Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1251 | 1252 | (Page 1253) | 1254 | 1255 | .... | 1898 | newer

  0 0


  0 0


  BY K-VIS BLOG/KHALFAN SAID.
  REPRESENTATIVES from more than 35 African Countries converge in Tanzanian commercial capital Dar es Salaam in capacity-building workshop on labour statistics and Africa Regional meeting of labour statisticians in preparation for the 20thICLS, to be held in Geneva, Switzerland in October, 2018.The regional workshop started Monday May 29, 2017 at Ramada Hotel in Dar es Salaam.
  ILO’s Assistant Director General and Regional Director for Africa, Mr. Aeneas Chuma, makes his welcoming remarks. With him is Madam Mary Kawar, Director, ILO Country Office for Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda and Burundi.

  Speaking on behalf of the ILO, The ILO’s Assistant Director General and Regional Director for Africa, Mr. Aeneas Chuma, (above), said, quality statistics are increasingly needed as the basis for sound policy advice and support to countries at a time when the economy are changing fast.
  “This regional meeting consists of two activities of capacity-bilding workshop on labour statistics highlighting the 19th ICLS resolution on work statistics and regional consultation of labour statistics in preparation for the 20thICLS.” He explained.
  Mr.Chuma also said, The 19th ICLS resolution, which was the latest labour statistics standard adopted in October 2013, is a core subject of the first activity.
  “I would like to recall that, ILO, we follow a learning approach which is a participatory and hands-on methodology emphasizing knowledge, experience and good practice sharing. I understand such will be the approach to be used in this meeting.” He insisted.

  Mr.Anthony Mavunde, (pictured above), is Tanzanian Deputy Minister of State in The Prime Minister’s Office (Labour,Youth, Employment and Persons with Disability), who was the Chief guest at the opening session.
  In his remarks, the Deputy Minister said, “We all understand that labour statistics play an essential role in the efforts of our countries to achieve decent work for all and for the ILO’s support to these efforts.” Said Deputy Minister. 
  “These statistics are needed for development and evaluation of policies towards this goal and assessing progress towards decent work. They are also an important tool for information and analysis, helping to increase understanding of common problems, explains actions and mobilizes interest.” He said.
  Mr. Mavunde further said, improving the collection and availability of labour statistics is an important factor in not only promoting employment creation and improved livelihoods but also in achieving the 17 SDGs, especially Goal 8. “Promoting sustained, inclusive and sustainable economic growth, full and productive employment and decent work for all.” He stated.
  The deputy minister also said, at the national level, labour market information is particularly important to the governments and all stakeholders, for policy formulation, planning and for monitoring and evaluation, increasingly , government requires labour market information to monitor  the implementation of programmes and legislation and to monitor and evaluate economic and labor market performance.
  Some of the participants attend the workshop

  On his part, the country manager of African Development Bank, (AfDB), who was represented by Mr.Simba Hamisi, (pictured), said, producing treliable and timely labour statistics, is essential to the research and information needs for sound, evidence-based policy-making. “It is for this reason that within the implementation framework of its statistical capacity building program, the African Development Bank (AfDB), in expertise with its regional member countries, identified the lack of expertise in data analysis of labour force surveys and this has been a major drawback in deliberate efforts of producing comprehensive  labour force statistics in many countries.  Director of Population, Census and Social Statistics, Ephraim Kwesigabo, speaks during the opening session


   Guest of honor, Deputy Minister Mavunde, (L), shakes hands with ILO’s Assistant Director General and Regional Director for Africa, Mr. Aeneas Chuma
   A cross section of participants follow the session
   Applauding the speakers
   Guest of honor in a group photo with participants
    Guest of honor in a group photo with participants
  0 0

  Hatimaye waziri mkuu KASIMU MAJALIWA ametimiza ahadi yake aliyotoa januari 5 mwaka huu, kwa wakazi wa halimashauri ya wilaya ya madaba mkoani ruvuma ya kuwaletea gari la wagonjwa ili iweze kusaidia katika EO matatizo.HABARI KAMILI HII HAPA

  0 0

   Bustani ambayo imehifadhi historia ya vita kuu ya kwanza ya dunia (1914-1918)ikiwa na Sanamu ya askari Mwafrika katika sare ya kijeshi ya King's African Rifles aliyeshika bunduki yenye kisu cha kando na kutazama upande wa bahari, imefanyiwa ukarabati mkubwa na Kampuni ya kizalendo ya Green Waste Pro Ltd. Kampuni hiyo kama sehemu ya kurejesha faida kwa jamii ilitengeneza bustani hiyo iliyozinduliwa jana kwa gharama zake wakisimamiwa na mamlaka husika za wilaya na halmashauri. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bustani hiyo iliyofungwa kwa muda mrefu kwa ajili ya ukarabati kwenye msafara wa mbio za Mwenge, Meneja Msaidizi wa Green WastePro, Erick Mark alisema wamefurahi kwa mwenge kuzindua bustani hiyo inayorembesha mji na kuufanya uwe nadhifu

  Muonekano wa bustani ya Askari monument kabla ya kuzinduliwa rasmi.

  Sanamu hiyo iliyowekwa 1927 na Waingereza kama kumbukumbu ya askari na wapagazi Waafrika waliopigana vita Afrika ya Mashariki iliyomuondoa Mjerumani, iliondoa sanamu ya mtawala wa kijerumani Hermann VonWissman iliyowekwa mwaka 1911.
  Eneo hilo ambalo sasa lina muonekano unaong'aa zaidi kutokana na kazi iliyofanywa na kampuni hiyo, ni sehemu ya kampeni kubwa ya kampuni ya Green WastePro Ltd iliyoanzishwa mwaka 2011 ikiwa na lengo la kusaidia halmshauri ya manispaa ya Ilala kuwa safi, ya kushawishi wakazi wa Dar kuupenda mji wao na kuusaidia kuuweka bora. Akifafanua zaidi kuhusu mradi wa upendezeshaji bustani ya sanamu ya askari maarufu kama Askari Monument, Mark alisema kazi waliyofanya ni kushawishi watanzania kutambua umuhimu wa usafi na kuringia kuwa na jiji safi hasa katikati ya Jiji.  Kiongozi wa mbio za mwenge, Amour Hamad Amour akiwa ameshika mwenge baada ya kufika mtaa wa Posta Mpya jijini Dar kwenye uzinduzi wa bustani ya Askari Monument katika manispaa ya Ilala iliyokarabatiwa na kampuni ya Green WastePro ltd.

  Alisema wanakazi kubwa ya kukabiliana na changamoto za ongezeko la takataka na udhibiti wa uchafuzi wa mazingira hususani hapa katikati ya jiji la Dar es salaam kwenye kitovu cha taifa, kazi ambayo wao wamekuwa wakifanya kwa ufanisi mkubwa usiku na mchana, bila kuchoka toka mwaka 2012 walipopewa dhamana hiyo na Halmashauri ya manispaa ya Ilala kwa mara ya kwanza.

  Mbali na kazi hiyo pia wamekuwa wakijihusisha na shughuli mbalimbali za kijamii kwa utaratibu wa kujitolea (Corporate Social Responsibility) kama vile upandaji wa miti, utoaji wa vifaa vya kuhifadhia taka mashuleni, usafishaji wa fukwe, utoaji wa vifaa vya kuhifadhia taka na utunzaji wa mazingira maeneo mbalimbali ya jiji letu la Dar es Salaam hususani kwenye Halmashauri yetu ya Manispaa ya Ilala.  Mkuu wa Idara ya usafi na mazingira Manispaa ya Ilala, Abdon Mapunda akisoma risala kwa mgeni rasmi ambaye ni kiongonzi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2017, Bw. Juma Khatibu Chum (hayupo pichani).

