Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1304 | 1305 | (Page 1306) | 1307 | 1308 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Mh.Christina Mndeme leo amefanya ukaguzi kwenye vituo vya mafuta ili kuona kama wafanyabiashara ya kuuza mafuta wanafuata sheria na taratibu za utoaji risiti na ulipaji kodi kwa kufunga mashine sahihi ya utoaji risiti iliyofungwa moja kwa moja kwenye pampu au mita ya mafuta. 

  Katika ZIARA hiyo Kati ya vituo 9 alivyovitembelea amegundua kituo kimoja tu ndiyo kinafuata sheria na kuchukua hatua ya kuvifungia vituo nane (08).

  Kazi hiyo imefanyika kwa kushirikiana na maafisa wa TRA Dodoma Mjini. Tunatekeleza kwa Hapa Kazi Tu, Lipa kodi kwa Maendeleo ya Taifa letu.

  Pichani kushoto ni  Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Mh.Christina Mndeme akishirikiana na Ofisa wa TRA kukifungia moja ya kituo cha mafuta mkoani humo kilichobainika kutofuata sheria na taratibu za utoaji risiti na ulipaji kodi kwa kufunga mashine sahihi ya utoaji risiti iliyofungwa moja kwa moja kwenye pampu au mita ya mafuta.
  Wasimamizi wa kituo wakipewa maelekezo baada ya kituo chao cha mafuta kufungiwa

  0 0

  Naibu waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani amesema daraja la Mto Momba lenye urefu wa mita 75 litakalounganisha Mkoa wa Rukwa na Songwe litaanza kujengwa  mapema mwaka huu.

  Eng. Ngonyani ametoa kauli hiyo mara baada ya kukagua barabara ya Kasansa hadi Kilyamatundu na eneo litakapojengwa daraja la Momba na kusema kuwa Serikali imeshampata Mkandarasi atakajenga daraja hilo.

  “Serikali imeshatoa kiasi cha sh. Bilioni tatu  fedha hizo zimetusaidia kutangaza zabuni na kumpata mkandarasi, tayari Mkandarasi wa ujenzi huu ameshapatikana na mkataba wa makubaliano ya ujenzi umeshakamilika hivyo mkandarasi atausaini rasmi hivi karibuni,” amesema Eng. Ngonyani.

  Aidha, Eng.Ngonyani amemtaka Meneja Wa Wakala wa barabara (TANROADS) Mkoa wa Rukwa kuhakikisha anatoa ajira kwa wakazi waliopo kata ya Kipeta ambapo ujenzi wa daraja hilo utafanyika.

  Naye Mbunge wa Jimbo la Kwela Mhe. Ignas Malocha ameishukuru Serikali ya awamu ya tano ya Mhe. Dkt. John Magufuli kwa kutekeleza ahadi ya ujenzi wa daraja hilo ambalo kukamilika kwake kutawaletea maendeleo wakazi hao kwa vile litaufungua Mkoa wa Rukwa na kuunganisha na Songwe na Katavi.

  “Kukamilika kwa ujenzi wa daraja hili kutarahisisha usafirishaji wa mazao ya biashara kutoka mkoa wetu kwenda mikoa mingine inayopakana na mkoa huu na kuokoa maisha ya wananchi ambapo awali walikuwa wa wakiliwa na mamba na wengine kusombwa na maji wakati kuvuka kwenye mto huu,” amesisitiza Malocha.
   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akielekea kukagua sehemu ambapo litajengwa Daraja la Momba litakalounganisha Mkoa wa Rukwa na Songwe .Kulia ni Meneja wa Wakala wa barabara  (TANROADS)Mkoa wa Rukwa  Eng. Msuka Mkina na Wa pili kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kwela Mhe. Ignas Malocha.
   Meneja wa Wakala wa barabara(TANROADS), Mkoa wa Rukwa  Eng. Msuka Mkina (aliyenyoosha kidole) akimwonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa tatu kulia) eneo lipakapojengwa Daraja la Momba wakati alipokagua sehemu ambapo litajengwa Daraja hilo litakalounganisha Mkoa wa Rukwa na Songwe.
   Muonekano wa Sehemu ambapo daraja la Mto Momba litakapojengwa. Daraja hilo litakalounganisha Mkoa wa Rukwa na Songwe.
   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Kulia) akitoa maelezo kwa wananchi wa kijiji cha Kilyamatundu kata ya Kipeta Mkoani Rukwa kuhusu  ujenzi wa daraja la Mto Momba litakalounganisha Mkoa wa Rukwa na Songwe.
  Wananchi wa kijiji cha Kilyamatundu kata ya Kipeta Mkoani Rukwa wakifurahi mara baada ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (hayupo picha) kutoa tamko la kupatikana kwa Mkandarasi atakayejenga daraja la Mto Momba litakalounganisha Mkoa wa Rukwa na Songwe.

