Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1303 | 1304 | (Page 1305) | 1306 | 1307 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saimon Sirro,  amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya.
   
  Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Polisi  Mohamed Mpinga anaenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu.
   
  Aidha,  Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya (DCP) Dhahiri Kidavashari amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi.
   
  Uhamisho huo ni wa kawaida katika kuboresha utendaji wa kazi za Polisi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.
   
   Imetolewa na:
  Barnabas D. Mwakalukwa – ACP
  Msemaji wa Jeshi la Polisi.
  Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

  0 0


  Karama Kenyunko-Globu ya Jamii

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia huru aliyekuwa Kamishna wa TRA, Tiagi Masamaki na Wenzake watano waliokuwa wakishtakiwa na makosa ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya sh. Bilioni 12.7.

  Washtakiwa hao wameachiwa na Hakimu Mkazi Huruma Shahidi baada ya upande wa mashtaka uliokuwa ukiongozwa na wakili wa Serikali Mwandamizi, Timon Vitalis kuiomba mahakama kufanya hivyo chini ya kifungu cha 91(1) ya makosa ya jinai (CPA)  kuwa DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

  "Mheshimiwa Hakimu kesi hii leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, hata hivyo tuna maombi, DPP amewasilisha Nolle Prosque, hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa", amesema Wakili wa Serikali Timon Vitalis.
  Hakimu Shahidi alikubaliana na ombi hilo na kuwaachia huru washtakiwa.

  Mbali na Masamaki, washtakiwa wengine waliokuwa katika kesi hiyo  iliyotokana na sakata la makontena 329 ni Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru  TRA, Habib Mponezya  (45) na Meneja Msimamizi na Ufuatiliaji wa Forodha, Burton  Mponezya (51).

  Msimamizi Mkuu Kitengo cha Ushuru wa Forodha  ICD Azam, Eliachi  Mrema (31),  Mchambuzi  Mwandamizi  wa Masuala ya Biashara  TRA,  Hamis Omary (48), Meneja wa Oparesheni  za Usalama na Ulinzi  ICD, Raymond Adolf Louis (39) na Meneja wa Azam ICD, Ashrafu Khan (59) na Haroun Mpande (28) wa kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta ICT TRA.
  Hata hivyo, DPP amewafutia mashtaka watuhumiwa watano tu ambao ni,Tiagi Masamaki, Eliachi Mrema, Habibu Mponezya, Burton Mponezya na Ashraf Khan.

  Hata hivyo, Raymond Louis, Haruni Mpande na Khakis Ally Omari wameendelea kushikiliwa na kusomewa mashtaka mapya pamoja na watuhumiwa wapya, Khalid Yusuph Hassan na Benson Vitalis Malembo.
  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo imemuachia huru aliyekuwa Kamishna wa TRA, Tiagi Masamaki (pichani kulia) na Wenzake watano waliokuwa wakishtakiwa na makosa ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya sh. Bilioni 12.7.
  -----  ------  --------


  0 0

  MBUNGE viti Maalumu Chadema, Mheshimiwa Upendo Peneza amewaomba wananchi waliombee Taifa liendelee kuwa na amani pamoja na kuwaombea viongozi wa kisiasa wawe na uvumilivu ili wazidi kusonga mbele kimaendeleo.

  Aliyasema hayo jana (Jumatano, Julai 12, 2017), katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa shule ya msingi Likangara wilayani Ruangwa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mkoani Lindi.

  “Wananchi wa Ruangwa nawatakia maisha mema ili mzidi kusonga mbele, tuombee amani ya nchi yetu na mtuombee viongozi tuwe na uvumilivu wa kisiasa.”

  Mbali na Mheshimiwa Upendo, pia mkutano huo uliudhuriwa na wabunge wengine ambao ni Mheshimiwa Hassan Masala (Nachingwea), Mheshimiwa Zubery Kuchauka (Liwale), Mheshimiwa Hassan Kaunje (Lindi Mjini) na Mheshimiwa Hamida Abdalaah (Viti Maalumu).

  Kwa pamoja wabunge hao walisema lengo la kushiriki kwenye ziara hiyo ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano katika kuwaletea wananchi maendeleo.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi aliwataka wananchi wa mkoa huo kuhakikisha wanaendelea kudumisha na kuilinda amani iliyoko kwa sababu ndiyo inayowawezesha kufanya shughuli zao za kimaendeleo.

  Alisema licha ya kuwepo kwa matukio machache ya uhalifu yanayojitokeza katika baadhi ya maeneo vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na mikoa jirani limejizatiti kukabiliana na wahalifu wa aina yoyote kwa mtu mmoja mmoja au vikundi.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa viti Maalumu Chadema, Mheshimiwa Upendo Peneza, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  0 0

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu imekwama kusikiliza kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili video Queen, Agnes Gerald 'Masogange' kwa sababu ana tatizo la kiafya.

  Hayo yalielezwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya wakili wa serikali, Costantine Kakula kueleza shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kusikilizwa.

  Hata hivyo, wakili wa Masogane, Ruben Simwanza alimueleza Hakimu kwamba mteja wake anaumwa hivyo anaomba kesi iahirishwe.

  Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 25, 2017 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa

  0 0

  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla ahimiza watumishi wa wizara hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuzingatia sheria, miongozo,  taratibu na maelekezo yao ya kazi.

  Akiwa katika ziara hiyo Mkoani Mtwara, alielekeza watumishi hao kuwa dhamana waliyopewa kuwahudumia wananchi wenzao ni kubwa hivyo hawana budi kuzingatia kanuni za Afya ili kuepuka maambukizi yatakayotokana na uzembe .

  Aliwataka kulipa kipaumbele suala la usafi wa mazingira, vifaa na maeneo yote wanayofanyia kazi hususan uhifadhi wa taka za hospitali katika utaratibu maalum unaozingatia  mfumo wa kinga na udhibiti wa taka  (Infection Prevention and Control) .

  Miongoni mwa mambo mengine aliyoyabaini katika ziara hiyo ni ubovu wa baadhi ya vifaa tiba katika maabara na vyumba vya upasuaji na kuagiza katibu mkuu wizara ya Afya kuchunguza mikataba yote ya usambazaji vifaa tiba na matengenezo.

   Aidha, Dk. Kigwangalla alibaini baadhi ya vifaa vya kisasa vilivyomo katika vituo hivyo havitumiki ipasavyo kwasababu watumishi waliopo hawana ujuzi wa kuvitumia na alimwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa kulishughulikia tatizo hilo haraka sana kwa kuwajengea uwezo wataalam hao.

