Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1257 | 1258 | (Page 1259) | 1260 | 1261 | .... | 1896 | newer

  0 0


  0 0


  Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti na Mahusiano na Serikali wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Sylvia Balwire akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh 110 milioni kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT Erwin Telemans, fedha hizo zimetolewa ili kusaidia matibabu kwa watoto wenye ugonjwa wa miguu pinde, hafla hiyo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT Erwin Telemans akifafanua jambo kwa wageni waalikwa wakati wa makabidhiano ya hundi yenye thamani ya Sh 110 milioni kwa hospitali ya CCBRT, fedha hizo zimetolewa ili kusaidia matibabu kwa watoto wenye ugonjwa wa miguu pinde, hafla hiyo ilifanyika mapema leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti na Mahusiano na Serikali wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Sylvia Balwire akihutubia wageni waalikwa wakati wa makabidhiano ya hundi yenye thamani ya Sh 110 milioni kwa hospitali ya CCBRT, fedha hizo zimetolewa ili kusaidia matibabu kwa watoto wenye ugonjwa wa miguu pinde, hafla hiyo ilifanyika mapema leo jijini Dar es Salaam.
  Mama mwenye mtoto mwenye ugonjwa wa miguu pinde akizungumza na vyoombo vya habari mara baada ya makabidhiano ya hundi yenye thamani ya Sh 110 milioni kwa hospitali ya CCBRT, fedha hizo zimetolewa ili kusaidia matibabu kwa watoto wenye ugonjwa wa miguu pinde, hafla hiyo ilifanyika mapema leo jijini Dar es Salaam.


  2 Juni 2017, Dar es Salaam: CCBRT imejikita kutoa huduma za tiba zinazofikiwa na wagonjwa wanazimudu, tiba vora na hali kadhalika kuzia ulemavu na kukuza kujumuishwa kwake nchini Tanzania. Moja ya tukio kubwa katika mkutano huo ilikuwa ni kukuza uelewa kuhusu umuhimu wa kutambua mapema, kutafuta tiba na na kufuatilia tiba yote ya miguu iliyopinda.


  Mguu uliopinda ni ulemavu unaosababisha ama mguu mmoja ay miguu yote kupinda. Mguu unaoathirika unasababisha sehemu ya unyayo kubinuka kuelekea ndani kuanzia katika kifundo au kutembelea pande za miguu badala ya unyayo. Hata hivyo utambuzi wa mapema pamoja na tiba katika umri mdogo, huwafanya watoto waliozaliwa na na mguu uliopinda kuweza kutembea na kushiriki ipasavyo katika shughuli za kijamii na kiuchumi ndani ya jamii zao.

  Kwa upande wake Mkuu wa Usimamizi wa masuala ya Kiserikali wa Tigo, Sylvia Balwire alisema kuwa Tigo imejikita kurudisha kwa jamii ambamo inaendesha shughuli zake kupitia mikakati wake wa kuwajibika kwa jamii. “Tuliona kuna haja ya kusaidia katika hili kwa sababu CCBRT inahudumia maskini walioko pembezoni ndani ya jamii na inajaribu kuondoa vikwazo vingi kadiri iwezekanavyo ili kuwawezesha watu kutafuta tiba. Jamii itaikumbuka CCBRT daima kutokanana mkakati wake huu wa kuwasaidia watu walio na ulemavu na kuwapatia fursa ya kutibiwa kwa gharama nafuu. Inatakiwa mtu kuwa na moyo wa ziada kutoa huduma ambayo CCBRT inatoa kwa jamii.

  Zaidi ya watoto 1,509 walishanufaika na upasuaji huu unaobadili maisha kutoka CCBRT katika kipindi cha zaidi ya miaka sita iliyopita. Haya ni mafanikio ambayo yanatufanya sisi sote tuliopo Tigo tunajivuania sana. Kupitia matibabu ya watu wanaoishi na ulemavu, Tigo na CCBRT wanaweka chapa ya kudumu katika ustawi wa watu binafsi, familia na jamii nchini Tanzania.

  “Katika kuadhimisha Siku wa Miguu Iliyopinda duniani kwa mwaka huu na kama sehemu ya kujitoa kwetu kukuza ustawi wa jamii tunatoa msaada wa shilingi milioni 110 kwa CCBRT kwa ajili ya kusaidia matibabu ya miguu iliyopinda katika hospitali yake. Msaada huu kwa matibabu ya miguu iliyopinda ni kielelezo kwamba Tigo inaendelea kujikita katika kusaidia utoaji wa huduma za afya katika CCBRT na nchini kwa ujumla.