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana amemjulia hali mtoto wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Khalfan Kikwete ambaye amelazwa katika wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam,Pichani kulia ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete akiwa na Mkewe Salma Kikwete. (# Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0

  Pichani kati ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa huduma za ajira, Saneslaus Chandaruba akizungumza jambo mbele ya Wanafunzi wa vyuo mbalimbali,waliohudhuria programu endelevu ya miaka mitatu nchini,iliyohusu jinsi ya kuwajengea Misingi bora wanavyuo ya ufanisi wa kazi katika ushiriki wa kazi kwa vitendo katika ofisi au kampuni tofauti Nchini (intern/ Field work).Programu hiyo imefanyika jijini na kuandaliwa na Wakala wa Huduma za Ajira Tz (TaESA ) kwa kushirikiana na Shirika la kazi la Kimataifa (ILO). Pichani kushoto ni Mkurugenzi wa huduma za ajira Tanzania ( TaESA),Kisa Vivian Kilindu na mwisho kulia ni Mwakilishi kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Paulina Mabuga
  Baadhi ya Wanafunzi wa vyuo hao wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye Programu hiyo endelevu ya miaka mitatu nchini,iliyohusu jinsi ya kuwajengea Misingi bora wanavyuo ya ufanisi wa kazi katika ushiriki wa kazi kwa vitendo katika ofisi au kampuni tofauti Nchini (intern/ Field work).Programu hiyo imefanyika jijini na kuandaliwa na Wakala wa Huduma za Ajira Tz (TaESA ) kwa kushirikiana na Shirika la kazi la Kimataifa (ILO).
  Pichani baadhi ya Wanafunzi wa vyuo mbalimbali,waliohudhuria Programu hiyo endelevu ya miaka mitatu nchini,iliyohusu jinsi ya kuwajengea Misingi bora wanavyuo ya ufanisi wa kazi katika ushiriki wa kazi kwa vitendo katika ofisi au kampuni tofauti Nchini (intern/ Field work).Programu hiyo imefanyika jijini na kuandaliwa na Wakala wa Huduma za Ajira Tz (TaESA ) kwa kushirikiana na Shirika la kazi la Kimataifa (ILO).

  0 0

  * Asema changamoto ya kukatika umeme Mkoa wa Lindi kuwa historia 
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema changamoto ya kukatika umeme katika mkoa wa Lindi kuwa historia baada ya kukamilika kwa mradi wa kusafirisha umeme wa kilovolti 132 Mtwara-Lindi.   
                            
  Amesema hayo leo (Alhamisi, Julai 13, 2017) alipotembelea mradi huo wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi. 
  Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa mradi huo uliogharimu sh. bilioni 16 kutamaliza changamoto ya upatikanaji wa umeme katika mkoa wa Lindi. 
  Amesema mkakati wa Serikali ni kuongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme ili Watanzania wapate umeme mwingi utakaosambazwa hadi vijijini kwa gharama nafuu. 

  “Mikoa wa Lindi ulikuwa na shida kubwa ya kukatika kwa umeme, kukamilika kwa mradi huu ni mkombozi kwetu, tunawakaribisha wawekezaji waje kuwekeza kwa sababu sasa tunanishati ya uhakika.”
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof. James Mdoe, wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne (katikati) ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Mnauye.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea maelezo ya mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi kutoka kwa Mhandisi Jafary Msuya, wakati alipotembelea mradi huo unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea maelezo ya mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi kutoka kwa Mhandisi Ferdinand Mwinje,wakati akikagua mradi huo unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiongea na wananchi, wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme wa Mahumbika, unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)​

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Rais wa Mstaafu wa Ireland, Mary Robinson ambaye pia ni Mjumbe wa Taasisi inayoshughulika na Amani,Haki za Binadamu na Huduma za Afya, Rais huyo Mstaafu aliongozana na Mjumbe mwingine wa Taasisi hiyo Bi. Graca Machel . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Rais wa Mstaafu wa Ireland, Mary Robinson ambaye pia ni Mjumbe wa Taasisi inayoshughulika na Amani,Haki za Binadamu na Huduma za Afya, Rais huyo Mstaafu aliongozana na Mjumbe mwingine wa Taasisi hiyo Bi. Graca Machel . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na  Rais wa Mstaafu wa Ireland, Mary Robinson pamoja na Bi. Graca Machel ambao ni Wajumbe wa Taasisi inayoshughulika na Amani,Haki za Binadamu na Huduma za Afya, wengine pichani ni Ujumbe ulioongozana na Viongozi hao pamoja na Wasaidizi wa Makamu wa Rais. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mjumbe wa Taasisi inayoshughulika na Amani,Haki za Binadamu na Huduma za Afya, Bi. Graca Machel ambaye aliongozana na  Rais wa Mstaafu wa Ireland, Mary Robinson kumtembelea Makamu wa Rais ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Mstaafu wa Ireland, Mary Robinson (kulia) ambaye pia ni Mjumbe wa Taasisi inayoshughulika na Amani,Haki za Binadamu na Huduma za Afya, kushoto ni Mjumbe wa Taasisi hiyo Bi. Graca Machel mara baada ya kumaliza mazungumzo kwenye ofisi za Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


