakyembe yaliyofanyika Kyela, Julai 19, 2017.
 Mwili wa Linah George Mwakyembe , mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ukiteremshwa kaburini katika mazishi yaoiyofanyika Kyela, Julai 19, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mbeya, Erasto Zambi (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songwe mkoani mbeya kuhudhuria mazishi ya Linah George Mwakyembe yaliyofanyika Kyela, Julai 19, 2017.

Tigo kuungana na wabia wengine kuongeza kasi katika upatikanaji wa Mtandao wa simu kwa wananchi 70,000 katika maeneo ya vijijini Tanzania

0
0
Kaimu Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Tigo Simon Karikari (wa kwanza kulia) akchangia mada wakati wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa na GSMA360 Afrika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
kampuni ya simu ya maisha ya kidigitali  inayoongoza Tanzania, Tigo, Pamoja na wabia wengine, wameshirikiana katika kuweza upatikanaji wa mtandao wa broadband kwa watu takribani 70,000 katika maeneo yaliyochaguliwa katika maeneo ya vijijini ya Tanzania.
Ushirikiano na waendeshaji  wengine wa mitandao ya simu (MNOs) (Mobile network Operators), serikali ya Tanzania na Chama cha kutetea maslai ya waendeshaji wa mitandao ya simu duniani GSMA (Global System Mobile Association), uliundwa kutatua changamoto za upatikanaji wa mtandao katika maeneo ya vijijini kwa kuanzisha maeneo ya majaribio kama sehemu inayokusudiwa ya mradi wa upatikanaji wa mawasiliano.  
Katika ujumbe wake katika kongamano linaloendelea la GSMA la 360 - Afrika lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam leo, Kaimu Mkurugenzi wa Tigo  Bwana Simon Karikari, alisema kwamba ni kwa kutumia ushirikiano wa sekta ya umma na sekta binafsi ndipo ambapo tunaweza kukabiliana na changamoto za kidigitali, hivyo kukuza mageuzi ya kidigitali ya Afrika.
"Kutoa uunganishaji wa simu wa Broadband kwa jamii za vijijini ni moja kati ya changamoto kubwa ambazo waendeshaji wanakabiliana nazo hapa Tanzania leo. Hii ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo: Upatikanaji wa Umeme, Mgawanyiko wa watu kijiografia, na uwezo wa kumudu gharama - hata ambapo huduma za data ni moja kati ya huduma za bei nafuu zaidi katika eneo hilo", alisema Karikari. 
Akielezea kuhusu ushirikiano, Karikari amesema kwamba wameingia katika makubaliano ya pande tatu ya roaming ambayo maeneo ya majaribio yatawezesha upatikanaji wa mtandao wa broadband kwa wateja wa mitandao yote kutoka katika mnara mmoja, jambo ambalo litawasaidia watumiaji kutumia mitandao ya kila mmoja wao katika eneo lililochaguliwa.
Mkurugenzi alipongeza ushirikiano wa sekta zaidi ya moja akieleza kwamba ushirikiano huo umewezesha kufanikisha mradi wa roaming wa njia tatu Afrika.
"Kudokeza baadhi tu ya matokeo yetu", Karikari aliongeza kwamba, "Tayari kulikuwa na watumiaji 17,000 wa simu kila siku baada ya uzunduzi. Leo zaidi ya wakaazi elfu 40 wa maeneo ya vijijini wanapata huduma ya 3G kwa mara ya kwanza, idadi inakadiriwa kuongezeka kufikia elfu 70 kufikia mwishoni mwa mwezi Juni 2017).
Akishukuru serikali ya uungaji mkono wake katika kutekeleza mradi huu, Hata hivyo Karikari alisema kwamba, aina fulani ya ruzuku, motisha na makubaliano kama vile kodi katika miundombinu kutoka serikalini, inakaribishwa kusaidia MNOs kupungaza baadhi ya gharama zinazotokana na uanzishaji wa maeneo ambayo hayaja lipwa na mapato yanyotokana na mradi.    
"Tunaamini kwamba mradi huu, pamoja na upekee wake, utaweka uwezekano kwa bara zima la Afrika. Tutaendelea kushirikiana na Serikali, TCRA (Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania), UCSAF (Mfuko wa upatikanaji wa huduma ya mawasiliano Tanzania), na taasisi zingine kutafuta ufumbuzi wa changamoto tulizo zigundua na kuangalia namna tutakavyotumia tuliyojifunza kutoka katika mradi huu kuboresha huduma zetu na hatimaye kuleta uunganisho wa simu Tanzania". Alihitimisha Karikari

