Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1261 | 1262 | (Page 1263) | 1264 | 1265 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Balozi wa Samsung,Latifa Ally akitoa elimu kwa mteja kuhusu stika mbili zinazohusishwa na kampeni ya Samsung inayotarajiwa kuanza hivi karibuni stika hizo inayolenga kutokomeza bidhaa feki nchini.
  Mabalozi wa Samsung wakitoa burudani na kutoa elimu kwa wateja juu ya stika mbili zinazohusishwa na kampeni ya Samsung katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
  Mabalozi wa Samsung wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0

  NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

  KATIBU wa NEC, Idara ya Organazesheni ya CCM Taifa, Nd. Pereira Ame Silima amewataka viongozi na watendaji wanaochaguliwa kwenye uchaguzi wa chama na jumuiya zake kwa sasa kuwa na fikra na mitizamo mipya itakayoongeza ufanisi wa kiutendaji ndani ya CCM.

  Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na Wajumbe wa Kamati za siasa za Mikoa ya CCM Mjini na Magharibi pamoja na wajumbe wa sekreterieti na kamati Tekelezaji za jumuiya za Chama hicho huko Amani Unguja, alisema chama hicho kitaendelea kuwa imara kutokana na utamaduni wa kupata viongozi kwa njia za kidemokrasia hasa Uchaguzi huru na wa haki.

  Alisema lengo la ziara hiyo ni kuimarisha chama sambamba na kujitambulisha kwa viongozi hao kwani tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni Mjini Dodoma hiyo ndio ziara yake ya mwanzo.

  Alizitaka kamati mbali mbali zilizopewa dhamana ya kusimamia na kuchuja viongozi katika uchaguzi wa chama hicho kuhakikisha wanapatikana viongozi wenye nia ya kweli ya kuleta mabadiliko ya kiutendaji ndani ya chama hicho na sio wababaishaji.

  Aidha Katibu huyo alisema Chama hicho kina nia ya kuanzisha utaratibu wa kutengeneza kadi za uanachama zitakazokuwa katika mfumo wa kielectroniki ili kupata idadi kamili ya wanachama kwa lengo la kujipanga katika michakato ya uchaguzi wa ndani na wa Dola.

  “ Viongozi na watendaji wenzangu tujue kuwa chama cha mapinduzi kipo kwa ajili ya wananchi wote hivyo lazima tufanye kazi kwa ushirikiano ili tutimize kwa vitendo dhamira ya mabadiliko yaliyofanywa ndani ya Katiba yanayolenga kuongeza ufanisi katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kiuchumi ndani ya chama chetu.”, alisema Katibu Amen a kuongeza kuwa dhana ya CCM mpya itekelezwe na kusimamiwa na fikra mpya na sio upya wa viongozi wanaochaguliwa kwa sasa.

  Alisisitiza umuhimu wa kufuata Katiba kwa kila hatua ya kufanya maamuzi ndani ya chama hicho kwa lengo la kupunguza malalamiko yasiyokuwa ya lazima kwa baadhi ya wanachama wanaokwenda kinyume na maadili ya Chama hicho.

  Hata hivyo aliyataja majukumu muhimu yanayotakiwa kutekelezwa na idara yake kuwa ni kusimamia Uchaguzi wa Chama na Dola pamoja na kusimamia jumuiya za CCM kuhakikisha zinatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa miongozo ya Kikatiba.

  Mapema akizungumza katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Bora Afya Silima Juma alisema Mkoa huo unaendelea kupanga mikakati ya kudumu itakayosaidia chama hicho kushinda katika Uchaguzi Mkuu ujao.

  Akisoma taarifa ya utekelezaji Katibu wa CCM Mkoa wa Magharibi, Aziza Ramadhan Mapuri alisema licha ya kuwepo kwa changamoto ndogo ndogo katika uchaguzi unaoendea hivi sasa ndani ya mkoa huo wamefanikiwa kuwapata viongozi makini na wachapaka kwa baadhi ya ngazi ambazo tayari zimeshakamilisha zoezi hilo.
    Ni  Baadhi ya Wajumbe wa  Kamati  ya siasa ya Mkoa ya CCM Mjini pamoja na Wajumbe wa sekreterieti na kamati Tekelezaji za jumuiya za Chama hicho wakimsikiliza kwa Umakini Katibu wa NEC, Idara ya Organazesheni CCM Taifa, Nd. Pereira Ame Silima   huko  Katika Ukumbi wa CCM  Amani Unguja.
  Katibu wa NEC,  Idara ya Organazesheni CCM Taifa,Nd. Pereira Ame Silima  akizungumza na Wajumbe wa  Kamati  ya siasa ya Mkoa ya CCM Mjini pamoja na Wajumbe wa sekreterieti na kamati Tekelezaji za jumuiya za Chama hicho huko  Katika Ukumbi wa CCM  Amani Unguja.                                                  


  0 0

  Benny Mwaipaja, WFM

  Serikali imesema inaendelea kupitia sheria, kanuni na taratibu za misamaha ya kodi mwaka hadi mwaka ili kuhakikisha kuwa misamaha yote isiyokuwa na tija inafutwa na hivyo kuiwezesha Serikali kuongeza mapato kwa ajili ya kupeleka huduma za maendeleo kwa wananchi wake.

  Kauli hiyo imetolewa Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Masasi, Mhe. Rashid Mohamed Chuachua (CCM), aliyetaka kujua namna Serikali inavyodhibiti misamaha ya kodi tangu irekodiwe kwa viwango vya juu Mwaka wa Fedha 2011/2012.

  Mhe. Chuwachuwa alihoji mwenendo wa utoaji wa misamaha ya kodi kwa wawekezaji kwa maelezo kuwa Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi zilizopoteza fedha nyingi kwa ajili ya misamaha ya kodi ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki kwa kigezo cha kuvutia Wawekezaji.

