Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

HAKUNA MGONJWA ATAKAYEKOSA DAWA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba na kwamba hakuna mgonjwa atakayekwenda kutibiwa katika hospitali, vituo vya afya au zahanati bila ya kupatiwa dawa.

Ameyasema hayo jana jioni (Jumatatu, Julai 10, 2017), wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Liwale katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Michezo wa Wilaya.

Waziri Mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa katika ziara yake ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, alisema Serikali haitaki kusikia wananchi wanakwenda hospitali, Vituo vya afya au zahanati na kukosa dawa.

Alisema moja kati ya ajenda muhimu ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake, ambapo kila mwezi halmashauri zote nchini zinapelekewa fedha za ununuzi wa dawa.

“Serikali hii ya Rais Dkt. John Magufuli inatoa fedha za kununulia dawa kila mwezi katika halmashauri zote nchini. Sasa kama hapa Liwale kuna malalamiko ya wananchi kukosa dawa katika hospitali yetu, Mkuu wa Wilaya kafuatilie huko Halmashauri ili kujua wanapeleka wapi fedha za dawa.”

Katika bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ya mwaka wa fedha 2017/2018 jumla ya shilingi bilioni 236 zimetengwa kwenye ununuzi wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi alisema hali ya upatikanaji wa dawa muhimu kwa kipindi cha mwaka 2016/2017 iliongezeka kwa asilimia 50 ikilinganishwa na ile ya mwaka 2015/2016.

Bw. Zambi alisema katika kipindi cha kuanzia Julai mwaka 2016 hadi Februari 2017 mkoa wa Lindi ulipokea sh milioni 538 kwa ajili ya ununuzi wa dawa kupitia Bohari ya Dawa (MSD).

“Hospitali ya mkoa ilipokea sh. milioni 195,328,186 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na pia ilitumia sh. Milioni 127,171,700 toka fedha za uchangiaji kwa ununuzi wa dawa.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji wa Halmashauri kwenda vijijini na kuwaelimisha wananchi umuhimu wa utunzaji wa mazingira ili kuliepusha Taifa kugeuka jangwa.

Pia amewaagiza Maofisa Kilimo wote kuhakikisha wanaacha kushinda maofisini na badala yake waende mashambani kwa ajili ya kuwaelimisha wakulima namna bora ya kulima kwa kufuata njia za kisasa ili kupata tija.

Kila ofisa kilimo awe na shamba lake ambalo litatumika kama darasa kwa wananchi

Baalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia alipotembelea Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Saba Saba jana

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Saud Arabia, HE Hemed Mgaza, wa pili kutoka kulia, akiwa na mfanyabiashara na Mkurugenzi wa Kampuni ya MIT Group of Companies kutoka Saud Arabia, Sameer Saleh Ahmed, wa pili kutoka kushoto wakiwa ndani ya banda la Kampuni ya Chai Bora kwenye maonyesho ya Kimataifa ya Sabasaba nchini Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mh Hemed Mgaza, akipata maelekezo yanayohusu utalii wa Tanzania kutoka kwa Aloyce Songay, Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni Binafsi ya Hifadhi Mazingira Karatu (HIMAKA).
Balozi wa Tanzania nchini Saud Arabia, HE Hemed Mgaza, akiwa kwenye banda la Mamlaka ya Korosho Tanzania katika Maonyesho ya Kimataifa ya Sabasaba nchini Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Saud Arabia, HE Hemed Mgaza, akiwa kwenye banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika Maonyesho ya Kimataifa ya Sabasaba nchini Tanzania.

Article 10

$
0
0


Targeted Participants:
This intermediate-levelpractical-oriented short course training is designed for mid-level and senior officials from private and public sectors, Marketing, Business, Banking, Trade Information and Public Relation officers/Managers in Regions and Districts and all those who wants to learn or are engaged in various types of  Protocol, Event Organization and Management and Public Relations related activities.  
 
Facilitators and Expected output:
These intensive practical-oriented training will be facilitated by Madam, ROSEMARY MWAKITWANGE and Career Diplomats, and will be useful to your agency and organization through staffs who will attend, whereby Participants will be equipped with tactics, analytical and practical skills 
 
DATE:   26 – 28 July, 2017 (Three Days)   VENUE: NCT Conference – POSTA CITY CENTRE, Dar es Salaam
   
TIME: 16:00 – 20:30 EVENING (4.5hrs P/Day)  AWARD: DETAILED CERTIFICATE
  
STUDY MODULES:

  1. Introduction to protocol and Event Organization/Management
  2. Basics of Event’ concept development and PR.
  3. Strategic event Planning, Execution and Evaluation
  4. Risk and Logistics Management
  5. Role of event Organizer/ manager and Protocol officer in organizing and during event
  6. Diplomatic and Business etiquette during event
  7. Sitting arrangement and planning table seating
       And Coaching,  Discussion, simulations and Practical issues

 
FEES:  280,000/=  which also covers Bites, Refreshments and Stationeries andCertificate
   
Payment A/C: 2361 000 1369 NMBBANK     A/C NAME: Economic Diplomacy – Training 
For more details, Invitation letters and in-house Training:  Please Contact Directorate of Training and Operations:
   
Mobile:+255 713 667 303,  +255 763 65 75 87        E-Mails:info@economicdiplomacy.ac.tz,    lucassoona@yahoo.com
   
Website:www.economicdiplomacy.ac.tz      NOTE: In-house training fee is Tsh.1,500,000/= for 10 – 15 participants