WILAYA YA GEITA KUTENGA MILIONI 50 KWA AJILI YA MAFUNZO YA KUBORESHA KILIMO

0
0


Mkuu wa Wilaya ya Geita Herman Kapufi akizungumza wakati akifungua  mafunzo ya siku moja kwa maofisa ugani  wa wilayani yake wilayani humo jana yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),  yenye lengo  la kuwakumbusha wataalamu hao wa kilimo nafasi yao pamoja na kuwapatia mbinu mpya za kisasa katika kulima mazao ya Mihogo, Pamba na Viazi vitamu katika kuelekea serikali ya viwanda.
Picha ya pamoja.
Maofisa ugani wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mratibu wa Jukwaa la bioteknolojia kwa maendeleo ya kilimo nchini OFAB bwana Philbert Nyinondiakizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo.
Mshauri wa Jukwaa la Masuala ya Bioteknojia OFAB, Dk.Nicholaus Nyange (kushoto), akitoa mada kuhusu matumizi ya Bioteknolojia katika kilimo.

Na Dotto Mwaibale, Geita

HALMASHAURI ya Wilaya ya Geita Mkoani Geita imesema itahakikisha inatenga bajeti  ya shilingi milioni 50 kuwezesha mafunzo na kuboresha sekta ya kilimo kutoka  kwenye fedha zake pamoja nakuwaomba  wadau wengine wa wilaya kama vileKampuni ya uchimbaji dhahabu ya geita GGM kuchangia milioni 200 ili kuinua sekta hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya hiyo,  Herman Clement Kapufi wilayani humo  jana wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa maofisa ugani wote wa wilayani yake  yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),  yenye lengo  la kuwakumbusha wataalamu hao wa kilimo nafasi yao pamoja na kuwapatia mbinu mpya za kisasa katika kulima mazao ya Mihogo, Pamba na Viazi vitamu katika kuelekea serikali ya viwanda.

Mkuu huyo wa wilaya amesema kazi hiyo nzuri iliyoanzishwa na COSTECH kupitia  Jukwaa la Bioteknolojia nchini (OFAB) hazitakuwa na maana endapo mafunzo hayo  hayatasimamiwana halmashauri yake ili kuhakikisha yanakwenda kuleta mabadiliko na  mapinduzi kwenye kilimo kwa wakulima kwenye maeneo mbalimbali. 

Kapufi amemtaka mkurugenzi wa halmashauri kuhakikisha anaweka bajeti kugharamia  mafunzo ya aina hiyo kwa maofisa ugani na wakulima badala ya kuwaachia COSTECH .
kufanya kazi hiyo peke yao wakati wanufaika ni wananchi wa wilaya hiyo na hivyo  kuahidi kuzungumza na wawekezaji wenye migodi kuweka bajeti kusaidia kilimo kwenye  fedha mbalimbali zinazotolewa nao kwaajili ya maendeleo ya halmahauri.

Amesema anatambua kuna wakulima wengine hawapendi kubadilika pale wanapofikishiwa  utaalamu lakini amewataka maofisa ugani hao kuto kata tamaa na badala yake wawe na mashamba yao binafsi ya mfano ambayo yatalimwa kwa kutumia kilimo cha kisasa na  mbegu bora ili waone badala ya kuzungumza kwa nadharia kila siku.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya hiyo Ali Rajabu,  amewapongeza watafiti hao kutoka COSTECH,OFAB na Kituo cha utafiti wa Kilimo Ukiriguru cha Mwanza  kwa kusaidia kuwawezesha maofisa ugani hao kupata mbinu bora  zaidia za kukabiliana na changamoto za kilimo kwa wakulima kwa kutumia teknolojia  za kisasa na kuiomba Halmashauri kuwapa vitendea kazi maofisa ugani wanaofanya  vizuri kwenye kata zao.

Amesema maofisa ugani ndio injini ya kilimo maana ndio wenye jukumu la kuwasaidia  wakulima kulima kisasa na kuzalisha kwa tija ikizingatiwa kuwa bila chakula hakuna  mtu anayeweza kufanya kazi na njaa hivyo tunahitaji chakula ili kuweza kufikiria 
kufanya kazi zingine za kimaendeleo.

