Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

MKURUGENZI APIGA MARUFUKU SHUGHULI ZA KILIMO KWENYE VYAZO VYA MAJI

$
0
0
Mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya MADABA SHIFII MPENDA ametembelea eneo ambalo limeaharibiwa vibaya na baadhi ya wananchi wanaojishughulisha na kilimo pamoja na ufugaji kwenye vyazo vya maji.Haikuwa rahisi kufikia eneo hilo kwani ilitupasa kutembea kwa mwendo mrefu kuweza kufikia eneo husika ambalo ni chazo cha mto NAMAOVI kijiji cha MWANDE kata ya MATETELEKA halimashauri ya MADABA mkoani RUVUMA HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE. 

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MKOANI LINDI KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TANO

$
0
0
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Mzee Mtopa wakati alipowasili Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi, katika ziara ya kikazi ya siku tano,(katikati) ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfey Zambi, Julai 10, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasili Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne, akiwa mkoani humo Waziri Mkuu ameanza ziara yake katika wilaya ya Liwale kwa ajili ya kukagua shughuli za maendele na jioni ya leo atukuwa na mkutano wa hadhara na kuzungumza na wananchi wa Liwale pamoja na kusikiliza kero zao

Waziri Mkuu ameongozana na Mke wake Mery Majaliwa ambapo walipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi pamoja viongozi wa wilaya za Mkoa wa Lindi ambao walifika katika mapokezi katika uwanja wa ndege wa Nachingwea.Waziri Mkuu hapo kesho anatarajia kuendelea na ziara yake wilayani Ruangwa.

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI JUNI,2017 WAPUNGUA KWA ASIMILIA 5.4

$
0
0
MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Juni, 2017 umepungua hadi asilimia 5.4 ikilinganishwa na asilimia 6.1 ilivyokuwa mwezi Mei, 2017.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo amesema Mfumuko wa Bei umepungua kutokana na kupungua kwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Juni, 2017 ikilinganishwa na kasi ya upandaji iliyokuwa kwa mwezi Mei, 2017.

“Mfumuko wa Bei wa mwezi Juni, 2017 umepungua hadi kufikia asilimia 5.4 kutoka asilimia 6.1 mwezi Mei, 2017. Hii inatokana na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Juni, 2017,” amesema Kwesigabo.

Amesema Mfumuko wa Bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umepungua kwa asilimia 0.1 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 0.2 ilivyokuwa mwezi Mei, 2017.Kwesigabo amesema Fahirisi za Bei zimepungua hadi 109.10 mwezi Juni, 2017 kutoka 109.26 mwezi Mei, 2017. Amesema Kupungua kwa Fahirisi za Bei kumechangiwa hasa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula.

Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa fahirisi ni pamoja na mahindi ambayo yamepungua kwa asilimia 5.1, unga wa mahindi kwa asilimia 2.4, unga wa mihongo kwa asilimia 1.9, machungwa kwa asilimia 2.4, dagaa kwa asilimia 3.2, mbogamboga kwa asilimia 5.7, maharage kwa asilimia 1.8 na viazi mviringo kwa asilimia 6.2.

Aidha Mfumuko wa Bei kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani kwa mwezi Juni, 2017 umepungua hadi asilimia 9.8 kutoka asilimia 11.8 mwezi Mei, 2017.

Uwezo wa Shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umeimarika kidogo na kufikia Shilingi 91 na senti 66 mwezi Juni, 2017 ikilinganishwa na Shilingi 91 na senti 53 ilivyokuwa mwezi Mei, 2017.

Hata hivyo, Mfumuko wa Bei nchini Tanzania una mwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki kwa kuwa Mfumuko wa Bei wa mwezi Juni, 2017 nchini Uganda umepungua hadi asilimia 6.4 kutoka asilimia 7.2 mwezi Mei, 2017; na nchini Kenya, Mfumuko wa Bei wa Mwezi Juni, 2017 umepungua hadi asilimia 9.21 kutoka asilimia 11.70 mwezi Mei, 2017.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigwabo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leokuhusu mfumuko wa bei wa Taifa kwa Mwezi Juni. Kulia ni Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira, Ruth Minja.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Balozi wa Italia atembelea Wizara ya Mambo ya Nje

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Suzan Kolimba (Mb), akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Roberto Mengoni na ujumbe wake kwa ajili ya kufanya mazungumzo. 
Dtk. Kolimba akisisitiza jambo kwenye mazungumzo na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Roberto Mengoni. Katika mazungumzo hayo alikuwepo pia Makamu wa Rais wa Shirika la Taifa la Reli la Italia, Bw. Giovanni Roca ambaye amekuja nchini kuangalia fursa za uwekezaji katika sekta ya reli baada ya kuhamasishwa na Mhe. Naibu Waziri alipotembelea Italia hivi karibuni. 
Ujumbe wa Italia uliofuatana na Mhe. Balozi ukifuatilia mazungumzo. 
Bw. Charles Faini (kulia), Katibu wa Naibu Waziri na Bw. Salvatory Mbilinyi wa Wizara ya Mambo ya Nje wakinukuu taarifa muhimu 
Picha ya pamoja

TUZO ZA MABALOZI WA USALAMA BARABARANI ZATOLEWA MKOANI DODOMA

$
0
0
 Mgeni Rasmi, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Simon Odunga, akisindikizwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani,Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) kuingia ukumbini wakati wa hafla ya kutunuku tuzo kwa Mabalozi wa Usalama Barabarani,iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hotel ya Royal,mkoani Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Mohamed Mpinga akionyesha tuzo ya balozi bora wa usalama barabarani, aliyokabidhiwa na Mgeni Rasmi, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Simon Odunga(kushoto) wakati wa hafla ya kutunuku tuzo kwa mabalozi hao,wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani,Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.Hafla hiyo  imefanyika mwishoni mwa wiki  katika Hotel ya Royal,mkoani Dodoma. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Mgeni Rasmi,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Simon Odunga, akimkabidhi  Kamishna Msaidizi wa  Jeshi la Polisi, Fortunatus Musilimu(kulia) cheti cha kutambua mchango wake katika masuala ya  usalama barabarani wakati wa hafla ya kutunuku tuzo kwa Mabalozi wa Usalama Barabarani,wapili kushoto  ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani,Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.Hafla hiyo  imefanyika mwishoni mwa wiki  katika Hotel ya Royal,mkoani Dodoma. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Mgeni Rasmi,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Simon Odunga, akimkabidhi  Mkurugenzi wa Barabara wa Mamlaka ya Usimamizi wa Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA), Johansen Kahatano (kulia) cheti cha kutambua mchango wake katika masuala ya  usalama barabarani wakati wa hafla ya kutunuku tuzo kwa Mabalozi wa Usalama Barabarani,wapili kushoto  ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani,Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.Hafla hiyo  imefanyika mwishoni mwa wiki  katika Hotel ya Royal,mkoani Dodoma. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mgeni Rasmi,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Simon Odunga (wakwanza  kushoto waliokaa) na Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani,Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto waliokaa), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani mara baada ya kutunukiwa vyeti ikiwa ni utambuzi wa mchango wao katika masuala ya usalama barabarani,iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hotel ya Royal,mkoani Dodoma. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA AKABIDHI NYUMBA 50 ZA WATUMISHI WA AFYA KATIKA MIKOA YA SIMIYU, KAGERA NA GEITA

