Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1297 | 1298 | (Page 1299) | 1300 | 1301 | .... | 1896 | newer

  0 0

   Kaimu Afisa Habari wa Jeshi La Kujenga Taifa (JKT),Kanal Separatus Lubinga  akitoa maelezo kwa Waziri wa kazi, Uwezeshaji, Wazee ,Vijana na Maendeleo kwa watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maudline Cyrus Castico alipotembelea Maonesho ya 41 ya Sabasaba
   SSGT. Faustine Mabata kutoka Suma JKT Furniture akitoa maelezo kwa Waziri wa kazi, Uwezeshaji, Wazee ,Vijana na Maendeleo kwa watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maudline Cyrus Castico alipotembelea Maonesho ya 41 ya Sabasaba

   CPL.Maximilian Joseph wa SUMA JKT Guard  akitoa maelezo kwa Waziri wa kazi, Uwezeshaji, Wazee ,Vijana na Maendeleo kwa watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maudline Cyrus Castico alipotembelea Maonesho ya 41 ya Sabasaba
    SSGT. Faustine Mabata kutoka Suma JKT Furniture akitoa maelezo kwa Waziri wa kazi, Uwezeshaji, Wazee ,Vijana na Maendeleo kwa watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maudline Cyrus Castico alipotembelea Maonesho ya 41 ya Sabasaba
   Waziri wa kazi, Uwezeshaji, Wazee ,Vijana na Maendeleo kwa watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maudline Cyrus Castico  akiangalia namna ya ufugaji Samaki kwa kutumia mfumo Raisi alipotembelea Maonesho ya 41 ya Sabasaba
  Waziri wa kazi, Uwezeshaji, Wazee ,Vijana na Maendeleo kwa watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maudline Cyrus Castico alipotembelea Maonesho ya 41 ya Sabasaba

  0 0

  · ‘App’ hii imelenga kuwasaidia watumiaji wake kupata taarifa muhimu kuhusu hoteli, usafiri, sehemu za vivutio, klabu, kasino, maduka makubwa, ubalozi na hospitali.

  Kampuni ya simu za mkononi Zantel ambao wanaongoza katika utoaji wa huduma bora za data, leo imezindua application ya simu inayojulikana kama ‘Discover Tanzania Mobile App” ambayo lengo lake ni kuhimiza utalii wa ndani na nje kwa lengo la kuwapatia watalii taarifa sahihi za maeneo ya utalii yanayopatikana na hapa nchini Tanzania.

  App hiyo itakuwa na taarifa zote za muhimu zinazopatikana hapa nchini zikiwamo kuhusu hoteli, usafiri, maeneo ya vivutio, kumbi za starehe, maduka makubwa, ubalozi na hospitali ambapo huduma hiyo itapatikana na kwenye Google Play Store kwa gharama nafuu ya Shilingi 500 tu.

  Akizungumzia huduma hiyo jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Zantel, Gasper Mbowa alisema, “Tunayofuraha kubwa kuzindua App hii ni kwa ajili ya wateja wetu, lakini jambo kubwa zaidi ni kuwa Zantel ndio Kampuni ya kwanza ya Mawasiliano kuanzisha huduma hii hapa nchini.” ‘Discover Tanzania mobile App’ ni rahisi kutumia na pia ni huduma ya bei nafuu kwa watu wote, kwa wageni na wenyeji. Kwa muda wa siku tatu mteja wa Zantel atatumia kiasi cha shilingi 500, kwa siku saba mteja atatozwa shilingi 2000 na kwa mwezi mzima mteja atatozwa 3,000. Aliongeza kuwa alama ya siri kwa ajili ya kupata huduma hiyo kupitia sms au sauti kwa wateja wa Zantel ni 15582 ambapo watatozwa Tsh. 1 tu kwa sekunde.

  Alisema, hivi sasa nchini Tanzania taarifa zinahitajika zaidi kwa watalii ili kujua maeneo ya vivutio, aina za vyakula vinvyopatikana, maeneo ya burudani na gharama mbalimbali za huduma ikiwamo malazi, upatikanaji wa usafiri wa uhakika, maeneo yenye ofisi muhimu kama vile ubalozi, huduma za hospitali na kadhalika.

  “Zantel sasa imekuwa ni sehemu ya kutangaza utalii ikiwa ni pamoja na uamuzi wa kurahisisha shughuli za utalii. Ni imani yetu kubwa kwamba huduma hii itatangaza utalii kwa sababu taarifa zote muhimu zitakuwa zinapatikana kwa watalii wa ndani na wa nje ya nchi. Tutahakikisha tunahimiza usalama ili kuwawezesha watalii kuunganishwa moja kwa moja na huduma za Zantel,” alisema.

  Aliongeza kuwa, application hiyo itapatikana kwenye simu zote za mfumo wa android pamoja na IOS kwa ajili ya simu aina ya I-Phones.

  Sekta ya utalii nchini Tanzania ni eneo muhimu linalozalisha ajira takribani 250,000 kwa wananchi kila mwaka. Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2014 kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Tanzania inaingiza mapato yatokanayo na utalii yanayofikia Dola bilioni 2.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Mtaalamu na mshauri wa masuala ya urembo na Ngozi Irene Moshi ametoa ushauri kwa kina mama hususani wasichana kutumia vipodozi vyenye vimea asilia ili kuepukana na kuharibu ngozi zao.

  Amesema hayo wakati akiongea na globu ya Jamii, Irene amesema kupitia saluni ya Timeless wameweza kuwasaidia watu wengi na kuwapatia tiba kuhusiana na masuala ya ngozi na hasa katika usahihi wa kutumia vipodozi vinavyoendana na ngozi ya muhusika.

  "Tunatoa ushauri wa kitaalamu kuhusiana na matumizi sahihi ya vipodozi kulingana na aina ya ngozi ya muhusika pia kutoa malekezo ya kutumia vitu sahihi kwa wakati sahihi kama vile kulingana na hali ya hewa kipindi cha joto na baridi,"amesema Irene.

  Amesema kuwa, anatoa ushauri kwa vijana hususani wa kike kujifunza zaidi masuala ya urembo kwani inaweza kusaidia katika kuboresha ngozi zao na wanaweza kutumia vipodozi sahihi na kutokuharibu ngozi zao.

  Mbali na kutoa tiba, Timeless walianza kutoa mafunzo rasmi mwaka 2016 Irene amesema kuwa wanatoa mafunzo kwa vijana wanaopendelea kufahamu shughuli mbalimbali za urembo ikiwemo tiba ya ngozi, upambaji ambapo wameweza kutoa vijana wengi kwa kipindi cha mwaka mmoja na tayari wengine wameshajiajiri katika sehemu zao na pia Timeless wanajishughulisha na masuala ya kupamba maharusi, nywele na kucha na mapambo ya maharusi ikwemo kadi.
  Mtaalamu na mshauri wa masuala ya urembo na Ngozi Irene Moshi akimuhudumia mteja aliyetembelea katika banda lao la Timeless Hair and Beauty Saloon kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es salaam.
   Mtaalamu na mshauri wa masuala ya urembo na Ngozi Irene Moshi akizungumza na Globu ya Jamii kuhusiana na masuala ya urembo wa ngozi na kuonyesha baadhi ya mapambo ya maharusi yanayopatikana kwenye saluni yao ya Timeless.
  Wateja wakiwa wanapata maelezo kutoka kwa  mfanyakazi wa Timeless Hair and Beauty Saloon katika banda laokwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es salaam.Picha na Emanuel Massaka,

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa DEar es salaam Mh. Paul Makonda akikagua moja ya magari 26 ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es salaam yaliyopelekwa katika Garage ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro kwa ukarabati ili yaendane na kazi ya jeshi la p0lisi
  Mkuu wa mkoa wa DEar es salaam Mh. Paul Makonda akijadiliana jamabo na uongozi wa Garage ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro wakati alipokagua magari ya polisi yanayofanyiwa ukarabati mkubwa.
  Mkuu wa mkoa wa DEar es salaam Mh. Paul Makonda akiakizungumza na uongozi wa Garage ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro
  Mkuu wa mkoa wa DEar es salaam Mh. Paul Makonda akikagua moja ya magari 26 ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es salaam yaliyopelekwa katika Garage ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro
  Mkuu wa mkoa wa DEar es salaam Mh. Paul Makonda akijadiliana jambo na mmoja wa viongozi wa Garage ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro.