  0 0

  --
  Diwani Kata ya Msigani, Ubungo, Israel Mushi ( 48 ) na Mrasimu ramani wa Manispaa ya Ubungo, Francis Mwanjela Peter ( 28 ) wamekamatwa na Tasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa  Sh.5,000,000/=.

  kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa  TAKUKURU wilaya ya  Kinondoni Teddy Mjangira, amesema kuwa Watuhumiwa walikamatwa Julai 12, 2017 baada ya kupokea kiasi hicho cha fedha toka kwa mwananchi ambaye jina lake limehifadhiwa na ambaye mbali na kutoa kiasi hicho cha pesa alitakiwa  na watuhumiwa kuwapa  rushwa ya Sh.10,000,000/=

  Inadawaiwa Watuhumiwa walishawishi na kupokea rushwa ili waweze kutoa ushawishi kwa wajumbe wa kamati ya mipango miji  inashughulikia maombi ya kubadilisha michoro, kubadilisha matumizi ya kiwanja na kupitisha kibali cha ujenzi katika Manispaa ya Ubungo.

  Uchunguzi wa tuhuma unaendelea na Watuhumiwa ambao wanatuhumiwa kutenda makosa kinyume na kifungu namba 15 cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007 wamepewa dhamana.

  Mkuu wa TAKUKURU (M) Kinondoni Bi.T. MNJAGIRA anawaasa Viongozi wote wa Umma, Wanasiasa na Watumishi wote wa Serikali, kuheshimu nyadhifa zao na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria bila kujihusisha na vitendo vya Rushwa. Pia, anatoa wito kwa  Wananchi wote kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU kwa kuwafichua wale wote wanaojihusisha na  vitendo vya rushwa ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria, Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tumezuia vitendo hivyo visiendelee kujitokeza katika Jamii


  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tigo, Simon Karikari akizungumza na waandishi wakati wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknologia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu uliyoandaliwa na GSMA 360 Afrika, jijini  Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Woinde Shisael. Picha kwa hisani ya Tigo

  Tarehe 12 Julai 2015 Dar es salaam - kampuni ya simu ya maisha ya kidigitali  inayoongoza Tanzania, Tigo, Pamoja na wabia wengine, wameshirikiana katika kufanikisha upatikanaji wa mtandao wa broadband kwa watu takribani 70,000 katika maeneo yaliyochaguliwa katika maeneo ya vijijini ya Tanzania.
  Ushirikiano na waendeshaji  wengine wa mitandao ya simu (MNOs) (Mobile network Operators), serikali ya Tanzania na Chama cha kutetea maslahi ya waendeshaji wa mitandao ya simu duniani GSMA (Global System Mobile Association), uliundwa kutatua changamoto za upatikanaji wa mtandao katika maeneo ya vijijini kwa kuanzisha maeneo ya majaribio kama sehemu inayokusudiwa ya mradi wa upatikanaji wa mawasiliano.  
  Katika ujumbe wake katika kongamano linaloendelea la GSMA la 360 - Afrika lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam leo, Kaimu Mkurugenzi wa Tigo  Bwana Simon Karikari, alisema kwamba ni kwa kutumia ushirikiano wa sekta ya umma na sekta binafsi ndipo ambapo tunaweza kukabiliana na changamoto za kidigitali, hivyo kukuza mageuzi ya kidigitali ya Afrika.
  "Kutoa uunganishaji wa simu wa Broadband kwa jamii za vijijini ni moja kati ya changamoto kubwa ambazo waendeshaji wanakabiliana nazo hapa Tanzania leo. Hii ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo: Upatikanaji wa Umeme, Mgawanyiko wa watu kijiografia, na uwezo wa kumudu gharama - hata ambapo huduma za data ni moja kati ya huduma za bei nafuu zaidi katika eneo hilo", alisema Karikari. 
  Akielezea kuhusu ushirikiano, Karikari amesema kwamba wameingia katika makubaliano ya pande tatu ya roaming ambayo maeneo ya majaribio yatawezesha upatikanaji wa mtandao wa broadband kwa wateja wa mitandao yote kutoka katika mnara mmoja, jambo ambalo litawasaidia watumiaji kutumia mitandao ya kila mmoja wao katika eneo lililochaguliwa.
  Mkurugenzi alipongeza ushirikiano wa sekta zaidi ya moja akieleza kwamba ushirikiano huo umewezesha kufanikisha mradi wa roaming wa njia tatu Afrika.
  "Kudokeza baadhi tu ya matokeo yetu", Karikari aliongeza kwamba, "Tayari kulikuwa na watumiaji 17,000 wa simu kila siku baada ya uzunduzi. Leo zaidi ya wakaazi elfu 40 wa maeneo ya vijijini wanapata huduma ya 3G kwa mara ya kwanza, idadi inakadiriwa kuongezeka kufikia elfu 70 kufikia mwishoni mwa mwezi Juni 2017).
  Akishukuru serikali ya uungaji mkono wake katika kutekeleza mradi huu, Hata hivyo Karikari alisema kwamba, aina fulani ya ruzuku, motisha na makubaliano kama vile kodi katika miundombinu kutoka serikalini, inakaribishwa kusaidia MNOs kupungaza baadhi ya gharama zinazotokana na uanzishaji wa maeneo ambayo hayaja lipwa na mapato yanyotokana na mradi.     
  "Tunaamini kwamba mradi huu, pamoja na upekee wake, utaweka uwezekano kwa bara zima la Afrika. Tutaendelea kushirikiana na Serikali, TCRA (Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania), UCSAF (Mfuko wa upatikanaji wa huduma ya mawasiliano Tanzania), na taasisi zingine kutafuta ufumbuzi wa changamoto tulizo zigundua na kuangalia namna tutakavyotumia tuliyojifunza kutoka katika mradi huu kuboresha huduma zetu na hatimaye kuleta uunganisho wa simu Tanzania". Alihitimisha Karikari