Ameiomba COSTECH kutoishia kwenye wilaya hii pekee bali mafunzo ya aina hiyo  yafanywe nchi nzima kwani uhitaji ni mkubwa kwenye kila wilaya ili kuwakumbusha  kazi wataalamu hao wa kilimo na pia kuwapa mbinu mpya za kutatua changamoto  zinazowakabili wakulima kwenye mazao hayo ya pamba mahindi, mihogo na viazi lishe

Amesema imefika wakati sasa wananchi wa mkoa huo kubadilika na kutofikiria dhahabu kila wakati badala yake wajishughulishe na shughuli za kilimo tena cha kisasa kwa kutumia fursa ya ziwa Victoria katika kulima kilimo cha umwagiliaji na hivyo kuongeza tija

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa wilaya Mratibu wa Jukwaa la  Biotehnolojia kwa maendeleo ya kilimo nchini (OFAB)Philbert Nyinondi kwa niaba ya  COSTECH amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwasaida wataalamu hao wa kilimo kupata  mbinu mpya za uzalishaji na kuwajengea uwezo kwenye kuzalisha mazao hayo muhimu  ambayo yana mchango mkubwa katika kusaidia kupata malighafi kwaajili ya viwanda.

Amesema mafunzo hayo baada ya kutolewa kwa maofisa ugani pia yatatolewa kwa  wakulima kwenye vikundi na kisha kuwapatia mbegu bora na safi za mihogo na viazi  lishe ili kuanzisha mashamba darasa kwenye vijiji vitakavyochaguliwa ili wakulima 

waweze kuona na kujifunza na kisha kuwa sehemu ya mbegu bora kwenye wilaya.

Nyinondi amesema mpango huu ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Taifa  ya Sayansi na Teknolojia katika kuhakikisha sayansi,teknolojia na tefiti nzuri  zinawafikia walengwa na kuleta tija kwenye sekta husika ili kuongea tija.

TAARIFA YA ONYO KALI KUTOKA WIZARA YA MAMBO YA NDANI

0
0

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA RIPOTI YA NCHI YA APRM

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya nchi kuhusu Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa afrika kujipima kwa Vigezo vya Utawala (APRM). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akionyesha kitabu chenye ripoti  ya nchi kuhusu Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa afrika kujipima kwa Vigezo vya Utawala (APRM) mara baada ya kuzindua taarifa hiyo kwenye Kituo cha Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amezindua Taarifa ya Nchi kuhusu Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa Afrika kujipima kwa Vigezo vya Utawala (APRM).Uzinduzi huo  ulihudhuriwa na  kiongozi wa Jopo la Mchakato huo kwa Tanzania ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo  la Watu Mashuhuri Bi. Brigitte Sylvia Mabandla, Viongozi wengine wa APRM Tanzania ni Balozi Ombeni Sefue, Profesa Hasa Mlawa na Balozi Aziz Mlima aliyemuwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na baadhi ya Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

APRM ni mpango wa hiari wa kujipima kwa vigezo vya utawala bora uliobuniwa mwaka 2003 na Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. Lengo la mpango huu ni kuziwezesha nchi  wanachama kujitathmini kwa vigezo vya utawala bora katika maeneo manne ambayo ni; Demokrasia na Utawala wa Kisiasa; Usimamizi wa Uchumi; Utendaji wa Mashirika ya Biashara; na Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi.

Akihutubia katika uzinduzi huo, Makamu Rais amewapongeza Wakuu wa Nchi na Serikali wanaoshiriki katika mchakato wa APRM kwa ujasiri wao wa kushirikishana taarifa za kuaminika kuhusu masuala ya utawala bora katika nchi zao. “Taarifa hizi zinaonesha wazi juu ya hali ya utawala bora katika Bara letu na kutupa nafasi ya kujirekebisha pale ambapo kuna dosari na kujipongeza pale tunapofanya vizuri na kuwapa wengine nafasi ya kujifunza zaidi’’ alisema Makamu wa Rais.

Aidha alisisitiza kuwa kupitia utaratibu huu tumeweza kuuonesha ulimwengu nguvu zetu za pamoja kama Bara la Afrika katika kuboresha demokrasia, amani na utulivu, utawala wa sheria na utawala bora kwa ujumla.