  Mbali na kujionea hali hizo, Dk. Kigwangalla pia alitoa maagizo mbalimbali kwa watendaji wa vituo na viongozi wa Wilaya husika kuhakikisha wanasimamia ipasavyo utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.

  Dk. Kigwangalla akiwa mkoani Mtwara, aliweza kutembelea katika Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali, kati hizo ni:  Kituo cha Afya Mahurunga, Kituo cha Afya Nanguruwe, Zahanati ya Kijiji cha Dinyecha.

  Pia ametembelea Hospitali ya Wilaya ya Newala na Kituo cha Afya Newala DC, Zahanati ya Lulindi, Zahanati ya Nagaga, Hospitali ya Halmashauri ya Masasi-Mkomaindo na Zahanati ya Mbonde.Aidha, ameendelea na ziara yake Mkoani Ruvuma ambayo  atatatembelea vituo vya Afya na Hospitali za Mkoa huo.
   Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisisitiza jambo wakati akizungumza na wafanyakazi na wa Hospitali ya Wilaya ya Masasi-Mkoamaindo (Hawapo pichani). Wengine anayemfuatia ni Mbunge wa Jimbo la Masasi  Mh. Abdalla Chuachua na kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msasi. 
   Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua kitanda maalum cha upasuaji alichokikuta katika hyali ya kutoridhisha kiafya.
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa watendaji wa Hospitali ya Wilaya ya Newala, Mkoani Mtwara wakati wa ziara yake hiyo ya kukagua mambo mbalimbali ya kiutendaji katikaa hospitali hiyo.

  0 0

   Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbas, akizungumza na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Barnabas Mwakalukwa, wakati Msemaji huyo  alipofanya ziara ya kikazi katika Idara hiyo kwa lengo la kujitambulisha tangu alipoteuliwa na Inspekta Jenerali wa Polisi kushika nafasi hiyo.Picha  na Demetrius Njimbwi wa Jeshi la Polisi.
   Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbas, akimkabidhi Jarida la Nchi yetu, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Barnabas Mwakalukwa, wakati Msemaji huyo  alipofanya ziara ya kikazi katika Idara hiyo kwa lengo la kujitambulisha tangu alipoteuliwa na Inspekta Jenerali wa Polisi kushika nafasi hiyo. .Picha na Demetrius Njimbwi wa Jeshi la Polisi.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbas akimuonyesha  Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Barnabas Mwakalukwa ofisi ya Msajili wa Magazeti wakati Msemaji huyo  alipofanya ziara ya kikazi katika Idara hiyo kwa lengo la kujitambulisha tangu alipoteuliwa na Inspekta Jenerali wa Polisi kushika nafasi hiyo.Picha  na Demetrius Njimbwi wa Jeshi la Polisi.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Ofisini kwake, Kaimu Balozi wa Marekani hapa Nchini, Inmi Pettersom,alipofika kwa ajili ya mazungumzo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, leo.
   Karibu uketi: Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Ofisini kwake, Kaimu Balozi wa Marekani hapa Nchini, Inmi Pettersom,alipofika kwa ajili ya mazungumzo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, leo. 
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipiga picah maalum na Kaimu Balozi wa Marekani hapa Nchini, Inmi Pettersom, alipofika kwa ajili ya mazungumzo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, leo.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Kaimu Balozi wa Marekani hapa Nchini, Inmi Pettersom, alipofika katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, leo.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpa mkono Kaimu Balozi wa Marekani hapa Nchini, Inmi Pettersom, baada ya kumfurahisha jambo wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, leo. 
  Kaimu Balozi wa Marekani hapa Nchini, Inmi Pettersom, akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake na Katibu Mkuu wa CCm Abdulrahman Kinana katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, leo.

   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipiga picha maalum na Blozi wa Algeria hapa nchini, Saad Belabed 
   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi wa Palestina hapa nchini Hazen Shabat, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo
   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimkaribisha Ofisini kwake Balozi wa Palestina hapa nchini Hazen Shabat, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo
   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimkaribisha Ofisini kwake Balozi wa Palestina hapa nchini Hazen Shabat, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo
    Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipiga picha maalum na Balozi wa Palestina hapa nchini Hazen Shabat, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo
   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi wa Palestina hapa nchini Hazen Shabat, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo
   Maofisa katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM, Suleiman  Serera (kushoto) na Cuthbert Midala wakichukua nukuu wakati wa mazungumzo ya Katibu Mkuu  na Balozi wa Palestina
   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi wa Palestina hapa nchini Hazen Shabat, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo
   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimsindikiza Balozi wa Palestina hapa nchini Hazen Shabat, baada ya mazungumzo yao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. PICHA BASHIR NKOROMO


  0 0

   Kaimu Katibu Mkuu,Wizara ya Nishati na Madini,  Profesa James Mdoe akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Uranium One, Vladimir Hlavinka katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam. Katikati ni Rais wa Uranium One Group, Vasility Konstantinov.
   Kaimu Katibu Mkuu,Wizara ya Nishati na Madini,  Profesa James Mdoe akiwa na Rais wa Uranium One Group, Vasility Konstantinov katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
   Viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, Mantra Tanzania na Uranium One wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mazungumzo katika Ofisi za Wizara ya Nihati na Madini jijini Dar es Salaam. Wa nne kulia ni Kaimu Katibu Mkuu,Wizara ya Nishati na Madini,  Profesa James Mdoe,  Wa Tatu kulia ni Rais wa Uranium One Group, Vasility Konstantinov, wa Tatu kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Uranium One, Vladimir Hlavinka, wa Pili kushoto ni Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, wa Pili kulia ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Mantra Tanzania, Frederick Kibodya.
  Kaimu Katibu Mkuu,Wizara ya Nishati na Madini,  Profesa James Mdoe akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mantra Tanzania, Frederick Kibodya  katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam. Katikati ni Rais wa Uranium One Group, Vasility Konstantinov.

  Na Teresia Mhagama, DSM

  Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa kampuni ya Uranium One na Mantra Tanzania ambao wanamiliki leseni ya uchimbaji wa Madini ya Urani kwenye eneo la Mto Mkuju Kusini mwa Tanzania. Mantra ni sehemu  ya  kampuni ya Uranium One na kampuni ya kimataifa ya madini ya ROSATOM-ya Shirikisho la Serikali ya Urusi ya Nishati ya Nyuklia.