  0 0

  MBUNGE wa Morogoro Mjini, Mheshimiwa Abdulaziz Abood, leo mjini hapa, amemkabidhi mshindi wa Sh Milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko, Elizabeth Damian, aliyetangazwa mshindi katika droo ya 22 ya bahati nasibu hiyo inayojulikana pia kama ‘Ijue Nguvu ya Buku’ iliyofanyika juzi Jumatano, jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza katika makabidhiano ya Sh Milioni 20 mjini Morogoro jana, Mbunge Abdulaziz, alisema bahati nasibu ni mchezo unaoweza kutoa fursa nzuri kiuchumi, huku akimtaka mshindi huyo azitumie vizuri pesa zake ili ziweze kumnufaisha kiuchumi.

  Alisema kwamba jinsi mchezo wa Biko unavyochezeshwa ni sehemu muafaka ya kuhakikisha kwamba kila mtu anatumia vyema fursa ya kupiga hatua kiuchumi kwa namna moja ama nyingine, hivyo wananchi wake wa Morogoro na Watanzania wote kwa ujumla waendelee kucheza ili wavune fedha za ushindi.

  “Wakati nawapongeza Biko kwa kubuni michezo hii inayotoa mamilioni kwenu washindi, lakini pia nakupongeza wewe mwananchi wangu wa Morogoro kwa kuwa kati ya wachezaji wenye bahati kubwa kiasi cha leo kukabidhiwa Sh Milioni 20,” Alisema.

  Akizungumzia ushindi wake, Elizabeth aliyekabidhiwa fedha zake katika benki ya NMB, mjini Morogoro, alisema hakuamini kama angeweza kuibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 kutoka Biko, jambo linalomfanya furaha yake isielezeke.

  “Kwa kweli siamini kama leo nimekabidhiwa fedha zangu kiasi cha Sh Milioni 20 nilizopata kutoka kwa Biko, hivyo nawakumbusha Watanzania wenzangu kucheza kwa wingi bahati nasibu hii maana ushindi upo nje nje na fedha zangu nitazitumia vizuri kwa mambo mengi kama vile biashara na ujenzi wa nyumba,” Alisema.

  Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kuacha kucheza Biko ni kukubali kukosa fursa za kiuchumi ambazo kila mtu anaweza kuzipata kwa kucheza mara nyingi bahati nasibu yao inayochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi wa Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel kwa kufanya miamala kwenye simu zao kuanzia Sh 1000 na kuendelea.

  “Kucheza Biko ni rahisi kwa sababu tiketi moja ya Sh 1000 inapofanywa kwa njia ya muamala kwenye simu husika, itampatia nafasi mbili za ushindi wa papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, pamoja na donge nono la Sh Milioni 20 zinazopatikana kila Jumatano na Jumapili, huku namba ya kampuni yetu ikiwa ni 505050 na kumbukumbu namba ni 2456.

  “Kila mtu anaweza kushinda zawadi nono kutoka Biko, hivyo unachotakiwa kufanya ni kucheza mara nyingi zaidi kama njia ya kujiwekea mazingira mazuri ya ushindi mnono kutoka kwenye bahati nasibu yetu ya Biko,” Alisema Heaven.

