Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1298 | 1299 | (Page 1300) | 1301 | 1302 | .... | 1897 | newer

  0 0


  *Asema nchi ina utulivu wa kisiasa na uchumi unaokuwa kwa kasi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewahakikishia uwekezaji wenye tija wawekezaji watakaokuja nchini kwa kuwa Tanzania ni nchi yenye amani, utulivu wa kisiasa na uchumi wenye kukua kwa kasi.

  Ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 09, 2017) alipomuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Aga Khan alipochaguliwa kuwa Imamu Mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani.

  Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua na kuthamini shughuli mbalimbali zinazofanywa na mtandao wa taasisi za Aga Khan zilizopo hapa nchini, hivyo Serikali itaendelea kushirikiana nao.

  Ameupongeza mtandao wa taasisi za Aga Khan kwa kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli katika kutoa kipaumbele cha kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji ili waweze kujikwamua kiuchumi.

  “Nawahakikishia kwamba uwekezaji wenu hapa nchini utakuwa na baraka kwa sababu nchi imetulia kisiasa na uchumi wake unakua kwa kasi. Nawaomba muendelee kuwaalika wanajumuia wa madhehebu ya Shia Ismailia popote walipo duniani waje kuwekeza nchini fursa bado zipo.”
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi waiyo hudhuria katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi waiyo hudhuria katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na mama Zakia Megji wakati wa maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, (kushoto) ni Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin Lakhani Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin Lakhani wakati wa maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sofia Mjema Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea shada la maua wakati akikaribishwa kwenye maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sofia Mjema Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha wageni kwenye maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, (kushoto) ni Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin Lakhani na (kulia) ni muwakilishi wa AKDN Resident Amin Kurji, wakati alipomwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sofia Mjema Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na Muwakilishi wa AKD resident Amin Kurji katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli,(katikati) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Aga Khan Suleiman Shabbudin Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta jambo na Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin Lakhani, katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, Julai 9, 2017. 
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea maandano ya maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Diamond Jubilee, Waziri Mkuu amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika sherehe hiyo, Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  ……………………………………………………………..

  0 0

  MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amtembelea Askofu wa Jimbo kuu Katoliki la Dar es salaam Mwadhama Kardinal Polycarp Pengo Ofisini kwake leo ,Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini leo.baada ya kutoka nje kwa matibabu. 
  Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akisalimiana na Askofu Mkuu wa jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Kardinal Polycarp Pengo alipomtembelea ofisini kwake mapema leo.
  Askofu Mkuu wa jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Kardinal Polycarp Pengo akizungumza na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita kuhusu hali ya afya yake alipomtembelea leo Ofisini kwake ,kanisa la Mtakatifu. Joseph.
  Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akimsikiliza Askofu Mkuu wa jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Kardinal Polycarp Pengo alipomtembelea ofisini kwake leo ,Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini hapa.
  Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akipata Baraka kutoka kwa Askofu Mkuu wa jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Kardinal Polycarp Pengo alipomtembelea ofisini kwake leo, katika kanisa la Mtakatifu Joseph leo alipomtembelea kumjilia hali yake.
  Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kumjulia hali Askofu Mkuu wa jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama KardinalPolycarp Pengo alipomtembelea ofisini kwake leo, katika kanisa la Mtakatifu Joseph leo alipomtembelea kumjilia hali yake.

  0 0

  DROO maalum ya kuwania Sh Milioni 10, iliyoandaliwa na waandaaji wa mchezo wa kubahatisha wa Biko, imeenda kwa kijana mwenye miaka 25, Said Juma, mkazi wa Mwanza, ikitolewa katika tamasha la burudani la Komaa Concert la EFM Radio, lililofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini hapa jana.

  Katika tamasha hilo, wasanii mbalimbali wa jijini Mwanza na Dar es Salaam, walipata nafasi ya kutoa burudani kwa mashabiki wao, huku likinogeshwa na Milioni 10 za Biko maalum kwa wakazi wa Mwanza pekee.

  Akizungumza katika droo hiyo ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema mshindi huyo alipatikana kwa kupigiwa simu kama wanavyopatikana wengine waliowahi kuvuna mamilioni kutoka kwenye bahati nasibu yao inayochezeshwa kwa njia ya ujumbe wa maandishi kwa kupitia mitandao ya simu za Tigo Pesa, Airtel Money na M-Pesa.

  Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kushoto mwenye kipaza sauti, akimtangaza Said Juma kulia, aliyefanikiwa kunyakua jumla ya Sh Milioni 10 za Biko zilizotolewa maalum kwa ajili ya Tamasha la Komaa Concert lililoandaliwa na EFM Radio Jumamosi iliyopita na kufanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

  Shabiki wa muziki wa kizazi kipya jijini Mwanza ambaye jina lake halikupatikana mara moja akifuatilia onyesho la Komaa Concert lililoandaliwa na EFM Radio na kudhaminiwa na Bahati Nasibu ya Biko, ambapo pia alitafutwa mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko na Said Juma mkazi wa jijini Mwanza kuibuka kwenye droo hiyo maalum.

  Baadhi ya mashabiki wa muziki wa jijini Mwanza, wakiwa katika shangwe kubwa huku mmoja wao akiwa amevaa tshirt ya Biko wadhamini wa tamasha la burudani la Komaa Concert lililoandaliwa na EFM Radio kwa udhamini wa waendeshaji wa bahati nasibu ya Biko, ambapo pia ilimtangazaa mshindi wake maalum kwa ajili ya tamasha hilo ambaye ni Said Juma wa jijini Mwanza aliyezoa Sh Milioni 10 za Biko Tamasha hilo lilifanyika jana Jumamosi na kufanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

  Alisema kuwa watu waliocheza kwa kufanya miamala kwenye simu zao kuanzia Sh 1000 na kuendelea walichezeshwa kwenye droo moja iliyompa ushindi Juma, huku wakicheza kwa kutumia namba ya kampuni ya 505050 na ile ya kumbukumbu ya 2456.

  “Biko limekolea na kuchanja mbuga baada ya leo kumpata kijana maalum katika droo maalum ya Sh Milioni 10 tuliyoandaa kwa ajili ya tamasha hili la burudani lililoandaliwa na EFM, ambalo pamoja na mambo mengine, tuliamua tujumuike na Watanzania wote, hususan wa jijini Mwanza kwa ajili ya kufurahia pamoja,” Alisema Heaven na kuwataka Watanzania waendelee kucheza Biko kwa ajili ya kuwania zawadi za kawaida za papo kwa hapo pamoja na droo kubwa ya Jumatano na Jumapili ya Milioni 20.