Kwa upande wa Tanzania, Makamu wa Rais alisema mchakato huu unatuonesha na kutukumbusha falsafa na maono ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Nyerere (Tujisahihishe, 1962) na Mwongozo wa TANU wa mwaka 1971.  Alisema nchi yetu imefanya mambo mengi katika kutekeleza mpango huo ikiwemo kuimarisha taasisi zinazoshughulikia masuala ya utawala bora ikiwemo Tume ya Haki za binadamu na Utawala Bora, taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa na sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma.

Kuhusu changamoto zilizobainishwa kwenye taarifa husika, Makamu wa Rais alisema kwa kiasi kikubwa zimepatiwa ufumbuzi katika Mkakati wetu wa Maendeleo 2025 unaolenga kukuza na kupanua wigo wetu wa uchumi ili kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.  Kuhusu suala la Muungano alisema muundo wa Muungano wetu ni wa serikali mbili ambazo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Makamu wa Rais alisema miongoni mwa maeneo ya vipaumbele katika mchakato wa kuelekea kuwa nchi ya viwanda  ni kuimarisha sekta ya nishati na umeme. “Kwa ujumla tumefanya jitihada kubwa katika huduma ya nishati kutokana  na ugunduzi mkubwa wa gesi asilia hapa nchini” alisisitiza Makamu wa Rais. Kwa sasa umeme unasambazwa kwa kasi katika vijiji vyetu kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Serikali imefanya jitihada kubwa katika kuzipatia ufumbuzi changamo za kijamii kama vile elimu, afya na maji ambazo zilitajwa kama vikwazo katika taarifa husika. Aidha, Serikali imeongeza uandikishaji wa wanafunzi kwa shule za msingi na sekondari, imeboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, imejenga madarasa na maabara, imeboresha maslahi ya walimu na kuhakikisha inajenga vyuo vya ufundi katika kila wilaya.

Pia Makamu wa Rais alisema Tanzania inatambua kuwa mchakato huu wa APRM ni endelevu hivyo serikali itaendelea na jitihada zake kuhakikisha kwamba changamoto zote zilizobainishwa ndani ya taarifa zinapatiwa majawabu kupitia serikali na taasisi zake, asasi binafsi na wananchi kwa ujumla.

Mwisho, alishukuru na kutambua mchango wa washirika wa maendeleo katika kufadhili kazi za APRM na kuwaalika kuendelea kuchangia shughuli za APRMTanzania ikiwemo mpango kazi wa Taifa.

TUTAWASHUGHULIKIA WANAOTOA MATAMSHI YA KICHOCHEZI-MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itawashughulikia watu wote wanaotoa matamshi ya kichochezi nchini bila ya kujali nyadhifa zao.

Amesema ni vema watu wakawa makini na kijiepusha kutoa matamshi ambayo yataathiri mfumo wa maisha kwa wananchi wengine.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Julai 19, 2017) wakati wa ibada ya mazishi ya mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe Bibi Linnah Mwakyembe iliyofanyika wilayani Kyela.

Amesema Serikali haitavumilia kuona baadhi ya watu wakitoa matamshi ambayo hayana tija kwa jamii na badala yake yanalenga kuwavuruga wananchi na kuchochea migogoro."Tutashughulika na watu wote wanaotoa matamshi ya kichochezi, popote walipo bila ya kujali uwezo wao, vyeo vyao na mamlaka walizonazo."

Pia amewaomba viongozi wa dini waendelee kuliombea Taifa na viongozi wake na kwamba Serikali inawategemea na iko pamoja nao. Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo baada ya Askofu wa Kanisa la Evarinjerical Brother Hood, Rabison Mwakanani kuonya vitendo vya baadhi ya watu kumtukana Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli.

Amesema ni vema watu hao wakajifunza namna ya kuwasilisha hoja zao bila ya kutumia lugha za matusi. “Rais Dkt. Magufuli amefanya mambo mengi makubwa kwa ajili ya maendeleo. Wanaofanya hivyo wasidhani kama wanamtukana Rais tu bali wanawatukana Watanzania wote waliomchagua wakiwemo viongozi wa dini.”