  Alisema kuwa kwa mujibu taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2009-2010, Tanzania ilipoteza asilimia 15 ya Pato la Taifa lililotarajiwa kukusanywa kutokana na misamaha ya kodi, mwaka 2010-2011 asilimia 8, kwa mwaka 2011-2012 asilimia 27 ya mapato ya Serikali yalipotea.

  “Je hali ya misamaha ya kodi kuanzia 2013-2014 hadi sasa ikoje’’. Alihoji Mhe. Chuachua.

  Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb),misamaha ya kodi kama sehemu ya asilimia ya Pato la Taifa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2013/14 hadi sasa imekuwa ikipungua mwaka hadi mwaka. 

  “Misamaha hiyo ilikuwa asilimia 2.2 ya Pato la Taifa mwaka 2013/14, asilimia 1.9 ya Pato la Taifa katika mwaka 2014/15 na asilimia 1.1 ya Pato la Taifa katika mwaka 2015/16” Alifafanua Dkt. Kijaji.  

  Aidha aliongeza kuwa misamaha ya kodi ikilinganishwa na mapato ya kodi imekuwa ikipungua kutoka asilimia 18 ya mwaka 2013-2014 hadi kufikia asilimia 8.6 ya mapato yote ya kodi katika mwaka 2015-2016.

  Dkt. Kijaji alifafanua kuwa misamaha ya kodi inatolewa na Serikali kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za kodi zilizopo, huku kukiwa na baadhi ya huduma zinazotolewa katika jamii ambazo hazistahili kulipiwa kodi kwa sababu hazina manufaa ya kibiashara.

  ‘’Pamoja na hatua nzuri zinazochukuliwa na Serikali za kupunguza misamaha ya kodi ni vema ikafahamika kwamba si kila msamaha wa kodi una madhara hasi katika jamii na uchumi kwa ujumla’’. Alisema Dkt. Kijaji.

  Alitolea mfano wa mashirika ya dini yanayopata misamaha ya kodi kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) (2014), kwa sababu huduma zinazotolewa na taasisi hizo hazina faida ya kibiashara kama ilivyo kwa kampuni za kibiashara.

  Katika swali la nyongeza Mbunge huyo, alitaka kujua mpango wa Serikali kuhusu misamaha ya kodi kwa mwaka wa fedha 2017-2018.

  Akijibu swali hilo la nyongeza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Kijaji, alimuomba Mhe. Chuachua awe na subira hadi tarehe 8 mwezi huu ambapo Serikali itapeleka mapendekezo yote katika Bunge, ili mapendekezo hayo yaweze kujadiliwa na kupitishwa na Bunge.

  0 0


   Wachezaji wa Yanga wakimbeba kipa wao Deogratias Munisi, baada ya kuamalizika kwa mchezo wao wa mashindano ya Kombe la SportPesa Super Cup na kutinga hatua ya Nusu Fainali ya michuano hiyo kwa kuwaondisha Tusker ya Kenya kwa mikwaju ya penati 5-3 baada ya kumalizika dakika 90 kwa timu hizo bila kufungana.
   Mshambuliaji wa Yanga Chipukizi, Said Mussa, akimtoka beki wa Tusker, Corins SHivachi, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
   Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa (kulia) akichuana kuwania mpira na beki wa Tusker, James Situma, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. 
   Chirwa akijaribu kukatiza katikati ya mabeki wa Tusker

  Mshambuliaji wa Yanga Chipukizi, Said Mussa, akijipinda kupiga shuti katikati ya mabeki wa Tusker, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
  ******************************************************
  TIMU ya Yanga SC ya jijini Dar es Salaam,leo imetinga hatua ya Nusu Fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup, baada ya kuifungashia vilago Timu ya Tusker ya Kenya kwa kuibanjua kwa jumla ya penati 5-3 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
  Mikwaju ya Penati baada ya kumshukuru Dakika 90 kwa sare Tasa kwenye uwanja wa Uhuru,  Dar es salaam
  Penati za Yanga zilifungwa na Nadir Haroub 'canavaro',  Obrey Chirwa , said Mussa na maka mwakalukwa.
  Kwa upande wa Tusker waliofunga ni  Noah wafula na Brian osumba
   Juma Maadhi akichuana na beki wa Tusker James Situma 

   Said Mussa, akipiga hesabu za kumtoka beki wa Tuske

  Kipa wa Yanga wakibebwa juu kushangilia ushindi leo dhidi ya Tusker.

  0 0


  Halila Tongolanga amefariki jana usiku katika hospitali ya Muhimbili. Alikuwa mwanamuziki wa siku nyingi na alifahamika kwanza kwa wengi baada ya kuanza kusikika kibao chake cha lugha ya Kimakonde cha Kila munu ave na kwao, chenye tafsiri ya ‘Kila mtu ana kwao’ ambacho alikirekodi akiwa bendi ya jeshi ya CTU Monduli, iliyojulikana kama Les Mwenge.
   
   Kwa kifupi ni kuwa baada ya hapo aliitwa kujiunga na bendi iliyokuwa mali ya Dr Alex Khalid, iliyokuwa ikiitwa Makondeko Six. Wakati huo Dr Khalid alikuwa na sehemu kubwa ya burudani iliyokuwa pia na ukumbi na ilikuwa inaitwa Makondeko ikawa na bendi ya watu sita hivyo bendi hiyo ikaitwa Makondeko Six. 
   
  Bendi hii awali ilikuwa ikipiga muziki kwa kufuata nyayo za bendi ya Tatu Nane, lakini Dr Khalid baada ya kuona bendi haina umaarufu kutokana na aina ya muziki iliyokuwa ikipiga, ndipo alipomuita Halila Tongolanga nae akaja na baadhi ya wanamuziki wakajiunga na kuanzisha kundi lililoendelea kutumia jina la Makondeko Six japo wanamuziki walikuwa wengi zaidi ya sita. 
   
