Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

Dau nono la Milioni 10 za Biko laenda kwa Junior Pesambili wa Makete

$
0
0
DAU nono la Sh Milioni 10 linalotolewa kama zawadi ya droo kubwa ya Mchezo wa Kubahatisha wa Biko limeenda kwa Junior Ashery Pesambili wa Lupela, Makete, mkoani Njombe, ikiwa ni mwendelezo wa kugawa fedha kwa washindi wake ikitokana na matokeo ya droo ya 11 iliyochezeshwa jana Jumapili.

Droo hiyo iliyochezeshwa jana iliendeshwa na Balozi wa Biko Kajala Masanja, akishirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid. Akizungumza katika droo hiyo jana, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, alisema wamedhamiria kugawa mamilioni kwa washindi wao wanaocheza mchezo wa Biko uliozidi kushika kasi katika kona mbalimbali nchini Tanzania.
Alisema tayari wameshafanya droo 11 kubwa ambapo watu mbalimbali wameendelea kupokea fedha zao ikihusisha vijana bila kusahau mzee Stanley Kapondo naye aliyekuwa miongoni mwa Watanzania waliovuna zawadi mbalimbali kutoka Biko.

“Kucheza Biko mara nyingi zaidi ndio nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi, hivyo ni wakati wa Watanzania kucheza mara nyingi ili washinde, ukizingatia kuwa mbali na donge nono la Milioni 10 linalotolewa Jumatano na Jumapili, pia mtu anaweza kushinda zawadi mbalimbali kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000, 1,000,000, huku droo ya Jumatano hii ikitoa Sh Milioni 20 kwa mshindi wake kama ilivyokuwa Jumatano iliyopita.

“Mchezo wetu unachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo utakapoingia kwenye kipengele cha Lipa Bili au lipa kwa Mpesa, mshiriki wetu ataingiza namba ya kampuni 505050 na baadaye kuweka namba ya kumbukumbu 2456, huku akianzia kucheza kwa Sh 1000 au zaidi,” Alisema Grace.


Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja, kulia akionyesha namba ya ushindi wa Sh Milioni ya mshindi wao wa Lupela, Makete,mkoani Njombe, Junior Ashery Pesambili aliyepatikana katika droo ya jana Jumapili. Kushoto ni mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.

Balozi wa Biko Kajala Masanja akifurahia namba ya mshindi wa Sh Milioni 10 kutoka Makete, mkoani Njombe, droo iliyochezeshwa jana jijini Dar es Salaam.
Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid, aliwapongeza Biko kwa kuchezesha bahati nasibu inayovutia na inayotoa ushindi mnono kwa kupitia simu za mikononi.“Ni utaratibu mzuri unaofanywa na Biko katika kuchezesha bahati nasibu yao, hivyo sisi watu wa Bodi tunachofanya ni kuangalia kama taratibu na sheria zinafuatwa ili kuhakikisha kuwa kila kitu kinakwenda vizuri, hivyo natoa rai kwa kila Mtanzania kucheza Biko ili waibuke na ushindi,” Alisema Maggid.
Akizungumza kwa simu wakati anatangazwa, mshindi huyo hakusita kuonyesha furaha yake, akisema haamini kama ameshinda Milioni 10 za Biko akiongeza kwamba ni wakati wake kukuza uchumi wake kwa kupitia mchezo wa Biko ambao umekuja na kuboresha kipato chake.

“Nashukuru kutangazwa mshindi wa droo ya 11 ya Biko, ambapo kushinda kwangu naamini ni wakati muafaka sasa wa kufanikiwa kimaisha kwa sababu Mungu amepanga jambo zuri kwangu,ukizingatia kwa sasa najishughulisha na kazi ya uchanaji wa mbao” Alisema. Baada ya kuibuka na donge hilo, mshindi huyo wa Biko anatarajiwa kukabidhiwa fedha zake haraka iwezekanavyo ili aziingize kwenye matumizi yake ya kimaisha kwa ajili ya kuinua kipato chake.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JUNE 5,2017

MAONENSHO YA SWAHILI FASHION WEEK YAFANA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Balozi wa Italia Nchini Tanzania, Roberto Mengoni (kushoto) akibadilishana mawazo na Mbunifu wa Mavazi nguli Mustafa Hassanal pia Mwasisi na Mtendaji Mkuu wa Basila Mwanukuzi Foundation, Basila Mwanukuzi katika maonesho ya Mavazi na bidhaa za Kitamaduni nyumbani kwa Balozi huyo Kando ya Barabara ya Kenyatta Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Maonesho hayo yaliratibiwa na Swahili Fashion Week. (Picha zote na Robert Okanda Blogspot) 
Mbunifu wa Mavazi nguli Mustafa Hassanal akiwa pamoja na Mbunifu mavazi Mkongwe Ailinda Sawe (kulia) na Mbunifu mchanga, Binti wa Ailinda walipokutana katika maonesho hayo. 
Mbunifu wa mavazi, Maryimaqulate Kavishe (kulia) akiwahudumia wageni waliotembelea kununua bidhaa zake wakati wa maonesho hayo. 
Mbunifu wa mavazi, Jesca Matei (kushoto) akiwasikiliza wageni waliotembelea kununua bidhaa zake wakati wa maonesho hayo. 
Mshiriki wa maonesho hayo Coleta Mzena (kushoto) akitabasamu kwa kamera pamoja na wageni waliotembelea kununua bidhaa zake wakati wa maonesho hayo. 
William Gilhi akiwaonesha wageni bidhaa za Kampuni ya African Splash zinazopatikana pia online walipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho hayo. 
Kazi za michoro pia zilikuwepo katika maonesho hayo. 
Wageni bidhaa wakichagua bidhaa zizizowavutia walipotembelea moja ya mabanda katika maonesho hayo. 
Hapo upo saafi' Mbunifu wa Agretifela, Agnes Felician akimhamasisha mteja wake kununua moja ya bidhaa katika banda lake. 
Wabunifu wa Giftedhand, wakiwa katika banda lao. 
Wageni wakijionea bidhaa walipotembelea mojawapo ya mabanda katika maonesho hayo. 
Mbunifu nguli Jamila Vera Swai naye akiandaa bidhaa zake kwa wageni waliojitokeza katika maonesho hayo. 
Mbunifu wa Mavazi nguli Mustafa Hassanal akiwa katika kumbukumbu na Mwasisi na Mtendaji Mkuu wa Basila Mwanukuzi Foundation, Basila Mwanukuzi katika maonesho ya Mavazi na bidhaa za Kitamaduni nyumbani kwa Balozi wa Italia Kando ya Barabara ya Kenyatta Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Maonesho hayo yaliratibiwa na Swahili Fashion Week. 
Mbunifu wa Mavazi pia Mtendaji Mkuu wa Kasikana Collection, Bertha Komba (kushoto) akiwa na Modal Bint Sadiq katika maonesho hayo. 

