Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1255 | 1256 | (Page 1257) | 1258 | 1259 | .... | 1898 | newer

  0 0  Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) imekutana na wadau wa huduma ya maji kujadili rasmu ya Mkataba wa Huduma Kwa Wateja ambapo mkataba utakaopitishwa na wadau utaanza kutumika kuanzia Julai Mosi ,2017.

  Warsha ya kujadili mkataba wa huduma kwa wateja imefanyika leo Jumatani June 1,2017 katika ukumbi wa Vijana Center Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro.

  Akizungumza katika warsha hiyo,Matiro aliwataka wadau wa maji kujadili rasmu hiyo kwa umakini zaidi ili kuweka mambo ya msingi ambayo yatapunguza malalamiko kutoka wateja ikiwemo ongezeko la bei ya maji kwa watumiaji wa majumbani.

  Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Reuben Mwandumbya alisema kutokana mamlaka hiyo kuwajali wateja wake imeona ni vyema kukutana na wadau ili kujadili mkataba mpya wa huduma kwa wateja.
   
  “Mkataba uliokuwepo umemaliza muda wake hivyo tumeleta kwenu rasmu ya mkataba ili tujadili kwa pamoja tuweze kuboresha zaidi huduma ya maji kwa wateja wetu”,alieleza Marco

  Miongoni mwa wadau walioshiriki katika warsha hiyo ni meya wa manispaa ya Shinyanga,madiwani,viongozi wa dini,viongozi wa taasisi mbalimbali,watendaji wa kata,wenyeviti wa serikali za mitaa,waandishi wa habari na wadau mbalimbali.

  Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufungua warsha/kikao cha kujadili rasmu ya huduma kwa wateja

  Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akizungumza katika warsha hiyo.Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA,Deogratius Sulla,kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Reuben Mwandumbya

  Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga ,Josephine Matiro akizungumza katika warsha ya wadau wa maji manispaa ya Shinyanga

  Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga ,Josephine Matiro akisisitiza jambo katika warsha hiyo .

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Reuben Mwandumbya akielezea umuhimu wa wadau wa maji kujadili rasmu ya mkataba wa huduma kwa wateja

  Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA,Deogratius Sulla akizungumza ukumbini

  Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Agnes Machiya akizungumza katika warsha hiyo

  Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Agnes Machiya akizungumza

  Afisa Uhusiano wa SHUWASA,Nsianeli Gelard akielezea kuhusu mkataba wa huduma kwa wateja


  Afisa Uhusiano wa SHUWASA,Nsianeli Gelard akiendelea kuelezea kuhusu mkataba wa huduma kwa wateja

  Afisa Rasilimaliwatu na Utawala wa SHUWASA,Kambira Mtebe akifafanua kuhusu mktaba wa huduma kwa wateja

  Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii manispaa ya Shinyanga,Hassan Mwendapole akiongoza majadiliano wakati wa warsha hiyo

  Warsha inaendelea

  Warsha inaendelea
  Diwani wa kata ya Ndembezi (CCM) David Nkulila akichangia hoja katika warsha hiyo

  Diwani wa viti maalum kata ya Shinyanga Mjini,Zenna Gulam (Chadema) akichangia hoja .

  Mchungaji Obeid Jilala ambaye pia ni diwani wa kata ya Lubaga (Chadema) akichangia hoja ukumbini

  Wajumbe wakiwa ukumbini

  Warsha inaendelea

  Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini

  Wajumbe wakiwa ukumbini

  Wadau wakiwa ukumbini


  Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

  0 0


  Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi Shose Kombe kwenye picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani Balozi, Dismas Assenga.
  Raisi wa Jumuiya ya watanzania waishio Houston Marekani Bw. Daudi Mayocha (kushoto) akimshukuru Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi Shose Kombe (kushoto) kwa kuwapelekea huduma za kibenki mijini Houston.
  Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi Shose Kombe (aliyesimama, wapilikushoto) akitoa maelekezo ya jinsi ya kujaza fomu za kujiunga na benki ya KCB kwa baadhi ya watanzania (pichani) wanaoishi katika mji wa Houston.
  Raisi wa jumuiya ya watanzania waishio Dallas Marekani Bw. Ben Kazora (kushoto) akimshukuru Meneja Mahusiano wahuduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi Shose Kombe (kushoto) kwa kuwapelekea huduma za kibenki mjini Dallas.
  Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi. Shose Kombe kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watanzania wanaoishi katika mji wa Dallas. 

   Benki ya KCB Tanzania kupitia dawati lake la Diaspora Banking inafanya ziara katika miji waishio watanzania nchini Marekani. Ziara hii imeanza tarehe 26 Mei na kutegemewa kumalizika tarehe 7 Juni. Miji inayotembelewa ni Washington Dc, Houston, Tx, Dallas, Durham Raleigh, Nc Boston, Ohio, Minnesota Na Chicago. 

  Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya Nchi, Bi. Shose Kombe akizungumza kuhusiana na ziara hii, alisema “Kuna watanzania wengi wanaoishi nje ya nchi na wanahitaji kuwekeza na kupata huduma za kibenki nyumbani wakiwa mbali na Tanzania, hivyo Benki ya KCB inatembelea miji ya Marekani yenye watanzania wengi ili kuwapatia huduma bora kwa haraka, usalama na bila usumbufu”. 

  Huduma za kibenki wanazopatiwa watanzania wanaoishi nje ya nchi ni; akaunti za akiba (savings), akaunti za uwekezaji (Investment), akaunti za wanafunzi, akaunti za watoto na fursa ya kununua nyumba (Mortgage) kwa lengo la kuwawezesha watanzania hao kuendesha shughuli zao za kibenki Tanzania huku wakiwa nje ya nchi na kupata akiba zao pindi watakapo rudi nchini Tanzania. 

  “Huduma hizi za kibenki kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi ni za papo kwa hapo (real time transactions), hivyo kuwawezesha wateja wake kufanya mambo kwa wakati na bila kadhia popote pale walipo duniani” alisema Bi. Kombe. 

  Akizungumza na Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya Nchi, Bi. Kombe na watanzania wanaofanya kazi ubalozini, Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Balozi Dismas Assenga alifuraia ujio wa benki ya KCB nchini Marekani. 

  “Watanzania wanaoishi Marekani wanahitaji sana kuwekeza nyumbani hivyo tutafurahi mkifikia watanzania wote kutoka miji tofauti ya Marekani” alisema Kaimu Balozi. Bi. Kombe alimaliza kwa kuwataka watanzania wanaoishi nje ya nchi na bado hawajajiunga na benki ya KCB kujiunga leo, mteja anahitaji kua na nakala ya Pasi ya kusafiria, Leseni ya udereva au risiti ya huduma za umeme au maji (utility bills).

