Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

RC Gambo, wadau wa utalii waweka mikakati kuipaisha Arusha

$
0
0

Na Nte Hosseah 

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo amekutana na wadau wa sekta ya utalii mkoani humo na kujadili nao namna mbalimbali wanazoweza kuboresha sekta ya utalii mkoani humo. 

"Mkoa wa Arusha unachangia mapato ya utalii nchini kwa zaidi ya asilimia 80 hivyo sisi kama mkoa tukiwa na mikakati madhubuti ya kuiboresha hii sekta tutakua tumeikuza sekta hii kiasi cha kuleta matokeo chanya kwa taifa kiujumla." Alisema Gambo. 

Nao chama cha wafanyabiashara wa utalii (TATO) walisema changamoto katika biashara hiyo ni nyingi lakini kwa sehemu kubwa wanaishukuru serikali ya awamu ya tano kwani katika awamu hii changamoto nyingi zimeonekana kutatuliwa, kwa kuongezea walisema kinachowapa hofu kwa kipindi hii kuelekea mwaka mpya wa fedha ni kuanza kwa tozo mpya ya ada ya mahoteli yanayolaza wageni porini (concession fee) ambapo wao kama walaji wa mwisho wanaona itawaathiri sana kwakua tangazo la serikali limetoka ndani ya muda mfupi, 

"Tangazo limetoka mwezi Mei na wageni walishafanya booking toka mwezi Machi na tuliwapa bei zisizokua na tozo hizi, hivyo tunaomba serikali ilifikirie hili mara mbili na kutuongezea muda tuanze kulipa januari ili isituathiri kibiashara.

" Alisema bwana Willy Chambulo mwenyekiti wa TATO. Akiwatoa hofu hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA bwana Allan Kijazi amekiri kua hiyo tozo kwa wakati ni changamoto ila akawatia moyo kuwa bado kuna muda wa kulizungumza hilo kwani serikali hii ya awamu ya tano ni sikivu, na aliwataka wakutane wadau wote wajadiline waone namna ya kuishauri wizara kuongeza muda ili isiathiri biashara hii kwa ujumla. 

Naye Mhe Gambo amewachagiza wadau hao kushirikiana na viongozi wa mkoa kuandaa tamasha kubwa la utalii la kimataifa litakalotumika kama jukwaa la kuutangaza mkoa na taifa kwa ujumla hasa kwa kualika mabalozi wa nchi ambazo huleta watalii wengi hapa nchini.

Vilevile akatoa rai kwa wageni wawe na amani wawapo mkoani hapa kwani kwa sasa mkoa ni shwari na kamati yake ya ulinzi na usalama imejikita katika kuzima viashiria vyote vya uvunjifu wa amani. Vile vile Mhe Gambo amepokea jumla ya mablanketi 200 kati ya 400 kutoka Leopard tours na kuyabidhi kwa jeshi la magereza kwa ajili ya wafungwa katika gereza kuu Kisongo,

Pia amekabidhi kompyuta moja na printer kwa wafungwa wa gereza hilo la Kisongo ikiwa ni katika utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa kwa wafungwa hao kipindi alipowatembelea mapema mwezi wa tano.
 Mkuu wa mkoa Mhe Gambo akiwa katika kikao na wadau wa utalii mkoani humo.
 Mkuu wa mkoa Mhe Gambo akiwa katika kikao na wadau wa utalii mkoani humo.
 Mkurugenzi wa TANAPA bwana Allan Kijazi akisikiliza kwa makini michango ya wadau katika kikao hicho,akifuatiwa na mkurugenzi wa Leopard Tours bwana Fazal,mwenyekiti wa TATO na bwana Willy Chambulo
 Mkurugenzi wa mamlaka ya Ngorongoro bwana Fredy Manongi akitoa mchango wake katika kikao hicho
Mhe Gambo akipokea msaada wa mablanketi kwenda katika gereza la Kisongo Arusha

NHC TANGA YAWATANGAZIA KIAMA WANAOGUSHI FOMU ZA UPANGISHAJI

$
0
0

 Meneja wa Shirika la Taifa la Nyumba(NHC) mkoani Tanga Mussa Kamendu katikati akionyesha moja kati ya chemba ambazo zinafanyiwa ukarabati eneo la mtaa wa market Jijini Tanga  na Fundi Mchundo wa Shirika hilo jana wakati alipotembelea kuona hali ya ukarabati huo unavyoendelea
 Meneja wa Shirika la Taifa la Nyumba(NHC) mkoani Tanga Mussa Kamendu katikati akionyesha waandishi wa habari maeneo mbalimbali waliokarabati
 Meneja wa Shirika la Taifa la Nyumba(NHC) mkoani Tanga Mussa Kamendu katikati akionyesha waandishi wa habari maeneo mbalimbali waliokarabati
Meneja wa Shirika la Taifa la Nyumba(NHC) mkoani
Tanga Mussa Kamendu kulia akionyeshwa moja kati ya chemba ambazo zinafanyiwa ukarabati eneo la mtaa wa market Jijini Tanga  na Fundi Mchundo wa Shirika hilo wakati alipotembelea kuona hali ya ukarabati huo unavyoendelea


 Meneja wa Shirika wa Shirika la Taifa la Nyumba Mkoani Tanga (NHC),Mussa Kamendu akikagua ukarabati wa nyumba za shirika hilo ambazo zinafanyiwa marekebisho
 Mafundi wakiendelea na kazi kama wanavyoonekana
Meneja wa Shirika wa Shirika la Taifa la Nyumba Mkoani Tanga (NHC),Mussa Kamendu akikagua mitaro iliyochimbwa kwa ajili ya kupitisha mfumo wa maji taka
SHIRIKA la Nyumba la Taifa Mkoani Tanga (NHC) limewa tahadharisha watu wanaoghushi fomu za maombi ya kupangisha katika nyumba zao na kuziuza kwa wananchi kuacha mara moja tabia hiyo kwani watakabanika watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya dola.
 
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Meneja wa Shirika hilo,Mussa Kamendu wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu mipango mbalimbali ya shirika hilo ikiwemo kuzifanyia ukarabati nyumba wanazozimiliki ili ziweze kuwa katika muonekana mzuri kwa zile ambazo zimeonekana  kuchakaa.

