Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1258 | 1259 | (Page 1260) | 1261 | 1262 | .... | 1904 | newer

  0 0  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua juu ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara baada ya kuwasili Butiama ambapo atakuwa mgeni rasmi kwenye  sherehe za siku ya mazingira Duniani ambazo Kitaifa zinafanyika Butiama mkoani Mara.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima mbele ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara baada kuweka shada la maua,Makamu wa Rais yupo Butiama kuhudhuria sherehe za siku ya mazingira Duniani ambazo Kitaifa zinafanyika Butiama mkoani Mara.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye kikao cha kupokea taarifa ya mkoa wa Mara mara baada ya kuwasili Butiama kwenye makazi ya Hayati Baba wa Taifa.
                                .............................................................................

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Mara alasiri ya leo 3-June-2017 akitokea mkoani Mwanza ambapo hapo kesho atakuwa ni mgeni rasmi katika kilele cha Siku ya Mazingira Duniani.


  Alipowasili kijijini Butiama, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Viongozi wa vyama vya siasa na watendaji mbalimbali wa Serikali ambao wameongozwa na Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt Charles Mlingwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba.


  Makamu wa Rais pia amepokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Mara na amepata fursa ya kuwasha mshumaa na kuweka shada la maua katika kaburi la baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere lililopo Mwitongo kijijini Butiama.

  Hapo kesho tarehe 4-June-2017 Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ataongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Mara na mikoa ya Jirani katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambapo kitaifa sherehe hizo zitafanyika katika kijiji cha Butiama mkoani Mara.
   

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bi. Seriel Mchembe mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe. (Picha na OWM).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Gairo, Bw. Ahmed Shabiby mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe nawa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bi. Seriel Mchembe (Picha na OWM).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Cliford Tandari mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero. (Picha na OWM).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipanda mti nje ya Ofisi ys Mkuu wa Wilaya ya Gairo mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Upandaji Miti Kitaifa. Wengine ni viongozi wa Mkoa na Wilaya wakishuhudia. (Picha na OWM).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimwagilia mche alioupanda nje ya Ofisi ys Mkuu wa Wilaya ya Gairo mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Upandaji Miti Kitaifa. Wengine ni viongozi wa Mkoa na Wilaya wakishuhudia. (Picha na OWM).
  Viongozi na watumishi wa Wilaya ya Gairo wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayupo pichani) katika mkutano aliouitisha mjini Gairo Juni 3, 2017. (Picha na OWM).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi na watumishi wa Wilaya ya Gairo (hawapo pichani) katika mkutano aliouitisha mjini Gairo Juni 3, 2017 (Picha na OWM).

  ………………………………………………………………………………………..

  * Ni la sh. milioni 213/- la fedha za maendeleo.

  *Ataka apewe taarifa ifikapo Juni 30. 

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Clifford Tandari aitishe kikao na uongozi wa Halmashauri ya Kilosa na kupata kauli yao ni lini watalipa zaidi ya sh. milioni 210 wanazodaiwa na Halmashauri ya Gairo.

  “Katibu Tawala itisha kikao cha Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri, waseme ni lini watazileta fedha hizo ambazo zilitumwa kwao wakati Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ikiwa haijafungua akaunti zake,” amesema.

  Ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Juni 3, 2017) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Morogoro, wilaya ya Gairo na watumishi wa Halmashauri ya Gairo mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa na wilaya katika kikao kilichofanyika Gairo mjini

  “Kilosa ni lazima wazilipe hizo fedha. Katibu Tawala simamia zoezi hilo na kama watachelewa, uzikate moja kwa moja kwenye fedha yao wanayoletwa kutoka Ofisi ya Rais (TAMISEMI). Nataka nipewe taarifa ya maamuzi hayo kabla Juni haijaisha,” amesema.

  Mapema akitoa taarifa ya wilaya hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bi. Siriel Mchembe alisema wanaidai Halmashauri ya Kilosa sh. 233,228,679 ambazo ziliingizwa huko wakati wilaya hiyo inaanzishwa na hawakuwa wamefungua akaunti ya wilaya.

  “Fedha hizi zilikuwa zinapitia Kilosa wakati wilaya ya Gairo imeanzishwa kwa kuwa kipindi hicho wilaya ya Gairo ilikuwa bado haijafungua akaunti. Fedha hizi zinajumuisha ruzuku ya uendeshaji, mapato ya ndani na miradi ya maendeleo,” alisema.

  Alisema Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) iliagiza wilaya ya Kilosa ilipe deni hilo kabla ya Juni 2016 lakini hadi sasa wameshalipa sh. milioni 20 tu ambapo sh. milioni 10 zililipwa Desemba 2015 na nyingine milioni 10 zililipwa Mei 2017.

  Akisisitiza kuhusu makusanyo ya mapato, Waziri Mkuu amewakumbusha watumishi hao kuwa Serikali imekwishatoa agizo la kutumia mashine za kielektroniki kukusanya mapato ifikapo Julai mosi.

  “Makusanyo ya mapato ya ndani ni eneo muhimu sana. Tumeshaagiza, mwisho wa kutumia mifumo ya kawaida ni Juni 30. Kuanzia Julai mosi, kila eneo ni lazima litumie mashine za kielektroniki,” alisema Waziri Mkuu.

  Alihoji ni kwa nini Halmashauri ya Gairo ililenga kukusanya sh.milioni 889.5 lakini kufikia Aprili mwaka huu, makusanyo halisi yalikuwa ni sh. milioni 356.2 sawa na asilimia 40.

  Alitumia fursa hiyo kuwapongeza Mamlaka ya Mapato (TRA) ya wilaya hiyo ambao hadi kufikia Aprili, 2017 wameweza kukusanya sh. milioni 601.5 ikilinganishwa na makadirio yao ya kukusanya sh. milioni 471 kwa mwaka. Waziri Mkuu aliwapongeza kwa sababu wamevuka lengo kwa asilimia 127.6.

  Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye ziara ya siku ya wilaya hiyo, asubuhi alipanda mti kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ikiwa maadhimisho ya siku ya upandaji miti hapa nchini.

  Pia alikagua mradi wa maji wa kijiji cha Chakwale, na mradi wa visima 10 ambayo imekuwa na mgogoro kwa muda mrefu. Pia atazungumza na wananchi wa Gairo mjini kwenye mkutano wa hadhara.

  0 0

  Sehemu ya fukwe wa Bahari ya Hindi maeneo ya Jiji la Dar es Salaam ikiwa imeathiriwa na uchafu 


  Na Boss Brown

  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Chares Tizeba ataongoza ujumbe kutoka Tanzania kushiriki katika Kongamano la Bahari Duniani linalotarajiwa kuanza Jumatatu tarehe 5 hadi 9 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York nchini Marekani.

  “Changamoto inayoikabili bahari ni kubwa kutokana na uchafuzi utokanao na taka sugu ambazo zinahatarisha uhai wa Bahari yetu, tunaunagana katika kushilikiana na wadau mbalimbali katika juhudi za kuiokoa bahari kwa pamoja.” Alisisitiza Tizeba.

  Akifafanua amesema kama nchi wanachama tanaadhimia kutekeleza kipengele cha 14 cha Malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ya agenda ya 2030 ya Umoja wa Mataifa Kinacholenga matumizi bora ya rasilimali za baharini.