  0 0  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeridhia ombi la upande wa mashtaka la kutaka ushahidi utakaotolewa na askari polisi kutoka Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kitengo cha kupambana na Ujangili,D 7847 Sajenti Beatus usikilizwe kwa usiri.

  Ushahidi huo ni katika kesi ya  uhujumu uchumi kwa kujihusisha na Meno ya Tembo ya bilioni 13 inayomkabili  raia wa China anayedaiwa kuwa Malkia wa Pembe za Ndovu, Yang Feng Glan (66)na watanzania wawili.

  Mapema wakili wa Serikali Paul Kadushi, aliiomba Mahakama hiyo  ushahidi wa askari huyo ambaye awali alikwishaanza kutoa ushahidi wake kwa uwazi, usikilizwe kwa usiri kwa sababu unahusisha masuala ya amani ndani ya nchi.

  Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alikubaliana na ombi hilo la upande wa mashtaka kusikilizwa kwa usiri.

  Hata hivyo, mmoja wa mawakili wa utetezi, wa Masumbuko Lamwai alilipinga hilo na kudai kuwa hakuna mahusiano juu ya Pembe za Ndovu na amani ya nchi.

  Alidai kuwa, upande wa mashtaka hawakueleza ni kwa namna gani ushahidi wa Pembe za Ndovu utaingiliana na amani na utulivu katika nchi hii.

  Aliongeza kuwa, mtu yoyote anayetuhumiwa kutenda kosa ni haki yake kikatiba,kesi isikilizwe hadharani ili kuhakikisha Haki ionekane imetendeka na umma ujue.

   Aliongeza kuwa kufanya hivyo kunaleta uwezekano wa mtu kuleta ushahidi wa kubambika.

  Alibainisha kuwa upande wa mashtaka haujaweza kutoa sababu kwa nini ushahidi wa shahidi huyo uendelee kusikilizwa kwa usiri wakati ndugu wana Haki ya kujua hii kesi inaendeleaje.

  " Kesi imekuwa kijamii mno, halafu isikilizwe kwa usiri kama mahakama ya kijeshi siyo Haki, mteja wangu amepewa Umalkia wa Pembe za Ndovu huo umalkia uthibitishwe hadharani siyo kisiri siri tunaomba hilo ombi likataliwe." Aliomba Lamwai.

  Kadushi akijibu hoja za Lamwai alidai kuhusiana na hoja ya upande wa mashtaka kutoeleza sababu ni rai yetu kama Jamuhuri itakuwa haina maana tukisema sababu.

  Akitoa uamuzi wake baada ua kusikiliza hoja za pande zote mbili, Hakimu Shaidi amesema upande wa mashtaka haulazimishwi kueleza kile ambacho wanafikiria, sababu Mawakili wa washtakiwa wapo,Lamwai na Nehemiah Nkoko tutajua kwa mini  usikilizwaji wa usiri ufanyike, isikilizwe kwa usiri.

  Baada ya uamuzi huo, watu wote walitolewa nje na kubakia Mawakili wa Serikali, washtakiwa na Mawakili wao.

  Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kwa usiri Juni 9, 2017.

  Manase,  raia wa China anayedaiwa kuwa Malkia wa Pembe za Ndovu, Yang Feng Glan (66) na Salvius Matembo wanakabiliwa na mashtaka ya kujihusisha na biashara ya nyara za serikali kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22,2014 zenye thamani ya Sh 13 bilioni .

  wanadaiwa kufanya biashara ya vipande 706 vya meno ya Tembo vyenye uzito wa kilogramu 1889 zenye thamani ya Sh 5.4 bilioni  bila ya kuwa na leseni iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyama Pori.

  Kwa upande wa Salvius na Manase wanadaiwa kuongoza makosa ya uhujumu uchumi kwa kusaidia biashara ya nyara za serikali kwa kukusanya, Kusafirisha na Kuuza Meno ya Tembo kwa nia ya kujipatia faida.

  Ilidai kuwa Mei 21, 2014 katika eneo la Sinza Palestina wilaya ya Kinondoni mshtakiwa Manase alitoroka chini ya ulinzi halali wa askari wa Jeshi la Polisi D 7847 Koplo Beatus ambaye alikuwa akimshikilia kwa makosa ya kujihusisha na biashara za nyara za serikali.

  0 0


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene 


  Na Mwandishi Wetu, Dodoma

  SERIKALI imeziagiza Halmashauri,Miji na Majiji nchini kutoa kipaumbele cha ajira kwa wahitimu wa chuo Kiongozi cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa(LGTI) ambao mafunzo wanayopata yanalenga kuongeza na kuleta ufanisi katika serikali za mitaa nchini.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amesema hivi karibuni kuwa Chuo Kiongozi cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa (Hombolo) kipo mahusiusi kwa ajiri ya kutoa mafunzo kwa ajili ya wafanyakazi wanaoajiliwa kwenye serikali za mitaaa nchini.

  “Naagiza kunapokuwa na nafasi za kazi kwenye halmashauri, miji na hata majiji ni vyema wahitimu wa chuo hiki wakapewa kipaumbele. Ni vizuri wakapata nafasi ya kushindanishwa na wengine kwani hawa ni walengwa,” alisema Waziri Simbachawene wakati alipokutana na viongozi na wawakilishi wa chuo hicho mjini Dodoma.

  Bila kumung’unya maneno, Waziri Simbachawene alisema wahitimu kutoka chuo Kiongozi cha Serikali za Mitaa ndiyo wabobezi kwenye taaluma za serikali za mitaa na hivyo kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuleta ufanisi zaidi.

  “Ni vizuri tukakumbuka kuwa chuo hiki kilianzishwa na serikali kwa lengo la kuwaandaa wafanyakazi wa kada zote katika serikali za mitaaa,” alisema na kuongeza kuwa serikali itaendelea kukijengea uwezo chuo hicho ili kiweze kutoa wahitimu bora.

  Waziri Simbachawene aliuagiza uongozi wa chuo hicho kutosita kutoa taarifa yeyeto endapo chuo kinapokuwa na upungufu wa watumishi.

  Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Martin Madale alimshukuru Waziri Simbachawene kwa kuwa karibu na chuo na pia kufuatilia maendeleo na ustawi.

  “Kwa niaba ya Bodi, Menejimenti, Wafanyakazi na wanachuo wote wana imani kubwa na uongozi wako kwani umekuwa karibu sana nasi na pia umekuwa msaada mkubwa katika utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazokikabili chuo,” alisema Dkt. Madale.

  Alimwomba waziri kukisaidia chuo kupata kompyuta zaidi, viti na vifaa mbalimbali ilikukabiliana na ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaoomba kujiunga na chuo hicho kwa sasa.

