Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

WANANCHI WATEMBELEA BANDA LA JESHI LA MAGEREZA KATIKA MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA YANAYOENDELEA JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
 Wakazi wa jijini Dar es Salaam waliotembelea Banda la Jeshi la Magereza, wakiangalia nafaka mbalimbali zinazolimwa katika mashamba ya Magereza nchini kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere,Barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Askari wa Jeshi la Magereza, Happy Kweka, akiwaonyesha vitambaa vinavyotengenezwa na jeshi hilo wakazi waliotembelea Banda la jeshi hilo katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea   katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere,Barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
 Wakazi wa jijini Dar es Salaam waliotembelea Banda la Jeshi la Magereza, wakiangalia vikapu vinavyotengenezwa katika viwanda vya ufumaji vya Magereza nchini kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere,Barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.Kulia ni askari wa  jeshi hilo,Issah Ramadhan
 Askari wa Jeshi la Magereza, Stesheni Sajenti, Elizei Naje aliyepo sehemu ya mapokezi katika Banda la jeshi hilo akiwa amekaa kwenyemoja ya samani (meza na viti) ambavyo hutengenezwa katika viwanda vya jeshi hilo katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere,Barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Samani zinazopatikana katika Banda la Jeshi la Magerezakwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere,Barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Samani zinazopatikana katika Banda la Jeshi la Magerezakwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere,Barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya NchiIMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI




SAFARI YA MWISHO YA MTANGAZAJI WA REDIO 93.7 EFM, SETH KATENDE MAARUFU BIKIRA WA KISUKUMA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitoa salamu zake wakati wa kuagwa kwa mwili wa Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma ambaye alikuwa Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha 93.7 EFM kupitia kipindi cha Ubaoni, likiwa katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam
 MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akitoa salamu zake wakati wa kuagwa kwa mwili wa Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma   leo kwenye viwanja vya Leaders leo jijini Dar.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akitoa salamu zake kwa famila, ndugu na jamaa.
Baba wa marehemu, Mzee Katende (wa kwanza kushoto) akiwa ndugu zake marehemu wakiaga mwili wa Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma   leo kwenye viwanja vya Leaders leo jijini Dar.
Mke pamoja na mtoto wa marehemu wakiaga mwili 
 MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akiaga mwili mwili wa Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma   leo kwenye viwanja vya Leaders leo jijini Dar
 Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob akiaga mwili mwili wa Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma  leo kwenye viwanja vya Leaders leo jijini Dar
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akiaga mwili mwili wa Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma   leo kwenye viwanja vya Leaders leo jijini Dar.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akiaga mwili mwili wa Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma   leo kwenye viwanja vya Leaders leo jijini Dar
Mkurugenzi na mzalishaji wa vipindi waClouds Media Group, Ruge Mutahaba(mwenye shati nyeusi) akiaga mwili mwili wa Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma   leo kwenye viwanja vya Leaders leo jijini Dar
Mtangazaji waClouds FM Gardner G Habash akiaga mwili

Mtangazaji wa EFM, Mpoki 'Mwarabu wa Dubai'( katikati) akiwa ameshikiriwa mara baada ya kuanga mwili wa Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma   leo kwenye viwanja vya Leaders leo jijini Dar

  

 

  Sehemu ya Waombolezaji wakiwa katika Viwanja Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam kunakofanyika misa ya kuaga mwili wake hivi sasa, ambapo baada ya kumalizika kwa misa hiyo, Mwili wa Marehemu utapumzishwa kwenye nyumba yake ya Milele katika Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es salaam mchana wa leo.
 

 
 Baba wa marehemu, Mzee Katende akiwa ameshikiliwa mara baada ya kuaga mwili wa Mtoto wake Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma   leo kwenye viwanja vya Leaders leo jijini Dar 


  



WASHABIKI WA MUZIKI NCHINI WAZISUBIRI KOLABO MATATA ZA COKE STUDIO KWA SHAUKU

$
0
0


Msanii Rayvanny (katikati) akiwa na wasanii wenzake wakifanya moja ya Mashup hivi karibuni
Mwanamuziki Izzo Business akiwa amepozi ndani ya studio jijini Nairobi
Baadhi ya wasanii nguli waliopo kwenye matayarisho ya Coke Studio msimu wa tano wakiwa katika picha ya pamoja jijini Nairobi hivi karibuni.


---

Wakati uandaaji wa onyesho la muziki la Coca-Cola Coke Studio msimu wa tano unaendelea jijini Nairobi nchini Kenya linalojumisha kolabo za wanamuziki wa kitanzania kwa kushirikiana na wanamuziki wa nje, washabiki wa muziki nchini wamezisubiri kwa shauku kolabo hizo.

Burudani za onyesho hili ambalo limepata umaarufu mkubwa nchini kutokana na kufuatiliwa na wapenzi wengi wa muziki kupitia luninga litaanza kurushwa mapema mwezi Septemba na kwa upande wa Tanzania wasanii ambao wako ndani ya nyumba ni Rayvanny, Izzo Bizness na Nandy.

Katika onyesho la Coke Studio msimu mwa mwaka jana wakali wa muziki nchini ambao walishiriki walikuwa ni Ally Kiba,Vanessa Mdee,Ben Pol na Fid Q ambao walishirikiana na wanamuziki Wangechi, Maurice Kirya, Victoria Kimani na 2Face.

Katika msimu wa Coke Studio wasanii wanaoshiriki wanatokea katika nchi za Kenya,Afrika ya Kusini, Uganda, Tanzania, Rwanda, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Angola, Zimbabwe, Togo, Cote d’Ivoire, Madagascar, Mauritius, Mozambique, DRC na Cameroon wakisindikizwa na mwanamuziki nguli wa kimataifa kutoka nchini Marekani Jason Derulo.