  Naye mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe, alisema droo hiyo ya Sh Milioni 10 imechezeshwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za michezo ya kubahatisha, huku akiwataka Watanzania waendelee kutumia fursa ya kucheza Biko.

  “Tangu kuanza kwa bahati nasibu ya Biko, Bodi yetu imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na wachezeshaji hawa ili kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda vizuri, hivyo tunaendelea kusisitiza kwamba Biko ni mchezo salama na halali kwa Watanzania wote,” Alisema.

  Mbali na kutoa droo hiyo maalum ya Sh Milioni 10, droo nyingine za kuwania zawadi mbalimbali za fedha taslimu kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000, 1,000,000 zinazolipwa kwa njia ya simu za washiriki, pamoja na droo ya Jumatano na Jumapili, huku mwezi Mei na Juni pekee Biko wakitoa zaidi ya Sh Bilioni moja iliyokwenda kwa washindi wao.

  0 0

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (katikati) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kiwanja cha ndege cha Mpanda Seth Lyatuu (kushoto) wakati alipokagua huduma za uwanja huo Mkoani Katavi.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani(Kulia) akikagua Mfumo wa ukatishaji tiketi kwa njia ya kielekroniki katika Stesheni ya Mpanda Mkoani Katavi. Katikati ni Meneja Mradi wa kampuni ya Makgroup Ltd Bw. Joseph Mrosso.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kampuni ya Reli Tanzania, Kanda ya Tabora Bw. Frederick Masangwa(Katikati), wakati alipokagua huduma za usafiri wa Reli Mkoani Katavi.
  Meneja wa Msimamizi wa Bandari ya Kigoma Bw. Morris Mchindiuza (aliyenyoosha mkono) akimwonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili kulia) eneo itakapojengwa bandari ya Kalema iliyopo Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili) akitoka kukagua kingo za bandari ya Kalema iliyopo Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi

  ……………………………………………………………………………….

  Serikali imemuagiza Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda kuwasiliana na Kampuni ya Uendelezaji Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KADCO) ili kupata gari la Zimamoto ili ndege za Shirika la ndege Tanzania (ATCL) ziweze kuanzisha safari zake katika Mkoa wa Katavi.

  Akizungumza mara baada ya kukagua uwanja huo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani amesema kwa muda sasa kiwanja hicho kimekuwa kikitumiwa na ndege chache za Shirika la kuhudumia wakimbizi (UNHCR), hivyo ni wakati sasa kutumika na ndege zetu ili kuboresha huduma za usafiri wa anga Mkoani hapa.

  “Kamilisheni mazungumzo na KADCO ili kupata gari la Zimamoto lenye ujazo wa Lita 4,000 litakalokuwa na uwezo wa kukabiliana na majanga ya moto endapo yatatokea, kutakapokuwa na gari hilo uwanjani hapa tutaanzisha safari za ndege za Shirika letu wakati ndege yetu ta tatu itakapowasili,” amesema Eng. Ngonyani.

  Aidha, amemtaka meneja wa Uwanja huo wa ndege kuhakikisha anaingiza uwanja huo katika mpango maalum kwa ajili ya ujenzi wa taa kiwanjani hapo ili uwanja huo uweze kutumika kwa mchana na usiku.

  Eng. Ngonyani ameongeza kuwa azima ya Serikali ni kuhakikisha usafiri wa anga nchini unaimarika kwa kutumia ATCL na mashirika mengine yalipo nchini hivyo kama Serikali imejipanga kuendelea kuboresha miundombinu ya viwanja ili viwe katika viwango vinavyokubalika.

  Kwa upande wake Meneja wa Uwanja huo Seneth Lyatuu amemuhakikishia Eng. Ngonyani kuwa changamoto ya kuwa na Gari la zimamoto itatatuliwa mapema ili wakazi wa Mpanda waweze kunufaika na huduma za ATCL na hivyo kuwapa unafuu watumiaji wa usafiri wa anga.

  “Kuanza kwa safari za ATCL hapa Mpanda kutawapunguzia gharama wananchi ambao kwa sasa hulazimika kwenda Mwanza au Mbeya ili kupata ndege ya kwenda Dar es Salaam na gharama huwa kubwa,” amesisitiza Lyatuu.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw. Saleh Mhando amesema kutalete tija na kutafungua fursa ya utalii wa ndani na nnje ya nchi hasa kwa kuwepo na Mbuga ya Katavi ambayo ina vivutio vingi.

  Katika hatua nyingine Eng. Ngonyani amelipongeza Shirika la Reli Tanzania (TRL) kwa kutekeleza agizo la Serikali la kutumia Mfumo wa kielektroniki katika kudhibiti mapato ambapo shirika hilo limeanza kukatisha tiketi kwa njia hiyo katika stesheni za Mpanda na Tabora.

  0 0

    Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Rashid Shebuge likiwasili kwenye eneo la makaburi  la kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
    Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigella na waombolezaji wengine wakiwa kwenye mazishi ya aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya  aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
   Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigella  akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya  aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
   Ndugu wa marehemu  akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya  aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
    Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya  aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
   Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya  aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
   Ndugu akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya  aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid hebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
    Ndugu akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya  aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid hebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
  Mwombolezaji kiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya  aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid hebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
  Msaidizi wa Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Kaganda akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya  aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga. 
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akitoa pole kwa wafiwa  kwenye msiba wa aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
   Baadhi ya wafiwa  kwenye msiba wa aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
   Mjane na watoto wa aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge wakiwa msibani  kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
    Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge ukiwa tayari kuswaliwa kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.

   Mufti Mkuu wa Tanzania  Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally akiongoza Swala ya kuswalia mwili wa aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
   Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge ukiwasili kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
   Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge ukiwasili kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akiteta jambo  na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigella  wakiwa kwenye mazishi ya aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
   Sehemu ya wafanyakazi na waombolezaji kwenye mazishi ya aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na waombolezaji wengie wakielekea kwenye eneo la makaburi   ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.


  0 0

  KATIBU Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Geofrey Mngereza amekubali kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Wasanii litakalofanyika Ijumaa jijini Dar es Salaam.

  Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA),Cassim Taalib alisema Mngereza atashuhudia michezo mbalimbali itakayofanywa na wasanii na wanamichezo.

