Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1252 | 1253 | (Page 1254) | 1255 | 1256 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi, Alhaj Abdallah Bulembo akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora leo, kuendelea na ziara yake ya mikoani kukagua na kuimarisha uhai wa chama na Jumuia zake, na pia kuzungumzia masuala ya uchaguzi unaoendelea ndani ya Chama. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Ndugu Wagasubi na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Sikonge Abisa Mbogo. Katibu wa CCM Wilaya ya Sikonge Emmanuel Alex akitoa maneno ya utambulizi kabla ya Ndugu Bulembo kuzungumza na Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo leo. Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi, Alhaj Abdallah Bulembo akifurahi jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Ndugu Wagasubi. Utambulisho. Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wzazi, Aljah Abdallah Bulembo akiwasilikiza viongozi wa CCM wilaya ya Sikonge, wakati wa kikao cha ndani katika Ofisi ya CCM Wilaya hiyo mkoani Tabora leo Kulia ni Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Emmanuel Alex na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Abisa Mbogo Mwenyekti wa CCM Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, Abisa Mbogo akifungua kikao hicho Katibu wa CCM Wilaya ya Sikonge Emmanuel Alex akikabidhi taarifa ya uchaguzi nchani ya Chama kwa Ndugu Bulembo
  Katibu wa CCM Wilaya ya Sikonge Emmanuel Alex akisoma taarifa hiyo Ndugu Bulembo akitoka katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Sikonge, kwa ajili ya kwenda kuongoza kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya, Mabalozi, watendaji wa Seikali na wa Chama Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza katika kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya, Mabalozi, watendaji wa Seikali na wa Chama, leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Ndugu Wagasubi na klia ni Mweneyekiti wa CCM Wilaya ya Sikonge bisa Mbogo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza katika kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya, Mabalozi, watendaji wa Seikali na wa Chama, leo. Katikati ni Mweneyekiti wa CCM Wilaya ya Sikonge Bisa Mbogo na kulia ni Katibu wa CCM Wilaya hiyo Emmanuel Alex
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza katika kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya, Mabalozi, watendaji wa Seikali na wa Chama, leo. Wajumbe ukumbini.Wajumbe Ukumbini. Picha zote na Bashir Nkoromo

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akisalimiana na mgeni wake Balozi wa Namibia katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Theresia Samaria Balozi wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
  1
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akizungumza na mgeni wake  Balozi wa Namibia katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Theresia Samaria Balozi wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
  2
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akifuatana na  mgeni wake  Balozi wa Namibia katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Theresia Samaria Balozi baada ya mazungumzo yao wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.]30/05/2017.

  0 0   
  Afisa Utumishi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Justo Herman akikagua noti halali wakati wa mafunzo yaliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania.1
  Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Singida Patrick Girigo Kasango na Afisa Elimu wa Mkoa wa Singida Florian Kimoro wakionyeshana alama za noti halali wakati wa mafunzo yaliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania.2
  Mwangalizi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida Khadija Hamisi na Mkaguzi wa ndani Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Alfred Kalama wakisikiliza kwa umakini alama zinazopatika katika noti halali wakati wa mafunzo yaliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania.3
   Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida George Kulwa akitoa shukrani kwa niaba ya watumishi wote waliopata mafunzo ya Benki kuu ya Tanzania.4
   Maafisa kutoka Benki Kuu ya Tanzania Rehema Zongo na Rajab Ibrahimu wakisikiliza maswali na kutoa ufafanuzi kwa watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa mara baada ya kutoa mafunzo ya alama za noti halali.5
   Maafisa kutoka Benki Kuu ya Tanzania Rehema Zongo na Rajab Ibrahimu wakisikiliza maswali na kutoa ufafanuzi kwa watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa mara baada ya kutoa mafunzo ya alama za noti halali.
  ……………………
  Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imetoa mafunzo kwa watumishi wote wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida juu ya alama zinazopatikana katika noti halali za fedha ya Tanzania leo asubuhi katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
  Akitoa mafunzo hayo Afisa Kutoka Benki Kuu ya Tanzania Rehema Zongo amewafafanulia watumishi hao namna ya kutambua noti halali kwa vitendo huku akisisitiza alama muhimu zinazopatikana katika noti halali ili waweze kutofautisha na zile bandia.

  Zongo amesema watumishi wanatakiwa kuichunguza noti halali, waipapase ili kuhisi mparuzo kwenye maneno yaliyoandikwa kwa maandishi maalumu mfano maandishi yanayoeleza fedha halali kwa malipo ya shilingi mia tano, elfu moja, elfu mbili, elfu tano na elfu kumi.

  Amewasisitizia kuwa wanaweza kuitambua noti halali kwa kuangalia sura ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere inayoonekana unapoimulika noti kwenye mwanga na pia kukagua utepe maalumu kwenye noti za shilingi 500, 1000, 2000, 5000 na 10,000 unaoonekana kama madirisha yenye umbo la almasi ambapo hubadilika badilika noti inapogeuzwa geuzwa. 

  Zongo ameongeza kuwa watumishi na wananchi wote wanapaswa kuchukua tahadhari kwa kuwa noti bandia zipo mtaani na kuwa hazina thamani yoyote.

  “Ukipata noti bandia au hata kama unaishuku ni bandia, ipeleke benki au kituo chochote cha polisi kilichopo karibu nawe, lakini pia tuwe na utaratibu wa kuthibitisha uhalali wa noti mara uzipatazo kwa kuzingatia alama tulizowafunzisha leo, na pia tunaomba muwe waalimu kwa kuwafundisha wengine alama hizo”, amesema Zongo.

  Amesisitiza kuwa kugushi pamoja na kumiliki fedha bandia kwa nia ya kuzitumia ni kosa la jinai linalosababisha mhusika kushitakiwa kwenye vyombo vya sheria hivyo wanapaswa kuwa makini, kutoa taarifa sahihi na katika sehemu husika, pia kuwa na utaratibu wa kuchunguza noti.

  Kwa upande wake Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida George Kulwa kwa niaba ya watumishi wote waliopata mafunzo hayo ameishukuru Benki kuu ya Tanzania kwa kutoa mafunzo hayo.

  George amesema elimu iliyotolewa kwa watumishi hao ni muhimu na itawasaidia si watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa pekee bali wananchi wote kwa ujumla kwakuwa watumishi hao watakuwa mabalozi wa elimu hiyo.

  Aidha ameiomba benki kuu kuendelea kutoa elimu hiyo mpaka ngazi za vijiji ili taifa lote liwe na elimu sahihi na ya kutosha juu ya alama za noti halali huku akiwakaribisha tena katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa kila mara wanapotaka kutoa elimu yoyote juu ya masuala ya fedha na uchumi wa Tanzania.

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi (Bajeti) ya Wizara yake ya zaidi ya shilingi trilioni 11.757, Bungeni Mjini Dodoma ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2017/2018, kwa mafungu yote 9 yaliyo chini ya Wizara hiyo.