  Kikao hicho kilijadili masuala mbalimbali ikiwemo ushirikiano kati ya Tanzania na kampuni hizo, kuporomoka kwa bei ya Urani katika soko la dunia na kampuni hizo kushirikiana na STAMICO katika miradi ya uzalishaji madini.

  Rais wa Uranium One Group, Vasility Konstantinov aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano inaoendelea kuutoa kwa kampuni hizo ili kuhakikisha kuwa lengo la kampuni hiyo kuendeleza mradi wa uchimbaji madini ya urani nchini linafanyika kwa ufanisi.

  Konstantinov pia alitumia nafasi hiyo kukanusha habari zilizoandikwa katika baadhi ya magazeti nchini hivi karibuni kuwa kampuni ya MANTRA Tanzania imesitisha (Suspension) uchimbaji wa Madini ya Urani kwenye leseni yao iliyoko eneo la Mto Mkuju moja ya sababu ikiwa ni mabadiliko katika Sheria ya Madini.

  Alisisitiza kuwa, maombi ya Mantra Tanzania ya kupata  ridhaa ili kusitisha uchimbaji madini ya urani  kwa muda wa miaka mitano yanatokana na kushuka kwa soko la madini hayo katika soko la dunia na kwamba suala hilo halijaiathiri kampuni hiyo pekee bali hata baadhi ya kampuni nyingine.

  “Mradi huu ni muhimu kwa kampuni ya ROSATOM, hatutaki kuondoka, tunataka kuendelea kuwa hapa, tuendeleze ushirikiano  mpaka hapo bei ya urani itakapopanda ili tutekeleze mradi kwa manufaa ya pande zote mbili,”alisema Konstantinov.

  Aliongeza kuwa, kampuni hiyo itaendelea kushiriki katika kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii katika mkoa wa Ruvuma, na tayari wameshajadiliana na uongozi wa mkoa huo kuona namna watakavyoshiriki katika miradi mbalimbali ya kijamii. 

  “Hii inaonyesha kuwa mradi huu ni muhimu kwetu na tunataka kuuendeleza mapema iwezekavyo lakini kikwazo kwa sasa ni kuporomoka kwa bei ya Urani,” alisema Konstantinov.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mantra Tanzania, Frederick Kibodya, alisema kuwa, uwasilishaji wa ombi la kusitisha uchimbaji urani serikalini haumaanishi kuwa kampuni hiyo itasimamisha shughuli zake zote nchini.
  Alisema kuwa, kampuni hiyo itaendelea kufadhili miradi ya kijamii na pia wameanza mazungumzo na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ili kushirikiana nalo katika uendelezaji miradi ya uzalishaji makaa ya mawe na dhahabu.
  Kaimu Katibu Mkuu, Profesa Mdoe aliwaeleleza watendaji wa kampuni hizo kuwa ombi lao la usitishaji wa uchimbaji madini ya Urani nchini limefika katika mikono ya Serikali na kwamba litatolewa uamuzi muda muafaka utakapofika.
  Kuhusu nia ya kampuni hiyo kushirikiana na STAMICO katika miradi ya uzalishaji madini, Profesa Mdoe aliikaribisha kampuni hiyo kushirikiana na Shirika hilo kwani lengo la Serikali ni kukaribisha wawekezaji mbalimbali nchini wenye nia njema ya kuendeleza miradi itakayoleta tija kwa Taifa.
  Kuhusu mabadiliko katika Sheria ya Madini, Profesa Mdoe alisema kuwa lengo la mabadiliko hayo ni kuhakikisha kuwa nchi inafaidika na rasilimali zake na kwamba kama mwekezaji anafuata matwaka ya nchi katika uwekezaji atakuwa hana sababu ya kuogopa mabadiliko.
  “Mabadiliko ya Sheria ya Madini ni kwa ajili ya kunufaisha pande zote mbili, na  si kumyanyasa mwekezaji, kama mwekezaji anakuja kwa nia nzuri hana sababu ya kuogopa,” alisema Profesa Mdoe.

  0 0

  Cathbert Kajuna-Kajunason Blog

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imevifungia vituo zaidi ya 10 jijini Dar es Salaam kwa kosa la kuendesha biashara bila mashine ya Kielektroniki. 

  Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa zoezi la kufungia vituo mbalimbali, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere amesema kuwa kwa sasa zoezi hilo linaendelea nchi nzima ili kuumbua vituo vyote vinavyokwepa kulipa kodi.

   "Tuliwapa muda wafunge mashine hizo mpaka mwaka jana 2016 mwishoni lakini mpaka sasa hawajatekeleza agizo hilo hivyo hatuna budi kuvifunga hivyo vituo mpaka pale watakapotekeleza matakwa ya serikali," amesema Kamshna Kichere. 

  Kwa upande wa Kamishna wa Mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya amesema wakati umefika kwa wafanyabiashara kufuata makubaliano wanayokuwa wakiwafanya na TRA ili kuepuka usumbufu unaojitokeza kwa sasa. Ameongeza kuwa sheria kali zitachukuliwa kwa wafanyabiashara wote ambao vituo vyao vya mafuta vimefungwa na wakakaidi. Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere (mwenye miwani kulia) akimuhoji msimamizi wa kituo cha GBP cha Sinza Mori jijini Dar es Salaam mara baada ya kufika kwa ajili ya zoezi la kukifungia kituo hicho kwa kukosa kuwa na mashine za kielektroniki. Wengine ni wafanyakazi wa TRA walioambatana nae.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere (aliyenyoosha mkono) akiwahimiza vijana wake wafunge kituo hicho.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere (kushoto) akiwa na  Kamishna wa Mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kulia) wakitoa msisitizo.
  Kituo cha GBP kikiwa kimeshafungwa.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere akikagua mashine za kituo cha PUMA kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo alikuta mashine zake za kielektroniki zipo salama.
  Kituo cha KOBIL kilichopo karibu na TCRA, Sinza kikiwa kimefungwa.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere (mwenye tai nyekundu) akimuhoji meneja wa kituo cha OIL COM kilichopo Mwenge mkabala na Vinyago jijini Dar es Salaama kabla hajakifunga.
  Kituo cha OIL COM kilichopo Mwenge mkabala na Vinyago jijini Dar es Salaamakikiwa kimefungwa.
  Mfanyakazi wa TRA akifunga kituo cha OIL COM Ubungo jijini Dar es Salaam.
   Kituo cha OIL COM Ubungo jijini Dar es Salaam kikiwa kimefungwa. Kituo cha TSN - Mwenge kikiwa kimefungwa.
   Kituo cha OIL COM Njia Panda ya Mabibo jijini Dar es Salaam kikiwa kimefungwa.
   Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere akihakikisha jinsi mashine za kituo cha LAKE OIL kilichopo njia panda ya Mabibo jijini Dar es Salaam kabla hakijafungwa.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere akimkabidhi risiti mteja aliyefika kuweka mafuta kituoni hapo.