  Akizungumzia mafanikio ya Kampuniya Green WastePro Ltd tangu ianzishwe, Mark alisema wameweza kutengeneza ajira zaidi ya 350 za kudumu pia wamefikia asilimia 80 ya uondoshwaji wa taka ngumu toka Julai 2012, ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo taka ziliondoshwa kwa asilimia 30% hadi 40. Pia wameweza kupanda miti maeneo mbalimbali kiasi cha miti 1,500 ndani na nje ya manispaa hii ya Ilala kwa miaka mitano iliyopita.

   "Mafanikio mengine ni huu mradi tunaouzindua leo wa ukarabati mkubwa wa bustani hii yenye historia kubwa kwa jiji letu la Dar es salaam bustani ya picha ya askari ibismini maarufu kama (Askari monument) nadhani wote tunajionea palivyopendeza, mwenye macho haambiwi tazama." alisema. Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ndugu Amour Hamad Amour (kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kushoto) wakisikiliza hotuba ya Mkuu wa Idara ya usafi na mazingira Manispaa ya Ilala, Abdon Mapunda aliyokuwa anaiwasilisha kwenye uzinduzi wa bustani ya Askari Monument jijini Dar es Salaam kwenye mbio za Mwenge Kitaifa.

  Hata hivyo alisema pamoja na mafanikio hayo, kampuni hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo tatizo la wizi. "Kwenye mradi huu wezi waliiba minyororo mara mbili. Pia kwenye mradi wa upandaji miti, nayo pia imekuwa ikiibiwa.Pindi tunapomaliza kuipanda hupita watu na kuifukua na kwenda kuiuza tena maeneo mengine. Changamoto ni nyingi sana ila hizi tumezitaja kwani zinahusiana na mradi huu." alisema  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (kushoto) akipiga makofi mara baada ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ndugu Amour Hamad Amour kuzindua mradi wa uboreshaji na utunzaji wa mazingira wa Bustani ya Askari Monument katikati ya jiji la Dar Es Salaam uliodhaminiwa na kampuni ya Green WastePro ltd.

  Uongozi wa kampuni hiyo hata hivyo ulimwambia Kiongozi wa Mbio za Mwenge na msafara wake kwamba wana matarajio makubwa ya kuanza ukarabati wa bustani ya makutano ya barabara ya Barack Obama na Ali Hassan Mwinyi maarufu kama bustani ya (salender bridge) ili kuendelea kubadilisha mwonekano wa jiji la Dar es Salaam. Aidha kampuni hiyo inategemea kuanzisha mradi wa kuchakata taka ili kupunguza takataka zinazopelekwa dampo na pia kuzalisha ajira nyingine kwenye kazi hiyo na kuongeza kipato cha serikali upande wa kodi.  Meneja Msaidizi wa kampuni Green WastePro ltd, Erick Mark akitoa ufafanuzi bustani ya Askari Monument iliyotengenezwa na kampuni hiyo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ndugu Amour Hamad Amour iliyozinduliwa Posta Mpya jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Green Waste Pro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo (kulia) akipokea mkono wa pongezi kutoka kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ndugu Amour Hamad Amour mara baada ya kumaliza uzinduzi wa mradi wa uboreshaji na utunzaji wa mazingira wa Bustani ya Askari Monument katikati ya jiji la Dar Es Salaam uliodhaminiwa na kampuni hiyo. Viongozi wa mbio za mwenge wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Ilala wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema mara baada ya kuzindua Bustani ya Askari Monument ambao ni mradi wa uboreshaji na utunzaji wa mazingira wa bustani hiyo katikati ya jiji la Dar Es Salaam uliodhaminiwa na kampuni ya Green WastePro Ltd. Wananchi waliojitokeza kwenye hafla ya uzinduzi wa bustani ya Askari Monument uliofanywa na Mwenge wa Uhuru katika eneo la Posta Mpya jijini Dar es Salaam. Wafanyakazi wa Green Waste Pro Ltd wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye bustani ya Askari monument jijini Dar es Salaam baada ya kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru. 
  Muonekano wa maua yaliyopandwa kuzunguka bustani ya sanamu ya bismini.   Muonekano wa bustani ya Askari monument ikiwa imeshamiri maua ya kupendeza. 
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Green WastePro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo katika picha ya kumbukumbu kwenye bustani hiyo.
  Muonekano wa usiku wa bustani ya Askari monument. 

  0 0  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza katika mkutano wa nane wa wadau wa mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF jijini Arusha juzi ,wakati akifunga mkutano huo ambapo aliwataka wastaafu watarajiwa kujiandaa kustaafu kwa kubuni miradi mbalimbali ya kuongeza kipato hali itakayosaidia wao kujiendeleza kimaisha(Habari Picha na Pamela Mollel Arusha)
  Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Eric Shitindi akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema ni vyema watumishi wakajianda mapema wakiwemo wa umma na sekta binafsi .
  Mkurugenzi wa mfuko wa GEPF Daudi Msangi alisema kuwa tayari kuna mikakati mbalimbali ambayo imeletwa kwenye mkutano huo na itaanza kufanyiwa kazi kwa malengo ya kuboresha maslai ya wanachama na nchi kwa ujumla.
  Mwenyekiti wa bodi Ya wadhamini,wa mfuko huo Joyce shaidi akizungumza katika mkutano huo.
  Kulia ni mkuu wa kitengo cha kusimamia amana za wawekezaji katika benki ya CRDB Bw.Masumai Ahmed.

  Wadau wa mkutano wakiwa wamesimama kuashiria kumalizika kwa mkutano huo  Mkuu wa mkoa wa arusha Mrisho Gambo amewataka Watumishi katika sekta za umma kuacha dhana ya kuogopa kustaafu kazi pindi wanapofikia muda wa kustaafu badala yake wanatakiwa kujipanga kabla muda haujafika.

  Aidha watumishi wanaogopa kustaafu kwa kuwa wanaanza kujiandaa miaka miwili kabla hali ambayo inawapa uoga mkubwa wastaafu watarajiwa.

  Mrisho Gambo ameyasema hayo jana wakati akifunga mkutano wa mfuko wa mafao ya kustaafu (GEPF) uliokuwa ukiendelea jijini Arusha.

  Gambo alisema kuwa kwa sasa wastaafu wanapata magonjwa ya moyo kwa kuwa hawajajiandaa na kubuni miradi ambayo inaweza kuwaletea vipato kama mishahara yao ilivyokuwa.

  Alisema maandalizi ni muimu sana kwa wafanyakazi hata kama bado hawajafikia muda wa kustaafu kwani kustaafu sio ajali bali ni kitu ambacho kipo na kimeshawekewa utaratibu na mifuko ya hifadhi jamii hapa nchini pamoja na Serikali.

  "Wastaafu wengi wanakufa pindi wanapoacha kazi hiyo sio sawa ni lazima kila mtu ajiandae na abuni njia mojawapo ya kujiongezea kipato kwani hata kama ukijiajiri mwenyewe ni lazima utapata kipato kama kile ulicho kuwa unalipwa kama sehemu ya ujira wako "aliongeza Gambo.

  Wakati huo huo aliwataka wakuu wa mifuko ya hifadhi hapa nchini kuhakikisha kuwa wanatoa elimu ya kujiandaa kustaafu kwa wafanyakazi wake kwani uzoefu unaonesha kuwa asilimia kubwa ya wafanyakazi hawana elimu hiyo

  Alisema kama wafanyakazi watakuwa na elimu hiyo ya kustaafu basi itasaidia kupunguza ulalamishi kwa wastaafu,magonjwa ya moyo,vifo visivyo na lazima vinavyotokea.