ALICHOKIZUNGUMZA KAIMU KAMISHNA WA USATWI WA JAMII BAADA YA MKUTANO ULIOANDALIWA NA UNHCR NA UNICEF

NAKURU ALL STARS WAJIFUA KUMKABIRI MNYAMA SIMBA KESHOKUTWA SPORTPESA SUPER CUP UWANJA WA UHURU

$
0
0
 Wachezaji wa timu ya Nakuru All Stars ya Kenya wakiwa katika mazoezi ya pamoja katika Uwanja wa karume jijini Dar es Salaam, jioni ya leo Juni 4, 2017  kujiandaa na michuano ya 'SportPesa Super Cup' inayoanza kutimua vumbi kesho Juni 5 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini, ambapo mechi ya kwanza itakuwa ni kati ya Singida Utd na AFC Leopards, mechi ya pili itakuwa ni kati ya wenyeji Yanga na Tusker Fc na Juni 6 mchezo wa kwanza utakuwa ni kati ya Simba vs Nakuru All Stars na mchezo wa pili utakuwa ni kati ya Gor Mahia Vs Jang'ombe Boys Fc.
 Wachezaji wa nakuru All Stars wakishuka katika gari lao walipowasili uwanja wa Karume kuanza mazoezi, leo jioni.

 Mazoezi yakiendelea. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
 Daktari wa timu akimchua mchezaji misuri kabla ya kuanza mazoezi...
 Dua na maelekezo kabla ya kuanza mazoezi...
 Mazoezi ya viungo
 Wachezaji wakiapasha misuri moto
 Makipa wa timu hiyo wakipasha misuri moto.


MWANAMUZIKI HALILA TONGOLANGA AFARIKI DUNIA

$
0
0

HALILA TONGOLANGA, mwanamuziki wa siku nyingi ambaye alikuwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. Halila alikuwa amesafirishwa kutokea Ndanda kuja Muhimbili akihisiwa kuwa na matatizo ya figo. Licha ya kuwa alifika Muhimbili juzi Ijumaa usiku, lakini alikuwa hakufanyiwa vipimo vyovyote vikubwa mpaka umauti unamkuta. 
Jana Jumapili ililazimika kuanza kufanya jitihada za kupata daktari ambaye angemshughulikia kwa karibu zaidi, na daktari alipatikana ambaye aliahidi angeanza kufwatilia swala lake leo asubuhi lakini mapenzi ya Mungu yalikuwa tofauti. Juzi nilipomuona alinambia kuwa ana mengi anataka kunambia, lakini moja aliloweza kunambia pale ni kuwa yeye anajihisi ana kansa, 'Nilimuuliza anajuaje hilo, kwa vile hajapimwa hakuwa na jibu"

Wengi tutamkumbuka Tongolanga kwa wimbo wake wa Kimakonde aliouimba kwa mara ya kwanza akiwa na Les Mwenge 'Kila Munu Ave Na Kwao"

Mwili wa marehemu unategemewa kusafirishwa leo saa tano kuelekea kwao Newala. Habari zaidi zitawafikia kupia hapa

