Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

DC- TABORA AONGOZA ZOEZI LA KUWAONDOA WAKULIMA WA MBOGA MBOGA WAVAMIZI WA BWAWA LA IGOMBE.

0
0

Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Tabora imeendesha oporesheni ya kung’oa mazao mbalimbali ya bustani yaliyokuwa yamepandwa na wavamizi katika maeneo ya vyanzo vya maji na kando kando ya Bwawa la Igome na hivyo kusababisha uzalishaji wa maji kupungua.

Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mwalimu Queen Mlozi iliendesha zoezi hilo jana mjini hapa baada ya kugunduliwa kuwepo kundi kubwa la watu wanaondeshea kilimo cha mazao mbalimabli ikiwemo matunda na kuhatarisha afya ya watumiaji.

Katika oporesheni hiyo mazao mbalimbali kama vile majani ya maboga, hoho, nyanya na matembele yaliweza kung’olewa.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya zoezi alisema kuwa wavamizi hao wakiendesha shughuli mbalimbali katika vyanzo vya Bwawa hilo ikiwemo kilimo cha mboga mboga na wakati mwingine wamekuwa wakiweka dawa ambazo wakati mwingine dawa hizo zimekuwa zikiingia katika maji hayo ambayo ndio wakazi wengi wa Wilaya ya Tabora wanatumia.

Mwalimu Mlozi aliongeza kuwa endapo maji hayo yasipowekewa dawa vizuri ya kusafisha upo uwezekano wa watumiaji kunywa dawa na kilimo zilizotoririkia majini.Aliongeza kuwa hali ya maji katika Bwawa hilo sio nzuri na endapo wavamizi hao wasipodhibitiwa upo uwezekano mkubwa wa wakazi wa Manispaa ya Tabora kukabiliwa na upungufu wa maji katika miezi ijayo.

Mkuu wa Wilaya huyo aliwaonya wavamizi hao kutorudi tena katika eneo hilo kwani atakayekamatwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya alisikitishwa na kitendo cha baadhi ya watu kuvijisha siri ambayo ilipelekea wavamizi hao wakimbie kabla ya kutiwa nguvuni.

Alisema wakati watakapotaka kuendesha zoezi la pili itabidi aende kwa kushitukiza bila kupanga kwa zoezi hilo kwa muda mrefu.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Tabora(TUWASA) Christopher Shinyanza alisema kuwa mavamizi hao wamesababishia kina cha maji kimepungua na kusababisha gharama uzalishaji wa ili yamfikie mtumiaji yakiwa safi bila kuwa na tope lilitokana na kilimo kando kando ya bwawa hilo.

Aliongeza kuwa shughuli za kilimo katika vyanzo vya maji vya bwawa hilo zimesababisha kupungua uzalishaji wa maji kwa ajili ya matumizi kwa wakazi wa Manispaa ya Tabora hasa kipindi hiki cha kiangazi ukilinganisha na kipindi cha masika.

Bwana Shinyanzi Alisema kuwa wakati wa masika kwa sababu ya kupata mvua kuwepo waliweza kuzalisha wastani mita za ujazo 16,500 ambazo kwa kiasi kikubwa yalikuwa yakitosha , lakini kwa hivi sasa kutokana na kuongezeka kwa shughuli za kilimo katika Bwawa hilo , hivi sasa wanazalisha mita za ujazo 11,000.

Alisema kuwa wamekuwa wakipita mara kwa mara lakini bado kumekuwepo na tatizo hilo la wavamizi kuendelea kuendesha kilimo hicho na kuathiri upatikanaji wa maji ya kutosha.

Kaimu Mkurugenzi huyo Mtendaji wa TUWASA alitoa wito kwa wananchi wenye mapenzi mema kuwafichua watu wanaoendesha kilimo katika eneo hilo kwa sababu kitendo cha kuendelea kuwaficha kinasababisha athari kwa wakazi wengi wa Manispaa ya Tabora kwa faida ya wachache.

Mwisho wa wiki Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri alikiwahotubia wananchi katika eneo la Soko Kuu aliwatahadharisha wananchi uwezekano wa Bwawa la Igombe kukauka kutokana shughuli za uharibifu wa mazingira ambazo ni ukataji miti ovyo ,uchomaji moto, kilimo cha kuhama hama na idadi kubwa ya mifugo katika vyanzo vya maji.
 Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mwalimu Queen Mlozi (aliyeshika miche ya nyanya) akiongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo kung’oa na kuwaondoa wakulima wa bustani walivamia kando kando ya Bwawa la Igombe na kusababisha uharibifu wa vyanzo vya maji vya Bwawa hilo. Zoezi hilo lilifanyika jana katika eneo la Bwawa hilo. 
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mwalimu Queen Mlozi (wa kwanza kushoto) akiongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo kung’oa na kuwaondoa wakulima wa bustani walivamia kando kando ya Bwawa la Igombe na kusababisha uharibifu wa vyanzo vya maji vya Bwawa hilo. Zoezi hilo lilifanyika jana katika eneo la Bwawa hilo.
Picha na Tiganya Vincent-RS  - Tabora

WAZIRI MKUU ATEMBELEA UJENZI WA DARAJA MTO LUKULEDI

0
0
*Asema watu wengi wamekufa wakikatiza katika eneo hilo

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa ujenzi wa daraja la mto Lukuledi lenye urefu wa kilomita 30.45 linalounganisha mikoa ya Lindi na Mtwara na na kusema kwamba ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wake.

Amesema ujenzi wa daraja hilo unatakaogharimu sh. bilioni 5.4 ni mkombozi kwa wananchi wa mikoa hiyo hasa wa wilaya za Ruangwa na Masasi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakishirikiana katika masuala mbalimbali yakiwemo kilimo na huduma za kijamii. 

Waziri Mkuu amesema hayo leo (Jumanne, Julai 11, 2017) alipotembelea mradi huo wa ujenzi wa daraja hilo katika kijiji cha Nandanga alipowasili wilayani Ruangwa akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi.

“Watu wengi wamepoteza maisha kwa kuliwa na mamba walipokuwa wakikatiza katika eneo hilo. Ujenzi wa daraja hili ni muhimu, watu wengi wa Ruangwa wanavuka kufuata matibabu katika hospitali ya Ndanda, wilayani Masasi na wakazi wa Ndanda wanavuka kufanya shughuli za kilimo wilayani Ruangwa.”

Pia Waziri Mkuu amewaomba wananchi wa maeneo hayo kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa mkandarasi anayejenga daraja hilo ili aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kumaliza mradi huo kwa wakati.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Ndanda, Mheshimiwa Cecil Mwambe ameipongeza na kuishukuru Serikali kwa jitihada zake za kuwaletea wananchi maendele0 na kubadilisha maisha yao.

Amesema mradi wa ujenzi wa daraja hilo ni faraja kwa wananchi wa mikoa hiyo kwa kuwa eneo hilo ni makazi ya mamba, hivyo kukamilika kwake kutaokoa maisha ya watu pamoja na kurahisisha usafiri wa watu na bidhaa.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vijiji vya Litama, Luchelegwa, Nandanga, Ipingo na Chiapi kuwa historia baada kuungwanishwa na mradi wa maji wa Mbwinji.

Ameyasema hayo leo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Litama, Chiapi, Nandanga, Luchelegwa alipowasili wilayani Ruangwa akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi.

Waziri Mkuu amesema Serikali inatekeleza Kampeni yake ya kumtua mama ndoo, hivyo itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini, hususan ni ya vijijini wanapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400.

