Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

TIGO YAFUTURISISHA WATOTO YATIMA MIKOA YA MWANZA NA MBEYA

$
0
0
Mwanafunzi wa darasa la nne wa  Islamic Yatima Foundation Fadhira  Hamidu, akipokea msaada wa chakula kwa niaba ya wengine,  kutoka kwa Meneja Mauzo Mkoa wa Mwanza  wa Kampuni ya Tigo Kassim Aziz Kassim, wakati wa hafla ya makabidhiano eneo la Ilemela jijini Mwanza juzi.Msaada wa Sh 3.5 Milion ulipokelewa
 Mwanafunzi wa darasa la saba wa  Islamic Yatima Foundation Zahor Hamoud, akipokea msaada wa chakula kwa niaba ya wengine, kutoka kwa Meneja Mauzo Mkoa wa Mwanza  wa Kampuni ya Tigo Kassim Aziz Kassim, wakati wa hafla ya makabidhiano eneo la Ilemela jijini Mwanza juzi.Msaada wa Sh 3.5 Milion ulipokelewa
Wanafunzi wa Islamic Yatima Foundation, wakipata futari iliyoandaliwa na Kampuni ya Tigo eneo la Ilemela jijini Mwanza juzi.
Wanafunzi wa Islamic Yatima Foundation, wakipata futari iliyoandaliwa na Kampuni ya Tigo eneo la Ilemela jijini Mwanza juzi.
Meneja wa  Kampuni ya Tigo Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Ladislaus  Karlo (kushoto) akimkabidhi sehemu ya zawadi kutoka kampuni hiyo kwa Mhasibu wa Kituo cha Kulelea watoto yatima Cha Nuru, kilicho Uyole Jijini Mbeya,Semu Mwansasu, (kulia) kabla ya wafanyakazi wa Tigo Mbeya kushiriki pamoja na watoto hao kwenye futari iliyoandaliwa na Tigo ofisi ya Mbeya.
Meneja wa  Kampuni ya Tigo Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Ladislaus  Karlo  akikabidhi sehemu ya zawadi kutoka kampuni hiyo kwa Kituo cha Kulelea watoto yatima Cha Nuru, kilicho Uyole Jijini Mbeya,Semu Mwansasu, (kulia) kabla ya wafanyakazi wa Tigo Mbeya kushiriki pamoja na watoto hao kwenye futari iliyoandaliwa na Tigo ofisi ya Mbeya.

IFAHAMU BAADHI YA SEHEMU ZA KITALII JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Na Jumia Travel Tanzania

Umaarufu wa Dar es Salaam kwenye shughuli za kibiashara umelifanya jiji hili kuwa vigumu kwa watu kuvizingatia vivutio vyake vya kitalii. Watu wengi huvifahamu kwa kuviona tu lakini bila ya kujua kihistoria sehemu hizo zina maana sana na wageni huja wakitokea nchi mbalimbali kujifunza.
 
Ukiachana na ufukwe wa Coco Beach unaopatikana pembezeni mwa bahari ya hindi eneo la Oyster Bay, Jumia Travel ingependa kukufahamisha kwamba unaweza kujifunza na kufurahia mambo mengi pindi utakapotembelea maeneo yafuatayo.

Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni. Makumbusho haya awali yalifunguliwa mwaka 1940 kama kumbukumbu ya Mfalme George wa tano ambapo kihistoria huwarudisha watanzania nyuma walipotokea. Makumbusho haya huonyesha mabaki muhimu ya binadamu wa kale yaliyogunduliwa na Dkt. Leakey aliyoyachimbua kwenye bonde la Olduvai. Wageni wanaweza kujifunza urithi wa kitamaduni kutoka kwa makabila mbalimbali Tanzania pamoja na athari za biashara ya utumwa kipindi cha utawala wa kikoloni. Baadhi ya vitu vingine vinavyopatikana katika makumbusho haya yaliyopo mtaa wa Shaaban Roberts ni zana za jadi, desturi, mapambo na vyombo vya muziki.  
 
Kijiji cha Makumbusho. Takribani maili 6 kutokea katikati ya jiji, kuna kiji cha makumbusho ambacho kimehifadhi tamaduni za makabila zaidi ya 120 yanayopatikana Tanzania. Wageni wanaweza kuzunguka kwenye vibanda kadhaa vya nyasi vinavyopatikana pale kwenye ukbwa wa takribani hekari 15 na kujionea ufundi wa kijadi katika kuchora, ufumaji na uchongaji. Kijiji hiki kinachopatikana eneo la Kijitonyama, barabara ya Bagamoyo pia huwa na ngoma na michezo ya jadi pamoja shughuli nyingize za kitamaduni.

Sanamu la Askari. Likiwa limetengenezwa kwa shaba sanamu hili ya Askari huonyesha askari akiwa amevalia vazi rasmi lililotumika kipindi cha vita ya Kwanza ya Dunia huku ncha ya mbele ya bunduki (kama kisu) ikiwa imeelekezwa karibu na bandari iliyopo jirani. Sanamu hili huonyesha kama kumbukumbu ya majeshi ya waafrika walioshiriki kupigana kwenye vita ya Kwanza ya Dunia na linapatikana mtaa wa Azikiwe na Samora.
 
Boma la Kale. Likiwa limejengwa mnamo mwaka 1866 mpaka 1867 na Majid Bin Said, Sultani wa Zanzibar, Boma hili la kale ni jengo lenye umri zaidi ambalo linapatikana kwa sasa jijini Dar es Salaam. Jengo hili lilitumika kuwakarabisha wageni wa Sultani ambaye alikuwa na kasri lake pembeni yake. Vitu vya kuvutia kwenye jengo hili lililopo mtaa wa barabara ya Sokoine ni namna lilivyojengwa kwa ndani vikiwemo mlango wa mbao kutokea Zanzibar na kuta zilizojengwa kutokana na matumbawe.

Kanisa la Mtakatifu Joseph. Jengo hili la Kanisa la Kiroma lilijengwa na wamisionari wa Kijerumani mnamo mwaka 1897 mpaka 1902, kwa kiasi kikubwa ni kivutio kinachoweza kuonekana eneo la karibu na bandarini. Jengo hili kwa ndani limejengwa kwa ufundi na ubunifu wa hali ya juu na kutumia stadi halisi kabiza za kijerumani. Jengo hili ndio Makao Makuu ya kanisa hilo na liinapatikana katika barabara ya Sokoine.   

Kanisa la KKKT Azania Front. Wajerumani walilijenga kanisa la KKKT Azania Front mnamo mwaka 1898. Namna jengo hili lilivyojengwa hususani paa lake kunalifanya kuwa ni nembo ya kivutio jijini Dar es Salaam. Kuna kipindi kanisa hili ndilo lilikuwa kituo kikuu cha shughuli za kimisionari mnamo karne ya 19, kwa sasa ndio makao makuu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania.

Ikulu. Ikiwa imejengwa kwenye miaka ya 1890, jengo la Ikulu ndilo lilikuwa ni makazi ya mwanzo kabisa ya Gavana wa Ujerumani. Mnamo mwaka 1922, Waingereza walifanya maboresho ya jengo hilo maeneo mbalimbali kufuatia kuliharibu katika kipindi cha vita ya Kwanza ya Dunia. Ingawa raia wa kawaida hawawezi kuingia ndani lakini bado linabaki kuwa kivutio kikubwa mtu akipita karibu nalo. Jengo hili linapatikana mtaa wa Luthuli barabara ya kuelekea Kivukoni.   
 
Kisiwa cha Mbudya. Kisiwa hiki kinapatikana umbali wa dakika kumi kwa mwendo wa boti kutokea Kunduchi kikiwa ni hifadhi ya majinii jijini Dar es Salaam. Ukiwa kisiwani hapa utasahau kabisa pilikapilika za katikati mwa jiji hili kwa kufurahia fukwe safi, michezo ya kwenye maji na kuogelea. Kisiwani haoa kuna vibanda vya kukodisha karibu na ufukwe huku vyakula vya baharini pamoja vinywaji vikipatikana pia. Sehemu hii ni maarufu sana kwa watu wanaopenda kutalii kwa siku moja wakitokea katikati ya jiji.

Kisiwa cha Bongoyo. Takribani maili 4 Kaskazini mwa jiji la Dar es Salaam eneo la Msasani kinapatikana kisiwa cha Bongoyo. Kwa wale wanaopenda kusafiri kwa siku moja na kurudi hii sehemu pekee na ya kuvutia ambayo unaweza kufurahia mambo mengi. Kisiwa kina fukwe safi, michezo ya kwenye maji, pamoja na kujionea aina kadhaa za samaki wa baharini. Nyuma ya kisiwa hiki kuna mibuyu mikubwa ambayo huleta hewa safi kwenye fukwe za kisiwa hiko huku vyakula vya baharini na vinywaji hupatikana kwa ajili ya wanaotembelea. Bongoyo kwa sasa inawezekana kuwa ni miongoni mwa visiwa vinne vinavyotembelewa zaidi kwenye hifadhi za maji jijini Dar es Salaam.
Dar es Salaam ina mambo mengi ya kujifunza ingawa mengi yamezingwa na shughuli za kibiashara zilizotapakaa kila kona. Jumia Travel inaamini kuwa inawezekana unaishi na vivutio vya kitalii karibu nawe lakini ulikuwa haufahamu. Hivyo basi kabla ya kufikiria kwenda mbali kutalii vivutio vingine anza na vilivyomo jijini hapa kwani vipo karibu nawe na haikugharimu sana kuvitembelea.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AONGOZA HARAMBE YA UJENZI WA KANISA PAROKIA YA ZUZU, DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa niaba ya familia yake akimkabidhi Mchango wa Shilingi Milioni Kumi, Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Nyumba ya Paroko pamoja na kufanyia Ukarabati wa Kanisa Parokia ya ZUZU Dodoma. Kushoto ni Msaidizi wa Askofu Jimbo la Dodoma Baba Chesco Msaga . Harambe hiyo imefanyika June 17, 2017 katika Makazi ya Waziri Mkuu Mstaafu Pinda yaliyopo ZUZU nje kidogo ya Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu,  Mizengo Pinda akiwaonyesha Wageni waalikwa (hawapo pichani) Shilingi Milioni Kumi Mchango aliokabidhiwa na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa kwa niaba ya Familia yake , Kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Nyumba ya Paroko pamoja na kufanyia Ukarabati wa Kanisa Parokia ya Zinje (ZUZU) Dodoma. Kushoto ni Msaidizi wa Askofu Jimbo la Dodoma Baba Chesco Msaga . Harambe hiyo imefanyika June 17, 2017 katika Makazi ya Waziri Mkuu Mstaafu Pinda yaliyopo ZUZU Nnje kidogo ya mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (Kushoto) akiwa ameongozana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu Pinda walipo mpokea katika makazi yao yaliyopo Zuzu nje Kidogo ya Mjini Dodoma June 17, 2017, kuhudhuria Misa ya kumbukumbu ya Marehemu Mzee Exavery Pinda Baba Mzazi wa Mizengo Pinda, Pamoja na kuongoza Uchangiaji wa Ujenzi wa Nyumba ya Paroko na Ukarabati wa Kanisa la Parokia ya ZUZU. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

