Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1260 | 1261 | (Page 1262) | 1263 | 1264 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimu Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Leonard  She Okitunda alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kuwasilisha ujumbe huo leo Juni 5, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea ujumbe kutoka kwa Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Leonard  She Okitunda alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kuwasilisha ujumbe huo leo Juni 5, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na  Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Leonard  She Okitunda na ujumbe wake na wa Tanzania alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kuwasilisha ujumbe huo leo Juni 5, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Ibrahim Al Najem alipofika kumtembelea Ikulu jijini Dar es salaam  leo Juni 5, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Ibrahim Al Najem alipofika kumtembelea Ikulu jijini Dar es salaam  leo Juni 5, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia malori mawili ya kuzolea taka baada ya kumaliza mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Ibrahim Al Najem alipofika kumtembelea na kukabidjhi msaada wa magari hayo Ikulu jijini Dar es salaam  leo Juni 5, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Mjumbe Maalumu wa Rais wa Msumbiji na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Jenerali  Atanasio Salvador Ntumuke alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kuwasilisha ujumbe huo leo Juni 5, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mjumbe Maalumu wa Rais wa Msumbiji na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Jenerali  Atanasio Salvador Ntumuke alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi ujumbe maalumu leo Juni 5, 2017

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe walioongozana na Mjumbe Maalumu wa Rais wa Msumbiji na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Jenerali  Atanasio Salvador Ntumuke alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi ujumbe maalumu leo Juni 5, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana baada ya  mazungumzo na Mjumbe Maalumu wa Rais wa Msumbiji na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Jenerali  Atanasio Salvador Ntumuke alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi ujumbe maalumu leo Juni 5, 2017

  PICHA NA IKULU

  0 0

   Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akitoa maelezo kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika mkutano wa kushajihisha wajumbe hao kuhusu kifua kikuu, Ukimwi na homa ya Ini katika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
   Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid ambae alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo akiufungua rasmi katika Hoteli ya Ocean View (kulia) Mnadhimu wa Baraza  Ali Salim Haji na (kushoto) Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo.
   Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia ufunguzi wa mkutano wa kuwashahishaji kuhusu Kifua kikuu, Ukimwi na homa ya Ini uliofanyika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
   Mratibu wa huduma za homa ya Ini Zanzibar Dkt. Sania Shafi akiwaelezea Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi hali halisi juu ya homa ya Ini katika mkutano uliofanyika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
   Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Rashid Makame Shamsi akitoa mchango katika mkutano huo.
  Meneja Kitengo Shirikishi Kifua kikuu, Ukimwi na homa ya Ini Dkt. Farhat Ahmed akijibu maswali ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika mkutano wa kuwashajihisha kuhusu maradhi hayo katika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga.

  Na Ramadhani Ali – Maelezao Zanzibar.

  Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wameshtushwa na idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na homa ya Ini wakati wananchi wengi hawana uelewa juu ya maradhi hayo na Serikali haijaandaa mikakati imara ya kupambana nayo.

  Wajumbe hao walieleza hisia zao wakati wakichangia mada ya hali halisi ya homa ya Ini katika mkutano wa kushajihisha wajumbe hao kuhusu maradhi ya Kifua kikuu, Ukimwi na Homa ya Ini ulioandaliwa na Kitengo Shirikishi cha maradhi hayo katika Hoteli ya Ocean View Kilimani.

  Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Rashid Makame Shamsi alisema wakati homa ya Ini inaongoza kwa kusababisha vifo vingi zaidi ikilinganisha na maradhi mengine haikuzungmzwa katika Bajeti ya mwaka huu ya Wizara ya Afya.

  Amesema kukosekana taarifa ya homa Ini ndani ya Bajeti ya Wizara huku wananchi hawana uelewa juu ya homa hiyo itapelekea kuenea kwa kasi na kupoteza maisha ya wananchi.

  Mwakilishi wa kuteuliwa Ahmada Yahya ameishauri Wizara ya Afya kupitia Kitengo Shirikishi kutoa taaluma zaidi kwa wananchi ili kuwa na uelewa mpana wa homa ya Ini na njia za kujikinga nayo.

  Spika wa Baraza la Wawakilishi ambae alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo ameishauri Kamati ya Bajeti ya Baraza hilo kuangalia uwezekano wa kukipatia fedha Kitengo Shirikishi cha Ukimwi, Kifua Kikuu na homa ya Ini ili kiweze  kukabiliana nayo.

  Mratibu wa huduma za homa ya Ini Zanzibar Dkt. Sania Shafi aliwafahamisha  wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuwa homa hiyo ni janga kama yalivyo maradhi ya Ukimwi na Kifua kikuu hivyo mashirikiano ya pamoja yanahitajika katika kukabiliana nayo.

  Aliwaeleza wajumbe hao kuwa njia kuu za maambukizi ya homa ya Ini ni sawa na zile za maambukizi ya Virusi vya Ukimwi lakini virusi vya homa ya Ini vinakasi zaidi.Alisema mtu anapopata homa ya Ini hupoteza uwezo wa  kufanyakazi kwa vile  Ini linaharibika na husababisha kupata saratani na hatimae kupoteza maisha.

  Aliwashauri vijana kujiepusha kufanya  vitendo vinavyosababisha kupata Virusi vya Ukimwi kwa vile maradhi hayo yanauhusiano mkubwa na homa ya Ini.

  Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya kwa kufahamu athari ya homa ya Ini inaendelea kufanya tafiti na hivi karibu itafungua kliniki katika hospitali kuu ya Mnazimmoja kwa ajili kushughulikia homa hiyo.

  0 0

    Kaimu Mkurugenzi  Idara ya  ya Uongozaji ndege na Huduma(ANS), John Chambo akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa Idara ya Uongozaji ndege uliofanyika Mkoani Morogoro.
   Wajumbe wakiwa kwenye mkutano wa mwaka wa Idara ya Uongozaji ndege na Huduma(ANS) wakifuatilia mkutano.

  0 0  0 0

  Sanduku lenye Mwili wa Marehemu wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo,ukiandaliwa tayari kwa kuagwa katika uwanja wa Majengo,mjini Moshi mkoani Kilimanjaro mapema leo mchana.
    Gari lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo lilielekea katika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili huo.
  Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiwapungia mkono wananchi waliofika kwenye uwanja  huo mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo.
  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akiwasili katika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili wa  aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo.
  Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwa wamebeba jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo. 
  Viongozi mbalimbali wa Kisiasa na dini wakiwa wamesimama mara baada ya mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo kuwasili uwanjani hapo

   Baadhi ya wakazi wa mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro wakiwa kwenye uzuni mara baada ya mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo ulipokuwa unaelekea katika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili huo.     

    

   

  0 0

  Mafunzo hayo ya siku mbili Juni 5 na 6, 2017, yanafanyika katika ukumbi wa Vigirmark Hotel mjini Shinyanga, na yamekutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka PS3, TAMISEMI, Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu, na wakufunzi kutoka mikoa mbalimbali ambako mradi unatekelezwa. 

  Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, alisema mfumo wa FFARS utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha kuwa vituo vya kutolea huduma vinakusanya na kuhifadhi taarifa za mapato na matumizi zilizotengwa na Serikali kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya vituo hivyo ili wananchi waweze kupata huduma bora. 

  “Ikumbukwe kuwa Mheshimiwa Rais katika kutekeleza mpango wa elimu bila malipo aliamuru kuwa fedha za ruzuku za gharama za uendeshaji wa shule lakini pia vituo vya kutolea huduma zitapelekwa moja kwa moja katika vituo hivyo, hivyo basi usimamizi wa ruzuku hizo utafanywa na vituo husika,” alieleza Msovela. 

  “Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo ili kuhakikisha kuwa vituo vyetu vya kutolea huduma kupitia fedha za ruzuku vinakuwa na mfumo maalum wa kuandaa taarifa za mapato na matumizi, hali ambayo itachangia uwajibikaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi,” aliongeza Msovela. 

  Aidha, alisema Serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na PS3 katika kuunganisha wadau, na kuongeza kuwa ni wakati mzuri watanzania wakaiga mfano wa nchi kama Marekani ambao wapo mbele zaidi katika masuala ya uwazi na utawala bora katika kuwapa taarifa wananchi zinazohusu maeneo yao. 

  Awali akizungumza katika mafunzo hayo, Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji, Tathmini na Tafiti Tendaji kutoka PS3, Dkt. Suma Kaare, alisema mfumo wa mpya wa uhasibu na utoaji taarifa - FFARS unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) kupitia Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3). 

  “Tumeandaa mafunzo ya kina kwa wakufunzi 490 katika ngazi ya taifa na halmashauri, yatakayofanyika mikoa minne nchini: Dodoma, Mbeya, Mtwara na Shinyanga, ili kuwawezesha watumishi katika vituo vya afya na elimu kupata ujuzi wa namna ya kutumia mfumo mpya wa FFARS,” alifafanua Dkt. Kaare. 

  “Wakufunzi hawa wataweza kutoa elimu hii kwa watumiaji wa mwisho wa mfumo wa FFARS katika zaidi ya vituo vya afya 550, zahanati 6800, hospitali za wilaya 135 na takribani shule za msingi na sekondari 20,000 katika mikoa 26 ya Tanzania bara, vikiwemo vituo vya kutolea huduma kutoka mikoa 13 na halmashauri 93 zinazotekeleza mradi wa PS3,” aliongeza Dkt. Kaare. 

  Katika hatua nyingine, alisema FFARS itaweza kufuatilia matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali katika kufikia malengo ya utoaji huduma na kuhakisha yanaendana na sheria ya manunuzi na utoaji taarifa, ili kuisaidia Serikali kuimarisha mfumo wa usimamizi wa fedha za umma na kuongeza uwazi na watoa huduma kuwa na wajibu kwa jamii wanayoihudumia. 

  Naye Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi kutpka TAMISEMI, Elisa Rwamiago, alisema mfumo wa FFARS utaanza kutumika kuanzia Julai 1, 2017, ambapo Serikali itaanza kupeleka rasilimali fedha moja kwa moja kwenye vituo vya afya kwa ngazi za halmashauri.

  “Vituo vya kutolea huduma vitakavyopokea fedha hizo ni pamoja na zahanati, vituo vya afya, na hospitali za wilaya. Zoezi hili ni sambamba na inavyotekelezwa kwenye sekta ya elimu, serikali za vijiji na ofisi za kata,” alieleza Rwamiago. 

  Mwandishi wetu, Kadama Malunde, ametuletea picha za matukio yaliyojiri wakati wa mafunzo hayo siku ya kwanza Jumatatu, Juni 5, 2017 .
  Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, amefungua mafunzo ya mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS) kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems Strengthening – PS3’.
  Mgeni rasmi, Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, akifungua mafunzo kuhusu mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS) katika ukumbi wa Vigirmark Hotel mjini Shinyanga 
  Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, akifungua mafunzo mafunzo kuhusu mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa kwa wakufunzi zaidi ya 130 kutoka mikoa ya kanda ya ziwa na kati waliohudhuria mafunzo hayo 
  Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, akizungumza ukumbini. Kulia ni Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago, na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji, Tathmini na Tafiti Tendaji kutoka PS3, Dkt. Suma Kaare 
  Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, alisema wananchi wana haki ya kuhoji pale ambapo mambo yanakuwa hayaendi sawa na serikali ina wajibu wa wananchi inayowatumikia hivyo kuwataka wakufunzi hao kutumia mafunzo wanayopatiwa kutoa elimu kuwapa pia watu wengine 
  Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji, Tathmini na Tafiti Tendaji kutoka PS3, Dkt. Suma Kaare akizungumza wakati wa ufunguzi
  Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji,Tathmini na Tafiti Tendaji kutoka PS3, Dkt. Suma Kaare akizungumza ukumbini 
  Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago, akielezea kuhusu umuhimu wa mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS) 
  Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago, akielezea jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo 
  Kaimu Mratibu wa Mradi wa PS3 mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia akizungumza wakati wa mafunzo hayo 
  Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini 
  Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini 
  Mshauri wa Masuala ya Usimamizi wa Fedha za Umma kutoka Mradi wa HPSS Dodoma, Elezeus Rwezaula, akitoa mada wakati wa mafunzo hayo 
  Mshauri wa Masuala ya Usimamizi wa Fedha za Umma kutoka Mradi wa HPSS Dodoma, Elezeus Rwezaula, akielezea kuhusu mfumo wa FFARS 
  Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada 
  Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada ukumbini 
  Mafunzo yanaendelea 
  Washiriki wa mafunzo wakisikiliza kwa makini kilichokuwa kinaendelea ukumbini 


  Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Mkuu wa Timu ya waangalizi ya SADC ya uchaguzi wa Lesotho akiwasilisha taarifa ya awali kuhusu uchaguzi huo .
  Waziri Mahiga akiendelea kuwasilisha taarifa ya awali ya uchaguzi wa Lesotho jijini Maseru .
  Waziri Mahiga bado anasoma taarifa ya awali ya uchaguzi wa Lesotho kwa wajumbe.   Serikali Mpya ya Lesotho yashauriwa kutekeleza Mageuzi - SADC

  Serikali itakayoingia madarakani baada ya Uchaguzi wa Wabunge uliofanyika nchini Lesotho Julai 3, imeshauriwa kutekeleza kikamilifu na kwa nia ya dhati maazimio yote ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC yanayohusu mageuzi kwenye sekta muhimu za katiba, sheria na mahakama, ulinzi na usalama, utumishi na sekta ya umma na vyombo vya habari kwa muda muafaka ili kuimarisha utawala bora na wa kidemokrasia nchini humo. 