  Naye mkurugenzi wa mfuko huo Daudi Msangi alisema kuwa tayari kuna mikakati mbalimbali ambayo imeletwa kwenye mkutano huo na itaanza kufanyiwa kazi kwa malengo ya kuboresha maslai ya wanachama na nchi kwa ujumla.

  0 0

  Wakulima wadogo nchini Tanzania hivi karibuni wataweza kupata taarifa mbalimbali za kijiditali kuhusu masuala ya pembejeo, ukiwemo ushauri utakaosaidia kutatua matatizo yanayowakabili kama vile upatikanaji wa fedha, pembejeo na mafunzo. 

  Mradi huo umezinduliwa na taasisi tatu za Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA), Positive International Limited (PIL), na Grameen Foundation katika sherehe zilizohudhuriwa na maofisa wa serikali, wawakilishi wa vyama vya wakulima, taasisi za fedha, kampuni za mbegu, wafanyabiashara wa nyenzo za kilimo na wale wanaojishughulisha na biashara za mazao ya sekta ya kilimo. Kifaa hicho cha dijitali kitawawezesha wakulima kulipia mapema pembejeo wanazohitaji kupitia simu za mkononi kwa bei nafuu.

   Pia kifaa hicho kitawapa wakulima pembejeo kulingana na mazao na malengo yao ya uzalishaji na pia kupata taarifa za ushauri kuhusu matumizi bora ya pembejeo hizo. “Moja ya changamoto kubwa zinazowakabili wakulima ni kwamba hukosa fedha mwanzoni mwa msimu wa upandaji mazao, jambo ambalo huwalazimisha kutafuta fedha hizo kwa ajili ya ununuzi wa pembejeo na hivyo kuwaongezea mzigo,” alisema Hedwig Siewertsen, kiongozi anayeshughulikia masuala ya fedha wa shirika la Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA). 
  “Kifaa hicho cha dijitali kwa ajili kusaidia upatikanaji pembejeo za kilimo ni ufumbuzi wa kipekee. 

  Kitawaimarisha na kuwasaidia wakulima kutenga fedha kwenye akaunti zao za simu ili waweze kununua pembejeo bora kwa muda muafaka na kwa bei nafuu ya asilimia 30.” Wakulima wadogo nchini Tanzania huzalisha asimia 70 ya chakula ingawa karibu nusu yao hawazalishi chakula cha kutosha kwa ajili ya mauzo. Wanakabiliwa na ukosefu wa teknolojia ya kilimo cha kisasa, hawana uwezo wa kujipatia pembejeo bora na wanakosa huduma za kiufundi za ughani zinazoweza kuwasidia kukuza kilimo pamoja na ukosefu wa mafunzo. Mwakilishi wa AGRA nchini, Bw. Vianey Rweyendela akifafanua jambo wakati wa uzinduzi huo.

   Badala yake wakulima hawa wanategemea zaidi kilimo cha mvua, zana duni za kilimo na mbegu hafifu ambazo ubora wake hupungua kila msimu wa kilimo. Isitoshe, wakulima wanaotaka kuwekeza katika kilimo cha kisasa wanashindwa kupata mikopo kwenye taasisi za fedha kwa vile ni asilimia 6 tu ya mikopo ya benki ndio imetengwa kusaidia sekta ya kilimo. 

  Wakulima wanatumia fedha zao chache kununua pembejeo za kilimo kutoka kwa walanguzi; pembejeo ambazo mara nyingi hazina uthibitisho wa ubora. Wakati huo huo, wafanyabiashara wa pembejeo za kilimo wa sekta binafsi wamegundua kwamba usambazaji wa huduma bora maeneo ya vijijini una faida ndogo kutokana na gharama kubwa za kufanya biashara hiyo, uwezo mdogo wa kifedha kwa upande wa wakulima na umaskini uliokithiri miongoni mwa wananchi wengi vijijini. 

  Matokeo yake ni kwamba wastani wa uzalishaji wa mazao mengi kwa hekta unakadiriwa kuwa ni tani 1.7 na kwamba mavuno ya mazao muhimu ya chakula kama vile mahindi yamekuwa yakipungua kwa sababu ya uharibifu wa ardhi na hali mbaya ya hewa. Jinsi ya kupeleka kifaa cha dijitali kwa wakulima Kifaa cha dijitali kitakuwa na mpango mahsusi wa mazao utakaowawezesha wakulima kupata pembejeo kwa kuzingatia malengo yao ya uzalishaji. 

  Pia, kupitia simu za mkononi, kitawezesha upatikanaji wa huduma za ughani kwa njia ya ujumbe (SMS) kuwaelimisha wakulima matumizi ya pembejeo. AGRA, shirika linaloongozwa na Waafrika wenye weledi wa kuwasaidia wakulima wadogo barani Afrika, ndilo linalogharimia ukuzaji wa kifaa hicho cha dijitali kupitia ufadhili wa MasterCard Foundation. 

  Taasisi ya Grameen Foundation, ambayo ni taasisi inayojitegemea inayotumia teknolojia ya dijitali kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya umaskini, ndio inasisimia ukuzaji wa chombo hicho cha dijitali. Kifaa hicho pamoja na huduma zake kitatolewa na kampuni ya pembejeo za kilimo ya Positive International Limited, ambayo nembo yake ya kibiashara ya Snow Brand imesaidia sana kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili wakulima nchini Tanzania. Mfumo huo wa ununuzi wa pembejeo utazingatia uwepo wa huduma za fedha za simu za mkononi zinazokua kwa kasi nchini Tanzania. Uzinduzi ukifanywa na Mkuu wa AGRA nchini Bw. Vianey Rweyendela (wa pili kulia) kwa kushirikiana na wawakilishi wa Positive International Limited (PIL), na Grameen Foundation.

  Mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miezi kumi na nane, ikiwemo awamu ya miezi sita ya utafiti na maendeleo, na miezi kumi na mbili ya awamu ya majaribio ya kifaa hicho cha dijitali. Majaribio yataanza na wateja 15 wa kampuni ya Positive International na wakulima wadogo 15,000 wa mikoa ya Arusha na Mbeya. Mazao yatakayohusika katika mradi huo ni mahindi na maharage, ambayo ni muhimu sana katika maeneo hayo.

   Kwa mfano, mkoani Arusha – moja ya maeneo yanayohusika katika mradi – mazao hayo mawili hulimwa katika eneo la hekta 150,000 ingawa kuna pengo la mavuno la asimilia 213 kwa upande wa mahindi na asilimia 152 kwa upande wa maharage. Matumizi ya pembejeo bora ndio njia pekee itakayosaidia kuongeza mavuno kwa asilimia 150 ili kutosheleza mahitaji ya chakula katika ngazi ya kaya na pia kukuza mapato. Mkurugenzi Mtendaji wa Positive International, Karan Kapoor, anasema soko la matumizi ya kifaa cha dijitali kwa mauzo ya pembejeo za kilimo nchini Tanzania ni kubwa. 

  “Mamilioni ya wakulima wadogo Tanzania wanahitaji upatikanaji wa pembejeo bora za kilimo kwa bei nafuu. Tutaanza matumizi ya kifaa hiki cha dijitali kwa kuwahusisha wafanyabiashara 15 kwa kipindi cha miezi 18 ijayo. Lengo litakuwa kuwafikia wakulima 15,000 ili kuthibitisha matumizi endelevu ya kifaa hicho.