  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi (Bajeti) ya Wizara yake ya zaidi ya shilingi trilioni 11.757, Bungeni Mjini Dodoma ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2017/2018, kwa mafungu yote 9 yaliyo chini ya Wizara hiyo.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi (Bajeti) ya Wizara yake ya zaidi ya shilingi trilioni 11.757, Bungeni Mjini Dodoma ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2017/2018, kwa mafungu yote 9 yaliyo chini ya Wizara hiyo.
  Viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake, wakifuatilia kwa makini Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo, Bungeni Mjini Dodoma, ambapo kiasi cha shilingi trilioni 11.757 kimeombwa ili Wizara hiyo iweze kutekeleza majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa mwaka wa Fedha 2017/2018.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa akimpongeza Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kwa uwasilishaji makini wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, akimpongeza Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kwa uwasilishaji makini wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango, akisalimiana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mhe. Peter Serukamba, mara baada ya Waziri Mpango kuwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni Mjini Dodoma ambapo ameliomba Bunge liidhinishe makadirio ya Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.757 ya Wizara hiyo.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akisalimiana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Juma Assad, kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
  Manaibu Katibu wakuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, na Bi. Dorothy Mwanyika, wakibadilishana mawazo nje ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dododma mara baada ya kuwasilishwa kwa Bajeti ya Wizara hiyo ambapo kiasi cha shilingi trilioni 11.757 zinatarajiwa kukusanywa na kutumiwa na Wizara ya Fedha na Mipango.
  Viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake, wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (wa tano kushoto), nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuwasilishwa kwa Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo. (Picha zote na
  …………………………..

  Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma

  Wizara ya Fedha na Mipango imeliomba Bunge iidhinishie makadirio ya mapato na matumizi (Bajeti) ya zaidi ya shilingi trilioni 11.757 ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2017/2018, kwa mafungu yote 9 yaliyochini ya Wizara hiyo.

  Maombi hayo yametolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizaya hiyo, Bungeni Mjini Dodoma, leo.

  Dkt. Mpango amesema kuwa kati ya fedha hizo, shilingi trilioni 10.328 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 1.429 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

  Amefafanua kuwa Matumizi ya Kawaida yanajumuisha shilingi bilioni 87.996 kwa ajili ya mishahara, shilingi bilioni 778.612 kwa ajili ya matumizi Mengineyo (OC) na shilingi trilioni 9.461 ni kwa ajili ya kulipa Deni la Taifa na Huduma nyingine.

  Aidha, katika fedha za matumizi ya maendeleo, shilingi trilioni 1.382 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 46.108 ni fedha za nje.

  0 0

  Mkulima mmoja Kitangili mkoani Shinyanga Francis Martin Kilalo (31)anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora kukutwa na sare na vifaa vingine vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) ambavyo anatuhumiwa kuvitumia kupateli na kuwadanganya kwa kuchukua fedha kutoka kwa vijana wanaotafuta nafasi ya kujiunga na Jeshi hilo.

  Taarifa hiyo imetolewa jana na Kamanda wa Mkoa wa Tabaora Wilbroad Mtafungwa alipokuwa anaongea na waandishi wa habari Ofisi kwake juu ya hatua mbalimbali walizochukua katika kupambana na uhalifu mkoani humo.

  Alisema kuwa Polisi walifanikiwa kumukamata mtuhumiwa huyo katika Hoteli ya JM iliyopo Wilayani Igunga akiwa na sare mbalimbali za Jeshi la waananchi Tanzania (JWTZ) zikiwa na cheo cha Koplo ambavyo ni pamoja na kofia tatu, begi, sweta, buti jozi moja, magwanda na mikanda mitatu.

  Mali nyingine zilikamatwa kwa mtuhumiwa huyo ni pamoja na fomu za likizo cha likizo , fomu za kujaza vijana wanaotaka kujiunga na Jeshi hilo na Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) kwa mujibu wa Sheria na hiari na mihuli zenye nembo inayofanana na Jeshi hilo.

  Kamanda Mtafungwa alisema kuwa mtuhumiwa alikuwa akitumia nyaraka na sare za Jeshi hilo kuchukua fedha kwa kuwadanganya na kuwatapeli wananchi mbalimbali kwa kudai atawatafutia ajira katika majeshi ya Kujenga Taifa na la Wananchi.

  Kamanda huyo wa Mkoa wa Tabora aliongeza kuwa mtuhimiwa huyo pia alikutwa barua kutoka Serikali za mitaa za Dar es salaam na gari aina ya Toyota Starlet yenye namba za Usajili T633 ARF ambalo wanaendelea kuchunguza uhalali wa umiliki wake na ambalo mtuhumiwa alikuwa akilitumia na kuwafanya baadhi ya wananchi wamuamini kuwa atawasaidia kupata nafasi katika majeshi.

  Aliongeza kuwa mtuhimiwa huyo pia alikuwa na barua za maombi ya watu ya kuomba kujiunga na Jeshi, Fomu za Matibabu za Hospitali ya Jeshi ya Lugalo na nakala ya Vyeti vya kumaliza elimu ya Sekondari vya baadhi ya watu.

  Kufuatia tukio hilo alitoa wito kwa waananchi waliowahi kutapeli ndani na nje ya Mkoa wa Tabora kujitokeza katika vituo vya Polisi ili waweze kutoa ushahidi utakasaidia kuonyesha ni jinsi gani walivyumizwa na mtuhumiwa huyo .

  Kamanda Mtafungwa alisema kuwa Polisi inaendelea kushirikiana na JWTZ ili iweze kubaini sare na vifaa hivyo alivipata wapi , kwa lengo lipi na ni nani aliyompatia ili wahusika wote waweze kufikishwa katika vyombo vya Sheria kwa hatua zaidi.

  Aidha , Kamanda huyo aliwaasa wananchi kuwa makini na matapeli wanaowadai fedha na kuwadanganya kuwa watawatafutia kazi katika Majeshi kwani vyombo hivyo vinaotaratibu wake ambao ndio unaotumika kuwapata vijana wanaojiunga kwa mujibu wa sheria na wale wa hiari na sio kwa kuchangishwa fedha.

  Wakati huo huo Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limefanikiwa kukamata watuhimiwa 17 kwa kukutwa na lita 205.25 za gongo wakati wa msako wa kukamata wa watumiaji na wauzaji wa bidhaa hizo haramu.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora Mtafungwa alisema kuwa watuhimiwa watafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zao wakati wowote.
  Aidha , alisema kuwa katika zoezi hilo pia Polisi ilifanikiwa kuteketeza ekari tano na nusu za mashamba ya zikiwa na uzito wa kilogramu 220 yalikuwa yamelimwa katika Msitu wa Hifadhi wa Igombe wilayani Uyui.

  Alisema kuwa jitihada za kuwasaka watuhumiwa wa mashamba hayo zinaendelea na kuwaomba wananchi wenye taarifa ya walipo wahusika walisaidie Jeshi la Polisi ili wahusika waweze kufikishwa Mahakama kujibu tuhuma zao

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Biko Tanzania Charles Mgeta mwenye miwani akishuhudia katika makabidhiano ya Sh Milioni 10 kwa mshindi wao wa jijini Arusha Leopard Mpande aliyepatikana katika droo ya Jumapili iliyopita. Aliyeshikana mikono na Mpande ni Balozi wa Biko Kajala Masanja.

  WAENDESHAJI wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, jana wamemkabidhi zawadi yake jumla ya Sh Milioni 10 mshindi wao wa jijini Arusha, Leopard Mpande, aliyetangazwa mshindi katika droo ya tisa iliyofanyika Jumapili, jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Biko, Charles Mgeta, alisema Mpenda ni mshindi akitokea jijini Arusha, baada ya kuamua kucheza bahati nasibu ya Biko.
  Mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko jijini Arusha, Leopard Mpande wa tatu kutoka kushoto akipokea nyaraka na fedha zake baada ya kukabidhiwa kutokana na ushindi wa droo ya nane ya Biko iliyochezeshwa Jumapili. Wengine wanaoshuhudia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja, Msanii Mpoki na maofisa wa NMB jijini Arusha.
  Mshindi wa Biko jijini Arusha akisikiliza ushauri wa kifedha kutoka kwa afisa wa NMB Jijini Arusha jana.