WARIOBA :TUTOE MAONI KUBORESHA SERA YA MADINI NA SHERIA ZAKE, ATAKA UONGOZI WA PAMOJA SUALA LA MAKINIKIA

$
0
0
Na Judith Mhina .

Wananchi hawahitaji mgawanyiko wa uongozi na malumbano wanataka maendeleo.Msaidieni Rais tushinde Vita ya Rasilimali za nchi
Suala la Makinikia sio la Chama wala Siasa ni la Watanzania wote

Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli alipokea ripoti ya Kamati ya kwanza na ya pili ya uchunguzi wa makontena 277 ya mchanga wa madini (makinikia) yaliyokuwa njiani kusafirishwa nje ya nchi na uchunguzi ulifanyika na kulibaini ndani ya mchanga huo kuna dhahabu na madini mengine kwa asilimia kubwa.

Aidha, Mhe Rais amechukua hatua mbalimbali kulingana na ushauri wa kamati husika, pamoja na maamuzi yake kama Rais. Kutokana na sakata la hilo, Idara ya Habari-MAELEZO imepata fursa ya kufanya mahojiano na Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu Mheshimiwa, Jaji Joseph Sinde Warioba katika ofisi zake zilizopo Osterbay Jijini Dar-es-salaam.

SWALI: Ninanukuu maneno ya Baba wa Tafa, Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere kuhusu raslimali za nchi na hususan madini alisema: “Madini yetu tuliyonayo ni vema kuyaacha mpaka Watanzania watakapokuwa na ufahamu wa kutosha wataamua kuyachimba” mwisho wa kunukuu nini maana yake?

JIBU: Mara baada ya Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 Hayati, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipokea nchi kama Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika huru akiwa hana wataalamu zaidi ya madaktari 2 na yeye mwenyewe ambaye alikuwa msomi kutoka chuo Kikuu cha Edinburg Uingereza. Kwa hali hiyo, Mwalimu alikuwa sahihi usingeweza kuruhusu rasilimali za nchi mfano madini kuchibwa na wageni kutoka nje maana yake Watanganyika wangekuwa watazamaji tu bila kufaidika na lolote.

Mwalimu alihakikisha anawekeza katika elimu ambayo ilikuwa bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu elimu ndio msingi wa kuondoa Ujinga Umasikini na Maradhi. Alitambua Watanganyika wakielimika na kupata utaalamu wa madini ikiwani pamoja na uchimbaji watakuja kuyachimba na kufaidika.

SWALI:Tanzania ni kati ya nchi zilizobarikiwa kuwa na raslimali nyingi za kila aina kuanzia madini, gesi, wanyamapori na hifadhi, misitu, milima, maporomoko ya maji, mabonde maziwa makubwa kwa madogo, bahari ya hindi na raslimali za mazao ya uvuvi, nchi yenye ardhi ya kutosha watanzania wenye uwezo wa kufanyakazi kwa ufanisi . Unadhani nini tatizo letu, nini cha kufanya?

JIBU Sioni kama kuna tatizo la msingi lakini, ni suala la uelewa mara nyingi kuna watu ambao huamini viongozi wao kwa kila kitu wanachosema. Lazima wananchi wawe makini kwa sababu tatizo la watanzania ni maendeleo kila mwananchi ana kiu ya kutaka tufikie mahala pazuri kama Taifa na mimi nakubaliana nao kabisa.

Tuna rasilimali nyingi, ambazo kimsingi tukiweza kuzishughulikia kwa makini kama lilivyoshughulikiwa suala la mchanga wa madini tutakuwa mbali sana kiuchumi.

Mosi, tuangalie rasilimali ya madini kwa mapana yake na kushughulikia wawekezaji wa ndani na wale wa nje, Barick na Acaccia ni sehemu ndogo sana ya madini, tuangalie wachimaji wa ndani mfano Tanzanite ni aibu madini yanachibwa Manyara biashara hii inatokaje Mererani na kufanyika Nairobi na New Delhi tujiulize kwa nini sio Arusha na Dar-Es-Salam.

Pili, upande wa rasilimali za maziwa makubwa tuliyonayo Victoria, Tanganyika na Nyasa, Bahari ya Hindi kuanzia Moa mpaka Tanga kwa kiasi gani tumeweza kutumia rasilimali za bahari maharamia wanakuja na meli zao wanavuna tu na kuwatajirisha watu wengine. Mfano ziwa Victoria linategemewa na wananchi wengi na sasa samaki hamna wamekwisha kwa sababu hatusimamii rasilimali zetu ipasavyo. Maana suala sio kuvuna tu tunalindaje hizi rasilimali zetu ili ziwepo leo kesho na vizazi vijavyo.

Tatu, Maliasili zetu za wanayamapori, mbuga za wanyama, vitalu vya utalii unampaje mfanyabiashara kibali cha kuwinda miaka 99 yaani atumie yeye, wanawe na wajukuu zake, watanzania watatumia lini, haya ni masuala ya msingi kabisa ya kuangalia upya.

Nne, Ardhi Mwalimu alisema ili tuendelee tunahitaji vitu vine Watu, Ardhi Siasa Safi na Uongozi Bora. Mwalimu Nyerere aliona ardhi ndio kilakitu hivyo vyote tulivyovitaja vipo ardhini pamoja na sisi wanadamu tunaitegemea kwa kila kitu. Maeneo mengi yaliyotumiwa na watu kwa shughuli za ufugaji aidha , yana matumizi mengine kama nyumba, kilimo cha mashamba makubwa, na idadi ya watu inaongezeka ardhi ni ileile hii imesababisha migogoro ya watumiaji wa asili wa maeneo hayo na wenye matumizi mengine tunatatuaje changamoto hii.

SWALI: Kwa kuwa umebobea katika masuala ya mikataba na sheria, ushauri gani unautoa katika masuala yote ya raslimali za Tanzania? Nani anatakiwa kusimamia raslimali hizi kwa ufanisi?

JIBU: Hii sio suala la mjua sheria au asiyejua, Mwanasheria lazima anazijua sheria ndio maana amepewa dhamana. Linalojitokeza ni ukosefu wa maadili ya uongozi, imani, utiii, uwazi na kutopenda nchi yako na Watanzania ambao wamekupa dhamana ya kusimamia jambo.

Ndio maana Mwalimu Nyerere aliweka miiko ya uongozi, maadili ya uongozi kwenye Azimio la Arusha. Kila mwananchi alikuwa anaweza kujua kiongozi huyu muadilifu au sio muadilifu na anachukuliwa hatua kabla mambo hayajaharibika.

Lakini sio vema kumhukumu mtu kwa jambo lolote lile, ni vema busara itumike kujua kilichotokea mfano hili suala la mchanga wa madini ya makinikia.

Jambo la msingi ni kutafuta suluhu itakayotupeleka mbele, tuone sera zetu zikoje na zinatusaidiaje kulinda rasilimali za Taifa, tunarekebisha vipi kuondoa tatizo, sheria na utendaji kwa ujumla. Naomba watanzania tutoe maoni na mawazo yatakayoboresha sera, sheria na utendaji au usimamizi wa rasilimali husika. Tunaweza kurudisha miiko na maadili ya uongozi katika kusimamia rasilimali za nchi, kila Mtanzania ajue sio mali yake ni ya Watanzania wote lazima aitunze vinginevyo atahukumiwa kwa hilo.

SWALI: Ni ukweli usiopingika kuwa kosa limeshafanyika kwa hili tuliloliona la mchanga wenye madini ya dhahabu, ambapo mhusika ambaye ni mmiliki wa Kampuni inayobeba mchanga huo tangu 1998 hadi 2017 amewasili nchini kuonana na viongozi wakuu wa serikali, nini maoni yako kuhusu hili?

JIBU Sisi hatukushughulika na uchimbaji wa madini, lakini utafiti tulifanya na kujua madini yapo na kuna maeneo mengi ambayo tumeweza kufanya vizuri tunapata mapato, lakini hatukupata mapato yote.

Lakini hili la mchanga sitaki kulizungumzia sana nadhani watu wanalichukulia kwa mihemko sioni faida kuzungumzia matukio badala ya kuona tafsiri nzima nini cha kufanya.

Ninachokiona na cha muhimu sana, Watanzania wamepata faida kwa mara ya kwanza tumeweza kujua mikataba ya madini ikipitiwa na Kamati zote mbili zimetueleza maeneo yote ya mikataba waliyopitia na kuja na mapendekezo. Tumetambua serikali ilikuwa na hisa au la mrahaba asilimia ngapi, kodi kiasi gani, na mambo kama hayo.