  Na ndipo katika kundi hili lilikuwa na wanamuziki wengine kama Innocent Nganyagwa, Anna mwaole wakaweza kurekodi tena wimbo wa Kila Munu Ave na kwao na kundi kupata umaarufu mkubwa mpaka baada ya kusambaratika kwa Makondeko baada ya kifo cha Dr Alex Khalid, lakini Tongolanga aliendelea kutumia jina la Makondeko.
  Baadhi ya wanamuziki waliowahi kufanya kazi na Tongolanga katika kundi la makondeko Six, wakiwa wanasubiri kusafirisha mwili wa mpendwa wao.Toka kushoto, Innocent Nganyagwa, Meneja wa bendi, mpiga solo, Waninga

  Tongolanga amefanya kazi nyingi za muziki ikiwemo kuwa mmoja wa kundi lililoundwa na wanamuziki wengine mahiri kama Moshi William, Muhidin Mwalim, Huluka Uvuruge, Kandaya na wengine lililojulikana kama Bana mwambe, ambapo waliweza kutoka nyimbo nyingi nzuri sana wakati biashara ya kuuza album ilipokuwa ina faida. 
   
  Tongolanga ameagwa na wapenzi wa muziki ndugu na marafiki, lakini kulikuwa na uhaba mkubwa wa wanamuziki wenzie katika kundi lililokuja kumuaga mwanamuziki huyu. Waliojitokeza hasa ni wanamuziki wale tu ambao waliwahi kupiga nae katika kundi la Makondeko na Bana Mwambe na wanamuziki wengine wachache wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki John Kitime, Katibu Mkuu wa Chamudara Hassan Msumari. 
   
  Serikali iliwakilishwa na Katibu Mtendaji wa BASATA. Katika jambo moja kubwa lililotokea wakati wa kuaga mwili ni kujitokeza kwa balozi wa Msumbiiji Bi Monica Patricio Clemente aliyefika Muhimbili kuaga mwili wa Tongolanga akiwa amesindikizwa na maafisa wengine, na pia Balozi huo alitoa rambirambi zake kama Balozi na alitoa rambirambi kutoka kwa Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji. 
   
  Hili lilikumbusha usemi wa wahenga ‘Nabii hathaminiwi kwao.’ Taarifa zilizopatikana pale ni kuwa Tongolanga alikuwa mtu maarufu sana nchini Msumbiji, na aliyekuwa ni msanii muhimu wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu nchini humo.
  Balozi wa Msumbiji Bi Monica Patricio Clemente akiaga sanduku lililokuwa na mwili wa Halila Tongolanga

  Nilipokutana nae kwa mara ya mwisho akiwa kitandani Tongolanda kwa sauti ya uchovu alinambia alikuwa na mengi ya kunambia, wakati tunasubiri taratib kukamilika za kuanza kusafirisha mwili, Innocent Nganyagwa ambaye alikuwa mmoja ya wanamuziki waliotengeneza kundi la Makondeko Six alinambia Tongolanga alikuwa amepanga kufanya onyesho la ‘Usiku wa Makondeko’ na alikuwa na mipango mingine mikubwa ya kufanya kupitia kipaji chake. Pengine ndiyo hayo aliyotaka kunambia Mungu pekee anajua.

  Shukrani za pekee zimfikie Mbunge wa Tandahimba Mheshimiwa Katani Ahmed Katani, kwani kwa juhudi zake Tongolanga alisafirishwa akiwa hai kutoka Ndanda hadi Dar es Salaam kwa matibabu, na pia ndie aliyeusafirisha mwili wa mwanamuziki huyu kwenda Mchichila kwa ajili ya mazishi.

  Toka kushoto Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Nyangamale, Balozi wa Msumbiji nchini, Katibu Mtendaji wa BASATA, Mbunge wa Tandahimba Mhe Katani Katani, afisa wa Ubalozi wa Msumbiji ,Tongolanga anategemewa kuzikwa kijijini kwao Mchichila kesho Junanne 6 Juni 2017.
  Mungu Amlaze Pema Halila Tongolanga
  Mpiga Kinanda Geophrey Kumburu, Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza, Katibu Mkuu wa CHAMUDATA Hassan Msumari

  John Kitime, wanamuziki wa Makondeko Six, Mngereza, Kumburu
  Sanduku alilolazwa Halila Tongolanga likitayarishwa kuingizwa kwenye gari la kusafirisha kuelekea Mcjichila


  Sanduku likiingizwa kwenye gari
  Imetayarishwa na John Kitime wa www.tanzaniarhumba.blogspot.com

  0 0


  Mkuu wa Itifaki mstaafu Balozi Cisco Mtiro (pichani) ambaye amefariki dunia leo asubuhi  katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu, anatarajiwa kuzikwa siku ya JUMATANO, kwa mujibu wa msemaji wa familia, Bw. Shaaban Kessy Mtambo

  Jioni hii Bw. Mtambo ameiambia Globu ya Jamii kwamba mazishi ya mwanadiplomasia huyo yamepangwa kufanyika siku ya JUMATANO saa saba adhuhuri katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. 
  Hiyo ni baada ya kuwasili watoto wake walioko Marekani ambao wanategemewa kuwasili Jumanne usiku, pamoja na mjane wa marehemu anayetegemewa kuwasili Jumanne mchana akitokea Bangui, Afrika ya Kati.
  Amesema mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili nyumbani kwa marehemu saa tano asubuhi siku hiyo ya JUMATANO ambapo utafanyiwa kisomo na kuswaliwa kabla ya kuelekea makaburini kwa mazishi.
   Msiba upo nyumbani kwa marehemu mikocheni B jijini Dar es salaam ambako ndugu, jamaa marafiki, majirani na waliofanya kazi na marehemu wamekuwa wakimiminika kutoa mkono wa pole kutwa nzima ya leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia msiba huu.

