Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1262 | 1263 | (Page 1264) | 1265 | 1266 | .... | 1898 | newer

  0 0


  0 0

  Frank Mvungi- Maelezo
  Serikali imetumia shilingi bilioni 16.9 kununua vifaa vya maabara na vile vya wanafunzi wenye mahitaji maalum vitakavyonufaisha shule za sekondari 1696 ambapo shule 1625 ni za Kata na 71 ni kongwe ambazo kwa sasa zipo katika ukarabati.

  Akihutubia wakati wa hafla ya kuzindua  mpango wa  kusambaza vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum leo Jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi, amesema dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa inaboresha sekta ya elimu  ili azma ya ujenzi wa Tanzania ya Viwanda itimie kwa kuwa Taifa litaweza kuzalisha wanasayansi kulingana na mahitaji.

  “Tunatoa vifaa hivi kwa awamu ya kwanza kwa shule zilizokamilisha ujenzi wa maabara, hivyo ni matumaini yangu kuwa wale ambao hawajakamilisha watafanya hivyo ili awamu ijayo nao wapate vifaa hivi.” Alisisistiza Majaliwa.

  Aliongeza kuwa dhamira ya serikali ni kuhakikisha zaidi ya shule 4,000 nchini zinakuwa na vifaa vya maabara, walimu, vifaa vya kujifunzia na kufundishia na mazingira rafiki ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora itakayowasaidia kushiriki katika ujenzi wa Taifa.

  Pia Waziri Mkuu ameonya kuwa Serikali itachukua hatua kali dhidi ya mtu yoyote atakaye sababisha mwanafunzi wa kike kupata ujauzito na kushindwa kuendelea na masomo ambapo atakabiliwa na adhabu ya kwenda jela miaka thelathini.

  “Awe baba au mama au mtu yoyote ambaye itathibitika kuwa amemsababishia ujauzito mwanafunzi, adahabu yake ni kifungo cha miaka thelathini jela.” Alisisitiza Majaliwa.

  Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema Serikali imetenga fedha katika bajeti ya mwaka 2017/2018 kwa ajili ya kuendelea kununua vifaa hivyo lengo likiwa kuendelea kuinua kiwango cha elimu kwa kushirikisha wadau wa maendeleo.

  “Vifaa hivi vinakidhi mahitaji ya wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita na upatikanaji wa vifaa hivi ni utekelezaji wa ahadi ya serikali ya Awamu ya Tano kwa wananchi katika kuboresha sekta ya elimu na vitawaongezea wanafunzi kasi ya kudadisi na  kujifunza.” Alisisistiza Prof. Ndalichako.

  Akifafanua kuhusu upatikanaji wa vifaa hivyo Prof. Ndalichako aliwashukuru wadau wa  Maendeleo ikiwemo Benki ya Dunia, Uingereza, Denmark na wengine kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuinua kiwango cha elimu nchini ili kuchochea maendeleo kwa kuwa ufaulu wa masomo ya sayansi utaongezeka.

  Kwa Upande wake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi amesema kuwa  kazi ya kupokea vifaa hivyo imefanyika kwa ufanisi na  kuahidi kuwa watatekeleza jukumu la kusambaza vifaa hivyo kama ilivyopangwa kupitia Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ).

  Vifaa hivyo vya maabara na vile vya wanafunzi wenye mahitaji maalum  vyenye thamani ya shilingi bilioni 16.9 vitasambzwa katika Kanda 11 na baadhi ya mikoa itakayonufaika katika Kanda hizo ni Dar es Salaam, Katavi, Kagera, Rukwa, Pwani, Tanga, Mwanza, Singida, Dodoma.
   Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya walimu na wanafunzi wa shule za sekondari za mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la  usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum  mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
   Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (mwenye tai nyekundu) akipata maelekezo toka kwa moja ya mwalimu wa masomo ya sayansi wakati wa uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum  mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
   Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (mwenye tai nyekundu) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa zoezi la usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
    Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia) akikabidhi moja ya kifaa cha kufundishia masomo ya sayansi kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Juhudi wakati wa uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum  mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakimsikiliza Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum  mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya wanafunzi  wa shule za Mkoa wa Dar es Salaam wakimsikiliza Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum  mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.

  Picha zote na Eliphace Marwa - Maelezo


  0 0  Na Jonas Kamaleki-MAELEZO.

  Zaidi ya vijana wapatao  1230  wametoa siri nzito kwa  Maaskofu na Mashekhe  kutoka katika Kamati ya Kitaifa ya Maadili , Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini  Nchini  kufichua mtandao  haramu  wa watu  wanaoendesha mauaji na uhalifu mwingine kwenye   mikoa  13, nchini kama njia muhimu ya kumpongeza IGP mpya, Saimoni Sirro.

   Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Askofu William Mwamalanga, siri hiyo imetolewa  jana  na vijana hao katika   siku ya  tatu  mkutano wa kujenga maadili kwa vijana unao fanyika Mbagala, jijini Dar es Salaam na kuwashirikisha   vijana  wa madhehebu mbalimbali ya dini  kutoka katika  mikoa ya Pwani, Tanga, Lindi,  Morogoro,Dar es Salaam  ambapo wameyataja maeneo ya Mkuranga, Rufiji  Kigamboni, Kibiti, Msata, Tanga mjini, Pemba na Unguja kuwa maeneo hatari yanayowajengea vijana imani za  kigaidi.