  Naye Rais wa Serikali ya wanachuo, Bw. Kelvin Mbuta alimwomba waziri kusaidia kufikisha ombi la wanachuo serikalini kuhusu mikopo kama wanachuo wa vyuo vingine wanavyopata.

  “Nipo hapa kwa niaba ya wanachuo ambao wameniagiza kilio chao kuhusu mikopo. Tunakuomba Mheshimiwa waziri utusaidie tupate mikopo kwaajili ya kujikimu kwani kuna wachuo wengi wanetoka kwenye familia maskini sana,” alisema.

  Chuo Kiongozi cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa maarufu kama Chuo cha Hombolo kina wanachuo zaidi ya 3,000 ambao wapo katika Kampasi Kuu ya Hombolo ambayo ipo pembeni kidogo mwa Mji wa Dodoma na ile Kampasi ya Mjini.

  Chuo kinatoa programu sita za Stashahada (Diplomas) na program sita za Cheti(Certificates) katika Usimamizi wa Raslimali Watu (Human Resource Management), Serikali za Mitaa na Utawala(Local Government and Administration)Uhasibu na Usimamizi wa Fedha Serikali za Mitaa(Local Government Accounting and Finance),Usimamizi wa Kumbukumbu na Nyaraka(Records and Archive Management),Manunuzi (Procurement)na Maendeleo ya Jamii (Community Development).
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. George Simbachawene akisalimiana na Rais wa Serikali ya Wanachuo Chuo Kiongozi cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa (Hombolo), Bw. Kelvin Mbuta hivi karibuni mjini Dodoma. Pembeni ni Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Martin Madale. 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. George Simbachawene akizungumza na Uongoza na Wawakilishi wa Serikali ya Wanachuo ya Chuo Kiongozi cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa (Hombolo)mjini Dodoma hivi karibuni.

  0 0

   Mwanasheria wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Oscar Mangula akiwasilisha mada inayohusu Sheria mpya ya Takwimu ya mwaka 2015 wakati wa mafunzo kwa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini yaliyofanyika leo mkoani Morogoro kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuifahamu Sheria mpya ya Takwimu ya mwaka 2015.
   Meneja wa Idara ya Mbinu za kitakwimu, Viwango na Uratibu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Emilian Karugendo akitoa ufafanuzi wa namna Ofisi ya Taifa ya Takwimu inavyokusanya takwimu rasmi nchini kwa kuzingatia kanuni za kitaifa na kimataifa wakati wa mafunzo kwa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini yaliyofanyika leo mkoani Morogoro kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuifahamu Sheria mpya ya Takwimu ya mwaka 2015.
   Baadhi ya Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakifuatilia uwasilishwaji wa mada wakati wa mafunzo kwa Maafisa hao yaliyofanyika leo mkoani Morogoro kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuifahamu Sheria mpya ya Takwimu ya mwaka 2015.
  Baadhi ya Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakifuatilia uwasilishwaji wa mada wakati wa mafunzo kwa Maafisa hao yaliyofanyika leo mkoani Morogoro kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuifahamu Sheria mpya ya Takwimu ya mwaka 2015.

  Na: Emmanuel Ghula
  OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetoa mafunzo kwa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini leo mkoani Morogoro kuhusu Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 ili kuwajengea uwezo wa kufahamu namna sheria hiyo inavyofanya kazi.

  Akifafanua sheria hiyo, Mwanasheria wa NBS, Oscar Mangula amesema sheria ya Takwimu No. 9 ya mwaka 2015 imeipa Ofisi ya Taifa ya Takwimu jukumu la kuratibu na kusimamia ukusanyaji wa takwimu rasmi nchini.

  “Sheria ya Takwimu No. 9 ya mwaka 2015 ni sheria inayoipa NBS jukumu la kuratibu na kusimamia shughuli zote za upatikanaji wa takwimu rasmi nchini. Hivyo, kama taasisi yoyote inataka kufanya utafiti kwa minajili ya kutoa takwimu rasmi ni lazima iwasiliane na NBS ili kupata miongozo ya ukusanyaji wa takwimu rasmi,” amesema Mangula.

  Mangula amesema kuwa, ni kosa kisheria kwa mtu yeyote ama taasisi kuendesha utafiti na kuchapisha au kutoa takwimu rasmi bila kuwasiliana na NBS kwani inaweza kukusanya takwimu ambazo hazina ubora na zinazoweza kupotosha umma.

  Aidha, Meneja wa Takwimu za Kodi kutoka NBS Fred Matola amesema NBS hutoa takwimu rasmi kwa kuzingatia miongozo ya kitaifa na kimataifa inayotolewa na Umoja wa Mataifa ili kukidhi mahitaji ya nchi pamoja na kutumika kimataifa.

  “Takwimu rasmi zinakusanywa kwa kuzingatia miongozo inayotolewa na umoja wa kimataifa ili kukidhi mahitaji ya nchi, hivyo NBS ina wajibu kisheria kusimamia upatikanaji wa takwimu rasmi nchini”, amesisitiza Matola.  

  Ofisi ya Taifa ya Takwimu ina jukumu la kuratibu na kusimamia ukusanyaji, uchambuzi na upatikanaji wa takwimu rasmi nchini.

  0 0

  Na Zainab Nyamka,Globu ya jamii.

  Mchezaji wa Zamani wa timu ya Everton ya Nchini Uingereza Leon Osman azindua programu ya timu za vijana nchini itakayosimamiwa na timu hiyo uzinduzi uliofanyika leo Jijini Dar es salaam.

  Osman aliyekuwa ameambatana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe walizindua programu hiyo kwa vijana wadogo ambapo itakuwa endelevu hapa nchini.

  Akizungumza na watoto kutoka katika vituo mbalimbali vya kukuzia vipaji vya soka Osman amewataka kujituma zaidi ili waweze kufikia malengo yao.

  Osman amewapatia zawadi ya mipira  vijana hao waliokuja na kuonyeshwa kufurahia namna wanavyojituma na kuonyesha vipaji vyao.
  Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe akiwa ameongozana na mchezaji wa zaman wa Everton Leon Osman (wa pili kulia) sambamba na Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara Yusuph Singo (kulia) na Mkurugenzi wa Timu ya Everton Robert Elstone leo Jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe akiwa ameongozana na mchezaji wa zamani wa Everton Leon Osman (anayewasalimia vijana ) sambamba na Mkurugenzi wa Timu ya Everton Robert Elstone leo Jijini Dar es salaam.
  Mchezaji wa zamani wa Everton Leon Osman akiwa uwanjani na baadhi ya vijana akiwapa maelekezo mbalimbali.
   Mchezaji wa zamani wa Everton Leon Osman  akitoa zawadi ya mipira kwa vijana waliojitokeza katika uzinduzi wa programu hiyo itakayokuw aendelelevu chini ya Timu ya Everton.
  Mchezaji wa zamani wa Everton Leon Osman akiwa katika picha ya pamoja na vijana kutoka vituo mbalimbali pamoja na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe na Mkurugenzi wa Timu ya Everton Robert Elstone.

  Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe akiwa na mchezaji wa zaman wa Everton leon Osman (wa kwanza kushoto) sambamba na Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara Yusuph Singo (kulia) na Mkurugenzi wa Timu ya Everton Robert Elstone (wanne kulia) na Mkurugenzi wa SportPesa Pavel Slavkov na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Sportpesa Tanzani Abbas Tarimba.

  0 0

   ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akihutubia baada ya wakati wa kutembelea Kituo cha Kutunzia Taarifa (Data centre) na na  kuzindua Mfumo wa Ukusanyaji Mapato wa Serikali kwa Njia ya kielektronini  kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akihutubia katika Kituo cha Kutunzia Taarifa (Data centre) wakati wa kuzindua Mfumo wa Ukusanyaji Mapato wa Serikali kwa Njia ya kielektronini  kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine akitoka kutembelea kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kabla ya kuzindua  Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akisalimiana na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika la simu Tanzania TTCL Bw. Waziri Kindamba wakati wa kutembelea Kituo cha Kutunzia Taarifa (Data centre)  na  kuzindua Mfumo wa Ukusanyaji Mapato wa Serikali kwa Njia ya kielektronini  kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akisalimiana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Bw. Joseph Kichere wakati wa kutembelea Kituo cha Kutunzia Taarifa (Data centre)  na  kuzindua Mfumo wa Ukusanyaji Mapato wa Serikali kwa Njia ya kielektronini  kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akionesha Ipad maalumu aliyopewa ili kumuwezesha  kufuatilia ukusanyaji wa mapato ya kila siku. Kulia kwake ni  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na kushoto kwake ni  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakati wa  kutembelea kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kabla ya kuzindua  Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein  akionesha Ipad maalumu aliyopewa kumuwezesha  kufuatilia ukusanyaji wa mapato ya kila siku. kushoto kwake ni  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakati wa  kutembelea kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kabla ya kuzindua  Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
   Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akionesha Ipad maalumu itayomuwezesha kufuatilia ukusanyaji wa mapato ya kila siku. Kulia kwake ni  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein na viongozi wengine wakati wa  kutembelea kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kabla ya kuzindua  Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akishuhudiwa  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine akizindua  Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi katika picha ya pamoja na wakuu wa makampuni ya mawasiliano mbalimbali nchini kwenye sherehe ya uzinduzi wa Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi katika picha ya pamoja na wakuu wa Mabenki mbalimbali nchini sherehe ya uzinduzi wa Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu


  0 0

  Wachezaji wa Taifa Stars wakipasha joto miili yao kabla ya kuanza mazoezi ya nguvu kwenye Uwanja wa Tolip Sports City jijini Alexandria leo asubuhi Juni 01, 2017. Taifa Stars  inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.
   Makipa wa Taifa Stars kutoka kushoto, Said Mohammed, Aishi Manula na Benno Kakolanya wakivuta pumzi baada ya mazoezi ya timu ya Tanzania ya Mpira wa Miguu ‘Taifa Stars’ yaliyofanyika jana usiku kwenye Uwanja wa Tolip Sports City jijini Alexandria jana usiku Mei 31, 2017. Taifa Stars  inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.
  Daktari wa Viungo wa Taifa Stars, Dk. Gilbert Kigadye akimfanyisha mazoezi ya kifundo cha mguu beki wa timu hiyo, Mohammed Hussein Zimbwe maarufu kama Tshabalala katika mazoezi ya timu ya Tanzania ya Mpira wa Miguu ‘Taifa Stars’ yaliyofanyika Uwanja wa Tolip Sports City jijini Alexandria jana usiku Mei 31, 2017. 
   Wachezaji wa Stars wakiwania mpira katika mazoezi ya nguvu yaliyofanyika leo. Taifa Stars inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.


   Wachezaji wa Stars kutoka kushoto, Mohammed Hussein, Simon Msuva, Said Mohammed, Ibrahim Ajib na Hassan Kessy wakionyesha faraja yao mara baada mazoezi ya nguvu yaliyofanyika leo. Taifa Stars  inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.

  0 0

  Wachezaji wa Taifa Stars wakipasha joto miili yao kabla ya kuanza mazoezi ya nguvu kwenye Uwanja wa Tolip Sports City jijini Alexandria leo asubuhi Juni 01, 2017. Taifa Stars  inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.
   Makipa wa Taifa Stars kutoka kushoto, Said Mohammed, Aishi Manula na Benno Kakolanya wakivuta pumzi baada ya mazoezi ya timu ya Tanzania ya Mpira wa Miguu ‘Taifa Stars’ yaliyofanyika jana usiku kwenye Uwanja wa Tolip Sports City jijini Alexandria jana usiku Mei 31, 2017. Taifa Stars  inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.
  Daktari wa Viungo wa Taifa Stars, Dk. Gilbert Kigadye akimfanyisha mazoezi ya kifundo cha mguu beki wa timu hiyo, Mohammed Hussein Zimbwe maarufu kama Tshabalala katika mazoezi ya timu ya Tanzania ya Mpira wa Miguu ‘Taifa Stars’ yaliyofanyika Uwanja wa Tolip Sports City jijini Alexandria jana usiku Mei 31, 2017. 
   Wachezaji wa Stars wakiwania mpira katika mazoezi ya nguvu yaliyofanyika leo. Taifa Stars inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.


   Wachezaji wa Stars kutoka kushoto, Mohammed Hussein, Simon Msuva, Said Mohammed, Ibrahim Ajib na Hassan Kessy wakionyesha faraja yao mara baada mazoezi ya nguvu yaliyofanyika leo. Taifa Stars  inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.

  0 0

  Wachezaji wa Taifa Stars wakipasha joto miili yao kabla ya kuanza mazoezi ya nguvu kwenye Uwanja wa Tolip Sports City jijini Alexandria leo asubuhi Juni 01, 2017. Taifa Stars  inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.
   Makipa wa Taifa Stars kutoka kushoto, Said Mohammed, Aishi Manula na Benno Kakolanya wakivuta pumzi baada ya mazoezi ya timu ya Tanzania ya Mpira wa Miguu ‘Taifa Stars’ yaliyofanyika jana usiku kwenye Uwanja wa Tolip Sports City jijini Alexandria jana usiku Mei 31, 2017. Taifa Stars  inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.
  Daktari wa Viungo wa Taifa Stars, Dk. Gilbert Kigadye akimfanyisha mazoezi ya kifundo cha mguu beki wa timu hiyo, Mohammed Hussein Zimbwe maarufu kama Tshabalala katika mazoezi ya timu ya Tanzania ya Mpira wa Miguu ‘Taifa Stars’ yaliyofanyika Uwanja wa Tolip Sports City jijini Alexandria jana usiku Mei 31, 2017. 
   Wachezaji wa Stars wakiwania mpira katika mazoezi ya nguvu yaliyofanyika leo. Taifa Stars inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.