Mbali na wasanii kutoka Tanzania wakali wengine wa muziki kutoka nchi za Afrika wanaoshiriki msimu huu ni Khaligraph Jones na Band Becca (Kenya),Sami Dan (Ethiopia),Bebe Cool, Eddy Kenzo , Sheebah, Ykee Benda ( Uganda).

Wengine ni Nasty C, Busiswa, Mashayabhuqe kutoka Afrika ya Kusini, Youssoupha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Runtown na Yemi kutoka Nigeria, Dji Tafinha kutoka Angola, Laura Beg kutoka Mauritius,Jah Prayzah na Slapdee kutoka Central Africa Republic,Bisa Kdei na Worlasi kutoka Ghana

Taarifa kutoka kampuni ya Coca-Cola ambayo iliyotolewa hivi karibuni imeeleza kuwa onyesho la Coke Studio ambalo umaarufu wake umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka msimu huu utakuwa na burudani za aina yake kutoka kolabo za wasanii nguli barani Afrika kuanzia Afrika Magharibi mpaka Afrika ya Kusini na litarushwa na vituo vya luninga kwenye nchi zaidi ya 30 barani Afrika na kuzidi kuifanya Afrika izungumze lugha moja tu ya muziki.

Imelielezea zaidi kuwa onyesho hilo kuwa lina lengo la kukusanya pamoja wasanii na kuonyesha uwezo na vipaji vya muziki vilivyopo Afrika ikiwemo kutoa fursa kwa wasanii chipukizi kufanya kazi na baadhi ya wasanii na watayarishaji wa muziki wa kimataifa,vilevile Kuwakusanya wasanii wanaofanya aina tofauti ya muziki, wanaotoka katika nchi tofauti za Kiafrika kuwawezesha kutengeneza sauti ya Afrika kupitia burudani ya muziki

Coca Cola Coke Studio pia inaleta burudani kubwa kwa washabiki wa muziki wa kiafrika na kuwaunganisha waafrika hususani vijana kupitia muziki.

TUFUATILIE WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII JINSI WAZEE NA WATOTO( IDARA KUU YA MAENDELEO YA JAMII) KATIKA MITANDAO YA KIJAMII.

WAKANDARASI WA KITANZANIA KUWEZESHA ILI KUFANIKISHA TANZANIA YA VIWANDA

$
0
0
Kampuni ya Mantrac Tanzania imezindua mpango maalum wa kukodisha na kumiliki mitambo kwa kulipa kidogo kidogo ili kuwarahisishia wateja mzigo wa kulipa fedha kununua mtambo kwa mara moja.

Hii inamaanisha kuwa wafanyabiashara na wakandarasi wataweza kukodisha mitambo kutoka katika kampuni ya Mantrac Tanzania kwa bei nafuu na kuanzia miezi sita na kuendelea anakuwa mmiliki kamili wa mtambo huo.Hayo yamesemwa na mkuu wa kitengo cha mipango na masoko Bw Valence Pantaleo. 

Alisema katika kipindi chote cha kukodisha, kampuni ya Mantrac Tanzania inagharamia matengenezo ya mtambo huo kadiri ya mwongozo wa kampuni ya CAT.Mpango wa kukodisha na kumiliki ni maalum ambao unamwezesha mkandarasi au mfanyabiashara kupata manufaa lukuki ya kutumia mitambo inayotumia tekinolojia ya kisasa kabisa ya kampuni ya CAT bila ya kununua mtambo huo mwanzo wa mradi.

Mpango huu unatoa unafuu mkubwa sana na huweza kupunguza sana gharama za uendeshaji kwa mkandarasi au mfanyabiashara.Kampuni ya Mantrac Tanzania inamhakikishia mteja mitambo na tekinolojia madhubuti ya Catepillar yenye historia pana ya kutengeneza na kuuza mitambo ya kisasa inayotumia katika miradi mikubwa ya kujenga miundombinu.
Miradi hii mikubwa ya miundombinu ni pamoja na ujenzi wa barabara, reli, majengo, madaraja, kwenye madini na kilimo.

Bidhaa zinazouzwa na kampuni ya Mantrac Tanzania zinapatikana katika matawi mbalimbali nchini kama vile Dar es Salaam, Mtwara, Mwanza, Mbeya, na Kilimanjaro.Bw Pantaleo alisema baada ya kupata mafanikio makubwa katika biashara kati ya kampuni ya Mantrac Tanzania na wateja kwenye  mitambo mipya, iliyotumika na kukodisha mitambo, sasa kampuni imeamua kuleta mpango huu wa kukodisha na kumiliki ambapo mteja atalipa kidogo kidogo hadi pale atakapomiliki mtambo wake.

Alisema kamupuni ina mitambo mingi inayofikia zaidi ya dola za kimarekani milioni 15 kwa ajili ya kutekeleza mpango huu mpya wa kukodisha na kumiliki.Kampuni ya Mantrac Tanzania ndio pekee yenye kibali cha kusambaza na kuuza mitambo mbalimbali inayotengenezwa na kampuni ya CAT hapa nchini Tanzania.

Kampuni pia ina vituo maalum vya huduma kwa ajili ya matengenezo ya mitambo, ina wataalamu wa hali ya juu na vifaa vyenye viwango vya kimataifa ambavyo hutumika katika kuchunguza tatizo na kutengeneza ubovu unaojitokeza katika mitambo.Katika mpango huu, vigezo na masharti vitazingatiwa.
Meneja Masoko wa Mantrac  Bw Valence Pantaleo.