 
Alisema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wananchi kughusi fomu ambazo zinatolewa na shirika hilo kwa kuzisambaza kwa wengine na kuwauzia jambo ambalo ni kinyume na utaratibu uliopo.

 
“Ukiangalia sisi kama shirika tumekuwa tukitoa fomu kwa wananchi ambao wanataka kupangisha kwenye nyumba zetu lakini katika hilo kumejitokeza baadhi ya watu wanazitoa kopi na kuziuza kitendo ambacho ni uvunjifu wa taratibu tulizoziweka “Alisema.

 
“Jambo hili ni hatari hasa kwa ustawi wa shirika letu kwani
linachangia kukosesha mapato hivyo tutahakikisha tunawa shughulikia watakaobainika kufanya hivyo bila kuangalia nafasi yake kwa maslahi ya ustawi wa shirika letu “Alisema Meneja huyo.

 
Aidha alisema licha ya jitihada hizo lakini pia wameweka mpango
kabambe wa kuhakikisha wadaiwa wote wanalipa madeni yao ya pango kwa wakati ili kuweza kutoa fursa kwa shirika hilo kuweza kujiendesha na kuweza kufanikisha mipango ya maendeleo.

 
Kamendu aliwataka pia wapangaji wao wazingatie mikataba walioingia na shirika hilo ikiwa pamoja na utunzaji mazingira ya nyumba hizo na kulipa kodi kwa wakati kabla ya hatua za kisheria hazijachukuliwa.

 
Aidha pia alisema hivi sasa tayari shirika hilo limekwisha anza
kufanya ukarabati wa nyumba hizo ikiwa pamoja na kuboresha mifumo ya maji taka, kuweka bati mpya na upakaji wa rangi katika nyumba zilizopo katika maeneo mbalimbali ndani ya Jiji la Tanga.

 
Alisema miongoni mwa nyumba walizoanza kuzifanyia ukarabati ni pamoja na zilizopo maeneo ya Chumbageni,kwa karatunga,barabara 4,6,Bombo na Raskazoni ambapo marekebisho hayo yanafanyika kwa lengo la kurudisha ubora wa nyumba hizo.

 
Aliongeza kuwa marekebisho yanayofanywa na shirika hilo yana lengo la kuhakikisha nyuma zao zinakuwa katika ubora mzuri ambao utamfanya mpangaji aweze kuishi kila kukumbana na usumbufu wa aina yeyote.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

MAZISHI YA NDESAMBURO KUFANYIKA KWA SIKU MBILI MFULULIZO

$
0
0
Kikao cha Wanafamilia,Viongozi wa siasa na Viongozi wa Dini kikifanyika nyumbani kwa marehemu Ndesamburo kwa ajili ya maandalizi ya mazishi yake.
Ndugu na Baadhi ya watoto wa marehemu Philemoni Ndesamburo wakiwa katika kikao hicho.
Baadhi ya Viongozi wa Chadema wakishiriki katika kikao hicho.
Baadhi ya watoto wa marehemu Philemoni Ndesamburo.
Baadhi ya Wabunge wakishiriki katika kikao hicho.
Baadhi ya wanandugu wa familia ya marehemu Ndesamburo.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini

MAZISHI ya Mbunge mstaafu wa jmbo la Moshi mjini na Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro Philemon Ndesamburo Kiwelu (82) yanataraji kufanyika kwa siku mbili mfululilizo huku watu zaidi ya laki 2 wakitaraji kushiriki katika mazishi hayo.

Shughuli nzima za mazisihi zinataraji kufanyika June 5 na sita katika uwanja wa mashujaa mjini Moshi kabla ya kuhitimishwa siku ya Jumanne kwa ibada itakayoanzia kanisani na kumalizikia nyumbani kwa marehemu. 

Hatua ya maziko ya Ndesamburo kufanyika kwa siku mbili inatokana na uwepo wa idadi kubwa ya marafiki wa familia kushiriki katika maziko hayo ya kihistoria yatakayotanguliwa na kutoa heshima za mwisho ,shughuli zilizopangwa kufanyika katika uwanja wa mashujaa mjini Moshi.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichodumu kwa zaidi ya saa nne ,Msemaji wa Chadema katika maandalizi ya mazishi hayo Amani Golugwa amesema uamuzi huo unatokana na kutoa nafasi kwa watu mbalimbali kutoa heshima za mwisho kwa Ndesamburo.

“Tumekua na kikao na wanafamilia viongozi wa chama na mashaurizano kuhusiana na msiba huu ,tumekuwa na watoto wa marehemu ,walikuwepo wachungaji na viongozi wa chama ,kimsini tumekubaliana mazishi ya mze wetu Ndesamburo yatafanyika kwa siku mbili mfululizo”alisema Golugwa.

Kutakuwa na siku mbili za maombolezi,siku ya jumatatu mwezi huu tutakuwa na state funeral (mazishi ya kitaifa) siku ambayo tutafanya kumbukizi ya maisha yake na tunataraji kuwa na idadi kubwa sana ya watu”alisema Golugwa.

Kwa upande wake msemaji wa familia ambaye pia ni motto mkubwa wa marehemu Ndesamburo,Sindato Ndesambur o alisema vikao mbalimbali vinaendelea kwa ajili ya maandalzi ya mazishi na kwamba yanataraji kutanguliwa na maandamano.

“Kama unavyoonabado tunaendelea na vikao kwa sasa ,kuona namna gani tunaweza kumuaga mzee wetu kwa heshima aliyojijengea kwa wakazi wa Moshi na taifa kwa ujumla “alisema Sindato.

Alisema wanatazamia kupokea wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi zikiwemo taasisi mbalimbali za kidini,kiserikali pamoja na wafanyabiashara watakao shiriki katika shughuli nzima ya mazishi .

Mapema jana vilio na Simanzi vilitawala chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ,wakati familia ya Marehemu  Ndesamburo  ikiongozwa na mtoto wake wa  Pili ,Lucy Owenya kushudia mwili wa mpendwa wao ukiwa umehifadhiwa.