$
0
0

 Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akimkabidhi Hati za Umiliki wa nyumba 50 za Watumishi wa Afya kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika uwanja wa michezo wa Mazaina Chato mkoani Geita. 
  Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akizungumza na wananchi wa Mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita kabla ya kukabidhi Hati za umiliki wa nyumba 50 za watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa na Taasisi ya (Mkapa Foundation) katika mikoa hiyo mitatu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita baada ya Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa kukabidhi nyumba 50 kwa wizara ya Afya.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya kukabidhi nyumba hizo 50 zitakazotumika katika Sekta ya Afya katika mikoa ya Kagera, Simiyu na Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa wakati Mbunge wa Chato ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini,  Dkt. Medard Kalemani alipokuwa akihutubia wananchi wa Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya kumaliza ziara yake Chato mkoani Geita ambapo alikabidhi nyumba 50 zitakazotumika katika sekta ya afya katika mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mama Anna Mkapa.
 Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akiangalia hotuba yake kabla ya kuhutubia wananchi mbalimbali katika uwanja wa michezo wa Mazaina Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wakati akiwasili katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita.
 Kikundi cha ngoma za asili cha Chato kikitumbuiza katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita.
Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Chato Shaaban Ntarambe hati ya kituo cha kukamua Mafuta ya Alizeti  (Double Refine) kilichojengwa Chato mkoani Geita kwa Msaada wa Serikali ya Japan. 

PICHA NA IKULU

Muhimbili yawezesha watoto kusikia kwa mara ya kwanza

$
0
0
Watoto watano waliofanyiwa upasuaji na kuwekewa vifaa maalum  vya kusaidia kusikia (Cochlear Implant) leo wamewashiwa vifaa hivyo ili waweze kusikia kwa mara ya kwanza.Zoezi hilo  limefanywa leo na wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na watalaam kutoka MEDEL .

Daktari Bingwa wa magonjwa ya Masikio, Pua na Koo Edwin  Liyombo amesema Juni   5 na 6 mwaka huu watoto hao walifanyiwa upasuaji huo kwa mara ya kwanza na kuwekewa vifaa maalum kwa ajili ya kusikia (Internal complete) lakini leo wamekuja kuwekewa na  kuwashiwa  vifaa vya nje(External complete) ili waweze kusikia.

Kwa upande wake mtaalam wa vifaa vya usikivu Fayaz Jaffer amesema baada ya kuwekewa kifaa hivyo watoto hao wanapaswa kurudi kila baada ya wiki mbili kwa miezi mitatu na baada ya hapo  watarudi  wiki mbili kwa miezi sita ili kufanyiwa mazoezi.

‘’Baada ya hapo wanaanza kuwafanyia mazoezi ya kuongea ( speech therapy) ndani ya mwaka mmoja na kadiri umri unavyozidi kwenda watakuwa wameshaanza kusikia na kujifunza kuongea na kupelekwa kujifunza zaidi katika shule za kawaida na si shule maalum kama ilivyozoeleka” amesema mtaalam huyo.

Juni 7 mwaka huu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alizindua huduma ya upasuaji wa kupandikizaji wa vifaa vya usikivu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili , ambapo katika Hospitali za Umma Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kutoa huduma hiyo  na ya pili katika nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki ikitanguliwa na Kenya.
 Muwakilishi wa Medel Afrika Mohamed El Disouky akimfanyia mazoezi ya kuzungumza mtoto Asma Athuman Mwinyi ambaye alipata matatizo ya kusikia akiwa na miaka sita.
Mtaalam Mohamed El Disouky akimfanyia majaribio ya kifaa cha usikivu mtoto Silas Machaku ( 3 ) ambaye aliwekewa kifaa maalum cha usikivu kwa ndani (Internal complete) lakini leo amewekewa kifaa kwa nje (External complete) ili aweze kusikia . zoezi hilo limefanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

WIZARA YA AFYA YAZINDUA MPANGO WA KUTEMBELEA HOSPITALI ZA UMMA NCHINI

$
0
0
Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezitaka hospitali nchini kutumia miongozo katika kutekeleza shughuli mbalimbali za huduma za afya  pamoja na kuimarisha mifumo ya TEHAMA ili kuwapo kwa mawasiliano kati ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na hospitali nyingine za rufaa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa wizara hiyo Dk. Mpoki Ulisubisya wakati akizindua mpango wa kufuatilia utoaji wa huduma za afya yakiwamo mafanikio na changamoto katika hospitali za umma nchini.

Dk Ulisubisya amesema mpango wa wizara yake ni kuzitembelea hospitali za umma nchini utaanzia kwenye hospitali za kibingwa ili ziwe kitovu cha kutoa mafunzo kwa hospitali nyingine nchini.

“ Malalamiko ni mengi yanapaswa kushughulikiwa kwa kuwekwa mifumo imara ya utekelezaji wa shughuli za huduma za afya kwa lengo la kuzuia kushuka kwa ubora wa huduma. Pia, hali hii itasaidia kuimarisha maadili miongoni mwa watumishi,” amesema Dk Ulisubisya wakati akizindua mpango huo leo.

Amesema wizara ya afya itaendelea kushirikiana na kitengo cha elimu ya afya kwa umma ili kuhakikisha watumiaji wa huduma za tiba wanafahamu mfumo na taratibu za upatikanaji wa huduma za tiba katika ngazi mbalimbali ili kuondoa usumbufu na malalamiko kutoka kwa wagonjwa.

Akizungumzia maslahi ya wafanyakazi, amesema serikali inafanyia kazi maombi ya kuboreshwa kwa maslahi yao na kwamba wachape kazi kwani inakumbuka suala hilo.

Pia, Dk Ulisubisya aliipongeza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa juhudi  kubwa ya kuboresha huduma za afya kwa kupanua huduma za afya, kusomesha wataalamu wa afya na kununua vifaa tiba.

“Muhimbili mnafanya kazi nzuri na kubwa, naamini taasisi nyingine zitajifunza kwenu, mna mambo makubwa ya kujivunia,” amesema.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Tiba, Dk. Dorothy Gwajima amefafanua lengo la ziara yake ni kuwezesha kupatikana kwa taarifa kwa wakati na utasaidia katika utekelezaji wa  huduma za afya katika hospitali nchini.