   Wachezaji wa Stars kutoka kushoto, Mohammed Hussein, Simon Msuva, Said Mohammed, Ibrahim Ajib na Hassan Kessy wakionyesha faraja yao mara baada mazoezi ya nguvu yaliyofanyika leo. Taifa Stars  inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.

  0 0

  Wachezaji wa Taifa Stars wakipasha joto miili yao kabla ya kuanza mazoezi ya nguvu kwenye Uwanja wa Tolip Sports City jijini Alexandria leo asubuhi Juni 01, 2017. Taifa Stars  inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.
   Makipa wa Taifa Stars kutoka kushoto, Said Mohammed, Aishi Manula na Benno Kakolanya wakivuta pumzi baada ya mazoezi ya timu ya Tanzania ya Mpira wa Miguu ‘Taifa Stars’ yaliyofanyika jana usiku kwenye Uwanja wa Tolip Sports City jijini Alexandria jana usiku Mei 31, 2017. Taifa Stars  inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.
  Daktari wa Viungo wa Taifa Stars, Dk. Gilbert Kigadye akimfanyisha mazoezi ya kifundo cha mguu beki wa timu hiyo, Mohammed Hussein Zimbwe maarufu kama Tshabalala katika mazoezi ya timu ya Tanzania ya Mpira wa Miguu ‘Taifa Stars’ yaliyofanyika Uwanja wa Tolip Sports City jijini Alexandria jana usiku Mei 31, 2017. 
   Wachezaji wa Stars wakiwania mpira katika mazoezi ya nguvu yaliyofanyika leo. Taifa Stars inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.


   Wachezaji wa Stars kutoka kushoto, Mohammed Hussein, Simon Msuva, Said Mohammed, Ibrahim Ajib na Hassan Kessy wakionyesha faraja yao mara baada mazoezi ya nguvu yaliyofanyika leo. Taifa Stars  inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  Tatizo la ugonjwa   wa macho katika nchi ni kubwa ambalo linachangiwa kwa kukosa rasilimali watu pamoja na vifaa vya kisasa katika kutatua changamoto hiyo.

  Akizungumza katika kikao cha wadau wanaoshughulika na masuala ya macho kilichoandaliwa na Sightsavers , Kaimu Meneja wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Macho wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto, Dk. Bernadetha Shilio amesema tatizo la macho ni dogo katika nchi lakini kutokana na kukosa kwa rasilimali watu pamoja na vifaa vya kufanyia oparesheni linafanya tatizo kuwa kubwa.

  Amesema kutokana na tatizo la ugonjwa wa macho kuwa kubwa wameandaa mikakati ya kutatua,ikiwemo kuongeza rasilimali watu pamoja na vitendea kazi kwa ajili ya kufanyia operesheni.

  Dkt.Bernadetha amesema kuwa kuna ushirikiano na mashirika mbalimbali katika yanayosaidia kutoa huduma ya ugonjwa wa macho katika sehemu mbalimbali nchini.Mkurugenzi Mkazi wa Sightsavers, Gosbart Katuzi amesema kuwa tatizo la ugonjwa wa macho unatokana na kitoto cha jicho na kufanya wengine kupofoka.

  Amesema kuwa katika mradi mwaka 2009 walipeleka vifaa katika mkoa morogoro ambapo katika kliniki hiyo zaidi watu 12000 walibainika kuwa na ugonjwa wa macho.Katuzi amesema kuwa kwa sasa ya watu milioni moja wana matatizo ya macho hali hiyo jitihada zinatakiwa kufanyika katika kuifikia idadi hiyo ambayo itakuwa ikiongezeka kwa kila mwaka.

  Mkurugenzi wa Help Age International, Smart Daniel amesema ugonjwa wa macho umekuwa ukiwakumba wazee ambapo hushindwa kufanya kazi zao kutokana na ugonjwa wa macho.

  Amesema kuwa kuna jitihada ambazo zimekuwa zikifanyika katika  kuwafikia wenye ugonjwa macho na watu wengine kwa kufanyiwa oparesheni.
  Kaimu Meneja wa Mapngo wa Taifa wa Huduma za Macho wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto, Dk. Bernadetha Shilio akizungumza katika kikao juu wadau wanashughulika na ugonjwa wa macho leo jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Sightsavers, Caroline Harper akizungumza juu ya taasisi hiyo ilivyoweza kusaidia maeneo mbalimbali nchini kwa watu wenye ugonjwa macho leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Help Age International, Smart Daniel akizungumza katika mkutano wa wadau wanaoshughulika na ugonjwa macho juu ya wazee walivyokuwa wahanga wa ugonjwa huo leo jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mahusiano na Masoko wa Standard Chartered ,Juanita Mramba akizungumza juu ya utoaji wa msaada wa benki hiyo kwa watu wenye ugonjwa wa macho leo jijini Dar es Salaam
  Wadau wa wanaoshulika na ugonjwa wa macho wakiwa katika picha pamoja leo jijini Dar es Salaam.

  0 0


  0 0


  Meneja miradi wa kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Ltd Hassan Swedi akimpa maziwa mlemavu

  Wanafunzi wa shule ya msingi JJ Mungai wakipewa maziwa ya Asas Dairies Ltd leo
  Wafanyakazi wa kampuni ya maziwa ya Asas wakigawa maziwa kwa wanafunzi

  Wanafunzi wa shule ya Msingi Ipogolo wakichukua maziwa

  wanafunzi wakichukua maziwa
  leo siku ya unywaji maziwa duniani
  Wanafunzi wakipewa maziwa kutoka kampuni ya Asas ya mkoani Iringa leo

  Walimu wa shule ya Msingi JJ Mungai wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wwao baada ya kupewa mgao wa maziwa leo

  Wanafunzi wa shule ya Msingi JJ Mungai Iringa mjini wakifurahia maziwa


  wafanyakazi wa kampuni ya Asas wakigawa maziwa kwa wanafunzi leo siku ya unywaji maziwa duniani

  Na MatukiodaimaBlog

  WAKATI leo ni siku ya unywaji maziwa duniani kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Limited imenywesha maziwa wanafunzi zaidi ya 4000 wa shule mbali mbali za Manispaa ya Iringa .