Mungu amlaze Pema peponi Halila Tongolanga 

MKOLANI VETERANI NDIYO MABINGWA WA 'JEMBE FM SPORTS RIPOTI BONANZA 2017' MWANZA

$
0
0
Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr. Sebastian Ndege (kushoto) akiwa na mgeni Rasmi Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Mwanza, Leonard Malongo (katikati) kwa pamoja wakikabidhi zawadi ya seti moja ya jezi kwa team captain wa Mkolani Veterani Fc mara baada ya kuibuka kuwa Mabingwa wa 'JEMBE FM SPORTS RIPOTI BONANZA 2017, katika uwanja wa Nyamagana. Chini ya udhamini wa Nebrix Limited wauzaji wa vifaa vya michezo na Lake Zone Tents Supply.
Si mchezo 'Miaka miwili ya changamoto hatimaye sasa nuru imeonekana'
Risala ya maadhimisho ilisomwa na Elikana Mathias.
Safu ya Meza kuu.
Mbele ya eneo la kivuli tulilolichagua kuwa jukwaa kuu.
Ni miaka miwili ya changamoto na mafanikio makubwa "Aksante sana Mwanza"
Mkurugeniz wa Jembe Media Group Dr. Sebastian Ndege akitoa shukurani kwa wananchi wa mkoa wa Mwanza wapenzi wa soka na burudani mara baada ya ushiriki wao kuweza kufanikisha tamasha la kusherehekea miaka miwili ya kipindi cha 'Sports Ripoti' kinachoruka kila siku usiku saa 3 kamili hadi 4 ikiwa ni kwa mara ya kwanza tukio hilo kufanyika, naye ameahidi kwamba maadhimisho hayo yatakuwa yakifanyika kila mwaka ambapo mwakani yataboreshwa zaidi. 
Meneja wa Vipindi Redio Jembe Fm Mwanza Timothy Ngalula aka Mbaba Vc sanjari na kutoa shukurani kwa wadau Mwanza na mikoa tofauti tofauti (kupitia enternet) hapa alitambulisha safu ya watangazaji vitengo na vitengo.
Natty E eneo la tukio uwanja wa Nyamagana.
Johari Ngassa na tambo zake.......
Vanessa aka Sports Lady.
Makeke ya Babu Mkombe .
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Mwanza, Leonard Malongo ambaye alikuwa Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya miaka miwili ya kipindi cha Sports Ripoti cha Jembe Fm akihutubia mamia ya wananchi mkoa wa Mwanza waliofika uwanja wa Nyamagana
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Mwanza, Leonard Malongo ambaye alikuwa Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya miaka miwili ya kipindi cha Sports Ripoti cha Jembe Fm akimlisha keki mtangazaji meneja wa kipindi husika Elikana Mathias.
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Mwanza, Leonard Malongo ambaye alikuwa Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya miaka miwili ya kipindi cha Sports Ripoti cha Jembe Fm akimlisha keki mtangazaji wa kipindi husika ambaye pia ni team captein Juma Ayoo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Mwanza, Leonard Malongo ambaye alikuwa Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya miaka miwili ya kipindi cha Sports Ripoti cha Jembe Fm akimlisha keki mtangazaji wa kipindi husika 'Masamaki'
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Mwanza, Leonard Malongo ambaye alikuwa Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya miaka miwili ya kipindi cha Sports Ripoti cha Jembe Fm akimlisha keki mtangazaji wa kipindi husika 'Sports lady' Vanessa. 
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Mwanza, Leonard Malongo ambaye alikuwa Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya miaka miwili ya kipindi cha Sports Ripoti cha Jembe Fm akimlisha keki mtangazaji wa kipindi husika Moses.
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Mwanza, Leonard Malongo ambaye alikuwa Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya miaka miwili ya kipindi cha Sports Ripoti cha Jembe Fm akimlisha keki Mwenyekiti wa zamani MZFA Jackson Songora.
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Mwanza, Leonard Malongo ambaye alikuwa Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya miaka miwili ya kipindi cha Sports Ripoti cha Jembe Fm akimlisha keki mchezaji wa zamani wa Pamba Fc na Yanga Africans Fumo Felician kama ishara ya shukurani.
Mshindi wa kufukuza kuku upande wa wanaume mkazi wa Igoma jijini Mwanza.
Mshindi aliyeibuka kufukuza kuku upande wa wanawake mkazi wa Mabatini jijini Mwanza.
Kwa hisani ya Heinkein ....mara baada ya vipute tulielekea kucheki fainali ya UEFA Champions League Juventus Vs Real Madrid.
Akisimulia mchezo na yatokanayo dimbani huyu ni mtangazaji wa Hit Zone majira ya saa 7 mchana hadi 10 jioni wakuitwa Babajuti.
Mtangazaji wa Sports Ripoti Juma Ayoo.
Kona ya kushoto upande wa Kaskazini Magharibu...
Wayaaaaaaa kipa wa Mjengoni Fc akiutizama mpira ....ukizama kimiani.
Macho kwenye soka.
Golikipa wa Mkolani Veterani ndiye aliyeleta shangwe kwa timu hiyo baada ya kudaka mkwaju wa kipa mwenzake wa Mjengoni Fc aka Bodaboda, ikiwa ni baada ya michomo yote kumi toka kwa wachezaji wa kila timu kushindwa kutoa mshindi.
Hureeeeeeee......
Mkolani Veterani wakisherehekea mara baada ya kuwafungwa kwa penati Mjengoni FC aka Bodaboda kutoka Sauti Malimbe jijini Mwanza


Nyuma ya kamera. 



TANZANIAN FANS TREATED TO AN EXCLUSIVE NIGHT OF STARS DURING THE UEFA CHAMPIONS LEAGUE FINALS

$
0
0
Consumers of Heineken® championing the match during the UEFA Champions League final viewing which pitted Real Madrid against Juventus. Real Madrid went on to win 4- 1 and were declared 2017 UCL winners. Heineken®, the world's leading international premium beer brand, is the official partner of the world's most prestigious club football competition.
Tanzanian football fans enjoying themselves during the 2017 UEFA Champions League final viewing in Dar es Salaam. Heineken®, the world's leading international premium beer brand, is the official partner of the world?s most prestigious club football competition. Real Madrid went on to win 4- 1 against Juventus football club and were declared 2017 winners. While championing the match, Tanzanians fans were also treated to free merchandise from Heineken Tanzania.
Tanzanian football fans enjoying themselves during the 2017 UEFA Champions League final viewing in Dar es Salaam. Heineken®, the world's leading international premium beer brand, is the official partner of the world?s most prestigious club football competition. Real Madrid went on to win 4- 1 against Juventus football club and were declared 2017 winners. 

While championing the match, Tanzanians fans were also treated to free merchandise from Heineken Tanzania. --- Thrilling match night for football fans across Tanzania as Heineken engaged patrons on the ‘#ChampionTheMatch’ consumer campaign Dar es Salaam, June 4 2017 - Heineken Tanzania yester night engaged and excited throngs of Tanzanian football fans at the culmination of 2017 UEFA Champions League (UCL) final which saw REAL MADRID whoop JUVENTUS FOOTBALL CLUB by four goals to one (4-1), hence crowned 2017 UCL champions. 

 Cardiff, Wales was the home of another history making football moment, with the UEFA Champions League finals between Juventus and Real Madrid. And, Tanzanian Football fans shared in the moment, at various outlets across the country, where Heineken once again presented the biggest viewing parties ever. The Heineken viewing parties, besides the main showpiece which is the UEFA Champions League Final, also featured chances to win awesome Heineken merchandize. 

 While the game officially kicked off at 9.45 pm, Heineken brought some thrills, fun and excitement to radio, TV presenters, print journalists, bloggers and celebrities from 6 pm and even after the final whistle – until midnight. For this year’s Heineken UEFA Champions League exclusive viewing Party, which was open to select media personalities, ice cold Heineken was on special during the event as well as a few special surprises. Heineken’s 2017 UEFA Champions League promotions hinging on Champion the match campaign also included thrilling bar promotions, which culminated on 3rd June 2017 at George & Dragon Pub, Samaki Samaki and other outlets spread across Tanzania. 

The premium brewer has reiterated that the campaign remains the base of their UEFA Champions league communication. The campaign has achieved broader appeal of match nights before, during and after the game. In addition football fans enjoyed additional entertainment and got opportunities to win prizes in the different establishments that Heineken activated at.

 In a statement released to news rooms, The Country Manager of Heineken Tanzania, Michael Mbungu noted that, ‘‘So far we have witnessed world class football performance in the Champions League games semi finals. 

We were very thrilled that Tanzanian soccer fans turned up in droves to bear witness to a battle of true champions. At Heineken we saw an opportunity to unite & encourage fans to champion the match whether watching the match from home or at the sports bar with their friends.’’