Dk. Gwajima amesema kuwa mfumo huo utasaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa wa katika Hospitali ya Taifa  ya Muhimbili.

“Kutakuwa na ratiba ya kudumu ya vikao kati ya wizara na watoa huduma kuhusu utekelezaji wa huduma za tiba. Taarifa za halmashauri lazima zikutane ili kujua hali za huduma za afya kwenye halmashauri zenu, hivyo kutakuwa na kamati mbalimbali ili kuwasilisha ufuatiliaji wa shughuli za huduma za afya.

Mkurugenzi wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru akizungumzia juhudi za kuboresha huduma za afya, amesema kuwa upatikanaji wa dawa MNH ni asilimia 95 kutoka asilimia 40. Pia, amesema Muhimbili inatarajia kupata wataalamu 18 kutoka Cuba wa masuala ya mionzi, usingizi, macho na masikio.

Pia, Profesa Museru ameiomba serikali kuipatia Muhimbili kibali cha kuajiri wataalamu mbalimbali kwa kuwa ina upungufu wa wafanyakazi karibu 300 kutokana na baadhi ya wafanyakazi kustaafu, kupoteza maisha na wengine  130 kubainika kuwa na vyeti feki.

 Ziara hiyo imeanza rasmi leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na maofisa wa wizara hiyo wametembelea Idara ya magonjwa ya Dharura na Ajali, Idara ya Maabara Kuu na idara mbalimba ambako wamezungumza na wafanyakazi pamoja na wagonjwa.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya akizungumza katika mkutano wa kuzindua mpango wa kuzitembelea hospitali za umma nchini ili kujua mafanikio na changamoto zilizopo kwenye hospitali hizo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tiba, Dk. Dorothy Gwajima wa wizara hiyo. Mpango huo umeandaliwa na wizara ya afya na ziara hiyo imeanza rasmi leo Muhimbili.
 Baadhi ya wataalamu wa afya kutoka Muhimbili na taasisi nyingine wakimsikiliza Katibu Mkuu, Dk Ulisubisya katika mkutano wa uzinduzi uliofanyika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
 Kaimu Mkurugenzi wa Tiba, Dk. Dorothy Gwajima (kushoto) wa wizara hiyo pamoja na wataalamu wengine wakifuatilia mkutano huo leo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza kabla ya kuzinduliwa kwa mpango wa kutembelea hospitali za umma ili kujua mafanikio na changamoto  zilizopo kwenye hospitali hizo.
 Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dk Juma Mfinanga wa Muhimbili akimwelekeza jambo Kaimu Mkurugenzi wa Tiba, Dk. Dorothy Gwajima (kushoto) wa wizara ya Afya wakati wa ziara ya kutembelea hospitali hiyo leo. Wengine ni maofisa kutoka wizara ya afya na hospitali ya Muhimbili.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Afya, Nsacris Mwamaja wakichukua maelezo kutoka kwa Sister Mushi  wakati wa ziara hiyo.

Uzinduzi Rock City Marathon; RT yazitangaza rasmi kuwa ni mbio za kimataifa

$
0
0


SHIRIKISHO la Riadha la Taifa (RT) limezitangaza rasmi mbio za Rock City Marathon kuwa mbio za kimataifa baada ya kukidhi vigezo vyote ikiwa ni pamoja na kuhusisha mbio za km 42 kwa mara ya kwanza. Hatua ambayo imepongezwa na wakuu wa mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, na Kagera kwa kuwa itachochea ukuaji wa utalii katika kanda hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw John Mongella kwenye hafla ya uzinduzi wa mbio hizo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Bi Mary Tesha mbali na kupongeza hatua hiyo alisema uwepo wa mbio hizo katika kalenda ya Riadha kimataifa itawavutia watalii wengi katika ukanda huo pia na hivyo kufungua fursa zaidi kupitia utalii.

“Tunatarajia kwamba sasa mbio hizi zitafahamika zaidi duniani na kuvutia washiriki wa kimataifa ambao tunatarajia pia watakuja kama watalii na pia watapata kufahamu fursa za kiuwekezaji,’’ alisema.

Alitoa wito kwa washiriki wa ndani hususani wa mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na wadhamini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Octoba 29 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba jijini humo kwa uratibu wa kampuni ya Capital Plus International.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainabu Telack alisema Mkoa wake unaenda kujipanga kuhakikisha kwamba unatoa washiri bora katika mbio hizo huku akitoa wito kwa waandaaji wa mbio hizo kwa kushirikiana na viongozi wa riadha nchini kuhakikisha wanazitangaza kimataifa mbio hizo ili zivutie washiriki wengi wa kimataifa watakaokuja na fursa nyingine za kiuchumi ikiwemo sekta ya utalii na uwekezaji.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Butiama alisema Mkuu wa Wilaya ya Butiama,Bi Annarose Nyamubi aliemuwakilisha mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa alisema mkoa wake unatarajia kunufaika na mbio hizo kimataifa kupitia vivutio vya kitalii vilivyopo kwenye mkoa huo ikiwemo utamuduni wa wakazi wake pamoja na kuwavutia watalii kutembelea kaburi na kumbukumbu nyingine za Hayati Mwl Julius Nyerere.

Mbio hizo zinazozidi kujiongezea umaarufu kila mwaka tayari zimefanikiwa kuwavutia baadhi ya wadhamini ikiwa ni pamoja na kampuni za TIPER, PUMA, Mwanza Hotel , Real PR Solutions Limited, Fabec na Afrimax Strategic Partnerships Limited.

Awali akitangaza mbio hizo kuwa kimataifa, Makamu wa pili wa RT, Dk Hamad Ndee alisema hatua hiyo inatokana na mbio hizo kukidhi vigezo vyote muhimu ikiwemo upimaji wa njia za kukimbia uliofanywa kitalaamu na mpimajia anayetambuliwa kimataifa Bw John Bayo pamoja na kuhusisha kwa mara ya kwanza mbio za KM 42.195

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mbio hizo Bw Zenno Ngowi mbali na kujipongeza kwa hatua hiyo alisema uhusishaji wa wawashiriki wengi wa kimataifa katika mbio hizo utakidhi lengo hasa la kutangaza utalii katika ukanda wa Ziwa ambayo ni moja ya agenda kuu ya mbio hizo ukiondoa ile ya kuibua na kukuza vipaji vya mchezo huo.

“Ukanda wa Ziwa una vivutio vingi ambavyo lazima vitangazwe kimataifa kwa nguvu kubwa na zaidi ni rahisi kwa watalii kufika hifadhi kama ya Serengeti akitokea Mwanza kuliko kanda nyingine,’’ alibainisha.