  Alisema tamasha hilo ambalo awali lilikuwa lifanyike kijiji cha Wasanii Mkuranga limehamishiwa jijini Dar es Salaam sababu kubwa ya kuhamisha tamasha hilo ni kutokana na mvua ya msimu uliopita kuharibu barabara ya kwenda kijijini.

  Taalib alisema tamasha hilo sasa litafanyika kwa siku mbili kuanzia Ijumaa Julai 14.7.2017 na kuhitimishwa Jumamosi Julai 15 mwaka huu katika viwanja vya Chuo cha Uhazili, splendid Ilala Bungoni.Alisema mpaka sasa wanatarajia kupokea wanamichezo kutoka sehemu mbalimbali kama vile Mkuranga, Kibiti, Zanzibar na Morogoro ambako zaidi ya wanamichezo 600 wamethibitisha kushiriki.

  Baadhi ya michezo ambayo itafanyika ni sarakasi, Tae kwon-do, muziki wa dansi, ngumi, soka,rede,muziki wa asili,wu shuu,ngoma,singeli na michezo mingine.Alisema kampuni ya SBC wanaotengeneza soda za Pepsi imekubali kuwa wadhamini wakuu wa tamasha hilo na kuongeza kuwa milango iko wazi kwa wadhamini wengine kujitokeza.

  Akizungumzia ujenzi wa nyumba zao kijijini alisema mgawo na makabidhiano ya nyumba 14 ndogo,kubwa tatu na viwanja 35 vilivyopimwa utafanyika Julai 16 siku moja baada ya kumalizika tamasha hilo.

  Alisema kuanzia sasa wanachama wanaotaka kujenga nyumba zao wenyewe wawasiliane na Shiwata ili wapewe maelekezo na utaratibu wa kufanya usafi kwenye makazi yao.Mwenyekiti alisema utaratibu wa kulipia umeme kupitia mpango wa umeme vijiijini (REA)unaendelea na mikakati ya kukarabati barabara ya kufika kijijini unafanyika.

  0 0

  Baadhi ya wananchi waliofika katika banda la Kampuni ya Uwekezaji UTT-AMIS wakipata maelezo kutoka kwa maofisa wa kampuni hiyo, Mfaume Kimario na Abbas Kandila, walipotembelea banda hilo katika Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).
  Mwananchi akisoa kipeperushi chenye taarifa za Kampuni ya Uwekezaji UTT AMIS wakati alipotembelea banda la kampuni hoyo kwenye Maonyesho ya Sabasaba. 
  Ofisa Masoko Mwandamizi wa Kampuni ya Uwekezaji UTT AMIS, Mfaume Kimario, akitoa maelekezo juu ya namna ya kujiunga na Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja inayoendeshwa na kampuni hiyo kwa mwananchi aliyefika katika banda la UTT AMIS baada ya kupata elimu juu ya kuhusu mifuko hiyo.
  Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Kampuni ya Uwekezaji UTT-AMIS, Mfaume Kimario, akitoa maelekezo juu ya namna ya kujiunga na Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja kwa mwananchi aliyefika katika banda la UTT AMIS.
  Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa UTT AMIS, Mfaume Kimario, akitoa Elimu Juu ya Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja kwa mmoja kwa wananchi waliofika katika banda la UTT AMIS katika Maonyesho ya Sabasaba.
  Ofisa wa Kampuni ya Uwekezaji UTT-AMIS, Abbas Kandila akitoa Elimu Juu ya Huduma wanazotoa kwa wananchi waliofika katika banda la kampuni hiyo.
  Maofisa wa Kampuni ya Uwekezaji UTT-AMIS, Nuru Thabit na Halfan Mnongane, wakitoa maelezo kwa wanachama walipofika katika banda la UTT AMIS katika Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).

  0 0


  Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel amesema kuwa katika serikali ya viwanda wakuu wa shule wanaweza kujenga msingi mzuri kwa wanafunzi kwani ni rasilimali katika sekta hiyo.

  Mollel aliyasema hayo wakati wa Rais wa Umoja wa Shule za Sekondari nchini (Tahossa)alipotembelea banda la Global Education Link katika maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam, Mollel amesema kuwa wa wakuu wa shule ndio wanaweza kuchukua dhamana ya serikali ya kauli ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa serikali ya awamu katika dhana ya viwanda.

  Mollel amesema kuwa serikali ya viwanda inahitaji watu wa masomo wa sayansi, sanaa na masoko kwa pamoja ndio wanajenga viwanda.

  Aidha amesema kuwa Global itaendelea kushirikiana wakuu wa sekondari katika ujenzi wa nchi ya viwanda.

  Naye Rais wa Umoja wa Wakuu wa Sekondari Nchini (Tahossa) Mwalimu Vitaris Shija amesema kuwa Global Education Link (GEL) ni chombo ambacho kinafanya wanafunzi wapende masomo ya sayansi ambao ndio watakaotumika katika sekta ya viwanda.

  Amesema kuwa sekta ya viwanda inahitaji wataalam wa sayansi, sanaa na biashara ndio mahitaji ya sekta ya viwanda kwa sasa kutokana na kauli ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa serikali ya awamu ya tano ni serikali ya viwanda.

  Shija amesema kuwa Global Education Link imeleta chachu ambapo inatakiwa kuanza kushawishi wanafunzi kusoma sayansi kuanzia shule ya msingi kutokana na mahitaji ya sekta ya viwanda.

  Shija amesema kuwa kutokana na mahitaji ya rasilimali katika sekta ya viwanda wakiwa wakuu wa shule za sekondari kuzungumza suala hilo kuanzia kwa wazazi juu ya nchi mahitaji yar rasimali katika sekta yaya viwanda.

  Amesema kuwa serikali kulipa wataalam wa nje ni gharama ambao sehemu kubwa watalipwa na kwenda kujenga kwao lakini wanafunzi wa waliokwenda watafanya kazi nchini na kujenga nchi yao.
   Mkurugenzi wa Global Education Link , Abdulmalik Mollel akiwa na Rais wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Nchini (Tahosa) Mwalimu Vitaris Shija katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.
   .Mkuu Idara ya Masoko kwa Njia ya Mtandao, Micky Musa akionesha mfumo wa Taarifa za wanafunzi wanaosoma nje kupitia Global Education Link (GEL) katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.