IGP SIMON SIRRO AFANYA ZIARA KISIWANI PEMBA

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro (aliyesimama), akizungumza na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa kaskazini na Kusini Pemba (hawapo pichani) leo wakati alipofanya ziara ya kikazi katika Kisiwa hicho, kulia ni Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Athuman, IGP Sirro yupo kisiwani humo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na watendaji wa Jeshi hilo.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Athuman (aliyesimama), wakati akitoa neno Mbele ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Kaskazini na Kusini Pemba, IGP Sirro yupo kisiwani humo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na watendaji wa Jeshi hilo.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini  IGP Simon Sirro, akipokea salamu ya heshima ya kijeshi kutoka kwa Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakati akiwasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi mkoa wa Kusini Pemba leo, IGP Sirro yupo kisiwani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na watendaji wa Jeshi hilo.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini  IGP Simon Sirro, akizungumza na Askari wa kikosi cha kutumia ghasi (FFU), Mara baada ya kupokea salamu ya heshima ya kijeshi,  IGP Sirro yupo kisiwani Pemba kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na watendaji wa Jeshi hilo huku akiwataka askari kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha suala la uhalifu na wahalifu linadhibitiwa.
 Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa kaskazini na kusini Pemba, wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, wakati akitoa neno kwenye kikao kazi Mara baada ya kuwasili kisiwani humo, IGP Sirro yupo kisiwani Pemba kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na watendaji wa Jeshi hilo.
( Picha zote na Demetrius Njimbwi - Jeshi la Polisi)

MAGEREZA KUPANUA KIWANDA CHAKE CHA VIATU CHA KARANGA MJINI MOSHI

$
0
0
Jeshi la Magereza nchini limeanza kutekeleza mpango wake wa kupanua shughuli za uzalishaji wa kiwanda cha Viatu cha Karanga  kilichopo mjini Moshi  mkoani Kilimanjaro  sambamba na kujenga Kiwanda Kipya cha Viatu  katika eneo hilo hilo ili kupanua huduma zake kwa wananchi na hivyo kukidhi mahitaji ya soko la sasa.

Hatua hii ni moja ya kati ya Mikakati ya Jeshi la Magereza nchini Tanzania linaloongozwa na Kamishna Jenerali Dk. Juma Malewa kuhakikisha fursa  zilizopo na wataalamu waliopo ndani ya Jeshi la Magereza nchini zinatumika na wanatumika  vizuri kwa manufaa ya watanzania wote sambamba na Jeshi hilo kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha Tanzania inafikia uchumi wa viwanda.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dr. Juma Malewa anasema baada ya upanuzi huo ambao umeanza kufanyika mapema mwezi Juni mwaka huu kiwanda hicho kitakuwa na  uwezo wa kuzalisha  jozi 400 kwa siku na hivyo kuongeza kasi ya upatikanaji wa viatu vinavyotengenezwa na Jeshi la Magereza kwa ubora kwa hali ya juu na kwa kutumia mitambo ama mashine  za kisasa.

Dk. Malewa anasema awali  kiwanda  hicho kilichopo Gereza la Karanga mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro kutokana na kutumia teknolojia ya zamani   kilikuwa na  uwezo wa kuzalisha jozi 150 kwa siku kiwango ambacho ni kidogo ukilinganisha na soko la sasa.
Anasema tayari Jeshi la Magereza limeingia Ubia na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF   kwa lengo la kupanua  shughuli za uzalishaji  wa Kiwanda  cha Viatu cha Karanga kilichopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro sambamba na kujenga  kiwanda  kipya cha viatu katika eneo hilo hilo. 

Dk. Malewa anasema  katika kutekeleza azma yake ya ujenzi wa Kiwanda kipya  cha Viatu tayari zimetengwa ekari 20 kwa ajili ya kiwanda hicho katika eneo hilo la Karanga mjini Moshi na kwamba eneo hilo hilo litakalotumika kujenga Kiwanda  cha Viatu pia litatumika kujenga Kiwanda cha Soli na Kiwanda cha kuchakata Ngozi na kwamba Kiwanda hicho kinategemewa kukamilika mapema Julai mwaka 2018.

Katika kuinua hali ya uchumi kwa watanzania “Uzalishaji huu utaongeza ajira kwa watanzania,  lakini pia utaongeza soko la uuzaji wa viatu hivi kwa kuwa tunategemea kutengeneza viatu kwa wingi kwa ajili ya Majeshi yetu yote ya Tanzania pamoja na viatu kwa ajili ya shule za Sekondari za Serikali kwa hiyo hii ni fursa nzuri na kubwa katika Jeshi letu la Magereza”. anasema Dk. Malewa.

 Dk. Malewa anasisitiza kuwa sambamba na upanuzi wa Kiwanda  kilichopo  Gereza la Karanga  mjini Moshi  pia Jeshi la Magereza  limeanza upanuzi wa Viwanda vya Samani vilivyopo Ukonga, Arusha na Tabora ili viweze kuongeza uzalishaji wa samani kwa ajili ya matumizi ya ofisi mbalimbali na majumbani.

Katika mwendelezo wa kupanua viwanda vyake ili viweze kuwa na tija kwa taifa na watanzania kwa ujumla kwa sasa Jeshi la Magereza nchini kwa kutumia rasilimali zake lina mpango wa kujenga Kiwanda Kikubwa cha Uzalishaji wa Samani  ambacho kitaweza kuhudumia  watanzania kwa kiwango kikubwa na tayari Serikali  imetenga  fedha  kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda hicho ambacho kitajengwa mkoani Dodoma.