Wakati kifo cha Mzee Ndesamburo kinatokea ,Lucy Owenya alikuwa akihudhuria vikao vya  Bunge la 11 ,vikao vya  Bajeti  ambapo alipata nafasi ya kuchangia mjadala wa bajeti ya wizara ya fedha kabla ya kupokea taarifa rasmi ya kifo cha Ndesamburo ambaye pia ni mfanyabiashara mashuhuri.


Majira ya saa 11:45 familia ilifika katika hospitali ya rufaa ya KCMC huku Mbunge wa jimbo la Rombo ,Joseph Selasini akisimamia zoezi la kuomba kuona mwili wa marehemu Mzee Ndesamburo ili kujiridhisha kama kweli baba yao amelala mauti.


Michuzi Blog ililifika KDC nyumbani kwa marehemu Ndesamburo na kushuhudia maandalizi ya shughuli za maziko yakiendelea huku waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali ya pembe ya nchi wakifika kutoa pole kwa familia ya marehemu.


Philemoni Ndesamburo atakumbukwa na mengi hasa katika siasa za mageuzi ambapo katika uchaguzi wa mwaka 2015 akiwa ni mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro alisaidia kupatikana kwa madiwani wengi katika baraza la madiwani wa manispaa ya Moshi.


Ndesamburo maarufu kama Ndesa Pesa ametumia muda wake mwingi katka siasa na biashara ,amefariki dunia wakati akitaka kukabidhi mchango wake kwa meya wa jiji la ARUSHA ,Kalist Lazaro kwa ajili ya familia za watoto wa shule ya msingi ya Lacky Vicent waliofariki katika ajali ya gari Wilayani  Karatu mkoani Arusha.


Mwisho.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNE 2,2017

WANAFUNZI 40 KUTOKA SHULE YA SEKONDARI WASICHANA SONGEA MKOANI RUVUMA WAUNDA KLABU USALAMA BARABARANI

$
0
0
Wanafunzi 40 kutoka shule ya sekondari wasichana SONGEA mkoani RUVUMA waunda klabu usalama barabarani ambayo itakuwa na lengo la kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya barabar inayohamasisha wamtumizi sahihi ya barabara

ADVANCED EXCEL FOR PROFESSIONALS ON JULY 24-28, 2017 AT MAKUMBUSHO BUSINESS COMPLEX - DAR

WAZIRI MKUU: TUMEBAINI MADAI HEWA YA BILIONI 21/-

$
0
0
* Ni kwenye malipo ya mawakala wa mbolea, awali yalifikia sh. bilioni 65.
*Akiri kukutana nao, asema wenye madai halali wote watalipwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imebaini madudu katika uhakiki wa madeni ya mawakala wa mbolea kwa sababu baadhi yao hawakuwa waaminifu.

“Tulipoanzisha mfumo wa kutoa pembeje kwa njia vocha kwa kuwatumia mawakala kupeleka pembejeo vijijini, tulibaini kuwa baadhi yao walikuwa siyo waaminifu. wakiorodhesha majina ya wakulima na kuandika kuwa wamewapa madawa napembejeo wakati hawapo.”

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Juni mosi, 2017) wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (Morogoro), Bi. Devotha Minja kwenye kipindi cha maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu bungeni mjini Dodoma.

Bi. Minja alitaka kujua ni kwa nini Serikali haijawalipa mawakala hao hadi sasa licha ya kuwa inatambua kwamba walifanya kazi ya kusambaza pembejeo hizo.

“Tulijikuta tuna deni la shilingi bilioni 65. Nilipokutana na mawakala wiki mbili zilizopita, niliwaahidi kwamba tutawalipa lakini ni lazima watupe muda tufanye uhakiki ili kubaini kama kweli pembejeo zilifika. Kati ya shilingi bilioni 35 za madeni ya awali, imebainika kuwa sh. bilioni 6 tu ndiyo za halali. Na bado kuna sh. bilioni 30 nyingine zinafanyiwa uhakiki,” amesema Waziri Mkuu.

“Tumewasihi waendelee kuwa wavumilivu ili tukamilishe zoezi hili na tujue Serikali inadaiwa kiasi gani. Napenda niwahakikishie kuwa kazi hiyo inaendelea na tuko kwenye hatua za mwisho, na wale wote wenye madai halali ambao ni waaminifu watalipwa na Serikali.”

Akijibu swali la nyongeza ni kwa nini Serikali isiharakishe malipo hayo kwani kuna baadhi nyumba zao zimepigwa mnada na mabenki, na wengine wamepoteza maisha kwa sababu ya mshtuko, Waziri Mkuu alisema siku ya mwisho ya kufanya uhakiki ilikuwa jana Mei 31 kwa hiyo anasubiri taarifa kutoka Halmashauri zote kupitia kwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Alisema wenye mabenki wameisikia kauli ya Serikali kwa hiyo hawana sababu ya kukimbilia kuuza mali za mawakala kwa njia ya mnada kwani hatua zinazochukuliwa na Serikali ni nzuri na zimeokoa mabilioni ya fedha.

Alisema watumishi wote wa umma waliohusika kwenye ubadhirifu huo, watachukuliwa hatua za kinidhamu.Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka wawekezaji nchini wasihofu hatua zinazochukuliwa na Serikali kuhusiana na usafirishaji wa mchanga wenye madini kwenda nje ya nchi.

Akijibu swali ya Bw. Emmanuel Mwakasaka, Mbunge wa Tabora “Ninawasihi wawekezaji wasiwe na shaka kwa sababu lengo la Serikali ni jema. Tunataka tujiridhishe kuwa kuna nini hasa ndani yake. Hatuna jambo ambalo tumelifanyia kazi isipokuwa kwa watu wetu wa ndani,” amesema.

“Kila kitu kitakuwa wazi, ninawaomba Watanzania na wawekezaji wawe watulivu. Kazi tunayoifanya ni kwa manufaa ya Watanzania. Nia yetu ni kulinda rasilmali za nchi yetu, na hadi sasa bado hatujatoa taarifa rasmi, bado tunasubiri taarifa ya kamati ya pili,” alisisitiza.

Akijibu swali la nyongeza ni mikakati gani Serikali imeweka kwa kufunga mashine kwenye chanzo ili kuhakikisha tatizo hilo haijirudii tena, Waziri Mkuu alisema Serikali imekuwa inapokea wawekezaji ambao wameonyesha nia ya kuwekeza kwenye eneo hilo. Alisema zamani kulikuw ana usiri wa kupata wawekezaji wa aina hiyo lakini hivi sasa kumeanza kuwa na uwazi katika eneo hilo.