  Picha mbalimbali za mafisa za Global Education Link (GEL) katika katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Meneja wa mawasiliano Tigo Tanzania, Woinde Shisael akionesha simu toleo jipya la Tecno aina ya TecnoX1 kwa bei ya Tsh. 99,000/- na Tecno R6 kwa 195,000/- kwa waandishi wa habari mapema mwishoni wa wiki iliyopita., ambazo zinapatikana kwenye banda la Tigo sabasaba na kwenye maduka ya Tigo. Pichani kulia ni Afisa mawasiliano wa Tecno Tanzania, Eric Mkomoya na kushoto Meneja vifaa vya Intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga.
  Afisa mawasiliano wa Tecno Tanzania, Eric Mkomoya akizungumza na wanahabari kwenye maonesho ya biashara ya 41 sabasaba jijini Dar Es Salaam  mapema mwishoni wa wiki iliyopita., kulia ni Meneja wa mawasiliano Tigo Tanzania, Woinde Shisael na kushoto Meneja vifaa vya Intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga.
  Meneja wa mawasiliano Tigo Tanzania, Woinde Shisael akifafanua jambo kwa waandishi wa habari . Pichani kulia ni Afisa mawasiliano wa Tecno Tanzania, Eric Mkomoya na kushoto Meneja vifaa vya Intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga.
  Mwandishi wa habari wa Clouds Media, Aziz Kindamba akionesha simu aina ya  TecnoX1aliyoshida kwenye droo ilichezeshwa kwenye banda la Tecno mapema mwishoni wa wiki iliyopita.
  Mwandishi wa habari wa gazeti la Habarileo, Regina Kumba akionesha simu aina ya  Tecno R6 aliyoshida kwenye droo ilichezeshwa kwenye banda la Tecno leo.
  Waandishi wa habari wakipokea zawadi mbalimbali toka kampuni ya Tecnokwenye  maonesho ya 41 ya sabasaba jijini Dar mapema mwishoni wa wiki iliyopita.


  0 0


  0 0

  Spika wa Bunge, Job Ndugai, ambaye pia ni mbunge wa Kongwa, akipokea mfano wa hundi  ya Sh. Milion 15 kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Tawi laDodoma, Rehema Hamisi kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa nyumba ya walimu katika Shule ya Sekondari Laikala iliyopo wilayani Kongwa. Kulia ni Diwani wa Kata ya Sagala, Simon Kamando, akishuhudia.
  Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Dodoma pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo.
   Wanafunzi wakifurahia mfano wa hundi iliyotolewa na Benki ya CRDB. 
    Sehemu ya mifuko ya sarui iliyokabidhiwa na Benki ya CRDB kwa Shule ya Sekondari Laikala. 
  Spika wa Bunge, Job Ndugai, akitoa shukrani zake kwa Benki ya CRDB baada ya kupokea mifuko 200 ya saruji pamoja na hundi ya Sh. Milioni 15.
   Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya hundi ya Sh. Milioni 15 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa nyunba ya walimu pamoja na kuboresha miundombinu katika Shule ya Sekondari Laikala.
   Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB.
   Baadhi ya wananchi wakifuatilia hafla ya makabidhiano ya mifuko ya saruji.
  Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
  Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kongwa, akisalimiana na Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Dodoma, Bi. Rehema Hamisi wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa mifuko 200 ya Saruji iliyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya kusaidia Ujenzi wa Nyumba ya Walimu wa shule hiyo iliyopo jimboni kwake Kongwa mkoani wa Dodoma.
  Spika wa Bunge, Job Ndugai, akisalimiana na Meneja wa Kituo cha Huduma kwa Wateja Njia ya Simu (Call Center), Ena Mwangama, wakati alipowasili katika Shule yua Sekondari ya Laikala.
  Spika wa Bunge, Job Ndugai na Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Dodoma, Rehema Hamisi wakielekea shuleni hapo.
  Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Tawi la Dodoma, Rehema Hamisi (wa pili kushoto), akipiga ngoma sambamba na wasanii wa kikundi cha Matumaini kilichokuwa kikitumbuiza katika hafla hiyo.

  Mkuu wa Shule ya Sekondari Laikala, Msafiri  Simon, akisoma historia fupi ya shule hiyo.
  Mkurugenzi waBenki ya CRDB  Tawi la Dodoma, Bi. Rehema Hamisi, akisoma hotuba katika hafla ya kukabidhi msaada wa mifuko 200 ya Saruji iliyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya Kusaidia Ujenzi wa Nyumba ya Walimu katika Shule ya Sekondari Laikala. 
   Baadhi ya walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Laikala wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Tawi la Dodoma, Rehema Hamisi.
  Spika wa Bunge, Job Ndugai, akizungumza katika hafla ya Benki ya CRDB kukabidhi mifuko 200 ya saruji.
  Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Laikala wakimsikiliza Spika wa Bunge na mbunge wa Jimbo la Kongwa, Job Ndugai wakati shule hiyo ilipopokea msaada wa Sh. Milioni 15 kutoka Benki ya CRDB kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule hiyo.

  0 0

  Tanzania imesisitiza uamuzi wake wa kuendelea na mpango wa kujenga mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge Hydro Power Project) yaliyopo ndani ya Pori la Akiba la Selous mbele ya wajumbe wa Kamati ya Urithi wa Dunia kutokana na umuhimu wake kwa maendeleo ya Watanzania.

  Akizungumza mwishoni mwa wiki katika mkutano wa 41 wa wajumbe wa Kamati ya Urithi wa Dunia unaoendeshwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) ambao unaendelea katika Jiji la Krakov nchini Poland, Kiongozi wa msafara huo ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo kuwa mpango huo ulikuwepo katika ajenda ya Serikali ya Tanzania tangu miaka ya 1960's na kwamba ukubwa wa eneo litakalotumika kutekeleza mradi huo ni asilimia tatu tu ya eneo lote la pori hilo ambalo lina ukubwa wa kilometa za mraba 50,000.

  Aliongeza kuwa, “Itakumbukwa kuwa mnamo mwaka 1982 wakati pori hili (Selous) limewekwa katika orodha ya maeneo ya urithi wa dunia, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhifadhi wa Asili (IUCN) liliutambua mradi huo wa Stiegler's Gorge kutokuwa na madhara makubwa katika uharibifu wa mazingira ukizingatia ukubwa wa pori hilo na eneo litakalotumika kujenga mradi huo”.