  ……………………………………………………………………………

  Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo ametembelea Garage ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro kukagua maendeleo ya ukarabati na ubadilishaji mwonekano wa Magari mabovu 26 ya Jeshi la Polisi yaliyosafirishwa kwenda Moshi Mkoani Kilimanjaro hivi karibuni.

  Akiwa katika Garage hiyo Mheshimiwa Makonda amejionea magari hayo yakiwa katika hatua mbalimbali za utengenezaji ambapo ameomba uongozi wa kampuni hiyo kukamilisha ukarabati wa magari hayo kwa wakati iliyaweze kuongezea ulinzi na usalama jijini Dar es salaam.

  Aidha Makonda amesema kuwa anataka kubadili mwonekano wa jeshi la polisi Mkoa wa Dar es salaam kwa kuhakikisha magari ya polisi yanakuwa na hali nzuri itakayowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa uufanisi kwa  kuyabadili magari hayo kuwa kama yale ya Askari wa umoja wa mataifa.

  *”Hakuna kitu kinachoninyima usingizi kama pale Mwananchi anapohitaji polisi wafike mahala pa tukio na polisi hawafiki, na kufanya hali ya amani kutoweka na wakati huohuo polisi wanataka kufanya kazi yao ila wanashindwa kutokana na uhaba wa vifaa.Hii ndiyo sababu ninahangaika ili siku moja Dar es Salam iwe na amani hata kufikia hatua ya watu kufanya Biashara zao masaa 24na kutembea kwa amani muda wote.”*alisema Makonda.

  *Nimepata Pikipiki 200, baiskeli 500 na kuweza kutengeneza magari haya 56 kuwa na viwango vya kimataifa kama magari ya Umoja wa Mataifa (U.N) yanavyoonekana,yaani kwenye gari ya doria itaweza kuwa na maafisa wa polisi tisa kwa nyuma,ambao watatu watakuwa kushoto na watatu kulia mwa gari hiyo huku wawili wakiwa nyuma ya gari hiyo na mmoja akiwa amesimama mbele na silaha kubwa.”*aliiongeza Makonda.

  Kwa upande wake kaimu kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam, (DCP) Lucas Mkondya amempongeza Mheshimiwa Makonda kwa juhudi anazozifanya kuhakikisha askari wanafanya kizi katika mazingira mazuri.

  Nae mkurugenzi wa ufundi wa kampuni ya RSA Ltd inayokarabati magari hayo Bwana Varinder Bhamra amesema kuwa watahakikisha ukarabati wa magari hayo unamalizika kwa wakati huku akieleza kuwa wataendelea kushirikiana na mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam bega kwa bega.

  Ikumbukwe kuwa Mnamo Mwezi 14 mwaka huu jumla ya magari mabovu ya polisi 26 yalisafirishwa kutoka Dar es salaam kuelekea Mkoani Kilimanjaro kwaajili ya kufanyiwa ukarabati na kubadili mwonekano

  0 0


  Na Ripota wa Mafoto Blog, Kibaha

  MBUNGE wa Kibaha mjini, Silyvestry Koka (kulia) na Diwani wa Kata ya Sofu, Yusuf Mbonde, wakishirikiana na wananchi wa kata hiyo Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani, kusafisha eneo lililo na majani kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa Zahanati. Mhe. Mbunge leo asubuhi alifanya ziara ya kushitukiza katika eneo hilo baada ya kupata tetesi kuwa eneo hilo limeuzwa.

  Aidha imeelezwa kuwa tetesi za kuuzwa kwa eneo hilo zilimfikia Diwani wa Kata hiyo, Bw.Mbonde, aliyeamua kumfuata Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Kibaha, Jenifer Ommolo, ambaye 'eti' alikiri kuwa jambo hilo nalitambua na kumwahidi kuwa wangepewa eneo mbadala wa hilo, jambo ambalo Diwani hakukubariana nalo na kuamua kulifikisha kwa Mhe.Mbunge wake.

  Mbunge huyo, alifika eneo hilo na kukutana na wapiga kura wake na kuamua kushiriki nao zoezi la kusafisha baada ya baadhi ya wananchi kukumbwa na hofu wakidai kuwa eneo hilo lilibadilishwa lengo la matumizi kwa kumgawia mtu aliyejulikana kwa jina la Mchome, ili kuliendeleza, ambaye pia hadi Mbunge anafika leo alikuwa bado hajaanza ujenzi wa aina yeyote.

  Imeelezwa kuwa eneo hilo baada ya kutolewa kwa ajili ya kujengwa Zahanati ambayo kwa kiasi kikubwa ilitakiwa kujengwa kwa ushirikiano mkubwa na wananchi ambao wengi wao walipigwa na butwaa na kurudi nyuma baada ya kusikia eneo hilo amegaiwa Mchome, aliyetakiwa kuliendeleza.

  Baada ya Mbunge Koka kuwasili eneo hilo hii leo asubuhi, wananchi wajitokeza na kuonyesha ushirikiano huo kwa kushirikiana na viongozi wao, na baadaye kubaki na matumaini ya kuona kinajengwa kile walichokikusudia baada ya Mbunge kutoa tamko kwa kusema eneo hilo linatakiwa kujengwa Zahanati ya wananchi na si kitu kingine.
  Mbunge wa Kibaha mjini, Silyvestry Koka, akizungumza na wananchi wa Kata ya Sofu Wilayani Kibaha, wakati wa zoezi la kufyeka na kusafisha eneo la kujenga Zahanati,ambapo alilaani kitendo hicho cha uuzwaji wa eneo la wananchi alichokiita cha kitapeli.
  Wananchi wakimsikiliza kwa makini mbunge wao, baada ya zoezi hilo.

  0 0


  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (kulia), akikabidhiwa kadi ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi, muda mfupi baada ya Mhe. Waziri kujiunga na Mpango huo leo Julai 8, 2017, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere kunakofanyika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, ambapo PSPF inatoa huduma zote kwenye Maonesho hayo.
  Waziri Dkt. Mpango, (kulia), akimsikilzia kwa makini Bw. Njaidi kuhusu faida zitokanazo na kujiunga na Mpango wa PSS

  Waziri Dkt. Mpango(kulia), akipokea fomu ya kujiunga na PSS, kutoka wka Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Msanii maarufu, Mrisho Mpoto. Katikati ni Afisa Habari Mwanamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi.
  Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Habari na Picha wa Idara ya Habari Maelezo, Bw. Rodney Thadeus, akiweka dole gumba kwenye fomu ya kujiunga na uanachama wa PSPF kupitia PSS, leo Julai 8, 2017
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango,(pichani) amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari na kuhimiza wananchi kufanya hivyo kwani moja ya faida kubwa ni kujihakikishia kuwa na bima ya Afya.