Naomba jambo hili lisibague, tunasema hatupati mapato ya kutosha ni lazima tujue kwa wachimbaji wa nje na wa ndani mfano nani anajua wachimbaji wadogo wadogo wamechimba madini kiasi gani tangu 1998 hadi 2017 na kodi kiasi gani imeimngia. Tumepata nafasi sasa ya kuangalia sera za kulinda rasilimali ya madini na nyingine zote katika nchi, kama maliasili ya bahari tunaitumiaje, gesi, makaa ya mawe, chuma, wanyama pori na mambo kama hayo.

Hii imetufungua macho sera ya aina gani sheria za aina gani, jinsi gani ya kutunza na kutumia rasilimali hizi tulizopewa na mungu.

SWALI: Kwa kuwa wananchi tulio wengi tunaenda kwa mihemko bila kupambanua hoja husika na kutoa mapendekezo au maoni yatakayo isaidia serikali kuboresha sera sheria na utendaji wa rasilimali zetu unadhani tatizo ni nini?

JIBU: Hatujaona uongozi wa Kitaifa katika hili suala la mchanga wa makinikia ninachokiona mimi ni uongozi wa chama na siasa nyingi, sio sahihi kabisa wanafanya makosa hili ni suala la rasilimali za nchi ni la kila Mtanzania.

Viongozi hawawatendei haki wananchi wanaowakilisha, wanakuwa na mihemko wanasema kamata, shitaki, wafunge. masuala ya kitaifa hayaendi hivyo sisi sio Polisi wala Mahakama waachieni wenye kazi yao.

Uongozi wa kulalamika hautusaidii, wananchi wanataka kuona rasilimali zetu zinanufaisha na kuboresha huduma za jamii ambazo wanalalamika kila leo hakuna dawa, elimu isiyowajenga vijana na mambo kama hayo.

SWALI: Mhe. Kutokana na sakata la mchanga wa dhahabu uliokuwa unasafirishwa nje ya nchi na matokeo yake watanzania tunajifunza nini kwa maoni yako?

JIBU: Kabla ya tuona funzo tulilopata nadhani ni vema nikazungumzia jambo hili, nimeona mjadala katika mitandao ya kijamii ambayo inafanywa kwa mihemko. Ukiangalia vyombo vya habari au viongozi tumejikita katika majina ya watu, nilikuwa nnaangalia Bunge wote wanakwenda kwa wale waliotajwa unakuta kuna wanaochangia na wanaolaumu ama unsahangilia au unalalamika kuhusu watu.

Kubwa ni utaratibu tulionao haitasaidia kulalamika juu ya watu waliofanya kazi huko nyuma, tunaweza kuwauliza wahusika nini kilitokea mpaka kufanya hivyo, lakini hilo sio kubwa, muhimu ni kutafuta ufumbuzi.

Mjadala huu umenikumbusha Awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere viongozi wote na wananchi walikuwa wanalalamika kila kitu wanachokikosa ni kwa sababu ya wakoloni. Mwalimu akasema namnukuu: “Ni kweli wakoloni wametuleta matatizo mengi sana lakini haitoshi kulaumu wakoloni bila kuondoa mateso ya wananchi”. Mwalimu akaja na Waraka ambao ulikuwa unaitwa “Act dont Argue” nadhani bado upo.

Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi nanukuu amesema. “Napenda kupata maoni tufanye nini kuhusu suala hili la mchanga wa dhahabu (makinikia).” Namuunga mkono, sasa tumepata nafasi ya kutoa maoni, mawazo ambayo ni muhimu sana maoni ya wadau katika uundaji wa sera na sheria

Sasa hivi siamini kama hatuna utaalamu, nina hakika tunao wa kutosha tatizo ni maadili na hilo lazima kutafuta ufumbuzi wake, pia tuunge mkono serikali inachofanya kupambana na rushwa na ufisadi.

“Lakini tusijidanganye bishara ya madini, mafuta ina changamoto kubwa sana duniani hususan Afrika, maana unapambana na watu wenye fedha biashara hii popote utakapo kwenda, ambapo uchumi unategemea mafuta na madini utaona jinsi wakubwa wanavyooneemeka na rasilimali hizo na kuwaaacha wananchi wakiwa masikini mfano mzuri Nigeria”.

Pamoja na kuangalia maadili na nidhamu lazima kuwe na uwazi katika mikataba ni muhimu sana.

SWALI: Una maoni na mapendekezo yako kwa viongozi wote na Mhe Rais katika kumuunga mkono?

Kwanza naliona hili la malumbano yatatugawa, waache tofauti zao hii lawama ya madini ingekuwa ni mwanzo kwa kuleta mawazo na maoni ya kutengeneza nchi yetu katika kulinda na kuzitumia rasilimali zote kwa maendeleo ya taifa letu.

Viongozi msaidieni Rais kulishughulikia kwa pamoja hili si jambo la chama wala Taasisi. Hakuna haja ya kupeana lawama ukishasema tumekosea unatakiwa ueleze tufanye nini, sio kusema serikali ichukue hatua kwani serikali ni nani si mimi na wewe sasa kwa nini hutaki wewe kulitolea maoni?

Tujiamini nimeona katika malumbano hayo, wengine wanaonekana kama hatujiami kama tukifanya hivi tunaweza kushitakiwa, mabadiliko yoyote yana machungu yake. Tusije tukapoteza imani tuliyonayo maana tunaweza tukapoteza mapato yetu lakini ni lazima tufanye kwa kujenga afya ya rasilimali zetu.

Rais amekutana na mmiliki wa Barick na kila upande una msimamo wake, tuiachie serikali na nina imani kabisa serikali itafanikiwa. Kinachonishangaza ni mazungumzo ya baadhi ya viongozi kuwa serikali ihakikishe tunapata hizo fedha walizo taja kwenye taarifa.

Nadhani hii sio sahihi, tuna imani na Viongozi wet wakuu haswa Rais, lolote litakaloafikiwa tulipokee na kulikubali tusije kuanza kulumbana ripoti imesema trilioni 108 ziko wapi? Pia nilisemee hili la dalili za kupoteza imani, eti tukifanya hivyo tutashitakiwa, sababu ya mikataba na wawekezaji hawatakuja mimi naamini watakuja tu rasilimali zipo kwetu hawana jinsi.

SWALI: Msaada wako binafsi kwa Rais au maoni yako kwa Rais

JIBU: Sisi tupo, Uongozi ni suala la kupeana vijiti mimi natoka Mara nimepitia utamaduni wa kabila langu kwa utamaduni wetu unafika mahali unangatuka watu wanadhani kungatuka ni kustaafu hapana sio sahihi. Ukitoka jandoni mzee wako lazima angatuke maana umekuwa sehemu ya jeshi la kabila na yeyote ambaye kijana wake yuko kwenye jeshi yeye anatoka.

Wazee hawaingii katika mambo ya vijana na sisi tupo lakini hatutaki kuingilia utendaji wao kama sisi tulivyoachiwa kuendesha nchi, ila Rais akituhitaji tupo tayari kwa ajili ya ushauri anaweza kuukubali au kuukataa. Nataka nimhakikishie kwa hili tupo pamoja na tutatoa maoni ya kurutubisha Sera, Sheria na Utendaji katika rasilimali za nchi hii.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA MAZISHI YA MARAYAPILI YA MZEE YUSTINO NDUGAI

$
0
0

Wziri Mkuu Kassim Majaliwa . akiweka Shada la Maua katika kaburi alipo Zikwa Kwamara ya Pili Marehemu Yustino Ndugai Baba Mzazi wa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Job Ndugai. Shughuli hiyo imefanyika June 17 , 2017 katika makaburi ya familia ya Ndugai Kijij cha Chimoloto Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.
Waiziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa Salamu za Serekali kwa Wananchi , Katika Tukio la Mazishi ya Mara ya Pili ya Marehemu Yustino Ndugai Baba Mzazi wa Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai . Marehemu Yustino alifariki Mwaka 1992 na amezikwa mara ya Pili June 17 , 2017 katika makaburi ya familia ya Ndugai Kijij cha Chimoloto Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Abdalah Bulembo (Mbunge) akitoa salamu kwa niaba ya Wabunge wa CCM , Katika Tukio la Mazishi ya mara ya Pili ya Marehemu Yustino Ndugai Baba Mzazi wa Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai . Marehemu Yustino alifariki Mwaka 1992 na amezikwa mara ya Pili June 17 , 2017 katika makaburi ya familia ya Ndugai Kijij cha Chimoloto Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

Vijana Wakumbushwa Umuhimu wa Kulipa Kodi

$
0
0


Mwalimu wa Elimu ya Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Bw. Gabriel Mwangosi akielezea jambo wakati wa Mdahalo wa Vijana kuhusu Nguvu ya Kodi, ulioandaliwa na Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TYVA Taifa Bw. Suleiman Makwita na Muongoza mada Bi. Nuria Mshare. Kauli mbiu ya mdahalo huo ni “Nguvu ya Kodi” Kodi kwa Huduma Bora za Jamii.
1
Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) Bw. Suleiman Makwita akifafanua jambo wakati wa mdahalo hukusu kodi ulioandaliwa na asasi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Muongozaji wa mdahalo huo Bi. Nuria Mshare na Mwalimu wa Elimu ya Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Bw. Gabriel Mwangosi
2
Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) Bi. Irene Kalumuna akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mdahalo hukusu kodi ulioandaliwa na asasi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
3
Muongozaji wa Mdahalo wa Vijana kuhusu umuhimu wa kodi  uliondaliwa na Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) Bi. Nuria Mshare akifafanua jambo wakati wa mdahalo huo leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni  Mwenyekiti wa TYVA, Bw. Suleiman Makwita na Mwalimu wa Elimu ya Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Bw. Gabriel Mwangosi. Kauli mbiu ya mdahalo huo ni “Nguvu ya Kodi” Kodi kwa Huduma Bora za Jamii.
4
Washiriki wa Mdahalo wa Vijana kuhusu umuhimu wa kodi  uliondaliwa na Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) wakichangia mada wakati wa mdahalo huo uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam leo. Mdahalo huo umeandaliwa na TYVA kupitia mradi wake wa Ushiriki wa Kijana katika masuala ya Kodi (YEGA) chini ya udhamini wa Shirika la Action Aid Tanzania
56
Baadhi ya washiriki wa Mdahalo wa Vijana kuhusu umuhimu wa kodi  uliondaliwa na Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) wakifuatilia mada wakati wa mdahalo huo uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam leo. Mdahalo huo umeandaliwa na TYVA kupitia mradi wake wa Ushiriki wa Kijana katika masuala ya Kodi (YEGA) chini ya udhamini wa Shirika la Action Aid.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO

WATENDAJI HAKIKISHENI MNASAFISHA TAARIFA CHAFU ZA WATUMISHI KWENYE MFUMO WA HCMIS

$
0
0

 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Susan Mlawi akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi kwa viongozi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Mbeya pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya na Halmashauri ya Wilaya ya mbeya alipofanya ziara ofisini hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017.
wat2
Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw.Micky Kiliba,akitoa ufafanuzi kuhusu ujazaji wa fomu za OPRAS zinazopima utendaji kazi wa Mtumishi wa Umma.
…………………………………………………………………………….
Watendaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wametakiwa kuhakikisha suala la taarifa chafu za Watumishi linamalizika haraka iwezekanavyo ili kurahisisha zoezi la uhakiki wa taarifa za kiutumishi kwenye Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS).

