Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1276 | 1277 | (Page 1278) | 1279 | 1280 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Frank Shija - MAELEZO

  SERIKALI imesema kuwa hakuna chombo chochote cha habari kitakachochukuliwa hatua kwa kuandika habari zenye mrengo wa kukosa sera na utekelezaji wake kama ambavyo wadau wengi wamekuwa wakiaminisha umma.


  Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassan Abbasi wakati akizungumza katika Kipindi cha Habari Kuu kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha Startv mjini Dodoma.


  Dkt. Abbasi amesema kuwa Sheria na 12 ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 kifungu cha 51 kinatoa ruhusa kwa chombo cha habari kukosoa kwa lengo la kuonyesha njia mbadala katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.


  “Hakuna chombo cha habari kitakachochukuliwa hatua kwa kukosoa, haki hiyo ipo kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 kifungu cha 51, tutaendelea kuthamini na kufanyia kazi ukosoaji huo,” alisema Dkt. Abbasi.Hata hivyo Dkt. Abbasi amesisitiza kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kwa chombo kitakachokiuka sheria na misingi ya maadili ya taaluma ya habari kwa lengo la kulinda maslahi ya taifa.


  Dkt. Amesisitiza kuwa ni vyema wamiliki wa vyombo vya habari wakatumia uhuru huo wa kisheria kuchapisha habari zenye nia njema kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi badala ya kueneza hofu miongoni ya mwa jamii.


  Akijibu swali la muongozaji wa Kipindi kuhusu kufungiwa kwa Gazeti la Mawio, Dkt. Abbasi amesema kuwa Gazeti hilo halijafungiwa kutokana na kuandika habari ya kukosoa Serikali isipokuwa limekiuka miiko ya taaluma kwa kuandika habari za kushushia heshima na hadhi ya mtu katika jamii pamoja na kukiuka maagizo halali ya Serikali.


  Alisema kuwa kama ingekuwa kulifungia Gazeti hilo kwa sababu ya kuandika habari za kukosoa pengine lingekuwa limefungiwa muda mrefu kutokana na ukweli kwamba Gazeti hilo mrengo wake unafahamika kuwa ni wa ukosoaji.


  Akizungumzia dhana ya uhuru wa habari, Dkt. Abbasi amesema kuwa ipo haja ya wadau wa habari kufahamu dhana halisi ya uhuru wa habari badala ya kuendelea kufanya makosa ya tafsiri isiyo sahihi jambo ambalo linapotosha dhana nzima ya uhuru wa habari.


  Dkt. Abbasi amesema kuwa Mkataba wa Kimataifa wa mwaka 1966 wa Haki za Kiraia na Kisiasa, ibara ya 19 inaeleza haki za kupata habari ambayo inaenda sambamba na ukomo wa kutoa taarifa kwa maslahi ya nchi.


  Aidha Dkt. Abbasi ametoa rai kwa wadau wa habari nchini kuisoma sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016 iliyoanza kutumika rasmi badala ya kuyaachia makundi ya wanaharakati wapotoshe uhalisia wake. 


  Akizungumzia utekelezaji wa Sheria hiyo, Dkt. Abbasi amesema kuwa sheria imekwishaanza kutekelezwa katika hatua kadha ambapo alizitaja baadhi ya hatua hizo kuwa ni pamoja na utoaji wa Vitambulisho vya Waandishi wa HabarI.Alisema kuwa utoaji wa Vitambulisho hivyo umelenga kuwajengea uwezo wa kujiendeleza waandishi wa habari katika kipindi cha mpito cha miaka mitano ili kufikia vigezo stahiki vya taaluma.


  Tanzania imeingia katika Historia baada ya kutunga Sheria na 12 ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 ambayo imefuta Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976 ambayo imepitwa na wakati kutokana na mabadiliko ya teknolojia, uchumi na utamaduni.

  0 0


  Mabenki yameombwa kuwa tayari kukopesha mnyonyororo mzima wa sekta ya kilimo na mifugo hili kuunga mkono juhudi za Serikali za kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini.

  Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Augustino Chacha wakati akifungua mafunzo ya awamu ya pili yanayohusiana na Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo yanayoendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya TADB, Benki ya Taifa ya Kilimo na Maendeleo Vijijini India (NABAD) na Programu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani Mazao na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).

  Bw. Chacha amesema kuwa mabenki na taasisi za kifedha nchini hazina budi kuwekeza mtaji wa kutosha ili kuweza kukopesha sekta ya kilimo ambayo ni uti wa mgongo wa Tanzania na ambayo inaajiri zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini na pia kutoa kiasi cha zaidi ya asilimia 65 cha mali ghafi kwa ajili ya viwanda vya nchi.