MTANNGAZAJI WA REDIO EFM SETH KATENDE AZIKWA MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR LEO

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh.Paul Makonda akiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma, ambaye alikuwa Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha 93.7 EFM kupitia kipindi cha Ubaoni,wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jioni ya leo jijini Dar.Marehemu Seth ameagwa mapema leo katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Bi.Zawadi Msalla akienda kuweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma, ambaye alikuwa Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha 93.7 EFM kupitia kipindi cha Ubaoni,wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jioni ya leo jijini Dar.Marehemu Seth ameagwa mapema leo katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali.
Mkurugenzi wa 93.7 Efm Dar Es Salaam Francis Ciza akiweka shada la maua katika kaburi la mtoto wake Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma, ambaye alikuwa Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha 93.7 EFM kupitia kipindi cha Ubaoni,wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jioni ya leo jijini Dar.Marehemu Seth ameagwa mapema leo katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali
Baba wa Marehemu,Mzee Katende akiweka shada la maua katika kaburi la mtoto wake Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma, ambaye alikuwa Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha 93.7 EFM kupitia kipindi cha Ubaoni,wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jioni ya leo jijini Dar.Marehemu Seth ameagwa mapema leo katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali .


Baadhi ya Ndugu jamaa na Marafiki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki Mazishi ya Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma, ambaye alikuwa Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha 93.7 EFM kupitia kipindi cha Ubaoni,wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jioni ya leo jijini Dar.Marehemu Seth ameagwa mapema leo katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali.
 
 

MAKAMU WA RAIS APOKEA UJUMBE MAALUM WA WAZIRI MKUU WA LESOTHO KWA NIABA YA RAIS MAGUFULI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akizungumza na Waziri  wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa nchi ya Lesotho Mhe. Lesogo Makgothi (kushoto) ambaye alifika ofisini kwa Makamu wa Rais kuwasilisha Ujumbe Maalum wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo ambapo Makamu wa Rais aliupokea kwa niaba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais-Ikulu, Dar Es Salaam)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimsikiliza Waziri  wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa nchi ya Lesotho Mhe. Lesogo Makgothi (kushoto) ambaye alifika ofisini kwa Makamu wa Rais kuwasilisha Ujumbe Maalum wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo ambapo Makamu wa Rais aliupokea kwa niaba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais-Ikulu, Dar Es Salaam)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akipokea Ujumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi ya Lesotho na kukabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa nchi ya Lesotho Mhe. Lesogo Makgothi (kushoto) ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais-Ikulu, Dar Es Salaam)

WAZIRI WA ZANZIBAR KUFUNGA MAONESHO YA 41 YA BIASHARA KIMATAIFA KESHO

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Global ya Jamii

Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Amina Salum anaratajiwa kuwa mgeni rasimi kesho katika ufungaji wa maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Viwanda , Biashara na Uwekezaji kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini (Tantrade) ilisema kuwa maonesho hayo yataitimishwa na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Amina Salum ambaye atatoa vyeti kwa washindi wa mabanda bora yaliyoshiriki maonesho hayo.

Taarifa hiyo ilisema kuwa maonesho hayo yatafungwa majira ya saa saba kwa hotoba ya Waziri huyo na kufuatana na viongozi mbalimbali wakiwemo waandaji wa Maonesho hayo.

Wakati huo katika maonesho hayo wananchi wameendelea kufika katika viwanja vya sabasaba kwa kupata huduma pamoja bidhaa za washiriki.

Mabanda ambayo yamekuwa na watu katika siku ya maonesho tangu siku kwanza hadi leo ni mabanda Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Katibu Mkuu wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji , Profesa Adolf Mkenda akimpa maelekezo Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) ,Mcharo Mrutu katika maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji , Profesa Adolf Mkenda akisaini kitabu cha wageni katika maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwananchi akipata huduma katika banda Chuo cha Taifa Usafrishaji (NIT) katika maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakipata huduma katika banda la Wakala Usajili , Ufilisi na Udhamini (RITA) katika maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa maonesho ya ya 41 ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

JICA watembelea hospitali yaTaifa ya Muhimbili

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na ujumbe kutoka JICA. Ujumbe huo umetembelea wagonjwa pamoja na miradi mbalimbali  ya kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo leo.
 Wageni kutoka JICA wakiwa katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru. Kutoka kushoto ni Ofisa wa Hospitali Kuu ya Shonan Kamakura, Emiko Shiono,  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JICA Idara ya Afrika, Komori Masakatsu, Mwakilishi wa Afrika nchini Japan, Milanga Mwanatambwe na Meneja wa Tiba, Injinia Katsumasa Shirai.
 Ofisa Mipango, Catherine Shirima (kulia) wa JICA na Yamae Mikuni kutoka Japan wakiwa kwenye mkutano huo leo.
Wageni hao pamoja na wenyeji wakiwa katika wodi ya wagonjwa Muhimbili leo.

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ni mkombozi Afrika Mashariki

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na ujumbe kutoka JICA. Ujumbe huo umetembelea wagonjwa pamoja na miradi mbalimbali  ya kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo leo.
 Wageni kutoka JICA wakiwa katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru. Kutoka kushoto ni Ofisa wa Hospitali Kuu ya Shonan Kamakura, Emiko Shiono,  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JICA Idara ya Afrika, Komori Masakatsu, Mwakilishi wa Afrika nchini Japan, Milanga Mwanatambwe na Meneja wa Tiba, Injinia Katsumasa Shirai.
 Ofisa Mipango, Catherine Shirima (kulia) wa JICA na Yamae Mikuni kutoka Japan wakiwa kwenye mkutano huo leo.
Wageni hao pamoja na wenyeji wakiwa katika wodi ya wagonjwa Muhimbili leo.

Na.Agness Moshi-MAELEZO

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imekua mkombozi kwa wagonjwa wa moyo Afrika Mashariki kufuatia kupungua kwa gharama za matibabu ukilinganisha na ilivyokua hapo awali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mbunge wa jimbo la Dokolo nchini Uganda Bi.Cecilia Barbara alipotembelea taasisi hiyo ili kuona na kujifunza jinsi Serikali ya Tanzania inavyotoa huduma za Afya kwa wananchi wake .