Ameitoa kauli hiyo baada ya wananchi wa vijiji hivyo kumueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye maeneo yao zikiwemo za maji, barabara, umeme, ambapo aliwahakikishia kwamba Serikali imeshaanza kuboresha huduma hizo.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amezindua Zahanati ya Nandanga ambayo imejengwa kwa fedha kutoka mfuko wa jimbo umegaharimu kiasi cha sh. milioni 73.47 na kuwahakikishia kwamba Serikali itawapelekea wataalam wa kutosha ili kuwahudumia.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, JULAI 11, 2017
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo ya mradi wa daraja la Nandaga, linalo unganisha Wilaya ya Ruangwa na Wilaya ya Masasi, kutoka kwa Mhandisi Josam Mlaki, kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) . 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua mradi wa daraja la Nandaga, linalo unganisha Wilaya ya Ruangwa na Wilaya ya Masasi, kutoka kwa Mhandisi Josam Mlaki, kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

JAFO AWATAKA WAHANDISI KUSIMAMA IMARA KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI

0
0
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewataka wahandisi wa Halmashauri nchini kutumia taaluma zao ipasavyo katika usimamizi wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu katika halmashauri zao.

Jafo aliyasema hayo leo alipokuwa katika ziara maalum ya ukaguzi wa miradi ya barabara na madaraja katika Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.

Katika ziara hiyo, Jafo alikagua ujenzi wa barabara ya Lami ya kilometa moja katika mji wa Bahi inayojengwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kupitia mfuko wa barabara.

Jafo alisema maagizo ya kuzingatia ubora wa barabara inayo jengwa ili iweze kudumu kwa muda ulio kusudiwa.Katika ukaguzi wa madaraja, Jafo alikagua ujenzi wa madaraja mawili ya Nkulugano na Chipanga pia daraja la barabara ya Chipanga- Kigwe yanayojengwa kwa mradi maalum wa kuondoa vikwazo kwa ufadhili wa fedha za DFID.

Jafo alimpongeza mhandisi wa halmashauri ya Bahi Eng. Geofrey Mkinga kwa usimamizi mzuri wa kazi hizo zinazoendelea.Akihitimisha ziara yake, Naibu Waziri Jafo aliwataka wahandisi wa halmashauri zote hapa nchini kusimamia ubora wa kazi za ujenzi kwa umakini na kuweka mbele maslahi ya Taifa.

Madaraja hayo mawili yanatarajiwa kukamilika mwezi oktoba mwaka huu na yatakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wanaotumia barabara hizo.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Bahi Omary Badwel ameishukuru sana serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk.John Magufuli kwa kuwa madaraja hayo yalikuwa ni kikwazo kikubwa sana kwa maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa daraja la Chipanga. 
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua daraja la Nkulugano ambalo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 95.
 Sehemu ya daraja hilo 
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa barabara ya lami mji Bahi huku akitoa maelekezo kwa wataalam kuhakikisha ujenzi huo unazingatia viwango ili kudumu kwa muda mrefu. 

DKT. PHILIP MPANGO ATATUA CHANGAMOTO YA MSONGAMANO WA WALIPAKODI TRA VINGUNGUTI DAR ES SALAAM

0
0
Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, eneo la Vingunguti Jijini Dar es Salaam na kuagiza kuongezwa kwa wafanyakazi na vitendea kazi katika ofisi hiyo baada ya kukuta msongamano mkubwa wa watu waliojitokeza kulipa kodi ya majengo.

Dkt. Mpango ambaye alitumia muda wake mwingi kusikiliza kero za baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kulipa kodi hiyo, ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania kuongeza wafanyakazi kumi pamoja na mashine za kieletroniki za kukusanyia kodi pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa kuwahudumia wazee na watu wenye ulemavu.

“Nimeagiza wafanyakazi waongezwe, viti 50 kwa ajili ya kutumiwa na wazee pamoja na akina mama wenye watoto vitaletwa, pamoja na kuongeza mashine za kielektroniki 5 kutoka 3 zilizokuwepo ambapo sasa zitakuwa mashine 8, hatua hii itaondoa changamoto hii” alifafanua Dkt. Mpango

Amerejea pongezi zake kwa Watanzania kwa kujitokeza kwa wingi kila mahali nchini kote kulipa kodi ya majengo akikielezea kitendo hicho kuwa ni cha kizalendo na kitaisaidia nchi kuondokana na umasikini kwa kuwa itakuwa na uwezo wa kuwahudumia wananchi wake kikamilifu.

Dkt. Mpango amewahakikishia Wazee waliotimiza umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea kwamba Serikali imewaondolea kodi ya majengo kwenye nyumba zao wanazoishi kutokana na kutambua mchango wao mkubwa katika kulitumikia Taifa wakati wa ujana wao.

Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kulipa kodi katika Ofisi hiyo ya TRA, Vingunguti, wamepongeza utaratibu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango wa kuwajibika na kutumia muda wake kuwatembelea na kuwahudumia wananchi na pia wamemmwagia sifa kem kem Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa hamasa kubwa aliyowapa na kwamba wako tayari kumuunga mkono kwa hali na mali ili nchi ipate maendeleo kwa haraka.

 Matukio mbalimbali ya picha zikionyesha Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akifanya ziara za kushitukiza katika maeneo muhimu kwa lengo la kuangalia utaratibu wa ulipaji kodi mbalimbali hususan ya majengo na vituo vya mafuta ili kubaini kasoro mbalimbali na kutoa maelekezo masuala muhimu anayoyabaini ambapo jana alikuwa Kigamboni, Jijini Dar es Salaam.
kob2kob3kob4kob5kob6kob7kob8kob9

DARAJA LA MTO KALAMBO LAKAMILIKA

0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa Mkandarasi anayejenga Kituo cha Mzani cha Singiwe Kilichopo katika barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga Port (112KM) Mkoani Rukwa wakati alipokagua ujenzi huo Mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Katikati) akipanda katika Daraja la Mto Kalambo Mkoani Rukwa wakati alipokagua daraja hilo ambalo ujenzi wake umekamilika.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili kulia) akikagua Daraja la Mto Kalambo Mkoani Rukwa wakati alipokagua daraja hilo ambalo ujenzi wake umekamilika.Wa kwanza ni Meneja wa Wakala wa barabara (TANROADS) Rukwa Eng. Msuka Mkina
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili) akielekeza jambo kwa Msimamizi wa bandari ya Kigoma,Bw. Morris Mchindiuza (Wa kwanza) wakati alipokagua huduma za bandari ya Katanga Mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili kulia) akipokea taarifa ya ujenzi ya barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasnga Port (112KM) Mkoani Rukwa wakati alipokagua ujenzi huo Mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (aliyenyoosha kidole) akiongea na wakazi wa kijiji cha Katete Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa wakati alipokagua barabara ya Matei-Kasesya (KM).


………………………………………………………………………………….

Serikali kupitia Wakala wa barabara nchini TANROADS mkoa wa Rukwa imekamilisha ahadi yake kwa wananchi ya kuwapunguzia changamoto ya usafirishaji wa abiria na mzigio kwa kukamilisha ujenzi wa Daraja la mto Kalambo pamoja na barabara ya Sumbawanga Matai hadi Kasanga port (112km) ambapo Kilomita 71.4 zimeshawekwa lami.

Akizungumza mara baada ya kukagua daraja na barabara hiyo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutafungua fursa za kiuchumi kwa wananchi wa mkoa Rukwa na nchi nyingine za jirani ikiwemo Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi.

“Tuliwaahidi wananchi kujenga darala na barabara hii ili wafanyabiashara na wakulima waweze kusafirisha bidhaa na mazao yao kwenda katika masoko kwa wakati na hivyo kukuza uchumi wao binafsi na taifa kwa ujumla,” ameaema Eng. Ngonyani.

Ameongeza kuwa chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli Serikali itahakikisha ndani ya kipindi cha miaka mitano inakamilisha ahadi zote walizoahidi kwa wananchi ili wananchi wanufaike na Serikali yao.

“Serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli ipo kwa ajili ya wananchi wote, na sisi kama wasimamizi tuliopewa dhamana kwenye Wizara tutahakikisha kile tulichokiahidi kwa wananchi tunakitekeleza kwa wakati ili wananchi wanufaike na uchumi wa nchi ukue,” amesisitiza Eng. Ngonyani.

Kwa upande wake Meneja wa Tanroads Rukwa amewataka wananchi kutunza miundombinu ya barabara na kuacha vitendo vya kung’oa alama za barabarani ambazo zimewekwa ili kuongeza usalama kwa madereva katika matumizi ya barabara hizo.

“Tumeweka alama hizi barabarani kwa ajili ya kuongoza madereva wanaotumia barabara ili kuepusha ajali zinazoweza kutokea kwa kutokuwepo na alama za tahadhari, hivyo ni wajibu wenu kuzilinda na kuzitunza kwani zipo kwa faida yetu sote,” amesema Eng. Msuka Mkina

Katika hatua nyingine Waziri Ngonyani amekagua huduma za bandari ya Katanga ambapo amesema Serikali itaendelea kuziboresha bandari zilizopo ukanda wa ziwa Tanganyika ili kuvutia wasafirishaji wa mizigo mikubwa kutumia bandari hizo.

“Tutaendelea kuimarisha miundombinu ya bandari ya Kalema, Kigoma na Katanga ili ziwe na uwezo wa kupakia na kupakua mizigo mikubwa kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi,” amesisitiza Eng. Ngonyani.

Naye Msimamizi wa Bandari Mkoa wa kigoma, Bw. Morris Mchindiuza amesema Mamlaka ya bandari TPA imejipanga na imetenga kwenye bajeti yake kiasi cha Sh. bilioni 1 kwa ajili ya upanuzi wa Gati namba moja na hivyo kuchochoa ukuaji wa wa kibiashara na ongezeko la Meli hususani nchi za jirani kama Burundi na DRC Congo.

Naibu Waziri Eng. Ngonyani yupo katika Ziara ya kukagua Miundombinu ya barabara, Viwanja vya Ndege, Ujenzi wa Nyumba za viongozi, huduma za mawasiliano ya simu, Bandari na Madaraja katika Mkoa wa Rukwa

WAZIRI MPANGO AKIFUNGIA KITUO CHA MAFUTA CHA GBP ENEO LA UWANJA WA NDEGE DAR ES SALAAM

0
0



Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (aliyevaa tai) akimhoji mmoja wa wahudumu wa Kituo cha mafuta cha GBP kilichopo karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kabla ya kukifunga kwa kosa la kutotumia Mashine za kierektroniki za EFDs.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akitoa agizo kwa msimamizi wa Kituo cha Mafuta cha GBP kilichopo karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nerere kukifunga maramoja kwa kutofuata maagizo ya Serikali ya kutumia Mashine za EFDs kwenye vituo vya Mafuta.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akizungumza na baadhi ya wakazi wa maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere pamoja na wamiliki wa vyombo vya moto kuhusu umuhimu wa kudai risiti wanaponunua mafuta kwenye vituo vya mafuta, wakati alipokifunga Kituo cha Mafuta cha GBP, baada ya mmiliki wake kubainika kukiuka masharti kwa kutotoa risiti za kielektroniki (EFD)kwa wateja wake.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akiwa katika mitaa ya maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, akizungumza na baadhi ya wakazi wa maeneo hayo kuhusu umuhimu wa kudai risiti wanaponunua mafuta kwenye vituo vya mafuta na kuitaarifu Serikali wanapobaini wamiliki wa vituo hivyo hawatoi risiti za EFD.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia) akizungumza na wananchi waliokuwepo karibu na kituo cha mafuta cha GBP kuhusu umuhimu wa kudai risiti kwa maendeleo ya Taifa. Mazungumzo hayo yalifanywa muda mfupi baada ya kufungwa kwa kituo hicho kwa kosa la kutotumia mashine za kielektroniki za EFDs.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akizungumza jambo wakati akishuhudia Mashine ya Kielektroniki iliyofungwa katika Kituo cha Mafuta cha Puma kilichopo karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ikitoa risiti na kukipongeza kituo hicho kwa kufuata taratibu za Serikali za kutumia Mashine hizo.
Kulia ni Ally Gidai Mkazi wa Vingunguti akimueleza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) kero wanayoipata katika vituo vya mafuta ambavyo havitoi risiti kwa kutumia Mashine za kielektroniki za EFDs. Hii ni baada ya Waziri huyo kueleza umuhimu wa kudai risiti katika vituo vya mafuta.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (mwenye miwani) akizungumza na wananchi pamoja na wafanyakazi wa Kituo cha Mafuta cha Puma, kuhusu umuhimu wa kutoa na kudai risiti baada ya kukagua kituo hicho na kuridhika namna mashine za kieletroniki za kutolea risiti zinavyofanyakazi ipasavyo.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

……………………………………………………………………………………

Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kuamuru kituo cha Mafuta cha GBP kifungwe hadi hapo kitakapo funga mashine maalumu za kutolea risiti baada ya kubainika hakitumii ipasanyo mashine za kieletroniki za kukusanyia kodi (EFD)

Dkt. Mpango amechukua hatua hiyo baada ya kujionea kituo hicho kikiwa na pampu nne za mafuta lakini kuna mashine moja pekee ya mkononi ya kutolea risiti jambo linasababisha wateja wao wengi kutopewa risiti na hivyo kuikosesha Serikali mapato yake na ni kinyume cha sheria za nchi.

“Sasa nawachukulia hatua ili liwe fundisho kwa wengine wote wanaouza mafuta nchini bila kufuata taratibu, na nitaanza na wewe, biashara yako isimame mpaka mashine zifungwe kwenye kituo chote na utekeleze mara moja” alisistiza Dkt. Mpango

Katika ukaguzi wa Kituo cha Mafuta cha Puma, Dkt. Mpango amesifu utaratibu mzuri uliowekwa na kituo hicho kwa kufunga mashine maalumu za kutolea risiti zilizounganishwa na kila pampu za mafuta kitu ambacho ndicho Serikali inavitaka vituo vyote vya mafuta vitumie mfumo huo

“Kituo hiki kimezingatia sheria sheria kwa kufunga mashine kwa kuzingatia maelekezo ya Serikali na hapa tunauhakika wa kupata fedha za kuwatumikia wananchi, kinyume kabisa na kituo cha mafuta nilichokifungia, hapa ndio ningeomba Watanzania wanunue mafuta” aliongeza Dkt. Mpango.

Ameiagiza Mamlaka ya mapato Tanzania-TRA kufanya ukaguzi nchi nzima ili kubaini wamiliki wa vituo vya mafuta wanaokiuka maagizo ya Serikali yaliyowataka wafunge mashine hizo maalumu tangu mwaka uliopita.

Waziri wa Fedha na Mipango amewageukia wenye vyombo vya moto wanaonunua mafuta kwenye vituo vya mafuta kote nchini kudai risiti wanapopata huduma ya kuwekewa mafuta kwenye vituo hivyo ili kuokoa fedha za Serikali zinazoishia mikononi mwa wajanja wachache wanaokwepa kodi kwa makusudi na kuikosesha Serikali mapato yake.