  Kongamano hili ni la muhimu katika kuokoa bahari na litakutanisha Serikali, Umoja wa Mataifa, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Mashirika yanayoshughulikia mazingira, Taasisi za elimu na wanasayansi ya Jamii, Asasi za Kirai, watu binafsi, makampuni na viwanda.

  Miongoni mwa changamoto za ongezeko la taka sugu ni bidhaa zitokanazo na plastiki ambazo huchukua zaidi ya miaka 500 kuoza na kuathiri viumbe vya baharini na hata kuhatarisha afya za wanadamu. Hivyo wadau wanategemewa kutoa hatua mbadala za kusafisha bahari na kurudisha uhai wake kwa maisha ya baadaye.

  Mambo mengine yatakayo jadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na kuongeza maeneo ya hifadhi baharini na kutunza rasilimali za bahari, kupunguza ongezeko la asidi itokayo viwandani inayoingia baharini; kudhibiti uvuvi haramu na kuweka mikakati ya kudhibiti uvuvi haramu; kuongeza elimu kwa jamii na utafiti wa kisayansi katika masuala ya bahari; kuongeza tija kwenye uchumi utokanao na baharini ambao hautakuwa na madhara makubwa kwa bahari pamoja na kutimizwa na kutekelezwa kwa sheria za kutumia bahari zilizowekwa na nchi wanachama.

  Matokeo yaliyo tolewa na wanasayansi yanabainisha kwamba takriban tani Million 8 za plasitiki huingia baharini ambapo kufikia 2050 kutakua na kiwango kikubwa cha plasitiki kuliko samaki na viumbe vingine vya baharini endapo hatua muhimu hazitachukuliwa kuiokoa bahari sasa.

  Pamoja na changamoto zote hizi zote zinazoikabili bahari ipo nafasi ya kuokoa bahari kabla athari zaidi hazijajitokeza. Shirika la kusafisha fukwe duniani Ocean Conservancy kwa miaka 32 limekua likijishughulisha na kusafisha fukwe za bahari duniani kote, katika riporti yao ya mwaka 2015 wanaeleza kuwa “kuna matumaini endapo kwa pamoja tukiungana katika kutatua tatizo hili na kufikia Mpango wa Maendeleo Bora ya Agenda ya Mwaka 2030”.

  Viumbe hai duniani kote kwa namna moja au nyingine maisha yao yote hutegemea bahari. Hewa unayovuta, maji unayokunywa, chakula unachokula, nguo unazovaa, magari tunayo tembelea n.k vyote hutegemea bahari kwa namna moja au nyingine. Bahari inatupa pia fulsa ya kupumzika, kustarehe, kuogelea, kucheza n.k. 

  “Kila mmoja ana mchango mkubwa sana katika harakati za kuiokoa kwani matatizo yanayoikabili bahari yamesababishwa na shughuli za wanadamu. Hivyo sisi wenyewe tuna uwezo wa kubadili mienendo ya maisha yetu ili kuiokoa bahari inayoelekea kutokomea”. Alisisitiza Tizeba

  Siku moja kabla ya kuisha kwa kongamano hili alhamis ya tarehe 8 Juni pia kutaadhimishwa Siku ya Bahari Duniani ambayo ina kauli mbiu inayosema “Bahari Yetu Maisha Yetu” katika kuhamasisha jamii ya watanzania kuunga mkono kampeni ya ‘Okoa Bahari’. Ambapo Marafiki wa Bahari kutoka Tanzania watakusanyika katika fukwe za Bahari kufanya usafi ikiwa ni jitihada za kuunga mkono kampeni hii ya Kimataifa.

  0 0

   Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu anaeshughulikia kazi, jira na maendeleo ya Vijana Mh Anthony Mavunde akiwa katika picha ya pamoja na waalikwa waliohudhuria katika uzinduzi huo wa mpango wa mafunzo ya ufundi wa kisasa wa kutengeneza viatu kwa njia za kisasa.
  Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu anaeshughulikia kazi, jira na maendeleo ya Vijana Mh Anthony Mavunde akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa mafunzo ya ufundi wa kisasa wa kutengeneza viatu kwa njia za kisasa uliofanyika kwenye chuo cha DIT Karakana ya Viatu jijini Mwanza leo.
  Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika uzinduzi huyo uliofanyika kwenye cho cha DIT Karakana ya Viatu jijini Mwanza.
  ……………………………………………………
  Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu anaeshughulikia kazi, jira na maendeleo ya Vijana Mh Anthony Mavunde amefungua mpango wa mafunzo ya ufundi wa kisasa wa kutengeneza viatu kwa njia za kisasa kwa vijana 1000 wanaotaka mikoa zaidi ya kumi nchini.

  Akizundua mpango huo, Mhe Mavunde, amesema mpango huo unalenga kuwajengea uwezo wa kujiajiri vijana na pia kutumia bidhaa zitokanazo na mazao ya mifugo kwa ajili ya kuzalisha viatu na bidhaa za ngozi nchini.

  Amesema, serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha inatekeleza azma ya ujenzi wa viwanda kwa kuwajengea uwezo vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa katika kujiandaa na mfumo wa mapinduzi ya viwanda ambavyo vimeshaanza kujengwa nchini.

  Aidha amewataka vijana kutochagua kazi au kubweteka kuwa kazi rasmi ni zile za ajira ya moja kwa moja serikali au sekta binafsi, amewataka vijana kubadilisha mtazamo wa maaana ya Ajira kwa kutokukaa na kusubiri nafasi za ajira.

  Amesema mpango huu wa miaka mitano unalenga kuwafikia vijana zaidi ya milioni 4 nchini katika kuwajengea uwezo ambao utawafanya kujiajiri au kuajiriwa katika Tanzania ya viwanda.

  Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano.
  Wizara ya kazi,ajira, ulemavu na maendeleo ya vijana
  03/06/2017

  0 0

   
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akitoa maelezo ya awali ya ufunguzi katika mijadala ya kuadhimisha siku Mazingira Duniani Wilayani Butiama Mkoni Mara. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Mahusiano Endelevu Kati ya Binadamu na Mazingira.”
  Wanajopo wa mada ya kwanza ya “Tanzania Bila Mkaa na Kuni Inawezekana?” kutoka kushoto ni Ndugu Charles Meshack Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo Mkurugenzi Mkuu, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Eng. Estomih Sawe Mkurugenzi Mtendaji TaTEDO (Center for Sustainable Modern Energy Initiative in Tanzania). Mjadala unaendelea Butiama katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani.
  Mjadala ukiendelelea pichani, Wanajopo wa mada ya kwanza ya “Tanzania Bila Mkaa na Kuni Inawezekana?” kutoka kushoto ni Ndugu Charles Meshack Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo Mkurugenzi Mkuu, wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Bi. Maria Sarungi (Mwendesha Mada) na Eng. Estomih Sawe Mkurugenzi Mtendaji TaTEDO (Center for Sustainable Modern Energy Initiative in Tanzania). Kongamano linaendelea Butiama katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. January Makamba akifuatilia mjadala katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki Butiama- Mara. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora. Mijadala mbalimbali inaendelea katika kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Mahusiano Endelevu Kati ya Binadamu na Mazingira.”