Bi.Cecilia amesema taasisi hii ni msaada mkubwa kwa Afrika Mashariki kwasababu itasaidia kupunguza idadi ya wagonjwa wa moyo wanaopelekwa  nchini India au Afrika Kusini kwa matibabu kama ilivyo awali baadala yake watatibiwa Tanzania au nchini kwao.

“Tunahitaji kubadilishana mawazo kama wana Afrika Mashariki, kwasababu kwa kuja hapa tumegundua tunavifaa na uwezo wa kupunguza gharama za matibabu ya moyo“ Alisema Bi.Cecilia.

Bi Cecilia amesema kutokana na ubora huduma zinazotolewa na taasisi hii tangu kuanzishwa kwake serikali ya Uganda imekubali kuja kutembelea Tanzania ili kujifunza na kuanzisha mradi kama huu.

“Hatukujua kama Tanzania kuna mradi mkubwa kama huu na unaofanya kazi nzuri lakini kwa kuja tumejua na tunategemea kuanzisha mradi kama huu japo itatuchukua muda kufikia hatua iliyofikiwa na Tanzania”aliongeza Bi.Cecilia .

Naye Afisa Mwandamizi Kitengo cha Utafiti wa Bunge la Uganda Mhe. Jonathan Enamu amesema kuwa amejifunza mengi kwenye ziara hii na ameona ni jinsi gani gharama za matibabu zimepungua kwa wagonjwa wa moyo. “Nimejifunza mengi, ikiwemo jinsi ya kupunguza gharama za matibabu na namna bima za afya zinavyoweza kutumika katika matibabu“ alisema Bw. Enamu.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi amesema kuwa , wanatoa huduma kwa watu wote kuanzia daraja la chini na watu kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Uganda,comoro,Yemen na Kenya.

Prof.Janabi amesema kuwa taasisi hiyo imefanikiwa kutumia shilingi bilioni 1.65 badala ya shilingi bilioni 4.72 ambayo ni sawa na kupunguza takribani asilimia 65 ya gharama za matibabu ya magonjwa ya moyo nchini kama wangewapeleka India kwa matibabu

Prof. Janabi alifafanua kuwa kwa mgonjwa mmoja wa maradhi ya moyo anatibiwa kwa shilingi milioni 35-40 tofauti na nchini India ambapo mgonjwa mmoja anatumia shilingi milioni 120.

Aidha Profesa Janabi ameishukuru Serikali kwa kuipa ushirikiano taasisi hiyo kwani kwa mwaka huu wa fedha Taasisi imepokea asilimia 100 ya bajeti itakayosaidia kuendesha shughuli zao kwa kiwango cha kuridhisha.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na Mbunge wa ilala Mhe. Azzan Mussa Zungu (MB) amesema kuwa wamewapeleka wageni hao kwenye taasisi ya moyo ili waweze kujifunza na kuona ni jinsi gani Tanzania imefanikiwa kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa wa moyo

“wameona namna sisi Tanzania tulivyopunguza gharama kutoka kuwapeleka watu 300 kwa mwaka nje kwa matibabu ya moyo mpaka sasa watu wanne tu, ambao tunawapeleka si kwa sababu hatuna uwezo bali ni kwa sababu ya vifaa havijakidhi “ alisema Mhe.Zungu. 

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ilianzishwa rasmi mwaka 2014 inashughulika na utoaji wa matibabu kwa wagonjwa wa moyo, kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa udaktari,ufamasia na uuguzi. Pia taasisi hii inashirikiana na nchi nyingine duniani kwa kubadilishana maarifa,uzoefu na kufanya mafunzo mbalimbali.                               

Milioni 20 za Biko zaenda Morogoro, Lohai naye avuta mkwanja wake

$
0
0
DROO ya 22 ya waendeshaji wa mchezo wa kubahatisha wa Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku, imefanyika leo jijini Dar es Salaam, huku mkazi wa Morogoro, Elizabeth Damian akifanikiwa kutangazwa mshindi wa Sh Milioni 20 zinazotolewa na bahati nasibu hiyo.

Mwanadada huyo kutoka mkoani Morogoro, alitangazwa mshindi katika droo iliyochezeshwa na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja kwa kushirikiana na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.

Akizungumza katika droo hiyo, Kajala aliwataka Watanzania kuendelea kucheza Biko ili wajiweke katika nafasi nzuri ya kuvuna mamilioni yanayotolewa na Biko tangu kuanzishwa kwake, huku hadi sasa kwa miezi miwili ya Mei na Juni, zaidi ya Sh Bilioni moja zikienda kwa washindi.

Alisema fursa inayotolewa na Biko ni nzuri kwa uchumi wa Watanzania kwa kuhakikisha kwamba wanacheza Biko mara nyingi zaidi ili wajiwekee mazingira mazuri ya kushinda zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, sambamba dau nono la Sh Milioni 20 linalotoka kila Jumatano na Jumapili, kianzio cha kucheza kikiwa Sh 1000 na kuendelea, huku namba ya kampuni ya Biko ikiwa ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456.

“Tangu Biko ianze kuchezeshwa Tanzania imekuwa ikitoa nafasi kubwa ya Watanzania kuvuna mamilioni, hivyo nawashauri Watanzania wenzangu kujitokeza kwa wingi kucheza Biko ili nao waweze kuvuna fedha zinazotolewa Biko kwa zawadi za papo kwa hapo pamoja na zile wiki ambazo ndio kubwa zaidi, nikiamini kuwa endapo mtu anafanikiwa kuzipata, naamini atapiga hatua kubwa kiuchumi,” Alisema Kajala.

Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid, alisema Biko ni mchezo rahisi na halali unaofuata sheria zote, hivyo wanaamini Watanzania wataendelea kutumia fursa za kucheza mchezo huo wa kubahatisha wa Biko.
 