  Mnamo mwezi Machi mwaka 2017, baada ya Mfalme Letsie wa III wa Lesotho kutangaza tarehe ya uchaguzi mkuu, kikao cha juu cha maamuzi cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC Summit), kilielekeza Serikali mpya itakayoshinda uchaguzi na kuingia madarakani, itekeleze maazimio hayo kwa kuweka muda maalum na vigezo vya utekelezaji ili kuepuka chaguzi za mara kwa mara. 

  Msimamo huo wa Jumuiya ya SADC umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Mheshimiwa Augustine P. Mahiga, Mwenyekiti wa Kamati ya Asasi ya Ushirikiano ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC alipokuwa akitoa taarifa ya awali ya timu ya uangalizi siku mbili baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika. 

  Mheshimiwa Mahiga alisema, japokuwa zoezi la kuhesabu kura bado linaendelea, ni dhahiri kuwa wapiga kura nchini Lesotho wanatarajia mageuzi makubwa kutoka kwenye Serikali mpya yatakayoandika historia mpya nchini Lesotho, ambayo imafanya chaguzi tatu kuu ndani ya miaka mitano. 

  Mapendekezo mengine yaliyotolewa kwenye taarifa hiyo ya awali ya SADC yanaitaka Serikali mpya kupitia na kufanyia mageuzi mfumo mzima wa uchaguzi ambao kwa sasa unatoa fursa kwa wabunge kuhama chama bila kupoteza ubunge wao (Floor Crossing). Alisema mfumo huo unayumbisha mfumo wa siasa na wa kibunge kwenye Falme ya Lesotho. 

  Kwenye upande wa ulinzi na usalama wa raia wakati wa uchaguzi, taarifa hiyo ilisifu Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho kwa kuendesha kwa weledi mkubwa zoezi la upigaji kura na kushirikiana na Jeshi la Polisi kuimarisha usalama vituoni kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi. 

  Hata hivyo taarifa za awali za waangalizi wa kimataifa zimeeleza kuwa Jeshi la Lesotho pia lilionekana kwenye baadhi ya maeneo, nje ya vituo wakiimarisha ulinzi kwa mujibu wa sheria ya jeshi hilo. Balozi Mahiga alieleza kuwa japokuwa uwepo wa jeshi hakuathiri mwenendo mzima wa upigaji kura, bado kuna umuhimu wa kufanya mageuzi ndani ya vyombo hivyo ili kuainisha majukumu ya kila taasisi na kuondoa muingiliano wa kimajukumu kama ilivyo sasa. 

  Mapendekezo mengine yaliyotolewa na Jumuiya ya SADC kwa Serikali mpya nchini humo ni kuweka mazingira bora yatakayowezesha wanawake na watu wanaoishi na ulemavu kushiriki kikamilifu kwenye shuguli za kisiasa bila ubaguzi. Vilevile kuifanyia mageuzi sekta ya habari nchini na kuwawezesha wananchi kupata habari za uhakika na kwa wakati.

  Matokeo ya uchaguzi wa Wabunge yanaendelea kutangazwa ambapo na yanatarajiwa kukamilika ndani ya siku mbili ambapo upinzani mkali unaonekana baina ya Chama cha Democratic Congress kinachoongozwa na Waziri Mkuu wa sasa Mhe. Pakalitha Mosisili na Chama cha All Basotho Convention kinachoongozwa na Waziri Mkuu wa zamani Mhe. Thomas Motsoahae Thabane.


  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
  Maseru, Lesotho, 05 Juni 2017

  0 0

   Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim  Majaliwa wakati wa hafla ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa mfumo wa kusafirisha na kusambaza maji safi pamoja na matenki ya kuhifadhi maji katika Jimbo la Chalinze. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Chalinze, Mhandisi Christer Mdomba, kulia ni Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo.
   Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo akizungumza wakati wa hafla ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa mfumo wa kusafirisha na kusambaza maji safi kutoka mto Wami pamoja na matenki ya kuhifadhi maji katika Jimbo la Chalinze. Kushoto ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga.
   Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi  wa  DAWASA, Mhandisi  Romanus Mwangingo (Kulia)    akitoa maelezo ya utekelezaji wa  mradi kusafirisha na kusambaza maji safi pamoja na matenki ya kuhifadhi maji katika Jimbo la Chalinze.
   Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwan Kikwete (Kulia) akiteta Jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bw.Majid Mwanga  Wakati wa hafla hiyo.
   Moja ya tenki la maji linalojengwa katika chanzo cha maji cha mto Ruvu ikiwa ni sehemu ya mradi huo.
   Mbunge wa Jimbo la ChalinzeChalinze, Mhe. Ridhiwan Kikwete akimshukuru Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Mhandisi Gerson Lwenge kwa hatua nzuri iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo.
  Mafundi wakiendelea na maandalizi ya ujenzi wa matenki yakuhifadhi maji katika chanzo cha maji Ruvu. (Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo)

  Frank Mvungi-Maelezo.

  Takriban wakazi 234,398 wa  Chalinze watanufaika na  mradi wa upanuzi wa mtambo na ujenzi wa mfumo wa kusafirisha na kusambaza maji safi pamoja na matenki ya kuhifadhi unaolenga kuondoa changamoto ya upatikanaji wake katika Jimbo hilo.

  Akizungumza  kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa hafla ya kukagua maendeleo ya mradi  huo, Waziri wa Maji na Umwagiliaji,  Mhandisi Gerson Lwenge amesema kuwa Serikali inaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo na kumtaka mkandarasi kuongeza kasi katika kutekeleza mradi huo.

  “Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maji safi na salama ndio maana tumeweka wataalamu wetu hapa kumsimamia mkandarasi ili afanye kazi  kwa ubora na kwa kasi kama ambavyo Waziri Mkuu aliagiza alipotembelea mradi huu mwezi Machi mwaka huu”, alisisitiza Lwenge.

  Akifafanua, Mhandisi Lwenge amesema kuwa hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa  mradi huo awamu ya tatu ni ulazaji wa mabomba ya kusafirisha na ya kusambaza maji, ujenzi wa matanki 19, na ujenzi wa  mtambo wa kusafishia maji ambao unaendelea. 

  Kazi nyingine zinazoendelea katika kutekeleza mradi huo ni ujenzi wa vituo 351 vya kuchotea maji ambapo vituo 27 vimekamilika,vituo 226 vipo katika hatua mbalimbali na vituo 98 havijaanza kujengwa.

  Akizungumzia hatua zinazochukuliwa na mkandarasi wa mradi huo, Mhandisi Lwenge amesema kuwa ni kuongezeka kwa upatikanaji wa vifaa kwa wakati katika eneo la mradi, kuongeza wafanyakazi na maeneo ya kazi na kuteua mwakilishi wa kampuni anayeweza kutoa maamuzi kwa niaba ya kampuni inayotekeleza mradi.

  Aidha, Waziri Lwenge amesema kuwa Serikali itatoa ufumbuzi wa changamoto ya wananchi wa Jimbo hilo kulipia malipo ya huduma  (service charge) hata pale wanapokuwa hawajapata huduma hiyo ili kuwe na utaratibu mzuri unaowezesha wananchi kulipia huduma pale wanapotumia tu na si vinginevyo.

  Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo hilo, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema yeye binafsi anaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa namna inavyoshughulikia  changamoto zinazowakabili wananchi wa Jimbo hilo ikiwemo ya maji.

  “Naridhika na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya mradi huo ambao ukikamilika utasidia kwa kiwango kikubwa kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji katika jimbo hili hivyo wananchi wataweza kuongeza kasi katika shughuli za maendeleo”, alisisitiza Ridhiwani.

  Akifafanua amesema anaunga mkono juhudi za Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo .

  Mnamo mwezi Machi mwaka huu, Waziri  Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alifanya ziara ya kutembelea mradi huo na kukagua shughuli za ujenzi wa miundombinu ya mradi  huo  Awamu ya Tatu na baada ya ziara aliagiza mkandarasi anayetekeleza mradi huo ambaye ni Overseas Infrastracture Alliance (OIA)Pv Ltd kutoka India  mwenye ubia na Kampuni ya Pratibha Industries nayo ya India kukamilisha kazi hiyo ,mkandarasi wa mradi huo ameshalipwa shilingi 38,716,375,627 ikiwa ni asilimia 42 ya gharama ya mradi.

  Uhaba wa maji safi na salama umelikumba jimbo la Chalinze kwa kipindi kirefu. Kwa sasa wanaopata huduma ya maji safi na salama ni 220,241, mradi ukikamilika, watakaopata huduma hiyo watafikia jumla ya 234,394.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi. Irina Bokova, katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, leo ametaka wananchi mbalimbali kutenga muda binafsi na kutembelea moja ya maeneo ambayo ni urithi wa dunia yakifadhiliwa na UNESCO.

  Amesema anaamini kuwa kwa wananchi kushiriki watashawishika kuendelea kuishi kwenye maeneo hayo na kuyaenzi.

  Amesema kitendo hicho kidhati kitakuwa kimewaunganisha watu na asili na hivyo kuondoa dhana ya zamani ya kuweka maeneo hayo mbali na watu.

  “Inaweza kuwa vigumu kuamini sasa, lakini miaka hamsini iliyopita ilidhaniwa kuwa njia bora ya kulinda asili ni kuiweka mbali na watu ...Hii leo, tunajua vyema zaidi kwamba kwa kadri uhusiano baina ya watu na mazingira yao unavyokuwa wa karibu zaidi ndivyo watu wanavyofahamu zaidi juu ya umuhimu wa asili na viumbe hai, urithi na maji, kwa ajili ya ustawi wao binafsi na kwa ajili ya hali ya baadaye ya sayari yetu.” Alisema.

  Mkuu huyo alisema hayo akizungumzia umuhimu na uhifadhi kwa maeneio zaidi ya 2000 duniani ya bayongahewa, maeneo ya hifadhi ya jiolojia ya na maeneo ya Urithi wa Dunia yanayodhaminiwa na UNESCO.

  Alisema maeneo hayo pamoja na kuhifadhi urithi wa dunia pia hutoa ajira kwa watu wanaoyazunguka na milango yake iko wazi kwa umma wote.

  “Maeneo ya hifadhi ya jiolojia ni vitabu vilivyo wazi vya kihistoria ambavyo huturudisha nyuma mamilioni ya miaka. Hifadhi za Bayongahewa ni mahali ambapo jamii hukabiliana na changamoto za maendeleo kwa kuunda njia mpya za kijamii na uchumi endelevu. Maeneo ya hifadhi ya jiolojia na hifadhi za Bayongahewa huunganisha uhifadhi na elimu kwa mbinu mpya ya maendeleo endelevu, kama vile utalii wa mazingira na kilimo hai.” alisema katika ujumbe wake kwa dunia.

  Aliwataka wananchi kuheshimu mazingira ya asili hutokana na uelewa.

  Aliwataka wananchi kupitia katika tafakari ya kina kujitumbukiza katika Bustani ya Kiajemi ya Iran ambako maji hufanya ishara za maumbo ya mapambo mbalimbali.

  Aidha alisema vyema kuona eneo la hifadhi ya jiolojia la UNESCO la Tumbler Ridge nchini Canada, na kuogelea katika maziwa ya Alpine yenye maji angavu kama kioo na kulala chini ya nyota.

  Pia amewataka kufanya safari ya kutembea kwa miguu katika hifadhi ya Bayongahewa ya Mujib huko Jordan ambayo ipo mita 420 chini ya usawa wa bahari ikiwa karibu wake na Bahari ya Chumvi.

  Mkuu huyo wa Unesco ametaka wakazi wa dunia hii wakati wakiadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, kutumia ipasavyo maeneo teule ya UNESCO kila mahali kuungana na asili inayowazunguka na inayoleta uzuri, maana na amani katika maisha.

  0 0

   Katibu  mkuu wa Chama cha Wananchi CUF ,Maalim Seif Sharif Hamad  akiwasili katika eneo la Vingunguti
    Katibu  mkuu wa Chama cha Wananchi CUF ,Maalim Seif Sharif Hamad akiwa ameketi kwenye kiti wakati alipojumuika kwenye futari na wakazi wa Vingunguti
   katibu mkuu maalim Seif Sharif Hamad akiwa amejumuika na  wakazi wa vingunguti katika futari katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani .
  katibu mkuu maalim Seif Sharif Hamad alijumuika na wakazi wa vingunguti katik futari  na wakazi wa vingunguti

  0 0


  NA KVIS BLOG/Khalfan Said

  MANISPAA ya Ilala jijini Dar es Salaam imesema iko kwenye mkakati mkubwa wa kutengeneza bustani za kupumzika wananchi na tayari wameanza kuboresha maeneo hayo kwa kuanzia na eneo bustani ya Samora (Kaburi la Sharif), barabara ya Samora.

  Akizungumza kwenye mdahalo wa mazingira uliotayarishwa na Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue Institute ya jijini Dar es Salaam leo Juni 5, 2017, Afisa Mazingira wa Manispaa hiyo, Bi.Esther Masomhe, alisema, pamoja na vipaumbele vingi ambavyo Manispaa hiyo inakabiliwa navyo, lakini moja ya hatua inazochukua ni kupendezesha jiji, (City beatification).

  “Kuna maeneo tayari tumeanza nayo kama vile bustani ya Samora pale kaburi la Shariff, barabara ya Samora, bustani ya Mnazi Mmoja namba mbili eneo laMcahfukoge, tunakusudia kuiboresha bustani hiyo ili wananchi wapate mahala pazuri pa kupumzika.” Alisema Bi.Masomhe.

  Akifafanua zaidi alisema, Wilaya ya Ilala ndiyo kitovu cha jiji la Dar es Salaam hivyo Manispaa inachukuajuhudi mbalimbali kuhakikisha wilaya hiyo inakuwa katika muonekano mzuri kwa kuboresha mazingira na bustani zake.