  Aliwaeleza wajumbe hao kuwa, Serikali ya Tanzania inatekeleza sera ya kujenga uchumi wa viwanda hali inayopelekea kuwa na mahitaji makubwa ya nishati ya umeme hivyo kwa kuzingatia vyanzo vilivyopo imekuwa ni muhimu sasa kufikiria tena ujenzi wa mradi huo kama chanzo kingine muhimu cha nishati kuwezesha kufikia azma hiyo.

  Alisema mradi huo utaongeza uzalishaji wa umeme nchini kufikia asilimia 144.8 hivyo kuondoa upungufu wa nishati uliopo kwa sasa na pindi utakapokamilika utawanufaisha watanzania wengi wanaoishi bila umeme ikiwa ni pamoja na kukidhi mahitaji yake ya kuendesha viwanda.

  Meja Jenerali Milanzi alilazimika kutoa maelezo hayo kwa kamati hiyo ili kuweka bayana dhamira ya dhati Serikali ya Tanzania ya kuendelea na ujenzi wa mradi huo kwa ajili ya maendeleo endelevu huku akitoa rai kwao kuwa Serikali bado ipo tayari kwa mazungumzo ya namna bora ya kutekeleza mradi huo kwa faida ya jamii, uchumi na mustakbali bora wa mazingira ya hifadhi ya Selous na taifa kwa ujumla.

  “Kwa kutumia teknolojia bora zilizopo, mipango imara na usimamizi thabiti, mradi huu utakua na faida kubwa kwa taifa ikiwa na pamoja na kuboresha maisha ya watu maskini na jamii kwa ujumla bila kuathiri mazingira yanayotoa faida hizo”, alisema Milanzi.

  Hapo awali, kabla ya mkutano huo, ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu huyo ulifanya mazungumzo na Maafisa Waandamizi wa Kituo cha Urithi wa Dunia na Bodi za Ushauri ya kituo hicho na kuwasilisha kwa maandishi msimamo wa Tanzania kuhusu ujenzi wa mradi huo.

  Tanzania ilipinga vikali rasimu ya azimio No. 41 COM 7 A.17 aya ya 7 ambalo liliitaka kusitisha kabisa (to permanently abandon) ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge Hydro Power Project). Baada ya tamko la Tanzania kupinga azimio hilo kipengele hicho kilifanyiwa marekebisho ipasavyo na neno “to permanently abandon” (kusitisha kabisa) liliondolewa katika azimio hilo kupisha majadiliano zaidi.

  Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama zilizosaini mkataba wa urithi wa Dunia wa mwaka 1972 huku ikiwa na maeneo saba yaliyorodheshwa katika urithi huo ikiwepo Pori la Akiba la Selous, Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Mji Mkongwe (Zanzibar), Hifadhi ya Ngorongoro na Michoro ya kondoa na Kilwa Kisiwani. Aidha, ni mwanachama wa Kamati ya Urithi wa Dunia kwa kipindi cha miaka minne hadi mwaka 2019.

  Tokea ijiunge na kamati hiyo mwaka 2015, Tanzania imekua na msimamo wa kuwa na maendeleo endelevu katika ajenda za mikutano yake pamoja na miongozo yake ili kuruhusu kuendeleza maeneo ya urithi wa dunia kuweza kufikia maendeleo ya kijamii na kiuchumi bila kuwepo kwa athari kubwa katika mazingira.

  Mkutano huo wa 41 wa wajumbe wa Kamati ya Urithi wa Dunia unaoendelea katika jiji la Krakov nchini Poland umehudhuriwa na nchi wanachama 193 na unajadili mambo mbalimbali muhimu kuhusu uhifadhi na ulinzi maeneo ya urithi wa dunia pamoja na kutangaza maeneo mengine mapya ya urithi wa dunia yaliyowasilishwa na nchi nyingine wanachama katika mkutano huo.

  Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo ulijumuisha pia Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa ambaye pia ni mjumbe wa kudumu wa UNESCO, Samwel W. Shulukindo na Maafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.  Mkutano huo ulianza tarehe 2 Julai na unategemewa kumalizika tarehe 12 Julai, 2017.
  Muonekano wa mto Rufiji kutokea angani ambao maporomoko yake yatatumika kuzalisha umeme katika mradi unaotarajiwa kujengwa na Serikali wa Stiegler's Gorge.
  Sehemu ya mto Rufiji unakatiza katika Pori la Akiba la Selous.
  Pori la akiba la Selous lina vivutio vingi vya utalii ikiwemo wanyamapori mbalimbali wakubwa kama Tembo, Simba, Nyati, Chui, Twiga na Viboko.

  HAMZA TEMBA - WMU
  ..............................................................

  0 0

  Machi 16 2017, Mubelwa Bandio na Viola walipata nafasi ya kufanya mazungumzo na Dj D-Ommy katika studio za Kilimanjaro Studios.Dj D-Ommy ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Marekani amezungumza mengi kuhusu maisha, kazi na tasnia nzima ya muziki.
  Pia akapata fursa kuzindua rasmi kifaa kipya cha kazi kwa studio yetu, Pioneer DDJ SZ2
  Karibu utazame ukisikiliza

  0 0

   .Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda akikabidhi kadi za bima ya afya kwa watoto chini ya miaka 18 kwa wanachama wapya katika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, ,Anne Makinda amesema wakuu wa shule binafsi wanachukua  fedha za huduma ya matibabu ya afya kwa wanafunzi lakini wanafunzi hao wamekuwa hawapati  huduma wanazostahili na kulingana na kiasi walicholipia.

  Wakuu wa Shule binafsi wamekuwa wakilipisha wanafunzi fedha za huduma ya matibabu ikiwa ni njia moja ya maelezo kujiunga (joining instruction) ila inapotokea mtoto anaumwa humrudisha kwa wazazi wake.

  Mwenyekiti huyo ameyasema hayo wakati alipotembelea banda la NHIF katika Maonesho ya biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam, amesema mwanafunzi akilipia bima ya afya lazima atumie na sio kubaki mzigo kwa mzazi wakati alishalipia fedha ya matibabu hiyo.

  Amesema kuwa wakuu wa shule wanatakiwa kujiunga na  mfuko wa taifa ya wa bima ya Afya NHIF ili kuweza kuwahudumia wanafunzi katika kupata matibabu.

  Anne Makinda amesema kuwa katika maonesho ya sabasaba wamesajili bima za afya kwa watoto 1600 na kuongeza kuwa wananchi wamekuwa na mwitikio mkubwa katika kupata bima za afya.