  Shule hizo za msingi zilizopo kanda ya Ruaha ambazo zimeanza kunufaika na unywaji maziwa ,huku walimu wao wakidai baadhi ya wanafunzi wa shule hizo wamekuwa na matokeo mabaya katika mitihani kutokana na unywaji wa pombe ya kienyeji aina ya ulanzi .

  Meneja wa miradi wa kampuni ya Asas Dairies Ltd Hassan Swedi alisema kuwa maadhimisha ya mwaka huu yamelenga zaidi vijana hasa wanafunzi wa shule za msingi mjini Iringa na ndio sababu kampuni yake imelazimika kutoa msaada wa maziwa na majaketi kwa wanafunzi wanaotoka katika familia duni .

  Alisema kuwa kampuni hiyo inaamini kuwa iwapo shule zitaweka utaratibu wa kutoa maziwa kwa wanafunzi afya za wanafunzi hao zitakuwa bora na kiwango cha elimu kinaweza kuongezeka zaidi mashuleni.

  Mbali ya unywaji wa maziwa kuhamasishwa zaidi mashuleni bado viongozi wa serikali wanapaswa kuanza kuhamasha unywaji wa maziwa katika ofisi hizo za umma badala ya kutumia maziwa kutoka nje ya nchi .
  Alisema kuwa kampuni ya Asas Dairies

  Ltd imeendelea kuunga mkono mpango wa lishe mashuleni kama njia ya kuboresha afya na uwezo wa wanafunzi kufanya vizuri kwenye masomo Iringa unazalisha maziwa zaidi ya lita milioni 14 kwa mwaka ila bado kiwanda cha Asas kinasindika lita 400,000 pekee kwa siku .

  Hata hivyo alisema suala la lishe bado ni kikwazo katika mkoa wa Iringa baada ya mkoa huo kuwa mkoa wa pili kwa utapiamlo kitaifa .

  Hivyo alitaka jamii ya wakazi wa mkoa wa Iringa kujenga utamaduni wa kutumia maziwa ili kuongeza lishe na kuwa na afya njema.


  Alisema kuwa mkoa wa Iringa umejipanga kuendelea kuboresha upatikanaji wa maziwa mashuleni kwa kushirikisha wafugaji kama njia ya kukomesha utapiamlo mkubwa mashuleni.


  Kwani alisema kuwa mkoa wa Iringa unapaswa kuondokana na aibu ya utapiamlo kwa watoto na kuwataka wananchi sasa kuanza kuongeza ufugaji wa ng’ombe za maziwa kupitia mradi wa kopa ng’ombe lipa ng’ombe.

  Hata hivyo alipongeza jitihada za kampuni ya maziwa ya Asas kwa kuendelea kuhamasisha unywaji wa maziwa na kuitaka jamii na mkoa wa Iringa kuachana na unywaji wa pombe na badala yake kunywa maziwa zaidi.

  Alisema kuwa mbali ya wanafunzi wa Manispaa ya Iringa kupewa maziwa pia kampuni hiyo imeendesha zoezi kama hilo mkoani Kigoma .

  Mwalimu mkuu msaidizi shule ya Msingi Ipogolo Makrina Mpogole pamoja na kushukuru kampuni ya Asas kwa kutoa maziwa kwa wanafunzi wote shuleni kwake bado alisema kampuni hiyo imetoa msaada wa majacketi kwa wanafunzi wanaotoka familia zisizo na uwezo .

  Mwalimu Mpogole alisema kuwa bado wanaomba wazazi kuangalia uwezekano wa kuwawezesha watoto wao kupata japo paketi moja ya maziwa fresh pindi wanapokwenda shule badala ya wanafunzi hao baadhi yao kunywa pombe aina ya ulanzi .

  Alisema matokeo mabovu kwa baadhi ya wanafunzi yanachangiwa na tabia ya kunywa ulanzi wakiwa mitaaani hivyo iwapo watapewa maziwa yatawasaidia kuongeza afya na kuwa na uwezo zaidi katika masomo .

  Wakati mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi JJ Mungai Haji Mpakati alisema kuwa iwapo utaratibu wa wanafunzi kupewa lishe unaweza kupunguza kiwango cha udumavu na utapiamlo kwa wanafunzi mashule.TAZAMA VIDEO HAPA CHINI


  0 0
 • 06/01/17--08:21: Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk. Tulia Ackson akijibu miongozo mbalimbali ya wabunge mara baada ya kumaliza kipindi cha Maswali ya Kawaida katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 01, 2017. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijibu maswali ya papo kwa papo mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017. Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe.George Simbachawene katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017. Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017. Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017. aziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akisoma Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Hussein Mwinyi akizungumza jambo na Mbunge wa Viti Maalum(CHADEMA) Mhe.Catherine Ruge katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma June 1, 2017. Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe.Anna Mollel akiuliza swali katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kantui kutoka Kilosa wakiwa Bungeni kujifunza Shughuli mbalimbali katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017. Wabunge wakifuatilia hoja mbalimbali katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017. Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO, DODOMA.
 •   Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk. Tulia Ackson akijibu miongozo mbalimbali ya wabunge mara baada ya kumaliza kipindi cha Maswali ya Kawaida katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 01, 2017.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijibu maswali ya papo kwa papo mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017.
   Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe.George Simbachawene katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017.
   Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017.
   Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017.
   aziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akisoma Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017.
   Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Hussein Mwinyi akizungumza jambo na Mbunge wa Viti Maalum(CHADEMA) Mhe.Catherine Ruge katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma June 1, 2017.
   Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe.Anna Mollel akiuliza swali katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017
   Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kantui kutoka Kilosa wakiwa Bungeni kujifunza Shughuli mbalimbali katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017.
   Wabunge wakifuatilia hoja mbalimbali katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017.
  Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO, DODOMA.

  0 0

  Frank Mvungi-Maelezo
  Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali imedhamiria  kuimarisha Ofisi za Kanda ili kusogeza huduma kwa wananchi katika Mikoa yote, ikiwa ni katika juhudi zake za kuimarisha utendaji na kuongeza tija na uwajibikaji.

  Kauli hiyo imetolewa  leo Jijini Dar es Salaam na Meneja Mawasiliano na Masoko wa Ofisi hiyo Bw. Cletus Mnzava ,alipozungumza na waandishi wa  habari juu ya   majukumu ya Ofisi hiyo na huduma zinazotolewa.

  “Mwelekeo ni kuimarisha Ofisi zetu za Kanda ili kusogeza huduma karibu  kwa wananchi, kwa sasa tunaendelea kuimarisha Ofisi ya Dodoma kama Makao Makuu ya Nchi ambayo pia itahudumia Mikoa ya Iringa,Morogoro na Singida” Alisisitiza Mnzava.