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Susan Mlawi alisema hayo katika kikao kazi na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya na  Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017.

“Sitegemei tena kusikia Halmashauri au Mkoa una taarifa chafu za watumishi wake, hivyo nawaagiza Maafisa Utumishi na Watendaji katika Mikoa na Halmashauri mhakikishe suala hili linafikia ukingoni” Bi.Susan alisema.

Aliongeza kuwa suala la uhakiki wa taarifa chafu za watumishi limefanyika kwa muda mrefu sasa, hivyo halitakiwi kuzungumzwa tena katika kipindi hiki.
Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu ,Ofisi ya Rais-UTUMISHI  Bw.Leornad Mchau aliongeza kuwa taarifa chafu za watumishi ni eneo ambalo linasabisha uwepo wa watumishi hewa.
“Unakuta taarifa za mtumishi hazionyeshi cheo chake wala hazionyeshi tarehe yake ya kuzaliwa, hili ni tatizo” Bw. Mchau alisema.

Alifafanua kuwa jitihada za kufanyia kazi taarifa chafu za Watumishi wa Umma zilianza toka mwaka 2010 ambapo Maafisa Utumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wanaohusika na Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS)  baadhi yao waliwajibishwa kwa kuzembea kufanyia kazi taarifa chafu.

Bw.Mchau alisisitiza kuwa Watumishi wa Umma watakaoonekana taarifa zao hazieleweke kwenye Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) watafutwa mara moja.

“Mwezi uliopita tuliondoa watumishi kadhaa ambao taarifa zao hazieleweki kwenye mfumo wa HCMIS na hakuna mtumishi hata mmoja aliyekuja kulalamika kuondolewa kwenye mfumo.” Bw. Mchau alisema na kuongeza kuwa kuanzia mwezi Julai 2017 takriban watumishi 16,000 ambao vyeo vyao havijulikani kwenye mfumo wa HCMIS wataondolewa.

Bw. Mchau alitoa rai kwa Watumishi wa Umma kuhakiki taarifa zao za kiutumishi kwa kujisajili katika Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) na kuangalia kama zipo sahihi kabla hawajaondolewa kwenye mfumo na pia kila mtumishi ahakikishe anajiandikisha na kupata kitambulisho cha Taifa ili utambulisho wake wa Taifa ujulikane.

“Mtumishi wa Umma ambaye hana kitambulisho cha Taifa au namba ya utambulisho wa Taifa tutamhesabu kuwa ni mtumishi hewa na yeyote ambaye ana mshahara usioeleweka ifikapo Julai 15, 2017 mfumo wa HCMIS utamtoa kimfumo (Automatically).

Hatima ya Watumishi walioghushi vyeti
Akitoa ufafanuzi kuhusu hatma ya Watumishi wa Umma walioghushi vyeti Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Susan Mlawi alisema kuwa inasubiriwa taarifa kutoka Baraza la Mitihani Tanzania ambayo itakuwa imejumuisha matokeo ya rufaa za Watumishi walio kwenye orodha ya vyeti vya kughushi.

 Katika hatua nyingine Bi. Susan aliainisha kuwa Ofisi ya Rais-UTUMISHI imeandaa mapendekezo ya namna ya kushughulikia suala la watumishi walioghushi vyeti.

 Upungufu wa Watumishi
Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Susan Mlawi alisema Serikali inaangalia namna ya kukabiliana na changamoto ya upungufu wa watumishi katika baadhi ya Halmashauri na Mikoa.
“Zipo baadhi ya ofisi ambazo zina watumishi wa ziada na nyingine zina watumishi wachache kwa maana hiyo ofisi yenye watumishi wa ziada itatakiwa iwahamishie kwenye ofisi nyingine yenye upungufu wa watumishi”Bi. Susan alisema.
Mfumo wa Wazi wa Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS)
Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri Kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw.Micky Kiliba alisema UTUMISHI inaangalia namna ya kufanyia marekebisho fomu za OPRAS za walimu, makatibu muhtasi na madereva ili kuhakikisha kuwa zinaendana na mipango mikakati yao ya kazi kwa mwaka mzima.
Wiki ya Utumishi wa Umma inatarajia kufikia kilele tarehe 23 Juni, ambapo nchi wanachama wa Umoja wa Afrika huitumia kutambua mchango wa watumishi katika utendaji kazi, na kuhudumia jamii. Ofisi ya Rais-UTUMISHI mwaka huu 2017 imepanga kuadhimisha kwa kukutana na Watendaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kujua changamoto wanazokutana nazo katika kutatua kero za Watumishi wa Umma.

BENKI YA DTB, EFM RADIO WATOA MSADA WA MADAWA TAASISI YA MIFUPA MOI

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa MOI, Dkt.Respicious Boniface, (kulia), akipokea sehemu ya msada wa madawa kutoka kwa Meneja wa Benki ya DTB Tawi la Morocco jengo la Airtel, jijini Dar es Salaam, Bi.Sheena .Y. Sinare, kwenye jengo jipya la MOI, leo Juni 18, 2017. DTB kwa kushirikiana na EFM Radio, wametoa msada wa madawa mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni 4 ili kusaidia watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi wanaopatiwa matibabu kwenye taasisi hiyo
 Dkt. Boniface, akipokea sehemu ya msada wa madawa kutoka kwa Afisa Uhusiano wa EFM Radio, Jesca Mwanyika kwenye jengo jipya la MOI jijini Dar es Salaam leo Juni 19, 2017. EFM kwa kushirikiana na Benki ya DTB wametoa msada huo wa madawa yenye thamani ya shilingi milioni 4 ili kusaidia watoto wenye matataizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi wanaopatiwa matibabu kwenye taasisi hiyo
 Mtayarishaji wa kipindi cha "Bustani ya Watoto" kinachopeperushwa na EFM, ambaye ndiye chachu ya kutolewa kwa msada huo, Bi. Flora Amon maarufu kama  Aunt FIFI, akikabidhi sehemu ya msada huo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Precious Boniface

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
BENKI ya DTB kwa kushirikiana na EFM Radio kupitia kipindi chake cha “Bustani ya Watoto”, wametoa msada wa madawa mbalimbali kwa Taasisi ya Mifupa MOT iliyoko Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, leo Juni 18, 2017.

Akikabidhi madawa hayo, Afisa Uhusiano wa EFM Radio, Bi.Jesca Mwanyika alisema, EFM kupitia kipindi chake cha watoto cha “Bustani ya Watoto” iliamua kuwashirikisha DTB ili kuona ni namna gani wanaweza kusaidia watoto waliolazwa kwenye Taasisi ya MOI hususan wale wenye matatizo ya kichwa kikubwa na mgongo wazi.

“Sisi kama EFM Radio tuna kipindi cha watoto cha Bustani ya Watoto, tumeona kwa vile tunashughulika na watoto, na kwa vile siku chache zilizopita Dunia iliadhimisha siku ya mtoto wa Afrika Duniani, basi tumeona tutoe kiasi hiki cha madawa kuwasaidia watoto hawa wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi waliolazwa hapa MOI.”Alisema Bi. Jesca.

Akizungumza kwa niaba ya DTB, Afisa Masoko wa benki hiyo, Bw.Baguma Ambari alisema, Benki kama taasisi inayotoa huduma kwa wananchi, inao wajibu mkubwa kutoa sehemu ya faida yake kusaidia jamii na hivyo imefurahishwa kuungana na EFM Radio katika kutoa msada huo wa madawa ambao anaamini utasaidia katika kuwahudumia watoto hao wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Akitoa shukrani zake, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface alisema, msada huo wa madawa utasaidia sana katika kuwapatia huduma za afyan watoto hao. “Kama mjuavyo wengi wa watoto hawa hutoka kwenye familia masikini kwa hivyo msada huu wa madawa utasaidia sana katika kuwapatia huduma.