  0 0


  MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akifungua semina ya siku mbili ya fursa mpya ya kuongeza mapato ya halmashauri nchini kwa wakurugenzi wa majiji na manispaa iliyoandaliwa na shirika la maendeleo la UNCDF iliyofanyika jijini Arusha jana.
   Mratibu wa mfuko wa mitaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) Peter Malika akizungumza

   Mratibu wa mfuko wa mitaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) Peter Malika akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo na kusema,mpango huo wa kuwezesha halmashauri za majiji na manispaa, umeanza kwa majiji matato na manispaa tatu.
   Baadhi ya wakuregenzi wa majiji na Manispaa waliohudhuria
  SHIRIIKA la maendeleo  ya mitaji la umoja wa Mataifa(UNCDF), jana limezindua  mpango wa kuziwezesha halmashauri za majiji na Manispaa kuweza kunufaika na masoko ya mitaji kwa kuwekeza katika soko la  la hisa kuuza vipande na kutoa hati za dhamana.

  Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, alizindua mpango huo jijini hapa kwa niaba ya Waziri wa nchi ofisi za Rais(TAMISEMI) George Simbachawene  na kuwataka watendaji na halmashauri za majiji na manispaa ,wanaohudhuria mafunzo hayo kujiandaa kutumia fursa hiyo.

  Gambo alisema katika mpango huo, ambao unatarajiwa kuongeza mapato kwa halmashauri za majiji na manispaa nchini, kutokana na kuelimisha ni jinsi gani wataweza kuwekeza katika soko la hisa na kupata fedha za miradi ya maendeleo.

  Alisema mpango huo, ambao unataribiwa na UNCDF unaziezesha halmashauri kupata fedha nyingi ambazo zitawezesha kuendesha miradi mikubwa ya miundombinu na hivyo kuchochea wanannchi.

  Awali, Mratibu wa mfuko wa mitaji wa umoja wa mataifa(UNCDF) Peter Malika alisema,mpango huo wa kuwezesha halmashauri za majiji na manispaa, umeanza kwa majiji matato na manispaa tatu.

  Malika alisema Majiji ambayo yatakuwa katika mpango huo ni Dar es Salaam,Mwanza, Arusha, Mbeya na Tanga na Manispaa ambazo zitahusika ni Kinondoni,Temeke,Ilemela na Dodoma.

  "Majiji haya na manispaa wanauwezo wa kuanza kuwekeza katika masoko ya hisa kwa kuuza hati za dhamana na wataweza kupata fedha kwa miradi mikubwa ya maendeleo"alisema.

  Mkurugenzi wa jiji la Arusha, Athuman Kihamia, alisema mpango huo tayari umeonesha mafanikio katika majiji kadhaa, ikiwepo Afrika Kusini,  Marekani na Asia na wanatarajiwa utaboresha mapato ya halmashauri.

  Kihamia alisema jiji la Arusha tayari limejiandaa kunufaika na mpango huo na tayari lina kampuni ya Arusha Investment ambayo inaweza kushiriki katika masoko ya hisa.

  0 0

   Muonekano wa Kiwanja. Ni Kuanzia mwanzo wa Picha mpaka mwisho wa Ukuta upande wa kushoto
  Mwanzo wa Picha Mpaka kwenye ukuta wa Ghorofa kule 

  Kiwanja Kipo KIGAMBONI KIBADA

  Ukubwa wa Kiwanja ni Mita za Mraba (Sqmeter) 1088

  Kiwanja kina hati safi na hakina mgogoro

  Bei ni Milioni 65 Maongezi kidogo yapo na Kiwanja hiki kinauzwa Na Mwenye Nacho 

  Kwa Mawasiliano 0786 821 613

  Karibu mwenye Uhitaji. Biashara Maelewano Hata

  0 0

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Sheikh Nurdin Kishik ambaye ni Mhadhiri wa Kimataifa wa Dini ya Kiislaam, (kulia) na ujumbe wake, ofisini kwake bungeni mjini Dodoma  Juni  2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kushiriki katika sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa  Al- Gadaf mjini Dodoma Juni 2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kuliombea Taifa ili liendelee kudumu katika hali ya amani na utulivu.

  Amesema suala la kudumisha amani na utulivu ni jukumu la kila mmoja, hivyo kila mwananchi kwa imani yake ahakikishe anashiriki kutunza hali hiyo.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Juni 2, 2017) baada ya kumaliza kuswali sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al-Gadaf, mjini Dodoma.

  Amesema ni vema kila mwananchi akajivunia hali ya amani na utulivu iliyoko nchini kwa kuwa ndiyo inayowezesha kufanyika kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo. “Tuendelee kudumisha amani, tufanye ibada kila mtu kwa imani yake. Serikali inaheshimu dini zote kwa sababu ndizo zinazojenga amani na mshikamano,” amesema.

  Pia amewataka wazazi wahakikishe wanawalea watoto wao katika mazingira ya kidini ili wanapokuwa watu wazima waje kuwa raia wema. “Tuendelee kuhamasisha watoto wetu wasikilize mahubiri ya dini; ni jukumu letu sisi kama wazazi kuwahimiza wahudhurie mahubiri ya viongozi wa dini ili waweze kujijenga vyema kimaadili na kiimani pia.”

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewakumbusha Waislamu wahakikishe wanautumia vizuri mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa kuzidisha ibada na kusaidia watu wenye mahitaji. “Leo ni Ijumaa ya kwanza katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, nawaomba tutumie vizuri mwezi huu ili tupate baraka,” amesema.