“Kutokana na Serikali kuhamishia Makao Makuu ya Nchi yetu Mkoani Dodoma ni wazi kutakuwa na uhitaji mkubwa wa samani kwa ajili ya matumizi ya ofisi na hata majumbani pia… hivyo tunategemea Jeshi la Magereza litajenga Kiwanda hiki kikubwa cha samani ili kukidhi mahitaji halisi ya samani hizo kwa watanzania wote na taasisi mbalimbali zilizopo mkoani Dodoma ,’’ anasema Dk. Malewa.

Dk. Malewa anasema ili kukidhi mahitaji halisi  samani kwa ajili ya Makao Makuu ya Nchi  yetu  Jeshi la Magereza lina mpango wa kununua vifaa hususani mashine za kisasa  zitakazoweza kuzalisha  samani kwa wingi zaidi na hivyo kutosheleza  mahitaji  ya samani mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa Dk. Malewa nguvu kazi itakayotumika katika uzalishaji kwenye kiwanda hicho itakuwa ya aina mbili ikiwemo wataalamu waliopo ndani ya Jeshi la Magereza na wananchi ambao wataajiriwa kutokana na utaalamu walio nao, hivyo Jeshi la Magereza linatarajia kuongeza fursa za ajira kwa wastani wa ajira 200 hadi 500.

 Katika kuhakikisha Jeshi la Magereza nchini linapanua wigo wa utoaji wa huduma zake kwa taifa  Jeshi la Magereza linategemea  kuingia ubia na GEPF  ili kutekeleza mradi wa upasuaji kokoto utakaofanyika mkoani Dodoma. 
Kwa mujibu wa Dk. Malewa Jeshi la Magereza linategemea kufunga mashine kubwa ya upasuaji wa kokoto ambapo kwa kiasi kikubwa inategemewa kukidhi mahitaji ya kokoto katika shughuli za ujenzi wa nyumba za wananchi hata Mashirika mbalimbali yanayohamia mkoani Dodoma.  

Dk. Malewa anasema, kwa kuwa tayari ujenzi wa nyumba za Taasisi na watu mbalimbali unaendelea  kutekelezwa  mkoani Dodoma, kupitia Mradi wa upasuaji wa Kokoto unaofanyika katika eneo la Msalato  mkoani humo, kokoto hizo zitauzwa kwa watu binafsi yaani wananchi na Serikali pia.

Dk. Malewa anasema Jeshi la Magereza ni Taasisi kubwa ambayo ina fursa nyingi za kiuchumi na endapo zitatumiwa vizuri zinaweza kuwa na mchango mkubwa kwa Taifa hili ambalo linaelekea kwenye uchumi wa viwanda.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira anasema kuwa pamoja na Jeshi la Magereza nchini kutumia wataalamu wake pamoja na wafungwa ambao hufundishwa stadi mbalimbali na kutumika kama nguvu kazi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuthamini na kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazoonyeshwa na Jeshi la Magereza ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa na Jeshi hilo hapa nchini yanatekelezwa kama yalivyokusudiwa.

Kwa upande wake mwananchi mmoja Crispin Aloyce Mkazi wa Ubungo jijini Dar es Salaam anasema yeye ni mtumiaji na mteja mzuri wa viatu vya ngozi vinavyozalishwa na Jeshi la Magereza nchini na amekuwa akinunua viatu hivyo kwenye Duka la Magereza lililopo Mtaa wa Uhindini jijini Dar es salaam, ‘‘Ni kweli viatu vyao ni vizuri na vina ubora wa hali ya juu, ila Magereza wanapaswa kuzalisha kwa wingi viatu vya rangi ya ‘‘brown’’ ambayo watu wengi pia tunaipenda imekuwa ni kawaida mteja unapotaka viatu vya rangi ya ‘brown’ unaambiwa rangi hiyo imeisha… haiwezekani kila siku unakosa rangi hii’’ anasema Bw. Aloyce.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZUNGUMZA NA WAKAZI WA KIJIJI CHA LIKWACHU, WILAYA YA RUANGWA

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Likwachu, Wilaya ya Ruangwa, akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Lindi, Julai 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Wananchi wa kijiji cha Likwachu, Wilaya ya Ruangwa, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipo ongea nao, wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Lindi, Julai 11, 2017.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Likwachu, Wilaya ya Ruangwa, akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Lindi, Julai 11, 2017.

Taasisi ya MO Dewji yatunukiwa tuzo ya ubora ya Superbrand

$
0
0
Taasisi ya MO Dewji Foundation inayojuhusisha na kusaidia jamii katika elimu, afya na maendeleo ya jamii imetunukiwa tuzo ya kimataifa ya ubora inayofahamika kama SuperBrand. Taasisi hiyo inayomilikiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mohammed Entreprises Tanzania Limited, Mohammed Dewji imetunukiwa tuzo hiyo kutokana na juhudi zake za kusaidia jamii kupitia miradi mbalimbali ambayo inaifanya. 

Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez amesema ni heshima kubwa kwa taasisi kupata tuzo hiyo lakini pia itawasaidia kufanikisha miradi mikubwa ambayo wamepanga kuifanya na taasisi kubwa kama ya Bill Gates.