Alisema mwaka huu mbio hizo zimezinduliwa mapema ili kutoa muda wa kutosha kwa washiriki waweze kujiandaa vizuri zaidi ili waweze kutoa ushindani zaidi huku akitaja makundi mengine ya mbio hizo kuwa ni kilomita 21 kwa wanaume na wanawake, kilomita 5 kwa ngazi ya ‘corporate’, kilomita 3 kwa ajili ya walemavu na zile za wazee umri zaidi miaka 55 na kuendelea pamoja na kilomita 2.5 kwa ajili ya watoto umri kati ya miaka 7 hadi 10.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Bi Mary Tesha (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Rock City marathon mwaka 2017 wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Butiama Bi Annarose Nyamubi (kulia) aliemuwakilisha mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mbio hizo Bw Zenno Ngowi (wa pili kushoto) na Makamu wa pili wa Shirikisho la Riadha Taifa (RT), Dk Hamad Ndee. Bi Tesha alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw John Mongella.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainabu Telack akitoa nasaa zake kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa Rock City Marathon uliofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Alitoa wito kwa washiriki wa ndani hususani wa mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na wadhamini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Octoba 29 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba  jijini Mwanza kwa uratibu wa kampuni ya Capital Plus International.
Mpimaji wa njia wa njia za riadha anayetambulika kimataifa Bw John Bayo akimuonyesha mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa njia zitakazotumika katika mbio hizo baada ya kupimwa kitaalamu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mbio hizo Bw Zenno Ngowi akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Makamu wa pili wa RT, Dk Hamad Ndee akitoa nasaha zake kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Butiama,Bi Annarose Nyamubi aliemuwakilisha mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa akizungumza kwenye hafla hiyo. 
Baadhi ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo.
Meneja Mkuu wa Hotel ya New Mwanza Hotel Bw Senthi Kumar akizungumza kwenye uzinduzi huo kwa niaba ya wadhamini wengine wa mbio hizo. Hotel hiyo ni moja ya wadhamini wa mbio za Rock City Marathon.
Wageni wote wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa mchezo wa Riadha pamoja na waandaaji wa mbio hizo.-

UFUTA KUUZWA KWA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imemuagiza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba akutane na Bodi ya mazao mchanganyiko kwa ajili ya kuliondoa zao la ufuta na kuliingiza katika mfumo wa stakabadhi ghalani.

Pia amewaagiza wakuu wa mikoa yote inayolima zao la ufuta kukutana na Dkt. Tizeba kwa ajili ya kupanga mfumo mzuri wa uuzaji katika msimu wa mwaka 2016/2017 wakati Serikali ikijipanga kuliingiza zao hilo katika mfumo wa stakabadhi ghalani.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Julai 10, 2017) wakati akisalimiana na wananchi katika vijiji vya Nangano, Kibutuka na Kiangara alipowasili katika wilaya ya Liwale kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Lindi.

Ametoa kauli hiyo baada ya mbunge wa jimbo la Liwale, Mheshimiwa Kuchauka pamoja na wananchi kuiomba Serikali iwasaidie kuboresha bei ya zao la ufuta ambayo imekuwa ikiyumba.

Waziri Mkuu amesema “tatizo lipo kwenye mfumo wa  uuzaji zao la ufuta, unauzwa kwa bei ya rejareja, wanunuzi wako huru. Serikali imemuagiza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuliondoa zao katika bodi ya mazao mchanganyiko na kuliingiza katika mfumo wa stakabadhi ghalani ili kuboresha bei yake.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Bw. Justine Monko kuhakikisha anamaliza tatizo la maji katika vijiji vya Nangano,Kibutuka na Kiangara.

Amesema  Serikali imedhamiria kuondoa tatizo la maji kwa kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400. “Ndio maana Serikali imekuja na Kampeni inayosema mtue mama ndoo kichwani.”

Pia amemtaka Mhandisi wa Maji Bw. Andrew Kilembe kuandika barua ya kufuatilia fedha za maji sh. milioni 76 kwa ajili ya kijiji cha Kiangara walizopangiwa katika bajeti ya mwaka 2016/2017 kwa Waziri wa Maji ili waweze kukamilisha uchimbaji wa kisima.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwaeleza   wananchi wa Kijiji cha Kiangala  jinsi serekali ya awamu ya tano inavyo shughulikia kero za za wananchi Nchini Wananchi hao   walijitokeza July 10, 2017  ili waweze kumueleza kero  zinazo wasumbua  Waziri  yupo Wilayani Liwale Mkoa wa Lindi kwa ziara ya Kikazi ya siku Nne.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  na Mkewe Mery Majaliwa wametembelea Hospitali  ya Wilaya ya Liwale July 10, 2017 na kuwapa zawadi  Watoto Mapacha wenye Siku Mbili  waliozaliwa katika Hospital ya  Liwale, Waziri Mkuu yupo wilayani Liwale Mkoani Lindi kwa ziara ya Kikazi katika Mkoa  wa Lindi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akihutubia umati wa wananchi wa  wilaya ya Liwale waliojitokeza kuja kumsikliza  Michezo wa  wilaya ya Liwale July 10, 2017 Waziri Mkuu yupo wilayani Liwale Mkoani Lindi kwa ziara ya Kikazi katika Mkoa wa Lindi.

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI WAKABIDHIWA GARI

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akisalimiana na Viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Iringa, mara baada ya kuwasili katika sherehe za makabidhiano ya gari la kuzimia moto lililotolewa na Mdau Ndugu, Zakaria Hanspoppe kwenye kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani humo mapema leo asubuhi. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakitoa salamu ya heshima kwa Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoani humo. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza ambaye ni Mgeni rasmi katika shughuli ya makabidhiano ya gari la kuzimia moto akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la ZImamoto na Uokoaji mara baada ya kuwasili kituoni hapo mapema leo asubuhi. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza ambaye ni Mgeni rasmi akisaini kitabu cha wageni ambaye ameketi meza kuu katikati. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Mdau Ndugu Zacharia Hanspoppe (wa kwanza kushoto) ambaye ndiye aliyetoa msaada wa gari la kuzimia moto kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji akitoa pongezi kwa Viongozi wa Jeshi hilo kwa jitihada wanazofanya katika kukabiliana na majanga ya moto, mafuriko, ajali za barabarani na majanga mengine. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza ambaye ni Mgeni rasmi akikata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi rasmi gari la kuzimia moto kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, tukio ambalo limeshuhudiwa na Kamaishna Jenerali wa Jeshi hilo, Viongozi mbalimbali wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani humo, Mdau aliyetoa msaada huo Ndugu, Zacharia Hanspoppe, Maafisa na Askari wa Jeshi hilo pamoja na wananchi. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji akionesha funguo ya gari hilo mara baada ya tukio la kukata utepe na kukabidhiwa rasmi na Mkuu wa Mkoa Bi. Amina Masenza ambaye alikuwa ni Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza mwenye kitambaa cheupe katikati, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye wa kwanza mbele, Mdau ndugu Zachalia Hanspope wa pili kutoka kushoto, pamoja na Viongozi wa kamati ya vyombo vya ulinzi na usalama Mkoani Iringa wakifurahi tukio la makabidhiano. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Gari lililokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoro na Uokoaji Thobias Andengenye. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza (kushoto) akiagana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kulia) mara baada ya kuhitimisha shughuli ya makabidhiano ya gari la kuzimia moto lililotolewa msaada na mdau Ndugu, Zacharia Hanspoppe. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji).