  Ibada hiyo ya sala ya Ijumaa iliongozwa na Sheikh Nurdin Kishki ambaye ni Imamu wa Msikiti wa Vetenari, wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam.

  Sheikh Kishki katika hotuba yake, aliwasisitiza Waislamu waendelee kufanya mambo mema yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu ikiwemo kuwatunza wazazi wao, kumswalia Mtume Mohammed (S.A.W) na kufunga katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.

  0 0


  0 0


  Na Ashraf Said, Globu ya Jamii .

  Vijana wazalendo wampongeza Rais, Dk. John Pombe Magufuli juu ya hatua stahiki anazoendelea kuchukua dhidi ya unyonyaji uliokithiri katika sekta ya Nishati na Madini.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa vijana hao, Mwita Nyarukururu amesema jitihada za Rais Dk. John Pombe Magufuli zinawapeleka watanzania katika uchumi wa kati wa nchi kuweza kujitegemea na kuachana na wanyonyaji wa rasilimali katika sekta ya nishati na madini kutokana na misaada wanayoitoa .

  Amesema kuwa Rais Dk. John Pombe Magufuli ameonyesha dhamira ya kweli katika kuhakisha watendaji waliopewa mamlaka wanawajibika na wanaposhindwa kufanya hivyo hatua zinachukuliwa alivyoweza kuiwajibisha Wizara ya Madini pamoja na Bodi ya Ukaguzi wa Madini (TMAA).

  “Unyonyaji na Uhujumu uchumi katika sekta ya madini umekuwa ukipigiwa kelele na wananchi kutokana na Mikataba kuwa ya siri na mibovu isiyonufaisha Taifa,”Amesema.

  Aidha wamemuomba Rais Dk. John Pombe Magufuli na Serikali yake kupeleka upya bungeni mswada wa sheria zote zinazohusu sekta ya Nishati na Madini kwa lengo la kujadiliwa upya kwa maslahi ya taifa na wananchi wote.

  Mwenyekiti wa vijana Vijana Wazalendo, Mwita Nyarukururu katikati akizungumza na waandishi wa habari juu hatua ambazo anazichukua Rais Dk. John Pombe Magufuli katika sekta ya Nishati na Madini leo jijini Dar es Salaam. Kushoto Halima Makoroganya kulia ni Rose Manumba

  0 0


  0 0

   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na waandishi wa habari baada ya Kuzindua Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Kuhudumia Wakimbizi, Harrison Mseke. 
   Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
   Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Kigoma (CCM), Mhandisi  Atashasta Nditiye (kushoto), akifuatiwa na Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Daniel Nsanzugwako pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Kuhudumia Wakimbizi, Harrison Mseke, wakifuatilia Mada inayohusu Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi iliyokuwa inatolewa na Mratibu wa Mpango huo kutoka Idara ya Huduma za Wakimbizi, Dk. John Jingu (hayupo pichani), muda mfupi kabla ya Uzinduzi wa Mpango huo.
   Sehemu ya Wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi zake nchini  pamoja na Wawakilishi wa Taasisi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga, akijibu maswali ya waandishi wa habari  wakati wa uzinduzi wa  Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamadi Masauni (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya Katavi, Tabora, Kagera na Kigoma, watendaji wa serikali na Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa yanayofanya kazi nchini, wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 

  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI –WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0 0

   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Juuia ya WazaziTanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akikabidhiwa chombo cha kiasili cha kuhifadhia chakula 'Hotpot' cha asili ya Kabila la Waha, alipopokewa kwenye Ofisi ya CCM, Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, leo, kuendelea na ziara yake ya Kichama mikoani. Anayemkabidhi ni Dynes Wiston. Watatu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kabourou 
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akifurahia zawadi ya 'Hotpot' baada ya kukabidhiwa na Umoja wa Vijana wa CCM, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Buhigwe, mkoani Kigoma, leo, kuendelea na ziara yake ya Kichama mikoani.
   Kijana wa Umoja wa Vijana wa CCM, Agatha Leon, akimvisha skafu, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya WazaziTanzania, Alhaj Abdallah Bulembo alipowasili Ofisi ya CCM Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, leo
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akienda Ofisini katika Ofisi ya CCM,Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, leo
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akiwasalimia baadhi ya viongozi kabla ya kuingia ofisini, katika Ofisi ya CCM wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma leo
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo (kushoto) akiwaunga mkono kuselebuka, wana CCM waliokuwa wakijimwayamwaya kwa nyimbo za mapokezi, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, leo
   Wana CCM wakihanikiza shamrashamra nje ya Ofisi ya CCM Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Ahaj Abdallah Bulembo alipowasili kwenye Ofisi hiyo,leo.