  Waziri aliyasema hayo leo Julai 8, 2017, wakati alipotembelea banda la PSPF lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, maarufu Sabasabawakati wa Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea.

  “Mimi nitoe wito kwa wananchi kujiunga zaidi na mpango huu kwani watafaidika na huduma ya afya na nyinyi muongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi ili wajiunge zaidi.” Alisema Mhe. Dkt. Mpango.

  Dkt. Mpango pia alikabidhiwa kadi yake ya uanachama muda mfupi baada ya kujiunga.

  “Mheshimiwa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari una faida nyingi na tumewalenga hasa watu wa kawaida kama vile wajasiriamali, wakulima, mama lishe, bodaboda, na machinga, na tumekuwa tukipata watu wengi wanaokuja kujisajili na Mpango huu na wengi wao wamevutiwa na hii Bima ya Afya ambayo ni moja ya faida azipatazo mwananchama” Alisema Afisa Uhusoano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi wakati akimkabidhi Mhe. Waziri akdi yake ya uanachama.

  Bw. Njaidi pia alimwambia Mhe. Waziri kuwa, kwa kujiunga kwake na Mpango huo wa uchangiaji wa Hiari, kutasaidia pia kuwakadia bima ya afya wasaidizi wake katika miradi kama vile ya shambani na ufugaji.

  “ Hawa wote wanawezakuingia kwenye mpango huu wa bima kupitia uanachama wako katika Mfuko.” Alimuhakikishia Mhe. Waziri.

  Waziri Mpango (kulia), akiuliza maswali kwa maafisa wa PSPF
  Mwananchi akisoma kipeperushi chenye taarifa za PSPF alipotembelea banda la Mfuko huo leo Julai 8, 2017
  Baada ya Mwanachi huyu kuelewa huduma za PSPF na faida zake kwake, hatimaye alikata shauri la kujiunga na Mpango wa PSS, kwa kujaza fomu kama picha hii inavyojieleza.
  Waziri Dkt. Philip Mpango, (kulia), akipokea mkoba wenye vipeperushi vya taarifa mbalimbali za PSPF, kutoka kwa balozi wa Mfuko huo, Msanii maarufu Mrisho Mpoto baada ya kutembelea banda la Mfuko huo leo Julai 8, 2017
  Mhandisi Ally Shanjirwa wa PSPF, akiwapatia maelezo wananchi hawa waliofika kutembelea banda la Mfuko huo
  Bw.Noah Amri, (kulia), Afisa wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akizungumza na mwanchi huyu aliyeshika fomu yakujiunga na Mpango huo
  Maafisa wa PSPF wakiwa kazini.

  0 0

  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini,Profesa James Mdoe, wakati alipoenda kukagua mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi II, Julai 8, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea maelezo ya maendeleo ya mradi kutoka kwa Meneja mradi Stephen Manda, wakati akikagua mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi II, Julai 8, 2017. 
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Tito Esau, wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi II, Julai 8, 2017. 
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiongea na Wananchi wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi II, Julai 8, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi II, Julai 8, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tanesco Balozi Dkt. James Nzagi, wakati alipoenda kukagua mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi II, Julai 8, 2017.

  *Asema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi ya kuzalisha umeme wa Kinyerezi II na kusema kwamba ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wake.

  Amesema hayo leo (Jumamosi, Julai 08, 2017) alipotembelea mradi huo wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia unaojengwa eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam.

  Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa mradi huo kutaliwezesha Taifa kuwa na umeme wa uhakika, utakaowezesha kuendesha viwanda.

  Amesema mkakati wa Serikali ni kuongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme ili Watanzania wapate umeme mwingi utakaosambazwa hadi vijijini kwa gharama nafuu.

  “Tunataka tupate umeme wa kutosha ili viwanda vitakavyojengwa viwe na nishati ya uhakika na ya gharama nafuu. Ni wajibu wetu kuendelea kuimarisha utekelezaji wa miradi hii.” Amesema.

  Naye, Meneja wa Mradi wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi, Mhandisi Stephen Manda amesema gharama za mradi wa Kinyerezi II ni dola milioni 344.

  Meneja huyo amesema tayari mradi huo umefikia asilimia 66.32 ya ujenzi wake na sasa wako katika hatua mbalimbali za kukamilisha, ikiwemo ujenzi wa misingi ya mitambo na jengo la kuendeshea mitambo.

  “Pia tunaendelea na ujenzi wa nguzo za kupokelea laini ya msongo wa kilovoti 220 kutoka Kinyerezi I hadi Kinyerezi II, ambapo mtambo wa kwanza wa megawati 30 utawashwa ifikapo Desemba 2017 na kila mwezi tutaingiza megawati 30 katika gridi ya Taifa.”

  Amesema miradi iliyoko katika eneo hilo ambayo iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji ni Kinyerezi 1 (150MW), Kinyerezi I Extension (185MW ) na Kinyerezi II (240MW).

  Mhandisi Manda ameongeza kuwa mradi wa Kinyerezi 1 (150MW) ulikamilika Machi 2015 na miradi mwili ya Kinyerezi 1-extension na Kinyerezi II inatarajiwa kukamilika mwaka 2018.

  Mhandisi Manda amesema miradi mingine inayotarajiwa kujengwa katika eneo hilo ni wa Kinyerezi III (600 MW) na Kinyerezi IV utakaozalisha (450 MW).

  Awali Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bi. Sophia Mjema ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda alisema mradi huo umewanufaisha wananchi wengi wa eneo hilo.

  Alisema hadi sasa wananchi 100 wa eneo la Kinyerezi wameajiriwa katika miradi hiyo ambapo ni sawa na asilimia 40 ya watumishi wote.

  Bi. Sophia alisema mbali na ajira pia wananchi wa eneo hilo watanufaika kwa kuboreshewa huduma mbalimbali za kijamii katika eneo hilo zikiwemo za maji na elimu ambapo wameahidiwa kupewa madawati ya shule tano.

  0 0

  Ndoo za maji zikiwa zimepangwa barabarani na wananchi wa Kijiji cha Magorofani Kata ya Igulwa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita kwa lengo la kumuonesha Mbunge wa jimbo hilo Doto Mashaka Biteko kisima ambacho kimekuwa Hakitoi maji kwa muda mrefu na adha ambazo wamekuwa wakikutana nazo kutokana na ukosefu wa maji Kijijini hapo.
  Wananchi wa Kijiji cha Magorofani wakiwa wamebeba ndoo wakizitoa Barabarani baada ya Mbunge kushuka kwenye gari na kuwasikiliza madai yao ya uhaba wa maji.
  Mbenge wa Bukombe Doto Biteko pamoja na viongozi wa Kata ya Igulwa akiwemo Diwani wa Kata hiyo,Richard Mabenga wakielekea kwenye eneo la kisima ambacho kimelalamikiwa na wananchi kutokutoa maji kwa muda Mrefu.
  Kisima ambacho kimelalamikiwa na wananchi ambacho kimekuwa akitoi maji .
  Mheshimiwa ,Doto Biteko akipatiwa maelezo na moja kati ya wananchi ambao wapo kijijini hapo juu ya kisima ambacho kimekuwa akitoi maji.
  Diwani wa Kata ya Igulwa Richard Mabenga akielezea jitihada ambazo zinaendelea kufanyika juu ya tatizo la maji kwenye kata hiyo,
  Mhandisi wa Maji Wilayani Bukombe Aaron Swai akielezea Jitihada ambazo zinaendelea za kumaliza au kupunguza tatizo la maji kwenye kata Hiyo.
  Mbunge wa Bukombe ,Doto Biteko akiwa amemsimamisha Mhandisi wa Maji kuelezea jitihada za kusambaza maji kwenye maeneo ambayo bado yanachangamoto ya maji.
  Mheshimiwa Doto Biteko akizungumza na wananchi wa Kijiji cha magorofani kwenye mkutano wa uzinduzi wa barabara.(PICHA NA JOEL MADUKA WA MADUKA ONLINE0)


  Wanakijiji wa kijiji cha Magorofani Kata ya Igulwa Wilayani Bukombe Mkoani Geita ,wamelazimika kufunga barabara kwa kutumia Ndoo za kuchotea maji wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo Hilo,Mh Dotto Biteko kwa madai ya kuwa na changamoto ya ukosekanaji wa maji kwa muda mrefu.