  Alisema wanajisikia faraja kubwa kuona watu wanaingia kwa wingi kucheza mchezo wao wa kubahatisha na kuzoa mamilioni ambapo zaidi ya Watanzania 35,000 wameshinda zawadi mbalimbali.

  Mgeta anasema hadi sasa wameshafanya droo kubwa tisa huku washindi wote wakiwa wameshakabidhiwa fedha zao hivyo kufanya jumla ya Sh Milioni 90 kuwafikia washindi wa droo kubwa za Sh Milioni 10.

  “Huku Jumatano ya kesho tukitoa Sh Milioni 20 kwa mshindi wetu wa droo kubwa, tunajivunia kuona idadi ya wanaovuna mamilioni kutoka Biko inaongezeka kwa kucheza kwa kupitia M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money ambapo jinsi ya kucheza ni kufanya miamala kwenye simu zao kwa kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kumbukumbu namba ikiwa ni 2456.

  “Mtu anaweza kucheza kuanzia Sh 1000 au zaidi huku kila tiketi moja inayopatikana kwa Sh 1000 ikiwa na nafasi mbili ya ushindi wa papo kwa hapo pamoja na nafasi ya kuingia kwenye droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 10, huku kwa Jumatano hii dau likipanda hadi Sh Milioni 20,” alisema Mgeta.

  Mgeta aliongeza kuwa zawadi za papo kwa hapo zinazopatikana katika bahati nasibu yao ni kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja ambayo hulipwa kwa mshindi kwa kupitia simu yake aliyotumia kuchezea bahati nasibu yao.

  Naye Mpande aliishukuru Biko kwa kumpa zawadi yake, akiamini kuwa kupokea kwa haraka kumemfanya aamini kuwa Biko ni waendeshaji wa bahati nasibu za kisasa na zenye uhakika mkubwa wa kushinda.

  Nimepokea zawadi yangu ya Sh Milioni 10 kwa furaha kwa sababu sikuamini kabisa kama nimeshinda, lakini pia kama napokea fedha zangu kwa haraka kiasi hiki, ikiwa ni siku moja baada ya kushinda kwenye droo ya Jumapili.

  “Nawaomba Watanzania wenzangu wasilaze damu, tuendelee kucheza Biko ili tuweze kuvuna mamilioni kwa sababu njia ya ushindi ni kucheza mara nyingi zaidi na tusikate tamaa, ukizingatia kuwa hata mimi sikuamini kama naweza kutangazwa mshindi,” Alisema.

  Bahati Nasibu ya Biko ni moja kati ya michezo iliyoibuka kwa siku za hivi karibuni na kufanikiwa kujizolea umaarufu mkubwa kutokana na utaratibu wake wa upatikanaji wa washindi na kugawa zawadi kwa wakati jambo linalotafsiriwa kama fursa za kiuchumi kwa wachezaji wake na Watanzania kwa ujumla.

  0 0

  Mfuko wa Pensheni wa PPF umeendelea kukabidhi vifaa tiba katika hospitali na vituo vya afya nchini kulingana na sera yake ya uchangiaji na udhamini. 
   
  Katika wilaya ya Kisarawe, Mfuko wa PPF umekabidhi vifaa tiba hivyo kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI,Utumishi na Utawala bora Mhe. Selemani Jaffo kwa ajili ya hospitali ya Wilaya ya Kisarawe ambavyo ni vitanda 2 vya kujifungulia wakinamama, vitanda 4 vya wagonjwa wa kawaida, mashuka 56 na vifaa vinavyotumika kujifungulia wakinamama. Akipokea vifaa hivyo, Mhe. Jaffo alisema Mfuko wa PPF walichofanya ni jambo kubwa kwa vile hospitali za wilaya ya Kisarawe zilikuwa zikikabiliwa na changamoto katika sekta ya afya. 
   
  Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele, alisema Mfuko umetoa vifaa tiba hivyo ikiwa ni muendelezo wa zoezi la kurudisha kwenye jamii kulingana na sera ya uchangiaji na udhamini ya PPF. Alisema Kisarawe ni wilaya ya nne kupata vifaa hivyo na kwamba wataendelea kutoa kwenye hospitali nyingine 12 nchini. 
   
  Lulu alisema Mfuko wa PPF, umetoa vifaa tiba vyenye jumla thamani ya Sh. 99,983,700/-. Shughuli hiyo ya kukabidhi vifaa tiba kutoka Mfuko wa PPF ilienda sambasamba na taarifa ya kukabidhi vifaa tiba kutoka kwa Mfamasia Mfawadhi wa Ofisi ya Rais (TAMISEMI),Regina Joseph kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Utumishi na Utawala bora Mhe. Selemani Jafo, alisema kuwa Rais Dkt. Magufuli ametoa vitanda 20 vya kulalia, vitanda sita vya kujifunguli. Vifaa kama hivyo vinasambazwa katika hospitali nyingine nchi nzima.
  Naibu wa Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora, Seleman Jaffo akiongea na wafanyakazi na wananchi waliojitokeza katika halfa ya kupokea vifaa tiba ikiwemo vitanda 2 vya kujifungulia wakinamama, vitanda 4 vya wagonjwa wa kawaida, mashuka 56 na vifaa vinavyotumika kujifungulia wakinamama kutoka kwa Mfuko wa PPF katika kutekeleza sera yake ya uchangiaji na udhamini. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG-KISARAWE. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Nedesa akielezea machache juu ya changamoto zilizokuwa zikiikabili wilaya yake katika upande wa afya. Pembeni yake ni Naibu wa Waziri (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora, Seleman Jaffo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kisarawe, Hamis Dikupatile. Meneja Uhusiano wa Mfuko wa PPF, Lulu Mengele akiongea wakati wa halfa ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika jana katika hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani. Naibu wa Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora, Seleman Jaffo akipokea msaada wa vifaa tiba kutoka Meneja Uhusiano wa Mfuko wa PPF, Lulu Mengele wakati wa halfa ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika jana katika hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani.
  Naibu wa Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoaa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora, Seleman Jaffo akimkabidhi vifaa tiba kwa Mganga mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Elizabeth Oming'o kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Kisarawe.

  Vifaa tiba vilivyotolewa na Mfuko wa PPF.
  Naibu wa Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoaa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora, Seleman Jaffo (wa tano toka kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Nedesa wakiwa katika picha ya pamoja baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa PPF na wafanyakazi wa wilaya ya Kisarawe.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kisarawe, Hamis Dikupatile akitoa shukrani Mfuko wa PPF kwa kutoa vifaa tiba.
  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF, Janet Ezekiel (wa pili kulia) na Afisa Uendeshaji wa PPF Kanda ya Ilala, Stella Mashiku wakiwaandikisha mwanachama mpya wa Wilaya ya Kisarawe, Pwani.

  Afisa Uendeshaji wa PPF Kanda ya Ilala, Stella Mashiku akiwaandikisha wanachama wapya wa Wilaya ya Kisarawe, Pwani.