   Mbunge wa Viti Maalum Josephine Ngezabuke, akishiriki kuselebuka na wana CCM waliokuwa wakijimwayamwaya kwa nyimbo za mapokezi ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa CCM, Alhaj Abdallah Bulembo kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, leo
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, leo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo Elisha Bagwanya
   Katibu wa CCM Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma Agnes Ndoriki akisoma taarifa kwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo.
   Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Elisha Bagwanya akimkaribisha Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk. Aman Kabourou
   Wana CCM wakishangilia wakati Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo alipokuwa akiwasili ukumbini kuendesha kikao cha ndani na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Buhigwe, Mabalozi, Watendaji wa Chama na wa Serikali, leo
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akiwasili ukumbini
   Wazee wa Chama wa Buhigwe, walioalikwa kwenye kikao hicho wakishangilia
   Wana CCM wakitoa burudani ya wimbo kabla ya kikao kuanza
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo akiwatuza wana-CCM hao kwa burudani yao nzuri ya wimbo.
   Wajumbe wakinyoosha mikono kuunga mkono jambo
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akimpongeza mmoja wa wanachama wapya wa CCM, waliojiunga wakati wa kikao hicho
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo akishirikiana na Mwenyekiti wa Wazee wa Kabila la Waha, Eliakim Balunguza, kumtawaza Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Kanali Marco Maguguti, kuwa Muha kwa kumvalisha vazi la Mpuzu la kabila hilo, wakati wa kikao hicho, leo. 
   Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Kanali Marco Gaguti, akikabidhiwa mkuki kulinda mipaka ya wilaya hiyo
   Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma akia ameketishwa kwenye kigoda kukamilisha kutawazwa kwake kuwa Muha, ambapo alipata fursa pia ya kuzungumzana wajumbe wa kikao hicho. 
   Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Kanali Marco Gaguti akizungumza huku ameketi kwenye kigoda. Katika tukio hilo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo na viongozi wengine walilazimika kichuchumaa kwa kuwa ni sharti kuwa kila mtu awe amekaa au amechuchumaa wakati kiongozi wa kabila la Waha mwenye kuheshimika anapokuwa anazungumza akiwa amekaa kwenye kigoda. 
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akimkabidhi zawadi ya mbuzi Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marco Gaguti, kwa niaba ya wazee wa Buhigwe. 
   Mwenyekiti wa Wazee wa Buhigwe Eliakim Balunguza akimkabidhi zawadi ya Mbuzi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo, wakati wa kikao hicho.
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kaborou akimkaribisha Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo kuzungumza kwenye Kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilayaya Buhigwe, Maalozi, Watendaji wa CCM na Wa Chama, leo. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma Naomi Kapambala na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo, Elisha Bagwanya.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo na meza Kuu wakiwa wamesimaa baada ya shamrashamra zilipolipuka ukumbini kabla ya kuanza kuzungumza na wajumbe kwenye kikao hicho.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na wajumbe kwenye kikao hicho.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Buhigwe, Mabalozi, Watendaji wa CCM na Wa Chama, akiwa katika ziara ya Kichama mikoani, leo. PICHA: BASHIR NKOROMO

  0 0

   Wachezaji wa timu ya Tusker ya Kenya wakiwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, tayari kwa ajili ya michuano ya Sportpesa itakayo anza kutimua vumbi  Juni 5 mwaka huu katika uwanja wa  Uhuru  maalufu kama shamba la bibi. Michuano hiyo imedhaminiwa na Kampuni ya Sport Pesa  kwa kuzishirikisha timu zinazo dhaiminiwa na kampuni hiyo za nchi ya Kenye na Tanzania.
  Wachezaji wa timu ya Tusker ya Kenya wakiwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, tayari kwa ajili ya michuano ya Sportpesa itakayo anza kutimua vumbi  Juni 5 mwaka huu katika uwanja wa  Uhuru  maalufu kama shamba la bibi.Michuano hiyo imedhaminiwa na Kampuni ya Sport Pesa  kwa kuzishirikisha timu zinazo dhaiminiwa na kampuni hiyo za nchi ya Kenye na Tanzania. Picha na Mafoto Blog

  0 0

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mwanza
  MFUKO wa Pensheni wa PSPF umewaleta poamoja watumishi wa umma kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza zaidi ya 450, ambao wanatarajiwa kustaafu hivi karibuni ili kuwapatia semina ya mafunzo itakayowawezwesha kujiandaa kustaafu kwa amani.
  Katika semina hiyo iliyoanza leo Juni 2, 2017 kwenye ukumbi wa chuo cha BoT Capri-point  jijini Mwanza, wadau wa PSPF ambao ni taasisi za fedha nao wametumia fursa hiyo kutangaza fursa mbalimbali ambazo wastaafu hao wanaweza kuzitumia ili kuendeleza maisha yao ya baadaye.
  Wadau hao ni pamoja na Mwalimu Commercial Bank, (MCB), NMB, CRDB, TPB na Mfuko wa UTT-AMIS, pia Shirika la Viwanda Vidogovidogo SIDO.
  Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko, Mwalimu Commercial Bank, (MCB),Bw. Valence Luteganya, akizungumzia huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo. "Beni hii imeanzishwa hivi karibuni na wamiliki wa benki hii kwa karibu asilimia 30 ni walimu. na huduma tunazozitoa ni pamoja na utoaji mikopo nafuu, ushauri wa kifedha lakini pia katika jiyihada za kurahisisha huduma za kibenki, MCB imo kwenye mtandao wa Umoja Switch ambao umetapakaa nchi nzima." hayo ni baadhi ya maneno ya Bw. Lutenganya
   Bw. Lutenganya, akifafanua zaidi huduma zitolewazo na benki ya MCB