Pia aliwaomba wananchi kufanya maandalizi mapema kwa sababu wote ni wapitaji, hivyo waandae roho zao kwa kuacha kufanya dhambi na maovu yote ili wawe na mwisho mwema. Vile Vile Waziri Mkuu amewaomba wananchi wote washirikiane kwa pamoja kumuombea Dkt. Mwakyembe na familia yake ili Mwenyezi Mungu aweze kuwafariji katika kipindi hiki kigumu.

“Wajibu wetu sote ni kumuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema. Tunajua kwa sasa Dkt. Mwakyembe yuko katika wakati mgumu, namuhakikishia kwamba hayuko peke yake kwani Serikali iko pamoja naye katika kipindi hiki kigumu.”

Naye, Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai alimpa pole Dkt. Mwakyembe huku akiitaka familia kuendelea kuwa na upendo kama ule uliokuwepo wakati wa uhai wa marehemu Bibi Linnah.

Kwa upande wake, Mtoto mkubwa wa marehemu, George Mwakyembe alisema anaamini mama yao, alijiandaa na kifo hicho kwa kuwa alikuwa mchamungu. "Mama alikuwa na ratiba kila siku ifikapo saa nne usiku lazima afanye ibada, Hivyo nina matumaini makubwa kupitia Uchamungu wake, Mwenyezi Mungu atamuweka mahala pema."


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, JUMATANO, JULAI 19, 2017

MASAUNI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA PWANI, AAMURU KAMANDA WA TRAFIKI PWANI AONDOLEWE

0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimuuliza maswali Dereva wa basi la Safari Express lifanyalo safari zake Dar es Salaam kwenda Arusha, wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Mabasi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani. Masauni alimuagiza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu (wapili kushoto) kumuondoa Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kukagua magari na kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiwauliza maswali abiria wa basi la Safari Express lifanyalo safari zake Dar es Salaam kwenda Arusha, wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Mabasi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani. Masauni aliiagiza Jeshi la Polisi kumuondoa Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kufanya ukaguzi wa magari na kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimpa maelekezo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi, Jonathan Shana, wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Mabasi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani. Masauni alimuagiza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu (wapili kulia) kumuondoa Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani, Abdi Isango (wapili kushoto) katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kukagua magari na kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akizungumza na waendesha bodaboda wa Mji wa Chalinze, wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Mabasi, Kibaha Maili Moja, Chalinze na Bagamoyo mkoani Pwani. Masauni aliwataka waendesha boda boda hao kufuata sheria za barabarani na pia alimuagiza Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu (wapili kulia) kumuondoa Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kukagua magari na kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akiwa katika ukaguzi wa mabasi katika kituo cha mabasi cha Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani ambapo alifanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo. Masauni alimuagiza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu (kulia) kumuondoa Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) mkoani humo katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kufuata maelekezo aliyowahi kupewa ya kukagua magari na kusimamia sheria za usalama barabarani.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimpa maelekezo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu (kulia) wakati alipokua anazungumza na askari wa usalama barabarani katika eneo la Sanzale, Bagamoyo. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza Kituo cha Mabasi Kibaha, Chalinze pamoja na kukagua barabara hadi kufika mjini Bagamoyo.