  Mola aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi - AMINA

  0 0

  --
   Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi Cuf , Maalim Seif Sharif Hamad  akizungumza na wakazi wa Kata ya Mgomeni Mzimuni ambao alijumuika nao katika futari ya pamoja iliyoandaliwa katika ofsi za umoja wa wabunge wa CUF iliyopo katika kata hiyo.
    Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi Cuf , Maalim Seif Sharif Hamad  akiomba dua pmoja na viongozi wengine waandamizi wa Chama Cha Wananchi CUF ambao walikusanyika kwa ajili ya futari katika kata ya Magomeni Mzimuni.
    Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi Cuf , Maalim Seif Sharif Hamad  akiwa ameketi katika kiti pamoja na Wanachama wengine wa CUF katika ofIsi za umoja wa wabunge wa Chama cha Wanachi CUF
   Baadhi ya wabunge wa Chama cha Wananchi CUF wakiwa wameketi wakifuturu futari iliyoandaliwa na kata ya Magomeni Mzimuni
    Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi Cuf , Maalim Seif Sharif Hamad  akiteta na Mwenyekiti wa Matawi ya CUF Rashid Abdullah mara baada ya kupata futari ya pamoja na wakazi wa Magomeni Mzimuni
    Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi Cuf , Maalim Seif Sharif Hamad   akiteta na Madiwani wa Manispaa ya Ilala wakiongozwa na Naibu Meya wa Manispaa hiyo  Kushoto, Omary Kumbilamoto mara baada ya kupata futari ya pamoja
   Mbunge wa Viti Maalum Chama cha Wananchi CUF kutokeaWilaya ya Mafia mkoa wa pwani , Riziki Ngwali akizungumza mara baada ya kupata futari ya pamoja katika ofsi za wabunge wa Chama cha Wananchi CUF
   Mwenyekiti wa Matawi ya CUF Rashid Abdullah Akizungumza kutoa shukrani kwa katibu mkuu wa CUF kwa kujmuika nao pamoja
   Sehemu ya wanachama wa CUF wakiwa wameketi kumsikiliza kiongozi wao
   Naibu meya wa Manispaa ya Ilala ,Omary Kumbilamoto akiwa anazungumza jambo na viongozi wengine wa Chama cha Wananchi CUF
  Sehemu ya Wanachama wa CUF wakijadili jambo mara baada ya kupata futari

  0 0  0 0


  Wengine waliamua kumkabidhi Ahaj Bulembo hadi bendera ya Chadema baada ya kulifunga tawi lao
  Baadhi ya kadi za Chadema zilizorejeshwa kwa Alhaj Bulembo

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akipokea kadia kutoka kwa Niniani Bakhari, aliyekuwa Kada machachari wa Chadema, ambaye alitangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano wa ndani uliofayika leo katika mji mdogo wa Ngara mkoani Kagera
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimpongeza Ninian kwa uamuzi wake wa kurejea CCM
  Baadhi washiriki wa kikao wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Ngara, Mabalozi na viongozi kutoka Jumuia zote za CCM wakimpongeza Ninian kwa furaha baada ya kukabidhi kadi yake ya Chadema kwa Bulembo wakati wa kikao hicho
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akisikiliza kwa makini wakati Ninian alipokuwa akieleza yake ya moyoni, alisema, aliamua kwenda Chadema baada ya kuona CCM ya wakati huo ina mambo mengi ya hovyo, lakini sasa ameamua kurejea baada ya kuona kuwa Mwenyekiti wa CCM Rais Dk Magufuli amekisafika Chama
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abadalla akitoa kadi kwa mmoja wa wanachama hao wapya 71 waliohamia CCM wakati wa kikao hicho

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo (kushoto) akishiriki wakati wachama wapya 71waliohamia CCM wakitokea Chadema, walipokuwa wakila kiapocha Mwana CCM, baada ya kukabidhiwa kadi za Chama kwenye kikao hicho,leo
  Ukumbi ukilipuka kwa nderemo na vifijo baada ya wanachama hao wapya kulakiapo
  Wajumbe wakiwa ukumbini kuendelea na kikao baada ya zoezi hilo la kupokea wanachama wapya 71 wa CCM kutoka Chadema
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Kagera Oliva Semgurika akisalimia baada ya kutambulishwa kwenye kikao hicho
  Mwenyekitiwa CCM wilaya ya Ngara Hudson Bagege akifunguakikao hicho. Kulia ni Alhaj Bulembo
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Constansia Buhiye akimkaribisha Alhaj Bulembo kuzungumza katika kikao hicho
  Mzee Said ramadhani Sudi akimkabidhi zawadi Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo kabla ya kuzungumza katika kikao hicho
  Mwenyekiti wa Kamati ya mapokezi Jason Bahema akikabidhi zawadi maalum ya kimila kwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaji Abdallah Bulembo kabla ya kuzungumza katika kikao hicho
  Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, Alhajj Abdallah Bulembo akizungumz na wajumbe wakati wa kikao hicho cha Wajumbwa wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ngara, Mabalozi, viongozi wa Jumuia zote za CCM na watendaji wa Serikali, leo
  Vijana wa UVCCM wakimvisha skafu mjumbea wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdalla Bulembo wakati wa mapokezi kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Ngara mkoani Kagera leo
  Vijanawa UVCCM wakionyesha ukakamavu wao wakati wa paredi la mapokezi
  Vijana wa UVCCM na Skauti wakifanya manjonjo yao ilimradi kunogesha mapokezi ya Mjumbea wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulebo alipowasili Ofis ya CCM Wilaya ya Ngara mkoani Kagera leo
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akiwasalimia baadhi ya viongozi alipowasili kweneye Ofisi ya CCM Wilaya ya Ngara mkoani Kagera,leo. Kushoto ni Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo Mwajemi Balagama
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akiwa na viongozi wengine meza kuu alipowasili ukumbini baada ya kutoka Ofisi ya CCM Wilaya ya Ngara mkoani Kagera leo
  Mjumbe wa NEC Ngara, Issa Saama akisalimia baada ya kutambulishwa
  Wazee maarufu walioalikwa kwenye kikao hicho wakiwa ukumbini. PICHA: BASHIR NKOROMO

  0 0

  Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

  Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewataka Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi na wakuu wa Idara za halmashauri zote za mkoa huo kutoa elimu ya usafi wa mazingira pamoja na matumizi sahihi ya vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu ili kukabiliana na ugonjwa wa malaria.