 He further stated, ‘‘UEFA Champions league is watched by more than a billion people worldwide, whether Real Madrid is playing Barcelona or Juventus is playing against Monaco, every final match brings along its own surprises and excitement. Heineken has been successfully partnering with the UEFA Champions League since 2005’’ The Dutch brewer is a keen sponsor of global sports tournaments and unlike other industry players steers clear from sponsoring specific teams.

DKT NCHIMBI ATOA RAI KWA VYUO KUTOA WASOMI WENYE TIJA NA SIO KUTENGENEZA MIGOMO.

$
0
0


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akipiga ngoma kwa furaha kama ishara ya kuzindua kikundi cha Bright Focus kilichopo chuo cha Uhasibu Singida, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo.
1
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia wanakikundi cha Bright Focus (hawapo pichani) kikundi hicho kipo chuo cha Uhasibu Singida.
2
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akipiga ngoma kama ishara ya kuzindua kikundi cha Bright Focus kilichopo chuo cha Uhasibu Singida, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo.
3
Wanachuo ambao ni wanakikundi cha Bright Focus kilichopo Chuo cha Uhasibu Singida wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida wakati wa uzinduzi wa kikundi hicho.
4
Makamu wa rais wa Bright Focus John Gama akiwasilisha malengo ya kikundi hicho kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida wakati wa uzinduzi katika chuo cha Uhasibu Singida.
………………………….
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ametoa rai kwa vyuo vikuu na vyuo vinavyotoa elimu ya juu kuwa sehemu ya kuwafundisha na kuwatengeneza wasomi wenye kutambua fursa na tija za maisha na sio sehemu ya kuendekeza migomo isiyo na faida katika maisha ya wanachuo hao.

Dkt. Nchimbi ametoa rai hiyo jana wakati akizindua kikundi cha Bright Focus kilichopo chuo cha Uhasibu tawi la Singida chenye wana kikundi 89 ambao ni wanachuo, walimu na walezi wenye malengo ya kutambua fursa za kuboresha maisha.

Amesema wakati akizindua kikundi hicho anatambua kuwa kikundi hicho kitasaidia kubuni mawazo yenye tija, fursa, na mwelekeo wa kuboresha uchumi huku akiwasisitiza kuelekezana namna bora ya matumizi ya rasilimali walizonazo hususani rasilimali fedha.

Dkt Nchimbi amekitaka kikundi hicho kuwa chachu ya mabadiliko ya tabia na mienendo yote mibaya iwe mizuri kutokana na baadhi ya wanachuo katika vyuo mbalimbali kuhusishwa na tabia zisizo njema.

Amesema kila mwanakikundi anapaswa anatakiwa mawazo yake yaendane na malengo ya kikundi cha Bright Focus kuanzia mwenendo wa maisha yake, ufaulu wake na hata matumizi ya rasilimali yawe yenye muono wa kutengeneza faida na hasa kujifunza namna ya kuhifadhi akiba.

Aidha Dkt Nchimbi amekubali ombi ya wana kikundi hao la kuwa mlezi wao huku akiwaasa kutoegemea kwenye changamoto bali wazitazame fursa zilizopo huku akiwapongeza kwa kuanzisha kikundi hicho.

Akiwasilisha malengo ya kikundi hicho Makamu wa rais wa Bright Focus John Gama amesema kikundi kina malengo mengi ikiwemo kutoa udhamini kwa wanachuo ambao watashindwa kulipa ada kutokana na sababu mbalimbali.

Gama ameongeza kuwa kikundi kitaanzisha miradi ya maendeleo kama vile kilimo, biashara ya bajaji na pikipiki, ufugaji wa nyuki na kuanzisha makapuni mbalimbali ziku za baadaye ili wana kikundi waweze kujiongezea kipato.

Amesema kikundi kina lengo la kutatua changamoto ya ukosefu wa uzoefu hasa linapokuja suala la ajira kwa kuwaajiri wana chuo katika makampuni watakayoanzisha ili waweze kupata ujuzi huo pamoja na kuandaa ziara za mafunzo.

Katika uzinduzi wa kikundi cha Bright Focus kulikuwa na mdahalo wa nani ana umuhimu zaidi kati ya mwanamke na mwanaume ambapo wana kikundi walichangia hoja, kila upande wa mwanamke na mwanaume ukijitahidi kuthibitisha yale wanayoamini.

Dkt Nchimbi alihitimisha mdahalo huo kwa kusisitiza kuwa thamani ya mwanamke na mwanaume iko sawa kwakuwa katika jamii hakuna maendeleo yanayoletwa na mwanaume peke yake au mwanamke peke yakena hivyo kuwataka wazitambue thamani walizonazo na kuzienzi.

KATIBU MKUU MAENDELEO YA JAMII ATEMBELEA NA KUKAGUA MAKAZI YA WAZEE NJIRO YALIYOPO MOSHI MKOANI KILIMANJARO.

$
0
0
 Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Makazi ya kulea wazee ya Njiro Bibi Ndeta Tenga (kushoto) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto(Maendeleo yaJamii) Bi. Sihaba Nkinga(kulia) wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea katika makazi hayo hivi karibuni.
Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Makazi ya kulea wazee ya Njiro Bibi Ndeta Tenga (katikati) akimuonesha mazingira ya kituo hicho Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto(Maendeleo yaJamii) Bi. Sihaba Nkinga(kushoto) wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea katika makazi hayo hivi karibuni.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto(Maendeleo yaJamii) Bi. Sihaba Nkinga akisalimiana na wazee mbalimbali waishio katika Kituo cha Makazi ya kulea wazee ya Njiro wakati alipotembelea katika makazi hayo hivi karibuni.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto (Maendeleo yaJamii) Bi. Sihaba Nkinga(kushoto) akisalimiana na na Mwenyekiti wa wazee waishio katika Makazi ya kulea wazee ya Njiro yaliyopo Moshi Mkoani kilimanjaro Bw.Nyasi Athanas wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea katika makazi hayo hivi karibuni.
Baadhi ya maeneo ya kituo cha Makazi ya kulea wazee cha Njiro yaliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro.


Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto(Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Makazi ya kulea wazee ya Njiro hivi karibuni.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto(Maendeleo yaJamii) Bi. Sihaba Nkinga (kulia) akizungumza na Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Makazi ya kulea wazee ya Njiro Bibi Ndeta Tenga (kushoto) wakati alipotembelea katika makazi hayo hivi karibuni.
Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO Moshi, Kilimanjaro.