Na Felix Mwagara (MOHA)
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amelitaka Jeshi la Polisi kumuondoa katika nafasi ya Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo.
Masauni akiwa ameambatana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu, alitoa agizo hilo katika Kituo cha Mabasi cha mjini Kibaha Maili Moja baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo leo, kwa ajili ya kufuatilia maelekezo yake aliyoyatoa alipofanya ziara kama hiyo mwaka jana.
“Mwaka jana nilipofanya ziara kituoni hapa nilitoa maelekezo nilipokuta kuna mapungufu katika ukaguzi wa magari, tukakubaliana atayafanyia kazi haraka iwezekanavyo, lakini hakuna mabadiliko yoyote, magari hayakaguliwi, huku ni kuhatarisha usalama wa abiria,” alisema Masauni na kuongeza kuwa;
“RTO ameshindwa kuendana na kasi ya awamu ya tano, nataka aondolewe katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua ya kinidhamu, hatutati uzembe, hatutaki kucheza na maisha ya watanzania.”
Masauni mara baada ya ukaguzi wa kituo hicho, aliendelea na ziara yake mkoani Pwani ambapo alifanya ukaguzi wa aina hiyo mjini Chalinze na baadaye Msata na kuimalizia ziara yake Bagamoyo.
Akiwa mjini Chalinze, Masauni alizungumza na waendesha bodaboda na kuwapa maelekezo kuhakikisha wanafuata sheria za usalama barabarani kwa kutobeba mishikaki, uvaaji wa kofia ngumu na pia kufuata sharia zote za usalama barabarani. 
“Mmenihakikishia kwa wale ambao hamkua na kofia ngumu kuwa mkitoka hapa mtakwenda kuzitafuta, hakikisheni mnafanya hivyo kwa usalama wenu pamoja na abiria mnaowabeba, ipendeni kazi yenu kwa kuheshimu sharia za usalama barabarani,” alisema Masauni. 
Akiwa njiani kuelekea Chalinze mpaka Bagamoyo, Masauni ambaye gari yake ilitolewa namba zinazomtambulisha nafasi yake (NWMNN), na kuweka namba za kawaida ili kujua kama akiendesha kwa mwendokasi barabarani matrafiki watalisimamisha gari lake, hata hivyo askari wa usalama barabarani sehemu kubwa hawakuwepo barabarani na pia waliokuwepo hawakuweza lisimamisha gari lake.
Kutokana na hatua hiyo, Masauni akagundua kuwa kuna uzembe mkubwa unaofanywa na matrafiki mkoani humo kwa kutofanyakazi zao kwa umakini, na kwa uzembe huo ndio chanzo cha ajali zinazotokea barabarani mara kwa mara.  
Akizungumza na matrafiki wilayani Bagamoyo ambao walifanya uzembe huo, aliwataka wabadilike haraka iwezekanavyo kufuata wajibu wao, na pia alitoa siku tatu kuhakikisha wanawakamata waendesha bodaboda wote ambao wanavunja sheria za usalama barabarani, na pia baada ya operesheni hiyo apewe ripoti haraka iwezekanavyo, na muda wowote atafanya ziara ya kushtukiza kuona kama maelekezo hayo wameyafanyia kazi.
“Bodaboda nimeziona nyingi zinapita hapa zikiwa zinavunja sheria, madereva na abiria hawajavaa kofia ngumu, na nyie mpo hapa mnaziangalia, sasa nawaagiza mtekeleze maagizo niliyotoa na pia sio nyie tu bali nchi nzima wahakikishe wanayakagua magari pamoja na bodaboda, na atakaepuuza atutacheka nae, tutapambana nae,” alisema Masauni.
Kwa upande wake Kamanda Msilimu, alisema ameyapokea maagizo yote na atahakikisha anayafanyia kazi ipasavyo kwa kuwasimamia matrafiki wote nchini kwa umakini mkubwa.

WAZIRI LUKUVI AMSIMAMISHA MUWEKEZAJI TANGA

0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesimamisha umiliki wa mwekezaji wa mashamba ya katani yanayomilikiwa na kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited yaliyopo kata ya Mnazi wilayani Lushoto mkoani Tanga.

Waziri Lukuvi amefikia uamuzi huo baada ya wakazi wa eneo hilo kuzuia msafara wake na kupata malalamiko mengi kutoka kwa wananchi hao na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto wakimlalamikia Waziri kuhusu mashamba matatu ya Mnazi yaliyotelekezwa na mmiliki wa mashamba hayo bila kuendelezwa na kusababisha migogoro kwa awakazi wa Mnazi.

Baada ya kupokea malalamiko hao Waziri Lukuvi aliamua kutembelea mashamba hayo na kuyakagua ili kujionea hali halisi na kuwasikiliza wananchi ambao wamekuwa wanakabiliwa na mgogoro huu kwa miaka mingi.

Baada ya kutembelea na kujiridhisha Waziri Lukuvi amesema kwamba shamba hilo linastahili kufutwa kama ilivyopendekezwa na ofisi ya Mkoa wa Tanga na ofisi ya Kamishna wa Ardhi Kanda ya Kaskazini kwa kuwa mmiliki ameshindwa kuwa na sifa za umiliki kwa kuwa hajalipa kodi ya ardhi tangu mwaka 2004, hajalipa wafanyakazi wake kwa muda mrefu, miundombinu yake na mazingira ya kazi hayaridhishi na ameshindwa kuliendeleza shamba hilo tangu akabidhiwe mwaka 1997 kwa kurithi mashine na mitambo ileile ya mkoloni ya mwaka 1937.

