Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1274 | 1275 | (Page 1276) | 1277 | 1278 | .... | 1898 | newer

  0 0  0 0

  Mmoja kati ya Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe akiuliza swali wakati wa kikao kazi na Naibu Katibu Mkuu-Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. #wikiyautumishi 2017
  Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri Kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw.Micky Kiliba,akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kiutumishi yaliyojitokeza katika kikao kazi na Watumishi wa Umma. #wikiyautumishi 2017
  Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri Kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw.Micky Kiliba,akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kiutumishi yaliyojitokeza katika kikao hicho. #wikiyautumishi2017
  Mkurugenzi Idara ya Ukuzaji Maadili Ofisi ya Rais,UTUMISHI Bw. Mathew Kirama akitoa mada kuhusu maadili katika Utumishi wa Umma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. #wikiyautumishi 2017
  Mmoja wa Watumishi wa Umma kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songwe akiuliza swali wakati wa kikao kazi cha Wiki ya Utumishi wa Umma na viongozi wa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. #wikiyautumishi 2017
  Viongozi na Watumishi wa Umma wa Halmshauri ya Wiaya ya Songwe waliohudhuria kikao hicho.#wikiyautumishi 2017

  0 0

  Meneja Miradi kutoka Social Action Trust Fund (SATF) Rogasian Massue akimkabidhi leo mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto watano.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimshukuru Meneja Miradi kutoka Social Action Trust Fund (SATF) Rogasian Massue mara baada ya kumkabidhi leo mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto watano.
  Meneja Miradi kutoka Social Action Trust Fund (SATF) Rogasian Massue akimsalimia mtoto Goodluck Msele ambaye amefanyiwa upasuaji wa moyo hivi karibuni katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na hali yake inaendelea vizuri. SATF imechangia shilingi milioni 10 fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto watano.
  Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa Watoto na Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau (katikati) akimwelezea Meneja Miradi kutoka Social Action Trust Fund (SATF) Rogasian Massue (kushoto) kuhusu aina mbalimbali za magonjwa ya moyo yanayowasumbua watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Kulia ni Msimamizi wa Wodi ya watoto Afisa Muuguzi Rogers Kibula.
  Meneja Miradi kutoka Social Action Trust Fund (SATF) Rogasian Massue akimsikiliza Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa Watoto na Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau wakati akimuelezea jinsi upasuaji wa moyo unavyofanyika katika Taasisi hiyo.Picha na JKCI

  0 0

   Prof. Kabudi akiwa na bibi Zaman balsa ya kumaliza mazungumzo ya yaliyofanyika ofisini kwake mjini Dodoma 

  ……………….

  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amemkutana na Mwakilishi mkazi WA Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto duniani-UNICEF bibi Maniza Zaman ofisini kwake mjini Dodoma. 

  Katika kikao hicho viongozi hao mbali na kufahamiana pia wamejadili namna ya kuboresha mahusiano baina ya Wizara na UNICEF .

  Katika maongezi hayo Bi. Zaman aliishukuru Wizara na taasisi zake kwa ushirikiano inayowapa UNICEF katika programu mbalimbali inazoshirikiana na Wizara.

  UNICEF inatekeleza kwa kushirikiana na Wizara katika maeneo ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano na kuwapa vyeti vya kuzaliwa, huduma ya msaada wa kisheria na mkakati wa haki mtoto.

  0 0

  Imeelezwa kuwa sababu kubwa inayochangia watoto kuendelea kunyanyaswa na kufanyiwa vitendo vya kikatili katika maeneo ya kanda ya ziwa ni jamii kukosa elimu kuhusu haki za watoto pamoja na kukosekana kwa ushirikiano pale kesi zinazopelekwa katika vyombo vya sheria.

  Hayo yamesemwa leo June 16,2017 na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Viwanja vya Shycom Mjini Shinyanga.

  Matiro alisema tatizo kubwa linalotokea wakati wa kutetea haki za watoto wanapofanyiwa ukatili ni kukosekana kwa ushirikiano wa jamii na wazazi pale kesi inapofika katika vyombo vya sheria ikiwemo mahakamani hivyo kusababisha kesi nyingi kufutika matokeo yake watoto wanaendelea kunyanyasika.

  “Naomba tuweke mkazo zaidi katika elimu kwa jamii kuhusu haki za watoto,jamii ikibadilika tunaweza kumaliza tatizo la unyanyasaji wa watoto,wazazi wakielimika watajitokeza katika vyombo vya sheria kutoa ushahidi kwa vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watoto wao”,alieleza Matiro.

  “Haki za watoto zinadidimizwaa sana kanda ya ziwa hasa mkoani Shinyanga kutokana na jamii kukosa elimu na kung’ang’ania mila na desturi zinazomgandamiza mtoto hususani mtoto wa kike hivyo mashirika na serikali tushirikiane kubadilisha fikra za jamii,wananchi wajue haki za watoto na wazilinde”,aliongeza Matiro.

  “Bado kuna mambo yanawanyima haki watoto,watoto wanabakwa,wanafukuzwa,wanalawitiwa na wengine hawapelekwi shule,yote haya yanatokea kwa sababu watu hawana udhubutu wa kutoa ushahidi kwenye vyombo vya sheria”,alieleza.

  Katika hatua nyingine aliwataka watoto kutambua haki zao na wawe wanashirikishwa katika mambo yanayowahusu badala ya wazazi pekee kujiamlia.

  “Tunaposema haki ya mtoto tunataka kwanza watoto wazijue haki zao,haki ya kuthaminiwa,kupata elimu,malezi,kutambulika lakini pia kushirikishwa,yapo mambo yanafanyika katika jamii zetu yanafanywa kinyume na haki za watoto,jamii yetu inatakiwa kutambua na kuziheshimu haki za watoto”,alisema Matiro.

  “Ni jukumu letu kumlinda mtoto,kutoa ushirikiano kwa vyombo vya sheria na serikali lakini pia kwa kuwa watoto ni taifa la kesho,tunapaswa kuwafundisha stadi za kazi,kuwafundisha haki zao”,alisema Matiro.