  ” “Baada ya hapo, tumepanga kupanua matumizi yake ili kuwafikia wafanyabiashara 500 nchini bila ya kuwepo miundombinu mpya.” “Watanzania milioni 19 wanaishi kwa kutegemea mashamba madogo ingawa mtu mmoja kati ya watu 25 hupata huduma ya umeme na watu wengi hawana maji safi na salama majumbani mwao,” anasema Raphael Wolf, Meneja Mradi wa Grameen Foundation. “Kifaa hiki kitaleta mapinduzi makubwa ya dijitali mashambani. Kwa mara ya kwanza, wakulima wengi wataweza kupata raslimali wanazohitaji kuongeza uzalishaji na mapato yao.

  ” Jinsi wakulima wanavyopata pembejeo muhimu za kilimo kama vile mbolea na kuongeza mavuno yao, shirika la AGRA litapata fursa ya kutumia uwepo wa ubia wake na vitega uchumi vilivyopo Tanzania kuwaunganisha wakulima na masoko kupitia ushirikiano na wanunuzi wa kimataifa, wawezeshaji wa biashara na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayoshughulika na upatikanaji wa masoko. 

  Mradi huu ukifanikiwa Tanzania, washirika wake wanakusudia kutumia uwezo wao wa pamoja kuanzisha dhana hii na kifaa hicho cha dijitali katika nchi nyingine za Afrika, ukiwemo mtandao wa wafanyabiashara za kilimo katika nchi za Malawi, Msumbiji, Zambia na nchi nyingine katika bara hili.

  0 0

  Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akitoa elimu kuhusu umuhimu wa wananchi kujiunga na mfuko huo kwa wakazi wa Jiji la Tanga kwenye banda lao lililopo katika eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya tano ya biashara ya kimataifa
   Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage akiptia kwenye banda la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) wakati alipofungua maonyesho ya kimataifa ya  biashara ya tano yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
   Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage akisalimiana na mmoja wa watumishi Tanapa wakati wakati alipotembelea banda lao kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella
   Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage akiendelea na shughuli ya kukagua mabanda ya Maonyesho
  Afisa Habari za Utalii (TTB William Akile kulia akiongeza na baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda lao
   Afisa Habari za Utalii (TTB William Akile kulia akiongeza na baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda lao
   Afisa Habari za Utalii (TTB William Akile kulia akiongeza na baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda lao

   Maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakitoa elimu kwa wakazi wa Jiji la Tanga katika Banda lao lililopo kwenye eneo la Mwahako Jijini Tanga kunapofanyika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Tano kutoka kushoto ni Msimamizi wa Ofisi ya Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo katikati ni Sabrina Komba ambaye ni Afisa Masoko na Elimu kwa umma makao makuu na kulia ni Afisa matekelezo Macrina Clemens
   kulia ni Sabrina Komba ambaye ni Afisa Masoko na Elimu kwa umma makao makuu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kulia ni Afisa matekelezo Macrina Clemens wakimsikiliza kwa umakini mkazi wa Jiji la Tanga ambaye alifika kwenye banda lao kupata ufafanuzi kuhusu huduma zinazotolewa na mfuko huo
   Afisa matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Macrina Clemens kulia akisitiza jambo kwa mkazi wa Jiji la Tanga kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na huduma mbalimbali muhimu ikiwemo za matibabu kushoto ni Meneja wa Mfuko huo Mkoani Tanga,Ally Mwakababu katikati ni  Msimamizi wa Ofisi ya Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo kulia kwake ni Afisa Masoko na Elimu kwa umma makao makuu Sabrina Komba

   Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akiwa na maafisa wengine wa mfuko huo wakiwa tayari kutoa elimu kwa wakazi wa Jiji la Tanga kuhusu namna wanavyoweza kunufaika kupitia mfuko huo
   Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akitoa elimu kwa mkazi wa Jiji la Tanga ambaye alitembelea banda lao
  Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao kuhusu faida za wakazi wa Jiji la Tanga kujiunga na mfuko huo lakini pia namna walivyojiandaa na ujio wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga
  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

  Muandaaji wa Semina hiyo iliyofanyika Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere na Mwenyekiti wa UNESCO Youth Forum Bw. Frank Joash akieleza namna ambavyo vijana wanaweza kujiunga katika programu mbalimbali za Umoja wa Mataifa.
  Vijana kutoka Maeneo mbalimbali wakiwa wanasikiliza kwa makini mambo mbalimbali yaliyokuwa yanazungumziwa wakati wa semina hiyo iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere Kigamboni .
  Mwakilishi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) Bw. Nelson akieleza namna viongozi katika sekta mbalimbali wanavyoweza kusaidia kudumisha amani katika Jamii.
  Mshauri wa mambo mbalimbali ya Kijamii na uchumi Bw. Anthony Luvanda akitoa masomo mbalimbali ya namna vijana wanavyoweza kujikwamua na kujitegemea kwa kufanya shughuli mbalimbali.
  Mwakilishi kutoka Raleigh Bi. Alice Norbert akitoa maelezo namna ya vijana ambavyo wanaweza kushiriki shughuli mbalimbali za kujitolea katika Asasi mbalimbali za Kiraia pia alielezea fursa zinazotokana na kujitolea
  Bwana Jackson Oganga akiwa anatoa maelezo kwa vijana jinsi ya kupata 'Scholarship' zinazotolewa sehemu mbalimbali, na kuwasihi kuwa wasikate tamaa kwa kuwa kuna nafasi nyingi za kusoma nje ya nchi.
  Bwana Charles Ndiku akiwaelekeza vijana namna mbalimbali ambazo zinaweza kuwasaidia kupata ajira,na aliwasisitiza ili waweze ishi kwa amani yawapasa kuishi maisha bora ikiwa ni pamoja na kuwa na kipato endelevu.
  Mwenyekiti wa programu kutoka Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Bw. William Peter akieleza namna vijana wanavyoweza kubadili mitazamo na kuwa na mawazo chanya ya maendeleo
  Vijana mbalimbali wakichukua yale yaliyokuwa ya Muhimu 
  Vijana wakiwa wananyoosha mikono ishara ya kuonesha kuwa wameelewa vizuri kwa yale yote waliyoyasikiliza
  Vijana wakiwa wanasikiliza kwa Makini.
  Semina ikiendelea

  Picha ya Pamoja


  Picha zote na Fredy Njeje

  "Kiongozi bora ni pamoja na yule ambaye anahakikisha kuwa kuna amani katika eneo la kazi na watu anaowaongoza" hayo yalisemwa na bwana Nelson aliyekuwa mwakilishi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) Nchini Tanzania wakati wa semina ya vijana katika kushiriki programu mbalimbali za Umoja wa Mataifa iliyoandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na Global Peace Foundation Tanzania. 

  Alisema kuwa kiongozi makini ni yule anayehakikisha kuwa kuna amani katika eneo la kazi na kuwafanya wafanyakazi wake waishi kama familia moja ili kuondoa migogoro mbalimbali ambayo inaweza ikazuirika.

  "Amani inatakiwa kudumishwa kuanzia ngazi ya familia, jamii na taifa kwa ujumla" alisema Nelson na kuongeza kukosekana kwa amani kunaweza kusababisha maafa kama vifo kwa sababu ya vita pia uchumi kuyumba kutokana na watu kuhofia kufanya shughuli za kimaendeleo kwa sababu ya machafuko.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa UNESCO Youth Forum Bw. Frank Joash alisema vijana wengi hawana uwelewa wa program mbali mbali za umoja wa mataifa hivyo waliamua kuwakutanisha ili kuwapa uelewa ili wapate kujiunga.