  0 0

  MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ametaja sababu kubwa iliyoifanya wilaya hiyo kurudi nyuma kiuchumi ni kutokana na kuchelewa kuwekeza kwenye suala la elimu na miundombinu ya barabara ambacho ni kilio cha muda mrefu.

  Hivyo kuitaka jamii kuona umuhimu wa kuwekeza kwenye elimu ili iwe chachu ya kuinua maendeleo yao lakini pia serikali iboreshe miundombinu ya barabara ya Tanga -Pangani hadi Sadaani ambayo imekuwa ikipigiwa kelele na wabunge waliopita bila mafanikio

  Aweso aliyasema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo ambapo alisema wazazi hawana budi kuwekeza kwenye elimu iliwaweze kupatikana wataalamu watakaosaidia harakati za kuinua maendeleo.

  Alisema ili katika mipango mikubwa ya kufanikisha azma hiyo ndio sababu kubwa wakaanzisha mpango mahususi wa niache nisome mwaka jana ambao umepata mafanikio makubwa.

  “Mpango wa niache nisome umekuwa mkombozi mkubwa wa kuihamasisha jamii ya wana pangani kuona umuhimu wa kupata elimu na mafanikio yaliyopatikana ni mengi ikiwemo kupata fursa mwaka huu kuwapeleka vijana wengi Jeshini “Alisema

  Aidha aliwataka viongozi chama na serikali kuendelea kushirikiana na wataalamu ili kuwezesha kuifungua wilaya ya Pangani ambayo inahitaji kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.

  “Uchumi wa Pangani ni zao la Mnazi na mtu mpaka aje wilayani hapa lazima awe na sababu maalumu ikiwemo kufiwa nah ii inasababishwa na miundombinu mibovu ya barabara hivyo ujenzi huo utakapoanza utasaidia kufungua uchumi huo “Alisema.

  Mbunge huyo aliwataka pia wananchi wa wilaya hiyo kutunza maeneo yao kwa kuacha kuyauza ovyo kutokana na fursa kubwa inayokuja mkoani hapa ikiwemo mradi mkubwa wa bomba la mafuta.
   Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akiingia ukumbini kuzungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kibondo, Mabalozi, watendaji wa CCM na wa Serikali, leo Wilayani Kibondo akiwa katika mwendelezo wa ziara zake za Kichama mikoani
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi, Tanzania, Alhajj Abdallah Bulembo akiwa amewasili ukumbini tayari kwa kikao hicho. Kushoto ni Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Kigoma Nicholaus Zakaria, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kaborou na kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Kigoma, Mbunge wa Viti Maalum Josephine Ngezabuke, Mbunge wa Mbambwe Atashasta Nditiye na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibondo Josephat Ntabindi.
   Wajumbe wakishangilia bada ya Bulembo kuingia ukumbini 
   Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kibondo Josephat Ntabindi akifanya utambulisho kabla ya kufungua kikao hicho
   Wajumbe wakishangilia ukumbini
   Mjumbe wa NEC Moshi Ngunga akisalimiabaada ya kutambulishwa kwenye kikao hicho. Kushoto ni Mbunge wa Mhambwe Atashasta Nditiye
   Ofisa wa Makao Makuu ya Jumuia ya Wazazi Omar Kalolo akitamba ukumbini wakati akijitambulisha.
   Ofisa kutoka Makao Makuu ya Jumuia ya Wazazi Ndu Mlami akisalimia baada ya kutambulishwa 
   Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Kigoma, Mbunge wa Viti Maalum Josephine Ngezabuke akijimwayamwaya ukumbini baada ya kutambulishwa
   Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Kigoma, Mbunge wa Viti Maalum Josephine Ngezabuke akijimwayamwaya ukumbini baada ya kutambulishwa
   Baadhi ya viongozi wa Chama, wakiwa ukumbini
   Mtaalam kutoka Idara ya Afya Wilaya ya Kibondo Joseph Kalogabwa akitoa maelezo kwa wajumbe kuhusu njia ya kujikinga na ugonjwa wa Ebola 
   Mwenyekiti wa CCM mkoa a Kigoma Dk Amani Kaborou akifanya utambulisho kabla ya kumkaribusha Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo, kuzungumza katika kikao hicho
   Mbunge wa Muhambwe Atashashta Nditiye akisalimia baada ya kutambulishwa
   Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazi mkoa wa Kigoma Nicholaus Zakaria akisalimia baada ya kutambulishwa
   Mjube wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj abdallah Bulembo akizungumza na wajumbe wakati wa kikao hicho
   Mjube wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj abdallah Bulembo akizungumza na wajumbe wakati wa kikao hicho
   Katibu Msaidizi wa CCM wilaya ya Kibondo Mfaume Mkusa na Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM katika Wilaya hiyo Pendo Machilu wakiwajibika kwa kuchukua dondoo katika kikao hicho
   Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Lous Bura akitoa maelezo ya namna alivyosimamia ilani ya CCM ya 2015/20
   Mmoja wa wajumbe akifuatilia kwa makini wakati Mkuu huyo wa wilaya akieleza utekelezaji wa Ilani
   Mbunge wa Muhambwe akitoa maelezo ya jinsi anavyosimamia ilani ya CCM ya 2015/20 
   Mwalimu Mstaafu John Busunzu akikabidhi waraka wake kwa Bulembo baada ya kuusoma, Waraka huo pamoja na mambo mengine ulihusu kudai haki za wazee wastaafu 
   Baadhi ya wajumbe wakimzawadia Bulembo asali
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimkabidhi sh 400,000/= Diwani wa Viti Maalum Kata ya Buzunzu, Grace Zakaria baada ya wajumbe kuchangishwa ukumbini kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Ofisi ya CCM Tawi la Busunzu.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimkabidhi sh 170,000/= Katibu wa UWT Kata ta Lugonga Jane Kabiga baada ya wajumbe kuchangishwa ukumbini kwa ajili ya ununuzi wa Baiskeli ya kufanyia kazi za Jumuia hiyo katika kata.PICHA: BASHIR NKOROMO