BULEMBO AWASILI WILAYANI BIHARAMULO MKOANI KAGERA JIONI HII

$
0
0
BULEMBO AWASILI WILAYANI BIHARAMULO MKOANI KAGERA JIONI HII
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk Amani Kaborou wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali, maofisa na wote waliomo kwenye msafara, wakati Viongozi wa mkoa wa Kigoma walipokuwa wakiagana na Bulembo na msafara wake, katika eneo la Nyakanazi, kabla ya kuendelea na msafara huo kwenda wilayani Biharamulo mkoani Kagera leo jioni. Bulembo ameingia mkoani Kagera baada ya kumaliza ziara yake katika mkoa wa Kigoma.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj Abdallah Bulembo akiagana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kaborou
 Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akiagana na Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma Naomi Kapambala 
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo akiagana na Mwenyekiti wa Jumuia hiyo mkoa wa Kigoma.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akiwa na Nkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala kabla ya kuagana
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala
 KUWASILI BIHARAMILO🔽
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akisalimia badhi ya wana CCM walimpokea katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera leo jioni
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimsalimia Mbunge wa Viti maalum
 Mbunge na shoga yake wakafurahi
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM na Jumuia zake waliompokea kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Boharamulo mkoani Kagera leo jioni
Baadhi ya madereva na Maofisa wa Jumuia ya Wazazi Tanzania wakipumzika kivulini baada ya Mkuu wa Msafara, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdalla Bulembo kuwasili hotelini kwa ajili ya mapumziko baa ya kuwasili Wilayani Biharamulo mkoani Kagera

KAULI YA MAKAMU WA RAIS MHE SAMIA SULUHU HASSAN KTK KILELE CHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI BUTIAMA

Taasisi kumi zaungana kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wenzao nchini Tanzania

$
0
0


Wanachama wa Taasisi za YAM – UMATI Johnbest Mwahaja (kushoto) na ZAFAYCO Amnah Ibuni (kulia) wakisaini makubaliano ya kuwa taasisi moja ya Tanzania Youth and Adolescent Reproductive Health Coalition (TAYAHR) ambao itakuwa na jukumu kutoa elimu ya uzazi wa mpango na afya ya uzazi kwa vijana wa Tanzania.

Wanachama wa Taasisi za AFRIYAN Fatma Said Ahmed (kushoto) na Hope Centre for Children, Girls and Women in Tanzania Penina Mgonela (kulia) wakisaini makubaliano ya kuwa taasisi moja ya Tanzania Youth and Adolescent Reproductive Health Coalition (TAYAHR) ambao itakuwa na jukumu kutoa elimu ya uzazi wa mpango na afya ya uzazi kwa vijana wa Tanzania.

Mwanachama wa Taasisi za AFRIYAN Fatma Said Ahmed (kushoto) akibadilishana mkataba na Mwenyikiti wa Taasisi ya Tanzania Youth and Adolescent Reproductive Health Coalition (TAYAHR) chairperson William Otuck baada ya kutia saini ya makubaliano ya kufanya kazi chini ya taasisi hiyo yenye lengo ya kutoa elimu ya uzazi wa mpango na afya ya uzazi kwa vijana wa Tanzania.

Jumla ya taasisi kumi za vijana zimeungana ili kuzidisha nguvu ya kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wenzao nchini Tanzania na zaidi ikilenga matumizi ya mpango wa uzazi. Vijana hao wamejizatiti kuhahakisha kuwa kuna uwekezaji wa kutosha kwenye elimu juu ya uzazi wa mpango na pia vijana kuhusisha kwenye maamuzi yanayohusu vijana na afya ya uzazi.

Taasisi hizo zimetiliana saini makubaliano na kuwa taasisi moja ikayoitwa Tanzania Adolescent and Youth Reproductive Health (TAYAHR) jana jijini Dar es Salaam ambapo taasisi hiyo itajikita zaidi kwenye kutoa elimu, kuhusisha vijana na kuhakikisha huduma inafika kwenye maeneo sahihi kwa muda sahihi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutia saini makubaliano hayo, Mwenyekiti wa TAYAHR William Otuck alisema Tanzania ina changamoto kuona ya kwamba asilimia 27 ya vijana wenye miaka 15-19 wana mtoto au ni wajawazito huku utumiaji wa uzazi wa mpango na hasa vidonge vya uzazi kati yao ikiwa ni chini sana – yaani asilimia 13 peke yake huku pia wakiwa hawana elimu yeyote kuhusu afya ya uzazi na hivyo kukosa uamuzi sahihi kwenye masuala ya kujamiiana.

‘Robo ya wasichana wenye umri kati ya 15 na 19 Tanzania wana watoto au ni wajawazito na hali ni mbaya kwenye mkoa wa Katavi yenye asilimia 45 na Tabora asilimia 42 kwa wasichana wenye umri huo. Hii inamaanisha kuna idadi kubwa ya wasichana ambao wanakatisha masomo na kuingia kwenye hali ya kuwa mzazi wangali wana umri mdogo na hii kwa kiasi kikubwa uchangia kuongeza hali ya umasiki kwenye jamii’, alisema Otuck huku akiongeza kuwa idadi kubwa ya wasichana wadogo wakipata mimba pia kunachangia kuongezeka vifo vitokanavyo na uzazi.

Akizungumzia kuhusu elimu na hali ya kupata mimba za utotoni, Otuck alisema tafiti zinaonyesha kuwa ni asilimia 10 wa wasichana ambao wana elimu mpaka ya sekondari ambao hupata mimba wakiwa na umri mdogo kulinganisha na wale wana elimu ya msingi ambao ni asilimia 34 na wale ambao hawana elimu kabisa ni asilimia 52.

Taasisi hiyo chini ya uongozi wa vijana pia imelenga kuhamasisha wenye kutoa maamuzi (policy makers) kuwekeza kwenye kupanua wingo la matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango ili kufikia walengwa ambao bado hawajafikia, ambapo kwa sasa inaonyesha asilimia 23 ya wanawake vijana wanatamani kutumia uzazi wa mpango lakini bado huduma hiyo
haiwajafikia na pia kuongeza matumizi ya uzazi wa mpango kwa vijana angalau kufikia asilimia 80 ifikapo 2010 na pia kuendeleza elimu ya afya ya uzazi kwa vijana.