“Kwa niaba ya Taasisi ya MO Dewji na kampuni ya MeTL Group tunashukuru sana kwa tuzo hii na huu ni mwanzo mpya wa safari yetu, kama mnavyojua taasisi yetu ilianzishwa mwaka 2014 na katika kipindi cha miaka miwili tumeanzisha miradi mbalimbali kama MO Entrepreneurs na MO Scholars ikiwa na lengo la kuwasaida vijana na tunafuraha Baraza la SuperBrands limetutambua.

“Tuzo hii inatusaidia katika miradi mikubwa kwa sasa kama taasisi ya Mohammed Dewji tunataka kufanya ushirikiano na taasisi kubwa kama Taasisi ya Bill Gates, kushirikiana na taasisi za Kenya, Uganda, UK, jina la Mohammed Dewji litakuwa la kwanza na SuperBrand litakuwa ya pili,” amesema Barbara. .
Mkurugenzi wa taasisi huru ya Superbrands Ukanda wa Afrika Mashariki, Jawad Jaffer akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez tuzo ya ubora ya SuperBrand.Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo ya ubora ya SuperBrand.
Tuzo ya SuperBrand ambayo Taasisi ya MO Dewji imetunukiwa.

WIZARA YA HABARI YASHAURIWA KUONGOZA MABADILIKO YA UTAMADUNI WA KUTUMIA MUDA KIMKAKATI.

$
0
0
Na Zawadi Msalla-WHUSM.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka  amewataka  watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu  kwa umma ya kuwa na utamaduni wa kutumia muda kimkakati ili kufanya kazi kwa bidii  na kufikia malengo.

Ayasema hayo wakati wa mkutano na watendajin hao  walipomtembelea ofisini kwake wakati wa ziara ya kutembelea mikoa ya kusini mwa Tanzania kwa lengo la kutembelea maeneo mbalimbali yanayojihusisha uhifadhi wa utamaduni usioshikika kama vile mila na desturi za Watanzania.

“Utamaduni wa kutumia muda kimkakati ni muhimu kwa Taifa na mtu binafsi kwa kuwa inasaidia katika kuweka motisha ya kufanya kazi kwa bidii na hivyo kufikia lengo lililokusudiwa” alisema Mhe. Ole Sendeka.
Aidha aliongeza kwa kueleza kuwa falsafa ya mabadiliko ya utamaduni chanya ya ufanyaji kazi ilianza tangu awamu ya kwanza ya uongozi wa Mwl. Nyerere iliyokwenda kwa jina la Uhuru na Kazi na baadaye ikifuatiwa na kazi ni kipimo cha Utu ambapo katika utawala wa awamu hii ya tano inaongozwa na hapa kazi tu lengo ikiwa ni kufanya kazi kwa ajili ya kukuza uchumi wetu.

Mhe. Ole Sendeka anaeleza kuwa dhumuni za falsafa hizo ni kuhakikisha kuwa kila mtu anatimiza wajibu wake wa kutumia muda kimkakati kwa kufanya kazi ili kujenga Taifa bora lenye maendeleo.  

“Endapo elimu ya kutosha ya utamaduni wa kufanya kazi itatolewa ni imani kuwa azma ya Mhe. Rais ya kuwatoa watanzania katika uchumi ulio nyuma na tegemezi kwa kuwapeleka katika uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea itawezekana” alisema Mhe. Ole Sendeka.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante  Ole Gabriel aliahidi kufanyia kazi mawazo hayo kwa kuhakikisha jamii inapata elimu ya kutosha namna ya kuwa na utamaduni wa kutumia muda kimakakati kwa kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Pia alieleza kwamba  ni kweli usiopingika ili  Taifa  liweze kufikia uchumi wa viwanda ni budi kwa wananchi wake kujengea utamaduni wa kufanya kazi kwa bidi ikiwemo kutumia muda kimkakati. 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante  Ole Gabriel (kushot) akimsikiliza  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka (kulia) alipofanya  ziara ya kutembelea Mkoa huo.Picha na Zawadi Msalla-WHUSM.

RATIBA KAMILI YA MAZISHI YA SETH KATENDE

EVERTON KUTUA NCHINI JULY 12 KUCHEZA NA GOR MAHIA

$
0
0
Na Anil Ricco, Globu ya Jamii
Timu ya Soka ya Everton inayoshiriki Ligi Kuu Soka nchini Uingereza (EPL) inatarajiwa kuingia nchini Tanzania, July 12 kucheza Mchezo wake wa Kirafiki na Klabu ya Soka ya Gor Mahia ya nchini Kenya, July 13 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Everton inaingia nchini ikiwa na Gwiji wake wa Soka, Wayne Rooney aliyesajiliwa hivi karibuni.

Katika mchezo huo baina ya Everton na Gor Mahia, Serikali kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Michezo, Yusuph Omary Singo amesema kuwa Mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akithibitisha ujio wa Kikosi hicho, Mkurugenzi wa SportPesa nchini Tanzania, Abbas Talimba amesema maandalizi yote yamekamilika kwa Everton kutua nchini, amesema Kikosi hicho kinakuja na Wanandinga wake wote.

Kwa upande wa Upatikanaji wa Tiketi, Selcom kupitia Meneja Miradi na Mshauri wa Mifumo, Galusi Lunyeta amesema watu watakaokuja kushuhudia mchezo huo watahakikisha wote wanapata tiketi kupitia Mfumo huo wa Selcom, kuanzia saa mbili asubuhi siku ya Mechi.