  0 0

  Maandalizo ya Mazishi ya marehemu Dkt ,Philemoni Ndesamburo yakiendelea nyumbani kwake KDC mjini Moshi.
  Kwaya ikihudumu kwa nyimbo kwa ajili ya kuwafariji wafiwa nyumbani kwa marehemu Dkt Philemoni Ndesamburo.
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson akitoa mkono wa pole kwa mama Mjane wa Marehemu Dkt Philemoni Ndesamburo ,Ndehorio Ndesamburo alipotembelea nyumbani kwa marehemu kuifariji familia. 
  Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni ,Freeman Mbowe akitoa mkono wa Pole kwa mjane wa marehemu Dkt Ndesamburo ,Ndehorio Ndesamburo nyumbani kwake KDC mjini Moshi.
  Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni ,Freeman Mbowe akitoa mkono wa Pole kwa mtoto wa marehemu Dkt Ndesamburo ,Filomena Ndesamburo nyumbani kwao  KDC mjini Moshi.
  Waziri wa Malisili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akitoa pole kwa mama mjane wa marehemu Ndesamburo nyumbani kwake KDC mjini Moshi.
  Mbunge wa jimbo la Same Magharibi ,David Mathayo David akitia saini katika kitabu cha waombolezaji nyumbani kwa marehemu Dkt Philemoni Ndesamburo.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro,Idd Juma akitia saini katika kitabu cha waombolezaji nyumbani kwa marehemu Ndesamburo KDC Mjini Moshi.
  Mkurugenzi wa Halmashauri wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) John Mrema akitia saini katika kitabu cha waombolezaji nyumbani kwa marehemu Dkt Ndesamburo KDC mjini Moshi.
  Baadhi ya Madiwani wakitia saini katika kitabu cha waombolezaji .
  Baadhi ya viongozi waliofika kutoa pole kwa familia ya marehemu Dkt Ndesamburo.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mstaafu ,Saidi Meck Sadiki akisalimiana na Mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe walipokutana nyumbani kwa marehemu Dkt Ndesamburo.
  Saidi Meck Sadiki akitoa mkono wa pole kwa watoto wa marehemu Dkt Ndesamburo.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akisalimiana na mume wa Mbunge wa viti maalumu Lucy Owenya,Dkt Fidelis Owenya alipofika nyumbani wa marehemu Dkt Ndesamburo kutoa salamu za pole.
  Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Rombo Joseph Selasini walipokutana nyumbani kwa marehemu Ndesamburo.
  Mjane wa marehemu Ndeamburo ,Bi Ndehorio Ndesamburo (mwenye nguo za rangi nyeusi ) akionekana ni mwenye huzuni.
  Baadhi ya waombolezaji .
  Mwenyekiti wa Chadema Taifa  na Kiongozi  wa kambi rasmi Bungeni ,Freeman Ndesamburo akisalimiana na Askofu wa KKKT Dkt Martin Shoo alipofika nyumbani kwa marehemu Dkt Ndesamburo .

  Baadhi ya watoto wa marehemu Philemoni Ndesamburo wakiwa nyumbani kwao.
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, aliongozana na Mkurugenzi wa Uendeshaji Bi. Neema Muro na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji Bw. Gabriel Silayo, baada ya kufungwa kwa semina kwa wastaafu watarajiwa wa wilaya zote za mkoa wa Mwanza iliyofanyika ukumbi wa chuo cha watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania, huko Capri-point jijini Mwanza. 


  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said 


  Katika hotuba yake aliyotoa Kati wa ufunguzi rasmi wa semina hiyo, Bw. Mayingu alisema, PSPF inatarajia kulipa wastaafu kiasi cha shilingi Trilioni 1.3 kwa mwaka huu tu wa 2017/18."Kwa mwaka 2017/18 pekee, Mfuko unatarajia kuwalipa wastaafu 9,552 jumla ya mafao yanayofikia shilinginTrilioni 1.3.

  Kisai hiki cha Mafao ni kikubwa, hivyo kupitia semina hii Wastaafu watarajiwa wa PSPF wamejifunza namna ya kupanga maisha yao baada ya kustaafu ikiwa ni pamoja na fursa za uwekezaji wa mafao yao ili mafao haya yaweze kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi na kuongeza fursa za ajira." Alisema Bw. Mayingu katika hotuba yake. 

  Miongozi mwa mambo waliojifunza wastaafu hao wanaokadiriwa kufika 450, ni pamoja na uanzoshwaji wa viwanda vidogo vidogo, namna bora ya utunzaji fedha kwenye taasisi za fedha, (mabenki), lakini pia mbinu mbalimbali za ujasiriamali. 

  Kuhusu mafunzo yaliyotolewa na SIDO, Bw. Mayingu alisema Mfuko ulikutana na Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo (SIDO) na kujadiliana namna ambavyo taasisi hizi mbili zinaweza kushirikiana na kuwafanya wastaafu wa PSPF wapate ujuzi wa kuwekeza na kuweza kutengeneza ajira kwa vijana. 

  "Lengo likiwa SIDO iwajengee uwezo kitaalamu na kuwapatia vifaa ili wastaafu wa PSPF waweze kuanzisha viwanda vidogo vidogo na shughuli nyingine za uzalishaji." Alisema Bw. Mayingu. Alisema wameamua kufanya hivyo kwa kzuingatia ukweli kuwa, katika kufuatilia wastaafu wa Mfuko wamegundua kuwa baadhi yao hujiingiza katika biashara mbalimbali ambazo hawakujiandaa vema na matokeo yake kupoteza mafao yao.
  Washiriki wakijadiliana
  Mkurugenzi wa Masoko wa wa Mfuko wa uwekezaji wa pamoja UTT-AMIS, Daudi Mbaga, akitoa mada ya namna wanachama wa taasisi hiyo wanavyoweza kufaidika kwa kuwekeza kwenye Mfuko huo.
  Mshiriki akizungumza kwenye semina hiyo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku mbili
  Mmoja wa wastaafu wa PSPF, ambaye kwa sasa ni mteja wa benki ya NMB, akitoa ushuhuda jinsi alivyofaidika baada ya kuitumia benki hiyo pale alipostaafu ambapo sasa anaedesha miradi mbalimbali kufuatia mikopo anayompewa na benki hiyo na kumfanya aishi maisha ya amani.
  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kushoto), Mkurugezni wa Uendeshaji, Bi.Neema Muro, (katikati) na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Bw. Gabriel Silayo, wakifurahia michango ya mawazo kutoka kwa washiriki wa semina.
  Meneja wa Mfunzo kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo SIDO, Bi. Beata Minga, (kulia), akiongoza kikao wakati wa kufungwa kwa semina ya siku mbili ya mafunzo kwa wastaafu watarajiwa
  Mshiriki akichangia mawazo yake kwenye semina hiyo
  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (katkati), akiwa na viongozi wengine wa Mfuko kutoka kushoto ni Meneja Mipango na Utafiti, Bw.Luseshelo Njeje, Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bi. Neema Muro, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Bw. Gabriel Sulayo, na Meneja wa Pensehini za Wastaafu, Bw.Mohammed Salim.
  Bw. Mayingu, (kushoto), akijadiliana jambo na Bwana Dominic Haule, Mkurugenzi IMADS, (wakwanza kulia), wengine wanaosikiliza kutoka kushoto ni Bi. Neema Muro, Bw. Gabriel Silayo, Bw.Bw.Luseshelo Njeje na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, baada ya kufungwa kwa semina hiyo

  Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ambaye awali aliifungua rasmis semina hiyo, akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, (watatu kulia waliokaa), Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw.John Mongella, (watatu kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (wapili kulia), na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa PSPF, Bw.Nyakimuro Muhoji, viongozi wengine na wafanyakazi wa PSPF
  Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa PSPF, Bw.Nyakimuro Muhoji, (kushoto) na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF, Bi. Neema Muro wakiwasili ukumbini
  Naibu waziri wa fedha na mipango, Dkt. Asshatu Kijaji, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, Bw. Nyakimuro Muhoji (katikati) na Mkurugenzi Mkuu, Bw. dam Mayingu wakiwasili ukumbini.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto(Maendeleo yaJamii) Bi. Sihaba Nkinga( wa pili kulia) akiongozana na watendaji kutoka Wizarani pamoja na viongozi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Misungwi alipotembelea katika Chuo hicho kwa ziara ya kikazi hivi karibuni.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto (Maendeleo yaJamii) Bi. Sihaba Nkinga(wa tatu kulia) akimsikiliza Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Misungwi Mhandisi Harold Jackson Mtyana (kulia) alipokuwa akimuelezea kuhusu chumba cha Kompyuta cha Chuo hicho wakati wa ziara yake ya kikazi hivi karibuni.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto (Maendeleo yaJamii) Bi. Sihaba Nkinga akitumia moja ya Kompyuta zilizopo katika Chumba cha Kompyuta cha Chuo cha Maendeleo ya Jamii Misungwi ikiwa ni mradi uliwezeshwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Korea ya Kusini.
  Muonekano Chumba cha Kompyuta cha Chuo cha Maendeleo ya Jamii Misungwi ikiwa ni mradi uliwezeshwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanznia na Serikali ya Korea ya Kusini.