Taasisi hizi kabla ya kufikia makubaliano yao zilianza mazungumzo mwezi Oktoba na Novemba mwaka jana chini ya FP2020 Secretariat, mradi wa Advance Family Planning (AFP) Tanzania pamoja na taasisi ya Torchlight Collectives. TAYAHR inaundwa na taasisi za Hope Centre for Children, Girls and Women in Tanzania, YAM-UMATI, AfriYAN, TYVA, SAYI, Restless Development, Zanzibar Youth Forum (ZAFAYCO), IYAFP/Young and Alive Initiative (YAAI), SHDEPHA+ na YUNA.

KAMPUNI YA ACACIA YACHANGIA KATIKA HARAKATI ZA GGM KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA MAPAMBANO YA VITA DHIDI YA UKIMWI.

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Tulia Ackson akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika lango la kupandia mlima Kilimanjaro,lango la Machame kwa ajili ya kutoa Baraka kwa washiriki wa changamoto ya kupanda mlima kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi zoezi linaloratibiwa na Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM).
Mgeni rasmi katika shughuli ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano Vita ya Ukiwmwi ,Dkt Tulia Ackson akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mshikizi ,Mrisho Gambo (kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ukimwi na Dawa za kulevya ,Dkt Faustine Ndugulile wakiimba wakipiga makofi.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Tulia Ackson kizungumza wakati wa kutoa baraka kwa wanaharakati 89 wakiwemo wafanyakazi wa Kampuni ya Acacia wanaoshiriki zoezi panda mlima kwa lengo lakuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano ,vita dhidi ya Ukimwi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM) Terry Melpeter akizungumza katika shughuli hiyo iliyofanyika katika lango la Machame.
Baadhi ya viongozi wa wilaya za Hai na Moshi mjini wakifuatalia  shughuli hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mshikizi Mrisho Gambo akizungumza wakati wa shuguli hiyo ambayo hufanyika kila mwaka.
Msanii Mrisho Mpoto ambaye ni Balozi wa TACAIDS akitoa burudani kwa washiriki wa changamoto hiyo.
Kampuni ya Acacia ,wamiliki wa Migodi ya Buzwagi,Bulyanhulu na North Mara ni miongoni mwa kampuni ambazo zimekua zikitoa michango yao kusaidia kampunu ya GGM katika mapambano ya vita dhidi ya Ukimwi ambapo wafanyakazi wake pia ni miongoni mwa wanaharakati waliopanda Mlima Kilimanjaro.
Naibu Spika Dkt Ackson akisalimana na Meneja wa Benki ya NMB,tawi la Moshi ,Emanuel Kishosha kabla ya kuanza kwa zoezi la kupanda mlima Kilimanjaro.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Acacia wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Spika ,Dkt Ackson kabla ya kuanza kwa zoezi la kupanda mlima.
Zoezi la kuapnda Mlima likianza rasi huku likiongozwa na Naibu Spika ,Dkt Tulia Ackson ,Mrisho Mpoto akiongoza kwa nyimbo za kuhamasisha.
Zoezi la kupanda lilianza huku mvua ikinyesha,

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

SHINDANO LA SPRITE BBALL KINGS LAINGIA HATUA YA 16 BORA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Shindano la Sprite Bball Kings 2017  limeingia katika hatua ya 16 baada ya timu 52 kukipiga wikiendi hii ikiwa ni ufunguzi wa michuano hiyo

Michezo hiyo 26 iliyochezwa katika viunga vya viwanja vya Jakaya M Kikwete Park (JKM Park) na kuzikutanisha timu hizo 52 katika mechi 26 za mtoano na 16 kufanikiwa kuingia hatua inayofuata.

Akitoa tathmini ya michuano hiyo Mratibu wa Sprite Bball Kings Basilisa Biseko amesema kuwa hatua ya mtoano imefanyika wikiendi hii na timu 16 kufanikiwa kuingua hatua inayofuata ila katika mechi hizo kuna baadhi walipewa ushindi wa mezani.

Basilisa amesema kuwa kuna baadhi ya timu hazikufanikiwa kufika siku hiyo na  ratiba ilikuwa tayari imeshapangwa katika droo iliyokuwa imepangwa na kupelekea timu iliyokuwa imefika uwanjani kupatiwa ushindi wa mezani.

"Katika michezo 26 iliyochezwa siku ya Jumamosi katika viwanja vya JMK Park timu 16 zimefanikiwa kuingia hatua ya 16 bora, ila kuna timu zingine zimeingia kwenye hatua hiyo bila kucheza na timu pinzani kutokana na mpinzani wake kutokufika na kupelekea kupewa alama zitakazomruhusu kuingia hatua inayofuata,"amesema Basilisa.

Amesema kuwa, kwa timu zilizopata alama nyingi ndizo zilizofanikiwa kuingia katika hatua ya 16 bora na mashindano hayo yataendelea tena ili kumpata mshindi wa Sprite Bball Kitaa kwa mwaka 2017.
 Timu zilizofuzu kuingia hatua ya 16 bora katika shindano la Sprite Baball Kings 2017 ni DMI, Dream Chaser, UDSM, Oysterbay, Ukonga Warriors, The Fighter, Ardhi na Bongo Hits.

Timu zingine ni Chanika Legends, Montfort, Heroes S/B, Kigamboni Heroes, TMT, Mchenga, Kurasini na Landforce.

Mashindano ya Bball Kings mwaka huu yanadhaminiwa na Sprite wakishirikiana na kituo cha East Africa Redio na TV  na yalizinduliwa mapema mwezi wa tano na kuanza usaili kwa wilaya za Teemek, Kindondoni na Ilala na kupata timu 4.52 zilizojitokeza kushiriki shindano hilo.
Timu ya mpira wa kikapu ya UDSM wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mtanange wao.
 Timu ya mpira wa kikapu ya UDSM (jezi ya njano) wakipambana katika hatua ya mtoano ya shindano la Sprite Bball Kings iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii katika viwanja vya  Jakaya M Kikwete Park (JKM Park).
 Mashabiki na timu zingine zilizoshiriki katika  hatua ya mtoano ya shindano la Sprite Bball Kings iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii katika viwanja vya  Jakaya M Kikwete Park (JKM Park) wakiwa jukwaani wakifuatilia baadhi ya michezo mingine.
Timu za mpira wa kikapu wakiwa wanachuana katika shindano la Sprite Bball Kings iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii katika viwanja vya  Jakaya M Kikwete Park (JKM Park).
Kamishna wa Ufundi na Uendeshaji Mashindano wa chama Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF) na Mratibu  wa Sprite BBall Kings Manase Zablon  (kushoto) akiwa pamoja na mtangazaji wa East African Drive David Rweganyira wakichambua baadhi mechi zilizokuwa zikiendelea.