  Mkuu wa kitengo cha  wateja binafsi benki ya NMB, Bw.Omary Mtiga, akitoa somo kuhusu fursa mbalimbali ambazo wastaafu hao watarajiwa wanaweza kuzipata. "Benki ya NMB ina matawi kote nchini na hivyo inaweza kukufikishia huduma hapo ulipo pasina shaka, kwenu nyinyi ambao wengi wenu ni wateja wetu, mnayo fursa ya kufungua Bonas account ambayo inakuwezesha kufikia malengo mbalimbali uliyojiwekea na inaweza kutunza amana zako kwa usalama na kufikia malengo yako ya baadaye uliyojiwekea, lakini kubwa zaidi hakuna gharama za kuendesha akaunti hii." alisema
   Mkurugenzi wa idara ya mikopo benki ya Posta Tanzania, (TPB), Bw. Henry Bwogi, akizoa mada kwa washiriki ambapo alisema, "TPB ndiyo benki kongwe kuliko zote hapa nchini ikiwa na matawi yaliyosambaa kila kona ya nchi na hivyo kuwa rahisi kwa wateja kufikiwa na huduma zake, lakini pia benki hiyo tayari imeonyesha nia ya dhati ya kuwajali wastaaafu ambapo imekwisha toa mikopo ya mabilioni ya shilingi kwa wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF.
   Bi Doris Mlenge, Afisa Masoko wa Mfuko wa UTT-AMIS, akiwapatia vipeperushi vyenye maelezo ya huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo. "Kwa mtu yeyote anayetegemea kupata kipato kwa mkupuo kutokana na pensheni au chanzo kingine cha fedha anatakiwa kuwekeza kwenye Mfuko huo ili aweze kupata kipato cha mara kwa mara na akasema kuwekeza kwenye mifuko ya kujikimu kama UTT-AMIS kunatoa faida kubwa ukilinganisha na uwekezaji wa namna hiyo kwenye masoko ya fedha.
   Bw. Denis Mwoleka, ambaye ni Meneja wa CRDB tawi la Chuo Kikuu cha SAUT jijini Mwanza, akizungumza kuhusu umuhimu wa wastaafu hao watarajiwa kujiunga nabenki hiyo kwa kutarajia kupata faida mbalimbali ikiwemo huduma mpya ya akaunti ya akiba ya dhahabu ambayo ni njia rahisi ya kujiwekea akiba ili kufanikisha malengo ya baadaye.
   Afisa kutoka Shirika la viwanda vidogo vidogo SIDO, akihamasisha wastaafu watarajiwa kuwekeza kwenye uanzishaji wa viwanda vidogo vidogo ambavyo vitawawezesha kujikimu kimaisha na ksutaafu kwa amani. yeye alsiema SIDO iki tayari kutoa ushauri na mafunzo ya uanzishaji wa viwanda hivyo

   Meneja Pensheni za Wastaafu wa PSPF, Bw.Mohammed Salim,(kulia), akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, (wapili kushoto) na Meneja Mipango na Utafiti wa Mfuko huo, Bw.Luseshele Njeje
   Meneja wa Fedha wa PSPF, Bw.Lihami Masoli. (kulia), na Mtafiti Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw.Mapesi Maagi, (katikati), wakibadilishana mawazo na Katibu Msaidizi wa TSC wilaya ya Kwimba, Bw. Fundikira R.K. James, wakati wa mapumziko ya semina hiyo
   Meneja Pensheni za Wastaafu wa PSPF, Bw.Mohammed Salim, (kushoto), akifafanua mambo kadhaa kuhusu pensheni
  Bw. Silayo (kushoto), akiteta jambo na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi

  0 0

  Mkurungezi Mtendaji na Muanzilishi wa IswapMyBooks.Com Shafiq Mpanja akifafanua jambo kwa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa Mtandao huo unaowezesha wasomaji wa vitabu kubadilishana vitabu mara tu wanapomaliza kuvisoma kwa njia ya mtandao huo.Hafla ya uzinduzi huo zilifanyika mapema jana katika makao makuu ya SOMA BOOK Cafe iliyopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam.


  Meneja Uendeshaji wa IswapMyBooks.com Viola Massawe akifafanua taratibu za matumizi ya mtandao huo , wakati wa uzinduzi wa Mtandao huo unaowezesha wasomaji wa vitabu kubadilishana vitabu mara tu wanapomaliza kuvisoma kwa njia ya mtandao huo.Hafla ya uzinduzi huo zilifanyika mapema jana katika makao makuu ya SOMA BOOK Cafe iliyopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam.