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto(Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkingaakitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Misungwi alipofanya ziara ya kikazi hivi karibuni.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto(Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akizungumza na Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Misungwi Mhandisi Harold Jackson Mtyana alipofanya ziara ya kikazi hivi karibuni.
  Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Misungwi Mhandisi Harold Jackson Mtyana (kulia) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto(Maendeleo yaJamii) Bi. Sihaba Nkinga(kushoto) wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Misungwi kwa ziara ya kikazi hivi karibuni.
  Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO Misungwi Mwanza.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Juma Samwel Sweda ( wa pili kulia) wakati alipomtembelea Ofisini kwake hivi karibuni.
  Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Juma Samwel Sweda akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga(kulia) alipomtembelea Ofisini kwake hivi karibuni.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw.Elliurd Mwaitekele(kushoto) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga(hayupo Pichani) wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi hivi karibuni kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Bi Deodata Makani na Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi kutoka Wizara hiyo Bi. Martha Chuma.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto(Maendeleo yaJamii) Bi. Sihaba Nkinga(kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw.Elliurd Mwaitekele(kulia) wakati wakijadiliana jambo mara baada ya Katibu Mkuu huyo kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi hivi karibuni.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga(kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe.Juma Samwel Sweda(kulia) wakati wakijadiliana jambo mara baada ya Katibu Mkuu huyo kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya huyo hivi karibuni.Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO Misungwi Mwanza.


  0 0

  Waziri wa Malisili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe kushoto akimkabidhi Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale tuzo ya mshindi wa banda bora la sekta ya nishati na mazingira katika maonyesho ya Kimataifa ya Biashara wakati alipokwenda kuyafunga kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella.
   Waziri wa Malisili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe kushoto akifurahia jambo na  Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale mara baada ya kumkabidhi tuzo ya mshindi wa banda bora la sekta ya nishati na mazingira katika maonyesho ya Kimataifa ya Biashara wakati alipokwenda kuyafunga kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella.
   Watumishi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakiongozwa na Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale kulia na katikati ni Mwanasheria wa TPDC Kelvin Gadi wakiwa na tuzo yao walioipata
   Watumishi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakiongozwa na Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale kulia na katikati ni Mwanasheria wa TPDC Kelvin Gadi wakiwa na tuzo yao waliyoipata
   Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kulia ni Mwanasheria wa Shirika hilo Kelvin Gadi
   Mwanasheria wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Kelvin Gadi kulia akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto mara baada ya kulitembelea banda lao
   Mkuu wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga,Godwin Gondwe wa pili kutoka kulia mwenye miwani akiteta jambo na watumishi wa shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) mara baada ya kulitembelea
  Mkuu wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga,Godwin Gondwe wa pili kutoka kulia mwenye miwani akiwa kwenye picha ya pamoja  na watumishi wa shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) mara baada ya kulitembelea 

  Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  0 0

  Tembo 110 wamevamia mashamba ya wananchi na kufanya uharibifu wa mazao katika kata za Mbati,Kalulu,Namwinyu na Jakika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma na kuua mk azi mmoja wa Mbwembwele aliyejulikana kwa jina moja la Kalengo mwenye umri wa miaka 70, Taarifa zaidi hii hapa video yake.

  0 0


  Suleiman Msuya


  IKIWA ni takribani miezi 10 sasa kwa Chama cha Wananchi (CUF), upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad kuvamiwa katika Ofisi Kuu za Bugurunina kundi la Profesa Ibrahim Lipumba chama hicho kimezindua ofisi mpya za chama hicho katika eneo la Mtaa wa Idrisa, Kata ya Mzimuni, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

  Aidha, Seif amesisitiza kuwa hatarajii kukutana na  Profesa Lipumba kwa kile alichodai kuwa hatambuliki katika chama na hana  sifa hizo kwa sasa.


  Akizindua ofisi hiyo ambayo lengo kubwa ni kwa ajili ya wabunge 40 wa CUF, Seif alisema  uamuzi wa wabunge hao kumpatia ofisi ya kufanyia kazi hapo ni cha kiungwana na kinahitajika kuungwa mkono na wanachama wote.


  Alisema kwa muda wa miezi 10 sasa wamekuwa wakishindwa kufanya kazi hasa upande wa Tanzania Bara jambo ambalo limewaathiri sana hivyo kupatiwa ofisi kutamsaidia kutimiza majukumu yake vilivyo bila hofu yoyote.


  Maalim Seif alisema kukosa ofisi kumewaathiri sana katika baadhi ya mambo hivyo anaamini kwa sasa akifikia Dar es Salaam anamahali pa kukutana na wakurugenzi wake.


  “Nimekuwa ni kija hapa nakosa sehemu ya kukutana na wakurugenzi, viongozi mbalimbali wanachama ila hiki ambacho wabunge wamefanya ni cha kuungwa mkono sijawahi kufanya kazi na wabunge wanao kipenda chama kama kipindi hiki,” alisema.


  Katibu huyo alisema atahakikisha kuwa anaanza kazi haraka iwezekanavyo kwa kukutana na wakurugenzi wake ili waweze kutekeleza majukumu ya chama.


  “Hakuna shaka kuwa hu u unaoitwa mgogoro umeturudisha nyuma sana hivyo naamini wakati wa kufanyakazi umerejea na hawa wabaya wetu hawata ambulia kitu kwani CUF ni  chama imara hakitikisiki,” alisema.


  Maalim Seif alisema jitihada zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukimaliza chama ni kubwa lakini hawataweza kufikia lengo hilo kutokana na misingi ya chama hicho.


  Alisema kwa sasaa atafanya kazi katika ofisi hiyo ambayo amepewa na wabunge hadi hapo muafaka wa ofisi kuu Buguruni utakapopatikana huku akisisitiza kuwa haki haipotei ila inachelewa.


  Katibu huyo alisema anaimani na   mahakama kuwa ita wapatia haki stahiki hivyo kuwataka wanachama kuendelea kuwa na subira.


  Aidha, alisema kupitia mgogoro huo hadi sasa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini inashikilia zaidi ya sh. bilioni 1.2 ambazo ni ruzuku ya chamahicho.


  Maalim Seif alisema fedha hizo ni pamoja na zile ambazo ofisi ya msajili ilimpatia Lipumba hivyo waamini mgogoro ukiisha wata pata haki yao.


  Kwa upande mwingine Katibu huyo alisema hana mpango wa kukutana naLipumba kuhusu mgogoro unaondelea ndani ya chama hicho kwa kile alichodai kuwa si kiongozi wala mwanachama wa chama hicho.