  0 0

   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akimkabidhi Mfano wa picha ya jengo la Bunge Rais Mstaafu wa Ireland ambae pia ni Mjumbe wa  “The Elders” Taasisi inayoshughulika na Amani, Haki za Binadamu na Huduma za Afya, Mhe. Mary Robinson katika tukio lililofanyika leo katika Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.
   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akizungumza wakati ugeni kutoka “The Elders” Taasisi inayoshughulika na Amani, Haki za Binadamu na Huduma za Afya ilipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, katikati ni Rais Mstaafu wa Ireland ambae pia ni Mjumbe kutoka Taasisi hiyo Mhe. Mary Robinson na kushoto ni Mjumbe wa Taasisi hiyo Ndg. Graca Michel
   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akimsikiliza Mjumbe wa  “The Elders” Taasisi inayoshughulika na Amani, Haki za Binadamu na Huduma za Afya, Ndg. Graca Machel (kushoto) katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, katikati ni Rais Mstaafu wa Ireland ambae pia ni Mjumbe kutoka Taasisi hiyo Mhe. Mary Robinson

  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Rais Mstaafu wa Ireland (katikati) ambae pia ni Mjumbe wa “The Elders” Taasisi inayoshughulika na Amani, Haki za Binadamu na Huduma za Afya, Mhe. Mary Robinson, kulia ni Mjumbe wa Taasisi hiyo Ndg. Graca Machel (kushoto) katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akisalimiana na Mjumbe wa  “The Elders” Taasisi inayoshughulika na Amani, Haki za Binadamu na Huduma za Afya,  Ndg. Graca Machel (kulia) katika tukio lililofanyika leo katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
    Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akisalimiana na Rais Mstaafu wa Ireland (kulia) ambae pia ni Mjumbe wa  “The Elders” Taasisi inayoshughulika na Amani, Haki za Binadamu na Huduma za Afya, Mhe. Mary Robinson katika tukio lililofanyika leo katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.

  (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0

  Serikali imeziasa taasisi za umma zinazoshughulikia viwango nchini kufanya kazi kwa ushirikiano ili kupunguza urasimu na kujiruidia kwa majukumu vitu ambavyo vinapelekea kukuza gharama za uwekezaji nchini.

  Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano uliowakutanisha watendaji wakuu wa mashirika ya viwango nchini jana Jijini Dar es Salaam kujadili uboreshaji wa namna ya kufikia viwango vya bidhaa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Adolf Mkenda amesema kuboresha na kurahisisha mazingira ya uwekezaji ndio kipaumbele cha sertiukali.

  Mkutano huo ambao uliandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) unatokana na mikutano ya wadau iliyofanyika awali kwenye mikoa ya Arusha, Mtwara na Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) ambapo wadau mbalimbali walipata fursa ya kutoa maoni juu ya uboreshaji wa sekta ya viwango nchini.

  “Taasisi za serikali za viwango zinafanya kazi nzuri, lakini kuna urudiwaji wa majukumu ambao unafanya mazingira ya uwekezaji kua magumu,” alisema Prof Mkenda.

  Alisema ipo haja ya kuweka pamoja miundombinu ya kudhibitisha viwango na kwamba TBS iongoze mchakato huo kwa kuwa wao ndio chombo kikuu cha udhibiti wa viwango nchini.

  “Katika utekelezaji wa jambo hili, taasisi zetu lazima zihakikishe kwamba tozo zao haziwi mzigo kwa wawekezaji na wajasiriamali na suala la kukusanya mapato kamwe lisiwe lengo la mashirika ya viwango nchini,” aliwaasa watendaji hao.

  Pia alionya kwamba taasisi hizo zisijisikie ufahari kutoza faini kwa makampuni yanayofanya makosa kuhusiana na viwango na badala yake wajikite katika kuwapa wawekezaji ushauri wa namna ya kuhakikisha kwamba wakaiti wote wanazingatia viwango.

  “Hatutaki kucheza na suala la ubora na suala hili halina mjadala lazima lizingatiwe, lakini tusijikite kwenye kuweka mazingira magumu na badala yake tuboreshe mazingira ya uwekezaji,” alisema.

  Prof Mkenda pia alirudia kusema kwamba serikali haitabishana na wataalamu katika masuala ya viwango vya bidhaa zinazozalishwa ndani na nje ya nchi.

  “Naendelea kusisitiza kwamba serikali haitaingilia mamlaka ya taasisi za viwango, lakini pia taasisi zinalojukumu la kufanya kazi kwa uadilifu na uhuru bila kumuonea au kumkomoa mtu,” alisema.

  Mkurugenzi wa TBS wa Upimaji na Ugenzi, Bi. Agnes Mneney alisema kwamba TBS na taasisi nyingine zitahakikisha kwamba maagizo ya Katibu Mkuu huyo yanafanyiwa kazi ili kuhakikisha kwamba nia njema ya serikali katika kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini inafanikiwa.

   “Napenda kuwaomba wawekezaji na wajasiriamali wabadilishe mtizamo wao juu yetu, wajue kwamba sisi tuko hapa kwa ajili ya kuwasaidia na kamwe wasijishauri wanapokua na tatizo lolote waje kwetu sisi tupo tayari  na tunajisikia fahari kuawahudumia,” alisema.

  Bi. Mneney alisema kwamba wadau mbalimbali waliohojiwa kwenye mikoa ya Tanga, Arusha, Mtwara na Dar es Salaam wamesema kwamba kukosekana kwa sera ya viwango nchini ni kikwazo katika kuimarisha na kurahisisha mchakato wa kupata ithibati ya taasisi za viwango.

  “Habari njema ni kwamba tayari serikali ipo kwenye mchakato wa kuitengeneza sera ya viwango nchini na kukamilika kwake kutaboresha kwa kiasi kikubwa mazingira uwekezaji na kurahisisha mchakato wa kupata ithibati ya viwango,” alisema.