  0 0  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma, Mei 30, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhajj Abdallah Bulembo akimkabidhi rambirambi ya CCM, mjane wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania Samwel Sitta, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika huyo wa zamani wa Bunge la Tanzania marehemu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo


  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhajj Abdallah Bulembo akimpa pole, Ben Sitta, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehemu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo 

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaji Abdallah Bulembo na Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri, wakiwa na nyuso za majonzi wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehemu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo


  Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa salam za rambirambi wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehemu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akitoa salam za rambirambi wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehemu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo 

  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Hassan Wakasubi akimpa pole Mjane wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania, Samwel Sitta, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika huyo wa zamani wa Bunge la Tanzania Marehemu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Hassan Wakasubi akimpa pole Hajjat Kagori ambaye ni Mama wa Marehemu, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani Bunge la Tanzania marehemu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo
  Mjane wa Spika wa zamani wa Bungela Tanzania, Samwel Sitta, Margareth Sitta, akimfariji Hajjat Kagori ambaye ni Mama wa Marehemu, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehemu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo
  Edward Sitta ambaye ni mdogo wa marehemu, akisoma wasifu wa marehemu, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehemu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo


  Baadhi ya waombolezaji wakiwa msibani, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania Marehemu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo
  Baadhi ya waombolezaji wakiwa msibani, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehemu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo


  Margareth Sitta ambaye ni mjane wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania, akiwa na baadhi ya wanafamilia, Baadhi ya waombolezaji wakiwa msibani, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehemu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo. Kulia ni Benjamin Sitta.
  Naibu Meya wa zamani wa Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam, Songoro Mnyonge, akitoa salam za rambi rambi, wakiwa msib wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehemu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhajj Abdallah Bulembo.
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Hassan Wakasubi akizunguma jambo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wzazi Alhajj Abdallah Bulembo, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehemu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo. Katikati ni Mbunge wa zamani wa Tabora Aden Rage.

  Jeneza lenye mwwili Peter John Sita, Mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania Marehemu Samwel Sitta, ukiwa katika eneo la kuagwa  Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tazania, Alhajj Abdallah Bulembo akitoa heshima za mwisho, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehmu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Hassan Wakasubi akitoa heshima za mwisho, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehmu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo  Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa heshima za mwisho, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehmu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo  Katibu wa Siasa na Oganaizesheni Makao Makuu ya Jumuiaya Umoja wa Wazazi Tanzania Ndugu Mgaya akitoa heshima za mwsho, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehmu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo


  Baadhi ya wanafamilia wakitoa heshima za mwisho, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehmu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo  Hajjat Kagori ambaye ni mama wa Marehemu, akitoa heshima za mwisho, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehmu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo


  Margareth Sitta ambaye ni mjane wa Spika wa zamani wa Bunge, Samwel Sitta, akitoa heshima za mwisho, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika huyo wa zamani wa Bunge la Tanzania marehmu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo
  Mmoja wa wanafamilia akiagua kilio, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehmu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo


  Kaburi likiwa tayari kwa ajili ya mazishi ya mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehmu Samweli Sitta, Peter John Sitta, Urambo mkoani Tabora leo


  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akiwa na badhi ya wanafamilia kwenye mazishi ya mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehmu Samweli Sitta, Peter John Sitta, Urambo mkoani Tabora leo
  Jeneza likishushwa kutoka kwenye gari malum, wakati mazishi ya mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehmu Samweli Sitta, Peter John Sitta, Urambo mkoani Tabora leo
  Jeneza likipekwa kwenye kaburi, wakati wa mazishi ya mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehmu Samweli Sitta, Peter John Sitta, Urambo mkoani Tabora leo  Jeneza likiwekwa kwenye kaburi wakati wa mazishi ya mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehmu Samweli Sitta, Peter John Sitta, Urambo mkoani Tabora leo  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdalla Bulembo (mwenye shati la kijani), akishiriki kuweka sawa jeneza, wakati wa mazishi ya mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehmu Samweli Sitta, Peter John Sitta, Urambo mkoani Tabora leo  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdalla Bulembo (mwenye shati la kijani), akishiriki kuweka sawa jeneza, wakati wa mazishi ya mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehmu Samweli Sitta, Peter John Sitta, Urambo mkoani Tabora leo  Jeneza lenye mwili likiombewa kabla ya kutumbizwa kaburini, wakati wa mazishi ya mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehmu Samweli Sitta, Peter John Sitta, Urambo mkoani Tabora leo  Jeneza likitumbukiwa kaburini hatua kwa hatua, wakati wa mazishi ya mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehmu Samweli Sitta, Peter John Sitta, Urambo mkoani Tabora leo  Waombolezaji wakiwa kwenye mazishi hayo  Waombolezaji wakiongoka makaburi baada ya kumzika mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehmu Samweli Sitta, Peter John Sitta, Urambo mkoani Tabora leo. PICHA: BASHIR NKOROMO

  0 0

  Watanzania wameaswa kuisaidia serikali katika kutatua changamoto katika sekta mbalimbali ili kujiletea maendeleo kwa haraka, badala ya kusubiri kila jambo lifanywe na serikali.

  Kauli hiyo imetolewa na Mdau wa maendeleo Boniface Myalla wakati alipotembelea shule ya Msingi Kunguru iliyopo Goba na kugawa Daftari kwa wanafunzi 300 wa darasa la kwanza.

  Mayala amesema, Watanzania hawana budi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali inayoongozwa na Rais Dk.John Pombe Magufuli za kuhakikisha inaleta maendeleo na huduma bora kwa wananchi.

  "Serikali imetekeleza jukumu lake la kutoa elimu bure, imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya wanafunzi kusoma bure, sasa imebaki upande wetu wazazi na walezi kuwawezesha wanafunzi kupata vifaasaidizi," amesema.

  Amesema lengo la kutoa madaftari hayo ni kuunga mkono serikali ya Rais Dk. John Pombe Magufuli katika dhamira yake ya kuhakikisha Tanzania mpya inajengeka, Tanzania ambayo kila Mtanzania atanufaika na nchi yake lakini pia kupata elimu bora.

  Akizungumza baada ya kupokea zawadi hizo, Mwalimu wa wanafunzi hao, Sikujua Ramadhani amemshukuru Myala na kuiomba serikali na wadau wengine kujitokeza na kutoa msaada ili kukamilisha malebgo na ndoto za wanafunzi. Amesema wapo wanafunzi walikjuwa wakishindwa kuandika kwa kukosa madaftari na vifaa vingine vya kujifunzia hivyo ujio wa madaftari hayo utapunguza kero changamoto hiyo.


  Mdau wa maendeleo Boniface Myala akizungumza na wanafunzi alipotembelea shule ya Msingi Kunguru Goba na kugawa madaftari kwa wanafunzi 300 wa darasa la kwanza leo jijini Dar es Salaam.
  Mdau wa maendeleo Boniface Myala akikabidhi daftari kwa Mwalimu wa wanafunzi hao, Sikujua Ramadhani leo jijini Dar es Salaam.(picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
  Mdau wa maendeleo Boniface Myala akigawa daftari kwa wanafunzi wa darasa la kwanza wa shule ya Msingi Kunguru Goba . Leo jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha Ernest Mpanda akiwa anazungumza katika kikao cha kuimarisha Utendaji  katika Halmashari ya Jiji ,aliyepo kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro ,aliyepo kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Juma Kihamia 
   
   Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro akizungumza na Watumishi wa Halamashauri ya Jiji la Arusha katika kikao hicho kilichofanyika leo 
   
   Baadhi ya watumishbi waliobhudhuria katika kikao hicho kilichofanyika leo.Picha na Vero Ignatus Blog.

  Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro akiwa anasisitiza jambo katika kikao hicho kilichofanyika katika leo Jijini Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog
  Katubu wa CCM mkoa wa Arusha Ernest Mpanda akisistiza jambo katika kikao kilichofanyia cha watumishi katika Halmashauri ya Jiji la Arusha


   Kikao kinaendelea baadhi ya watumishi wakiwa wanafuatilia yanayoendelea Picha na Vero Ignatus Blog.


  Na,Vero Ignatus Arusha.

  Katibu wa CCM mkoa wa Arusha Ernest Mpanda amekutana na watumishi katika Halmashauri ya Jiji  la Arusha ambapo amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inatambua na kuthamini kazi kubwa wanayoifanya ,huku chama hicho kikiwa na imani ya kwamba binadamu wote nisawa,heshima ,kutambuliwa pamoja na Ujamaa na kujitegemea.