  Ameongeza kuwa kuanzinshwa kwa TADB kunalenga kuwezesha mabenki ya biashara kupata fedha zenye masharti nafuu na endelevu ili ziweze kukopesha sekta ya kilimo ili kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

  “Hakuna haja ya kuogopa kukopesha sekta ya kilimo kwani ni sekta yenye umuhimu mkubwa kwenye uchumi wa nchi yetu, TADB kama benki kiongozi ya maendeleo ya kilimo, pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi nyingine za kifedha kutoa fedha kwenye mnyororo mzima wa kilimo, imejipanga kusaidia upatikanaji wa fedha zenye masharti nafuu na endelevu, ili kuinua ushiriki wa wakulima wadogo katika mfumo wa kifedha,” alisema.

  Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Majanga na Vihatarishi, Bw. Adam Kamanda kwa kutambua umuhimu wa kuendeleza sekta ya kilimo TADB imejipanga uwa benki ya mfano na ya kisasa katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania kutoka kilimo cha kujikimu kwenda katika kilimo cha kibiashara na uzalishaji wenye tija katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini.

  Bw. Kamanda ameongeza kuwa TADB imejipanga kupunguza changamoto za ukopeshaji zinazoikabili sekta ya kilimo nchini.
   Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Augustino Chacha akizungumza wakati akifungua mafunzo ya awamu ya pili yanayohusiana na Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo. Mafunzo hayo ya awamu ya pili yatafanyika kwa siku sita yanaendeshwa kwa pamoja kati ya TADB, NABAD na MIVARF.
  Mkuu wa Idara ya Majanga na Vihatarishi, Bw. Adam Kamanda (kulia) akizungumza nafasi ya TADB katika kuwezesha Mabenki na Taasisi za Fedha nchini kuweza kukopesha wakulima.
  Meneja Msaidizi wa Mafunzo kutoka NABAD, Dkt. R.S. Reddy akifundisha namna ya kufanyia uchambuzi miradi ya kilimo ili kuongeza tija kwenye utoaji wa mikopo kwenye sekta hiyo.
  Meneja Msaidizi wa Mafunzo kutoka NABAD, Bw. M.R. Gopal akifafanua jambo kuhusu nafasi ya NABAD katika mapinduzi ya kilimo ya India.
  Washiriki wa Mafunzo ya Awamu ya Pili ya Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa mafunzo hayo. Mafunzo hayo yanafanyika katika Hoteli ya Beach Comber, jijini Dar es Salaam.
  Washiriki wa Mafunzo ya Awamu ya Pili ya Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo wakiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi na viongozi kutoka TADB.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akiwa na Naibu Katibu wa Wizara hiyo Bi.Nuru Millao na Viongozi Waandamizi wa Wizara wakifuatilia mijadala mbalimbali katika kikao cha hamsini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 19, 2017.
  Wabunge kutoka Bunge la Msumbiji ambao ni wajumbe wa kamati ya Serikali za Mitaa kwa ambao wamekuja kwa ziara ya mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja katika viwanja vya Bunge leo Mjini Dodoma Juni 19, 2017.
  Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Azzan Zungu akiongoza kikao cha hamsini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 19, 2017.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) Mhe.Luhaga Mpina akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 19, 2017.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Hamad Masauni akifafanua jambo katika kikao cha hamsini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 19, 2017.
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Isack Kamwelwe akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 19, 2017.
  Naibu Waziri wa Kilimo ,Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao katika kikao cha hamsini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 19, 2017.
  Naibu Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.Eng Stella Manyanya akiteta jambo na Mbunge wa Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega katika kikao cha hamsini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 19, 2017.
  Maafisa habari wa chama cha Public Relations Society of Tanzania (PRST) kutoka Jijini Mwanza wakifuatilia kwa makini shughuli za Bunge katika kikao cha hamsini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 19, 2017.

  0 0
 • 06/19/17--06:10: Kigogo TRA ajitosa urais TFF
 • MBIO za kuwania uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zimezidi kushika kasi baada ya Ofisa wa juu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shija Richard kujitosa kuwania urais wa shirikisho hilo.

  Shija ambaye ni Meneja ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, amechukua fomu hiyo leo Jumatatu katika ofisi za TFF Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, ingawa hakuzungumza lolote kwa maelezo kuwa muda wa kampeni bado. 

  “Ni kweli nimechukua fomu kuwania urais wa TFF, wengi mtataka kujua mengi kuhusu mimi na kwa nini nimejitosa katika nafasi hii, tuvute subira wakati wa kampeni ukifika nitazungumza, ila kwa leo itoshe kuuthibitishia umma kwamba nimechukua fomu ya urais,” alisema Shija. 