  Mkurugenzi wa Mafunzo na Huduma za Mikoa  wa Shirika la Kuendeleza Viwanda Vidogo (SIDO), Bi. Joyce Meru alisema kwamba taasisi yake tayari imeanza kufanya kazi kwa kushirikiana na TBS pamoja na taaisi nyingine za viwango nchini katika kurahisisha mchakato wa wajasiriamali kubata ithibati ya viwango vya bidhaa zao.

   Naye Mkurugenzi Mtendaji wa  Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini, Bw. Godfrey Simbeye aliipongeza serikali kwa nia yake nyema ya kuboresha na kuimarisha sekta binafsi nchini.

  Alisema kwamba adhima hiyo ya serikali ni lazima iungwe mkono na taaisi zinazohusika na viwango nchini ili kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini na kukuza sekta binafsi.
  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo kwenye mkutano uliowakutanisha watendaji na wakuu wa mashirika ya viwango nchini ambapo aliwataka kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuchochea uwekezaji. Kushoto ni Mkurugenzi wa Upimaji na Ugenzi wa TBS na kulia ni Meneja wa Viwango wa TBS, Bi Mary Meela. Mkutano huo ulifanyika jana Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya watendaji wakuu wa mashirika ya viwango nchini wakiwa kwenye mkutano uliofanyika jijini Dar Es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (wa pili kushoto)akibadilishana mawazo baadhi ya wakurugenzi mara baada ya kufungua mkutano uliowakutanisha watendaji na wakuu wa mashirika ya viwango nchini ambapo aliwataka kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuchochea uwekezaji. Kushoto ni Mkurugenzi wa Upimaji na Ugenzi wa TBS na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye. Mkutano huo ulifanyika jana Jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tulizo Shemu  na mwenzake kutoka Taasisi ya Madaktari Afrika  ya Nchini Marekani Mathew Sackett wakimwekea mgonjwa kifaa maalum cha kurekebisha  mapigo ya moyo ili yawe sawa (kwa jina la kitaalamu Pacemaker) kifaa hicho huwekewa wagonjwa ambao mapigo yao ya moyo yako chini sana. Tangu kuanza kwa kambi maalum ya matibabu ya moyo jumla ya wagonjwa nane wameshawekewa Pacemaker na wengine wanne wanatarajia kuwekewa leo na kesho.  
   Wataalamu wa Magonjwa ya  Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  na wenzao wa Taasisi ya Madaktari Afrika  ya Nchini Marekani wakimwekea mgonjwa kifaa maalum cha kurekebisha  mapigo ya moyo ili yawe sawa (kwa jina la kitaalamu Pacemaker) kifaa hicho huwekewa wagonjwa ambao mapigo yao ya moyo yako chini sana.

    Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu kambi maalum ya matibabu ya Moyo inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Madaktari Afrika ya nchini Marekani kwa wagonjwa ambao mapigo yao ya moyo yako chini sana na hivyo kuwekewa kifaa maalum cha kurekebisha mapigo ili yawe sawa (kwa jina la kitaalamu Pacemaker) . Kushoto ni Daktari Bingwa na Magonjwa ya Moyo Mathew Sackett. Tangu kuanza kwa kambi hiyo mwanzoni wa juma hili jumla ya wagonjwa 20 wameshapatiwa matibabu kati ya hao nane wamewekewa Pacemaker na wengine wanne wanatarajia kuwekewa leo na kesho.  
   Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Madaktari Afrika  ya Nchini Marekani Mathew Sackett akizungumza na waandishi wa habari  na  kuipongeza Serikali kwa uwekezaji mkubwa ulioufanya katika matibabu ya Moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu ya Moyo inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kwa wagonjwa ambao mapigo yao ya moyo yako chini sana na hivyo kuwekewa kifaa maalum cha kurekebisha mapigo ili yawe sawa (kwa jina la kitaalamu Pacemaker). Kushoto ni Daktari Bingwa na Magonjwa ya Moyo Peter Kisenge. Tangu kuanza kwa kambi hiyo mwanzoni wa juma hili jumla ya wagonjwa 20 wameshapatiwa matibabu kati ya hao nane wameshawekewa Pacemaker na wengine wanne wanatarajia kuwekewa leo na kesho.  
   Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akiwaonyesha waandishi wa Habari jina la Dkt.  Mathew Sackett wa  Taasisi ya  Madaktari Afrika  ya Nchini Marekani lilivyoandika katika nguo yake wakati wa mkutano baina yao uliozungumzia kambi maalum ya matibabu ya Moyo inayoendelea katika Taasisi hiyo  kwa wagonjwa ambao mapigo yao ya moyo yako chini sana na hivyo kuwekewa kifaa maalum cha kuyarekebisha ili yawe sawa (kwa jina la kitaalamu Pacemaker) .


  Picha na JKCI

  0 0

   Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (katikati) akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu kwa mkoa wa Mwanza.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (wa tano kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (wa sita kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wabunge, watendaji kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la  Umeme  Tanzania (TANESCO) na viongozi wengine wa kitaifa mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi huo.
   Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani akielezea mikakati ya serikali ya kupeleka umeme katika vijiji na vitongoji vyote mkoani Mwanza kupitia  Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu kwenye uzinduzi huo.
   Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akielezea hali ya umeme katika mkoa huo kwenye uzinduzi huo.
   Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga (kushoto)  na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini Dkt. Gideon Kaunda  (kulia) wakifuatilia  hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani ( hayupo pichani) kwenye uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu kwa mkoa wa Mwanza uliofanyika katika kijiji cha Nyamatala wilayani Kwimba mkoani humo tarehe 13 Julai, 2017.
   Sehemu ya  wananchi wa kijiji cha Nyamatala wilayani Kwimba mkoani Mwanza wakifuatilia hotuba ya uzinduzi iliyokuwa inatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani ( hayupo pichani) kwenye uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu kwa mkoa wa Mwanza uliofanyika katika kijiji cha Nyamatala wilayani Kwimba mkoani humo tarehe 13 Julai, 2017.
   Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa akieleza jambo kwenye uzinduzi huo.
   Sehemu ya wataalam kutoka mkandarasi atakayejenga miundombinu ya umeme katika mkoa wa Mwanza kupitia Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) kwenye uzinduzi huo.