“Madawa haya ni anti-biotic pamoja na kwamba watoto hawa wanaletwa hapa wakiwa na matatizo ya vichwa  baadhi yao huwa na infection sehemu mbalimbali za miili kama vile vifua au tumboni, lakini pia husaidia kutibu vidonda n.k.” Alifafanua Dkt. Boniface.
 Dkt. Boniface (mbele) akiongozana na Meneja wa DTB Tawi la Morocco jijini Dar es Salaam, Bi.Sheena Y. Sinare, wakati wakitembelea kuwajulia hali watoto hao wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi waliolazwa kwenye taasisi ya mifupa MOI jijini Dar es Salaam
 Dkt. Boniface (kushoto), akizungumza jambo na Bi. Sinare wakati walipokuwa kwenye moja ya wodi za watoto hao
 Dkt. Boniface (kushoto), akizungumza jambo na Bi. Sinare wakati walipokuwa kwenye moja ya wodi za watoto hao kuwajulia hali
 Afisa Masoko wa DTB, Bw. Baguma Ambar(kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya kutoa msada huo. Kulia ni Kaimu Afisa Uhusiano wa MOI, Bw.Frank Matua
 Afisa Masoko wa DTB, Bw. Baguma Ambar, (kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya kutoa msada huo.
  Mtayarishaji wa kipindi cha "Bustani ya Watoto" kinachopeperushwa na EFM, ambaye ndiye chachu ya kutolewa kwa msada huo, Bi. Flora Amon maarufu kama  Aunt FIFI,akielezea kilichomsukuma kuwa na mpango huo wa kutoa msada
   Mtayarishaji wa kipindi cha "Bustani ya Watoto" kinachopeperushwa na EFM, ambaye ndiye chachu ya kutolewa kwa msada huo, Bi. Flora Amon maarufu kama  Aunt FIFI,akielezea kilichomsukuma kuwa na mpango huo wa kutoa msada. Kulia anayesikiliza kwa makini, niAfisa Uhusiano wa EFM, Bi. Jesca Mwanyika
 Dkt. Boniface akitoa neno la shukurani baada ya kupokea msada huo
  Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface akitoa neno la shukurani baada ya kupokea msada huo
 Baadhi ya wafanyakazi wa EFM na DTB waliohudhuria hafla hiyo
  Baadhi ya wafanyakazi wa EFM  waliohudhuria hafla hiyo
 Mfanyakazi wa EFM, Bw.Sali Mlindila, akiwa amebeba boksi lenye dawa zilizotolewa msada kwa MOI
Wafanyakazi wa EFM na DTB wakisikiliza kwa makini wakati Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface alipokuwa akielezea umuhimu wa jamii kuwasaidia watoto hao.
Wafanyaakzi wa EFM na watoto wao na wale wa DTB wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface

UNIC yataka wahitimu Academic International kutojiingiza katika dawa za kulevya

$
0
0


Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo (kulia) na mgeni rasmi katika Maafali ya wahitimu wa Darasa la Saba katika shule ya Academic International (Academic International Primary School) ya jijini Dar es Salaam akiwasili katika ukumbi wa mahafali hayo. Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi ya Academic International, Bi. Natasha Karamagi akimuongoza mara baada ya kupokea heshima ya vijana wa Skauti shuleni hapo baada ya kupokewa. Mgeni rasmi kwenye Mahafali ya wahitimu wa Darasa la Saba katika Shule ya Academic International (Academic International Primary School) na Ofisa Habari wa UNIC, Stella Vuzo (katikati) akimkabidhi cheti mmoja wa wanafunzi wahitimu wa darasa la saba kwenye hafla ya maafali hayo. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi wa shule hiyo, Tom Bowyer. Mgeni rasmi kwenye Maafali ya wahitimu wa Darasa la Saba katika Shule ya Academic International (Academic International Primary School) na Ofisa Habari wa UNIC, Stella Vuzo (wa pili kulia) akimkabidhi zawadi mmoja wa wanafunzi wahitimu wa darasa la saba aliofanya vizuri katika masomo yake. Wa kwanza kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi wa shule hiyo, Tom Bowyer pamoja na meza kuu wakishuhudia Picha ya baadhi ya wahitimu wa Darasa la Saba katika shule hiyo wakiwa na mgeni rasmi na viongozi wa Shule ya Academic International (Academic International Primary School) ya jijini Dar es Salaam. Burudani ya ngoma ikitolewa na wanafunzi wa Shule ya Academic International (Academic International Primary School) katika hafla ya Maafali ya wahitimu wa Darasa la Saba katika shule hiyo Wanafunzi waliohitimu Darasa la Saba wa 'Academic International Primary School' wakiwa katika picha ya pamoja Baadhi ya wazazi wa wanafunzi wahitimu Darasa la Saba katika shule ya Academic International wakiwa katika hafla ya maafali hayo.

 KITUO cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kimewaonya wanafunzi wa 'Academic International Primary School' waliohitimu Darasa la Saba kutojiingiza katika dawa za kulevya, kwani ni eneo linaloharibu kwa kasi maisha ya vijana wengi kupitia makundi. 

Ushauri huo umetolewa jana na Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akizungumza na vijana hao wahitimu darasa la saba katika shule hiyo ya jijini Dar es Salaam. Afisa huyo kutoka UNIC, Bi. Vuzo ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya mahafali hayo alisema wamekuwa na program ya kutoa elimu kwa jamii juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya, wamebaini kuwa vijana wengi wanaotumia dawa za kulevya wamefuata mkumbo toka kwa marafiki zao na kwenye makundi na kupata madhara makubwa ikiwemo kuharibu maisha yao.

 "Ukweli ni kwamba matumizi ya dawa za kulevya hayajaribiwi, ukianza tu matumizi ndio umeingia rasmi maana kiu ya kuendelea itakushinikiza. Vijana wengi wameharibu mustakabali wa maisha yao kabisa kwa madawa ya kulevya. Hii tu ni kwa kuwa walikosea katika kufanya maamuzi awali, walifanya maamuzi mabaya. Msikubali kutumika pia katika ubebaji madawa haya nje ya nchi kwa ahadi ya kupewa fedha nyingi au kazi nzuri. Msikubali kubeba mizigo ya watu hovyo mnaposafiri, mnaweza kujikuta mnaingia katika kesi ya kusafirisha madawa haya," alisema Bi. Stella Vuzo akizungumza na wahitimu na wazazi wao.  Picha ya pamoja kati ya Meza Kuu na moja ya kikundi cha burudani cha wanafunzi wa Shule ya Academic International (Academic International Primary School) kwenye Maafali ya wahitimu wa Darasa la Saba katika shule hiyo ya jijini Dar es Salaam.[/caption]   [caption id="attachment_79878" align="aligncenter" width="800"] Picha ya pamoja kati ya Meza Kuu mgeni rasmi na baadhi ya wahitimu wa Darasa la Saba katika shule ya Academic International walioshinda tuzo mbalimbali za masomo.

  Aidha aliwaeleza kuwa hatua wanaoingia ni ya kuchagua kuwa na marafiki wazuri ambao watakuwa mwongozo kwao na wasiogope kuzungumza nao juu ya changamoto mbalimbali zitakazo wakabili na kuangalia namna ya kuzitatua. Aliwahimiza kutambua kuwa kuanzia sasa wanaingia katika hatua ya mabadiliko kimaisha hivyo umakini unahitajika. 

"...Mnaingia kwenye hatua ambayo wewe mwenyewe utaanza kufanya maamuzi juu ya maisha yako. Si kitu kirahisi kama mnavyodhani umakini, nguvu na jitihada binafsi zinaitajika ili kujenga mustakabali wa maisha yenu." Alisisitiza mgeni huyo rasmi kutoka UNIC. "Bila shaka walimu hapa shuleni wamefanya kazi yao ipasavyo, kwa kuwafundisha na kuwasaidia katika masomo mbalimbali, Walimu wamewatia moyo na kuwapa motisha ili muweze kufanya vizuri katika mitihani yenu ya mwisho. 

Kwa upande wa wazazi wenu wamejitahidi kujitoa tangu mkiwa wadogo hata kuwasaidia kuwapa mazoezi madogo madogo nyumbani hadi leo hii ambapo mnaingia katika hatua nyingine ya maisha ya mwanadamu, hata hivyo kadri mnavyo endelea kukua mnatakiwa kuendana na tamaduni zetu za Kiafrika kuheshimu wakubwa zenu. Mnaitaji kuwa karibu na wazazi wenu na kuwasikiliza zaidi kuna mengi ya kujifunza kwao ambayo nyinyi hamna." 

Hata hivyo aliwataka kutambua kuwa kila hatua ya maamuzi wanayoifanya leo inaweza kujenga ama kuharibu maisha yao ya kesho, hivyo umakini zaidi unaitajika. Aliwataka wahitimu hao kutumia muda kujisomea vitabu, magazeti na machapisho mbalimbali ili kupata habari mbalimbali za ndani na nje ya nchi na hata kujua nini kinaendelea nchini kwao na hata nje ya nchi. "...Kuweni sehemu ya kutatua changamoto mbalimbali za ulimwengu. Muwe wabunifu na hata kuwasaidia wengine katika maisha mazuri. Msikubali kuingizwa katika tamaduni zisizofaa ama kupitwa na wakati. Teknolojia ni nzuri lakini msikubali kutekwa nayo, hata kuwaingiza katika mambo yenye madhara.

 Leo mnamaliza darasa la saba (std 7) ni hatua muhimu ya masomo, lakini huwezi kupata kazi kwa kutegemea cheti cha darasa la saba, endeleeni kusonga mbele kielemu. Hakuna haja ya kupoteza muda “Fanya la wakati, wakati unawakati, kwani utakuja wakati utahitaji kufanya la wakati na hakutakuwa na wakati wa kufanya ya wakati” Picha ya pamoja kati ya wahitimu wa Darasa la Saba na mgeni rasmi pamoja na Meza Kuu katika hafla ya maafali yao. Picha ya pamoja kati ya Meza Kuu mgeni rasmi na baadhi ya wahitimu kumi bora waliofanya vizuri katika masomo yao. Baadhi ya wahitimu wa Darasa la Saba katika shule ya Academic International wakiwa katika hafla ya maafali yao yaliofanyika shuleni hapo juzi.

