Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46129 articles
Browse latest View live

MSAMA: SERIKALI IKO BEGA KWA BEGA NA WAFANYABIASHARA,WALE MAHARAMIA WA KAZI ZA SANAA KAMATA KAMATA KUANZA WIKI IJAYO

0
0

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMANNE LEO JULAI 18,2017

0
0




















Mtanzania "Sensei Fundi Rumadha ( 4th Dan) Yondan" Apandishwa cheo na baraza la Karate Duniani

0
0
 

Sensei Kinjo, Gima, Yoshihiro Kancho Miyazato, sensei Fundi Rumadha na Sensei Rony Kluger toka Israel. Katika where za kupandiswa ngazi walimu kadhaa.
Masensei toka Ujerumani, Ureno, Uingereza, Japan, na Tanzania katika semina "Gasshuku" wakiwa na furaha nyingi.


Masters au walimu wakuu wa Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu Karate-Do chini ya usimamizi wa mwenye kiti wake mkuu duniani, aliwafanyia mitihani ya mikanda myeusi zaidi ya walimu 15 toka nga ya pili" Nidan" hadi ngazi ya saba "Nanadan". Ngazi hizi zote kwa uramaduni wa mtindo huu wa Okinawa Goju Ryu huchukua miaka mingi sana kupandiswa ngazi kulinganusha na mitindo mingine.

Kongamano la Karate mtindo wa Goju Ryu katika chama cha Jundokan So Honbu hufanyika kila mwaka nchi za ulaya kwa kutembelewa na wakuu wake toka katika visiwa vya Okinawa kuwasahihisha mbinu za mafunzo na mikakati mipya ya chama na hatimae sasa kuwaalika walimu toka nje ya bara la ulaya kwa muda wa miaka zaidi ya miwili sasa ikiwemo Tanzania na Angola.

Mwaka huu, wakuu wapatao watano chini ya mwenye kiti sensei Yoshihiro "Kancho" Miyazato, Tetsu Gima sensei, Tsuneo Kinjo sensei na Miyazaki sensei na mjumbe mwingine pia. Wakuu wa Okinawa Goju, wametilia mkazo na msisitizo mkubwa sana kwa kuzimudu mbinu kwa kina na matuzi yake, na pia watoto wadogo kwani ndio walimu wa kesho.

Mengi juu la misafara hii nikuwajumuisha masensei wote wa chama cha Jundokan So Honbu, kuwasahihisha na kuwafundisha ngazi kwa wana Swahili kufanyiwa hivyo, kulikoni kufanya gharama za kwenda Okinawa, Japan kimafunzo.

Sensei Fundi Rumadha aliweza kufanya mitihani wake toka Dan ya tatu "Sandan" kwenda ngazi ya nne "Yondan" na kufauli vizuri chini ya waamuzi masters toka Okinawa chini
ya Miyazato sensei. Sensei Fundi Rumadha amepewa mamlaka kuwasaidia wanafunzi wake wa Tanzania, kuwafanyia mitihani na kuwapa "Dan" hadi ngazi ya pili " Nidan" sababu chama chake kuanzia Dan ya 3 hutolewa na Master Miyazato pekee hadi leo hii.

Nimatumai yetu wanachama wa Jundokan So Honbu Tanzania kujiwajibisha kimafunzo, na kuimarisha umadhubuti wa mbinu" Techniques" kulikoni kulenga sana ngazi bila msingi mazuri kimafunzo, hasa katika kufanya "Kata" na "Bunkai".

Sensei Fundi Rumadha ingawa sasa anashikilia ngazi ya daraja la nne "Yondan", na umahili wake wa Karate kwa zaidi ya miaka 38, alitoa Shukran zake kwa mlezi wake wa mafunzi tokea utotoni, mwalimu "Sensei Magoma N. Sarya chini ya uongozi wake "Bomani Brigade" kama ilivyojilikana "BB" na mwanzilishi hayati Nantambu Camara Bomani sensei, mwanzilishi wa Okinawa Goju Ryu Tanzania 1973.

Tanzania na Angola zinatarajia kuhudhuria maadhimisho ya miaka 65 tangu kuanzishwa kwa chama cha "Jundokan" na Master Eiichi Miyazato sensei huko Naha City, Okinawa mwezi wa Novemba 1918, kwa sasa kinaongozwa na mwanae Yoshihiro Kancho Miyazato.


https://www.facebook.com/fundi.romi
www.instagram.com/fundi_romi

JAFO ATOA AGIZO KWA MAAFISA WA ELIMU KUBORESHA MAZINGIRA YA SHULE

0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Maneromongo katika mkutano wa kuhamasisha maendeleo.
Ujenzi wa madarasa na mabweni unaoendelea katika shule ya sekondari Maneromango
Wananchi wa kata ya Maneromango wakiwa katika mkutano wa pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akishuhudia upangaji wa mawe katika moja ya majengo yanayojengwa wilayani Kisarawe.

…………………………………………………………………….

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo ameagiza maafisa elimu nchini kuboresha mazingira ya shule za msingi na sekondari katika halmashauri zao wanazoziongoza ili ziwe na mandhari ya kuvutia.

Jafo ametoa maagizo hayo alipokuwa akitembelea ujenzi wa madarasa, vyoo, na mabweni katika wilaya ya Kisarawe.

Katika ziara yake, Jafo amefurahishwa sana na ujenzi unavyo endelea wilayani humo kwa ulazaji wa matofali katika majengo yote kutokana na ujengaji wa aina hiyo unayafanya majengo kuwa na ubora mkubwa.

Naibu Waziri Jafo ametaka mazingira ya shule zote nchini yawe safi kwa kupanga mawe pembeni na barabara, kupanda majani, maua na miti ili shule ziwe kivutio kwa watoto.

Jafo alitembelea na kukagua ujenzi katika Shule ya msingi Kwala ambayo kuna ujenzi wa vyumba vya Madarasa matatu, matundu ya vyoo kumi na mbili pamoja na ujenzi wa ofisi ya walimu.

Pia alitembelea ujenzi wa mabweni mawili, vyoo matundu kumi na sita, madarasa matatu, na ujenzi maktaba katika shule ya sekondari Maneromango ambayo inatarajiwa kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano.