WALIOKULA FEDHA ZA USHIRIKA WATAZILIPA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitahusika na ulipaji wa deni la fedha za Ushirika na badala yake kila aliyekula fedha hizo atazilipa mwenyewe.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Julai 10, 2017), wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Liwale katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa wilaya.

Waziri Mkuu ambaye yuko katika na ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, amesema Serikali haiwezi kukubali Ushirika ukafa nchini kwa ajili ya watu wachache wasiokuwa waaminifu.

Amesema watu wote waliopewa dhamana ya kuongoza Vyama vya Ushirika na kuamua kujinufaisha kwa kula fedha za vyama watazilipa.

Waziri Mkuu amewaagiza Viongozi wa Mkoa wa Lindi kufanya ukaguzi katika Vyama vyote vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) ili kubaini ni wakulima wangapi wanadai.

Amesema baada ya kufanya uchunguzi na kubaini idadi ya wakulima wanaodai na kiasi cha fedha wawachukulie hatua wahusika wote kwa mujibu wa sheria.

Awali, Waziri Mkuu alizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale katika Ukumbi wa Tengeneza, ambapo amewataka Watumishi wa Umma Nchini kutojihusisha na vitendo vya rushwa katika utoaji wa huduma kwa Wananchi.

Amesema Watumishi wanawajibu wa kuwahudumia Wananchi bila ya kutengeneza mazingira ya kuomba rushwa na atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Amesema Watumishi wa Umma wanatakiwa kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia maadili ya kiutumishi jambo litakaloondoa malalamiko kutoka kwa Wananchi.

“Lazima Wananchi waone na wanufaike na kazi inayofanywa na Serikali yao, hivyo ni wajibu wa Watumishi kuwatumikia Wananchi popote walipo na si kukaa maofisini.”

Pia amewataka Watumishi hao kupanga mipango itakayoleta tija kwa Wananchi na si vinginevyo.



IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU, JUMATATU, JULAI 10, 2017

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO ZANZIBAR AZUNGUMZA NA WAANDISHI KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA IDADI YA WATU DUNIANI

$
0
0
Na Maelezo Zanzibar 
Wakati dunia inaungana kuadhimisha siku ya Idadi ya Watu duniani bado uzazi wa Mpango unaonekana ni changamoto katika baadhi ya maeneo ya Zanzibar.
Hali hiyo hupelekea ongezeko la idadi ya watu lisiloendana na kasi ya ukuaji wa uchumi na upatikanaji wa huduma za jamii katika maeneo mbalimbali nchini.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Khalid Salum wakati akitoa taarifa yake kwa Vyombo vya habari kuelekea maadhimisho hayo hapo kesho.
Amesema ni vyema jamii kujenga mwamko juu ya umuhimu wa suala la uzazi wa Mpango ili kujenga jamii bora, iliyoimara na chachu katika kuongeza kasi ya maendeleo.
Dkt. Khalid amesisitiza jamii kuendelea kutumia njia za asili za uzazi wa mpango ambazo ni salama kwa afya ya mama na kuhudhuria katika Vituo vya afya kupata taaluma ya matumizi ya njia za kisasa pale inapohitajika.
Ameongeza kuwa suala la uzazi wa Mpango limesisitizwa hata katika Vitabu vya Dini ili kumpa nafasi Mama mzazi kurudisha afya na nguvu anazozitumia wakati wa kubeba mimba na kujifungua.
Kila ifikapo July 11, Zanzibar huungana na nchi zingine duniani kuadhimisha Siku ya Idadi ya Watu duniani ambapo kwa mwaka huu Kauli mbiu ni “Uzazi wa Mpango:Kuwawezesha Watu,kuendeleza Mataifa”
 Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na maadhimisho ya siku ya Idadi ya Watu duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo July,11. Kulia yake ni Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Zanzibar Juma Hassan Reli.
 Baadhi ya wandishi wa habari wakifuatilia mkutano wao na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed hayupo pichani uliofanyika wizarani kwake Mjini Zanzibar.
 Mwandishi wa habari wa Idara ya Habari Maelezo Faki Mjaka akiuliza swali kwa Waziri wa Fedha na Mipango juu ya siku ya Idadi ya Watu duniani katika mkutano uliofanyika Wizarani kwake Vuga.
 Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed akitoa ufafanuzi wa maswali alioulizwa na wandishi wa habari.
Picha na Makame Mshenga.

Tehama yaongeza ufanisi wa Utoaji wa huduma kwa wakazi wa mkoa wa Dodoma

Rais Magufuli amteua Prof. Florens D.A.M Luoga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TRA


MSTAAFU ATOA WITO WANANCHI KUJIUNGA NA PSPF KUPITIA UCHANGIAJI WA HIARI PSS, ASEMA AMEONA FAIDA ZAKE IKIWEMO BIMA YA AFYA

$
0
0

 Mwanachama mpya wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia Uchangiaji wa Hiari, (PSS), Bi. Sania M.Noor, akionyesha kadi yake ya uanachama baada ya kujiunga leo Julai 10, 2017, alipotembeela banda la Mfuko huo, lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, ambako kunafanyika maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MSTAAFU wa utumishi wa umma, Bi. Marcella Isidori Chanda, amewahimiza wananchi na wastaafu wenzake, kujiunga na Mfuko wa Pensehni wa PSPF, kupitia mpango wake wa uchangiaji wa Hiari, (PSS), kwani kuna faida nyingi mwanachama atazipata.