  MSIKILIZE HAPO CHINI MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA AKIZUNGUMZA WAKATI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA
  ANGALIA PICHA MATUKIO MBALIMBALI YALIYOJIRI WAKATI WA MAADHIMISHO HAYO
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Viwanja vya Shycom Mjini Shinyanga.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ambapo aliwataka watoto kusoma kwa bidii kwani elimu ni mkombozi wa maisha yao
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na watoto waliopo katika kituo cha huduma ya watoto Shirika la Compassion katika kanisa la KKKT Shinyanga
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia masweta na nguo mbalimbali zilizotengenezwa na watoto hao
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia kazi za watoto hao
  Hata mikate wanatengeneza.......
  Mtoa huduma katika kituo cha huduma ya mtoto Compassion katika kanisa la KKKT Clara Charo,akisoma risala
  Mwinjilisti Elisha Shayo akizungumza kwa niaba ya uongozi wa kanisa la KKKT mjini Shinyanga
  Watoto wakicheza wakati wa maadhimisho ya Mtoto wa Afrika June 16,2017
  Watoto wakicheza
  Meneja wa Benki ya CRDB Shinyanga,Said Pamui akizungumza wakati wa maadhimisho hayo
  Kiongozi wa shirika la Compassion akizungumza
  Zawadi ya jezi kwa watoto walioshiriki michezo wakati wa maadhimisho hayo
  Mtoto akipokea zawadi ya saa
  Maofisa wa Benki ya CRDB wakifungua akaunti kwa ajili ya mtoto Picha zote na Moses Kiamani - Malunde1 blog

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Bilinith Mahenge ametoa shilingi milioni tatu, ili kusaidia kikundi cha watu wenye ulemavu wa ngozi na macho albino cha wilaya ya songea, kwa ajili ya kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku wa nyama. Akikabidhi kiasi hicho cha fedha mkuu wa mkoa amewaka wanakikundi hao kutimiza malengo ili waweze kuwasaidia hata watu wengine wenye matatizo mbalimbali.hbari kamili hii hapa video yake.

  0 0


  Mwakilishi kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Shomari Mchongoma (kushoto) akizungumza katika mkutano wa vyombo vya habari pamoja na viongozi wa dini kutoka BAKWATA, Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
  Ofisa Miradi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Godfrida Jola (kulia) ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo akizungumza katika mkutano wa vyombo vya habari ulioandaliwa na kushirikisha viongozi wa dini kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Kutoka kushoto ni Sheikh Shomari Mchongoma (BAKWATA), Bw. Lucas Singili (CCT), pamoja na Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose.
  Mwakilishi kutoka Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Bw. Lucas Singili (katikati) akizungumza katika mkutano wa pamoja na viongozi wa dini kutoka BAKWATA, CCT na Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Mkutano huo uliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA). Kulia ni Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose na Sheikh Shomari Mchongoma wa BAKWATA (kushoto).

  VIONGOZI wa Dini wamekemea vitendo vya ukatili kwa watoto na kwani vimekemewa hata katika vitabu vya dini, huku wakimtaka kila mmoja kumlinda mtoto pamoja na kueneza elimu ya malezi. Viongozi hao walioshiriki katika mkutano wa vyombo vya habari ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa pamoja waliungana na TAMWA kukemea vitendo vya kikatili wanaofanyiwa watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.

  Akizungumza Mwakilishi kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Shomari Mchongoma alisema jamii kwa pamoja inapaswa kuungana na kukemea vitendo vya kikatili kwani ni kinyume cha imani zetu. Alisema jambo pekee ambalo linaweza kufanikisha mapambano hayo ni jamii kumrudia mwenyezi Mungu na kukemea vitendo viovu anavyochukizwa navyo.

  “…Wakati umefika tuangalie ni namna gani kumkomboa mtoto wetu kwenye wimbi la mateso ya kikatili ambayo wamekuwa wakitendewa baadhi ya watoto wetu. Mtoto anaweza kuwa salama endapo tutaungana na kukemea vitendo hivyo bila kujali tofauti zetu,” alisema Sheikh Mchongoma.

  Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Bw. Lucas Singili alisema mtoto anaitaji malezi ya pamoja kwa ushirikiano ikiwa ni kuwaweka karibu ili waweze kukua katika malezi mema. Watoto hawapaswi kutengwa wala kufanyiwa vitendo vya kikatili zaidi ya kuwapa msaada kutoka kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla ili waweze kuwa raia wema wenye maadili katika taifa la baadaye.

  Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose (wa kwanza kulia) akizungumza katika mkutano wa pamoja na viongozi wa dini kutoka BAKWATA, CCT kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Mkutano huo uliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA). Wengine kushoto ni viongozi wa dini.
  Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose (kulia) akizungumza katika mkutano wa pamoja na viongozi wa dini kutoka BAKWATA, CCT kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Kulia ni Ofisa Miradi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Godfrida Jola akifuatilia mazungumzo hayo.
  Sehemu ya wanahabari na maofisa wa TAMWA wakiwa katika mkutano huo.

  Aidha aliongeza kuwa mtoto hapaswi kuchokozwa kwa nmna yoyote kama wanavyofanyiwa ukatili na mambo yasio mema na baadhi ya watu.Alisema hata vitabu vya dini vimekemea aina yoyote ya uchokozi dhidi ya watoto, hivyo kuiomba jamii kushirikiana katika kutoa elimu ya malezi mema kwa watoto waje kuwa raia wema na bora baadaye. “…Mtoto achokozwi, usimchokoze mtoto hata maandiko ya dini yanasema hivyo…,” alisisitiza Bw. Singili wa CCT.

  Naye Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose akizungumza na wanahabari katika mkutano huo, alisema yapo madhara makubwa yanayomtokea mtoto endapo akipitia katika vitendwa vya unyanyasaji. Alisema mtoto anapokumbana na vitendo vya unyanyasaji anapoteza matumaini kwa jamii, anapoteza imani, anajenga hofu na thamani yake inashuka hivyo kuishi katika maisha mabaya zaidi.

  Alieleza kuwa, mtoto anayefanyiwa vitendo vya kikatili asipo badilishwa huenda akawa mkatili zaidi hapo baadaye jambo ambalo tunaweza kujikuta tunaandaa taifa hatari, hivyo kumtaka kila mmoja katika nafasi yake kukemea vitendo vya kikatili dhidi yao ili kumlinda mtoto.

  0 0

  Na Baltazar Mashaka, Mwanza

  Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Mwanza Bw. Raymond Mwangwala amesema kuwa uchaguzi wa chama hicho wa mwaka huu umelenga kuwapata viongozi bora watakaokivusha kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2019 na Uchaguzi Mkuu wa 2020.

  Ameonya kuwa wana CCM watakaobainika kutumia rushwa ili wachaguliwe na watakaopokea rushwa hiyo wote watashughulikiwa kwa taratibu zilizowekwa.

  Bw. Mwangwala alitoa kauli hiyo juma hili wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, ambapo aliomba ushirikiano wa wanahabari hao katika utekelezaji wa majukumu yake.

  Alisema CCM mpya ya “hapa kazi tu” haitamchekea mtu yeyote mwenye kupanga kukiharibu chama hicho kwa namna anayotaka na haitakuwa tayari kupokea mamluki wanaojiunga nayo kwa maslahi binafsi badala ya wananchi na wana CCM.

  Katibu huyo alieleza kuwa ili wapatikane viongozi waadilifu watakaoinua mapato ya CCM na kukisaidia chama hicho tawala kwenye uchaguzi wa 2020, wanachama wenye sifa na uwezo wakachukue fomu ili wapigiwe kura kwani ndio watakaokifikisha kwenye uchaguzi huo na kukiwezesha kupata kura za ushindi za urais, ubunge na udiwani.