PROF. MBARAWA: FIDIA ZITALIPWA KWA WANAOSTAHILI KISHERIA

0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akipokea taarifa kutoka kwa Mkandarasi wa Kampuni ya CHICO (katikati), anayejenga barabara ya Mwigumbi-Maswa KM 50.3 inayojegwa kwa kiwango cha lami ambao ujenzi wake umefikia takribani asilimia 77.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Mwigumbi, wakati alipokagua ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa KM 50.3 inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Muonekano wa sehemu ya Barabara ya Mwigumbi-Maswa KM 50.3 inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Shinyanga.
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mwanza Eng. Marwa Rubirya (kushoto), akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), kuhusu maendeleo yaliyofikiwa ya ujenzi wa barabara ya Usagara-Kisesa KM 16.135 inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani humo

Muonekano wa sehemu ya Barabara ya Usagara-Kisesa KM 16.135 inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Mwanza.

…………………………………………………………………

Serikali imesema itawalipa fidia kwa mujibu wa sheria wananchi wote waliopisha ujenzi wa barabara katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Amesema hayo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati akizungumza na wananchi wa Mwigumbi mkoani Shinyanga alipokagua ujenzi wa barabara ya Mwigumbi – Maswa yenye urefu wa KM 50.3 inayojengwa kwa kiwango cha lami na mkandarasi wa Kampuni ya CHICO na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wake ambao unagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 61.

“Kila anayestahili kulipwa fidia atalipwa kama sheria inavyoelekeza na endapo akatokea yeyote mwenye malalamiko Serikali ipo itamsikiliza”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi na Viongozi wa Wakala wa Barabara (TANROADS), wa mkoa ili kuhakikisha barabara hiyo inakamilika kwa wakati na spidi inayotakiwa.

Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amewahimiza makandarasi wote nchini kutoa kipaumbele cha ajira kwa wakazi wa maeneo husika inapopita miradi ya maendeleo ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ili kuwapatia kipato na kuinua uchumi wao.

Naye, Kaimu Meneja wa TANROADS mkoa wa Shinyanga Eng. Batholomeo Ndirimbi, amesema mpaka sasa tayari fedha zimetengwa kwa ajili ya ulipaji fidia na watahakikisha kuwa fedha hizo zinalipwa kwa watu sahihi wanaostahili fidia hizo.

“Tutasimamia zoezi hili kwa umakini na kutoa fidia kwa wale wote wanaostahili kisheria”, amesema Eng. Ndirimbi.

Ameongeza kuwa ujenzi wa barabara hiyo umefikiwa asilimia 77 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Katika hatua nyingine, Waziri Prof. Mbarawa amekagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Usagara-Kisesa KM 16.1 inayojengwa kwa kiwango cha lami ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 75 na daraja la Nyashishi lenye urefu wa mita 67.9 ambalo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.5 mkoani Mwanza.

Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mwanza Eng. Marwa Rubirya, amesema ujenzi wa barabara hiyo unaendelea vizuri na mkandarasi atamaliza kwa wakati uliopangwa na viwango walivyokubaliana katika mkataba.

MWALIMU COMMERCIAL BANK (MCB) YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA "WEKA AKIBA NA USHINDE"

0
0
Meneja wa Tawi la Samora la Benki ya Mwalimu, (Mwalimu Commercial Bank, Plc), Leticia Ndongole, (kushoto), akimkabidhi IPAD, Bw. Shukuru Sanga kutoka Waning’ombe mkoani Njombe, wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni ya “Weka akiba na ushinde” inayoendeshwa na benki hiyo.Hafla hiyo imefanyika leo Julai 18, 2017 kwenye tawi lam benki hiyo Mtaa wa Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam. Wengine ni washindi kutoka kulia, ni Bw. Benester Lazaro na Bi. Grace Machemba wote kutoka Dar es Salaam.



NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

WATEJA wanne wa Mwalimu Commercial Bank PLC wamejishindia zawadi za IPAD na vocha za manunuzi baada ya kuibuka washindi kwenye Droo iliyochezeshwa na benki hiyo kufuatia kweney promosheni ya “Weka Akiba na Ushinde” kwa Wateja wake na wananchi kwa ujumla.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 18, 2017 wakati wa kukabidhi zawadi za washindi, Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko cha benki hiyo, Bw. Valence Luteganya, (pichani juu), alisema, Droo hiyo ilikuwa wazi kwa wateja wote waliopo na watakaojiunga na benki kwa kufungua akaunti kwa kuweka akiba ya Shilingi 50, 000 au zaidi.

Akifafanua zaidi Bw. Lutenganya alisema, kampeni hiyo ilizinduliwa Mei 18, 2017 na wamepokea wateja wengi ambao walishiriki kwenye Droo hiyo iliyochezeshwa chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha, (Gaming Board of Tanzania).






Aliwaja washindi hao kuwa ni pamoja na Bw. Shukuru Sanga, kutoka Waning’ombe mkoani Njombe ambaye alijinyakulia IPAD, wakati Bw. Benester Lazaro, na Grace Machemba kutoka Dar es Salaam, walijinyakulia vocha za manunuzi kama ilivyo kwa Bi. Joyce Sangusangu kutoka mkoani Dodoma.

Akifafanua zaidi jinsi kampeni hiyo ilivyoendeshwa, Bw. Lutenganya alisema, kadiri mteja alipoweka akiba zaidi ndivyo alivyojiwekea nafasi nzuri ya kushinda zawadi na amewataka wateja na wananchi wengine kuweka akiba kwani droo nyingine itachezeshwa baadaye mwezi huu.

Aidha alisema hudma za benki hiyo, ni pamoja na kutoa gharama nafuu na rafiki za kibenki na ni suluhisho la kifedha kwa walimu, watumishi wa serikali na wananchi kwa ujumla na kutoa wito kwa wateja wapya kuja kufungua Akaunti na kuweka akiba.

Alisema, “Huduma za kibenki za MCB ni bora na nafuu, nakuwahakikishia wateja na wananchi kufanya maamuzi ya kifedha yaliyo sahihi kwani benki inatoa huduma mbalimbali za kibenki zilizo nafuu ikiwemo huduma ya ATM kwenye mtandao mpana wa UMOJA switch wenye ATM zaidi ya 200 kote nchini.