  Aidha Afisa huyo wa Mazingira wa wilaya ya Ilala alisema, kwa kuzingatia kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani, ““Hifadhi Mazingira, kama Muhimili wa Maendeleo ya Viwanda”

  “kauli mbiu hii ina maana kuwa viwanda vingi hapa nchini vimejengwa bila kuzingatia uhifadhi wa mazingira, utakuta mtu mwenye kiwanda, anashindwa kuhifadhi maji taka anayozalisha na badala yake anatiririsha kwenye mito, ambako huko kuna viumbe hai, sihilo tu lakini pia kuna watu wanaendesha kilimo cha mboga mboga, kwa vile maji wanayotumia ni hayo hayo ya mto ambayo tayari yanakuwa yamechanganyika na maji taka ya viwandani, walima bustani hutumia maji hayo kunyweshea bustani zao na hivyo kuwalisha wananchi mboga mboga zenye kemikali, nah ii ni hatari kwa afya,” alisema

  Alisema kwakuwa sheria zipo wazi, watasimamia sheriahizo kikamilifu ili kuhakkiikisha kiwanda kitakachoanzishwa kwenye Manispaa knazingatia uhifadhi wa mazingira.

  Naye Mwenyekiti wa mdahalo huo, ambaye pia ni mdhamini wa taasisi hiyo ya Kilimanjaro Dialogue Institute, Bw. Habib Miradji amesema, “hakuna mtu ambaye hafahamu umuhimu wa mazingira, lakini kumekuwepo na tatizo kubwa la kimazingira, sisi tunaetembea dunia tunaona kuna milima misitu ya asili na mbuga, kwa kweli inabidi ukae ufikirie jinsi maliasili ilivyotunzwa, lakini hapa kwetu, vitu kama hivi havipo, ilikuwa zamani tu maana hata milio ya ndege na miti asili imetoweka.” Alisema.

  Bw. Miradji alihoji nini mikakati ya Manispaa katika uhifadhi wa mazingira kwani maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu hususan uswahilini, (urban slams) haya yanakuwa na ongezeko la watu kwa haraka, familia moja inawezakuwa na watu 10 na zaidi, nini mkakati ya Manispaa katika kukabiliana na misongamano ya watu?

  Akijibu hoja hiyo Bi. Masomhe alsiema, kumekuwepo na mikakati mbalimbali ikiwemo ya utoaji elimu mashuleni, kupitia klabu za mazingira za shule, lakini pia kuboresha miundombinu kwenye maeneo hayo na kutoa elimu kwa wakazi wa maeneo hayo kupitia kwa maafisa afya wa Manispaa ambao hutembelea mara kwa mara ili kutoa elimu ya usafi wa mazingira.
  Afisa Mazingira wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Bi.Esther Masomhe, (kulia), akizungumza jambo wakati wa mazungumzo ya meza ya duara kuhusu mazingira kwenye Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Juni 5, 2017, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya mazingira duniani. Kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue Institute iliyoandaa majadiliano hayo, Bw. Habib Miradji. 
  Bi.Esther Masomhe, akizungumzia mikakati ya Manispaa yake kuhusu mazingira na utunzaji wake
  Mwenyekiti wa mdahalo huo, ambaye pia ni mdhamini wa taasisi hiyo ya Kilimanjaro Dialogue Institute, (KDI), Bw. Habib Miradji 
  Mshauri wa masuala ya vyombo vya habari, Bw. Felix Kaiza akisikiliza kwa makini mjadala huo.
  Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue Institute (KDI), Bw.Hassan Mzighani, (kulia), akizungumza kwenye mdahalo huo ambapo alisema anasikitishwa na jinsi Manispaa inavyoshindwa kudhibiti maji taka, yakiwemo yale yanayosababishwa na mvua na kutolea mfano nchi kama Norway, ambayo hupata mvua muda mwingi lakini sio rahisi kukuta barabara au makazi ya watu yakiwa yamezingirwa na maji.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua kiwanda cha kutengenezea Chaki cha Arwa kilichopo Tarime.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna chaki zinavyotengenezwa kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Arwa Bw. Tobias Raya mara baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho kilichopo Tarime mkoani Mara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna chaki zinavyotengenezwa kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Arwa Bw. Tobias Raya mara baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho kilichopo Tarime mkoani Mara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna chaki zinavyotengenezwa kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Arwa Bw. Tobias Raya mara baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho kilichopo Tarime mkoani Mara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa kijiji cha Bisarwi kata ya Manga, Tarime  mkoani Mara.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
   
   

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi waache tabia ya kuhujumu miradi ya maendeleo ikiwemo ya wawekezaji kwani kufanya hivyo ni kurudisha nyuma jitihada za Serikali za kuharakisha shughuli za maendeleo za wananchi.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wilayani Tarime mkoani Mara wakati akikagua miradi ya maendeleo, kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda cha chaki,kutembea eneo litakalojengwa kiwanda cha sukari na kwenye mkutano wa hadhara kijijini Biswari wilayani humo katika ziara yake ya kikazi ya siku Tatu mkoani Mara.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema tabia ya wananchi kupinga kila kitu hata uwekezaji haifai hata kidogo kwani inachangia kuzorotesha shughuli za maendeleo hivyo ni lazima ikomeshwe.

  Amewataka wananchi kote nchini washirikiane na Serikali pamoja na wawekezaji wanaokuja nchini kuja kuwekeza kwani kufanya hivyo taifa litapata mapato na wananchi watapata ajira kwenye viwanda vitakavyojengwa nchini.

  Akihutubia wananchi wa kijiji cha Biswari katika mkutano wa hadhara, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameunga mkono kauli ya wananchi wa Tarime ya kutaka kuharakishwa kwa ujenzi wa kiwanda cha Sukari katika Bonde la Mto na kusema uwekezaji huo utaongeza maradufu mapato ya halmashauri ya Tarime na kutoa ajira nyingi kwa wananchi wa mkoa huo.

  Amesema ataiagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuharakisha mchakato wa kutoa vibali ili shughuli za kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda hicho cha miwa kujengwa haraka na kuanza kufanya kazi kwa ajili ya manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.

  Wawekezaji hao kutoka nchini Uganda wanataka kujenga kiwanda sukari kitakachogharimu zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 200 na kuanzisha kilimo cha miwa kwenye eneo la ekari zaidi ya elfu 30 katika bonde la Mto wilayani Tarime.

  Kuhusu kilimo cha bangi wilayani Tarime, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewaagiza wote wakaze kamba katika kupambana na kilimo hicho ili kikomeshwe wilayani huo.

  Amesisitiza viongozi katika ngazi zote na wananchi kwa ujumla washirikiane katika kukomesha kilimo hicho ambacho kimekithiri wilayani Tarime.

  Kuhusu Kero ya maji wilayani Tarime, Makamu wa Rais amesema Serikali inatambua tatizo hilo na itafanya kila inavyowezekana ili kuondoa kero ya maji kwa wananchi wa wilaya ya Tarime.