  Ameyasema haya leo katika kikao cha kuimarisha utendaji kazi na  kuwataka watumishi hao kuutanguliza Uzalendo mbele,wafanye kazi kwa manufaa ya Taifa na kwa Watanzania kwa ujumla , kwa maadili na kwa usahihi.

  "wakati wa kupiga umekwisha,hatutakubali tumekupa uongozi  hukuwa na mali nyingi, ndani ya miaka miwili  unakutwa unazo mali nyingi ulizojilimbikizia bila kufahamika vyanzo vyake lazima tutakuhoji,kila mtu atimize wajibu wake kwa kumuogopa Mungu" alisema katibu huyo.

  Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro amesema kuwa ni vyema kila mtumishi akasimamia eneo lake la kazi ipasavyo bila kuingiza undugu kwenye kazi,kwani kila mmoja akisimamia eneo lake kikamilifu hakuna mtu yeyote yule atakayekuwa na shida na wao.

  "Umepewa eneo lako la uitumishi lisimamie ipasavyo usilete undugu kwenye kazi,ukifanya kazi yako vizuri hakuna mwenye shida na wewe,unalipwa mshahara ni vyema ukajiuliza je unafanya kazi kama ipasavyo?"alihoji mkuu wa wilaya .

  Aidha Daqqaro amewataka watumishi hao kuwahudumia wananchi kwa moyo safi,lugha nzuri ,kila mmoja afanye kazi yake kwa usahihi japokuwa wananchi wengine wanakera ,amewataka kutambua kuwa mwisho wa siku wao ndiyo wameajiriwa na siyo wale ambao wanawahudumia. 

  "Wahudumieni kwa moyo safi na lugha nzuri,tendeni kazi kwa kuzingatia maadili na kwa usahihi,usije ukapigiwa simu na kiongozi wako ukaanza kuingiwa na hofu na kujiuliza kuna jambo gani tena" alisisitiza Daqqaro.


  0 0

   Meneja wa Jukwaa la Bioteknolojia Afrika (OFAB), Daniel Otunge, akizungumza wakati akitoa mada kwenye semina ya siku tatu iliyowakutanisha wanahabari na watafiti wa kilimo kutoka nchi tano za Afrika Uganda, Kenya, Burknafaso, Ethiopia na Tanzania ambayo ilikuwa mwenyeji wa semina hiyo iliyoanza juzi jijini Mwanza.
   Watoa mada wakijiandaa. 

   Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB),Dk. Emmarold Mneney akitoa mada kwenye semina hiyo.
   Usikivu katika semina hiyo.
   Maswali yakiulizwa kwenye semina hiyo.
   Wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo. 
   Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Filbert Nyinondi (kushoto),akiteta jambo na Meneja wa Jukwaa la Bioteknolojia Afrika (OFAB), Daniel Otunge wakati wa muda wa mapumziko.

   Mshauri Mkuu wa Mradi wa Utafiti wa Mahindi Yanayostahimili Ukame Afrika (WEMA) Tawi la Tanzania Dk.Alois Kulaya akitoa mada.
   Mratibu wa Jukwaa la Bioteknojia kutoka nchini Uganda, Philip Chemonges, akitoa mada.
   Mtaalamu wa masuala ya kilimo kutoka  Nairobi nchini Kenya, Paul Chege akitoa mada.
  Mtafiti wa kilimo kutoka Ethiopia, Dk.Endale akitoa mada.
  Washiriki wa Semina hiyo na watoa mada wakiwa katika picha ya pamoja.


  Na Dotto Mwaibale, Mwanza

  NCHI za Afrika zimetakiwa kuwekeza kwenye kilimo kwa kuwa kilimo ni biashara na chakula.

  Mwito huo umetolewa na Mratibu wa Jukwaa la Bioteknojia kutoka nchini Uganda, Philip Chemonges jijini Mwanza jana wakati akitoa mada kwenye semina ya siku tatu iliyowakutanisha wanahabari na watafiti wa kilimo kutoka nchi tano za Afrika Uganda, Kenya, Burknafaso, Ethiopia na Tanzania ambayo ilikuwa mwenyeji wa semina hiyo.

  "Hivi sasa kilimo ni muhimu hivyo ni vizuri nchi za Afrika ziamke na kuwekeza katika kilimo kwani kilimo ni biashara na kinatukomboa kwa chakula" alisema Chemonges.

  Katika hatua nyingine Meneja wa Jukwaa la Bioteknolojia Afrika (OFAB), Daniel Otunge amewataka waandishi kutoka nchi hizo kushirikiana na wataalamu wa kilimo ili kupata fursa ya kuandika habari za kilimo kwa ufasaha pasipo kuwepo  upotoshaji.


  Otunge alisema lengo la semina hiyo iliyoandaliwa na Jukwaa la Bioteknolojia Afrika (OFAB) kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti na Maendeleo kwa ajili ya Manufaa ya Wakulima Wadogo (AATF) ni kuwakutanisha waandishi wa habari na wataalamu wa kilimo waweze kukutana na kupeana uzoefu wa jinsi ya kuandika habari za kilimo cha Bioteknolojia kwa ufanisi.

  Alisema wakati wote wamekuwa wakihitaji kilimo cha kisasa ambacho kinafanyika kisayansi ili kiweze kumsaidia mkulima kutumia mbegu bora zenye uwezo wa kukinzana na wadudu na magonjwa na zile zinazostahimili ukame.

  Alisema changamoto kubwa iliyopo hivi sasa ni kushindwa kuanza kwa matumizi ya bioteknojia baada ya watafiti kufanya utafiti ambao umekuwa ukisubiri kuruhusiwa na nchi husika.

  Mtaalamu wa masuala ya kilimo kutoka Nairobi nchini Kenya, Paul Chege alisema teknolojia hiyo mpya ya kilimo ambayo inafanyika katika nchi tatu za Afrika Kusini, Sudan na Burknafaso ambayo imesimama kwa kuwa wanashughulikia nyuzi za pamba imewasaidia wakulima mazao yao yasishambuliwe na wadudu kwani mimea yake yenyewe inakuwa na kinga.  Mshauri Mkuu wa Mradi wa Utafiti wa Mahindi Yanayostahimili Ukame Afrika (WEMA) Tawi la Tanzania Dk.Alois Kulaya alisema muhimu kilimo kifanyike kwa kutumia bioteknolojia kwa kuzalisha mbegu badala ya kuendelea na matumizi ya kilimo cha zamani ambacho hakina tija.

  Alishuri kuendeleza kilimo cha matumizi ya teknolojia za uhandisi jeni (GMO), kwani kina tija kwa wakulima baada ya kuonesha mafanikio kwa baadhi ya nchi kama ya Burknafaso kwenye kilimo cha  pamba.

  Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB),Dk. Emmarold Mneney alisema wakati ufike nchi iwekeze kwa kuongeza watafiti wa kutosha ili kusaidia wakulima katika kilimo chenye tija.