SHIRIKA LA ANGA LA ETIHAD KUTOA OFA ZA BURE KWA ABIRIA WAKE WA DARAJA LA UCHUMI WA MASHARIKI YA KATI, AFRIKA NA PAKISTAN AbuDhabi.

$
0
0
Shirika kuu la anga la Umoja wa nchi ya falme za kiarabu litatoa nafasi kwa abiria wake kutoka mashariki ya kati, Afrika na Pakistan kupumzika katika hoteli ya Raddison Blu jijini Abu Dhabi kisiwani Yas. Fursa hii imeanza rasmi hivi karibuni na kumalizika tarehe 15, Novemba 2017.

Mohammad Al Bulooki, Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa shirika la anga la Etihad alisema “Shirika la Etihad lina furaha kuwaalika wageni wote kuja kuliona na kulifahamu katika mji wa Abu Dhabi kwa macho yao wenyewe. Jiji hilo kuu la Umoja wa falme za Kiarabu lina mengi ya kuwaonesha abiria wote wanaosafiri endapo wanavutiwa na utamaduni, kupumzika sehemu mbali mbali kama visiwa vya bahari, michezo nk.

Kama shirika la ndege la kitaifa la Etihad ni sehemu muhimu ya jiji hili zuri na wote wanaosafiri kupitia Abu Dhabi wanatakiwa kuhamasishwa kuja kujionea uzuri wa jiji hili. Ofa hii ni kwa wateja ili waweze kutenga muda wao na kuja kutembelea vivutio mbalimbali vya Abu Dhabi wakiwa katika safari zao. Kutembelea jangwa hilo zuri pamoja na msikiti mkubwa wa sheikh Zayed, moja kati ya misikiti mikubwa sana duniani, kuembelea vivutio mbalimbali vya kisiwa cha Yas, na kupata nafasi ya kufurahia kwa mara ya kwanza katika hoteli kubwa za kitalii duniani.

Zaidi ya wageni milioni 4.4 walirekodiwa kutembelea jiji la Abu Dhabi mwaka 2016 na kuthibitisha kuwa Umoja wa falme hizo za kiarabu ni moja kati ya vivutio vingi vya wasafiri wanaopitia hapo wakati wanaposafiri. Wageni wanaweza kujipatia fursa hii kuzifahamu vivutio vya burudani mbalimbali maarufu kibiashara ikiwemo pwani za bahari zenye mchanga mweupe, hifadhi zenye mandhari tofauti kama Yas Waterworld na Ferrari World, jangwa la misafara ya safari   Sanaa, taasisi za kitamaduni kama Manarat Al Saadiyat na makumbusho ya Louvre yanayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni, sehemu nzuri za kitaifa na kimataifa za kupata chakula, sehemu za kucheza mchezo wa golf kimataifa, na kanuni ya 1 ya shirika la Etihad ya kufuatilia mbio kubwa Zaidi jijini Abu Dhabi.

Jiji la Abu Dhbi pia linatoa nafasi kupata sehemu mbalimbali za kununua mahitaji ya kila aina kuweza kukidhi mahitaji yao. Jiji hilo linajivunia maduka makubwa kama Yas, Abu Dhabi, Marina na Galleria- moja kati ya sehemu kubwa za kifhari za kununa mahitaji.

Shirika la ndege la Etihad limekua na programu ya kupitisha wasafiri wake sehemu mbali mbali wakiwa safarini kuanzia mwaka 2011, na kutoa huduma mbali mbali ikiwa nia pamoja na kukutana viwanja vya ndege, na kusaidia usafiri, mahala pa kupumzikia, ziara mbali mbali na huduma za upatikanaji wa hati za kusafiria

MAKAMU WA RAIS AFUNGA KONGAMANO LA KITAIFA LA MAZINGIRA MKOANI MARA

$
0
0
unnamed
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kufunga Kongamano la Kitaifa la Mazingira lililofanyika kwenye ukumbi wa kanisa Katoliki, Mwitongo Butiama. 
1
Mama Maria Nyerere akichangia maoni yake wakati wa kufunga Kongamano la Taifa la Mazingira lililofanyika Mwitongo Butiama kwenye kilele cha Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa imeadhimishwa Butiama mkoani Mara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Waziri Lukuvi Kupewa Tuzo ya Uwajibikaji na Utendaji Bora

$
0
0
Na Jonas Kamaleki- MAELEZO.

Viongozi wa Dini wanajiandaa kumpa tuzo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi kwa utendaji mzuri uliojaa ubunifu na uwajibikaji.

Hayo yameelezwa katika mahojiano maalum jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Dini zote Tanzania, Askofu William Mwamalanga.

Askofu Mwamalanga amesema kuwa Waziri Lukuvi amekuwa kiongozi imara katika kufuatilia masuala yanayohusu ardhi ikiwemo utatuzi wa migogoro ambayo imedumu kwa muda mrefu.

“Lukuvi ameing’arisha Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuendana na kasi ya Rais John Pombe Magufuli, hakika amevaa viatu vya Magufuli, hivyo tumeamua kumpa tuzo maalum kwa ajili utendaji wake”, alisema Askofu Mwamalanga.

Ameeleza kuwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imefanya jambo zuri kwa kutoa elimu ya ardhi kiasi kwamba karibu kila mtu amefahamu matumizi ya ardhi na umuhimu wake.

Askofu Mwamalanga amesema kuwa ardhi imefanywa kuwa lulu na kufanya sura mpya ya ardhi kuonekana ambapo takriban asilimia 85 ya Watanzania wameiona kuwa ni mali.

Mhe. Lukuvi amewapa nafasi ya kwanza wananchi kuliko Sheria jambo ambalo limewafanya Watanzania kujisikia kuwa wanathaminiwa na Serikali yao, aliongeza Askofu Mwamalanga.