“Lakini si hivyo tu pia huduma bora za kibenki kupitia simu za mkononi (Mobile Banking), huduma ya bure ya ujumbe wa SMS ukiwa na usalama na kuwawezesha wateja kupata taarifa za mara kwa mara kuhusiana na Akaunti zao. Hivyo natoa wito kwa wananchi kwa ujumla kuja na kujiunga na Benki yetu kwa huduma bora na za uhakika.” Alisema.
Bw. Lutenganya akiwa na maafisa wa benki hiyo wakati akizungumzia zawadi hizo
Mshindi wa IPAD, Bw. Shukuru Sanga kutoka Waning’ombe mkoani Njombe, akiongea kwa niaba ya washindi wenzake.
Wafanyakazi wa MCB wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mshindi wa IPAD, Bw. Shukuru Sanga kutoka Waning’ombe mkoani Njombe, akiongea kwa niabaya washindi wenzake. Kushoto ni Afisa Mikopo wa benki hiyo, Bw.Isaya Hagamu.
Mshindi wa IPAD, Bw. Shukuru Sanga kutoka Waning’ombe mkoani Njombe, akiongea kwa niaba ya washindi wenzake.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko, cha benki ya Walimu Tanzania, (Mwalimu Commercial Bank Plc-MCB), Valence Lutenganya, (kulia), akizungumza mbele ya washindi wa promosheni ya kwanza ya “weka akiba na ushinde” kwenye tawi la benki hiyo barabara ya Samora jijini Dar es Salaam, Julai 18, 2018. Wateja wane wa benki hiyo walijishindia IPAD na Vocha za manunuzi, baada ya kuingia kwenye droo iliyowaibua kuwa washindi. Kwa mujibu wa Lutenganya, mshindi ni lazima aweke akiba si chini ya shilingi elfu 50,000 au kufungua alkaunti na kuweka kiasi hicho cha akiba na hivyo kuingia kwenye promosheni hiyo moja kwa moja. Kutoka kushoto ni Meenja wa tawi la benii hiyo, Leticia Ndongole, Mshidni wa IPAD, Shukuru Sanga, Grace Machemba, (Voucher), and Benester Lazaro, also he won a voucher.
Afisa Mikopo wa MB, Bw. Isaya Hagamu, (kushoto), akimkabidhi zawadi ya vocha ya manunuzi, mshindi wa promosheni ya "Weka akiba na ushinde" inayoendeshwa na benki hiyo, Bw. Benester Lazaro wa jijini Dar es Salaam hukuMeneja wa tawi la Samora la benki hiyo, Bi. Leticia Ndongole, akishuhudia.
Bw. Lutenganya(kulia). akimpongeza Bw. Lazaro kwa ushindi. Kushoto ni Bi Leticia Ndongole
Bi Leticia Ndongole(kushoto), akimkabidhi zawadi ya IPD, Bw. Sanga.
Meneja wa Tawi la Benki wa Mwalimu, (Mwalimu Commercial Bank, Plc), Leticia Ndongole, (katkati), akishuhudia jinci Meneaj wa Huduma kwa wateja wa tawi hilo, Flora C. Mbogo, (kushoto), akimkabidhi vocha ya manunuzi mteja wa benki hiyo, Grace Machemba, baada ya kuwa mionhoni mwa washindi wa promosheni ya weka akiba na ushinde ya benki hiyo. Hafla ya kukabidhi zawadi hizo ilifanyika kwenye tawi la benki hiyo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam Julai 18, 2017. Ambapo washindi wengine waliibuka na IPAD na vocha.
Mwanahabari akiwa kazini akitekeleza majukumu yake wakati wa hafla hiyo.

DARAJA LA FURAHISHA MWANZA LAKAMILIKA

0
0


Muonekano wa daraja la waenda kwa miguu lililopo eneo la Furahisha, mkoani Mwanza. Ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99 na limejengwa na kampuni ya Nyanza Roads Works.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongela (kulia), wakishuka ngazi za daraja la waenda kwa miguu lililojengwa eneo la Furahisha, alipokagua ujenzi wake mkoani Mwanza.
Mhandisi Mkazi anayesimamia uboreshaji wa kiwanja cha ndege cha Mwanza Bw. Geofrey Asulumenye, akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, upanuzi wa njia za kurukia ndege katika kiwanja hicho mkoani humo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mkazi Bw. Geofrey Asulumenye (kulia), kuhusu uboreshaji wa kiwanja cha ndege cha Mwanza, alipokuwa akikagua uwanja huo. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema ujenzi wa Daraja la waenda kwa miguu lililopo eneo la Furahisha na barabara ya kutoka Furahisha hadi Pasiansi yenye urefu wa KM 2.7, imekamilka kwa asilimia 99 Mkoani Mwanza.

Prof. Mbarawa amesema hayo wakati alipokuwa akikagua maendeleo ya ujezi wa daraja hilo katika ziara yake ya kikazi mkoani humo na kuridhishwa na ukamilishwaji wa ujenzi wake.

“Daraja hili litaondoa changamoto kwa wananchi wanaotembea kwa miguu na litapunguza au kuondoa adha ya msongamano wanaovuka kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine”, amesema Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amewataka wananchi kutunza daraja hilo na miundombinu yake ili liweze kutumika kwa muda mrefu kwani limekuwa nembo ya Mkoa wa Mwanza.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongela, ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kujenga Daraja la Furahisha kwa kuwa limebadilisha mandhari ya Jiji hilo.

“Jiji la Mwanza ni kitovu cha Kanda ya Ziwa, wananchi wameguswa moja kwa moja na mradi wa ujenzi wa daraja hili”, amesema Bw. Mongela.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mwanza, Eng. Marwa Rubirya amemweleza Prof. Mbarawa kuwa kazi iliyobaki katika daraja hilo nikuweka taa za urembo.

Ameongeza kuwa Daraja hilo pamoja na barabara yake zimegharimu kiasi cha zaidi ya cha shilingi Bilioni nne na linatarajiwa kuanza kutumika ndani ya siku mbili zijazo.

Katika hatua nyingine, Prof. Mbarawa amekagua upanuzi wa barabara ya Makongoro hadi Uwanja wa Ndege wenye urefu wa KM 5.3, ambapo malipo ya awali yameshalipwa kwa mkandarasi na mradi unatarajiwa kukamilika mapema kabla ya muda ambao umepangwa mwezi Mei mwakani.

Prof. Mbarawa amekagua uboreshaji wa kiwanja cha ndege cha Mwanza ambao umehusisha ujenzi wa jengo la mizigo, barabara za njia za ndege, jengo maalum la kuongozea ndege (Control Tower) na upanuzi wa urefu wa uwanja hadi kufikia KM 3.8 na kuagiza TANROADS kusimamia uboreshaji wa kiwanja hicho ili kikamilike kwa wakati uliopangwa.

Amesema kuwa hatua inayofuata ni kujenga jengo la kisasa la abiria lenye hadhi ya kimataifa ambalo litachukua na hadhi ya kiwanja hicho.

Uboreshaji wa viwanja vya ndege nchini ni moja ya mkakati wa Serikali katika kukuza sekta ya usafiri wa anga na kuongeza pato la Taifa.