  0 0


  0 0

  Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi akitia saini katika kitabu cha wageni mara bada ya kuwasili katika kituo cha kulea Wazee cha Kibirizi mkoani Kigoma mapema wiki hii.
  Afisa Mfawidhi wa kituo cha kulea Wazee cha Kibirizi Bw. Heradius Mushi (kulia) akifafanua mambo mbalimbali yahusuo kituo hicho kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi(katikati) wakati Kamishna huyo alipotembelea kituo hapo mapema wiki hii Mkoani Kigoma.
  Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi(katikati) akitoa maelekezo kwa Afisa Mfawidhi wa kituo cha kulea Wazee cha Kibirizi Bw. Heradius Mushi (kulia) wakati wa ziara yake kituo hapo mapema wiki hii Mkoani Kigoma kushoto ni Mkurugenzi wa Manunuzi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ( Idara ya Ustawi wa Jamii) Bibi Martha Chuma.
  Mkurugenzi wa Manunuzi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ( Idara ya Ustawi wa Jamii) Bibi Martha Chuma pamoja na Afisa Mwandamizi Ustawi wa Jamii Kigendi Maige wakimsikiliza Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi (hayupo pichani) wakati akitoa maelekezo mabalimbai kwa uongozi wa kituo cha kulea wazee cha Kibirizi Mkoani Kigoma alipotembeleaa kituoni hapo mapema wiki hii.
  Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi akisalimiana na Katibu wa Wazee waishio katika kituo cha Kibirizi Mkoani Kigoma Bibi. Veronika Ramadhani alipotembelea kituoni hapo mapema wiki hii.
  Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi akikabidhi baadhi ya zawadi kwa uongozi wa wazee waishio katika kituo cha kulea wazee ya Kibirizi Mkoani Kigoma alipotembelea kituoni hapo mapema wiki hii , kulia ni Mwenyekiti Bw. Said Lekegwa na kushoto ni Katibu Bibi. Veronika Ramadhani
  Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi( wa tatu kulia) akizungumza na uongozi wa Wazee waishio katika kituo cha kulea wazee cha Kibirizi Mkoani Kigoma watendaji kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na uongozi wa kituo hicho alipowatembelea mapema wiki hii.
  Katibu wa Wazee waishio katika kituo cha kulea Wazee cha Kibirizi Bibi. Veronika Ramadhani ( wa tatu kushoto)akieleza changamoto mbalimbali zinazowakumba wazee waishio katika kituo hicho kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi( wa tatu kulia) alipofanya ziara katika makazi hayo mapema wiki hii Mkoani Kigoma.
  Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi (wa tatu kulia) akifurahi jambo pamoja na uongozi wa wazee waishio katika kituo cha kulea wazee cha kibirizi Mkoani Kigoma na watendaji kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na uongozi wa kituo hicho.

  Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO Kigoma

  0 0

  NA ALLY DAUD-WAMJW DODOMA

  ASILIMIA 24.9 ya watanzania huvutishwa moshi wa tumbaku katika sehemu za kazi hivyo kuchangia kuongezeka kwa wagonjwa wa saratani nyingi hapa nchini.

  Hayo yamebainishwa kwenye taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu inayohusu Maadhimisho ya siku ya kutotumia tumbaku duniani.

  “Hali hii isipodhibitiwa vifo vitaongezeka kufikia asilimia 80 kwenye nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania na milioni 8 kwa mwaka duniani kote ifikapo 2030” iliongeza taarifa hiyo.

  Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa katika uchunguzi uliofanywa mwaka 2013 na Wizaya ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia Taasisi ya Utafiti wa Maradhi ya Binadamu(NIMR) wakishirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) ulionyesha asilimia 24.9 huvutishwa moshi wa tumbaku sehemu za kazi, asilimia 14 ya watanzania hutumia tumbaku na asilimia 17 ya watanzania hawavuti lakini wanavutishwa moshi wa tumbaku.

  Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa tumbaku inaua watu takribani milioni 6 kila mwaka na moshi wake huua zaidi ya watu laki 6 ambao sio wavutaji wa tumbaku duniani .

  Mbali na hayo Wizara ya afya imedhamiria kupiga vita matumizi ya tumbaku kwa kuhakikisha hakuna matangazo ya tumbaku kyupitia kwenye mabango barabarani,luninga,redio,sinema,au kubandikwa ukutani na kwenye magari ya matangazo.

  Madhimisho ya Siku ya kutovuta Tumbaku huadhimishwa Mei 31 kila mwaka duniani kote na kwa mwaka huu imebeba kauli mbiu isemayo”TUMBAKU-TISHIO KWA MAENDELEO” .