Pia katika Suala la Ulinzi na Usalama, Inspekta wa Jeshi la Polisi, Hasheem Abdallah amesema kuwa njia zitakazotumika kuingia Uwanjani siku ya Mchezo huo katika Uwanja wa Taifa ni Mandela Road na Kilwa Road, watu kufika Uwanjani na kutoka.
Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Omary Singo akizungumza kwa niaba ya Serikali katika kuupokea ugeni wa Timu ya Everton wanaokuja kucheza Mchezo wa Kirafiki na Gor Mahia ya nchini Kenya, July 13 mwaka huu.
 Mkurugenzi wa SportPesa nchini, Abbas Talimba akifafanua jambo juu ya ujio wa Timu ya Everton ya Uingereza July 12 mwaka
 Afisa Usalama wa TFF na FIFA, Inspekta Hasheem Abdallah akifafanua kuhusu Ulinzi katika Mchezo huo utakaopigwa July 13 katika Dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Meneja Miradi na Mshauri wa Mifumo - SELCOM, Galusi Lunyeta akifafanua juu ya upatikanaji wa Tiketi siku ya Mchezo huo July 13.

Wawili kizimbani kwa kuingilia mawasiliano nchini ma kuisababishia TCRA hasara ya 210.2m

$
0
0
Na Karama Kenyunko blog ya jamii.

RAIA wa Uganda, Edwin Gusongoirye (30) na Mfanyabiashara, Steven Simon (45) wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia serikali hasara ya Sh milioni 210.2.

Gusongoirye ambaye ni mfamasia pamoja na Simoni wamesomewa mashitaka yao sita  mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa.

Hati ya mashitaka hayo, imsomwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga na kudai kuwa kati ya Machi 6 na Juni 22, mwaka huu jijini Dar es Salaam, washitakiwa walitengeneza mfumo wa kutumia huduma za mtandao kwa lengo la kukwepa kodi ya kupokea na kusambaza mawasiliano bila kuwa na kibali kutoka TCRA

Imedaiwa kuwa kati ya Machi 6 na Juni 22, 2016, washitakiwa hao kwa pamoja waliendesha mfumo wa kupokea na kusambaza mawasiliano ya Kimataifa bila kuwa na leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Katika shtaka la tatu kuwa, imedaiwa kuwa,  Gusongoirye na Simon waliingiza vifaa vya mawasiliano nchini ambavyo ni maboksi matatu ya simu bila kuwa na kibali cha TCRA.

Aidha, washtakiwa hao wanadaiwa, kabla ya Machi, 2012 jijini Dar es Salaam, walisimika vifaa mbalimbali vya mawasiliano zikiwemo kompyuta mpakato mbili aina ya Dell na Hp bila kibali.

Pia washitakiwa wanadaiwa kutumia vifaa vya mawasiliano ambavyo havijathibitishwa kwa lengo la kupokea na kusambaza viashiria vya mawasiliano bila kuthibitishwa na TCRA.

Machi 6 na Juni 22, mwaka huu, kwa makusudi na washitakiwa kwa pamoja waliisababishia serikali hasara ya Sh milioni 210.2.

Washitakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi na kwamba mahakama hiyo haiwezi kutoa dhamana kwani mashitaka hayo ni zaidi ya Sh milioni 10 ambayo wanatakiwa kuomba Mahakama Kuu.

Imedaiwa,  upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 25, mwaka huu kwa kutajwa.

  Watuhumiwa, Steven Simon, aliyetangulia mbele na Edwin Gusongoirye, raia wa Uganda, wakipelekwa mahakamani kusomewa kesi yao ya uhujumu uchumi.

Filamu ya "Tusijisahau" yatambulishwa rasmi leo

$
0
0
 Msanii wa Filamu nchini Issa Mussa maarufu kama Clod 112 (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitambulisha filamu yake mpya ijulikanayo kama “Tusijisahau,” katikati ni Mtayarishaji wa filamu hiyo Bi. Amina Musa na kushoto ni Mwakilishi toka Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Esther Ibrahim.
 Mtayarishaji wa filamu ya “ Tusijisahau”  Bi. Amina Musa (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakitambulisha filamu hiyo mapema hii leo jijini dare s Salaam, katikati ni Muigizaji wa filamu hiyo Bw. Issa Mussa maarufu kama Clod 112 na kulia ni Mhasibu wa kampuni ya AMUS Entertainment Bw. Abdul Vencha.

Picha na Eliphace Marwa - Maelezo

RC MAKONDA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA JENGO LA HUDUMA ZA DHARURA HOSPITAL YA TEMEKE

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya uwekeji wa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la kisasa la huduma za dharura Hospitali ya Temeke ambalo ujenzi wake utagharimu zaidi ya shilingi Million 800 linalofadhiliwa na ubalozi wa Japan Nchini Tanzania.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda  akikata utepe kwa kushirikia na Mkuu wa Wilaya wa Temeke,Felix Lyaniva pamoja Mwakilishi wa Balozi wa Japani Nchini,Hiroyuki Kubota,kwenye hafla fupi ya uwekeji wa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la kisasa la huduma za dharura Hospitali ya Temeke, ambalo ujenzi wake utagharimu zaidi ya shilingi Million 800 linalofadhiliwa na ubalozi wa Japan Nchini Tanzania.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akipongezana na Mwakilishi wa Balozi wa Japani Nchini Tanzania,Hiroyuki Kubota.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda na viongozi wa halmashauri ya manispaa ya temeke wakikagua ujenzi wa jengo la huduma za dharura.
 Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda. Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa halmashauri ya manispaa ya temeke na watumishi wa Hospitali hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la kisasa la huduma za dharura Hospitali ya Temeke ambalo ujenzi wake utagharimu zaidi ya shilingi Million 800 linalofadhiliwa na ubalozi wa Japan Nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mheshimiwa Makonda amesema jengo hilo litakuwa na uwezo wa kusaidia zaidi ya watu 2,000 kwa siku ambapo litakuwa na chumba cha upasuaji,chumba cha ICU,vyumba vya uangalizi maalumu wa wagonjwa pamoja na vyumba vya madaktari.