  Bw. Mwangwala alisisitiza kuwa watakaotumia rushwa hawatapitishwa kugombea nafasi wanazoomba kwani wanatakiwa viongozi wa kusimama na kuielezea CCM badala ya mamluki.

  Hata hivyo katibu huyo alisema chama hicho kinafanya uhakiki wa mali zake kuanzia ngazi ya matawi, wilaya hadi mkoa ili zitambulike na kufahamu mapato yake yalikuwa yanatumikaje.

  “Zipo mali watu walikuwa wakizutumia vibaya kutokana an mikataba mibovu iliyopo, watakaobainika kwenye zoezi la uahkiki watashughulikiwa na wapo waliodiriki kuziuza mali hizo na kuzigeuza shamba la bibi,
  “Tunataka tujue mali zetu zilipo na zingine zilizotelekezwa tuzijue na mapato yake yanatumikaje.Ifikapo Julai mwaka huu zote ziwe na hati,”alisema. 
  Katibu wa CCM wa Mkoa wa Mwanza Bw. Raymond Mwangwala akizungumza na wanahabari ofisini kwake katikati ya juma hili.

  0 0

   Mashabiki wakiwa ndani ya Dar Live.

  SIKU zikiwa zinahesabika kuelekea Usiku wa Nishushe Dar Live utakaofanyika Sikukuu ya Idd Mosi ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo MbagalaZakhem jijini Dar, wakali kibao watakaoliamsha dude siku hiyo wamefungukia makamuzi watakayotoa. 

  Katika usiku huo, pazia la burudani litafunguliwa rasmi mapema kuanzia saa 8:00 asubuhi ambapo burudani ya watoto itatolewa chini ya kundi la sarakasi na kudensi la Wakali Dancers pamoja na Kundi la Muziki wa Asili la Makhirikhiri kutoka Tanzania. Wakizungumza na Mikito Nusunusu kwa nyakati tofauti, wakali hao watakaoongozwa na R.O.M.A Mkatoliki walisema kuwa wataliamsha dude mwanzo mwisho sambamba na kutoa sapraizi kibao jukwaani.ROMA “Kwa muda mrefu sijafanya shoo tangu nipate matatizo hapa kati. Mara ya mwisho nilifanya shoo Dar Live nikiwa na Darassa ilikuwa Usiku wa Michano (Mkesha wa Mwaka Mpya) na waliofika waliona na ambao hawakufika walisimuliwa. Safari hii nisingependa ikupite hii. Nimepona na nipo fiti hivyo mje kwa wingi kushuhudia shoo yangu ya kwanza tangu mwaka huu uanze nikikinukisha kwa ngoma kali kuanzia Viva Roma Viva, K, Ivan, Kaa Tayari na nyingine kibao.”Darasa Mara ya mwisho kutinga Dar Live ilikuwa Mkesha wa Mwaka Mpya.
  [/caption] DARASA “Mara ya mwisho kutinga Dar Live ilikuwa Mkesha wa Mwaka Mpya nikiwa na ngoma ya Taifa ya Muziki. Safari hii nakanyaga tena jukwaa hilo Idd Mosi nikiwa na ngoma nyingine ambayo nayo ni habari nyingine ya Hasara Roho. Sina maneno mengi; ‘Dunia iweke tuzo za wachukiaji, Bongo kuna watu wana vipaji, Utarusha madongo kwenye maji, Bora upige michongo utanipa midadi.’ Mr Blue akiwapagawisha mashabiki wake.[/caption] MR BLUE “Sikukuu hii ya Idd Mosi sehemu pekee ya kijanja ni Dar Live tu! Nitaliamsha dude na ngoma zangu zote kali kama Pesa, Mboga Saba, Baki Na Mimi na nyingine kibao. Muhimu mashabiki wajitokeze kumuona Byser mpya najua mnajua muziki wangu jukwaani upoje. Haina kukata pumzi hiyo!”STAMINA “Sina maneno mengi ila jukwaa linaongea. Battle za jukwaani kama kawa, mashabiki wajiandae kumsikia na kumuona Stamina akiwa na ngoma kibao mpya ikiwemo Love Me na siku hiyo ni mperampera mwanzo mwisho hadi kuchee.” Snura Akifanya yake ndani ya Dar Live na wacheza shoo wake.[/caption]SNURA “Nina zawadi kibao za kuwapa mashabiki wangu Sikukuu ya Idd Mosi Dar Live. 
   
  Mbali na kuwaimbia nitawaonesha live staili ya kucheza nyimbo zangu zote kuanzia Ushaharibu, Majanga, Chura, Najidabua, Shindu hadi wa sasa huu wa Nionee Wivu nilioimba na Yamoto Band.” BAMBO “Nitaliamsha kuanzia asubuhi mpaka mida ya jogoo akitoka bandani. Mkongwe niliyebaki katika uchekeshaji Bongo nitakuwepo kufanya yangu kwa watoto na wakubwa wote watakaofika Sikukuu ya Idd Mosi Dar Live.” ZANZIBAR STARS Mmoja wa wanaounda Kundi la Zanzibar Stars, Sabaha Mchacho alisema; “Zanzibar Stars itazaliwa upyaaa Idd Mosi Dar Live. 
   
  Wapenda Muziki wa Mwambao hii si ya kukosa kwani tumewaandalia vibao vipya kabisaa kutoka kwa wakali wengi wakiwemo Bi. Mwanahawa, Jokha Kassim, Mosi Suleiman na Zubeda Mlamali MTONYO JE? Mratibu na Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo aliweka wazi kuwa licha ya uwepo wa wakali wengi, kiingilio kwa siku hiyo upande wa shoo ya kibabe itakayoanza saa 8:00 usiku kitakuwa kiduchu yaani shilingi 7,000 huku watoto kikiwa shilingi 3,000 tu na bonasi ndani yake ya kuteleza bure, kubembea bure, kupanda ndege bure, kuogelea bure na vingine vingi bureee. 

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  Diwani wa Kata ya Kivukoni, Henry Massaba ametoa pikipiki mbili kwa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kati zenye thamani ya sh. Milioni Tano ili ziweze kutumika kwa masuala ya usalama kwa wananchi wa kata hiyo Kivukoni.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi pikipiki hizo , Massamba amesema kuwa kumeibuka wizi wa kutumia pikipiki hivyo hata polisi wanatakiwa kutumia pikipiki kwa ajili ya kuwakimbiza wahalifu hao.

  Massamba amesema kuwa wahalifu wamekuwa na njia tofauti za kufanya uhalifu na kuamua kutumia pikipipiki kwa kutambua hawawezi kukamatwa kutokana na polisi kwa muda mwingi wanatumia magari.

  Aidha amesema kuwa ataendelea kushirikiana na jeshi la polisi kwa namna juu ya kuhamasisha masuala ya ulinzi ili wananachi waishi kwa amani pamoja na mali zao.

  Nae Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kati , Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Amon Kakwale amesema kuwa msaada huo ni mkubwa na kuwataka watu wengine waendelee kuliunga mkono jeshi la polisi.