  0 0

  Makampuni ya kiwango cha kati yanatimiza jukumu muhimu katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania. Kwa kutambua hilo, KPMG na Mwananchi Communications walianzisha utafiti wa makampuni 100 bora yafanyayo biashara ya kiwango cha kati. Banki M Tanzania ndiye mdhamini mkuu wa tuzo zitakazotolewa baada ya utafiti huo muhimu.
  Utafiti huo hubainisha mafanikio ya makampuni yafanyayo biashara ya kiwango cha kati na jinsi yanavyochangia ukuaji wa uchumi kwa ujumla.
  Washindi wa utafiti huo watatangazwa katika hafla ya utoaji tuzo za makampuni bora yafanyayo biashara ya kiwango cha kati mwezi Septemba, hafla itakayofanyika jijini DSM.
  Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa KPMG, Vincent Ongala alisema kuwa idadi ya makampuni ambayo yanajitokeza kwa hiari kushiriki katika utafiti huu inazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka. “tunatarajia kiasi cha makampuni 250 kushiriki katika tuzo za mwaka huu wa 2017.
  Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications, Bakari Machumu alielezea mafanikio waliyoyapata kutokana na kuandaa utafiti huu,” kuna makampuni ambayo hayatafanikiwa kushinda mwaka huu, lakini yasivunjike moyo kwani mwakani yanaweza kufanya vizuri zaidi.”Machumu pia aliwashukuru Bank M kwa kuendelea kuwaamini na kuendelea kuwa wadhamini wakuu kwa mwaka wa tatu mfululizo.
  Wadhamini wengine ambao wameshikana mikono na KPMG pamoja na MCL mwaka huu ni Azam Media.
  AZAM MEDIA: Wamevutiwa kuungana mkono na wadhamini wengine ilikutoa fursa kwa wafanyabiashara 100 wa kiwango cha kati ilikuweza kupata fursa ya kutangaza biashara zao kupitia vyombo vyake vya habari ikiwemo Television na (Online as AZAM APP ONLINE). Hii ni fursa ya pekee kwa kutumia AZAM media unaweza kutanua wigo wa biashara katika nchi jirani kwani Azam Media imekuwa ikiangaliwa sana hapa nchini na nje ya nchi zikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi na baadhi ya sehemu kama nchi za kongo, Sudan. Hivyo itasaidia kupanua soko na kukuza biashara kwa bei nafuu ilikuwezesha kutangaza biashara kimataifa.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya KPMG Partner, Vincent Onjara akiongea na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa utafiti wa makampuni 100 bora yafanyayo biashara ya kiwango cha Kati 2017 (Top 100 Mid-Sized Companies). Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Flightlink Kapteni Munawer Dhiran ambaye Kampuni yake illibuka Mshindi wa Kwanza wa Mkampuni 100 yaliyoshiriki mwaka jana na Meneja Mauzo wa Azam Media, John Mbele ambao ni mmoja wa wadhamini wa mashindano hayo na Mhariri Mtendaji Mkuu wa MCL, Bakari Machumu. Mdhamini Mkuu wa Mashindano hayo ni Bank M. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogspot)
  Mhariri Mtendaji Mkuu wa MCL, Bakari Machumuakiongea na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa utafiti wa makampuni 100 bora yafanyayo biashara ya kiwango cha Kati 2017 (Top 100 Mid-Sized Companies). Kutoka (kushoto) ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Flightlink Kapteni Munawer Dhiran ambaye Kampuni yake illibuka Mshindi wa Kwanza wa Mkampuni 100 yaliyoshiriki mwaka jana, Meneja Mauzo wa Azam Media, John Mbele ambao ni mmoja wa wadhamini wa mashindano hayo na Mkurugenzi wa Kampuni ya KPMG Partner, Vincent Onjara. Mdhamini Mkuu wa Mashindano hayo ni Bank M.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Flightlink Kapteni Munawer Dhiran ambaye Kampuni yake illibuka Mshindi wa Kwanza wa Mkampuni 100 yaliyoshiriki mwaka jana, akiongea machache na wana habari katika uzinduzi huo. Pamoja naye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya KPMG Partner, Vincent Onjara (kulia) na Meneja Mauzo wa Azam Media, John Mbele ambao ni mmoja wa wadhamini wa mashindano hayo.
   Afisa Tehama Mkuu wa Kampuni ya SoftNet, ambapo Kampuni yao ilikuwepo katika washindi Kumi Bora kati ya washindi wa Mkampuni 100 yaliyoshiriki mashindano ya mwaka jana, Gilbert Herman akitoa ushuhuda wa jinsi kampuni hiyo ilivyoweza kufanya vizuri kutokana na ushiriki wao katika mashindano hayo. Pamoja naye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya KPMG Partner, Vincent Onjara (kushoto) na Mhariri Mtendaji Mkuu wa MCL, Bakari Machumu.
  Mhariri Mtendaji Mkuu wa MCL, Bakari Machumu akifafanua jambo kwa waandishi wa habari walioshiriki katika uzinduzi huo. Kulia (kwake) ni Mkurugenzi wa Kampuni ya KPMG Partner, Vincent Onjara na Meneja Mauzo wa Azam Media, John Mbele ambao ni mmoja wa wadhamini wa mashindano hayo.
  Sehemu ya wana habari na wageni wengine walioshiriki uzinduzi huo.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya KPMG Partner, Vincent Onjara (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa waandaaji na wadhamini wa mashindano hayo. Mdhamini Mkuu wa Mashindano hayo ni Bank M.
  Tanzania Top 100 Mid-sized Companies Survey Launched
  The search for the top 100 mid-sized companies is back. This year’s Tanzanian top 100 mid-sized companies’ survey was officially launched in Dar es Salaam yesterday.
  Speaking at the launch, the KPMG Partner Mr Vincent Onjala, said the survey shows that an increased competition tops the list of challenges facing mid-sized companies.
  “This survey has a lot of benefits to the Tanzanian companies. But the most important one is mileage. When your company is ranked in the top 100 mid-sized companies, you are in what I call the mileage zone. You get a lot of publicity, recognition and respect from all stakeholders,” said Mr. Onjala. He said the mid-sized businesses need to change perception and come up with the best ways through which they can make their companies more marketable. He encouraged all Tanzanian mid-sized companies to seize this opportunity and participate in the survey as it has multiple benefits.
  Top 100 mid-sized companies’ survey was initiated by KPMG and Mwananchi Communication Limited (MCL). It is organized annually and aims to recognize mid-sized companies that are doing better than their peers in economic development of Tanzania. For the fourth year in a row, Bank M is the platinum sponsor of the survey.
  Companies that qualify for the survey are those with a turnover range between TZS 1 to 20 billion, audited financial records for the last 3 years, not listed on a stock exchange market and must not be a bank/ insurance company/SACCO/Law firm/Accounting or auditing firm. The Top 100 Mid-Sized Companies are selected from all participating companies on the basis of their revenue growth over the past three years.
  The Executive Editor for Mwananchi Communications Limited (MCL), Mr Bakari Machumu, stated the survey is not only to help the participating companies build their brands beyond the borders, but also to drill them on how to deal with and stay ahead of competition or better still, how to thrive amid growing competition. “We are here to support the mid-sized companies to grow despite the challenges”. 
  The purpose of the Top 100 Survey is to identify Tanzania’s fastest growing medium-sized companies with a view to showcase their business excellence and highlight their most successful entrepreneurship stories. Over the last six years, we have had over 1000 companies seeking to be among the Top 100 Mid-sized companies. However, not all have been eligible for participation.
  Winners of the renowned Tanzania Top 100 Mid-Sized Companies Survey will be announced in September during a grand gala dinner event to be held in Dar es Salaam. 
  Other sponsors that joined hands with KPMG and MCL are Azam TV.

  0 0  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 13.5 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa awamu ya tatu wa jengo jipya la Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) linalotegemewa kukamilika na kuanza kutumika kwa asilimia mia moja mwaka huu.

  Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku nne ya madaktari kutoka nchi mbali mbali za Afrika.

  Dkt. Boniface amesema kuwa changamoto kubwa inayoikabili taasisi hiyo ni ongezeko la wagonjwa sababu iliyopelekea kuanzishwa kwa mradi wa ujenzi wa jengo jipya litakalokuwa na vifaa vya kutosha hivyo kupanua huduma za afya pamoja na kupunguza gharama za rufaa za wagonjwa kutibiwa nje.

  “Awamu ya tatu ya mradi wa ujenzi wa jengo jipya la MOI ulianza na jumla ya shilingi bilioni 17.9 ambazo ni fedha za mkopo kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) lakini fedha hizo hazikuweza kukamilisha ujenzi hivyo tumeongezewa na Serikali jumla ya bilioni 13.5 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo,”alisema Dkt. Boniface.

  Mkurugenzi huyo amemshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwezesha kupatikana kwa fedha hizo ambazo zitasaidia kumalizika haraka kwa ujenzi wa jengo hilo ambalo litaondoa changamoto ya kujaa kwa wagonjwa.

  Akizungumzia mafunzo hayo ya madaktari, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Msiru amesema kuwa huu ni mwaka wa tano tangu mafunzo hayo yaanze kufanyika nchini ambapo yanashirikisha wakufunzi kutoka MOI pamoja na Marekani.

  “Lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu ya tiba za majeruhi wa ajali kwa madaktari kutoka nchi mbalimbali za Afrika zikiwemo za Zimbabwe, Liberia, Sudan,Ethiopia, Namibia na Malawi yakiwa na nia ya kubadilishana ujuzi wa jinsi ya kutibu wagonjwa wenye ulemavu na kuzuia vifo,”alisema Prof. Msiru.

  Kwa upande wake Daktari bingwa wa Mifupa MOI, Edmund Ndalama amesema kuwa nchi nyingi bado hazijachukulia ajali kama ni jambo la kuwekewa msisitizo wakati ajali ni tatizo kubwa linalopoteza maisha ya watu wengi na kuwaacha wengine wakiwa na vilema vya maisha.

  “Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa takribani watu milioni sita wanafariki kwa ajali kila mwaka na kati ya watu milioni 20 hadi milioni 50 wanabaki na ulemavu wa maisha, hii ni idadi kubwa ya watu ambayo hata ukilinganganisha na idadi ya vifo vinavyotokana na magonjwa mengine havifikii idadi hiyo”, alisema Dkt.Ndalama.

  Amemalizia kuwa umefikia muda kwa madaktari kufahamu njia nyingi zinazohusiana na kutibu magonjwa ya mifupa yanayosababishwa na ajali ili kupunguza idadi ya vifo vya wananchi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dkt. Respicious Boniface akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku nne kwa madaktari kutoka nchi mbali mbali za Afrika, Kushoto ni Daktari bingwa wa MOI, Dkt. Edmund Ndalama.Ufunguzi huo umefanyika leo Jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Msiru akiongea na waandishi wa habari juu ya uendeshaji wa mafunzo hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku nne kwa madaktari kutoka nchi mbali mbali za Afrika.