  Akifafanua Mnzava alisema Ofisi hiyo imejipanga kuendana na sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga Tanzania ya Viwanda  kwa sababu viwanda vitakuwepo kila kona ya nchi na viwanda vinatumia kemikali hivyo vinatakiwa vifuatiliwe kwa ukaribu ili matumizi yafanyike kwa mujibu wa Sheria na taratibu zilizowekwa.

  Aliongeza kuwa moja ya mikakati ya Ofisi hiyo ni kuwepo kwa watumishi wanaodhibiti uingizwaji wa kemikali usiofuata taratibu ambapo wakaguzi hao kwa sasa wako katika mipaka ya Namanga,Holili na Horohoro kwa upande wa kanda ya Kaskazini.

  Kwa upande wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wakaguzi hao wako katika mipaka ya Tunduma,Kasumulu na Mutukula ,Sirari kwa upande wa Kanda ya Ziwa ambapo mpango mkakati wa Ofisi hiyo ni kuhakikisha kuwa Lengo la Serikali kusogeza huduma karibu na wananchi linatimia.

  Kwa upande wake Meneja wa Ukaguzi wa Kemikali Bw. Fidelis Segumba amesema Maabara hiyo imejipanga kuwahudumia wananchi vizuri nyakati zote.
  Meneja Mawasiliano na Masoko wa kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw. Cletus Mnzava akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu uimarishaji wa Ofisi za Kanda ili kusogeza huduma karibu na wananchi. Kushoto ni Afisa Habari wa Ofisi hiyo Bw. Sylivesta Omari.
  Meneja ukaguzi wa Kemikali Bw. Fidelis Segumba akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.kulia ni Meneja Mawasiliano na Masoko wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw. Cletus Mnzava (Picha na Frank Mvungi-Maelezo)

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh. Christopher Ole Sendeka akiweka jiwe la msingi kwenye  nyumba za waalimu shule ya sekondari ya wasichana Anne Makinda.Nyumba zenye uwezo wa kuishi waalimu 6 katika nyumba moja "6 in 1".
  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akikagua uimara wa milango kwenye moja ya madarasa katika shule ya sekondari ya wasichana Anne Makinda.Nyuma yake ni Mh. Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri.
  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akisisitiza jambo kwa Wananchi (hawapo pichani)  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Luponde mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye jengo la OPD  kituo cha afya Luponde wa kwanza kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Edwin Mwanzinga
  Wananchi wa Kijiji cha Luponde wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa katika mkutano wa hadhara
  Mkuu wa Mkoa wa Njombe akiwa katika Picha ya pamoja na uongozi wa wanafunzi shule ya sekondari ya wasichana Anne Makinda,Shule hiyo ya Kata ilifanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne mwaka jana na kushika nafasi ya Tano Kimkoa na Nafasi ya Kwanza Kiwilaya.

  0 0

  Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Anne Makinda akiwahamasisha Madiwani wanawake wa Jiji la Dar es Salaam walioudhuria mafunzo  ya uongozi, jinsia na bajeti yenye mlengo wa kijinsia pamoja na kutoa uzoefu wake kwenye maswala ya uongozi  kwa wanawake hasa ngazi za juu leo kwenye ukumbi wa TGNP Mtandano jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi Lilian Liundi akizungumza na Madiwani Wanawake kuhusu nguvu ya mwanamke kwenye  jamii  pamoja na kuwapa miongozo kuhusu nafasi zao kwenye uongozi ili kufikia lengo la hamsini kwa hamsini.

  Mwanachama wa TGNP Mtandao na mkufunzi wa Mafunzo ya Madiwani wanawake wa Jiji la Dar Es Salaam Profesa Ruth Meena akiwasilisha  mada kuhusu kujitambua kwa mwanamke kwenye jamii, kujua thamani yake pamoja na mchango wake kwenye jamii katika mafunzo yaliyofanyika kwenye ukumbiwa TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Idara ya Ijenzi wa Nguvu Pamoja wa TGNP Mtandao, Grace Kisetu akizungumza jambo kwenye mafunzo ya madiwani wanawake wa Jiji la Dar es Salaam leo
  Madiwani wanawake wa Jiji la Dar es Salaam wakiwa kwenye mafunzo ya uongozi, jinsia na bajeti yenye mlengo wa kijinsia leo kwenye ukumbi wa TGNP Mtandano.
  Mkutano ukiendelea
  Mwenyekiti wa Muda wa Umoja wa Madiwani Wanawake wa Jiji la Dar es Salaam, Bi. Saada  Mandwanga akitoa shukrani kwa TGNP Mtandao kutoa mafunzo ya uongozi, jinsia na bajeti yenye mlengo wa kijinsia ambayo kwao yamekuwa ni chachu kwenye jamii inayowazunguka.
  Baadhi ya wafanyakazi wa TGNP Mtandao wakiwa kwenye mafunzo ya Madiwani wanawake yanayofanyika kwa siku tatu


  Madiwani wanawake wa vyama mbalimbali vya siasa katika Mkoa wa Dar es Salaam wamesema suala la kubadili mtazamo katika ushirikishwaji wa wanawake kwenye maendeleo ni la msingi na linapaswa kutekelezwa kuanzia ngazi za chini. 


  Wakizungumza katika warsha ya siku tatu ya Uongozi wa Kijinsia iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP Mtandao), madiwani hao wamesema haki za wanawake bado zinakandamizwa katika jamii huku vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vikishika kasi.   Akizungumza katika mafunzo ya siku tatu Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Anne Makinda amesema wanawake wanapaswa kuungana kwa pamoja wanapokuwa wanapigania haki zao za msingi. Amewasisitiza kuachana na masuala ya vyama kwenye jambo linalowahusu wanawake wote. Wakifanya hivyo wataweza kupunguza tabaka kubwa kwenye utawala na hata kwenye uzalishaji mali.  Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi Lilian Liundi amesema watoto wa kike wanakosa vipindi vya masomo kutokana na ukosefu wa elimu ya kujihifadhi hasa wanapokuwa katika hedhi. 


  “Elimu ya hedhi bado duni sana, hasa vijijini kwa sababu watoto wengi wa kike wanapokuwa katika hedhi huhisi kwamba ni wagonjwa, hivyo hushindwa kuhudhuria vipindi ipasavyo lazima elimu hii itolewe kwa jamii ili kuwawezesha watoto hawa wapate elimu kama ilivyo kwa wale wa kiume,” alisema Lilian Liundi.