TGGA YAENDESHA KAMBI YA MAFUNZO YA MTOTO WA KIKE KUJIAMINI, KUJITAMBUA NA KUWA JASIRI

$
0
0

Washiriki wa Kambi ya Mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake wakiimba wimbo wa Taifa baada ya kujifunza jinsi ya kufunga kamba vifundo na kupandisha bendera ya Taifa katika kambi ya siku tano iliyoandaliwa na Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Mombasa, Dar es Salaam
Wakiimba wimbo wa Taifa

Walimu na viongozi wa chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), wakijenga mahema kwa ajili ya kambi ya kumjengea uwezo mtoto wa kike yaliyoandaliwa na TGGA, Mombasa, Dar es Salaam jana. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG





Wakitundika vikombe kwenye matawi
Wapika chakula
Wakiwa kwenye kalo la kuoshea vyombo waliliolitengeneza wenyewe
Sehemu ya kutupia taka
Usafi eneo la vyoo
Kamishna Msaidizi wa TGGA Mkoa wa Tanga, Fatuma Juma akiwafundisha washiriki jinsi ya kufunga vifundo vya kamba vinavyoo kwa daraj, bendera na mapambo hotelini
Wakiunga vifundo hivyo
Washiriki wakiwa busy kujifunza kufunga vifundo
Fatuma akiwasimamia washiriki
Sehemu ya kambi ambamo Girl Guides hao wanalala
Fatuma ambaye ni Msimamizi wa kambi hiyo akimwelekeza kufunga vifundo mmoja wa washiriki
Wakijifunza kufunga vifundo kwenye mti




Na Richard Mwaikenda

MAFUNZO ya kujiamini na kujitambua kwa mtoto wa kike yamepamba moto katika kambi maalumu inayoendelea eneo la Mombasa, Ilala, Dar es Salaam.

Kambi hiyo iliyoandaliwa na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), inashirikisha walimu na viongozi wa chama hicho kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Akizungumza na mwandishi wetu aliyetembelea kambi hiyo leo,Kamishna wa TGGA,Mkoa wa Tanga, Modesta Mshata alisema kuwa lengo la kambi hiyo ni kuwajengea uwezo walimu na viongozi wa kujiamini na kujitambua.

"Tunata mtoto wa kike popote alipo ajiamini, ajitambue na kuwa jasiri ikiwemo pia kumudu maisha kwa kushirikiana vyema na jamii inayomzunguka."Alisema Mshata.

Pia alisema kuwa, lengo ni kumfundisha mtoto wa kike kuwa mama na kiongozi bora wa familia na taifa kwa ujumla. Washiriki 36 wa kambi hiyo ya siku tano wanatoka Kondoa, Dodoma, Tanga, Lindi, Rukwa na Dar es Salaam pamoja na nchi za Uganda, Rwanda na Madagascar.

Naye Emiliana Stanslaus ambaye ni Mkufunzi Mkuu wa mafunzo kutoka Makao Makuu ya TGGA, alisema kuwa lengo la kambi hiyo ni kutoa mafunzo kwa washiriki ili wakirudi mikoani wakawafundishe watoto wa kike.

Alisema washiriki hufundishwa jinsi ya kutengeneza karo, bafu, shimo la uchafu, kichanja cha kuanikia vyombo, kamba ya kuanikia nguo, sehemu ya kunawia mikono, sehemu ya kupata maji ya kuoga, kuandaa eneo la kulala, jiko na kufanya mazoezi mbalimbali ya viungo.

Emiliana ambaye amewahi kuhudhuria Kambi ya Kimataifa ya Skauti wa kike nchini Norway, alisema kuwa kambi hiyo inakuwa kama ya kijeshi kwani hujifunza mambo mengi ya ukakamavu na jinsi ya kujiamini na kuwa na ujasiri katika mazingira yoyote.

Kiongozi wa Girl Guides, Rachel Baganyila kutoka Uganda, ambaye yupo nchini kwa mafunzo ya miezi sita ya kubadilishana uzoefu, alisema kuwa amefarijika sana kupata mafunzo hayo ambayo asilimia kubwa ni mapya na kwamba atakaporejea kwao atawafundisha wenzie.

Alisema kuwa amejifunza utamaduni wa kitanzania na masuala ya uongozi pamoja na jinsi ya kutengeneza mafundo yanayosaidia kupandisha na kushusha bendera ya taifa na kuiheshimu pia.

Sharifa Mkwango ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, alisema kuwa mafunzo aliyoyapata atahakikisha akirejea kwao atawafundisha watoto wa kike kuhusu ukakamavu, kufunga mafundo, alama za TGG, stadi za kazi na jinsi ya kuandaa kambi za mafunzo.

KIJANA ABDULMJID MUJAHID KUTOKA YEMEN AMEIBUKA MSHINDI WA MASHINDANO YA KIMATAIFA YA QUR-AN

$
0
0

KIJANA Abdulmjid Mujahid kutoka Yemen ameibuka mshindi wa mashindano ya kimataifa ya Qur-an yaliyozishindanisha nchi kumi ambapo mshindi  amezawadiwa dola 5000 za kimarekani huku ubalozi wa Kuwait ukimzawadia dola 500, mshindi wa pili wa mashindano hayo ni Omary Abdallah kutoka Tanzania ambaye nae amezawadiwa dola 4000 na dola 300 kutoka ubalozi wa Kuwait.

Mashindano hayo yameshirikisha nchi kumi zikiwemo Uganda, Mali, Tanzania Bara, Yemen, Russia, Uingereza, Libya, Bangladesh, Marekani na Jumuiya ya Falme za kiarabu (United Arab Emirates).
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akimkabidhi hundi ya dola za Kimareni 5,000 mshindi kwanza wa mashindano ya kimataifa ya Qur-an Abdulmjid Mujahid kutoka Yemen leo jijini Dar es Salaam. 

Pia Mashindano hayo yameudhuriwa na viongozi mbalimbali yakiongozwa na makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddy, na mlezi wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi, Muft Mkuu wa Tanzania Abubakar Zuber, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum, mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete na mgeni maalum kutoka Saudi Arabia Abdallah Basfar ambaye ni msomaji Qur-an wa kimataifa.

Akihutubia katika mashindano hayo Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Ally Seif Iddy ameeleza kuwa vijana wamekosa adabu na matendo ya ulawiti, mauaji kwa watoto wachanga, unyanyasaji, mauaji ya wenye ulemavu wa ngozi yamekuwa yakiripotiwa, huku akieleza kuwa aamini kama Mwenyezi Mungu anayaridhia matendo haya, hivyo tabia za watanzania na waislamu ziendane na maamrisho ya Qur-an.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akimkabidhi hundi ya dola za Kimareni 4,000 mshindi pili wa mashindano ya kimataifa ya Qur-an wa Tanzania,Omary Abdallah leo jijini Dar es Salaam. 

Pia Makamu wa Rais Balozi Seif Ally Iddy ameongeza kuwa mbora ni mwenye kujifunza Qur-an na akawafundisha wengine Mwenyezi Mungu amewanasihi waislamu katika kitabu chake kitukufu.

Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi awapongeza wanafunzi wa kiislamu wanaojifunza Qur-an kwani kufanya hivyo ni kuiendea jamii njema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Tanzania Sheikh Othman Ally Kaporo amewataka wadau wa masuala ya Qur-an kuhakikisha Qur-an inakaa katika nyoyo za vijana ili jamii iweze kuwa bora na kuheshimiana wakubwa kwa wadogo.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi, akipokea tuzo ya heshima kutoka Muft wa Tanzania Abubakar Zuber iliyotolewa na Jumuiya ya kuhifadhisha Qur-an Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur-an yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo.

Huku Muft Mkuu wa Tanzania Abubakari  amesema ni vyema watu wakajifunza Qur-an kwasababu ni dawa ya kila tatizo, endapo waja wataifuata kwa mafunzo yaliyoamrishwa na kuacha yaliyokatazwa, kwani Qur-an imekataza kuuana, kuchukiana, kuvuruga amani.

Jumuiya ya kuhifadhisha Qur-an imetoa tuzo za heshima kwa wanahakati wa Qur-an akiwemo Abdallah Basfar na Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi, huku ikitambua mchango huo kwa masheikh mbalimbali akiwemo Sheikh Ismail Mohammed, Sheikh Adam Ahmad, Marehemu Hashim Haji, Isihaka Abdehell, Marehemu Yahya Hussein na Sheikh Mohammed.

Mashindano hayo yameanzishwa 1992 yakiwa yakimkoa na mpaka sasa ni mashindano ya kimataifa huku yakiwa niya 25 tangu kuanzishwa kwake.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi, akizungumza katika mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur-an yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd, akizungumza katika mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur-an yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo.
Muft Mkuu wa Tanzania Abbakar Zubeir akizungumza katika katika mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur-an yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo.
Picha ya pamoja

Sehemu ya viongozi mbalimbali na wananchi wakifatilia mashindano haoyo leo jijini Dar es Salaam.

SPIKA NDUGAI AONGOZA WABUNGE KATIKA HARAMBEE YA UJENZI WA JENGO LA JUMUIYA YA KIKRISTO TANZANIA TUKIO LILILOFANYIKA LEO MJINI DODOMA.