Aidha jengo hilo litakuwa na vyumba maalumu vya watoto (njiti) akinamama na wababa ambapo lengo ni kuhakikisha mgonjwa yoyote wa dharura iwe wa ajali,upasuaji kwa kinamama wajawaziito,malaria ya ghafla,moto na wanaobanwa na kifua wanapatiwa huduma ya haraka ambapo kwa hatua hiyo itasaidia kupunguza mlundikano wa wagonjwa wa dharura Hospital ya Taifa Muhimbili kama Rais Dkt.Magufuli anavyotaka.

“Mimi nimeshuhudia watu wengi wakipoteza maisha kwa kukosa huduma za dharura, hii ndio iliyonisukuma kutafuta kila njia ili wananchi wangu wasipoteze maisha kwasababu tu ya kukosa hutuma ya haraka, nikaamua kumtafuta balozi wa Japani na kumshirikisha jambao hili, Balozi aliponisikiliza na kunielewa akakubali kuniunga mkono katika mapambano yangu ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi hasa wanyonge na ameshanipa fedha kwaajili ya ujenzi wa jengo hilo na hivi tunavyoongea tayari mkandarasi ameanza na ujenzi” Alisema Makonda.

Aidha Mheshimiwa Makonda amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo utachukuwa miezi sita hadi kukamilika na kueleza kuwa dhamira yake ni kuhakikisha Dar es salaam inakuwa mkoa unaotoa huduma bora za Afya.

“Watu hatukumbukwi kwa maneno bali kazi tulizofanya, kwa kuwa Rais Magufuli amenipa Mkoa niongoze na mimi ni lazima nitumie akili na kipaji ambacho Mungu amenipa kutatua Changamoto za Afya katika Mkoa wangu”, Alisisitiza Makonda.

Kwa upande Mwakilishi wa Balozi wa Japani Nchini Tanzania Bwana Hiroyuki Kubota amesema serikali ya Japan itaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali huku mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa Felix Lyaniva akimpongeza Makonda kwa namna anavyopambana kutatua kero za wananchi

MAMA MERY MAJALIWA ATAKA WAZAZI KUWASOMESHA KWA BIDII WATOTO WA KIKE

$
0
0
Mke wa Waziri Mkuu  Mery  Majaliwa  ametoa Wito kwa Wazizi kupeleka  Watoto wa Kikeke  Shule  ametoa  wito huo katika  mkutano wa hadhara  Uliofanyika  Kiwanja cha  Michezo wilaya ya Liwale July 10, 2017 ,Mama majaliwa  ameongozana na Waziri Mkuu Kassim  Majaliwa  katika ziara ya kikazi  ya siku Nne  Mkoani   Lindi.Pcha na Ofisi ya Waziri Mkuu. 
Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa  akiangalia Dawa zilizopo katika Stoo ya Dawa Hospital ya  Wilaya ya Liwale July 10, 2017 ,kushoto  kwa  Waziri  Mkuu  ni  Mbunge  wa Wilaya ya Ruangwa(CUF)   Zuberi  Kichauka  na  kulia ni  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Lindi Dr Maulid Majala, Waziri Mkuu Kassim  Majaliwa  yupo  katika ziara ya kikazi  ya siku Nne  Mkoani Lindi

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MOBILE 360 AFRICA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kusimamia na kuweka mazingira bora yatakayosaidia mamia ya wananchi nchini wanapata huduma za mawasiliano ya simu kwa njia ya kisasa zaidi mjini na vijijini.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati anafungua Mkutano wa mwaka wa Chama cha Makampuni ya Simu Duniani (GSMA MOBILE 360) Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassana amesema anaimani kuwa wadau hao wa makampuni ya simu watajadili kwa kina namna bora ya kufikisha mawasiliano ya kisasa kwa wananchi na kuweka mipango mizuri ya kufikia wananchi wengi zaidi hasa maeneo vijijini ambayo baadhi ya maeneo hayafikiki kutokana na uduni wa miundombinu.

“Ningependa kusema kwamba Tanzania inakubali sana ushirikiano na GSMA na tunatamani kupanua ushirikiano wetu na uwezeshaji kwa Watu wetu kwa njia ya sekta ya simu ili kufikia utekelezaji wa ajenda za Maendeleo endelevu ya Umoja wa Afrika AU na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa 2020”.Amesisitiza Makamu wa Rais.

Ameleeza kuwa kwa sasa Tanzania ni miongoni mwa nchi kadhaa Kusini mwa Bara la Afrika ambayo inafanya vizuri kwa wananchi wake kutuma fedha kwa kutumia simu za mkononi na kusema kuwa hilo ni jambo zuri hasa kutokana na baadhi ya wananchi kutokuwa na akaunti za benki hivyo huduma hiyo huwasaidia kwa kiasi kikubwa kwa kutuma fedha kwa urahisi.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza umuhimu wa kuimarishwa zaidi kwa huduma za kisasa za kimtandao ili wananchi waweze kunufaika zaidi kwa njia hiyo katika sekta za elimu,afya, kilimo, biashara na masuala ya kijinsia.