  Amesema kuwa wameboresha bima ya afya katika mfuko wa afya ya jamii katika halmashari kwa kila aliyepata bima kutibiwa mkoa mzima tofauti na hapo nyuma kutibiwa katika Wilaya husika.

  Aidha amesema kuwa wataendelea kutoa huduma za bima za afya ikiwa ni pamoja na serikali kuweka mpango wa kila mtu kuwa na bima ya afya.
  .Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, , Anne Makinda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea banda la NHIF katika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
   Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda akipata maelezo kutoka Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti , Angela Mziray katika banda la NHIF katika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
   Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda akipata maelezo kutoka kwa Meneja Wanachama wa NHIF, Ellentruda Mbogoro katika banda la NHIF katika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
   Sheik Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akipata maelezo kutoka kwa Meneja Wanachama wa NHIF, Ellentruda Mbogoro katika banda la NHIF katika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
   Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Rose Mdami wakati alipotembelea banda la NIDA katika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
   Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda akipata maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi , Sebera Fulgence katika banda la Mfuko huokatika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry (wa tatu kutoka kushoto) akimpokea mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (wa pili kushoto) kwa ajili ya kushiriki mkutano mkuu waJumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya kanda ya ziwa mwaka 2017 uliofanyika katika Kijiji cha Sungamile kata ya Mwalugulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
  Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack na wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano huo.
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akitoa hotuba yake wakati wa kutano mkuu waJumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya kanda ya ziwa mwaka 2017.
  Viongozi mbalimbali wa serikali wakiwa eneo la tukio. Kushoto ni Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akifuatiwa na Afisa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Maria Yondani.
  Waumini na wananchi wakiwa eneo la tukio.  0 0

  Kwa majonzi makubwa, uongozi na wafanyakazi wote wa Efm radio na tv-E , unasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi mwenzetu Seth Katende – maarufu kama bikira wa kisukuma kilichotokea Julai 9 katika hospitali ya taifa Muhimbili.

  Ni vigumu sana kuamini na kukubali msiba huu mzito kwetu lakini kwakuwa sisi ni binadamu na kila nafsi lazima ionje umauti, tunamuomba mwenyezi mungu aipumzishe roho ya marehemu mpendwa wetu seth katende mahali pema, Amina.

  Uongozi na wafanyakazi wa Efm radio na tv-E unatoa pole kwa familia ya marehemu na wasikilizaji wetu wote walioguswa na msiba huu.

  Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe, Amina.
   Marehemu Seth Katende (Bikira wa Kisukuma) enzi za uhai wake akiwa  studio, Efm redio. 
  Kutoka kushoto marehemu Seth Katende akiwa na timu nzima ya kipindi cha ubaoni alichokua akitangaza.

  0 0


  Tazama matangazo ya moja kwa moja kutoka Chato Mkoani Geita ambapo Mhe. Rais John Pombe Magufuli atashuhudia makabidhiano ya nyumba 50 za watumishi wa afya za mikoa ya Geita, Kagera na Simiyu. 

  Pia atashuhudia makabidhiano ya kiwanda cha alizeti za Chato. Sherehe hizo zinahudhuriwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na Balozi wa Japan Mhe. Masaharu Yoshida.

   Matangazo haya yatarushwa moja kwa moja na TBC1, Azam TV, TBC Taifa, Clouds TV na kupitia tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz kuanzia saa 4:00 asubuhi hii. 

  Karibuni.

  0 0

  NA LUGENZI KABALE

  AKIITIKIA agizo la Rais John Pombe Magufuli alilowataka wateule wake kuwa wabunifu na kujituma ili kuwaondolea wananchi shida mbalimbali , Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ametatua migogoro takribani 8, 000 iliyowahusisha zaidi ya watu 80, 000 ndani ya takribani miezi minane kati ya Disemba mwaka jana na Mwezi Juni mwaka huu.

  Makonda ametekeleza jukumu hilo kupitia timu ya wanasheria 35 wanaojitolea kutoa huduma ya msaada wa kisheria bure kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.

  Kiongozi wa timu ya Wanasheria hao, Georgia Kamina, aliitaja baadhi ya migogoro ambayo timu yake imekuwa ikisuluhisha kupitia Ofisi za Wakuu wa Wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam kuwa ni ile ya umiliki wa ardhi na michakato ya mirathi mahakamani na katika ngazi ya familia,

  Migogoro mingine ambayo timu hiyo ya wanasheria imekuwa ikimsaidia Makonda kuitatua kwa kushirikiana na Wakuu wa wilaya ya Ilala (Sofia Mjema), Kinondoni (Ally Hapi), Temeke ( Felix Lyaniva ), Ubungo (Kisare Makori ) na Kigamboni (_Hashimu Mgandilwa ) ni pamoja na ndoa na matunzo ya watoto kwa ndoa zilizo sambaratika, ajira na mikataba ya ajira, ubakaji, faili kupotea mahakamani, ucheleweshwaji wa kesi mahakamani, umiliki wa nyumba, umiliki au mauziano ya ardhi, mikopo kutoka mabenki ya biashara, uuzwaji mali mbalimbali kwa kukiuka sheria au makubaliano na hata ukosefu wa uaminifu.

  Akiiongea kwa niaba ya Makonda, Kamina aliliambia Habari LEO katika mahojiano maalum yaliyofanyika hivi karibuni katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa, Ilala Boma Jijini Dar es Salaam hivi karibuni, alitaja migogoro wanayopokea na inayotia fora katika mkoa wa Dar es Salaam kuwa ni ile inayohusisha masuala ya mirathi, umiliki wa ardhi, ajira na mikataba kati ya waajiri na waajiriwa, ndoa na matunzo ya watoto kwa ndoa zilizo sambaratika na baadhi ya wananchi kuingia mikataba mibovu na mabenki katika harakati za kupata mitaji ya biashara.

  "Mheshimiwa Paul Makonda alichukua jukumu la kuanzisha huduma ya msaada wa kisheria bure kwa wananchi kutokana na uzoefu alioupata katika ziara ya kukutana na wananchi aliyofanya mkoa mzima mwezi Novemba mwaka jana," alibainisha Kamina na kuongeza kuwa ili kuwaepusha wananchi na mchakato mrefu na unaoumiza wa kumaliza migogoro yao mahakamani aliamua kuunda timu ya wanasheria wa kujitolea ili kutekeleza dhamira hiyo ya kuwasaidia wananchi wenye migogoro mbalimbali ya kisheria.
  Kiongozi wa timu ya wanasheria hao aliongeza kwa kusema kuwa Mkuu wa Mkoa aliguswa na namna baadhi ya wananchi walivyokuwa wakipoteza mashamba, nyumba, mali na hata kufukuzwa kazi kwa uonevu kwa kukosa uelewa wa sheria.