  Tangu kuanza kwa bahati nasibu ya Biko nchini Tanzania ikiwa ni miezi miwili tu, tayari imeshatoa zaidi ya Sh Bilioni moja kwa washindi wake katika kipindi cha mwezi Mei na Juni pekee, ikiwa ni ishara kuwa Watanzania wengi wamekuwa wakiitumia fursa ya kuvuna mamilioni kutoka Biko.
  Mbunge wa Morogoro Mjini, Mheshimiwa Abdulaziz Abood, kushoto akimkabidhi hundi ya Sh Milioni 20 mshindi wa Biko Morogoro saa chache kabla ya kukabidhiwa fedha taslimu katika benki ya NMB, mjini hapa jana. Anayeshuhudia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven wa pili kutoka kulia.
  Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood wa tatu kutoka kulia akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wa Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku, mshindi wa Morogoro Mjini, Elizabeth Damian wa pili kutoka kushoto. Wa kwanza kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven wakati wanamkabidhi mshindi huyo katika Tawi la benki ya NMB Morogoro jana.  Mshindi wa Shilingi Milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', Elizabeth Damian baada ya kukabidhiwa jana mjini Morogoro.
  Duh! Siamini kama fedha zote hizi zangu! Ndivyo anavyoonekana kusema, mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko aliyepatikana mkoani Morogoro ambapo jana alikabidhiwa mzigo wote.

  0 0


  Meneja wa Kitengo cha chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa (kushoto) akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wakuu wa vitengo vya mawasiliano kutoka kampuni mbalimbali Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa GSMA Mobile 360 Africa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jana jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja wa Mawasiliano wa Tigo Tanzania Woinde Sishael.
  Meneja wa Kitengo cha chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa (kushoto) akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wakuu wa vitengo vya mawasiliano kutoka kampuni mbalimbali Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa GSMA Mobile 360 Africa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jana jijini Dar es salaam. Katikati ni Meneja wa Mawasiliano wa Tigo Tanzania Woinde Sishael na Kulia ni Meneja Ushirikiano wa Masoko wa Africa-GSMA, Adreni Mhuhura.
  Meneja wa Kitengo cha chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa (kulia) akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wakuu wa vitengo vya mawasiliano kutoka kampuni mbalimbali Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa GSMA Mobile 360 Africa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jana jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mwakilishi kutoka Idara ya Mambo ya nje na biashara Australia Dan Woods.
  Meneja wa Kitengo cha chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa (katikati) akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wakuu wa vitengo vya mawasiliano kutoka kampuni mbalimbali Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa GSMA Mobile 360 Africa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jana jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mwakilishi kutoka Idara ya Mambo ya nje na biashara Australia Dan Woods na Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Safaricom Eunice Mumma.

  Meneja wa Kitengo cha chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa (katikati) akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wakuu wa vitengo vya mawasiliano kutoka kampuni mbalimbali Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa GSMA Mobile 360 Africa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jana jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Safaricom Eunice Mumma.
  Mwakilishi kutoka Idara ya Mambo ya nje na biashara Australia Dan Woods akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wakuu wa vitengo vya mawasiliano kutoka kampuni mbalimbali Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa GSMA Mobile 360 Africa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jana jijini Dar es salaam Pamoja nae ni Meneja wa Kitengo cha chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa.

  0 0

   Waziri wa  Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (MB) Mhe. Balozi Amina Salum Ali akifurahia zawadi ya begi lililotengenezwa kwa bidhaa za ngozi ya Tanzania.
   Waziri wa  Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (MB) Mhe. Balozi Amina Salum Ali akifunga maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara ya Dar es Salaam leo Katika Viwanja vya JK Nyerere ,Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji (Biashara na uwekezaji) Prof. Adolf Mkenda akiongea wakati wa hafla yakufunga maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara ya Dar es Salaam Leo Katika Viwanja vya JK Nyerere ,Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bw. Edwin Rutageruka akitoa maelezo mafupi kuhusu maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara ya Dar es Salaam.
   .Kikundi cha kwaya ya TOT kikitumbuiza wakati wa hafla ya kufunga maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara ya Dar es Salaam Leo Katika Viwanja vya JK Nyerere ,Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

   Mtaalamu wa ushonaji mavazi Bw. Abdalah Nyangalio ambaye ni mlemavu wa macho akifurahia hafla ya kufunga maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara ya Dar es Salaam Leo Katika Viwanja vya JK Nyerere ,Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam
  Baadhi ya washiriki wa hafla ya ufungaji wa maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara ya Dar es Salaam  wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani).
                                       

  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  SERIKALI imesema kuwa itapitia mikataba yote katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere pamoja na kufanya mabadiliko ya uongozi huo kutokana na kufanya kazi kwa mazoea.