Aidha, katika ziara hii Waziri Lukuvi amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera ili kutatua migogoro ya mipaka iliopo kati ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara na Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga ikiwa ni muendelezo wa mikutano ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro huu ambao umesababisha uvunjifu wa amani.

Waziri Lukuvi anatekeleza agizo la Waziri Mkuu Mhe. Khassim Majaliwa ambae alimuagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kutatua mgogoro huu uliodumu kwa miaka mingi kati ya Wilaya hizo mbili pindi alipofanya ziara yake mkoani Tanga.

Mnamo tarehe 18 Januari, 2017 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya  ziara Wilayani Kilindi katika Kijiji cha Mafisa na kuzungumza na wanachi Kijijini hapo kuhusiana na mgogoro huo na kutoa maagizo kwa viongozi wa kuchaguliwa kuacha kutumia nafasi zao vibaya kuongoza kwa mihemko au ushabiki kwa kuwa kufanya hivyo kunapelekea wananchi kufuata ushabiki na kuvunja sheria zilizopo.

Ili kutekeleza agizo hili wakuu wa mikoa hii miwili wakiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wamekutana ikiwa ni muendelezo wa vikao vya kulitafutia ufumbuzi suala hili.

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA KAGOMA-BIHARAMULO-LUSAHUNGA YENYE UREFU WA KILOMETA 154

0
0
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli, akipungia vikundi vya kwaya,ngoma na Burudani alipowasili kwenye viwanja vya stendi ya Biharamulo tayari kwa kuzindua Barabara ya Biharamulo, Kagoma, Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154,Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 Julai 2017.
Baadhi ya waananchi waliohudhuria uzinduzi wa Biharamulo,Kagoma ,Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154,wakimsikiliza kwa makini Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, wakati akiwahutubia 19 Julai 2017.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mustafa kijuu akisoma taarifa ya mkoa wake mbela ya Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,wakati wa ufunguzi wa Barabara ya Biharamulo,Kagoma ,Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154,Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 Julai 2017.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, akihutubia wananchi wa Biharamulo wakati wa ufunguzi wa Barabara ya Biharamulo,Kagoma ,Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154,Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 Julai 2017.
Umati Waananchi waliohudhuria uzinduzi wa Biharamulo, Kagoma, Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154, wakimsikiliza kwa makini Mh Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli, wakati akiwahutubia 19 Julai 2017.
Umati Waananchi waliohudhuria uzinduzi wa Biharamulo, Kagoma, Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154,wakimshangilia,Mh Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli, mara baada ya kuwahutubia kwenye mkutano wa hadhara wa ufunguzi wa barabara kwenye viwanja vya stendi ya Biharamulo 19 Julai 2017.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kuwahutubia kwenye mkutano wa hadhara wa ufunguzi wa barabara kwenye viwanja vya stendi ya Biharamulo 19 Julai 2017.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, akiondoa kitambaa kwenye jiwe kuashiria ufunguzi wa ufunguzi wa Barabara ya Biharamulo, Kagoma, Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154, Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 Julai 2017.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Viongozi wengine akiwemo Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano wakikata utepe kuashiria ufunguzi Barabara ya Biharamulo,Kagoma, Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154,.Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 Julai 2017
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli, akipeana mkono na Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano Makame Mbarawa mara baada ya kufungua Barabara ya Biharamulo,Kagoma ,Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154,Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 Julai 2017
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na akiwa ameambatana na mkewe mama Janeth Magufuli Viongozi wengine akiwemo Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano wakisaimiana na wananchi waliohudhuria ufunguzi Barabara ya Biharamulo,Kagoma ,Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154, Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 Julai 2017
Mhandisi wa maji wa wilaya ya Biharamujlo mh Patrice Jarome na Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji Bukoba Ndugu Allen Marwa wakijibu hoja ya maji mbele ya Mh Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli, mara baaada ya kuelezwa kero ya maji katika mji huo na wao kuahidi ndani ya siku kumi kufunga mitambo ya maji na kuwasambazia wananchi maji 19 julai 2017.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wa wananchi kijiji cha Nyakahura waliokuwa njiani kumpokea akiwa njiani akielekea Ngara Mkoani Kagera, 19 Julai 2017. Picha na Ikulu.
Viewing all 46129 articles
Browse latest View live




Latest Images