Amewahakikishia wadau hao wa makampuni ya simu kuwa Serikali ya awamu ya Tano itaendelea kushirikiana nao bega kwa bega ili kuhakikisha sekta hiyo inaimarisha huduma zake kwa njia ya kisasa kwa wananchi.

Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali ya itaendelea kujifunza kutoka nchi zingine ambazo zimefanya vizuri katika sekta ya mawasiliano ili taifa na wananchi wake liweze kunufaika ipasavyo na huduma hizo kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Kwa upande wake, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa amesema akizungumza katika mkutano huo ameeleza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na Makampuni ya Mawasiliano ili kuhakikisha huduma zinazotolewa kwa wananchi zinakuwa na ubora unaotakiwa.


Imetolewa na 
Ofisi ya Makamu wa Rais wa 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ikulu- Dar es Salaam.
11-Julai-2017.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa GSMA Mobile 360 Africa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Baadhi ya Wageni waalikwa mbalimbali wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa GSMA Mobile 360 Africa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI, DKT. ALOYCE NZUKI AFUNGUA WARSHA YA KUKUSANYA MAONI YA KUBORESHA RASIMU YA SERA MPYA YA MISITU YA MWAKA 2016 KWA WAKAZI WA MIKOA YA KANDA YA KATI MJINI DODOMA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki akizungumza wakati akifungua warsha iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa wadau wa Mikoa ya Kanda ya Kati kwa ajili ya kukusanya maoni ya kuboresha Rasimu ya Sera Mpya ya Misitu ya mwaka 2016 iliyofanyika mjini Dodoma leo. 
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ezeckiel Mwakalukwa akizungumza katika warsha iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa wadau wa Mikoa ya Kanda ya Kati kwa ajili ya kukusanya maoni ya kuboresha Rasimu ya Sera Mpya ya Misitu ya mwaka 2016 iliyofanyika mjini Dodoma leo. 
 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kushoto) akipokea vitabu vya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mpingo Conservation Initiatives, Makala Jasper ambao wamesaidia kuchapisha nakala 1304 za sera hiyo kwa ajili ya kusaidia zoezi linaloendelea la kukusanya maoni ya kuboresha Rasimu ya Sera Mpya ya Misitu ya Mwaka 2016 katika warsha iliyoandaliwa na Wizara hiyo mjini Dodoma leo. Kulia anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezeckiel Mwakalukwa.
 Baadhi wa watumishi wa Wizara ya Maliasili na wadau wa sekta ya Misitu na Nyuki wakiwa kwenye warsha iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya kukusanya maoni ya kuboresha Rasimu ya Sera Mpya ya Misitu ya mwaka 2016, mjini Dodoma leo.
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo.
Baadhi ya wakazi wa kanda ya kati walioshiriki warsha iliyoandaliwa na Wziara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya kukusanya maoni iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya kukusanya maoni ya kuboresha Rasimu ya Sera Mpya ya Misitu ya mwaka 2016, mjini Dodoma leo.
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo kutoka mikoa ya Kanda ya Kati.
  Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo.
 Picha ya pamoja ya Naibu Katibu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki na washiriki wa warsha hiyo.
 Picha ya pamoja ya Naibu Katibu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (katikati walioka), Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezeckiel Mwakalukwa (kulia kwake)na Wawezeshaji wa warsha hiyo.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa kwenye vikundi kazi vya kukusanya maoni ya kuboresha Rasimu ya Sera Mpya ya Misitu ya mwaka 2016 lililoandaliwa na Wizara hiyo mjini Dodoma leo.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Alen Richard akizungumza na baadhi ya wadau wa Misitu wa Mikoa ya Kanda ya Kati wakati wa warsha iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa ajili ya kukusanya maoni ya kuboresha Rasimu ya Sera Mpya ya Misitu ya mwaka 2016 lililoandaliwa na Wizara hiyo mjini Dodoma leo.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa kwenye vikundi kazi vya kukusanya maoni ya kuboresha Rasimu ya Sera Mpya ya Misitu ya mwaka 2016 lililoandaliwa na Wizara hiyo mjini Dodoma leo. (PICHA ZOTE NA HAMZA TEMBA - WMU)

SOMA HOTUBA YA NAIBU KATIBU MKUU NA MKURUGENZI WA IDARA YA MISITU NA NYUKI HAPA CHINI


NAIBU WAZIRI LUHAGA MPINA AFANYA ZIARA KUKAGUA MAZINGIRA YA MTO MSIMBAZI

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akizungumzana wanahabari katikati ya Mto Msimbazi chini ya Daraja la jangwani baada ya kupima kiwango cha hewa ya Oxygen katika maji ya mto msimbazi na sampuli za maji hayo kupelekwa katika katika maabara ya mkemia mkuu wa serikali kwa vipimo zaidi, ili kujua kama maji hayo yana madhara kwabinadamu, mazingira na viumbe hai wengine. 
Mto Msimbazi unavyoonekana 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akiangalia kiasi cha hewa ya Oxygen kilichopo katika maji ya Mto msimbazi akisaidiwa na wataalamu kutoka katika maabara ya mkemia mkuu wa serikali hawapo pichani, katika eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Evelyn Mkoko

TRA YAFANIKIWA KUKUSANYA TRILLIONI 14.4 KWA MWAKA WA FEDHA 2016/17

Stella Manyanya akabidhi bendera kwa wanafuunzi watakaoiwakilisha nchi katika mashindano ya first lbal Robotic Challenges nchini Marekani

$
0
0
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya leo amekabidhi Bendera ya Taifa kwa wanafunzi saba wanaosoma masomo ya sayansi wanaokwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya First Global Challenges nchini Marekani. Makabidhiano hayo yamefanyika katika shule ya Sekondari ya wasichana Jangwani. 