  Kakwale amesema kuwa Diwani wa Kata ya Kivukoni amejitoa kwa ajili ya wananchi kuweza kupata usalama.
  Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kati , Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Amon Kakwale akizungumza wakati hafla ya kukabidhiwa pikipiki mbili zilizotolewa na Diwani wa Kata ya Kivukoni leo jijini Dar es Salaam.
  Diwani wa Kata ya Kivukoni, Henry Massaba akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi pikipiki kwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kati katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Diwani wa Kata ya Kivukoni, Henry Massaba akikabidhi msaada wa Pikipiki Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kati Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Amon Kakwale katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu Polisi wa Wilaya ya Kati pamoja na wananchi wa kata ya kivukoni wakiwa katika hafla ya kukabidhiana Pikipiki iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

  Jumuiya ya Kuhifadhi Qur-an Tanzania imeandaa  mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur-an yanayotarajia kufanyika kesho siku ya Jumapili katika ukumbi wa Diamond Jubilee,ambapo Mgeni rasmi anatarajai kuwa Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddy. 

  Akizungumza mbele ya Waandishi wa habari,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhi Qur-an Tanzania Sheikh Othman Ally Kaporo amesema kuwa jumuiya hiyo imetenga kiasi cha dola za kimarekani elfu 25 kwa ajili ya washindi watakaoibuka kwenye mashindano hayo.

  Sheikh Kaporo amesema kuwa mashindano hayo ya sita Kimataifa tangu waanze kuratibu, yanatarajia kuzishirikisha nchi 18 ambazo ni Kenya, Uganda, Mali, Nigeria, Algeria, South Africa, Bangladesh, Sudan, Kuwait, Libya, Djibouti, UAE, Russia Federation, USA, Yemen, UK, Dubai, Tanzania Bara na Visiwani (Zanzibar). Muhamedi Saidi 

  Amesema kuwa matarajio yao yalikuwa ni ushiriki wa nchi 35 lakini baadhi yao ziliomba udhuru wa kutohudhuria kutokana na sababu zilizonje ya uwezo wao.

  Sheikh Kaporo amesema mgeni wa heshima katika mashindano hayo atakuwa Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddy akiambatana na mlezi wa Jumuiya hiyo Alhaj Ally Hassan Mwinyi Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Sheikh Kaporo ametoa wito kwa watanzania kuhudhuria mashindano hayo na kujitokeza kwa wingi ukizingatia huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo katika kumi la mwisho iliteremka Qur-an tukufu hivyo ni vyema wakahudhuria ili waweze kupata ujira kutoka kwa mola wao (Allah).

  Mshiriki wa Tanzania Omary Abdallah Salum, ambaye amewaomba watanzania kuwaombea dua kwa wingi ili waweze kupata ushindi.
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Tanzania, Sheikh Othman Ally Kaporo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam,kuhusiana na  mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur-an ambayo yanayotaraji kufanyika siku ya Jumapili katika ukumbi wa Diamond Jubilee. kulia ni Katibu wa Kamati ya maandalizi ya mashindano hayo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya fursa za ajira kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kati ya Tanzania na China ambapo makampuni ya China yatatoa ajira kwa wasomi wa Tanzania . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Baadhi ya vijana wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakizungumzwaa kwenye ufunguzi wa awamu ya pili ya fursa za ajira kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kati ya Tanzania na China ambapo makampuni ya China yatatoa ajira kwa wasomi wa Tanzani, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi. 
  Sehemu ya Vijana waliojitokeza kwenye ufunguzi wa awamu ya pili ya fursa za ajira kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kati ya Tanzania na China ambapo makampuni ya China yatatoa ajira kwa wasomi wa Tanzani, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya fursa za ajira kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kati ya Tanzania na China ambapo makampuni ya China yatatoa ajira kwa wasomi wa Tanzania . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Balozi wa China nchini Dkt.Lu Youqing akizungumza kwenye ufunguzi wa awamu ya pili ya fursa za ajira kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kati ya Tanzania na China ambapo makampuni ya China yatatoa ajira kwa wasomi wa Tanzani, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi.
  Sehemu ya Vijana waliojitokeza kwenye ufunguzi wa awamu ya pili ya fursa za ajira kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kati ya Tanzania na China ambapo makampuni ya China yatatoa ajira kwa wasomi wa Tanzani, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na balozi wa China nchini Dkt.Lu Youqing ,MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala na viongozi wengine wa Serikali na wa Chama cha Wafanyabiashara wa China nchini Tazania mara baada ya ufunguzi wa awamu ya pili ya fursa za ajira  kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kati ya Tanzania na China ambapo makampuni ya China yatatoa ajira kwa wasomi wa Tanzania.

  0 0

  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala (wa tano kushoto) akipokea karatasi yenye orodha ya Vifaa vya kutolea huduma za Afya kutoka kwa Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyvestry Koka (kushoto kwake) wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo vyenye thamani zaidi ya Sh. milioni 400 iliyofanyika kwenye Kituo cha Afya Mkoani, mjini Kibaha, leo mchana. Kulia kwa Waziri ni MKuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumta Mshama. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO).
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, akikagua sehemu ya vifaa hivyo wakati akikabidhiwa na Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyvestry Koka (kulia kwake).
  Mbunge wa Kibaha mjini, Silyvestry Koka, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa vya kutolea huduma za Afya, iliyofanyika kwenye Kituo cha Afya cha Mkoani mjini Kibaha. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mjini, Asumta Mshama.


  Akizungumza katika hafla hiyo, Mbunge Koka, alisema kuwa alifanikiwa kupata msaada wa vifaa hivyo kutoka kwa rafiki zake waishio nchini Marekani, wakati alipokwenda katika shughuli zake za kibiashara, ambapo walimhakikishia kupata vifaa hivyo kwa kuchangia gharama za usafirishaji hadi kuingia nchini.

  Baada ya uhakika huo Koke alitumia gharama zake kuwasafirisha baadhi ya wataalamu (Wazungu) kutoka nchini Marekani na kuja nchini hadi Mji wa Kibaha kwa lengo la kukagua na kujiridhisha juu ya uhitaji wa vifaa hivyo vya kutolea huduma za afya, ambapo alitumia jumla ya Sh. milioni 12.

  Aidha alisema kuwa vifaa hivyo vilichelewa kutokana na uhitaji kutoka mataifa mengine yaliyokuwa yakipata matatizo na magonjwa ya mlipuko, na hivyo kampuni hiyo ya Project Cure, kulazimika kughairisha kusafirisha kuja nchini na kutoa kipaumbele kwa mataifa hayo yaliyokuwa yakipata matatizo kwanza.

  Mbali na Mbunge kuchangia kiasi cha Sh. milioni 12, pia Halmashauri ya Mji wa Kibaha pia ilichangia kiasi cha Sh milioni 32, zilizosaidia kusafirisha vifaa hivyo kutoka nchini Marekani hadi kuwasili nchini. Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa hii leo vina thamani ya zaidi ya Sh. milioni 400.