  Mgombea huyo ana Shahada ya Uzamili katika masuala ya Sheria za Kodi na Utawala kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pia ana Stashahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Fedha kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dar es Salaam na Stashahada ya Juu ya Uhasibu kutoka Chuo Kikuu cha Uhasibu Arusha (IAA). 

  Pia Shija amehudhuria mafunzo mbalimbali ya uandishi wa habari na ameandikia magazeti mbalimbali hapa nchini kuanzia mwaka 1997.

  Mgombea huyo aliwahi kuitumikia Taasisi ya Kuzuia na Kupambaana na Rushwa (TAKUKURU) kabla ya kujiunga na Mamlaka ya Mapato Tanzania. Kwa sasa ni Mhazini Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), akiwa pia amepata kuongoza klabu mbalimbali za mpira wa miguu kwa ngazi tofauti. 

  Mwaka 2008 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Chama cha Soka wilayani Chato (CDFA), ambapo alisimamia usajili wa chama hicho kuelekea kwenye uchaguzi ambao hata hivyo hakugombea. Pia Shija amepata kuwa Katibu Mkuu wa Klabu ya Michezo ya Bukoba Veteran iliyopo mkoani Kagera.

  0 0


  0 0

  Frank Mvungi-Maelezo 

  Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imezindua mkataba wa huduma kwa wateja ikiwa ni nyenzo mojawapo inayowezesha kutolewa kwa huduma bora katika kiwango cha kimataifa na kutekelezwa kwa vitendo juhudi za Serikali katika kuwahudumia wananchi kwa weledi na uwajibikaji. 

  Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Doroth Gwajima wakati akizindua mkataba wa huduma kwa wateja wa Mamlaka hiyo leo Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu. 

  Akizungumza kuhusu mkataba huo Dkt. Gwajima amesema kuwa ni jambo la faraja kuona kwamba uzinduzi wa mkataba huu unafanyika katika kipindi cha maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma mwaka 2017 ambayo msingi wake ni kutoa huduma bora zinazoridhisha wateja kwa kuzingatia mkataba shirikishi wa huduma kwa wateja. 

  “Nawapongeza TFDA kwani kwa kutekeleza mkataba huu,watumishi wataweza kuepuka uzembe,upendeleo, na rushwa mambo ambayo husababisha malalamiko kwa wananchi dhidi ya watumishi na Serikali yao” Alisisitiza Gwajima. 

  Akifafanua amesema mkataba huo utawezesha wateja kutambua haki zao, wajibu wao hali itakayosaidia TFDA kuweka mfumo dhabiti wa upimaji wa viwango vya huduma (service standards) kwa mujibu wa mkataba ili kubaini ufanisi wa mkataba huu na kuchukua hatua stahiki za uboreshaji wa huduma pale inapobidi. 

  Aidha, alipongeza TFDA kwa kuweka namba ya simu ambayo mteja anapiga bure wakati wa kazi, kuhusiana na huduma zinazotolewa na TFDA ambayo ni 0800110084 na kuitumia inavyostaili. 

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Hiiti Sillo amesema utaratibu wa kuwa na mkataba wa huduma kwa wateja umesaidia kuongeza tija ambapo kwa sasa huduma za usajili wa maneno ya biashara za bidhaa zinazodhibitiwa na TFDA awali zilitolewa ndani ya siku 45 mwaka 2006 na kufikia 2016 zinatolewa ndani ya siku 10 tu. 

  Utoaji wa vibali vya kuingiza na kusafirisha bidhaa nchini na nje ya nchi (Bidhaa zilizosajiliwa) mwaka 2006 zilitolewa ndani ya siku 5 na sasa ni siku  moja tu, wakati usajili wa dawa zinazozalishwa nchini awali ulikuwa unafanyika ndani ya siku 360 na sasa ni siku 120 tu. 

  Mkataba wa huduma kwa wateja uliozinduliwa unaonesha ahadi za TFDA katika kuhudumia wateja wake na pia wajibu wa wateja katika kuwezesha Mamlaka kuwahudumia kwa ufanisi bila kuathiri ubora,Usalama na ufanisi wa chakula,dawa,vipodozi,vifaa,tiba na vitendanishi. 