MAKAMU WA RAIS MH.SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA MAMIA KUAGA MWILI MAREHEMU LINAH MWAKYEMBE JIJINI DAR LEO

0
0
Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan akiongoza Viongozi mbalimbali wa Serikali,ndugu jamaa na Marafiki katika kutoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa Marehemu Linah George Mwakyembe,mapema leo katika kanisa la KKKT Kunduchi,jijini Dar.Marehemu Linah Mwakyembe aliyefariki mwisho mwa wiki anatarajiwa kusafirishwa leo jioni kwenda wilayani Kyela mkoani Mbeya kwa mazishi.
Pichani wa tatu kulia ni Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo,Dkt Harisson Mwakyembe akiwa sambamba na Familia yake ndani ya kanisa la KKKT Kunduchi wakishiriki kwa pamoja misa ya kuaga mwili wa Marehemu Linah Mwakyembe aliyefariki mwishoni mwa wiki.
Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan akimpa mkono wa pole kwa Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo,Dkt Harisson Mwakyembe,kufuatia kifo cha mke wake mpendwa Linah Mwakyembe,kilichotokea mwishoni wa wiki jijini Dar. 
Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan akitoa salamu za pole wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Linah George Mwakyembe,mapema leo katika kanisa la KKKT Kunduchi,jijini Dar.Marehemu Linah Mwakyembe aliyefariki mwisho mwa wiki anatarajiwa kusafirishwa leo jioni kwenda wilayani Kyela mkoani Mbeya kwa mazishi.
Misa ya kuaga mwili wa Marehemu Linah George Mwakyembe ikiendelea mapema leo katika kanisa la KKKT Kunduchi,jijini Dar.Marehemu Linah Mwakyembe aliyefariki mwisho mwa wiki anatarajiwa kusafirishwa leo jioni kwenda wilayani Kyela mkoani Mbeya kwa mazishi.
Baadhi ya Viongozi wa chama na Serikali wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kuaga mwili wa Marehemu Linah George Mwakyembe,mapema leo katika kanisa la KKKT Kunduchi,jijini Dar.Marehemu Linah Mwakyembe aliyefariki mwisho mwa wiki anatarajiwa kusafirishwa leo jioni kwenda wilayani Kyela mkoani Mbeya kwa mazishi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimfariji Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo,Dkt Harisson Mwakyembe kufuatia kuondokewa na mke wake Linah Mwakyembe mwishoni mwa wiki.

MAMLAKA ZA AJIRA NCHINI ZAAGIZWA KUREKEBISHA TAARIFA ZA WATUMISHI WA UMMA WANAOTARAJIA KUSTAAFU ILI WAPATE STAHILI ZAO KWA WAKATI

0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo - Kata ya Ubungo alipofanya ziara ya kikazi katika Kata hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Maji (Water Institute), Dkt. Shija Kazumba akiwasilisha hoja mbalimbali zinazowahusu watumishi wa umma kutoka taasisi anayoiongoza wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo - Kata ya Ubungo kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Afisa TEHAMA wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Dotto Namkaa akiwasilisha mada kuhusu namna ya kujisajili katika Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo -Kata ya Ubungo kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akifafanua hoja mbalimbali alizopokea kutoka kwa watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo - Kata ya Ubungo (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi na watumishi hao leo Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori na kushoto kwake ni Meya wa Manispaa ya Ubungo, Mhe. Boniface Jacob.
Sehemu ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo - Kata ya Ubungo wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (Hayupo pichani) wakati wa kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.


Mamlaka za ajira katika utumishi wa umma nchini zimeelekezwa kufanya marekebisho ya taarifa za watumishi wa umma wanaotarajiwa kustaafu ili waweze kupata stahili zao kwa wakati kama inavyostahili.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo - Kata ya Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Kairuki amesema wapo watumishi wa umma ambao walipandishwa vyeo lakini muda wao wa kustaafu umekaribia na bado hawajafanyiwa mabadiliko yoyote katika taarifa zao.

“Natumia fursa hii kuwaelekeza waajiri wote katika utumishi wa umma warekebishe taarifa za watumishi hawa wanaokaribia kustaafu ili waweze kupata haki na stahili zao,” Mhe. Kairuki amesema serikali inawajali watumishi wa umma na kuongeza wale ambao tayari wameshastaafu, watafutwe na wajaze fomu maalum za madai kupitia kwa waajiri wao ili serikali iwalipe stahili zao kadri inavyostahili.

“Nawaagiza waajiri kupitia kwa Maafisa Utumishi wao, wawatafute ili waweze kujaza fomu maalumu na kuweza kupata haki zao kwani Serikali ipo kwa ajili ya watu wote hivyo hakuna haki ya mtumishi wa umma yeyote itakayopotea,” Mhe. Kairuki amesema.Mhe. Kairuki amewata watumishi wa umma kutimiza wajibu wao kwa weledi ili kuboresha utendaji kazi. “Serikali ni mimi na wewe hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kutimiza wajibu wake ipasavyo ili kujenga uchumi wa nchi yetu”.

Awali, akimkaribisha Mhe. Kairuki kuzungumza na Watumishi wa Kata ya Ubungo, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori amempongeza Mhe. Waziri Kairuki kwa utaratibu anaoufanya wa kukutana na watumishi wa umma kwa kusikiliza maoni pamoja na changamoto wanazozikabili katika utendaji kazi na kuzifanyia kazi.

“Kinachofanyika sasa ni jambo la kipekee sana kwa Waziri Kairuki mwenye majukumu mazito kutoka ofisini kwake na kuja kuzungumza katika kikao kama hiki na watumishi wa umma, kwa niaba ya viongozi wenzangu wa Wilaya ya Ubungo, nampongeza sana,” Mhe. Makori amesema.

Mhe. Makori amewataka watumishi wa umma wa Ubungo kuitendea haki ziara ya Waziri Kairuki kwa kutekeleza maagizo yote yanayotolewa.Mhe. Kairuki yupo katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Dar es salaama ambapo leo ni siku ya saba akiwa katika Kata ya Ubungo kwa kukutana na watumishi wa umma wa kada zote katika vikao kazi.

Lengo la kukutana na watumishi wa umma ni kusikiliza malalamiko, ushauri na changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili kuweza kuzifanyia kazi na kuleta mabadiliko katika Utumishi wa Umma nchini ili kufikia malengo yaliyopangwa na Serikali.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI

OFISI YA RAIS-UTUMISHI

18.07.2017

DAKTARI BINGWA MAGONJWA YA MOYO JKCI ASHINDA TUZO YA WATAFITI VIJANA WA KIAFRIKA KWA MWAKA 2017

0
0

Airtel Tanzania PLC undertakes strategic efficiency enhancement exercise

0
0

 Airtel Tanzania PLC has embarked on a strategic efficiency enhancement exercise aimed at making the company more flexible and agile and to innovate and respond better to the market demands. 
 