  “Ili kupata suluhisho la matatizo hayo hapo juu na kwakuwa yeye binafsi akiwa msaidizi wa Rais kwa mkoa wa Dar es Salaam basi ndio akaja na wazo la kuanzisha kitengo cha kutatua migogoro ya kisheria kwa njia ya kutoa huduma ya msaada kisheria bila malipo kwa wananchi katika kila wilaya ya mkoa wa Dar es Salaam.

  "Tupo jumla ya wanasheria 35 ambao tumegawanyika katika Wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam yaani Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo na Kigamboni. Tukiwa katika Ofisi za Wakuu wa Wilaya nilizotaja tunafanya kazi nao kwa karibu sana na pengine wakati mwingine tunajumuika na Makatibu Tawala wa Wilaya husika (DAS) na hata wakati mwingine Wakurugenzi Watendaji wa manispaa za mkoa wa Dar es Salaam katika kutatua migogoro hiyo kisheria,” alifichua Mkuu huyo wa Timu ya Wanasheria.

  Akizungumzia uzoefu waliopata katika kipindi cha miezi saba walichofanya kazi ya kutoa huduma ya msaada wa kisheria bure kwa wananchi kwa kusuluhisha migogoro mbalimbali wamegundua wananchi wengi ama hawana au wana uelewa mdogo wa sheria na kila wakati wanafanya makosa makubwa ya kisheria yanayoishia kuwaumiza kimaisha.

  "Kuna kina baba na kina mama wengi tu wamekuja mara baada ya kunyang'anywa nyumba zao na mabenki kutokana na kukubali kutoa hati za nyumba hizo kudhamini mikopo ya jamaa zao wakiamini kuwa kama kutakuwa na kutokuelewana kati ya mabenki na ndugu zao nyumba hizo hazitauzwa jambo ambalo sio kweli," alisimulia Kamina.

  Akitaja baadhi ya migogoro iliyowagharimu muda na juhudi za ziada kuisuluhisha, Kamina alitaja mgogoro wa umiliki wa ardhi ya hekari 28 unaomhusisha Ogwari Nashon na wakazi wa kijiji cha Viwege, Mbondela eneo la Chanika katika Wilaya ya Ilala.

  “Mgogoro huu ulifika mahala ukahatarisha maisha ya ndugu Nashon kwani baadhi ya wanakijiji wasioheshimu sheria walivamia eneo lake, kuchoma moto majengo na kuharibu mazao kama mihogo, mananasi na michungwa.


  Mara baada ya Nashon kuja ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ilala alikutanishwa na wanasheria wa Mkuu wa Mkoa wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria  bure kwa wananchi walioko wilayani hapo na kueleza tatizo lake ambapo timu yetu iliingilia kati kwa kushirikiana na Mkuu wa wilaya ya Ilala Sofia Mjema, ili kupata ufumbuzi wa mgogoro huo.

  Ni jambo la kutia faraja kwa sasa tumepiga hatua kubwa kuelekea kutatua mivutano iliyokuwepo kwani Nashon ana vielelezo halali vya nyaraka za kiserikali zinazothibitisha umiliki wa eneo hilo," alibainisha Kamina.

  Licha ya kujitokeza picha nzuri iliyojaa mafanikio ya huduma hii ya msaada wa kisheria kwa wananchi katika Mkoa wa Dar es Salaam, Habari Leo imearifiwa juu ya changamoto lukuki zinazowakabili watoa huduma hiyo katika kutekeleza majukumu yao.

  Baadhi ya changamoto hizo ni wananchi kutokuwa na uelewa wa sheria, kanuni na taratibu za kukopa fedha kwa watu binafsi na katika taasisi za fedha, wananchi hawana uelewa wa sheria na taratibu za mirathi na hata wasimamizi wa mirathi hawajui wajibu wao kwa warithi na kwa mahakama jambo ambalo linapelekea warithi kuchelewa au kutopatiwa haki zao hata baada ya mchakato wa mirathi kukamilika katika Mahakama.

  “Katika eneo la ajira huko ndio kunatisha kwa uvunjaji wa sheria za ajira na nchi uliokithiri kwani makampuni mengi hasa ya ujenzi na ulinzi hayatoi mikataba ya ajira kwa wafanyakazi, wakati mwingine mikataba inakuja kutolewa baada ya mwajiriwa kuwa amekwisha fanya kazi muda mrefu na inapotolewa inakuwa inakiuka makubaliano ya awali,” alisema na kuwanyooshea kidole viongozi wa serikali za mitaa na kata, katika baadhi ya maeneo kwa kuwa chanzo cha migogoro kwa kufanya majukumu ambayo si yao kisheria na uendeshwaji wa kesi mahakamani kuchukua muda mrefu pasipo na sababu za msingi huku Mabaraza ya kata nayo kuwa dhaifu katika kutekeleza majukumu yake ya kimsingi katika kuwahudumia wananchi na hasa wale wa kipato cha chini.

  Akizungumzia huduma hiyo, Makonda alisema aliamua kuanzisha huduma ya msaada wa kisheria kupitia wanasheria hawa (35) katika kila wilaya ya mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) inayoagiza kusikiliza na kutatua kero au malalamiko ya wananchi.

  Mkuu huyo wa Mkoa alifafanua kuwa katika ziara ya mkoa wa Dar es Salaam mwishoni mwa mwaka 2016 aligundua wananchi wengi hawakuwa na uelewa wa sheria jambo lililowafanya kupoteza haki zao aidha kwa kutapeliwa, kuonewa au kutojua mahala sahihi pa kupeleka matatizo hayo.

  "Pamoja na changamoto nyingi zinazoambatana na huduma hii ya kutafuta suluhu ya matatizo ya wananchi kwa kuzileta pande husika mezani kuongea bado nina dhamira ya kuendelea kuwasaidia Watanzania wenzangu kwa juhudi na maarifa yangu yote.

  Na hii ndio gharama ya kuteuliwa na Rais, unapoteuliwa na Mkuu wa nchi anakuwa na matarajio mengi kutoka kwako. Mimi nimeamua kufanya ninayoweza kwa nguvu na juhudi zote ili kumuondolea Rais John Pombe Magufuli na mashinikizo juu ya shida mbalimbali za Wana Dar es Salaam," alimaliza Makonda.