  Mkurungezi Mtendaji wa Soma Book Cafe Demera Kitunga akielezea umuhimu wa kujisomea kwa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi  wakati wa uzinduzi wa Mtandao wa IswapMyBooks.com, Mtandao huo unaowezesha wasomaji wa vitabu kubadilishana vitabu mara tu wanapomaliza kuvisoma kwa njia ya mtandao huo.Hafla ya uzinduzi huo zilifanyika mapema jana katika makao makuu ya SOMA BOOK Cafe iliyopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam.


  Mdau akichangia jambo wakati wa uzinduzi wa IswapMyBooks.com , Mtandao huo unaowezesha wasomaji wa vitabu kubadilishana vitabu mara tu wanapomaliza kuvisoma kwa njia ya mtandao huo.Hafla ya uzinduzi huo zilifanyika mapema jana katika makao makuu ya SOMA BOOK Cafe iliyopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam.
  Mkurungezi Mtendaji wa Koncept Krantz Mwantepele (mwenye koti la suti) na wadau wa usomaji wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa mtandao wa IswapMyBooks.com , Mtandao huo unaowezesha wasomaji wa vitabu kubadilishana vitabu mara tu wanapomaliza kuvisoma kwa njia ya mtandao huo.Hafla ya uzinduzi huo zilifanyika mapema jana katika makao makuu ya SOMA BOOK Cafe iliyopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam.
  Wageni waalikwa na Wadau wa usomaji wakijisajili kwa kufungua akaunti zao  kwenye mtandao wa IswapMyBooks.com , wakati wa uzinduzi wa Mtandao huo unaowezesha wasomaji wa vitabu kubadilishana vitabu mara tu wanapomaliza kuvisoma kwa njia ya mtandao huo.Hafla ya uzinduzi huo zilifanyika mapema jana katika makao makuu ya SOMA BOOK Cafe yaliyopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam.
  Mkurungezi Mtendaji na Muanzilishi wa IswapMyBooks.com  Shafiq Mpanja akiwa kapozi wa picha  mara baada ya  uzinduzi wa Mtandao huo unaowezesha wasomaji wa vitabu kubadilishana vitabu mara tu wanapomaliza kuvisoma kwa njia ya mtandao huo.Hafla ya uzinduzi huo zilifanyika mapema jana katika makao makuu ya SOMA BOOK Cafe iliyopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam.
  Mkurungezi Mtendaji na Muanzilishi wa IswapMyBooks.com Shafiq Mpanja (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wadau waliofika kwenye uzinduzi wa  Mtandao huo unaowezesha wasomaji wa vitabu kubadilishana vitabu mara tu wanapomaliza kuvisoma kwa njia ya mtandao huo.Hafla ya uzinduzi huo zilifanyika mapema jana katika makao makuu ya SOMA BOOK Cafe yaliyopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam.


  Wadau wa usomaji vitabu wakipozi kwa picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa mtandao wa IswapMyBooks.com .Mtandao huo unaowezesha wasomaji wa vitabu kubadilishana vitabu mara tu wanapomaliza kuvisoma kwa njia ya mtandao huo.Hafla ya uzinduzi huo zilifanyika mapema jana katika makao makuu ya SOMA BOOK Cafe iliyopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam.


  0 0


  Tanga, SERIKALI imeshauriwa kuweka kanuni ya majengo ya gorofa na taasisi za huduma za kijamiii kujenga miundombinu maalumu kwa walemavu lengo ikiwa ni kuzifikia huduma kama ilivyo kwa wengine. 

  Wakizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa mbalimbali vilivyokabidhiwa kwa uongozi wa Kituo cha Watoto Walemavu (YDPC), na kuishauri kutoruhusu ujenzi wa majengo ya huduma za kijamii bila kuwepo kwa miundombinu ya walemavu. 

  Imesemwa kuwa majengo mengi ya huduma za kijamii hayana miundombinu kwa walemavu hivyo kunyimwa fursa ya kupata huduma kama ilivyo kwa wengine. 

  Imesemwa katika kongamano hilo, kuwa kutokuwepo kwa sheria watu wengi hujenga majengo bila kuweka miundombinu ya walemavu.
  Imesemwa kuna baadhi ya walemavu wa viungo wenye elimu hupoteza nafasi ya kazi kutokana na majengo wanayopangiwa kazi kutokuwa na njia maalumu kwa walemavu wa viungo na kuwa kero kwao.

  Mtaalamu wa tiba sanifu kwa njia ya Mazoezi kwa njia ya Mazoezi na Vitendo, Amina Mbowe, akitoa maelekezo ya kazi wanazozifanya katika kitengo chake ikiwa na pamoja na kuwaonyesha vifaa vya mazoezi kwa watoto wenye ulemavu.
  Mwanafunzi mlemavu kituo cha Watoto wenye Ulemavu wa viungo na ngozi, Imamu Amir, akipanda mbegu ya muhongo katika shamba la kituo hicho kijiji cha Mleni Amboni Tanga, ujumbe huo pia ulitembelea katika shamba hilo ambalo watoto walemavu wamekuwa wakiendesha kilimo cha chakula na mbogamboga.