Bodi yetu imekuwa ikihudhuria droo zote za Biko na leo amepatikana mkazi wa Morogoro anayejulikana kwa jina la Elizabeth Damian, hivyo tunampongeza kwa ushindi wake pamoja na kuwahakikishia usalama mkubwa juu ya mchezo huu,” Alisema.

Katika hatua nyingine, mshindi wa Sh Milioni 20 wa droo ya 21 kutoka mkoani Tanga, Yassin Lohai, leo amekabidhiwa fedha zake, huku akiwashukuru Biko na kuahidi kuwa atazitumia vizuri fedha zake katika hali ya kuziingiza katika harakati za kumletea maendeleo makubwa.

“Nashukuru Mungu kwa kukabidhiwa fedha zangu Sh Milioni 20 kutoka Biko, hivyo nawakumbusha Watanzania wenzangu kuwa mchezo huu ni kweli washindi wanapewa zawadi zao haraka, jambo linaloweza kutusaidia kutukwamua kiuchumi,” Alisema Lohai na kuwataka Watanzania waendelee kucheza Biko.

Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven alisema kuwa Biko unazidi kuchanja mbuga kwasababu washindi wengi wa papo kwa hapo wamekuwa wakipatikana sambamba na wale wanaoibuka na mamilioni 20 wanaoshinda na kukabidhiwa fedha zao haraka kwa ajili ya kuwapatia mwangaza wa kiuchumi.

Kwa miezi miwili ya Mei na Juni, washindi wa Biko wameshinda na kukabidhiwa fedha zao zaidi ya Sh Bilioni moja, jambo linalotafsiriwa kuwa ni sehemu ya kuwakwamua Watanzania wanaoitumia fursa ya uwapo wa mchezo wa kubahatisha wa Biko unaochezwa kwa njia ya ujumbe wa maandishi kwa kufanyaa miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money.
Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko, Yassin Lohai akipiga picha ya shangwe baada ya kukabidhiwa fedha zake katika tawi la Madaraka la NMB jijini Tanga leo mchana. Lohai alikabidhiwa na Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven hayupo pichani.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kulia akimkabidhi Sh Milioni 20 mshindi wa Tanga, Yassin Lohai baada ya kushinda donge nono la Biko Jumapili iliyopita. Kushoto ni Afisa wa NMB, Tawi la Madaraka, jijini Tanga, akishuhudia makabidhiano hayo kwa mshindi wa Biko mkoani Tanga.
Balozi wa Biko Kajala Masanja, kulia akisalimiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid, katika droo ya kumtafuta mshindi wa Milioni 20 wa droo ya 22, ambapo Elizabeth Damian alitangazwa mshindi leo asubuhi.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AMRITHI MAMA SALMA KIKWETE ULEZI WA TANZANIA GIRL GUIDES

$
0
0
Na Abraham Ntambara. 

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wasichana ambo ni wanachama wa chama cha Tanzania Girl Guides Association (TGGA) kuzingatia mafunzo wanayopatiwa kwa ajili ya maisha yao ya baadaye. 

 Kauli hiyo aliitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akikabidhiwa kijiti cha kuwa mlezi wa chama hicho kutoka kwa Mama Salma Kikwete anayesitaafu nafasi hiyo aliyoihudumu kwa zaidi ya miaka 12.

 “Niwatake tu watoto wangu kutochukulia kwa mzaha mafunzo mnayopatiwa kwani ni tija kwa maendeleo ya Taifa,” alisema Makamu wa Rais. 
Aidha aliwaahidi wanachama kutowaangusha katika kutekeleza majukumu ya kukilea chama hicho ambapo alimpongeza Mama Salma Kikwete kwa kuweza kukiongoza vizuri kwa mafanikio makubwa licha ya kuwa na majukumu mengine.
Aliyekuwa Mlezi wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Mama Salma Kikwete (kushoto) akimkabidhi  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan bendera ikiwa ni ishara ya kumpatia ulezi wa chama hicho katika hafla iliyofanyika, kwenye viwanja vya Jumba la Makumbusho Dar es Salaam leo
Mama salma akimkabidhi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mpango mkakati wa TGGA
Samia Suluhu Hasan akimkabidhi Mlezi mstaafu wa TGGA zawadi ya saa aliyopewa zawadi na uongozi wa TGGA kwa ajili ya kumbukumbu.

Mama Salma Kikwete akisalimiana na Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi
Salma Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba
Mama Salma Kikwete akisalimiana na Kamishna wa TGGA

Samia akiangalia kazi mbalimbali zinazofanywa na Girl Guides

VIJUSO VYA MAGAZETI YA ALHAMIS LEO JULAI 13,2017

WAZIRI MKUU AKABIDHI PIKIPIKI 49 KWA VIJANA WA RUANGWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekabidhi pikipiki 49 kwa vijana wa wilaya ya Ruangwa ili waweze kujiajiri na kujikwamua kiuchumi.

Amekabidhi pikipiki hizo jana (Jumatano, Julai 12, 2017), baada ya kumaliza kuhutubia wananchi kwenye uwanja wa shule ya msingi Likangara.

Baada ya kukabidhi pikipiki hizo, Waziri Mkuu amewataka vijana hao kuhakikisha wanakuwa waaminifu kwa kufanya kazi kwa bidii ili pikipiki hizo ziwe na tija.

Amesema vijana wanaoendesha pikipiki maarufu bodaboda wanatakiwa kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali. “Ukiendesha pikipiki lazima uhakikishe kwamba una leseni, bima, vaa kofia ngumu wewe na abiria wako na marufuku kubeba abiria zaidi ya mmoja.”

Wakizungumza baada ya kukabidhiwa pikipiki hizo vijana hao ambao walikuwa wakiendesha pikipiki za watu ambazo hazina tija, wameahidi kufanya kazi kwa bidii. Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika zahanati ya Nandagala na kuridhishwa maendeleo yake.

Amesema kukamilika kwa majengo hayo kutarahisisha upatikanaji wa haraka wa huduma za afya kwa mama na mtoto. Pia itawapunguzia kutembea umbali mrefu kwenda kufuata huduma hizo katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa.