  Kwa mara ya kwanza,TFDA ilitayarisha mkataba wa huduma kwa wateja kwa kushirikiana na wadau wake mwaka 2006 na baadaye kurejewa mwaka 2012,marejeo ya mara kwa mara yanatokana na msukumo wa mabadiliko ya kijamii,maboresho ya mifumo ya utendaji,kuongezeka kwa rasilimali watu na ukuaji wa sayansi na teknolojia katika utoaji huduma. 
   Kaimu Mkurugenzi wa Tiba toka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Dkt. Doroth Gwajima akisisitiza umuhimu wa Mamlaka ya Chakula na dawa (TFDA) kuendelea kusimamia utoaji wa huduma zake katika viwango vya Kimataifa wakati akizindua mkataba wa huduma kwa wateja wa Mamlaka hiyo leo Jijini  Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA ) Bw. Hiiti Sillo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkataba wa huduma kwa wateja uliofanyika Leo Jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Mkurugenzi wa Tiba toka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Dkt. Doroth Gwajima (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi mkataba wa huduma kwa wateja wa Mamlaka hiyo leo Jijini  Dar es Salaam  kwa niaba ya Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
   Kaimu Mkurugenzi wa Tiba toka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Dkt. Doroth Gwajima (katikati) akionesha mkataba wa huduma kwa wateja wa TFDA mara baada ya kuuzindua leo Jijini Dar es Salaam.kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA ) Bw. Hiiti Sillo na kushoto Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Usahuri wa kazi toka Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Bw. Mick Kiliba. 
   . Kaimu Mkurugenzi wa Tiba toka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Dkt. Doroth Gwajima akikata utepe kuzindua namba maalum itakayotumiwa na wananchi kuwasilina na Mamlaka hiyo ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa mkataba wa huduma kwa wateja.
   Kaimu Mkurugenzi wa Tiba toka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Dkt. Doroth Gwajima (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa TFDA mara baada ya kuzindua mkataba wa huduma kwa wateja wa Mamlaka hiyo. 
  Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Usahuri wa kazi toka Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Bw. Mick Kiliba akipongeza TFDA kwa kuwa moja ya Taasi za Serikali inayotoa huduma zake kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu wakati wa uzinduzi wa mkataba wa huduma kwa wateja.

  (Picha zote na Frank Mvungi –Maelezo).


  0 0


  Kulia ni daktari feki ambaye amekuwa akijitambulisha kwamba ni Dk bdallah Juma ambaye amekuwa akifanya kazi katika Maabara Kuu, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kulia ni mmoja wa askari wa Muhimbili aliyemkamata daktari huyo.

  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imemtia mbaroni kijana mmoja aliyekuwa akijifanya daktari na alikuwa akijitambulisha kwa wagonjwa kwamba anaitwa Dk Abdallah Juma.

  Mtu huyo alikuwa akijifanya kutoa huduma katika Maabara Kuu. Uongozi wa hospitali hiyo umesema kuwa kijana huyo ni daktari feki na si daktari kama alivyokuwa akijitambulisha na kwamba amekamatwa baada ya kuwekewa mtego na askari wa hospitali hiyo.

  Uongozi wa hospitali hiyo umesema kuwa walinzi walikuwa wakimtilia shaka na kuanza kumfuatilia hadi walipofanikiwa kumkamata.

  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha amesema hospitali imeweka mikakati mbalimbali ya kupambana na wahalifu wakiwamo watu wanaojiita ni madaktari kama huyo ambaye amekamatwa leo.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango na Bajeti wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Amani Mashaka(katikati), akitoa maelekezo kwa watumishi ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakati wa kikao cha Mpango Kazi na Mpango wa Ununuzi wa bajeti ya wizara hiyo.Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Bwalo la Jeshi la Magereza,Ukonga,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Mtumishi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Fatuma Mohamed (aliyevaa miwani), akiomba ufafanuzi kutoka kwaKaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango na Bajeti wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Amani Mashaka(aliyesimama kulia) wakati wa Kikao cha Mpango Kazi na Mpango wa Ununuzi wa bajeti ya wizara.Kikao kimefanyika leo katika Ukumbi wa Bwalo la Jeshi la Magereza,Ukonga,jijini Dar es Salaam.
  Mratibu Mwandamizi wa Uhamiaji,Colla Kayumba, akizungumza na watumishi wengine wa idara hiyo,Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji,Said Kassim(katikati) na Mkaguzi Msaidizi Sanga Hussein, wakati wa Kikao cha Mpango Kazi na Mpango wa Ununuzi wa bajeti ya wizara.Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Jeshi la Magereza,Ukonga,jijini Dar es Salaam

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Kamusi Kuu ya Kiswahili baada ya kuizindua kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Juni 19, 2017. Kulia ni Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu. Kushoto ni Balozi wa Kiswahili Afrika, Mama Salma Kikwete. Wapili kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua Kamusi Kuu ya Kiswahili kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Juni 19, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Kamusi Kuu ya Kiswahili kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Juni 19, 2017 (kushoto) ni Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu nakala ya Kamusi Kuu ya Kiswahili baada ya kuzindua kamusi hiyo kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, Juni 19, 2017. 

  0 0


  Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

  Mkurugenzi wa kampuni ya VIP Engendering na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL James Rugemalira na Habinder Seth Sigh, Mwenyekiti mtendaji wa PAP wamefikishwa mahakamani kujibu mashtaka sita.