Baadhi ya wananchi wamepongeza uamuzi wa Serikali kupitia Waziri wa Fedha na Mipango wa kufanya ziara za kushitukiza kwenye vituo vya mafuta na kutaka hatua hiyo iwe endelevu kwa maafisa wengine wa Serikali ili kukomesha vitendo vya wenye vituo vya mafuta kukwepa kodi ya Serikali

Katika siku yake ya kwanza ya ziara za namna hiyo, Julai 10 mwaka huu, Dkt. Mpango alikifungia kituo cha Mafuta cha Mawenzi kilichoko Kigamboni, Jijini Dar es Salaam baada ya kubaini kuwa kituo hicho kimefunga mashine maalumu za kutolea risiti za kielektroniki lakini hazitumiki na kuamuru kituo hicho kifungwe hadi kitakapo rekebisha kasoro hiyo na kuvionya vituo vya mafuta vya OilCom kufunga mashine za aina hiyo mara moja.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMATANO LEO JULAI 12,2017

0
0


Kagera yote kupata umeme wa uhakika 2021, Bilioni 45.43 kutumika sehemu ya kwanza ya mradi

0
0
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Kagera uliofanyika katika kijiji cha Rwabigaga wilayani Kyerwa. Kulia kabisa ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Kagera uliofanyika katika kijiji cha Rwabigaga wilayani Kyerwa. Kulia kabisa ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga na kushoto ni Mbunge wa Kyerwa, Innocent Bilakwate.
Waliosimama ( kuanzia wa pili kutoka kulia mbele), Mbunge wa Kyerwa, Innocent Bilakwate, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Dkt. Gideon Kaunda wakiwa katika picha ya pamoja na wanakijiji wa Rwabigaga wilayani Kyerwa mkoani Kagera mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Kagera uliofanyika kijijini hapo mapema Julai 11, 2017
Mbunge wa Kyerwa, Innocent Bilakwate akielezea hali ya upatikanaji wa nishati ya umeme katika wilaya ya Kyerwa kwenye uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, akielezea utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) kwenye uzinduzi huo.
Waliokaa meza kuu mbele kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, Mbunge wa Kyerwa, Innocent Bilakwate pamoja na watendaji wengine kutoka serikalini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na wakandarasi wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga (hayupo pichani) kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Dkt. Gideon Kaunda akisisitiza jambo kwenye uzinduzi huo.
Sehemu ya Mameneja kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika wilaya za Karagwe, Ngara, Misenyi, Muleba na Biharamulo wakifuatilia hotuba ya uzinduzi iliyokuwa inatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) kwenye uzinduzi huo.

Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Rwabigaga wilayani Kyerwa mkoani Kagera wakishangilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) kwenye uzinduzi huo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akisisitiza jambo kwenye uzinduzi huo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akitoa maelekezo kwa wakandarasi na wa watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) (kulia) kwenye uzinduzi huo.


Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (mwenye suti ya bluu) akicheza pamoja na kikundi cha ngoma za asili kutoka katika kijiji cha Rwabigaga wilayani Kyerwa mkoani Kagera kabla ya uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) uliofanyika mkoani humo mapema Julai 11, 2017 
 ……………………………………………………………..

Na Greyson Mwase, Kagera

Julai 11, 2017

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amesema vijiji na vitongoji vyote vya mkoa wa Kagera vinatarajiwa kupata umeme wa uhakika ifikapo mwaka 2021 kama sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III)

Dkt. Kalemani aliyasema hayo mapema Julai 11, 2017 kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) utakaosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) iliyofanyika katika kijiji cha Rwabigaga wilayani Kyerwa mkoani Kagera pamoja na kumtambulisha mkandarasi atakayefanya ujenzi wa sehemu ya kwanza ya mradi katika mkoa huo.

Alisema utekelezaji wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika mkoa wa Kagera utahusisha vipengele vitatu ambavyo ni pamoja na kusambaza umeme katika maeneo ambayo hayajafikiwa kabisa na miundombinu ya umeme na kuongeza wigo wa usambazaji umeme katika vijiji ambavyo vimefikiwa na miundombinu ya umeme lakini baadhi ya maeneo na vitongoji havikuungwa.

Waziri Kalemani alisema kipengele cha tatu kinahusisha usambazaji wa umeme utokanao na vyanzo vya nishati jadidifu kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi hususan visiwani.

Aliendelea kusema kuwa utekelezaji wa mradi huu utatekelezwa kwa vipindi viwili tofauti ambapo sehemu ya awali itahusisha upelekaji umeme katika vijiji 141 kwa gharama ya shilingi bilioni 45.43 na kuongeza kuwa utekelezaji wa sehemu ya kwanza ulianza tangu mwezi Februari mwaka huu ambapo inatarajiwa kukamilika mapema Aprili, 2019

Alieleza kuwa kazi hii itafanywa na mkandarasi ambaye ni kampuni ya M/S Nakuroi Investment Company Limited na kuongeza kuwa sehemu ya pili ya mradi huu wa kusambaza umeme vijijini kwa vijiji 180 vilivyobakia utaanza kutekelezwa baada ya sehemu ya kwanza kukamilika mwaka 2019, hivyo kufikisha umeme katika vijiji vyote vya mkoa wa Kagera ifikapo mwaka 2021.

Dkt. Kalemani aliwaomba wananchi kutumia fursa ya umeme wa uhakika kwa kuboresha maisha yao kupitia miradi ya uzalishaji mali pamoja na huduma mbalimbali za jamii ili uwekezaji huu wa Serikali ulete manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi.

“Wananchi sasa ninawaomba mtumie fursa hii ya umeme wa uhakika kwa kujenga viwanda vya kusindika mazao pamoja na huduma za afya, elimu, maji, kilimo na viwanda vingine, mashine za kusaga, useremala, kuhifadhi vinywaji na vyakula pamoja na kuchomelea vyuma shughuli ambazo zitawapatia kipato na kuboresha maisha yenu,” alisisitiza Dkt. Kalemani.

Aidha, Dkt. Kalemani aliwataka wananchi watakaounganishwa na huduma ya umeme kukamilisha utandazaji wa nyaya katika nyumba zao mapema ili mkandarasi atakapofika katika maeneo yao wawe tayari kulipia na kuunganishiwa na huduma ya umeme.

Aliongeza kuwa, wananchi ambao nyumba zao si kubwa sana wanahimizwa kuomba kufungiwa kifaa maalum kijulikanacho kama Umeme Tayari (UMETA) ambacho hakihitaji kutandaza nyaya katika nyumba.

Waziri Kalemani aliwaomba wananchi kutoa maeneo yao kwa ajili ya kupitisha miundombinu ya umeme bila ya kudai fidia kama mchango wao kwenye mradi huu na kuwezesha fedha iliyotengwa kuunganisha wateja wengi zaidi.

Katika hatua nyingine, Dkt Kalemani aliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika mkoa wa Kagera kusogeza huduma karibu na wananchi wa wilaya ya Kyerwa ili kuepuka gharama ya kufuata huduma mbali.

Wakati huo huo akielezea kwa kifupi Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Gissima Nyamo- Hanga, alisema mradi unalenga kufikisha huduma ya umeme kwenye vijiji 7,873 katika wilaya na mikoa yote Tanzania Bara ambavyo bado havijafikiwa na huduma ya umeme.

Alisema kwa mujibu wa taarifa ya maeneo rasmi ya kiserikali kutoka Ofisi ya Rais –Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Tanzania Bara ina vijiji 12,268 ambapo vijiji vilivyofikiwa na umeme hadi Juni, 2016 vilikuwa ni 4,395 sawa na asilimia 36.

Mhandisi Nyamo-Hanga aliongeza kuwa kati ya vijiji 7,873 ambavyo havijapata umeme, vijiji 7,697 vimepangwa kupatiwa umeme wa gridi na vijiji 176 pamoja na visiwa vitapatiwa umeme wa nje ya gridi kwa kuwa ndiyo njia muafaka ya kuvipatia umeme kwa sasa na kusisitiza kuwa mradi huu umepangwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka wa fedha 2016/17 hadi 2020/21.