  Mh,Dotto ambaye alikuwa kwenye moja kati ya shughuli za kukagua na kujionea ujenzi wa barabara pamoja na kufungua kijijini hapo amekutana na kundi la wanawake pamoja na watoto wakiwa wamefunga barabara na wakiomba kutatuliwa adha hiyo ambayo imekuwa ikiwasumbua ya kukosekana kwa maji.

  Wakizungumza kwa Nyakati tofauti na mtandao wa Madukaonline baadhi ya wananchi wa kijiji hicho,Faines James,Mirembe Ngussa na Happynes Hai,wameelezea kuwa wamekuwa na shida ya maji kwa muda mrefu na kwamba kilichimbwa kisima lakini nacho hakitoi maji hivyo uamuzi wa kuweka ndoo kwenye barabara walitaka kumuonesha mbunge wao namna ambavyo wamekuwa wakipata shida ya maji.

  Aidha kwa Upande wake Diwani wa Kata Hiyo ,Richard Mabenga amekiri kuwepo kwa tatizo la maji na kwamba hadi sasa kuna visima vitatu tu ambavyo vinahudumia kata nzima na watu ambao wanategemea visima hivyo ni wakazi elfu kumi na tisa mianane (19800).

  Kutokana na tatizo Hilo ambalo wananchi wameliwakilisha kwa Mbunge wao,Mhandisi wa Mji wilayani hapo Aaron Swai ,amesema kuwa serikali kwenye bajeti yake ya mwaka 2017/18 imepanga kujenga mtandao wa maji safi na salama kwenye kata hiyo ambao utahudumia watu zaidi ya elfu kumi na nane na kwamba watu zaidi ya asilimia 81 watakuwa wanapata maji safi na salama.

  Hivyo kutokana na hali hiyo Mbunge Dotto Biteko amewahakikishia wananchi kuwa kwa sasa wana miradi kumi ya maji na kwamba moja kati ya kata ambayo imetengewa fedha
  nyingi za kujenga mradi wa maji ni pamoja na kata hiyo na kwamba watahakikisha
  wanaleta maji kwenye kata hiyo na kwamba mwisho wa mwezi huu mkandarasi atakuwepo kwenye kata hiyo.

  Kata ya Igulwa inawakazi zaidi ya elfu 22,000 na ambao wanapata maji safi na salama ni aslimia kumi tu ambayo ni sawa na wananchi 2,000.

  0 0
  0 0

  Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akipewa Maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na Mahakama ya Tanzania katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi Mhe. Joachim Tiganga alipotembelea banda hilo sehemu ya Mahakama Kuu.
  Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akizungumza jambo na watumishi wa Mahakama alipotembelea banda la Mahakama ya Tanzanaia sehemu ya Mahakama Kuu Divisheni ya kazi leo jijini Dar es salaam.
  Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akizungumza jambo na watumishi wa Mahakama alipotembelea banda la Mahakama ya Tanzanaia sehemu ya Mahakama Kuu Divisheni ya kazi leo jijini Dar es Saalaam.
  Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akiangalia ukuta uliojegwa kwa kutumia Teknolojia ya Moladi alipotembelea banda la wadau wa Mahakama (Moladi Tanzania). Mahakama ya ya Tanzania inatumia Teknolojia ya Moladi kujenga baadhi ya Mahakama zake.
  Fundi Mchundo wa Mahakama ya Tanzania, Hassan Dunia akimuelezea Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu kuhusu ujenzi wa majengo ya Mahakama kwa kutumia teknolojia ya Moladi leo alipotembelea banda la wadau wa Mahakama (Moladi Tanzania).
  Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi Mhe. Joachim Tiganga akimsindikiza Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu baada ya kumaliza kutembelea banda la Mahakama ya Tanzania

  0 0

  Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiongoza maandamano ya Mabalozi wa Usalama Barabarani kuingia Uwanja wa Mashujaa, wakiadhimisha siku yao iliyofanyika kitaifa mkoani Dodoma leo.Kulia ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo,Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,DCP Mohamed Mpinga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani ambapo aliwaasa madereva kufuata sheria ili kuweza kupunguza tatizo la ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na kuacha idadi kubwa ya wahanga wa ajali hizo.Wapili kushoto ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo,Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,DCP Mohamed Mpinga na anayefuatia ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma,Lazaro Mambosasa. Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa Uwanja wa Mashujaa,leo mkoani Dodoma.
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambae pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,DCP Mohamed Mpinga, akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani ambapo aliwaasa askari wa usalama barabarani kusimamia sheria ili kuweza kupunguza tatizo la ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na kuacha idadi kubwa ya wahanga wa ajali hizo.Kulia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na kulia ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma,Lazaro Mambosasa. Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa Uwanja wa Mashujaa,leo mkoani Dodoma.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma,Lazaro Mambosasa akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani ambapo aliwashukuru mabalozi hao kuchagua mkoa wa Dodoma kufanyia maadhimisho hayo na kuahidi kuelimisha watumiaji wa vyombo vya moto sheria na kanuni za usalama barabarani ikiwa anaongoza mkoa ambao ni Makao Makuu ya nchi .Wakwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambae pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,DCP Mohamed Mpinga.Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa Uwanja wa Mashujaa,leo mkoani Dodoma.
  Mabalozi wa Usalama wa Barabarani wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani ambapo aliwaasa madereva kufuata sheria ili kuweza kupunguza tatizo la ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na kuacha idadi kubwa ya wahanga wa ajali hizo. Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa Uwanja wa Mashujaa,leo mkoani Dodoma.

  Msanii Faustine Matina ambae ni Balozi wa Usalama Barabarani, akiimba wimbo wa kuhimiza masuala ya kuzingatia sheria za usalama barabarani wakati wa Siku ya Maadhimisho ya Mabalozi wa Usalama Barabarani, iliyofanyika kitaifa leo katika Uwanja wa Mashujaa,mkoani Dodoma.
  Mhanga wa ajali anayefahamika kwa jina la Mpemba Asilia, akizungumza na Mabalozi wa Usalama Barabarani, alipofika katikaMaadhimisho ya Mabalozi wa Usalama Barabarani yaliyofanyika kitaifa leo katika Uwanja wa Mashujaa,mkoani Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(watano kulia),akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mabalozi wa Usalama Barabarani wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani yaliyofanyika kitaifa Uwanja wa Mashujaa,leo mkoani Dodoma.Wasita kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambae pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,DCP Mohamed Mpinga

  0 0

  Watemi wa Kisukuma Kanda ya Ziwa Victoria na viongozi wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania( Tanzania Albinism Society -TAS) wamefanya usafi wa mazingira kisha kula chakula cha pamoja na watoto wenye ualbino wanaolelewa katika kituo cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.