  Watuhumiwa hao wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma uhujumu uchumi na kula njama, kughushi, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuisababisha hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

  Washtakiwa hao wote wamesomewa mashtaka yao na mwendesha mashtaka, wakili wa serikali, Paul Kadushi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi. Hata hivyo, wamerudishwa rumande hadi Julai 3 mwaka huu kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza wala kutoa dhamana kwa kesi ya uhujumu uchumi.

  Wanadaiwa kuwa kati ya Oktoba 18 ,2011 na Machi 19 , 2014 jiji Dar es Salaam walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

  Imedaiwa kuwa, katika shtaka la kujihusisha na mtandao, washtakiwa hao kati ya Oktoba 18,2011na Machi 19,2014 jijini Dar es Salaam wakiwa siyo watumishi wa umma na wakisaidiana na watumishi wa umma walitekeleza mtandao huo wa uhalifu kwa lengo la kujipatia faida.

  Katika shtaka la nne mtuhumiwa Sethi anadaiwa kuwa Oktoba 10,2011 katika mtaa wa Ohio Ilala DSm akiwa na nia ya ulaghai alighushi fomu namba 14 a ya usajili wa makampuni na kuonesha yeye ni Mtanzania anayeishi Kitalu namba 887 Mtaa wa Mrikau Masaki wakati akijua si kweli.

  Seth anadaiwa kutoa nyaraka hiyo ya usajili wa kampuni kwa ofisa msajiri wa kampuni,Seka Kasera kwa njia ya kuonesha kwamba yeye ni Mtanzania na Mkazi wa Mtaa wa Mrikau.

  Aidha katika shtaka jingine, Washtakiwa wote, wanadaiwa kuwa kati ya Novemba 28/29, 2011 na Januari23,2014 makao makuu ya benki ya Stanbic kinondoni na Benki ya Mkombozi tawi St Joseph kwa ulaghai, walijipatia kutoka Benji Kuu ya Tanzania (BOT), USD 22,198,544.60 na shilingi 309, 461,300,158.27. 

  Iliendelea kudaiwa kuwa katika shtaka la kusababisha hasara, washtakiwa hao wanadaiwa, Novemba 29, 2013 katika Benki ya Stanbic tawi la kati Kinondoni kwa vitendo vyao waliisababishia Serikali hasara ya USD 22, 198, 544.60 na Tsh 309,461,300,158.27.

  Baada ya kumaliza kusomewa mashtaka yao, wakili wa utetezi Respicius Didas kwa niaba ya mawakili wenzao aliomba mahakama iwapatie wateja wao dhamana kwa sababu Mashtaka yanayowakabili yanadhaminika.

  Hqta hivyo, upande wa mashtaka ulipinga vikali hoka hizo na kuiomba mahakama kuyatupilia mbali maombi ya utetezi ya kuwapatia dhamana washtakiwa hao.

  Akiwasilisha hoja zake, Kadushi amesema mahakama ya Kisutu haina mamlaka si tu ya kutoa dhamana bali hata kusikiliza maombi ya dhamana.

  Amesema mahakama pekee yenye mamlaka ya kufanya hivyo ni Mahakama Kuu na ndiyo maana washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote wakati wakisomewa mashtaka yao.

  Ameongeza mazingira pekee ambayo yangeifanya mahakama ya kisutu iweze kusikiliza maombi hayo na keai kwa ujumla ni pale ambapo Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) angetoa cheti maalum cha kuipa mamlaka mahakama ya Kisutu kuisikiliza kesi hiyo.

  " Maombi ya dhamana yameletwa katika mahakama isiyoweza kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria" amesema Kadushi.

  Naye Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alisisitza na kuomba mahakama kutupilia mbali hoja zote za maombi ya dhamana zilizotolewa na upande wa uetezi na ijielekeze kwa Jinsi inavyoona inafaa washtakiwa waende mahabusu wakati wakisubiri taratibu za kesi zinazoendelea. 

  Akijibu hoja hizo, Hakimu Shaidi amesema sheria inaelekeza kwamba kesi za uhujumu uchumi zinazozidi milioni 10 Mahakama hii haina mamlaka ya kuisikiliza wala kutoa dhamana isipkuwa kwa Cheti maalum kutoka kwa DPP kinachoiwezesha mahakama kufanya hivyo.

  Kesi hiyo itatajwa Julai 3,2017, watuhumiwa wameenda gereza la Segerea.