$
0
0
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya kikristo Tanzania, Askofu Dkt. Alex Malasusa kabla ya kuanza harambee kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Jumuiya ya kikristo Tanzania, katika tukio lililofanyika leo Mjini Dodoma, Spika Ndugai pia ni Mgeni rasmi na aliongoza Wabunge katika harambee hiyo. 
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Mizengo Pinda (kushoto) kabla ya kuanza harambee kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Jumuiya ya kikristo Tanzania, katika tukio lililofanyika leo Mjini Dodoma. katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya kikristo Tanzania, Askofu Dkt. Alex Malasusa 
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kulia)akiongoza Wabunge Mbali mbali kucheza nyimbo ya injili kama njia moja wapo ya kuhamasisha uchangiaji kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Jumuiya ya kikristo Tanzania, tukio lililofanyika leo Mjini Dodoma 
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza jambo kabla ya kuanza harambee kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Jumuiya ya kikristo Tanzania, tukio lililofanyika leo Mjini Dodoma. kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Mizengo Pinda na katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya kikristo Tanzania, Askofu Dkt. Alex Malasusa 
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akiteta jambo na Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah (kulia) baada ya kumalizika kwa harambee kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Jumuiya ya kikristo Tanzania, tukio lililofanyika leo Mjini Dodoma, Pia Spika Ndugai aliongoza Wabunge katika harambee hiyo. 
Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Mizengo Pinda (kushoto) akisalimiana na Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah (kulia) baada ya kumalizika kwa harambee kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Jumuiya ya kikristo Tanzania, katikati ni Ndg. Elton Mapesa Mwakilishi wa Harambee kutoka External, Ubungo Jijini Dar es Salaam. Katika harambee hiyo, Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai aliwaongoza wa Bunge katika uchangiaji wa ujenzi wa jengo hilo. 
Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Mizengo Pinda (wa pili kushoto) akizungumza jambo baada ya kumalizika kwa harambee kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Jumuiya ya kikristo Tanzania, kulia ni Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah, kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya kikristo Tanzania, Askofu Dkt. Alex Malasusa na wa pili kulia ni Ndg. Elton Mapesa Mwakilishi wa Harambee kutoka External Ubungo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Hamidu City Park, Kigamboni Bw.Hamidu Mvungi awaandalia futari Waislamu, ndugu jamaa na marafiki

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Hashim Mgandilwaakimshukuru Bw. Hamodu H. Mvungi mara baada ya kushiriki katika futari hiyo pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria.
Bw. Hamidu H. Mvungi miliki wa kijiji cha Hamidu City Park, Mikwambe Kibada Kigamboni chenye nyumba 1500 akizungumza na wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika futari aliyowaandalia wageni wake wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mh .Hashim Mgandilwa ambapo aliwashukuru wageni waalikwa hao kwa kujumuika naye katika futari hiyo katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan, huku akiwatambulisha makazi hayo yenye nyumba za kuuza ambapo ameshirikiana na mabenki mbalimbali na kukopesha kwa watu wanaohitaji nyumba katika kijiji hicho.
Mtangazaji wa Chanel Ten na MC wa Shughuli hiyo ya Futari Bw. Albert Kilala akikaribisha wageni mbalimbali waliohudhuria katika futari hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Hashim Mgandilwa na Mwenyeji wake Bw. Hamidu Mvungi wakiongoza wageni waalikwa katika futari hiyo.
 
Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika futari hiyo wakichukua chakula.
 
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Hashim Mgandilwa katikati , Mwenyeji wake Bw. Hamidu Mvungi pamoja na wageni wake wakipata futari.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rahel Mhando pamoja na wageni mbalimbali waalikwa wakishiriki katika futari hiyo iliyoandaliwa na Bw. Hamidu Mvungi nyumbano kwake Kigamboni.
    
Baadhi ya wageni mbalimbali walioshiriki katika futari hiyo.
Bw. Hamidu Mvungi na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mh. Hashim Mgandilwa wakiwa katika picha ya pamoja. 
Bw. Hamidu Mvungi na Mkewe wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni wao.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JUNE 19,2017

WAZIRI WA MALIASILI, PROF. JUMANNE MAGHEMBE AZINDUA MRADI WA UHIFADHI NA MAENDELEO YA IKOLOJIA YA PORI LA AKIBA LA SELOUS (SECAD) ULIOFADHILIWA NA SERIKALI YA UJERUMANI

$
0
0
NA HAMZA TEMBA - WMU
..............................................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe kwa kushirikiana na Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Egon Konchanke amezindua Mradi wa Uhifadhi na Maendeleo ya Ikolojia ya Pori la Akiba la Selous SECAD (Selous Ecosytem Conservation and Development Program) ambao umefadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania, mradi huo utatekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, WWF (World Wildlife Fund) na FZS (Frankfurt Zoological Society).


Akizungumza katika hafla iliyofanyika jana, Matambwe na Tagalala Selous, Mkoani Morogoro, Waziri Maghembe alisema Serikali ya Ujerumani kupitia benki ya KFW imechangia Euro Mil. 18 (sawa na Shilingi Bil. 45.124) katika mradi huo wa miaka mitano huku mashirika ya WWF (World Wildlife Fund) na FZS (Frankfurt Zoological Society) yakichangia Euro laki 4 kila moja (sawa na Shilingi bil. 2.005) katika mradi huo. Pamoja na uzinduzi huo alizindua pia Mpango Kazi wa Dharura wa kuendeleza pori hilo.


"Mradi huu ni muhimu sana kwakua utasaidia kuongeza nguvu kwenye jitihada zetu za kuendeleza na kuimarisha hifadhi ya pori hili la Selous ikiwemo upatikanaji wa vitendea kazi muhimu pamoja na kutuongezea nguvu kwenye mapambano dhidi ya ujangili", alisema Prof. Maghembe.


Alisema jitihada ambazo Serikali imeshazifanya katika pori hilo ni pamoja na kuimarisha doria za ndege zenye rubani na zisizo na rubani (drones), kutoa mafunzo ya jeshi usu kwa askari, kuongeza maaskari pamoja na vitendea kazi ambapo katika mwaka ujao wa fedha Serikali itatoa magari mengine 15 kusaidia pori hilo.


"Pamoja na jitihada hizo tunawekeza dola za kimarekani Milioni 156 (sawa na Shilingi bilioni 349.441) kwa ajili ya kuboresha pori hili (Selous), Ruaha, Mikumi, Rungwa na Kitulo kuhakikisha watalii wanatembelea maeneo haya na kuondoa kile kikwazo cha wao kutotembelea hifadhi za kusini, hiyo inaenda sambamba na kuimarishwa kwa shirika la ndege la Serikali la Air Tanzania na kuondoa changamoto iliyokuwepo ya usafiri wa anga", alisema Prof. Maghembe. 


Akizungumzia changamoto ya ujangili katika pori hilo alisema Serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupambana na tatizo hilo ambapo majangili wengi wameshakamatwa katika maeneo ya Tunduru, Namtumbo na maeneo ya katikati ya Selous. Alisema changamoto hiyo bado ipo katika maeneo ya Mkoa wa Ruvuma ambapo imeripotiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa huo kuwa kuna upatikanaji wa silaha za kivita kutoka nchini Msumbiji ambazo zinapatikana kwa watu kubadilishana na magunia ya mchele changamoto ambayo inaendelea kufanyiwa kazi.


Wakati huo huo, Prof. Maghembe akijibu swali aliloulizwa na wanahabari kuhusu hatua iliyofikiwa juu ya kauli aliyoitoa bungeni hivi karibuni ikiwa na dhamira ya kuunganisha taasisi zote za uhifadhi nchini alisema, tayari ameshaunda kamati ya watu sita ikiongozwa na Mkuu wa Chuo cha Wanyamapori Mweka, Prof. Japhary Kidegesho kwa ajili kuangalia namna bora ya kutekeleza azma hiyo. "Tayari kamati hiyo imeshaanza kazi na itaonana na wadau mbalimbali kupata maoni yao na katika kipindi cha mwezi na nusu watatuletea ripoti", alisema.


Kwa upande wake Balozi Konchanke alimuahakikishia Prof. Maghembe kuwa Serikali ya Ujerumani itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili hifadhi hiyo ikiwemo ubovu wa miundombinu na uvamizi  pori hilo kwa faida ya jamii kwa ujumla. Aidha, alitoa wito kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA kubuni mbinu mpya za kukabiliana na changamoto zilizopo.


Meja Jenerali Gaudence Milanzi ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, alisema "Serikali kwa kushirikiana na wadau wa uhifadhi imefanya kazi kubwa kuhakikisha Selous haiondolewi katika orodha ya maeneo ya urithi wa dunia yaliyopo hatarini kutoweka,  hiyo ni pamoja na kunzishwa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyanapori Tanzania TAWA, kuanzishwa kwa mkakati wa kitaifa wa kukabiliana na ujangili na miradi mbali ikiwemo huu wa SECAD uliozinduliwa leo ambayo kwa kiasi kikubwa imeasaidia katika kuendesha hifadhi zetu pamoja na kusaidia kwenye mapambano dhidi ya ujangili".


Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, TAWA, Martin Loibooki aliishukuru Serikali ya Ujerumani kwa mradi huo na kusema kuwa utasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na changamoto mbalimbali katika pori hilo ikiwemo ya uhaba wa vitendea kazi, miundombinu ya barabara na ujangili na hivyo kuifanya hifadhi hiyo iendelee kuwa miongoni mwa maeneo ya urithi wa dunia.