Benki ya NBC yashinda Tuzo ya Superbrand Afrika Mashariki

0
0
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto),akipokea tuzo ya ubora ya Superbrand Afrika Mashariki kwa mwaka 2017-18 kutoka kwa Mkurugenzi wa Miradi wa Superbrands Afrika Mashariki, Jawad Jaffer katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Hii ni mara ya pili kwa NBC kupokea tuzo hiyo mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 2015-16.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (​wa tatu kushoto), akipozi kwa picha pamoja na baadhi ya wawakilishi wa makampuni yaliyoshinda tuzo za Superbrand Afrika Mashariki katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo jijini Dar es Salaam jana. Hii ni mara ya pili kwa NBC kupokea tuzo hiyo mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 2015-16

DKT NCHIMBI APOKEA MADAWATI ZAIDI YA 2000 KUTOKA BUNGENI KWA NIABA YA MIKOA YA KASKAZINI

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi leo ampokea madawati 2579 kutoka kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro.

Akipokea madawati hayo yaliyosafirishwa katika magari 19 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Dkt Nchimbi amelipongeza jeshi hilo kwa uzalendo huo wa kuhakikisha mali za umma zinafika Singida kwa ajili ya kuanza kusambazwa katika halmashauri husika zikiwa salama na katika hali nzuri.

Dkt Nchimbi amelipongeza Bunge kwa uzalendo wa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika kuhakikisha sekta ya elimu inaboreka nchini  ili kutimiza azma ya kufikia uchumi wa kati na wa viwanda. 

Amesema madawati hayo yataongeza motisha kwa wanafunzi kujisomea kwakuwa mazingira yatawawezesha kuandika na kusoma kwa ufanisi zaidi.
Aidha Dkt Nchimbi amezitaka halmashauri zitakazopokea madawati hayo kuhakikisha wanayatunza ili yadumu na kuwanufaisha wanafunzi kwa muda unaostahili.

“Madawati na yenyewe yanahitaji ukarabati, sio kwakuwa mmepewa basi muyaache tu, hapana, ukiona ubao unalegea kidogo basi hakikisha unarekebisha na sio kuanza kusubiri waliotupatia ndo waturekebishie”, amesema na kuongeza kuwa.

“Ili madawati haya yadumu waalimu na wanafunzi kwa pamoja wahakikishe wanayatunza vizuri, hasa walimu wasimamieni wanafunzi na muaelekeze namna ya kuyatunza kwakuwa hii ni mali yetu sote”, Amesisitiza.

Aidha Dkt Nchimbi ameongeza kuwa mkoa wa Singida uko tayari kupokea vifaa na mambo mbalimbali ya kitaifa kutokana na kuwa katikati mwa Tanzania hivyo kuwezesha usambazaji kwa mikoa mingine kuwa rahisi.

“Tunakaribisha taasisi, mashirika, na hata serikali kuu kama kuna vifaa vingine leteni Singida ni katikati na usambazaji utakuwa ni rahisi, lakini pia hata shughuli zozote za kitaifa mkoa wa Singida uko tayari kabisa kuzipokea” amesema Dkt Nchimbi.

Kwa upande wake Afisa Elimu Vifaa na Takwimu wa halmashauri ya Wilaya ya Meru Frank Paul Mwambachi amelishukuru Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa kuwapatia madawati ambapo halmashauri yake imepata madawati 400.

Mwambachi amelishukuru  JWTZ kwa kuyasogeza madawati jirani na halmashauri yake hivyo itakuwa rahisi na salama zaidi kwake kuyasafirisha na kuyafikisha yakiwa katika hali nzuri na kwa uharaka zaidi.

“Madawati 400 wakikaa wanafunzi watatu watatu ina maana ni wanafunzi 1200 wamenufaika, kwa kweli tunalishukuru sana bunge kwa uzalendo wao, pia jeshi limetusaidia sana kuyaleta madawati yetu Singida ambapo ni jirani” amesema Mwambachi.

Aidha ameongeza kuwa madawati hayo yataboresha mazingira ya ufundishaji na ya kujifunzia hivyo halmashauri itahakikisha wanayatunza ili wanafunzi wanufaike kwa kipindi kirefu.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akipokea kwa furaha moja ya magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyokuwa yamebeba Madawati hayo 2579 yanapelekwa katika mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro. Madawati hayo yametolewa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akimpongeza kwa furaha mmoja wa mwanajeshi aliyehusika kusafirisha Madawati 2579 yaliyotolewa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro. Madawati hayo yamefikishwa Singida kwa ajili ya urahisi wa kuyasambaza katika mikoa hiyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akishirikiana na wanajeshi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Askari wa Magereza kushusha madawati yalitolewa na Bunge. Madawati hayo 2579 yanapelekwa katika mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro.

 Askari wa Magereza wakipanda moja ya magari ya JWTZ na kusaidia kushusha sehemu ya madawati 2579 yaliyopokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa niaba ya mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro.
Afisa Elimu Vifaa na Takwimu wa  halmashauri ya Wilaya ya Meru Frank Paul Mwambachi akisaidiana na askari kubeba madawati waliyopatiwa na Bunge ambapo halmashauri yake imepewa madawati 400.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa afungua Zahanati katika kijiji cha Nandaka Wilayani Ruangwa

0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifungua Zahanati katika kijiji cha Nandaka Wilayani Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 11, 2017.

Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Wananchi wa Nandanga mara baada ya kufungua Zahanati katika kijiji cha Nandaka Wilayani Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi,
Julai 11, 2017.
Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Wananchi wa Nandanga mara baada ya kufungua Zahanati katika kijiji cha Nandaka Wilayani Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi,
Julai 11, 2017.

HUAWEI YADHAMIRIA KUKUZA MAENDELEO YA JAMII NA KIUCHUMI AFRIKA KUPITIA MFUMO MOBILE BROADBAND

0
0

Dar es Salaam Tanzania. 12 Julai 2017. Huawei kampuni ambayo inaoongoza kwenye Teknolojia ya Mawasiliano (ICT) duniani, imesema ipo tayari kufanya kazi na serikali za Afrika na taasisi binasfi ili kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa Bara la Afrika kupitia kuhimiza mfumo wa mawasiliano ya mobile broadband, ambapo wametangaza simu ya GSMA 360 kwa Afrika wakianza na Dar es Salaam leo.

Huawei imeonyesha dhamira yake ya kuboresha jamii kwa kushirikiana na wadau wengine kusaidia kuongeza wigo wa matumizi ya matandao na kuanzisha simu za mezani za nyumbani za wireless ambazo zitatuma mfumo wa mawasiliano wa simu za mkononi (MBB) jambo ambalo litaogeza matumizi ya kidijitaji katika maeneo ya mjini na vijijni.

Kupanua wigo wa matumizi ya MBB maeneo ya nchi mbalimbali za barani Afrika itasaidia kupunguza umaskini na kuimarisha huduma za afya na elimu pamoja na kupanuna wigo wa kuimarika kifedha.

GSMA inakadiria kwamba baada ya miaka mitano iajyo kutakuwa na takribani simu milioni 720 za smartphone ambazo zitakuwa zinatumika na asilimia 60 ya mfumo wa MBB utakuwa umeunganishwa kwenye soko la Afrika.

Kuunganishwa kwa mfumo huo kutaongeza ushindani kwenye nchi, pia ubunifu na kuongezeka kwa uzalishaji.

Changamoto kubwa katika viwanda vinakabiliwa na uwezo wa kujitanua katika maeneo ya mijini na vijiji inajumuisha suala la ugumu wa upatikanaji wa maeneo, gharama za juu za miundombinu na kutorudi kwa mitaji yao wanayowekeza.