Katika makabidhiano hayo Mhandisi Manyanya amewataka wanafunzi wote nchini kusoma kwa bidii masomo ya sayansi, teknolojia na ubunifu ili kuhakikisha ndoto ya Tanzania ya kuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda na biashara inafanikiwa na kwamba wizara tutaendelea na jukumu lake la kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ili wanafunzi wote waendelee kufanya vizuri katika masomo ya sayansi.

Shule zilizotoa wanafunzi watakaoshiriki katika mashindano hayo ni pamoja na Jangwani, Azania, Jamhuri, Benjamini Mkapa, Feza na Kisutu.

Naye mratibu wa mashindano hayo kwa upande wa Tanzania ndugu Mkufu Shabani Tindi alisema mashindano haya yameanzishwa na kufadhiliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Marekani liitwalo FIRST yenye maana ya for inspiration and recognition of science and technology lenye lengo la kuhamasisha ulimwenguni kote vijana wanaosoma masomo ya sayansi, uhandisi, teknolojia na hesabu kuweza kutatua changamoto mbalimbali ulimwenguni 

Wanafunzi watakaoshiriki wanatarajia kuondoka kesho Juni 12, 2017 na watakuwa nchini Marekani kwa ajilia ya mashindano hayo makubwa kiulimwengu ambapo zaidi ya nchi 170 zitashiriki.

Naye mmoja wa washiriki Raymond Benedict kutoka Shule ya Sekondari Jamhuri amesema yeye wenzake wamejiandaa vizuri katika kuhakikisha wanaiwakilisha nchi katika mashindano hayo vizuri na kwa ufahari.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akikabidhi Bendera ya Taifa kwa wanafunzi watakaoshiriki katika mashindano ya First Global Robotic Challenges nchini Marekani.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya pamoja na baadhi ya wanafunzi watakaoshiriki katika mashindano ya First Global Robotic Challenges wakiwaonyesha wanafunzi wa shule ya wasichana Jangwani (Hawapo pichini) Roboti walioibuni. 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akipata maelezo kutoka kwa mwanafunzi Raymond Benedict kutoka shule ya sekondari Jamhuri ya namna roboti iliyobuniwa inavyofanya kazi. 

HAFLA YA TUZO ZA SUPERBRANDS AFRIKA MASHARIKI ZAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Wakurugenzi na wawakilishi wa kampuni yaliyopata tuzo ya Superbrands wakiwa na mkurugenzi wa Superbrands Afrika Mashariki, Jawad Jaffer (wa tatu kutoka kushoto).
Mkurugenzi wa Superbrands Afrika Mashariki, Jawad Jaffer akiongea mapema leo katika halfa ya kukabidhi vyeti vya kudhibitisha ubora wa kampuni na bidhaa zinazokubalika Afrika Mashariki iliyofanyika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, Dar es Salaam. Picha na Kajunason/Cathbert Kajuna.
Wakurugenzi na wawakilishi wa kampuni yaliyopata tuzo ya Superbrands wakimsikiliza mkurungenzi wakati wa hafla ya kutoa vyeti kwa kampuni zenye sifa katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Superbrands Afrika Mashariki, Jawad Jafer (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya ChemiCotex (kushoto), Sumit Bhatnagar watengenezaji wa dawa ya meno ya 'Whitedent' cheti cha kudhibitisha ubora wa kampuni na bidhaa zinazokubalika Afrika Mashariki.
Mkurugenzi wa Superbrands Afrika Mashariki, Jawad Jafer (kulia) akimkabidhi Mhariri Mkuu wa ITV Tanzania, Steven Chuwa (kushoto) cheti cha kudhibitisha ubora wa kampuni na bidhaa zinazokubalika Afrika Mashariki.
Mkurugenzi wa Superbrands Afrika Mashariki, Jawad Jafer (kulia) akimkabidhi Mhariri Mkuu wa The Guardian Ltd, Jesse Kwayu (kushoto) cheti cha kudhibitisha ubora wa kampuni na bidhaa zinazokubalika Afrika Mashariki.
Mkurugenzi wa Superbrands Afrika Mashariki, Jawad Jafer (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez (kushoto) cheti cha kudhibitisha ubora wa kampuni na bidhaa zinazokubalika Afrika Mashariki.
Mkurugenzi wa Superbrands Afrika Mashariki, Jawad Jafer (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Red Gold, Darsh Dandit (kushoto) cheti cha kudhibitisha ubora wa kampuni na bidhaa zinazokubalika Afrika Mashariki.
Mkurugenzi wa Superbrands Afrika Mashariki, Jawad Jafer (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Wateja Maalum wa benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto) cheti cha kudhibitisha ubora wa kampuni na bidhaa zinazokubalika Afrika Mashariki.

Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images