Kiongozi huyo wa Dini amesema kuwa Mhe. Lukuvi ni mfano wa kuigwa na mawaziri na viongozi wenzake kwa uchapakazi wake. Amesema kuwa ni Waziri ambaye anawashirikisha watendaji waliochini yake katika maamuzi mbali mbali, hivyo anastahili kupewa tuzo.

“Tumepanga kumpa tuzo Waziri Lukuvi kwa kuzingatia yafuatayo: Kuiweka ardhi mikononi mwa watanzania, kuonyesha kuwa ardhi ni chanzo kikuu cha uchumi wa watu na utatuzi wa migogoro ya ardhi hasa iliyodumu kwa muda mrefu”, alisema Askofu Mwamalanga. 

Migogoro hiyo ni kama vile mgogoro wa kijiji cha Mabwegere, Mkoani Morogoro, mgogoro wa Chasimba, jijini Dar es Salaam na migogoro mingine mingi katika mikoa ya Arusha, Mbeya, Kigoma, Tanga na Mwanza.

Askofu Mwamalanga amesema Kamati yake imewasiliana na Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi ili watoe mapendekezo ya tuzo ambayo anastahili kupewa Mhe. Lukuvi kwa utendaji kazi wake mzuri. 

Amezitaja baadhi ya Taasisi hizo kuwa ni Vyuo Vikuu vya Umma na Binafsi, Marais wastaafu na mawaziri wakuu wastaafu, Vyama vyote vya siasa ambavyo kwa ujumla wake vimeonyesha kutambua mchango wa waziri Lukuvi.

Baada ya kupokea mapendekezo na kuyafanyia kazi ndipo itatangazwa siku ya kutoa tuzo hiyo kwa Mhe. Lukuvi, alisema Askofu Mwamalanga.

Tangu Waziri Lukuvi aiongoze Wizara ya ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mwisho mwa uongozi wa awamu ya Nne hadi sasa, 

mabadiliko yenye tija katika wizara hiyo yameonekana. Migogoro mingi ya ardhi imetatuliwa, utoaji wa hati za viwanja umerahisishwa na huduma kwa wateja imeboreshwa.

MWENGE WA UHURU WAKABIDHIWA RASMI WILAYA YA MKURANGA UKITOKEA WILAYA YA RUFIJI.

$
0
0
Mwenge wa Uhuru umekabidhiwa rasmi wilaya ya Mkuranga ukitokea wilaya ya Rufiji huko mkoani Pwani na umetembelea miradi 11 ya Maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi billion 24.7.

Akizungumza wakati wa kubadhiwa mwenge wa Uhuru mkuu wa wilaya ya Mkuranga, Filibeto Sanga amesema miradi hiyo 11 iliyotembelewa ni pamoja na afya, elimu, kilimo na mradi wa ujasilia Mali kwa vijana.

Aidha katika miradi hiyo kumi na moja mwenge wa Uhuru umezindua miradi mitatu ambayo ni huduma ya upasuaji katika kituo cha afya Kilimahewa, kufungua nyumba za walimu katika shule ya sekondari Mkugilo pamoja na kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Mwanambaya wilayani humo.

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2017 Amour Hamadi Amour ametoa wito kwa watanzania kuwa na uzalendo wa kuthamini vya kwao ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi na kuifanya Tanzania ya viwanda.

Kiongozi huyo ameongeza kuwa katika kuelekea nchi ya viwanda ni vyema Watanzania wakawa na utamaduni wa kutumia bidhaa za ndani ili kukuza uchumi wa nchi na taifa kwa ujimla.

Hata hivyo mbio hizo za mwenge wa Uhuru wilayani mkuranga mkoani Pwani zimeudhuriwa na watendaji mbalimbali wa Halmashauri hiyo akiwemo Mkurugenzi injinia Mshamu Munde na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Abeid.

 Mkuu wa Wilaya ya mkuranga, Filibeto Sanga (kulia) akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Rufiji Juma Abdalah tayari kwaajili ya kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya hiyo.mkoani Pwani.
 Mganga mkuu Wilaya ya Mkuranga Dkt.Steven Mwandambo wa (kwanza kulia) akitoa maelekezo mbele  ya viongozi wengine ya namna chumba upasuaji kitakavyo saidia kinamama wajawazito kijiji cha kilomahewa.mkoani Pwani. 
 Kiongozi Mkuu wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,Amour Hamad Amour akizindua nyumba za walimu katika shule ya Sekondari Mkugilo mkoani Pwani.
 Kiongozi Mkuu wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,Amour Hamad Amour akipanda mti katika shule ya Sekondari Mkugilo mkoani Pwani ikiwa  ni ishara ya kuhimiza wananchi kutunza na kuhifadhi mazingira,
 Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Abeid wa (kwanza kulia akiwa katika picha ya pamoja na Madiwani wa Wilaya ya Mkuranga. 
 Mkuu wa Wilaya ya mkuranga, Filibeto Sanga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Njopeka waliojitokeza kuupokea mwenge wa uhuru,mwenge huo unatarajia kupitia miradi 11 ya maendeleo yenye thamani ya bilion 24.7 mkoani Pwani.

WAZIRI MBARAWA APOKEA KIVUKO CHA MV KAZI

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd. Bw. Major Songoro (kulia)  wakati wa makabidhiano ya Kivuko cha MV. KAZI mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mtendaji Mkuu toka Wakala wa Ufundi na Umeme  (TEMESA) Dkt. Mussa  Mgwatu.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kulia) akizungumza na baadhi ya wananchi waliopanda Kivuko cha MV. KAZI mara baada ya kukabidhiwa kwa Serikali toka kwa  Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd. Iliyokuwa ikikijenga Kivuko hicho.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliana Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akizungumza na mmoja  ya mkazi wa Kigamboni wakati wa kukabidhiwa kivuko cha MV. KAZI kwa Serikali toka kwa Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd. Iliyokuwa ikikijenga Kivuko hicho.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliana Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akizungumza na mmoja  ya mkazi wa Kigamboni wakati wa kukabidhiwa kivuko cha MV. KAZI kwa Serikali toka kwa Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd. Iliyokuwa ikikijenga Kivuko hicho.
Baadhi ya wananchi wakiteremka katika Kivuko cha MV. KAZI mara baada ya kukabidhiwa rasmi kwa Serikali mapema hii leo Magogoni jijini Dar es Salaam toka Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd. Iliyokuwa ikikijenga Kivuko hicho.
Picha na MAELEZO
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live


Latest Images