  Amesema Serikali imejipanga vyema katika kuhakikisha tatizo la maji linakuwa historia nchini kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maji ili kuhakikisha wananchi wanafanya kazi za kiuchumi ipasavyo badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji. Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt Charles Mlingwa amemhakikishiwa Makamu wa Rais kuwa Serikali ya mkoa huo imejipanga vyema ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kijamii kwa wakati pamoja na kuimarisha hali ya ulinzi usalama kwa wananchi mkoani humo.

  0 0  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akisaini mkataba wa kuipatia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) fedha za kuiongezea mtaji kiasi cha shilingi bilioni 209.5. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw. Francis Assenga, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam
  td2
  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sheria kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Eligius Mwankenja (kushoto), na Mchumi kutoka Wizara hiyo  Bw. Said Nyenge (kulia) wakiwaelekeza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bw. Francis Assenga, maeneo maalumu ya kutiwa saini kwenye Mkataba wenye thamani ya Sh. 209.5 bilioni utakaoiwezesha Benki hiyo kutoa mikopo ya muda wa kati na mrefu kwa riba nafuu kwa wakulima wadogo wadogo, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam
  td3
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto) akibadilishana mkataba na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania-TADB, Bw. Francis Assenga mara baana ya kusainiwa mkataba wa kuiongezea mtaji Benki hiyo wenye thamani ya Sh. Bilioni 209.5 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/2021, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
  td4
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu wakionesha mkataba waliokwisha usaini kwa waandishi wa habari (hawamo pichani) na kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam
  td5
  Wajumbe waliohudhuria hafla ya utiaji saini mkataba wa kuiongezea mtaji Benki ya Kilimo wenye lengo la kuunganisha maboresho ya sekta ya kilimo na mpango wa mageuzi ya viwanda wenye thamani ya Sh. 209.5 bilioni, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
  td6
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto) akitoa ufafanuzi wa maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari (hawamo pichani) na kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania-TADB, Bw. Francis Assenga, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam
  td7
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania-TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) akiongea na waandishi wa habari pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo (hawamo pichani).
  td8
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania-TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) akiongea na waandishi wa habari pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo (hawamo pichani).
  td9
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania-TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) akiongea na waandishi wa habari pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo (hawamo pichani).
  td10
  Wajumbe wa Bodi wakifuatilia kwa makini zoezi la utiaji saini mkataba wa Serikali kuipatia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) shilingi bilioni 209.5. kwa ajili ya kuiongezea mtaji. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya TADB Bw. William Mhoja, Mkurugenzi wa Fedha na TEHAMA – TADB Bw. Severin Ndaskoi, Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha Bw. Albert Ngusaru, Mkuu wa Idara ya Utimilifu-TADB, Bw. Adam Kamanda, Mkaguzi wa Ndani Mkuu Bi, Joyce Maduhu, na Mkurugenzi wa Mikopo wa TSDB, Bw. Augustino Matutu.
  …………………………………………………………………………
  Benny Mwaipaja, WFM- Dar es Salaam
  SERIKALI imeipatia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), shilingi 209.5 bilioni kwa ajili ya kuendeleza Sekta ya Kilimo na Mifugo hapa nchini, leo, Jijini Dar es salaam.
  Akiongea kwa niaba ya Serikali wakati wa tukio la utiaji saini mkataba wa makabidhiano ya fedha hizo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, alisema kuwa kiasi hicho cha fedha ambacho ni mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), ni sehemu ya shilingi 800 bilioni ambazo Serikali inatarajia kuipatia Benki hiyo ili iweze kukuza mtaji wake.
  “Ninaishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB kwa kuipatia Serikali mkopo wa Dola za Marekani 93.5 milioni ambazo ni sawa na kiasi hicho cha fedha cha Sh. 209.5 bilioni kwa ajili ya kuiongezea mtaji TADB ili iweze kuwafikia wakulima wengi zaidi kwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu” alisema Dkt. Kazungu.
  Alisema kuwa fedha hizo zitasaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya sekta ya kilimo na mifugo ili kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo ili sekta hiyo iweze kuchangia zaidi katika ukuaji wa pato la Taifa kuliko ilivyo sasa.
  “Mwaka jana kilimo ambacho kinategemewa na idadi kubwa ya Watanzania kilichangia wastani wa asilimia 29.1 ya Pato la Taifa lakini tunataka kupitia Benki hiyo Sekta ya kilimo iiwezeshe nchi kukua kiuchumi kwa zaidi ya asilimia 7 hadi 10 katika kipindi kifupi kijacho” aliongeza Dkt. Kazungu.
  Akiongea baada ya kutia saini makubaliano ya kupokea fedha hizo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB), Bw. Francis Assenga, ameishukuru Serikali kwa kuiongezea Benki yake mtaji utakaotumika kuendeleza Sekta ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Ufugaji nyuki.
  Alisema kuwa kiasi hicho cha fedha kitaiwezesha Benki hiyo ambayo imekwisha wafikia wakulima zaidi ya 3,700 hapa nchini, kuanza kutoa mikopo ya muda mrefu kwa wakulima wadogo na wa kati ili kuinua Sekta hiyo kwa kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao yatokanayo na kilimo na mifugo.
  Ameihakikishia Serikali kwamba Benki yake itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa matunda ya fedha hizo yanaonekana na kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Ras Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwakwamua wananchi wake katika lindi la umasikini.
  “Riba za Mikopo ya Benki yetu ziko chini ikilinganishwa na Benki nyingine ambapo sisi tunatoza asilimia 8 hadi 12 kwa wakulima wadogo na asilimia 15 kwa wakulima wa kati wenye viwanda wakati viwango vya riba katika soko ni asilimia 18 na wakati mwingine vinafika hadi asilimia 40.” alisema Bw. Assenga wakati akijibu maswali ya wanahabari.

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB , Ineke Bussemaker (kulia) baada ya kupokea mfano wa hundi wa gawiwo la shilingi bilioni 16.5 ambazo Serikali kama mwanahisa imepata katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa wanahisa wa Benki hiyo uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya Benki hiyo ambayo kwa mwaka ulioishia Disemba 31,2016 ilipata faida ya shilingi bilioni 153.8 licha ya changamoto za kibenki, likiwa ni ongezeko la asilimia 2, ukilinganisha na mwaka 2015 ambapo ilipata faida ya shilingi bilioni 150.3.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Isdor Mpango (Mb) akiishukuru Benki ya NMB kwa kutoa gawiwo la shilingi bilioni 16.5 kwa Serikali wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa wanahisa uliofanyika jijini Dar es Salaam .
  Wanahisa wa Benki ya NMB wakiwa katika Mkutano wao Mkuu wa Mwaka ambapo uliofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo Benki hiyo imetangaza jumla ya shilingi bilioni 52 kama gawiwo kwa wanahisa wote. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

  …………………………………………………………………….

  Benki ya NMB imepata faida ya ya shilingi bilioni 153.8 kwa mwaka 2016 hivyo kuiwezesha kutoa gawiwo la shilingi bilioni 16.5 kwa Serikali ambayo inamiliki asilimia 32 ya hisa za Benki hiyo.