“This exercise, which shall be completed soon aims to improve organizational efficiency and flexibility by delayering and simplifying the operational structure and thereby enhancing empowerment to its employees. 
 
This exercise will help Airtel Tanzania to be closer to customers, ensure quicker responses to the customer’s needs, thus, enhancing Airtel Tanzania’ position in the market place”. Said Colaso in a statement issued by Company

The Managing Director for Airtel Tanzania PLC Mr. Sunil Colaso also said, “The exercise will result in some of the current positions in the current structure becoming redundant. As a responsible corporate, the company shall take all necessary steps to support the impacted employees financially as prescribed by the prevailing laws in Tanzania, while helping them find new opportunities. 
 
Amongst several other benefits, Airtel Tanzania has engaged a reputed organization to impart skills/ training to the impacted employees, in the endeavor that this will help open up fresh opportunities for such employees. The Company shall bear the full cost of providing this support to the concerned employees”.

Airtel remains committed to the Tanzanian market. The company has made significant investments in the market to drive innovation, network quality and customer service, and will continue to do so. Through its Corporate Social Responsibility programs, Airtel has supported various secondary schools across Tanzania, touching 58,000 students in over 1,300 schools. Insisted Colaso

UTAFITI WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI WA AWAMU YA PILI KUFANYIKA MWEZI AGOSTI, 2017

0
0

Na: Veronica Kazimoto.

Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania wa awamu ya pili unatarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Akizungumza wakati wa mafunzo ya wadadisi yanayoendelea kufanyika mkoani Dodoma Meneja  wa Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Wilfred Mwingira amesema  lengo kuu la utafiti huo ni kufuatilia viashiria vilivyowekwa kwenye utafiti wa awamu ya kwanza ili kutathmini na kujua kama kuna athari yoyote iliyotokea.

"Utafiti huu ni wa kitaifa na utafanyika Tanzania Bara na Zanzibar kwa lengo la kutathmini na kujua kama kuna athari yoyote iliyojitokeza kwenye viashiria vilivyowekwa kwenye utafiti wa awamu ya kwanza", amesema Mwingira.

Nae Mratibu wa utafiti huo Rainer Kiama amesema kuwa utafiti huu unafanyika ili kutathmini kama mpango unaleta manufaa yaliyokusudiwa katika ngazi ya kaya kwa kutumia viashiria kama vile elimu, afya, kazi na matumizi ya muda, shughuli za kaya zisizo za kilimo, mapato, mikopo, akiba na uhamishaji fedha.

Viashiria vingine ni  shughuli za kilimo,  makazi ya kaya na upatikanaji wa maji, matumizi na usalama wa chakula katika  kaya, maamuzi katika kaya, ukatili kwa wanawake na matarajio ya vijana, mahusiano ya kaya na jamii pamoja na mtazamo wa kaya kuhusu Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania wa awamu ya pili utahusisha kaya takribani elfu saba (7,000)  ambazo zilihojiwa katika utafiti wa awamu wa kwanza uliofanyika mwezi Juni, 2015.
 Meneja  wa Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Wilfred Mwingira akizungumza na wadadisi wakati wa mafunzo ya Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania yanayoendelea kufanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.
 Wadadisi  wakijifunza kwa vitengo namna ya kutumia vifaa vya kielektroniki - tablets vitakavyotumika wakati wa Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Mafunzo ya Wadadisi wa utafiti huo yanaendelea kufanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.
 Wadadisi  wakijifunza kwa vitengo namna ya kutumia vifaa vya kielektroniki - tablets vitakavyotumika wakati wa Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Mafunzo ya Wadadisi wa utafiti huo yanaendelea kufanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.
Wadadisi  wakijifunza kwa vitengo namna ya kutumia vifaa vya kielektroniki - tablets vitakavyotumika wakati wa Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Mafunzo ya Wadadisi wa utafiti huo yanaendelea kufanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.

Benki ya KCB Tanzania yaendelea kuwapatia ushauri wa kibiashara wanachama wa KCB 2jiajiri

0
0
Afisa Sheria Bi. Doris Mugarula (wakwaza kushoto) na Afisa Fedha Bi. Happiness Kisanga (wapili kushoto) wa Benki ya KCB wakimsikiliza mjasiriamali Bi. Batula akielezea maendeleo ya biashara yake ya nguo mkoani Arusha. 

Afisa Masoko wa Benki ya KCB Bi. Ghati Muhere (kulia) akimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Hafsa Ali (kushoto) katika duka lake la nguo za kiume, H&D Collection Shop, Kariakoo, jijini Dar es Salaam.
Afisa Fedha wa Benki ya KCB Bi. Happiness Kisanga (wakwanza kulia) akimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Hawa Mabrouk (katikati) katika ofisi yake ya Video production, Ilala, jijini Dar es Salaam.
Afisa Sheria, Bi. Doris Mugarula (wakwanza kulia) na Afisa Fedha Bi. Happiness Kisanga (wapili kulia) wa Benki ya KCB wakimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Shamsa Ally (kushoto) katika duka lake la vifaa vya magari makubwa mkoani Morogoro.
Afisa Masoko, wa Benki ya KCB, Bi. Ghati Muhere (kulia), akimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Jac Bazaar (kushoto) katika duka lake la vifaa vya umeme mkoani Morogoro.
Afisa Masoko Bi. Ghati Muhere (aliyechuchumaa) na Afisa Fedha Bi. Happiness Kisanga (aliyesimama) wa Benki ya KCB wakimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Violeth (aliyeinama) katika biashara yake ya kilimo mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Afisa Masoko, Bi. Ghati Muhere (wakwanza kulia), Afisa Sheria, Bi. Doris Mugarula (watatu kushoto) na Afisa Fedha, Bi Happiness Kisanga (wapili kushoto) wa Benki ya KCB wakimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Mercy (wakwanza kushoto) katika biashara yake ya huduma za Interneti mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Afisa Masoko wa Benki ya KCB Bi. Ghati Muhere (kushoto) akimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Selina (kulia) katika duka lake la bidhaa za watoto Jijini Mwanza.
Afisa Sheria wa Benki ya KCB Bi. Doris Mugarula (kushoto) akimsikiliza mjasiriamali Bi Fatma (katikati) akielezea kuhusu biashara yake ya vipodozi na mikoba ya kike Jijini Mwanza.