  Mtaalamu wa kilimo kwa watoto walemavu kituo cha Walemavu, Sabra Swai akitoa maelekezo kwa ujumbe wa umoja wa wanawake wa Makanisa ya Free Pentacostal Church of Tanzania wakati walipotembelea shamba la Mleni ambalo watoto walemavu wa viungo, ngozi, viziwi na wengineo huendesha kilimo shamba lililoko kilometa 20 kutoka Tanga mjini. Mkurugenzi wa kituo cha Watoto Walemavu (YDPC) William Hendry wa pili kulia akiongoza maombi na kutoa shukurani kwa Ujumbe wa Umoja wa Wanawake Makanisa Free Pentacoastal Church of Tanzania wakati alipopokea zawadi mbalimbali kwa kituo hicho. blog ya kijamii ya tangakumekuchablog 0655 902929

  0 0

   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kasulu, Mabalozi, Watendaji wa CCM na wa Serikali, katika kikao cha ndani kilichofanyika leo, Juni 2, 2017, mjini Kasulu, akiwa katika mwendelezo wa ziara zake za Kichama mikoani.
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kasulu, Mabalozi, Watendaji wa CCM na wa Serikali, katika kikao cha ndani kilichofanyika leo, Juni 2, 2017, mjini Kasulu, akiwa katika mwendelezo wa ziara zake za Kichama mikoani.
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kasulu, Mabalozi, Watendaji wa CCM na wa Serikali, katika kikao cha ndani kilichofanyika leo, Juni 2, 2017, mjini Kasulu, akiwa katika mwendelezo wa ziara zake za Kichama mikoani. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kaborou na Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kasulu Ezekiel Kaloba.
   Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kaborou wakati akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza katika kikao hicho. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Josephine Ngezabuke, Katibu wa Siasa na Oganaizesheni Makao Makuu ya Jumuia ya Wazazi Tanzania Daniel Mgaya, Katibu wa CCM Wilaya ya Kasulu Ndugu Manyonyi na Kuliani Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma Naomi Kapambala, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kasulu Ezekiel Kaloba na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo
   Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma, Naomi Kapambala alipokuwa akitoa maneno ya utangulizi katika kikao hicho. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kaborou na Mgeni Rasmi Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo
   Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kasulu Ezekiel Kaloba alipokuwa akifungua kikao hicho
   Wajumbe wakishangilia wakati Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo alipokuwa aliposema maneno yenye mguso wakati akizungumza nao kwenye kikao hicho. 
  Wajumbe wakimsikiliza kwa makini Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo alipokuwa alipokuwa akizungumza nao kwenye kikao hicho.PICHA: BASHIR NKOROMO

  0 0

  Wazazi wametakiwa kuwa mstari wa mbele kwa kutoa elimu kwa vijana wao, ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa katika maadili mabaya, yanayopelekea wengi wao kujiingiza katika mazingira hatarishi ambayo yanaviashiria vya uvunjifu wa Amani.

  0 0


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Semina kwa wastaafu watarajiwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza
  Baadhi ya washiriki wa Semina ya Wastaafu Watarajiwa wakisikiliza kwa makini hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Mwanza.
  Baadhi ya washiriki wa Semina ya Wastaafu Watarajiwa wakisikiliza kwa makini hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Mwanza.
  Baadhi ya Wadau wakifuatilia ufunguzi wa Semina kwa Wastaafu Watarajiwa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha Vitabu vya PSPF kwenye kutoa elimu kwa Wanachama wa mfuko huo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu kabla ya ufunguzi wa Semina kwa wastaafu watarajiwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewaagiza waajira wasiopeleka au kuchelewesha michango ya wanachama kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii nchini wachukuliwe hatua za kisheria ili kukomesha tabia hiyo.

  Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo 3-June-2017 Jijini Mwanza wakati anafungua semina ya maisha baada ya kustaafu,fursa ya mafao,uwekezaji iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kwa ajili ya wastaafu watarajiwa 450 kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza.

  Makamu wa Rais amesisitiza kuwa waajiri wakichangia kwa mujibu wa sheria kwenye mifuko hiyo watawezesha wanachama wao kupata mafao kikamilifu na kwa wakati.

  Kuhusu madeni ya Serikali kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini, Makamu wa Rais amewahakikishia Wakurugenzi wa mifuko hiyo kuwa Serikali inashughulikia madeni hayo na baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki wa madeni hayo basi malipo yatafanyika haraka iwezekanavyo.


  Makamu wa Rais amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha michango ya pensheni kwa wafanyakazi wa taasisi zinazopata ruzuku kutoka Serikalini inalipwa kwenye mifuko hiyo kwa wakati.Aidha, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahimiza wastaafu watarajiwa kote nchini waache tabia ya kukata tamaa baada ya kustaafu bali wajipange vyema na kuwekeza katika miradi mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo viwanda vidogo, kilimo na biashara.