  Watemi hao wakiongozwa na Katibu Watemi wa Kisukuma Kanda ya Ziwa, Mtemi Charles Balele Itale wa Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza walitembelea kituo hicho leo Jumamosi Julai 8,2017. 

  Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba alisema chama hicho kimekuwa na ushirikiano mkubwa na machifu wa kanda ya ziwa hicho kuamua kushiriki nao katika kufanya usafi wa mazingira katika kituo cha Buhangija. 

  “Malengo ya kuja hapa kwanza ni kuunga mkono serikali ya awamu ya tano kuhusu masuala ya usafi,pili ni kuwapa ujumbe watoto hawa kuwa wawe na utamaduni wa kufanya usafi hata wanaporudi kwenye familia zao,tatu tumekuja kula chakula cha pamoja na watoto hawa ili kuonesha kuwa tuko pamoja nao”,alieleza Temba. 

  Temba alitumia fursa hiyo kuiomba serikali kuchunguza utitiri wa mashirika yaliyoanzishwa nchini ambapo sasa yapo zaidi ya 10 na kufuatilia vituo mbalimbali vilivyoanzishwa kwa lengo la kuwahudumia watu wenye ualbino hususani watoto kwani sasa vipo takribani 20 lakini wahusika wa vituo hivyo hawasaidii walengwa. 

  Temba alisema mashirika mengi yamekuwa yakijikita katika kupiga vita mauaji ya watu wenye ualbino huku yakisahau kuwa watu wenye ualbino wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa elimu na saratani ya ngozi ambayo imekuwa ikiua watu wengi wenye ualbino. 

  Katibu Watemi wa Kisukuma Kanda ya Ziwa, Mtemi Charles Balele Itale wa Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza alimpongeza mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ualbino kuwakutanisha pamoja katika kituo hicho. “Juhudi hizi zinaonesha jinsi tunavyowatambua,tunavyowapenda na tunavyowajali watu wenye ualbino,kwa hiyo katika nafasi zetu za nyadhifa mbalimbali tunajitahidi kuelimisha na kuwezesha jamii iwatambue,iwajali,iwapende na kuwapokea katika jamii na watoto warudi kwenye familia zao na kuishi kama watoto wengine”,alieleza Mtemi Balele. 

  “Nimefurahishwa na taarifa ya uongozi wa kituo hiki kuwa sasa watoto wameanza kwenda likizo kuwaona wazazi wao,hili ni jambo jema sana,Sisi machifu tuna jukumu letu ni kuielimisha jamii iwapokee,iwakubali,isiwanyanyase,isiwanyanyapae hivyo sisi kwa kushirikiana na TAS tutashirikiana katika kutafikia hayo malengo”,aliongeza Mtemi Balele. 

  Awali akizungumza katika kituo hicho,Mwalimu Mlezi wa Shule ya Msingi Buhangija, Frola Kakutebe alisema kati ya watoto wenye ualbino 140,waliopo katika kituo hicho,72 wameenda likizo na 68 wamebakia kituoni baada ya shule kufungwa kinyume na miaka ya nyuma ambapo watoto hao walikuwa hawaendi likizo kuonana na ndugu zao. 

  Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,Selemani Kipanya aliiambia Malunde1 blog kuwa,sasa Kituo hicho kimepoteza sifa ya kuitwa kituo bali ni shule kwani tofauti na siku za nyuma hivi sasa watoto wanaoishi hapo wote wanasoma shule na wanaishi katika mabweni yaliyopo katika shule hiyo.
  Katibu Mtendaji wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa,Mussa Mussa akizungumza katika kituo/Shule ya Msingi Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.Kulia ni Katibu wa Umoja wa Watemi wa Kisukuma kanda ya Ziwa, ambaye ni chifu/mtemi wa Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza Charles Dotto Balele.Kushoto ni Mwalimu Mlezi wa Shule ya Msingi Buhangija, Frola Kakutebe-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
  Katibu wa Umoja wa Watemi wa Kisukuma kanda ya Ziwa, ambaye ni chifu/mtemi wa Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza Charles Dotto Balele Itale akizungumza katika kituo cha Buhangija.Kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba 
  Mtemi Balele akizungumza katika kituo cha kulelea watoto wenye ualbino cha Buhangija.
  Kushono Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba akifuatiwa na Mtemi Nyamilonda III Mikomangwa Aron wa Mwanza ‘Ng’wanza (katikati),kulia ni Mtemi Wenceslaus Seni wa Kanadi mkoani Simiyu wakiwa eneo la tukio. 
  Kushoto ni Mtemi Wenceslaus Seni wa Kanadi mkoani Simiyu,akifuatiwa na Mtemi Charles Gagambaseni Dogani wa Seke – Kishapu mkoani Shinyanga,kulia ni Mtemi Charles Lubasha Kimwaga Kaswende wa Luhumbo mkoani Shinyanga.
  Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo aliiomba serikali kuona umuhimu wa kuwapa nguvu viongozi wa kimila kama zamani kwani wanazungukwa na watu wengi hivyo kuwa na nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko katika jamii.
  Watoto,walimu na maafisa kutoka TAS wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
  Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba akizungumza katika kituo cha Buhangija.
  Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba akizungumza.
  Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba akisisitiza jambo.
  Watoto na maafisa kutoka TAS wakiwa eneo la tukio
  Katibu wa Umoja wa Watemi wa Kisukuma kanda ya Ziwa, ambaye ni chifu/mtemi wa Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza Charles Dotto Balele Itale akila chakula na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.
  Mtemi Wenceslaus Seni wa Kanadi mkoani Simiyu akila chakula na watoto wa wanaolelewa katika kituo cha Buhangija,ambapo wapo wenye ualbino,wasiosikia na wasioona.
  Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba,Mtemi Wenceslaus Seni wa Kanadi mkoani Simiyu na Mtemi Charles Gagambaseni Dogani wa Seke – Kishapu mkoani Shinyanga wakila chakula na watoto kituo cha Buhangija.
  Mtemi Charles Gagambaseni Dogani wa Seke – Kishapu mkoani Shinyanga akila chakula na watoto.
  Watemi na Viongozi wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS wakiendelea kula chakula na watoto katika kituo cha Buhangija.
  Mtemi Charles Lubasha Kimwaga Kaswende wa Luhumbo mkoani Shinyanga akila chakula na watoto.
  Mtemi Nyamilonda III Mikomangwa Aron wa Mwanza ‘Ng’wanza akila chakula na watoto.
  Afisa Mahusiano na Habari kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS)Josephat Torner akila chakula na watoto.
  Kushoto ni Katibu wa Umoja wa Watemi wa Kisukuma kanda ya Ziwa,Charles Dotto Balele Itale ambaye ni Mtemi wa Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza akifuatiwa na Afisa Mahusiano na Habari kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) Josephat Torne (katikati) na Afisa Programu kutoka Chama cha watu wenye ualbino Tanzania Severin Edward wakifanya usafi katika kituo cha kulelea watoto wenye ualbino cha Buhangija manispaa ya Shinyanga.
  Mtemi Wenceslaus Seni wa Kanadi mkoani Simiyu akifanya usafi karibu na choo wa watoto katika kituo cha Buhangija.
  Mtemi Nyamilonda III Mikomangwa Aron wa Mwanza ‘Ng’wanza akiweka uchafu kwenye ndoo. 
  Kulia ni Afisa Programu kutoka Chama cha watu wenye ualbino Tanzania Severin Edward na Mwalimu Mlezi wa Shule ya Msingi Buhangija, Frola Kakutebe wakifanya usafi katika kituo cha Buhangija.


  Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog

  0 0

  Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini William Mkapa akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo jipya la upasuaji kwenye kituo cha afya cha Nkomo kilichopo kijiji cha Mwalushu,Wilayani Itilima-Simiyu
  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Itilima Dkt. Anold Musiba akitoa maelezo kwa Rais Mstaafu,kulia ni Balaozi wa Japan nchini Tanzania Mhe.Masaharu Yoshida. Jengo hilo limejengwa na Ubalozi wa Japan kupitia Taasisi ya Benjamini Mkapa na kugharimu kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 270.
  Rais Mstaafu akiangalia moja ya vifaa vilivyomo kwenye chumba cha upasuaji .Ujenzi wa jengo hilo kwa asilimia kubwa itawasaidia akina mama wajawazito ambapo awali wananchi wa kijiji hicho walikua wakitembea kilometa arobaini kwenda kupata huduma za namna hiyo.
  Jengo hilo la upasuaji linavyoonekana
  Msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo kutoka Taasisi ya Benjamini Mkapa Geofrey Nyaluke (mwenye fulana ya jano) akitoa maelezo kwa Viongozi waliofika kushuhudia ufunguzi wa jengo hilo
  Rais Mstaafu akicheza mara baada ya ufunguzi wa jengo hilo,kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Antony Mtaka na kulia ni Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Daudi Njalu  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwahutubia wananchi(hawapo pichani)ambapo alisema katika bajeti ya mwaka 2017/2018 Wilaya ya Itilima ametengewa kiasi cha shilingi milioni 584 kwa ajili ya ununuzi wa dawa ukilinganisha na bajeti iliyopita ya mwaka 2016/2017 ambapo shilingi milioni 315 zilitengwa.
  Wananchi wa kijiji cha Mwalushu wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa jengo la upasuaji katika kituo cha afya cha Nkomo.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA AFYA)

  Baadhi ya Viongozi waliohudhuria ufunguzi huo akiwepo mke wa Rais Mstaafu Mama Anna Mkapa

  0 0

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini'TFS', Prof ; Dos  Santos Silayo  akiwa katika banda la TFS na Familia yake katika Maonesho ya 41 ya Sabasaba jijini Dar es Salaam ambapo aliweza kukagua namna ya shughuli za Tasisi hiyo zinavyofanywa .
  Afisa  Ufugaji Nyuki kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Mwanahamisi Mapolu   akizungumza na wawekezaji kutoka Oman waliofika katika  banda la TFS cujus ni aina gani ya Asali zinapatikana niching
  Mjumbe wa Bodi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) , Sauda Kilumanga akipata maelezo kutoka kwa Afisa Ufugaji Nyuki kutoka TFS, Mwanahamis Mapolu wakati alipotembelea Banda hilo katika maonesho ya 41 ya Sabasaba jijini Dar es Salaam
  Mjasiliamali kutoka Viana Kushoba wanaotengeneza Mashine ya make Mbadala akiwapa make wakazi wa jiji waliomtembelea katika Maonesho ya 41 ya Sabasaba na kununua mkaa huo ambao ni rafiki wa mazingira na unazuia ukataji miti hivyo kusaidia katika kulinda misitu yetu.
  Afisa ufugaji Nyuki wa Shamba la miti la serikali la Sao Hill linalomilikiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS),Said Abubakary  akionesha waandishi wa habari moja ya malighafi inayotokana na misitu katika kutengeneza vipodozi vya aina mbalimbali

  0 0

   Kamishna wa Vibali na Pasi nchini, Musanga Etimba akitoa maelezo kwa mwananchi Oliver Gabriel, aliyetembelea Banda la Idara ya Uhamiaji katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
   Mwananchi aliyetembelea Banda la Idara ya Uhamiaji, Oliver Albert akiuliza maswali kwa Kamishna wa Vibali na Pasi nchini, Musanga Etimba baada ya kutembelea Banda la Idara hiyo katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mdhibiti wa Pasipoti nchini, Mrakibu Mwandamizi Peter Mwitwa.
   Mkaguzi wa Idara ya Uhamiaji nchini, Mustafa Kipingu (kushoto), akitoa huduma kwa mwananchi aliyetembeleaBanda la Idara hiyo katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
  zi wa Idara ya Uhamiaji, Kitengo cha Uhusiano, Aziz Kirondomara (kushoto), akitoa huduma kwa mwananchi aliyetembeleaBanda la Idara hiyo katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0 0

   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akipeana mkono na Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. LU Youqing, walipokutana katika viwanja vya Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (sabasaba), Jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuhusu namna ya kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kukata bima ili kujikinga na majanga, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango lilipo katika viwanja vya maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (sabasaba), Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Bw. Sam Kamanga.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi wa uendeshaji wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Naftal Sigwejo baada ya kuulizwa kuhusu ubora wa baadhi ya bidhaa zinazotolewa Serikalini baada ya kutembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akimpongeza Mzazi wa kijana Msuya Mageta (katikati) aliyejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF kupitia mpango wa Wote Scheme katika Banda la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), Jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa saba kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF baada ya kutembela Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia) akiwa tayari kupokea fomu ya kujiunga kupitia mfumo wa uchangiaji wa hiari kupitia Mfuko wa Pensheni wa PSPF kutoka kwa Msanii Mrisho Mpoto baada ya kutembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), Jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akipata maelezo kutoka Mfuko wa Pensheni wa GEPF kuhusu huduma na mchango wa mfuko huo katika maendeleo ya viwanda, alipotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akipata maelezo kutoka  Banda la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuhusu njia ya kisasa ya ufugaji Samaki alipotembelea Banda hilo katika Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akimpongeza mtumishi wa Suma JKT baada ya kutoa maelezo ya mtambo wa kuvuta maji katika viwanja vya maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es salaam.

   Afisa Mwandamizi wa Idara ya Bajeti wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Adam Msumule akitoa elimu ya Bajeti kwa wananchi waliotembelea katika banda la Wizara hiyo katika maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es salaam.
  (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

  0 0

  · Yaanza kuuza makaa hayo kwa kasi
  · Yakiri kuwa na akiba ya makaa ya mawe ardhini ya kuchimba kwa zaidi ya miaka mia moja. 

  Na Koleta Njelekela-STAMICO

  Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeanza rasmi kuuza makaa ya mawe yanayozalishwa katika Mgodi wake wa Kabulo ili kukidhi mahitaji ya watumiaji wakiwemo viwanda vya saruji na nguo na hivyo kukuza Pato la Taifa.

  STAMICO ilianza uzalishaji wa majaribio wa makaa ya mawe katika mgodi wa Kabulo uliopo Kijiji cha Kapeta, Wilaya ya Ileje Mkoa wa Songwe mnamo tarehe 30 Aprili 2017 na mpaka sasa imeweza kuzalisha tani 6,197.

  Akihojiwa na Mwandishi wa Habari hii, mara baada ya zoezi la uuzaji makaa ya mawe kuanza rasmi huko Kabulo jana (6 Julai 2017), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Bwana Hamis Komba, amesema Shirika kupitia mradi wake wa makaa ya mawe wa Kabulo, sasa linaweza kukidhi mahitaji ya watumiaji wote wa makaa ya mawe nchini, katika kipindi cha miaka mia mfululizo kutokana na kuwepo kwa mashapo ya kutosha (mineral resources) na nyenye ubora wa juu katika mgodi huo.