Benki ya KCB Tanzania inaendelea kuwapatia wanawake wajasiriamali waliopitia mafunzo ya ujasiriamali ya KCB 2jiajiri ushauri wa kibiashara kwa vitendo ofisini kwa wafaidika wa 2jiajiri. Maafisa watatu ambao ni; afisa fedha, sheria na masoko wanawatembelea wafaidika hao wajasiriamali waliomaliza mafunzo ya KCB 2jiajiri katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Moshi, Morogoro na Zanzibar.

KCB 2jiajiri ni programu inayolenga kumkomboa mwanamke mjasiriamali kutoka katika matatizo yanayosababisha biashara yake ishindwe kukua na kuwa endelevu. Matatizo yanayolengwa kutatuliwa kutoka kwa wanawake wajasiriamali hawa ni elimu ya kifedha, kufikiwa na huduma za kifedha, ukosefu wa dhamana, kutokujua vizuri masuala ya kisheria, uelewa finyu wa sera za serikali na kiuchumi, njia hafifu za kuendesha biashara endelevu, ukosefu wa mtaji, utaalamu wa kuanzisha biashara kubwa n.k.

“Programu hii ilizinduliwa rasmi Desemba, 2016, ambapo hadi sasa tumewapa stadi za biashara endelevu wanawake wajasiriamlai 258 kutoka mikoa 6 ya Tanzania.” Alisema Christine Manyenye, Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB.

Akielezea kuhusiana na programu ya KCB 2jiajiri Bi. Manyenye alieleza kuwa, wafaidika wa KCB 2jiajiri baada ya kumaliza mafunzo ya siku tatu darasani, kwa sasa wananufaika kwa kupata ushauri wa kibiashara na kitaalamu kutoka kwa washauri watatu katika nyanja za Kifedha Kisheria na Masoko.

Akizungumza kuhusiana na mafunzo ya KCB 2jiajiri, Bi. Janeth Kipangula mjasiliamali mwenye biashara ya hardware na mfaidika wa KCB 2jiajiri

Aliishukuru Benki ya KCB kwa kutoa mafunzo ya kibiashara ambayo yamepanua ufahamu wa jinsi yakuendesha biashara. “kupitia KCB 2jiajiri nimeweza kujua umuhimu wa kurasimisha biashara, kuwa na leseni ya biashara, kuweka kumbukumbu katika biashara na jinsi ya kuendesha biashara kiujumla” alisema Bi. Kipangula.

Benki ya KCB kimsingi inatambua mchango mkubwa wa wanawake wanaoutoa katika sekta binafsi hususani katika Ujasiriamali mdogo na wa kati (SMEs) hivyo lengo kwa ujumla ni kuwezesha wafanyabiashara wanawake wa Kitanzania kuandaa mikakati ambayo inaboresha stadi zao na uwezo hivyo kuunda fursa nyingi za kibiashara kwa ajili yao.

Bi. Manyenye alimaliza kwa kusema kuwa programu ya KCB 2jiajiri ni endelevu na kwa wanawake wajasiriamali ambao bado hawajajiunga na KCB 2jiajiri wajiulize kwa nini wahangaike wakati KCB 2jiajiri ipo kwa ajili yao.

BAKWATA YAITAKA SERIKALI KUMCHUKULIA HATUA MTU MMOJA ANAYEJIITA MTUME MKOANI PWANI.

0
0
Baraza la ulamaa limetoa wito kwa vyombo vya dola kumchukulia hatua stahiki mtu aliyejitokeza katika mkoa wa pwani na kudai yeye ni Mtume. 

Akisoma wito huo, kwa niaba ya Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Ally, Mwenyekiti wa Halmashauri kuu Bakwata Sheikh Hamisi Said Mataka amesema, anachodai mtu huyo aliyetajwa kwa jina la Hamza Issa kuwa yeye ni nabii hayako kabisa katika mafundisho ya kiislamu.

Amesema kauli ya Issa kudai yeye ni mtume na kisha kwamba ni Muislamu kwa kutumia maandiko ya Uislamu, ni upotoshaji mkubwa ambao ukiachwa bila kudhibitiwa ni kuruhusu fujo na uvunjifu wa amani. 

"Kwa mujibu wa maelezo yaliyoenea katika mitandao ya kijamii na ya kutoka baraza za Masheikh wa Mkoa wa Pwani chini ya kiongozi wake Sheikh na Qadhi wa Mkoa wa Pwani, amedai kuwa yeye ni Nabii Ilyasa kwa maana ya kwamba roho ya Nabii Ilyasa imemuingia yeye Hamza Issa na kwa hiyo yeye amekuwa Nabii Ilyasa" amesema Sheikh 

Ameongeza maelekezo na mafundisho ya uislamu yako wazi kuwa hakuna Mtume mwingine katika Uislamu baada ya Mtume Muhammad (S.A.W) na kwamba upatikanaji wa MTU ndani ya uislamu na kudai kuwa yeye ni Mtume ni kutaka kuamsha hisia Kali za waislamu nchini.

"Baraza la Ulamaa linapenda kuwafahamisha waislamu kwamba, yeyote atakayemfuata mpotoshaji huyu atakuwa ametoka ndani ya uislamu" amesema Sheikh Mataka. 

Pia Baraza limetoa wito kwa Masheikh wa Mikoa, Wilaya na viongozi wa taasisi mbali mbali za Kiislam kutotoa fursa ya aina yoyote kwa huyo anayejiita Nabii ( Hamza Issa), ili kuzuia kuipotosha jamii.
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu Bakwata ,Sheikh Khamis Said akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, juu ya Vyombo vya Dola kuchukua hatua stashiki kwa mtu mmoja mkazi wa Mkoa wa Pwani, Hamza Issa anaejiita Nabii IIyasa .
Waandishi wa Habari wakimsilikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu Bakwata, Sheikh Khamis Said, leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

‘COCA-COLA BILA SUKARI’ YAZINDULIWA KUKIDHI MAHITAJI YA SOKO MWANZA

0
0
Kampuni ya Coca-Cola leo imezindua katika soko la Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla, soda mpya ya “Coca-Cola Bila Sukari”. Uzinduzi wa soda hii mpya umefanyika katika kiwanda cha Nyanza Bottlers mkoani Mwanza, ambapo pia baadaye utafanyika katika mikoa Dar es Salaam na Mbeya ambapo awali ulifanyika mjini Moshi .

Soda mpya ya ‘Coca-Cola Bila Sukari’ ladha yake imeboreshwa zaidi kutokana na soda isiyo na sukari iliyokuwa inatengenezwa hapo awali ya Coca-Cola Zero ambapo soda mpya ladha yake inashabihiana na soda ya Coca-Cola asilia lakini haina sukari kabisa.