  Hayo ameyasema leo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa wakati alipotembelea uwanja wa ndege huo baada ya kuwepo kwa taarifa ya wasafiri wakichukua muda mrefu kutoka uwanjani hapo.

  Mbarawa amesema kuwa watu wanapoingia kutoka nje ya nchi wanaanza kusoma Tanzania ilivyo ikiwemo na uwanja wan degu kukaa kwa muda mrefu kutokana na mifumo ya watu kushindwa kujipanga.

  Amesema kuwa mikataba katika uwanja huo wameingia wale watu waliofanya mikataba hawakuangalia masilahi ya nchi ndio maana mapato yanakuwa kidogo tofauti na ilivyo katika uhalisia.

  Aidha amesema kuwa watakaa kikao kimoja kati ya watoa huduma katika uwanja wa mwalimu Julius Nyerere wakiwemo Idara ya Uhamiaji pamoja na benki ambako ndio inafanya watu wakae muda mrefu.

  Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Salim Msangi amesema kuwa wanazifanyia kazi changamoto ambazo Wazari amezianisha licha ya kuwa na miundombinu finyu.

  Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuangalia utoaji huduma katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Salim Msangi akizungumza na waandishi wa habari juu Uboreshaji wa Huduma katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo.
  Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akipata maelezo KaimuMkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Josepp Nyahende alipofanya ziara katika uwanja huo leo .
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akipata maelezo Afisa Maidizi wa Ushuru uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Hezron Gibe jinsi wanafanya kazi katika uwanja huo.
  Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akipewa maelezo na watoa huduma Ushuru uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo .

  0 0


  0 0  Mbunge wa Jimbo la Ndanda Cecil Mwambi akiwa na Mbunge wa Masasi Rashid Chuwachuwa (Kushoto) na Diwani wa Kata ya Ndanda Costancia Bernad, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipo simama katika kijiji cha Nanganga, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nanganga, wakati alipo simama, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amkabidhi Mbunge wa Jimbo la Ndanda Cecil Mwambi mipira, wakati alipo simama katika kijiji cha Nanganga, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017.

  Wananchi wa kijiji cha Nanganga wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati alipo simama katika kijiji hicho, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Wananchi wa kijiji cha Mtama wakishangilia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati alipo simama kuweka jiwe la msingi katika kituo cha Polisi kijijini hapo, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Mtama,Nape Mnauye alipo simama kuweka jiwe la msingi katika kituo cha Polisi kijijini hapo, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mtama, wakati alipo simama kuweka jiwe la msingi katika kituo cha Polisi kijijini hapo, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akisalimiana na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba (NHC),wakati alipofungua Zahanati katika kijiji cha Mnolela, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne (katikati) ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Mnauye Julai 13, 2017.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akikata utepe wakati alipofungua Zahanati katika kijiji cha Mnolela, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne (kutoka kushoto) ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Mnauye, Diwani Kata ya Mnolela Omar Liveta, Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba (NHC) kutoka kulia ni Meneja NHC Lindi Gibson Mwaigomole, Meneja NHC Mtwara Nehemia Msigwa, Mkuu wa Mkoa Lindi Godrey Zambi Julai 13, 2017.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akikagua wakati kifaa katika Zahanati ya Mnolela, baada ya kuifungua, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akizungumza na wananchi wa Mnolela mara baada ya kuifungua Zahanati hiyo iliyopo katika Kijiji cha Mnolela, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  …………………………………………………………………

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi wa Shirika la Nyumba (NHC) kwa kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mnolela mkoani Lindi kwa muda mfupi.

  Amesema ujenzi wa zahanati hiyo ya kisasa mwezi Machi, 2017 na sasa tayari kimekamilika, jambo ambalo litarahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo na wa jirani.

  Waziri Mkuu alitoa pongezi hizo jana jioni (Alhamisi, Julai 13, 2017) alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Mnolela baada ya kuzindua zahanati hiyo iliyosimamiwa na NHC.

  Alisema ujenzi wa zahanati hiyo ni muendelezo wa mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kuboresha huduma za afya kwa kusogeza huduma karibu kwa wananchi wake.

  “Rais wetu Dkt. John Magufuli amedhamiria kuwaondolea wananchi changamoto za mbalimbali zikiwemo za huduma za afya, hivyo tuendelee kumuunga mkono.”

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa NHC, Bw. Nehemia Mchechu alisema mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo ulisimamiwa na NHC na umegharimu sh. milioni 65.5.

  “Shilingi milioni 15 zilitolewa na Rais. Dkt. Magufuli, sh. milioni 10 zilitolewa na Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye, NHC ilitoa sh. milioni 10 na kiasi kilichosalia ni mchango wa halmashauri.”

  Awali Mbunge wa jimbo la Mtama, Mheshimiwa Nape alimshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa mchango mkubwa alioutoa katika mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo.