  Amesema kuwa kama wastaafu hao watawekeza katika maeneo hayo watatoa ajira kubwa kwa vijana badala ya kutumia mafao yao kwenye matumizi yasiyo ya lazima.

  “Wazee ni rasilimali na hazina kubwa kwa taifa kama waswahili wasemavyo panapo wazee hapaharibiki jambo hivyo basi ni matumaini yangu kuwa mfuko wa PSPF mtaendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu kuhakikisha kuwa hazina hii ya wazee wetu wanapata haki zao kwa mujihu wa sheria za nchi pale wanapohitaji huduma toka kwenu.”Amesisitiza Makamu wa Rais.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameonya wastaafu hao watarajiwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima bali watumie fedha watakazopata katika shughuli za kiuchumi kwa ajili ya maslahi yao ya baadaye.Makamu wa Rais pia amepongeza jitihada zinazofanywa na mfuko wa PSPF kwa kutoa mafunzo kwa wastaafu watarajiwa kwa ajili ya kuwasaidia kujipanga vyema pindi watakapostaafu utumishi wao.

  Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji amewahakikishia wastaafu hao watarajiwa kuwa wa mkoa wa Mwanza kuwa Serikali itaendelea kusimamia vyema mifuko ya hifadhi ya jamii ili iweze kutoa mafao bora na kwa wakati.

  Dkt Ashatu Kijaji pia amehimiza wastaafu hao watarajiwa kutumia vizuri mafao wanayopata kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.
   

  0 0

  Mwili wa marehemu Mzee Francis Maige Kanyasu umeagwa leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kusafirishwa na serikali kwenda kijijini kwao Igokero wilayani Misungwi. 

   Shughuli ya kuuaga mwili huo imeongozwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamaii , Jinsia , Wazee na Watoto, Marcel Katemba ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk. Mpoki Ulusubisya. 

   Akizungumza katika shughuli hiyo Bwana Katemba ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa jitihada kubwa walizofanya za kumpatia tiba na kumuhudumia kwa kipindi alichokuwa amelazwa hospitalini hapo. 

   “Nawapongeza Muhimbili kwa juhudi zenu ni kweli mlitaka kuokoa maisha ya mzee wetu, lakini kazi ya Mungu haina makosa, Pia sina budi kuwashukuru majirani zake na uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Malapa kwa kujitoa - naomba mfanye hivyo hata kwa wazee wengine’’ amesema Katemba.  
  Naye Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dk. Juma Mfinanga amesema walimpokea Mzee Kanyasu Mei 25, 2017 akitokea Hospitali ya Amana alikokua akipatiwa matibabu na walipomfanyia vipimo vya awali waligundua kwamba ana maradhi ya Kifua Kikuu ambayo alikuwa nayo kwa muda mrefu kutokana na mazingira aliyokua akiishi. 

   Hivyo Dk. Juma ametoa rai kwa wananchi kujenga tabia ya kwenda hospitalini mapema pindi mtu anapoona hali yake ya kiafya si nzuri kwani ukiwahi hospitali ni rahisi kupata tiba na kupona kuliko kusubiri hadi ugonjwa uwe sugu. 

   Mzee Francis Maige Kanyasu alizaliwa 1931 na kufariki dunia Mei 29 , 2017 saa mbili na nusu usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
   Waombolezaji wakiongozwa na  Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Godfrey Mungereza (kushoto) na Bw. Eric Shigongo wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu  tayari kwa safari ya kuelekea Misungwi mkoani Mwanza ambako mazishi yatafanyika.

  Baadhi ya wafanyakazi wa Muhimbili wakisubiri kuuaga mwili huo leo. Kulia ni Zuhura Mawona ambaye amemwakilisha Mkurugenzi wa Uuguzi, Agness Mtawa na Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dk Julieth Magandi. Pembeni yao kushoto ni Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Godfrey Mungereza
   Baadhi ya wanahabari na wawakilishi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiaga mwili wa marehemu Francis Maige Kanyasu (86) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo. Marehemu alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo na wakati akiendelea na matibabu mauti yakamkuta.
   Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Marcel Katemba ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Mpoki Ulusubisya akizungumza kabla ya shughuli za kuaga mwili huo leo.
   Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali wa Muhimbili, Dk Juma Mfinanga akieleza kwa wanahabari jinsi Hospitali ya Muhimbili ilivyokuwa ikimpatia matibabu mzee Francis Maige Kanyasu.
   Mkurugenzi wa Huduma na Upasuaji wa Muhimbili, Dk Julieth Magandi akiwashukuru watu mbalimbali walofika kuuaga mwili huo leo.
   Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali wa Muhimbili, Dk Juma Mfinanga akieleza jinsi Hospitali ya Muhimbili ilivyokuwa ikimpatia matibabu mzee Francis Maige Kanyasu.
  PICHA NA JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

  0 0

  Bi. Anna Mghwira


older | 1 | .... | 1257 | 1258 | (Page 1259) | 1260 | 1261 | .... | 1896 | newer