Tangia mwaka 2006 wakati soda ya Coke Zero imeingia kwenye masoko, kampuni ya Coca-Cola imekuwa ikifanya jitihada kuhakikisha inatengeneza soda mpya ya Coca-Cola isiyo na sukari lakini yenye ladha sambamba na Coca-Cola asilia na imefanikiwa kuja na soda mpya ya ‘Coca-Cola Bila Sukari’ kinywaji ambacho kitawezesha watumiaji wa Coca-Cola kuipata kwa ladha asilia hata kama watachagua kuipata isiyotengenezwa kwa sukari.

“Soda ya Coca-Cola Zero ina ladha nzuri pia, lakini pamoja na ubora wake timu ya Coca-Cola imekuwa ikifanyia kazi kuhakikisha inapatikana soda isiyo na sukari lakini yenye ladha inayoshabiana na Coca-Cola asilia”. Alisema Meneja Mauzo Mwandamizi wa Nyanza Bottlers, Deus Kadico.

Kadico aliongeza kuwa; “Ubunifu wa wataalamu wetu umewezesha kupatikana soda mpya ya ‘Coca Cola Bila Sukari’ ambayo inatoa wigo kwa wateja kuwa na chaguo la kupata kinywaji cha Coca-Cola kwa radha asilia kwa kadri wanavyotaka,ikiwa na ladha ya sukari ama isiyo na sukari”. 

Pamoja na hayo, Kadico alisisitiza kuwa lengo kubwa ni kuhakikisha watumiaji wa soda ya Coca-Cola wanafurahia ladha yake halisi na asilia wanapokunywa soda yenye sukari au ‘Coca-Cola Bila Sukari’.

Soda za ‘Coca Cola Bila Sukari’ zimeanza kuwa kwenye soko la Tanzania kuanzia mwezi uliopita katika sehemu zote zinapouzwa soda na bei yake ni sawa na soda aina nyingine zote zinazotengenezwa na kusambazwa na kampuni ya Coca-Cola.
Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini Tanzania, Sia-Louise Shayo akizungumza na umati wa wasambazaji na mawakala wa soda ya Coca-Cola jijini Mwanza wakati wa hafla maalumu ya uzinduzi wa kinywaji kipya cha ‘Coca-Cola Bila Sukari’. Uzinduzi wa soda hii mpya umefanyika katika kiwanda cha Nyanza Bottlers mkoani Mwanza, ambapo pia baadaye utafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam na Mbeya.

Lissu Ashauriwa Kuacha Propaganda na Upotoshaji

0
0



Na: Lilian Lundo – MAELEZO

Serikali imemshauri Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu kutekeleza wajibu wake kwa kusimamia weledi akiwa kama Wakili wa Mahakama Kuu badala ya kufanya Propaganda kwa kutumia lugha ya kejeli, kuudhi na uchochezi kuituhumnu Serikali kuwa inabana demokrasia nchini.

Hayo yameelezwa leo, Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi katika taarifa kwa Umma aliyoitoa juu ya ufafanuzi kuhusu propaganda na upotoshaji wa Mbunge huyo.

“Vyombo mbalimbali vya habari leo vimemnukuu Mbunge wa Singida Mashariki Ndugu Tundu Lissu ambapo pamoja na mambo mengine, huku wakati fulani akitumia lugha za kuudhi, uchochezi na kejeli, ameituhumu Serikali kuwa inabana demokrasia nchini,” imefafanua taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema kuwa madai kwamba Serikali inakandamiza demokrasia ni propaganda tu za kisiasa, kutokana na Lissu kuonekana kuchanganya kati ya haki katika demokrasia ambazo hata yeye amezitumia kuongea na wanahabari bila tashtiti kwa upande mmoja na misingi ya wajibu kwa upande mwingine ambayo kila mmoja, iwe Tanzania au kwingineko duniani, anayo na pale anapoikiuka hatua huchukuliwa.

Dkt. Abbasi amesema kuwa tofauti na upotoshaji wa Lissu, Tanzania ikiwa nchi kiongozi Afrika na duniani katika kuenzi demokrasia na kupigania haki, si tu inaendelea kuenzi misingi hiyo bali pia imechukua hatua za wazi kuhakikisha kuwa misingi hiyo inalindwa na pale mtu na hata taasisi zinapokiuka basi mkondo wa sheria, jambo muhimu katika utawala bora,  huchukua nafasi yake.

Vile vile ameeleza kuwa, Tanzania ni ikiwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa (UN), hivyo imeridhia Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa wa mwaka 1966 na huwasilisha taarifa zake za utekelezaji wa demokrasia na haki za binadamu katika Kamisheni ya UN ya Haki za Binadamu.

Pia ni mwanachama kiongozi wa Umoja wa Afrika (AU) ambapo imeridhia Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu na ni miongoni mwa nchi za kwanza kabisa Afrika kukubali kushtakiwa na wananchi wake kwa kuridhia itifaki ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na pia kukubali kufanyiwa ukaguzi katika utawala bora kupitia Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM).

“Ni kwa sababu hizi basi tunamuasa Ndugu Lissu na wananchi kwa ujumla kujiepusha na propaganda, kejeli na uzushi usio na msingi dhidi ya Serikali au taasisi zake na pale ambapo wanadhani kuna haki zimekiukwa badala ya kuvunja sheria ni vyema kutafuta haki kupitia mkondo wa kisheria ambao tumeuainisha hapo juu,” imefafanua taarifa hiyo.

Dkt. Abbasi amesema kuwa Serikali itaendelea kuenzi na kuilinda misingi ya demokrasia, uhuru wa watu na kuwapa fursa wananchi kushiriki katika uchumi wa nchi hasa wakati huu wa mageuzi makubwa ya kiutendaji chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli lakini haitavumilia mtu yeyote au kikundi chochote kitakachojaribu kutumia uhuru wowote vibaya ili tu kukwaza azma hiyo ya Taifa.