  Alisema CUF haimtambui Lipumba kwa sifa yoyote tofauti na kumfukuza uanachama hivyo yeye hawezi kukukutana na mtu  kamahuyo.


  Maalim Seif alisema pamoja na kuwa hawamtambui Lipumba kama kiongozi au mwanachama ila akiomba msamaha wapo tayari kumsamehe.


  Akizungumza baada ya kuzinduliwa ofisi hizo Mbunge wa Viti Maalum na Kiongozi wa Wabunge wa CUF bungeni, Riziki Ngwali alisema wamelazimika kufungua ofisi nyingine ili wapate mahali pa kukutana wakiwa nje ya Bunge.


  Ngwali alisema kupitia ofisi hiyo wataweza kujadiliana mambo mbalimbali yanayo wahusu wabunge na wananchi na kuja na ufumbuzi.


  Kwa upande wake Mbunge wa Temeke CUF, Abdallah Mtolea alisema katika ofisi hiyo wanatarajia kuajiri wataalam mbalimbali ambao watasaidia kufanya tafiti na kupitia tarifa mbalimbali za Bunge ili kuwarahisishia katika uchangiaji bungeni.
  Alisema katika ofisi hizo wameingia mkataba wa kulipa sh. milioni 18 kwa mwaka ambazo zitatolewa na wabunge wenyewe kwa maslahi ya chama chao.


  0 0

  Waziri wa Malisili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho ya tatu ya kimataifa ya Utalii yanayofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu Ushirika mjini Moshi.
  Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Devota Mdachi akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho makubwa Afrika Mashariki ya Utalii na Viwanda yanayofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu Cha Ushirika mjini Moshi.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB,Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akisalimia wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo.
  Mkurugenzi Mwenza wa Kampuni ya Kili Fair inayoratibu maonesho hayo Dominic Shoo akisoma taarifa kuhsu maonesho hayo yanayofanyika wa mara ya tatu sasa .
  Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akitoa neno kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya Kili Fair yanayojumuisha zaidi ya washiriki 300 kutoka nchi tisa.
  Mkurugenzi wa Kili Fair ,Dominic Shoo akimuongoza mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho hayo,Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe kutembelea sehemu maonesho katika uwanja wa Ushirika mjini Moshi.
  Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akimsadia Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii,TTB Bi Devota Mdachi kufika katika eneo la mfano wa Kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
  Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe ,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi (TTB) Jaji Mstaafu ,Thomas Mihayo,Mkuu wa wilaya ya Moshi Kippi Warioba na viongozi wengine wakiwa katika kilele cha Uhuru cha Mfano kilichopo katika maonesho yanayoendelea katika uwanja wa chuo kikuu cha ushirika mjini Moshi.
  Waziri wa Malisili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine mara baada ya kufungua maonesho ya Kili Fair.
  Waziri Prof Maghembe akitizama ngoma ya kikundi cha jamii ya Maasai kikitoa burudani katika maonesho hayo.
  Bidhaa mbalimbali na zikiwa katika mabanda ya maonesho ndani ya uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi ambako maonesho ya Kili Fair yanafanyika.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Britam-Tanzania, Stephen Lokonyo akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam wiki iliyopita, wakati wa uzinduzi wa bima ya afya hapa nchini. Katikati ni Mkuu wa Bima ya Afya ya kampuni hiyo, Christine Mungi na kulia ni Mkuu wa Fedha na Utawala, Irene Godson.


  Na Dotto Mwaibale


  KAMPUNI ya Bima ya Britam-Tanzania imezindua bima ya afya inayolenga kuhudumia makampuni makubwa, biashara ndogo na za kati (SMEs).

  Bima hii inajumuisha gharama za matibabu ya wagonjwa waliolazwa, vipimo vya magonjwa mbalimbali pamoja na majeraha yaliyotokana na ajali kwa waajiriwa wasiopungua 10. Bima hii itagharimu kati ya shilingi milioni 5 mpaka milioni 200.

  Akiongea katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo,Steven Lokonyo alisema bima hii itagharamia kumsafirisha mgonjwa mahututi mpaka hosipitali, ushauri wa daktari, gharama za chumba maalumu cha uangalizi (ICU), mazoezi ya viungo, tiba ya mionzi, pamoja gharama za upasuaji.

  Pia bima hii itagharamia kumsafirisha mgonjwa mahututi kwa ndege au gari kwenda hosipitali kupata huduma za matibabu, gharama za uchunguzi za eksirei na uchunguzi wa  kimaabara.  

  "Bidhaa hii tunayoileta kwenye soko inakuja kuleta mabadiliko katika sekta ya afya na itaenda mbali kusaidia biashara ndogo na za kati na makampuni makubwa hivyo kukuza ustawi pamoja na uzalishaji wa wafanyakazi wao" alisema Lokonyo.

  Lokonyo alibainisha pia kwamba bima hiyo ina faida za nyongeza kama vile tiba ya ugonjwa sugu uliogunduliwa, magonjwa ambayo mtu anayo kabla ya kuanza kutumia bima,UKIMWI na magonjwa mengine kama kisukari, kansa, magonjwa ya figo, ukurutu, maumivu ya viungo, magonjwa ya ini na kadhalika.

  Uzinduzi wa bima hiyo umefanyika kwa kuzingatia uhitaji wa soko pia ni mkakati wa kampuni kupanua biashara yake ya bima nchini kwa kuangalia makundi ya watu ambayo yalikuwa hayajafikiwa na huduma za bima.

  "Bima hii imeanzinduliwa kwa kuangalia uhitaji wa biashara ndogo na za kati pamoja na makampuni. Kampuni yenye wafanyakazi 10 sasa inaweza kupata huduma ya bima ambayo kila mtu anajua afya ya wafanyakzi ni muhimu kwa biashara yoyoye" aliongeza Lokonyo.

  Takwimu za hivi karibuni zimeonyesha kuwa matumizi ya bima nchini Tanzania ni chini ya asilimia moja ya pato la taifa ambacho ni kiwango cha chini ukilinganisha na nchi zilizoendelea na nchi nyingine nyingi za kiafrika. Katika jitihada zake za kufikia watanzania wengi zaidi, Britam inapanua matawi yake nchini ambapo kwa sasa wapo katika mikoa saba ya Dar-es-salaam, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Mtwara, na Arusha.