  Mheshimiwa Nape alisema zahanati hiyo ni mkombozi kwa wakati wa kijiji cha Mnolela na wananchi wengine wanaoishi kwenye maeneo yaliyo jirani na kijiji hicho.

  0 0


  Marehemu  Patricia Ndenengo Shang'a enzi za uhai wake.

  Familia ya marehemu Mzee Michael John Shang'a ya Msasani Beach (Mlalakua darajani) jijini Dar es salaam inasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao  dada mpendwa Patricia Ndenengo Shang'a kilichitotokea jana July 13, 2017  hapo nyumbani.

  Mazishi yanatarajiwa kufanyika Jumamosi July 15, 2017.
  Msiba upo hapo hapo nyumbani Mlalakua darajani. 


  Habari ziwafikie Familia zote za Shang'a, Kimesera, Mosha, Mmari, Ngowi, Mmasi pamoja na  ndugu, jamaa, marafiki na majirani popote pale walipo.

  MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI  PEMA PEPONI-AMEN.

  0 0

  Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba, akizungumza na Naibu Balozi wa Marekani nchini,Dk. Inmi Patterson na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Siasa na Uchumi wa Ubalozi huo, Marilyn Gayton(kulia), walipomtembelea ofisini kwake kujadili masuala mbalimbali ya Ulinzi na Usalama,jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Katibu wa Waziri,Nelson Kaminyoge. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Naibu Balozi wa Marekani nchini, Dk. Inmi Patterson, akizungumza na Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, alipomtembelea Waziri huyo kujadili Masuala ya Ulinzi na Usalama, jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Siasa na Uchumi wa Ubalozi huo,Marilyn Gayton na kushoto ni Katibu wa Waziri,Nelson Kaminyoge. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba, akimsikiliza Naibu Balozi wa Marekani nchini, Dk. Inmi Patterson(kulia) alipomtembelea ofisini kwake kujadili Masuala ya Ulinzi na Usalama, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba, akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Balozi wa Marekani nchini, Dk. Inmi Patterson(kulia), baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu Masuala ya Ulinzi na Usalama.Kikao hicho kimefanyika leo jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akizungumza na Viongozi wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara yake, mkoani Tanga wakati kiongozi huyo alipofanya ziara yake kikazi mkoani humo. Katika mazungumzo yao, Masauni aliwahasa viongozi hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa kujituma zaidi na kuwahakikishia kero zote walizompa atahakikisha anazifanyia kazi. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Benedict Wakulyamba.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimfafanulia jambo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela (kulia) kabla ya kiongozi huyo kuanza ziara yake mkoani humo. Katika mazungumzo yao ambayo yalifanyika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huyo, Masauni aliwataka maafisa uhamiaji pamoja na Polisi kuongeza kasi ya kutafuta mizizi ya wahamiaji haramu mkoani humo. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Benedict Wakulyamba. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela (katikati) alipokua anatoa taarifa ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo, kabla ya kiongozi huyo kuanza ziara yake mkoani humo. Katika mazungumzo yao, Masauni aliwataka Maafisa Uhamiaji pamoja na Polisi kuongeza kasi ya kutafuta mizizi ya wahamiaji haramu mkoani humo. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Benedict Wakuliamba. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akitoka kulikagua jengo la Ofisi ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tanga ambalo linahitaji matengenezo ili kulirudisha katika hali yake ya kawaida. Hata hivyo, Masauni alimuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba (kulia) kuhakikisha jengo hilo linatengenezwa haraka iwezekavyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimfafanulia jambo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela (katikati) na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Zena Saidi, kabla ya kiongozi huyo kuanza ziara yake mkoani humo. Katika mazungumzo yao ambayo yalifanyika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huyo, Masauni aliwataka maafisa uhamiaji pamoja na Polisi kuongeza kasi ya kutafuta mizizi ya wahamiaji haramu mkoani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

  0 0

  WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amewaasa watumishi wa mahakama kushughulikia vitendo vya rushwa kwani vinaipatia mahakama taswira hasi na kuzitaka tume za  mahakama na maadili kuchunguza vitendo vya ukiukwaji wa maadili na kuchukua hatua stahiki.

  Waziri Kabudi, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na watumishi wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani juu ya mustakabali wa taasisi hiyo, ikiwa ni mara yake ya  kwanza kufanya ziara tangu alipoteuliwa kuwa Waziri.

  Amesema, majaji na mahakimu mara nyingi, wamekuwa wakihusishwa na vitendo vya rushwa hivyo, na kuchangia kuwepo kwa kutokuwa na imani kwa wananchi wanaokuwa na shida ,mbali mbali katika taasisi hizo, hasa wale wenye kesi.