Kutokana na kuwapo vikwazo hivyo kwa ukuaji wa maendeleo, Huawei imedhamiria kusaidiana na wadau jkupitia kupunguza gharama za uendeshaji, kwa kuamua kuwekeza kupitia kuimarisha mawasiliano.

Huawei imekuja na njia tatu za kukabiliana na hali hiyo ambazo niu PoleStar, TubeStar na RuralStar. Njia hizi tatu zitasaidia kuleta suluhisho ambapo italeta urahisi na gharama nafuu.

Makamu wa Rais wa Huawei, anayeshughulikia masuala ya Wireless Networks Marketing na ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Global Demand Generation, Dk Mohamed Madkour alisema dhamira ya Huawei ni kukuza maendeleo ya kijamii na uchumi kwa Afrika kupitia mawasiliano.

Dar Mohamed Madkour alisema, “Licha ya kuanzisha huduma ya mtandao katika mataifa mbalimbali Afrika, pia tunafanya biashara tatu na kuendeleza viwanda. Jambo la kwanza ni mifumo ya simu kwa mfano video cloud, game cloud a music cloud. Pili uunganishaji wa mifumo viwandani na tatu ni uunganishaji mifumo ya nyumbani.

Ongezeko la matumizi ya mitandao ya simu imefungua mlango kuimarika kwa biashara ya matumizi ya simu na mitandao ambapo kumekuwapo na 4G, 4.5G na nyingine ya 5G inakuja.

“Tumekuwa mstari wa mbele katika kuangalia fursa za Afrika licha ya changamoto zote ambazo tumezibainisha. Huduma ya mawasiliano inahitaji kuonyeshwa vitendo na kuanzisha biashara inayofaa ili kuzitumia fursa zote,” alisema Mohamed.


Kuhusu Huawei

Huawei ni Kampuni inayoongoza ulimwenguni kwenye utoaji wa teknolojia za mifumo ya mitandao. Lengp letu ni kuboresha maisha na kuleta ufanisi kupitia kuiunganisha dunia na wananchi, pia ubunifu katika kuiwezesha jamii kukua katika mawasiliano na kuwa mchangiaji mkubwa wa sekta ya viwanda.

Huawei imeimarisha mfumo wa ICT ambao umekuwa suluhisho na kuwapa wateja ushindani katika sekta ya mawasiliano na kuimarika kwenye huduma ya mtandao, vifaa na mifumo ya kompyuta.

Huawei inajumla ya wafanyakazi 170,00 duniani kote walioajiriwa katika sekta ya mawasiliano ya simu, kwenye kampuni na wateja. Mfumo wetu wa ICT, bidhaa na huduma umeenea katika zaidi ya nchi 170 duniani na ukanda wote huku ukihudumia zaidi ya thuluthi ya idadi nzima ya watu duniani.

Huawei ilianzishwa mwaka 1987 ikiwa ni kampuni binafsi ambalo inaendeshwa na waajiriwa wenyewe. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti yetu ya Huawei www.huawei.com au tufuatilie kupitia:

http://www.linkedin.com/company/Huawei

http://www.twitter.com/Huawei

http://www.facebook.com/Huawei

http://www.google.com/+Huawei

http://www.youtube.com/Huawei

Mshindi wa wiki Droo ya Tigo Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi akabidhiwa zawadi yake jijini Mbeya leo

0
0

kurugenzi wa Kampuni ya Simu za mkononi Tigo, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jackson Kiswaga akifungua simu aina ya Sumsang, yenye thamani ya Shilingi milioni 1.9/= na pembeni yake ni mshindi wa wiki wa promosheni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi, mkazi wa jijini Mbeya, Chiku Miyeka jana eneo la Kabwe Jijini hapa mapema jana.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu za mkononi Tigo, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jackson Kiswaga akimkabidhi simu aina ya Sumsang, yenye thamani ya Shilingi milioni 1.9/= mshindi wa wiki wa promosheni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi, mkazi wa jijini Mbeya, Chiku Miyeka jana eneo la Kabwe Jijini hapa.

Wakazi wa Jiji la Mbeya wakishuhudia makabibidhiano hayo mapema jana.

MAONESHO YA SABASABA 2017: WATU ZAIDI YA 500 WATEMBEELA BANDA LA PSPF, ASILIMIA 70 YA HAO WAJIUNGA NA PSS

0
0

Mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akipitia taarifa ya michango yake, baada ya kukabidhiwa na Maafisa wa Mfuko huo, alipotembelea banda la PSPF kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, leo Julai 12, 2017. Wakati wa maonesho hayo yakitarajiwa kufikia kilele kesho Alhamisi Julai 13, 2017, zaidi ya watu 500 wametembeela banda la Mfuko huo hadi mchana huu na kati ya hao asilimia 70 walifika kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS), unaomuwezesha mwananchi yeyote ambaye anafanya kazi za kumuingizia kipato kuwa mwanachama. Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi, alisema na kuongeza faida za mwanachama kujiunga na PSS, ni pamoja na kupata bima ya afya. (NA K-VIS BLOG/Khalfan Said)
Afisa Msaidizi wa Uendeshaji wa PSPF, Bw.Mussa Mfaki, (kulia), akimkabidhi kadi ya kujiunga na PSPF kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari, PSS, Bi.Damare B. Nampwani, leo Julai 12, 2017.
Bi.Damare B. Nampwani, akionyesha kadi yake baada ya kukabidhiwa.
Mwananchi akijaza fomu ya lujiunga na PSPF kupitia Mpango wa PSS, huku Mwanasheria kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti MHifadhi ya Jamii, (SSRA), Bi.Imani Masebu, (kulia), na Mhandisi Ally Shanjirwa, (katikati), wakishuhudia.
Mwananchi akionyesha dole gumba baada ya kujaza fomu.

Mwananchi akijaza fomu.
Afisa Michango wa PSPF, Bw. Noah Amri, akiwa kwenye mashine ya kutoa vitambulisho vya papo kwa hapo.
Afisa Uhusiano wa PSPF, Bi. Coleta Mnyamani, (kulia), akimkabidhi kadi ya uanachama ya PSPF, Afisa wa Polisi wa Usalama Barabarani, David S.Mlilo.
Afisa Uhusiano wa PSPF, Bi. Coleta Mnyamani, (kulia), akimkabidhi kadi ya uanachama ya PSPF, Afisa wa Polisi wa Usalama Barabarani, Salvatory A. Chacky.
Moja ya faida azipatazo Mwanachama wa PSPF,ni kuwa na uwezo wa kukopa kiwanja cha ujenzi wa nyumba na hapa ni Afisa Mipango Miji kutoka kampuni mshirika ya Adhi Plan Limited, Bi. Anna Lukando, (kulia), akimpatia maeelzo ya jinsi gani mwanachama anaweza kupata mkopo wa kiwanja au kununua kabisa.
Hiki ndio kikosi kazi cha PSPF ambacho kwa takriban wiki moja na nusu kimekuwa kikitoa huduma kamambe kwenye banda la Mfuko huo kwenye jengo la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, ambako kumekuwa na maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Kutoka kushoto waliosimama ni Isack Kimaro, Mussa Mfaki, Chaula Miteko, Mhandisi Ally Shanjirwa, Abdul Njaidi, Noah Amri,Win-God, Bw.Msina. Waliokaa kutoka kushoto, ni Bi. Coleta Mnyamani, Bi. Mariam Saleh, Bi. Irine Musetti na Bi. Asmahan H.Haji.
Win-God, (kushoto), Afisa wa uendeshaji msaidizi wa PSPF, akiwahudumia wananchi waliofika banda la Mfuko huo leo Julai 12, 2017.