“Tutaamua kujenga mashine zetu hapa hapa nchini au kuwakaribisha wawekezaji katika eneo hili au kuona uwezo wa Serikali ili tuweze kutatua tatizo la kupoteza mchanga ambao tunalazimika kuupeleka nje ya nchi kwa ajili ya uyeyushaji wa madini yaliyomo,” alisema.

Waziri Mkuu alisema hatua zilizochukuliwa na Serikali ni mwitikio wa kilio cha siku nyingi cha wananchi wa maeneo husika pamoja na waheshimiwa wabunge ambapo Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli alimtuma aende Kahama kuchukua sampuli za mchanga na alipompa taarifa, Rais akaunda tume mbili za kufuatilia suala hilo.

EXIM BANK TANZANIA YAPATA TUZO YA BENKI BORA YA MWAKA

$
0
0
 Exim Bank Tanzania imetambuliwa kama Benki bora ya mwaka katika wateja binafsi na biashara ndogondogo na saizi ya kati, yaani ‘Retail banking’ katika tuzo za Banker za Afrika Mashariki zilizofanyika Nairobi, Kenya. 

Tuzo za Banker za Afrika Mashariki zimedhamiria kuhamasisha ubora kwenye sekta ya fedha katika kanda ya Afrika Mashariki. Kupitia kura 77,000 zilizopigwa na jamii ya sekta ya fedha katika kanda hii benki ya Exim ilichaguliwa kama mshindi wa mwaka huu katika wateja binafsi na biashara ndogo - Retail. 

Akiongea kwa niaba ya benki hiyo, Mkuu wa kitengo cha fedha Selemani Ponda alisema, “Tunajivunia sana na kushukuru kwa tuzo hii. Tumefanya kazi kubwa kwa muda mrefu kujenga msingi wa kuendeleza operesheni zetu za baadae. Matokeo yanajionyesha, katika miaka ya karibuni amana kutoka kwa wateja wetu imeongezeka na wateja pia wameongezeka. Vilevile faida baada ya kodi imeendelea kukua hadi kufikia kiasi cha shilingi bilioni 72 kwa mwaka 2016.” 

Ponda ambaye alihudhuria hafla ya tuzo hizo alitoa pongezi kwa waandaaji kwa kuandaa tukio lenye mafanikio kwa miaka mine mfululizo. Hadi sasa tuzo hizo zimevutia ushiriki wa wanataaluma wengi zaidi katika sekta ya benki katika kanda hii. Zaidi ya hapo aliongeza kuwa washirika muhimu kama vile kampuni za teknolojia ambazo husaidia kubadilisha sekta hii pia zilitambuliwa kwa mchango wao. 

Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi na biashara ndogo Rahul Singh, alisema kuwa uvumbuzi pia umechangia kwa kiasi kikubwa katika kuifanya Exim kuwa benki bora nchini Tanzania na inaheshimika sana katika utoaji huduma na operesheni kupitia jukwaa la kiwango cha juu katika teknolojia. “Uvumbuzi ni ahadi tunayowapa wateja wetu. Benki hii imepata upenyo mkubwa kwa kuweka teknolojia ya viwango vya kimataifa na bidhaa zinazolenga mahitaji ya wateja,” aliongeza.

Benki ya Exim bank imechukua hatua nyingi katika kitengo hiki ikiwa ni pamoja na kuanzisha huduma ya kipekee inayoitwa "Preferred Banking" ambayo inaruhusu mteja kupata mhudumu wa benki wa kumhudumia, huduma za kipekee katika matawi ya benki, bei upendeleo ya bidhaa na faida za kipekee za kimaisha. Benki ya Exim ilikuwa ndiyo ya kwanza nchini kutambulisha kadi za kimataifa za malipo za MasterCard na Visa Platinum, Tanapa na kadi za Visa za malipo baadaye. Benki hii pia ilianzisha matumizi ya mashine za kutolea fedha yaani ATM na mpango wa mikopo kwa wanawake Tanzania. 

Juhudi za uanzilishi za Exim zimepitiliza mipaka, mwaka 2007 ilikuwa ni benki ya kwanza kuwa na operesheni nje ya nchi katika nchi ya Comoro. Benki ya Exim pia iliendelea kutanua mbawa zake zaidi katika nchi ya Djibouti Machi 2011, na kuweza kuunganisha kimkakati nchi hizi zilizo katika pembe ya Afrika. Mwaka 2016, Benki ya iliejitanua zaidi kikanda kwa kuwa na matawi matano nchini Uganda. 

Singh alimalizia kwa kuitambua timu nzima ya benki hiyo haswa wanaotoa huduma moja kwa moja kwa wateja katika matawi ya benki kwa kazi nzuri na kutimiza wajibu wao ipasavyo. Pia aliwashukuru wateja wote wa benki ambao wamechagua kuwa nao na ambao wanaisaidia benki hiyo kuweza kupata mafanikio kwa kuwapa biashara. Benki inajikita kuendeleza mindombinu yake, kuboresha huduma kwa wateja na operesheni ili kutoa huduma za kiwango cha juu kwa wateja. 





WFT, TGNP MTANDAO,HAWA NA OXFAM TANZANIA WAWAKUTANISHA WANAWAKE VIONGOZI KATIKA KUJADILI MASWALA YA KUMKOMBOA MWANAMKE KISIASA NA KIUCHUMI, SERENA JIJINI DAR.