MASAUNI APOKEA MSAADA WA VIFAA VYA TEHAMA KWA AJILI YA CHUO CHA UHAMIAJI CHA KIKANDA (TRITA), MJINI MOSHI

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia), Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala (kulia) wakipokea moja ya kompyuta kutoka kwa Balozi wa China nchini, Dk. LU Youqing (wapili kushoto) katika hafla ya makabidhiano ya vifaa msaada vya Tehama vyenye thamani ya shilingi milioni 33 vilivyotolewa na Ubalozi huo kwaajili ya kukisaidia Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) kilichopo mjini Moshi. Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho, Maurice Kitinusa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia-waliosimama) akishuhudia Balozi wa China nchini, Dk. LU Youqing (kushoto) na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala walipokua wakitia saini Mkataba wa Makabidhiano wa msaada wa vifaa vya Tehama vilivyotolewa na Serikali ya China kwa ajili ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA), kilichopo mjini Moshi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala (kushoto), Balozi wa China nchini, Dk. LU Youqing (aliyevaa saa) pamoja na maafisa wengine wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Tehama, Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA), Mkaguzi wa Uhamiaji, Zawadi Chazuka alipokua anawaonyesha kifaa cha kuangalia alama au maandishi ambayo hayawezi onekana kwa macho ya kawaida mpaka kifaa hicho kitumike. Ubalozi wa China ulitoa msaada wa vifaa vya Tehama vyenye thamani ya shilingi milioni 33 kwa ajili ya matumizi ya chuo hicho kilichopo mjini Moshi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati waliokaa), Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala (watatu kushoto), Balozi wa China nchini, Dk. LU Youqing (watatu kulia), Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mtafungwa wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa Uhamiaji na Ujumbe kutoka China mara baada ya Balozi wa China kutoa msaada wa vifaa vya Tehama kwa ajili ya matumizi ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) kilichopo mjini Moshi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akipokelewa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala, wakati kiongozi huyo alipokua anawasili Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA), mjini Moshi kwa ajili ya kukabidhiwa vifaa vya Tehama vilivyotolewa na Ubalozi wa China nchini kwa ajili ya matumizi ya chuo hicho.


Taarifa ya Msiba Wa Mtanzania Prof Henslay Kabisama Nchini Marekani

$
0
0
WaTanzania nchini Marekani wanaomboleza msiba wa Profesa Henslay Kabisama aliyefariki huko California mwishoni mwa mwezi June
Mjane wa Marehemu pamoja na wadau kadhaa waliungana na Mubelwa Bandio katika kipindi cha NJE-NDANI kuongelea mipango ya mazishi ilipofikia sasa.

Unaweza kushiriki kusaidia gharama za kuusafirisha mwili kupitia akaunti HII ya GoFundME
 
Karibu uwasikilize

UBA takes its Read Africa Initiative to Ghana

$
0
0


On Tuesday July 4th, 2017, The UBA Foundation, the Corporate Social Responsibility arm of the United Bank for Africa (UBA) Plc, continued on its quest to educate and empower African youths as it visited the Accra High School in Ghana.

UBA Foundation Read Africa Initiative was launched in 2011 and has been changing the lives of African students across the continent for six years. The Project is aimed at encouraging children to improve their vocabulary and communication skills through reading. Through its Read Africa initiative, the UBA Foundation is helping rekindle the dwindling reading culture amongst African youths as they pursue their education.

Over a hundred thousand books and educational materials have been donated to various schools across Africa as UBA Foundation continues to traverse the continent, contributing positively to the development of African youths.

The Accra High school assembly hall was packed with over 500 energetic and enthusiastic high school students who were already in reading mode as they prepare for their exams next week. They were eager to talk about their own ambitions and to read passages from The Fishermen.

Bola Atta, Acting CEO of the UBA Foundation, told the children that the Foundation was eager to give back to society and to contribute to creating dynamic educational platforms for future generations on the continent. She encouraged the students to read voraciously saying:‘the pursuit of knowledge should be a lifelong activity that starts at a very young age. You should read all types of books so that you can explore and shape your own narrative.’

Abiola Bawuah, the CEO of UBA Ghana who was also present, advised the students to pay a lot of attention to studying. ‘Don’t spend all your time glued to your mobile phones. Spare some moments for reading also’ said Bawuah.

The Assistant Head master of Accra High School, Michael Addo thanked the UBA Foundation for coming to their Aid.

United Bank for Africa (UBA)Plc, Africa's global bank, is committed to being a socially responsible company and role model for all businesses in Africa. UBA understands that there is a need for a social contract between the bank, the communities in which it operates, and its people. To this end, in 2006, UBA became the first bank in Nigeria to institute a foundation, the UBA Foundation. As the Corporate Social Responsibility arm of the UBA Group, UBA Foundation is committed to the socio-economic betterment of communities across the African continent focusing on development in the areas of Environment, Education, Economic Empowerment and Special Projects.

'CASTLE LITE UNLOCKS' YASISITIZA WASHIRIKI KUJIANDIKISHA KWA WINGI KWA AJILI YA TAMASHA LA MUZIKI LINALISUBIRIWA KWA HAMU NCHINI

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

KAMPENI ya Castle lite unlocks inahamasisha washiriki kuhudhuria kwa wingi katika tamasha kubwa la muziki ambalo halijawahi kushuhudiwa Tanzania.

Wito huo umetolewa na Meneja wa mahusiano ya wateja wa kampuni ya Tanzania Brewaries Limited (TBL) kwa Afrika Mashariki, George kavishe katika taarika yake kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo, ambapo alitumia fursa kuwataja wadhamini na wabia wa kampeni hiyo. 