  0 0


  Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Vida Mmbaga akisisitiza juu ya baadhi ya juhudi zilizofanywa na Serikali kupitia Mpango wa taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele mbele ya viongozi kutoka timu ya Everton na mwakilishi kutoka Liverpool katika zoezi lililofanyika leo jijini Dar Es salaam.
  Mratibu wa Mpango wa taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt Upendo Mwingira akibadilishana Mawazo na Mwakilishi kutoka Liverpool wakati wa tukio la kusaidia waliokuwa wagonjwa wa mabusha na matende liliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam. picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
  Mmoja ya Viongozi kutoka timu ya Everton iliyopo ligi kuu nchini Uingereza na aliekuwa mchezaji wa timu hiyo Leon Osman akigawa zawadi kwa waliokuwa wagonjwa wa Matende na Mabusha katika zoezi lakuwasaidia lililofanyika leo jijini Dar Es salaam.
  Picha ya pamoja ya Viongozi kutoka timu ya Everton iliyopo ligi kuu nchini Uingereza, Viongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na waliokuwa wagonjwa wa Matende na Mabusha katika zoezi lakuwasaidia lililofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

  NA WAMJW-DAR ES SALAAM

  UONGOZI wa timu ya mpira wa miguu ya Everton kutoka nchini Uingereza imeridhishwa na huduma inayotolewa kwa wagonjwa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ikiwemo mabusha na matende hapa nchini.

  Hayo yamezungumzwa na mmoja wa viongozi wa Everton Bw. Darren Griffiths ambao ni washiriki katika kuchangia huduma ya magonjwa hayo hapa nchini ambaye ameongozana na timu yake ili kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Gor Mahia kutoka chini Kenya.

  “Tunayo furaha kuona wagonjwa wengi waliokuwa wanaumwa mabusha na metende nchini Tanzania kwa sasa wamepona kabisa na tunahaidi kuwa na Wizara ya afya bega kwa bega katika kutokomeza magonjwa haya” alisema Bw. Darren Griffiths

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kinga Wizara ya Afya Dkt. Vida Mmbaga amesema kuwa kutokana na ushiriki wa Everton katika kuchangia utoaji wa Huduma ya kutibu ugonjwa huo wamefanikiwa kupata ujuzi wa upasuaji hasa kwa wagonjwa wa mabusha na matende hapa nchini.

  Aidha Dkt. Vida amesema kuwa Serikali ikishirikiana vyema na wananchi na mashirika mbalimbali ya afya magonjwa hayo yatatokomea kwa kiasi kikubwa hapa nchini mpaka kufikia mwaka 2025.

  Mbali na Hayo Dkt. Vida amesema kuwa anawashukuru watu wa Everton kwa kupitia ushirikiano wao katika sekta ya afya kwa kutoa huduma pamoja na mafunzo kwa wataalamu ambapo imesaidia kuwafanyia upasuaji wagonjwa elfu moja.

  Kwa upande wake Bw. Yahya Ally Kidege mkazi wa pugu stesheni amesema kuwa anaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwajali wananchi wake kwani amepata upasuaji wa ugonjwa wake wa busha na amepona kabisa kwan alikua na ugonjwa huo takribani miaka 20.


  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki, Mb (kulia) akiwasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni leo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wilaya hiyo kuzungumza na Watumishi wa Umma. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally S. Happi akimkaribisha Waziri Kairuki, na kushoto ni Mkurugenzi wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Aron Kagurumjuli
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally S. Happi akizungumza na watumishi wa umma wa wilaya ya Kinondoni leo (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) katika Wilaya hiyo kuzungumza na Watumishi wa Umma,  Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa Wilaya ya Kinondoni (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya  kikazi katika wilaya hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
  Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni Bibi. Sixtha Kevin Komba akiwasilisha hoja wakati wa kikao kazi  kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika wilaya ya Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam.
  Afisa Utumishi Mwandamizi kutoka Idara ya Ukuzaji Maadili Ofisi ya Rais- Utumishi Bi. Leyla Mavika akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya maadili katika Utumishi wa Umma wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) katika Wilaya ya Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam.
  Mstahiki Meya Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamini Sitta (kulia) akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) baada ya kupokea hoja za watumishi wa Umma wa Wilaya ya Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam. Pichani- Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb)  na kushoto ni Mkurugenzi Manispaa ya Kinondoni Bw. Aron Kagurumjuli. Picha na: Genofeva Matemu - MAELEZO

  Waajiri nchini wametakiwa kufanya uhakiki wa kina wa vyeti vya elimu kwa ajira mpya zitakazotolewa ili kuwa na watumishi wa umma wenye sifa zinazostahili katika utumishi wa umma.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya  Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

  Mhe. Kairuki amesema uhakiki wa kina utasaidia sana kuepukana na kutojirudia tena kwa suala la watumishi wa umma wanaoghushi vyeti.
   “Jana tumetoa vibali vya ajira 10,184 kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, Wakala za Serikali, pamoja na Taasisi na Mashirika ya Umma ili kujaza nafasi zilizoachwa na watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti vya elimu, hivyo napenda niwasisitize sana waajiri wote kufanya uhakiki wa kina ili tusiwe tena na watumishi wa umma wasiostahili katika orodha ya malipo” Mhe. Kairuki amesema.

  Waziri Kairuki amesisitiza kuwa zoezi la uhakiki ni endelevu ambapo lazima lifanyika pale mtumishi wa umma atakaporudi katika kituo cha kazi kutoka masomoni, na watakaorejea katika utumishi wa umma  baada ya likizo bila malipo au sababu nyingine.

  “Tunafanya hivi sio kwa nia mbaya, bali tunataka tuwe na watumishi wanaostahili kuwepo katika utumishi wa umma kwa sababu wanaoghushi wanaziba nafasi za wale wanaostahili kuwepo na wenye sifa katika utumishi wa umma” Mhe. Kairuki aliongeza

  Pia amewataka Waajiri kusafisha taarifa wa watumishi wa umma mara kwa mara katika Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS).
  “Kuna watumishi ambao muda wao wa kuwepo kazini umemalizika (wamestaafu) lakini bado wanaendelea kuwepo, Mfumo wa HCMIS sasa kila ifikapo saa 06:01 usiku utakuwa unawaondoa wale wote ambao muda wao wa kuwepo kazini umefika lakini bado wanaendelea kuwepo kwenye Mfumo.

  Mhe, Kairuki yuko katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Dar es Salaam, ambapo leo ni siku yake ya nne aliyoitumia kukutana na Watendaji na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni,  baada ya kuzungumza na watumishi wa umma wa Temeke na Mbagala.