Bi. Chanda, ameyasema hayo muda mfupi baada ya kujiunga na Mpango huo wa PSS, leo Julai 10, 2017, baada ya kupatiwa elimu ya huduma zitolewazo na PSPF kwa wanachama wake.
“Mimi nilikuwa mtumishi wa benki na nimestafu mwaka 2013, ni meona iko haja ya kujiunga na mpango huu ambao hatimaye moja ya mambo yaliyonivutia ni kupatiwa bima ya afya, kwani nimeelzwakuwa ukiwa mwanachama wa PSS, basi unapata sifa za kujiunga na bima ya Afya, tofauti na ukiwa mtu binafsi gharama zinakuwa kubwa mno na zinafikia hadi shilingi 1,500,000nkwa mwaka.” Alisema Bi. Chanda.
Akieleza zaidi, Bi. Chanda alisema, amefikia uamuzi wa kujiunga naPSPF, baada ya kupata taarifa nyingi kupitia vyombo vya habari kuwa, lakini pia majirani na jamaa zngu kuwa wamekuwa wakifaidika na huduma ya afya kupitia bima ya afya.
Mstaafu huyo alsiema, leo amejiunga na PSS na pia atamueleza mumewe naye pia ajiunge. “Natoa wito wka wastaafu wenzangu na wananchi kwa ujumla kujiunga na PSPF ili kujihami na gharama za matibabu. Kwa upande wake, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi alisema, karibu asilimia 60 ya wananchi wanaofika kwenye banda hilo, wamekuwa wakijunga na Mpango wa PSS na moja ya sababu kubwa ni kupatiwa bima ya Afya.
Mwananchi akijaza fomu kujiunga na PSS
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani, (kulia), akizungumza jambo mbele ya Afsia Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi alipotembelea banda la Mfuko huo leo Julai 10, 2017.

 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma, wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Bi. Sarah Kibonde Msika, (kushoto) akimsikiliza Bw. Njaidi kwenye banda la PSPF, Julai 10, 2017. SSRA imeweka maafisa wake katika kila banda la Mifuko ya Hifadhio ya Jamii, ili kufuatilia utoaji huduma wa Mifuko hiyo kwa wananchi kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa huduma za Habari na Utangazaji wa Mamlaka ya Utangaza Tanzania, (TCRA), Bw. Freddyb Ntobi, (kulia), aimskiliza Bw. Njaidi alipotembeela banda la Mfuko huo.
 Afsia Msaidizi wa Uenddshaji wa PSPF, Bw. Win-God Simon, (kushoto), akiwahudumia maafisa hawa wa polisi ambao ni wanachama wa Mfuko.
 Mama huyu (kushoto), akiuliza kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na PSPF alipotembelea banda la Mfuko huo leo Julai 10, 2017.
 Afisa Uendeshaji wa PSPF, Bi. Irine Musetti, (kushoto), Afisa Mkuu wa TEHAMA wa Mfuko huo, Bi. Mariam Saleh, (katikati), na Afisa wa Sheria wa SSRA, Bi.Imani Masebu, wakijadiliana jambo kwenye banda la PSPF.
 Bereket S. Singili, (kushoto), akiangalia jinsi Afsia huyu wa PSPF, anavyomjazia fomu ya kujiunga na Mfuko huo kupitia PSS.
 Bw. Singili, (kushoto), akikabidhiwa kadi yake ya uanachama na Afisa wa Fedha wa PSPF, Bw.Msina


 Mhandis Ali Shanjirwa, (kushoto), wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, akimuhudumia mwananchi huyu aliyefika kwenye banda la Mfuko huo ili kupatiwa huduma
Afisa Uendeshaji wa PSPF, Bw. Noah, (kushoto), akitoa huduma kwa wananchi hawa waliofika banda la PSPF leo Julai 10, 2017.

WAZIRI LWENGE AKUTANA NA WAZIRI WA MAJI WA MISRI

$
0
0

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Misri, Dkt. Mohamed Abdel Aty (wa kwanza kushoto), akifuatiwa na Balozi wa Misri nchini Tanzania Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf (katikati) na Kansela wa Ubalozi wa Misri nchini Tanzania, Moataz Kareem.
le2Katibu Mkuu wa Wizara ya Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akizungumza akiwa na Mwenyekiti wa Sekta ya Maji ya Nile, Ahmed Bahaa Eldin Mohamed (kulia), Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge (kushoto) katika kikao.
le3Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akizungumza mbele ya ujumbe wa Misri na Tanzania katika kikao.
le4Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akiwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Misri, Dkt. Mohamed Abdel Aty na ujumbe wake katika sehemu ya mabanda katika Maonesho ya Sabasaba.
le5Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akikabidhiwa zawadi na mmoja wa wafanyabiashara kutoka Misri pamoja na Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Misri, Dkt. Mohamed Abdel Aty katika banda kwenye Maonesho ya Sabasaba.

…………………………………………………………………………………

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge amekutana na Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Misri, Dkt. Mohamed Abdel Aty kwa mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali za Tanzania na Misri katika utekelezaji wa miradi ya Sekta za Maji na Umwagiliaji.

Kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi za Wizara za Dar es Salaam kilihusisha mazungumzo ya utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano wa mataifa ya Misri na Tanzania, hususani katika utekelezaji wa miradi ya majisafi na kilimo cha umwagiliaji nchini kwa serikali hizo mbili.

Katika kikao hicho Inj. Lwenge alisema Tanzania na Misri ni mataifa yanayoshirikiana katika sekta mbalimbali, na kupitia ushirikiano huo lengo kubwa ni kuinua Sekta za Maji na Umwagiliaji.

“Kwa msaada wa Serikali ya Misri, serikali imefanikiwa kutekeleza mradi wa maji wa visima 30 kwa ajili ya uboreshaji wa huduma ya majisafi kwa wilaya kame za Same, Mwanga, Kiteto, Bariadi na Itilima kwa awamu ya kwanza na bado wapo katika mazungumzo ya kutekeleza miradi mingine mingi”, alisema Waziri Lwenge.

“Lakini pia tuna lengo la kuendeleza kilimo cha umwagiliaji, kwa kutumia teknolojia ya kisasa yenye kutumia maji kidogo na kuzalisha chakula kingi. Hivyo, kwa kushirikiana na wenzetu wa Misri wenye utaalamu wa hali ya juu, tunataka kufanikisha jambo hilo ili tuhakikishe usalama wa chakula na chakula kutosha kwa ajili ya wananchi”.

Inj. Lwenge alisema ushirikiano baina ya Serikali za Tanzania na Misri utaleta tija kwa Tanzania, hasa ikizingatiwa taifa hilo limepiga hatua kubwa katika Sekta za Maji na Umwagiliaji na kwa kubadilishana uzoefu, kutaisaidia Tanzania kupiga hatua kubwa katika sekta hizi muhimu kwa taifa katika kutizima azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania kuwa Nchi ya Viwanda.

Naye, Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Misri, Dkt. Mohamed Abdel Aty alisema wataendelea kudumisha uhusiano wake na  Tanzania kwa kuchangia maendeleo ya Tanzania kupitia ushirikiano kwenye sekta za maji, umwagiliaji na hata usafirishaji utakaoleta tija kubwa kwa ustawi wa mataifa haya.