$
0
0

Mkurugenzi wa Women Fund Tanzania Bi. Marry Lusimbi akitoa neno la utangulizi na kuwashukuru wanawake viongozi wote waliojumuika kwa pamoja katika Futari,na kujadili mambo ya msingi hasa ukombozi wa Mwaamke katika maendeleo,kisiasa,kiuchumi na jamii inakuwa ajenda kuu ya kitaifa.
Dr. Eve Maria Semakafu,(wa katikati) akichangia jambo juu ya namna ya wanawake viongozi wanavyoweza kusaidia katika kuhakikisha wanafunzi wa kizazi cha sasa wa Shule za Msingi na Sekondari wanapata elimu iliyobora na kubadili mfumo wa ufundishwaji kwani kwa sasa inaonekana wamekuwa wakidumaa sana kwa sababu ya kurahisishiwa kila kitu.
Bi. Fortunata Manyeresa(wa kwanza kushoto) akieleza namna mbalimbali za kuwafikia wanawake ikiwa ni pamoja na njia ya Vikoba,pia alielezea namna wanavyofanya kazi kupitia Asasi yao ya kiraia ya Tree of Hope yenye makazi yake Tanga
Bi. Eluka Kibona kutoka Oxfam Tanzania akielezea kwa undani maswala ya Siasa za ndani majumbani ambapo maana yake ni majukumu ya wanawake katika kulea familia zao majumbani bila malipo na kuongeza kuwa hayo yote yana mahusiano ya karibu baina ya matokeo ya uzoefu wa maisha ya wanawake na mfumo wa nchi ikiwa ni pamoja na Sera pia siasa.


Mmoja wa Viongozi wanawake Profesa Ruth Meena akieleza namna wanawake na wasichana wanavyopoteza muda mwingi katika kufanya kazi ambazo hazina malipo na kuwanyima kufanya kazi ambazo zingeweza kuwapatia kipato, alisema kupitia mkutano huu kunapaswa kuwa na maadhimio ambayo yatamsaidia mwanamke kuwa licha ya kufanya kazi za ndani lakini pia apate muda na wakufanya shughuli ambazo zitamsaidia kuingiza kipato


Mkurugezi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria wanawake Tanzania Bi. Tike Mwambipile (Kulia) akichangia jambo wakati wa Futari hiyo ambapo alisema kuwa ushirikishwaji wa wanawake vijana katika ukombozi wa mwanamke katika kuleta maendeleo ni muhimu kwa kuwa wananguvu na wanatakiwa mwongozo bora na kuwasaidia katika mambo mengine ili waje kuja kuwa viongozi bora wa Baadae.
Happiness Maruchu kutoka TGNP Mtandao ambaye alijikita katika nafasi ya vijana katika kuhakikisha kwamba ukombozi wa wanawake kimapinduzi unakuwa ajenda kuu ya kitaifa huku usawa wa kijinsia ukiwa nguzo ya kufanikisha maswala hayo,na kuongeza kuwa wanawake vijana wanaweza kufanya mambo makubwa ya kuwakomboa wanawake wengi zaidi.
Irene Kiria kutoka HAWA akichangia jambo na kuwashukuru viongozi wote ambao walifika katika Futari kwa kuwa amejifunza mengi na ataenda kuyafanyia kazi zaidi katika kazi zake na aliongeza kuwa vyombo vya Habari ni muhimu sana katika kufikisha taarifa hizi juu ya ukombozi wa wanawake.
Bi. Jane Remme Kutoka Asasi ya kimataifa ya kiraia Oxfam akichangia jambo wakati wa jukwaa hilo.



Mkurugezi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania Bw. Francis Odokorachi (kulia) akizungumza na baadhi ya waliofika katika futari.




Kikao kikiendelea.







Asasi za Kiraia za Women Fund Tanzania,HAWA,TGNP Mtandao na Oxfam Tanzania wamewakutanisha wanawake viongozi kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali nchini ili kujadili namna ya ukombozi kwa wanawake ikiwa ni kisiasa,kijamii na kiuchumi na kuhaki kisha hiyo ndio inakuwa ajenda kuu ya kitaifa.








Akizungumza kwa niaba ya Asasi zilizo andaa futari hiyo ya pamoja Mkurugenzi wa Women Fund Tanzania Bi. Mary Lusimbi alisema kuwa mjadala huo ulilenga kuwajenga viongozi hao kwenye mahusiano na ushirikiano wa wanawake kufungua nafasi kwa viongozi wanawake wengine kushiriki pamoja ili kuleta uwiano kijinsia .










"Tunaposema Masuala ya Siasa za Ndani Majumbani tunaongelea majukumu ya Wanawake katika kulea familia na nyumba bila malipo ukiwa na maana pana pia ni kwamba kuna mahusiano ya karibu baina ya matokeo na uzoefu wa maisha ya wanawake na mfumo wa nchi, sera, na siasa.," alisema






Wakati wa mjadala huo mpana wanawake hao viongozi waligusia kwa kina kuwa nguvu ya malengo ya ukombozi wa mwanamke kisiasa, kijamii na kiuchumi itasukumwa kwa pamoja kutokana na umoja wa wanawake waliopo katika nafasi za uongozi kupitia nafasi zao binafsi,taasisi na taaluma zao.






Walisema kuwa katika jamii zetu kuna mila na desturi ambazo zinahusiana na jinsia zinazo onesha kwamba katika jamii nyingi wanawake na wasichana hufanya kazi za nyumbani za kuhudumia familia na kulea kwa muda mrefu zaidi kulipo wanaume kazi hizo ni pamoja na kutunza wazee pamoja , kulea watoto, kuhudumia wagonjwa, kuandaa chakula, kusafisha, kuchota maji na kukusanya nishati kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, na kuongeza kuwa Takwimu zinaonesha kwamba pato la taifa lingeweza kukuwa kati ya asilimia 10 hadi 39 endapo Serikali ingewekeza katika kazi za nyumbani zisizo na malipo.



Pia ili kufanikisha haya Makundi mbalimbali, Wadau na Serikali wanatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo ambayo ni pamoja na Kupunguza kazi za nyumbani zisizo na malipo kwa kuweka mifumo sahihi itakayo rahisisha na kupunguza muda, Kuzitambua kwa kuziweka katika mifumo ya kisera na kibajeti na pamoja na Kuhakikisha makundi mbalimbali ya wanawake na wasichana yanapata uwakilishi katika ngazi za maamuzi, Kugawanya kazi hizi kwa makundi tofauti na kwa uwiano unaofaa kati ya wanawake na wanaume, jamii na familia.

WADAU WAMTEMBELEA NAIBU SPIKA DKT TULIA MJINI DODOMA

$
0
0
Jana, Juni 1, 2017, Wakurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Soka Tanzania (TFDF), Derek Murusuri na Taasisi ya Media Tanzania (TMF) Ernest Sungura, walimtembelea Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson, ofisini kwake mjini Dodoma. Pichani, Bw Sungura akiongea na Mh Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.