  Sehemu ya vifaa hivyo.

  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyvestry Koka, wakitoka kutembelea katika Wodi ya Wazazi, katika Kituo cha Afya Mkoani, leo mchana wakati alipofika kukabidhi Vifaa vya kutolea huduma za Afya vyenye thamani ya zaidi ya Sh.milioni 400. 
  NAIBU Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mfanyakazi wa Chumba cha Maabala cha Kituo cha Afya Mkoani, Farida Chagulaga, wakati waziri huyo alipotembelea chumba hicho na kukagua taratibu za ufanyaji kazi, alipofika kwa ajili ya kukabidhi vifaa vya kutolea huduma za afya.
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mfanyakazi wa Chumba cha Maabala cha Kituo cha Afya Mkoani, Farida Chagulaga, wakati waziri huyo alipotembelea chumba hicho na kukagua taratibu za ufanyaji kazi, alipofika kwa ajili ya kukabidhi vifaa vya kutolea huduma za afya.
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala (wa pili kushoto) Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyvestry Koka (kushoto kwake) Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumta Mshama (kushoto) wakikabidhi karatasi ya orodha ya vifaa vya kuhudumia wagonjwa kwa Madaktari wa Kituo cha Afya cha Mkoani mjini Kibaha, wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 400.
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala (wa tatu kulia) Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyvestry Koka (kulia kwake) Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumta Mshama (wa pili kulia) na baadhi ya waganga wa Kituo cha Afya cha Mkoani Kibaha, wakikagua badhi ya Vitanda vya wagonjwa, baada ya makabidhiano ya vifaa hivyo vya kutolea huduma kwa wagonjwa vyenye thamani zaidi ya Sh. milioni 400. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Kituo cha Afya Mkoani, mjini Kibaha.
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, akiimba wimbo maalumu kwa pamoja na Mkuu wa Wilaya Asumta Mshama (kulia), Mbunge wa Kibaha mjini, Silyvestry Koka, alipokuwa akizungumza na wananchi wa mji wa Kibaha, Wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Mkoani (hawapo pichani) wakati wa hafla ya makabidhiano ya Vifaa vya kutolea huduma za afya kituoni hapo
  Dkt. Kigwangala, akizungumza wakati wa hafla hiyo.....
  Baadhi ya wananchi wakimsangilia mgeni rasmi wakati akitoa hotuba yake katika hafla hiyo.
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wa mji wa Kibaha baada ya hafla hiyo. 
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, akiagana na baadhi ya wanachi waliohudhuria hafla hiyo.
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, akiagana na baadhi ya wanachi waliohudhuria hafla hiyo.
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, akiagana na baadhi ya wanachi waliohudhuria hafla hiyo.
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, akiagana na Diwani Selina.  Wasanii wa Kikundi cha Malaika Dance, cha Kibaha wakitoa burudani katika hafla hiyo

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza na Waandishi wa Habari na kuwatahadharisha wale wote ambao wamekua wakichochea migogoro ya Ardhi katika Mtaa wa Mbondole kwa Muhaya eneo la Msongola jijini Dar es Salaam.

  Mkuu wa Wilaya amesema atawachukulia hatua za kisheria wale wote wanaotoa taharifa za uongo kuwa hukumu ya kubomolewa eneo hilo limetoka hivyo watu hao wanatakiwa waondoke wakati hukumu hiyo inataraji kutoka tarehe 28 June 2017.

  aidha ametoa wito kwa wakazi wa Mbondole kuwa wapole na kuacha kufata maneno ya Matapeli ambao wamekuwa wakiwadanganya kuwa eneo hilo hukumu imetoka na kutaja kuwa mtu anayewatisha wanatakiwa wamwambie awaonyeshe hukumu iliyo tayari hivyo kama ana hukumu wamlete ofisini kwake hili taratibu za kisheria zifuatwe.
  Sehemu ya mji Mbondole kwa Muhaya ambayo mtu mmoja amejitokeza na kusema eneo hilo lake na kuwadanganya kuwa hukumu ya mahakama imetoka hivyo wanatakiwa waondoke
  Wananchi wa Mbondole wakiwa wameshika mabango na kuandamana kupinga kubomolewa nyumba zao mara baada ya kutolewa taharifa ya uongo kuwa hukumu ya kubomolewa imetoka

  Wakazi wa Mbondole wakiwa wameshika bango kuandamana kupinga kubomolewa nyumba zao mara baada ya kutolewa taarifa ya uongo kuwa hukumu ya kubomolewa imetoka mahakamni hivyo waondoke eneo hilo
  Sehemu ya Wananchi wa Mbondole ambao walikusanyika na kuandamana kupinga kubomolewa nyumba zao mara baada ya kutolewa taharifa ya uongo kuwa hukumu ya kubomolewa imetoka mahakamani hili waondoke katika eneo hilo

  0 0

  Mtaalamu wa masomo ya Sayansi, Fadhil Leonard akiwaelekeza wanafunzi wa Shule ya Msingi namna ya kutengeneza gari linalojiendesha bila ya kuwa na dereva wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Sayansi Afrika Tanzania iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Al-Murtaza Upanga jijini Dar es Salaam leo. 
  Mtaalamu wa masomo ya Sayansi kutoka Shule ya Ilboru Arusha, Vedasto Biyaka akiwaelekeza wanafunzi wa Shule ya Msingi namna ya kutengeneza magari hayo.
  Wanafunzi wakipata maelekezo ya kutengeneza magari hayo kutoka kwa mtaalamu wa masomo ya sayansi, Gibson Kawago kutoka Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT)
  Mtaalamu wa masomo ya Sayansi kutoka Shule ya Ilboru Arusha, Vedasto Biyaka akiwaelekeza wanafunzi wa Shule ya Msingi namna ya kutengeneza magari hayo.
  Wanafunzi wakiendelea kujifunza kutengeneza magari hayo.
  Balozi wa NEF, Aneth David ambaye ni mwanataaluma wa sayansi na mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akizungumza na wanahabari kuhusu kongamano hilo.
  Wanafunzi wakielekezwa jambo kwenye hafla hiyo.   Na Dotto Mwaibale

  KONGAMANO la Next Einsten (NEF) ambalo ni mpango wa Taasisi ya kuendeleza Hisabati na Sayansi Afrika (AIMS) kwa kushirikiana na Taasisi ya Robert Bosch Stiftung leo imetangaza uzinduzi wa wiki ya sayansi Afrika kupitia kongamano la NEF jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza katika uzinduzi wa kongamano hilo jijini Dar es Salaam jana, Balozi wa NEF, Aneth David ambaye ni mwanataaluma wa sayansi na mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alisema kongamano hilo wanataaluma wa ndani, mabingwa wa sayansi na teknolojia wataongoza kwenye tukio hilo.

  "Kongamano la Next Einsten la wiki ya sayansi Afrika ni wiki la kwanza la sayansi kuratibiwa ndani ya Afrika" alisema David.