Dkt. Abdel Aty aliambatana na ujumbe uliojumuisha Balozi wa Misri nchini Tanzania Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf, Mwenyekiti wa Sekta ya Maji ya Nile, Ahmed Bahaa Eldin Mohamed na Kansela wa Ubalozi wa Misri nchini Tanzania, Moataz Kareem, huku ujumbe wa Inj. Lwenge ukijumuisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo, Mkurugenzi Msaidizi wa Majishirikishi, Sylivester Matemu, Mkurugenzi Msaidizi Mipango na Utafiti, Dkt. George Lugomela na Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Simon Nkanyemka.

Aidha, Waziri Lwenge alimpeleka mgeni wake, Waziri Abdel Aty kutembelea Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa – Sabasaba, kwa nia ya kumuonyesha maendeleo ya Sekta ya Biashara nchini, yaliyovutia kampuni 25 kutoka Misri na kushiriki katika maonesho hayo.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JULAI 11, 2017

DKT. MPANGO ASHITUKIZA TRA NA VITUO VYA MAFUTA KIGAMBONI NA KUTOA MAAGIZO MAZITO

$
0
0

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt. Philip Isdor  Mpango  (Mb)  akiongea na mmoja wa wananchi (anayemuonesha karatasi ) waliofika kulipa kodi ya majengo katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) – Kigamboni, ambapo alieleza kuridhishwa na utendaji wa watumishi katika mamlaka hiyo.
mafu2
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), aliyevaa miwani na kukunja mikono, akiwa amejichanganya katika kundi la wakazi wa mji wa Kigamboni waliojitokeza kulipa kodi ya majengo katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania-Kigamboni, akiwa na lngo la kuchunguza namna wananchi wanavyopata huduma.
mafu3
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt. Philip Isdor Mpango  (Mb) (kulia) akisalimiana na mmoja wa wakazi wa Mji wa Kigamboni waliojitokeza kulipa kodi katika Ofisi za mamlaka ya mapato Tanzania TRA-Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
mafu4
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Msaidizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Hussein Shah alipotembelea ofisi za Mamlaka hayo, Kigamboni, Jijini Dar es Salaam.
mafu5
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt. Philip Isdor Mpango  (Mb) (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Ukaguzi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA-Bw. Beatus Nchota (kulia) wakati Dkt. Mpango alipotefanya ziara ya kushitukiza katika Ofisi za TRA-Kigamboni, Jijini Dar es Salaam kujionea utendaji kazi wa Mamlaka hayo wakati wananchi wakijitokeza kwa wingi kulipa kodi ya majengo. Katikati ni Afisa wa (TRA) Bw. Theraphin Mbwambo.
mafu6
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt. Philip Isdor  Mpango  (Mb), akiwapongeza na kuwashukuru wananchi wa Kigamboni waliojitokeza kulipa kodi ya majengo na kutoa rai kwa wananchi kujenga utamaduni wa kulipa kodi kwa hiari ili kufikia uchumi wa viwanda na kuendesha huduma za jamii.
mafu7
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akimsikiliza Msimamizi wa Kituo cha Mafuta cha Mjimwema, Kigamboni Jijini Dar es Salaam, Bw. Yusuph Abbass baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika kituo hicho na kubaini kuwa mashine za kielektroniki za kutolea risiti hazitumiki.
mafu8
Moja kati ya  Mashine mbili za Kielektroniki zilizofungwa katika Kituo cha Mafuta cha Mjimwema Kigamboni, Jijini Dar es Salaam lakini hakitumiki baada ya kudaiwa zimeharibika, na kumfanya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, kuamuru Kituo hicho kifungwe hadi mashine hizo zitakapoanza kufanyakazi.
mafu9
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akimsikiliza Msimamizi wa Kituo cha Mafuta cha Mjimwema, Kigamboni Jijini Dar es Salaam, Bw. Yusuph Abbass baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika kituo hicho na kubaini kuwa mashine za kielektroniki za kutolea risiti hazitumiki.
mafu10
Moja kati ya  Mashine mbili za Kielektroniki zilizofungwa katika Kituo cha Mafuta cha Mjimwema Kigamboni, Jijini Dar es Salaam lakini hakitumiki baada ya kudaiwa zimeharibika, na kumfanya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, kuamuru Kituo hicho kifungwe hadi mashine hizo zitakapoanza kufanyakazi.
…………………………………………………………………………………
Benny Mwaipaja, WFM-Dar es Salaam
Wakazi wa Kigamboni mkoani Dar es Salaam, wameiopongeza Serikali kwa kusimamia vizuri masuala ya kodi na kwamba wako tayari kuiunga mkono Serikali kwa kulipa kodi kwa hiari ili iweze kutimiza malengo yake ya kuwahudmia wananchi kimaendeleo.

Wametoa kauli hiyo wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, alipofanya ziara ya kushitukiza kwenye Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Kigamboni, ili kujionea zoezi la wakazi wa Mji huo wanavyolipa kodi ya majengo na kutembelea baadhi ya vituo vya mafuta ili kuona kama wamiliki wanatoa risiti ipasavyo kwa wateja wao.

Wakitoa maoni yao kuhusu zoezi hilo la kulipa kodi ya majengo, wakazi hao wameelezea kuridhishwa na huduma wanayopata kutoka kwa wafanyakazi wa TRA na kuiomba Serikali iangalie namna ya kuongeza muda wa kulipa kodi hiyo kutokana na mwamko mkubwa uliopo hali inayoonesha kuwa huenda baadhi yao wasikamilishe zoezi hilo ifikapo Julai 15 Mwaka huu.

“Ninampongeza sana Mhe. Rais kwa kutupatia Waziri huyu (Dkt. Mpango), anajibu vizuri na kwa kuamua kututembelea, pia wafanyanyakazi wa TRA wanatuhudumia vizuri sana, tunakushukuru Mhe. Waziri” alisema kwa furaha Bi. Mary Laizer, Mkazi wa Kigamboni

Akizungumza na wakazi hao, Dkt. Philip Mpango amewafikishia watanzania salaam na pongezi za Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna walivyoitikia wito wa kulipa kodi na kwamba hatua hiyo itaiwezesha Serikali kuboresha huduma za jamii kama afya, elimu, maji na miundombinu mbalimbali kutokana na mapato ya kodi hizo

“Mkiona barabara zinajengwa, tunafanya jitihada kuongeza dawa hospitalini, kulipa wanajeshi wetu ili watulinde usiku wakati sisi tumelala, inatokana na nguvu tunayoipta kutoka kwenu kupitia kodi” alisisitiza Dkt. Mpango.