  Bw. Mwanri alitoa wito huo jana mjini Tabora wakati akifungua mkutano wa siku moja kwa viongozi mbalimbali mkoani humo kuhusu mpango endelevu wa ugawaji wa vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu kupitia vituo vya kutolewa huduma za afya na shule za msingi. Alisema kuwa elimu sahihi itasaidia wananchi kuacha kutumia vyandarua kwa matumizi mengine badala ya kujikinga na mbu ili kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa na malaria . 

  Mkuu huyo Mkoa aliongeza wananchi wakifahamu juu ya usafi wa mazingira utasaidia kuondoa mazalia mbu katika makazi yao. Kwa upande wa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara alitoa wito kwa watalaam kusaidia mkakati wa kuangamiza kabisa mazalia ya mbu kama sehemu ya kuondoa ugonjwa wa malaria hapa nchini.
  Aidha , Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Tabora aliiomba jamii kubadirika na kuanza kutumia vyandarua vyenye viutilifu ili kuokoa maisha ya Mama na mtoto.

  Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Gunini Kamba alisema mpango wa kugawa vya ndarua katika vituo vya kutoa huduma za afya ,shule za msingi na katika ngazi ya familia unakusudia kupunguza maambuzi ya maralia hapa nchini.

  Aliongeza kuwa vyandarua hivyo vitasaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria mkoani hapa kutoka asilimia 19.5 ya sasa na kushuka zaidi.

  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri akifungua Mkutano jana mjini Tabora wa viongozi mbalimbali kuhusu mpango endelevu wa ugawaji wa vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu kupitia vituo vya kutolea huduma za afya na shule msingi mkoani humo.

  Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara akisisitiza umuhimu wa wataalam kutafuta mbinu ya kuangamiza mazalia ya mbu kama njia ya kukabiliana na malaria nchini wakati wa mkutano uliofanyika jana mjini Tabora kuhusu mpango endelevu wa ugawaji wa vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu kupitia vituo vya kutolea huduma za afya na shule msingi mkoani humo. Picha na Tiganya Vincent-RS-Tabora.
   

  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akimkabidhi Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira huku Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi pamoja na wakuuu wa Wilaya za Ubungo na Ilala wakipiga makofi.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akila kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakishuhudia tukio hilo Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akila kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akisaini Hati ya Kiapo cha Udilifu kwa Viongozi Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akizungumza mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira, Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.Kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ,Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na viongozi wengine Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akielekea kwenye gari tayari kabisa kwa kuondoka mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akiwa amekaa kabla ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

  0 0

   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (kulia), akimkaribisha Rais Mstaafu, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, katika futari waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Katikati ni Meneja Mahusiano wa benki hiyo, William Kallaghe.
   Rais Mstaafu, Alhaji Ali Hasaan Mwinyi (wa pili kushoto), akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki  ya NBC kwa wateja wake jijini Dar es Salaami. Kutoka kushoto ni  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi, Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Filbert Mponzi na Waziri Mkuu wa zamani, Salim Ahmed Salim .  
   Rais Mstaafu, Alhaji Ali Hasaan Mwinyi (katikati), akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (kushoto), katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Filbert Mponzi.  
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), akimpa zawadi Waziri Mkuu wa zamani, Salim Ahmed Salim katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam.
  Rais Mstaafu, Alhaji Ali Hasaan Mwinyi (kushoto), akizungumza na Meneja wa Tawi la Corporate, Mariam Kombo (kulia), baada ya kuhudhuria hafla ya futari  iliyoandaliwa na NBC jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi na Meneja Mahusiano wa benki  hiyo, William Kallaghe.

  0 0

  Mshambulaji wa kitanzania Jerome Nturukundo (kushoto) anayekipiga katika timu ya Nakuru Stars ya nchini Kenya.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Mshambulaji wa timu ya Nakuru All Stars Mtanzania Jerome Nturukundo amesema kuwa mechi yao dhidi ya Simba itakuwa ni ngumu sana ila watahakikisha wanafanya vizuri ili kuingia hatua ya nusu fainali.

  Nakuru wanatakutana na mabingwa wa kombe la FA Simba katika mchezo wa mtoano utkaoafanyika leo saa 10:15 alasiri kwenye dimba la uwanja wa Uhuru.

  Nturukundo amesema kuwa wanajua Simba ni timu nzuri sana lakinina wao wamekuja kupambana na kuhakikisha wanapata ushindi na kuingia hatua inayofuata.

  "Tutajua simba ni team nzuri lakini na sisi  pia tunekuja kiushindani na wafahamu timu yetu imekamilika na leo wapo katika wakati mgumu kwa sababu  sisi pia tumekuja kushinda,"amsema Jerome

  Kwa upande wa beki wa kati  James sadicky mukhwana yeye amesema kuwa ujio wao Tanzania ni kwa ajili ya kuhakikisha wanapat ushindi katika michezo yao na malengo yao ni kuona kombe la Sportpesa Super Cup likienda nchini Kenya.

  "Simba wasifikiri itakua rahisi kuweza kuoata ushindi katika mchezo wetu wa leo kwani tunataka kombe liiende nyumbani Nchini Kenya na mimi kama mlinzi nitahakikisha hakuna makosa yatakayofanyika katika eneo langui,"amesema  mukhwana.  

  Timu ya Nakuru inanolewa na kocha mzawa George Maina imekuja nchini katika michuano ya Sportpesa Super Cup iliyoandaliwa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Sportpesa.