  Kampuni ya bima ya Britam Tanzania amabayo ilijulikana kama kama 'Real Insurance' hapo mwanzo ni kampuni tanzu ya 'Britam Holdings' ambayo inatoa huduma mbalimbali za kifedha katika bima, usimamizi wa mali, na benki.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipanda mti kwenye Msitu wa asili ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye kilele cha siku ya mazingira duniani ambapo kitaifa imeadhimishwa Butiama. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimwagia maji mti alioupanda kwenye Msitu wa asili ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye kilele cha siku ya mazingira duniani ambapo kitaifa meadhimishwa Butiama. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shda la maua kwenye Mnara wa kumbukumbu ya ajali ya ndege ya kivita iliyotokea mwaka 1978 kwenye Msitu wa Muhunda ,wilayani Butiama mkoani Mara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na Mama Maria Nyerere nyumbani kwa Mama Maria Butiama leo mara baada ya kuhutubia kwenye kilele cha siku ya mazingira Duniani.#Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
   
  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Wananchi kijijini Butiama mkoani Mara wakati wa kilele cha siku ya mazingira Duniani.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kiatu cha kusaidia walemavu wakati alipotembelea banda la Kituo cha Walemavu cha Ziwa Victoria (Lake Victoria Disability Centre) kinachoshughulika na kutengeneza viungo bandia kwa watu wenye ulemavu kabla ya kuhutubia kwenye kilele cha siku ya mazingira duniani ambapo kilele chake kimefanyika kwenye viwanja vya Mwenge,Butiama
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia namna samaki anaweza kufugwa vizuri bila kuharibu mazingira na kuleta manufaa kabla ya kuhutubia kwenye kilele cha siku ya mazingira duniani ambapo kilele chake kimefanyika kwenye viwanja vya Mwenge,Butiama

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameagiza kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kwa viwanda na migodi ambayo inafanya shughuli zake za uzalishaji kwa kuharibu mazingira ikiwemo utitirishaji wa kemikali kwa wananchi kwani kufanya hivyo kunahatarisha usalama wa wananchi na viumbe hai wengine.

  Makamu Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo tarehe 4-Jun-2017 kijijini Butiama mkoani Mara wakati anahutubia wananchi katika kilele cha siku ya mazingira Duniani.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema uharibifu wa mazingira ukiachiwa uendee nchini ni hatari kwa usalama wa maisha na viumbe hivyo ni muhimu kwa viongozi katika ngazi zote kuchukua hatua zitakazosaidia kukabiliana na vitendo hivyo kote nchini.

  Makamu wa Rais amesisitiza kuwa umefika wakati kwa viongozi kwa ushirikiano na jamii kuhakikisha wanaweka mikakati ya kuokoa mifumo ya ikolojia, uhifadhi wa bioanuai, kudhibiti uchomaji miti kiholela ili kurejesha uoto wa asili ambao umeharibiwa na shughuli mbalimbali za kibinadamu katika maeneo mengi nchini.

  “Kutozingatia hifadhi ya mazingira kunaweza kusababisha kuparaganyika kwa mfumo huo na kufanya maisha yetu na ya vizazi vijavyo kuwa mashakani”. Amesisitiza Makamu wa Rais.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema katika kuadhimisha siku ya mazingira Dunia viongozi wanapaswa kuchukua hatua za kuelimisha wananchi na kuwahamasisha ili kila mtu ashiriki katika juhudi za kuwa na uchumi unaozingatia hifadhi ya mazingira.

  Kuhusu wananchi kutembelea hifadhi za taifa nchini, Makamu wa Rais aipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuruhusu wananchi kutembelea hifadhi za taifa bila kiingilio na kusema mpango huo ni mzuri na unatakiwa kufanyika kila mwaka.

  Amesema kuwa mkakati huo unalenga kuhamasisha wananchi ili kuwa mahusiano rafiki na mazingira kwa kuzingatia ukweli kwamba jinsi wananchi wanapoona ndipo wanapoamini na kuelewa umuhimu wa uhifadhi wa mazingira.

  Ameeleza kuwa katika kuadhimisha siku hiyo inapasa jamii kutafakari mchango wa kila sekta na kila mwananchi katika uhifadhi wa mazingira kwenye maeneo wanayoishi.

  Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira January Makamba amesema Serikali imeamua kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani kijijini Butiama kama hatua ya kuenzi mchango mkubwa uliofanya na baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere katika uhifadhi wa mazingira.

  Amesema baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere alifanya kwa vitendo katika kuhifadhi mazingira ambapo alianzisha msitu wake katika eneo la Butiama hivyo wananchi wote ni lazima waige mfano huo katika kulinda na kutunza mazingira.

  Kwa upande wa familia na mwalimu Nyerere wameishukuru Serikali kwa kupeleka maadhimisho hayo kijijini Butiama ikiwa ni sehemu ya kuenzi na kutambua mchango wa baba wa taifa katika uhifadhi wa mazingira nchini.

  Kabla ya Kuhutubia katika Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan alipanda miti katika msitu wa Mwalimu Nyerere na kuweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya ajali ya Ndege ya Kivita ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) uliopo katika msitu wa Muhunda katika kijiji cha Butiama mkoani MARA.

  0 0

  Wa kwanza kushoto ni Muasisi wa Tanzania Tour Guide Awards Sadock Mugetta, aliyepo kushot kwake ni Katibu wa Freelance Guides Society of Tanzania(FGST )anayefuata ni mjumbe wa  wakiwa katika maonyesho ya (3)Utalii ya Kilifair  katika uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro.


  Na.Vero Ignatus Kilimanjaro.

   Wito umetolewa kwa waongoza watalii nchini kutoa ushirikiano ,kuwapendekeza watakaoingia katika kinyang'anyiro cha kumtafuta mshindi wa Tuzo ambayo imeandaliwa kwaajili ya kumpata Balozi atakaewawakilisha waongoza utalii nchini Tanzania,Afrika ya Mashariki na Kati .

  Akizungumza na blog hii Muasisi na mwenyekiti wa Tuzo hiyo Sadock Mugetta amesema kuwa tuzo  inafahamika kama  TANZANIA TOURGUIDE AWARDS   ambapo mwaka jana ilikuwa imegawanyika   katika vipengele vya kumtafuta muongoza watalii bora wa Mlima,Safari pamoja na Wapagazi,ila mwaka huu wameongeza vipengele viwili ambavyo ni Muongoza utalii wa Utamaduni pamoja na Mpishi bora.

  Sadock amesema kuwa wameamua kuwepo kwa Tuzo hiyo kutokana hali halisi iliyopo ya ugumu wa kazi wanayoifanya waongoza watalii (Mabalozi) ili mshindi atakayepatikana atawawakilisha katika mambo yao ambayo wanataka Serikali iyafahamu,pamoja na wageni mbalimbali waitambue Tanzania pamoja na vivutio vya Utalii vilivyopo.

   Ameongeza kuwa tangia kuanzishwa kwa huduma ya  utalii hapa nchini waongoza Watalii  hawajawahi kupewa kipaumbele, hivyo ni vyema Serikali ikatambua kuwa muongozaji watalii huwa  anatumumia 99% ya muda wao  kukaa na mgeni awapo nchini na anapewa taarifa zote sahihi na muhimu  hadi anaondoka nchini. 

  "Ikumbukwe kuwa tangia kuanzishwa kwa huduma hii ya utalii waongozaji hawajawahi kupewa kipaumbele wakati anatumia 99%ya muda wake na mgeni akiwa hapa nchini ,anahakikisha mgeni yupo salama,anahakikisha mgeni anapata taarifa zote sahihi hadi anaondoka nchini,muongozaji huyu anafanya kazi yake kama mwalimu,Daktari pale mgeni anapopata taizo anampatia huduma ya kwanza,mpishi,mpatanishi na Balozi mwaminifu".alisema Sadock.