“Kwa mara nyingine tena tunawakumbusha wapenzi wa muziki, hasa walioko katika jiji la Dar es salaam na maeneo ya karibu kujiandikisha kwa wingi kwani tukio hilo la aina yake linakaribia” alisema Kavishe, akiongeza kuwa washiriki watapata fursa adimu sana ya kufurahia bonanza lamuziki litakalo tayarishwa na brand ya kipekee ya bia, Castle Lite hivi karibuni.

Akitangaza washirika, kavishe alipongeza mchango wao, akisema kwamba wametekeleza jukumu kubwa katika mafanikio ambayo kampeni hiyo imefikia mpaka sasa.

Alitaja wadhamini kama vile Tigo Tanzania (mshirika  rasmi wa mawasiliano ya Simu), Clauds FM (Mshirika kama chombo cha habari), CFAO Motors  (Mshirika katika usafirishaji), Marlborona Serena Hotel Dar es Salaam (Mshirika katika malazi).

“Tunawashukuru sana washirika wetu kwa kukamilisha juhudi zetu katika kuelekea kwenye tamasha la nne la muzikiambalo linahakika kuwa litakuwa ni chanzo cha mabadiliko makubwa katika tasnia ya muziki wa wandani”, Kavishe amesema kuhusu Bonanza kubwa ambalo limepangwa kufanyika tarehe 22 mwezihuu wa julai katika ukumbi wa Leader’s Club hapa Dar es salaam. 

Kwa mujibu wa Kavishe, kampeni ya Castle Lite Unlocks ni harakati kubwa ambapo bia ya Castle  Lite  imekuwa  inabadilisha  mwelekeo  wa  mchezo  kwa  kuleta wasanii wakubwa na mashuhuri wa imataifa kuja kufurahia pwani za Afrika kwa kutoa burudani ya kipekee ya ‘Extra Cold’ katika tamasha kubwa la‘Castle Lite Unlocks’

“Tamasha la mwaka huu litakuwa na neema ya kutembelewa na wanamuziki maarufu na wakongwe wa Hip Hop, huku wanaochipukia wakiwa wanasindikizwa na wanamuziki maarufu wanaotikisa bongo flava Tanzania wakiongozwana Diamond Platnumz” alisema Kavishe, akiwataja wasanii wengine watakao kuwepo kuwa ni, Casper Nyovest Kutoka Afrika kusini, Vanessa Mdee, kundi la Weusi  na Navy Kenzo ambao ni wa hapa hapa nchini Tanzania.

Kavishe alishauri wapenzi wamuziki kununua tiketi kupitia Tigo Pesa namba 0674 444 444 na kwenda kuzichukua katika Tigo Shop yoyote hapa Dar es salaam. Mitandao  mingine ya simuinaweza kununua tiketi kwa kuchagua “mitandaomingine” katika menyu ya simu pesa zao na kununua kwa kupitia namba hiyo hiyo ya malipo. 

“Manunuzi ya tiketiyanaenda kwa kasi sana kwa hiyo ni na wasisitiza watu wote kununua tiketi zao sasa kwa sababu hii ni tukio ambalo haupaswi kukosa. Castle Lite ni bidhaa bora ambayo inakuletea uzoefu wa hali ya juu. 

Watu wategemee burudani ambayo haijawahi kutokea hapa Tanzania, tumeandaa tamasha hili kwa hali ya juu, kiwango cha usalamani cha hali ya juu na mpangilio wakipekee wa ukumbi wa tamasha ambao utawaacha watu wakiwa katika hali ya mshangao” alisema Kavishe.

“Gharama ya tiketi ni Tshs 20,000 akini  watejawatakaol ipa kwa Tigo  Pesa watafurahia punguzo la bei la Tshs 5,000, hivyo watalipa Tshs 15,000 kwatiketi moja,” alisema Kavishe, huku akiongeza kwamba wateja wataweza kujipatia tiketi zao kutoka katika maduka ya huduma kwa wateja ya Tigo (Tigo shop) yaliyopo karibu nao. 

Alizitaja sehemu ambalko wanaweza kwenda kuchukua tiketi zao kuwa ni pamoja na: Mlimani City-Mlimani City Mall, Makumbusho (mkabala na), Palm Beach Residence-Ocean Road, Nkurumah- Nyerere Road- Gold Star, Buguruni-Rozana, Quality Center-Quality Center Mall, JM Wall- Hotel Harbor View, Masaki- Haille Selassie Road, Kariakoo-Msimabazi/Pemba Street, Manzese Darajani, Kigamboni-Ferry, Tegeta-Kibo Complex na Mbagala- Oil Com Gas Station.

Kwa upande mwingine, Kavishe aliongeza kwamba wateja pia wanaweza kupata tiketi kwa pesa taslimu Sh 20,000/= katika maeneo yafuatayo, Clouds Fm-Mikocheni, Funzone Shamo Tower-Mbezi Beach, Leader’s Club-Kinondoni na duka la Bron to Shine-Mwenge.

Kampeni ya Castle lite Unlocks itahudhuriwa na washindi 22 kutoka Zambia na 19 kutoka Tanzania ambao wamejishindia tiketi za “kiwango cha VIP” ambayo itawapatia fursa ya kusafirishwa kwa ndege mpaka Jijini Dar es salaam, kukaa katika hotel maarufu kwa siku mbili, kufurahia burudani ya hali ya juu, kupelekwa na kurudishwa kutoka katika tamasha wakati huo huo ukiwa unapokea huduma za VIP kwa wakati wote. 
 Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Idara ya Kuunganisha Wateja Afrika Mashariki, George Kavishe (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu kuhamasisha washiriki kuhudhuria kwa wingi katika tamasha kubwa la muziki ambalo halijawahi kushuhudiwa Tanzania. Kutoka kushoto ni Mratibu wa Malipo wa kwa Tigo Pesa, Newton David na Meneja Masoko wa TBLKitengo cha Bia Laini Afrika Mashariki, Amou Majok.