  Nae Bw. Jackson Oganga ambao walishawahi kusoma nje ya nchi kupitia ufadhili ‘Scholarship” walielezea kwa kina namna walivyo fika huko, changamoto na jinsi zinavyotokea na kuwasihi vijana hao kutokata tamaa na kuendelea kuomba nafasi hizo mpaka pale watakapo fanikiwa nao kutimiza ndoto zao za kwenda kusoma nje.

  Mwisho Mshauri na mwezeshaji katika mambo mbalimbali ya Bw. Anthony Luvanda aliwasihi vijana kujitambua na kufahamu vipaji vyao na kujua namna ya kutimiza ndoto zao, ambapo aliwaomba pia vijana wasitegemee sana kazi za kuajiliwa bali wawe na mawazo chanya ili kuweza kutimiza malengo yao.

  Semina hiyo ilihudhuriwa na zaidi ya vijana 180, kutoka vyuo vikuu vya Mwalimu Nyerere,CBE, TIA, Bagamoyo, Kampala International University na St. Joseph, wanavyuo waliomaliza pamoja na vijana wengine .


  0 0

  Picha ya juu na chini ,Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akizungumza na Wadau wa Maendeleo na viongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF ofisini kwake mjini Unguja.
  Picha ya pamoja
  Balozi Seif Ali Idd akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga baada ya kupata maelezo ya utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo kisiwani Zanzibar,anayewaangalia ni Msimamizi wa shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia ,Bwana Muderis Mohamed.
  Mmoja wa wanafunzi wa shule ya Msingi Kizimbani,Unguja ambaye anatoka kwenye Kaya ya Mlengwa Wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini akikokotoa hesabu, anayemwangalia ni Msimamizi wa shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia Bwana Muderis Mohamed.
  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga(aliyesimama)akizungumza na baadhi ya wananfunzi wanaotoka katika Kaya za Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika shule ya msingi Kizimbani kisiwani Zanzibar.
  Msimamizi wa shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia akiwa katika picha na baadhi ya kununua kikapu kilichotengenezwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini huko Kizimbani, kisiwani Zanzibar. Nyuma yake ni bidhaa zilizotengenezwa na walengwa hao kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.  NA Estom Sanga- Zanzibar 

  Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi amesema mchango unaotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF katika kuhamasisha wananchi kupambana na umasikini unapaswa kuungwa mkono kwani unakwenda sambamba na dhamira ya serikali zote mbili za kuwaondolea wananchi kero ya umasikini. 

  Balozi Iddi ametoa kauli hiyo alipokutana na baadhi ya wadau wa Maendeleo na Maafisa wa TASAF ofisini kwake mjini Unguja baada ya viongozi na wadau hao wa maendeleo kuhitimisha ziara ya kuwatembelea Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini kisiwani humo. 

  Amesema mafanikio makubwa yanayojitokeza katika nyanja za elimu, afya na ongezeko la shughuli za kiuchumi miongoni mwa walengwa wa Mpango huo ni ushahidi tosha kuwa wananchi hususani wale ambao wamekuwa wakikabiliwa na umasikini , wanahitaji kwa kiwango kikubwa utekelezaji wa shughuli za Mpango huo ambao umekuja kwa wakati hasa kutokana na ukubwa wa tatizo la umasikini nchini. 

  Balozi Iddi amesema kwa kutambua hilo serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuunga mkono utekelezaji wa shughuli za TASAF kisiwani humo na kuwataka wananchi hususani wale walioko kwenye Mpango wa kunusuru kaya masikini kutumia fursa hiyo vizuri ili hatimaye waweze kuboresha maisha yao. 

  Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga amesema hatua zilizochukuliwa na serikali katika kuweka msukumo wa kutosha katika utekelezaji wa Mpango huo zimeendelea kuzaa matunda ambapo katika maeneo mengi nchini kote walengwa wameonyesha kuanza kubadilika kwa kuboresha maisha hususani katika nyanja za makazi, elimu, afya na kuunda vikundi vya kuweka akiba na vya uzalishaji mali. 

  Kwa Upande wake Msimamizi wa Shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia,Bwana Muderis Mohamed, amesema wadau wa maendeleo wameonyesha kuridhishwa na matokeo mazuri yaliyoanza kuonekana kwa kaya za walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya masikini jambo linaloendelea kuwavutia wadau wengi kujitokeza kuchangia fedha kwa ajili ya Mpango huo. 

  Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF inaendesha Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini kote ambapo takribani kaya MILIONI MOJA NA LAKI MOJA zinazokadiriwa kuwa na wakazi takribani walengwa milioni SITA zinanufaika na mpango huo.

  0 0


  0 0
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mtaa wa Mkwepu Posta jijini Dar es salaam wakati akielezea habari ya gazeti moja la wiki lililoandika habari za kwamba amefilisika na anatafutwa na mahakama,ikiwemo na kudaiwa kuwakimbia Wafanyakazi wake. 

  Akizugumza hayo jijini Dar Es Salaam,Alex Msana amesema yeye ana kampuni nyingi tu,ambazo zote ni zina Wakuregenzi wake na Mameneja wake,ambao wanakwenda kwenye shughuli zao za kiofisi kila siku, na Wafanyakazi wapo na wanaendelea na shughuli zao za kila siku .

  "Sijaona mtu yeyote kutoka Mahakamani akileta ujumbe wa yeye kuitwa mahakamani, lakini pia hakuna hata taarifa ya yeye kuitwa polisi kwa tuhuma yoyote kama ilivyodaiwa kwenye hilo gazeti,hivyo habari hizo ni za uzushi na zinalenga kumpaka matope, lakini baya zaidi zinaihusisha familia yake" alisema Msama . 

  Msama amesema kuwa ni kweli amepungunza Wafanyakazi,hasa katika kitengo cha uchapishaji wa Magazeti,ili kukidhi hali halisi ya sasa,na kwamba kampuni yake si ya Kwanza kupunguza Wafanyakazi,anasema kufuatia hatua hiyo amekuwa akisikia maneno na mengine yakisambazwa kwenye mitandao ya kijamii yenye lengo la kumchafua yeye pamoja na familia yake.

  Amesema kwa sasa ameamua kuchukua hatau,anajadiliana na wanasheria wake ili kuchukua hatua za kisheria kuwafikisha mahakamani wahusika, kwa sababu wamelenga kumvunjia heshima yeye, kampuni zake na familia yake mbele ya jamii ya Watanzania. 

  Amesema kuwa mara baada ya kuandaa utaratibu wa kisheria, watapeleka mashtaka mahakamani ili kudai haki yake ya msingi ya udhalilishaji uliofanywa na wahusika hao. 
   
  Msama amewaasa Waandishi wa Habari kutumia kalamu zao vizuri sambamba na weredi wao katika majukumu makubwa ya kuielemisha jamii,katika masuala muhimu,ikiwemo na kujenga Nchi kwa kila nyanja husika,na si kukaa na kutunga ama kuzusha habari zisizokuwa na ukweli wowote.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana  kuhusiana na Madai yake kuchafuliwa yeye na Familia yake kupitia gazeti moja litakalo kwa wiki.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akionesha kukerwa na habari hizo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye moja ya ofisi zake jijini Dar es salaam jana

  0 0

  Barclays Bank Tanzania hosted its customers for a live match viewing of the FA Cup at the ‘Karambezi by Barclays’ restaurant. After the match, customers who were able to correctly predict the winner of the match received signed jerseys and footballs from Premier League. The match ended with Arsenal lifting the trophy for a record 13th time. Go Goooners! All Barclays Premier customers who pay their bill with a Barclays Visa card qualify to receive up to 20% off food and drinks. More details in pictures;
  Barclays Bank Tanzania Retail and Business Banking Director, Kumaran Pather (left) posing for a memento photograph with some of banks valued customers. 
  Barclays Bank Tanzania Retail and Business Banking Director, Kumaran Pather (left) and banks Marketing Manager, Joe Bendera (second left), with some premier customers; Africa Practice Country Manager, Charles Washoma (right) and ENGEN Petroleum Tanzania Managing Director, Paul Muhato.
  Barclays Bank Tanzania Premier Centre Manager, Sophia Mang’enya (left) and BBT Retail and Business Banking Director, Kumaran Pather (second left) greets customers. 
  Invited customers celebrate one of the best Arsenal scores. 
  Barclays Bank Tanzania Retail and Business Banking Director, Kumaran Pather (right) celebrate a goal with a Chelsea fan. 
  Barclays Bank Tanzania Retail and Business Banking Director, Kumaran Pather (centre), handing over a ball to a customer who correctly predicted the winning team. Left is BBT Marketing Manager, Joe Bendera. 
  A customer predicted a winning team receives an award from BBT Retail and Business Banking Director, Kumaran Pather (left). 
  A customer predicted a winning team receives a gift from Barclays Retail and Business Banking Director, Kumaran Pather (centre). 
   