  Kwa upande wake Katibu wa Waongoza watalii wa kujitegemea Ally Mtemvu amesema kuwa hakuna mgeni anayekuja nchini kufanya utalii pasipokuwa na muongozajiamesema tuzo hiyo inawashirikishwa makampuni yote ya utalii ,wadau wa utalii KIATO,TATO, pamoja  KGA,TTGA,FGST,KTAS,TTG,KILIMERU,TPO,MMPA,NCPG na NMPA

  " Hivyo tunaiomba Wizara ya Utalii na Maliasili watuunge mkono kuhakikisha kuwa tuzo hii ya Afrika Mashariki na Kati zinakuwa bora zaidi kwakuwa tumewatangulia na imeasisiwa nchini Tanzania "alisema Ally.

  Aidha Tuzo hii ilizinduliwa rasmi mwaka 2016 mkoani Arusha ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Anjelina Madete,ambapo mwaka huu 2017 itafanyika jijini Dar es salaam kwenye maonyesho ya SITE october 13-15,2017 ambapo mgeni rasmi atafahamika hapo baadae.

  Mwisho wa mapendekezo ya majina ni tarehe 30/6/2017  0 0

   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj Abdallah Bulembo akipandisha bendera, kuzindua Shina namba sita la CCM la Kiyobela, Katika Kijiji cha Kabiko wilayani Kakonko mkoani Kigoma, leo.
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj Abdallah Bulembo akiondoa bendera kwenye jiwe la Msingi, kuzindua Shina namba sita la CCM la Kiyobela, Katika Kijiji cha Kabiko wilayani Kakonko mkoani Kigoma, leo.
   Wanacha wa Jumuia ya Wazazi wakimpa zawadi ya asali baada ya kuzindua Shina hilo.
   Viongozi wa Shina hilo, wakimkabidhi Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj Abdallah Bulembo risala yao waliyosoma wakati wa uzinduzi wa shina hilo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Kakonko Ayub Ngaramo na Watatu kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kaborou
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj Abdallah Bulembo akishiriki kuselebuka na Kinamama wa CCM waliompokea alipowasili kuzindua shina Namba Sita la CCM la Kiyobela, Katika Kijiji cha Kabiko wilayani Kakonko mkoani Kigoma, leo.
   Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Kigoma, Mbunge wa viti maalum Josephine Ngezabuke (watatu kushoto), akiselebuka na Kina mama wa CCM wakati wa uzinduzi wa Shina hilo.
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj Abdalla Bulembo akisaini kitabu cha wageni Kabla ya kuzindua Shina namba Sita la CCM la Kiyobela, Katika Kijiji cha Kabiko wilayani Kakonko mkoani Kigoma, leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kabourou na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kakonko Ayub Ngaramo
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulelmbo akimwambia jambo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala, baada ya kuzindua Shina namba Sita la CCM la Kiyobela, Katika Kijiji cha Kabiko wilayani Kakonko mkoani Kigoma, leo. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma Naomi Kapambala
   Mjube wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya viongozi, alipokagua ujenzi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, leo
   Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma, Naomi Kapambala na Baadhi ya viongozi wakitazama ujenzi wa ofisi hiyo unavyoendelea. 
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo 'akitroti' kidogo, wakati akitoka kukagua ujenzi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma leo
   Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Kakonko

   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akipandisha bendera kuzindua Shina la CCM Namba Sita, Tawi la Kakonko Msufini, Wilayani Kakonko mkoani Kigoma, leo. Kulia (aliyeketi) ni Mwenyekiti wa Shina hilo Ramadhan Adam ambaye ana ulemavu wa miguu. 
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akiondoa kitambaa kuzindua Shina la CCM Namba Sita, Tawi la Kakonko Msufini, Wilayani Kakonko mkoani Kigoma, leo. 
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj Abdallah Bulembo akimsalimia Mwenyekiti wa Sina la CCM Namba Sita, Tawi la Kakonko Msufini, Wilayani Kakonko mkoani Kigoma, Ramadhan Adam mwenye ulemavu wa miguu, baada ya kuzindua shina hilo.
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ahlaj Abdallah Bulembo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM, baada ya kuzindua shina hilo hilo
   Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kakonko, Mabalozi, Viongozi na watendaji wa CCM, Watendaji wa Serikali na Viongozi mbalimbali wa CCM na Jumuia zake. Walisimama kwa nderemo na vifijo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj Abdallah Bulembo alipokuwa akiingia ukumbini kuzungumza nao katika kikao cha ndani.
   Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kakonko, Mabalozi, Viongozi na watendaji wa CCM, Watendaji wa Serikali na Viongozi mbalimbali wa CCM na Jumuia zake. Walisimama kwa nderemo na vifijo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj Abdallah Bulembo alipokuwa akiingia ukumbini kuzungumza nao katika kikao cha ndani.
    Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kakonko, Mabalozi, Viongozi na watendaji wa CCM, Watendaji wa Serikali na Viongozi mbalimbali wa CCM na Jumuia zake. Walisimama kwa nderemo na vifijo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj Abdallah Bulembo alipokuwa akiingia ukumbini kuzungumza nao katika kikao cha ndani.
    Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kakonko, Mabalozi, Viongozi na watendaji wa CCM, Watendaji wa Serikali na Viongozi mbalimbali wa CCM na Jumuia zake. Walisimama kwa nderemo na vifijo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj Abdallah Bulembo alipokuwa akiingia ukumbini kuzungumza nao katika kikao cha ndani.
  KIKAO CHA NDANI🔻 
   Katibu wa CCM wa CCM mkoa wa Kigoma Naomi Kapampala akifanya utambulisho kabla ya Mjumbe wa Kamati ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo kuzungumza  katika kikao cha ndani cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kakonko, Mabalozi, Watendaji wa Serikali na Watendaji wa CCM na viongozi mbali mbali wa CCM na Jumia zake, leo.
   Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akisalimia baada ya kutambulishwa kwenye kikao hicho 
   Nwebyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Kigoma, Mbunge wa Viti Maalum Josephine Ngenzabuke akisalimia baada ya kutabulishwa kwenye kikao hicho
   Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kakonko Ayub Ngaramo akifungua kikao hicho.
   Ofisa kutoka Makao Makuu ya Jumuia ya Wazazi Tanzania Omar Kalolo akitamba ukumbini wakati akisalimia baada ya kutambulishwa
   Msaidizi katika Ofisi ya Siasa na Oganaizesheni Makao Makuu ya Jumuia ya Wazazi Tanzania Fadhili Mlami akisalimia baada ya kutambulishwa kwenye kikao hicho
   Baadhi ya maofisa na wadau wakiwa kwenye kikao hicho
   Katibu wa Siasa na Oganaizesheni Makao Makuu ya Jumuia ya Wazazi Tanzania Daniel Mgaya akisalimia baada ya kutambulishwa kwenye kikao hicho
   Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk. Amani Kaborou akikmaribisha Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo kuzungumza katika kikao hicho
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kakonko, Mabalozi, Viongozi na watendaji wa CCM, Watendaji wa Serikali na Viongozi mbalimbali wa CCM na Jumuia zake, kikao hicho cha ndani.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kakonko, Mabalozi, Viongozi na watendaji wa CCM, Watendaji wa Serikali na Viongozi mbalimbali wa CCM na Jumuia zake, kikao hicho cha ndani. PICHA: BASHIR NKOROMO

older | 1 | .... | 1258 | 1259 | (Page 1260) | 1261 | 1262 | .... | 1904 | newer