  Bwana Komba amesema matarajio ya Shirika ni kuongeza kiwango cha uchimbaji makaa ya mawe kutoka tani 600 hadi tani 1000 kwa siku, hatua ambayo itaiwezesha STAMICO kuzalisha zaidi ya tani 300,000 kwa mwaka. 

  “Nchi yetu ina rasilimali nyingi za madini yakiwemo makaa ya mawe, hivyo tunapenda kuwahikishia wenye viwanda vinavyotumia makaa hayo hususani viwanda vya Saruji (Cement), kwamba nchi ina makaa ya kutosha hivyo Serikali haitoshindwa kutosheleza mahitaji na makaa yam awe huku ikitekeleza kwa vitendo azma yake kujenga Tanzania yenye viwanda, ili kukuza uchumi wa Taifa" Alifafanua Bwana Komba.

  Amewataka wenye viwanda nchini, kuwasilisha maombi ya kununua malighafi ya makaa ya mawe, ili STAMICO iweze kuwauzia makaa hayo, ambayo yana viwango vya ubora vinavyofaa katika uzalishaji wa nishati ya umeme viwandani. 

  Aidha Kiongozi Mtendaji Mkuu wa STAMICO amesema hivi sasa Shirika linaendelea kuimarisha mradi huo wa Kabulo, kwa kuboresha miundombinu, maabara ya kudhibiti ubora wa makaa na kununua mashine mpya (Crusher) kwa ajili ya kuponda makaa, kulingana na mahitaji mahususi ya vipimo vinavyhitajiwa na wateja katika soko.

  “changamoto zilizopo katika utekelezaji wa mradi huu ni pamoja na mtaji mdogo, mabadiliko ya hali ya hewa hasa nyakati za mvua na ubovu wa kipande cha barabara yenye urefu wa zaidi ya kilomita 15 kutoka katika eneo la mgodi, mpaka eneo la mauzo, ambapo barabara hiyo haiwezi kumudu malori ya zaidi ya uzito wa tani 15 kupita”. alibainisha Bwana Komba.

  Awali Mratibu wa Mradi wa Makaa ya Mawe wa Kabulo-Kiwira Bwana Alex Rutagwelela, amesema amefurahishwa na matokeo chanya ya mradi huo ya kufikia hatua ya uuzaji makaa ya mawe, kwani ni fursa nzuri kwa Shirika, baada ya Serikali kuweka zuio la kuagiza makaa ya mawe kutoka nchi za nje; wakati nchi ikiwa na makaa mengi ya mawe ardhini.

  Amesema STAMICO kupitia mradi huo, itaendelea kuimarisha viwango vya uzalishaji wa makaa ya mawe ili kuwafikia wateja wote kulingana na mahitaji yao

  “Uwezo wetu na utaalam katika uchimbaji makaa ya mawe ni wa kimkakati ili kuweza kukidhi soko la ndani na nje ya nchi. Lengo kuu la mradi huu ni kutosheleza mahitaji ya kuzalisha umeme wa viwango mbalimbali katika Mradi wa Umeme wa Kiwira na pia kutosheleza mahitaji ya Viwanda nchini vikiwemo vya saruji.”

  Naye Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa STAMICO, Bwana Deusdedith Magala amewasihi watumishi na wataalam wa Shirika hilo, kuendelea kujifunga mkanda na kufanya kazi kwa bidii ili kuivusha salama STAMICO katika kipindi hiki cha mpito, ambapo Shirika linafufua miradi yake ya uchimbaji madini; itakayoleta mafanikio makubwa na yenye maslahi mapana kwa Taifa.

  Bwana Magala amesema STAMICO imeweza kuanza uzalishaji wa makaa ya mawe katika Mgodi wa Kabulo kwa kutumia mtaji mdogo na kubana matumizi; hatua ambayo imedhihirisha kwamba STAMICO tumethubutu na tunaweza kutekeleza miradi yetu kwa wakati, pamoja na hali ngumu ya kifedha inayolikabili Shirika kwa sasa.

  “ni matumaini kuwa katika kipindi cha muda mfupi ujao, watumishi wote STAMICO tutafurahi, kwani tutaweza kupanua uzalishaji wa makaa ya mawe huku tukileta matokeo makubwa ya uzalishaji yenye maslahi makubwa kwa Shirika” Alifafanua Bwana Magala.

  Awamu ya kwanza ya Mradi wa uchimbaji makaa ya mawe wa Kabulo inatekelezwa kupitia leseni zake mbili za uchimbaji mdogo wa madini Primary Mining Licences (PMLs) zilizopo ndani ya leseni ya utafiti ya Kabulo zenye ukubwa wa Hecta 16.52. 

  Leseni hizo mbili za Uchimbaji wa Awali wa Madini katika eneo hilo la Kabulo, zina zaidi ya tani milioni 35 zilizothibitishwa za mashapo ya makaa ya mawe, yaliyoko karibu na uso wa ardhi, katika mgodi huo wa Kabulo. 

  Kamishna wa Madini Tanzania Mhandisi Benjamin Mchwampaka akiwa katika picha ya pamoja na timu wa wataalam wa STAMICO (wanaotekeleza Mradi wa Uchimbaji Makaa ya Mawe-Kabulo) alipotembelea Mgodi huo hivi karibuni kukagua maendeleo ya mradi huo ambao ulianza rasmi uzalishaji makaa yam awe tarehe 30 Aprili, 2017 na kufanikiwa kuzalisha tani 6197 mpaka sasa. Soko la ndani la makaa hayo linawalenga wazalishaji viwandani hususani wale wa viwanda vya Saruji (Cement) na watengenezaji wa nguo, pamoja na magereza na watumiaji wengine wa majumbani.

  Shughuli za Uchimbaji Makaa ya Mawe zikiendelea katika mgodi wa Kabulo Kiwira, uliopo katika Kijiji cha Kapeta, wilaya ya Ileje, Mkoa wa Songwe. Leseni za Uchimbaji wa Awali wa Madini katika eneo hilo la Kabulo, zina zaidi ya tani milioni 35 zilizothibitishwa za mashapo ya makaa ya mawe, yaliyoko karibu na uso wa ardhi, katika mgodi huo wa Kabulo. Mashapo hayo yanaweza kuchimbwa kwa mfululizo kwa miaka mia moja ijayo.

  Mratibu wa Mradi wa Uzalishaji Mkaa ya Mawe wa Kabulo-Kiwira Bwana Alex Rutagwelela ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji wa STAMICO akielekeza kuhusu zoezi zima la upakiaji makaa ya mawe katika Malori tayari kwa ajili ya kupeleka katika eneo la mauzo lililopo katika kijiji cha Kasumulu, Wilaya ya Kyela, mkoa wa Mbeya. Mgodi huo wa Kabulo-Kiwira uliopo katika kijiji cha Kapeta, Wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe unamilikiwa na kuendeshwa na STAMICO kwa niaba ya Serikali.
  Malori ya Kampuni ya Lake Cement yakipakia Makaa ya Mawe katika eneo la mauzo ya makaa hayo, lililopo umbali wa kilometa mbili kutoka katika barabara kuu ya Mbeya, iendayo nchini Malawi. Eneo hilo la mauzo lipo katika kijiji cha Kasumulu, Wilaya ya Kyela, mkoa wa Mbeya. Makaa hayo ya Mawe yanazalishwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), katika mgodi wake wa Makaa ya Mawe wa Kabulo, ulipo katika kijiji cha Kapeta, Wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe.