  Mmiliki wa VIP Engineering and Marketing, James 
  Rugemarila na Mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Habinder Seth Sigh wakiwa Ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam tayari kwa kusomea Mashitaka yao ikiwemo la Uhujumu Uchumi.
  Mmiliki wa VIP Engineering and Marketing, James Rugemarila na Mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Habinder Seth Sigh wakipandishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam
  Mmiliki wa VIP Engineering and Marketing, James 
  Rugemarila na Mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Habinder Seth Sigh wakipandishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam wakitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kukosa dhamana na kutakiwa kupelekwa mahabusu.

  Mmiliki wa VIP Engineering and Marketing, James 
  Rugemarila na Mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Habinder Seth Sigh wakipakiwa kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa Rumande mara baada ya kukosa Dhamana kutokana na Makosa yanayo wakabili
  Mmiliki wa VIP Engineering and Marketing, James 
  Rugemarila na Mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Habinder Seth Sigh wakipakiwa kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa Rumande mara baada ya kukosa Dhamana kutokana na Makosa yanayo wakabili
  Mmiliki wa VIP Engineering and Marketing, James 
  Rugemarila na Mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Habinder Seth Sigh wakipakiwa kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa Rumande mara baada ya kukosa Dhamana kutokana na Makosa yanayo wakabili

  0 0


  Meneja wa tigo mkoa Tabora Brighton akitoa neno la kuwakaribisha wageni kwa niaba ya Meneja wa tigo mkoa Kigoma wakati wa hafla ya futari ya pamoja baina ya watoto wanaoishi kwenye kituo hicho na uongozi wa tigo ambayo ilienda sambamba na kukabidhi misaada ya vyakula mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 1.2

  Mkuu wa wilaya Kigoma Samson Anga (aliyesimama) akizungumza katika hafla ya kutoa misaada na futari ya pamoja kwa watoto yatima na wanaoishi mazingira magumu cha MWOCACHI cha mjini Kigoma iliyoandaliwa na kampuni ya simu ya mkononi ya tigo

  Mkuu wa wilaya Kigoma Samson Anga ( wa pili kulia) na Mkurugenzi wa kanda ya ziwa wa kampuni ya simu ya mkononi ya tigo Gwamaka Mwakilembe (kulia) wakikabidhi kwa uongozi wa kituo cha kulea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha MWOCACHI misaada mbalimbali vya vyakula kwa ajili ya kituo hicho misaada ambayo ilienda sambamba na futari ya pamoja baina ya viongozi wa tigo,wadau mbalimbali na watoto hao iliyoongozwa na Mkuu wa wilaya Kigoma.
  Wageni waalikwa na watoto wanaoishi kwenye kituo cha watoto yatima na mazingira magumu cha MWOCACHI cha mjini Kigoma wakishiriki kwenye futari ya pamoja iliyoandaliwa na kampuni ya simu ya mkononi ya tigo kwa watoto hao.
  Mkurugenzi wa kanda kanda ya ziwa wa kampuni ya simu ya mkononi ya tigo Gwamaka Mwakilembe (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa tigo Kigoma,viongozi wa kituo cha kulea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha MWOCACHI na baadhi ya watoto wa kituo hicho baada ya kukabidhi misaada mbalimbali ya vyakula.

  0 0


  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akimsalimia Meneja Mradi wa kushawishi Siasa Shirikishi katika kuimarisha vyama vya Siasa hapa nchini, hasa katika ushiriki wa Wanawake na Vijana katika masuala ya Siasa, unaoendeshwa na Kituo cha Demokrasia ya Vyama Vingi cha Uholanzi (NIMD) kwa kushirikiana na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Arjan Van Der Waal, wakati alipokutana na ujumbe wa Meneja huyo na Mwakilishi wa NIMD Kanda ya Afrika Dk. Augustine Magolowondo (kulia), katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM,Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Watatu kulia ni Mwenyeji wa ugeni huo, Daniel Loyc kutoka TCD.
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akimsalimia Mwakilishi wa Kituo cha Demokrasia ya Vyama Vingi cha Uholanzi (NIMD) Kanda ya Afrika Dk. Augustine Magolowondo kutoka Malawi, alipopokea na kufanya mazungumzo na ugeni huo kutoka NIMD, leo
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akiwakaribisha kuketi kwa ajili ya kuendelea na mazungumzo.
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akizungumza na ujumbea kutoka Kituo cha Demokrasia ya Vyama Vingi cha Uholanzi (NIMD) katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Katika Mazungumzo hayo, Polepole aliitaka NIMD kuja kufanya kazi nchini kwa lengo la kuinua hadhi ya siasa nchini badala ya kubomoa. "Hatutarajii NIMD ije kufanya mambo hasi, mradi usilenge kuondoa madarakani Chama tawala, bali uwe chachu katika kuhamasisha uungaji mkono mambo mazuri yanayofanywa na Rais Dk. John Magufuli kama haya ya kulinda rasilimali za nchi", alisema Polepole. MAELEZO/PICHA NA BASHIR NKOROMO

  0 0  0 0


  0 0


  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Mtwara (MTUWASA) ifanye bidii na kuhakikisha Mtwara inapata maji kwa asilimia 100, ikizingatiwa ni mji ulio na viwanda vikubwa, ili kuunga mkono Sera ya Viwanda inayotekelezwa na Serikali.