  Daktari bingwa wa Mifupa wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dkt. Edmund Ndalama akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya ajali ilivyo nchini wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku nne ya madaktari kutoka nchi mbali mbali za Afrika. Ufunguzi huo umefanyika leo Jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya madaktari kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakisikiliza mafunzo yenye lengo la kubadilishana ujuzi wa jinsi ya kutibu wagonjwa waliopata ajali. Mafunzo hayo ya siku nne yameanza leo Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi (katikati waliokaa) akipiga picha ya pamoja na wanachama wa chama cha wapima Ardhi Tanzania, baada ya kumaliza semina iliyofanyika jana katika hoteli ya Morena Mjini Dodoma.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi (wa pili kulia) akisisitiza jambo wakati akifungua semina ya wanachama wa chama cha wapima Ardhi Tanzania, iliyofanyika jana katika hoteli ya Morena Mjini Dodoma.
  Wanachama wa chama cha wapima ardhi Tanzania wakifwatilia semina iliyoendelea leo katika hoteli ya Morena Mjini Dodoma.

  0 0

   Katibu Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Nyakimura Muhoji akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu majukumu mbalimbali yaliyotekelezwa na Tume hiyo katika mwaka wa fedha 2016/17 kwa ajili ya kuboresha utendaji katika utumishi wa umma. Kushoto ni Katibu Msaidizi wa Tume hiyo Bw. Peleleja Masesa.
  Katibu Msaidizi Idara ya Afya kutoka Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Peleleja Masesa akifafanua kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Sheria ya Utumishi wa Umma Na.8 inayoelezea majukumu ya Tume hiyo. Kulia ni Katibu Msaidizi Idara ya Utumishi Serikalini kutoka Tume hiyo Bw. John Mbisso.
  Katibu Msaidizi Idara ya Utumishi Serikalini kutoka Ofisi ya RaisTume ya Utumishi wa Umma Bw. John Mbisso akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taratibu za kupokea na kushughulikia rufaa za watumishi wa umma katika Tume hiyo. Kulia ni Katibu Msaidizi wa Tume hiyo Bw. Peleleja Masesa.(PICHA ZOTE NA FATMA SALUM- MAELEZO)


  Na Fatma Salum (MAELEZO)

  Serikali imewataka Waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu kote nchini kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo inayosimamia Utumishi wa Umma ili kuleta ufanisi katika usimamizi na uendeshaji wa masuala ya Rasilimali Watu kwenye Utumishi wa Umma.

  Kauli hiyo imetolewa na Katibu Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma Bw.Nyakimura Muhoji wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

  Muhoji alisema kuwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Tume hiyo imefanya ukaguzi wa Rasilimali Watu katika Taasisi 41 na kubaini kwamba kuna baadhi ya Waajiri, Mamlaka za Ajira na Nidhamu hazitekelezi ipasavyo majukumu yao hususan katika usimamizi wa masuala ya ajira na nidhamu hivyo kupunguza ufanisi katika utendaji kazi.

  “Ukaguzi wa Rasilimali Watu umefanyika katika Taasisi 41 ambazo ni Sekretariet za Mikoa mitano ikiwemo Morogoro, Iringa, Mbeya, Arusha na Mwanza, Mamlaka za Serikali za Mitaa 30 zilizopo kwenye mikoa hiyo pamoja na Wakala na Taasisi 6 kwa lengo la kuangalia ni kiasi gani Waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu wanafanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Utumishi wa Umma.” alieleza Muhoji.

  Naye Katibu Msaidizi Idara ya Afya kutoka Tume hiyo Bw. Peleleja Masesa alisema kuwa hali ya uwasilishaji wa taarifa zinazohusu usimamizi wa Rasilimali Watu hairidhishi kwa kuwa zipo baadhi ya Taasisi za Umma hazitekelezi jukumu hilo la kisheria.

  “Nasisitiza kuwa uwasilishaji wa taarifa kwa Tume ni jukumu la kisheria hivyo Waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu ambao hawajawasilisha taarifa hizo wanakumbushwa kuziwasilisha kwa mujibu wa mwongozo uliotolewa.” alisisitiza Masesa.

  Aidha Masesa alieleza kuwa Tume hiyo pia ina jukumu la kupokea na kushughulikia Rufaa na malalamiko yanayohusu masuala ya kiutumishi kutoka kwa Watumishi wa Umma ambao hawakuridhika na jinsi masuala yao ya kiutumishi yalivyoshughulikiwa na mamlaka zao.

  Pia alitoa wito kwa Watumishi wa Umma na Watendaji wote kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, maadili ya Utumishi wa Umma na taaluma zao ili Utumishi wa Umma ukidhi matarajio ya wananchi.

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa Wilunze kata ya Manchali katika uzinduzi wa mradi wa maji.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Chilonwa Joel Mwaka wakipiga makofi baada ya kuzindua mradi wa maji Wilunze.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa kwenye kigoda cha kigogo huku akiwa amevishwa mgolole na kupewa fimbo ikiwa ni ishara ya shukrani kutoka kwa wananchi baada ya kuwezesha kukamilika mradi wa maji Wilunze.
  Jiwe la msingi la Mradi wa maji Wilunze
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza mara baada ya kumtwisha ndoo ya maji mmoja wa wananchi wa kijiji cha Wilunze.

  …………………………

  NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewataka wakandarasi wanaojenga miradi ya miundombinu mbalimbali kwenye Halmashauri nchini kuhakikisha miradi hiyo inakamilika ndani ya muda na inakuwa na ubora unaotakiwa.

  Jafo alitoa kauli hiyo leo katika uzinduzi wa mradi wa Maji Wilunze wilayani humo.

  Mradi huo umefanikiwa kukamilika na kuzinduliwa rasmi kufuatia maagizo aliyoyatoa Machi,26 mwaka huu baada ya kutembelea na kubaini kuna uzembe Mkubwa katika utekelezaji wa mradi huo.

  Baada ya kubaini hilo, Jafo alitoa kalipio kwa watendaji wa Halmashauri pamoja na Mkandarasi wa ujenzi wa mradi na kuagiza mradi huo ukamilike haraka ifikapo leo Mei 30, mwaka huu, kinyume cha hapo atawachukulia hatua kali watendaji na Mkandarasi endapo angeshindwa kukamilisha ndani ya muda huo.

  Aidha, Jafo alimwambia mkandarasi wa Mradi huo kuwa endapo asipotekeleza asitegemee kupata kazi yeyote iliyo chini ya Halmashauri yeyote hapa nchini kwani Ofisi ya Rais Tamisemi haiwezi kuvumilia wakandarasi wazembe. 

  Kukamilika kwa mradi huo, kumepokewa kwa shangwe kubwa kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Wilunze maarufu kwa jina la Chalinze nyama kwa kuwa awali walilazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.

  Akizindua mradi huo, Jafo alisema wakandarasi wengi wamekuwa wababaishaji katika kutekeleza miradi kwa wakati na kuwa kikwazo cha miradi mingi kushindwa kukamilika kwa wakati huku wananchi wakiendelea kupata shida.

  Alifafanua kuwa katika awamu hii ya tano hakuna nafasi kwa wakandarasi wababaishaji ambao wamekuwa wakibembelezwa katika kukamilisha miradi ya jamii na kuwaonya kuwa dhama zimebadilika hakuna wakati tena wa kufanya kazi kwa mazoea kama ilivyokuwa zamani.

  Naye, Mbunge wa jimbo la Chilonwa, Joel Mwaka alimshukuru sana Naibu Waziri kwa umakini mkubwa katika utendaji wake kwa kuwa amekuwa ni kiongozi wa kuigwa hapa nchini.“Mheshimiwa Jafo anafuatilia mambo kwa umakini na kupata matokeo makubwa kwa kila miradi anayo isimamia hapa nchini nimeona hilo mikoa mbalimbali hapa nchini,”alisema Mwaka.

older | 1 | .... | 1252 | 1253 | (Page 1254) | 1255 | 1256 | .... | 1897 | newer