   Aidha, Askofu Mwamalanga alisema kuwa vijana 147  wa kiislamu wanaohudhuria mkutano huo  wamewataja  baadhi ya watu  ambao ni   hatari  na wamekuwa wakieneza elimu ya mauaji  kwenye  misikiti mbali mbali nchini kwa kuiita Serikali ya Awamu ya Tano jina la katili na kwamba elimu hiyo imesambazwa kwa kasi  katika mikoa ya  Kagera, Tanga, Mwanza, Arusha, Pemba, Unguja, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Morogoro, Iringa, Singida, Dodoma, Pwani na Kigoma huku vikosi vya vijana vikiandaliwa kufanya mauaji  mara baada ya mufungo mtukufu wa Ramadhani kama yale ambayo yamekuwa yakifanywa  Mukuranga, Kibiti  na Rufiji. 

  Vijana hao wanamuomba  IGP  Sirro kuwachukulia hatua kali maafisa wa jeshi hilo ambao wanatumia jeshi kupandikiza Umngiki, na  kwamba wana imani na IGP Sirro amabaye kwa mujibu wa hao vijana hatamwangusha Rais  Magufuli na watanzania kwa ujumla.

  Akifunga  Mkutano huo  Askofu Mwamalanga  amemtaja IGP  Sirro kama polisi mahiri wa maadili na jemadali  mweledi wa mapambano hivyo amewataka  vijana kote nchini kumuunga mkono kwa kuwafichua polisi wote wanaoenzi uhalifu. “Tusipofanya hivyo tutakuwa  kama  pipa zuri  tunalo jaza maji wakati tukijua chini limetoboka”,alisema Askofu Mwamalanga na kuongeza kuwa raia wema ni asilimia 99.9  wahalifu ni 0.1   hii ina maana kuwa ukiondoa polisi wahalifu  ndani ya jeshi hilo wahalifu ni wachache mno  mitaani  watayeyuka wenyewe. 

  Aidha,  Askofu huyo amewahimiza vijana na viongozi wa dini kushiriki kwenye mafunzo hayo kote nchini ili  wapewe ufahamu wa elimu ya maadili ya kweli  ili wawe walinzi wa taifa na kupenda amani  na kuweka uchu wa kuchukia rushwa  na kujiwekea  mitazamo ya kupenda kazi za baraka.

  Kiongozi huyo wa dini amekemea vikali nyumba za ibada   kugeuzwa  eneo la mafunzo ya uhalifu kwani ni aibu kwa msikiti au kanisa kufanya  mafunzo ya kigaidi  ndani  ya  nyumba  za ibada  kufanya hivyo ni ibada ya sanamu, watu wa jinsi hiyo hawana uhusiano wowote na Mwenyenzi MUNGU ambaye kusudi lake ni kuondoa uovu kwa mwanadamu.

  Hivi karibuni yametokea mauaji ya viongozi wa Chama Tawala maeneo ya Kibiti, Mukuranga na Rufiji na kufanya wakazi wa maeneo hayo kuishi kwa wasiwasi na mashaka juu ya maisha yao. Wakati akiipishwa kuwa IGP, Kamanda Simon Sirro alisema kupambana na kuondoa uhalifu kwa kushirikiana na raia wema ni moja ya vipaumbele vyake.

  0 0


  Wahasibu zaidi ya 130 kutoka halmashauri za wilaya za mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kati wamepatiwa mafunzo ya Mfumo wa Kielekroniki kuhusu Usimamizi wa fedha ngazi za msingi zikiwemo zahanati,vituo vya afya,hospitali na shule za msingi na sekondari.

  Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS) kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems Strengthening – PS3’ unaotarajiwa kuanza kutumika Julai 1,2017 katika halmashauri mbalimbali nchini.

  Wahasibu hao wanashiriki katika mafunzo yanayofanyika katika ukumbi wa Vigimark Hotel Mjini Shinyanga ambayo yamekutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka PS3,TAMISEMI,Wizara ya afya,wizara ya elimu.

  Mwezeshaji wa Mafunzo hayo, Elizeus Rwezaula ambaye ni Mshauri wa Masuala ya Usimamizi wa Fedha za Umma kutoka Mradi wa HPSS Dodoma,alisema mfumo wa kutumia njia za kielektroniki (kompyuta) katika kuingiza taarifa za kifedha za vituo vya kutolea huduma unasaidia kurahisisha kazi.

  “Katika Afrika Mashariki,Tanzania ndiyo nchi pekee itakayoanza kutumia mfumo huu wa kisasa wa kielektroniki katika uingizaji taarifa za fedha katika ngazi za msingi za kutolea huduma,na umetengezwa na vijana wa hapa nchini ili kuhakikisha kuwa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma (FFARS) unafanikiwa”,alieleza Rwezaula.

  “Tunawashauri wale wanaoendelea kutumia mfumo wa zamani wa ujazaji taarifa kwa kutumia vitabu (manual) waanze kutumia mfumo huu mpya wa uingizaji taarifa kwa mfumo wa kompyuta ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia”,aliongeza Rwezaula.

  Kwa upande Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji,Tathmini na Tafiti Tendaji kutoka PS3, Dk. Suma Kaare alisema mfumo wa ujazaji taarifa kwa njia ya kieletroniki ulipendekezwa na PS3 na tayari serikali imeukubali na utaanza kutekeleza mwezi Julai,2017 katika halmashauri mbalimbali.

  Naye Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago alisema baada ya wahasibu hao kupatiwa mafunzo kuhufu FFARS nao wataenda kutoa elimu kuhusu mfumo kwa watoa huduma wengine wa ngazi za chini.

  Mafunzo ya siku mbili kuhusu mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma (FFARS) kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) yamemalizika leo mjini Shinyanga.

  Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago akizungumza wakati wa mafunzo kuhusu mfumo huo kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems Strengthening – PS3’ unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID)

  Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago akielezea kuhusu mfumo wa kielektroniki katika ujazaji taarifa za fedha katika vituo vya kutolea huduma.

  Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago akizungumza ukumbini

  Mwezeshaji wa Mafunzo ya FFARS ,Elizeus Rwezaula ambaye ni Mshauri wa Masuala ya Usimamizi wa Fedha za Umma kutoka Mradi wa HPSS Dodoma,akitoa mada kuhusu njia/mfumo wa kielektroki katika ujazaji taarifa za fedha katika vituo vya kutolea huduma

  Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Elizeus Rwezaula akionesha kwa vitendo namna ya kujaza taarifa za fedha kwa kutumia njia ya kompyuta/kielektroniki

  Muonekano wa sehemu ya kujazia taarifa katika kompyuta

  Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Elizeus Rwezaula akiendelea kutoa somo

  Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini

  Bwana Elizeus Rwezaula akizungumza ukumbini

  Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji,Tathmini na Tafiti Tendaji kutoka PS3, Dkt. Suma Kaare akizungumza ukumbini ambapo alisema mfumo wa ujazaji taarifa kwa njia ya kielektroniki ulibuniwa na PS3 kisha kuwasiliana na serikali ambayo kwa pamoja wameamua kutekeleza mfumo huo katika halmashauri mbalimbali nchini

  Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akijifunza kwa vitendo jinsi ya kuingiza taarifa za fedha kwa njia ya kielektroniki

  Washiriki wa mafunzo hayo wakijifunza kwa vitendo namna ya kujaza taarifa za fedha kwa kutumia kompyuta

  Mwenyekiti wa mafunzo hayo ya FFARS ,Samson William akizungumza ukumbini wakati akiendesha majadiliano mbalimbali

  Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano PS3, Leah Mwainyekule akielezea utaratibu utakaotumika kwa wakufunzi waliopata mafunzo ya FFARS watakavyokwenda kutoka elimu kuhusu FFARS katika vituo vya kutolea huduma
  Kabla ya kufundishwa njia ya kieletroniki katika kujaza taarifa za fedha,washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika kikundi wakijadili namna ya kujaza taarifa kwa njia ya zamani ya kutumia vitabu.Walijadili namna ya kutunza kumbukumbu za miamala ya kifedha na nyaraka kwa kutumia vitabu
  Washiriki wakiendelea na kazi ya vikundi.Washiriki hao walijifunza pia namna ya kuandika miamala ya kifedha kwenye nyaraka na vitabu vya uhasibu.
  Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji,Tathmini na Tafiti Tendaji kutoka PS3, Dkt. Suma Kaare akifunga mafunzo ya mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS) kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems Strengthening – PS3’ yaliyofanyika kwa siku mbili kuanzia Juni 5,2017- Juni 6,2017katika ukumbi wa Vigirmark Hotel mjini Shinyanga.


  Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

  0 0


  Mhifadhi mwandamizi wa hifadhi ya Taifa ya Ruaha Moronda Moronda akitangaza washindi wa tuzo za uhifadhi mazingira za TANAPA .

  Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza kulia na mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah wakimpongeza mwakilishi wa kikundi cha familia ya Festo Mhanga wa Kilolo kwa kushinda tuzo ya Mazingira ya Tanapa na kuzawadiwa shilingi milioni jana wakati wa kilele cha siku ya Mazingira na utoaji wa Tuzo za TANAPA kwa wananchi wa mikoa ya Iringa , Njombe na Mbeya


  Mgeni rasmi katika kilele cha siku ya mazingira duniani jana Amos Makala mkuu wa mkoa wa Mbeya akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na meneja ujirani mwema wa Tanapa Ahmed Mbugi kushoto .

  Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akitoa salam siku ya Mazingira Duniani mkoani Mbeya .

  Kikundi cha skauti cha elimisha jamii wilaya ya Mufindi wakikabidhiwa hundi ya shilingi milioni 1 toka Tanapa

  Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akitoa salam siku ya mazingira duania

  Na matukiodaimaBlog


  SERIKALI Imewataka wananchi wanaolima kilimo kwenye maeneo oevu maarufu kama vinyungu kutafuta shughuli nyingine ya kufanya nje ya kilimo hicho kulinda mto Ruaha mkuu kukauka.

  Akitoa salam za mkoa wa Iringa wakati wa sherehe ya tuzo ya TANAPA ya uhifadhi mazingira na kilele cha siku ya mazingira Duniani leo maadhimisho yaliyofanyika kwa kijiji cha Madabaga wilaya ya Mbarali mkoa wa Mbeya Jana mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema iwapo ulimaji wa vinyungu utafumbiwa macho mto Ruaha mkuu utaendelea kukauka.

  Alisema kuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa ikolojia ya mto Ruaha mkuu pamoja na hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

  Kwani alisema uhifadhi wa hifadhi ya Ruaha ni pamoja na uhifadhi wa mto Ruaha mkuu hivyo mikoa ya Iringa,Njombe na Mbeya wana wajibu wa kulinda mto Ruaha mkuu na kuchukua hatua kwa wote wanaolima kwenye vyanzo vya maji.
  Wakuu wa wilaya ya Mbeya na Mufindi wakijadili jambo

  Mgeni rasmi katika kilele cha siku ya mazingira duania Amos Makala mkuu wa mkoa wa Mbeya na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na viongozi wengine wakiwasilia uwanja wa maadhimisho ya siku ya mazingira duniani

  Masenza alisema wajibu wa kulinda mto Ruaha mkuu upo mikononi mwa viongozi wote wakianza wale wa serikali za vijiji." Niwaombe sana wananchi wote tuungane kulinda mto Ruaha na jambo hili uwe ni utamaduni wetu na halihitaji suluti "

  Mhifadhi mwandamizi wa hifadhi ya Taifa ya Ruaha Moronda Moronda alisema kwa siku ya mazingira ambayo ni mwaka wa pili kufanyika mikoa ya Njombe,Mbeya na Iringa huambatana na tuzo kwa vikundi na mtu mmoja mmoja anayefanya vema katika uhifadhi.