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, anatarajia kufanya ziara rasmi ya siku tatu kuanzia tarehe 05 Juni, 2017 Mkoani Mara.

  Kwa mujibu wa ratiba ya Mkoa, Mhe Samia atatembelea Wilaya ya Tarime, katika Kituo cha Afya cha Nyamwaga kinachojengwa na wananchi kwa msaada wa Mgodi wa Acacia North Mara.

  Pia, Mhe. Makamu wa Rais atapata fursa ya kutembelea Bonde la Mto Mara kunakokusudiwa kuanza kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari. Mchana siku hiyo hiyo atafanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Bisarwi; katika eneo hilo kunakusudiwa kujengwa kiwanda cha sukari.

  Aidha tarehe 6/6/2017 Mhe. Makamu wa Rais ataenda Wilaya ya Serengeti ambapo ataweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Wilaya; mchana atafanya Mkutano wa Hadhara katika Uwanja wa Mbuzi, Mugumu mjini.

  Tarehe 7/6/2017 Mhe. Makamu wa Rais atakuwa Musoma ambapo ataweka jiwe la msingi kwenye barabara ya km.9.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Musoma. Pia atatembelea kiwanda cha Samaki cha Musoma Fish Processors (T) Ltd na kufanya Mkutano wa Hadhara katika uwanja wa Mukendo Musoma Mjini.

  Hii ni mara ya kwanza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa na ziara rasmi Mkoani Mara.


  Jamal Zuberi
  Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano
  Mkoa wa Mara.
  30/05/2017

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Kibamba Chama-Dar es salaam
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza na Waandishi wa habari

  Mwenge wa Uhuru Mwaka 2017 utawasili kesho Tarehe 31 Mei 2017 katika Wilaya ya Ubungo kuanzia saa moja kamili asubuhi na kuzuru katika Miradi mitano ya Maendeleo.   
       
  Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori amesema kuwa katika mbio hizo za Mwenge wa Uhuru Mradi mmoja wa kituo cha Polisi Gogoni utawekwa jiwe la msingi.

  Alisema kuwa Miradi mingine itakayozinduliwa ni Mradi wa Ujenzi wa Jengo la kutolea huduma za VVU katika Kituo cha afya Mbezi, Uzinduzi wa madarasa nane katika shule ya Msingi Malambamawili iliyopo Kata ya Msigani, Uzinduzi wa Kituo cha mabasi SIMU 2000 Kata ya Sinza na Uzinduzi wa Zahaanti ya Mburahati.

  Mhe Makori alisema kuwa Miradi yote hiyo itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 itagharibu Bilioni 2,854,647,991.89

  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori amewasihi wakazi wa Manispaa ya Ubungo kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru ambao utawasili katika eneo la SAISAI Kata ya Gobaukitokea Manispaa ya Kinondoni.

  Pia amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi katika Viwanja vya Barafu, Shule ya Msingi Mburahati kwenye mkesha wa Mwenge wa Uhuru.

  Imetolewa Na:
  Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

  Mfuko wa Sekta Binafsi Nchini (TPSF) umesema kuwa katika kujenga mazingira ya biashara kunahitaji kuwepo kwa sekta ya umma pamoja na sekta binafsi katika kuandaa maeneo tengefu ya biashara.

  Hayo ameyasema leo Makamu Mwenyekiti wa TPSF, Salum Shamte kwa niaba ya Mwenyekiti wa TPSF wakati akifungua mkutano wa 17 wa mwaka wa Mfuko wa Sekta ya Binafsi (TPSF) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Shamte amesema kuwa katika kuendana na mipango ya kufikia uchumi wa kati sekta binafsi na sekta ya umma zinatakiwa kushirikiana katika kuangalia mazingira ya kufanya uwekezaji wa viwanda. 

  Amesema katika maagizo ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa wakuu wa mikoa , kutenga maeneo ya viwanda ambapo kuna uwezekano huo upo lakini changamoto ni miundombinu ya maeneo hayo.


  Aidha ameiomba serikali kuanizisha Benki ya kuendeleza viwanda ili sekta hiyo iweze kukua na kufikia uchumi wa kati kwa kuajili watanzania wengi.
  Shamte ameimba serikali kuongeza bajeti kwa mamlaka ya EPZA ili kuweza kutenga maeneo tengefu ya viwanda.

  Hata hivyo amesema kuwa sekta binafsi ndio inaajiri kwa sehemu kubwa kuliko sekta ya umma, kutokana na takwimu zinaonesha kwa mwaka vijana wanahitimu 800,000 kwa sekta ya umma inaajiri vijana 40,000. 

  Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye amesema mkutano 17 kwa majadiliano yatayofanyika yataongeza uhai wa TPSF .Amesema ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi unazidi kuimarika hivyo kunaleta tija juu mahusiano.
  Makamu Mwenyekiti wa TPSF, Salum Shamte akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa 17 wa Mfuko wa Sekta Binafsi nchini uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye akikaribisha wajumbe wa mkutano mkuu wa mfuko huo leo katika uliofanyika katika ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa EPZA ,Joseph Simbakalia akiwasilisha mada katika mkutano mkuu wa 17 wa TSPF, uliofanyika katika ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam.
  Sehemu wajumbe wa Mkutano 17 wa TPSF uliofanyika katika ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii.

  0 0


  Ofisa Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga, Athuman Rajabu (kushoto), akimwandikisha mwanachama mpya wa Hiari wa mfuko huo, Moses Francis, baada ya kupata elimu juu ya mafao yatolewayo na NSSF wakati wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Tanga Trade Fair) yaliyofanyika katika viwanja vya Mwahako jijini Tanga, mwishoni mwa wiki.
  Ofisa Matekelezo Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Tanga, Abuu Mshangama (kulia), akimkabidhi fulana ya NSSF, Hamis Chika, mmoja wa watu waliotembelea banda la NSSF kwenye Maonyesho ya Biashara-Tanga Trade Fair yaliyofanyika katika viwanja vya Mwahako jijini Tanga, mwishoni mwa wiki.
  Ofisa Matekelezo Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Tanga, Abuu Mshangama (kulia), akimkabidhi fulana ya NSSF, Hamis Chika, mmoja wa watu waliotembelea banda la NSSF kwenye Maonyesho ya Biashara-Tanga Trade Fair yaliyofanyika katika viwanja vya Mwahako jijini Tanga.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akipata maelezo alipotembelea banda la NSSF.
  Ofisa Masoko na Uhusiano wa NSSF, Anna Nguzo akitoa elimu juu ya mafao yanayotolewa na NSSF kwa wananchi waliofika katika maonyesho ya Biashara ya Tanga Trade Fair.