Pori la Akiba la Selous ni hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania ikiwa ukubwa wa Kilomita za mraba 50,000. Hifadhi hiyo ambayo ipo katika mikoa ya Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara na Ruvuma ina vivutio vingi vya utalii huku ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu ya barabara, ujangili, rasilimali watu na vitendea kazi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizindua Mradi wa Uhifadhi na Maendeleo wa Ikolojia ya Pori la Akiba la Selous (SECAD) ambao umefadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika hafla iliyofanyika jana Matambwe, Selous Mkoani Morogoro. Wanaoshudia kulia kwake ni Balozi wa Ujerumani, Egon Konchanke, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili, Meja Jenerali Gaudence Milanzi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Prof. Faustin Kamuzora.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa Wizara hiyo, Prof. Alexander Songorwa Mpango Kazi wa Dharura wa Kuendeleza Pori la Akiba la Selous baada ya kuuzindua sambamba na mradi wa Uhifadhi na Maendeleo ya Ikolojia ya Pori la Akiba la Selous (SECAD). Kulia kwake ni Balozi wa Ujerumani, Egon Konchanke, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi, Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Prof. Faustin Kamuzora, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Martin Loibooki na Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Dkt. Dembe. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) na  Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Egon Konchanke wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa magari sita aina ya Land Cruiser ambayo ni sehemu ya Mradi aliouzindua wa Uhifadhi na Maendeleo ya Ikolojia ya Pori la Akiba la Selous (SECAD).
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akijaribu moja ya gari baada ya uzinduzi wa magari sita aina ya Land Cruiser ambayo ni sehemu ya Mradi huo.
 Magari sita aina ya Land Cruiser yaliyotolewa na Serikali ya Ujerumani kama sehemu ya mradi wa SECAD.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (kushoto) akijadiliana jambo na Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira Prof. Faustin Kamuzora (katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Meja Jenerali Mstaafu, Hamisi Semfuko (kulia).
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Mghembe (kushoto) akipokea zawadi ya picha yenye ujumbe wa Mashujaa wa Kuokoa Selous kutoka kwa Mkurugenzi wa Afrika wa WWF Ujerumani, Philipp Goltenboth (kulia). Anaeshuhudia katikati ni Mkurugenzi Mkaazi wa WWF Tanzania, Dkt. Amani Ngusaru.
Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Mghembe (wa tatu kushoto), Balozi wa Ujerumani, Egon Konchanke (wa pili kushoto) na viongozi wengine wakuu wa Wizara na Taasisi pamoja na washiriki wa hafla hiyo. Nyuma yao ni ziwa Tagalala ambalo ni sehemu ya kivutio cha utalii ndani ya hifadhi hiyo. 
 Baadhi ya watumishi wa Pori la Akiba la Selous wakiwa katika hafla hiyo.
Taswira mwanana ya baadhi ya Twiga ndani ya Pori la Akiba la Selous.
 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akipokelewa jana katika uwanja mdogo wa ndege wa Matembwe uliopo Selous na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Martin Loibooki (wa pili kushoto) alipowasili kwa ajili ya hafla hiyo. Nyuma yake anayeshuka kwenye ndege ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof. Alexander Songorwa (kushoto).
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana katika kituo cha Tagalala, ndani ya Pori la Akiba la Selous Mkoani Morogoro.
Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Egon Konchanke akizungumza katika hafla hiyo.
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akizungumza katika hafla hiyo jana.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Prof. Faustin Kamuzora akizungumza katika hafla hiyo. Kushoto Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Meja Jenerali Mstaafu, Hamis Semfuko akizungumza katika hafla hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Martin Loibooki akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana, Tagalala, Selous.

Mshindi wa Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya NBC akabidhiwa gari lake

$
0
0

Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Andrew Lyimo (katikati), akikabidhi kadi ya gari kwa Rose Richard Getenyi kwa niaba ya mumewe, Lawrence Njozi aliyeshinda zawadi ya gari mpya aina ya Toyota Double Cabin Pick Up baada ya kushiriki katika kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo. Anayeangalia ni Meneja Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza, Dorothea Mabonye. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Andrew Lyimo (katikati), akikabidhi ufunguo wa gari mpya kwa Rose Getenyi kwa niaba ya mumewe, Lawrence Njozi aliyeshinda zawadi ya gari mpya aina ya Toyota Double Cabin Pick Up baada ya kushiriki katika kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo. Anayeangalia ni Meneja Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza, Dorothea Mabonye. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Rose Gitenyi akifurahia kuwasha gari lao Toyota Double Cabin Pick Up jipya ambalo mumewe alijishindia katika kampeni ya akaunti ya Malengo iliyoendeshwa na NBC. Familia ya mteja wa Benki ya NBC Lawrence Njozi aliyeibuka mmoja wa washindi wawili wa kampeni ya Malengo ya benki hiyo na kujishindia gari jipya aina ya Toyota Double Cabin Pick Up wakipozi kwa picha mbele ya gari hilo mara baada ya Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa NBC, Andrew Lyimo (kulia) kumkabidhi mke wa mshindi huyo, Rose Getenyi (wa tano kushoto), jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

MASAUNI ADHAMINI MASHINDANO MAKUBWA YA KUHIFADHI QUR-AN, ZANZIBAR NA TANZANIA BARA

$
0
0

Mgeni rasmi katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an, Waziri wa Nchi, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Abood akimkabidhi zawadi mshindi wa maswali ya papo kwa papo, Ilham Idrisa (kulia). Kushoto ni Mdhamini ya  mashindano hayo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni. Watatu kushoto,  Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nassor Salim Jazeera. Mashindano hayo yaliyoshirikisha Madrasa mbalimbali za Jimbo la Kikwajuni pamoja na maeneo mbalimbali ya Zanzibar na Tanzania Bara, yalifanyika katika Viwanja vya Mnara wa Kisonge mjini Unguja. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauniakizungumza kabla ya mgeni rasmi katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an, Waziri wa Nchi, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Abood(katikati) kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano hayo.Mashindano hayo yaliyoshirikisha Madrasa mbalimbali za Jimbo la Kikwajuni pamoja na maeneo mbalimbali ya Zanzibar na Tanzania Bara, yalifanyika katika Viwanja vya Mnara wa Kisonge mjini Unguja na kudhaminiwa na Mbunge wa Jimbo hilo. Kulia ni Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nassor Salim Jazeera.
Mwanafunzi Khamis Mussaa kionyesha jitihada zake katika Mashindano ya kuhifadhi Qur-an katika Jimbo la Kikwajuni, Unguja, Zanzibar, linaloongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, na mdhamini wa mashindano hayo, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani). Mashindano hayo yalishirikisha Madrasa mbalimbali za Jimbo la Kikwajuni pamoja na maeneo mbalimbali ya Zanzibar na Tanzania Bara.

Sehemu ya washiriki katikaMashindano ya Kuhifadhi Qur-an wakimsikiliza mdhamini wa Mashindano hayoNaibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati nalipokua akitoa hotuba yake. Katika hotuba yake Masauni alisema washiriki wameonyesha uwezo mkubwa wa kuhifadhi Qur-an.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsalimia Diwani wa Wadi ya Kikwajuni, Ibrahim Ngasa wakati alipokuwa anawasili katika Viwanja vya Mnara wa Kisonge, Unguja, Zanzibar leo kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kuhifadhi Qur-an katika jimbo lake la Kikwajuni yaliyoshirikisha Madrasa mbalimbali za jimboni mwake pamoja na maeneo mbalimbali yaZanzibar na Tanzania Bara.Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Mgeni rasmi katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an, Waziri wa Nchi, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Abood (kushoto) akimsalimia Mwenyekiti wa Taasisi ya TAYI, Abdalla Miraji, wakati kiongozi huyo alipokuwa anawasili katika Viwanja vya Mnara wa Kisonge, Unguja, Zanzibar leo kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kuhifadhi Qur-an katika Jimbo la Kikwajuni yaliyoshirikisha Madrasa mbalimbali za Jimbo la Kikwajuni pamoja na maeneo mbalimbali ya Zanzibar na Tanzania Bara.Katikati ni mdhamini wa mashindano hayo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni.

MSIICHUKIE SERIKALI ILIYOPO MADARAKANI KWA KUKOSA AJIRA.

$
0
0
Wanafunzi wa shirikisho la vyuo vikuu nchini wa chama cha mapinduzi wanaomaliza masomo yao wametakiwa kuacha kukichukia chama hicho kwa madai ya kukosa ajira kwani kufanya hivyo nikwenda kunyume na ilani ya chama.

BENKI YA CBA TANZANIA YAWAANDALIA IFTAR WATEJA WAKE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Afrika Tawi la Tanzania (CBA Tanzania), Gift Shoko akizungumza na baadhi ya wateja wakubwa wa benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, wakati benki hiyo ilipoandaa futari mahsusi. Kati ya mengi aliyoeleza, Shoko aliwahakikishia wateja wa benki hiyo jitihada madhubuti na endelevu zinazoendelea kufanya na benki ya CBA kwa kuboresha huduma na bidhaa zake wakati wote. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangala kama mgeni rasmi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Benki ya Biashara Afrika Tawi la Tanzania (CBA Tanzania), Jijini Dar es Salaam.
Wateja wakubwa wa Benki ya Biashara Afrika Tawi la Tanzania (CBA Tanzania), wakipakua futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Masoko wa Benki ya CBA Tanzania, Solomono Kawiche (wa kwanza kulia) akimuongoza na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla pamoja na Mke wake kupakua futari. Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Afrika Tawi la Tanzania (CBA Tanzania), Gift Shoko (wa kwanza kushoto) akipakua futari pamoja na wateja.
Wateja wakipata futari kwa pamoja.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Afrika Tawi la Tanzania (CBA Tanzania), Gift Shoko (kulia) akibadilishana mawazo na  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla pamoja na mteja wa CBA Benki.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUTARISHA NA KUTOA VYETI VYA SHUKRANI KWA WADAU WA MAZINGIRA

$
0
0
Viongozi na Waumini ya Dini ya Kiislam mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye sala ya magharibi wakati Iftar maalum iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.
 Raia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wakisoma Qasida kwenye Iftar maalum iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti cha shukrani Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Bw. Ruge Mutahaba kwa ushiriki na ufanikishaji wa maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa ilifanyika Butiama.
Wengine waliopokea vyeti hivyo ni TBC, Lake Gas, TBL, WWF na ZANTAS.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti cha shukrani Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL,Roberto Jarrin  kwa ushiriki na ufanikishaji wa maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa ilifanyika Butiama.
Wengine waliopokea vyeti hivyo ni TBC, Lake Gas, Clouds Media, WWF na ZANTAS.
Ndugu, Jamaa, Marafiki na Wadau kutoka sekta mbali mbali wakipata futari kwenye Iftar maalum iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amejumuika na waumini wa dini ya Kiislamu,wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam, viongozi mbalimbali wa Serikali na wa vyama vya siasa katika halfa ya futari aliyoiandaa katika makazi yake Oysterbay Jijini Dar es Salaam.


Katika Hafla hiyo ya futari, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan alishiriki katika utoaji wa vyeti kwa wadau wa mazingira ambao walishiriki kikamilifu katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani iliyofanyika Kitaifa tarehe 4-June-2017 - Butiama mkoani Mara.


Baadhi ya taasisi zilizopatiwa vyeti na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ni Shirika la Utangazaji Tanzania- TBC, Clouds Media, Lake Gas limited, Tbl, Zantas Air na WWF.

Akizungumza kwa Niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan katika hafla hiyo ya futari, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba alimshukuru Makamu wa Rais kwa kuanda futari hiyo katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwani amesema ni jambo zuri na linalompendeza Mwenyezi Mungu.

Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images