  0 0


  0 0

  Mkufunzi anayesimamia mafunzo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 (2017/18 HBS) Sergiy Redyakin akimwelekeza mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) namna ya kujaza dodoso litakalotumika katika utafiti huo unaotarajia kufanyika nchini kuanzia mwezi Agosti, 2017.
  Baadhi ya Watakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakifuatilia kwa makini mafunzo yanayotolewa na mkufunzi anayesimamia mafunzo hayo Sergiy Redyakin (hayupo pichani) wakati wa mafunzo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 yaliyofanyika hivi karibuni katika makao makuu ya NBS Dar es Salaam.
  Baadhi ya watakwimu kutoka NBS wakijifunza namna ya kujaza madodoso kwa njia ya kieletroniki wakati wa mafunzo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 unaotarajia kufanyika nchini kuanzia mwezi Agosti, 2017.
  Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Hellen Mtove (wa kwanza kulia) akimhoji mmoja wa wanakaya wakati wa majaribio ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 unaotarajia kufanyika nchini kuanzia mwezi Agosti, 2017.


  (PICHA NA EMMANUEL GHULA)

  0 0

  Afisa Afya Bw. Peter Alfred (katikati) akikagua hati ya kusafiria ya Bw. Paluku Ngahngondi (kushoto) Mkongo anayeishi Zambia, kabla ya kupanda ndege ya Fastjet kuja Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Afya Bi. Shukrani Nkonjeka akiwa kwenye mashine maalum inayompima kila abiria anayepita mbele yake kwa kupiga picha na kutoa mlio wa endapo anajoto kali la mwili.
  Bi. Shukrani Nkonjeka, Afisa Afya akimpa maelezo kuhusiana na ugonjwa wa Ebola, mmoja wa wafanyakazi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Songwe (SIA), Bw. Fred Martin (kushoto).
  Bi Shukrani Nkonjeka, Afisa Afya akiwapa maelezo yanayohusiana na ugonjwa hatari wa Ebola madereva wa taxi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Songwe (SIA).
  Madereva wa taxi wa kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Songwe (SIA), wakipokea vipeperushi vyenye maelezo mbalimbali yanayohusu ugonjwa hatari wa ebola kutoka kwa Afisa Afya, Bi. Shukrani Nkonjeka

  ………………………

  MAAFISA Afya toka kitengo cha magonjwa ya dharura mkoa wa Songwe wameweka kambi kwenye kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Songwe (SIA), ili kubaini abiria wenye dalili za ugonjwa wa Ebola ulioibuka hivi karibuni kwenye nchi ya jirani ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.

  Kiwanja cha Kimataifa cha Songwe kilichojengwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) mwaka 2012 kinapokea abiria 500,000 kwa mwaka kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi, ikiwemo nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. TAA inahudumia viwanja 58 vilivyopo chini ya serikali.

  Afisa Afya Bw. Peter Alfred amesema wamefunga mashine maalum na ya kisasa kiwanjani hapo, ambayo abiria akipita umbali wa mita tano hadi 10 inampiga picha na kuonesha joto alilonalo mwilini, na endapo atakuwa na joto la nyuzijoto 37.5 mashine hiyo itatoa mlio wa kengele.

  Bw. Alfred amesema abiria atakayekuwa na joto hilo, atachukuliwa na kupelekwa eneo maalum lililotengwa umbali wa mita 300 kutoka eneo la kiwanja cha ndege na baadaye kupelekwa hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya matibabu zaidi.

  Hata hivyo, amesema mbali na kuangaliwa kwa abiria wenye joto kali la mwili, pia hukagua na kupata maelezo binafsi kwa kujaza fomu maalum kwa abiria wote wanaopita kwenye kiwanja hicho wakitokea kwenye nchi za Kongo, Guinea, Sierra Leone, Mali, Nigeria, Liberia, Senegal, Marekani na Hispania kutokana na nchi hizo ziliwahi kukumbwa na ugonjwa huo. 

  “Hadi sasa tangu zoezi hili limeanza baada ya kupatikana kwa taarifa za ugonjwa kuwa hapo Kongo, bado hatujapata mgonjwa mwenye dalili hizo na tunaendelea kuudhibiti kwani hapa ni njia kuu kwa abiria wanaotoka Kongo ni wengi,” amesema Bw. Alfred.

  Bw. Alfred amesema ugonjwa wa Ebola unasababishwa na virusi vya Ebola vinavyoingia mwilini mwa binadamu na wanyama kupitia puani, masikioni na machoni, na huambukiza kwa kugusa majimaji ya mwili toka kwa mtu aliyeambukiwa virusi hivyo, yakiwemo matapishi, damu, jasho, mkojo, machozi, kamasi na mate.

  Pia binadamu anaweza kupata ugonjwa huu kwa kugusa au kuosha maiti ya aliyefariki kwa ugonjwa huu au kugusa shuka, godoro, nguo na blanketi lililotumika na mgonjwa; pia kuchomwa na sindano au vifaa visivyo safi na salama vilivyotumiwa na mgonjwa wa ebola; au kula matunda yaliyoliwa nusu na wanyama na kugusa mizoga au kula wanyama pori kama nyani, sokwe na popo.

  Bw. Alfred amesema dalili za ugonjwa huu zinaanza kujitokeza kati ya siku mbili hadi 21 baada ya kupata maambukizi, ambapo mgonjwa hupata homa kali ya ghafla, maumivu ya kichwa, maumivu ya mwili, misuli na viungo, vipele mwilini, kuvia damu chini ya ngozi, kutokwa damu mdomoni, puani, masikioni, machoni, kuharisha na kutapika kunakoweza kuambatana na damu.

  Hata hivyo, Bw. Alfred amesema ugonjwa huu hauna tiba maalum wala chanjo, lakini mgonjwa hupatiwa tiba saidizi kulingana na dalili alizonazo kama vile kushusha homa na maumivu, kuongezewa damu na maji mwilini na tiba lishe.