  0 0

  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mchungaji Anthony Lusekelo (kulia) alipomtembelea leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akipiga picha ya pamoja na ugeni kutoka Kanisa la Maombezi (GRC) ukiongozwa na Mchungaji Anthony Lusekelo (wa tatu kulia) baada ya kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akizungumza jambo wakati alipotembelewa na ugeni kutoka Kanisa la Maombezi (GRC) ulioongozwa na Mchungaji Anthony Lusekelo (wa pili kulia) katika kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kulia) akimsikiliza Mchungaji Anthony Lusekelo (kulia) kutoka Kanisa la Maombezi (GRC) pale alipomtembelea leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.

  0 0

  Wananchi wa wilaya ya Mbogwe wametakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha kuwafichua wavunaji haramu wa mazao ya misitu. 
   
  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mhe Martha Mkupasi alipofanya doria maalumu iliyoandaliwa na ofisi ya TFS kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W) - Mbogwe kwa lengo la kukamata mazao ya misitu yaliyovunwa kinyume cha Sheria ya Misitu. Katika doria hii jumla ya mbao 1889 za vipimo tofauti tofauti na mabanzi 570 vilikamatwa kwenye kijiji cha Masumbwe, vitongoji vya Kibondo A na B.

  Akiongea wakati wa zoezi hilo meneja wa TFS wilaya ya Mbogwe Yohana France aliwasisitiza wananchi wahakikishe wanazingatia taratibu za biashara ya mazao ya misitu ikiwa ni pamoja na kuwa na usajili, kulipa ushuru wa serikali na kuzingatia taratibu za uvunaji wa mazao ya misitu kama unavyoelekeza mwongozo wa uvunaji wa mazao ya misitu wa mwaka 2015, “Mazao yote yanayomilikiwa kinyume cha utaratibu ni haramu na yakikamatwa yatataifishwa na wamiliki kupewa adhabu kwa mujibu vifungu 88,89, 95 vya Sheria ya Misitu Na. 14 ya mwaka 2002 na marekebisho yake”.

  Pamoja na hayo Bwana Yohana aliwatahadharisha wananchi kujiepusha na matapeli wanaojiita watumishi wa Idara ya Maliasili na wanaopita mitaani kuwatapeli wananchi mali zao na kuwaomba rushwa kwa madai kuwa wametumwa na ofisi, tayari watu wawili ambao ni walinzi wa kampuni ya ulinzi ya Summit iliyopo Masumbwe wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani.

  Akitoa taarifa fupi wakati wa zoezi la kusaka wavunaji haramu wa misitu, Meneja wa TFS (W) amemueleza Mkuu wa Wilaya kuwa wameshatoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu taratibu za kuzingatia mtu anapotaka kufanya biashara ya mazao ya misitu na umuhimu wa kulinda rasilimali za misitu.

   baadhi ya mazao ya misitu  yaliyokamatwa
  Meneja Tfs akikagua mazao ya misitu  yaliyofichwa ndani

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Kampuni ya Saruji nchini ya Tanzania Portland Cement inayozalisha Twiga Cement, imesema kuwa itaendelea kuwa kinara kwa mauzo ya Saruji hapa nchini, licha ya kuwepo wa viwanda vingi katika miaka ya hivi karibuni.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo Alfonso Velez, alipokuwa akitoa ripoti ya mauzo ya kampuni hiyo na changamoto inazokabiliana nazo katika mkutano wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

  “licha ya makampuni mengine kuja na mpango wa ujanja wa kushusha gharama za saruji bado Twiga Cement imeendelea kuwa ndio saruji bora kwenye soko licha ya changamoto ya kupambana na bei ya soko”

  Amesema wao wameshuhudia wakiona washindani wao wakihangaika juu ya upataji wa mali ghafi ambazo zitaweza kuwasaidia kuendelea kufanya bishara kwa bei ya chini lakini TPCC bado haijatetereka.

  Amesema kuwa mshindani wake bado ana wakati mgumu kwani yuko mbali na soko na inamchukua muda mrefu kusafirisha mzigo mpaka sokoni hivyo wakati wowote atapandisha bei ya saruji na Twiga itabaki pale pale, kwani ameweza kufanya hivyo katika nchi zingine alizowekeza ambapo amepandisha bei kuwa juu hili kufidia gharama za uzalishaji.
  Mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya TPCC , Osward Urasa akizungumza katika mkutano huo juu ya wanahisa kutoa taharifa zitakazosaidia kujenga kampuni kuwa imara.
  Mwenyekiti wa kampuni ya Tanzania Portland Cement, Alfonso Rodriguez akizungumza katika mkutano huo wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika leo katika hotel ya Ramada
  Mkaguzi wa Mahesabu wa kampuni hiyo kutoka kampuni ya Ernerst nd Young , Elibariki Fanuel akieleza juuya mehesabu ya mwaka ya kampuni hiyo
  Mkurugenzi wa Twiga Cement Alfonso Velez akizungumza juuya mafanikio ya kampuni hiyo mara baada ya kuwepo ushindani wa makampuni mengine nchini
  Sehemu ya Wanahisa katika mkutano huo wakiwa wanasikiliza kwa makini
  Profesa akijadili jambo na wakurugenzina uongozi wa juu wa Twiga Cement
  Katibu wa kampuni TPCC,Brain Kangeta akizungumza wakati wa mkutano huo wa wanahisa na wateja wa Twiga Cement
  Mwanahisa Christopher Mvemo akichangia jambo juu ya kuboresha kampuni hiyo ili izidi kuwa kinara wa mauzo ya Saruji
  Mwana hisa , Godfrey Marik akiuliza swali juu ya mipango ya kampuni katika kuhimili ushindani na makampuni mengine
  sehemu ya wajumbe wa mkutano huo waliohudhuria

  0 0

  Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto) akisalimiana na Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kagera katika ziara yake mkoani humo kuzungumzia operesheni ya kuondoa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi pamoja na taratibu sahihi za kuendesha minada ya mifugo iliyotaifishwa kisheria na mahakama. Anayeongoza utambulisho huo (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa huo, Meja Jenerali Mst. Salum Kijuu. 
  Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kagera, mjini Bukoba kuhusu operesheni ya kuondoa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi pamoja na taratibu sahihi za kuendesha minada ya mifugo iliyotaifishwa kisheria. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo, Meja Jenerali Mst. Salum Kijuu na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawiro. 

  NA HAMZA TEMBA - WMU
  ---------------------------------------------------------

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Kagera unaongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Meja Jenerali Mst. Salum Kijuu kwa kufanikisha operesheni ya kuondoa mifugo katika maeneo ya hifadhi mkoani humo huku akitoa tahadhari kwa watumishi wa hifadhi hizo kupoteza ajira zao endapo wataruhusu mifugo hiyo kurudi tena katika hifadhi hizo.

  Ametoa pongezi na tahadhari hiyo jana mjini Bukoba wakati akizungumza na uongozi wa mkoa huo na kusema kuwa, kazi hiyo ni ya kupongezwa sana kwakua imeleta matumaini ya uhifadhi mkoani Kagera na taifa kwa ujumla.

  “Napenda niwashukuru kipekee kabisa kwa jinsi ambavyo mlifanya ile operesheni ya kuondoa mifugo kwenye hifadhi zetu, tulifanya kwa ueledi uliotukuka, hata kama umesikia watu wanalalamika lakini hakuna aliyesema kuku wangu waliuawa, walipigwa risasi, tulinyang’anywa mifugo, kazi hii ilifanywa vizuri na kwa ueledi mkubwa sana”, alisema Prof. Maghembe.