  Alisema lengo la msingi la kongamano hilo ni kuendeleza wanasayansi na wanateknolojia wa kesho kwa kuwahusisha watoto na vijana katika shughuli za kisayansi kama vile kujumuika pamoja na kushiriki maonesho.

  "Shughuli zetu pia zitaonesha matokeo chanya ya sayansi kwa jamii nzima kwa kuwakutanisha wadau muhimu kutoka sekta zote na kuchochea uwekezaji katika tafiti na maendeleo pamoja na kujadiliana njia nzuri za kuwavutia na kuendeleza vijana hususan wasichana na wanawake katika nyanja ya sayansi" alisema Rais wa AIMS ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa NEF, Thierry Zomahoun.

  Alisema wiki ya Sayansi Afrika inayofanyika hapa nchini itashuhudia vipindi vya kusisimua kama vile kuhusisha wanafunzi katika kujifunza kwa vitendo somo la kemia, Teknolojia na Uhandi kwa kutumia vifaa shirikishi vya sayansi ambapo pia wanafunzi watashiriki katika shughuli za vitendo na mashindano ya miradi ya sayansi na baadaye kufuatia na sherehe ya kutoa tuzo kwa washindi.

  Kongamano hilo linafanyika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Seminari ya Al-Murtaza Upanga jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Nchi yetu. Nyumba zetu. Mustakabali wetu. Hii lazima iwe kauli mbiu yetu leo - hasa katika mapambano dhidi ya kuenea kwa jangwa. Mchango wa mabadiliko ya mazingira katika uhamiaji na makazi ya watu uko wazi duniani kote. Idadi kubwa ya 'wakimbizi wa mazingira' sasa huwasilishwa kama moja ya matokeo makubwa ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuenea kwa jangwa. 

  Na hili hii inategemewa kundelea kuongezeka. Kufikia 2030, Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Kuenea kwa Jangwa imeonya kuwa, kufikia mwaka 2030 watu wapatao milioni 135 wako katika hatari ya kuhama makazi yao kwa sababu ya kuenea kwa jangwa, na watu milioni 60 wanatarajiwa kuhama kutoka Kusini mwa jangwa la Sahara kuelekea Afrika ya Kaskazini na Ulaya. 

  Utabiri huu unaonyesha kuwa sehemu zilizo kame na zile zilizo kame zaidi huathirika zaidi na kuenea kwa jangwa na kuhama kwa watu. Watu wanaokaa vijijini amabao hutegemea ufugaji wa wanyama, kilimo na maliasili watakuwa katika hatari zaidi ya kuwa wahanga wa athari hizo, ambazo hujumuisha umaskini, kudorora kwa elimu, ukosefu wa uwekezaji, umbali kutoka huduma muhimu, na kutengwa.

   Ni lazima tukabiliane na hali hii na hii inamaanisha kufanya kazi katika ngazi mbili: Kwanza, ni lazima tusimamie ardhi kwa usahihi,hii ni muhimu katika kuzuia kuenea kwa jangwa na katika kulinda kiwango chake cha uzalishaji. Hifadhi ya Bayongahewa ya Las Bardenas Reales ya UNESCO iliyoko nchini Hispania inaonyesha kwamba usimamizi wa ardhi kame unaotumia taarifa sahihi, kwa kuzingatia kupishana kati ya matumizi ya malisho, ukulima na vipindi ya bila ya kuilima ardhi hupelekea si tu kusitisha kuwepo hali ya kuenea kwa jangwa lakini pia huleta uwezekano wa kurejesha ardhi kama ilivyokua awali. 

  Hii ndio sababu Programu ya Kimataifa ya UNESCO ya Nishati-Maji imejikita katika kujenga uwezo na kutoa mwongozo wa sera na zana za kushughulikia ukame, kuenea kw jangwa na changamoto zinazotikana na hayo, hasa kuhusiana na usimamizi wa rasilimali maji, kwa njia ya Mtandao wa Kimataifa unaohusika na Maji na Maendeleo ya Taarifa ya Ardhi Kame (G- WADI). 
   
  Pili, inatupasa kuimarisha ustahimilivu wa watu walio katika mazingira hatarishi kwa kuwawezesha kuwa na njia mbadala za kujipatia kipato ili tuweze kuuharibu mduara wa kuenea kwa jangwa na madhara yake ya kijamii na kiuchumi ambayo mara nyingi husababisha watu kuyahama makazi yao. Katika kutafuta na kuendeleza elimu na kujenga uwezo katika sayansi, teknolojia na uhandisi, kwa wasichana na wavulana katika nchi zilizo katika hatari zaidi, 

  Programu ya Sayansi ya Msingi ya Kimataifa ya UNESCO inafanya kazi ya kujenga fursa mpya za ajira kwa vijana, kupunguza utegemezi wa rasilimali zinazotegema hali ya hewa, ili kuwapatia watu maisha yenye ustahimivu katika makazi yao. Katika siku hii, ni lazima tutambue kuwa hali ya kuenea kwa jangwa ni jambo la kimataifa ambalo linalomtishia kila mtu na ni lazima lishughulikiwe kwa pamoja ili kujenga mustakabali endelevu na imara kwa wote. Ujumbe kutoka kwa Bi. Irina Bokova, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO katika Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Kuenea kwa Jangwa na Ukame Duniani, 17 Juni 2017

  0 0

  NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

  NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar , Abdulla Juma Saadalla “ Mabodi” amesema CCM itaendelea kufanya ushindani wa sera za maendeleo zitakazowanufaisha wananchi wa makundi yote mijini na vijijini.

  Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua Mafunzo ya Wanawake na Uongozi kwa wanachama na viongozi wa UWT Mkoa wa Mjini huko Amani Zanzibar, Dkt. Mabodi alisema wananchi wa visiwa vya Zanzibar kwa sasa wanachohitaji ni siasa za ushindani wa kisera katika kukuza kipato cha mwananchi mmoja mmoja hadi taifa kwa ujumla.

  Dkt. Mabodi alisema taifa lolote linalotamani kuendelea kiuchumi ni lazima wananchi wake wakubali kwa vitendo dhana ya siasa za ustaarabu katika kudumisha amani na utulivu wa nchi ili kufanya kazi za kujiongezea kipato na kukuza uchumi wa nchi.

  Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo alisema ushindi wa CCM katika chaguzi mbali mbali za dola unatokana na nguvu za Wanawake wa UWT katika kuunga mkono harakati mbali mbali za kisiasa hadi kuhakikisha chama kinaingia madarakani.

  “ kila mtu ndani ya Chama Chetu anajua na kutambua mchango wa Wanawake katika medali za kisiasa, wao ndio wamekuwa mstari wa mbele kwa kila kitu ikiwemo kujitokeza kwa wingi kupiga kura halali za kuiletea ushindi CCM.