  Lengo la ziara ni kukutana na watumishi wa umma na kusikiliza malalamiko, ushauri na changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili kuweza kuzifanyia kazi na kuleta mabadiliko katika Utumishi wa Umma nchini.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  13.07.2017

  0 0


  0 0


  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na fundi anayejenga mnara wa kuweka tanki la maji la lita elfu 10 katika kijiji cha Ghalunyangu, Wilayani Singida.
  Mhandisi wa Maji Mkoa wa Singida Mhandisi Lydia Joseph (aliyeinama) akikagua mabomba yatakayotumika kupeleka maji kwenye vituo vitatu vya kuchotea maji katika kijiji cha Ghalunyangu, Wilayani Singida.
  Wanakijiji cha Ghalunyangu wakichota maji katika bomba pekee lililopo katika chanzo cha maji na maradi wa maji kijijini hapo. Fedha za malipo kwa matokeo zimeelekezwa kijijini hapo ili kujenga vituo vitatu vya kuchotea maji kwa kuanzia ikiwa vituo vingine vitajengwa hapo baadaye.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na wana kijiji cha Ghalunyangu, Wilayani Singida waliokusanyika katika chanzo cha maji na eneo ulipo mradi wa maji kijjini hapo.
   
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amewapongeza wana kijiji cha Ghalunyangu kilichopo kata ya Makuro Wilayani Singida kwa uzalendo wa kujitolea nguvu kazi ya kuchimba mtaro wenye urefu wa mita 670 katika mradi wa maji kijijini hapo.

  Dkt Nchimbi ametoa pongezi hizo mara baada ya kushuhudia mtaro huo utakaopitisha maji kutoka katika chanzo cha maji hadi katika tenki la ukubwa wa lita elfu 10 na kuelekea katika vituo vitatu vya kuchotea maji ikiwa ni jitihada za kufanikisha ukarabati wa mradi wa maji kijijini hapo.

  Amesema “nguvu ya kuchimba mtaro huu haitaenda bure, tuna uhakika maji yatafika katika vituo hivyo vitatu kwa kuanzia ili kuwaepusha kuendelea kuchota maji katika bomba moja lililopo eneo la chanzo cha maji”.

  Dkt Nchimbi ameongeza kuwa, “uzalendo huu usiishie kwenye kuchimba mtaro tu, nawaomba mtoe ushauri na mapendekezo ili ukarabati wa mradi huu uwe wa ufanisi mkubwa, na hata mkiona mambo yanaenda ndivyo sivyo toeni taarifa mapema, lakini nina imani na halmashauri ya Singida, itatekeleza kwa ufanisi mradi huu kwa manufaa yenu wana Ghalunyangu”.

  Aidha amewataka wana kijiji hao kuwa walinzi wa miundo mbinu ya mradi huo pamoja na kutunza chanzo cha maji hasa kwa kuongeza eneo la hifadhi ya chanzo cha maji kutoka mita 60 mpaka mita 100 na kupanda miti ya kutosha katika chanzo hicho.

  Kwa upande wake Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Edward Kisalu amesema ukarabati wa mradi huo wa maji unatokana na fedha za malipo kwa matokeo jumla ya shilingi milioni 37 walizopatiwa kutokana na kutekeleza vizuri miradi ya maji Wilayani humo.

  Kisalu amesema halmashauri iliamua kutumia fedha hizo kukarabati mradi wa maji katika kijiji hicho kwa kuwa ni mradi pekee ambao unahudumia wakazi zaidi ya elfu mbili huku ukiwa umechakaa kutokana na mashine ya kusukuma maji ya mradi huo kuwa na zaidi ya miaka kumi toka inunuliwe.

  Amesema fedha hizo zitatumika kununua mashine mpya ya kusukuma maji, kununua tenki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita elfu 10, ujenzi wa mnara wa kuhifadhia tenki, mabomba ya kupitishia maji pamoja na ujenzi wa vituo vitatu vya kuchotea maji.

  Kisalu amefafanua kuwa kutokana na fedha hizo kutotosheleza kukamilisha kazi zote ikiwemo uchimbaji wa mitaro wanakijiji waliamua kwa pamoja wajitolee nguvu kazi zao kuchimba mtaro huo bila malipo yoyote ili ukarabati wa mradi ufanikiwe kwa uharaka zaidi.

  Ameongeza kuwa licha ya kuwepo kwa tanki lenye ujazo wa lita elfu 90 kijijini hapo, mabomba ya kupeleka maji katika tanki hilo yamekatika hivyo halmashauri kwenye bajeti ya mwaka 2017/2018 imetenga shilingi milioni 300 za ukarabati mkubwa wa kupeleka maji katika tenki hilo na kuongeza vituo vya kuchotea maji hivyo kufuta kabisa kero ya maji kijijini hapo.

  Kwa upande wao wanakijiji cha Ghalunyangu wamempongeza Dkt Rehema Nchimbi kwani amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kwanza kufika kijijini hapo hali iliyowapa faraja kubwa na ari zaidi ya kujitolea katika miradi ya maendeleo.

  Wanakijiji hao licha ya kuwa na itikadi tofauti za kichama kwa kauli moja wamesema wana imani kubwa sana na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli kwakuwa matokeo chanya yanaonekana na sio maneno tu.

  Wamesema wana imani na Rais Magufuli sio tu kwenye miradi ya maji kuwa itatekelezwa vizuri bali hata miradi mingine ikiwa ni pamoja na miundombinu ya barabara ambayo tayari mkandarasi ameanza kazi ya ukarabati wa barabara kijijini hapo.

  Naye Mhandisi wa Maji Mkoa wa Singida Mhandisi Lydia Joseph amesema kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17 halmashauri tatu kati ya saba Mkoani Singida zimepokea fedha za malipo kwa matokeo ambapo halmashauri hizo ni Mkalama, Manyoni na Halmashauri ya Wilaya ya Singida.

  Mhandisi Lydia amesema halmashauri hizo zimepata fedha hizo kutokana na kazi nzuri ya kuwasilisha taarifa za miradi ya maji kwa wakati na mfululizo hivyo Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji imezipatia fedha hizo kama motisha.

  Ameongeza kuwa halmashauri ya Wilaya ya Manyoni imepatiwa shilingi milioni 16.6, halmashauri ya wilaya ya Mkalama shilingi milioni 20.1 na halmashauri ya wilaya ya Singida shilingi milioni 37.8.