NRA WAMLILIA PHILEMON NDESAMBURO

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDD.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd , Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Picha ya pamoja

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MHE PAUL MAKONDA AMKABIDHI MWENGE WA UHURU MKUU WA MKOA WA PWANI MHE EVARIST NDIKILO

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda jana Alhamisi June 1, 2017 amemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo katika dhifa ya Makabidhiano iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1 tayari kwa kuelekea Mafia Mkoani Pwani.

Mwenge wa Uhuru ni chombo kilichoasisiwa na baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961 ikiwa ni Tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo  Mhe Paul C. makonda  amesema kuwa jumla ya Miradi 40 imepitiwa na Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2017 katika Mkoa wa Dar es salaam yenye thamani ya Shilingi 244,392,530,334 huku akibainisha kuwa Miradi 12 imezinduliwa, Miradi 15 imewekewa mawe ya Msingi, Miradi miwili imefunguliwa na Miradi 11 imetembelewa.

Rc Makonda alisema kuwa Mbio za Mwenge wa Uhuru tangu mwanzo zimekuwa kichocheo kikubwa katika kuhamasisha Maendeleo , uzalendo, Umoja , Mshikamano na kudumisha Amani ndani na nje ya nchi.

Alisema kuwa Mwenge wa Uhuru Mwaka 2017 wenye kauli mbiu isemayo Shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu pia umebeba jumbe mbalimbali ikiwemo kupiga Vita Maambukizi mapya ya UKIMWI na Malaria sambamba na kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya.

Katika mapambano dhidi ya Dawa za kulevya jitihada ya kudhibiti ni ajenda muhimu kwa mustakabali wa maisha ya mtanzania kwa kuwa linagusa nguvu kazi ya Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda kwenye dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. jana Alhamisi June 1, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akitoa taarifa ya Miradi iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wake mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kwenye dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. jana Alhamisi June 1, 2017
Baadhi ya Wananchi waliozuru katika dhifa ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. jana Alhamisi June 1, 2017
Viongozi mbalimbali wa serikali na wadau akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakifatilia dhifa ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. jana Alhamisi June 1, 2017.

PSPF YAWAPIGA MSASA WASTAAFU WATARAJIWA ZAIDI YA 300 KUTOKA WILAYA ZOTE MKOANI MWANZA

$
0
0



NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mwanza


MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufungua rasmi semina kwa wastaafu watarajiwa iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na kufanyika kwenye ukumbi wa chuo cha mafunzo kwa watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), jijini Mwanza.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, kwenye ufunguzi wa semina hiyo iliyoanza leo Juni 2, 2017, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Bw. Gabriel Silayo alisema, semina hiyo inalenga kuwandaa kwa kuwapa mafunzo watumishi wa umma ambao wanatarajiwa kustaafu hivi karibuni, ili hatimaye wastaafu kwa amani.

“Na kwa kufanikisha hilo, tunao maafisa wetu watatoa mada mbalimbali, wapo washirika wetu, SIDO, na mabenki kama vile NMB, CRDB, TPB, MCB na UTT, ambao watatoa elimu ya namna bora ya kutunza na kutumia fedha zako za mafao.” Alibainisha Bw. Silayo.

Bw. Silayo pia alisema, kwa kutambua kipaumbele cha serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake, Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kauli mbiu ya semina hiyo ni “Mafao ni Mtaji wa Uwekezaji Sahihi”. “Na ndio maana tumewaleta SIDO hapa ili wawaelimishe jinsi mtakavyoweza kuanzisha viwanda vidogo vidogo baada ya kustaafu utumishi wa umma na ndugu zangu napenda niwahakikishie hilo linawezekana.” Alisema

Alisema semina hiyo itakuwa ya siku mbili na kwamba, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ataifungua rasmi kesho Jumamosi Juni 2, 2017.

Zaidi ya watumishi 300 kutoka sekta mbalimbali za utumishi wa umma kwenye wilaya zote za mkoa wa Mwanza wanahudhuria semina hiyo ya mafunzo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo ya mafunzo kwa wastaafu watarajiwa 
Meneja Pensheni wa PSPF, Bw. Mohammed Salim, akitoa mada juu ya maandalizi na fursa za wastaafu
Afisa Mwandamizi wa Utafiti wa PSPF, Bw. Mapesi Maagi, akigawa vitendea kazi kwa washiriki wa semina mwanzoni mwa mafunzo hayo
Bw. Silayo, (Kushoto), akiteta jambo na Meenja wa Mipango na Utafiti wa PSPF, Bw. Luseshele Njeje.
Mshiriki akizunguzma wakati wa semina hiyo

Afisa Uhusino Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi akitoa utaratibu wa namna semina hiyo itakavyoendeshwa
Mshiriki akinukuu kilichokuwa kikiendelea
Wanasemina wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa
Baadhi ya wadau wa PSPF, na washiriki wa semina wakifuatilia mada zilziokuwa zikitolewa
Washiriki wa semina wakiwa kwenye ukumbi wa chuo cha mafunzo BoT jijini Mwanza
Bw. Silayo, (Kushoto), akimsikiliza kwa makini Meneja wa Fedha wa Mfuko huo, Bw.Lihami Masoli
Kuonyesha semina hiyo ilikuwa muhimu kwa wastaafu hawa watarajiwa, mshiriki wa semina akinakili kwa uangalifu mkubwa yaliyokuwa yakielezwa (mafunzo)
Afisa Mfawidhi wa PSPF, mkoani Mwanza, Bw.Salim Salum, akifafanua baadhi ya hoja zilizojitokeza. Kulia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo na katikati ni Meenja wa Pensheni wa Mfuko huo, Bw. Mohammed Salim
Sehemu ya washiriki wa semina
Mshiriki akipitia ratiba
Washiriki hawa wakipitia vipeperushi vya PSPF vyenye taarifa mbalimbali za Mfuko

MWIGULU AKABIDHI AMBULANCE NA KUSISITIZA LISITUMIKE VIBAYA.