  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) alikabidhiwa hundi kifani ya gawiwo hilo katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa wanahisa wa Benki hiyo uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

  Dkt. Mpango amezipongeza juhudi za watendaji wa Benki hiyo waliofanikisha kupatikana kwa faida iliyowezesha Serikali kupata gawiwo. Aidha, Serikali inajivunia mafanikio makubwa ya kiutendaji ya NMB na uwekezaji wake ambao unatija na unaifanya serikali isijutie uamuzi wake wa kuibinafsisha Benki hiyo.

  Amesema fedha hizo zilizopatikana kutokana na gawiwo zitaelekezwa kwenye maendeleo ili kutatua baadhi ya kero zinazowakabili wananchi.

  Ameahidi kuwa, Serikali kama mwanahisa itaendelea kuitumia Benki hiyo kikamilifu katika huduma za kibenki ili kuiwezesha kuongeza mapato.

  “Shughuli ambazo Serikali itazifanya kupitia NMB Bank Plc ni pamoja na malipo ya mishahara ya wafanyakazi wa Umma na pia kukusanya mapato ya Serikali yanayotokana na kodi na yasiyo ya kodi.

  Waziri Mpango ametumia nafasi hiyo kuagiza kampuni ambazo zenye ubia na Serikali kuiga mfano wa NMB Benki Plc na kupeleka gawiwo katika faida wanayopata.

  “Katika Serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli haiingii akilini kusikia kila mwaka mnapata hasara lakini mpo hamtoki, tumevumilia vya kutosha sasa imetosha, haiwezekani unawekeza miaka 10 lakini watanzania hawapati chochote” alionya Dkt. Mpango.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ineke Bussemaker amesema jumla la gawiwo lote litakalolipwa kwa wanahisa ni shilingi Bilioni 52 kiwango ambacho kinaendana na sera ya Benki ya kutoa theluthi moja ya asilimia 33.3 ya faida baada ya kodi kwa wanahisa wake.

  Bussemaker alisema kuwa mafanikio ya Benki hiyo katika mwaka ulioishia Disemba 31,2016 ilipata faida ya shilingi bilioni 153.8 licha ya changamoto za kibenki, likiwa ni ongezeko la asilimia 2, ukilinganisha na mwaka 2015 ambapo ilipata faida ya shilingi bilioni 150.3

  Wanahisa wa Benki hiyo wamekubaliana kubadili jina la Benki hiyo kutoka National Microfinance Bank na kuwa NMB Bank Plc. Waziri mpango amesema mapendekezo ya kubadili jina yalifika Serikalini na Serikali imeridhia.

  Hii itakuwa mara ya pili kwa Serikali kupata gawiwo kutoka Benki ya NMB ambapo mwaka uliopita, Benki hiyo ilitoa gawiwo la kiasi kama hicho cha shilingi bilioni 16.5 baada ya kutengeneza faida.

  0 0


  0 0

   Barclays Tanzania Chief Finance Officer, Obedi Laiser (centre), talking to some University of Dar es Salaam (UDSM) students about the career opportunities being offered by Barclays and introduce them to an exciting scholarship program that will allow students the opportunity of receiving one full year of tuition fees and other student fees paid by BBT. It was during the banks career fair day at the University of Dar es Salaam Business School premises in Dar es Salaam at the weekend. On his left is Barclays Head of Marketing and Corporate Relations, Aron Luhanga and Dakshit  Pandya (on the right), the banks Head of IT and Change. 
   Barclays Tanzania Head of Learning and Leadership Training, Veronica Muumba (right), talking to some University of Dar es Salaam (UDSM) students about the career opportunities being offered by Barclays and introduce them to an exciting scholarship program that will allow students the opportunity of receiving one full year of tuition fees and other student fees paid by BBT. It was during the banks career fair day at the University of Dar es Salaam Business School premises in Dar es Salaam at the weekend.
   Barclays Bank Tanzania Head of Marketing and Corporate Relations, Aron Luhanga (right), talking to some University of Dar es Salaam (UDSM) students during the banks career fair day at the University of Dar es Salaam Business School premises in Dar es Salaam at the weekend. A group of Barclays employees were also at the University to equip the students with important life and professional skills. 
   Barclays Bank Tanzania Head of IT and Change, Dakshit Pandya (right),  talking to some University of Dar es Salaam (UDSM) students during the  banks career fair day at the University of Dar es Salaam Business School premises in Dar es Salaam at the weekend.
   Barclays Bank Tanzania Head of Human Resources, Patrick Foya (left)   talking to some University of Dar es Salaam (UDSM) students during the function.
   Barclays Bank Marketing and Communications Manager, Joe Bendera (right), giving some hints on some career opportunities being offered by Barclays during the career day event at the UDBS hall at the Hill.

   A cross section of UDSM students during the Barclays career fair event in Dar es Salaam at the weekend.
  Some Barclays employees poses for a moment photograph with the students.

  0 0

  Muonekano wa Daraja la Chilonwa lililopo kata ya Chilonwa, wilayani Chamwino mkoani Dodoma. Daraja hilo ni kiungo kati ya mkoa wa Dodoma, Manyara na Arusha.
  Sehemu ya daraja la Chilonwa iliyoathirika kutokana na shughuli za kibinaadamu kama vile kilimo na hivyo kupelekea kwa daraja hilo kufukiwa na mchanga na kuwa fupi.


  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani, akisalimia wananchi wa kata ya Chilonwa, wilayani Chamwino mkoani Dodoma alipotembelea wilayani hapo leo, ikiwa ni kutekeleza ahadi yake ya kukagua daraja la Chilonwa kwa Mbunge wa jimbo la Chilonwa, Mhe. Joel Makanyaga.
  Mbunge wa jimbo la Chilonwa, Mhe. Joel Makanyaga, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani (kushoto kwa Mbunge), alipofika jimboni hapo kukagua daraja la Chilonwa, wilayani Chamwino mkoani Dodoma leo.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani, akizungumza na wananchi wa kata ya Chilonwa, wilayani Chamwino mkoani Dodoma leo mara baada ya kukagua daraja la Chilonwa lililopo mkoani humo
  . ………………………………………………………………..

  Wananchi wa kata ya Chilonwa, wilaya Chamwino mkoani Dodoma wameiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kujenga daraja la Chilonwa lililopo katika kata hiyo ili kutatua kero ya usafiri kwa wananchi hao na maeneo jirani hususan katika kipindi cha masika.

  Wakieleza kero yao kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, wananchi hao wamesema wanaamini kuwa ujio wa Naibu Waziri huyo katika kata yao kutaleta ufumbuzi wa kero hiyo.

  “Tunaamini sasa tutapata mwarobaini wa daraja hili kwani tatizo hili ni la muda mrefu, siku hadi siku daraja linakuwa fupi kutokana na kufukiwa na mchanga na hivyo hupelekea maji kujaa darajani hapa kipindi cha masika na watu kushindwa kuvuka”, amesema mmoja wa wananchi hao.