  Prof. Mkumbo alisema hayo katika ziara yake ya kikazi aliyoifanya mkoani Mtwara, alipokuwa akitembelea mamlaka hiyo kwa nia ya kujua utendaji kazi wake na mipango ya utekelezaji wa miradi yake.

  “MTUWASA imeshika nafasi ya 8 kati ya mamlaka 25 nchini mwaka huu kulingana na ripoti ya EWURA, ni moja ya mamlaka zinazofanya vizuri. Hivyo, hamna budi kutoka asilimia 60 ya huduma mnayotoa sasa na kufikisha asilimia 100, ili kuendana na mahitaji ya wananchi pamoja na viwanda vikubwa vilivyopo mjini hapa”, alisema Katibu Mkuu.

  Prof. Mkumbo alisisitiza kuwa ili kuendana na Sera ya Viwanda huduma ya maji haina budi kuwa ya uhakika na endelevu, na MTUWASA inabidi wahakikishe Serikali inafanikiwa kufikia lengo hilo kama watoa huduma wa maji.

  Aidha, aliwaasa wananchi wa Mtwara kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji, kwani pamoja na juhudi za Serikali za kuwekeza katika miradi mikubwa ya maji, itakuwa ngumu kufanikisha lengo la kutoa huduma ya uhakika na endelevu ya majisafi na salama kama vyanzo vya maji havitatunzwa na kuwa endelevu.

  Naye Mkuregenzi Mtendaji wa Mamlaka ya ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Mtwara (MTUWASA), Inj. Mashaka Sitta alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha mamlaka hiyo inakuwa bora nchini ndani ya miaka miwili; baadhi ya mipango yao ikiwa ni kutunza vyanzo vya maji, kuongeza mitandao ya miundombinu ya maji, kuongeza uzalishaji na wateja ili kufikia lengo hilo.

  Katika ziara hiyo Katibu Mkuu alitembelea pia Ofisi za Bonde la Mto Ruvuma na Pwani ya Kusini na kukutana na baadhi ya watendaji wake na kuzungumza nao kuhusu usimamizi na maendeleo ya rasilimali za maji katika bonde hilo na kukamilisha ziara yake ya siku mbili katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akipokea maelezo kutoka kwa Mkuregenzi Mtendaji wa Mamlaka ya ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Mtwara (MTUWASA), Inj. Mashaka Sitta alipotembelea chanzo cha maji cha Mtawanya, mkoani Mtwara pamoja na Inj. Najib Asumbwile kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akiwa kwenye Mtambo wa Maji wa Kusafishia Maji, mkoani Mtwara.
   Sehemu ya Mtambo wa Kusafishia Maji, mkoani Mtwara.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akikagua sehemu ya majengo mapya ya Ofisi za Bonde la Mto Ruvuma na Pwani ya Kusini ambayo ujenzi wake unaendelea, akiwa na Afisa Bonde, Msiru Msengi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akizungumza kwenye ofisi ya Katibu Tawala Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji mkoa wa Mtwara.


  0 0  0 0  0 0

  Serikali imesema ni marufuku kwa shule ambayo itakuwa haina viwanja vya michezo kupatiwa kibali cha kufungua shule ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Elimu namba 25 ya mwaka 1978.

  Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Masindano ya kwashule za msingi nchini UMITASHUMTA mkoani Mwanza, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMO) Mh. George Simbachawene, amemuagiza Kamishna wa Elimu nchini, kutozipatia vibali shule zinazo hitaji kufunguliwa endapo zitakuwa hazina viwanja vya michezo.

  Simbachawene, amesema kutokana na sheria ya Elimu namba 25 ya mwaka 1978, ambayo inataka kila shule inapofunguliwa lazima iwe na viwanja visivyo pungua vitano hivyo nilazima hili lizingatiwe, “nichukue nafasi hii kumuagiza kamishna wa Elimu kuanzia sasa asisajili shule yeyote ile ambayo itakuwa haina Viwanja vya michezo, kwani bila kufanya hivyo azma yetu yakuinua michezo nchini haiwezi kutimia” alisema.

  Mbali na kutoa maagizo hayo waziri Simbachawene, ameziagiza pia halmashauri na wilaya kote nchini kutenga sehemu ya mapato yao ya ndani kwaajili ya kitengo cha michezo, huku akizihimiza kuweka katika bajeti ijayo ya serikali fedha kwenye vifungu vinavyo husiana na michezo na kuonya kuwa endapo Halmashauri itashindwa kufanya hivyo basi yeye kama waziri mwenye dhamana hatakubali ipite. 