  Bw. Alfred amesema wananchi wanaweza kujikinga na ebola kwa kuepuka kusalimiana kwa kupeana mikono au kukumbatiana, kuepuka kugusa majimaji yaliyotoka mwilini mwa mgonjwa au kuosha maiti, kuacha kutumia godoro, shuka na nguo za mgonjwa na pia wawahi haraka kituo cha kutolea huduma za afya endapo wataona dalili za ugonjwa wa ebola.  IMETOLEWA NA KITENGO CHA SHERIA NA MAHUSIANO, MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni William Makufwe awashukuru BAY PORT Taasisi ya kifedha kwa msaada wa kompyuta mbili walizozitoa Jana kwa Idara ya Utumishi na Rasilimali watu..

  Mkurugenzi Mtendaji alisema kuwa anashukuru kwa msaada wa kumpyuta hizo ambazo zitakwenda kwenye Idara ya Utumishi na Rasilimali watu ili kuimarisha Idara na ufanisi wa Idara hiyo kwa kuzingatia unyeti wa eneo hilo na huduma wanayoitoa kwa watumishi.

  Miongoni mwa Halmashauri 80 ambazo zimelenga kufikiwa na BAYPORT tunashukuru Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imekuwa moja wapo na tunaahidi kutumia vifaa hivi vya TEHAMA kwa kuongeza ufanisi na utendaji kazi ulioboreka zaidi.

  Mratibu wa masoko na mawasiliano wa huduma za kifedha za BAYPORT Mercy Ndunguru alisema kuwa BAYPORT imeamua kurudisha faida ambayo wameipata ambapo kwa sasa wameona waguse sekta ya utumishi ambayo imekuwa na msaada mkubwa katika kufikia malengo.

  Mercy alisema kuwa, Tunaamini kwa kutoa vifaa hivi vya TEHAMA itasaidia kuongeza ufanisi kwenye sekta ya utumishi na watumishi watapata huduma kwa wakati, BAYPORT inamuunga mkono Raisi kwenye utendaji kazi kwa watumishi.

  Meneja wa BAYPORT Handeni Kanji Masanji alisema kuwa, anashukuru kwa ushirikiano anaoupata kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na kwamba taasisi yao inajipanga kufanya mambo mengine makubwa zaidi ya haya ikiwa ni pamoja na kujipanga kufadhili timu mbalimbali za mipira na kuinua vipaji vya vijana waliopo Wilayani Handeni.

  BAYPORT wametoa msaada huo wa kompyuta mbili ikiwa ni miongoni mwa kompyuta zenye thamani ya zaidi ya milioni 500 zinazoendelea kutolewa kwenye taasisi nyingine za Kiserikali.

  Alda Sadango

  Afisa Habari
  Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni William Makufwe kushoto akipokea Msaada wa kompyuta kutoka Kwa Mratibu wa masoko na mahusiano kutoka BAYPORT Mercy Ndunguru.

  Afisa utumishi Wilaya Noel Abel akipokea Msaada wa kompyuta kutoka Kwa Mratibu wa masoko na mahusiano kutoka BAYPORT Mercy Ndunguru.
  Picha ya pamoja baada ya makabidhiano ambapo kushoto ni Afisa utumishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na kulia ni Mratibu wa masoko na mahusiano na meneja wa tawi LA BAYPORT Handeni

  0 0

  Wananchi wilayani Handeni wapigwa marufuku kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka katika vyanzo vya maji na kutakiwa kutunza mazingira ili kuwezesha uendelevu wa maisha.

  Marufuku hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe aliyekuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yaliyofanyika ngazi ya wilaya katika Kata ya Mkata katika bwawa la Tulafimbo. 

  Gondwe alisema kuwa wananchi lazima wazingatie sheria ya Mazingira inayozuia kufanya shughuli za kibinadamu pamoja na kujenga kwenye maeneo yote ya vyanzo vya maji ndani ya mita 60. “Kwa kuzingatia sheria hiyo, kupiga marufuku kwa wananchi kufanya shughuli zozote za kibinadamu zenye kuhatarisha usalama wa maji na uchafuzi wa mazingira kwenye maeneo yanayozunguka vyanzo vya maji wilayani Handeni” alisema Gondwe. 

  Aidha, aliwataka maafisa Tarafa, maafisa watendaji wa Kata na wenyeviti wa Vijiji kuhakikisha wanatengeneza mipaka kwenye maeneo ya vyanzo vya maji vyote vilivyopo Wilayani Handeni msimu huu ambao mvua imenyesha ya kutosha na vyanzo vingi vimejaa maji. “Hii itasaidia kuzuia uvamizi wa maeneo hayo na kurahisisha kuchukua hatua kwa watu watakaokwenda kinyume na amri hiyo” alisema Gondwe.

  Gondwe, aliwataka wananchi wote walionunua mashamba kwa lengo la kilimo kusafisha mashamba yao kwa kuacha asilimia 30 ya uoto wa asili badala ya kusafisha maeneo yote ambayo wamenunua. “Tusipotunza mazingira, itakuwa ni ubinafsi kwa kizazi chetu na kizazi kijacho. Tukitendee haki kizazi hiki na kijacho kwa kuondoa ubinafsi wa kuharibu mazingira” alisema Gondwe.

  Wakati huohuo, aliwataka viongozi ngazi ya Wilaya, Tarafa, Kata na Vijiji kutunza kutunza mazingira kwa kusimamia uwiano wa ardhi uliyopo na idadi ya mifugo ili kutunza mazingira kwa kuwa na mifugo inayoendana na rasilimali ardhi iliyopo. Aliwataka kuweka mikakati ya kupiga chapa mifugo ili kurahisisha utambuzi wa mifugo hiyo wilayani Handeni.

  Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, William Makufwe aliwataka wananchi kutunza rasilimali maji kidogo inayopatikana kwa kipindi cha mvua kwa kupanda miti kwenye maeneo yanayozunguka vyanzo vya maji. Alisema kuwa Serikali inaendelea kushughulikia changamoto ya upatikanaji maji ya kudumu Wilayani Handeni. 