Afisa Uendehsji wa PSPF, Bw. Isack Kimaro, (kulia), akiagana na Mwananchi huyu aliyefika kupatiwa huduma
Afisa Uendeshaji wa PSPF, anayeshughulikia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), Bi. Asmahan Haji (kulia), akimsaidia mwanachama huyu wa PSPF kuelewa michango yake.

Waziri wa Ujenzi, Prof. Mbarawa akagua mradi wa barabara za juu TAZARA

0
0
 Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd inayojenga barabara za juu eneo la Tazara, Kiyokazu Tsuji (kulia) akitoa maelekezo kewa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati) maendeleo ya daraja hilo wakati alipotembelea kuangalia maendeleo ya mradi huo. Kushoto ni Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida akishuhudia.

 WAZIRI wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa leo amevamia mradi wa ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la Tazara jijini Dar es Salaam na kuridhishwa na kasi ya ujenzi inayoendelea chini ya Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd ya nchini Japan. 

Akizungumza katika ziara hiyo alisema lengo ni kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ili kuhakikisha unakamilika mapema kama ulivyopangwa. Prof. Mbarawa alisema ameridhishwa na maendeleo ya mradi huo ambao mara baada ya kukamilika utarahisisha shughuli za usafiri kwa wananchi watumiao barabara hizo mbili za Nyerere na Mandela jijini Dar es Salaam. 

Mradi huo wa ujenzi unatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2018 huku ukitarajiwa kugharimu takribani shilingi bilioni 100, ambapo kati ya fedha hizo shilingi bilioni 93.44 zitatolewa na Japan kupitia Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA), na Serikali ya Tanzania itatoa shilingi Bilioni 8.3.  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akipata maelezo juu ya maendeleo ya mradi huo. Muonekano wa ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la Tazara jijini Dar es Salaam. Muonekano wa ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.

WAZIRI WA MAJI WA MISRI ATEMBELEA MTAMBO WA KUSAFISHA MAJI WA RUVU CHINI

0
0



Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge, akiwa na mgeni wake Waziri wa Maji na Umwagilia wa Misri Dk. Mohamed Abdel ATY (wapili kulia), baada ya kuwasili jana katika eneo la kusuku maji la Ruvu chini na kujionea maji yanavyoingizwa katika mtambo huo kutoka mtoni.(kushoto ni ) Mkurugenzi wa Sekta ya Maji na Umwaghiliaji wa Misri Dk. Ahmed BahaaEl Deen na kulia ni Mkurugenzi wa DAWASCO, Cyprian Luhemeja




Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge, akimwonyesha Mtambo Mpya wa kisasa wa Kusukuma maji wa Ruvu Chini unaomilikiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA), mgeni wake Waziri wa Maji na Umwagilia wa Misri Dk. Mohamed Abdel ATY (wapili kulia), baada ya kuwasili jana katika eneo la kusuku maji la Ruvu chini na kujionea maji yanavyoingizwa katika mtambo huo kutoka mtoni.(kushoto ni ) Mkurugenzi wa Sekta ya Maji na Umwaghiliaji wa Misri Dk. Ahmed BahaaEl Deen na kulia ni Mkurugenzi wa DAWASCO, Cyprian Luhemeja


Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge, akiwa na mgeni wake Waziri wa Maji na Umwagilia wa Misri Dk. Mohamed Abdel ATY (wapili kulia), baada ya kuwasili jana katika eneo la kusuku maji la Ruvu chini na kujionea maji yanavyoingizwa katika mtambo huo kutoka mtoni.(kushoto ni ) Mkurugenzi wa Sekta ya Maji na Umwaghiliaji wa Misri Dk. Ahmed BahaaEl Deen na kulia ni Mkurugenzi wa DAWASCO, Cyprian Luhemeja


Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge, akimwonyesha Mtambo Mpya wa kisasa wa Kusukuma maji wa Ruvu Chini unaomilikiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA), mgeni wake Waziri wa Maji na Umwagilia wa Misri Dk. Mohamed Abdel ATY (wapili kulia), baada ya kuwasili jana katika eneo la kusuku maji la Ruvu chini na kujionea maji yanavyoingizwa katika mtambo huo kutoka mtoni


Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge, akiondoka katika eneola Ruvu chini pamoja na mgeni wake Waziri wa Maji na Umwagilia wa Misri Dk. Mohamed Abdel ATY (wapili kulia), baada ya kumaliza kukagua katika eneo la kusukuma maji la Ruvu chini na kujionea maji yanavyoingizwa katika mtambo huo kutoka mtoni

WAZIRI MKUU AKABIDHI ‘AMBULANCE’ MBILI RUANGWA

0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua vifaa ndani ya gari la kubebea wagonjwa baada ya kukabidhi gari mbili za kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa na amekabidhi magari mawili ya kubebea wagonjwa. Amesema kati ya magari hayo moja ni kwa ajili ya hospitali hiyo ya wilaya na la pili litapelekwa katika kituo cha afya cha Mandawa.

Waziri Mkuu amekabidhi magari hayo leo (Jumatano, Julai 12, 2017), alipotembelea hospitali hiyo, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi Mkoani Lindi. Amesema magari hayo ni muendelezo wa mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake.

 “Rais wetu Dkt. John Magufuli amedhamiria kuwaondolea wananchi kero mbalimbali zinazowakabili zikiwemo za huduma za afya, hivyo tuendelee kumuunga mkono.”
 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimjulia hali mtoto Nasib Robert,(kushoto) ni mama wa mtoto Veronica Chilala,wakati alipo tembelea wodi ya watoto katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.

Waziri Mkuu amesema magari hayo ya kisasa yatasaidia kurahisisha usafiri kwa  wagonjwa wanaohitaji matibabu ya dharura katika hospitali kubwa. Kabla ya kukabidhi magari hayo, Waziri Mkuu alitembelea wodi ya  akina  mama na ya  watoto waliolazwa katika hospitali hiyo na amesema kwamba ameridhishwa na hali ya utoaji huduma.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Mheshimiwa Rashid Nakumbya amesema magari hayo ni faraja kwao kwa kuwa walikuwa na changamoto ya usafiri kwa wagonjwa wa dharura.

“Tunatambua na kuthamini jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika halmashauri yetu na Taifa kwa ujumla, nasi tutayatumia magari haya kama ilivyokusudiwa.”
 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipo kabidhi gari mbili za kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.

Awali, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa, Dkt. Regan Rajuu amesema hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika hospitali hiyo umeongezeka kutoka asilimia 80 Desemba, 2016 na kufikia asilimia 90 Juni 2017.

Pia Waziri Mkuu alitembelea shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa iliyoanza kujengwa Desemba, 23, 2016 kwa michango ya Halmashauri, fedha za mfuko wa jimbo pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Kaimu Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Emmanuel Sechawe alisema msingi wa kuanzisha shule hiyo ulitokana na uwepo wa wanafunzi 319 waliofaulu darasa la saba mwaka 2016 kukosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza katika shule zilizopo.

Mbali na kutembelea shule hiyo, pia Waziri Mkuu alifanya ukaguzi wa maendeleo ya mradi wa ujenzi wa gereza la wilaya ya Ruangwa, ambalo litakapokamilika litapunguza msongamano wa wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Nachingwea.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua gari ya kubebea wagonjwa wakati alipokabidhi gari mbili za kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wakati alipo tembelea hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.

UTILIAJI SAINI MKATABA WA USHIRIKIANO WA MANISPAA YA MJINI UNGUJA NA JIJI LA POSTDOM WAFANYIKA ZANZIBAR.

0
0
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mjini Zanzibar Abdulrahman Khatib kulia akitiliana saini na Mstahiki Meya wa Postdam Ujarumani Jan Jacob kuhusiana na mkataba wa mashirikiano kati ya Baraza la manispaa ya mjini na Jiji la Postdam la Ujerumani katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar.



Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mjini Zanzibar Abdulrahman Khatib kulia wakibadilishana hati baada ya kitiliana saini na Mstahiki Meya wa Postdam Ujarumani Jan Jacob kuhusiana na mkataba wa mashirikiano kati ya Baraza la manispaa ya mjini na Jiji la Postdam la Ujerumani katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mjini Zanzibar Abdulrahman Khatib kulia akiwa pamoja na Mstahiki Meya wa Jiji la Postdam Ujarumani wakionesha hati walizotiliana saini kuhusiana na mkataba wa mashirikiano kati ya Baraza la manispaa ya mjini na Jiji la Postdam la Ujerumani katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR. 






Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mjini Zanzibar Abdulrahman Khatib akitoa hotuba katika Sherehe ya kusaini mkataba wa mashirikiano kati ya Baraza la manispaa ya mjini na Jiji la Postdam la Ujerumani katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Mstahiki Meya wa Postdam Ujarumani Jan Jacob akitoa hotuba katika Sherehe ya kusaini mkataba wa mashirikiano kati ya Baraza la manispaa ya mjini na Jiji la Postdam la Ujerumani katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar. 

Mashine ya kuzalisha mkaa mbadala utokanao na takataka yatengenezwa

0
0

 Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Kujanakushoka Tools Manufactures Group Bw. Leonard Kushoka (kushoto) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitambulisha mashine ya kuzalisha mkaa mbadala utokanao na takataka, kulia ni mmoja ya wafanyakazi wa kampuni hiyo Bi. Zainabu Mtiga.
blu2
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Kujanakushoka Tools Manufactures Group Bw. Leonard Kushoka wakati akitambulisha mashine ya kuzalisha mkaa mbadala utokanao na takataka mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
blu3
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Kujanakushoka Tools Manufactures Group Bw. Leonard Kushoka akielekeza waandishi wa habari (hawapo pichani) namna mashine inavozibadili takataka na kuwa nishati ya mkaa mbadala.

ECOBANK YAINGIA MAKUBALIANO NA TICTS

0
0



Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Raphael Benedict (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam kuhusu ushirikiano wa Benki hiyo na TICTS ambapo wateja wa kampuni hiyo wataweza kufanya malipo yao kwa haraka na ufanisi zaidi kupitia tawi lolote la Ecobank hapa nchini ambapo katika kufanikisha jambo hilo benki imefungua Tawi lake katika jengo la PSPF linalopakana na geti la ofisi za TICTS, huku muda wa huduma ukiongezwa kuanzia saa 8:00 asubuhi hadi saa 4:00 usiku kwa siku za kazi, na saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni kwa siku ya Jumamosi. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa TICTS Jared H. Zerbe na kushoto ni Katibu Mkuu wa Tanzania Freight Forwarders Association (TAFFA), Tony Swai.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Raphael Benedict (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa TICTS Jared H. Zerbe wakisaini mkataba wa makubaliano wa kushirikiana katika kuhakikisha wateja wa TICTS wanafanya malipo yao kwa haraka na ufanisi zaidi kupitia tawi lolote la Ecobank hapa nchini. Mkataba huo ulisainiwa jana katika tawi la Ecobank lililopo PSPF Towers jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Katibu Mkuu wa Tanzania Freight Forwarders Association (TAFFA), Tony Swai.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Raphael Benedict (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa TICTS Jared H. Zerbe (katikati) wakipeana mkono baada ya kutia saini ya mkataba wa makubaliano wa kushirikiana katika kuhakikisha wateja wa TICTS wanafanya malipo yao kwa haraka na ufanisi zaidi kupitia tawi lolote la Ecobank hapa nchini. Mkataba huo ulisainiwa jana katika tawi la Ecobank lililopo PSPF Towers jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia (kulia) ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa fedha wa Ecobank Africa, Isaac Kamuta, Katibu Mkuu wa Tanzania Freight Forwarders Association (TAFFA), Tony Swai (wa pili kushoto), na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya TICTS, Donald Talawa (kushoto).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Raphael Benedict (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa TICTS Jared H. Zerbe (katikati) wakibadilisha mikataba ya makubaliano ya kushirikiana katika kuhakikisha wateja wa TICTS wanafanya malipo yao kwa haraka na ufanisi zaidi kupitia tawi lolote la Ecobank hapa nchini. Mikataba hiyo ilisainiwa jana katika tawi la Ecobank lililopo PSPF Towers jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Katibu Mkuu wa Tanzania Freight Forwarders Association (TAFFA), Tony Swai.






Benki ya Ecobank Tanzania leo imeingia katika ushirikiano rasmi na TICTS, ambapo wateja wa kampuni hiyo wataweza kufanya malipo yao kwa haraka na ufanisi zaidi kupitia tawi lolote la Ecobank.

Benki hii imeanzisha mfumo ambao utawawezesha wateja wa TICTS kufanya malipo yao papo kwa hapo kupititia mfumo huu rahisi. Huduma hiyo itakuwa inapatikana kwa wateja wa Ecobank na wasio wateja wa benki hii.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaaam leo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank, Raphael Benedict alisema benki hiyo inataka kuhakikisha huduma ya uagizaji na utoaji mizigo bandarini katika Bandari ya Dar es Salaam inakuwa rahisi zaidi na ya haraka zaidi kwa wateja wa TICTS.

Benedict aliongeza kuwa ili kuwezesha jambo hilo, Ecobank Tawi la PSPF ambalo linapatikana karibu na geti la ofisi za TICTS, limeogeza muda wa huduma zake na sasa litakuwa likifunguliwa saa 8:00 asubuhi hadi saa 4:00 usiku kwa siku za kazi, na saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni kwa siku ya Jumamosi.

Hata hivyo mipango ya benki hiyo ni kupanua zaidi huduma zake hadi siku ya Jumapili. Kwa maana hiyo, muda ulioongezwa utawawezesha wateja kuwa na wigo mpana zaidi wa kufanya shughuli zao na kukamilisha shughuli za upakuaji wa makontena.

Alisema kupitia mfumo mpya wa benki wa kidijitali, Eckobank Tanzania imekuwa katika mchakato wa kukamilisha hatua za utoaji huduma kwa saa 24 za malipo kwa wateja wa TICTS.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania International Container Services (TICTS), Jared Zerbe alisema kampuni hiyo imekuwa ikijitahidi katika kuboresha huduma zake ili kuendana na mahitaji ya wateja wake.

“Tunafuraha sana kuingia ushirikiana huu na Ecobank ambao utatusaidia kuboresha huduma zetu za kila siku. Kwa kuboresha huduma zetu, tumefungua akaunti yetu Ecobank ambapo wateja wataweza kufanya malipo yote ya huduma za TICTS. Pia Benki imefungua tawi jipya jirani na ofisi zetu za TICTS ghorofa za jengo la PSPF pembezoni mwa Barabara ya Sokoine Drive ili kurahisisha utoaji huduma kwa wateja,” alisema.

“Wateja wetu wanashauriwa kutumia matawi matano ya Ecobank yaliyopo jijini Dar es Salaam kwa huduma za malipo ya huduma mbalimbali za TICTS.”

TICTS na Ecobank watatambulisha njia mpya ya malipo kupitia mtandao wa simu ya mkononi na vituo vya mauzo kwa pamoja kwa mtindo mwingine wa malipo kupitia Ecobank. Taarifa itatolewa mara mpango huo utakapokamilika. Pia wateja watajulishwa kuhusu sehemu na tarehe ya kuhudhuria semina kwa wateja ili kukuza uelewa kuhusu malipo kwa mtandao na kupunguza usumbufu jinsi ya kutumia huduma za kibenki kwa mtandao.
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images