  0 0

   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Balozi Lou Youqing (kulia) kabla ya kuanza ziara ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo iliyopo wilaya ya kongwa Mkoa wa Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Banyibanyi wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo iliyopo wilaya ya kongwa Mkoa wa Dodoma.​
    Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo iliyopo wilaya ya kongwa Mkoa wa Dodoma. kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa Balozi Lou Youqing na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya kongwa, Mheshimiwa Deogratius Ndejembi
   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kulia) akiongozana na Balozi wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa Balozi Lou Youqing wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo iliyopo wilaya ya kongwa Mkoa wa Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati)akitembelea shule ya msingi ya Ibwaga, shule aliyosoma wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo iliyopo wilaya ya kongwa Mkoa wa Dodoma. wa pili kushoto, ni Balozi wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa  Balozi Lou Youqing.

  0 0

   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya WazaziTanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka wilaya za Uvinza, Kigoma Vijijini na Kigoma Mjini, Mabalozi, Watendaji wa Chama na wa Serkali, mjini Kigoma, leo
   Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka wilaya za Uvinza, Kigoma Vijijini na Kigoma Mjini, Mabalozi, Watendaji wa Chama na wa Serkali, mjini Kigoma, wakishangilia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya WazaziTanzania, Alhaj Abdallah Bulembo alipokuwaakizungmza nao katika kikao kilichofanyika Kigoma mjini, leo.
   Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho, 
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya WazaziTanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akisaini kitabu cha wageni bada ya kuwasili meza kuu kuhutubia kikao hicho. Kushoto ni Mjumbe wa NEC kutoka Wilaya ya Uvinza Asha Baraka
   Wajumbe wakiwa ukumbini
   Wajumbe kutoka Uvinza wakishangilia walipotambulishwa
   Baadhi ya madiwani wakishangilia baada ya kutambulishwa
   Maofisa wa Makao Makuu ya Jumuia ya Wazazi, wakisaini vitacbu vya wageni wakati wa kikao hicho
   Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma, Naomi Kapambala akizungumza mwanzoni kwa kikao hicho
   Katibu wa Siasa na Oganaizesheni kutoka Makao Makuu ya Jumuia ya Wazazi Tanzania, Ndugu Mgaya akisalimia baada ya kutambulishwa kwenye kikao hicho
   Wajumbea wakimshangilia Ndigi Mgaya wakti akijitambulisha
   Ofisa kutoka Makao Makuu ya Jumuia ya Wazazi Tanzania akijitambulisha
   Baadhi ya madiwani wakitambulishwa
   Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk Amani Kabirou akifungua kikao hicho. Kulia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya WazaziTanzania, Alhaj Abdallah Bulembo na kushoto mi Mjumbe wa NEC kutoka Uvinza Asha Baraka 
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya WazaziTanzania, Alhaj Abdallah Bulembo, akitaka ufafanuzi wa jambo, kutoka kwa Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma, Naomi Kapambala baada ya kukabidhiwa Taarifa ya Uchaguzi nfani ya Chama, wakati wa kikao hicho
   Afisa Afya wa mkoa wa Kigoma, Ambakisye Mhune akitoa darasa kwa wajumbe wa kikao hicho namna ya kujihami na ugonjwa wa Ebola, ambao alisema, hivi sasa umelipika ena katika nchi jirani ya Congo DRC.
   Mjumbe wa NEC, Kirumbe Ng'enda akifuatiia kwa makini mada hiyo iliyokuwa ikitolwa na mtaalam huyo 
   Mtaalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma akitoa taarifa kuhusu mwenendo wa hali ya uchumi katika mkoa huo
   Wajmbea wakiwa ukumbini
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya WazaziTanzania, Alhaj Abdallah Bulembo, akizungumza na wajumbe kutoka ufafanuzi wa maswala mbalimbali ikiwemo uhaguzi ndani ya Chama, Ndugu Bulembo kabla ya kuzungumza na wajube hao alitawazwa kufalishwavazi la heshima la Waha laaina ya Mpuzu, ambalo ni ishara ya kiongozi makini na mwenye kuheshimika
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya WazaziTanzania, Alhaj Abdallah Bulembo, akizungumza na wajumbe kutoka ufafanuzi wa maswala mbalimbali ikiwemo uhaguzi ndani ya Chama, Ndugu Bulembo kabla ya kuzungumza na wajube hao alitawazwa kufalishwavazi la heshima la Waha laaina ya Mpuzu, ambalo ni ishara ya kiongozi makini na mwenye kuheshimika
   "Hii Katiba ya Chama ndiyo mwongozo wa mambo yote ndani ya CCM,ikiwemo namna ya kuomba uongozi", alisema Bulembo akizungumza na wajumbe hao
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo akiwasomea wajumbe taratibu na kanuni za uchaguzi ndani ya Chama
   Mjumbe wa KamatiKuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akiondoka meza kuu bada ya kikao hicho
   Bulembo akiondoka ukumbini
    
   Bulelbo akiagana na baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya WazaziTanzania, Alhaj Abdallah Bulembo, akimpongeza msoma risala, baada ya kusomewa risala hiyo kabla ya kufungua Shina la Umoja wa Vijana wa CCM, la Dk. John Magufuli 
   Katibu wa CCMmkoa wa Kigoma, NaomiKapambala akimpatia maenelezo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya WazaziTanzania, Alhaj Abdallah Bulembo, kabla ya kuzindua Shna la Imoja wa Vijana wa CCM la Dk. John Magufuli katika eneo la Mwanga mkoani humo leo
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya WazaziTanzania, Alhaj Abdallah Bulembo, akigawa kadi za UVCCM kwa mmoja wa wanachama Wapya kabla ya kuzindua shina hilo
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya WazaziTanzania, Alhaj Abdallah Bulembo, akipandisha bendera ya CCM, kuzidua Shina la Umoja wa Vijana wa CCM a Dk. John Magufuli, kaika eneo la Mwanga mkoani Kigoma, leo
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya WazaziTanzania, Alhaj Abdallah Bulembo, akisoma mandhishi, bada ya kuondoa kitambaa ikiwa ni ishara ya kuzidua Shina la Umoja wa Vijana wa CCM, la Dk John Magufuli katika eneo la Mwangamkoani Kigoma, 
   Shamra shamra kwenye shina hilo baada ya kuzinduliwa
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya WazaziTanzania, Alhaj Abdallah Bulembo, akikabidhi fedha kwa uongozi wa shina hilo, fedha hizo alichangisha kwa wadau waliokuwemo kisha akajazia mwenyewe. PICHA: BASHIR NKOROMO

older | 1 | .... | 1255 | 1256 | (Page 1257) | 1258 | 1259 | .... | 1898 | newer