  Alisema kwa mwaka jana ndipo zoezi la utoaji tuzo lilianzishwa kwa kuwa na washiriki 200 ila idadi ya washiriki kwa mwaka huu imeingezeka hadi kufikia washiriki zaidi ya 500.

  Maronda alisema kuwa uharibifu wa ikolojia ya mto Ruaha mkuu umeendelea kuharibiwa na urejeshaji wa mto unaoharibiwa gharama yake ni kubwa zaidi.

  Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala alisema kimataifa maadhimisho hayo yamefanyika nchini Canada na kitaifa yamefanyika mkoani Mara.

  Hivyo alisema maendeleo ya uchumi wa nchi uende sambamba na uhifadhi wa mazingira na kuwa suala la uchomaji ovyo pamoja na kilimo kisichoendelevu hakitavumilika.

  Alisema tayari makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameunda kikosi kazi kwa ajili ya kunusuru ikolojia ya mto Ruaha mkuu hivyo viongozi wote wanapaswa kusimamia Sheria zilizopo na kuepuka siasa zinazochangia uharibifu wa mazingira.

  " Hivyo nawaomba sana viongozi na wananchi wote kusimamia sheria kwa kutoa elimu na kazi ya kusimamia sheria inatupaswa tuifanye sisi wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya maana sisi hatupigiwi kura.

  Hivyo alisema njia pekee ya kulinda mazingira ni kupanda miti kwa kila wilaya miti milioni 1.5 na kwa kila mkoa miti milioni 15.

  Kuhusu mifugo kuongezeka alitaka senza ya mifugo kufanyika na baada ya hapo ng,ombe zote zitapigwa chapa kuitambua na mifugo iliyopo katika hifadhi kama Ihefu kuondolewa haraka.

  0 0

  Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe wameadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kwa kupanda miti kwenye eneo la Gereza la Kanegere.
  Akiongea baada ya kupanda miti Kaimu Mkurugenzi  Mtendaji (W), Bi Furaha Chiwile amewataka wananchi  na watumishi  kwa ujumla kupanda miti kwa wingi na kuitunza na waepuke kukata miti ovyo  kwani kwa kufanya hivyo wanahatarisha mazingira na  vyanzo vya maji.

  Jumla ya miti 200 ilipandwa lengo likiwa ni kupanda miche 2500 kwenye eneo hilo la magereza. Miche hiyo inayofadhiliwa na TASAF awamu ya tatu inapandwa kwenye Taasisi za serikali  wilayani  Mbogwe.

  Wakati huo huo Afisa Mazingira wa Wilaya Charles  Karibu Tuyi alisema “ Kauli Mbiu ya Siku ya Mazingira    kitaifa ni Hifadhi Mazingira Mhimili kwa Tanzania ya Viwanda”. Amewashukuru watu wote waliojitokeza kupanda miti na amewaomba waonyeshe ushirikiano wa kuitunza  miti hiyo kwani itasaidia sana kutunza vyanzo vya maji.

  Pamoja na  hayo ,Afisa  Mazingira (W)  alikabidhi jumla ya miche 920 kwa mwakilishi wa mkuu wa Gereza  Sgt. Kuyi  Kalulumila ambaye ameahidi kuitunza miche hiyo na amemshukuru Mkurugenzi kwa kulikumbuka gereza hilo kwani lina eneo kubwa na linauwezo wa kutunza miti hiyo.
   Afisa Mazingira (W) Charles Karibu Tuyi akipanda mti kwenye zoezi la upandaji miti ambalo kiwilaya lilifanyikia kwnye gereza la Kanegere wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani 
   Afisa Mazingira(W) Charles Karibu Tuyi akimkabidhi Kaimu mkuu wa Gereza Kuyi Kalulumila miche ya miti inayotakiwa kupandwa kwenye Eneo la Gereza wakti wa Siku ya Mazingira Duniani.
  Baadhi ya Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe Wakiwa Wanapanda Miti na kuimwagilia.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa  hospitali ya wilaya ya Serengeti inayojengwa makao makuu ya wilaya Mugumu.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia mfano wa majengo ya hospitali ya wilaya ya Serengeti inayojengwa makao makuu ya wilaya Mugumu kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Kisaka.

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mbuzi Mugumu Serengeti ikiwa sehemu ya kukamilisha ziara yake ambapo alitumia fursa hiyo kuwashukuru wakazi wa Serengeti na kuwapongeza kwa kutunza mazingira. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameuagiza uongozi wa wilaya ya Serengeti na wa mkoa Mara kukamilisha haraka awamu ya kwanza ya ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo ili kuondoa adha ya wananchi kusafiri kwenda mikoa ya jirani ya Arusha na Mwanza kwenda kupata huduma afya.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo leo 6-June-2017 kwenye mkutano wa hadhara mjini Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara mara baada ya kutembelea ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya  na kuweka jiwe la msingi.

  Makamu wa Rais amesema kutokana na wilaya ya Serengeti kupata wegeni wengi kutoka nje ya nchi ambao wanaenda kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti  hivyo ni muhimu kwa viongozi wa wilaya na mkoa kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo kukamilisha ujenzi huo haraka ili wananchi waweze kupata huduma za afya za uhakika katika wilaya yao.
  Makamu wa Rais amesema kukamilika kwa ujenzi huo wa awamu ya kwanza kutaondoa taabu kubwa wanayopata wananchi wa wilaya ya Serengeti katika kupata huduma ya afya karibu na maeneo yao.

  Katika kuunga mkono jitihada hizo za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Serengeti, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni Tano na amewaahidi wananchi wa wilaya ya Serengeti kuwa atakikisha fedha kutoka Serikalini ambazo zinatakiwa kupelekwa wilayani humo zinapelekwa haraka ili kukamilisha ujenzi huo.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan pia amewataka wananchi kote nchini kuunga mkono jitihada za Serikali za kupambana na rushwa na ufisadi ili kuhakikisha miradi inayotekelezwa inakuwa na manufaa kwa wananchi wote.