  Aliongeza, “Hatutaruhusu tena mifugo hiyo irudi huko ndani ya hifadhi, hili ni jambo kubwa ambalo ni wajibu wa wahifadhi wote kuhakikisha  kwamba hakuna mifugo itakayokuwa inaingia humo ndani, Kuanzia sasa kama tutakuta mtu ameingia kwenye hifadhi yako wakati tunamuondoa tunamuondoa yeye na wewe na familia yako yote ili mbegu yako mbaya isibaki katika uhifadhi wa wanyamapori”.

  Alisema ili kuimarisha ulinzi katika hifadhi hizo, utaratibu wa kutumia ndege maalum za doria na “drones” (ndege zisizo na rubani) utawekwa ili kuwabaini wahalifu watakaokuwa wamekaidia agizo hilo ili wachukuliwe hatua za kisheria.  

  “Tutakua tunarusha ndege mara moja kila baada ya wiki tatu au wiki mbili kuhakikisha kwamba hakuna mtu anaingia na mifugo humo ndani, lakini pili tutafanya doria na ndege zile ambazo hazina marobani kuhakikisha kwamba tunaangalia kinachotokea humo ndani wakati wote.

  “Najua wanaweza kubadilisha “system” (utaratibu) ikawa ya usiku na hawa askari hawa tutawapa mafunzo maalum chini ya jeshi la wananchi wa Tanzania, kuanzia miezi sita mpaka tisa, wajifunze namna ya kuhangaika na hawa ambao wanaingia kwenye hifadhi zetu”, alisema. 

  Akizungumzia operesheni hiyo, alisema ulitolewa muda maalum kwa watu kutoa mifugo yao kwa hiari katika mapori ya akiba na hifadhi za misitu mkoani humo ambapo wale wote waliotii hakuna mashtaka yeyote yalifunguliwa dhidi yao ispokuwa wale waliokaidi walifikishwa mahakamani na mifugo yao ikataifishwa kwa mujibu wa Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori kifungu namba 111 sehemu ya kwanza ambayo inaruhusu kutaifisha mali itakayokutwa hifadhini.

  Alisema kuwa kumekuwepo na malalamiko mbalimbali juu ya utaratibu wa upigaji mnada mifugo iliyotaifishwa ikiwemo minada hiyo kufanyika ndani ya maeneo ya hifadhi, wenye mifugo kutoruhusiwa kuingia na wakati mwingine kuwepo kwa malalamiko ya idadi tofauti ya mifugo iliyotaifishwa na inayopelekwa mnadani.

  Ili kuondoa malalamiko hayo alielekeza kuwa baada ya amri ya mahakama kutoka ni lazima mamlaka ya Wilaya husika ijulishwe na zoezi hilo lifanyike katika maeneo ya wazi ili kila mwananchi anayehitaji aweze kushiriki mnada husika.

  “Minada hii ifanywe kwa maelekezo ya mamlaka, hukumu ikitoka mkuu wa wilaya ajulishwe, na kwamba mifugo kadhaa itapigwa mnada, na yeye ataamua mnada ufanyike wapi na lini, na iwe sehemu ambayo kila mtu anaweza kufika, minada hiyo iwe ya wazi na matangazo yatolewe ili malalamiko yasiwepo ndio maana maelekezo yametoka minada isitishwe kwa muda wa siku saba mambo haya yawekwe sawa”, alisema Maghembe.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mst. Salum Kijuu alishukuru kwa ushirikiano alioupata kutoka Wizara ya Maliasili katika kipindi chote cha utekelezaji wa operesheni hiyo ambayo amaeielezea kuwa na mafanikio makubwa ikiwemo wanyamapori kuanza kurudi kwenye maeneo yao katika Mapori ya Akiba ya Biharamulo Burigi na Kimisi.

  “Niishukuru wizara yako mmetupa ushirikiano mzuri, kule tumesafisha tumehakikisha hakuna mifugo, hakuna kilimo, vitendo mbalimbali vya kibinadamu vilivyokuwa vikifanywa kule vya kilimo, ukataji miti hovyo, kuchoma mikaa, kulima mashamba mbalimbali ya mahindi, bangi, mirungi sasa hayapo tena, Nashukuru kwa muda huu mfupi wanyama wengi wamesharudi, wengi tuu, hadi Simba wamesharudi kwenye maeneo yao” alisema Kijuu.

  Operesheni ya kuondoa mifugo na wananchi waliovamia Hifadhi ya Misitu ya Biharamulo, Nyantaka na Ruiga na Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi na Kimisi mkoani Kagera ilianza tarehe 30 Machi, 2017 ambapo jumla ya mifugo 5,939 ilikamatwa (Ng’ombe 5754, Mbuzi 140 na kondoo 45) na watuhumiwa 185 walikamatwa na kufikishwa mahakamani.  
  Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kagera, mjini Bukoba kuhusu operesheni ya kuondoa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi pamoja na taratibu sahihi za kuendesha minada ya mifugo iliyotaifishwa kisheria. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa huo, Meja Jenerali Mst. Salum Kijuu, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawiro (kulia), Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Diwani Athuman (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof. Alexander Songorwa. 
  Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kagera, mjini Bukoba. 
  Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Maliasili (katikati waliokaa) na kamati ya ulinzi na usala ya Mkoa wa Kagera muda mfupi baada ya kikao cha kujadili operesheni ya kuondoa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi pamoja na taratibu sahihi za kuendesha minada ya mifugo iliyotaifishwa kisheria.
   Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii (katikati waliokaa), Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mst. Salum Kijuu (wa pili kulia waliokaa), Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawiro (wa pili kushoto waliokaa), Katibu Tawala Mkoa huo, Diwani Athuman (kulia waliokaa), Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof. Alexander Songorwa (kushoto waliokaa), Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Martin Laibooki (katikati waliosima) na maofisa wa Mamlaka hizo.
  Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mst. Salum Kijuu (kushoto) akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Martin Laibooki (wa pili kushoto) Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Kudhibiti ujangili, Faustine Masalu (kulia).
  Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof. Alexander Songorwa (kulia), Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo (katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Martin Laibooki (kushoto). 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akisalimiana na uongozi wa Wilaya ya Biharamulo alipotembelea wilayani humo kwa ajili ya kutoa maelekezo ya Serikali kuhusu operesheni ya kuondoa mifugo katika maeneo ya hifadhi pamoja na taratibu sahihi za kuendesha minada ya mifugo iliyokamatwa na kutaifishwa na mahakama. Anayeongoza utambulisho huo (kulia) ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Sada Malunde.
   Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na viongozi wa Kamati ya Ulinzi na usala ya Wilaya ya Biharalamulo na watumishi wa sekta ya wanyamapori wilayani humo. 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza Kamati ya Ulinzi na usala ya Wilaya ya Biharalamulo na watumishi wa sekta ya wanyamapori wilayani humo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Sada Malunde na Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Diwani Athuman (kushoto). 
   Baadhi ya askari na watumishi wa Idara ya Wanyamapori wa Wilaya ya Biharamulo.
  Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, viongozi wa mamlaka za uhifadhi, watumishi na kamati ya ulinzi na usala ya Wilaya.
  Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akiagana na Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Diwani Athuman pamoja na viongozi wengine wa chama na Serikali wa Wilaya ya Biharamulo baada ya kumaliza ziara yake Mkoani humo ya kujadili operesheni ya kuondoa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi pamoja na taratibu sahihi za kuendesha minada ya mifugo iliyotaifishwa kisheria.

older | 1 | .... | 1251 | 1252 | (Page 1253) | 1254 | 1255 | .... | 1898 | newer