  Pia nakuahidini kwamba nitaendelea kuwa nanyi bega kwa bega kwa lengo la kuimarisha chama na jumuiza zake sambamba na kuwaletea wananchi maendeleo ya kudumu.”, alisema Dkt. Mabodi.

  Kupitia Mkutano huo Dkt. Mabodi aliwasihi viongozi na watendaji wa Umoja wa Wanawake Tanzania kushuka ngazi za chini za uongozi hasa matawi na mashina kwa lengo la kuratibu changamoto zinazowakabili wananchi ili zitafutiwe ufumbuzi wa kudumu na serikali.

  Aliwapongeza viongozi wa UWT waliojitolea kuanzisha mafunzo ya uongozi kwa wanawake wenzao ili wapate ujuzi wa kufanya siasa za maendeleo zitakazowajengea ujasiri wa kujenga hoja imara zinazokubalika katika ulimwengu wa siasa za ushindani.

  Sambamba na hayo alimpongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Zanzibar Dkt. John Pombe Magufuli kwa juhudi zake za kulinda rasilimali za nchi hasa kuthibiti mianya ya usafirishaji wa Mchanga wa Madini unaosababisha upotevu wa fedha nyingi za umma.

  Akizungumzia Uchaguzi wa ngazi ya Wadi unaoendelea hivi sasa katika Chama na Jumuiya aliagiza kwamba kamati zinazosimamia zoezi hilo zifanye kazi ya ziada ya kuhakikisha wanapatikana viongozi safi wasiokuwa na sifa za usaliti.

  Mapema akizungumza katika Mkutano huo Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mjini, Bi. Waridi Juma Othman aliahidi kuwa wanawake hao watatumia vizuri mafunzo ya uongozi katika siasa kama muongozo wa kufanya kazi za kisiasa kwa ufanisi mkubwa.

  Akitoa neno la shukrani Mbunge wa Viti Maalum wanawake( MNEC), Khadija Hassan Aboud alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanawake wa CCM ili waweze kuzitumika vizuri fursa za uongozi zinazopatikana ndani ya chama na serikali kwa ujumla.

  Mafunzo hayo ya siku moja yameandaliwa na Mbunge wa Viti Maalum wanawake( MNEC), Khadija Hassan Aboud kwa kushirikiana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini, Faharia Shomari Shomari Khamis.

  0 0  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito E. Mwinuka (katikati), akiongozana na  Meneja wa mradi wa upanuzi wa Kinyerezi I, Mhandisi   Simon Jilima,(kushoto) na Meneja Mwandamizi wa Miradi wa TANESCO, Mhandisi Gregory Chegere, wakitembelea kukagua maendeleao ya ujenzi wa mradi wa Kinyerezi II na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I jijini Dar es Salaam, leo Juni 17, 2017.

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
  SHIRIKA la Umeme Nchini, (TANESCO), limewahakikishia watanzania kuwa mradi wa umeme wa gesi wa Kinyerezi II unaendelea kwa kasi kubwa na utakamilika kama ilivyopangwa.

  Hakikisho hilo limetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito E. Mwinuka, wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi wa umeme wa gesi wa Kinyerezi II jijini Dar es Salaam, ambao unatarajiwa kutoa Megawati 240 za umeme.
  “Niwahakikishie watanzania kuwa ifikapo Agosti mwakani (2018), mradi wa umeme Kinyerezi II utakamilika na hivyo tutaongeza Megawati 240 kwenye gridi ya Taifa.” Alisema Dkt. Mwinuka wakati akitoa majumuisho ya ziara yake.
  Dkt. Mwinuka alifuatana na wakurugenzi watendaji wasaidizi, Mhandisi Abdallah O. Ikwasa, (anayeshughulikia Uzalishaji), Mhandisi Khalidi James, (anayeshughulikia uwekezaji miradi) na Mhandisi Kahitwa Bishaija (anayeshughulikia Usambazaji).
  Dkt. Mwinuka alisema watanzania wanahitaji umeme ulio wa uhakika na kwamba Serikali kupitia TANESCO imejipanga kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana kwa watanzania na hivyo kuchangia pato la taifa.

  “Kama mjuavyo serikali imefanya juhudi kubwa katika kuhakikisha Shirika linatekeleza miradi hii na tayari shilingi Bilioni 110 zimetolewa na serikali katika kutekeleza mradi huu wa Kinyerezi II.” Alifafanua Dkt. Mwinuka.

  Awali Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Stephens S.A.Manda, alisema, wataanza kuingiza umeme kwenye gridi ya taifa kila mwezi kuanzia Desemba mwaka huu 2017 ambapo Megawati 30 zitaingizwa kwenye gridi ya Taifa.

  “Tuna mashine 8 ambazo zitafua umeme huo kwa hiyo kuanzia Desemba Mosi mwaka huu, tutaingiza megawati 30 kwenye gridi ya taifa na tutafanya hivyo kila baada ya mwezi mmoja kwani tunaelewa kuwa serikali ambayo imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda, tunaona umeme ni hitajio muhimu kwa hivyo kila tutakapokamilisha mtambo mmoja tunaingiza umeme kwenye gridi ya taifa hatutasubiri kuwasha mitambo yote minane.” Alisema Mhandisi Manda.
  Mhandisi Manda alisema, mradi mzima ambao umeanza kutekelezwa rasmi Machi 3, 2016, utagharimu kiasi cha Dola za Kimarekani 344,059,746.00 kati ya hizo asilimia 15 zimetolewa na serikali.

  “ Kufikia leo Juni 17, 2017, asilimia 63 ya ujenzi wa mitambo imekamilika, na tunahakika ya kukamilisha ujenzi wa jumla kwa vile tayari mitambo yote inayohitajika imeshalipiwa na mingine iko njiani inaletwa nchini.” Alifafanua na kuongeza mitambo yote iliyoagizwa na TANESCO imo kwenye makontena 900 na tayari makontena 400 na ushee yamekwishawasili na baadhi ya mitambo imefungwa na tunatarajia mashine zingine kwenye hayo makontena yaliyosalia zitawasili nchini wakati wowote. Alisema.

  Akizungumzia kuhusu makontena 20 yaliyokuwa yamezuiliwa na TRA bandarini, Mhandisi Manda alisema, taarifa hizo hazina msingi wowote kwani kiasi hicho cha makontena 20 ni sehemu ya makontena 900 na tayari TANESCO imeshalipa fedha hizo za kodi na mizigo hiyo imefika site.