Alisema kuwa amekwenda Kigamboni kuwashukuru wakazi wa Mji huo kwa mwitikio wao mkubwa wa kulipa kodi hususan ya majengo kwa hiari na kuangalia changamoto zinazokabili zoezi la ukusanyaji kodi ikiwemo msongamano mkubwa wa watu na kugundua uhaba wa baadhi ya vitendeakazi kama vile kompyuta na watumishi

Kwa upande wake Meneja Ukaguzi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Beatus Nchota, alitoa wito kwa Watanzania kuendeleza moyo huo wa kulipa kodi kwa hiari hata kwenye kodi nyingine za biashara ili Serikali iweze kupata mapato ya kutosha ya kuwahudumia wananchi wake.
Wakati huo huo Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, 

ameamuru kufungwa kwa kituo cha Mafuta cha Mawenzi kilichoko Kigamboni hadi mmiliki wake atakaporekebisha kasoro baada ya kubaini kuwa mashine maalumu za Kieletroniki zilizofungwa kwenye pampu za mafuta kwa ajili ya kutolea risiti hazitumiki, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Akiwa katika kituo hicho cha mafuta, Dkt. Mpango alishuhudia mashine mbili za kielekroniki zikiwa hazifanyikazi badala yake wahudumu wanatumia mashine za kieletroniki za kawaida ambazo haziwezi kupima kiwango cha mafuta kinachotoka kwenye pampu za mafuta hatua mabayo inaikosesha serikali mapato yake halisi.
Msimamizi wa Kituo hicho Bw. Yusuph Abbass alisema kuwa mashine hizo zote mbili zilipata hitilafu juma moja lililopita na kulazimika kutumia mashine za EFD za kawaida jambo ambalo lilipingwa na Waziri Dkt. Mpango kwa kuwa ni kinyume cha taratibu na sheria na maelekezo ya Serikali.
Kufuatia hatua hiyo Dkt. Mpango ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuvikagua na kuvifunga vituo vyote vya mafuta nchini ambavyo havijafunga machine hizo za kutolea risiti kama wamiliki wake walivyoagizwa na Serikali tangu mwaka jana hatua ambayo inaikosesha Serikali mapato yake.

Masauni aliagiza Jeshi la Polisi kufungua kituo makazi ya kabila la Wahadzabe

$
0
0

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Flatei Massay (wapili kulia) wakicheza ngoma ya Wabarbaig/Watatoga kabla ya Masauni kuzungumza na mamia ya wananchi wa Kabila maarufu la Wahazabe na makabila mengine yaliyopo katika Bonde la Yueda Chini, Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara. Masauni aliiagiza Jeshi la Polisi mkoani humo, kujenga Kituo cha Polisi kwa uharaka ili jamii hiyo ambayo inaishi pembezoni mwa mji wa Mbulu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
HAZA2
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na mamia ya wananchi wa Kabila maarufu la Wahazabe na makabila mengine yaliyopo katika Bonde la Yueda Chini, Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara. Masauni aliiagiza Jeshi la Polisi mkoani humo, kujenga Kituo cha Polisi kwa uharaka ili jamii hiyo iweze kupata ulinzi wa kutosha katika eneo hilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
HAZA3
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akijadiliana na maafisa wa halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara pamoja na watendaji mbalimbali wa wilaya hiyo, ndani ya jengo la mifugo lililopo Yaeda Chini katika makazi ya Wahazabe, ambalo linatarajiwa kufunguliwa Kituo cha Polisi. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Manyara (RPC), Francis Massawe, na kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Flatei Massay. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
HAZA4
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwafafanulia jambo Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Flatei Massay (kulia) na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mjini, Zakaria Isaay mara baada ya Naibu waziri huyo kukagua Jengo la Mifugo (nyuma yao) ambalo linatarajiwa kufunguliwa Kituo cha Polisi ili kuwasaidia wananchi wa kabila la Wahazabe na wengineo wanaoishi katika Bonde la Yueda Chini, Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara kuleta ulinzi wa raia hao pamoja na mali zao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
HAZA5
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Francis Massawe alipokuwa akijibu maswali mbalimbali ya uhalifu ambayo yaliulizwa na wananchi (hawapo pichani) wa Kijiji cha Yueda Chini Wilaya ya Mbulu mkoani humo, ambalo kuna makazi ya jamii ya Kabila la Wahazabe.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
HAZA6
Wananchi wakimshangilia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati alipowatangazia kufunguliwa Kituo cha Polisi hivi karibuni katika Kijiji cha Bonde la Yueda Chini, lililopo wilayani Mbulu, Mkoa wa Manyara. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
…………………………………………………………..
Na Felix Mwagara (MOHA)
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amelitaka Jeshi la Polisi mkoani Manyara kufungua Kituo cha Polisi katika Makazi ya Kabila la Wahazabe wanaoishi katika Bonde la Yueda Chini, wilayani Mbulu.
Masauni alisema hayo jana wakati akizungumza na mamia ya wananchi wa kabila  hilo mara baada ya kukagua jengo la mifugo katika eneo la bonde hilo ambalo jamii hiyo ilijitenga kwa kuweka makazi pembezoni mwa Mji wa Mbulu.
“Hivi karibuni Kituo cha Polisi kitafunguliwa hapa ili kulinda usalama wenu katika eneo hili ambalo lilikua halina kituo cha Polisi kwa miaka mingi. Serikali ya Rais Magufuli ni sikivu ndio mana nimekuja hapa kuwasikiliza matatizo yenu na kuwatekelezea.” Alisema Masauni huku akishangiliwa na wananchi hao.
Aliongeza kuwa, mchakato wa kujenga kituo hicho umeanza na tayari ametoa maelekezo kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa huo, kwa kushirikiana na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Wabunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini na Mbulu Mjini.
 Pia aliongeza kuwa, uhalifu katika eneo hilo sasa umepata tiba kwa maana Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi watahakikisha hali ya usalama unaimarishwa zaidi katika eneo hilo ambalo lipo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Flatei Massay alisema wananchi wa jimbo lake wanavamiwa, wanaporwa mali zao ikiwemo mifugo, wanajeruhiwa na wanaingizwa katika umaskini zaidi kutokana na waalifu kuwa wengi kutokana na ukosefu wa Kituo cha Polisi.
“Nilimuomba na nilimsumbua sana Naibu Waziri kule Bungeni ili aweze kufika katika eneo hili, ninamshukuru sana kwa kufika na kutoa maelekezo ya kufunguliwa kituo cha polisi, sasa wakazi wa eneo hili tunatarajia kupata ulinzi wa kutosha baada ya kituo hicho kufunguliwa hivi karibuni,”alisema Massay.
Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Francis Massawe alisema amepokea maelekezo kutoka kwa Naibu Waziri na mchakato utaanza rasmi na hatimaye kituo cha Polisi kitakuwepo katika eneo hilo na wananchi wataendelea na shughuli zako za kutafuta mahitaji yao kwa usalama zaidi.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images