Tigo yajiongeza zaidi uboreshaji wa mtandao

0
0
Ofisa Mkuu wa Ufundi na Mawasiliano wa Tigo,Jerome Albou,akizungumza na wahabari mbalimbali jijini Dar es Salaam juzi,Juu ya Uwekezaji katika ku vya habari kwenye warsha ya uwekezaji katika kuboresha upatikanaji wa mtandao wa Tigo kote nchini.
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, ambayo ni kinara wa ubunifu wa mitindo ya maisha ya kidijitali nchini, imetangaza mageuzi katika uwekezaji  ili kuboresha upatikanaji wa mtandao ili kuweza kuwapatia huduma bora zaidi wateja wake wa matumizi ya sauti na data.
Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari nchini, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ufundi na mawasiliano wa Tigo, Jerome Albou,amesema  kampuni  hiyo imewekeza kiasi cha dola za kimarekani millioni 75 kwenye mradi mkubwa wa kuendeleza mtandao huo.
Alisema moja ya malengo yao kimkakati ni kubadilisha uzoefu wa wateja kwa kuwapatia mtandao wenye ufanisi kulingana na viwango vya sekta ya mawasiliano ambapo katika miaka mitatu iliyopita Tigo imeweza kuongeza msingi  wa wateja wake kufikia zaidi ya milioni 10.
“Kadri tunavyoendelea kukua, kupanua  mtandao na kuufanya kuwa wa kisasa zaidi, ni jambo la lazima kutoa huduma bora zaidi,” alisema Albou huku akiongeza kwamba kuanzia mwaka jana kampuni ya Tigo imefanya upanuzi mkubwa wa miundo mbinu ili kuweza kufikia maeneo mengi nchini .

“Mahitaji ya matumizi ya data yamekuwa yakiongezeka kila siku, hivyo Tigo imeweza kuhakikisha matumizi ya 3G na 4G yanaweza kuwafikia watumiaji vijijini,” aliongeza Albou

WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA NISHATI YA BIOGAS ILI KURAHISISHA MAISHA

0
0

Mkufunzi wa semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas ,pamoja na wamiliki wa mitambo hiyo pamoja na mafundi Rowah Spear akiendelea kutoa elimu katika semina hiyo inayofanyika leo jiji hapa

wakwanza kulia ni Mratibu wa Ubunifu kutoka ECHO Harold Msanya akiwa anafafanua jambo mbele ya wakufunzi hao

baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiendelea kufanya kazi ya majadiliano katika makundi


Mkufunzi wa semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas ndugu Rowah Spear akiwa anawaelekeza baadhi ya wadau waliouthuria semina jinsi biogas inaweza kufanya kazi

wadau wakiendelea kufatilia mada ilikuwa inaendelea




Mkurugenzi wa ECHO Erwin Kinsey akiwa anaonyesha wakulima na wadau walioshiriki semina hiyo mmea aina ya gugukaroti ambalo ,alisema kuwa gugu ilo kwa asilimia 90% huku asilimia 10% ni gugu ambalo linaweza kutumika kutengeneza biogas(na woinde shizza,Arusha)

wadau wakiendelea na majadiliano katika makundi yao ikiwa ni sehemu ya kujifunza njia mbalimbali na matumizi ya biogas
Habari picha na Woinde Shizza,Arusha .


Wananchi wametakiwa kutumia Gesi Bayogesi kwani inapunguza gharama za watumiaji wa vyanzo vingine vya nishati ,pia gesi hii inasaida kutunza mazingira .

Hayo yamebainishwa leo na Mratibu wa Ubunifu kutoka ECHO Harold
Msanya wakati akitoa mada katika semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas , wamiliki wa mitambo hiyo pamoja na mafundi wanaofunga na kutengeneza mitambo hiyo .

Alisema kuwa gharama za nishati ya umeme na gesi asilia ni ghali sana hasa kwa mtumiaji atakayedhamiria kutumia jiko la umeme au jiko la gesi lakini kwa gesi hii ya  samadi mtumiaji au mabaki ya nyasi aina mbalimbali zitamgharimu muda wake tu kujaza samadi na maji kila siku na atakuwa
hana malipo ya pesa kila mwezi kama itakavyomlazimu kulipia umeme na gesi asilia kila mwezi, na hata kuni ambazo watumiaji wengine hununua

Alibainisha kuwa njia hii imeweza kuwasaidia na kuwapa
faida baadhi ya wananchi ambao wameanza kutumia teknoligia hii na pia wengi wao wameshanufaika na huduma hii .

Aidha Bayogesi ambayo aghalabu hutokana na kinyesi cha wanyama, masalia ya mimea na kinyesi cha binadamu inaweza kuzalishwa na kutumika kupikia na hata matumizi mengine kama vile kuendeshea
mitambo mbalimbali.

“ Matumizi ya gesi hii kwa mtu ambaye ana mifugo kama vile nguruwe, ng’ombe yanaweza kusaidia kuondokana na gharama za kununua nishati ya kuni, mkaa, umeme na hata gesi asilia inayochimbwa ardhini.”alisema
Msanya  .
Kwa upande wake mkufunzi wa Mkufunzi wa semina ya wadau mbalimbali wanaotumia Teknologia ya biogas ,pamoja na wamiliki wa mitambo hiyo pamoja na mafundi Rowah Spear alisemak uwa ni wajibu wa kila mtanzania kuwakikisha anakuwa na mtambo huo kwani mtambo huo unapunguza gharama  ubwa ambazo awali walikuwa wanatumia ,na pia pale mwananchi anapotumia mtambo huu anakuwa rafiki wa mazingira kwani kwanza kabisa akati miti ovyo na pili yale majani ,vyakula ,na uchafu uchafu wa aina wowote anaweza kuukusanya na kuingiza katika mashina na
ikamsaidia kupatikana kwa Biogas.
  Pia alisema kuwa mbali na kupata nishati yakupikia tu pia uchafu ambao unakuwa umetokana na mabaki haya unaweza kufanywa kama mbolea kwa mazao mbalimbali tunayoyalima hivyo ni vyema kila mwananchi kuhakikisha nyumbani kwake anamtambo huu

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMATANO LEO JULAI 19,2017

0
0

MEYA WA JIJI LA ISAYA MWITA DAR AFANYA ZIARA KITUO CHA MABASI UBUNGO

0
0
 Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na wafanyabiashara wa Stendi ya Mabasi Ubungo,wajumbe wa Kamati ya Fedha na uchumi ya Halmashauri ya Jiji alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha mabasi ubungo jana,kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji.
 Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akiwasikiliza Askari Polisi wa Ubungo alipofanya ziara ya kushtukiza jana katika kituo cha mabasi yaendoyo mikoani. katikati Mwenye Shati jeupe ni Diwani wa kata ya segerea ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya fedha na uchumi ya Halmashauri ya Jiji, Patrick Asenga.wa kwanza kushoto ni Meneja wa Kituo cha mabasi ubungo Iman Kasagara.
  Meneja wa Kituo cha mabasi Ubungo , Iman Kasagara akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita na Kamati ya fedha na Uchumi walipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha mabasi Ubungo.
 Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na waandishi wa habari jana alipofanya ziara ya kushtukiza ya kutembelea kituo cha mabasi ubungo. 
 Mbunge wa Jimbo la Ubungo, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ziara iliyofanywa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Kamati ya fedha ya jiji.
Viewing all 46129 articles
Browse latest View live




Latest Images