  Aliwataka wakuu wa shule za msingi na sekondari kuhakikisha kila mwanafunzi anayeanza darasa la kwanza hadi la saba na kidato cha kwanza hadi cha nne anakuwa na mti wake anaoutunza ili anapomaliza shule akikabidhiwa cheti na yeye akabidhi mti alioutunza kwa kipindi chote alichokuwa shuleni. 

  Maadhimisho ya wiki ya mazingira kiwilaya yalitanguliwa na upandaji miti 28,954 yakiongozwa na kaulimbiu isemayo “hifadhi ya mazingira muhimili kwa Tanzania ya viwanda”.
   Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akipanda mti kwenye maadhimisho.
   Mkurugenzi Mtendaji Bw William Makufwe iyeshika chepeo na mwenyekiti wa Halmashauri ya Handeni Mh Ramadhani Diliwa wakipanda mti.
   Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akizungumza na wananchi.
   Mkurugenzi Mtendaji Bw William Makufwe akizungumza na wananchi wakati wa maadhimisho.
   Mwenyekiti wa Halmashauri Mh Ramadhani Diliwa akizungumza na wananchi.
  Wanafunzi wa shule ya sekondari Mkata  wkisherehesha kwa Ujumbe wa utunzaji mazingira.

  0 0

  Gari lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo likielekea kwenye kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kiboriloni kwa ajili ya kuombewa. Maziko ya Marehemu Ndesamburo yanafanyika leo nyumbani kwake mtaa wa  KDC- Moshi,mkoani Kilimanjaro.
  Gari lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo likiingia kwenye kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kiboroloni.
  Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe akiiingia katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kiboroloni kwa ajili ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo.
  Viongozi mbali mbali wa Chadema wakiingia katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kiboriloni.
  Viongozi mbali mbali wa Chadema wakiingia katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kiboriloni. Waziri mkuu wa Zamani ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa akiingia kanisani.
  Wabunge wa Chadema wakiwa wamejipanga kupokea mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kiboriloni.
  Wajukuu wa Marehemu Phillemon Ndesamburo wakielekea kanisani.
  Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo ukiingizwa kanisani.
  Waziri mkuu wa Zamani ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa akibadilishana mawazo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi katika ibada ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo.
  Viongozo wa Chadema wakiwa katika ibada ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo.
  Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo ukiwa kanisani tayari kwa maombezi.
  Mke wa Marehemu aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo (wa pili toka kushoto) akiwa kanisani.

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd  akimsikiliza  Mkurugenzi Mkuu wa  Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania { Tanzania Media Foundation – TMF } Bwana Ernest Sungura alipokuwa akizungumza nae jambo ofisini kwake.

   Mkurugenzi Mkuu wa  Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania { Tanzania Media Foundation – TMF } Bwana Ernest Sungura  amesema hadhi ya Sekta ya Habari Nchini itaheshimika na kuaminika zaidi endapo wanahabari wenyewe watajiwekea malengo ya kufanya kazi kwa agenda katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

  Alisema mfumo wa agenda kwa Wanahabari ndio njia pekee itakayosaidia  kuamsha ari sambamba na kuibua changamoto zinazokwaza Jamii na kuzipa nguvu za uwajibikaji Taasisi za Umma na hata zile binafsi katika kuwahudumia kwa umakini Wananchi.

  Nd. Ernest Sungura  Alisema hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye Jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar akiuongoza Ujumbe wa Viongozi Wanne wa TMF uliokuwepo Zanzibar  kwa ziara maalum ya kukagua  Maandalizi na Mikakati  ya mradi wa kuwapatia Mafunzo Wanahabari wa Zanzibar.

  Alisema kupitia Mfuko wa Vyombo vya Habari zipo agenda zilizowahi kuibuliwa na Wanahabari wa Vyombo tofauti Nchini akizitolea mfano  vita dhidi ya Dawa  za Kulevya, Udhalilishaji wa Kijinsia na ubalozi wa Usalama barabarani ambazo zimesaidia kuleta faraja kwa Jamii na kuzipunguzia matumizi mabovu yasiyo na msingi Serikali zote mbili.

  Alieleza kwamba yapo mambo mengi na mazuri ya kujivunia  kutokana na kuanzishwa kwa mfumo huo wa agenda  jambo ambalo limeziletea sifa Taasisi za Habari kwa Taifa na Wananchi jambo ambalo lilisaidia kuibua changamoto zinazokwaza Serikali na Jamii kwa ujumla.

  Bwana Sungura alimueleza Balozi Seif  kwamba katika kuwajengea uwezo uliobobea Waandishi wa Habari katika utekelezaji wa kazi zao.

  Alisema kuwa tangu kuanzishwa kwake, TMF tayari imeshatoa ruzuku kwa   Wanahabari  binafsi zaidi ya 600 na taasisi za  kutoka kihabari 120 nchini.

  Alisema mkazo zaidi wa mafunzo hayo utawekwa kwa wale waandishi na Vyombo vya Habari visivyo na uwezo wa kufanyakazi vizuri  ili navyo viweze kupiga hatua itakayokwenda sambamba na wenzao wenye nguvu za uwezeshaji kifedha.

  Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliushukuru Uongozi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania { TMF } kwa uamuzi wake wa kuwafinyanga Wanahabari katika misingi ya kuwajibika Kitaaluma zaidi badala ya kukurupuka katika Uandishi wao.

  Balozi Seif alisema kitendo cha Taasisi hiyo cha kuwajengea uwezo wa Kitaaluma Wana Tasnia hao wa Habari kitawawezesha kuzalisha zao litakalopokewa vyema tena kwa Heshima kutoka kwa Jamii.


  Othman Khamis Ame

  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

  5/6/2017

older | 1 | .... | 1261 | 1262 | (Page 1263) | 1264 | 1265 | .... | 1897 | newer