  0 0

   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, Sezaria Makota, mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Wapili kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Winnie Kitazi, na kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani humo, SSP Mohamed Kitia.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiwasalimia Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Kondoa na Chemba mara baada ya kuwasili mjini Mkondoa kwa ajili ya ziara ya kikazi. 
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masaunia kizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Kondoa na Chemba mkoani Dodoma. Masauni amefanya ziara ya kikazi katika wilaya hizo. Wa kwanza kushoto  ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Sezaria Makota, na wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simoni Odunga.Wa kwanza Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani humo, SSP Mohamed Kitia.
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, Sezaria Makota wakati alipokua akitoa taarifa yake ya Wilaya kwa kiongozi huyo ambaye yupo ziarani katika Wilaya ya Kondoa na Chemba. 
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Chemba, mkoani Dodoma, Simon Odunga,wakati alipokua akitoa taarifa yake ya Wilaya kwa kiongozi huyo ambaye yupo ziarani katika Wilaya ya Kondoa na Chemba. 
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kondoa, SSP Mohamed Kitia wakati alipokua akitoa taarifa yake ya Ulinzi na Usalama wilayani humo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Sezaria Makota, na Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga. Masauni yupo ziara ya kikazi katika Wilaya hizo ambapo alizitembelea Taasisi zilizopo ndani ya Wizara yake.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa Chato mkoani Geita. Rais Mstaafu Mkapa katika siku ya kesho anatarajiwa kukabidhi nyumba 50 za watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa na Taasisi ya (Mkapa Foundation) katika mikoa ya Simiyu, Kagera na Geita.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa Chato mkoani Geita. Rais Mstaafu Mkapa katika siku ya kesho anatarajiwa kukabidhi nyumba 50 za watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa na Taasisi ya (Mkapa Foundation) katika mikoa ya Simiyu, Kagera na Geita. Kushoto ni Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita. Balozi huyo wa Japan katika siku ya kesho anatarajiwa kukabidhi mtambo wa kukamua Mafuta ya Alizeti (Double Refine) uliojengwa Chato mkoani Geita kwa Msaada wa Serikali ya Japan.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa Chato mkoani Geita.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa pamoja na wageni mbalimbali waliofika Chato kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazotarajiwa kufanyika kesho.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Geita Joseph Kasheku Msukuma aliyefika Chato pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita. PICHA NA IKULU.

  0 0

  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa hotuba yake wakati wa fainali za shindano la Bongo Style, lililofanyika makumbusho ya Taifa Jijini Dar ,linalohusisha fani za ubunifu wa mavazi,upigaji picha na uandishi wa miswada ya filamu ambapo aliipongeza Taasisi isiyo ya kiserikali ya Faru Arts and Development Organization(FASDO) kwa kuandaa mashindano hayo, alisema kuwa Serikali inalojukumu la kusaidia Asasi kama FASDO ambazo zinaingia katika maswala ambayo Serikali hawakuyawekea msingi mkubwa. "Naomba niagize na kuwa kuna watendaji wetu wa wizara katika sherehe hii mkae chini na watu wa FASDO ili mwaka kesho zoezi hili lifanyikie Bungeni Dodoma" Alisema Dkt. Mwakyembe.
   Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe (wa tatu kutoka kulia) akimkabidhi Agnes Nyahonga  tuzo na zawadi ya mfano wa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda   shindano la Bongo Style katika kipengele cha ubunifu wa mavazi.
   Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe(wa pili kutoka kulia) akimkabidhi Goodhope Elieskia maarufu kwa jina la Zagamba  tuzo na zawadi ya mfano wa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda   shindano la Bongo Style katika kipengele cha uandishi wa miswada ya Filamu
   Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na MichezoMh.  Dkt. Harrison Mwakyembe(wa kutoka kulia) akimkabidhi Masoud Masoud  tuzo na zawadi ya mfano wa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda   shindano la Bongo Style katika kipengele cha ubunifu wa mavazi.

   Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na MichezoMh.  Dkt. Harrison Mwakyembe(wa pili kutoka kulia) akimkabidhi Philip Florian  tuzo ya Best Personality aliyopokea kwa niaba ya Kelvin Mwanasoko ambaye hakuweza fika katika Mashindano hayo.
   Msanii Dullah Aka DY akitumbuiza wakati wa Fainali hizo
   Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mngereza akizungumza wakati wa fainali za Shindano la Bongo Style na kuipongeza Asasi ya Kiraia ya FASDO kwa ubunifu mkubwa.
   Mratibu wa FASDO Nchini Tanzania Bi. Joyce Msigwa akizungumza wakati mambo mbalimbali yanayohusu Asasi hiyo ikiwa ni pamoja na mafanikio waliyoyapata kama kuendesha shindano la Na mimi nipo pamoja na FASDO CUP na mengine mengi yahusuyo asasi hiyo.
  Ilikuwa ni 'Surprise' Kati kati ya Sherehe za Shindano la Bongo Style ambapo Mratibu Mkuu wa FASDO na Muasisi wa Asasi hiyo isiyo ya kiserikali Bi. Lilian Nabora(Aliyevaa Gauni Jekundu) alipofanyiwa Hafra fupi ya siku yake ya Kuzaliwa ambapo alitimiza miaka 50. Waliomsindikiza ni 'Team' ya FASDO pamoja na washiriki wa shindano hilo kwa mwaka 2017.
  Mratibu Mkuu na Muasisi wa FASDO Lilian Nabora akiongea wakati wa fainali za Bongo Style, alisema kuwa wamewekeza sana katika mitandao ya kijamii na hasa tovuti ya www.fasdo.org ili kuwafikia vijana wengi zaidi Tanzania nzima ambao wanauwezo na wanajiamini kuwa wanavipaji katika mambo mbalimbali wapate kujiunga katika taasisi hiyo,aliongeza kuwa mchakato wa kuwapata washindi ulipitia mchujo mpaka kuwapata washiriki bora 30,kisha 15, mpaka kufikia washindi watatu(3) "Mpaka sasa tumeweza kuwafikia vijana wanaokadiliwa kuwa 1,500 na mpaka sasa bado tunawahimiza wapate kujiunga nasi" alisema Bi. Lilian.
   Waliokaa katika Meza ni Majaji Upande wa ubunifu wa mavazi, na walio mstari wa mbele ni Majaji upande wa Miswada ya Filamu na upigaji picha.
  Baadhi ya washiriki upande wa Ubunifu wa Mavazi wakiwa wanaonesha Mavazi yao waliyo yabuni wao wenyewe
   Wageni waalikwa  wakifuatilia sherehe za Fainali za shindano la Bongo Style
   Mwenyekiti wa FASDO Bw. Stanley Kamana akitoa neno la Shukurani wakati wa Fainali za Bongo Style
   Washiriki wa Shindano la Bongo Style kwa Mwaka 2017 wakiwa wanafuatilia mambo mbali mbali wakati wa Shindano hilo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kiraia ya FASDO Bw. Tedvan Nabora akitoa neno la Shukurani kwa wote waliohudhuria katika Fainali za shindano la Bongo Style
  Picha ya pamoja ya  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe,Uongozi na Team ya FASDO,Majaji na washindi wa Bongo Style Competition kwa mwaka 2017.
  Picha zote na Laden Tedvan Nabora.

older | 1 | .... | 1297 | 1298 | (Page 1299) | 1300 | 1301 | .... | 1896 | newer