  Katika ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Mwinuka ;pia alitembelea mradi wa umeme wa upanuzi wa Kinyerezi II ambako nako ameridhishwa na kasi ya ujenzi wake. 
  Mradi huo ambao unasimamiwa na Mhandisi Simon Jilima, utawezesha ongezeko la megawati 35 na hivyo Kinyerezin I ambayo inatoa Megawati 150 itakuwa na uwezo wa kutoa Megawati 185 za umeme.
   Meneja wa Mradi Kinyerezi II, Mhandisi Stephens S.A.Manda
   Meneja wa mradi wa upanuzi Kinyerezi IMhandisi Simon Jilima
   DKT. Mwinuka, (kulia), Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James, (katikati) na Meenja Mradi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephen A.S.Manda, wakijadiliana jambo
   Mitambo ikiteremshwa eneo la ujenzi
   Mkurugenzi wa Business Times, Imma Mbuguni, (kulia) akizungumza jambo na Mhandisi, Khalid James
   Meneja Mwandamizi wa Miradi wa TANESCO, Mhandisi Gregory Chegere(kulia), akiteta jambo na Kaimu Meneja Uhisano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji
   Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji umeme (Generation), Mhandisi Abdallah O. Ikwasa(kulia), akimsikiliza Meneja Mwandamizi wa Miradi wa TANESCO, Mhandisi Gregory Chegere
   Mhariri Mtendaji wa Business Times, Bw. Imma Mbuguni, akizungumza ili kuoata ufafanuzi wa maswala kadhaa
   Baadhi ya mitambo ikiwa eneo la ujenzi ikisubiri kuunganishwa
   Mtandao wa nguzo za umeem ukiwa tayari kwa sehemu kubwa
   Kaimu Meenja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji akifafanua baadhi ya mambo kuhusu namna Shirika hilo linavyotekeleza sera ya kusaidia jamii (Corporate Social Responsibility), ambapo alisema, licha ya shirika imekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii sio tu kwenye maeneo ambako mradi unapita bali pia maeneo mengine na kutolea mfano wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera, kamati ya kikosi kazi cha kuokoa mazingira, na hata shule. Kushoto ni Dkt. Mwinuka na Mhandisi Khalid James
   Dkt. Mwinuka akiwa amezungukwa na wasidizi wake akizungumza kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Kinyerezi II
   Dkt. Mwinuka (kulia), akiongozana na wakandarasi toka kampuni ya kijapani SUMITOMO amabao ndio wanajenga mradi huo
  Dkt. Mwinuka (kushoto), Mhandisi Ikwasa(katikati) na Mhandisi Chegere

  0 0

  MAMBO yamezidi kunoga katika bahati nasibu ya ‘SMS’ ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’, baada ya mkulima kutoka wilayani Handeni, mkoani Tanga, Yahaya Ally Khamis, kuibuka kidedea kwa kuzoa Jumla ya Sh Milioni 20 kutoka kwenye bahati nasibu hiyo inayozidi kushika kasi nchini Tanzania, ikiwa ni droo yake ya 15 tangu kuanzishwa kwake.

  Bahati nasibu hiyo imechezeshwa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa kushirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein.

  Akizungumza katika droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba bahati nasibu yao imezidi kupanua mbawa zake kwa kutua wilayani Handeni, mkoani Tanga kwa mshindi wao Yahaya ambaye ana umri wa miaka 50 anayejishughulisha na kilimo.

  Alisema ni faraja yao kuona mchezo wao umekuwa ukitoa washindi katika sehemu mbalimbali za Tanzania, akiamini kuwa ni mwendelezo wa kuhakikisha kwamba kila mtu anaibuka na mamilioni ya Biko.

  “Tunafarijika sana kuona mkulima wa Handeni Tanga naye ameibuka na mamilionin ya Biko, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linaweza kumpatia utajiri mkubwa kwa kuzitumia fedha hizi kwa umakini katika shughuli zake za ukulima, ukizingatia kuwa amepatikana kwa kucheza Biko ambao ni mchezo rahisi kwa kuingiza namba ya kampuni 505050 na ile ya kumbukumbu ambayo ni 2456, huku kiasi cha kucheza kikianzia Sh 1000 na kuendelea.


  Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania, Humud Abdulhussein kushoto, akiagana na Balozi wa Biko, Kajala Masanja mara baada ya kumaliza kuchezesha droo ya 15 leo jijini Dar es Salaam, ambapo mkulima wa wilayani Handeni, mkoani Tanga, Yahaya Ally Khamis aliibuka kidedea kwa kuzoa jumla ya Sh Milioni 20.

  Balozi wa Biko Kajala Masanja akichezesha droo ya 15 ya Bahati Nasibu ya Biko ambayo donge nono la Sh Milioni 20 liliangukia kwa mkulima wa wilayani Handeni, mkoani Tanga, Yahaya Ally Khamis baada ya kuchezeshwa droo hiyo jana, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein.
  Kucheza mara nyingi zaidi ndio nafasi ya ushindi, hivyo tunawaomba Watanzania wacheze kwa wingi na mara nyingi zaidi kwa kupitia mitandao ya simu za mikononi ya Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo mbali na donge nono la Sh Milioni 20 linalotolewa kwa washindi Jumatano na Jumapili, pia tunatoa zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni 1,000,000 zinazolipwa kwenye simu za washindi walizotumia kuchezea bahati nasibu yetu,” Alisema Heaven.

  Akizungumza kwa simu saa chache baada ya kutangazwa mshindi, Khamis, alimshukuru Mungu kwa kumletea zawadi nzuri ya Sh Milioni 20 kwa kupitia mchezo wa Biko unaochezeshwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa mitandao ya simu ya Tigo, Vodacom na Airtel.

  “Namshukuru Mungu kwa kunipa zawadi hii kutoka Biko, nikiamini kuwa fedha hizi zitanipatia mafanikio makubwa kwa kupitia biashara zangu za kilimo ninazoshughulika nazo,” Alisema Khamis. Naye mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdulhussein, aliupongeza mchezo wa Biko na kuongeza kuwa unachezeshwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zote.

  0 0

  Mh. Balozi George Kahema Madafa katika tukio la kukabidhi hati za utambulisho kwa Rais Wa Jamhuri ya Italia Mh. Sergio Mattarella kwenye Ikulu ya Rais jijini Roma hapo hivi karibuni. Mh. Balozi Madafa aliambatana na maafisa wawili wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia pamoja na mkewe Bi. Esther Bhoke Madafa.
  Mh. Balozi George Kahema Madafa akikabidhi hati za utambulisho kwa Rais Wa Jamhuri ya Italia Mh. Sergio Mattarella kwenye Ikulu ya Rais jijini Roma hapo hivi karibuni. Mh. Balozi Madafa aliambatana na maafisa wawili wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia pamoja na mkewe Bi. Esther Bhoke Madafa.
  Mh. Balozi George Kahema Madafa akizungumza jambo na  Rais Wa Jamhuri ya Italia Mh. Sergio Mattarella kwenye Ikulu ya Rais jijini Roma hapo hivi karibuni mara baada ya kabidhi hati za utambulisho.
  Baadhi ya  maafisa wawili wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia pamoja na mkewe Bi. Esther Bhoke Madafa wakisalimiana na  Rais Wa Jamhuri ya Italia Mh. Sergio Mattarella kwenye Ikulu ya Rais jijini Roma.

older | 1 | .... | 1274 | 1275 | (Page 1276) | 1277 | 1278 | .... | 1898 | newer