$
0
0
Waziri wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Mkoani Singida Mwigulu Nchemba akiwasha gari la kubebea wagonjwa (ambulance), katika kijiji cha Urughu tarafa ya Ndago jimbo la Iramba.
Waziri wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba mkoani Singida Mwigulu Nchemba akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa (ambulance) katika kijiji cha Urughu tarafa ya Ndago jimbo la Iramba.
Mkazi wa kijiji cha Urughu jimbo la Iramba mkoani Singida Jumanne Hatibu akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya gari la kubebea wagonjwa lililotolewa na serikali kupitia wizara ya afya jinsia, wazee na watoto.

…………………………………..

Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Mkoani Singida Mwingulu L. Nchemba, amekabidhi gari la kubebea wagonjwa mpya na la kisasa ambalo limetolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kituo cha afya cha Ndago kilichopo Wilayani Iramba.

Mwigulu ameagiza gari hilo lisitumike kama taksi au gari la kubebea mkaa, bali litumike kwa kazi iliyokusudiwa ambayo ni kubebea wagonjwa na akina mama wajawazito tu.

Mbunge huyo ameyasema hayo juzi wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi ‘ambulance’ hiyo iliyofanyika katika kijiji cha Ndago jimbo la Iramba na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi.

Aidha, amesema ni marufuku wagonjwa kuombwa kuchangia mafuta ya ambulance hiyo au gharama yo yote ile, gari hili wagonjwa walitumie bure.

“Gari hilo lipatikane kituoni wakati wote. Liwe na mafuta ya kutosha na dereva awepo. Gari hili ambalo ni la kisasa, litunzwe na kulindwa ili liweze kutumika kwa miaka mingi ijayo”, alisema Mwigulu.

Mbunge huyo ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya rais Magufuli na waziri Ummy kwa msaada huo ambao utaokoa wapiga kura wake na wananchi kwa ujumla.

Awali mganga mfawidhi wa kituo cha afya cha Ndago, Dkt Lyoce Mgelwa, alisema kituo hicho kinahudumia tarafa nzima ya Ndago yenye wakazi 89,882.

Pia alisema kituo hicho kinapokea wagonjwa wanaopata rufaa katoka kwenye zahanati 10 zilizopo katika tarafa ya Ndago.

Dkt Lyoce alisema msaada huo wa kupatiwa gari la kubeba wagonjwa ambulance, utapunguza kero zinazowakabili wagonjwa wanaopewa rufaa kuchelewa kufika kwa wakati katika hospitali ya wilaya.

“Wagonjwa wanaopewa rufaa watawahishwa hospitali ya wilaya ili kuokoa maisha ya wagonjwa na hasa akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano. Upunguzaji wa vifo hivyo, wilaya itakuwa imepiga hatua kubwa kufikia lengo namba nne na tano la maendeleo ya milenia hadi kufika mwaka 2020”, alisema.

Aidha, Dkt Locye ametumia fursa hiyo kuomba wadau mbalimbali kuwaunga mkono katika kukamilisha jengo lao la kulaza wagonjwa (wodi).

“Wananchi wa jimbo la Iramba, tunaendelea kukushukuru wewe mbunge wetu Mwingulu kwa misaada mingi unayoendelea kuitoa kwenye maeneo mbalimbali katika kuboresha huduma za jamii, ikiwemo huduma muhimu za afya”, alisema.

Kwa upande wake Jumanne Hatibu mkazi wa kijiji cha Urughu tarafa ya Ndago alisema kabla ya ujio wa ambulance hiyo kijiji hicho kilikuwa kinakabiliwa na tatizo sugu la usafiri kwa wagonjwa hasa akina mama wajawazito.

“Kijiji chetu kwa miaka mingi tulikuwa tukitegemea usafiri wa basi na lilikuwepo basi moja tu. Likiondoka asubuhi kwenda Singida hakuna tena usafiri kwa siku husika hadi kesho asubuhi. Kwa hiyo kwa wagonjwa na hasa akina mama wajawazito, ilikuwa ni changamoto kubwa. Ambulance hii, itaokoa maisha ya wakazi wa tarafa ya Ndago na maeneo jirani”, alisema Hatibu ambaye ni mlemavu wa miguu.

Wakati huo huo, Mbunge Mwingulu ameahidi kuchangia ujenzi wa wodi ya kituo cha afya Ndago kwa kutoa mifuko mia moja ya saruji.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAZISHI YA MAREHEMU MZEE FRANCIS MAIGE KANYASU

$
0
0
 Umma unaarifiwa kuwa Serikali imefanya jitihada za kuwatafuta na hatimaye kuwapata  ndugu wa marehemu Mzee Francis Maige Kanyasu (86) anayetajwa kuwa mmoja wa wachoraji wa nembo ya Taifa. Mzee Kanyasu alifariki dunia usiku wa tarehe 29 Mei, 2017 saa mbili na nusu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mwili wa marehemu utaagwa rasmi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kuanzia saa mbili na nusu asubuhi  Jumamosi ya tarehe 3 Juni, 2017 na mara baada ya kuagwa mwili marehemu atasafirishwa na Serikali kwenda kijijini kwao Igokero, Wilaya ya Misungwi kwa ajili ya mazishi.

Taarifa zaidi kuhusu mazishi ya Mzee Kanyasu zitaendelea kutolewa kwa umma kadiri inapobidi.

 Imetolewa na:

Bi. Sihaba S. Nkinga
KATIBU MKUU
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
(MAENDELEO YA JAMII)

Rais wa Zanzibar Dk.Shein akutana na Balozi wa Morocco

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akisalimiana na mgeni wake Balozi wa Morocco katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Abdelilah Benryane wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akizungumza na mgeni wake Balozi wa Morocco katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Abdelilah Benryane wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo. (Picha na Ikulu)

KAMPUNI YA MOOVN DRIVER YAANZISHA HUDUMA YA USAFIRI JIJINI DAR ES SALAAM, NI SALAMA ZAIDI, KUWANUFAISHA MADEREVA WA BAJAJI, PIKIPIKI NA TAX

$
0
0
Moovn Driver Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo,Godwin Ndugulile akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati akizungumzia kampuni yake ya Moovn Driver kuhusu huduma ya usafiri kutumia Aplikesheni waliyoibuni.
Moovn Driver Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo,Godwin Ndugulile akionesha jinsi aplikesheni hiyo inavyofanya kazi mbele ya waandishi wa habari.

................................................................................