  Amewaomba wananchi nchini wasirudi nyuma katika mapambano dhidi ya rushwa bali waendelee kubaini watu wanaofanya vitendo hivyo ili Serikali iweze kuwachukulia hatua kali za kisheria .

  Kuhusu tatizo la mimba mkoani Mara, Makamu wa Rais ameonyesha kuchukizwa na vitendo hivyo na kuomba vyombo vya dola na wananchi kwa ujumla kushirikiana katika kukomesha mimba za utotoni mkoani Mara.
  Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt Charles Mlingwa amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa maelekezo yote anayoyatoa katika ziara yake yatafanyiwa kazi ipasavyo ili kuondoa kero na changamoto zinazowakabili wananchi.

  Mkuu huyo wa mkoa wa Mara ameomba wananchi wa Mkoa wa Mara kuwepa pembeni tofauti zao za kisiasa bali washirikiane na Serikali katika utekelezaji wa miradi yao ya maendeleo.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan bado anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Mara ambapo hapo kesho atafanya ziara katika wilaya za Butiama na Musoma mkoani Mara.

  0 0


  0 0

  MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi akizungumza na wananchi wa Igohole wakati kukadhi gari la kubebea wagonjwa ambalo amepewa na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto 
  MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi sambamba na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa mafinga Charles Makoga wakikata utepe wa gari la kubebea wangonjwa la kituocha afya cha Igohole
  hawa ni baadhi ya wananchi waliojitokeza wakati wa kupokea msaada wa gari hilo la kubebea wagonjwa lilotelewa na mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi kwa kushirikiana na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto 


  Na Fredy Mgunda,Mafinga

  MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi kwa kushirikiana na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wametoa msaada wa gari la kubeba wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya matumizi ya kituo cha afya cha Igohole ya wilayani Mufindi, mkoani Iringa iliyopo katika jimbo lake hilo.

  Gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser lilikabidhiwa kwa uongozi wa halmashauri ya mji wa Mafinga inayosimamia uendeshaji wa kituo hicho katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Igohole, mjini Mafinga.

  Akikabidhi msaada huo Chumi alisema; “napenda ifahamike kwamba gari hilo limenunuliwa na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Uadilifu na uaminifu kwa serilikali ndio umetufanya tushirikiane vyema katika mambo mengi kwa faida ya wananchi wa jimbo langu la Mafinga.”

  Alisema gari hilo la wagonjwa ni rafiki kwa wagonjwa na wajawazito kwa kuwa lina vifaa tiba vinavyoweza kutumika kutolea huduma wakati wakipelekwa hospitalini.

  Baada ya kukabidhi gari hilo, Chumi ambaye ni mbunge wa kwanza wa jimbo hilo jipya, mkoani Iringa alikumbusha vipaumbele vyake kwa wapiga kura wake kuwa ni kuhakikisha jimbo la mafinga mjini linapata huduma bora ya maji, elimu, afya na miundombinu ya barabara.

  Akishukuru kwa msaada huo, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Dk Innocent Mhagama alisema kabla ya msaada huo, kituo hicho cha afya kilikuwa hakina gari hata moja la kubeba wagonjwa.

  “Pamoja na kuhudumia hospitali hiyo ya wilaya, kurikuwa na magari mawaili tu ambayo yalikuwakihudumia vituo vingine 18 vya kutolea huduma katika wilaya hiyo hivyo,” alisema Mhagama.

  Alisema kupatikana kwa gari hilo jipya kutasaidia kuboresha huduma hiyo kwa kuokoa maisha ya wagonjwa na maisha ya mama na mtoto ambayo ni kipaumbele katika utoaji wa huduma za afya.

  Akizungumzia huduma ya mama na mtoto katika hospitali hiyo ya wilaya, Dk Mhagama alisema kwa wastani wajawazito 500 wanajifunga kila mwezi hospitalini hapo.

  “Kati yao wajawazito zaidi ya 100 huwa wanapata huduma za dharula huku wastani wa wajawazito 10 wakipatiwa huduma za rufaa,” alisema dr Mhagama.

  Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Charles Makoga alisema halmashauri yake kwa kushirikiana na mbunge huyo itahakikisha inatekeleza ahadi mbalimbali zilizotolewa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk John Magufuli, mbunge na madiwani ili kuboresha huduma kwa watu wake.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Serengeti Mhe. Marwa Ryoba Chacha wakati wa ziara yake katika wilaya ya Serengeti, Mbunge huyo alimwambia Makamu wa Rais kuwa jimboni kwake wanafanya kazi kwa kushirikiana na Serikali bila kujali itikadi za vyama.

  0 0


  Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Temeke, Eric Kilangwa (wa pili kulia) na Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick wakifurahia baada ya kuzinduzi wa madarasa matano, ofisi ya walimu na eneo la makusanyiko baada ya kufanya ukarabati katika shule ya sekondari Barabara ya Mwinyi iliyopo Buza jijini Dar es Salaam Juni 6 2017. Pamoja nao ni Mwenyekiti wa shule hiyo, Sostenes Nyenyembe (kulia), Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Bam International Africa Noreen Mazalla (kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Emmentrudice Chilewa.(Imeandaliwa na Robert Okanda Blogspot) .

  Sehemu ya Madarasa na eneo lililofanyiwa ukarabati na kampuni ya Bam International Africa.

  Sehemu ya Madarasa na eneo lililofanyiwa ukarabati na kampuni ya Bam International Africa.


  Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Emmentrudice Chilewa akiwatembeza wageni kujionea ukamilishwaji wa mradi wa ukarabati wa madarasa na ujenzi wa eneo la makusanyiko kabla ya kufanya uzinduzi.


  Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Barabara ya Mwinyi alipotembelea mojawapo ya madarasa matano, kampuni hiyo iliyoyakarabati eneo la Buza jijini Dar es Salaam Juni 6 2017. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Emmentrudice Chilewa .

  Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick kulia akipata ufafanuzi wa jambo kutoka kwa Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Bam International Africa Noreen Mazalla alipokuwa akikagua mazingira ya Shule hiyo.

  Juu na chini, Baadhi ya wanafunzi wakionesha umahiri wa kucheza 'Martial Arts' kunogesha hafla hiyo.


  Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Emmentrudice Chilewa akifanya utambulisho wa walimu wa shule kwa wageni.

  Wanafunzi nao wakitambulishwa.

  Waalimu wa shule hiyo wakimtambulishwa kwa wageni na viongozi.

  Meneja Maendeleo ya Biashara, Kampuni ya Bam International, Noreen Mazalla akimtambulisha Meneja Ubora kwa Afrika wa kampuni hiyo, Lily Naah.

  Meneja Maendeleo ya Biashara, Kampuni ya Bam International, Noreen Mazalla akimtambulisha Afisa usalama wa kampuni hiyo.

  Skauti wa shule hiyo wakipandisha bendera ya Bam International kwenye shule yao

  Mgeni Rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Temeke, Eric Kilangwa (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick (aliyevaa miwani), Mwenyekiti wa shule, Sostenes Nyenyembe (wa pili kulia), Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Bam International Africa, Noreen Mazalla na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Emmentrudice Chilewa (kushoto) baada ya kuzinduzi wa madarasa matano, ofisi ya walimu na eneo la makusanyiko baada ya kufanya ukarabati katika shule ya sekondari Barabara ya Mwinyi iliyopo Buza jijini Dar es Salaam Juni 6 2017.
  Waalimu na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bam International wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Barabara ya Mwinyi iliyopo Buza jijini Dar es Salaam wakati wa hafla hiyo.
  Mwalimu akisoma risala.

  Wanafunzi wakiimba shairi la kuwashukuru viongozi wa kampuni hiyo.  Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick akizngumza machache na wanafunzi wa shule hiyo.

  anafunzi wakiaga kwa madaa baada kuimba shairi la shukrani kwa viongozi wa kampuni hiyo.  Mgeni Rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Temeke, Eric Kilangwa (wa pili kulia) akimkabidhi cheti cha shukrani kwa Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick.
  Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick na Meneja Maendeleo ya Biashara, Noreen Mazalla wakipanda mti wa ukumbusho katika eneo la makusanyiko la shule hiyo uliofanywa kampuni hiyo katika shule ya Barabara ya Mwinyi Buza jijini Dar es Salaam Juni 6 2017. Wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Eric Kilangwa (wa tatu kushoto) na Mwenyekiti wa shule hiyo Sostenes Nyenyembe.  Picha ya pamoja viongozi wa Bam International, Waalimu na baadhi ya wafanyakazi wa shule ya Sekondari Barabara ya Mwinyi iliyopo Buza jijini Dar es Salaam.

  Picha ya pamoja viongozi wa Bam International na baadhi ya wazazi wa wananfunzi wa shule ya Sekondari Barabara ya Mwinyi iliyopo Buza jijini Dar es Salaam.  Picha ya pamoja viongozi wa Bam International na baadhi ya wananfunzi wa shule ya Sekondari Barabara ya Mwinyi iliyopo Buza jijini Dar es Salaam.  Viongozi wa Bam International wakifurahia na kucheza baada wakati wa kumalizika kwa hafla hiyo.  Viongozi wa Bam International wakifurahia na kucheza baada wakati wa kumalizika kwa hafla hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Shule hiyo, Sostenes Nyenyembe.

  Mgeni Rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Temeke, Eric Kilangwa akimpatia mmoja wa wanafunzi zawadi kwa kufanya vizuri zaidi darasani.

  Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Bam International Africa, Noreen Mazalla akimpatia zawadi Mwalimu aliyetoa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha mradi wa ukarabati huo.

  0 0

  Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akipokea zawadi, ikiwa ni ishara ya pongezi kwa uteuzi wake mpya alioupata. Anayemkabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya watumishi wa wizara ni Naibu Katibu Mkuu; Dkt Mosses Kusiluka.

  Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akizungumza na watumishi alipokua akiwaaga. Dkt. Kayandabila ameteuliwa na Mhe. Rais kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania. (BoT). 

  Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika picha ya pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo; Dkt. Yamungu Kayandabila mara baada ya kuwaaga.

  ………………………………………

  Aliyekuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila amesisitiza utumishi bora unaozingatia Miongozo na Sheria.

  Dkt. Kayandabila aliyeteuliwa hivi karibuni na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), akiwaaga Watumishi wa Wizara alihimiza utendaji bora kazini katika kutoa huduma kwa Wananchi na kusihi Watumishi kuendelea na kasi hiyo.

  Aidha, aliwashukuru Watumishi wa Wizara ya Ardhi kwa ushirikiano wao walioonyesha kwake ambao umesababisha kudhihirisha matukio chanya kwa Wizara. Alisema; “ Tukumbuke kuwa sisi ni Watumishi wa Umma, tuendelee kufanya kazi kwa bidii kwa kuwahudumia Wananchi kwa bidii”.

  Awali akizungumza kwa niaba ya Watumishi wa Wizara; Afisa Mipango Miji, Baltazar Sumari alisema; “ Tunakushukuru Katibu Mkuu kwa jinsi ulivyotuwezesha kufanya kazi kwa umoja na nidhamu, Mungu akuwezeshe uweze kuendelea kudumisha utendaji wako wa kazi Benki Kuu kama jinsi ulivyofanya Wizarani hapa na tutaendelea kuhitaji ushauri wako”.