  0 0

  Kampuni ya simu za mkoni ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na GSMA wameandaa mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia simu za mkononi ambayo yanafanyika jijini Dar es Salaam kwa mwaka wa pili mfululizo.
  Mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa na Airtel money na Comviva wakishirikiana na muungano wa mashirika ya simu za mkononi ulimwenguni GSMA yanajumuisha washiriki kutoka Africa. Wajasiriamali wa TEKNOHAMA kutoka Ghana, Kenya, Uganda na Tanzania watachuana kutengeza suluhu kwenye maeneo makuu matatu, yaani malipo kwenye sekta ya usafirishaji, mfumo wa malipo ya jumla (bulk payment )na mfumo wa malipo ya pochi ya Comviva na Airtel yaani ( Airtel Comviva mobile wallet).  
  Tanzania imepata fursa ya kuandaa mashindano hayo kwasababu inajulikana kama kiongozi katika sekta ya simu za mkononi inayoongoza katika kujenga mifumo ya malipo ya simu ( mobile money payment) Hivyo ni fursa ya kipekee kwa wajisiriamali wa kitanzania kuweza kutengeneza suluhu za mifumo ya malipo ya simu za mkononi zitakazotumika barani Africa.
  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo, Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda alisema ushirikiano huu ni muhimu kwa vile unawezesha wajasiriamali wa TEKNOHAMA kuja na suluhu ambayo itaweza kusaidia kufanya malipo kupitia simu za mkononi kwa haraka na hivyo kuokoa kupoteza muda kupanga foleni kusubiria kufanya malipo.
  Sisi Airtel Tanzania tumekuwa msitari wa mbele kuwezesha wajasiriamali kwa njia mbali mbali. Kwa kupitia mashindano tunaendeleza uwezeshaji huo kwani kwa kila suluhu itakayopatikana haitaishia hapa mbali itaendelea kuboresha na kuwekwa kwenye mfumo wa malipo ya simu za mkononi, alisema Nchunda.
  Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha Teknohama GSMA Gareth Pateman alisema washiriki wa mashindano hayo wanaweza kutengeneza suluhi moja au mbili katika zile tatu huku mshindi akipata ticketi ya kwenda Barcelona, Spain huku akiwa amelipiwa gharama zote.
   Mkuu wa Ktengo cha TEKNOHAMA kutoka GSMA Gareth Pateman akitoa mafunzo kwa washiriki kutoka Tanzania wakati mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia simu za mkononi yanayodhaminiwa na Airtel money na Comviva wakishirikiana na muungano wa mashirika ya simu za mkononi ulimwenguni GSMA.
   Mkuu wa Ktengo cha TEKNOHAMA kutoka GSMA Gareth Pateman akitoa mafunzo kwa washiriki wa mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia simu za mkononi yanayodhaminiwa na Airtel money na Comviva wakishirikiana na muungano wa mashirika ya simu za mkononi ulimwenguni GSMA
   Mkuu wa Ktengo cha TEKNOHAMA kutoka GSMA Gareth Pateman akitoa mafunzo kwa washiriki wa mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia simu za mkononi yanayodhaminiwa na Airtel money na Comviva wakishirikiana na muungano wa mashirika ya simu za mkononi ulimwenguni GSMA
  Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Isack  Nchunda, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana baada ya ufunguzi wa mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia simu za mkononi yanayodhaminiwa na Airtel money na Comviva wakishirikiana na muungano wa mashirika ya simu za mkononi ulimwenguni GSMA.

  0 0

  Na Veronica Kazimoto 

  WADADISI wa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 wameaswa kuzingatia maadili ya kazi wakati wa zoezi la kuorozesha kaya linalotarajia kuanza kesho ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utafiti huo.

  Akizungumza wakati wa mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa wadadisi hao, Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu, Sylvia Meku kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu amesema ili kufanikisha zoezi la uorodheshaji wa kaya, ni lazima wadadisi hao wakazingatia maadili ya kazi pamoja na kufuata taratibu zote za Utumishi wa Umma.

  “Ofisi ya Taifa ya Takwimu inawaagiza kwenda kwenye jamii kwa ajili ya kuorodhesha kaya zitakazofanyiwa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Natumaini mtatii na kuheshimu maadili ya Utumishi wa Umma ili muweze kufanikisha kazi hii kwa ufanisi,” amesema Slyvia Meku.

  Amesema Zoezi la Uorodheshaji wa Kaya litafanyika mikoa yote ya Tanzania Bara kwa takribani siku 15 kuanzia kesho Julai 11, 2017 na baadae kufuatiwa na utafiti wenyewe unaotarajia kuanza mwezi Desemba, 2017.

  Sylvia Meku amesema utafiti huu unafanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango na baadhi ya Wadau wa Maendeleo kwa lengo la kuangalia kiwango cha umasikini nchini. 
   Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu Bi. Sylvia Meku akizungumza wakati wa mafunzo ya Wadadisi watakaokwenda kuorozesha kaya mikoa yote kwa ajili ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya litafanyika kwa muda wa siku kumi na tano (15) kuanzia kesho tarehe 11 Julai, 2017.
    Baadhi ya Wadadisi wakimsikiliza kwa makini Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu Bi. Sylvia Meku (hayupo Pichani) wakati wa mafunzo ya Wadadisi watakaokwenda kuorozesha kaya mikoa yote kwa ajili ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya litafanyika kwa muda wa siku kumi na tano (15) kuanzia kesho tarehe 11 Julai, 2017.
  Baadhi ya Wadadisi wakiwa kwenye gari wakielekea Kata ya Mchikichini, Ilala na Kawe jijini Dar es Salaam kufanya mazoezi ya kuorozesha kaya kwa vitendo kwa ajili ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya litafanyika kwa muda wa siku kumi na tano (15) kuanzia kesho tarehe 11 Julai, 2017.
   Baadhi ya Wadadisi wakielekezwa namna ya kutumia ramani wakati wa kufanya mazoezi ya kuorozesha kaya kwa vitendo na Mtalaam wa Ramani Jumanne Msuya wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (katikati) kwa ajili ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya litafanyika kwa muda wa siku kumi na tano (15) kuanzia kesho tarehe 11 Julai, 2017.
  (PICHA ZOTE NA EMMANUEL GHULA)

older | 1 | .... | 1298 | 1299 | (Page 1300) | 1301 | 1302 | .... | 1897 | newer