Mratibu wa Malipo wa kwa Tigo Pesa, Newton David (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Ofisa Masoko kutoka Kampuni ya CFAO Motors Ltd, Angelina Ndege akizungumza katika mkutano huo kuhusu kudhamini tamasha hilo.
Meza kuu.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wasanii wa hapa nchini watakaotoa burudani katika tamasha hilo. Kutoka kulia ni Vanessa Mdee, Nahreel Mkono na Aika Marealle.




Barclays Bank launches a bonus savings account campaign

$
0
0




Double your deposit and earn double interest up 10% with Bonus Savings Account .

Tanzanian’s can now earn up to 10% interest when they double their savings with Barclays.

Speaking at the launch, which took place at the bank’s Head Office, Barclays Liability Manager, Innocent Chonya said “After carefully analysing the saving patterns of Tanzanian’s, we found out that many of our customers do not open savings accounts for multiple reasons, one being low interest rates.

Following our research, we decided to develop an offering that will help address our customers concerns. Customers who currently have a Bonus Savings account need to double their existing balances to qualify to earn double the interest that they were originally receiving.

For new customers, they simply need to visit any of our branches, open a bonus savings account, and make a deposit of their choosing and they will qualify to receive double the interest up to 10%”

Barclays Bonus Savings account provides customers the opportunity of earning the highest interest rate in the country for a saving product that is not a fixed deposit product. This savings account allows you to earn a bonus interest payment in addition to the ordinary interest if you do not withdraw more than once within a given quarter.

He continued, “At Barclays, we believe in delivering products that meet the need of our customers and the ever changing economic landscape of the country. Our customers are why we exist as a bank, and it’s therefore our duty to ensure that we offer them with solutions that help them achieve their saving goals. Let your money start working for you, open a Bonus Savings account with Barclays today!.”

 Barclays bank Tanzania Marketing and Communications Manager, Joe Bendera (left) and banks Liability Product Manager, Innocent Chonya launch the bank's bonus savings account campaign in Dar es Salaam yesterday to enable customers to earn a bonus up to 10% interest on their savings.  
 Barclays bank Tanzania Liability Product Manager, Innocent Chonya (centre), and banks marketing and Communications Manager, Joe Bendera (on his left) during a media conference to launch the Barclays bonus savings account campaign in Dar es Salaam yesterday.


Jamii Media, CIPESA Wakutanisha Wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, ICT

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Mello (wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa kongamano la wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania, lililoandaliwa na Kampuni ya Jamii Media ya Tanzania wamiliki wa mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na Kampuni ya CIPESA ya nchini Uganda. Wengine ni Mkurugenzi wa CIPESA, Dk. Wairagala Wakabi (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Jamii Media, Mbaraka Islam (kushoto). Kongamano hilo lilifanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Mello (wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa kongamano la wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania, lililoandaliwa na Kampuni ya Jamii Media ya Tanzania wamiliki wa mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na Kampuni ya CIPESA ya nchini Uganda. Wengine ni Mkurugenzi wa CIPESA, Dk. Wairagala Wakabi (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Jamii Media, Mbaraka Islam (kushoto). Kongamano hilo lilifanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mmoja wa washiriki katika kongamano hilo, Joseph Ngwegwe-mdau wa ICT akijadili jambo katika mjadala wa wadau wa ICT, wengine ni Robert Madziva- Maxcom Africa (kulia) na Chambi Chachage wakiwa katika mjadala huo. Mmoja wa washiriki katika kongamano hilo, Catherinerose Barretto (wa kwanza kulia) akizungumza katika mjadala na wadau wa ICT kwenye kongamano hilo. Kutoka kushoto ni Chambi Chachage-Udadisi Blog, Joseph Ngwegwe-mdau wa ICT pamoja na Robert Madziva- Maxcom Africa wakiwa katika mjadala huo. Meneja Mkuu wa Kampuni ya Jamii Media, Asha Abinallah akizungumza na washiriki wa kongamano la wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania.

 KAMPUNI ya Jamii Media ya Tanzania wamiliki wa mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na Kampuni ya CIPESA ya nchini Uganda imefanya kongamano la kuwakutanisha wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania ikiwa ni kujadili masuala mbalimbali ya huduma za habari na mawasiliano pamoja na kuangalia namna ya kulinda usiri wa taarifa za wateja wanaotumia huduma hizo. 

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kongamano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Mello alisema kongamano hilo limekuwa na matokeo chana baada ya wadau kujadili masuala mbalimbali ya ICT lengo likiwa kuboresha zaidi huduma hiyo na usalama kwa watumiaji. Alisema wadau wengi kwenye kongamano hilo wameunga mkono hatua ya uwekaji wa sheria za kusimamia huduma nzima ya ICT lakini wakashauri ufanywe kwa kutoa fursa za maendeleo na si kuminya ubunifu wala uhuru na usiri wa watumiaji wa huduma za ICT. 

Alisema wadau wengi katika kongamano hilo walihoji kitendo cha Sheria ya Makosa ya Mtandao (The Cyber Crimes Act, 2015) kuanza kutumika bila ya uwepo wa kanuni jambo ambalo limewapa ugumu hata watekelezaji na wasimamizi wa sheria husika. Mkurugenzi huyo aliongeza Jamii Media itaendelea kusaidia kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa huduma za mawasiliano wakiwemo bloggers ili kuona wanakuwa na uelewa na matumizi mazuri ya mitandao yao kupunguza mkanganyiko kwa wanufaika.   Maria Sarungi (kushoto) Mkurugenzi Uzalishaji kutoka 'Compass Communications Ltd' akiongoza majadiliano kwenye kongamano hilo. Mmoja wa washiriki katika kongamano hilo, Catherinerose Barretto (wa kwanza kulia) akizungumza katika mjadala na wadau wa ICT kwenye kongamano hilo. Kushoto ni Robert Madziva- Maxcom Africa wakifuatilia mjadala huo.
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images