  Naye muwakilishi wa Taasisi za Wizara; Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipangomiji (TPRB); Helena Mtutwa alisema kuwa Dkt. Kayandabila ana karama ya kipekee ambayo imemuwezesha kuongoza vyema kwa kuweza kuonyesha njia bora katika utendaji kazi na kuonya kwa hekima.

  Dkt. Kayandabila anakwenda kutumika katika Benki Kuu ya Tanzania kama Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha (Economic and Financial Policies – EFP), akiwa na Naibu Gavana mwenza aliyeteuliwa naye kwa kipindi kimoja; Dkt. Bernard Yohana Kibese atakayehusika katika eneo la Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha (Financil Stability and Deepening – FSD).

  Na kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

  0 0  0 0

  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akiongoza kikao cha kamati ya Uongozi na kamati ya Bajeti leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. kulia  kwake ni Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa na Kushoto kwake ni Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah na anaefuata ni Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson 

  (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alijumuika na Waislamu,Viongozi mbali mbali na Wananchi katika kumswalia Marehemu Mzee Prof.Ishau Abdalla Khamis katika Msikiti wa Ijumaa Donge leo,Marehemu aliwahi kushika nyazifa mbali mbali katika Serikalia ya Mapinduzi Zanzibar na Chama cha Mapinduzi.
  1
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja,(wa pili mkushoto) pamoja na Viongozi wengine wakielekea katika kaburi wakati wa mazishi ya  Marehemu Mzee Prof.Ishau Abdalla Khamis yaliyofanyika leo kijiji cha Donge,Wilaya ya Kaskazini BUnguja.
  2
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto waliosimama) alijumuika na Waislamu,Viongozi mbali mbali na Wananchi katika mazishi ya Marehemu Mzee Prof.Ishau Abdalla Khamis katika kijiji cha Donge leo
  3
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein  akitia udongo katika kaburi la Marehemu Mzee Prof.Ishau Abdalla Khamis aliyezikwa leo katika kijiji cha  Donge,Willaya ya Kaskazini B Unguja,[Picha na Ikulu.]07/06/2017

  0 0   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Bungu, wilayani Kibiti Mkoa wa Pwani, kuhusiana na masuala mbalimbali ya kupambana na wahalifu wilayani humo. Masauni ambaye aliambatana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro aliwataka wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuwasambaratisha wahalifu hao
  1
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipokea maoni ya wananchi wa Kijiji cha Jaribu Mpakani wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi wilayani humo. IGP ambaye aliambatana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) walizungumza na wazee, viongozi wa dini na watu maarufu kutoka Wilaya Rufiji na Kibiti kuweka mikakati ya kuimarisha zaidi ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
  2
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wazee, viongozi wa dini na watu maarufu (hawapo pichani) kutoka Wilaya Rufiji na Kibiti kuhusu masuala mbalimbali na  kuweka mikakati ya kuimarisha zaidi ulinzi na usalama wa raia na mali zao. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, na kushoto ni Mkuu wa Wilaya Kibiti, Gulam Hussein. 
  3
  Wazee, viongozi wa dini na wa vyama vya siasa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati alipokuwa akizungumza na wananchi hao katika Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari ya Kibiti, mkoani Pwani. Masauni na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro pamoja na wananchi hao waliweka mikakati ya kuimarisha zaidi ulinzi na usalama wa raia na mali zao kupitia maoni ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0


   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akizungumza na Kamishna Mkuu wa Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga, wakati Kamishna huyo alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kupambana na dawa za kulenya nchini. 
  1
  Kamishna Mkuu wa Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga (kulia), akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati Kamishna huyo alipomtembelea Masauni ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kupambana na dawa za kulenya nchini.
  2
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsikiliza Kamishna wa Intelejensia wa Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya, Fredrick Kibuta (kulia), alipokua anatoa ufafanuzi jinsi ya kupambana na dawa za kulevya nchini. Katikati ni Kamishna Mkuu wa Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Masauni, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

   Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Najma Giga akiongoza kikao cha 43 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 07, 2017.
   Naibu Waziri Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angeline Mabula akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 41 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 5, 2017.
   Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Mhe.Dk Ashatu Kijaji akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 43 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 7, 2017.
   Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Dk Medard Kalemani akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 43 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 7, 2017.
    Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Prof Makame Mbarawa akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 43 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 7, 2017.
   Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde  katika kikao cha 43 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 7, 2017.
    Mbunge wa Kigamboni (CCM) Mhe,Faustine Ndugulile  akiuliza swali katika kikao cha 43 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 7, 2017.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dk Philip Mpango akizungumza jambo na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Gerson Lwenge katika kikao cha 43 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 7, 2017.
   Mbunge wa Kasulu Mjini Mhe.Daniel Nsanzugwako akifurahia jambo na Mbunge wa Madaba Mhe.Joseph Mhagama katika kikao cha 43 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma June 7, 2017.
   Mbunge wa Tarime Mjini (CHADEMA) Mhe.Esther Matiko akiuliza swali katika kikao cha 43 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 7, 2017.
  Mbunge wa Nyamagana(CCM) Mhe.Stanslaus Mabula akiuliza swali katika kikao cha 43 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 7, 2017.
    
  Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.