  Aidha, wananchi hao wamemwomba Naibu Waziri huyo kurekebisha daraja hilo kwa kulijenga juu zaidi ili kupitisha maji na kupitika katika vipindi vyote vya mwaka kutokana na kwamba lililopo sasa lipo chini zaidi mara baada ya kufukiwa na mchanga.

  Wananchi hao wameeleza masikitiko yao kwa Naibu Waziri huyo hususan katika kipindi cha masika ambapo wamesema hutumia kiasi cha shilingi elfu kumi kuvushwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine na wengine hupoteza maisha wakiwa wanavuka.

  Sambamba na hilo wananchi hao wamependekeza kuwa ujenzi wa daraja hilo uhusishe wataalamu waliobobea na ambao watahakikisha daraja hilo linakamilika mapema na kwa viwango.

  Kwa upande wake Naibu Waziri Ngonyani, amewataka wananchi hao kuacha tabia ya kufanya shughuli za kibinaadamu kama kilimo katika njia ya mto kwani hali hiyo hupelekea udongo kumung’unyuka na hatimaye mchanga kufunika daraja.

  Amemtaka Mbunge wa jimbo la Chilonwa, Mhe. Joel Makanyaga, kwa kushirikiana na viongozi wa kata na kijiji kuhamasisha wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinaadamu kando ya mto.

  Amefafanua kuwa Wizara yake kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani Dodoma itahakikisha kwanza ina utengeneza mto huo kwa kuelekeza maji yote katika mto.

  Naye, Mbunge wa jimbo la Chilonwa, Mhe. Joel Makanyaga, amempongeza Naibu Waziri huyo kwa kutembelea jimboni hapo na kuahidi kuwasimamia wananchi wake katika kulinda miundombinu hiyo.

  Naibu Waziri Ngonyani leo ametembelea na kukagua Daraja la Chilonwa, wilayani Chamwino mkoani Dodoma ikiwa ni kutekeleza ahadi yake ya kutembelea na kukagua daraja hilo kwa Mbunge wa jimbo la Chilonwa, Mhe. Joel Makanyaga.

  0 0


  Wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali za sekta ya Uchukuzi jana wakifanya usafi ndani ya soko la Mabibo, wakishirikiana na wananchi ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, iliyoadhimishwa jana
  Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakifagia nje ya uzio wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani iliyofanyika jana kwa kusafishwa mazingira hayo na ndani ya soko la Mabibo.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dk. Leonard Chamuriho aliyekuwa Mgeni rasmi akiwahutubia wafanyakazi wa taasisi zilizopo chini ya sekta hiyo, kabla ya kuanza kwa zoezi la kufanya usafi wa mazingira kwenye Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) na Soko la Mabibo, ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani iliyoadhimishwa jana.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho akimwagilia maji mti aliopanda ndani ya Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), ikiwa ni moja ya kazi zilizofanyika jana kwenye kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, iliadhimishwa kwa kufanyika usafi maeneo ya nje ya chuo hicho na soko la Mabibo.
  Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege vya Mikoa (DRA), Bw. Valentine Kadeha (katikati) akishirikiana kupanda mti na wanafunzi wa shule ya Mpakani ya Mabibo, katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, iliyoadhimishwa jana kwa wafanyakazi wa taasisi mbalimbali wa Sekta ya Uchukuzi kufanya usafi nje ya Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) na Soko la Mabibo.
  Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakiungana na wenzao kutoka taasisi mbalimbali za Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) jana kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira kwenye Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) na Soko la Mabibo ikiwa jana ni Siku ya Mazingira Duniani. 


  0 0

  Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

  Wakazi wa Mkoa wa Tabora wametakiwa kuweka akiba ya chakula cha kutosha ili kuepuka njaa inayoweza kuwakabili kutokana na mavuno ya msimu huu kutokuwa mazingira kufuatia mvua kuchelewa kuanza na kuwahi kukatika.

  Wito huo umetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri wakati wa kilele cha maadhimisho siku ya mazingira duniani ambapo kimkoa yalifanyika katika Manispaa ya Tabora.

  Alisema mvua za msimu huu zilikuwa kidogo na hivyo mavuno ya mazao kama vile mahindi , mpunga na maharagwe ni hayaridhishi hivyo ni vema wananchi wakahakikisha wanatenga chakula cha kutosha kwa ajili ya matumizi yao kabla ya kuanza kuuza.

  Mkuu huyo Mkoa alisema kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara kutoka Mikoa mbalimbali wamekuwa wakipita katika maeneo mbalimbali ya vijiji na kuwarubuni wakulima wawauzie mahindi yao nao bila kuchukua tahadhari wanafanya wamekuwa wakiuza bila kuweka akiba ya kutosha jambo ambao sio jema.

  Aliongeza kuwa watu aina hiyo ambao wanakimbilia kuuza mahindi yao bila kuweka aakiba ya kutosha kwa ajili ya familia zao ndio wamekuwa wakimbilia kwa viongozi wa Serikali wanaishiwa chakula.

  Mkuu huyo wa Mkoa alisisitiza kuwa ameamua kuwatahadharisha mapema ili kila mkazi wa Tabora akatumia fursa hii ya upatikanaji wa vyakula vya kutosha katika masoko kuweka akiba kwa ajili ya familia zao badala ya kukaa ili kugonja msaada na wakati mwingine kulaumu Serikali bila sababu za msingi.

  “Nawaombeni tunzeni chakula mlichokipata kwa ajili ya matumizi ya baadaye badala kukimbilia kuuza na kutengenezea pombe za kiinyeji…jambo hili ni hatari kwa kuwa unapokosa chakula unageuka mtumwa na wakati mwingine unaweza hata kudhalilishwa na mtu mwenye chakula” aliwatahadharisha wakazi wa Tabora

  Aidha Bw. Mwanri aliwaagiza Wakuu wa Wilaya zote kuhakikisha wanasimamia zoezi la kufanya tathimini ya chakula kilichopo katika maeneo yao na kuhakikisha hakuna uuzaji wa holela holela wa mahindi ili kuchukua tahadhari ya kukabiliana na tishio upungufu wa chakula kwa wakazi wa Tabora.

  Alisema kuwa mtu asiuze chakula kama hana akiba inayoweze kumfikisha mkulima katika mavuno ya msimu ujao.

  Bw. Mwanri alisisitiza kuwa Wakuu hao wa Wilaya wahakikishe viongozi wote wa Serikali za Vijiji na Mitaa wanasimamia zoezi la kuhakikisha kuwa mtu anayeuza mahindi anayo akiba ya kutosha na sio vinginevyo ili kuepuka tabia ya watu kukimbilia kuuza mahindi hivi sasa wakiishiwa wanaanza kukimbilia kwa viongozi.

  0 0


older | 1 | .... | 1260 | 1261 | (Page 1262) | 1263 | 1264 | .... | 1897 | newer