TANZANIA inatarajia kunufaika na teknolojia ya kisasa ya usafirishaji ya Moovn Driver, kwa watu wanaohitaji kupiga simu ya mkononi kuhitaji usafiri. Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo,Godwin Ndugulile amesema huduma hiyo itawasaidia madereva wa taksi, pikipiki na bajaji nchi kufanya biashara kwa wakati na kukuza kipato chao na nchi kwa kulipa kodi ikiwa ni pamoja na kufanya huduma hiyo kuwa ya uaslama zaidi. 
 
Amesema mtu atahitaji usafiri wa taxi au bodaboda, bajaji kwa nyakati tofauti ataweza kupata huduma hiyo kupitia teknolojia tuliyoibuni kupitia vijana mainjinia wa masuala ya Teknohama ambao ni watanzani wa hapa hapa nyumbani Tanzania na kupelekwa popote aendapo. Ndugulile amesema kuwa dereva huyo kwa mfumo huo ataonekana kila sehemu atakapokwenda kupitia tekinolojia hii. 
 
Amesema watumiaji satelaiti ambapo abiria atakapo kuwa akiitumia kumtafuta dereva itamuonesha dereva aliyekuwa karibu yake na kuongeza kuwa endapo dereva huyo naye atakuwa akiitumia atapata taarifa kuwa katika eneo Fulani kuna abiria. 
 
Alisema aplikesheni hiyo inapatikana bure kwa wateja wote ili kuweza kutoa huduma nafuu kwa vyombo vya usafirishaji mbalimbali kama taxi bodaboda, na bajaji. Amesema madereva wataongeza kipato, watarahiaisha biashara, usalama dhidi ya mteja aliyempakia, mawasiliano, ripoti ya mapato na malipo ya kirahisi ya kulipwa kwa njia ya mtandao kupitia teknolojia hiyo.

Wakati kampuni nyingine zinamkata dereva asilimia 25 mpaka 45 ya mapato ya siku na haziruhusu kupokea Bakshishi kutoka kwa mteja kampuni hiyo ya Moovn Driver itamkata dereva asilimia 15 tu ya mapato yote ya siku ikiwa ni pamoja na kumruhusu dereva kupokea tipu au (Bakshishi) kutoka kwa mteja.

Kabla ya kuanza kwa huduma hiyo serikali imeshirikishwa ambapo pia Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda Mohamed Mpinga alitaarifiwa kuhusu huduma hiyo ambayo italeta tija na manufaa kwa kupunguza uhalifu, uwezo wa kukusanya kodi sahihi ya mapato ya madereva na kuongeza kipato,ikiwa ni pamoja na kuhakikisha madereva wanafuata sheria na vibali na kurahisisha ajira.

Ameongeza kwa kuwahamasisha madereva kujiunga na huduma hiyo ambayo itakuwa na faida kubwa kwao lakini pia itawafanya kuendesha kazi zao kwa usalama zaidi kwa kuwa watakuwa kwenye mfumo wa Setilaiti hivyo kuimarisha pia usalama wa wateja.

MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE NCHINI (TAA) YAADHIMISHA SIKU YAMAZINGIRA DUNIANI KWAKUFANYA USAFI

$
0
0
MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) imeshiriki kufanya usafi katika maeneo yanayozunguka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku mazingira duniani.

Wafanyakazi wa mamlaka hiyo wameshiriki shughuli hizo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani, ambayo kitaifa inaadhimishwa kesho katika Wilaya ya Butiama, mkoani Mara.

Akizungumza leo wakati wa kufanya usafi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Salim Msangi amesema, ndege za abiria zimekuwa zikizalisha hewa ya ukaa kwa asilimia mbili duniani kote, hivyo ni muhimu kupanda miti maeneo ya viwanja vya ndege ili kutunza mazingira.

Amesema kila mwaka wamekuwa wakipanda miti katika maeneo ya viwanja vya ndege ili kufyonza hewa ya ukaa ambayo kwa kiasi kikubwa inachangia kuharibu mazingira na kuongeza joto.

"Lakini pia nimeagiza mameneja wote kuhakikisha wanapanda na nitakuwa natoa zawadi kila mwaka kwa meneja atakayeonekana kufanya vizuri," amesema Msangi.

Amesema utunzaji wa mazingira ni muhimu kwani binadamu wote na viumbe hai vingine vinahitaji mazingira na kwamba hata kaulimbiu ya kitaifa ya mwaka huu ya “Hifadhi mazingira, Muhimu kwa Tanzania ya Viwanda” haiwezekani kuwa na viwanda katika mazingira ambayo si salama.
 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Salim Msangi wa (kwanza kushoto) akiongoza ufanyaji  katika maeneo yanayozunguka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
 Wafanyakazi wa Mamlaka Viwanja vya Ndege nchini (TAA), wakiendelea na  usafi.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka Viwanja vya Ndege nchini (TAA),Salim Msangi akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA KIKAO CHA MAAFISA WAANDAMIZI, MAKAMANDA WA MIKOA NA VIKOSI WA JESHI LA POLISI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaga baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 20. Picha na IKULU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saini kitabu cha wageni alipowasili kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017. Kushoto ni Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba na Kulia ni Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Simon Sirro
Kwaya ya Polisi ikitumbuiza wakati wa kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 
Sehemu ya wajumbe katika  kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiongea machache wakati wa ufunguzi wa  kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro akitoa muhtasari wakati wa ufunguzi wa kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
Police Brass band wakisiliza hotuba wakisubiri zamu ya kutumbuiza
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
Ukumbi wote ukimsikiliza kwa makini wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
Meza kuu ikimpongeza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
Kamishna wa Jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar Afande Hamdan Omar makame akitoa shukurani kwa niaba ya wote kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar Afande Hamdan Omar makame akipeana mikono na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kumshukuru kwa niaba ya wote kwa kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka ukumbini baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu akipata picha ya pamoja na Makamishna, makamanda wa Wakuu wa Vikosi wa Jeshi la Polisi baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu akipata picha ya pamoja na Makamanda wa Polisi wa mikoa baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu akipata picha ya pamoja na Makamanda wa Vikosi vya  Polisi baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu akipata picha ya pamoja na Makamanda wa Vikosi vya  Polisi baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017

Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images