  Amesema Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015 sehemu ya (61) inatambua suala la Michezo lakini pia Sera ya Elimu ya Mwaka 1995, hivyo kama Serikali lazima waweke kipaumbele katika suala zima la michezo.

  Ameongeza kuwa, Msingi wa Michezo nchini ni michezo ya UMITASHUMTA NA UMISETA ndio Dira ya timu zetu za Taifa, “Tukiwaandaa vijana wetu vizuri na kutokana kaulimbiu hii ya masula ya viwanda, hatuna wasiwasi kuwa hawa ndio viwanda vyenyewe, mchezaji mmoja aliyefikia viwango vya kimataifa huweza kugharamia hata bajeti ya nchi” alisema Simbachawene.

  Katika hatua nyingine Simbachawene, amewaagiza makatibu Tawala kote nchini, kusimamia suala la taaluma na michezo, amesema hakuna taaluma bila Michezo na Hakuna michezo bila Taaluma kwa mantiki hiyo lazima nidhamu ya hali ya juu iongezwe miongoni mwa vijana na wanamichezo kwa ujumla. 
    
  Naye Mkurugenzi wa Michezo nchini kutoka Wizara ya Habari, Michezo Sanaa na Wasanii Dkt. Yusuph Singo amesema Tayari Wadau Mbali mbali wa Michezo wakiongozwa na Chama cha Mpira wa Miguu na Riadha wapo Mkoani Mwanza kwaajili ya Kuangalia Vipaji kwa ajili ya Timu mbali mbali za Taifa lakini pia vilabu vyao.

  Aidha amesema kuwa wizara ipo katika Mazungumzo na Timu Manchester City kupitia wakala wao wa TECHNO kwaajili yakuchukuwa Vijana wapatao kumi kutoka Tanzania kwaajili yakuwaendeleza kimichezo.

  Awali akimkaribisha Mgeni rasmi, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, aliishukuru serikali kwakuichagua Mwanza kuwa mwenyeji wa mashindano hayo huku akiomba kwa mwaka ujao mashindano hayo kufanyika tena mkoani humo, kutokana na madhari mazuri lakini pia ubora wa viwanja na hali ya ulinzi na usalama inayotamalaki katika mkoa huo, “Mh. Waziri mimi niombe tu, haya mashindando katika mwaka ujao myalete tena Mwanza sisi tupo tayari, huo ndio mtazamo wangu lakini pia wenzangu wataniunga mkono” alisema Mongella.

  Mashindano ya shule za msingi (UMITASHUMTA) ya 2017 ni mashindano ya 22 ambapo yanashirikisha wanamichezo wapatao 2522 kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara.
  Baadhi ya Viongozi wa Serikali wakiongozwa na Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI George Simbachawene, wakionekana wenye furaha wakati wa Uzinduzi wa UMITASHUMTA 2017.

  Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI George Simbachawene, akisalimiana na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Projestus Rubanzibwa alipofika kufungua rasmi Mashindano hayo.
  Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI George Simbachawene akipeana mkono na Katibu Mkuu Baraza la Michezo la Taifa Mohamed Kiganja  wakati wa Uzinduzi wa UMITASHUMTA 2017.
  RUBANZIBWA-- Mh. George Simbachawene, akisalimiana na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Projestus Rubanzibwa alipofika kufungua rasmi Mashindano hayo.

  0 0

   Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Ibrahim Mahumi akitoa ufafanuzi kuhusu taratibu zinazohusu  menejimenti ya  Rasilimaliwatu serikalini kwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe katika Ofisi za  Halmashauri hiyo  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe Bi. Amina Kiwanuka.
   Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakizungumza masuala ya kiutumishi na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2017.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe, Bi. Amina Kiwanuka akieleza utekelezaji wa masuala ya kiutumishi katika eneo lake la   kwa Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma waliomtembelea ofisini kwake leo alasiri kuhimiza uwajibikaji ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017.
   Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe Bw. Abdullfariq Mkata (wa pili kulia) akitoa taarifa  ya kiutendaji ya Idara yake kwa Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma walipoitembelea Halmashauri hiyo leo kuhimiza uwajibikaji ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017.
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wa Ofisi ya Rais,Menenimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Issa Ng’imba akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya kiutumishi  kwa Mkurugenzi  wa  Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe Bi. Amina Kiwanuka ofisini kwa mkurugenzi huyo leo  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi. Amina Kiwanuka akisikiliza kwa makini.


older | 1 | .... | 1276 | 1277 | (Page 1278) | 1279 | 1280 | .... | 1898 | newer