   ‘’Pamoja na mabadiliko makubwa katika mahakama bado kumekuwa na changamoto ya uadilifu hususan vitendo vya rushwa na uwajibikaji ambavyo vimeleta taswira hasi kwa wananchi wanaotafuta haki na kusababisha ushiriki mdogo,’’alisema Profesa Kabudi.

  Ameongeza, watendaji wanapaswa kubuni mbinu mbali mbali za kuweza kubadili taswira hiyo kwa kuwachukulia hatua za kinidhamu wanaokiuka maadili na kusogeza huduma kwa wananchi.Kwa mujibu wa Profesa Kabudi, mahakama inanafasi kubwa ya kuchangia maendeleo ya nchi na kwamba jambo wanalopaswa kufanya ni kuimarisha utendaji kazi na kutokomeza rushwa.

  Kwa upande wake, Kaimu Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma alisema kuwa wataendelea kutumia sheria kwa ajili ya kuwainua wananchi wengi kwa lengo la kukuza uchumi.

  Profesa Juma alisema majaji na mahakimu ni sehemu ya jamii ambao wanapaswa kushiriki kustawisha wanaqnchi ili kutokomeza umasikini.
  Akiwasilisha ripoti kuhusu mahakama, Mtendaji Mkuu wa mahakama, Hussein Katanga alisema kuwa idadi ya majaji imeshuka kutoka 100 hadi 80 huku uhitaji wake ukiwa ni kati ya 100 hadi 120.

  Katanga alisema majaji 20 wameacha kazi kwa sababu mbalimbali ikiwemo kustaafu na kwamba uhitaji huo unachangia kasi ya kuongezeka kwa ufunguaji mashauri.

  0 0


   Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Zanzibar,Amina Salim Ali (wa pili kulia) akimkabidhi Cheti cha Ushindi wa pili kundi la Nishati na Madini,Afisa Uhusiano Tanesco Makao Makuu,Yasini Didas Silayo (kushoto) huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Profesa Adolf Nkenda,(kulia) na Kiongozi wa Tantrade.
   Afisa Uhusiano Tanesco Makao Makuu,Yasini Didas Silayo (kushoto) akishikilia chena na  Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi Tanesco,Dk, Lugano Wilson,baada ya kukabidhiwa.
   Afisa Uhusiano Tanesco Makao Makuu,Yasini Didas Silayo (kushoto) akishikilia chena na  Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi Tanesco,Dk, Lugano Wilson,baada ya kukabidhiwa.
  Afisa Uhusiano Tanesco Makao Makuu,Yasini Didas Silayo (kushoto) akishikilia chena na  Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi Tanesco,Dk, Lugano Wilson,baada ya kukabidhiwa.

  0 0


  Timu ya Soka ya Everton inayoshiriki ligi kuu nchini Uiungereza imemaliza ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania na kuelezwa kufurahishwa na namna Watanzania walivyoipokea timu hiyo.

  Timu ya Everton iliwasili Tanzania siku ya Jumatano wiki hii ambapo jana ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia kutoka Kenya.

  “Imekuwa ni uzoefu mpya kwangu kuja hapa (Tanzania) na nina tumaini sasa Makamu wa Rais atakuwa akiishabikia Everton”, alieleza Wayne Rooney kupitia tovuti ya timu hiyo.

  Pia katika akaunti yake ya mtandao wa tweeter, Rooney aliwashukuru washabikji wa Tanzania kwa kuiunga mkono Everton katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia kutoka Kenya.

  “Great start to the pre-season. Special thanks to the fans supporting us in Tanzania”, aliandika Rooney akitoa shukrani za pekee kwa washabiki wa Tanzania.

  Kwa upande wa Kocha wa timu hiyo, Ronald Koeman alielezea kufarahia ziara ya kuja Tanzania na zaidi ni kutokana na hali ya urafiki iliyooneshwa na washabiki wa soka nchini.

  Rooney pia aliungana na wachezaji wengine kama Morgan Schneiderlin, Jonjoe Kenny na Kevin Mirallas wa timu hiyo walipata fursa ya kujifunza tamaduni za kimsai, kujifunza kupika chakula cha asili, kutembelea shule yenye wanafunzi wenye mahutaji maalum na pia kufanya mazoezi na timu ya vijana wenye ulemavu wa ngozi (Albino United).

  Timu ya soka ya Everton ilifanya ziara nchni Tanzania ambapo ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa Mgeni Rasmi, Marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na wageni mbalimbali kutoka ndani na nche ya nchi. 


  Wayne Rooney (wa tatu kushoto) kushoto akiwa na wachezaji wenzake walipokuwa Jijini Dar es Salaam ambapo timu ya Everton ilicheza na timu ya Gor Mahia katika mchezo wa kirafiki ulichezwa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

older | 1 | .... | 1304 | 1305 | (Page 1306) | 1307 | 1308 | .... | 1898 | newer