  Aidha Mhandisi Lydia amezisisitizia halmashauri zilizopokea fedha hizo kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ambayo ni kukarabati miradi ya maji iliyopo vijijini, kuanzisha na kuimarisha jumuiya za watumia maji pamoja na kutunza na kuhifadhi vyanzo vya maji.

  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi SACAP. Rajab Nyange, wakati alipo tembelea na kukagua ujenzi wa Gereza la Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi SACAP. Rajab Nyange, wakati akikagua ujenzi wa Gereza la Wilaya Ruangwa,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi seti ya tv na king’amuzi chake Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi SACAP.  Rajab Nyange,  wakati akikagua ujenzi wa Gereza la Wilaya Ruangwa,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Ruangwa Mjini akiwa kwenye,mkutano wa hadhara aliyo uitisha,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017. 
    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Ruangwa Mjini katika mkutano wa hadhara aliyo uitisha,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi mipira Mbunge wa Liwale Zuberi Kuchauka, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi mipira Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Lindi Hamida Abdallah katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi mipira Mbunge wa Nachingwea Elias Masala, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017. 
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi mipira Mbunge wa Lindi Manispaa,  Selemani Kaunje, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi mipira na jezi Diwani wa Kata ya Luchelegwa, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.


   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea pikipiki aina ya SANLG kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Alan Lin katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Wauza Pikipiki na spea Taifa Martin Mbwana katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi pikipiki kwa niaba ya waendesha bodaboda 49 wa Wilaya ya Ruangwa waliokabidhiwa pikipiki Juma Selemani, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na waendesha bodaboda waliokabidhiwa pikipiki 49 kwa mkopo, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0


  Jengo la mradi wa viwanda vidogo vidogo lililopo eneo la Karakana Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Awamu ya kwanza ya jingo hilo limepangwa kutumia shilingi milioni 190, ambapo inatarajiwa mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu utakuwa umekamilika kwa asilimia 82.(Picha zote na Christina Mwagala, Ofisi ya Meya wa jiji)
  Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita mwenye shati la kijivu akitoa maelekezo kwa maofisa Utumishi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam leo alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ya jiji karakana ya Mwananyamala jijini hapa.
  Mhandisi katika Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Swalehe Nyenye akifafanua jambo kwa Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita alipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa viwanda vidogo Karakana ya Mwananyamala.
  Mkurugenzi wa kampuni ya Kuja na Kushoka tool Manufucture Leodard Kushoka akitoa maelezo jinsi namna ambavyo mashine ya kutengenezea nishati ya mkaa kwa kutumia malighafi inavyofanya kazi wakati wa ziara waliofanya kwenye kikundi hicho kilichopo Tandika. Wa kwanza kulia ni Diwani wa Kata ya Segerea Pratrick Asenga.
  Mashine inayotumika kutengeneza nishati ya mkaa
  Jengo la kikundi cha Upendo Smart kinachofanya shughuli ya kuzalisha nishati ya mkaa kwa kutumia malighafi.
  Mwenyekiti wa kikundi cha Mwangaza Vikoba kilichopo Pugu stesheni Mariam Mzigilwa akisoma risala kwa Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita aliyeambatana na wajumbe wa kamati ya fedha ya jiji leo alipotembelea kikundi hicho, ikiwa ni moja ya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ya jiji.

  …………………………………………………………………………..

  CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

  MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo amefanya ziara ya kutembelea miradi ya Maendeleo ya jiji ambapo ameridhishwa na vikundi vinavyo tengeneza mkaa kwa kutumia malighafi ambapo amesema itasaidia kupunguza uchafu uliopo kwenye maeneo mbalimbali na kuliweka jiji katika hali ya usafi.

  Ziara hiyo ambayo imehusisha Kamati ya Fedha ya Halmashauri ya Jiji, ilitembelea vikundi vya Maendeleo ya ujasiriamali cha Upendo Smart kilichopo mtaa wa Kilimahewa Kata ya Tandika kinachojihusisha na uzalishaji wa mkaa mbadala ( mkaa poa).

  Aidha mbali na kikundi hicho Meya Mwita pia amejionea shuguli za uzalishaji wa mkaa unaofanywa na kikundi cha Maendeleo cha Mwangaza Vikoba kilichopo Pugu stesheni jijini hapa.

  Akizungumza na wanakikundi hao, Meya Mwita amesema kuwa vikundi hivyo vinafanya kazi kubwa kutokana na ubunifu walionao jambo ambalo litasaidia kuweka jiji kwenye hali ya usafi.

  Alifafanua kuwa mbali na kuweka jiji safi pia litapunguza grama kwa wananchi wanaotumia nishati ya mkaa kutokana na nishati hiyo kuuzwa kwa bei nafuu ukilinganishwa na ule unaotumika hivi sasa kwakuwa unagharama kubwa.

  ” Mmefanya kazi nzuri sana wakina mama ,nimeona juhudi zenu, lakini nimesikia changamoto kubwa hapa ninamna ya kuwafikia hao watu waweze kununua nishati hii, niwahakikishie madiwani wenu wapo hapa, Meya wenu nipo hapa tutaendelea kuwaunga mkono” amesema Meya Mwita.

  Amesema” wananchi wanatumia gharama kubwa kununua mkaa unaochomwa kwa kutumia miti, lakini unapotumia huu ambao unatengenezwa na vikundi hivi , kwakutumia malighafi , unawezesha kuinua kiuchumi lakini pia tunatoka kwenye matumizi ya mazoea na kuingia kwenye matumizi ya kisasa.

  Awali ziara hiyo ilianzia kwenye mradi wa ujenzi wa viwanda vidogo vidogo katika eneo la karakana ya Mwananyamala ambapo lengo la mradi huo ni kuwahudumia wananchi na wajasiriamali wadogo wadogo ilikuinua hali za kiuchumi hususani wakina mama na vijana.

  Mradi huo unatokana na fedha zilizotengwa na Halmashauri ya Jiji katika bajeti ya mwaka 2016 /2017 ambapo kwa awamu ya kwanza mradi huo umepangwa kutumia kiasi cha shilingi milioni 190, hadi kufikia mwisho wa mwezi huu utakuwa umekamilika kwa asilimia 82.

  Hata hivyo Mhandisi wa mradi huo katika Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Swalehe Nyenye amesema kuwa awamu ya kwanza ya mradi huo kutajengwa majengo makubwa mawili yenye vyumba vitatu kila moja kwa ajili ya biashara.

older | 1 | .... | 1303 | 1304 | (Page 1305) | 1306 | 1307 | .... | 1897 | newer