  0 0


  Mkuu wa Kitengo cha Tehama na mawasiliano kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) bwana Desderi Wengaa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wakufunzi wa mfumo wa Uhasibu na utoaji taarifa za fedha. Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya wakufunzi wa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kutoka mikoa ya Ruvuma, Lindi, Mtwara, Pwani, Tanga na Dar es salaam wakishiriki mafunzo hayo yaliyofunguliwa jana
  Mtoa mada wa mafunzo ya wakufunzi wa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa njia ya kielektroniki kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI bwana Hamis Zikatimu akitoa mada wakati wa mafunzo hayo yanayofanyika mkoani Mtwara.
  Mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara bwana Elias Nyamusami.(aliyeketi katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki kutoka mkoa wa Tanga. Aliyeketi kushoto kwa Mgeni rasmi ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama na mawasiliano kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) bwana Desderi Wengaa na kulia kwa Mgeni rasmi ni bwana Lucas Mrema ambaye ni mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI

  Mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara bwana Elias Nyamusami.(aliyeketi katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3).

  ……………………..

  Na Mathew Kwembe,Mtwara

  Serikali imesema kuanza kutumika kwa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ifikapo julai mosi, 2017, kutapunguza changamoto za halmashauri kupata hati zenye mashaka pindi zinapokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

  Mfumo huo utaiwezesha Serikali kupeleka rasilimali fedha moja kwa moja kwenye vituo vya afya kwa ngazi za halmashauri. Vituo vya kutolea huduma ambavyo vitapokea fedha hizo vinajumuisha Zahanati, Vituo vya Afya, na Hospitali za Wilaya. Zoezi hilo litaenda sambamba na inavyotekelezwa kwenye sekta ya elimu, Serikali za Vijiji na Ofisi za Kata.

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bwana Alfred Luanda ameyasema hayo jana mjini Mtwara wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wakufunzi wa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma kwa wahasibu kutoka halmashauri za mikoa sita ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Tanga, Pwani na Dar es salaam.

  Mafunzo kama hayo pia yanafanyika katika kanda nyingine za Mbeya, Dodoma, na Shinyanga ambapo jumla ya wakufunzi 490 kutoka katika taasisi mbalimbali za Serikali pamoja na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening, (PS3) wanashiriki.

  Alisema kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa taarifa sahihi za rasilimali fedha zilizopo katika vituo vya huduma na hivyo kusababisha halmashauri nyingi nchini kushindwa kutoa taarifa sahihi za matumizi ya ruzuku zinazotolewa katika vituo hivyo.

  Katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Miundombinu bwana Elias Nyamusami, Katibu Tawala wa Mkoa aliongeza kuwa kukosekana kwa mfumo wa uhasibu na utoaji wa taarifa za fedha umezifanya halmashauri zionekane kwamba zinasababisha kwa makusudi upotevu wa fedha.

  “Ukweli ni kwamba hakukuwa na mfumo sahihi wa kuzisaidia halmashauri kulizuia hilo,” alisema.

  Aliongeza kuwa mfumo huo mpya wa kupatiwa rasilimali fedha utatoa motisha kwa vituo vya kutolea huduma za afya na kuongeza kipaumbele cha utoaji huduma bora kwa wananchi wa Tanzania na kuongeza usawa na uwazi.

  Alisema kuwa mfumo huo umeundwa kuweza kukidhi changamoto mbalimbali za miundombinu, ikiwemo umeme, na kutokuwa na upatikanaji wa mtandao kwa baadhi ya vituo vya kutolea huduma katika halmashauri mbalimbali na hivyo mfumo huo hautakuwa tu katika muundo wa kielektroniki, lakini pia kutakuwa na muundo wa kujaza kwenye vitabu.

  “Mfumo wa kujaza katika vitabu na wenyewe umeboreshwa na kuwa rahisi kwa mtumiaji kujaza taarifa sahihi, na huu utatumika kwa vile vituo ambavyo changamoto ya upatikanaji wa miundombinu wezeshi katika matumizi ya kielektroniki,” alisema na kuongeza kuwa mara baada ya kujaza katika vitabu, takwimu hizo zitaingizwa katika mfumo kwenye ngazi ya halmashauri na vituo kupatiwa taarifa ya vituo vyao.

  Alisema kuwa upelekaji wa Rasilimali Fedha moja kwa moja kwa vituo vya kutolea huduma utahakikisha kuwa Fedha zinazotolewa na Serikali zinatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa. Mkakati huo mpya wa kuboresha sekta za afya na elimu ni msaada kutoka Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).

  Awali Mkuu wa Kitengo cha Tehama na Mawasiliano kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) bwana Desderi Wengaa alisema kuwa mfumo huo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa unaojulikana kwa Kiingereza kama Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS) unasaidia utekelezaji wa utoaji wa rasilimali fedha moja kwa moja kwa ngazi za vituo vya kutolea huduma kwa kuimarisha uhitaji wa kuwepo kwa usimamizi wa fedha katika ngazi ya vituo vya kutolea huduma.

  Alisema kuwa FFARS itawapatia watoa huduma mfumo sanifu uliorahisishwa ambao utawawezesha kutunza taarifa za fedha zinazotolewa na zilizopo katika vituo vyao.

  Bwana Wengaa aliongeza kuwa FFARS itaweza kufuatilia matumizi ya fedha hizo katika kufikia malengo ya utoaji huduma na kuhakikisha yanaendana na sheria za manunuzi na utoaji taarifa.

  “Taarifa hizi zitasaidia Serikali kuimarisha Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma na kuongeza uwazi, na hivyo watoa huduma wa afya kuwa na wajibu kwa jamii wanayoihudumia,” alisema.  Wakufunzi 490 wataweza kutoa elimu kwa watumiaji wa mwisho wa mfumo wa FFARS katika zaidi ya Vituo vya Afya 550, Zahanati 6800, Hospitali za Wilaya 135, na takribani Shule za Msingi na Sekondari 20,000 katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara, vikiwemo vituo vya kutolea huduma kutoka Mikoa 13 na Halmashauri 93 zinazotekeleza Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3).

  0 0
 • 06/07/17--05:22: Article 9


older | 1 | .... | 1262 | 1263 | (Page 1264) | 1265 | 1266 | .... | 1898 | newer